Professional Documents
Culture Documents
Annuur 1033
Annuur 1033
ISSN 0856 - 3861 Na. 1033 SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPTEMBA 7-13, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa. Kwa mawasiliano: +255 22 2181577, +25 22 2182370, 0717 000065, 0786383820, 0754 261910 E-mail: tmht@live.com, info@hajjtrusttz. org Website: wwwhajjtrusttz.org
Ndio wale wale waliouwa Mwembechai! Mkawapongeza 2001 walipouwa watu 27 Mngepiga kelele kama hizi za Daudi labda
Ni kupinga kamatakamata ya sensa Mbunge Kilwa naye atiwa nguvuni Viongozi wa Jumuiya waitwa wizarani
Adhana yakusanya Waislamu Polisi Baada ya Swala, Dua, mmoja asilimu Gari Polisi yagoma kubeba watuhumiwa Mwanza: DC, Masheikh waviziwa Butimba
2
AN-NUUR
Tahariri/Tangazo
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
AN-NUUR
MAONI YETU
kwa nguvu mikutano hii au maandamano. Bila wao, ni nadra sana kutokea vurugu. Kwa jinsi hali ilivyo, hatudhani kwamba raia waliokuwepo katika mkutano huo walibeba silaha za moto kama bunduki na mabomu ambazo kwazo zingeweza kumdhuru Mwangosi. Silaha za ina hiyo walikuwa nazo polisi. Wa l a h a t u d h a n i kwamba ni jiwe, mkuki, pinde, panga au kisu, kilichotumika kuondoa uhai wa Mwangosi. Maana hizi ndizo silaha ambazo raia anaweza kuwa nazo au kuzimiliki na kuzibeba bila hofu. Tunajiuliza, Mwangosi kauliwa na bomu kutoka kwa nani kama si mmoja katika polisi miongoni mwa waliokuwa wakitawanya watu? Ni katika mantiki hii, ndio maana polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwandishi huyo ambaye alikuwa kazini kuhakikisha kwamba umma unapata habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo wa CHADEMA. Tu k i r e j e a n y u m a , mwaka 1998 polisi walidaiwa kuua watu wawili na kusababisha vilema kwa baadhi ya raia akiwemo Chuki Athumani, ambaye sasa ni mlemavu baada ya kupewa ulemavu kwa risasi za polisi alipokuwa mtoto mdogo kabisa. Pamoja na polisi kuua tena hadharani, serikali ilipiga kimya
na zaidi iliwapongeza polisi waliofanya mauwaji yale. Waislamu wakataka iundwe tume huru ya kuchunguza mauaji katika tukio lile la Mwembechai, lakini hakuna aliyewasikiliza na kuishia kupuuzwa. Aidha tunakumbuka pia mauaji yaliyofanywa na Polisi Zanzibar Januari 26 na 27 mwaka 2001. Hiki kilikuwa kipindi cha uongozi wa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa. Makumi kwa makumi ya raia wa Zanzibar waliuliwa. Kama ilivyo ada, wauaji walipongezwa kwa kazi nzuri na watawala na kupandishwa vyeo, na hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi ya wauaji. Katika awamu ya kwanza ya Rais Jakaya Kikwete, polisi waliua wafanyabiashara ya madini kutoka Morogoro jijini Dar es Salaam na kupora fedha zao. Tume ikaundwa na Rais Kikwete kuchunguza Tukio hilo. Majibu ya tume yalionyesha kuwa kuna kesi ya kujibu kwa polisi wakiongizwa na Kamishna wao wa Upelele ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe. Lakini kwa kuwa mpelelezi, mwendesha mashitaka, ndiye huyo huyo mshitakiwa, ushahidi wa uhakika haukuwasilishwa mahakamani na watuhumiwa wa mauaji wakashinda kesi. Leo wote wapo nje na wanaendela na maisha huku marehemu wakikosa haki. Siku za nyuma huko Arusha, matukio ya polisi kuua raia yalishawahi kuripotiwa na vyombo vya habari. Lakini kwa mazoea haya ya polisi wetu kuua bila kukishwa mahakamani, hatudhani kwamba kuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa kwa wauaji hao. Hii ni mifano kiduchu tu ya polisi
kuhusishwa na mauaji lakini wauaji wakiachwa bila kuchukuliwa hatua stahiki. Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba limekuwa ni jambo la kawaida au hulka kwa askari polisi kuua na kuachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria hapa nchini. Upolisi umekuwa kazi inayoweza kumkinga muuaji dhidi ya sheria. Ndio maana kuua kwao si taabu wala si jambo la kuogofya. Ni suala la kuamua tu na kuweka mazingira ya kupoteza ushahidi. Na mara nyingi wanapotuhumiwa kuua, hutoa visingizio kama vile marehemu alikuwa jambazi, askari walikuwa wakijihami, aliyeuliwa alikuwa na silaha ya moto akiwashambulia askari nk. na mwishowe kesi huishia hapo hapo polisi. Kwa staili hii ndio maana wanaendelea kuua raia pale wakijisikia kufanya hivyo na wana uhakika
wa usalama wao mbele ya sheria. Tunaambiwa kuwa tayari Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Emmanuel Nchimbi ameshateua Tume ya uchunguzi wa mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi. Lakini kutokana na utamaduni wa watumishi hawa, hatudhani kama wauaji wa mwandishi Mwangosi watachukuliwa hatua stahiki japo wapo kazini. Wasiwasi wetu ni kwamba hata wakipatikana, yanaweza kuwa kama yale ya Afande Zombe. Ni kwa sababu hiyo, tunadhani ingekuwa vyema Tume iliyoundwa ikajaribu kuwa makini, ikazingatia ukweli wa mambo, ikajali haki na kuweka mbele masilahi ya taifa hili kuliko kuangalia mazoeya ya huko nyuma. Amani ya nchi hii haitadumishwa kwa kuwaficha au kuwafumbia macho wauwaji.
UBUNGO55105, Tel: 2450069, 0754 260241 ISLAMIC HIGH SCHOOL P.O. Box
Fax: 2450822 Dar es Salaam E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com
Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu. Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana. Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni: 1. Elimu ya Dini ya Kiislamu 2. English Language 3. Arabic Language 4. Mathematics 6. Introduction to Computer Ni programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012) Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu. Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107 MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU Wabillah Tawfiiq MKUU WA SHULE
3
Na Mwandishi Wetu
n a Wa k r i s t o w e n z a o , Waislamu wao wanapoingia serikalini hutupa Uislamu wao na kama ni kufanya dini hufanya kama jambo la dharura. Kufuatia makombora hayo, ilimbidi Waziri Mheshimiwa Mwinyi kila mara kukatisha wazungumzaji kufafanua mambo aliyodhani kuwa yanapotoshwa. Awali, katika kikao hicho kilichofanyika Agosti 24, Waziri aliwaambia Masheikh hao wa Uamsho kuwa alikuwa amewaita ili washauriane juu ya namna ya kufanikisha sensa. Katika kile walichosema kuwa sensa hiyo haitakuwa na manufaa kwa Wazanzibari walisema kuwa, ilivyo hivi sasa kuna watu sio Wazanzibari waliowaita wa kutoka Msumbiji, lakini wana vipande vya ukaazi wakati Wazanzibari wenyewe halisi hawapewi. Wakasema, Zanzibar hakuna mamlaka ya kudhibiti wanaoingia na wanaotoka, kwa hiyo hata ikifanyika sensa kupanga mambo kwa mujibu wa idadi ya watu itakayopatikana, inakuwa sawa na kutia maji katika pakacha badala ya ndoo. Wa k a s e m a h u w e z i kuweka harusi ya kuingia kwa kadi wakati mahali inapofanyika hakuna madirisha, milango wala watu wa kudhibiti waingiaji. Wakadai kuwa hivyo ndivyo ilivyo Zanzibar kwa sasa. Kwa hiyo ili sensa iweze kuwa na maana, basi Zanzibar yenye mamlaka na dola kamili ipatikane kwanza. Pamoja na jitihada za Mufti wa Zanzibar ambaye naye alikuwa katika kikao hicho kujaribu kuwarai masheikh hao, lakini mpaka mwisho wa kikao msimamo wa Masheikh wa Uamsho ulibaki kuwa ule walioingia nao Ikulu. Wakati huo huo, hali si shwari Pemba na jana Polisi walikuwa katika heka heka kuwakusanya watu katika kituo cha Polisi Wete na kuwarai kuandikishwa. Habari zilizotukia jana zinafahamisha kuwa watu takriban 200 waliitwa katika kituo cha Polisi kwa barua ya OCD. Hata walipofika waliambiwa kuwa ilikuwa waonane na Waziri wa
Habari
AN-NUUR
RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na Makamu kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad. Sheria na Mambo ya Katiba. Hata hivyo, hakutokea Waziri huyo na badala yake walioongea ni Polisi na baadhi ya maosa wa serikali wa Wilaya. Katika kikao hicho, takbira zilikuwa zikivuma mara kwa mara wakati waliohudhuria wakitoa hoja za kuonyesha mantiki ya msimamo wao wa kususia sensa. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinafahamisha kuwa ilibidi OCD, SSP Juma S Khamisi, pamoja na kuwa ni Muislamu kusimama na kutaka Takbira hizo ziachwe akidai kuwa zinakera, kauli ambayo ilileta mtafaruku watu wakitaka kutoka na kususia kilao hicho. Kwa upande mwingine, polisi wamekuwa wakitumia mtutu wa bunduki kuhakikisha kuwa sensa inafanikiwa kama ilivyopangwa. Katika tukio moja huko Pemba, Sheikh na Imam mmoja, Sheikh Omar Swaleh alijikuta akinaswa kibao na kutiwa pingu kabla ya mkewe naye kuelekezewa mtutu wa bunduki akitakiwa kutoa taarifa zilizotakiwa na karani wa sensa. Akisimulia tukio hilo, Sheikh Swaleh amesema kuwa akiwa kazini kwake Jumamosi iliyopita Septemba 1, alipigiwa simu na mtu asiyemjua akimwambia kuwa mke wake ameanguka na hali yake mbaya. Anasema, alikimbilia nyumbani lakini alipoka alikuta kikosi cha polisi kikiongozwa na OCD wa Wete ambaye alimwambia kuwa ndiye aliyempigia simu. Baada ya kukataa kuhesabiwa kibabe anasema kuwa alipigwa kibao na OCD huyo na kisha kuwekwa pingu. Akisimulia zaidi Sheikh Swaleh anasema kuwa baada ya kumtia pingu walimfuata mkewe na kumwelekezea mtutu wa bunduki wakimtisha kuwa kama hatatoa taarifa naye watamtia pingu na kumpeleka rumande. Katika hali hiyo, ilibidi mkewe atoe taarifa zilizohitajika na kisha kuachiwa. Mumewe naye aliachiwa pia baada ya kuhesabiwa kupitia maelezo yaliyotolewa na mkewe. Matukio kama hayo yameelezwa kutokea sehemu mbalimbali Unguja na Pemba baada ya watu wengi kukataa kuhesabiwa wakisema kuwa wanafuata maelekezo ya viongozi wao. Ni kutokana na hali hiyo, awali kabla ya zoezi la sensa kuanza hapo Agosti 24, Masheikh wa Uamsho waliitwa Ikulu ambapo walikutana na Waziri katika Osi ya Rais, Mheshimiwa Mwinyi Haji Makame. Uzanzibari kwanza sensa baadae; mwenye sensa hii ndiye anayetuibia. Wenzenu (Bara viongozi wa serikali Wa k r i s t o ) w a n a f a n y a kazi na Ukristo wao, nyie Uislamu wenu mnautupa mkiingia serikalini (vipi?), wanadaiwa kusema Masheikh hao wakimkabili Waziri Makame. Ilikuwa baada ya Masheikh wa Uamsho kukataa tenda ya kuhamasisha Waislamu kushiriki sensa, Polisi walimjia Sheikh Abdallah Madawa usiku wa saa 6 wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi. Hali hiyo ilipelekea m a m i a y a Wa i s l a m u kufurika Madema kutaka kujua nini hatma ya Sheikh wao. Haikupita muda Sheikh Abdallah akaachiwa lakini Polisi wakahamishia vipigo na vitisho kwa wananchi wa Mashamba, hasa Nungwi ambapo inadaiwa kuwa watu wengi walikuwa wamekataa kushesabiwa.
4
Na Waandishi Wetu, Mwanza, Rukwa, Tanga
WA K AT I muda ulioongezwa wa sensa ya watu na makazi ukimalizika, matuki yasiyo ya kawaida yameendelea kuripotiwa yakitawaliwa na msuguano kati ya vyombo vya dola na Waislamu waliogoma kuhesabiwa. Kutoka Sumbawanga inaripotiwa kuwa mtu mmoja amesilimu nje ya kituo cha Polisi Sumbawanga mjini baada ya kushuhudia Waislamu wakiswali na kuleta Dua ndefu. Dua hiyo ilifuatia Swala ya Alasiri iliyoswaliwa nje ya kituo hicho cha Polisi wakati mamia ya Waislamu wakisubiri kujua hatma y a Wa i s l a m u w e n z a o waliokuwa wamefikishwa kituoni hapo baada ya kukamatwa kutoka vijiji vya Muze, Laela na Kirando, Sumbawanga Vijijini. Awali kabla ya tukio hilo ilikuwa imetolewa taarifa katika swala ya Ijumaa iliyopita kuwa kulikuwa na Waislamu waliokamatwa katika maeneo mbalimbali ya Sumbawanga vijijini. Taarifa hiyo ilitolewa katika misikiti ya Qiblatain, Salaam, Rahmaan, Rawdha, Jadidah, Tawba, Taqwa na Ibaadhi, ambapo waumini walitakiwa kuwa tayari tayari wakisikia Adhana isiyo na haiya ala swalaa watoke kwa wingi kwenda kuwanusuru Waislamu wenzao walio kuwa wamekamatwa tangu jana yake. Wa k a t i Wa i s l a m u wakitawanyika, Maimamu walikaa Shura na ndio katika kikao chao zikaja habari kuwa Waislamu waliokamatwa tayari wamekishwa kituoni. Kwa mara ya kwanza katika historia ya mji wa Sumbawanga ilisikika adhana tofauti na ya kawaida ya siku zote huku Muadhini akisema Hayyaalal jihad Hayyaalal Jihaad. Katika muda usiozidi d a k i k a 1 5 , Wa i s l a m u wakawa wamefurika katika Msikiti wa Qiblatain ambao ndio Msikiti Mkuu wa Ijumaa huku wengine wakikusanyika na Masjid Taqwa na kwa pamoja
wakaelekea kituo cha polisi. Wakiwa katika barabara kuu iendayo mbeya, Waislamu hawa walitembea kwa nidhamu wakiwa wawili wawili. Ilikuwa baada ya kuona umati huo wa Waislamu, harakati za kuwapatia dhamana waliokamatwa ziliharakishwa. Hata hivyo, muda wa swala ulifika kabla ya zoezi kukamilika ndio ikapigwa Adhana Waislamu wakasimama safu kuswali na kisha kuleta Dua iliyowaliza Waislamu wengi. Kitendo hicho kiliwaacha na mshangao watu waliokuwepo eneo hilo ambapo mtu mmoja alipoona Waislamu wakiswali nje ya kituo cha polisi tena katika vumbi na mchanga aliuliza kuna nini na kufahamishwa k u w a h a w a Wa i s l a m u wamewafuata wenzao waliokamatwa na polisi kwa ajili ya kugoma kuhesabiwa sensa, sasa muda wa sala yao umeka wanaswali. Mtu yule baadae alisilimu na kufuatana na Waislamu wenzake kwa shangwe baada ya kuachiwa Waislamu kurejea msikitini. Tukio hilo lilifanya mji kuzizima kwa shangwe, maandamano na kivumo cha Hakuna Sensa! Hakuna Sensa!!!!, hususan katika barabara ya Mbeya-Mpanda na maeneo ya soko kuu la Manispaa. W a l i o k u w a wamekamatwa na kuwa sababu ya tukio hili la kihistoria Sumbawanga ni Abdalla Masoud alokamatwa Laela, Zuena Juma na Hassan Said wa Kirando, na Omary Ally, Ashura Kasonso, Haji Kiyoso, Amru Sinah na Hassan Mohamed, wote wakazi wa Muze, Sumbawanga Vijijini. Mwanza Wa k a t i h u o h u o , habari kutoka Mwanza zinafahamisha kuwa zoezi la sensa limefanikiwa kwa kiwango kikubwa baada ya muda kuongezwa na serikali kupiga propaganda kubwa. Hata hivyo inakisiwa kuwa bado wamebaki Waislamu, si haba ambao hawakuhesabiwa mpaka
Habari
AN-NUUR
Uhuru. Taarifa zinafahamisha kuwa baada ya Waislamu kupata taarifa kwamba Masheikh hao walishiriki katika msafara wa DC kwenda kuhamasisha sensa kwa mahabusu, hali yao si shwari mitaani. Kwa upande wa Sheikh Mahuba, waumini walipomwendea na kumkosa walimwendea anayedaiwa kuwa mfadhili (jina tunalo) wake ambaye walimwambia amwonye Sheikh huyo na kumwachia ujumbe mzito wa maneno na maandishi. Uchunguzi wa kina wa mwandishi wa habari hizi, unaonyesha kuwa kabla ya kuongezwa siku za sensa, idadi kubwa ya Waislamu walikuwa hawajahesabiwa. Hata hivyo kufuatia vitisho na propaganda iliyopigwa baada ya kuongezwa siku, idadi kubwa ya waliogoma wamehesabiwa kwa vitisho. Hata hivyo, bado inaaminika kuwa kuna wengi hawajahesabiwa.
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
NAIROBI KAMISHENI ya Uchaguzi ya Somalia imetangaza kuwa anayetaka kugombea Urais wa nchi hiyo na kuunda serikali
wanaokubalika pamoja mamlaka za usimamizi za Taifa. Mfumo huu ambao umeanzishwa miaka mingi iliyopita katika nchi za Ulaya, wataalam wana matumaini kwamba utaratibu huu mpya wa kibenki wa Kiislamu nchini Ujerumani, utakuwa na mafanikio zaidi kuliko yale yaliyopatikana katika nchi za Uingereza na Ufaransa. Nukta muhimu itakuwa kama Benki za Kiislamu zitatoa huduma nzuri na inayovutia, amesema El-Mogaddedi kutoka Institute for Islamic Banking and Finance. Ikiwa imekaidi kwa miaka mingi kujaribu mfumo huu unaokua kwa kasi, Taasisi ya mfumo wa kiuwekezaji wa Kiislamu iliundwa nchini Ujerumani Mei 2012 na kampuni moja kutoka Malaysia ya CIMB Principal. Fedha ziliidhinishwa na German Financial Supervisory Authority (BaFin). Bidhaa za kifedha kwa mfumo was Kiislamu zimekuwa haraka zaidi kwa mara ya kwanza baada ya mashambulio ya 9/11 nchini Marekani.
kuungwa mkono na wabunge wasiopungua 20. Rais wa sasa wa Somalia Sheikh Sharif Ahmad na spika wa zamani wa bunge Muhamamd Ali Gaas ni miongoni mwa watu wanaowania kiti cha Rais. Uchaguzi wa rais wa Somalia umepangwa kufanyika tarehe 10 mwezi huu wa Septemba. Uchaguzi huo utahitimisha kipindi cha miaka 8 ya serikali ya mpito. Serikali ya kwanza ya mpito ilichukuwa madaraka nchini Somalia mwaka 2004 na haikuweza kutatua matatizo na mapigano ya ndani kutokana na uongozi duni na usiofaa. Katika kipindi chote cha miaka 8 iliyopita Somalia imekuwa katika ghasia na machafuko ya mara kwa mara. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa nchi za Magharibi hususan Marekani hazikuwasaidia wananchi wa Somalia katika kipindi chote cha mapigano ya ndani licha ya kutoa ahadi chungu nzima zaidi ya kuhusika kwa njia moja au nyingine katika kuchochea machafuko hayo. Kwa upande mwingine, Jumuiya ya nchi za Kiarabu imetangaza kuunga mkono serikali ya Somalia kwa ajili ya kuvuka kipindi cha mpito. Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Nabiil al Arabi, amewataka maasa wa serikali ya Somalia kuchukua hatua zaidi za kutimiza mwenendo wa kipindi cha mpito nchini humo.
6
Na Shaban Rajab.
WAISLAMU kutoka misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wanatarajiwa kujitokeza barabarani kuandamana hadi Wizara ya Mambo ya Ndani kupinga vitendo vilivyokithiri hivi sasa vinavyofanywa na vyombo vya dola na watendaji vya kukamatwa, kudhalilishwa na kuwekwa ndani Waislamu wanaokataa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayokia tamati leo. Taarifa kutoka Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini zimeeleza kuwa tayari uongozi wa Jumuia umeshapeleka barua Wizara ya Mambo ya Ndani kumjulisha kuhusu kuyapokea maandamano hayo na ujumbe utakaotolewa na Waislamu.
Habari
AN-NUUR
wamekamtwa. Alifahamisha Sheikh Ponda. Amesema kuwa kabla ya kukamatwa viongozi hao, awali walikamatwa Waislamu waliogoma kuandikishwa akiwemo mke wa Sheikh wa Kilwa Kivinje Ahmad Juma Slim aitwaye Kulthumu Abrahaman. Kufuatia kukamatwa kwa mkewe, Sheikh Slim ndipo alipokwenda kituo cha polisi kumwekea dhamana mkewe naye akaswekwa ndani. Baadae taarifa za kamatakamata zikam fikia Mbunge wa Kilwa Kusini Bw. Suleiman Bungara, ambaye alikwenda kituoni kutafuta suluhu na kuwawekea dhamana waliokamatwa akiwemo Sheikh
ya Zanzibar ya mwaka 1964. Chama cha CUF kimemteua Bw. Issa Khamis Issa kusima katika Uchaguzi huo Mdogo wa Jimbo la Bububu, kuwa Mgombea wake. Mbali ya CCM na CUF, vyama vingine vilivyoweka Wagombea katika uchaguzi huo ni pamoja na TADEA, ADC, na NCCR-Mageuzi, ambapo vyama vingine kikiwamo CHADEMA, walitangaza kususuia Uchaguzi huo. Aidha, CUF wamewaomba wananchi wa Jimbo la Bububu kumchagua Mgombea Mwakilishi kutoka Chama hicho ili aongeze idadi ya kushughulikia kero za Muungano ili kupata Muungano ulio imara Kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hayo yalielezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar Ismail Jussa Ladhu wakati wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kiti cha baraza wakilishi ulifanyika katika viwanja vya Skuli ya Bububu. Ladhu alisema ni vyema wananchi wa Bububu kumchagua Issa Khamis Issa kwani yeye ndie pekee mwenye nia ya kukubali mabadiliko ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Zanzibar ina matatizo mengi lakini kama mutatuongezea Issa basi mutafanya kazi yetu kuwa rahisi sana ya kuipatia maendeleo yaliyo boraq katika watu wa visiwa hivi alisema Ladhu. Ismail Jussa Ladhu yeye na wenzake ndio wanaongoza katika Baraza la Wawakilishi katika kupigania haki za Zanzibar ndani ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania . Ladhu alifahamisha, hivi sasa Tanzania imo katika hatua ya kukusanya na kuratibu maoni kwa ajili ya Katiba mpya na kusema ni vyema kwa Wazanzibari kutoa maoni ambayo yataleta Zanzibar kuwa na mamlaka yake na Tanganyika pia, halafu uandaliwe Muungano wa Mkataba (shirikisho). Sisi hatutomnyanganya mtu kadi kwamba hakufuata sera za chama lakini wananchi wa Zanzibar ni vyema kutoa maoni ambayo yataleta Muungano wa mkataba baina ya Tanganyika na Zanzibar. Akimkaribisha Mgombea, Mkurugenzi wa Haki za binaadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Bw. Salim Bimani, aliwambia umati huo uliofurika katika viwanja vya Bububu Skuli kwamba watawaunga mkono wale wote ambao wanapigania uhuru wa Zanzibar. Tunaelewa ni wengi sasa walioguswa maslahi ya Zanzibar na wenye uchungu na hivyo hakika yetu tutawaunga mkono wale wote ambao wanaitakia mema Zanzibar kwa kuwa na mamlaka yake alisema Machano. Aliwaambia wananchi hao kuwa Zanzibar imo katika vita vikubwa vya kutafuta uhuru kamili kwani Muungano umekuwa na dhulma kubwa dhidi ya Zanzibar lakini kupitia Tume ya Kuratibu Maoni Juu ya Marekebisho ya Katiba mpya ndio njia pekee ya kupata haki hizo. Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Mawaziri wote wa SMZ kutoka Chama cha Wananchi, CUF ulikuwa kivutio kikubwa kwa umma uliofurika ambapo ulipambwa na Matarumbeta, Rusha roho, na ngoma za jadi.
Na Haji Mtumwa, Zanzibar JUMUIYA ya Vijana, Elimu na Maadili Zanzibar (ZAYEM) imesema inakusukusudia kufanya kila aina ya jitihada ili kuhakikisha utamaduni wa Zanzibar unaimarika zaidi haraka iwezekanavyo. Hali ambayo kwa kiasi kikubwa itaweza kuifanya Zanzibar kudumu katika sifa yake ya amani na upendo kwa wageni na wenyeji, ambayo inajivunia kwa kipindi kirefu. Kauli hiyo imetolewa na Amiri wa Jumuiya hiyo Masoud Saleh Issa wakati akizungumza na gazeti hili mara baada ya kukamilika kwa kikao cha kamati tendaji cha Jumuiya hiyo kilichofanyika huko Asini kwake Magomeni Mkoa wa Mjini Unguja. Alisema kuwa katika makusudio hayo jumuiya yao imejipanga zaidi kutoa elimu katika Shule mbali mbali za Unguja na Pemba zikiwamo za Mjini na vijijini. Amiri huyo alifahamisha kuwa shule hizo zitakuwa zile za Serikali na binafsi hatua ambayo wanategemea kupata asilimia Inaendelea Uk. 7
na Adamu anatokana na udongo mbora wenu ni yule amchao Mwenyezi Mungu sana, hakuna mwarabu wala asiye mwarabu utukufu isipokuwa uchamungu tuu kwa ahakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na anahabari Surat Hujurat aya 13 Kwa hakika uislam umeweka msimamo na mwongozo kwa ajili ya kuungwa watu wote Kati ya watu wote ; huko ndiko kuunga undugu. Baina ya muslimina wao kwa wao ni kuunga udugu kwa kutembeleana kwa ndugu zako Kati ya mke na mume kwa kiasi cha ukubwa kwa mpangilio wa kifamilia, ni uungaji wa ukoo maalum. Hebu tuanze na mawasiliano ya watu wote, Mwenyezi Mungu ametupangia mahusiano ya watu wote kwa binadamu ni jengo
Makala
AN-NUUR
Inatoka Uk. 6 kubwa ya mafanikio kutokana na ushirikiano watakaoufanya kati yao mna walimu wa shule hizo. Alisema kuwa wameamua wameamua kuchukua umamuzi huo wa kutoa elimu mashuleni kutokana na maeneo hayo kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya vijana kuingia katika vishawishi vibaya, vikimo vya utumiaji wa madawa ya kulevya. Tumejipanga kutoa katika shule mbali mbali za Zanzibar tukiwa na shabaha ya kuwa maeneo hayo ndimo waliomo vijana wengi,huku tukiwa na matumaini kuwa lile lengo letu linaweza kukiwa kwa wepesi zaidi alisema Amiri huyo. Aliongeza kusema kuwa Njia hii kwa kiasi kikubwa tunategemea kuwa ile dhamiri yetu ya kuimarisha utamaduni wa Zanzibar inaweza kufikia kwa hatua kubwa. Aidha alisema kuwa pamoja na kuingia katika kutoa elimu hiyo shuleni lakini pia Jumuiya yake imejipanga kuingia hadi mitaani (Maskani), ili kuweza kufanikisha malengo yao waliyokusudia. Pamoja na kufanya shughuli zeti mjini lakini pia tutafika hadi vijijini ili nako kutoa elimu kama ilivyo mjini tukiwa na makusudio makubwa ya utamaduni wa Zanzibar unaimarika na kukuwa kwa wanajamii wote wa Zanzibar alisema Amiri huyo. Amiri huyo alisema kuwa hatua hiyo ya kutaka kurudisha utamaduni wa Zanzibar kupia Jumuiya yao ni miongoni mwa malengo ya jumuiya yao, malenfgo ambayo yanawahusu vijana ambao wao ndio tegemeo kubwa kwa maisha sasa na
baadae. Aidha Amiri Masoud alisema kuwa Jumuiya yao pamoja na jitihada hizo lakini pia wanatoa elimu ya kuachana na utumiaji wa madawa ya kulevya, Elimu na maadili Michezo pamoja na elimu nyemngine mbali mbali. Alisema kuwa hatua zote hizo hufanya kwa lengo la kuifanya jamii hasa vijana kudumu katika kufanya shughuli zao kwa kielimu zaidi huku wakiachana nay ale yote yatakayoweza kuwanfa kuingia katika matatizo hapa duniani na akhera. Mipango yote hiyo tuniafanya sisi wenyewe huku ndani yake tukionesha na kutangaza imani ya dini ya kiislam, ili vizazi viweze kufumbua macho na kuona maadili mazuri na si vyenginevyoalisema Amiri huyo. Hata hivyo alisema kuwa pamoja na hayo pia Jumuiya ina mpango wa kufungua vituo maaluma vya utoaji wa elimu ya maadili hasa kwa vijana ambao wao ndio walengwa wakubwa. Alisema kuwa hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itaweza kufanikisha yale malengo yao waliyokusudia kupia Jumuiya yao ya Vijana, elimu na maadili Zanzibar. Kabla ya kuanza shughuli zetuy za jumuiya huwa tunafanya utati kupitia kitengo cha utati cha Jumuiya yetu ili kuweza kugundua ni matatzo gani yanayowakuba wanajamii hasa vijana hadi kukia katika njia mbayaalisema Amiri huyo Jumuiya ya Vijana , elimu na Maadili Zanzibar imaeanza kazi zake ikiwa na usajili halali wa Zanzibar kuanzia mwaka 2005, na hivi sasa ina Ju,mla ya wanachama 140, wakiwamo wanaume na wanawake.
tu ndio ambao atawarehemu Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mshindi na mwnye hekima surat Tauba 71 na katika hadithi muislam ni ndugu wa musilamu basi asimdhulumu na wala asimlengeshe kwa adui ; na yatosha madhambi kwa mtu kumdharau ndugu yake. Na haki za kuungana na muislamu na muislamu ni jambo ambalo ameamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume (S.A.W) pale aliposema Mtume (S.A.W) ninaapa hatokuwa muumini mara tatu alirudia neno hili. Wakauliza masahaba ni nani huyo ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ? akasema, yeyote atakayelala ameshiba na jirani yake ana njaa na yeye anajua. Muungano wa kifamilia Pale alipowekwa mke kuwa ni utulivu kwao na akawafanyieni kati yenu mapenzi na huruma Surat Rum aya ya 21 Mwisho : kwa hakika Mwenyezi Mungu yeye ni mrehemevu ameiumba rehema na akapasua humo jina miongoni mwa majina yake na yeyote mwenye kuunga basi Mwenyezi Mungu atamuunga na mwenye kukata basin aye atakatwa (kutengwa) amesema Mwenyezi Mungu katika Surat Muhammad aya ya 22 (Jee mwaonaje pale mtakapotawalishwa na mkafanya uharibifu katika dunia na mkakata koo zenu) yaani mkaacha kutembeleana na kuwasiliana. Jee hili ni jambo zuri ?
Muda: Saa 2:00 asubuhi - 10:00 jioni Mahala: Osi Kuu ya T AMPRO Magomeni Usalama, Dar es Salaam Mada: Njia za ufugaji wa kuku, Uchaguzi wa kuku kwa ajili ya kufuga, Kuandaa chakula bora, magojwa ya kuku na tiba yake, Utunzaji wa vifaranga na mayai nk. Vile vile mafunzo ya kutafuta soko la bidhaa zinazotokana na kuku, kutunza mahesabu na kumbukumbu za fedha pamoja jinsi ya kukuza mtaji yatatolewa. Kujisajili: Shilingi 50,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, Kitabu cha muongozo,na chakula kwa siku zote tatu) Muhimu: Washiriki watapatiwa vyeti na kitabu cha muongozo wa ufugaji kuku kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kukidhi haja. Kujisajili: IIi kujisajili piga 0714 151 532, 0767 151 532,0716 574 266 au ka TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni. Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151 532,0767 151 532,0716 574 266 au info(@)tampro.org MRATIBU MAFUNZO TAMPRO MAKAO MAKUU
Makala
AN-NUUR
AWA L I y a y o t e ningependa kuchukua fursa hii kuungana na Watanzania wote waliosalia japo na chembe ya huruma, imani na ubinadamu kulani kwa nguvu zote mauwaji yanayodaiwa kufanywa na Polisi. Hivi sasa watoto wa Marehemu Daudi wamekuwa yatima kwa baba na mkewe amekuwa mjane. Haya ni katika matokeo mabaya ya mauwaji haya ambayo athari yake ni ya daima dumu. Ni matarajio yangu kuwa Tume iliyoundwa na serikali kuchunguza mauwaji haya itafanya kazi yake kwa makini na haraka na mwishowe wahusika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Japo kuwajibishwa huko hakutawaondolea uyatima watoto wa Daudi Mwangosi, kwa maana kuwa hakutamrejesha tena duniani baba yao, lakini hiyo itakuwa namna moja ya kutenda haki. Kubwa zaidi ni kuzuiya mauwaji kama hayo yasiwe ni jambo la kuzoeleka kwa maana kuwa wauwaji wakajiona kuwa wanaweza wakauwa na isiwe lolote. Inapojengeka hali kama hiyo, uhai wa binadamu unakuwa hauna thamani tena na janga hilo huwa sasa ni balaa katika nchi ambalo litamtafuna kila mmoja kwa namna na kwa wakati wake. Ufupi wa maneno hakuna atakayesalimika. Ndio maana kwa upande mwingine naona kuna kila sababu ya kuwapongeza wote waliojitokeza na kupaza sauti ya kulani mauwaji haya vikiwemo vyombo vya habari, wanasiasa na viongozi wa dini. Katika watu waliotoa matamko makali kulaani mauwaji hayo ni waandishi wa habari ambapo hawakuishia hapo bali wamechukua hatua ya kusema kuwa hawatafanya kazi na Polisi kwa maana ya kuripoti habari zao angalau kwa kipindi
Makala
AN-NUUR
ASKARI wa jeshi la polisi Zanzibar wakiwa wamemkamata mmoja wa waumini wa dini ya Kiislamu kisiwani humo kwa madai ya kufanya maandamano isiyo halali na vyombo vya habari, viongozi wa vyama vya siasa na Maaskofu. Wakaja wakauwa Imam wa Msikiti Januari 2001. Huyu hakuwa katika maandamano wala katika kugomea sensa. Alikuwa ndio anatoka Masjid baada ya kuswalisha Ijumaa pale Mwembetanga, Unguja. Polisi wakapongezwa. Matokeo yake ndio haya. Polisi wanazoeya kuuwa. Wa n a o n a w a n a w e z a kuuwa na isiwe kitu bali wapongezwe na hata kupandishwa vyeo. Ipo kauli moja imesemwa na mmoja wa Wachungaji waliojitokeza kulani
10
SHUKRANI zote zinamstahiki Allah ambaye ana hukumu kwa ukweli na Haki na ana waongoza Awatakao kwenye Njia Iliyonyooka. Anaamua mambo yote kwa (Busara) Hekima yake na ana faradhisha mfumo wa maisha (dini), naye ni mwenye Hakima ya juu, Mjuzi wa yote. Alituma Mitume kama wapasha habari za kufurahisha na kama waonyaji, na aliwateremshia Kitabu ili wahukumu watu kutokana na waliyokuwa wakitofautiana miongoni mwao. Ili wahukumu kwa uadilifu na kumpa kila mtu haki stahiki bila upungufu au kuzidisha. Nakiri kuwa hapana Mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah pekee bila washirika. Yeye ni mfalme, Anastahiki shukrani zote na ni muweza wa kila kitu. Nakiri kuwa Muhammad ni mja na Mjumbe wa Allah, Rehema na Amani za Allah zimwendee, kizazi chake na wote walio mfuata (wafuasi) kwa ubora mpaka siku ya Hukumu. Enyi watu! Mcheni Allah aliye Tukuka, jitoeni kwa utiifu na kumuunga mkono na Atakuhakikishieni ushindi, mtiini Yeye na atakulipeni. Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu Mtukufu. Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote (22:40 41). Enyi watu! Imani haipatikani kwa kupenda au matarajio. Bali Imani mahali pake ni moyoni na hutekelezwa kwa vitendo ambavyo vina thibitisha ukweli wake na asili yake kwa kufanya vitendo vya ibada na kujitenga na makosa. Kila mmoja wetu anaweza kujiita Muislam na hata kudai kuwa ni Mumin (Muumini). Kila mmoja wetu anaweza kutangaza kuwa hapana Mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah na kuwa Muhammad (S.A.W) ni Mjumbe wa Allah. Hata wanaki, ambao watakaa chini kabisa ya Jahanamu (motoni), wana mtaja Allah kwa maneno yao. Wanafiki walikuwa wakitangaza mbele ya Mtume (S.A.W), Tunashuhudia kuwa wewe ni Mjumbe wa Allah . Pia waliapa kwa Mtume (S.A.W) na Maswahaba zake kuwa walikuwa pamoja nao, japokuwa walikuwa dhidi yao. Pamoja na hayo na ahadi na viapo vyote havikuwasaidia chochote; hapa wapo chini kabisa Motoni chini ya kila Mushriki (Washirikina), Mpagani, Myuhudi na Mkristo! Hii ni kwa sababu viapo vyao havikutoka mioyoni mwao iliyojaa Yaqin (uaminifu), Imani, kujisalimisha au utii. Na katika watu, wako (wanaki) wasemao; Tume mwamini Mwenyezi Mungu wa siku ya mwisho; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini (2:8). Imani yenye nguvu na thabiti ambayo inazaa matunda ya kauli za ukweli, vitendo adilifu, mapenzi katika Njia ya Allah, uaminifu katika utekelezaji wa
Makala
AN-NUUR
Tauhid na utii kwa Mjumbe wake (S.A.W). Imani inahitaji utatuzi, maisha, juhudi, uvumilivu na moyo kujizatiti kwa inaloliona kuwa gumu; kumtii Allah na kuizuia nafsi na tamaa na kumuasi Allah. Kuna dalili nyingi za Imani zilizo tajwa na Allah ndani ya Kitabu chake na Mjumbe wake (S.A.W) na kufafanuliwa ndani ya Sunnah yake ifuatavyo:Allah amesema: Hakika wanao amini kweli ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu; na wanapo somewa Aya zake huwazidishia imani, na wakamtegemea Mola wao tu basi; (hawana kuamini mizimu wala pango wala shetani wala makaburi wala mengineyo). Ambao wana simamisha sala na wanatoa katika yale tuliyowapa. Hao ndio wanao amini kweli kweli. Wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora (kabisa huko Akhera) (8:2 4). Aidha Allah amesema: Na inapo teremshwa sura (mpya ya Quran) wako miongoni mwao (watu wanaki) wasemao: Ni nani miongoni mwenu (Sura) hii imemzidishia imani? Ama wale walioamini ina wazidishia imani, nao wa furahi. Ama wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao, basi inawazidishia ubaya (mpya) juu ya ubaya walio kuwa nao; na wanakufa na hali ni makari. Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili (au zaidi)? Kisha hawatubu wala hawakumbuki (9:124 126). Kwa hiyo ndugu Waislam, ni nani miongoni mwetu mwenye sifa hizi? Nani miongoni mwetu mwenye hisia za woga ndani ya nafsi yake kwa sababu ya Allah na Anatukuza utajo wake anapotajwa? Nani miongoni mwetu ambaye Imani yake imeongezeka na anaye furahia wakati akisomewa Ayat za Mola wake? Anaye hisi furaha ya
kuamini Ayat na kutekeleza Sharia zake? Nani miongoni mwetu anamhisi kwa dhati Allah, bali zaidi ya kiumbe yeyote? Nani miongoni mwetu anaye simamisha sala kama inavyo takiwa, kwa usahihi na kwa wakati? Nani miongoni mwetu anatoa katika vile alivyo ruzukiwa na Allah kwa kutoa zakat na kuwasaidia wenye kuhitaji, jamaa na masikini? Tunapo tafakari hali ya Waislam katika zama zetu, tunawaona Waislam wengi wasiotia kwenye vitendo Imani au Uislam, isipokuwa yule aliye ridhiwa na Allah miongoni mwao kuwa na imani. Kwa ujumla, Waislam wana udhaifu, hususani katika kutimiza haki za Allah, haki za mtu kwa mtu, na kuwa na Imani za yaqin (uhakika). Waislam wengi katika ulimwengu wa Kiislam hawafuati kanuni za tabia/mwenendo au kusahihisha matendo yao na wengi wao wame athirika na utamaduni mbovu wa makari. Athari yake inaonekana kwa baadhi ya Waislam wenye wasiwasi na mashaka mioyoni mwao juu ya wahyi wa Allah. Ubashiri wa Mtume, uwepo wa malaika na majini na usahihi wa Ujumbe wa Mtume kwa ujumla. Baadhi yao walitilia mashaka kuwepo kwa Allah, Mola na Muumba! Utukufu ni wake Allah! kuwa yeyote mwenye mashaka na kuwepo kwa Allah, bali kutilia mashaka kuwepo kwake mwenyewe? Nani aliye muumba basi, iwapo Allah hakufanya hivyo? Hii ndio sababu tunawaona Waislam wengi leo hii ambao mioyo yao haitikisiki wakisikia Allah anatajwa, kama vile hawakusikia chochote cha kuwafanya wawe wa pole na wanyenyekevu. Baadhi ya Waislam hawaongezi imani yao wakati Ayat (Quran) zinasomwa. Bali wana zidisha uovu na dhambi, wakidhihaki Ayat za Allah na hawakuza kutekeleza kwa sababu ya ujinga. Baadhi ya Waislam
wa leo hawana uaminifu kwa Allah, bali wana imani na mali na maisha ya dunia. Kwa sababu hiyo hawatafuti mali kwa njia za halali, wanadhani wakifanya hivyo, fursa ya kujilimbikizia mali inapungua, wanafanya bidii kutafuta mali kutoka rasilimali zozote, ima ni halali au haramu. Baadhi ya Waislam leo wana wategemea maadui wa Allah ili kupata usalama na amani, ambayo inawafanya kuwatii makari kwa kuto mtii Allah na Sharia yake. Kwa hakika wanaorudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, shetani huyo amewashawishi na amewaghuri. Hayo ni kwa sababu waliwaambia waliochukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakutiini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wana wapiga nyuso zao na migongo yao! Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao. (47: 25 28) Tunaona kuwa wale Waislam wanao watii na kuwafuata maadui zao kwenye masuala yanayo pingana na Sharia ya Kiislam, wanafanya hivyo kwa sababu ya udhaifu na imani kwa Allah na utegemezi mkubwa kwa kitu kingine minghairi yake! Wana shangazwa na nguvu za maadui wa Allah na kudhani kuwa nguvu zote ziko mikononi mwao. Wana sahau kuwa yule Aliye waumba maadui, kwa hakika ana nguvu zaidi yao lau watu hawa wangelitumia hofu yao kwa kusabilia utii wao kwa Allah pekee, na wakatafuta njia za kupata ushindi, kama kufuata dini na Sharia ya Allah inayohusu mambo yao ya maisha, watapata nguvu ya kutosha. kama wakifanya hivyo, Allah atakuwa pamoja nao, na yeyote aliye na Allah, hatoshindwa.
11
IMPORTANT NOTICE TO NEW STUDENTS IN THE ACADEMIC YEAR 2012/2013
STUDENTS JOINING IN THE ACADEMIC YEAR 2012/2013 ARE HEREBY ASKED TO OBSERVE THE FOLLOWING INSTRUCTIONS: 1. ADMISSION LETTER/JOINIING INSTRUCTIONS - STUDENTS ARE ADVISED TO TAKE THEIR ADMISSION LETTERS AT THE FOLLOWING POINTS: (I) ZANZIBAR (UNGUJA); AT UKUEM OFFICES (II) PEMBA (CHAKECHAKE); - AT UKUEM OFFICES (III) DSALAAM AT ANNUUR OFFICES, MANZESE TIP TOP USANGI HOUSE (IV) MTWARA CONTACT MR. LENGA; 0787501081 (V) IRINGA CONTACT MR. ZUBERI; O714522122 (VI) MOROGORO AT MUM ADMISSIONS OFFICE (VII) TANGA CONTACT MAAWA S.S.; 0713549504 (VIII) KNJARO (MOSHI) CONTACT MR. OMARI; 0715185285 (IX) SINGIDA CONTACT MR. KINDI; 0784841055 (X) TABORA CONTACT MR. MANGI; 0783079146 (XI) MWANZA CONTCT MR. BEN; 0655889330 2. PAYMENT - THE STUDENT SHOULD MAKE THE NECESSARY PAYMENTS BEFORE REPORTING TO THE UNIVERSITY FOR REGISTRATION
Matangazo
AN-NUUR
- ALL THOSE WHO HAVE BEEN ALLOCATED LOANS BY THE HESLB SHOULD PAY NOT LESS THAN A QUARTER OF THE AMOUNT OF TUITION FEE NOT ALLOCATED BY THE HESLB - THE SELF SPONSORED STUDENTS SHOULD AT LEAST PAY NOT LESS THAN HALF OF THE TUITION FEE THE STUDENTS SHOULD ALSO PAY THE FOLLOWING: - ADMINISTRATION/REGISTRATION COSTSHS. 35,000.00 - CAUTION MONEY. 20,000.00 - IDENTITY CARD 3,000.00 ALL PAYMENTS SHOULD BE MADE THROUGH THE FOLLOWING MUM A/C NUMBER AND NAME: 01J1013380601 CRDB MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO 3. REGISTRATION - THE STUDENTS ARE REQIRED TO REPORT AT THE UNIVERSITY ON 1ST OCTOBER, 2012, FOR REGISTRATION. STUDENTS SHOULD COME WITH THEIR ORIGINAL CERTIFICATES, MEDICAL REPORT, FOUR (4) PASSPORT SIZE PHOTOGRAPHS AND BANK PAY IN SLIP, FOR ANY PAYMENT MADE. - THE DEADLINE FOR REGISTRATION IS 7TH OCTOBER, 2012 4. ORIENTATION WEEK - ORIENTATION WEEK FOR THE NEW STUDENTS BEGINS ON 8TH OCTOBER, 2012 5. LECTURES - LECTURES BEGIN ON 15TH, OCTOBER, 2012 F. A. TAMIM For DVC (ACADEMIC)
NB: Kwa wanafunzi waliochanguliwa MUM waliopo Dar es Salaam wake katika osi za gazeti la AN-NUUR wakiwa na Copy ya cheti cha Kidato cha Nne. 0714 111669
Munazzamat Al- Daawa Al- Islamiyya Osi ya Tanzania inayo furaha kuwatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha (International University of Africa) kilichopo Khartoum-Sudan kwa mwaka wa masomo 2012/2013. Usajili tarehe 15-30/9/2012, Masomo yataanza tarehe 2/10/2012. FACULTY OF ENGINEERING 1 MARIAM ABDALLAH MOHAMMAD (ZNZ) 2 OMAR MBAROUK OMAR (ZNZ) 3 RAMADHANI SAID (MWANZA) 4 RAMADHANI ZILI RAMADHANI (DSM) 5 KARIM ADAM (DSM) 6 KHANIFA AMANA (DSM) 7 SEIF HAMZA (DSM) FACULTY OF PHARMACY 8 UMMU-L-KHAYR SADRI ABDULLAH (ZNZ) 9 ASIA MOHAMED SULEIMAN (ZNZ) 10 HADIJA ATHUMANI MBELWA (DSM) 11 ABDALLAH NURDIN ABDALLAH (DSM) 12 ALLY JUMA OMARY (DSM) FACULTY OF PURE SCIENCE 13 NASSOR KHAFIDH MAJID (ZNZ) 14 ALI MAKAME AME (ZNZ) 15 KHALID WALID BAHORERA (ZNZ) 16 ABDALLAH MOHAMED (DSM) 17 AMINA ATHUMANI NADA (DSM) FACULTY OF DENTIST 18 WALIID RASHID SEIF (ZNZ) 19 HAMID HASSAN KARAMA (DSM) 20 HAMIS JUMA ASSEDI (DSM) FACULTY OF ECONOMICS 21 22 23 24 KHADIJA MOHAMED NAWAB (MWANZA) AHMAD SAID KAPAYA (MWANZA) JUMA SHABANI (MWANZA) AMASHA JUMA (DSM) FACULTY OF SHARIA 28 SULEIMAN KHAMIS ISSA (ZNZ) 29 ASHA MOHAMED OMAR (ZNZ) 30 SAID ALI SALEH (ZNZ) 31 IBRAHIM MUSA KAVINWA (MWANZA) 32 ALAWI NUHU BUKENDE (MWANZA) 33 ISMAIL ABDALLAH NAYAMBE (MWANZA) 34 JAFARY RAJABU SHOMARY (MWANZA) 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 HAMIMU SHABANI MASONJO (DSM) HAMISI ABRAHAMANI CHIMA (DSM) KINANDA YUSUPH SHOMARI (DSM) OMARI YUSUFU ALLY (DSM) JAFARI OMARI MWINDADI (DSM) SULTANI SAID MUHANI (DSM) SAADU ABDUL-MAJID (DSM) ABDRAHMANI HUSEINI SULEIMANI (DSM) MBWANA HAJI MJAJA (DSM) ABDALLAH ALLY CHUMBE (DSM) IS-HAQ MUSA ALLY (DSM) ALLY SHOMARI RAMADHANI (DSM)
FACULTY OF EDUCATION 47 MARIAM HUSSEIN MUSSA (MWANZA) 48 ALAWI NUHU (MWANZA) 49 SAID RAJABU NYANGE (DSM) 50 51 52 53 KHAMIS RAJABU SIMBA (DSM) MAJID MAULID OMARI (DSM) ABDALLAH HAMIS KABELELA (DSM) HASSANAT MANGO (DSM)
FACULTY OF MEDICINE 54 WASILA MMANGA MUSA (ZNZ) 55 HAWA OMARY RAMADHANI (DSM) FACULTY OF LABORATORY SCIENCE 56 AMEIR JAKU VUAI (ZNZ) 57 HAMAD JONAS (MWANZA)
FACULTY OF COMPUTER SCIENCE 25 SALIM MOHAMED SALIM (ZNZ) 26 RASHID RAJABU (DSM) 27 ISMAIL MUSA GALAWA (DSM)
Kwa maelezo zaidi ka kituo ulichofanyia mtihani au piga simu : Zanzibar: 0773 415 835, Mwanza: 0782 382 434, DSalaam: 0786 806 662/ 0652 806 662. Khamis Mohamed Liyenike KNY, Mkurugenzi- MDI
12
Maoni katiba mpya (2)
Karibu tena safuni, kwa ya katiba maoni, Sehemu hii jamani, ni ya pili tambueni, ZINGATIA kwa makini, kila ubeti unani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. UHURU iuthamini, wa KUABUDU nchini, Katiba isiukhini, kwawe unyu uoni, Ibada si kanisani, bali kote maishani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. Na SHERIA ya kihuni, iondoshwe katibani, Si nyingine hadharani, nathubutu kubaini, Haki zetu sothamini, ya UGAIDI nchini, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. MAENEO ya KIDINI, katiba iyabaini, Kwa ya insafu mizani, bila kubagua dini, Si KUHODHI moja dini, HAKI kubwa ARDHINI, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. NAFASI SERIKALINI, zigawiwe kwa mizani, Wasijazwe waumini, wa dini moja safuni, UWIANO wa KIDINI, uwe wazi katibani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. UWAKILISHI BUNGENI, utamkwe hadharani, Si mwingine wa KIDINI, kwa maslahi ya dini, Yawakilishwa na nani, maoni ya wanadini, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. Kadhalika UDIWANI, si dhambi kwa wanadini, SERIKALI MITAANI, uwe pia mwake ndani, Lengo maoni ya dini, siwe ombwe wala duni, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. MAHAKAMA iwe ndani, ya KATIBA ikhiwani, Vipengele katibani, itoe yake maani, Nazo sheria kinzani, batilishwe katibani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. MAHAKAMA elezeni, za HAKIMU MAKAZINI, Ziondoshwe katibani, kwa za wilaya nchini, MAMLAKAYE WIANI, kuwa MBILI kulikoni, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. Na FASILI ya yakini, ya NIKAHI katibani, Yainishwe kwa makini, sijekuwa matatani, Kwa ndoa za KISHETWANI, za jinsi moja jamani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. HAKI za KIHAYAWANI, zisiwemo katibani, LIWATWI kama kifani, si HAKI ya KIINSANI, Ni HAKI za KISHETWANI, tunopaswa kuzilani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. Ithnashara mwishoni, sije dhani wa maoni, Pamoja tena tuweni, juma lijalo safuni, Kwa akthari maoni, ya kutoa katibani, Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.
Barua/Shairi
AN-NUUR
Ndugu Mhariri,
Assalaam alaikum. Hakuna shaka wala hofu kwamba UDINI upo katika nchi yetu na mtu wa kwanza kabisa kuileta dhambi hii si mwingine bali ni Nyerere! Wa k o l o n i w o t e waliotutawala waliziheshimu dini zetu, lakini kuja uhuru na Nyerere, limekuwa balaa. Sensa ya kikoloni ya mwisho iliyofanyika katika nchi hii ilikuwa
Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie: Mhariri AN-NUUR, S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
dini! Tunashuhudia kila mwaka makanisa yakichukua mabilioni ya pesa za Watanzania kama wao ndio Watanzania halisi na wengine hawana haki. Je, huo sio udini? Watanzania wenzangu huu sio wakati wa danganya toto, na kutoleana vitisho visiokua na maana. Huu sio wakati ule wa kusema zidumu kra sahihi za mwenyekiti wa CCM. Watu wanajua mambo mengi ambayo zamani yalikuwa w akiyajua baadhi tu ya waheshimiwa na na watumishi fulani wa Mungu. Serikali inawapeleka Wa t a n z a n i a m a h a l i ambapo ni vigumu kuja kuwarudisha. Hapa mlipotufikisha pana tosha! Mwananchi Dar es Salaam
Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO. Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa). Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.
VIROBA MURUA
w), ogopa dua ya mwenye kudhulumiwa kwani haina pazia kati yake na Mola wake. D h u l m a mnayowafanyia Waislamu haitoenda patupu. Allah (AWT) atawaonyesha hapa hapa duniani na kesho Akhera pia mtaadhibiwa. Issa Ibrahim Kimweri Dar es Salaam.
13
Na Rajab Nkawa
(Hili ni) tangazo, ni tangazo la kujitoa katika dhima (ahadi) litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina. (Quran 9:1). Hii ni Aya ya kwanza ya surat Tawba ambayo ni sura ya tisa katika mpangilio wa sura ndani ya quran tuikufu.. Kushuka kwa Aya hii kunafuatia tabia za washirikina wa Kiarabu wa Makkah ambao walikuwa hawatekelezi ahadi au mikataba waliyokubalina baina yao na Waislamu. Kwa maneno mengine ni kuwa mikataba hiyo ilikuwa ikitekelezwa na Waislamu pekee. K a t i k a Ay a y a 4 , Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, Isipokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa hao washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote wala hawakumsaidi yeyote dhidi yenu Katika Aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweka bayana kuwa sio mikataba yote inayotakiwa kuvunjwa, bali ile tu ambayo washikina hawatekelezi upande wao. Lakini kwa ile ambayo washirikina walikuwa wakiitekeleza hakukuwa na sababu ya kuivunja kwa kuwa Uislamu unachunga ahadi. Matukio yaliyofanya aya hizi kushushwa yalijiri wakati wa Mtume Muhammad SAW. Mwenyezi Mungu Mtukufu angeweza tu kumpa maelekezo mtume wake juu ya kadhia hii ya kuvunja mikataba na washirikina, lakini hakufanya hivyo, bali ameijaalia kadhia hii kuwamo ndani ya Quran, ikimaanisha kuwa ni ujumbe kwetu tunaotakiwa kuufanyia kazi. Serikali yetu ya Tanzania haina dini, kwa maana nyingine ni serikali ya kipagani, na upagani ni ushikina. Na kwa kuwa raia wa nchi hii tuna dini zetu tofauti tofauti, basi waasisi wa dola hii wakaona ni vema tukawa na mkataba/ makubaliani/ahadi baina yetu, ya kwamba serikali itakuwa ya kishirikina na raia watabaki na dini zao na kwamba ni marufuku dini ya mtu au kundi fulani la watu kuwa na ushawishi wa kimaamuzi katika serikali. Lakini kwa bahati mbaya sana wakati Waislamu wakitekeleza ahadi, serikali ikishikiliwa na mawakala wa kanisa pamoja na Wakristo kupitia Nyerere hawakufanya hivyo. Nyerere akaanza kulipa kanisa better chance dhidi ya Waislamu. Hapa sitaki kwenda ndani zaidi kwani kitabu maarufu cha Dr. Sivalon chatosha kuthibitisha hoja hii. Mwislamu mmoja shujaa aliyeona mbali alimkabili Nyerere na kumwabia wewe hutatekeleza ahadi. Utawapa kipaumbele Wakristo wenzako tu. Kwa kutokujua Waislamu
Makala
AN-NUUR
14
Makala
AN-NUUR
WAISLAMU wakionesha umoja wao katika maandamano ya kupinga dhulma ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya baraza hilo kuwadhulumu wanafunzi Waislamu katika mitihani ya Kidato cha Sita 2012. Kwa umoja wao huo pia wamepinga zoezi la Sensa.
kuendeleza dini. Waislamu wa zama hizi asilani wasingekubaliana na upuuzi huu. Jambo jingine ambalo lilifanywa na serikali dhidi ya Waislamu ni kuruhusu kuwepo ubalozi wa Vatican nchini, ubalozi ambao ni mahsusi kushughulikia masuala ya Wakristo Wakatoliki. Wakati hili linafanyika watawala, kuanzia Rais wa zamani hayati Mwalimu Julius Kambarage, alitutangazia kuwa nchi haina dini wala kufuata misingi ya kidini katika kuendesha shughuli zake. Msimamo wa kususia zoezi la sensa uliotangazwa na taasisi karibu zote za Kiislamu ikiwemo hiyo BAKWATA, bila shaka serikali ilijawa na wasiwasi wa kutekelezwa msimamo huo ikiamini taasisi yenye nguvu na kuisikilizwa ni BAKWATA ambayo ipo chini ya himaya yake. Serikali ilijua kwamba msimamo huo wa taasisi za Kiislamu ungevunjika punde tu, baada ya kukutana wabia wao, viongozi wa taasisi wa BAKWATA hasa Mufti Issa Simba na jopo lake. Kweli punde Mufti Simba akatangaza kutengua msimamo wake alioutoa kwa Waislamu hapo awali na kukubaliana na matakwa ya serikali. Alifanya hivyo bila hata kuona haja ya kueleza sababu gani zimemfanya kubatilisha msimamo wake wa awali na wala hakuona sababu ya kuwahusisha
viongozi wenzake wa taasisi nyingine walioweka msimamo wa pamoja wa awali. Bila shaka taasisi nyingine zilitambua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa BAKWATA kubadilika wakati wowote kutokana na historia za viongozi wa baraza hilo. Hili halikuwashtua na wakaendelea kubaki na msimamo wao ule ule wa Waislamu kutoshiriki zoezi la sensa iwapo marekebisho waliyopendekeza hayatazingatiwa. Pia taasisi hizo zilijua nguvu yao kutoka kwa Waislamu katika miaka ya hivi karibuni. Ni wazi serikali ilidhani k a m a Wa i s l a m u b i l a BAKWATA wanajidanganya, akina Ponda na Mohammed Issa, Kundecha hawana utii unaoweza kuwafanya Waislamu wampuuze Mufti Simba. Serikali haikujua kuwa taasisi hizi mbadala wa BAKWATA sasa zimekuwa na kuimarika na kuaminiwa zaidi na umma wa Kiislamu. Leo tunaona kama wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza azma ya Waislamu licha ya kuwepo propaganda za upotoshaji za kuwachangaya Waislamu juu ya sensa na jitihada za wanaki. Leo serikali imeingia gharama kwa kuongeza muda wa zoezi la sensa wa siku saba zaidi, huku wakifahamu kampeni mbalimbali kwa
kuwatumia Masheikh maslahi na nguvu za dola na vitisho kujaribu kuzima msimamo wa Waislamu zimekwama. Serikali imezoea kutumia nguvu za dola kuzima mambo mbalimbali yanayofanywa na taasisi za Kiislamu zisizounga mkono BAKWATA. Kwa mfano waliwahi kupigwa wanafunzi wa BASUTA eti kwasababu wameswali Idd kabla ya BAKWATA kutangaza kuonekana mwezi Shawal. Leo watu wanaoswali Idd isiyokuwa ya BAKWATA wameongezeka hivyo hakuna tena mweye ubavu wa kuwabughudhi. Lakini kupitia zoezi hili, kuna haja ya serikali kujifunza jambo kama itahitaji. Kwa taasisi yao kongwe waliyoianzisha miaka zaidi ya 40 iliyopita imedhooka na kupoteza maana ya kuwepo kwake. Lakini zaidi ni kwamba haiaminiwi na Waislamu walio wengi. Hakuna Muislamu wa kweli anayesikiliza Bakwata inasemaje. Hata hao Waislamu walioshiriki sensa, sio kwa kufuata kauli za Masheikh wa Bakwata bali kwa kuona tu washiriki kiserikali. Yote hayo ni matokeo ya kuifanya taasisi hiyo kama idara ya serikali badala ya kuwa chombo cha Waislamu na kujiingiza zaidi katika kutetea maslahi ya serikali kama Baraza la Mawaziri badala ya kusimamia shida za Waislamu.
15
Inatoka Uk. 15
Habari
SHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012 Alisema, kupitia msimamo wa Waislamu ni kuwa neno Islamu limesikika kwa asilimia mia moja ndani ya wiki moja ndani na nje ya Tanzania. Katika zoezi la Sensa, hakuna eneo lililotawala ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kama Islamu, kila alipokiwa Muislamu, alisema sisi au mimi ni Muislamu sihesabiwi. Kalma ya Mwenyezi Mungu imesikika. Alisema Ponda.
AN-NUUR
Issa. Alisema, Jumuiya na Taaisi za Kiislamu nchini zipo katika mchakato wa kuikumbusha Serikali juu ya majibu ya Waislamu kuhusu NECTA, hivyo a l i w a t a k a Wa i s l a m u kuonyesha msimamo na kuitikia wito wa viongozi wao kama walivyoitikia katika kuigomea Sensa, pindi watakapoitwa kulikabili Serikali dhidi ya NECTA. Akizungumzia suala la Sensa, lililoanza Agosti 26, 2012, na kumalizika Ijumaa ya wiki iliyopita, kabla ya kuongezwa muda wa wiki moja mbele, ili kutoa nafasi kwa wale ambao hawaja hesabiwa, Sheikh Ponda alisema, kwa Sensa hii ni wazi, Tanzania ndio nchi ya kwanza kutoa Sensa ya ajabu duniani. Alisema, mwitikio wa Waislamu ulikuwa mkubwa na kila mmoja ni shahidi na kwamba, kwa muda mrefu nchini haijawahi kutokea mshikamno ulionyeshwa na Waislamu kama katika tukio hili maana kila kona ya nchi Waislamu
serikali kuongeza marupurupu ya walimu. Wa n a f u n z i nao wameingiwa na hofu kwani mitihani ya kitaifa katika shule za Msingi na Sekondari hufanyika katika muhula huu wa tatu.
WAANDAMANAJI nchini Afghanistan wakipinga kuchomwa Qur'an na askari wa Marekani nchini humo.
katika machafuko hayo. Hukumu hiyo dhaifu iliyotolewa na mahakama ya Marekani dhidi ya wahalifu hao, pia huenda ikazusha upinzani na maandamano makubwa nchini Afghanistan na kwingineko. Msemaji wa Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, amesema ofisi ya kiongozi huyo inachunguza uamuzi uliochukuliwa juu ya askari hao wa Marekani na kutoa mtazamo wake kuhusu suala hilo hivi karibuni. Aw a l i s e r i k a l i y a Afghanistan ilitoa wito wa
kupelekwa mahakamani askari wa Marekani waliochoma moto kitabu cha Qurani, ambapo Osi ya Rais Hamid Karzai ilitaka shirika la kijeshi la nchi za Magharibi N AT O k u w a f u n g u l i a mashitaka askari wa Marekani walioivunjia heshima Qurani na kuwahukumu katika mahakama ya wazi na ya kiadilifu. Aidha Rais Karzai alimtaja afisa mmoja wa jeshi la Marekani kuwa ndiye aliyehusika na kitendo cha kuchomwa moto Qurani katika kituo cha anga cha Bagram.
16
AN-NUUR
16
Mtandao wa Tawheed
AN-NUUR
BARAZA la Mitihani Ta n z a n i a ( N E C TA ) ni lazima lifanyiwe marekebisho ili likidhi matarajio ya wananchi. Hayo yamebainishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, akiongea na Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Idrisa, Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita. Sheikh Ponda, alikuwa akitoa tathmini na uhalisia wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, lililoanza Agosti 26, 2012, na msimamo wa Waislamu kwa ujumla na kuelezea nini kinachofuata kwa sasa. Alisema kuwa Baraza hilo halina sura ya kitaifa na hata utendaji wake umelikosesha imani kwa wateja wake na hivyo, haliwezi kuachwa likabaki lilivyo. Katika maelezo yake Ponda libainisha jinsi NECTA inavyohusika kutoa matokeo ya mitihani yasiyo halisi kwa maana yasiyowakilisha uwezo wa mwanafunzi halikadhalika makisi alizopewa na
wasahihishaji. Na kwamba katika uchakachuaji huo, wanaobamizwa ni watoto wa Kiislamu kwa vile kamati maalum ya kutunuku madaraja imekuwa kama kitengo cha Parokia ya Kanisa. Baraza la Mitihani la Taifa, limekuwa ni moja kati ya Taasisi za Kiserikali, ambazo Waislamu kwa muda mrefu wamekuwa wakililalamikia kuwa toka kuundwa kwake, mwaka 1973, limekuwa likiongozwa na Wakristo, na hivi karibuni kubainika kuwa kuna uchakachuaji wa mitihani ya wanafunzi wa Kiislamu. Lazima Baraza lile livunjwe, na wale wanaochakachua maksi za watoto wa Kiislamu waondoke, umoja tulioutumia katika kuigomea Sensa ndio tutautumia katika kulisafisha Baraza la Mitihani, Bakwata iacheni kama ilivyo maana imejidhirisha kuwa ni moja ya Taasisi za Serikali na si Taasisi ya Waislamu. alisema Sheikh Ponda
Inaendelea Uk. 15
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.