Taarifa Kwa Waandishi Wa Habari - Usafiri Kipindi Cha Chrimass 2014 Na Mwaka Mpya .

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

HALI YA USAFIRI KIPINDI CHA SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA

MPYA 2014.
Kila mwezi wa Desemba, Watanzania wengi sasa wamejenga utamaduni wa
kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka. Hili ni
jambo jema kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya vijiji wanakotoka.
Kutokana na wingi wa abiria hao, mahitaji ya usafiri huwa ni makubwa
kuliko huduma ya usafiri uliopo. Kwa sababu ya mahitaji makubwa ya
usafiri, baadhi ya watoa huduma huchukulia kipindi hicho kama njia ya
kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji kinyume na masharti ya leseni zao.
Aidha, kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali
kulipa zaidi kusudi wapate huduma ya kusafiri.
Kutokana na hali hiyo, Baraza linawakumbusha watoa huduma kufuata
masharti

ya

leseni

zao

na

kutoza

nauli

kama

ilivyoidhinishwa

na

SUMATRA. Baraza linatoa wito kwa wamiliki wote wa Mabasi kuwahimiza


wafanyakazi na mawakala wao wanaokata tiketi katika vituo mbali mbali nchini
kuwa waaminifu kwa wajiri wao na wateja wao.
Baraza linatoa wito kwa watu wote hasa ABIRIA wanaotarajia kusafiri
kipindi cha mwisho wa mwaka kufanya maandalizi ya safari zao mapema
ili kuepukana na matatizo ya kulanguliwa tiketi. Abiria hakikisha unatumia
haki yako ya kuchagua kwa kufanya maadalizi mapema ya safari yako ikiwa ni
pamoja na kufanya booking ya basi utakalo safiri nalo kutoka ofisi za wamiliki
wa Mabasi/mawakala wa kampuni ya mabasi husika.
Aidha, Baraza linatoa wito kwa abiria wote kutonunua tiketi za safari zao
kutoka kwa wapiga debe au vishoka katika eneo la kituo cha mabasi cha
Ubungo au vituo vingine nchini kote.

Page 1 of 3

Baadhi ya abiria wanalalamika kwamba, baadhi ya watoa huduma


wanakataa abiria wasifanye bookings mapema. Kuwakatalia abiria kufanya
booking mapema, kunasababisha abiria kurundikana kituoni siku ya safari bila
sababu yoyote na hivyo kutoa mwanya kwa wapiga debe na vishoka kuwalaghai
abiria hao. Tunaomba Abiria watakaokataliwa kufanya bookings zao mapema
kutoa taarifa kwetu au kwa Mamlaka ya SUMATRA kwa kutumia namba za
simu za Baraza 022 2127410, 0787787621; SUMATRA 0800110019 au
0800110020; barua pepe: info@sumatracc.go.tz.
Baraza la SUMATRA linatoa wito kwa abiria wote kuhakikisha unasafiri
kwa tiketi yenye jina na yenye kiwango cha nauli uliyolipa. Baadhi ya abiria
wanalipa kienyenji tu, analipa elfu 70 anapewa risti ya elfu 50. Abiria wa
namna hii huwa ndio wa kwanza kulalamikia mamlaka ya SUMATRA na Jeshi la
Polisi kitengo cha usalama barabarani. Tunawasihi sana abiria kuwa makini na
kutoa taarifa iwapo vitendo vya namna hiyo vitajitokeza mwaka huu. Tunatoa
wito kwa TABOA kuwa makini na wafanyakazi wao kutojihusisha na vitendo
vya namna hiyo kwani ikigundulika tiketi za kampuni husika zinalanguliwa,
mwenye kampuni atawajibishwa.
Mwisho, Baraza la SUMATRA linatoa wito kwa TABOA kuhakikisha madereva
wao wanaendesha magari kwa mwendo unaokubalika kiusalama. Kuna taarifa
kuwa kipindi cha XMASS mabasi mengi huenda mwendo wa kasi kusudi
wageuze siku hiyo kwa ajili ya kutengeneza fedha zaidi. Jambo hili
huhatarisha usalama wa abiria. Tutangulize usalama wa abiria na fedha iwe
baadaye. Biashara inabidi iendelee hata baada ya Xmass na Mwaka mpya.
Baraza linawatakia heri ya Xmass na Mwaka mpya.
Dr. Oscar Kikoyo
Katibu Mtendaji,

Page 2 of 3

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na


Majini,

Page 3 of 3

You might also like