Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA.


RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
E-mail:- rpc.cmbeya@tpf.go.tz



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE TAREHE 28.06.2014.


MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA
KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI.

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MWENYE UMRI
WA SIKU TANO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA
TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA.

KATI KA TUKI O LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LILANGI MLAWE @
MTAFYA (38) MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA KIJIJI CHA INSANI
ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KISHA KUONDOKA NA PIKIPIKI YAKE AMBAYO BADO
HAIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 20:00
USIKU KATIKA KITONGOJI CHA NAMKOMI, KIJIJI CHA BARA, KATA NA TARAFA
YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKODISHWA NA ABIRIA ILI AMPELEKE
WILAYA YA CHUNYA KISHA KUUAWA WAKATI WAKIWA NJIANI. JUHUDI ZA
KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATI KA TUKI O LA PILI :

MWANAUME MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA OBEDI MAKUPA (37)
MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYANI KYELA ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MCHANGA MWENYE
UMRI WA SIKU TANO AITWAYE DAVID SEMENI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 04:00
ALFAJIRI KATIKA KIJIJI CHA LUSUNGO, KATA YA LUSUNGO, TARAFA YA
NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA KABLA YA KUTENDA KOSA HILO
ALIWAVIZIA WAZAZI WA MTOTO HUYO AMBAO NI SEMENI OGADA (28) NA
TUMPALE SAKWISYA (20) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WAKIWA
WAMELALA USINGIZI NA KUFUNGUA MLANGO WA NYUMBA ULIOTENGENEZWA
KWA MATETE KISHA KUMUIBA MTOTO NA KUKIMBIA NAE.

HATA HIVYO BABA WA MTOTO ALISHTUKA NA KUPIGA KELELE ZA
KUOMBA MSAADA HIVYO MAJIRANI WALIJITOKEZA NA KUMKIMBIZA
MTUHUMIWA NA KUMKAMATA AKIWA NA MTOTO HUYO. MTUHUMIWA
AMEJERUHIWA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI.

MTUHUMIWA ALIOKOLEWA NA ASKARI POLISI WALIOFIKA ENEO LA
TUKIO NA AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA AKIWA CHINI YA
ULINZI. AIDHA MTOTO AMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA
KUKABIDHIWA WAZAZI AKIWA SALAMA.




MI SAKO:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADAM KYANDO (27)
MFANYABIASHARA, MKAZI WA KAWETELE CHINI ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA KETE 09 ZA
DAWA ZINAZODHANIWA KUWA ZA KULEVYA AINA YA COCAINE ZENYE UZITO
WA GRAM 10.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA
12:00 MCHANA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO UNDER
GROUND ILIYOPO MTAA WA WAIGO, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA
TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.

KATI KA MSAKO WA PI LI :

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOEL MWAKANYANGWA (24)
MKAZI WA NDANDALO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA AKIWA AMEIFICHA KWENYE MFUKO
WA RAMBO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA
11:00 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MACHINJIONI, KATA YA KYELA KATI, TARAFA
YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA
ZINAENDELEA KUFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KABISA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU
MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA
ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.


Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

You might also like