Professional Documents
Culture Documents
tz
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1074 RAJAB 1434, IJUMAA JUNI 7 - 13, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Wasiotaka Dola kamili wajitokeze Mgombea Urais asitokee Dodoma Wakumbusha ya Kura za Karume
Inaendelea Uk. 3
Wajumbe wa kikao cha uzinduzi wa mihutasari ya somo la dini na maadili wakisiliza kwa makini na utulivu. Habari Uk. 12
tutumie akili ya asili kuchanganua mambo. Vita kubwa iliyoko mbele yenu ni kuondoa dhulma iliyoshamiri nchini. Lengo liwe ni kutafuta j i n s i g a n i Wa i s l a m u wanaweza kuushinda huu "MFUMO" ili Wananchi wote wa nchi hii wawe na haki sawa na waishi kwa amani kama ilivyokawaida. Uk. 8
2
www.annuurpapers.co.tz
Tahariri/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
AN-NUUR
kwa mtu kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi. (Sehemu ya Tatu Kif: 12 (4)) Katika kufafanua nini maana ya ubaguzi kifungu 12 (5) kinasema kuwa Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa mashariti ya Ibara hii neno kubagua maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au mashariti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya mashariti au sifa za lazioma Bible Knowledge na Islamic Knowledge yote n i m a s o m o ya d i n i , unaposema kuwa A kwa Mkristo ni 75 lakini kwa A hiyo hiyo Muislamu ni lazima apte 85, je huu sio ubaguzi? Je, ubaguzi huu ndio Mbatia anaohimiza Dr. Joyce Ndalichako aendelee kuufanya bila kuogopa? Ukiweka pass mark ya A kuwa ni 75 mpaka 100, maana yake ni kuwa kwanza unafanya kuwa wepesi kwa watahiniwa kupata A, lakini pia unatoa fursa kwa watahiniwa wengi kupata hiyo A. Na kwa upande mwingine unapopandisha k u wa 8 5 m p a k a 1 0 0 ni kuwa unaweka ugumu na kupunguza idadi ya watakaopata hiyo A. Nini lengo la ubalakala huu? Huku
ni kuwawekea vikwazo Waislamu au mashariti na vipingamizi vya kufaulu ambapo Wakristo wanarahisishiwa. Je, hii inafanywa makusudi ili kuziwezesha zile shule zinazotakiwa kutesa ziendelee kutesa kila mwaka? Je, hii ndiyo kazi Mheshimiwa Mbatia anayomwambia Dkt. Ndalichako aendelee kuifanya bila kuogopa? Baraza la Mitihani limeajiri Mchungaji anayeratibu somo la Bible Knowledge, lakini limegoma kabisa kuajiri Maratibu wa Somo la Maarifa ya Uislamu. Je, huu nao sio ubaguzi kwa m u j i b u wa K a t i b a ya nchi? Wakati NECTA ikiajiri Mchungaji na wataalamu wa lugha za Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa, imegoma pia kuweka Mtaalamu wa Lugha ya Kiarabu na kufanya somo hilo kuratibiwa na mtu asiyejua hata Alifu. Je, huu ndio utaalamu unaotokana na PhD First Class? Moja ya tafiti zinaonyesha kuwa katika somo la Hesabu, mwaka 2011 ili kupata A mtahiniwa alitakiwa kupata alama 75. Lakini mwaka 2012 ili upate A ilikuwa lazima uwe na alama 86 ambayo inaongeza ugumu wa kupata alama kwa point
Al-farouq Seminary Secondary school is seeking for the suitable Headmaster for the school. Qualications: The person should: 1. Be a Tanzanian. 2. Be a holder of at least a degree in Education. 3. Have held the position for not less than three years or have served as a deputy for not less than ve years. 4. Have a proven good track record. 5. Knowledge of Arabic will be an added advantage. A good package would be offered. He should be ready to assume ofce immediately. Applications with C.V and testimonials, should reach the undersigned through emails below on or before 15th June 2013. The Director, P.O.Box.9211.Dar-es-salam. Email: tanzania@direct-aid.org. cc. abuibrahim05@yahoo.com
Vacancy-Headmaster
Habari
AN-NUUR
MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MARIDHIANO ZANZIBAR KUHUSU UPI UWE MWELEKEO WA WAZANZIBARI KATIKA KUIJADILI RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ITAKAYOTOLEWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
UTANGULIZI: Baada ya wananchi wa Zanzibar kutoa maoni yao juu ya vipi Muungano wa Zanzibar na Tanganyika unapaswa kuwa, hatimaye Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajiwa kutoa rasimu ya awali ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwishoni mwa mwezi Mei na mwanzoni mwa mwezi Juni 2013. Wakati tunaisubiri kwa hamu rasimu hiyo itolewe na kujua kilichomo, sisi wa j u m b e wa K a m a t i ya Maridhiano Zanzibar tumekaa na kutafakari juu ya u p i u n a p a s wa k u wa mwelekeo wa Wazanzibari katika kuadili rasimu hiyo pale itakapotoka. Baada ya mashauriano ya kina kati ya wajumbe wa Kamati ya Maridhiano na pia kwa kuwahusisha watu wengine mashuhuri hapa Zanzibar, tumekuja na mapendekezo yafuatayo ambayo leo hii tunayawasilisha kwa wananchi wa Zanzibar kupitia Kongamano hili. Haya si maagizo bali ni mashauri yenu na pindi mkiyakubali basi tutakuombeni tuyafanyie kazi kwa pamoja kwa kuyatumia katika kuipokea na kujadili rasimu pale itakapotolewa. Mapendekezo yetu ni kama ifuatavyo: 1. Jina la Muungano: Muungano huu umetokana na Jamhuri mbili kuungana kwa hiyari. Jamhuri hizo ni Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Jina la awali lililotajwa katika Mkataba wa Muungano la muungano wa jamhuri hizi mbili lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jina hili baadaye mwezi Oktoba 1964 lilibadilishwa na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukiangalia mifano ya nchi nyingine zilizoungana, jina la muungano huweka bayana kwamba zilizoungana ni zaidi ya nchi moja, zaidi ya falme moja au zaidi ya jamhuri moja. Kwa mfano, muungano wa nchi (states) za Marekani unaitwa kwa kiingereza United States of America (USA), ule uliokuwa muungano wa jamhuri za kisovieti ukiitwa Union of Soviet Socialist Republics (USSR) na ule muungano wa falme za kiarabu unaitwa United Arab Emirates (UAE). Ili kuondosha dhana iliyojengeka kwamba muungano wa jamhuri zetu mbili umeunda nchi moja na kuzifuta nchi zetu, Katiba Mpya inapaswa kuweka jina linalotambua msingi huo na historia hiyo. Hivyo basi, jina jipya liwe ni Muungano wa Jamhuri za Tanzania na kwa kiingereza United Republics of Tanzania. Jina hili litasaidia utambulisho wa nchi wanachama katika uwanja wa kimataifa pale litapoambatanishwa katika nyaraka zote rasmi pamoja na jina la nchi husika. Kwa maana hiyo katika uwanja wa k i m a t a i f a n a k a t i k a pasi za kusafiria utaweka wazi na kuwa na UNITED REPUBLICS OF TANZANIA REPUBLIC OF ZANZIBAR na UNITED REPUBLICS OF TANZANIA REPUBLIC OF TANGANYIKA. 2. Mipaka ya Zanzibar na Tanganyika: Wa k a t i z i n a u n g a n a , Zanzibar na Tanganyika zilikuwa tayari ni nchi zenye m a m l a k a k a m i l i z i k i wa ni wanachama wa Umoja wa Mataifa na hivyo kila moja ilikuwa na mipaka yake inayoeleweka. Katiba na sheria za nchi mbili hizi ziliweka bayana mipaka hiyo na mipaka hiyo ilitambuliwa chini ya sheria za kimataifa. Rasimu ya Katiba Mpya ni lazima itamke kwa uwazi kabisa na kutambua na kuheshimu mipaka ya nchi mbili hizi kama ilivyokuwa kabla ya siku ya Muungano tarehe 26 Aprili, 1964. Baada ya hapo, Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanganyika (itakayotungwa baada ya kupata Katiba mpya ya Muungano) kila moja iweke wazi mipaka yake. 3. Uraia: Uraia ndiyo msingi wa ujananchi. Kwa vyovyote vile Katiba Mpya isumuishe suala la Uraia kuwa la pamoja kupitia Muungano. Kila nchi mwanachama katika muungano ibakie na uraia wake na iratibu masuala yote yanayohusu uraia wake na raia zake. Kwa kufuata mfano kama wa Muungano wa Ulaya (European Union), u n a we z a k u wa n a h a k i inayotambulika kikatiba ya uhuru wa raia wa nchi moja mwanachama kwenda katika nchi nyengine mwanachama kupitia utaratibu maalum utakaowekwa (free movement of people). Hata hivyo, kila nchi mwanachama iwe na haki ya kuweka utaratibu wa vipi raia hao watafaidi haki na fursa za nchi mwanachama nyingine. Hili ni la muhimu hasa kwa nchi ndogo kama Zanzibar ambayo ina rasilimali ndogo ya ardhi na hasa ikizingatiwa kuwa ardhi ilikuwa mojawapo ya sababu kuu za kufanyika Mapinduzi. Katika hali kama hiyo, Zanzibar ina sababu nzito za kuona inadhibiti na kusimamia wenyewe Uraia wake na utambulisho wa raia hao. Hivyo basi, suala la Uraia lisiwemo katika mambo ya Muungano na badala yake kila nchi isimamie yenyewe
Inaendelea Uk. 4
Umesema uchambuzi huo na kutoa wito kwa Wazanzibari kusoma Rasimu ya Katiba kwa undani ili kugundua dosari kama hizo. Kwa hofu hiyo unapigwa mfano wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ambapo katika kura za maoni za mgombea Urais kwa upande wa Zanzibar, waliokuwa wametakiwa na CCM Zanzibar, sio walioteuliwa kugombea Urais. Waliteuliwa waliokuwa na kura chache za Wazanzibari lakini waliokuwa wakipendeza zaidi kwa wana CCM Bara. Baadhi ya ambo yaliyotajwa katika uchambuzi huu wa awali, yanawiana kwa karibu na mapendekezo yaliyotolewa na ile Kamati ya Mzee Moyo. Katika mapendekezo yake kamati hiyo imesema kuwa, Uraia ndiyo msingi wa ujananchi. Kwa vyovyote vile Katiba Mpya isumuishe suala la Uraia kuwa la pamoja kupitia Muungano. Kila nchi mwanachama katika muungano ibakie na uraia wake na iratibu masuala yote yanayohusu uraia wake na raia zake. Kwa kufuata mfano kama wa Muungano wa Ulaya (European Union), u n a we z a k u wa n a h a k i inayotambulika kikatiba ya uhuru wa raia wa nchi moja mwanachama kwenda katika nchi nyengine mwanachama kupitia utaratibu maalum utakaowekwa (free movement of people). Hata hivyo, kila nchi mwanachama iwe na haki ya kuweka utaratibu wa vipi raia hao watafaidi haki na fursa za nchi mwanachama nyingine. Kamati hiyo ikasema kuwa Uraia ni jambo muhimu h a s a k wa n c h i n d o g o kama Zanzibar ambayo ina rasilimali ndogo ya ardhi na hasa ikizingatiwa kuwa ardhi ilikuwa mojawapo ya sababu kuu za kufanyika Mapinduzi. Katika hali kama hiyo, Zanzibar ina sababu nzito za kuona inadhibiti na kusimamia wenyewe Uraia wake na utambulisho wa raia hao. Ikasisitiza Kamati hiyo kuwa, kwa vyovyote itakavyokuwa suala la Uraia lisiwemo katika mambo ya Muungano na badala yake kila nchi isimamie yenyewe masuala ya Uraia. Na kwa sababu hizo hizo ikapendekezwa kuwa hata Uhamiaji, kila nchi iwe na Idara yake ya Uhamiaji. Kamati inasema, kutokana na sababu tulizozitaja hapo juu kuhusiana na suala la Uraia inapelekea wazi kuwa kila nchi mwanachama idhibiti na kusimamia wenyewe mambo ya Uhamiaji. Hivyo b a s i , r a s i m u ya K a t i b a Mpya isijumuishe suala la
Inaendelea Uk. 4
Habari
AN-NUUR
Uhamiaji kuwa ni suala la Muungano. Wa k a t i h u o huo, wasiotaka Mamlaka kamili ya Serikali na Dola ya Zanzibar, wametakiwa kujitokeza hadharani kama ilivyo kwa wanaopigania mambo hayo. H a yo ya m e s e m wa n a Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiunga mkono kauli iliyotolewa awali na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Eddi Riyami ya kuwataka Wa z a n z i b a r i wa s i o t a k a mamlaka kamili ya Zanzibar wajitokeze hadharani kama wanavyofanya wale wanaodai mamlaka kamili ya Zanzibar. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF ametoa wito huo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliolenga kusherehekea Umoja wa Wazanzibari ulioasisiwa kufuatia maridhiano ya kisiasa. Maalim Seif amesema, hatua ya Wazanzibari kudai mamlaka ni haki yao, na kwamba hakuna dhambi ya kudai jambo hilo. A m e f a h a m i s h a k u wa Wazanzibari walio wengi wameungana kudai mamlaka ya nchi yao kwa njia ya amani na demokrasia, na kutoa wito kwa wale wasiotaka mamlaka ya Zanzibar wajitokeze hadharani. Amewahakikishia wananchi kuwa hatorudi nyuma katika kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka yake, ili iweze kutambulika kimataifa na kuweza kuratibu na kushughulikia mambo yake ya nje. Kwa upande wake Katibu wa kamati ya maridhiano Ismail Jussa Ladhu, amewaomba viongozi wa vyama vyote kushirikiana na wananchi katika kudai mamlaka ya nchi, ili Wazanzibari waweze kujikomboa kutokana na kile alichokiita ukoloni wa Tanganyika. Katika risala ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar iliyosomwa na Ameir bin A m e i r k u t o k a B we j u u , amesema pamoja na mambo m e n g i n e , k a t i b a m p ya izingatie uwepo wa Jamhuri ya Zanzibar na uraia wake. Mambo mengine waliyotaka yatolewe katika orodha ya mambo ya Muungano ni pamoja na sarafu, Benki Kuu, Mambo ya Nje, vyama vya siasa, Baraza la Mitihani pamoja na mafuta na gesi.
Inatoka Uk. 3
M A P E N D E K E Z O Y A K A M AT I Y A MARIDHIANO ZANZIBAR KUHUSU UPI U W E M W E L E K E O WA WA Z A N Z I B A R I KATIKA KUADILI RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ITAKAYOTOLEWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
na badala yake kila nchi isimamie yenyewe mamlaka yake juu ya mambo ya nje. Hata hivyo, uratibu wa sera ya mambo ya nje (foreign policy coordination) inaweza kuwa ni suala la muungano lakini utekelezaji wake kila nchi ikausimamia kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje. Uratibu wa sera ya mambo ya nje unaweza kufanywa kupitia chombo cha pamoja kitakachoundwa na Wizara za Mambo ya Nje za nchi mbili hizi kwa mfano kuwa na Council on Foreign Policy. Kutokana na hoja hizo hapo juu inabaki kuwa kila nchi iwe na uanachama na kiti chake katika Umoja wa Mataifa na jumuiya nyengine za kimataifa. Hayo si ajabu katika miungano. Umoja wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti (USSR) ulikuwa na uanachama na kiti chake Umoja wa Mataifa lakini miongoni mwa nchi wanachama, Jamhuri tatu za Ukraine, Belarus na Georgia ziliamua kuwa na uanachama na viti vyao katika Umoja wa Mataifa na hilo liliwezekana. Kwa msingi huo huo, Zanzibar iwe na uanchama wa k e k a t i k a U m o j a wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya SADC na jumuiya nyengine za kikanda na za kimataifa. 6. Sarafu, Benki Kuu, Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje, Ushuru wa Forodha, Kodi ya Mapato na Kodi ya Mashirika: Uchumi si suala la Muungano hata katika Katiba inayotumika sasa. Hata hivyo, nyenzo za kuendeshea na kusimamia uchumi wa nchi kwa maana ya sera za fedha na uchumi (scal and monetary policies) zimeendelea kudhibitiwa kupitia Serikali ya Muungano. Vyombo vikuu vinavyosimamia sera hizo ambavyo ni Benki Kuu (BOT), Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha ya Serikali ya Muungano vimekuwa vikifanya maamuzi na kuyatekeleza bila ya kuzingatia kuwa kwa maumbile uchumi wa Zanzibar ambao ni uchumi unaotegemea utoaji wa huduma (service oriented economy) hauwezi kuwa sawa na uchumi wa Tanganyika ambao unategemea rasilimali (resource based economy). Sera za fedha na uchumi zikiwemo zile zinazohusu udhibiti wa sarafu na viwango vya kodi, ushuru na riba katika mabenki zimekuwa zikitungwa bila ya kuzingatia msingi huo wa chumi mbili zilizo tofauti na badala yake mara zote zimeegemezwa kwenye kulinda maslahi ya uchumi wa Tanganyika. Sarafu ya pamoja imekuwa ikishuka thamani kwa kasi kila uchao kutokana na sababu nyingi lakini miongoni mwake zaidi zinatokana na uendeshaji mbaya wa uchumi wa Tanganyika. Serikali inapochapisha sarafu zaidi ili kudhibiti mfumko wa bei athari zake zinaikumba pia Zanzibar. Zanzibar inahitaji kujikomboa kiuchumi ili iweze kutekeleza malengo ya Mapinduzi kwa wananchi wake na hivyo inahitaji kuwa na mamlaka yake kamili katika kusimamia masuala ya sera za fedha na uchumi yakiwemo masuala yote yanayohusu sarafu, viwango vya kodi na ushuru pamoja na riba katika mabenki, mikopo na biashara ya nchi za nje. Kutokana na hali hiyo, masuala ya sarafu, benki kuu, mikopo na biashara ya nchi za nje, ushuru wa forodha, kodi ya mapato na kodi ya mashirika kila nchi inapaswa iyasimamie yenyewe. 7. Polisi: Pamoja na kuwemo katika mambo ya awali ya Muungano lakini uendeshaji wa Polisi u m e k u wa n a m a t a t i z o yake katika muungano. Miaka yote Polisi Zanzibar imekuwa ikilalamika kuwa inachukuliwa kama vile ni Mkoa tu na hata bajeti na mahitaji yake mengine yanachukuliwa hivyo hivyo na makao makuu ya Polisi yaliyopo Dar es Salaam. Katika nchi nyingi duniani Polisi ambayo inashughulika na usalama wa raia na mali zao imekuwa ikiendeshwa chini ya Serikali za Manispaa na hata Majimbo seuze kwa nchi kama ilivyo Zanzibar. Ukiondoa mishahara na bajeti ndogo ya uendeshaji inayotolewa na makao makuu ya Polisi, gharama nyengine za uendeshaji wa polisi kwa Zanzibar zimekuwa zikichangiwa na mamlaka za Zanzibar ikiwemo Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Hivyo basi, wakati umeka kuona mamlaka kuhusu Polisi yanaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano na kila nchi ishughulikie yenyewe Polisi yake. 8. Mafuta na Gesi Asilia (pamoja na maliasili nyengine zote):
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa niaba ya Wazanzibari lilishafanya m a a m u z i m we z i A p r i l i 2009 kuyaondoa masuala ya mafuta na gesi asilia kutoka kwenye orodha ya mambo ya Muungano. Mbali na maazimio ya Baraza la Wawakilishi, masuala ya mafuta na gesi asilia yanahusu uchumi ambalo si suala la Muungano. Katiba Mpya haipaswi kuyajumuisha masuala hayo mawili (pamoja na maliasili nyengine kwa ujumla) kuwa mambo ya Muungano. Hivyo basi, rasimu yoyote itakayoyajumuisha masuala hayo ya Mafuta na Gesi Asilia (pamoja na maliasili nyengine zote kwa ujumla) kuwa masuala ya Muungano haitakubalika kwa Wazanzibari. 9. Vyama vya Siasa: M u u n g a n o u l i u n d wa n a J a m h u r i y a Wa t u wa Zanzibar na Jamhuri ya Ta n g a n y i k a k u p i t i a serikali zao. Mazungumzo yaliyopelekea muungano huo na hata utekelezaji wa hatua za kuunganisha nchi mbili hizi katika muungano hayakuhusisha vyama vya siasa vya wakati huo, ASP kwa upande wa Zanzibar na TANU kwa upande wa Tanganyika. Ndiyo maana kwa miaka 13 ya Muungano (kuanzia 1964 hadi 1977) kila nchi kati ya nchi mbili hizi iliendelea kuongozwa na chama chake cha siasa. Moja kati ya dhoruba kubwa dhidi ya makubaliano ya asili ya muungano huu ambayo ni Mkataba wa Muungano ilikuwa ni kuunganisha vyama vya siasa vya ASP na TANU na kuunda CCM ambacho kilitangazia kushika hatamu na kuwa juu ya vyombo vyengine vyote vya nchi zikiwemo Serikali. Utaratibu huo uliingizwa ndani ya Katiba za nchi na hivyo kuuhalalisha kisheria. Tokea wakati huo, Zanzibar imekosa mamlaka ya kisiasa ya kufanya maamuzi yake kwa mambo yanayoihusu. Na pale ilipofanya hivyo ilifanya kwa kutegemea na kujiamini kwa uongozi uliopo Zanzibar ingawa majaribio ya kutumia nguvu ya vyama kuzuia maamuzi kama hayo yamekuwa yakifanyika na baadhi ya wakati kufuzu. Maongozi ya nchi yoyote yanategemea historia, mila na utamaduni wa watu wa nchi husika. Kwa msingi huo basi, na ili Zanzibar iweze kurejesha mamlaka yake ya kisiasa katika kufanya na kusimamia maamuzi kwa mambo yake, rasimu ya Katiba haipaswi kujumuisha suala la vyama vya siasa kuwa ni jambo la Muungano. Zanzibar na Tanganyika kila moja iweze kuandikisha vyama vyake vya siasa. 10. U t a r a t i b u w a uendeshaji wa Mambo ya Inaendelea Uk. 5
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
WA N A H A R A K AT I w a Hizbullah nchini Lebanon wamewaangamiza waasi 20 wanaopigana dhidi ya serikali ya Syria nchini Lebanon. Habari zinasema, wanamgambo hao wameuawa katika mapigano yaliyotokea Jumapili iliyopita mjini Balabak, kusini mwa Lebanon. Awa l i wa a s i h a o wanaopambana dhidi ya serikali ya Syria waliushambulia mji huo kwa maroketi kutoka katika maeneo ya mpakani ya Syria na kusababisha uharibifu wa mali.
Hizbullah waangamiza waasi 20 Lebanon Tanzania yaiomba Japan kusaidia masomo ya sayansi na hisabati
Aidha siku ya Ijumaa waasi hao waliyashambulia kwa maroketi 14 maeneo ya Nabi Shith na Nasiriya, yaliyo karibu na mji wa Balabak upande wa mashariki mwa Lebanon. Kuendelea mashambulizi ya waasi dhidi ya maeneo ya mpakani ya Lebanon, yamewatia hasira kubwa raia wa nchi hiyo. Hali hiyo imewalazimu v i o n g o z i wa H i z b u l l a h kutoa onyo kwa waasi hao n a k u b a i n i s h a k wa m b a hawarudi nyuma kutokana na vitisho vyao. Hivi karibuni Naibu wa Baraza la Utendaji la Wanarakati hao, Sheikh Nabil Kaouk, alinukuliwa akisema kuwa mashambulizi ya waasi wa Syria dhidi ya maeneo ya mpakani ya Lebanon hayawezi kuwafanya wanaharakati hao kubadili mwelekeo wake kuhusiana na masuala ya Syria.
vyama mbalimbali vya upinzani nchini Misri wamepinga ujenzi wa bwawa kwenye mto Nile nchini Ethiopia. Wa j u m b e h a o walifikia uamuzi wa k u i z u i a s e r i k a l i ya Ethiopia isenge bwawa kwenye maji ya mto Nile kufuatia kikao kilichoitishwa na Rais wa Misri, Mohamed Morsi mapema wiki hii, kujadili hatua ya hiyo jirani kutaka kujenga bwawa hilo. Ta a r i f a z i n a e l e z a kuwa kiongozi mmoja wa upinzani nchini Misri amesema kuwa, kadhia ya ujenzi wa bwawa hilo ni ya kitaifa hivyo kuyataka makundi yote nchini humo yashikamane kwa lengo la kutafuta njia za kuutatua mgogoro huo. Kikao hicho pia kimesisitiza juu ya kufuatwa sheria na taasisi za kimataifa kwa lengo la kuizuia Ethiopia isenge bwawa hilo, ambalo huenda likaziathiri Misri na Sudan katika sekta ya kilimo. Aw a l i R a i s Mohammad Morsi wa
TOKYO S e r i k a l i y a Ta n z a n i a imeiomba Japan kusaidia walimu wa hisabati na sayansi namna ya kufundisha walimu wa masomo hayo, kama njia ya kukabiliana haraka na uhaba mkubwa wa walimu wa masomo hayo nchini. Rais Kikwete alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya elimu nchini, ni ukosefu
wa walimu wa hisabati na sayansi, masomo ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya nchi. Ombi hilo kwa Japan l i m e t o l e wa J u m a t a t u wiki hii, wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Misaada ya Kimataifa la Japan ( JICA), Dakta Akihiko Tanaka, mjini Yokohama. Aidha Rais Kikwete
ameiomba Japan kusaidia uchapishaji wa vitabu vya sayansi na hisabati, ili kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi wa Tanzania anakuwa na nakala ya vitabu vya masomo hayo kama njia ya kuongeza ubora wa elimu nchini. Rais Kikwete alikuwa Japan kwa ziara ya siku saba kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Tano wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD), ambao umemalizika Jumanne wiki hii.
wito wa kushiriki katika kikao hicho. Uamuzi wa ghaa wa Ethiopia wa kubadilisha mwelekeo wa maji ya mto Nile kwa lengo la kujenga bwawa la al Nahdha, umezusha hofu kubwa kwa viongozi na wananchi wa Misri na Sudan.
6
Na Shaaban Rajab
MATUKIO ya jeshi la polisi kuhusishwa na vitendo vya uhalifu nchini yamezidi kushika kasi nchini. Ni jambo linalofahamika kwamba kazi kubwa ya jeshi la polisi, ni kulinda usalama wa watu na mali zao na kuzua vitendo vyote vya kihalifu nchini. Hayo ndio majukumu ya msingi ya kuhalalishwa kuwepo jeshi hilo. Kutokana na majukumu hayo ya kiusalama ya jeshi letu la polisi, wananchi waliwaamini, kuwaheshimu na kuwategemea sana kiulinzi na kiusalama. Hata hivyo kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, jeshi hili limezidi kuporomoka kimaadili na kiutendaji, hali inayowafanya wananchi kukosa imani na jeshi hilo. Tamaa ya fedha kwa baadhi ya askari na watendaji wa ngazi za juu wa jeshi hilo imekuwa sababu kubwa ya chombo hiki kuyumba kiufanisi na kutiliwa mashaka. Rushwa inayotokana na tamaa ya kupata fedha au maslahi kwa njia za mkato, imewafanya askari wengi katika jeshi hilo kuweka pembeni wajibu wao wa msingi kwa wananchi na kujiingiza katika vitendo vya kihalifu. Badala ya kuwa vinara wa kupambana na uhalifu, sasa wamekuwa vinara wa kutumia sare za jeshi kuchuma chumo h a r a m u . Wa n a d h u l u m u , wanapora, wanabambikia watu kesi, wanaonea na kutesa watuhumiwa. Ile kazi ya msingi ya kuzuia uhalifu imekuwa ni chaguo la pili katika utendaji wa kazi zao. Ni hivi karibuni tu, gari la mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Arusha, lilikamatwa huko Himo Mkoani Kilimanjaro likisarisha bangi magunia 18 kwenda Tarakea Rombo. Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, zilipasha kuwa gari hilo lilikamatwa siku ya Jumamosi majira ya saa 4:00 usiku. Tukio hili linaonyesha ni jinsi gani baadhi ya askari wa jeshi letu la Polisi, tena wengine wakiwa ni vigogo katika jeshi hilo badala ya kuzuia uhalifu, wao ndio vinara wa uhalifu wenyewe. Jambo la kushangaza ni kwamba, hata yule askari dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo, naye ameripotiwa kutoroka akiwa mikononi mwa polisi wenyewe baada ya kukamatwa. Bila shaka utoro wa askari huu, hauwezi kuacha kuleta dhana za kuhusika kigogo ndani ya jeshi hilo katika tukio hilo. Siku za nyuma kidogo, Jeshi hilo mkoani Morogoro liliingia kwenye kashfa nzito baada ya askari wake watatu kukamatwa wakiwa na kichwa cha binadamu. Tukio hilo lilitokea Mei 7 mwaka huu katika eneo la Mgudeni huko Dumila wilayani Kilosa. Taarifa zinaelezwa kuwa polisi hao kwa kushirikiana na raia, walikwenda nyumbani kwa
MAKALA
AN-NUUR
mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Samson Mura na kutaka kumbambikizia kesi ya mauaji. Polisi hao walidaiwa kuwa waliomba shilingi milioni 25 kutoka kwa mfanyabiashara huyo, ili wasimpeleke kituoni, kwa kosa hilo la kubambika. Harakati zote hizo bila shaka zinatokana na tamaa ya kupata fedha kwa njia haramu ya kutumia vibaya nafasi zao. Mei mwaka huu, jeshi la polisi pia liliingia katika kashfa hizo hizo za kihalifu, pale askari wake walipotuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara wanaokwepa kodi na maafisa wa Mamlaka ya Kodi-TRA, kuingiza bidhaa kupitia njia za panja za pwani ya bahari ya Hindi, yaani pwani ya Dar es Salaam na Bagamoyo. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ilitangaza kuwakamata askari wake 16 kwa tuhuma za kushiriki na kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa magendo wanaovusha bidhaa zao kupitia bandari bubu kandokando ya Bahari ya Hindi na maeneo mengine. Hatua hiyo ilitokana na kubainika kuwa baadhi ya askari wametengeneza mtandao ulioanzishwa zaidi ya miezi sita kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao hukusanya fedha kinyume cha sheria kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru halali Serikalini. Si hayo tu katika tukio jingine, baadhi ya polisi walidaiwa kuhusika katika upotevu wa fedha zinazokadiriwa kufikia milioni 150 katika tukio la ujambazi lililotokea Kariakoo jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo lililotokea Desemba mwaka jana, Jeshi la
barabarani. Kwa staili hii, ni wazi kwamba hata yale makusanyo ya faini halali kwa wakosaji barabarani, yatakuwa ni kiduchu ikilinganishwa na kiasi kinachoishia mifukoni mwa askari hao na serikali kuambulia pato haba. Lakini ni polisi hao hao ambao hufanya kazi yao kwa weledi na uhodari kabisa, pale wanapopewa jukumu la kuthibiti mikutano ya hadhara ya kisiasa, mihadhara ya kidini au maandamano. Hapa wanaonyesha ufundi wao wa kudhibiti raia wasiokuwa na silaha kiasi cha kupiliza hata kuua. Haya ni baadhi tu ya matukio ya kihalifu, ambayo Jeshi letu la polisi limekuwa likihusishwa nayo. Matukio ya namna hii ndio yanayochochea zaidi wananchi kujichukulia sheria mikononi. Yote haya ni kwasababu kwa ushahidi wa matukio kama haya, wananchi wanafikia mahali wanakosa imani na utendaji wa jeshi lao. Lakini pia inaonekana kuwa jeshi la polisi limekuwa likitumika zaidi kisiasa. Hasa kwa kuzingatia kwamba jeshi letu limekuwa likitumia nguvu na vifaa vingi kudhibiti watu wanaoshiriki katika matukio ya kisiasa kama maandamano na mihadhara, kuliko yale ya kihalifu. Pamoja na askari wa jeshi la polisi mara kwa mara kuhusishwa na vitendo vya kihalifu, lakini mara nyingi askari wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu, kesi zao hazijulikani zinaishia wapi na wala hakuna taarifa zinazotolewa kwa umma kuhusu hatua walizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao na hatma yao imekia wapi. Ili kukomesha mazea haya ya vyombo vya nguvu za dola
7
Na Shaaban Rajab. RAIS Barack Obama wa Marekani, anatarajiwa kuzuru nchini Julai Mosi mwaka huu. Hivi sasa serikali ipo katika harakati kubwa za maandalizi ya ujio wa mgeni huyo, ambaye tumeelezwa kuwa atatua nchini na ujumbe usiopungua watu 700. Huyu ni Rais wa tatu wa Marekani kuzuru nchini achilia mbali Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Taifa hilo kubwa. Kabla ya kuja Rais Obama, Juni 11 hadi 13, 2011, aliyekuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Bi. Hillary Clinton, ambaye pia ni mke wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, naye alizuru nchini kwa ziara ya siku tatu. Kwa mara ya kwanza Rais wa Marekani kuzuru Tanzania tangu utawala wa marais 45 waliowahi kuliongoza Taifa hilo kubwa, ni Rais mstaafu Bill Clinton. Clinton alizuru nchini Agosti 27, 2000 kwa lengo la kushuhudia utiaji saini mkataba wa amani wa kumaliza mzozo nchini Burundi, haa iliyofanyika jijini Arusha ambapo msuluhishi mkuu wa mzozo huo alikuwa ni Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela. Hata hivyo katika ziara hiyo, mwenyeji wake alikuwa ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa. Pamoja na kwamba Tanzania ni nchi inayosika kwa amani na utulivu na ukarimu wa watu wake duniani kote, hilo halikuifanya Marekani kuiamini. Kabla ya kuja Clinton m a z i n g i r a y a Ta i f a yalibadilika. Makachero wa Marekani walitamalaki karibu maeneo yote nyeti ya Taifa letu. Tunakumbuka hata pale alipotua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, kabla ya kuondoka uwanjani hapo na mwenyeji wake Rais Mkapa, mbwa wa Kimarekani walikagua barabara gari la kifahari alilotumia Rais wetu, chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Marekani. Ulinzi wa serikali yetu uliwekwa kando. Mbwa aliokuja nao Clinton walinusa kila kona ya gari la Rais wetu, huku Maofisa wetu wa Usalama wa Taifa na viongozi wetu wakiwa kimya kando kushuhudia. Katika ziara hiyo, pamoja na kwamba Bw. Clinton alikuja kwa uzito wa jukumu la Burundi, lakini katika hali ya kushtusha kidogo, tulisikia kwamba Rais wetu Mkapa na Rais Clinton tayari wameshatiliana saini mkataba wa anga huru. Fursa ambayo Marekani imekuwa ikipata wakati mgumu sana kuridhiwa na mataifa mengine yanayofahamu vyema sera na tabia za ndani za Taifa hilo.
Makala/Matangazo
AN-NUUR
Lakini serikali yetu haikuona sababu ya kutafakari kwa kina juu ya hatua hiyo kabla ya kukia maamuzi. Ziara ya Clinton ilifungulia fursa zaidi za viongozi wa Marekani kuzuru nchini. Bila shaka Clinton aligundua jambo hapa kwetu na kulifikisha jikoni White House kwa ajili ya kufanyiwa kazi hata baada ya yeye kuondoka. Tukio la kulipuliwa ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam na kule Nairobi Kenya Agosti 7, 1998, kunaweza kuwa kichocheo muhimu cha White House kuitambua vyema Tanzania na kuona kuna haja ya kuwepo mikakati kabambe ya kiusalama na ya kuvumbua fursa za kiuchumi pia. Tangu kipindi hicho, ziara za vigogo wa ngazi za juu wa White House zilikolea nchini kwa nyakati tofauti, ikilinganishwa na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Yawezekana ziara za vigogo hawa zikawa nyingi zaidi nchini ikilinganishwa na nchi zile wanazofanya katika nchi nyingine za bara la Afrika. Julai 13, 2005 mke wa Rais George Walker Bush, ambaye alichukua nafasi ya Clinton, Bi. Laura Bush alitua jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili. Februari 2008 Rais George Walker Bush, akawa Rais wa pili wa Marekani kuja nchini, akiwa ameambatana na mkewe Bi. Laura, ambaye yeye alishakuwa mwenyeji kidogo kufuatia ziara yake ya awali. Hata hivyo safari hii ugeni huo wa Rais wa Marekani ulisababisha adha kubwa kwa Watanzania. Makachero walitanda Ikulu ya Dar es
GEORGE W. Bush
Serikali ilionekana kushughulishwa barabara katika kutimiza matumizi ya sheria hiyo, licha ya wengi waliopata misukosuko kutodhihirika kuhusiana na ugaidi wenyewe. Kupokelewa haraka na kwa bashasha sheria hii ilionekana kukidhi haja ya aliyeileta kiasi cha kuimarisha urafiki wa pande mbili. Miradi ya vyandarua na MCC imeonekana kuwa kivutio kikubwa cha kuimarisha uswahiba wa pande mbili. Hatupingi viongozi wa
Msikiti wa Mtambani, unawatangazia Waislamu wote Muhadhara. Utakaofanyika:- Msikiti hapo (Mtambani) Siku:- Ijumaa, Juni 7/2013 (Leo). Baada ya Swala ya Al-Ijumaa. Muhadhiri:- Ustadhi SULEIMAN FILAMBI, toka Morogoro. Imam, Masjidi Mtambani Wabillah Tawq
Inawatangazia Waislamu ibada ya ITIKAF. Mahali:- Masjidi Idrisa, Kariakoo. Siku:- Jumamosi, Juni 8/2013 Muda:- Baada ya Swalat Ishai Masheikh Mbalimbali watakuwepo, Inshaallah. Wabillah Tawiq
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Na Khalid S Mtwangi
HIVI sasa imekubalika na watu wengi kuwa kweli uhusiano kati ya Waislam na ndugu zao Wakristo sio mzuri kama inavyostahili. Wa n a o h u s i k a n a utawala wanatafuta njia ya kuinusuru nchi hii na majanga yanayoweza kutokea kutokana na hali hii isiyoridhisha. Tayari Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na viongozi wa dini kulizungumzia jambo hilo. Imependekezwa vile vile kuwa viongozi wa dini mbalimbali, hasa wale wa Kiislam na Kikristo wawe na mijadala na maongezi kuhusu jambo hili ili kutafuta njia ya kupoza yale yaliyochemka. Ni maoni ya msomi Dkt. Evarist Magoti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwamba mazungumzo kama hayo (dialogue) hayatakuwa na tija na tatizo litabaki pale pale. Soma maoni yake katika THE CITIZEN ON SUNDAY of May 26, 2013. Kuna sababu za msingi kabisa ambazo zinaweza kutolewa kuhakiki maoni hayo. Dkt. Evarist Magoti, katoa sababu za kitaalam za kisayansi ya siasa na za kisaikologia; lakini ziko pia za msingi kabisa. K w a n z a Wa i s l a m wanakumbuka, pengine zaidi ya ndugu zao Wakristo, kuwa katika mazungumzo hayo ya pamoja kumekuwa na msisitizo usiokuwa wa kawaida kuhusu mihadhara inayoitwa ya kashfa, ama pale wahadhiri wanashutumiwa kuwa wanakashifu dini za wengine. Jambo hili kwa kiasi kikubwa sana limemalizwa na mahakama kutokana na kesi ya Ustadh Rajab Dibagula, ambayo hukumu yake ilitolewa na Mahaklama ya Rufaa (ingawa hukumu ile ilikuwa ya kisiasa zaidi kuliko kutoa haki tupu). Hebu Wa i s l a m wakumbuke; hivi kweli malalamiko yao ya dhulma yanaweza kuondolewa pale ile inayoitwa mihadhara ya kashfa itapusitishwa ama itakapokoma? Bila shaka jibu
la swali hili la msingi litakuwa LA! Sasa inawezekana kabisa kuwa kumekuwa na msisitizo usiokuwa na kifani, juu ya kile kinachoitwa KASHFA kuliko lile la msingi la DHULMA wanayoipigia kelele Waislam. Ikiwa kweli kutakapokuwa hakuna ile kelele kuwa dini moja inakashifu dini nyingine, hapo ndipo tuamini patakuwa mwisho wa MFUMOKROSTO? Waislam wajiulize na watoe jibu wenyewe. Lakini muhimu zaidi ni kuwa macho, wasiwe wanadanganywa walale usingizi, ati hali sasa ni shwari wakati MFUMIOKRISTO ndio unapata nguvu zaidi. Masheikh wanaweza kuwa wanazungumza kila siku na Maaskofu kutafuta ridhaa (gani?) lakini hawa Maaskofu sio watendaji wanaotekeleza MFUMOKRISTO katika kazi na majukumu yao ya kila siku Serikalini. Kadhia ya mitihani ya somo la ISLAMIC KNOWLEDGE ni mfano mzuri sana. Uamuzi umetolewa na kuanza kutekelezwa wakati kila mtu, na hata Rais, anatia mkazo juu ya dialogue kati ya viongozi wa Kiislam na wa Kikiristo. Ni wazi kabisa kuwa kitendo hicho kilichotekelezwa na maafisa humo Wizara ya Elimu ni dhulma dhidi ya Waislam. Wamefanya hivyo wakati kuna kutoelewana kwa hali ya juu kabisa kati ya Waislam na Wakristo. Hawa watekelezaji ambao wengi wao, kama sio wote ni Wakristo, walionyesha dharau kubwa dhidi ya Waislam wa nchi hii. Baya zaidi ni kuwa hawa jamaa viongozi wa Kikristo walikuwemo katika njama za hujuma hiyo bila hata kuwatahadharisha wenzao Wa i s l a m . I n g a w a h i l o lisingetegemewa kutokea, Wakristo wasingeweza ama wasingetaka kuwajulisha Waislam hata kidogo. Basi kuna haja gani kuwa na hiyo inayoitwa dialogue? Ikubalike kuwa hivi sasa kuna vita vya maneno kati ya Waislam na Wakristo nchini humu. Inawezekana kabisa, kama baadhi ya watu wanavyodai, kuwa vita hivi vinachochewa na watu kutoka nje na wale wasioitakia mema Tanzania. Ati Waislam na wananchi wenzao Wakristo
Franklin Delano Roosevelt, aliwatoa kafara askari wake na Wananchi wengine ili kupata kile alichokitaka. Nalo ni kutaka kujitosa vitani. Wa s o m a j i w a j a r i b u kukumbuka wataona kuwa kuna mikasa mingi imetokea humu Tanzania, ambayo haielezeki imetokea wapi na wala kwa nini imetokea. Lawama kubwa wametwikwa Waislam ingawa mpaka leo hii, Jeshi la Polisi Tanzania halijaweza kuwafikisha mahakamani watu hao waliochoma makanisa, kwa mfano. Hali kadhalika misikiti ilichomwa huko Tunduma mpaka leo imekuwa kimya bila taarifa yeyote kutoka kwa vyombo vya usalama. Waislam tuwe macho, tutumie akili ya asili kuchanganua mambo. Vita kubwa iliyoko mbele yenu ni kuondoa dhulma iliyoshamiri nchini kutokana na ule ambao sasa unajulikana wazi kama MFUMOKRISTO. Mihadhara sio jambo zito hata kidogo kwa vile Uislam umakuwa ukikashwa katika vijitabu vinavyozagazwa na Makanisa kwa muda mrefu sana. Hapajatokea rabsha kuhusu hilo. Lengo liwe ni kutafuta jinsi gani Waislam wanaweza kuushinda huu MFUMOKRISTO, ili Wananchi wote wa nchi hii wawe na haki sawa na waishi kwa amani kama ilivyokawaida.
Almadrasat Munawara Shaziliya ya Jibondo Maa, inakabiliwa na tatizo kubwa la vitabu hususan Misahafu, Juzuu na kitabu cha kufundishia cha Fath-lbaarii Sharhe Ibukharii. Tunaomba msaada wenu. Kwa mawasiliano tumia: 0715 059250, 0784 059250 Wabilah Tawq
Msaada wa vitabu
Makala/Tangazo
AN-NUUR
gani kwa Waislamu kulaani matukio hayo bila kikomo? Matatizo kadhaa yanakuja kichwani. Kwanza, kwa viongozi wa Waislamu kulaani matukio hayo jumla jumla bila ya uangalifu, inahamisha mzigo wa lawama kutoka kwa mshambuliaji halisi na sababu zilizomsukuma afanye hivyo. Yaani inapoteza maboya! Pili, kulaani sana kifo cha mtu mmoja kwa kiasi kikubwa, inapunguza thamani ya maisha ya maelfu ya watu waliouawa katika matukio mengine mabaya kama hayo, ambao mauaji yao hayapewi umuhimu mkubwa na wala hakuna anayelaani. Ta t u , i w a p o t a t i z o linaonekana lipo kwa jamii ya Waislamu, sera za kupambana na tatizo hilo zitalenga jamii nzima ya Waislamu. Kwanini Muislamu asiyehusika na uhalifu aadhibiwe kw a kosa ambalo hakufanya? Tunahitaji kuwa makini sana na baadhi ya vyombo vya habari vinapoendesha mijadala kuhusu matukio haya. Ukichunguza kwa makini, utaona ni mbinu tu ya kuwatuhumu Waislamu, japo hawasemi moja kwa moja. Jamii ya Waislamu ndiyo imekuwa begi la mazoezi ya masumbwi kwa wanasiasa na watendaji wa Serikali wanaolinda Mfumo Kristo. Vyombo hivi vimekuwa kimya kabisa kuzungumzia hatari za Mfumo Kristo kwa mustakabali wa taifa, lakini viko tayari kuwakaanga Wa i s l a m u y a n a p o t o k e a mauaji ya padri, makanisa kuchomwa moto au shambulio la bomu kanisani, kabla hata uchunguzi kufanyika! Badala ya kuwafichua wale walioasisi Mfumo Kristo hapa nchini, ambao unatishia kulisambaratisha taifa, wenyewe wanaendesha kampeni za kuwadhalilisha Wa i s l a m u w a n a o k e m e a mfumo huo. Baadhi yetu wamepoteza kujiamini na wamekubali kutumikia mfumo huo kama majaaliwa yao. Kuna funzo kubwa sana kwetu Waislamu jinsi ya kulaani matukio haya yanayoitwa ya kigaidi wakati yanapotokea. Tuache jazba na kufuata mkumbo wa kulaani. Kuna matokeo mabaya yasiyoonekana katika kulaani kwetu, iwapo hatutakuwa waangalifu.
10
Tangazo
AN-NUUR
Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. Kwa wale ambao walisharudisha fomu wanatakiwa wawasilishe result slips za matokeo mapya mapema kwenye osi waliporejesha fomu hizo ili yaunganishwe na fomu zao. Waombaji wapya wenye sifa wanashauriwa kuendelea kuchukua fomu. Waliokwisha omba wataleta result slip ya matokeo ya pili wakati wa kuripoti shuleni. Tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu ni tarehe 23/06/2013. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
Arusha Kilimanjaro Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627
Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Dar es SalaamMorogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -
6. Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha.
11
Na Mwandishi Wetu ILE Mahakama ya Kadhi iliyokuwa ikililiwa na Waislamu nchini, wakitaka irejeshwe na kutambuliwa rasmi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haipo katika rasimu ya mapendekezo ya katiba mpya. Hayo yamebainika katika haa ya uzinduzi wa Mapendekezo ya Rasimu ya Katiba Mpya uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alisema Tume imependekeza kutoingizwa mahakama hiyo ndani ya katiba baada kuchambua na kutizama kwa kina utendaji wa Mahakama ya Kadhi ya Zanzibar, ambayo alidai imekuwa ikifanya kazi zake bila kuingizwa katika katiba ya Zanzibar. Aliongeza kuwa Waislamu watakuwa huru na haki ya kuanzisha na kuendesha Mahakama yao ya Kadhi hata bila ya mahakama hiyo kutambuliwa na Katiba ya nchi. Kwa muda mrefu Waislamu nchini wamekuwa wakiitaka serikali kurejesha mahakama ya Kadhi nchini, ili kutenda haki katika masuala ya kiibada, ambayo yamekuwa yakipindishwa katika mahakama za kawaida pale yanapotokea matatizo. Aidha walitaka mahakama hiyo ambayo itashughulika na mambo ya madai katika Uislamu, itambuliwe na katiba ili hata pale hukumu itakapotolewa na mahakama hiyo kwa misingi ya Shariah, basi yasiweze kupuuzwa na kutupwa na mahakama ya kawaida kwa kutotambuliwa kwake na katiba. Pia igharimiwe na serikali kwa kuwa Waislamu ni sehemu ya jamii ya watanzania na walipa kodi kama wananchi wengine. Masuala yaliyokuwa yashughulikiwe na Mahakama hiyo kuwa ni pamoja na Ndoa na Talaka, Mirathi, Wasia, Hiba, zawadi, tunu, wakfu, malezi ya watoto na usuluhishi wa migogoro ya Kiislamu. Serikali ya Tanzania mwaka jana ilikubaliana na Waislamu juu ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliunda Kamati maalum kati ya Taasisi za Kiislamu na
Makala/Tangazo
AN-NUUR
BI Aisha Sururu (katikati) akiongea katika kongamano la Waislamu lililofanyika Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita.
Mahakama ya Kadhi na Sharia chini ya Dini ya Kiislamu. Alinukuliwa akisema Mh. Pinda. Aliongeza kuwa katika kikao cha mwisho cha Kamati Kuu inayosimamia suala hilo, iliamuliwa na pande zote kuwa baadhi ya wajumbe kutoka upande Waislamu na Serikali wakafanye ziara ya mafunzo katika nchi za India, Uingereza, Kenya na baadaye Zanzibar ili wakajifunze namna ya kuratibu na
Masjid Aswabirina
Kitunda kibeberu Dar es salaam. Uongozi wa Masjid Aswabirina Tunapenda kutoa shukran zetu za Dhati kwa Waislamu wote waliofanikisha Msikiti huu kukia hapa ulipo. Hivyo basi tunatarajia kufanya ufunguzi wa msikiti huo tarehe 28 Shaaban ili uanze kutumika Rasmi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ili kufanya ufunguzi huo tunaomba msaada wenu wa kujengewa choo, Kisima cha maji pamoja na ununuzi wa Uwanja uliopo mbele ya Msikiti gharama ya uwanja huo ni Milioni Tisa ( 9) kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa shule ya awali na chuo. Pia Tunaendelea kuwaomba wahisani waendele kutusaidia ili kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huu. Tuma Mchango wako Account Na: K.C.B 3300386233 jina la A/c Aswabirina au kwa Tigo Pesa 0714 565619 au Mpesa 0753 673820 Amir Khatibu Yunus
12
AN-NUUR
MAKALA
12
BABA Askofu Nestory Timanywa Jimbo Katoliki La Bukoba, ambaye amestaafu hivi karibuni mmoja wa washiriki uzinduzi somo Dini na Maadili. Balaza la Maaskofu Tanzania (TEC), Balaza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT). Imesema taarifa ya mtandao wa TBC. Kuzinduliwa kwa somo hili maana yake ni kuwa mwanafunzi Muislamu badala ya kufundishwa somo la Dini na Mwalimu Muislamu aliye na Elimu ya Dini ya Kiislamu, sasa anaweza kufundishwa na Mkatoliki, Sabato au hata Yahudi. K a m a inavyokumbukwa harakati za kuvunja taasisi ya Waislamu ya EAMWS n a b a a d a e k u u n d wa kwa Bakwata, ilianzia Bukoba na walitumika vijana na Masheikh wa Bukoba ambao baadhi yao walikuja kuwa viongozi wa Bakwata Makao Makuu kwa muda mrefu. Suala hili na Dini Mseto kuibukia tena Bukoba chini ya UMAKA, limewafanya Waislamu wengi kuhoji, Bukoba kunani? Baadhi ya Masheikh kutoka Zanzibar waliohojiwa wanasema kuwa Dua yao ni balaa hili lisiwakute kwa maana kuwa kama ingewezekana Zanzibar huru yenye mamlaka yake ije kabla ya somo la Dini Mseto k u a n z a k u s o m e s h wa skulini. Wanasema, pamoja na yote, lakini wanaamini kuwa hakuna kiongozi wa Zanzibar atakayekubali kuona mtoto wa Kizanzibari akisomeshwa Dini mseto. Habari zaidi zinasema kuwa kwa Dini Mseto kufanywa somo la lazima na lenye kutahiniwa, huenda kwa muda yale ya Maarifa ya Kiislamu yakafanywa kuwa somo la hiyari na yasiyotahiniwa na Serikali kabla ya kupigwa marufuku kabisa.
MKUU WA SHULE YA MATANGINI ISLAMIC HIGH SCHOOL ILIYOPO DAR-ES SALAAM ANAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO YA KIDATO CHA TANO KATIKA MICHEPUO YA HKL, HGK, HGA, HKA NA KLA. NAFASI KWA WANAOHAMIA NURSERY, PRIMARY NA SECONDARY ZIPO. FOMU ZINAPATIKANA: TANGA: MUONE MKUU WA SHULE YA MAAWA SECONDARY SCHOOL. KIGOMA: MUONE MKUU WA SHULE YA JIHADI SECONDARY SCHOOL. MOROGORO: MUSLIM UNIVERSITY MOUNE USTADH FILAMBI. DAR-ES SAALAM: KWA MKUU WA SHULE YA MATANGINI ISLAMIC HIGH SCHOOL NA MSIKITI WA KIBO MUONE USTADH YAHYA. SHULE NI YA BWENI NA KUTWA, KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIM 0719089737, 0712305928 AU 0715381405. MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MAADILI YA DINI(TUPO KIMARA MWISHO-DAR-ES SALLAM) MASOMO YATAANZA TAREHE 01/07/2013 (Wahi nafasi ni chache) NB:WANAFUNZI WOTE WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA WAMEFAULU KUINGIA CHUO KIKUU.(2013) KARIBU SANA
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.