Tangazo 2014

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

TANGAZO

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2013/2014 Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Watalamu wote wanatakiwa kuripoti kwa waajiri wao ndani ya siku 14 tokea tangazo hili lilipotolewa. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa. Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za afya. Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali. Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi, na ninawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka. KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII 8 Aprili, 2014

You might also like