Katiba Ya Nacte Inter College Tanzania-Kiswahili

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 20

P.o.

Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
1
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KATIBA- NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA (FESTIVAL, BONANZA, TOURNAMENT,
SUPER-CUP, BALOZI, AMBASSADOR)

Ni mashindano maalumu ya michezo mbalimbali kutoka kwenye vyuo vya elimu ya kati
vilivyosajiliwa na NACTE. Mashindano haya yatasaidia kuwapata wawakilishi wa michezo
ambao wataunda timu moja kwa kila kanda kwa lengo la kuleta changamoto ya kukuza ufanisi
wa michezo kwa jamii. Vijana ambao watakuwa wanatoka kwenye elimu ya sekondari
wanatakiwa wapate mwendelezo wa michezo kwa lengo la kujenga afya pamoja na kudumisha
vipaji vyao. Kwa njia ya Kidemokrasia kila mwaka mashindano yatafanyika katika mikoa yote
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kupata washindi ambao wataiwakilisha Tanzania
kitaifa na kimataifa.

SEHEMU YA PILI
Utangulizi

Baada ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, ni mafanikio makubwa ya kukua kwa Demokrasia
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni wakati wa mabadiliko katika kutambua haki za
binadamu hasa haki za wanawake katika kushiriki kwenye uongozi wa serikali, misingi ya haki
za binadamu pamoja na utamaduni wa kushiriki katika Michezo.

Kwa nini NACTE Inter-College Tanzania.
"Festival, Bonanza, Tournament, Super-Cup"

Mashindano ya NACTE Inter-College Tanzania yameanzishwa na kampuni ya Miss
Demokrasia Tanzania and Entertainment C.o Ltd, mwaka 2014 baada ya kufanya uchunguzi
wa kina kwenye Vyuo mbalimbali.Uchunguzi ulibaini kuwa asilimia 90 ya wanavyuo walikuwa
wakiitaji jambo hili lifanyike. Hivyo Kwa busara za MIDETA iliweza kulifanyia kazi suala hilo
na hatimaye kupata Kibali cha kufanya hivyo kutoka NACTE TANZANIA.Lengo kubwa ni
kutoa fursa kwa taasisi zilizosajiliwa na NACTE TANZANIA kama Vyuo binafsi au vya
Serikali kushiriki kikamilifu.

MIDETA ENTERTAINMENT C.O LTD, kwa pamoja Zimekubaliana kuweka kanuni za
kuendesha mashindano pasipo kuwepo na migogoro isiyokuwa ya lazima. Kanuni hizi lengo lake
kuu ni kuwa na mashindano bora zaidi, ambayo yataweza kuleta ushindi kwa timu shiriki na pia
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
2
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

kutoa burudani halisi kwa watazamaji.

Mashindano haya ambayo yatasimamiwa na makampuni haya tanzu katika uendeshwaji wake
kwa ngazi za wilaya, mikoa, kanda na taifa, yatakuwa ni kioo kwa wanafunzi wa elimu ya
msingi na sekondari.Mashindano yatawezesha kupata wachezaji bora watakaounda timu bora ya
Wanavyuo itakayoweza kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, mashirika na
Taasisi. Mafanikio haya yataweza kukuza na kuendeleza kiwango cha soka, netball, football,
voleyball, handball, debate, riadha, mitindo na mengi zaidi katika Taasisi zetu na pia kujenga
heshima katika medani ya michezo hapa nchini.

MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD, zinaamini na kufahamu kuwa Michezo ya NACTE
Inter-College Tanzania, inapendwa na watu wengi hapa Tanzania na Dunia kwa ujumla na
itaendelea kuvutia watu wengi kwa sababu tutazingatia kanuni, taratibu na sheria za michezo.Ili
kuendelea kuvutia watu wengi kanuni za fair play zinapaswa kuzingazingatiwa na wachezaji,
makocha, waamuzi, viongozi, mashabiki, na wengine wote ambao kwa njia moja au nyingine
wanahusika na michezo ya soka, netball, basketball, riadha, volleyball, kuvuta kamba, kukimbiza
kuku, kukimbia na magunia,sarakasi, maigizo, ngonjela, michezo ya ufukweni(Beach),urembo,
modal, kutunisha misuli, pool table, kuimba, kucheza, handball na Debate.

MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD inaagiza taasisi, makocha na waamuzi kuzisoma
kwa makini kanuni hizi na kuzielewa na kuzifuata kwa ajili ya kufanikisha mashindano.
MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD zinapenda kuwakumbusha washiriki wote kuwa,
soka, netball, riadha na basketball, kama ilivyo michezo mingine yote inalindwa na sheria
pamoja na kanuni. Bila sheria ya michezo hii ya NACTE Inter-College Tanzania itakuwa ni
vurugu tupu. Hivyo waandaaji wa NACTE Inter-College Tanzania wanaziomba taasisi
kuhakikisha kuwa kanuni hizi pia zinaeleweka vizuri kwa wachezaji wake, kwani zitawafanya
wawe wachezaji bora zaidi na wataepuka kuadhibiwa kwa makosa ambayo yanaweza kuepukika.

Kanuni na sheria huwekwa kwa ajili ya kuifanya michezo iwe na ladha katika kuicheza na
kuiangalia na hivyo kuifanya iwe ni burudani zaidi. Tukitumia nguvu na hamasa ya soka, netball,
na basketball inayotakiwa, tutaweza kuijenga jamii bora yenye afya zaidi, amani, upendo, furaha
na usawa.
MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD siku zote zitahakikishamashindano ya NACTE
Inter-College Tanzania yanakuwa na heshima, kwa kusimamia Kwa uadilifu wa kanuni na sheria
za michezo hii, kutoa adhabu inapobidi, kuelimisha na kuhakikisha siku zote
Mshindi anapatikana uwanjani Kwa kufuata na kuzingatia kanuni na taratibu za mchezo na si
kwa kutumia njia chafu zisizokubalika.


P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
3
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


MICHEZO NI FURAHA NA AJIRA
MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD Tunajenga afya ya maisha, upendo, umoja, amani
na mshikamano katika elimu,michezo na burudani katika Vyuo vya Elimu ya Kati na Vyuo vya
Elimu ya Juu(College & University) Tanzania. MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD
misingi imara ya demokrasia kama falsafa ya Kijamii na kisiasa katika kuleta maendeleo ya
binadamu, thamani ya mtu binafsi na katika kipengele chochote cha jamii ya binadamu kwa njia
ya kidemokrasia ya maisha.

KANUNI ZA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU NACTE INTER-COLLEGE
TANZANIA

KANUNI YA KWANZA (1) NAMNA YA UENDESHAJI WA MASHINDANO YA NACTE
INTER-COLLEGE TANZANIA.

Mashindano ya NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA, yatashirikisha Taasisi
zinazojiuhusisha na masuala ya utoaji wamafunzo ya elimu mbali mbali (vyuo vya elimu ya kati
na elimu ya juu).Kwa ngazi ya vyuo vya Elimu ya Kati ni vile vilivyopata Usajili wa Serikali
(NACTE) pamoja na timu mbili waalikwa ambao ni kombaini ya vyombo vya habari (TASWA),
TASWA FC ambao wameruhusiwa kushiriki kwa kuwa TASWA ni mdau mkubwa wa utoaji
Elimu kwa njia ya habari na timu nyingine ni MIDETA inaweza kushiriki kwa kuwatumia
wachezaji wa kombaini wa mwaka uliopita itakaowapendekeza kwa lengo la kuleta changamoto
na msisimko wa mashindano kwa mchezo husika.

Mashindano yataendeshwa katika utaratibu ufuatao:-
1. Mashindano yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano katika hatua ya awali. Timu
itakayofungwa katika hatua hiyo itaaga mashindano.
2. Timu itakayoshinda itaingia hatua ya pili ya mashindano (Robo Fainali).
3. Katika hatua ya awali mshindi Kama hakupatikana katika dakika 90 za mchezo timu
zitapigiana penalti tano tano.

KANUNI YA PILI (2) UWANJA WA MASHINDANO

Uwanja utakaotumika kuchezea mashindano ya NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA
utachaguliwa na kamati ya mashindano ya NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA
FESTIVAL-BONANZA.



P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
4
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA TATU (3) TIMU ZITAKAZOFANIKIWA KUINGIA ROBO FAINALI

1. Mshindi katika hatua hii ya mtoano atapatikana kwa kufunga magoli mengi zaidi ya timu
pinzani.
2. Endapo timu zitatoka sare ya aina yoyote, timu hizo zitapigiana penalty tano tano (5).
3. Iwapo baada ya kupigwa kwa penalti tano mshindi hakupatikana, timu zitachagua
mchezaji wa kupiga penalty ya sita nakuendelea.Mchezaji alikwisha piga penalty
hataruhusiwa kupiga tena mpaka wachezaji wote pamoja na mlinda mlango wamepiga.

MSHINDI KATIKA HATUA YA ROBO FAINALI, NUSU FAINALI NA FAINALI.

1. Iwapo timu zitakwennda sare/suluhu baada ya dakika tisini (90) timu zitapigiana penalty
tano tano ili kupata mshindi wa kuingia nusu fainali.
2. Iwapo baada ya kupigwa kwa penalti tano mshindi hakupatikana, timu zitachagua
mchezaji wa kupiga penalty ya sita nakuendelea.Mchezaji alikwisha piga penalty
hataruhusiwa kupiga tena mpaka wachezaji wote pamoja na mlinda mlango wamepiga
3. Iwapo kutakuwa na giza litakalosababisha mchezo usimalizike na hakuna uwezekano wa
kuwa na siku za ziada kabla ya siku ya fainali kuwezeshwa mchezo kurudiwa, kura
itatumika kumpata mshindi.
4. Iwapo kuna siku za ziada kuwezesha mchezo kurudiwa kabla ya siku ya fainali mchezo
utarudiwa siku inayofuata.
5. Iwapo baada ya kurudiwa timu zikaenda sare/ suluhu penalty tano tano zitapigwa ili
kumpata mshindi. Iwapo penalty hazikutoa mshindi penalty moja moja zitapigwa mpaka
mshindi apatikane, iwapo kutakuwa na giza kura itatumika kumpata mshindi.
6. Kura itakuwa aidha ya kuandika karatasi na kuokota ama kurusha sarafu na kuchagua
upande wa sarafu hiyo.

KANUNI YA NNE (4) RATIBA YA MASHINDANO YA NACTE INTER-COLLEGE
TANZANIA.

1. MIDETA ENTER-TAINMENT C.O LTD zitatangaza tarehe za kuanza na kumalizika
Mashindano ya NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA.
2. Ratiba ya Mashindano itaandaliwa na kutolewa na kamati kuu angalau wiki mbili kabla
ya Mashindano kuanza.
3. Ratiba ikishatolewa haitabadilishwa isipokuwa kama kuna dharura au sababu nzito na za
msingi.


P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
5
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA TANO (5) TARATIBU ZA MCHEZO.

1. Uwanja / Viwanja vyote vitakavyotumika kwa michezo yote vitaidhinishwa na MIDETA
ENTER-TAINMENT C.O LTD ambapo kamati ina madaraka ya mwisho ya kuhamisha
mchezo au kubadilisha uwanja wa mchezo zikibaini kuna sababu za msingi kufanya
hivyo.
2. Manaodha wa timu zinazoshindana wanatakiwa kuvaa vitambulisho vya rangi tofauti na
jezi zao kwenye mikono ya jezi zao.
3. Wachezaji wanaruhusiwa kushangilia goli kwa wastani. Ushangiliaji wa kupitiliza kiasi
cha kupoteza muda kama kutoka uwanjani na kufanya ishara yoyote isiyo ya
kiuanamichezo au ya kashfa au matusi kwa timu pinzani au watazamaji hairuhusiwi.
4. Mchezaji / Wachezaji watakaofanya vitendo hivyo wataadhibiwa na mwamuzi kwa
kuoneshwa kadi ya njano.
5. Mchezaji atakayevua jezi kushangilia ataadhibiwa na mwamuzi kwa kuoneshwa kadi ya
njano.
6. Michezo yote ya NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA itachezwa kwa vipindi viwili
vya jumla ya dakika zitakazo pendekezwa na kamati kuu ya mashindano kulingana na
mchezo husika, na mapumziko ya dakika zisizopungua tano (5) na zisizozidi kumi na
tano (15) .
7. Timu zinatakiwa kufika uwanjani si chini ya dakika thelathini (30) kabla ya wakati
uliopangwa kuanza mchezo.
8. Timu itakayochelewa itatozwa faini ya Tsh. 50,000/=
9. Ni marufuku kwa viongozi kuingia uwanjani kinyume na taratibu za mchezo kabla,
wakati au baada ya mchezo. Kiongozi / Viongozi watakaokiuka kipengele hiki timu yao
itatozwa faini ya Tsh. 50,000/= .Iwapo timu husika haitalipa faini, itatolewa katika
mashindano.
10. Ni marufuku kwa mashabiki kuingia uwanjani kabla, wakati au baada ya mchezo. Timu
itakayokiuka kipengele hiki itatozwa faini ya Tsh. 50,000/=
11. Iwapo timu zitakaguliwa na mgeni rasmi kiwanjani kwa kupeana naye mikono, pia kwa
timu kupeana zenyewe na waamuzi zitafanya hivyo kwa heshima zote zinazostahili. Timu
itakayokataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi au timu pinzani itatozwa faini ya
Tsh. 50,000/=
12. Timu itatumia wachezaji walioorodheshwa katika fomu hiyo tu. Mchezaji ambaye
hakuorodheshwa hatahesabika kama mchezaji wa siku hiyo.
13. Wachezaji wote watatambulika kwa kutumia vitambulisho vyao vilivyoidhinishwa na
MIDETA ENTERTAINMENT C.O LTD, katika mashindano hayo. Mchezaji yeyote
ambaye hatakuwa na kitambulisho hataruhusiwa kushiriki katika mchezo wowote.
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
6
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

14. Iwapo itathibitika bila kujali kukatwa au kutokatwa Rufaa, kupitia taarifa za mchezo za
kamisaa ama kwa njia yeyote kuwa timu imechezesha mchezaji / wachezaji ambao si
halali au ni batili kiusajili (non-qualified) timu hiyo itapoteza mchezo na kutolewa
kwenye mashindano.
15. Wanaoruhusiwa kukaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba ni wachezaji tisa (9) wa
akiba na viongozi watano(5) ambao ni mwalimu mkuu, mwalimu msaidizi, daktari,
mchua misuli na mtunza vifaa wa timu.
16. Mwamuzi atalazimika kutoanzisha mchezo hadi masharti ya kanuni ya 5(15) ya kanuni
hii yametekelezwa.
17. Iwapo hata baada ya mwamuzi kuitaka timu itekeleze masharti ya kanuni ya 5(15) timu
husika ikashindwa kufanya hivyo, basi timu hiyo itatozwa faini ya Tsh. 100,000/=
Mwamuzi ataomba msaada wa wanausalama kuwaondoa wasiohusika kabla ya kuanzisha
mchezo.
18. Mwamuzi na Kamishna wa mchezo wanatakiwa kutoa taarifa zao za maandishi kwa
kamati kuu ya Mashindano, endapo hali iliyoelezwa katika kanuni ya (17) itatokea.
19. MIDETA ENTERTAINMENT C.O LTD zitapeleka uwanjani mipira minne au zaidi
yenye sifa zinazokubalika kisheria itakayotumika kwa ajili ya mchezo. Pamoja na hivyo,
kila timu inatakiwa kufika kiwanjani angalau na mpira mmoja wenye sifa hizo hizo.
20. Ni marufuku kwa timu yoyote kukataa kucheza mpira wowote uliochaguliwa na
mwamuzi.
21. Mwamuzi ataanzisha mchezo iwapo tu kama kuna mipira miwili au zaidi yenye sifa
zinazokubalika kisheria.
22. Mwamuzi ataanzisha mchezo iwapo kila timu ina wachezaji 11. Endapo timu yoyote
haitimizi wachezaji 11, mchezo unaweza kuanzishwa ikiwa tu wachezaji wa kila timu
hawapungui saba (7), mmoja wao akiwa mlinda mlango. Lakini kanuni hii haitahusu timu
iliyosalia na wachezaji pungufu ya saba kutokana na baadhi yao kuumia au kutolewa nje
na mwamuzi wa mchezo.
23. Timu inaruhusiwa kubadilisha wachezaji watano (5) tu wa akiba.
24. Timu itakayokosa kufika uwanjani na kusababisha mchezo kutofanyika, itatozwa faini ya
shilingi 100.000/= na iwapo pesa hiyo haitalipwa timu haitaruhusiwa kushiriki
mashindano ya msimu unaofuata hadi ilipwe.
25. Timu yeyote iliyopewa adhabu ya faini chini ya kanuni hii haitaruhusiwa kucheza hadi
itakapotekeleza adhabu.
26. Wachezaji na Viongozi hawaruhusiwi kunywa pombe (kulewa) wakati michezo
inaendelea. Iwapo itabainika kufanyika mchezo na mchezaji, kiongozi amelewa wakati
wa mchezo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kushiriki
katika mchezo iwapo wana mechi mbele.


P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
7
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA SITA (6) KUAHIRISHA MCHEZO

Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
1. Sababu yoyote ya dharura nzito na yenye msingi itakayokubaliwa na kamati.
2. Mchezo wowote ulioahirishwa utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na kamati
isipokuwa kama ni dharura ya mvua au dharura yoyote nyingine basi mchezo huo
utachezwa siku inayofuata iwapo ratiba inaruhusu.
3. Iwapo mchezo ulianza na kuvunjika kwa sababu ya mvua au dharura yoyote nyingine na
ukapangwa kurudiwa, magoli yaliyofungwa katika mchezo huo, kadhalika kadi
walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo ulioahirishwa au uliovunjika hazitaendelea
kuhesabika.
4. Taarifa ya maombi ya kuahirisha mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi

KANUNI YA SABA (7) WAAMUZI

1. Katika mchezo wowote Uamuzi wa Mwamuzi ni wa mwisho.
2. Kila mwamuzi atawasilisha kwa kamisaa taarifa ya mchezo aliouchezesha iliyojazwa
katika fomu maalum katika muda usiozidi dakika 15 baada ya mechi kuchezwa.
3. Taarifa ya Mwamuzi inatakiwa ijazwe kwa unadhifu na ukamilifu.
4. Mwamuzi atakayeshindwa kutoa taarifa sahihi ya mchezo kwa mujibu wa kanuni ya 7(2)
ataondolewa katika orodha ya waamuzi wanaochezesha mashindano ya NACTE INTER
COLLEGE TANZANIA.
5. Waamuzi wa mchezo watapangwa na Mwamuzi kuu wa Mashindano na timu yoyote
hairuhusiwi kumkataa mwamuzi yeyote.

KANUNI YA NANE (8) HUDUMA YA KWANZA

MIDETA ENTERTAINMENT C.O LTD itaandaa huduma ya kwanza na Daktari katika kila
mchezo.

KANUNI YA TISA (9) MAOMBI YA FOMU YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA NACTE
INTER COLLEGE TANZANIA.

Kutakuwa na fomu za maombi ya kushiriki mashindano ya NACTE INTER COLLEGE
TANZANIA. Tarehe ya mwisho kuthibitisha itatangazwa na kamati Kuu. Timu au Taasisi
ambayo itashindwa kuthibitisha kushiriki hadi kufikia tarehe ya mwisho ya kufanya hivyo
itakuwa imejiondoa yenyewe kwenye mashindano.

P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
8
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA KUMI (10) USIMAMIZI WA MASHINDANO

Mashindanoo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA yatasimamiwa na kamati Kuu ya
Mashindano.

KANUNI YA KUMI NA MOJA (11) RUFANI NA UTARATIBU WAKE

Rufaa zote zinazohusiana na mashindano ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA
zitasikilizwa na:-

1. Kamati Kuu ya mashindano na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.
2. Ni marufuku kupeleka malalamiko yoyote yahusuyo Michezo yote Ikiwemo Soka katika
Mahakama za Kisheria. Timu au mtu yoyote atakayepeleka malalamiko yake katika
Mahakama za Kisheria atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufutwa kabisa kushiriki kwa
namna yoyote kwenye Hafla za Mashindano na burudani zozote za
NACTE INTER COLLEGE TANZANIA.

KANUNI YA KUMI NA MBILI (12) UTARATIBU WA KUKATA RUFANI

1. Rufani ya kupinga matokeo ya mchezo wowote iwasilishwe kwa maandishi kwa
kamishna wa mchezo sio zaidi ya dakika kumi na tano (15) baada ya mchezo kumalizika
na iwe imeambatanishwa na ada ya rufaa.
2. Kamishna wa mchezo atawasilisha kwenye kamati kuu ya mashindano sio zaidi ya
dakika kumi na tano (15) tangu kupokea rufaa hiyo.
3. Kamati husika itaketi kusikiliza na kuitolea uamuzi Rufaa hiyo katika kipindi kisichozidi
saa (48) arobaini na nane. Timu au mtu anayekata Rufaa itawasilisha vielelezo kuhusu
rufaa yake, rufaa isiyokuwa na vielelezo na ambayo haijalipiwa ada itatupwa.
4. Rufaa yoyote itakayowasilishwa baada ya muda uliyowekwa chini ya kanuni hii,
haitasikilizwa na ada ya rufaa haitarudishwa kwa mrufani.
5. Michezo itakayohusika na masuala ya rufani ni pamoja na soka, netball, basketball,
debate, pool table na riadha

KANUNI YA KUMI NA TATU (13) ADA ZA RUFAA

Rufaa yoyote itakayokatwa inatakiwa ilipwe ada ya Tsh.50,000/=



P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
9
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA KUMI NA NNE (14) KUJITOA KWENYE MASHINDANO

1. Iwapo timu yoyote ina lengo la kujitoa katika Mashindano baada ya kuthibitisha kwa
sababu zozote zile za msingi, ni lazima itoe taarifa ya maandishi kwa MIDETA
ENTERTAINMENT C.O LTD, ikieleza sababu inayoilazimisha ijitoe, siku saba (7)
kabla ya mashindano kuanza.
2. Iwapo timu itajitoa baada ya mashindano kuanza na baada ya kuwa imeshacheza baadhi
ya mechi kwenye ngazi ya makundi, matokeo ya michezo yote iliyowahi kucheza
itafutwa. Kwa ngazi ya robo / nusu fainali na fainali timu iliyokuwa ipambane nayo
itapewa ushindi.

KANUNI YA KUMI NA TANO (15) KUTOFIKA UWANJANI / KUVURUGA MCHEZO

Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani na kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na
adhabu zifuatazo:-
1. Itapoteza ushindi na itatolewa kwenye mashindano na matokeo ya michezo yake yote
iliyokwishacheza yatafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye
mashindano.
2. Wachezaji na viongozi wa timu itakayosababisha mchezo kuvurugika kwa namna yoyote
ile na hatimaye kuvunjwa, itapoteza mchezo huo ( na inaweza kuondolewa kwenye
mashindano) hata kama ilikuwa inaongoza kwa magoli na timu pinzani itapewa ushindi,
iwapo timu pinzani inaongoza kwa magoli zaidi ya mawili, itabakia na idadi ya magoli
hayo iliyokwishafunga.

KANUNI YA KUMI NA SITA (16) KUPANGA MATOKEO

Iwapo timu zozote zitabainika zimepanga kwa namna yoyote ile, matokeo ya mchezo wowote
waliocheza kwa madhumuni yoyote yale zitachukuliwa hatua zifuatazo:
1. Matokeo ya mchezo huo yatafutwa na kila timu itatozwa faini ya shilingi laki tano
(Tsh.500,000/=)
2. Timu zitaondolewa kwenye mashindano
3. Viongozi wa timu hizo waliohusika na njama za kupanga matokeo, watafungiwa
kushiriki michuano ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA kwa kipindi cha miaka
miwili.
4. Iwapo timu husika itashindwa kulipa faini, basi timu hiyo haitapangwa katika
mashindano yanayofuata.


P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
10
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA KUMI NA SABA (17) UDHIBITI WA WACHEZAJI

Kamati ya Mashindano itadhibiti mienendo ya wachezaji kwa kuchukua hatua kama zifuatazo:-
1. Mchezaji atayetolewa nje kwa kadi nyekundu baada kupata kadi mbili za njano
katika mchezo hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake.
2. Mchezaji atayetolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja (Straight-red)
atakosa mchezo mmoja.
3. Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga / kupigana
atasimama kushiriki michezo (3) mitatu inayofuata ya timu yake na italipa faini ya
shilingi laki moja za kitanzania Tsh. 100.000/=
4. Kamati ya mashindano itaangalia mazingira ya kosa hilo na kulingana na mchezo
husika na kamati kuu ya mashindano itakuwa na uamuzi dhidi ya kosa hilo kama
inavyoelezwa hapo juu.
5. Timu ambayo wachezaji wataonyeshwa kadi zaidi ya nne katika mchezo mmoja
itatozwa faini ya shilingi za kitanzania Tsh. 100.000/=
6. Timu na wachezaji wanatakiwa kutunza kumbukumbu zaidi. Timu
itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi moja (1)
Nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi 3 na magoli
3. Iwapo timu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa
maandishi toka kwa katibu wa kamati kuu ya mashindano.
7. Mchezaji yeyote atakayefanya jambo lolote kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kwa
kufungiwa kucheza michezo mitatu (3) au, kutozwa faini ya shilingi za kitanzania
laki moja (Tsh. 100.000/=) au vyote kwa pamoja.
a) Kupigana / kupiga kabla, wakati au mara tu baada ya mechi kumalizika.
b) Kumshambulia mwamuzi, kiongozi au mtazamaji yoyote kwa namna yoyote
ile, iwe kwa matusi au kwa kumgusa.
c) Kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani, kukataa
kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa
matusi au kuonyesha ishara yoyote inayoashiria matusi.
d) Kusababisha kuvurugika kwa amani kiwanjani kabla au baada ya mchezo.
e) Kufanya Vitendo vyenye kuonyesha Imani za ushirikina au uchawi hadharani;
Kama vile kuvunja nazi, kupasua mayai, kufukia hirizi na kumwaga maji
makombe.

f) Kufanya kitendo chochote kinyume cha maadili ya mchezo wa mpira, kwa
mfano kuruka uzio badala ya kupita kwenye mlango maalum.
g) Timu yoyote itakayomchezesha mchezaji aliye chini ya adhabu kwa mujibu wa
kanuni hii itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi.
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
11
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA KUMI NA NANE (18) UDHIBITI NA ADHABU KWA WAAMUZI

Mwamuzi yeyote atakayefanya jambo lolote kati ya haya yafuatayo ataondolewa kwenye orodha
ya waamuzi wa mashindano ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA:-
1. Akishindwa kumudu mchezo kwa uzembe, woga au kutozingatia sharia kiasi cha
kuvuruga mchezo, kuhatarisha amani.
2. Akibainika kuwa anadai hongo au amepokea hongo au akitoa taarifa yenye mazingira
ya hongo.
3. Akishindwa kufika au akichelewa kufika uwanjani bila sababu ya msingi au kutotoa
taarifa.
4. Akifanya kitendo chochote ambacho ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uamuzi.
5. Mwamuzi atakayemaliza mchezo kabla ya wakati bila ya sababu za msingi.

KANUNI YA KUMI NA TISA (19) ADHABU KWA TAASISI / TIMU

1. Timu ina wajibu na jukumu la kuhakikisha kuwa wachezaji, viongozi, wanachama, na
wapenzi wake wanajiheshimu na hawajihusishi na vitendo vyovyote vya utovu wa
nidhamu kama vile matusi, vitisho, vurugu, vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina
na vitendo vyovyote vingine visivyokuwa vya kimichezo kwenye viwanja vya michezo.
Timu ambayo washabiki wake watafanya vitendo hivyo itatozwa faini ya Shilingi Laki
moja za Kitanzania (Tsh.100.000/=). Mshabiki atakayekamatwa akifanya vitendo hivyo
atachukuliwa hatua za kisheria na atakayepatikana na hatia atazuiwa kuhudhuria katika
mashindano ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA.
2. Timu itapoteza mchezo ambao utavunjika kutokana na vurugu za washabiki wake.
3. Timu pia itawajibika kulipa gharama za matibabu na kulipa gharama za mali
iliyoharibika kwa waathirika wa vurugu za washabiki wake itakayofanyika kabla, wakati
au baada ya mchezo.

KANUNI YA ISHIRINI (20) KIPINDI CHA USAJILI

1. Kipindi cha usajili kitakuwa kuanzia June ya kila mwaka
2. Usajili wa wachezaji ni suala la kiufundi. Mwalimu Mkuu wa timu atawajibika kutambua
wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa. Katibu Mkuu atafanya masuala ya utawala,
atakamilisha zoezi la usajili wa wachezaji na kuwasilisha fomu ya majina kwa kamati ya
mashindano wakati uliopangwa.
3. Taasisi / Timu zina wajibu wa kutumia fomu iliyotayarishwa na MIDETA
ENTERTAINMENT C.O LTD , kusajili wachezaji wake zikiambatanishwa na picha
mbili za passport za kila mchezaji.
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
12
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA ISHIRINI NA MOJA (21) USAJILI KWA WACHEZAJI

Fomu za Usajili wa wachezaji zitatolewa na MIDETA ENTERTAINMENT C.O LTD kila June
ya kila mwaka.

KANUNI YA ISHIRINI NA MBILI (22) UTHIBITISHO WA USAJILI

1. Kamati kuu ya Mashindano itathibitisha usajili wa timu. Taasisi / Timu zinatakiwa
kukamilisha na kuwasilisha usajili wa wachezaji pamoja na majina ya makocha wa timu
katika kipindi cha usajili. Usajili na uhakika ukishakamilika majina yatatangazwa kwa
kila timu itakayoshiriki.
2. Mchezaji yeyote hataruhusiwa kujiunga na Taasisi / Timu yeyote katika mashindano ya
NACTE ENTER COLLEGE TANZANIA hadi usajili wake uwe umethibitishwa.
3. Mchezaji atakuwa na kitambulisho atakachoonesha wakati wa mechi ambacho
kitakaguliwa na mwamuzi / kamisaa na naodha wa timu pinzani katika kila mechi.

KANUNI YA ISHIRINI NA TATU (23) MAJINA YA WACHEZAJI

Mchezaji atalazimika kujaza majina yake kamili matatu katika Fomu ya usajili.


KANUNI NYA ISHIRINI NA NNE (24) IDADI YA WACHEZAJI

1. Kila Taasisi / Timu itaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi ishirini.
2. Kati yao 17 wakiwa ni Wanafunzi wa chuo husika na 3 wawe ni Walimu wa Chuo / Timu
husika.
3. Wachezaji wengine wanaweza kutoka katika Idara zingine za Taasisi husika au kutoka
Campas ingine ya Taasisi hiyo bila kujali Mkoa au Umbali wa eneo la tukio.
4. Wachezaji watakaoruhusiwa kutoka Campas ya Tawi la Taasisi husika hawatakiwi kuzidi
watatu. Pia ni lazima wawe Wanafunzi au Walimu wa Campas katika Taasisi hiyo.

KANUNI YA ISHIRINI NA TANO (25) KUTENGULIWA UTHIBITISHO WA USAJILI

Uthibitisho wa usajili wa wachache wa Taasisi / usajili unaweza kutenguliwa na Kamati Kuu ya
mashindano endapo itathibitika kuwa usajili huo umekiuka masharti ya Kanuni hizi.



P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
13
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


KANUNI YA ISHIRINI NA SITA (26) KATAZO

1. Haitaruhusiwa kwa mchezaji yeyote kutia saini Fomu ya Taasisi / timu zaidi ya moja
ndani ya msimu wa mashindano ya NACTE ENTER COLLEGE TANZANIA. Mchezaji
atakayesaini Fomu za timu mbili tofauti kwa wakati mmoja usajili wake utabatilishwa.
2. Taasisi (College) inaruhusiwa kuwa na Wanafunzi zaidi ya kumi na nne (14) wa kozi
yoyote kwenye orodha ya usajili, lakini hairuhusiwi kuwa na wachezaji wanaozidi sita
kutoka kwenye tawi lililoko nje ya Kanda, Mkoa husika hata kama ni Campas ya tawi
lake na hairuhusiwi kutumia Walimu zaidi ya watatu (3) katika usajili huo.

KANUNIN YA ISHIRINI NA SABA (27) ADHABU ZINAZOHUSU USAJILI

1. Mchezaji yeyote atakayebadili jina lake halisi kwa madhumuni ya kudanganya ili
asajiliwe kinyume cha masharti ya Kanuni hizi ataondolewa kwenye Mashindano.
2. Timu iliyomchezesha mchezaji aliyebadili jina kwa nia ya kudanganya italipa faini ya
shilingi lakini moja (100.000/=) kwa kila mchezo ambao mchezaji huyo alicheza lakini
matokeo ya uwanjani hayatabadilika.
3. Timu itakayothibitika kumchezesha mchezaji ambae hajasajiliwa na timu hiyo itapoteza
michezo yote ambayo huyo mchezaji alicheza iwapo timu pinzani itakata rufaa.
4. Kamati ina uwezo wa kutoa adhabu iwapo itathibitika timu imemchezesha mchezaji
ambae hakusajiliwa hata kama timu pinzani haitakata rufaa.
5. Taasisi (College)/ Timu yeyote itakayowasilisha usajili wake baada ya tarehe
itakayotangazwa na Kamati Kuu ya Mashindano, hautapokelewa na itahesabika kuwa
imejiondoa yenyewe kwenye mashindano.

KANUNI YA ISHIRINI NA NANE (28) UFAFANUZI

1. Mashindano haya yataendeshwa kwa kuzingatia sharia / kanuni za Shirikisho la Mchezo
Husika.
2. Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) chini ya waamuzi
watakaoteuliwa kuchezesha Mashindano haya.
i) Na sheria za mchezo wa mpira wa Kikapu Nchini zitatumika katika mchezo huo
ii) Na sheria za mchezo wa Riadha Nchini zitatumika katika mchezo wa huo.
iii) Na sheria za mchezo wa Netball Nchini zitatumika katika mchezo wa Netball.

KANUNI ZAMASHINDANO YA NACTE INTER COLLEGE TANZANIA MCHEZO WA NETBALL

KANUNI YA KWANZA (1) USIMAMIZI WA MASHINDANO
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
14
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


1. Mashindano haya yatasimamiwa na kuratibiwa na kamati kuu ya mashindano na ndio
chombo cha mwisho cha uamuzi

2. Timu zote shiriki zinatakiwa kuwepo uwanjani siku ya ufunguzi na ufungaji wa mashindano
zikiwa zimevaa sare.

KANUNI YA PILI (2) USAJILI

1. Kila timu inapaswa kujisajili kwa kutumia fomu maalum zitakazotolewa na Kamati Kuu
ya mashindano. Fomu hizo zitakuwa na sehemu ya picha ya wachezaji
2. Wachezaji wasiozidi 12 wataruhusiwa kusajili kwa mchanganuo ufuatao:-
i. Saba (7) kati yao wawe ni wanafunzi wa taasisi husika.

ii. Watano watoke kwenye tawi la taasisi au Campas ya chuo husika, na walimu
wanatakiwa wasizidi wawili (2) kwenye usajili huo
iii. Usajili wote unatakiwa kukamilika mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa mashindano.

KANUNI YA TATU(3)VITAMBULISHO

1. Wachezaji wote watakaoshiriki ashindano haya lazima wawe na vitambulisho vya
uchezaji yenye picha ya mchezaji husika na vionyeshwe siku ya michezo yao bila ukosa.
2. Mchezaji asiyekuwa na kitambulisho hicho Hataruhusiwa kucheza.
3. Kitambulisho cha Mwanafunzi au Mwalimu kitahakikiwa na kamati kuu ya mashindano
kabla ya kutoa kitambulisho cha mchezaji au mwalimu.
4. Taasisi / Timu au mchezaji anapaswa kuwatambua pia wahusika (waandaaji wa
Tamasha, Bonanza, Tournament) kwa sare na Vitambulisho watakavyokuwa navyo kwa
suala lolote ikiwa ni pamoja na itaji la huduma yoyote kwenye maeneo ya Viwanja /
Michezo.wahusika katika kundi hili ni watu wa Ulinzi (Usalama), Wandishi wa Habari,
Wageni Waalikwa pamoja na mgeni rasmi.

KANUNI YA NNE(4) RATIBA YA MASHINDANO

1. Ratiba ya mashindano itaandaliwa na kamati kuu ya mashindano.

2. Ratiba inaweza kubadilika iwapo kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya Hivyo
kwa sababu maalumu na kwa manufaa ya mashindano.

KANUNI YA TANO (5) USHINDI
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
15
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


1. Ushindi utahesabiwa kwa pointi 3 timu itakayoshinda, na timu zitakazofungana Magoli
sawa zitagawana pointi moja kwa kila timu. Timu itakayoshindwa itapata pointi sifuri (0).
2. Iwapo timu zitafungana katika mambo yote matatu, magoli ya kufunga na kufungwa
yataangaliwa.
KANUNI YA SITA (6) JEZI

Jezi za kila timu ziwe nadhifu na fupi kiasi cha kuwawezesha wachezaji kuruka. Bibs ziwe
zimeandikwa vizuri mbele na nyuma kwa herufi kubwa ili zisomeke kwa ufasaha.

KANUNI YA SABA (7) TARATIBU ZA MCHEZO

1. Kabla ya mchezo kuanza makapteni wa timu wajitambulishe kwa waamuzi waingiapo na
timu zao uwanjani.
2. Timu zote zinatakiwa kuwepo kituo cha mashindano nusu saa kabla ya michezo.
3. Timu inawajibika kuwasilisha majina 12 ya wachezaji kila siku ya mchezo wakiwa 7
wanaoanza kucheza na 5 wa akiba.
4. Meneja wa kila timu awe mwanamke na ndiye atakaye wajibika katika masuala yote ya
timu.
5. Kila mchezo utakuwa wa dakika 40 au 60 kulingana na muda na siku zilizopangwa.
6. Baada ya mchezo kumalizika timu mbili zilizomaliza kucheza zitajipanga na kupeana
mkono.
KANUNI YA NANE (8) MALALAMIKO/RUFAA

1. Malalamiko ya aina yeyote yawe kwa maandishi na yawasilishwe kwa kamati kuu ya
mashindano saa moja na nusu kabla ya mchezo.
2. Iwapo timu inahitaji rufaa hiyo iwe ya maaandishi na malipo ya shilingi 50,000\= na
iwasilishwe ndani ya muda wa dakika 15 baada ya mchezo Kumalizika. Rufaa hiyo
inatakiwa iwe na vielelezo vya ushahidi na si tuhuma. Zaidi ya muda huo rufaa
haitapokelewa.
3. Fedha zote za kukata rufaa hazitarejeshwa.
4. Maamuzi ya kamati ya mashindano yatakuwa maamuzi ya mwisho.

KANUNI YA TISA (9) MAKOSA YA KINIDHAMU

1. Ni makosa kukataa kutoa mkono kwa mgeni rasmi, ikithibitika kufanya hivyo,faini ya
Tshs.50,000/= itatozwa kwa timu na ilipwe ndani ya dakika 15 kabla ya mchezo kuanza.
2. Timu itakayogomea mchezo kwa sababu yoyote ile itapoteza mchezo na timu iliyopo
uwanjani itajipatia ushindi kwa mujibu wa sheria.
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
16
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

3. Timu iliyogoma itatozwa faini ya Tshs 50,000/= na isipolipa faini hiyo haitaruhusiwa
kucheza mchezo unaofutia.
4. Hairuhusiwi kumchezesha mchezaji mjamzito. Timu itakayobainika kukiuka agizo hili
michezo yake yote itafutwa na hatua za kinidhani zitachukuliwa. Viongozi wa timu
wawajibike kwa hili.
5. Wachezaji na viongozi hawaruhusiwi kunywa pombe (kulewa) wakati michezo
inaendelea. Iwapo itabainika kufanyika na mchezaji/ kiongozi amelewa wakati wa
michezo hatua za kinidhamu zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kucheza/
kushiriki katika mchezo iwapo wana mchezo.

HITIMISHO

1. Iwapo kutatokea jambo ambalo halitaweza kuamuliwa kwa kufuata kanuni hizi au sheria
za IFNA, basi jambo hilo litaamuliwa kwa kikao cha dharura cha kamati kuu ya
mashindano na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.
2. Mashindano haya yataendeshwa kwa kuzingatia sheria za ushiriki wa mchezo wa
Netiboli ulimwenguni (IFNA Netiball Rules) chini ya waamuzi Watakoteuliwa
kuchezesha mashindano haya.
3. Timu zote zizingatie kanuni hizi na kuziheshimu.Ni katika mawazo na ubunifu huu
kwamba Mashindano ya "NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, yatafanyika kama
Bonanza, Tamasha, ligi, mzunguko, mtoano, robo fainali, nusu fainali, na fainali kwa
dakika zitakazopendekezwa na kamati kuu ya mashindano.

KANUNI ZA MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA

1. Mashindano yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano katika hatua ya awali. Timu
itakayofungwa katika hatua hiyo itaaga mashindano.
2. Timu itakayoshinda itaingia hatua ya pili ya mashindano (Robo Fainali).
3. Viwanja vyote vitaidhinishwa na MIDETA Entertainment C.o LTD
4. Sheria zinazotumika kuhusu Mavazi ni zile za Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania,
kwamba si ruhusa mchezaji kucheza bila kuvaa viatu, soksi, na jezi zote ni lazima ziwe ni
zile zinazotumika popote na wachezaji wengine kwenye mchezo huu wa Kikapu(bukta na
fulana iliyokatwa mikono).
5. Sheria za waamuzi zitabaki kuwa kama zilivyoainishwa kwenye mchezo wa mpira wa
miguu.
6. Taasisi inaweza kushirikisha timu mbili za wanaume na wanawake kwenye mchezo huu
wa kikapu.
7. Waamuzi wote watathibitishwa na Kamati kuu ya Mashindano.
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
17
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

8. Timu inapaswa kusajili wachezaji kumi na mbili (12) watano wataingia kucheza na
wachezaji saba (7) watakuwa wa akiba na watacheza kwa kufuata sheria zote za mchezo
huu wa Kikapu.
9. Dakika zitakazotumika ni zile zitakazokubaliwa na kuwekwa wazi na kamati kuu kabla
ya mchezo kuanza baina ya viongozi wa timu zote mbili.
10. Mipira itakayotumika itafikishwa uwanjani na waandaaji MIDETA ENTERTAINMENT
C.O LTD, isipokuwa kila timu inapaswa kuwa na angalau mpira wake kwa ajili ya
mazoezi ya viungo wakati wa maandalizi ya mchezo.
11. Sheria zingine zote zitatumika zilizoainishwa kwenye orodha ya Kanuni za mpira wa
miguu, kwa ajili ya Mashindano haya ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA.

KANUNI ZA MASHINDANO YA DEBATE NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA

1. Sheria zingine zote kuhusiana na Taasisi, Mshiriki, Maeneo ya Viwanja, Ukumbi, Fomu,
Vitambulisho, zimeshaainishwa huko juu kwenye sharia za Soka, Netball na Basketball.
2. Kila Taasisi inawajibika kuwa na wawakilishi wawili (jinsia zote)
katika mashindano ya mijadala
(Debate)
3. Washiriki watashindana kujibu maswali, kuelezea mada mbalimbali zitakazohusiana na
elimu, viongozi, utawala, jamii, siasa na michezo kulingana na waandaaji wa
mashindano (Kamati kuu) itakavyopendekeza.
4. Waamuzi (majaji) wa Mijadala hii watakuwa ni Maafisa wa Usalama wa Taifa,
Takukuru, Tume za Haki za Binadamu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Basata, kwa
kushirikiana na Jaji Mkuu kutoka MIDETA ENTERTAINMENT ambaye atakuwa na
jukumu la kuwatangaza washindi.
5. Washiriki wote wanapaswa kuwa nadhifu, wenye kujiheshimu wenyewe na wanapaswa
kuvaa mavazi ya heshima kama Suti au nguo ndefu kwa kina dada zisizowadhalilisha
miili yao pindi awapo jukwaani (Official wear).
6. Ni marufuku kwa mshiriki yeyote wa mijadala hii kupanda jukwaani akiwa amevaa
kanda mbili, Kofia, nguo fupi zinazoonyesha mapaja, kata K. kwa wavulana, nyele
zilizowekwa rangi, kunyoa denge, bila mkanda, soksi, na kusema yale ambayo ayastaili
kama Matusi, au kutukana akiwa juu ya jukwaa.
7. Mshiriki akishapanda jukwaani anatakiwa kutokuwa na aina yoyote ya karatasi, simu au
komputa kwa lengo la kujipatia majibu au kujiongezea uelewa kwa wakati huo kwani
anapaswa kutunza kumbukumbu ya mambo yote apaswayo kuzungumza katika kichwa
chake.
8. Ikumbukwe kwamba, majaji wote watakuwa na jukumu la kuondoa maksi kwa kila
mshiriki kutokana na makosa yake kutokana na sharia hizi.
9. Ushindi wa mshiriki utaangaliwa kwa namna nyingi ikiwemo, ueledi wake, mavazi,
P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
18
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

muonekano, kujiamini kwake wakati wa kuwasilisha au kujibu maswali.
10. Ikumbukwe washindi kwa kila kanda watakuwa ni wawili (2) ambao wataitwa na
kutambulika kutokana na kanda husika mfano:-
BALOZI WA DEMOKRASIA TANZANIA-DAR ES SALAAM

KANUNI ZA MASHINDANO YA RIADHA NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA

1. Kila Taasisi inapaswa kuwakilishwa na Washiriki wawili (2) mvulana na msichana katika
kila mbio zitakazoainishwa na Kamati Kuu kulingana na mahitaji ya Taasisi
zilivyojiandikisha.
2. Kila mshiriki anawajibika kuwa na vitendea kazi vyake ikiwa ni pamoja na nguo za
kukimbilia kulingana na yeye mwenyewe atakavyojisikia.
3. Inashauriwa kuwa kila mshiriki awe amevaa viatu chini ya miguu yake (raba).
4. Washindi wote wanatakiwa wawe wameanza safari ya mashindano eneo husika, na
watapokewa na majaji kutokana na Umbali wa kila kilomita na washindi ni 3 kila Mbio.

B: LENGO LA MASHINDANO YA NACTE INTER COLLEGE TANZANIA

Lengo la mashindano kama ifuatavyo:
1. Kuendeleza vipaji mbalimbali kwa vijana, kuwapa uzoefu katika kufikia malengo
waliyojiwekea.
2. kuwaandaa vijana kuwa Viongozi na watawala kwa kuwajengea misingi ya utawala bora
3. Kurekebisha mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
4. Kuitangaza Tanzania Kitaifa na Kimataifa
5. Kuelimisha jamii katika mavazi,
6. Kuwapa mafunzo vijana juu ya elimu ya kutambua misingi ya Demokrasia na Historia ya
Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa changamoto kwa viongozi na msukumo wa
uwajibikaji katika kuleta Maendeleo.
7. Shindano la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA litasaidia kupata na kukuza Vijana
wa Taifa makini na watawala wa taifa la kesho wakiwa na vipaji mbalimbali kulingana na
mahitaji ya nchi.
8. Kusaidia kukuza tasinia ya michezo, burudani na elimu ya kisasa ya teknolojia endelevu.
9. Kutoa mwamko kwa makampuni kusaidia na kutunza vijana ikiwa ni pamoja na kujenga
moyo wa ushirikiano na mshikamano kwa uzalendo na upendo, amani, umoja wa taifa.
10. Kuwaandaa vijana kuwa viongozi kitaifa na kimataifa ambao watakuwa na majukumu ya
kuhamasisha maelewano, ushirika na umoja miongoni mwao, nchi na mabara yote
ulimwenguni



P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
19
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd


MFUMO WA SHINDANO
Mashindano haya ni tofauti na mashindano mengine

MFUMO WA KWANZA (1)
Timu zitapangwa kwenye makundi kisha zitacheza mtoano kwa mfumo wa bonanza kwenye
uwanja / viwanja. Eneo mmoja itachezwa michezo mingi kulingana na mchezo husika na timu
/washiriki waliojitokeza kwa dakika zitakazokubaliwa na Kamati Kuu ya Waandaaji.

MFUMO WA PILI WA MASHINDANO
1. Baada ya timu zote kujiandikisha kushiriki, zitapangwa kwenye makundi kulingana na idadi ya timu. Timu
hizi zitacheza hatua ya kwanza katika mzunguko, timu mbili (2) zitakazopata pointi nyingi kwa kila kundi
zitaingia hatua ya pili ya Mtoano (mchujo) kabla ya kuingia robo fainali, nusu fainali na fainali.
2. Timu mbili zitakazocheza fainali zitaingia hatua ya Fainali ya Bonanza la Taifa itakayoshirikisha wachezaji
mbali mbali kutoka kanda zote za Tanzania ambayo itakuwa ni Fainali kubwa ya mashindano haya ya.
NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA- DAR ES SALAAM2014 / 2015
1. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA-MWANZA 2014 / 2015
2. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA-ARUSHA 2014 / 2015
3. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA-MBEYA 2014 / 2015
4. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA-DODOMA 2014 / 2015
5. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA-ZANZIBAR 2014 / 2015
6. NACTE INTER-COLLEGE TANZANIA 2014 / 2015

MWISHO:

Msimamizi Mkuu, Mtunzi na Mwenye Haki Miliki ya Ubunifu ni:-
Mpalule Shaaban.

WENGINE NI
Mlezi Mr. Anthony Komba
MdhaminiMarry Komba
Katibu Mkuu- Fredy Anthony Njeje
Muhuri wa Kampuni
Sahihi ya Mkurugenzi Mkuu wa mradi:

Haki zote zimeifadhiwa
(COSOTA)
Copyright society of Tanzania
Ref No. CST/APP/REG/WORKS/VOL.XV/86 -ACT, NO. 7 (CAP 218 RE 2002)
Dar es Salaam-TANZANIA.


P.o.Box-8017-Dar-es-Salaam, Tanzania:Phone:+255767869133/+255713869133;
missdemokrasiatanzania@yahoo.com,www.missdemokrasia.blogspot.com,www.missdemocrasiatz.com.
20
baloziwademokrasiatanzania@yahoo.com,
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com,www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com,
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd

You might also like