Redio

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Serikali na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano


kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya
haraka wananchi wao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph
Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa
miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau
wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa
nchini.

Redio za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii
katika suala zima la kujiletea maendeleo alisema Joseph Munga.

Munga aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha
matangazo mwezi Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa taarifa
mbali mbali kwa jamii wilayani Loliondo na kuibua changamoto
mbalimbali zinazoikabili jamii huku akiitaka serikali na halmashauri
wilayani humo kuisaidia katika kufikia malengo ya kuitumikia jamii na
kuwashukuru wadau mbali mbali wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambayo imetoa mnara wao kurushia
Matangazo ya redio Loliondo.

Suala hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona
umuhimu wa kutumia redio hii katika matukio mbali mbali yanayofanyika
kwenye halmshauri vikiwemo vikao vya baraza la madiwani ili wananchi
walioshindwa kufika waweze kujua baraza lao limepitisha nini sanjari na
huduma kwenye sekta za afya na elimu, alisema Munga.

Redio Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO
wilayani humo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya RAMAT kwa
kufadhili miradi ya Maktaba,kutoa elimu kwa jamii ya kifugaji yenye
malengo ya kuinua uelewa na ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni
hasa katika suala zima la kujiletea maendeleo.

Nae Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al
Amin Yusuph, alisema kuwa misingi ya redio hiyo inalenga kuikomboa
jamii ya Loliondo kwa kutoa elimu ya kifugaji na elimu kwa wananchi
wilayani humo ambao hapo awali hawakupata fursa ya kupata taarifa na
matukio mbalimbali yanayoendelea wilayani humo.

Akifafanua faida za redio hiyo kwa jamii ni kupata taarifa mbali mbali
zinazoendana na shughuli zao za ufugaji hususan taarifa za chanjo ya
mifugo na madawa na kupata taarifa nyingine kuhusiana na masuala mbali
mbali ya kijamii ndani na nje ya wilaya hiyo ambayo hapo awali yalikuwa
vigumu kupatikana kwa wakati kutokana na jiografia ya wilaya hiyo.

Pamoja na kwamba malengo ya mradi huu yameanza kuonekana dhahiri
machoni petu,wafadhili kutoka UNESCO pamoja na kampuni ya simu za
mikononi ya Airtel ambayo mnara wake umekuwa ukitumika kurusha
matangazo ya redio hii, tunataka kuhakikisha kwamba mnaweza
kujiendesha wenyewe hapo baadae ili mradi kama huu uweze kuwanufaisha
na wenzenu sehemu zingine, alisema Al Amin.


Akizungumzia miradi inayoletwa na wafadhili wilayani humo Mkuu wa
wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa imechangia kwa kiasi
kikubwa kuwahamasisha vijana ambao wana shauku ya kuishi mijini
kurudi nyumbani na kuendeleza jamii hali ambayo imetafsiriwa kutoa
uelewa kwa wanajamii na hivyo ni faraja kubwa kwa wananchi wilayani
Loliondo.

Ameyataka mashirika na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuingalia
Ngorongoro kwa ukaribu na kuwa wadau wazuri wa kuiletea maendeleo
wilaya hiyo kwani miradi iliyopo itachochea ukuaji wa uchumi na kusaidia
uelewa wa wakazi wilayani Loliondo katika dhana nzima ya kujileta
maendeleo na kukuza uelewa wa wananchi wa kupata taarifa mbalimbali
kwa wakati.

You might also like