KK

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Na Mwandishi wetu

Wakati usajili kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za


Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa
kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam
ukiendelea kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo
wamezindua mpango wa kujenga kituo cha michezo eneo la
msoga mkoani pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck
alisema,kamati ya uhurumarathon imeona umuhimu wa
kuanzisha kituo hicho ambapo jumla ya shilingi bilioni nne
nukta nane (4.8bl) zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha
mpango huo.
Tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uhurumarathon
imenunua shamba eneo la msoga mkoani pwani lenye ukubwa
wa ekari ishirini na tano kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha
kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo
la msoga na kitajulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru
Sports Accademy na jumla ya michezo kumi na moja itahusishwa
katika mkakati huo.
Tunatarajia kumkabidhi mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu
wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya michezo nchini
ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na
kukuzwa katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada
ya miaka mitano hadi kumi tutaweza kuanza kupata mafanikio.
Kituo hiki ndicho kituo pekee katika ukanda wan chi za Afrika
mashariki na kati ambapo jumla ya wanamichezo 2300
wataweza kuwa katika mpango wa awali.
Tunatarajia kupata nguvu toka katika wahisani mbalimbali wa
ndani nanje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji kuona Tanzania
ikipata mafanikio kupitia michezo.
Wakati huo huo Zaidi ya wakimbiaji 2700 wameshachukua form
kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku malengo makuu

yakiwa ni kuhitaji kushirikisha Zaidi ya wakimbiaji elfu kumi na


tano.
Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni 1.Triple seven
Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi supermarkets,Uwanja wa
Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi moshi
mjini,Arusha
na
katika
tovuti
ya
WWW.UHURUMARATHON.COM
au
kwa
kupiga
simu
0688108384.

You might also like