Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 19

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA RUKWA

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA MHE. MAMA SALMA KIKWETE (MNEC), MKE WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 25 - 27 FEBRUARI, 2013.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, S.L.P 128, SUMBAWANGA. Simu. Na. 025 - 2802137/2802138 Nukushi: 2802217/2802318 Barua pepe rasrukwa@yahoo.com

Februari, 2013

YALIYOMO
VIFUPISHO...................................................................................................................................................3 UTANGULIZI...............................................................................................................................................3 Jedwali A: Idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya katika mikoa ya Rukwa/Katavi...............................5 Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya.........................................................................................5 HALI YA AFYA...........................................................................................................................................7 Hali ya Maambukizi ya Virus vya UKIMWI................................................................................................8 Jedwali C-ii: Matazamio ya Mama wajawazito kujifungulia Kliniki..........................................................10 Jedwali E: Kiwango cha Chanjo katika Mkoa.............................................................................................12 Afya ya Mazingira.......................................................................................................................................13 Vyanzo vya Mapato katika Idara ya Afya..................................................................................................13 Vyuo vya Afya katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.....................................................................................13 MAFANIKIO KATIKA MALENGO YALIYOPANGWA.......................................................................14 CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KATIKA MALENGO YALIYOPANGWA KUTEKELEZWA..17 MWELEKEO WA IDARA YA AFYA.......................................................................................................17 MATARAJIO..............................................................................................................................................18 HITIMISHO.................................................................................................................................................19

VIFUPISHO AMREF OPV TB PEPFAR PMTCT UKIMWI VVU WRP African Medical Research Foundation Oral Polio Vaccine Tuberculosis Presidents Emergency Plan for AIDS Relief Preventing Mother to Child Transmission Upungufu wa Kinga Mwilini Virusi Vya UKIMWI Walter Reed Program

1.0 UTANGULIZI 3

Mkoa wa Rukwa ni moja kati ya mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini. Kiutawala una Halmashauri za wilaya nne ambazo ni Sumbawanga vijijini, Manispaa ya sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Kwa upande wa sekta ya afya mkoa wa Rukwa bado unashirikiana na mkoa wa Katavi. Mkoa umepakana na nchi ya Zambia upande wa kusini magharibi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande magharibi pia unapakana na mikoa ya Katavi (kaskazini magharibi) na mkoa wa Mbeya (kusini). Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002 mkoa wa Rukwa una jumla ya watu wapatao 1,037,196 Shughuli kuu za kiuchumi za watu wa mkoa huu ni kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara. Mkoa wa Rukwa una wilaya tatu (3), majimbo ya uchaguzi matano (5), Halmashauri nne (4), Tarafa kumi na sita (16), Kata sitini na nne (64), Vijiji mia tatu kumi na sita (316) Vitongoji elfu moja mia sita hamsini na nane (1,658) na Mitaa mia moja tisini na sita (196). Mkoa huu unajumuisha Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo. Mkoa pia una hospitali nne (4), vituo vya afya thelathini na nne (34) ,na zahanati mia mbili thelathini na moja (231), kama inavyojionesha kwenye jedwali Na.1 hapa chini. Taarifa hii inaainisha malengo, mafanikio na changamoto tulizokumbana nazo kwa kipindi cha mwaka 2012 katika Mkoa wa Rukwa na hususan katika Sekta ya Afya.

2.0. HUDUMA ZA AFYA MKOANI RUKWA


4

2.1.

Idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya katika mkoa wa Rukwa

Mkoa wa Rukwa una upungufu mkubwa sana wa vituo vya kutolea huduma za Afya kwa asilimia 56%. Sera mpya ya Afya ya mwaka 2007 inaelekeza pawe na Zahanati moja katika kila Kijiji, Kituo cha Afya katika kila Kata na Hospitali moja katika kila Wilaya. Jedwali na 1: VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA Aina ya Kituo Serikali Mashirika yasiyo ya Kiserikali Hospitali Vituo vya Afya Zahanati Jumla 2 24 196 222 2 9 14 25 0 1 11 12 4 34 231 259 2 62 121 185 Binafsi Jumla Upungufu

Jedwali hili linaonesha uwiano wa vituo vinavyomilikiwa na Serikali, Mashirika yasiyo ya kiserikali na binafsi na upungufu kuwepo. Halmashauri zinategemea hospitali za mashirika ya dini (Manispaa ya Sumbawanga na Nkasi) na Halmashauri ya Sumbawanga vijijini haina hospitali hivyo hutumia hospitali ya mkoa kama hospitali ya wilaya. Pia jumla ya kata 62 (65%) hazina vituo vya afya na vijiji vipatavyo 221 (50%) havina zahanati. Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya

2.2.

Kwa kushirikiana na wahisani Serikali imekuwa ikitoa fedha MMAM za Ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za Afya kwa kukarabati majengo ya vituo, kununua samani, kununua vifaa tiba, kujenga mifereji ya maji machafu, vyoo na vichomea taka(incinerator) kwa ajili ya kujikinga na maambukizi. 2.3. Hali ya Watumishi katika Idara ya Afya
5

Mkoa wa Rukwa umeendelea kuwa na upungufu mkubwa wa kada za kitaalamu. Uwiano uliopo ni Daktari mmoja kwa wagonjwa 200,000 (Taifa 1:25,000) zaidi ya mara nane na Muuguzi mmoja wagonjwa 30,000 (Taifa 1:50,000) zaidi ya mara sita. Ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa watumishi wenye taaluma, Mkoa unajitahidi kuwaendeleza kitaaluma watumishi wachache waliopo na kuomba vibali vya kuajiri watumishi wapya. JEDWALI NA. 2: HALI YA WATUMISHI KATIKA IDARA YA AFYA
Na 1. 2. 3. 4. 6. 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 KADA Wataalamu bingwa Madaktari Madaktari wasaidizi Fundi sanifu maabara Afisa tabibu Afisa wauguzi Afisa wauguzi wasaidizi Wafamasia Fundi sanifu madawa Afisa Tabibu wasaidizi Wauguzi Fundi sanifu maabara wasaidizi Afisa afya mazingira Afisa takwimu za afya (Medical Recorder) Katibu wa Afya Wahudumu wa Afya Daktari wa meno Daktari wa meno wasaidizi Wateknolojia mionzi Wateknolojia mionzi wasaidizi Optometria Fiziotherapia Muhasibu Mtoa dawa ya usingizi msaidizi Watawala wa hospitali Public Health Nurse MCHA Afisa ustawi wa jamii Wauguzi wakunga Fundi sanifu meno 6 MAHITAJI 13 25 84 10 507 97 210 9 42 57 94 71 52 15 5 353 7 4 2 6 2 3 1 2 2 87 87 1 379 1 WALIOPO 4 14 59 5 141 4 80 1 7 8 51 14 26 3 2 346 2 4 0 2 2 1 1 1 1 15 25 1 89 0 UPUNGUFU 9 13 25 5 366 93 130 8 35 49 43 57 26 12 3 7 5 0 2 4 0 2 0 1 1 72 62 0 290 1

Jumla 3.0.

2531

967(30%)

1564 (62%)

HALI YA MAGONJWA KATIKA MKOA WA RUKWA

Kwa magonjwa yanayoathiri sana jamii (Burden of Disease), Ugonjwa wa Malaria bado unaongoza kwa wagonjwa wa nje, kulazwa na vifo Mkoani. Kwa mwaka 2012 jumla ya wagonjwa 273,546 wameripotiwa kutibiwa OPD wakiwa na moja ya magonjwa makuu kumi. Malaria ikiwa inaongoza. Kwa wagonjwa waliolazwa bado malaria inaongoza kwa asilimia 56%, na kwa magonjwa yaliyosababisha vifo vingi malaria bado imeongoza kwa asilimia 40%. Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa iliyohatarini kupata maambukizi ya magonjwa hayo. Jamii inaendelea kuhamasishwa kuhusu kutambua na kutoa taarifa mara inapohisiwa kuwepo ugonjwa katika eneo husika
JEDWALI NA 3: IDADI YA WAGONJWA MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WA NJE KWA MWAKA 2012. Aina ya Ugonjwa WATOTO CHINI YA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA MIAKA MITANO (5) MITANO (5+) IDADI IDADI 1 Malaria 124,713 100,207 2 ARI 121,588 60,785 3 Diarrhoea 64,837 25,511 4 Pneumonia 38,642 22,810 5 Intestinal worms 14,444 15,057 6 Eye infections 18,870 10,997 7 Skin infections 16,484 10,603 8 `UTI 19,452 19,105 9 Anaemia 5,017 4,732 10 Minor surgery 8,681 14,872

Sekta pia ilitoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa kwa magonjwa mbalimbali. Katika mwaka 2012 jumla ya wagonjwa 27,716 walilazwa katika vituo vya kutolea huduma. Kati yao 14,117 walikuwa watoto chini ya miaka mitano (5). Magonjwa kumi sugu yaliyoongoza kwa wagonjwa waliolazwa ni kama yanavyoonekana katika jedwali Na 2.

JEDWALI NA 4: MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WALIOLAZWA


WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO (5) Aina ya Ugonjwa Malaria Intestinal worms Pneumonia Anaemia ARI Urinary Tract Infections Non Gastrointestinal Diseases Burn Severe Protein Energy Malnutritions(PEM) Other Nutritional Disorders Idadi 5,663 2,007 1,721 689 847 349 199 173 76 65 UMRI WA ZAIDI YA MIAKA MITANO(5+) Aina ya ugonjwa Malaria ARI Diarrhoeal diseases Pneumonia Intestinal worms Urinary Tract Infections Genital Discharge syndrome Pelvic Inlammatory Diseases Minor surgical conditions Skin infections Idadi 4,748 822 685 660 648 422 335 328 327 264

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 3.1.

Hali ya Maambukizi ya Virus vya UKIMWI

Hali ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI inaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa mkoa mzima kimeshuka toka 6.0% mwaka 2005 hadi 4.9% mwaka 2012. Pia mkoa una jumla ya vituo 41 vya kutolea huduma (CTC) ya tiba na malezi kwa wenye maambukizi na wasio na maambukizi. Hadi kufikia Desemba 2012 jumla ya wagonjwa 29,942 walikuwa wameandikishwa na kati ya hao wanaume ni 11,677(39%) na wanawake ni 18,265(61%). Kati ya wateja walioandikishwa, 15,534 (52%) wanapata dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (ARV) na kurefusha maisha.

Jedwali 5: Viashiria vya HIV/AIDS


VIASHIRIA Kiwango cha maambukizi ya VVU Wateja wanaotumia ARV 2005 6% 230 2008 4.9% 5,401 8 2009 4.9% 6,106 2010 4.9% 8401 2011 4.9% 12,538 2012 4.9% 15,534

Walioandikishwa CTC Vituo vyenye CTC Vituo vyenye huduma ya PMTCT Vituo vyenye VCT Vituo vyenye HBC Vituo vyenye huduma STI Wagonjwa wenye STI Kiwango cha PMTCT Vituo vya kutolea dawa za TB Wagonjwa wa TB Vituo vyenye huduma ya TB/HIV Vituo vya kutolea huduma ya tohara kwa wanaume

1,221 4 38 37 23

10,880 20 68 57 41 201

21,634 20 104 65 63 223 19,352 5% 20 793 20 0

21,634 20 156 65 76 223 19,450 5% 20 985 20 0

22,377 41 156 65 76, 223 12,983 5.6% 36 668 36 1

29,942 41 177 172 95 223 8,121 5.6% 41 315 41 10

10,659 7% 1 300 0 0

12,311 6.2% 20 834 20 0

3.2. 3.2.1.

Afya ya Mama Wajawazito : Vifo vya Mama na Mtoto na Hali ya Chanjo katika Mkoa

Hali ya afya ya mama wajawazito mkoani Rukwa inaendelea kuimarika. Kwa mwaka 2012 mahudhurio ya mama wajawazito katika vituo vya kutolea huduma yameongezeka hasa baada ya huduma kuimarika. Idadi ya akina mama wajawazito waliojifungulia katika vituo vya huduma nayo imeongezeka, hivyo kufanya idadi ya vifo vinavyosababishwa na uzazi kupungua.

Jedwali 6: HALI YA CHANJO Viashiria Vifo vitokanavyo na uzazi (HSSP 2015: 265)

Mwaka 2009 2010 2011 2012

Mkoa 55 107 71 78 53%

Uzazi katika vituo vya kutolea huduma (%)


9

2009

2010 2011

63% 58% 65.4% 53% 63% 58% 65.4% 28.2% 8.1% 23.3% 23% 18% 25% 20% 42% 41% 49.3% 30.3%

Waliozalishwa na watumishi wenye ujuzi (%) (HSSP 2015: 80%)

2012 2009 2010 2011 2012 2009 2010 2011 2012 2009 2010 2011 2012 2010 2011 2012

Mahudhurio baada ya kujifungua (%)

Uzazi wa mpango (%) (HSSP 2015: 30%)

Mahudhurio kabla ya wiki 16 za ujauzito

3.2.2.

: Matazamio ya Mama wajawazito kujifungulia Kliniki

Kiwango cha wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhudumiwa na wahudumu wenye mafunzo.
Viashiria 2008 61,489 61,489 (98.2%) 44,190 44,085 177/10000 0 32,494 32,494 3% 2009 65,435 70,503 (107%) 48,814 48,378 134/100000 35,319 (50%) 35,319 3% 10 2010 68,703 89,042 62,218 60,548 177/100000 43,352 (48.7%) 43,352 3% 2011 71,457 83941 56,244 55,634 128/100000 41,558 41,558 3% 2012 74,095 16,163 63,574 61,257 127/100000 48,513 (65.4%) 48,513 (65.4%) 4%

Wanaotazamiwa kujifungua Mahudhurio ya kwanza kliniki Jumla ya waliojifungua Jumla ya vizazi hai Vifo vya wajawazito Waliojifungulia vituo vya afya Waliozalishwa na wataalamu wa afya Vituo vyenye vifaa vya kutolea

huduma ya dharura ya uzazi Uwezo wa kuzaa Uwiano wa umri kwa uzazi wa kwanza Wajawazito waliopata dawa ya SP mara 2 Wajawazito waliopata dawa za kuongeza damu Wajawazitowaliop ata dawa ya kuzuia minyoo

6.9 18 37,831 (61%) 32,515 (52%) 42,100 (68%)

7 20 40,428 (56%) 45,185 (63%) 52,878 (74%)

7 20 37,510 (44%) 48,033 (62%) 66,428 (86%)

7 20 27,989 (33%) 38653 (46%) 56436 (67%) 54,130 (46.5%) 64,41615,534 (59.7%) 42,396 (36.4%)

Idadi ya vifo vya mama wajawazito imeshuka toka 128 kati ya vizazi hai 100,000 hadi 127/100,000 ukilinganisha na idadi ya vifo kwa taifa zima ambayo ni 454/100,000. 3.2.3. : Afya ya Mtoto na Chanjo

Katika mwaka 2012 huduma ya chanjo iliyotolewa kwa watoto wachanga iliongezeka ukilinganisha na miaka iliyotangulia. Mafanikio haya yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na wiki ya chanjo iliyoanzishwa na Mkoa kila mwezi ili kuongeza idadi ya watoto wanaopata huduma hii hasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kufikika. Hata hivyo

pamoja na mafanikio hayo Vifo vya watoto wachanga vimepanda toka 0.7 kati ya vizazi hai 1000 hadi 1.2 mwaka 2012. Viashiria Mwaka 2009 2010 2011 2012 2009 2010
11

Mkoa 3.5 4.2 0.7 1.2 17.7 3

Vifo vya watoto wachanga(siku 0-28)

Vifo vya watoto chini ya mwaka 1

2011 2012

1.7 1.7 147 463 883 69 94 97 113% 95.4% 105% 104.2% 113% 91.4% 105% 109 2% 0.9% 1% 0.6%

Vifo vya watoto chini ya miaka 5

Watoto chini ya mwaka 1 waliokamilisha chanjo ya pentavalent (DPT-HB3) (HSSP 2015: 85%) Watoto chini ya mwaka 1 waliokamilisha chanjo ya surua (HSSP 2015: 85%)

2009 2010 2011 2012 2009 2010 2011 2012 2009 2010 2011 2012 2009 2010 2011 2009 2010 2011 2012

Watoto chini ya mwaka 1 waliopata matone ya vit A mara 2 kwa mwaka (HSSP 2015: 80%) Watoto wenye uzito pungufu chini ya miaka 5 (HSSP 2015: 2%)

3.2.4. : Kiwango cha Chanjo katika Mkoa

MWAKA 2010

BCG 85,046 (124%)

DPTHB3 67,174 (98%) 88,369 (97%) 78690 (113%)

MEASLES 71,900 (105%) 74,491 (104.2%) 147,452 (113%)


12

T.T 2 69,703 (80%) 73,673 (88%) 92,893 (94%)

2011

83,966 (117.5%)

2012

91,048 (131%)

3.3.

Afya ya Mazingira Wastani wa kiwango cha watu wanaopata maji toka vyanzo salama katika Mkoa wa Rukwa ni sawa na asilimia 63%. Asilimia 70 kwa wakazi wa Mjini na asilimia 55% kwa wakazi wa Vijijini.

Mazingira ya miji na viijiji vyetu kwa upande wa usafi ni ya wastani sana.

Uzoaji taka ngumu ni asilimia 38% na majitaka ni asilimia 7%. Hili linatokana na tatizo la kutokuwepo kwa magari ya kuzolea taka. Jitihada za kuelimisha zinaendelea kutolewa.

Wastani wa kaya zenye vyoo bora imefikia asilimia 79%. Wilaya ya

Sumbawanga ina kiwango cha chini ya asilimia 63.3% ikilinganishwa na wilaya zingine. Vyanzo vya Mapato katika Idara ya Afya

3.4.

Vyanzo vikuu vya mapato kwa ajili ya huduma za afya katika mkoa wa Rukwa ni kama ifuatavyo: 1. Ruzuku toka Serikali Kuu 2. Ruzuku toka Serikali za Mitaa 3. Block grants 4. Basket Funds 5. Cost sharing 6. Wafadhili mbali mbali kama (PEPFAR, Global Fund, MEDA, WALTER REED (WRP), WHIRE RIBBON ALLIANCE TANZANIA, UTU MWANAMKE, PSI, JHPIEGO, AFRICARE, IFAKARA HEALTH INSTITUTE, ENGENDER HEALTH) 7. Vyanzo vingine. Vyuo vya Afya katika Mikoa ya Rukwa na Katavi Chuo cha maafisa tabibu wasaidizi Sumbawanga (Serikali)
13

3.5.

Mkoa una jumla ya vyuo vya Afya viwili ambavyo ni:

Taasisi ya afya ya Mtakatifu Bhakita Namanyere (Dini). Aidha mkoa kwa kushirikiana na wafadhili uko mbioni kuanzisha Chuo cha Uuguzi ili kupunguza upungufu mkubwa wa kada hiyo mkoani hapa. MALENGO YA MKOA KATIKA SEKTA YA AFYA

4.0.

Katika mwaka wa 2011/2013, Mkoa ulilenga kuendeleza huduma za Afya kwa kufanya yafuatayo:(i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) Kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza Kupunguza kiwango cha magonjwa na vifo kwa watoto wachanga na wanawake wajawazito Kupunguza tatizo la upatikanaji wa rasilimali katika vituo vya kutolea huduma ya afya (Watumishi na Vifaa) Kukarabati vituo vya kutolea huduma za Afya na matengenezo ya vifaa. Kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wetu. Kuongeza idadi ya mama wajawazito wanaohudhuria kliniki kupata huduma. Kuinua kiwango cha chanjo

5.0.

MAFANIKIO KATIKA MALENGO YALIYOPANGWA Kuongezeka vituo vya kutolea huduma kutoka 234 mwaka 2008 mpaka 259 mwaka

2012.

Kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka 177/100,000 mwaka 2008 mpaka 127/100,000 mwaka 2012. Kupunguza maambukizi ya VVU 6.0 mwaka 2005 mpaka 4.9% mwaka 2012.

14

Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma ya kupunguza maambukizi mwaka 2012.

ya VVU

kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, vituo 68 mwaka 2008 mpaka vituo 177 Kuongezeka kwa vituo vya kutolea dawa za kupunguza makali ya VVU na dawa za TB kutoka vituo 20 mwaka 2008 mpaka vituo 41 mwaka 2012.

Kuongezeka kwa idadi ya wanaume waliopata huduma ya tohara kutoka 300 mwaka 2010 mpaka 13,972 mwaka 2012.

Mahusiano mazuri kati ya idara, Serikali na wafadhili mbalimbali. Kuongezeka kwa idadi ya wadau wa kutoa huduma za afya kutoka wadau wanne (4) wa awali na kufika kumi na mbili (12) mwaka 2012. 6.0. WASHIRIKI WENGINE KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA Mkoa wa Rukwa umekuwa ukipokea na kupata huduma mbalimbali za kiafya kutoka Wadau mbalimbali ambao wameshirikiana nasi katika kazi hizi. Ingawa kazi hizi zimetokana na nguvu ya mikono ya Wadau mbalimbali, haitakuwa sahihi kutowataja baadhi ya watu ambao wamesaidia matokeo ya kazi hii. Japo si rahisi kutaja majina ya wote ambao kwa namna moja au nyingine wamesaidia kufanikisha kazi hii. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafuatao:- Awali ya yotenimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya njema ya mwili na roho zinazotufanya kutoa misaada hii. Na hivyo kwa namna ya pekee napenda kutoa shukrani za dhati kwa misaada ya hali na mali inayotolewa na Serikali yetu pamoja na wadau wengine kutoka ndani na nje ya nchi yetu, ambao wamekuwa bega kwa bega katika uboreshaji wa huduma za Afya katika mkoa wa Rukwa ambao ni :Walter Reed Program (WRP) pamoja na kutoa mafunzo - Hutoa huduma za mapambano dhidi ya UKIMWI

(i)

kwa ajili ya kupunguza VVU/ huduma za tohara kwa

wanaume na ununuzi wa vifaa na madawa kwa ajili ya shughuli za UKIMWI.

15

(ii)

AFRICARE - Kutoa huduma za uzazi na mtoto hasa katika ngazi ya jamii. JEPIEGO Hutoa huduma za uzazi na mtoto na kutoa elimu kwa watumishi juu ya uzazi salama / vifaa katika vituo vya Afya. ENGENDER HEALTH- Hutoa huduma ya uzazi na mtoto, hususani kutoa huduma ya mkoba ya uzazi wa mpango, mafunzo kwa watumishi juu ya njia za uzazi wa mpango za muda mrefu.

(iii)

(iv)

(v)

PSI - Hutoa huduma za uhamasishaji wa jamii kuhusu kujikinga na magonjwa mbalimbali kama Ukimwi, Malaria, Magonjwa ya kuhara n.k UTU MWANAMKE Hutoa huduma ya uzazi na mtoto, hasa kwa akinamama katika kuzuia kupata fistula. PLAN INTERNATION - Shirika la kimataifa linalofanyakazi kwa kushirikiana na AFRICARE na JHPIEGO katika kutoa huduma za uzazi na mtoto, hasa kwa kutoa huduma ngazi ya jamii, wahudumu wa Afya ya msingi kwa kuwapatia baiskeli na vitendea kazi vingine. MEDA - Hutoa huduma za usambazaji wa vyandarua vyenye dawa RODI - Mapambano dhidi ya Ukimwi katika maeneo ya ujenzi wa barabara.

(vi)

(vii)

(viii)

(ix)

(x)

BENJAMIN MKAPA AIDS FOUNDATION Hutoa huduma ya maboresho katika vituo vya afya kwa kutuletea wataalamu wa Afya na pia Ujenzi wa nyumba za Watumishi katika vituo vya huduma ya Afya kama vile vituo vya Afya na Zahanati. WHITE RIBBON ALLIANCE TANZANIA - Hutoa huduma ya uzazi na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito.
16

(xi)

(xii)

AMREF - Hutoa huduma za uzazi na mtoto na matibabu ya Fistula. Najisikia kudaiwa shukrani zangu kwa Mashirika ya Kidini na Asasi zisizo za Kiserikali na jamii kwa ushirikiano katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wetu. Aidha niwashukuru sana watumishi wa Idara ya Afya kwa kukubali kufanya kazi katika mkoa wetu licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
7.0.

CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KATIKA MALENGO YALIYOPANGWA KUTEKELEZWA Mzigo wa magonjwa hasa malaria bado ni tatizo kubwa katika jamii Milipuko ya magonjwa ya kuambukiza yanayozuilika kwa chanjo bado ni tatizo kubwa kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu toka nchi jirani. Upungufu wa vituo vya kutolea huduma ya afya (186) ukilinganisha na idadi ya kata na vijiji. Upungufu mkubwa (62%) wa watumishi wa kada zote za afya. Kiwango cha maambukizi ya VVU bado kiko juu(4.9%) Idadi kubwa ya wajawazito wanaojifungulia nyumbani (34%). Kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga (0.7% mpaka 1.2%) Uhaba wa vifaa tiba na madawa. Mwiingiliano wa watu toka nchi za jirani(Kongo,Zambia,Burundi,Rwanda). Uhaba wa magari ya wagonjwa. Hali ya jiografia ya mkoa. Ushiriki mdogo wa wanaume katika huduma ya mama na mtoto. Baadhi ya wananchi kutokubali kutumia vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa bure kwa wananchi. Kuongezeka kwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele MWELEKEO WA SEKTA YA AFYA MKOANI RUKWA

8.0.

Katika kipindi cha mwaka 2011/2012 Idara ya Afya imeendelea kutoa huduma za Afya ikiwa ni utekelezaji wa malengo mbalimbali iliyojiwekea. Yafuatayo ni baadhi ya malengo
17

ambayo idara imejiwekea ili kuboresha huduma ya afya katika mkoa wa Rukwa kwa mwaka 2012/13. Kuanzisha vituo vya kutolea huduma ya tohara kwa wanaume angalau kituo kimoja kwa kila Halmashauri. Kuanzisha utaratibu wa kuwapongeza wanaume wanaofika na wenza wao Kliniki kipindi cha ujauzito. Kuhakikisha kila familia inapatiwa vyandarua vyenye dawa ili kutokomeza ugonjwa wa malaria. Kuhakikisha vifo vya mama wajawazito vinaendelea kupungua Kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata chanjo OPV 0 kutoka siku 0 mpaka siku 14. Kuhakikisha kila mama mjamzito anayehudhuria Kliniki au kuja kujifungua amepimwa virusi vya UKIMWI. Kuhakikisha kila mtoto aliyezaliwa na mama mwenye maambukizi ya VVU anapata dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi. Kutoa mafunzo kwa watumishi ili kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali. Kila Halmashauri ifanye hamasa kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya wilaya kuhusu umuhimu wa akina mama wajawazito kuzalia katika vituo vya afya.

9.0.

MATARAJIO

Sekta ya Afya Mkoani itaendelea kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu tiba

na kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali yanayoikabili jamii yakiwemo ya malaria, kifua kikuu, Ukimwi na Kipindupindu. Ili kuongeza ufanisi na utoaji wa huduma bora, mkoa unaendelea kuweka katika bajeti ajira ya watumishi wapya pamoja na motisha Mkoa utaendelea na juhudi zake za kuongeza na kuboresha vifaa muhimu na vya kisasa vya tiba .

18

Mkoa unaendelea kuimarisha huduma ya rufaa kwa wagonjwa katika hospitali na vituo vya Afya. Mkoa unaendelea kuimarisha huduma za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Mkoa unaendelea na Harakati za kuboresha usafi wa mazingira ili kuzuia magonjwa ya milipuko. HITIMISHO NA SHUKRANI KWA TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) Mkoa unazo changamoto mbalimbali za Kimaendeleo unazokabiliana nazo. Changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Rukwa ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha elimu hasa kwa watoto wa kike hapa mkoani. idadi ya wasichana huwa ni asilimia 39. Tunaishukuru Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kuendelea kuwachagua na kuwasomesha watoto wa kike yatima na wanaotoka katika mazingira magumu kwa kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ambapo toka mwaka 2010 hadi 2013 vijana wa kike 12 wanasomeshwa na Taasisi ya WAMA. Tunafahamu kuwa umekuja kutoa msaada wa vifaa vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wetu, tunapenda tukuhakikishie kuwa tuko tayari kuupokea msaada huu na kukuhakikishia matumizi mazuri ili kuboresha Afya za wananchi wa Mkoa wa Rukwa, Idara ya Afya itahakikisha inatoa huduma Bora ili kutimiza malengo yake iliyojipangia. Naomba kuwasilisha. Eng. Stella M. Manyanya (Mb) MKUU WA MKOA WA RUKWA
19

10.0.

Wengi wetu sisi kama wazazi

hatuthamini elimu hasa kwa watoto wa kike. Katika jumla ya watoto wanaoacha shule

You might also like