Professional Documents
Culture Documents
Kuhusu Fungu La Kumi KTK Agano Jipya!
Kuhusu Fungu La Kumi KTK Agano Jipya!
1. Utangulizi
Nani anayekula zaka? Siyo Mlawi wala siyo kuhani! Katika Israeli, kila
jamaa ilitarajiwa kwenda Yerusalemu mara moja kwa mwaka kutembelea
Hekalu. Baadhi ya zaka zilitumika kulipia gharama za safari na pia
zingetumika kutoa matoleo ambayo yaliamriwa chini ya Sheria. Walikula
na kunywa zaka zao wenyewe, Kumb.14:24,25,26. Zaka zilitumika
kugharimia hija ya familia kwenda Yerusalemu mara moja kwa mwaka,
Kumb.14:27,28,29.
Je, inaweza kusemwa vipi ikiwa mtu hatoi kwa lazima ikiwa anaitii
Sheria ya zaka? Je, ni kwa vipi itasemekana ikiwa mtu hatoi kwa
lazima, ikiwa anashawishika kwamba atalaaniwa na umaskini ikiwa
atashindwa kulipa zaka? Katika waraka wa kwanza wa Wakorintho, kwa
nini Paulo hawakumbushi waamini kwamba inawalazimu kulipa zile
zaka na kwamba ana haki ya kuzipokea zile zaka?
Fungu hili linasema kwamba, ukitoa zaka kwa uaminifu utabarikiwa. Tatizo
ni kwamba huruhusiwi kuchukua na kuchagua sheria zipi za Agano la
Kale ambazo unataka uzipokee na zipi uziache. Ahadi zile zile
zinaambatana na sheria zingine pia, Kumb.12:28; 28:1-6; Wal.26:3-6. Pindi
unapojifunga na ahadi yo yote inayohusiana na utii wa sheria, umeingia
tayari katika agano la Sheria, Yak.2:10.
Cho chote kile unachohesabu kwako kama haki yako ndipo kutokana
na hicho unapata ujasiri wako mbele za Mungu. Ukijisikia kwamba
umeliweka sawa swala la fedha na Mungu kwa kulipa zaka, basi
umekuwa chini ya laana: umekuwa na haki yako mwenyewe.
Hakuna rekodi kwamba Bwana wetu alilipa zaka baada ya kuanza huduma
Yake. Wale wote wanaodai moja ya kumi ya kila kitu unachopata
wanatambulishwa na waandishi na mafarisayo, waliokuwa adui wa
kihistoria wa Kristo. Wakati wa Bwana wetu, kulikuwa na kanisa “rasmi”
moja tu la Israeli:Hekalu la Yerusalemu. Waalimu wa leo wa zaka
wanafanya nyumba (jingo) ya kanisa lao kuwa sawa na Hekalu la Mungu na
hujitia kukaa katika kiti cha Musa, Math.23:1-3. Lakini kumbuka Mungu
haishi tena ndani ya mahekalu yaliyofanywa kwa mikono ya wanadamu,
Mdo.7:48. Kama imejiwekea wajibu kwa mtu mwingine anayekaa kwenye
kiti cha Musa, basi kulipa zaka hizo ni lazima. Kuna gharama za kutunza
jingo, watumishi na mambo mengine yanayotolewa. Tofauti ya Mafarisayo
wa Israeli ya Kale na Mafarisayo wa Ukristo Mkengeufu iko katika mstari
wa Mdo.17:24,25. Angalia pia Mdo.7:48; Math.23:38. Mapambo ya
majengo hayo ni kwa ajili yako wewe siyo kwa ajili ya Mungu.
Mwisho, katika Biblia kuna mtu mmoja aliyedai kulipwa moja ya kumi ya
kila kitu ulichopata. Mtu huyo ni Mfalme Sauli, 1Sam.8:15,17. Hapa
kwenye mistari hii hakuna nyongeza. Sauli atachukua moja ya kumi ya kila
kitu ulichonacho au kupata. Lakini sikia yale anayosema Bwana kuhusu
Mfalme Sauli katika 1Sam.8:18. watu pamoja na hayo waliendelea
kuvumilia maovu ya Sauli, 1Sam.8:7, kwa sababu ni rahisi kumlipa yeye
moja ya kumi yake kwa sababu ni rahisi kufanya hivyo kuliko kuchukuliana
na maneno ya Bwana Yesu Kristo, Luk.18:22. Angalia pia kuhusu hawa
Mafarisayo katika Luk.18:11,12.