Press Release RSW 2 WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KITAIFA MWAKA HUU KUFANYIKA MKOANI MWANZA013 Final

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

NATIONAL ROAD SAFETY COUNCIL OF TANZANIA (NRSC)

Baraza la Taifa la Usalama Barabarani - Tanzania

TAARIFA KWA UMMA Ndugu Waandishi wa habari, Mabibi na Mabwana, BARAZA la Taifa la Usalama Barabarani linategemea kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mikoa yote nchini Tanzania kati ya tarehe 23.09.2013 - 27.09.2013. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa makundi yote ya watumiaji wa Barabara. Pamoja na kuwa maadhimisho haya yatafanyika mikoa yote nchini kwa kupitia Kamati za mikoa za usalama barabarani zilizopo kila mkoa, kitaifa maadhimisho haya yatafanyika mkoani Mwanza. Kaulimbiu ya mwaka huu ni Usalama Barabarani unaanzia kwangu, kwako na sisi sote (Road safety starts with me, you and all of us) Kaulimbiu hii inasisitiza kuwa kila mtumiaji barabara ana wajibu wa kuhakikisha Usalama Barabarani unaimarika. Takwimu za ajali za barabarani kwa kipindi cha miezi sita iliyopita Jan June 2013 zinaonesha kumetokea jumla ya ajali 11,361 zilizosababisha vifo vya watu 1,759 na kujeruhi watu 9,938. Aidha kwa upande wa pikipiki peke yake kumetokea ajali 3,016 zilizosababisha vifo vya watu 457 na kujeruhi 2,963

Mwelekeo wa takwimu hizo sio mzuri kabisa, niwatake watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria na kanuni za Usalama Barabarani. Tukumbuke kuwa miongoni mwa vitendo vinavyoongoza sana katika kusababisha ajali hizi ni: Mwendokasi Ulevi Kulipita gari la mbele bila kuchukua tahadhari Ujazaji wa abiria na mizigo. Tunatoa wito kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia yafuatayo; Kukagua vyombo vya moto mara kwa mara ili kuepusha ajali zinazotokana na ubovu wa vyombo hivyo. Madereva kuzingatia udereva wa kujihami, kuepuka mwendokasi, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara ikiwa ni pamoja na kuyapita magari mengine sehemu ambayo ni salama na kuchukua tahadhari kubwa wanapopita kwenye kona, mteremko, eneo la makazi na kwenye hifadhi za wanyama. Madereva wote wa magari kujiepusha kuendesha magari wakiwa wamechoka au wakiwa wametumia kilevi. Tunawahimiza madereva na abiria kufunga mikanda ya usalama wawapo safarini, kwani kwa kiasi kikubwa mikanda hii husaidia kupunguza vifo na ukubwa wa madhara ya majeraha katika matukio ya ajali. Wito kwa abiria kutoshabikia vitendo vya ukiukwaji wa sheria kama vile mwendokasi, abiria wanatakiwa kukemea na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi waonapo ukiukwaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani wasisite kutuma taarifa hizi kupitia namba za simu za viongozi wa Polisi katika mikoa husika ambazo zimebandikwa kwenye baadhi ya mabasi. Ninawasihi wapanda pikipiki kuacha tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja (mshikaki), kufuata alama na ishara zinazotolewa na wasimamizi wa sheria, kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu (helmet) na pia kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi pindi wanapohusika katika ajali. Wito kwa wananchi walio kandokando ya barabara kutojichukulia sheria mkononi inapotokea ajali katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuepuka kuchoma matairi na kuweka magogo kwa nia ya kufunga barabara na hivyo kuleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara ambao wana matatizo mbalimbali. Mwisho, BARAZA la Taifa la usalama barabarani linasisitiza kuwa:Usalama Barabarani unaanzia kwangu, kwako na sisi sote

(Road safety starts with me, you and all of us)

IMETOLEWA: 31/07/2013 Mhe. PEREIRA A. SILIMA (MB), NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)

You might also like