Professional Documents
Culture Documents
Kitabu Cha Sala 1
Kitabu Cha Sala 1
YALIYOMO KITABUNI
(1) Neno la mwandishi 1 (21) Imamu akikosea 42
(2) Usafi-Tohara 7 (22) Adhana 48
(3) Kuoga 9 (23) Sala ulizoziacha 49
(5) Kutia udhu 9 (24) Sala ya msafiri 51
(6) Uchafu-najsi 13 (25) Sala ya ndegeni 54
(7) Damu 14 (26) Sala ya mgonjwa 55
(8) Dua za udhu 16 (27) Sala za sunna 58
(9) Kutayammam 17 (28) Sala za usiku 61
(10) Sala 22 (29) Witri 64
(11) Sala za faridha 25 (30) Taraweh 67
(12) Nguzo za sala 26 (31) Sala ya tawafu 69
(13) Namna ya kusali 29 (32) Kuomba haja 70
(16) Sala ya jamaa 34 (33) Kupatwa mwezi 73
(20) Yanayoharibu sala 38 (34) Sala ya maiti 74
basi (Muhammad) vumilia wanayoyasema na mtakase Mola wako (kwa kusoma sifa
zake) na msifu na kumshukuru (kwa kutaja wema wake) (yaani MUABUDU) kabla
kuchomoza jua na kabla kutua. Na nyakati za usiku mtakase (pia) na ncha za mchana ili
uridhike ( na utakayopewa).
(wafasiri wa Qur-an wengi, ikiwa ni pamoja na Skeikh Abdulla Saleh, wanasema kuwa sala tano
zimetajwa katika aya hii. Tazama tafsiri ya sheikh . Abdulla. Surat 20-130).
UTANGULIZI
Kitabu Kipya cha Sala
Chapa ya mara hii ni kitabu chengine kabisa kwani takriba nimefuata sawa sawa maagizo
niliyoyapata kutoka kwa wasomaji wa chapa za kabla yake isipokuwa kidogo sana. Pia nimeyatoa
mengine na kuongeza yale ambayo umuhimu wake umefurutu ada. Muhimu ni kuwa hichi kitabu
ni kidogo hakiwezi kuchukua mambo mengi. Kwa hivyo tutayaacha baadhi hasa yale yenye
kukataliwa na mashekhe wengine. Ndio maana mara nyengine hutumia neno baadhi kama baadhi
ya sunna na mara nyengine hata hatusemi baadhi ujuwe kama yako mengine tumeyaacha.
Naomba samahani kwa makosa yote ya lugha na uchapishaji na mengineyo, makosa
mkituonesha itakuwa bora tutayasahihisha katika chapa za baadae.Kwa kukusudia tumekariri
(tumeripiti) baadhi ya mambo usijali.
Na aliyemuusia:-
Nakuusia na sala
Usiiache Allah allah
Tutosheke na maneno hayo.
au
Kuanzia leo huna haja ya mwalimu wala somo wa kukuosha ujusi wala kukutoa kizuka! Au vipi?
Mola akuekee. Amyn.
Namna ya kuoga
Kuoga kama tulivyosema ni kutia nia na kueneza maji mwili wote, inatosha. Ukitaka ukamilifu
wake kwa ufupi ni hivi:-
(1) Tia nia kama tulivyoeleza.
(2) Osha viganja.
(3) Osha tupu mpaka ziwe safi.
(4) Osha midomo na pua.
(5)Tia udhu kamili ila inatosha kusema usiikamilishe.
(6) Osha kichwa upande wa kulia kisha wa kushoto.
(7) Osha uso, masikio, shingo, na mwili wote upande wa kulia kisha wa kushoto.
(8) Unapoosha iwe unapitisha mkono na kusuguwa kwa sabuni ikiyumkinika, sabuni sio sharti.
(9)Kuhusu kuosha maiti tumetoa kitabu kiitwacho Huduma za Maiti jipatie ukisome.
(10) Sio lazima kufuata mpango huu.
Kutia Udhu
Muislamu akitaka kusali, kuhirimia hijja au umra, na hata kukamata mas-hafu, kwa kauli ya
maulamaa wengi, ni lazima awe na udhu. Ni jambo la maana sana unapojifunza kutia udhu na
kusali ujifunze kwa kumtazama anayejua ili umuige usitosheke na maelezo haya machache.
Ukishajua kutia udhu na kusali mwambie anayejua akutazame kama unafanya ndivyo.
Lazima au Sunna
Wengine wanasema ni sunna kubwa na wengine wanatilia mkazo kuwa ni lazima:-
(1) Kufikisha maji mpaka chini ya mashina ya ndevu, wengine wanasema ni lazima ndio udhu
ukamilike.
(2) Kutokatiza. Usitawadhe kidogo kisha ukakamalisha baadaye. Na hivi pia wengine wanasema
ni lazima.
(3) Kutia udhu kwa kufuata nidhamu, mpango. Na ni kuosha kwa mpango tuliotaja kwa mfano
usitangulize miguu kabla ya mikono. Na pia wengine wanasema kutawadha kwa mpango ni
lazima.
Sunna za Udhu
(1) Kusuaki kabla ya kutia udhu.
(2) Kuosha viganja kabla kutia udhu.
(3) Kuosha viungo mara tatu tatu.
(4) Kuosha masikio ndani kisha nje kwa maji mengine
(5) Kuvisugua viungo au kupitisha mkono ukitawadha.
(6) Kuvibagua vidole yaani kupitisha kidole chenye maji baina ya vidole.
(7) Kuanza na kiungo cha upande wa kulia.
(8) Kutilia udhu mkono wa kulia.
(9) Kuzungusha pete hasa ikiwa imebana. Ikiwa imebana sana ni lazima.
(10) Kuelekea kibla ikiyumkinika.
(11) Kukaa kitako ikiyumkinika.
(12) Kuomba dua baada ya kutia udhu.
(13) kusali sala ya rakaa mbili baada ya kutia udhu, baada ya dua ya udhu.
Masikio ni sehemu ya kichwa kwa hivyo kukosha masikio wengine wanasema ni lazima sio hiari
kama nilivyosema kabla kidogo.
Yanayoharibu Udhu
Udhu unaweza kuharibika ikabidi utie tena. Yanayoharibu udhu ni mengi. Baadhi ya hayo ni:-
(1) Kutoka damu popote mwilini au usaha mwingi au kidogo ukiwa na damu.
(2) Kutoka chochote kwenye tupu mbili hata pumzi au sauti.
(3) Kutapika au kucheua.
(4) Kutamka, inasemekana na hata kusikiliza, kila baya kama kusema uongo, kusengenya,
kufitinisha, kutukana, kulaani, kuapiza na kama hayo.
(5) Kutazama mwili wa mwanamke ajnabi kwa kuupekuwa kwa macho. Mwanamke kinyume cha
mwanamme.
(6) Kulala usingizi au kusinzia ikatoka fahamu.
(7) Kugusana na uchi wowote.
(8) Kutazama uchi na zaidi kutazama kwa hamu.
(9) Kugusa najsi maji maji.
(10) Kupoteza fahamu hata kughumiwa, kuchanganyikiwa.
(11) Kucheka au kutabasamu ndani ya sala kunaharibu udhu kwa kauli ya maulamaa wengine..
Wengine wanasema inaharibika sala tu.
(12) Kumshirikisha Mola, kushiriki. Tunamuomba Mola atuepushe na kila aina za shirki.Amyn.
(13) Kwa mujibu wa kauli ya mashekhe wengi ni kuwa kumgusa mwanamke ajnabi kwa mikono
na hata mwili kwa mwili kunatengua udhu. Kwa mwanamke ni kinyume chake.
(14) Kugusana na maiti hata wa kibinaadamu.
(15) kugusana na mbwa au nguruwe.
(16) Kutia udhu uchi na kukaa uchi mbele za watu hupelekea kutoka udhu.
Yale yenye khitilafu kuwa hayatengui udhu nimeyatia kwa kuchukuwa hadhari zaidi na kuepuka
khitilafu ili mtu asiharibikiwe ni bora au vipi? Na anayetaka kuyatoa aulize kwanza apate fikra za
mashekhe. Na ni kama nilivyosema haya ni baadhi tu.
Makruhu
Yasiyofaa kufanya au kupelekea kuharibu udhu pia si kidogo. Haya huitwa makruhu baadhi ya
hayo ni:-
(1) Kutumia maji mengi-israfu.
(2) Kutumia maji yamoto sana au baridi sana.
(3)Kuzidisha mara tatu tatu.
(4)Kuzungumza.Inasikitisha watu wengi huzungumza ndani ya kutia udhu.
(5) Kuvipiga viungo kwa maji.
(6) Kutia udhu usimama.
(7) Kusimama juu ya pahala pachafu.
(8) Kutia udhu chooni. Sio vyoo vya aina zote.
(9) Kutilia udhu vyombo vya dhahabu au fedha.
(10) Kutofikisha mara tatu tatu.
(11) Kutia udhu uchi pahala siri. Tumetaja kuwa ikiwa si pahala siri udhu haushiki, haukai. Na
Mola Anajua zaidi.
Najsi (Uchafu)
(1) Kila chenye kutoka kwenye tupu mbili ni najsi kama mavi, mkojo, manii, madii, madhii,
damu maji, maji yatokayo baada ya hedhi, mdudu, minyoo vijiwe na kama hayo.
(2) Matapishi na macheuo.
(3) Damu hata ile inayotoka puani na ya viumbe wengine ni najsi isipokuwa samaki kwa
madhehebu yetu. Hata hivyo si muruwa kusali na damu ndani ya mwili au nguo hata hiyo ya
samaki ila iwe hapana budi.Lisilo budi hutendwa.
(4) Mizoga (maiti).
(5) Mbwa na nguruwe.
(6) Vya kulewesha, maji maji.
(7) Usaha ukiwa na damu. Bora kuchukuliwa kuwa usaha wowote ni najsi.
Damu
Maelezo ya damu ni marefu yanahitaji kitabu peke yake, karibu kitatoka. Kwa hivyo hapa tutatia
kwa ufupi yale ambayo ni vibaya kuyapuuza.
Damu ni najsi na ni namna nne.
(1) Ya kawaida, hii hutoka kwa kujikata au kujichoma pia huweza kutoka bila mpango kama vile
mdomoni au puani.
(2) Ya Nifasi, hii ni kwa kuzaa hata kama hakutoka mototo.
(3) Ya istihadha, hii hutoka ukeni bila ya kuwa ya kawaida wala nifasi wala hedhi.Utaifahamu
katika maelezo yafuatayo. Damu hii nyekundu wekundu wa kawaida. Haina harufu. Ni nyepesi.
(4) Ya hedhi,hii hupata wanawake wanapofikia utu uzima takriban kila mwezi katika hali ya
uzima. Wekundu wake umekwendea weusi, umekoza. Ina harufu mbaya. Nzito nzito.
Kuhusu uzito na wepesi imekusudiwa ukichukua damu ya istihadha nusu kikombe kwa mfano na
ya istihadha nusu kikombe vilevile basi ya hedhi itakuwa ndiyo nzito. Si mwambii mtu afanye
hivyo lakini anaweza kukisia. Na ikibidi nimeshasema kabla lisilo budi hutendwa.
(1) Wakati wa kuanza kutia udhu mashekh wengi wanasema kuwa hii bismillahi
ni lazima:-
(2) Kusukutuwa:-
Kutayammam
Kutayammam ni kutumia mchanga badala ya maji kwa kuoga au kutia udhu. Wengi wetu
zinatupita sala kwa kukosa maji au kushindwa kuyatumia au kukataa kutayammam. Kuna sababu
kama tatu hivi za kujiingiza katika makosa hayo:-
(1) Dharau. Mtu huona atasali akipata maji au atapoweza kuyatumia, wala hajishughulishi kwa
hoja kuwa atasali vipi naye hana maji. Hiyo si sababu ya kuitoa sala ndani ya wakati wake wala
hakuna nyengine, labda kuwa umelala au umesahau. Na si kawaida. Mtume (S. A. W.) aliulizwa
ni ipi amali bora kabisa akajibu kuwa ni sala ndani ya wakati wake, kama tulivyosema kabla.
Tutafute njia ya kujitoa katika vizuizi ili tusali ndani ya nyakati zake.
(2) Kuona kuwa kutayammam ni kitendo kigeni hivi wala hajapatapo kukifanya na pengine
hajamuona mtu hata mmoja kutayammam.
(3) Kuna na waliokuwa hawajui kutayammam. Au hata hawajasikiapo kusikia, mambo haya ni
mageni kwao hawajapatapo kuyaona. Na pengine akikifanya, watu wote watamkodolea macho na
pengine waulizane anafanya nini yule!?
Sababu za kutayammam.
(1) Kuyakosa maji baada ya kuyatafuta kwa juhudi zote.
(2) Kudhuriwa na maji au kuchelewesha kupoa maradhi.
(3) Kuyahitajia maji kwa haja kubwa kama kunywa. Na hapana mengine.
(4) Kuwa maji ni baridi bila kiasi, hayagusiki, wala hapana uwezekano wa kuyazimua.
(5) Ukingojea maji utaikosa sala au utakuwa wakati umeshatoka. Na hii hasa ni sala ya idi au ya
maiti. Hatokezea makaburini, mavani hakuna maji ya kutosha au mifereji ni kidogo, waliongojea
zamu za mifereji wakakosa kumsalia maiti.. Usisali nje ya wakati kwa kuwa huna maji au
mchanga.
Sharti za Kutayammam
(1) Kuepo japo moja ya sababu za kutayammam ambazo tumeshazieleza hapo mwanzo.
(2) Kuwa na mchanga safi. Maulamaa wengine (sio wote) wanasema pia uwe haujatumika.
(3) Maulamaa wengine (sio wote) wanasema kutayammam baada ya kuwa umeshaingia wakati
wa ile haja.
Namna ya Kutayammam
(1)Tia azma yaani tia nia ya kujitoharisha lile ulilokusudia.
(2) Soma kamili kama ukitia udhu kwa maji.
(3) Weka au pangusa viganja vyako viwili vilivyokunjuliwa juu ya mchanga.
(4) Pangusa uso wote kwa marefu kwa viganja venye athari ya huo mchanga mara moja tu. Kabla
ungeweza kuupuliza kupunguza vumbi la mchanga.
(5) Weka au pangusa tena mara ya pili viganja vyako viwili vilivyokunjuliwa juu ya mchanga ule
ule. Maulamaa wengine wanasema inatosha kuweka mchanga mara moja tu.
(6) Pangusa mkono wa kulia kwa athari ya mchanga wa kiganja cha mkono wa kushoto na
pangusa mkono wa kushoto kwa athari ya mchanga wa kiganja cha mkono wakulia. Mikono
hupanguswa mpaka vifundoni tu vilipoanza viganja, panapovaliwa saa si dhiraa kamili. Na
hupanguswa kwa kuanzia nyuma ya viganja ncha ya vidole mpaka chini kifundoni na ndani
kiganja chote.
(7) Usisahau nidhamu, uso kabla viganja.
(8) Ukinyanyua mikono kupangusa uso ni uzuri ulete takbir.
(9) Pasiwe na muda baina ya kupangusa uso na viganja.
Jee umejaribu, umeona ugumu wowote!.Basi usiitowe sala ndani ya wakati wake kwa kukosa
maji.Wakati hauna mbadala ama maji yanao na ni mchanga.
Yanayoharibu Tayammam
(1) Ni yale yote yanayoharibu udhu.
(2) Kuondoka ile sababu ya kutayammam.
(3) Kutayammam nje ya wakati na hii kwa wale wanaosema kutayammam iwe wakati
umeshaingia.
(7) Kuna sala husaliwa hapa, nayo pia imetiliwa mkazo. Inaitwa sala ya baada ya udhu. Ni rakaa
mbili, bora uisali. Hakikisha kuwa wakati unatosha na pia utaiwahi jamaa. Usiache jamaa
ikakupita.
SALA
Kuna mambo mengi yahusuyo sala ambayo ni lazima mtu ayajuwe. Mabingwa hawajayaeleza
yote katika kitabu kimoja. Ukitaka kuyajua yote au mengi itabidi usome na vitabu vyengine.
Soma hapa haya machache:-
(1) Mtu azisali sala zote za faridha jamaa msikitini. Mwanamme jirani na msikiti asiposali faridha
msikitini sala zake huwa hazitimii au ni kama hakusali ila kwa sababu za kukubalika. Sala ya
jamaa ni mara 27 ya mtu peke yake na Mola Humuongeza Amtakaye.
(2) Sala za sunna bora kuzisali nyumbani ila zile kama tahiyyatul masjid, ya baada ya kutufu,
tarawehe na ziko nyengine sunna za kawaida tu kwa mfano mwenye kufanya itikafu atasali zala
zote msikitini. Tutaeleza itikafu pahala pengine..
(3) Ama mwanamke atasali nyumbani kwake sala zote isipokuwa kama zile tulizosema na kusali
chumbani kwake ni bora zaidi.
(4) Siku ya Ijumaa sala ya Ijumaa ni lazima sio pendekezo.
(5) Msafiri akikamilisha masharti ya kusali safari basi lazima asali sala ya msafiri asilinganishe
na kufunga ambako ni bora kuliko kuakhirisha.
(6)Hakuna sababu ya kuacha sala ila hedhi, nifasi, utoto na kichaa. Kama huna hata moja ya hizo
basi usiache sala ndani ya wakati wake kwa hali yoyote ile.
(7) Sala ulizoziacha lazima uzilipe hata kama hujuwi ni ngapi au ni ujanani au popote pale. Pia
ulipe na suna za asubuhi na sala za witri.
(8) Maulamaa wengine wameeleza juu ya kafara ya mwenye kuacha sala. Na wengine
hawakulipa umuhimu jambo hili. Tutaeleza pahala pengine inshaallah. Kafara ni adhabu au
kutiwa adabu ya kufanya kosa. Mfano wa kafara ni kama kuambiwa ufunge siku kumi au uchinje
mnyama au ufunge miezi miwili mfululizo au uwalishe masikini na kama hayo.
(9) Ni uzuri kuvalia kwa kupendeza wakati wa sala na kujitia uturi yaani manukato hata kama
mtu yuko peke yake. Yawe kidogo sana ama mwanamke akiwa atasali nje au msikitini haifai
kufanya hivyo.
(10) Mtu awe anajisikia kisomo chote akisali peke yake.
This document was created with Win2PDF available at http://www.daneprairie.com.
The unregistered version of Win2PDF is for evaluation or non-commercial use only.