Press Release

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

OFISI YA MKUU WA MKOA,


S.L.P. 128 Sumbawanga Simu: 025-2802137/2802138/ 2802318 Nukushi: 025-2802217/ 2802144 Barua pepe: rasrukwa@pmorallg.gp.tz / rasrukwa@yahoo.com Website: www.rukwa.go.tz / www.laketanganyikazone.go.tz Blogu: rukwareview.blogspot.com

8 MEI, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)


UTANGULIZI Wauguzi kote duniani hufanya maadhimisho ya wauguzi kila mwaka tarehe 12/05/2013 kukumbuka kazi ya mwanzilishi wa uuguzi duniani Bi. FRORENCE NIGHT NGALE ambaye alizaliwa tarehe 12/05/1820 huko Florencen Italy. Aidha siku hiyo hutumika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutafakari utendaji wa shughuli za wauguzi kwa ujumla. Sherehe hizo hufanyika kitaifa Mwaka huu, Chama cha wauguzi Tanzania (Tanzania National Nurses Association -TANNA) kitaadhimisha sherehe hizo kitaifa Mkoani Rukwa katika Manispaa ya Sumbawanga. Mgeni rasmi katika sherehe hizi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Hussein Ally Hassan Mwinyi (MB). MADHUMUNI YA SHEREHE Pamoja na kumkumbuka Muasisi wa huduma za Kiuguzi, laikini madhumuni mengine ya sherehe ya wauguzi kitaifa ni kutathimini mafanikio na changamoto zinazoikabili taaluma ya kiuguzi, na kubaini mambo ambayo yanaweza kuboreshwa. Mfano: Kutoa elimu kwa Umma kuhusu huduma zinazotolewa na taaluma hii na jinsi inavyo simamiwa Kuonesha kwa vitendo huduma zinazotolewa na taaluma hii Kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma kati ya wauguzi na wanataaluma wengine wa afya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu Ni sehemu ya kuutangaza Mkoa wetu na kuangalia changamoto zinazoikabili secta ya afya hususani upungufu wa rasilimali watu.

Pamoja na kamati hizo wadau mbalimbali wameshirikishwa ili kuweza kupata michango ya kufanikisha sherehe hiyo kama vile: Wafanyakaizi wengine wa Afya na wasio wauguzi kutoka idara nyingine Mashirika mbalimbali ya dini Asasi mbalimbali Mashirika mbalimbali Wafanyabiashara na watu binafsi KAULI MBIU YA SHEREHE YA WAUGUZI - 2013 Kauli mbiu ya sherehe ya mwaka huu inalenga kutekeleza mpango wa millennium ifikapo mwaka 2015, kuwa wauguzi wako bega kwa bega katika kupambana, kupunguza na kuthibiti magonjwa, kuboresha afya na kupunguza vifo katika maeneo yafuatayo: Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano MDG. 4 - wauguzi kuendelea kutoa huduma zinazolenga kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kama kutoa tiba, huduma ya chanjo na kutoa elimu mbalimbali Kuboresha Afya ya mama MDG 5 wauguzi kuendelea kutoa huduma ya Afya ya mama kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua kutoa tiba na elimu ya afya ya mama mjamzito ili kupunguza vifo vya akinamama na kuhakikisha uzazi salama Kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, malaria na magonjwa mengine ya kuambukiza kama kifua kikuu n.k. MDG 6. - Wauguzi wanashiriki kikamilifu katika kuhakikisha tiba ya magonjwa ya kuambukiza inatolewa pamoja na elimu ya afya ya kujikinga na magonjwa hayo pamoja na lishe bora na kutoa ushauri nasaha. SHUGHULI MBALIMBALI MAADHIMISHO ZITAKAZOFANYIKA KATIKA

Katika kuadhimisha sherehe hizi zitakazoanza terehe 10 12/05/2013 ratiba kwa ujumla itakuwa kama ifuatavyo: Ufunguzi wa sherehe Maonesho ya shughuli mbalimbali za uuguzi na ukunga Kutoa huduma mbalimbali Kongamano la Kisayansi kwa wauguzi

Shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga ambapo kutakuwa na mabanda mbalimbali ya maonesho na huduma mbalimbali zitatolewa bure kwa wananchi. Vile vile kutakuwa na vikundi mbalimbali vya kusherehesha kama vile ngoma, maigizo n.k. RATIBA YA MATUKIO/SHUGHULI ZA SHEREHE TAREHE/SIKU SHUGHULI 10/05/2013 Ufunguzi wa maadhimisho ya sherehe 11/05/2013 Kongamano la Kisayansi kufanyika 12/05/2013 Maandamano ya Wauguzi na hotuba ya mgeni rasmi MAHALI Uwanja wa Mandela MHUSIKA Mgeni rasmi wa Ngazi ya Mkoa

Libori Centre TANNA Makao Makuu Hosptali ya Mkoa Uwanja wa Mandela Wauguzi wote na wafanyakazi wengine wa Afya /Mgeni rasmi wa Kitaifa

SIKU YA KWANZA - 10/05/2013 - Siku ya kwanza ni siku ya ufunguzi, kutakuwa na mabanda ya kutolea huduma na maonyesho mbalimbali kama ifuatavyo: Huduma ya mama na mtoto Ushauri nasaha na kupima Virusi vya Ukimwi (VVU) Damu salama Huduma ya macho

Kisukari Tohara Banda la Banda la Banda la Banda la Banda la

huduma ya dharura (Emergency) muuguzi Mkuu wa Serikali (CNO) chama cha wauguzi Taifa (TANNA) mafunzo ya wauguzi (Training) Baraza la wauguzi (TNMC)

SIKU YA PILI - 11/05/2013 Kutakuwa na Kongamano la Kisayansi ambapo mada mbalimbali zitatolewa na wauguzi watapata nafasi ya kujifunza rejea mbalimbali kuhusiana na taaluma ya kiuguzi. Kongamano hili litafanyika katika Ukumbi wa Libori Centre SIKU YA TATU 12/05/2013 Kutakuwa na maandamano ya wauguzi kuanzia Hosptali ya Mkoa kuelekea Uwanja wa Mandela na mgeni rasmi atapokea maandamano na kutoa hutuba. Aidha ni siku ambayo wauguzi watatembelea wagonjwa katika Hospitali na kutoa zawadi mbalimbali na baadaye kutakuwa na tafrija katika Ukumbi wa St. Maurus Chem chem Sekondari. HITIMISHO Natoa wito kwa wananchi na wadau wote wa afya kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nelson Mandela ili kufanikisha maadhimisho hayo muhimu. Kama ambavyo sisi wananchi tunavyowaomba wauguzi kutupatia huduma bora, basi nasi tuonyeshe upendo upendo wetu kwao siku hiyo ya kilele ya tarehe 12/05/2013 kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu sherehe hizo. Asiyejua umuhimu wa muuguzi bado hajaumwa Mhandisi Stella M. Manyanya (Mb) MKUU WA MKOA WA RUKWA

You might also like