Zanzibar Daima Online Toleo La Nane

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 22

ZANZIBAR DAIMA ONLINE COLLECTIVE I TOLEO NAMBARI 08 DISEMBA 2013

Zanzibar Daima
ONLINE

43

kukupeleka kwenye Mtandao wetu Kurasa TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 > zimepangwa na HK DESIGNER

Unaweza kuscan codes hizi

DPP ANA KIBARUA KIGUMU KWA UAMSHO


Kesi hiyo inawahusu masheikh 11 ambao wanasota gerezani

04
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

>

YALIOMO
04 06 10
AHMED RAJAB Tunapaswa kuwasikiliza vijana wa leo JABIR IDRISSA DPP anakabiliwa na kibarua kizito cha kuwabana UAMSHO IBRAHIM HUSSEIN Muungano, Zanzibar na Watumwa Wawili MOHAMMED ABDULRAHMAN Kwa la CHADEMA Vyama havichekani ALLY SALEH Tusipime Maendeleo kwa Miradi ya Ujenzi JABIR IDRISSA Wazanzibari na hamu kubwa ya kujua ni kitu gani kimo ndani ya Rasimu mpya DESIGNERS SPECTACULAR Lublium modiena, publibu nulescit, noviri prisIgno MOHAMMED GHASSANI Sisi ni kizazi cha waliopundua na waliopinduliwa FARREL JUNIOR Zanzibar inataka Muungano wa Heshima, Haki na Usawa

Zanzibar Daima Online


Timu Yetu
MHARIRI MKUU Ahmed Rajab Email: ahmed@ahmedrajab.com MHARIRI MSAIDIZI Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com MHARIRI MSANIFU Hassan M Khamis Email: hassan@zanzibarimage.com MSIMAMIZI WA MAWASILIANO Hassan M Khamis WAANDISHI Jabir Idrissa Email: jabirgood@yahoo.com Othman Miraji Email: mwinjuu@hotmail.com Hamza Rijal Email: babujimba@hotmail.com Mohamed Abdulrahman Email: mamohamed55@hotmail.com Ally Saleh Email: allysaleh126@gamil.com WASAMBAZAJI mzalendo.net zanzibardaima.net zanzibardaima/facebook MATANGAZO Hassan M Khamis Simu: +44 7588550153 Email: hassan@zanzibarimage.com WASIALIANA NASI zanzibardaimaonline@gmail.com JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA Zanzibar Daima Collective 233 Convent Way Southall UB2 5UH Nonnstr. 25 53119 Bonn Germany
3

06

10

12 16 20

18 24 28

BURUDANI
12 16 30 34 38 39 40
TUFUNGUE KITABU Vuta Nkuvute kielelezo cha Uandishi wa Kizanzibari HEKAYA ZA ZANZIBAR Meza fupa

LADHA YA BETI Nitabaki Zenjibari

LADHA YA BETI Lingekuwa la kujua MICHEZO Challange Cup: Mashujaa wa Zanzibar washindwa kabla ya Mashindano kuanza

20

24

www.zanzibardaima.net
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TAHARIRI

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

TUNAPASWA TUWASIKILIZE

Na Ahmed Rajab HUU ni wakati muwafaka kwetu Wazanzibari kutafakari. Tuyatafakari yaliyopita, tuyatathmini na tujipangie yajayo. Tarehe 10 mwezi huu ilitimu miaka 50 tangu visiwa vyetu vipewe uhuru wake na Mwingereza. Tarehe 12 mwezi ujao itatimu miaka 50 tangu Mapinduzi yaliyoingoa kwenye madaraka Serikali ya kwanza ya Zanzibar huru iliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja na siku mbili.

Jisajili kwenye inbox yetu ya Zanzibar Daima Online Collective kupata nakala yako kwenye email yako

>

Matukio yote hayo mawili ni matukio makubwa katika historia yetu. Tunavyoambiwa ni kwamba Zanzibar haijawahi kuwa koloni la Uingereza lakini tangu mwaka 1890 visiwa hivi vyetu vilikuwa chini ya himaya ya Uingereza mpaka tarehe 10 Desemba, 1963. Unaweza kuitafsiri hali hiyo kuwa labda Zanzibar ilikuwa dola huru ambalo Uingereza ikilihami.
4

kamili vya kisiasa vilivyosajiliwa rasmi na Serikali ya kikoloni. Vikubwa miongoni mwa vyama hivyo vilikuwa vyama vya Afro-Shirazi Party (AS), Zanzibar Nationalist Party (ZNP), Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) na Umma Party. Vilikuwepo pia vyama vingine vidogodogo kama vile Zanzibar Communist Party na Haki za Binadamu. Vyama vyote hivyo viliudai uhuru wa Zanzibar. Hakuna hata kimoja kilichoiambia Uingereza isitoe uhuru. Kweli, kwa muda ASP kilikuwa na kaulimbiu ya zuia, ya kuitaka Uingereza iakhirishe tarehe ya kutolewa uhuru. Lakini kampeni hiyo ilidumu kwa muda tu na haikumaanisha kwamba kimsingi ASP ikipinga uhuru. Ndio maana ulipotolewa uhuru kiongozi wa ASP Sheikh Abeid Amani Karume aliukaribisha uhuru huo. Na alitoa hotuba iliyostahili kutolewa na kiongozi wa hadhi yake. Hakuiambia Uingereza kuwa hatuutaki uhuru endeleeni kututawala. Bila ya shaka kuna waliohisi kwamba uhuru ulikabidhiwa mikono siyo. Na hiyo ndiyo moja ya sababu za Mapinduzi ya Januari, 1964. Wazanzibari wa kizazi cha leo wanasema kwamba hawataki matukio hayo mawili ya Uhuru na Mapinduzi yaigawe jamii yetu. Wanasema kwamba wao ni kizazi cha waliopindua na waliopinduliwa. Wanachosisitiza ni mambo mawili. La kwanza, kuwa na umoja na la pili, kujifunza kutoka historia yetu ili tusiweze tena kutawaliwa. Hayo ndio maudhui ya makala ya Mohamed Khelef katika toleo hili. Ni hoja nzito na yenye nguvu ambayo sote tunapaswa tuisikize

Ukweli wa mambo unaonyesha hali nyingine. Ukweli huo unaonyesha kwamba tafauti baina ya kuwa koloni na kuwa himaya ilikuwa ndogo mno kama unyoya wa paka. Kwa kila hali Zanzibar ilikuwa ikitawaliwa kikoloni na Uingereza na ndio maana Sultan wa Zanzibar hakuwa na nguvu za kiutawala. Madaraka yote alikuwa nayo Balozi wa Uingereza aliyekuwa Zanzibar akiiwakilisha Serikali ya Uingereza. Hivyo, mtawala halisi wa Zanzibar alikuwa Mngereza. Hii ndiyo sababu ya kwa nini wananchi wa Zanzibar walisimama kidete kuupinga utawala wa Kiingereza na kudai uhuru wao. Mwamko wao wa kisiasa ulizidi kuhamasishwa na matukio yaliyozuka kwingine duniani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Matukio hayo yalikuwa pamoja na hatua ya wazalendo wa Indonesia ya kujitangazia uhuru mwaka 1945 na vuguvugu la kudai uhuru wa Bara Hindi (siku hizo Pakistan ilikuwa bado haijajiengua kutoka Bara Hindi na hivyo hata hapajakuwepo Pakistan ya Mashariki, ambayo baadaye nayo ilijitenga kwa nguvu na kuwa Bangladesh.) Bila ya shaka mavuguvugu mengine ya kupigania uhuru yaliokuwa yakivuma kwingineko Afrika nayo pia yaliwahamasisha wazalendo wa Kizanzibari waudai uhuru wa visiwa vyetu. Wazalendo hao wa Kizanzibari nao walianza kuwa na mavuguvugu ambayo baadaye yaligeuka na kua vyama
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

Uchambuzi wa kina kutoka wa waandishi wenye uzoefu Kwenye jarida hili Makala za uhakika Taarifa sahihi na sio za udaku Hakuna upendeleo, ni jarida lenye

kuandika habari za Zanzibar kwa asilimia 100. Jiandikishe kwa kupitia ukurasa wetu wa Zanzibar Daima Collective kupitia mtandano wa kijamii wa Facebook.

ANUANI YETU NI

www.zanzibardaima.net zanzibardaimaonline@gmail.com


WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

KIBARUA KIPEVU CHAMKABILI DPP KUWABANA UAMSHO


Na Jabir Idrissa Zanzibar
6

>

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar inacho kibarua kigumu cha kusuka au kunyoa kuhusiana na kesi yake dhidi ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) iliowapeleka mahakamani. Kesi hiyo inawahusu masheikh 11 ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya mwaka sasa wakikabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama na kuharibu mali. Masheikh hao wakiongozwa na Amir wao Sheikh Farid Ahmed Hadi, mkazi wa Mbuyuni mjini Zanzibar mwenye umri wa miaka 41, wana kesi mbili mahkamani wakidaiwa kuvunja Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1968 inayosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kesi nyingine ipo mbele ya hakimu wa wilaya kwenye Mahkama ya Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar ambayo watuhumiwa walifanikiwa kupata dhamana lakini wakazuiwa kutoka rumande kwa amri ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee. . Masheikh wengine walio ndani ni Mselem bin Ali Mselem (52) wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) wa Makadara, Azzan Khalid Hamdan (48) wa Mfenesini, Suleiman Juma Suleiman (66) wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) wa Mwanakwerekwe, Abdalla Said Ali (48) wa Misuni na Majaliwa Fikirini Majaliwa wa Magomeni.
Viongozi wa UAMSHO, kutoka kushoto Sheikh Azzan Khalid, Sheikh Msellem Ali, Sheik Farid Sheikh Farid Hadi

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Wanakabiliwa na mashitaka matatu kwa pamoja ya kuharibu mali, kufanya uchochezi kwa kushawishi na kuhamasisha fujo, na kula njama ya kutenda kosa. Sheikh Azzan ana shitaka moja zaidi la peke yake la kutoa maneno ya matusi kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani. Makosa hayo ambayo wote wameyakana, wanadaiwa kuyatenda katika maeneo tafauti ndani ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar, kati ya Oktoba 17, 18 na 19 mwaka jana. Wako gerezani kutokana na kuzuiwa kwa dhamana yao kwa kibali cha DPP Mzee. Baada ya kesi zao kutajwa na kutajwa tena na tena, mojawapo iliyoka Mahkama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam, kwa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka wa Zanzibar, inaanza kusikilizwa wiki hii na Jaji Mkuu Omar Othman Makungu. Taarifa za ndani ya serikali na osi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Zanzibar , zinasema kazi ngumu kwa Mkurugenzi huyo ndiyo inaanza sasa anapotakiwa kuwasilisha mashahidi. Sasa ndio kazi hasa inaanza. Unajua kesi hii baada ya kupigwa danadana na serikali, imekia mahali pagumu kwa DPP kutoa ushahidi utaoiridhisha mahkama ili hatimaye watuhumiwa wakutwe wanayo kesi ya kujibu. Tunaona wanavyohangaika kuingia katika hatua hii. Haraka-

ti nyingi kwelikweli, lakini ngoja muda uke tuone wamejiandaaje, chanzo cha habari kimeliambia jarida la Zanzibar Daima Online. Chanzo chetu kingine cha habari ni cha ndani ya Polisi ambako inasemekana kwa wiki kadhaa askari wa upelelezi wamekuwa wakiitwa na kujasirishwa watoe ushahidi mahkamani. Haitazamiwi kama watakuwa na mashahidi wasiokuwa askari polisi. Tunawaona baadhi ya raia wanaingia osi ya upelelezi lakini sijasikia kama wapo watakaopandishwa kizimbani kutoa ushahidi, kilisema chanzo hicho. Jarida hili lilipouliza iweje wakosekane raia wa kutoa ushahidi ilhali matukio ya fujo wakati ule yalitendeka mitaani na kushuhudiwa na wananchi mbalimbali, chanzo hicho kilisema nadhani wanahoa migogoro ya mitaani. Siku zote wanafalsafa wanapozungumzia dhana ya utawala wa sheria katika nchi zenye demokrasia changa, husema kuwa kesi ya jinai inapokia hatua ya kusikilizwa ndipo utabaini ushujaa wa serikali iliyoko madarakani. Hata baadhi ya majaji wenye ujasiri, mara nyingi hutamka kauli kama hii kuhusu usikilizwaji wa kesi za jinai, hasahasa wakati wa kusoma hukumu za kesi. Aliwahi kueleza haya jaji aliyesikiliza kesi ya maosa wa

polisi walioshitakiwa kwa kutuhumiwa kuwaua wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, mkoani Morogoro, pamoja na dereva wa jijini Dar es Salaam, aliposema hapakuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa. Alisema upande wa mashtaka ulishindwa kutoa ushahidi madhubuti, au ulitoa ushahidi dhaifu usio na nguvu za kisheria. Akitangaza kuwaachia watuhumiwa wote kwa sababu hiyo ya kukosekana ushahidi, jaji alisema anataka serikali imsake osa wa polisi aliyejulikana kutenda mauaji hayo ili apelekwe mahkamani. Kulingana na ushahidi uliotolewa mahkamani na zaidi ya mashahidi kumi, ilionekana yule askari aliyekuwa na bunduki wakati wa tukio, na kuifyatua na kuua wafanyabiashara waliotajwa, hakukamatwa na kupelekwa mahkamani, bali waliopelekwa hawakuhusika maana hakukuwa na ushahidi uliowabana. Hata katika hukumu ya kesi iliyomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, Hakimu Nongwa, alisema kesi ikishafunguliwa kazi inayobaki mbele yake ni kuwasilishwa ushahidi wa nguvu kuishawishi mahkama kuwapata na hatia washitakiwa. Hapa nataka kuieleza osi inayosimamia ushahidi, kwamba kazi inabaki kwao kuleta ushahidi imara utakaoiridhisha mahkama kuwapata na hatia washitakiwa.

Siyo wanaleta kesi hapa halafu wanaingia machoni wakitumainia mahkama iwafunge washitakiwa. Hii mahkama inafuata sheria, alisema Hakimu Nongwa. Katika kesi hiyo ya tuhuma za uchochezi na wizi wa maligha za kampuni ya Agritanza zenye thamani ya Sh. Milioni 59, Sheikh Ponda alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kukaa gerezani karibu mwaka mzima. Alikutwa na hatia ya kuingia kwa jinai kwenye kiwanja cha Changombe Markaz, kinachodaiwa kumilikiwa na kampuni hiyo ya Agritanza na ambacho utata wake wa umiliki ndio sababu kukamatwa kwa Sheikh Ponda na Waislamu wengine. Mahkama inawaachia huru washitakiwa wengine 49 baada ya kukosa kuwatia hatiani kwa makosa matano yote waliyokuwa wakishtakiwa nayo. Sababu ya kuwaachia ni upande wa Jamhuri kushindwa kuleta ushahidi wa kuishawishi mahkama iwaone wana hatia na kwamba upelelezi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika kesi hiyo ni dhaifu na kwamba mahkama haiwezi kumfunga mtu kwa ushahidi wa hisia tu, alisema Hakimu Nongwa. Sheikh Ponda na wenzake 49 kwa mara ya kwanza walikishwa mahkamani Oktoba 18, mwaka jana, muda unaofanana na walipokamatwa masheikh wa Uamsho. Walikamatwa wakati kukiwa na harakati nyingi za viongozi wa taasisi za Kiislamu

kupigania haki za Waislamu zikiwemo za kikatiba. Hali kama hii inaweza kuwakuta serikali wakati wa usikilizaji wa kesi. Mashitaka waliyowafungulia masheikh ni mazito yanayohitaji ushahidi uliotimia na sio wa kubahatisha. Hichi ndo kitu muhimu kinachotarajiwa kutoka kwa DPP, amesema mtumishi ndani ya Osi ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Zanzibar. Mwanasheria mmoja wa Zanzibar aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, amesema shtaka la kuhatarisha usalama ni gumu kulithibitisha ambapo mwendesha mashitaka atatakiwa kueleza kwa ufasaha namna wale anaowatuhumu walivyohusika kuhatarisha usalama. Masheikh wa Uamsho walikamatwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka jana mara tu Sheikh Farid alipoibuka baada ya kutoonekana kwa siku tatu mfululizo. Kuibuka kwake kulizusha mjadala mkali huku viongozi wenzake wa Kiislamu wakishinikiza Jeshi la Polisi litoe taarifa kwa kuwa hicho ndicho chombo mahsusi cha nchi chenye jukumu la kusimamia na kuwahakikishia raia ulinzi na usalama wao na wa mali zao. Hata hivyo, badala yake Polisi , walimtaka Sheikh Farid ake kituoni na kueleza alikokuwa. Viongozi wakuu wa Polisi walikanusha tuhuma kwamba

Sheikh Farid alitekwa na wanausalama na kuchwa kusikojulikana, isipokuwa wanasema alijicha makusudi ili kuisingizia uovu serikali. Sheikh Farid aliitika wito wa Kamishna wa Polisi Zanzibar (ZCP), Mussa Ali Mussa kuripoti Makao Makuu ya Polisi yaliyo Mwembemadema, ambako alihojiwa. Hakupewa dhamana, badala yake waliendelea kumshikilia hadi walipompeleka mahakamani kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa nia ya kuzusha tafrani kati ya wananchi na serikali yao. Kutoka hapo, Polisi wakawa wanamwita sheikh mmoja baada ya mwengine na waliwaita hata watumishi wa osi ya Uamsho. Sheikh Azzan amekuwa nje kwa dhamana tangu mwezi uliopita baada ya kuruhusiwa na Mahkama Kuu kusari nchini India kwa ajili ya matibabu. Amekuwa akiumwa go ambazo zimeota vijiwe, hali iliyomzidia akiwa gereza la Kiinua Miguu, Kilimani, mjini Zanzibar. Uamsho ni taasisi kama taasisi nyingine za Kiislamu zinazofanya kazi kwa mujibu wa sheria baada ya kusajiliwa rasmi. Kwa sehemu kubwa Uamsho ilisaidiwa na Osi wakilishi ya Ubalozi wa Marekani iliyopo mjini Zanzibar, katika kupata vifaa na samani za osi yake iliyopo mtaa wa Mkunazini, na kuiwezesha kusajiliwa mwaka 2003

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Muungano,Zanzibar na watumwa wawili

mkoloni wa Kireno aliyekuwa katili laisalkiasi. Ni bahati mbaya kwamba, miaka zaidi ya 150 baada ya kumshinda mkoloni wa Kireno, walikuja Waomani wengine, chini ya Sultan Said al-Busaid, kuja kuweka himaya ya utawala. Hii ni bahati mbaya iliyoikumba Zanzibar na ambayo ilijirejea tena baada ya mwaka 1964 pale baadhi ya Wazanzibari walipokwenda kuwaomba msaada watu wa Tanganyika kuipindua serikali iliyoundwa baada ya uchaguzi wa 1963. Baada ya Mapinduzi hayo ya Januari 1964, Watanganyika nao wakabakia na kuitawala Zanzibar hadi sasa, miaka 50. Kama ambavyo kuna Waomani waliouawa wakati wa kumwondoa mkoloni wa Kireno na kuukomboa upwa wa Afrika ya Mashariki, kuna pia Watanganyika waliopoteza maisha yao wakati wa Mapinduzi ya 1964 kwa ajili ya kuiondoa serikali na ufalme kwa wakati mmoja. Hilo linasema kwamba mahusiano baina ya Mzanzibari na Muomani hayawezi kudhalilishwa kama vile ambavyo haifai kuyadhalilisha mahusiano kati Mzanzibari na Mtanganyika. Lakini vile vile halisemi kwamba Zanzibar haipaswi kuwa huru inayotawaliwa na watu wake wenyewe kando ya ushawishi wa Kiomani na wa Kitanganyika. Wala halisemi kwamba mtu hawezi kuwa Mzanzibari kwa kuwa ana asili ya Kiomani au ya Kitanganyika. Hapana. Ukiangalia na kutafakari kauli za wanasiasa katika madai ya usultani, utumwa, utwana, ubwana, uarabu na uungwana ndani ya siasa za Tanzania, utakuta hakuna pengine popote maneno yanapo-

tumika isipokuwa kwenye vinywa vya viongozi wanaotumiwa kupandikiza tna, majungu, ubaguzi na chuki dhidi ya wale wanaojiita Wazanzibari. Viongozi hawa wanatumiwa kuharibu mahusiano yaliyopo baina ya makabila mbalimbali kwenye nchi na pia baina ya nchi na watawala wa zamani. Lakini hilo linafanyika kwa upande wa Zanzibar tu, tena dhidi ya Waarabu na watawala wa Kiomani tu. Sio Tanganyika, ambayo chini ya utawala wa Kijerumani na baadaye wa Kiingereza, watu wake waliteswa, kufungwa jela na kujengeshwa njia za reli kwa mijeledi, huku wengi wao wakifa kutokana na mateso na madhila waliyoyapata. Huko kila mwaka husherehekewa uhuru wa tarehe 9 Desemba, lakini hatukuwahi kumsikia Mwalimu Julius Nyerere wala waliomfuatia kwenye utawala kuwalaani au kuyakumbusha yale waliyoyatenda Wajerumani na baadaye Waingereza wakati walipoitawala Tanganyika. Nimalizie kwa hoja kwamba unapolinganisha madhara ya biashara ya watumwa na biashara ya kuuza nchi, basi ya kuuza nchi ni mbaya zaidi, maana inachukuwa kila kitu. Hii inawafanya wote waliomo ndani ya nchi iliyouzwa kuwa watumwa, wakitafautiana baina yao kwa kutumia ule mfano wa Mtumwa wa Nyumbani na Mtumwa wa Mitaani kama ulivyotolewa na Malcom X, mwanaharakati wa haki za weusi nchini Marekani. Mtumwa wa Nyumbani anaishi katika nyumba na bwana wake. Anavaa na anakula vizuri zaidi kulinganisha na wa Mtaani kwa kuwa yeye hula na kuvaa makombo ya bwana wake. Analala humo humo

ndani ya nyumba ya bwana wake ingawa yeye hulala sakafuni. Huyu humpenda bwana wake kuliko hata huyo bwana anavyojipenda mwenyewe. Mtumwa huyu hudiriki hata kujitolea maisha yake ili kulinda nyumba ya bwana wake tena kwa moyo mkubwa kuliko hata huyo bwana mwenyewe. Kama bwana wake akisema: Tuna nyumba nzuri hapa, basi mtumwa huyu atarukia haraka Kweli bosi tuna nyumba nzuri. Kila wakati ambapo bosi hutumia sisi na yeye hatosita kutumia neno hilo. Kama nyumba ya bwana imeshika moto, Mtumwa wa Nyumbani anakimbilia zaidi kuuzima moto kuliko hata mwenye nyumba mwenyewe. Kama bwana akiumwa, utamkuta mtumwa wake anaumia zaidi kuliko bwana mwenyewe, maana kila wakati hujifanya kumtambua bosi wake zaidi ya bwana wake anavyojitambua mwenyewe. Mtumwa wa Mitaani anapomtembelea mwenzake wa ndani kumuasa watoroke, anamkuta Mtumwa wa Nyumbani anamuangalia kwa jicho la mshangao na kusema: He! Una wazimu? Una maana gani unavyosema tutoroke? Wapi nitakaa katika nyumba nzuri kama hii? Wapi nitavaa nguo nzuri kuliko hizi? Wapi nitakula kizuri kuliko hiki? Huyo ndiye Mtumwa wa Nyumbani, ambaye bado tunaye humu ndani ya visiwa vyetu hivi sasa. Anaipenda nyumba ya bwana wake (Muungano) kuliko anavyoipenda yake (nchi yake ya Zanzibar). Na kama mwenzake akija kumshauri kuondoka kwenye nyumba hiyo, humuuliza kwa ukali: Unamaanisha nini kusema tutoke katika Muungano? Muungano huu ni mzuri wa Waafrika

10

Na Ibrahim Hussein Makala Maalum


MAKALA ya Mohamed Seif Khatib kwenye gazeti moja la kila Jumapili lililotoka tarehe 13 Januari mwaka huu, ilibeba kichwa cha habari kisemacho Si Njozi, ikijenga hoja ya unyama na ubaya uliofanywa na gengi la ukoo wa kinyonyaji la watu wa Oman. Mwandishi anaelezea namna Oman ilivyowanyonya Wazanzibari na kuwadhalilisha wenyeji wa visiwa hivi, huku akishadidia kwamba baya zaidi kuliko yote ni ile biashara ya kuuza watu, yaani biashara ya utumwa. Lengo hasa la mwandishi lilikuwa ni kuwafahamisha vijana wa leo, kwani walikuwa hawajui wala kuyaona yaliyotokea nyuma, si njozi. Ndio maana anawauliza vijana hao ikiwa wanajuwa kuwa wapo watu wakiitwa watumwa, watwana na masuria?

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akimvisha nishani ya utumishi uliotukuka Bwana Mohammed Seif Khatib

>

11

Kujaribu kukumbusha mambo ya Waomani na usultani, utumwa na Uarabu katika milenia mpya ni ubutu wa mawazo ya siasa au unyu wa dhamira ya historia ya mambo hayo. Mtu anaweza akajiuliza, inakuwaje mwandishi huyu, ambaye ni kiongozi na mwanasiasa aliyeshika nafasi kadhaa kubwa serikalini, akaweza kuandika mambo ambayo yanaweza kuleta chuki baina ya watu wa Visiwa hivi ambao wengi wao wamechanganya damu na watu wa Oman tokea zamani? Si dhamira ya makala haya kusema kwamba utawala wa Kiomani visiwani Zanzibar ulikuwa wa malaika wasiofanya uovu. Hapana, lakini mantiki inatulazimisha kuandika mambo kwa mizani. Unapomuelezea kijana wa leo maovu ya utawala huo, basi pia

unapaswa kumueleza na mema yake kama unataka kuyaona na kama hutaki kuyaona, basi angalau kumuelezea kwamba utawala huo ulioitwa wa Kiomani ulikuwa na msingi, asili, na mjengeko gani. Lakini pia ni busara zaidi kutenganisha baina ya Waomani watawala, kwa maana ya ukoo wa Busaidi na wenzao, na Waarabu wengine walioingia kwenye upwa wa Afrika ya Mashariki karne kadhaa kabla ya hata majilio ya utawala wa Kibusaidi, na hata ambao walikuja baada ya hapo, lakini hawakuwa kabisa sehemu ya utawala. Ama mimi nibakie huko huko kwenye hao watawala na uovu na wema wao kwa Visiwa hivi. Waomani kama watawala hawakujileta wenyewe kwenye upwa wa Afrika ya Mashariki, bali waliitwa na wenyeji wa eneo hilo katika karne ya 16 kuwasaidia kupambana na

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

KWA LA CHADEMA VYAMA HAVICHEKANI


12

Na Mohamed Abdulrahman Nionavyo


MIAKA iliyopita baada ya kurudi mfumo wa vyama vingi nchini Kenya mwanzoni mwa miaka ya 1990, misukosuko ilianzia ndani ya chama tawala cha KANU chini ya uongozi wa Rais mstaafu Daniel Arap Moi. Chanzo kilikuwa ni kuhojiwa na wanasiasa vijana kwa uamuzi wake wa kutaka mrithi wa kiti chake awe Uhuru Kenyatta. Wanasiasa hao walitaka mgombea apatikane kwa njia ya uchaguzi wa kidemokrasi ndani ya chama. Kundi lililopinga mkakati wa Moi, liliongozwa na wanasiasa mahiri, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na William Ruto na kujienguwa kwao na kuunda chama cha Liberal Party baadaye kulifungua njia ya kuibuka vyama vyengine. Yaliofuata baadaye ni marefu,lakini la kusisimua na kuwashangaza Watanzania ulikuwa ule mtindo wa wanasiasa kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwengine na hasa wanapokosa nafasi ya uongozi. Miaka ya karibuni yale yaliokuwa yakitushangaza kuhusu Kenya yamevisibu vyama vyetu vya kisiasa Tanzania. Wingu lililotanda hivi karibuni, ni uamuzi wa Kamati kuu ya Chama kikuwa cha upinzani Chadema kuwavua nyadhifa zao viongozi wawili Zitto Zuberi Kabwe, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, na mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo. Walishutumiwa kula njama za kukivuruga chama. Matukio haya yamesababisha gumzo kubwa linaloendelea sio tu miongoni mwa wanachama na wapenzi wa Chadema bali hata wa vyama vyengine na wale wasio na vyama. Kubwa katika kadhia hii ni suala zima la demokrasia. Kilichowachongea kina Zitto ni ule unaoitwa waraka wa siri wa kukihujumu chama. Waraka huu unasemekana ulikuwa na mkakati wa kundi hilo kujipanga kwa uchaguzi wa chama 2014 pale uongozi wa sasa utakapomaliza muda wake. Inasemekana wahusika wamekiri kuwa waliandaa kitu kama hicho, lakini mtu unajiuliza kuna ubaya gani kwa sababu makundi katika vyama ni sehemu ya karata za kisiasa. Hivi ni kusema kuwa upinzani ndani ya chama cha kisiasa ni jambo la kawaida, huibua hoja za kujadiliwa ili kuweka msingi wa makubaliano na hiyo ndiyo demokrasia na kinyume cha hayo si kingine bali ni udikteta. Kwetu si mapya Mtikisiko ndani ya Chadema unaotajwa kuwa mzito tangu kilipoundwa miaka 20 iliopita hata hivyo si kitu kipya katika siasa za
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

13

Tanzania. Haya yametokea takriban katika vyama vyote. Ndani ya chama cha CCM,tutakumbuka jinsi Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi alipolazimishwa na kamati kuu ya CCM, chini ya Mwalimu Julius Nyerere, kujivua vyeo vyote 1984 kutokana na kile kilichoelezwa ni kuchafuka hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar, alipohoji mfumo wa Muungano. Kuna kadhia pia ya kufukuzwa CCM, Maalim Seif Shariff Hamad, na kundi lake la watu sita. Baadaye ulipoanza mfumo w a

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

vyama vingi wimbi likakikumba chama cha NCCR-Mageuzi kilicholeta msisimko na kukitia homa CCM wakati wa uchaguzi wa 1995. Chama hiki kilichokuwa kikiongozwa na Augostino Mrema aliyejitoa CCM kiliandamwa na mgogoro na uchaguzi uliofuata kikaporomoka kikipoteza hata idadi ya wabunge. Kilifufuka baada ya uchaguzi wa 2010.Kuenguliwa wanasiasa kadhaa katika kura za maoni wakati wa kutafuta wagombea kwa uchaguzi chamani au kitaifa ni mtindo wa takriban vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Kuna sababu mbali mbali zilizotajwa ikiwemo ya ukiukaji wa maadili na mwongozo wa chama. Lakini kumekuweko na matukio ya kutengwa na hata kufukuzwa kwa sababu tu wamediriki kupinga au kuhoji utendaji wa viongozi wa ngazi ya juu. Baadhi ya hao walikimbilia vyama vingine vikawasimamisha kwenye uchaguzi na wakashinda. Mfano mmoja katika CCM ni kuondolewa jina la baadhi ya wagombea walioshinda katika kura za maoni katika majimbo yao, dharuba iliomkumba John Shibuda aliyejiunga na Chadema na ikamsimamisha katika jimbo lake la Maswa magharibi Mkoa wa Shinyanga na akashinda. Pamoja na hayo hata huko Chadema nako ukosoaji wake umemponza mara kadhaa, kiasi cha kuambiwa anakisaliti chama kwa manufaa ya CCM alikotoka. Walio Zanzibar hawana tafauti.

Vyama vikubwa ambavyo vina mvutano Zanzibar na bara ni CCM na CUF, ingawa Chadema kinabakia kuwa chama kikubwa na kiongozi wa upinzani katika Bunge la Muungano. Janga ninalolizungumzia halikuwabakisha CCM na CUF visiwani. Chama Cha Wananchi (CUF) Kiliingia kwenye mgogoro na baadhi ya watendaji wake akiwemo mbunge wa jimbo la Wawi Pemba, Hamad Rashid Mohamed , wakati aliyekuwa kiongozi wa Umoja wa vijana Blue Guards Said Miraji alipotangaza kujitoa na kuanzisha chama chake Democratic Alliance. Hamadi alifukuzwa na kwenda mahakamani. Mahakama iliamuru utaratibu haukufuatwa na kuwa aendelee kuwa mbunge. Hamadi anaendelea kuwa bungeni lakini CUF hamtambuwi kuwa ni mwanachama wao. Agosti mwaka huu,CCM Zanzibar nayo ilimfukuza mwanasiasa anayeinukia Zanzibar Mansur Yussuf Himidi kwa sababu ya msimamo wake kuhusu Muungano akiunga mkono muungano wa mkataba, kinyume na msimamo wa chama chake. Ni dhahiri yaliyomsibu Himidi aliyepoteza kiti chake cha Kiembe samaki yalitokana na shinikizo la wahadhina Zanzibar waliokuwa na sababu zao za binafsi, kwani kuna viongozi kadhaa katika CCM pande zote mbili za Muungano wenye misimamo tafauti na chama katika suala hilo na hawakuathirika hata kidogo. Kiroja cha mambo Mwenyekiti Jakaya Kikwete alitamka kuwa kila mtu

ana uhuru wa kuuzungumza Muungano katika kipindi hiki ambapo Tanzania imo katika mchakato wa Katiba mpya. Wanasiasa wengi wanaonekana kuwa na uwoga unaotokana na hofu ya kuhatarisha masilahi yao. Hali hii itaendelea hadi pale utaratibu mzima wa demokrasia utakapokuwa nguzo katika maamuzi ndani ya vyama vyote vya kisiasa. Kama viongozi wana nia ya dhati ya kujenga demokrasia basi hapana budi paweko na utaratibu wa kutumia njia za kidemokrasia kukia uamuzi katika masuala yanayohusika na muhimu ni kuwepo na uwazi na kuvumiliana. Kinyume chake vyama vitaendelea kuidumaza demokrasia vikiendelea kuimba nyimbo hiyo na kucheza udikteta. Yanayoendelea Chadema yanaweza kuwa na athari si kwake tu lakini kwa jukwaa zima la siasa nchini Tanzania Kwa ujumla la Zitto na Dr Kitila ni muendelezo tu wa visa na matukio ya kila wakati ndani ya vyama. Viongozi hawana budi kufahamu vyama si mali ya mtu zaidi ya wanachama na kama lilivyo taifa kwa raia wake, wanachama ndiyo wenye mamlaka ya vyama na ndiyo waamuzi. Takriban vyama vyote vina wanasiasa vijana wenye mvuto na kama si mkubwa basi wa kiasi fulani kwa wapiga kura. Pana wajibu mkubwa wa kuwalea vijana hawa pamoja na kuteleza baadhi ya wakati, kwani ni rasilimali kama viongozi wa siku zijazo. Hili lisiangaliwe kwa matazamo wa itikadi za kichama bali masilahi ya taifa

Nunua nafasi hii kuweka matangazo yako ya vifaa uuzavyo kama mfano wa hapa chini

MATANGAZO YA BIASHARA

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

14

15
JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako. JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako. JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

TUSIPIME MAENDELEO KWA MIRADI YA UJENZI


Na Ally Saleh Barza ya Jumbamaro
KUANZIA sasa na kwa mwezi mmoja ujao Zanzibar itakuwa na fete ya Mapinduzi. Hizi ni sherehe za kuadhimisha miaka 50 tokea kuondoshwa kwa Sultan wa Zanzibar au kwa lugha sahihi zaidi kupinduliwa Ufalme au Mfalme ambaye alikuwa mtawala wa Zanzibar. Mapinduzi hayo yalifanywa mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kupata uhuru wake kutoka kwa Waingereza ambao ndio waliokuwa na mamlaka halisi ya Zanzibar na sio Mfalme.
16

>

Uhuru huo wa Desemba 10, 1963 umekuwa hoja kubwa ya kisiasa na hata kiitikadi na umeigawa Zanzibar lakini vyovyote iwavyo kwa uhuru huo Zanzibar ilipata kiti chake, na hata kukikalia, katika Umoja wa Mataifa. Zanzibar imefanya sherehe nyingi za kuadhimisha Mapinduzi na hii ya Januari 12, 2014 itakuwa ni ya 50. Na kila baada ya miaka 10 zimekuwa zikifanywa sherehe kubwa kwa kufurahia kuingia muongo mpya na
17

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

18

kusonga mbele kwa nchi. Mara nyingi pia sherehe hizo zimekuwa zikitumika kupima hatua za maendeleo zinazopigwa. Mara zote hatua hizo za maendeleo zinapimwa kwa kuangalia idadi ya nyumba zilizojengwa na serikali, au hospitali, barabara au viwanda vilivyojengwa. Hapo ndipo kipimo chetu cha kusonga mbele huwekewa alama. Kwa hivyo kila sherehe ya mwaka mmoja, muongo mmoja na sasa miaka 50 tunapima maendeleo yetu kwa kutizama tumejenga nini, kikubwa gani, wapi na kadhalika. Kwa kra zangu kwa muda wote tumekuwa tukipima sivyo. Kwanza, kwa sababu mara nyingi miradi kama hiyo haiwi ni matakwa ya wananchi kwa sababu hawaulizwi wala hawashauriwi na kwa hivyo kama tutarudi nyuma kutizama miradi hiyo basi pengine tunaweza kuona kuwa

mingi yao ama imekufa, haikusonga mbele au imewekwa kando na wananchi. Pili, miradi hii hutumia fedha nyingi na tunaweza kusema kjuwa wakati wa ujenzi huwa ni wakati wa manufaa kwa wengi serikalini maana ununuzi wa vifaa vya ujenzi huo hauna udhibiti madhubuti na kwa hivyo inawezekana kinachopatikana hakiakisi thamani halisi ya fedha. Miradi ni muhimu lakini si vyema kutumika kuwa ni kipimo pekee cha maendeleo hasa iwapo miradi hiyo hutumika kuwa ni sehemu ya sherehe. Tumeona hili linavyokosa kina pale kwa mfano Mwenge wa Uhuru ulipotumika kwa dhana hiyo hiyo na wananchi kulikataa hilo. Swali langu katika hili ni vipi wananchi au Wazanzibari wanashiriki katika sherehe hizi mbali ya kuhudhuria sherehe

zinazosimamiwa na viongozi za kufungua au kuzindua miradi katika maeneo yao, miradi ambayo wao hawakuulizwa lakini imeota maeneo yao au imeshushwa kama Manna na Salwa. Ni vipi umma au mwananchi mmoja mmoja atapewa au amepewa nafasi ya yeye kutoa tathmini yake ya Mapinduzi toka yalipoanza hadi leo ili aweze kweli kueleza ni vipi amefaidika, wapi amepunjwa na kwa hivyo ni kitu gani anataka miaka 50 ijayo. Ningependa kujua wakati tukisherehekea mbali ya kujipima kwa majengo na miradi tunapima vipi hisia, hamasa na mapenzi ya kizalendo ya wananchi wetu tukielekea miaka mengine 50 ya Mapinduzi ambayo ni migumu na yenye majaribu zaidi. Tumeanza 1964 tukiwa na utawala wa Kimapinduzi na wa chama kimoja, imeka wakati

tukarejelea kuwa na vyama vingi japo shingo upande mwaka 1992 lakini hakuna dalili kuwa mfumo wa vyama vingi utaondoka tena hapa kwetu. Na pia kwa upande mwengine tulianza kuwa na Serikali ya Muungano hapo mwaka 1964 ukiwa na Serikali mbili. Serikali hizo ni ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake imo na imekuwemo Serikali ya Tanganyika, mfumo ambao umeleta changamoto nyingi. Wakati tukiadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi mfumo huo wa Serikali mbili ndani ya Muungano hauelekei tena kuwa na sababu, mashiko wala hoja na kwa hivyo kuna uwezekano wa Muungano sasa kuwa wa Serikali tatu. Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa nchi baada ya viongozi na vyama

vya siasa kuchoka na magomvi na hivyo kuamua kukubali kuwa Zanzibar iendeshwe kwa mfumo wa muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Tumekuwa na kizazi cha pili sasa cha mapinduzi na tunaelekea kuwa na kizazi cha tatu na kwa hivyo kuna zaidi ya nusu ya Wazanzibari ambao hawakuyaona kabisa Mapinduzi hayo na kwa hivyo kiungo chao na Mapinduzi hayo ni taarifa wanazozipata na fursa yao ya kusoma. Kwa hivyo ni kra zangu kuwa sherehe hizo hazitanoga kwa kufungua na kufunga miradi tu. Itakuwa ni kosa kubwa kutochukua bidii yoyote ya kuhimiza na kuchapuza mijadala mbali mbali ya watu wa umri na kra tafauti. Kuna haja ya sauti za watu kusikika ili watoa mawazo yao, waeleze hisia zao, watamke vipaumbele vyao, waeleze wanata-

kaje kutawaliwa, kama ni vijana waeleze matarajio yao, waseme wanataka nini ndani ya Muungano na iwapo kutakuwa na mabadiliko ya muundo wa Muungano pia wajue wataongozwaje katika zama mpya. Miaka 50 imepita ni zama nzima, na sasa zama mpya zinaanza. Si vyema, si sahihi na si halisi kuingia katika zama mpya bila ya watu kujitizama upya. Ni kwa kujitizama ndipo watapojiona na watasema wanatakaje Zanzibar yao iwe. Wenye sauti ya kusema wanaitaka Zanzibar ielekee wapi, kwa kasi gani na kwa faida ya nani. Wao ni wenye nchi na Serikali haina njia isipokuwa kuwasikiliza, la sivyo sherehe zitaishia kuwa sherehe tu

19

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMAMAGAZINE ONLINE TEMPLATE 03 BOXED CREATIVE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

MATARAJIO YA WAZANZIBARI KATIKA RASIMU YA PILI

Mikusanyiko mbali mbali ya Wazanzibari katika kudai Katiba mpya

Na Jabir Idrissa

Kauli ya Mwinyi Mkuu

>

20

WAZANZIBARI wana hamu kubwa ya kujua ni nini hasa kimo ndani ya rasimu ya mwisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanataka kufahamu wamewekwa wapi katika Katiba ijayo? Hawa wanajiuliza kwani hadhi yao itakuwa vipi ikapo Aprili mwaka 2014, muda uliotajwa kuwa Katiba itakuwa imepatikana? Sasa wanajiuliza rasimu itatambua kilio chao cha kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano au itakuja na mfumo uleule unaotakiwa kwa udi na uvumba na Chama Cha Mapinduzi (CCM)? Kila Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipopita na kukusanya maoni ya wananchi Unguja na Pemba, ilikuta sauti ya mabadiliko ya mfumo imeshtadi. Hata wenyewe wajumbe wa Tume walikiri ukweli huu. Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, alieleza mbele ya hadhara ya watu walioshuhudia akitangaza rasimu ya awali ya Katiba kwenye viwanja vya Karimjee, mjini Dar es Salaam, kwamba waliotaka serikali ya mkataba ni wengi na walikuwa na hoja nzito. Sawasawa kabisa. Wazanzibari walio wengi wanatarajia rasimu itakayotoka wakati wowote kuanzia wiki ijayo, itatambua mahitaji yao hayo ya kuletewa mfumo wa Muungano wa Mkataba. Tume ilishakengeuka kilio hichi cha kupatikana Muungano wa Mkataba, lakini Wazanzibari hawataki kuamini hata chembe kuwa tume itabadilisha msimamo iliouridhia kwa kueleza katika rasimu ya awali kuwa mfumo wa serikali tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano haukwepeki. Nasema kwa ufasaha kuwa wanachokitaka pasipokuwa na Muungano wa mkataba, angalau rasimu ijayo iridhie kwamba Katiba itakayopelekwa mbele ya wananchi kwa ajili ya uamuzi, itakuwa ni ile inayotandika msingi wa kuwepo kwa serikali ya Tanganyika, baada ya zile mbili wanazoishi nazo. Kwa maana hiyo basi, ni matarajio ya Wazanzibari kuwa Tume haitanya macho kwa kutimiza ahadi yao hiyo, hata kama wanatume wanajua kwa asilimia zote watakoroshana na wakuu wa CCM. Chama hichi kinachoshika dola tangu uhuru, viongozi wake wamejitia pamba na kutaka kungangania mfumo wa serikali mbili, kama vile wamethibitisha utaleta maajabu ya kuuinua uchumi wa Zanzibar unaoaminika unaathiriwa na chusha

21

Caption
za mifumo ya kodi ya Muungano. Kujitegemea na kupata mamlaka ya kujenga uchumi wake kwa mipango yake yenyewe, ndio hasa kilio cha Zanzibar kwa sasa, kama ilivyo kwa muda wote tangu pale ilipodhihirika kuwa nchi hii imekuwa inatumikia minyororo inayoinyima fursa za kustawisha uchumi na hivyo kunufaisha watu wake. CCM waliazimia kuwa wanachama wao wajadili rasimu ile ya awali iliyotolewa Juni 03 mwaka huu na watoe maoni yao wanataka mfumo gani. Hata hivyo, wakati uongozi wa juu ulitoa uhuru kwa wanachama, ulichapisha mwongozo unaoelekeza kuwalazimisha kuabudu mfumo wa serikali mbili. Waziwazi viongozi wakuu wa CCM wamepita nchi nzima wakihimiza wanachama wao na kuwalaghai wananchi wengine kutambua ulazima

> WWW.YOURDOMAIN.COM ISSUE 03 - WINTER 2012

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

wa kuwepo mfumo huo uliopitwa na wakati. Wamesema mfumo wa serikali tatu utaongeza gharama, lakini wameshindwa kueleza kama mfumo wanaoapia kubaki umesaidia vipi kukuza uchumi wa Zanzibar na kuipatia mamlaka ya kufanya mambo inayoona yanawafaa watu wake. Wazanzibari wanaamini wanayo haki ya kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano, kwa kuwa kwa muda mrefu wamenyimwa haki ya kiutu kuujadili Muungano ingawa waliambiwa kuwa ni Muungano wao. Hakuna anayeamini kuwa kikwazo kikubwa cha kukubaliwa mfumo wa serikali tatu au Muungano wa mkataba utakayoipa Zanzibar mamlaka yake kamili ya kujiamulia ipendacho na kujiongoza itakako, ni gharama

kubwa. Suala hili limefafanuliwa vya kutosha na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wamekuta gharama zinaweza kukidhiwa na nchi washirika kwa kila moja kusabilia ushuru wa bidhaa zinazoingizwa nchini. Serikali ya shirikisho itapata trilioni kadhaa za fedha za kujiendesha. Lakini hiyo haitoshi. Mbona viongozi wa CCM hawajaeleza namna watakavyoziba mianya ya kisadi inayochangia kupoteza mapato mengi kila mwaka na kuinyima serikali uwezo wa kukidhi bajeti ya maendeleo hadi kutegemea wahisani? Mbona hawajasema wataukomesha vipi usadi? Kinachoonekana ni kwa viongozi wa CCM kuzama ndani ya tope zito la usadi kwa kuwa hata chama chao wamekifutika makwapani mwa masadi. Hili ni dhahiri hata

Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete anakiri chama kimeishiwa pumzi kwa usadi katika uchaguzi wao. Wanapodai mamlaka kamili, Wazanzibari wanataka masuala ya fedha na sarafu, mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, uhamiaji na uraia yabaki kwenye himaya za nchi washirika wa Muungano. Ninachelea kuwa iwapo Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakuja na rasimu isiyowapa matumaini Wazanzibari, na wakajiridhisha kuwa wamebezwa, watakuja kutoa sauti yao kwa nguvu kubwa kwenye Kura ya Maoni. Je, wakikishwa hapo, yupo wa kujibu swali la kwamba hasara kubwa itaanguka kwao au itawajia watawala wanaodhani wana hatimiliki ya nchi?

LOGO YAKO
www.tunauza.com

Tangaza biashara kupitia ZANZIBAR DAIMA ONLINE Bei ni nafuu...

22

23

TANGAZIA BIASHARA YAKO


bei nafuu na pia tutakupa offer ya matoleo mawili bure!

Lete picha za Bidhaa zako

Chagua nafasi

Pamoja na maelekezo yako

Siku zote wasiliana nasi kwa matangazo yako ya aina yoyote, nasi tutafanya kazi vyema nawe Bila ya kutegemea kuuza bidhaa zako kupitia mtu wa kati [Dalali] Tangaza biashara yako moja moja kwetu Jarida letu inasomwa karibu nchi 87 ulimwenguni, China, UK, Russia, USA, UAE, Oman, Dubai, Tanganyika, Kenya na sehemu nyengine.

Jee unataka ukurasa mzima ama nusu?


Una kila sababu ya kutangaza na Zanzibar Daima Online. Jarida la mtandaoni lisomwalo karibu na nchi 80 duniani.

Tangazia bidhaa zako Bure kwa toleo moja na nusu bei kwa toleo jengine

35%
> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

OFFER MAALUMU TOLEO LIJALO


TUMEPUNGUZA

Ukiwa na Nyumba Kiwanja Gari Bidhaa za dukani hata mtandao wako

Unakila sababu ya kutangazia kwetu.

Wasiliana nasi kupitia anuani hizi


Zanzibar Daima Collective TEL +44 7588 550 153 WEBSITE www.zanzibardaima.net

WASILIANA NASI

ANUANI ZETU ZIPO KWENYE UKURASA 23

ZANZIBAR DAIMA ONLINE


WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Sisi ni kizazi cha waliopindua na waliopinduliwa


Na Mohammed Ghassani Ngurumo la Mkama Ndume
WAKATI Mapinduzi yanafanyika tarehe 12 Januari 1964, baba yangu (Mungu amrehemu) alikuwa ndio kwanza amewasili kisiwani Unguja akitokea Bara, ambako alikuwa ameishi kwa takribani miaka mitano mtawalia. Katika pirikapirika za Mapinduzi hayo, siku ya Jumatatu akakamatwa na watu wenye silaha kutokea Bara akiwa mitaa ya Kikwajuni. Jambo la kwanza aliloulizwa lilikuwa ni jina lake. Naitwaga Massanja! Ndilo lililokuwa jibu lake. Lakini rangi yake ya kahawia na nywele zake laini zikamsaliti ingawa alikuwa kweli na lafudhi ya Kimasanjamasanja. Wakati mimi nakua, nilikuta bendera ya CCM ikipepea kwenye paa la makuti la nyumba yetu

>

Hakupigwa sana, lakini alikishwa kwenye kambi ya Raha Leo na pale usuhuba wake wa utotoni na Salim Ghar, nao pia ukamsaliti, maana alipomuona tu akainuka na kuanza kulia: Khelef nawe umeletwa huku!? Baada ya rabsharabsha za Mapinduzi kutulia, baba yangu alirudi kwao Pemba. Akaanzisha maisha yake, akiwa kiongozi si tu wa ukoo wake wa Ghassani, bali pia baadaye akaja akawa balozi wa nyumba kumi kumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Wakati mimi nakua, niliikuta bendera ya CCM ikipepea kwenye paa la makuti la nyumba yetu. Hata tarehe yangu halisi ya kuzaliwa ilibadilishwa kutoka mwezi Januari na kuwa 5 Februari 1977. Baba yangu hakuwa sehemu ya waliopindua. Hakuwahi kuwa muumini wa Afro-Shirazi (ASP) wala wa Umma Party. Ukoo mzima wa baba yangu ulikuwa wanachama wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP ama Hizbu). Lakini mazingira yaliyomkuza yalikuwa ya ustahamilivu wa kisiasa. bao Khelef atakuwepo, hakuna kutajwa siasa za vyama. Na ndivyo ilivyokuwa pia wakati familia ya Bwana Mohamed ilipokuwa ikitembelea kwetu Pandani. Nadhani familia ya Rais Mstaafu Amani Karume ina hadith ya kusisimua zaidi katika hili, kwani mke wake, Bi Shadya anaotkana na kizazi cha waasisi wa siasa za utaifa wa Zanzibar, huku Amani akiwa mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Sisemi kwamba hakukuwa na visa vya karaha na kukomoana kati ya wafuasi wa kambi hizo mbili kwengineko visiwani Zanzibar. Ninachosema ni kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Wazanzibari wa leo ni wale waliozaliwa na kuishi baada ya Uhuru wa Desemba 1963 na Mapinduzi ya 1964. Miongoni mwao pia, muna idadi isiyo ndogo ambayo pande mbili za wazazi zimetokea kwenye mitazamo tafauti ya kisiasa, panapohusika dhana hizo mbili za Uhuru na Mapinduzi. Nadhani familia ya Rais Mstaafu Amani Karume ina hadithi ya kusisimua zaidi katika hili, kwani mke wake, Bi Shadya, anatokana na kizazi cha waasisi wa siasa za utaifa
25

24

Katika Zama za Siasa, alikuwa na raki yake mkubwa, Bwana Mohammed Fakih wa Kangani Mkoani (Mungu amrehemu), ambaye ukoo wake mzima ulikuwa ASP. Wakati wa msimu wa karafuu, baba aliondoka na aila yake kwenda kupiga kambi kwenye familia ya Bwana Mohammed Fakih Mkoani kwa ajili ya biashara ya mikate ya Ajemi, ambayo ni urithi wa ukoo wetu. Lakini wiki nzima kabla ya aila ya baba kuwasili Mkoani, wazee wa Bwana Mohammed (Mungu awarehemu) walikuwa wakitoa tangazo kwamba muda wote am-

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Rais wa Jamhuri za Tanzania, Jakaya Mrisho akishuhudia moja wa utiaji mikataba baina ya Oman na Zanzibar kwenye ziara ilifanyika hivi karibuni huko Oman

26

27

za Zanzibar, huku Amani mwenyewe akiwa mtoto wa Rais wa Kwanza wa baada ya Mapinduzi. Wapo wengi pia ambao ni matokeo ya mchanganyiko sio tu wa wazazi wenye mitazamo tafauti ya kisiasa, bali pia mchanganyiko wa visiwa viwili vikuu vya Unguja na Pemba na pia mchanganyiko wa pande mbili za Muungano, yaani Zanzibar na Tanganyika. Kuna wengine pia ambao waliinukia wakiwa wafuasi wa kambi moja

ya kisiasa lakini wamebadilika sasa na kuwa waumini wa mtazamo mwengine wa kisiasa. Vyama vikuu vya siasa vya Zanzibar hivi sasa sio tena kielelezo cha Zanzibar ya miaka 50 iliyopita nyuma. Kuna ambao walikuwa wafuasi wa ASP na Umma Party, lakini ama wao wenyewe au watoto wao wamekuwa leo wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF). Kuna ambao wanatoka kwenye mizizi ya Hizbu na Zanzibar and Pemba Peoples Party

(ZPPP), lakini hivi leo ndio wafuasi namba moja wa CCM. Baraka Muhammed Shamte ni kada mkubwa wa CCM akiwa ndiye mtoto wa kwanza wa muasisi wa ZPPP na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Muhammad Shamte (Mungu amrehemu). Kuna pia wasiokuwa na chama chochote cha siasa, na ambao kwao siasa za vyama hazina nafasi katika maisha yao. Wote hawa ndio sehemu ya sisi leo. Sisi Wazanzibari. Binafsi nimeishi kwenye

visiwa vyote viwili vikuu vya Zanzibar. Maisha yangu ya kifamilia pia ni mchanganyiko wa visiwa hivi na mitazamo hiyo ya kisiasa. Ndani ya familia yangu mnatembea damu za walioupokea Uhuru wa 1963 pale Maisara, siku hizo ukiitwa Uwanja wa Coopers na waliokuja kuupindua Uhuru huo Jumamosi, tarehe 12 Januari 1964. Kuna ambao walikuwa viongozi na watumishi wa umma kabla ya Mapinduzi na ambao walikuwa hivyo hivyo baada ya 1964. Zote hizo ni pande zangu.

Na zote hizo ni historia zangu. Na wala si peke yangu mwenye pande hizo. Tuko wengi jumla yetu, maana kila taifa lina historia yake, mazuri na mabaya, kupanda na kushuka. Lakini mwisho wa yote, kila taifa hupaswa kusimama kama taifa, likiitukuza historia yake na wakati huo huo likijifunza kwa matukio na matokeo ya historia hiyo kwa minajili ya kusonga mbele. Wakati tukiadhimisha

nusu karne ya Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar, hatupaswi hata kidogo sisi kizazi cha sasa kuyachukulia matukio hayo ya kihistoria kama msingi wa kutugawa. Hatuna sababu ya kuwapa fursa wazee ambao dunia yao inawalizikia, kuturithisha dunia ya matatizo na migogoro kwa msingi wa historia ya kabla na baada ya Uhuru na Mapinduzi. Sisemi kwamba hatuna chochote cha kujifunza kwao, lakini nasisitiza kwamba tuchukue ma-

zuri kutoka kwao na tuwaachie wafe na mabaya yao. Moja ya mabaya hayo ni kosa walilolifanya wote wawili wakati huo, ambapo upande wa Hizbu/ZPPP wakajisahau kwamba Zanzibar ni ya wote na kupatwa na kiburi cha madaraka na uluwa, huku upande wa ASP/Umma Party ukijiona kwamba wao tu ndio wenye haki ya kuitawala Zanzibar kwa msingi wa wingi wa watu. Wote hawakutaka kujua kuwa Zanzibar ni yetu sote. Matokeo yake, pande zote mbili, ama kwa ku-

jua ama kutokujua, zilichangia kuja kuifanya historia ya kutawaliwa kwa Zanzibar kuwa refu zaidi. Hilo halimaanishi kwamba pande hizi mbili hazikuifanyia mema yoyote nchi yao. Hapana. Zilifanya mengi. Lakini sisi wa leo, tunapaswa kuyatumia mafunzo haya ya kihistoria kupunguza urefu wa nchi yetu kutawaliwa. Si vyenginevyo

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Zanzibar inataka Muungano wa heshima, haki na usawa


Na Farrel Foum Jr. Zanzibar Tuitkayo
NATUANGALIE namna ya kuufanya mfumo wa Muungano uwe bora ili uwe na nguvu za kisheria, uhalali kwa wananchi na pia maendeleo yaliyokusudiwa katika uundwaji wake. Kwa sasa mfumo wa serikali mbili kuelekea moja umefeli na kuundeleza ni kuendeleza makosa yalioleta chuki, tna na ukiritimba mkubwa wa maendeleo nchini. Sina haja ya kurejea historia ya Muungano huu au uasisi wake kwa sababu ya mazonge mengi yanazouzonga mfumo mzima wa Muungano kuanzia uundwaji wake na miaka karibu 50 ya uhai wake. Ila tutatazama namna ya kuufanya uwe bora na kuhakikisha mfumo ujao utajenga utamaduni wa kuaminiana, kufahamiana na kurejesha heshima iliokuwa kama ni lengo la kuungana hasa kwa namna ya Wazanzibari waliowengi walivyoufahamu muundo

>

kwamba mabadiliko ya Katiba ya Muungano yamekuwa yakichochewa na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 hasa baada ya kuona kwamba Katiba mbili haziendani kimantiki hata kisheria. Na kwa vile katika kura ya maoni ya Zanzibar idadi kubwa ya wananchi walioipitisha hakukuwa na budi zaidi ya kuifanyia marekebisho Katiba ya Muungano ili iendane na sauti ya asilimia 66 ya Wazanzibari. Muundo ambao Jaji Mstaafu Joseph Warioba na tume yake walioupendekeza umethamini kauli ya wananchi kwamba ile dhana ya udogo wa sehemu ikawa ndio kigezo cha kuburura maoni yao iliondoshwa. Kwa vile msingi mkuu wa Muungano ni nchi mbili zilizoungana bila kujali ukubwa au idadi ya watu

faka baina yao na kuunda kitu kitachokubalika na wote. Ndio maana ukakuta hata maoni ya mamilioni ya Watanganyika waliotamani serikali moja hayakuridhiwa kuwekwa katika Rasimu ya kwanza ya Katiba kwa sababu yalipingana na ya Wazanzibari hata wakiwa na idadi ndogo ya watu kulinganisha na Bara. Maoni yangu ni kwamba Jaji Warioba ametupa heshima tunayostahili Wazanzibari katika Muungano huu. Pia ametupa matumaini kwamba mfumo ujao utaweza kuwa ni kielelezo kipya cha mabadiliko makubwa zaidi katika mfumo wa Muungano utaojengwa kwa misingi thabiti ya kuheshimiana, kuaminiana, haki na usawa. Wengi tunaamini mfumo wowote wa Muungano katika ndoto ya Wazanzibari uendane na kauli mama ya Zanzibar kama ni nchi na yenye kujiendesha yenyewe kimamlaka. Mifumo butu yenye taswira moja lakini lengo lililojicha haitakubaliwa katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi hasa ukizingatia kwamba ari ya kuwa na mfumo wa Mkataba haukuasisiwa na chama chochote bali na wananchi wa kawaida ndani na nje ya visiwa hivi. Wao waliona mbali zaidi na walitaka kuhakikisha mfumo ujao

hautakuwa na kigugumizi chochote juu ya uhalali wa kuwepo kwa taifa la Wazanzibari. Hili linawezekana hata ndani ya mfumo wa serikali mbili ikiwa yaliomo ndani ya Muungano yatazingatia maoni ya wengi yalioweka wazi msimamo wa Zanzibar kama ni nchi yenye kila nyenzo ya kujitosheleza na kujiendesha yenyewe. Jaji Warioba kafahamu maana kamili ya Muungano wa Mkataba na ndio maana akapendekeza rasimu ya mwanzo ya mfumo wa serikali tatu na ukakuta wengi waliopendekeza mfumo wa Mkataba hawakuwa na upinzani wa serikali tatu kwa sababu ya yaliyomo ndani ya rasimu hio iliopunguza mambo ya Muungano kutoka zaidi ya 30 hadi kukia saba. Ndio ukakuta wanamageuzi wa kweli hawazingatii jina la mfumo wa Muungano bali yaliyomo kwenye Muungano wenyewe na kwa sasa nguvu zimeelekezwa katika kuyafuta yale yatayokwenda kinyume na azma ya mamlaka kamili. Hoja zisizo na mashiko kama gharama za Muungano katika mfumo wa serikali tatu zenye kujitegemea zinaelekezwa zaidi kama khofu hususan kwa wazanzibari kama vile nchi hii haitaweza kujiendesha yenyewe wakati wahubiri hawa wanashindwa basi kuwaeleza watu kabla ya Muungano huu
TOLEO 08 - DISEMBA 2013

28

Waziri wa anaeshughulia Muungano Samia Suluhu [kulia]


huu na kuamini kama ndio maudhui makuu ya uundwaji wake. Sababu ni kuwa kumetokea taswira za aina mbili za upokewaji wa Muungano: upande mmoja hususan ndani ya mamlaka ya Zanzibar wakiamini uwepo wa nchi ya Zanzibar kama ni muhimu sana na adhimu katika maamuzi yoyote ya uwepo wa Muungano huu wakati upande wa pili ukijijenga zaidi katika safu za kuhakikisha Muungano huu utatafsiriwa kama ni wa nchi moja iliokamilika. Tuonavyo sisi Wazanzibari tulio wengi ni kwamba Zanzibar ni nchi iliokamilika na kujiendesha kwa misingi ya kimamlaka yanayoongozwa na ule uongozi mkuu wa ya Rais pamoja na serikali alioiunda baada ya kuridhiwa na uchaguzi unaotegemewa kuendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Katiba ya Zanzibar hususan baada ya mabadiliko ya 2010 imeonyesha kwa uwazi bila ya kuweweseka kwamba ni nchi kamili; na ikaenda mbali zaidi kuhakikisha mamlaka ya mkuu wa nchi hii hayatakuwa na kigugumizi kwa kuingiliwa na nguvu nyengine ndani ya Muungano hasa baada ya kuhakikisha kwamba ni Rais wa Zanzibar pekee mwenye madaraka na uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa bila ya ushauri wa yeyote kinyume na ilivyokuwa awali. Uthibitisho wa haya ni kura ya maoni ambayo hadi sasa inatazamwa kama ni mfano wa uchaguzi pekee ulioendeshwa kwa uwazi zaidi huku kundi la walipiga kura ndio likibeba nguvu ya zaidi ya asilimia 66 ya wananchi walioikubali hiyo kura ya maoni. Katika ilani ya CCM ya mwaka 2010 suala la mabadiliko ya Katiba halikuwemo. Wengi tunaamini

29

Miongoni mwa viongozi wakuu wa Tanzania, Waziri Mkuu Mizengo Pinda [kushoto] na Makamo wa Rais Mohammed Bilal

wao, ni lazima mabadiliko yoyote yathamini maoni ya pande mbili huru ili paweze kupatikana mua-

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

VUTA NKUVUTE, KIELELEZO CHA UANDISHI WA KIZANZIBARI


TANBIHI
Hii ni sehemu ya pili ya uhakiki ulioandikwa kwa lugha ya Kiingereza na FLAVIA AIELLO TRAORE kwa jina la INVESTIGATING TOPICS AND STYLE IN VUTA NKUVUTE BY SHAFI ADAM SHAFI. Hapa tumeutafsiri kwa minajili ya kuwapa wasomaji wetu mtazamo wa wengine kwa fasihi ya Kizanzibari. Sasa endelea.

30

31

Tufungue Kitabu

JAMBO la kufurahisha ni kuwa upinzani na mapambano kwenye riwaya hii hayajumuishi vitendo vya kutumia nguvu dhidi ya binaadamu wengine, bali maandamano na mashambulizi dhidi ya alama ya nguvu za kikoloni (kama vile mikahawa iliyotengewa watu wa matabaka fulani tu), kusambaza kazi ambazo zinachukuliwa na serikali kuwa ni haramu na uanzishaji wa gazeti liitwalo Kimbunga. Mambo yote haya yanaelezewa kwenye Vuta nkuvute kama kipimo cha majaribu ya mapambano ya kusaka uhuru. Hapa pia, kama ilivyo kwenye kazi

>

nyingi za Kizanzibari, tunaona uhusiano wa wazi baina ya jina na maudhi, ambao ishara yake inajidhihirisha wazi kwenye mtiririko wa visa unaomsaidia msomaji kuitafsiri riwaya katika muktadha wa kihistoria. Katika Vuta nkuvute, uhuru wa mawazo na kujieleza ni sehemu muhimu ya mapambano ya jumla, lakini baadhi ya wakati pande hizo mbili hukinzana. Kwa mfano, wakati mwengine mtu kusimamia haki yake kwenye mapenzi ni jambo la anasa linapolinganishwa na suala la ulinzi wa nchi, kama anavyoungama Denge katika ukurasa wa 145: Yasmin mimi najua kama unanipenda, na mimi nakupenda

vile vile, lakini kuna kitu kimoja napenda uelewe. Kuna mapenzi na wajibu wa mtu katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirikiana na wenzangu ambao wengine unawajua na wengine huwajui ili kuona kwamba nchi hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu, ina matatizo mengi na inahitaji kujitolea muhanga na mimi ni miogoni mwa hao waliojitolea muhanga kufa, kupona, potelea mbali. Tupo wengi tuliojitolea namna hiyo, tena wengi sana, maelfu. Maisha ya Denge yametolewa muhanga kwa kile akiaminicho, ikiwemo kutengwa au kuishi uhamishoni, na Yasmin anapaswa

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

kukubali majaaliwa yake ya upweke, na kushika njia akaenda zake. Kwa mara nyengine, Yasmin anakabiliwa na upotoshaji wa kikabila. Makutano yake na Bukheti, aliyewahi kuwa jirani yake Mombasa, yanapingwa na familia zote mbili, zikionesha khofu na dharau zao kwake kama mkando. Anadhalilishwa kwa kila aina ya maneno machafu, kama anavyoibuka na kutoa kauli kwenye ukurasa wa 254: Iko wapi heshima ya binadamu, ikiwa Muhindi anamwita Mswahili golo na Mswahili naye anamwita Muhindi ponjoro? Upatanishi uliofanywa na
32

marafiki wa zamani wa kifamilia na ambao ni watu wenye mwamko, unasaidia kuzitenga kando dharau hizo; na riwaya hiyo inamalizia kwenye muunganiko wa furaha, unaofunikwa na ghamu ya Yasmin. Tukio la mwisho lenye kumuacha msomaji na athari kubwa kutoka riwaya hiyo linaelezewa kwa nyimbo ya Kihindi ambayo Yasmin aliisikiliza Mombasa, na kudimka peke yake kutuliza roho yake na pia kuiimba kwenye kundi la taarab kisiwani Unguja. Daima Yasmin anauchukulia muziki kama kimbilio binafsi na beti za nyimbo hizo zinamkumbusha utamu na ukali wa uhuru.

Sasa natuangalie baadhi ya vipengele vya usimulizi wa riwaya hii ya Vuta nkuvute, tukichunguza zaidi muundo wa hadithi yenyewe, mitindo na matumizi ya lugha. Kama zilivyo kazi nyingi za Kizanzibari, kazi hii ina kiwango kikubwa cha kisanii, ikiwa imejengwa kwa kwa sura fupifupi kumi na nane, zinazokwendana na mjengeko wa matukio, mikasa, na mapigo yanayomfanya msomaji azidi kupata hamu ya kuisoma. Kipengele cha wakati kwenye riwaya hii kwa jumla kimetumika vyema ni nadra kukuta matukio yanayoelezewa kwa kurudi nyuma, kama lile la maisha ya Denge barani Ulaya. Mtiririko wa visa unasimulia

hadithi mbalimbali za maisha ya wahusika wakuu, wakati mwengine zinazopishana na wakati mwengine kuoana. Matukio mengi ni muhimu sana kwa mjengeko mzima wa riwaya. Ufundi huu wa uandishi unaipa riwaya sifa ya kuwa riwaya ya masimulizi bila ya kuondosha mantiki ya matukio kama lile la mazingira ya Roger na Salum kumtembelea Mwajuma na ugomvi uliozuka baina ya wanaume hao wawili. Mwandishi amefanikiwa kwa ustadi mkubwa kuweka mizani baina ya mbinu za kuonesha (ambapo matukio huwa yanasimuliwa na wahusika) na ile ya kuelezea (ambapo matukio yanasimuliwa na msimulizi, yaani mwandishi mwenyewe).

Uwasilishaji wa msimulizi aliye wazi na aliyejificha ni miongoni mwa vipengele vya ubora kwenye kazi za fasihi, na katika riwaya hii tangu awali kabisa msimulizi huyo huonekana kwa sura zote mbili na katika viwango tafauti. Kwa mfano, riwaya hii imejengwa kwa majibizano ambapo msimulizi anakuwa haonekani kabisa sio tu kwenye mazungumzo mafupi mafupi, lakini zaidi kwenye mistari mirefu ya kujenga hoja, lakini wakati mwengine majibizano haya huchukua nafasi muhimu sana katika kutoa taarifa kuhusu wahusika na au ujumbe muhimu, ambao mwandishi anauwasilisha kwa hadhira yake, kama dondoo zilizotajwa hapo juu za Denge na Pazi.

Ndani ya riwaya hii, msomaji anagundua pia matumizi ya kauli zisizo za moja kwa moja, ambako maneno au mawazo yanasimuliwa na msimulizi lakini yakinasibishwa kwa ukaribu sana na mhusika, kama vile kwenye ukurasa wa 49 pale mwandishi anapoelezea namna Yasmin alivyomuona Denge kwa mara ya kwanza: Kwa Yasmin huyo alikuwa ndo Mwaftika wa kwanza kuambiwa ametoka Ulaya. Shilingi mbili za kununua ukanda wa kufungia suruali yake zinamshinda, na ile suruali isiyokuwa na pasi aliyovaa imezuiliwa kiunoni kwa tai labda aliyorudi nayo kutoka huko Ulaya, na hivyo viatu alivyovaa, karibu vidole vingine vinataka kuchungulia nje. Itaendelea....
33

Fani

Polisi Zbar yatakiwa kuwa adilifu


raia na mali zao, jeshi hilo pia linapaswa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji na usimamizi wa sheria. Akizungumza na Kamishna mpya wa Polisi wa Zanzibar, Hamdani Omar Makame, aliyekwenda ofisini kwake Migombani kumsalimia, Maalim Seif alilitaka jeshi hilo kuondosha muhali katika kusimamia utekelezaji wa sheria, ili kuona kwamba sheria zilizotungwa zinafuatwa na kuleta ufanisi katika jeshi hilo na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Kamishna Hamdani amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa atatekeleza majukumu yake ya kusimamia sheria, ili wananchi waendelee kuishi katika hali ya amani na usalama. Aidha amesema jeshi la polisi kupitia kitengo chake cha Intelijensia kitaimarisha utafiti ili kupata taarifa za uhakika za kuweza kukabiliana na wahalifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Ameongeza kuwa atatumia uzoefu alionao katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano ili kuona kuwa kitengo hicho kinafanya kazi kwa uhakika na kuleta ufanisi uliokusudiwa. Kamishna Hamdani amesema mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 30 ndani ya jeshi la polisi, yametokana na mashirikiano aliyopata kutoka kwa viongozi na wananchi, na kuomba mashirikiano zaidi ili aweze kuyafikia matumaini na matarajio ya taifa katika ulinzi wa raia na mali zao

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema licha ya polisi kuwa na jukumu kubwa la kulinda usalama wa

>

Maalim Seif akizungumza na kamishna mpya wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame

Chanzo, MKR1znz.wordpress.com

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

34

Na Ally Hilal

Hekaya za Zanzibar
Mwanangu, ahsante, miye naishi kijiji cha Maukioni, nnakuja njini kutimiza utumwa wa shoga yangu aliyenileta huku, ni mzee sana tena wa miaka mingi, kutokana na hali yake, basi hawezi kuishi siku nyingi na na Alikohoa na kuugua kwa maumivu na baadaye akaendelea: Kanituma nintafutie kijana mwenye mapenzi na nchi hii ambaye ana dira nzuri ya maisha yake lakini sijamuona, nlikuwa narudi bila ya mafanikio na ndio maana baada ya kukuona weye nahisi unanifaa, nenda kwa huyu bibi ana kitu cha kukwambia, aitwa Bi Msiri Alikohoa na kuvuta pumzi yake ya mwisho na hapo ndi-

MEZA FUPA
TANBIHI
Ilipoishia toleo lililopita: Hakuna aliyemjali mgonjwa, kila mmoja alijishuhulisha na kazi zake, baadhi ya wauguzi walimtazama mgonjwa wa Miftaha kwa dharau bila ya kujali kuwa alikuwa katika hali mbaya kwani sumu ya nyoka ilikuwa inazidi kumuenea mwilini. Daktari wa zamu alikuwa amekaa nje anasoma kitabu cha riwaya. Miftaha alitoka hadi nje baada ya kuambiwa kuwa daktari wa zamu alikuwepo nje, alimkuta daktari amewacha kitabu na sasa anacheza karata na vijana wa mtaa. Ilimuuma sana kumuona daktari anacheza karata huku wagonjwa wakiumia bila ya matibabu, alimsogelea daktari na kumwambia kuwa kuna mgonjwa yuko hali mbaya.

35

WALIPOFIKA ndani alianza kuchukuwa jina la mgonjwa na maelezo mafupi, baada ya hapo alimchoma sindano ya kuondosha sumu ile lakini ilikuwa imeshaenea mwili mzima. Bi Tausi alijiona kuwa hawezi kuendelea kuishi, alimuomba daktari amruhusu Mwalimu Miftaha apite ndani kwani kulikuwa kitu akitaka kumwambia. Daktari aliomba apewe yeye ule ujumbe aukishe kwa Miftaha lakini Bi Tausi alikataa katakata, akidai kuwa kuagiza nmaviza Mwalimu Miftaha aliruhusiwa apite ndani kumsikiliza Bi Tausi; naye Bi Tausi alimtaka daktari asubiri nje mara moja ili azungumze na Miftaha.

>

.... Sasa endelea...


> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013
WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

po alipoaga dunia. Miftaha aliumia sana, alimwita daktari kumuangalia mgonjwa wake lakini alikuwa ameshapoteza maisha. Alirudi nyumbani kwao na kuchukuwa farasi wake, aliupakia mwili wa marehemu na kuupeleka kijiji cha Maukioni, alika kjijini hapo saa mbili usiku. Aliwaulizia ndugu wa bibi yule na kuwapata. Baada ya kuwakabidhi maiti wao aliwaaeleza yote yaliyomkuta bibi yule halafu aliaga na kuahidi kurudi baada ya siku mbili. Baada ya siku mbili, aliamua kwenda kijiji cha Maukioni pamoja na wenzake wawili, dada yake aliyeitwa Maimuna na mwalimu mwenzake aliyeitwa Suheli. Ilikuwa ni asubuhi mapema, vijana hawa walielekea kijijini kumtafuta Bi Msiri. Walikuwa na farasi wawili, mmoja alipanda Miftaha na Maimuna na mwengine alipanda Suheli. Walikia nyumbani kwa Bi Tausi ambaye alizikwa siku moja kabla, walikaa matangani kwa muda wa masaa mawili, walikaribishwa vizuri sana na wenyeji wao. Baada ya hapo waliomba wafahamishwe sehemu aliyokuwa akiishi Bi Msiri. Kijana mmoja mdogo aliyekuwa akianika nguo, alitakiwa awapeleke bondeni ilipokuwepo nyumba ya bibi huyu.
36

Msiri alisikitika sana alipotajiwa shoga yake mpenzi aliyepoteza maisha siku mbili tu zilizopita, aliwachangamkia wageni wake baada ya kubaini kuwa ndio waliouleta mwili wa marehemu. Aliumia sana kwa sababu safari ya Bi Tausi kwenda mjini ilikuwa ni kutekeleza agizo lake Bi Msiri aliyemtaka akamtafutie mtu mwenye uchungu wa nchi yake, mzalendo wa kweli na si wa kinaki. Baada ya kushindwa kutimiza lengo lake aliamua kurudi kijijini kwao na hapo ndipo yakamka matatizo. Hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya kifo chake. Bi Msiri aliwakaribisha chini ya mwembe na kuwatandikia mkeka. Bibi huyu alikuwa malenga mzuri sana, alizungumza maneno kwa ufupi sana lakini yalibeba maana nzito, Kiswahili chake kilimfurahisha sana Miftaha. ************************ Wanangu natakalitema fupa, nimelimeza likanikwama, hakuna anayejua lakini ntaka wajuvya nyiye, naamini mumetoka kwenye udongo wenye rutuba nzuri, ingawa maji machafu huuathiri udongo wenu lakini naamini kuwa bado kuna michirizi ya maji sa ipitayo kwenye udongo huo, pia hewa sa kutokea pande za janibu ya kaskazini na kusini yake zaweza ipunguza sumu hii ya hatari. Nimeona kuwa kumeza fupa si suluhu ya kunifanya nisiwe na njaa tena, wala si sababu ya kuwatia njaa mbwa wanaohaha huku na kule kwa kulitafuta fupa. Nataka mujuwe wanangu kuwa mimi nimekula chumvi sana. Hakuna anayejua hata mmoja kuwa mimi nimepindukia na kupindukia kuishi, nayajua hayo wasiyoyajua mababu wa babu zenu, katika wahenga na miye nimo na nshahengeka. Nayajua hayo meusi yaitwayo meupe na meupe yaitwayo kijani. Umri wangu unapotea sasa, hebu tulieni niwajuvye. Nina miaka mia mbili, na nimeishi kijijiini hapa tangu baada ya baba yangu kuuwawa na familia yangu yote isipokuwa mimi. Mimi peke yangu nilisalimika, nilikosa bahati kwetu, wazazi wangu walinifanya kama mtoto waliyeniokota. Nyumbani kwetu alikuwepo mfanyakazi, nilimhurumia

sana kwa kazi nyingi alizokuwa nazo, hili liliwakera wazazi, na kwa vile nilikosa bahati walizidi kulifanya hili kama kosa la jinai. Niliambiwa kuwa kuanzia wakati huo nitakuwa mfanyakazi wa ndani na yule mfanyakazi alifukuzwa nyumbani. Maisha yangu yalikuwa magumu pamoja na kuwa niliishi na wazee wangu tena hawakuwa na maisha magumu. Baba yangu alikuwa waziri wa ardhi na majengo. Siku moja, nilitoka kuelekea mtoni kufua kama ilivyokuwa kawaida yangu. Nilikusanyiwa nguo za nyumba nzima, sijawahi kulalamika hata siku moja, nilizifua nguo zote. Baada ya kumaliza nilirudi nyumbani na kumkuta mama yangu kwenye mlango wa jikoni akiwa ameshafariki, alikuwa anavuja damu kichwani. Nilipoingia ndani niliwakuta ndugu zangu wawili wa miaka kumi na tano wameshafariki, hawa walikuwa pacha, nilichanganyikiwa na kuanza kuita kwa sauti kubwa iliyojaa kitetemeshi. Hakuna aliyeitika, nililia sana, niliamua kuingia chumbani kwa baba ambako moyo wangu ulizidi kushituka nilipomkuta baba yangu amelala kitandani, kichwa chake kilikuwa kinaninginia chini na miguu ilikuwepo kitandani. Alikuwa amekatwa katwa mkono wake na kichwa chake kilivuja damu nyingi. Sikujua nifanye nini, nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza kuhusiana na aliyefanya mauji yale ya kutisha. Nilibaini baada ya kuokota kitambulisho chenye picha ya mtu. Kilikuwa ni kitambulisho cha asa wa polisi kilichokuwepo sakafuni, pia kilikuwepo kipochi mlangoni. Nilikifungua na kukuta makaratasi mengi, nilipojaribu kukifungua kikaratasi kimoja niliona kimeandikwa jina la asa yule yule. Baada ya dakika mbili nikiwa nimezubaa pasipokujua cha kufanya, nilisikia mvumo wa gari nje ya nyumba yetu. Nilijicha mvunguni mwa kitanda cha baba. Niliweza kuviona viatu vya buti nyeusi. Nilitamani niione sura yake lakini sikuweza kuiona kwa wakati ule. Nilisikia sauti mbili zikijinadi na kusema bila woga. Pochi yangu na kitambulisho hivi hapa Yule mwengine akajibu:

Mawaziri kama hawa tunafyeka sisi, hawatuyumbishi, hivi unaijua sababu ya kuteketea kwa hili jamaa? Aliuliza yule askari. Najua, huyu juzi alisema kuwa raisi inabidi abadilike asiburuzwe na matakwa yake kwani yeye amewekwa na wananchi Ah! Kumbe wewe wajua hivyo tu! Huna ujualo

Walianza kubishana, niliroa jasho na miguu ilinitetemeka huku masikio yangu yakisikiliza zile sauti. Wewe hujui, huyu jamaa amepewa usimamizi wa ardhi, ameamua kuwatafuta wananchi wenye umiliki halali wa eka zao na wengine amefanikiwa kuwarudishia eka zao za mashamba na hayo mengine yamefuatia juu tu, na sasa wameamua kuuziba huu mdomo Haya yote niliyasikia, nilifanya kuchungulia kidogo nikaweza kuziona sura zao. Alikuwa ni asa wa polisi pamoja na waziri ambaye alikuwa anakuja sana nyumbani, alikuwa ni raki wa karibu sana na baba yangu Ama kweli kikulacho kinguoni mwako, waziri huyu huyu ndiye aliyemuahidi baba kuwa hamu yake ni kuona familia yetu na familia yao zinazidi kuungana kupitia ndoa za watoto wao, yaani mimi na mtoto wake waziri huyu. Baada ya muda walitoka nje na kuondoka. Nilijifungia chumba cha mabandani hadi usiku na nikaondoka. Nilikuwa nikizisikia sauti za watu waliokuwa wakiingia na kutoka. Ilipoka usiku nilitoka na kuelekea chumba cha marehemu baba yangu, mwili wake ulikuwa umeshaondoshwa, na hata miili ya mama na wadogo zangu haikuwepo tena. Iliniuma sana, nilichukuwa begi langu la nguo na kuondoka nikiwa sijui ninapokwenda. Waswahili wanasema Kua uone mambo! Itaendelea

37

Ilikuwa ni kibanda kidogo kilichoezekwa kwa makuti, baadhi ya sehemu kilizibwa kwa makuti, nje alikuwepo bibi anatwanga unga wa muhogo. Alikuwa amekaa kwenye gogo la mnazi, alivaa nguo zilizochakaa sana. Kanga yake iliandikwa NIMESTAHAMILI TABU KUPATA SI AJABU Ujumbe huu ulimfanya Miftaha atabasamu peke yake, walisogea alipokuwepo Bi Msiri na kumsalimia. Shikamoo bibi Bi Msiri alikuwa haoni vizuri lakini aliweza kusikia vizuri, aliwaitikia na kuwauliza maswali mengi. Marahaba wanangu, sijawajua nnani nyiyee! Macho yenyewe yankwisha zake, sioni taaaa ule nkono wangu. Miftaha alijitambulisha kwa kutoa mkasa wa Bi Tausi. Bi

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Nitabaki Zinjibari
Siuki sina nendapo, pano ni pangu ngamani Nendapi we uonapo, nifikie kileleni Nasema mie sinapo, pengine kwa duniani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani Ingelikuwa nnapo, ningetoweka zamani Kitambo ngekuwa sipo, nishauka kiamboni Pa kwenda mie hapapo, pangu ni hapa shinani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani

Lingekuwa Lakujua
Laitani ningajuwa, hiyino ndio safari Tiketi singenunuwa, kwanza ningajishauri Kamwe singeliamuwa, chombo nikakiabiri Lingekuwa la kujuwa, kwamba nendako ku mbali Akiba ningachukuwa, mapeni na maakuli Haepuka kuishiwa, nisijafika mahali Ningajuwa ningajuwa, njia ina majangili Misafara huvamiwa, zikatwawa zote mali Bunduki ninganunuwa, na upanga haamili Halekuwa la kujuwa, kupita kwenye nadhari Kwamba niliyoamua, yena ugumu safari Kufumba na kufumbuwa, nedhani ningewasili Bali madhali ya kuwa, nishaianza safari Japokuwa sikujuwa, ugumuwe na hatari Kurudi havitakuwa, naiandama kwa ari Lolote litalokuwa, njiani litalojiri Nitalipiga kifuwa, nipambane kijasiri Pindu nitalipinduwa, ama roho ihajiri Kwa hapa nishapokuwa, siwazii kughairi Kurudi nyuma si dawa, hivyo sitawa rijali Rijali akiamuwa, shoti itimu dhamiri Mohammed Ghassani 7 Desemba, 2013
39

Si dharuba ya upepo, unovuma baharini Wala si kwa mitetemeko, ivunjayo miambani Sitaseguka nilipo, kwa nguvu au amani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani Nimeshakula kiapo, siondoki asilani Hapa mie takuwepo, leo na kesho amini Nitakita papo hapo, hasa mwanitakiani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani Naapa sijaonapo, sawa na kwetu nyumbani Na kila nitembeapo, Unguja i akilini Kwa mfanowe haupo, Zenji ni nambari wani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani Nawaaga mliopo, narudi zangu mwambani Wasia ni huo hapo, watoka mwangu moyoni Cha kukicha hakipo, Zenji ipo kifuani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani. Mbarouk Sharif (Mnyonge wa Nyali), Waco, Texas Marekani

38

BETI BETI
YA
LADHA

YA

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

LADHA

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

Mashujaa wa Zanzibar walishindwa kabla mashindano kuanza


Na David Kambona
40

CHALLENGE CUP 2013

Michezo
Ikumbukwe mwaka jana walishika nafasi ya tatu wakiwafunga ndugu zao wa Bara lakini safari hii waliishia hatua ya makundi. Moja kati ya sababu kubwa ya Zanzibar kushindwa safari hii na kubwa kuliko zote ni kuwa Zanzibar ilishashindwa tangu ilipotwaa nafasi ya Tatu mashindano yaliyopita baada ya wachezaji wa Zanzibar kugawana fedha. Jambo hilo liliwakera viongozi wa ZFA wakati chama kilipokuwa kikiongozwa na Ibrahim Amani Makungu. Mmoja kati ya wachezaji waliokumbwa na mkasa wa kufungiwa alikuwa nahodha wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambaye safari hii hakuwemo kikosini. Wapo wachezaji wengine ambao hawakujumuishwa kikosini pia kama Agrey Moris ,Abdihalim Homoud,Twaha Mohammed japokuwa Nassor Cholo Masoud aliitwa. Jambo la pili ambalo liliikosesha Zanzibar ushindi safari hii ilikosa kabisa kupata japo hata mechi ya kiraki katika kujiandaa na michuano hiyo japo ilijaribu kuomba mechi ya kiraki dhidi ya Kenya lakini ilikataliwa kwa kuibagua kuwa haitambuliwi na Fifa. Huu ulikuwa mwiba mkali kwa Zanzibar Heroes mwiba ulioanzishwa na Kim Poulsen, meneja wa timu ya taifa ya Tanzania. Zanzibar Heroes ilibakia kuwa yatima aliyeachwa katika kina kirefu cha Bahari bila kupata msaada wowote na ndipo ilipoamua kucheza mechi ya kiraki na klabu ya ndani ya Zanzibar. Lakini kabla ya Zanzibar kukwea pipa kwenda nchini kenya baadhi ya wadau walianza kulalamika kuhusu uteuzi uliofanywa na kocha Salum Bausi kwa kuchagua wachezaji wa upande mmoja wa Unguja kitu ambacho kiliigawa tena Zanzibar Heroes na kuonekana kuwa ni timu isiyo na usawa katika uteuzi. Ni dhahiri kuwa tayari Zanzibar Heroes ilishaaingia katika msongo wa mawazo kwa wachezaji,kocha,pamoja na viongozi pasina kusahau mashabiki. Zanzibar Heroes ambayo iliagwa na naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Bihindi Hamad Khamis waliondoka huku wakiahidiwa zawadi kem kem. Tuje kiwanjani Zanzibar Heroes ilifungua dimba na Sudan Kusini ambayo ndio mechi pekee walioshinda. Yawezekana ilikuwa ni k a m a b a 41

KUANZIA tarehe 27 Novemba hadi 12 Disemba kila mwaka huwa kunafanyika mashindo ya Chalenji ambapo nchi za Afrika Mashariki na Kati huwa zinashiriki. Tanzania huwa inawakilishwa na timu mbili kutokana na taratibu za kitawala za nchi mbili ambazo zimeungana lakini hujitegemea kwa baadhi ya mambo, yakiwemo ya michezo. Moja kati ya timu iliyokuwa ikishiriki ni Zanzibar Heroes - Vijana wa Mzee Sheikh Karume Muasisi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar - ambao walikuwa kundi moja na Sudan ya Kusini, Kenya na Rwanda. Timu hiyo iliishia kushinda mechi moja na kufungwa mechi mbili. Lakini jambo la msingi ni kujiuliza kwa nini mabingwa hawa wa mwaka 1995 wamechemka mapema?

> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014

>

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR


Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakifanya mazoezi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kabla ya kuondoka kwenda kushiriki mashindano ya Challenge Cup 2013 huko Kenya

RAIS WA ZFA
Naelewa kila kitu kinacholikwamisha soka letu na nazijua shida mlizonazo hivyo naomba mniamini kuwa nitasimamia kanuni na katiba katika kuziondoa na kwamba mjue wajumbe sote tutakuwa na hadhi sawa na hakuna alie juu ya mwengine kikubwa ni maelewano tu 42 43

michuano hiyo. Zanzibar ilishinda magoli mawili kwa moja mchezo ambao Zanzibar ilicheza lakini sio kwa kiwango ambacho wengi wetu tulikitegemea. Jahazi la Zanzibar lilionekana linazama baada ya timu hiyo kukutana na Rwanda na baadaye Mwenyeji Kenya ambapo katika mechi zote mbili Zanzbar Heroes iliishia kupata vipigo. Lakini kwa nini hasa timu yetu hii inafungwa au kwa nini ina> WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013

fanya vibaya kwani hata Brazil huwa inafungwa. Sababu nadhani ni mipangilio mibovu ya kiundeshaji. Tutazame mechi ya kiraki Zanzibar ingeweza kuomba mechi ya kiraki na nchi zifuatazo kama Somalia, Eritrea au hata timu za vijana za Uganda, Rwanda au hata Burundi kwa sababu tayari Kenya walishaweka kizingiti cha kuwa Zanzibar haimo katika Fifa . Ni wazi Zanibar ilikwisha shindwa kabla ya kukwea pipa

shida moja kuu ambayo inaiumiza Zanzibar hasa katika maendeleo ya kisoka ni kukosa uzalendo ,kutokuwa na uchungu ,kukata tamaa, na uwekezaji mbovu. Hadi kuka sasa bado hatujapata hasa aina ya mchezo wetu binafsi kiwanjani. Kwa Zanzibar Heroes michuano pekee ya kimataifa ni mashindano ya Chalenji. Kama ingekuwa ipo katika uangalizi mzuri ndio timu ambayo ingechukua ubingwa wa mashindano haya mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote kwani ndani ya miaka sita au saba ijayo nchi kama Kenya, Uganda na Rwanda sitashangaa kama zitakuwa zinaleta timu za vijana katika mashindano haya kwa sababu tunaona tayari baadhi ya wachezaji wao wameanza kupata nafasi za kucheza soka katika nchi za Magharibi.

Lakini Zanzibar na Tanzania Bara bado hatujaweza kufanikiwa kwa hilo. Wachezaji wengi wa Zanzibar ukiwatazama wanapocheza katika timu ya taifa ya Zanzibar ni wachezaji ambao wanacheza soka wakiwa wana vipaji ambavyo havikuendelezwa na huu ndio umekuwa ugonjwa wa kudumu. Binafsi ningeona ZFA kuwa ina watu wa maana kama wataaliangalia suala hili kwa utimilifu baada ya mashindano haya kumalizika. Tungeanza mchakato wa kutafuta timu bora itakayoshiriki michuano ya Chalenji mwakani kwa kuwafuatilia wachezaji kwa ukaribu kwa sababu bado sijashawishika na uteuzi unaofanywa sasa katika Timu ya Zanzibar. Je, ni kweli makocha wanafanya kazi wanavyositahili? Jukumu la timu ya taifa sio la kocha mmoja ni

la makocha wote wa Zanzibar na benchi la ufundi ni jambo la kitaifa sidhani kama kunakuwa na takwimu za kuwatazama kila baada ya mechi za ligi kujua uwezo, tabia, maana kuna mambo mengi ya kiufundi kujua faida na hasara za mchezaji za kila mchezaji. Ninamaliza kwa kusema kama hatutazingatia mambo haya na tukiendelea kuchagua timu kiholela hatutoweza kufanya vizuri katika mashindano yoyote kwani mpira ni mchezo unaochezwa mchana kweupe. Hauchezwi kizani kana kwamba hatutaona makosa. Tutazame kwa nini tunajihujumu sisi wenyewe; kweli wanacheza wachezaji kumi na moja lakini wakifungwa tumefungwa nchi nzima . Yatupasa kuwa na uchungu

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET

TOLEO 08 - DISEMBA 2013

>

You might also like