Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 3

1

Matukio Muhimu Yatakayokuwepo Katikati ya Juma la 70 la


Danieli

1. Kwa muhtasari

 Shetani anatupwa chini duniani kutoka mbinguni, Ufun.12:12;


 Shetani anampa uwezo Mpinga Kristo, Ufun.13:12; 2Wathes.2:9;
 Ulinzi wa yeye azuiaye unaondolewa, 2Wathes.2:7; Dan.12:1;
 “mtu wa kuasi” anafunuliwa, 2Wathes.2:3;
 Chukizo la uharibifu linatendwa ndani ya hekalu, Math.24:15;
 Agano na Israeli linavunjika, Dan.9:24;
 Mpinga Kristo anajiinua mwenyewe juu ya wote, 2Wathes.2:4;
 Mpinga Kristo anadai kuabudiwa na ulimwengu wote, Ufun.13:3-
4, 12, 14b-15;
 Kahaba wa Babeli anangamizwa, Ufun.13:3-4,8,12-15; 17:16;
 Injili ya milele na onyo kwa wale watakaoipokea chapa ya Mpinga
Kristo linatolewa kwa ulimwengu na wajumbe malaika wa
Mungu, Ufun.14:6,8-9;
 Mashahidi wawili wanaanza huduma yao, Ufun.11:1-14;
 Mateso ya Waisraeli waaminifu (yaani mwanamke) na kanisa la
kweli (mabaki ya wazao wake ambao wanazishika amri za Mungu
na kutunza ushuhuda wa Yesu) yanaanza, Dan.12:1; Math.24:20b,
22-23; na
 Ukengeufu mkuu unaanza, Math.24:9-12; 2Wathes.2:3.

2. Kahaba wa Babeli

Kahaba wa Babeli ni viongozi wa mfumo wa dini ya uongo au mifumo


iliyoanzia Babeli wa kumuabudu Mama (Malkia wa Mbingu na Mtoto),
mfumo ambao Shetani ameutumia na atautumia tena kuwadanganya
mataifa kuhusu Kristo (uzao wa kweli wa mwanamke, Mwa.3:15, katika
jitihada yake ya kuwaangamiza wateule wa Mungu, Dan.11:39;
Ufun.17:1-7,9,15,18. Huu ni ukahaba wa kiroho. Angalia pia mlango wa
18 wa kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

Israeli pia ilionywa kwa kumuabudu malkia wa mbingu, Yer.44:16-19,


24-28 na matokeo yake mabaya kwa wale ambao hawakutii:

 Mfumo huu wa dini ya uongo utakaa juu ya maji mengi, yaani juu
ya watu wengi wengi, mataifa na lugha mbali mbali
2

watakaotawaliwa kutoka upande mmoja wa dunia mpaka


mwingine;
 Mfumo huu wa dini ya uongo utakuwa na nyenzo ya kisiasa,
maana Maandiko yanatuambia kwamba, “atawala juu yaw
wafalme wa dunia”;
 Mfumo huu wa dini ya uongo kwa nguvu zote utaupinga Ukristo
wa Kibiblia, yaani utalewa na “damu ya watakatifu na mashahidi
wa Yesu”; na
 Mfumo huu wa dini ya uongo utawakilisha “mji mkuu, utawalao
juu ya wafalme wa dunia”, Ufun.187:18; 18:10,18,19,21)

Mfumo huu wa dini ya uongo kwa karne nyingi kwa ujanja kabisa
umemuondoa “uzao wa mwanamke” (Kristo) na kuweka kumuabudu
mama na mtoto au “Malkia wa Mbingu” kulikolaaniwa kwa nguvu zote
na manabii wa kale, Yer.44:16-19; 24:28. Angalia pia Ufun.17:2,3,6.
Mwanamke kahaba huyu amewatawala kwa miaka mingi wafalme wa
dunia. Vivyo hivyo, katika siku za mwisho, uhusiano ule ule na ufalme
wa mwisho wa mnyama wa Shetani, kwa kutumia umaarufu wake wa
kimatatifa alioujenga hapo kale, atamsaidia Mpinga Kristo kukusanya
muungano wa mataifa kumi ambao utakuja kutawala dunia,
Ufun.17:12,13.

3. Kipimo (test) kwa namna mbili

Mpinga Kristo, mnyama wa kwanza atafunuliwa kama mtu aliyekuwa


amekufa na kurudia tena uzima katikati ya juma la 70, ambapo atajiinua
mwenyewe katika hekalu la Yerusalemu lililojengwa tena, na
kujitangaza kuwa yeye ni Mungu na kudai kuabudiwa na ulimwengu
wote.

Ndipo atakapoanzisha kipimo (jaribio) la namna mbili ili kuwatambua:

 wale watakaomuabudu na
 wale watakaokataa kumuabudu na kujitoa kikamilifu kwake.

Kipimo hiki kitatekelezwa na “mwingine” au “mnyama wa pili” ambaye


ndiye mkaziaji mkuu wa maagizo ya Mpinga Kristo na “anatumia
mamlaka yote ya mnyama wa kwanza”, Ufun.13:12.

Kipimo hiki kitakuwa na mambo mawili maalumu:


3

 Kwanza, kila mtu atatakiwa “kuiabudu sanamu ya mnyama au


kuuawa, Ufun.13:15; na
 Pili kila mtu atatakiwa kuipokea chapa ya mnyama ama sivyo
hawataweza kununua wala kuuza cho xhote, Ufun.13:16-18.

Msiba mkuu ni kwamba wengi wanaojiita Wakristo ndani ya Kanisa


lililokengeuka watajisalimisha kwa madai ya masanamu ya kishetani
yaw Mpinga Kristo, Ufun.14:9,10. Paulo analionya kanisa katika,
1Tim.4:1. Pia vile vile, Ezekieli anatabiri kwamba uzao wa asili wa
Ibrahimu utachagua kuyaabudu masanamu haya, kabla ya ghadhabu ya
Mungu haijawaangamiza, Ezek.7:19,20.

Kristo pia anawaambia wanafunzi Wake kuhusu muda huu maalumu


katika siku za mwisho, Math.24:9,10,12.

4. Subira ya Watakatifu, Ufun.3:10

Katika wakati huo, subira na imani ya watakatifu itajaribiwa vilivyo


tangia hapo katika historia ya kanisa, Ufun.13:10; 14:12. lakini Bwana
anawapa watakatifu Wake waaminifu ahadi katika Ufun.3:10.

Ndiyo maana, kanisa linaagizwa kwa umakini kabisa katika siku za


mwisho, kudumu ndani Yake Yesu, ili Atakapoonekana tusiaibike,
2Yoh.2:28. Kwa wale watakatifu watakaovumilia katika kipimo cha
Kishetani kwa wanadamu wote, kuna ushindi, Ufun.14:12,13.
Watakatifu hawa hawataingia katika adhabu ya milele ambayo iko tayari
kuijilia ulimwengu wa wasioamini katika Siku ya Bwana.

Kwa hiyo, kabla ya ghadhabu ya Mungu haijamwagwa juu ya


ulimwengu usioamini, Mungu atalinyakua kanisa Lake lenye subira,
akiliondoa katika eneo la hatari. Ufun.3:10b,11a. Na baadaye ndipo
ghadhabu Yake Mungu itamwagwa kwa wale watakaobakia duniani,
wakati muhuri wa saba wa gombo mwisho utakapovunjwa.

You might also like