MEM45

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 10

HABARI ZA

NISHATI &MADINI

NewsBulletin
Australia
http://www.mem.go.tz

Toleo No. 45

Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM

Tarehe - 5-11 Desemba, 2014

yaipa kipaumbele Tanzania

Somahabari Uk.2

Balozi wa Australia nchini anayemaliza muda wake, Geoff Tooth (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Ngosi Mwihava. Balozi huyo alimshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka katika Wizara na kumhakikishia kuwa Serikali ya Australia
imedhamiria kuuenzi ushirikiano huo ambao ni wa kihistoria. Alisema Tanzania ijiandae na uwekezaji mkubwa kutoka kwa kampuni kubwa za
Australia hususani katika masuala ya mafuta na gesi asilia.

Uturuki yasaini makubaliano kwa ajili ya kuimarisha sekta ya madini -Uk2


Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

NewsBulletin

NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

Australia yaipa kipaumbele Tanzania


Na Mohamed Saif

Tanzania imepewa kipaumbele cha pekee


na Serikali ya Australia katika programu
maalumu ya uwekezaji katika nchi za
Afrika.
Hayo yalielezwa na Balozi wa Australia nchini anayemaliza muda wake,
Geoff Tooth wakati alipotembelea Makao
Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini
kwa ajili ya kuagana na watendaji wakuu
pamoja na kutoa shukrani kwa ushirikiano
mzuri alioupata kutoka katika wizara.
Balozi Tooth alisema Kampuni kubwa
za nchini Australia zinatarajiwa kufanya
uwekezaji mkubwa nchini hususan katika masuala ya mafuta na gesi. Tunatarajia Tanzania kuwa kituo kikubwa cha
uwekezaji kwa Afrika. Kampuni kubwa
za Australia ambazo pia ni miongoni mwa
kampuni kubwa duniani zinatarajiwa kuwekeza hapa Tanzania, alisema Balozi
Tooth.
Alisema uhusiano baina ya Tanzania
na Australia ni mzuri na ni wa muda mrefu
ambao unapaswa kuendelezwa. Vilevile,
alisema kuwa Serikali ya Australia imejitolea katika kuwajengea uwezo wananchi
wa Tanzania kwa lengo la kujiletea maendeleo. Wawekezaji wanapaswa kuajiri
watanzania na hii itafanikiwa zaidi endapo
watanzania watajengewa uwezo. Hili tumelipa umuhimu sana na tunaimani litasaidia kuongeza idadi ya wataalamu na pia
kupunguza tatizo la ajira, alieleza Balozi
Tooth.
Aidha, Balozi alieleza kuwa, katika

Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) katika picha ya pamoja na Balozi Geoff Tooth (wa pili kutoka kulia).
Wa kwanza kushoto ni Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje katika Idara ya Asia na Australia, Bertha Makilagi, anayemfuatia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Rasilimaliwatu Lusius Mwenda kutoka wizara ya Nishati na Madini.

suala la kujenga uwezo, Serikali ya Australia imeamua


kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA), ili kutoa mafunzo yatakayowawezesha watanzania wengi kuajiriwa na kampuni za kigeni. Suala hili si tu kwamba litawanufaisha watanzania katika
kupata ajira lakini litawanufaisha wawekezaji kwa kujenga mahusiano mazuri na pia itapunguza gharama
kwa wawekezaji zitakazotokana na kuajiri wataalam-

wakigeni, alisema Balozi Tooth.


Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alimshukuru
Balozi Tooth kwa ushirikiano wake na wizara na pia
aliishukuru Serikali ya Australia kwa juhudi zake katika kuhakikisha watanzania wanajengewa uwezo ambao utawafanya wawe mahiri katika sekta mbalimbali.
Mhandisi Mwihava alitoa wito kwa wizara kush-

iriki kikamilifu katika suala la kutambua maeneo yenye


uhaba wa wataalamu wa kitanzania ili kuweza kupunguza uhaba huo.
Aidha, Mhandisi Mwihava alisema serikali ipo
tayari kushirikiana na wawekezaji kutoka Australia.
Hii ni habari njema, tunazo fursa nyingi za uwekezaji
kwahiyo wawekezaji wanakaribishwa sana, aliongeza
Mhandisi Mwihava.

Uturuki yasaini makubaliano kuimarisha sekta ya madini


Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

erikali ya Uturuki kupitia


Kurugenzi yake ya Utafiti wa Madini imesaini
makubaliano
ya awali
na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST) kwa ajili ya kuimarisha sekta
ya madini nchini kupitia wakala
huo.
Akizungumza kabla ya utiaji
wa saini wa makubaliano hayo,
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, amesema kuwa Tanzania ina hazina
kubwa ya madini ambayo bado
hayajachimbwa, hivyo inahitaji
wawekezaji, teknolojia na wataalamu kutoka nje ya nchi ili kuboresha sekta hiyo kwa manufaa ya
watanzania
Alisema kuwa, kutokana na
sekta ya madini kuwa na mchango
mkubwa katika pato la Taifa, Serikali imeweka mikakati mbalimbali
ya kuboresha sekta hiyo ikiwa ni
pamoja na kuimarisha Wakala wa
Jiolojia Nchini (GST) ambao una
majukumu mbalimbali ikiwemo
kukusanya, kuchambua, kutafsiri
na kutunza takwimu na taarifa
za kijiosayansi ambazo ni muhimu
katika kufahamu uwepo wa madini
mbalimbali nchini.

Aidha, Profesa Muhongo


alitaja maeneo ambayo Tanzania
itashirikiana na Uturuki kuwa ni
pamoja na kuwapo kwa programu
za kubadilishana utaalamu, uzoefu na teknolojia.
Tanzania kwa sasa ina madini ambayo hutumika katika
vifaa vya kielektroniki kama vile
saa, televisheni, simu za mikononi
ambayo yana soko kubwa duniani,
hivyo tunawakaribisha wawekezaji
kutoka popote ulimwenguni wenye
uwezo ili tushirikiane nao kuhakikisha kuwa tunapiga hatua kubwa
katika ukuaji wa uchumi, alisema
Profesa Muhongo.
Kwa upande wa sekta ya nishati Prof. Muhongo alisema kuwa
Tanzania ina uhitaji mkubwa wa
nishati ya umeme na kuongeza
kuwa hivi sasa Serikali inakamilisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka
Mtwara hadi jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kukamilika kwa
bomba hilo kutapelekea Tanzania kupiga hatua kubwa kiuchumi
kwani kutajengwa pia kiwanda
cha gesi kimiminika ( LNG), viwanda vya mbolea na saruji hali
itakayochochea kuongezeka kwa
fursa za ajira kwa wazawa na kuimarika kwa miundombinu kama
vile barabara, bandari pamoja na
viwanja vya ndege.
Akielezea ukuaji wa sekta ya
nishati nchini Prof. Muhongo
alisema kuwa ifikapo mwaka 2005

asilimia 10 tu ya watanzania walikuwa wameunganishiwa nishati


ya umeme lakini hadi kufika mwaka huu asilimia 36 ya wananchi
wameunganishwa na nishati ya
umeme.
Alisema kuwa lengo la Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa ifikapo
mwaka 2025 asilimia 75 ya watanzania wanakuwa wameunganishwa na nishati ya umeme na kuwa
nchi ya kipato cha kati.
Ili kufikia malengo haya serikali imekuwa ikisambaza umeme
vijijini kupitia Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) kwa kushirikisha
pia makampuni kutoka India na
China na bado tunazialika nchi
nyingi zenye uwezo ili kufikia
lengo lililowekwa aliongeza Prof.
Muhongo.
Aliongeza kuwa, Tanzania
ina hazina kubwa ya vyanzo vya
umeme kama vile jotoardhi, bayogesi, maji, gesi na kuitaka nchi ya
Uturuki kuhamasisha wawekezaji
wenye vigezo kuwekeza Tanzania
kupitia sekta za Nishati na Madini.
Naye Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Ngosi Mwihava aliongeza kuwa Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) lipo tayari
kushirikiana na taasisi binafsi ili
kuongeza nishati ya umeme nchini.
Naye Naibu
Mkurugenzi

Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti


wa Madini Nchini Uturuki, Dkt.
Abdulkerim Yorukoglu alisema
kuwa idara hiyo ipo tayari kushirikiana na GST kwa kubadilishana utaalamu na uzoefu ili kuhakikisha kuwa sekta ya madini
nchini inaimarika.
Akielezea uwezo na uzoefu
wa kurugenzi hiyo Dkt. Yorukoglu alisema kuwa kurugenzi hiyo

imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali


ambazo huhifadhiwa katika maktaba yake kubwa ya utafiti wa kijiolojia nchini Uturuki.
Alisema kuwa idara hiyo ambayo hutumia Dola za Marekani
milioni 100 kwa mwaka imekuwa
ikishirikiana na nchi mbalimbali za
kiafrika katika utafiti wa madini na
kusisitiza kuwa wapo tayari kushirikiana na Tanzania

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma


(kushoto waliokaa) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti wa Madini
ya Uturuki Dkt. Abdulkerim Yorukoglu ( kulia waliokaa) wakisaini makubaliano ya
awali (MoU) kwa ajili ya ushirikiano wa taasisi hizo katika masuala ya utafutaji wa
madini na ubadilishanaji wa ujuzi, uzoefu na teknolojia. Waliosimama kushoto ni
Kamishna Msaidizi wa Madini, Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje na kulia ni
Balozi wa Uturuki Nchini, Ally Davutoglu.

NewsBulletin

MAONI

http://www.mem.go.tz

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Ziara ya Norway ilete


manufaa kwa Taifa

uanzia tarehe 22 Novemba hadi tarehe 29 Novemba


mwaka huu viongozi mbalimbali wa dini walitembelea mji wa Stavanger nchini Norway kujifunza
kuhusu sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa Norway ilikuwa nchi ya tatu duniani kwa uuzaji wa gesi nje ya nchi na
nchi ya 10 duniani kwa uuzaji wa mafuta nje ya nchi. Uuzaji wa mafuta na gesi ulifikia Krooner ya Norway bilioni 564
(Dola moja ya Marekani sawa na Krooner 6.6) mwaka 2013,
ambazo ni sawa na asilimia 49 ya mauzo yote ya nje ya nchi
hiyo.
Ziara hiyo iliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini
kwa kushirikiana na Serikali ya Norway ilifanyika katika mji
huo kwa sababu ndio kitovu cha sekta ndogo ya mafuta na
gesi nchini Norway.
Katika ziara hiyo, viongozi hao wa dini walipewa mada
kutoka kwa wataalamu mbalimbali mafuta na gesi na maafisa
wa Wizara ya Nishati na Petroli na taasisi zake.
Viongozi wa dini wamejifunza mengi kutokana na ziara
hiyo na ni matumaini yetu kama viongozi wa jamii wenye
ushawishi na ufuasi mkubwa watalisaidia Taifa kunufaika na
sekta hiyo ndogo.
Kwa mfano, wamejifunza jinsi Norway ilivyodhibiti siasa
kuingia kwenye mambo ya mafuta na gesi na imesababisha
nchi hiyo kunufaika kwa amani.
Aidha viongozi hao wamejifunza jinsi ya kupunguza matarajio makubwa waliyonayo wananchi juu utajiri wa gesi na
mafuta. Hili ni eneo muhimu ambalo viongozi wa dini wa nafasi ya pekee kuwaelimisha wananchi kuwa utajiri huo hautatokea ndani ya siku moja, tunahitaji muda na uvumilivu
kwani hata Roma haikujengwa siku moja.
Lakini viongozi wa dini wamejifunza namna ya kuweka
tayari wananchi ili waweze kunufaika na sekta hii ndogo ya
mafuta na gesi. Hivi sasa kampuni kubwa duniani zipo Mtwara zikifanya utafiti na uchorongaji wa visima vya gesi.
Kwa mfano, walipokuwa nchini Norway, viongozi wa dini
waliambiwa kampuni ya Statoil ndio mnunuzi mkubwa wa
bidhaa na huduma duniani.
Sasa kampuni hii ipo mkoani Mtwara na kwa kushirikiana
na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) na kampuni
za Statoil, BG, ExxonMobil, Ophir na Pavilion zinatarajia kujenga mtambo wa kuchakata gesi asilia kwa ajili ya matumizi
mbalimbali (LNG) mjini Mtwara unaotarajiwa kutoa ajira za
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa watu 10,000.
Ukubwa wa mradi huu na miradi mingine ya gesi yanahitaji utayari wa wananchi ili waweze kunufaika na miradi hiyo.
Utayari huo ni pamoja na elimu ya kutosha ili wapate ajira
hizo, uanzishwaji vikundi ili viweze kutoa huduma na kuuza
bidhaa kwa kampuni hizo kubwa na kujiongezea kipato na pia
mafunzo ya ujasiriamali.
Ni matumaini yetu makubwa kuwa viongozi wa dini watatumia ushawishi wao katika jamii kuwaelimisha wananchi
juu ya utayari unaohitajika ili waweze kunufaika na sekta hii
ndogo ya mafuta na gesi.
Tunaupongeza uongozi wa Wizara na Serikali ya Norway
kwa kuandaa ziara hii na tunaamini kuwa manufaa yake kwa
Taifa yatakuwa makubwa.

Serikali kusimamia mikataba


ya gesi, mafuta - Mwihava
Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam

aibu Katibu Mkuu wa Wizara ya


Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava, ameeleza kuwa, Wizara
itaendelea kusimamia kwa umakini
mkubwa masuala yanayohusu mikataba ili kuhakikisha kwamba, Serikali na Wawekezaji
wananufaika sawa katika kugawana mapato yanayotokana na sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Naibu Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa Kampuni ya CNOOC
International ya China inayohusika na utafutaji na
uchimbaji wa mafuta na gesi waliokutana katika
kikao kujadili namna kampuni hiyo ilivyojipanga
kufanya shughuli zake katika sekta ya mafuta na gesi
nchini.
Win- win situation ndio lengo letu, tunataka
kufaidikika katika uwekezaji huu, lakini na ninyi
pia. Jambo hilo ni la msingi kwetu sote, aliongeza
Mhandisi Mwihava.
Kampuni ya CNOOC International ni miongoni
mwa kampuni zilizoomba kufanya tafiti za mafuta
na gesi katika Kitalu 43A pia ni moja ya kampuni

zilizokidhi vigezo kufuatia Zabuni ya Nne ya Vitalu vya Utafiti wa Mafuta na Gesi iliyotangazwa
na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) na maombi yake kufungwa rasmi
mwezi Mei mwaka huu.
Kwa upande wake Meneja katika Idara ya
Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya CNOOC
International Hu Gencheng alieleza kuwa kampuni
yake iko tayari kushirikiana na kufanya kazi na
Tanzania katika sekta husika kutokana na uhusiano
mzuri uliopo baina ya nchi hizo na zaidi kufuatia
uzoefu katika shughuli za utafutaji na uchimbaji
wa mafuta na gesi na kuongeza kuwa, kampuni hiyo
inalenga kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kiteknolojia na Tanzania ili taifa liweze kunufaika na
rasilimali hizo.
Tuko tayari kwa majadiliano na TPDC na
Wizara ili kufanya kazi na Tanzania katika sekta
hii. Tuna masoko, teknolojia na uzoefu mkubwa.
Tunataka kubadilishana ujuzi na ninyi ili maendeleo
tuliyofikia katika masuala haya yainufaishe na Tanzania, aliongeza Gecheng.
Kwa mujibu wa Gencheng, kampuni ya
CNOOC International ni kampuni ya pili Duniani
kwa ukubwa, teknolojia na utaalamu katika masuala
ya Gesi iliyosindikwa. (LNG).

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia), akiongea
jambo katika kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya CNOOC International ya China. Katikati ni
Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Ngosi Mwihava.

KWA HABARI PIGA SIMU


KITENGO CHA MAWASILIANO

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MHARIRI : Leonard Mwakalebela
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta

FIVE
PILLARS OF
REFORMS
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS

NewsBulletin

http://www.mem.go.tz

Mahafali chuo cha


Madini Dodoma

Baadhi ya wakufunzi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) wakielekea


eneo la mahafali.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Nishati) Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto)
akiwa kwenye maandamano ya mahafali ya Chuo cha Madini Dodoma (MRI), kulia
kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Prof.Abdulkarim
Mruma na watatu ni Makamu Mkuu wa Chuo Bw. Ramadhani Singano

Mkuu wa Chuo cha


Madini, Dodoma,
Sudian Chiragwile
akitoa taarifa ya
chuo kwa mgeni
rasmi wa mahafali
hayo ambaye ni
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini,
Charles Kitwanga.

Naibu Waziri wa Nishati


na Madini (Nishati)
Charles Kitwanga
akitoa hotuba kwa
wahitimu wa Chuo Cha
Madini (hawapo pichani)
wakati wa Mahafali.

Chuo cha Madini


(MRI) chafanya
mahafali ya kwanza
Na Robert Mukunirwa,
Dodoma

huo Cha Madini (MRI)


kilicho chini ya Wizara ya
Nishati na Madini kimefanya mahafali ya kwanza
mjini Dodoma ambapo
jumla ya wahitimu 368 walitunukiwa
vyeti katika ngazi ya stashada kwenye
fani mbalimbali.
Mahafali hayo yalifanyika tarehe 28 Novemba 2014 ambapo kati
ya wahitimu 368 waliotunukiwa vyeti, wanaume walikuwa 300 na wanawake 68.
Wahitimu hao walitunukiwa vyeti baada ya kufaulu katika kozi za
stashahada ya jiolojia na utafutaji madini, stashahada ya uhandisi uchimbaji madini na stashahada ya uhandisi
uchenjuaji madini.

Mahafali hayo yalienda sanjari na


uzinduzi wa madarasa mapya mawili
yaliyojengwa kwa ushirikiano wa serikali na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi asilia na mafuta ya BG
Tanzania Ltd.
Akizindua madarasa hayo,
Mgeni Rasmi katika mahafali hayo,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga aliwashukuru wote
waliochangia katika ujenzi wa madarasa husika. Pia aliishukuru kampuni
ya uchimbaji madini ya Resolute Tanzania Ltd kwa kujenga miundombinu
kwa ajili ya kufundishia masomo
hayo katika tawi la Nzega mkoani
Tabora.
Naibu Waziri kitwanga aliwasisitiza wahitimu hao kuitumikia nchi
kwa manufaa ya watu wote kwa kufuata maadili ya kazi, kuheshimu sheria za kazi, kuepuka rushwa, wizi na
vitendo vitakavyoweza kuleta maambukizi ya Ukimwi.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Nishati) Charles Kitwanga (katikati) akijiandaa kukata utepe
kufungua madarasa mapya mawili ya Chuo Cha madini. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Sudian
Chiragwile na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Prof. Abdulkarim Mruma.

NewsBulletin

http://www.mem.go.tz

Wawakilishi wa Kampuni ya CNOOC International Mjiolojia Mkuu wa kampuni


hiyo, Cui Hanyun (wa kwanza) na Meneja katika Idara ya Maendeleo ya
Biashara wa kampuni ya CNOOC International Hu Gencheng anayeonekana
kwa mbali wakiangalia Ramani ya shughuli za Utafiti kuonesha maeneo ambayo
wana nia ya kuyafanyia kazi za Utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi.

Waziri wa Nishati
na Madini
Profesa Sospeter
Muhongo (kulia)
akisisitiza jambo
kwenye ufunguzi
wa kikao kwa
ajili ya kusaini
makubaliano ya
awali (MoU) kati
ya Kurugenzi ya
Utafiti wa Madini
ya Uturuki na
Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi


Ngosi Mwihava (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa
Uturuki Nchini Ally Davutoglu.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akibadilishana


mawazo na Makamu wa Rais- Ukanda wa Jangwa la Sahara wa Kampuni
ya Maire Tecnimont Davide Pelizzola. Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni
hiyo Dario Giuliani.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa


Abdulkarim Mruma akielezea majukumu ya wakala huo kabla ya
kusaini makubaliano ya awali (MoU) kati ya Kurugenzi ya Utafiti
wa Madini ya Uturuki na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho kutoka ujumbe wa Uturuki akichangia mada kabla ya kusaini
makubaliano ya awali (MoU) kati ya Kurugenzi ya Utafiti wa Madini ya Uturuki na Wakala wa
Jiolojia Tanzania (GST)

NewsBulletin

http://www.mem.go.tz

Tanzania yaelezwa kuwa


na utajiri wa Mionzi ya Jua
Na Teresia Mhagama

afiti zinaonesha kuwa


eneo lote la Tanzania
hususan
Kanda ya
Kati, Kaskazini na Magharibi, lina mionzi
mikali ya jua inayofaa kuzalisha
umeme unaotokana na nishati
hiyo, na hivyo kuongeza kiwango
cha upatikanaji wa nishati hiyo
kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Capello
ya Italia, Bw. Giorgio Capello
ambaye pamoja na watendaji
wa kampuni hiyo walifika katika

Makao Makuu ya Wizara ya


Nishati na Madini kueleza nia ya
kampuni hiyo kujenga mitambo
ya kuzalisha umeme wa jua
pamoja na kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme jua nchini.
Bw. Capello aliwaeleza
watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, wakiongozwa
na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo kuwa
Kampuni hiyo ya Italia imeingia
ubia na kampuni ya kitanzania
ya Derm Electrics na kuunda
kampuni inayoitwa DermCapello
ili kwa pamoja waweze kuwekeza
kwenye umeme wa jua.
Tunataka kuanza kuzalisha

umeme wa megawati moja na


kuuingiza kwenye gridi ya Taifa
ili kuongeza kiwango cha umeme
kinachoingia kwenye gridi hiyo,
na mazungumzo ya uwekezaji
yakikamilika tunatarajia kukamilisha mradi huu ndani ya miezi
Sita.
Lengo letu la kuzalisha
umeme wa jua halitaishia katika
kuzalisha megawati moja pekee,
bali tutakuwa tukiongeza kiwango
hicho kadri muda unavyoendelea,
endapo tutapata kibali cha kufanya hivyo. Ila sasa tunataka tuanze
na hii megawati moja kwanza ili
kuwa na ufanisi katika utekelezaji
wa mradi, alisema Capello.

Mkurugenzi wa kampuni ya DermCapello, Mhandisi Ridhwani Mringo (wa kwanza kushoto), akizungumza
masuala mbalimbali kuhusu kampuni hiyo inayotaka kuwekeza katika umeme jua na kujenga kiwanda cha
kutengeneza vifaa vya umeme jua nchini.Wanaomsikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (katikati) na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na kampuni ya DermCapello

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na kampuni ya


DermCapello waliohudhuria kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (haonekani pichani) na watendaji wa
kampuni hiyo wakifuatilia mazungumzo kati ya pande hizo. Wa pili
kulia ni Mchumi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Nicolaus Moshi,
Mwanasheria wa Wizara, Abbas Kisuju, na Eng. Innocent Luoga,
kamishna Msaidizi Nishati anayeshughulikia Umeme. Wa kwanza kulia
ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Capello ya Italia, Giorgio Capello.
Kwa upande wake, Profesa Sospeter Muhongo, aliwaeleza watendaji
wa kampuni hiyo kuwa mradi huo ni muhimu kwa nchi lakini lazima
wataalam wanaohusika na masuala ya Nishati wajiridhishe kuwa kampuni hiyo inao uwezo wa kuwekeza kwenye miradi hiyo. Hivyo aliwaagiza watendaji hao wa DermCapello kuanza mazungumzo na Taasisi
zinazohusika na masuala ya nishati nchini.
Waziri Muhongo, alieleza kuwa umeme wa jua unahitajika kuongezwa katika gridi ya taifa ili kupunguza utegemezi wa maji na mafuta
mazito katika uzalishaji umeme, vilevile kusaidia katika maeneo ya huduma za kijamii kama hospitali, vituo vya afya, sehemu za ibada na ofisi
za umma katika maeneo ambayo yako nje ya gridi ya Taifa
Hivi sasa Serikali inaendelea na kazi ya ujenzi wa maabara katika
shule nchini, hivyo umeme wa jua utasaidia katika kuwezesha maabara
hizo kupata umeme hata katika maeneo ambayo hayajafikiwa na gridi ya
Taifa.Hivyo Tunataka kuona uwekezaji wa umeme jua unaanza kuzaa
matunda na si mazungumzo yasiyoisha, alisema Waziri Muhongo.
Kuhusu kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme jua, amesema
serikali inapenda kuwa na kiwanda hicho ili kuwezesha upatikanaji wa
vifaa hivyo hapa nchini badala ya kuagiza nje ya nchi jambo ambalo pia
litasaidia katika kukuza ajira kwa watanzania.
Aliwaeleza watendaji hao wa DermCapello kuwa, kuwepo kwa
kiwanda hicho nchini kutazinufaisha pande zote mbili yaani Tanzania
na DermCapello kwani kampuni hiyo itaweza kuuza vifaa vyake katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi zilizo
Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo Tanzania ni mwanachama.
Lakini ninachowaeleza ni kwamba msiweke miradi hii yote jijini
Dar es Salaam bali mwende mikoani kwa mfano mkoa wa Tanga, ambao
utaiwezesha kampuni kusafirisha vifaa kwa njia ya bahari na mtakuwa
karibu na mifumo mingine ya usafiri kwa nchi za Afrika Mashariki,
hivyo itakuwa rahisi kwenu kupeleka bidhaa katika nchi hizo, alisema
Profesa Muhongo.

Rais wa kampuni ya Capello ya Italia, Capello Giuseppe akizungumza wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini. Kampuni hiyo iliyoungana na
watanzania na kuunda kampuni ya DermCapello walifika Wizara ya Nishati na Madini ili kueleza nia yao kuwekeza katika umeme wa jua.

NewsBulletin

http://www.mem.go.tz

Wachimbaji
wadogo kunufaika
miradi ya SMMRP
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja, akizungumza jambo
wakati wa kikao cha Kamati Tendaji inayoratibu miradi kupitia Mradi wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali Madini Nchini (SMMRP), iliyokutana kujadili masuala
mbalimbali kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizopangwa
kutekelezwa katika Awamu ya pili.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji inayoratibu miradi kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa
Rasilimali Madini Nchini (SMMRP), wakimsikiliza Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Paul Masanja
(hayupo Pichani), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,

Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam

meelezwa kuwa, wachimbaji wadogo wa madini nchini wanatarajiwa kunufaika kutokana


na utekelezaji wa Awamu ya pili wa miradi
mbalimbali ya kuwasaidia wachimbaji kupitia
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali
Madini Nchini (SMMRP) unaosimamiwa na Wizara Nishati na Madini.
Akizungumza katika kikao cha Kamati Tendaji
inayoratibu utekelezaji wa miradi hiyo, Meneja Miradi,
Mhandisi Idrisa Yahya ameeleza kuwa, awamu ya pili
ya utekelezaji wa miradi hiyo inalenga kuwezesha maeneo kadhaa ambayo wachimbaji wadogo wanatarajiwa
kunufaika zaidi.
Aidha, aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na
kuboresha sekta nzima ya madini Tanzania, Kuimarisha Utawala Bora na uwazi katika tasnia ya madini,

kuchochea uwekezaji, na ufuatiliaji wa utekelezaji


miradi hiyo.
Akizungumzia namna ya uboreshaji wa sekta ya
madini utakavyotekelezwa, alieleza kuwa, uboreshaji
utalenga katika uongezaji thamani madini ya Vito
ambapo Serikali imepanga kukiimarisha na kukiboresha Kituo cha Jiomolojia Tanzania (TGC) kilichopo
jijini Arusha ambapo kituo hicho kinatarajiwa kutoa
mafunzo mbalimbali ya uchongaji na ukataji madini,
kwa lengo la kuongeza thamani madini. Alieleza kuwa,
tayari ukarabati na uboreshaji miundombinu katika
Chuo hicho upo katika hatua za mwisho. Aidha, mkazo
utakuwa uongezaji thamani madini ya viwandani ambayo yanachimbwa na wachimbaji wadogo.
Aliongeza kuwa, mradi pia utawezesha utoaji
wa mafunzo mbalimbali katika tasnia ya kusanifu,
kuchonga na ukataji wa madini ya vito na vinyago
vya mawe; lengo likiwa ni kuongeza ushindani na
kupata bei nzuri ya madini nchini na katika masoko ya
Kimataifa. Aidha, alisema lengo lingine ni kuongeza

Meneja Miradi wa SMMRP Mhandisi Idrisa Yahya (wa kwanza kulia), akiongea
jambo wakati wa kikao cha Wajumbe wa Kamati Tendaji inayoratibu miradi kupitia
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini nchini (SMMRP), anayesikiliza
ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kitengo cha Baruti, Oforo Ngowi
ajira kwa vijana wa Tanzania na Pato la
Taifa, Vilevile, aliongeza kuwa, wachimbaji
madini wanatarajiwa kunufaika kupitia
ruzuku ambayo imeongezwa kiwango
huku kipaumbele kingine kikitolewa
kwa wanawake wanaofanya shughuli za
uchimbaji kwa kuongezewa ruzuku ya dola
za Marekani 30,000 ikiwa ni kiwango cha
juu, itakayowawezesha kufanya shuguli
nyingine za kiuchumi tofauti na shughuli
za madini.
Kwa upande wa wachimbaji madini
wadogo katika awamu ya pili ya ruzuku
imeongezewa kiwango kutoka Dola za
Marekani 50,000 hadi Dola za Marekani
100,000 na wakina mama au vikundi vya

wakina mama wanaojishughulisha na


uchimbaji mdogo wa madini wanahamasishwa kuomba mara matangazo ya
kuomba ruzuku yatakapo toka katikati ya
mwezi huu wa Disemba 2014.
Kama alivyoeleza Kamishna Msaidizi
wa Madini anayeshughulikia wachimbaji
wadogo Julius Sarota wakati akiwasilisha
mada katika mkutano wa wadau wa
madini ya Shaba uliofanyika hivi karibuni,
aliongeza Idrisa.
Kuhusu utekelezaji wa miradi na
shughuli nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika awamu ya pili, Mhandisi Idrisa
alieleza kuwa, lengo limekamilika kwa
asilimia 95.

STAMIGOLD KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Na Jacqueline Mattowo &


Godfrey Francis -STAMIGOLD

Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo kupitia


wataalam wake wa Idara ya Jioloji umeahidi
kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kutoka
Kijiji cha Mavota kilichopo takribani kilomita 7
kutoka eneo la mgodi. Wataalamu hao watawasaidia wachimbaji wadogo kutambua maeneo yote
ya uchimbaji yanayomilikiwa na mgodi huo ili
kuwawezesha kufanya shughuli zao katika maeneo
halali na kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina
ya Kampuni na wenyeji.
Ahadi hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mjiolojia
Mkuu wa mgodi wa STAMIGOLD, Ayoub Nyenzi
katika kikao baina ya wataalam wa Jiolojia na
kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini mara
baada ya kupokea barua yao. Barua ya wachimbaji
wadogo kupitia Idara ya Uhusiano wa jamii iliomba
msaada wa kitaalamu pamoja na vifaa na vilevile

kuutaarifu uongozi wa mgodi uwepo wa kikundi


hicho chenye jumla ya wanachama 20.
Mjiolojia Nyenzi, alianza kwa kukipongeza
kikundi hicho kwa kuwa na uthubutu na pili hatua
za msingi walizofikia baada ya kuunda kikundi
ambazo zimezaa maamuzi ya busara ambayo
wameafikiana pamoja.
Sisi kama mgodi tunayo ramani na leseni za
maeneo yetu yote ya uchimbaji na kama mnavyoelewa ukanda huu wote uko kwenye ramani kuu ya
dunia, hivyo kuna baadhi ya maeneo mengine tayari
yanamilikiwa na watu lakini naamini kuwa bado
yatakuwepo maeneo yaliyo wazi, hivyo msije kukata
tamaa. Sisi tunaahidi kushirikiana nanyi katika hatua
zote kuhakikisha eneo mtakalopata halipo ndani ya
mipaka ya mgodi,alieleza Nyenzi.
Aliongeza kuwa STAMIGOLD ipo tayari kutoa
wataalam kwa ajili ya utaalam wa kutambua maeneo
yenye migodi na kuwasaidia mambo mengine yaliyo
ndani ya uwezo wa mgodi na vilevile wachimbaji hao
wanapaswa kufahamu sera na sheria za uchimbaji

madini nchini kwani mchimbaji mdogo hawezi kupewa ama kumiliki eneo la mchimbaji mwenye leseni
kubwa japokuwa mchimbaji mkubwa anaruhusiwa
kumiliki eneo la mchimbaji mdogo kisheria.
Katika kuthibitisha hayo Nyenzi alionyesha leseni
kadhaa za STAMIGOLD na jinsi ya kuingiza Kodineti katika ramani za umiliki wa maeneo na kuweza
kutambua kama eneo hilo liko ndani ya mgodi wa
STAMIGOLD.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Husein Kavula
alifafanua kuwa, kikundi chao kinaendelea kufuata
taratibu zote za kisheria ili kupata eneo lililo wazi kwa
ajili ya kuanzisha shughuli za uchimbaji madini hivyo
STAMIGOLD kama mgodi wa jirani ni vyema
kufahamu hilo.
Tunaomba ushirikiano wa namna yoyote aidha
wa kiushauri ama kitaalamu ili kufanikisha azma
yetu kwani shughuli za uchimbaji hasa upimaji wa
kodineti kwa ajili ya utafiti wa eneo lililo wazi na
lenye madini linahitaji msaada wenu. Hivyo, sisi
kama wachimbaji wadogo tunaomba ushirikiano

wenu kutambua maeneo hayo ili kuepusha migogoro


ya maeneo ya uchimbaji, alieleza Kavula.
Naye Katibu Mkuu wa kikundi hicho, Jonathan
Joseph aliusifu mgodi wa STAMIGOLD kwa
kukubali wito na kutoa wataalam ambao wamewapa
elimu pamoja na mawazo mazuri ya jinsi ya kuendeleza kikundi chao. Tunashukuru pia kwa utayari
wa wataalam hao ambao wameahidi kutuchukulia
kodineti wakati wowote tutakapokuwa tayari,
aliongeza Bw. Joseph.
Zoezi la kusaidia wachimbaji wadogo ni
utekelezaji wa wito uliotolewa wakati wa uzinduzi wa
tofali la kwanza la dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo.
Waziri Muhongo alitoa wito wa mgodi na
uongozi wa Wilaya na Mkoa kusaidia vikundi vidogo
vinavyotaka kujihusisha na uchimbaji wa madini ili
kupunguza migogoro sehemu za uchimbaji na vile
vile kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na hasa kwa
vijana.

NewsBulletin

http://www.mem.go.tz

Kampuni ya Uingereza yaomba


kuandaa Kongamano la Mafuta na Gesi
Na Teresia Mhagama,
Dar es Salaam

ampuni ya Global Event


Partners (K) Ltd yenye
makao makuu yake jijini
London Uingereza imewasilisha ombi kwa Wizara ya Nishati
na Madini la kuandaa kongamano
kubwa la kimataifa la mafuta na gesi
ambalo litahusisha wawekezaji zaidi
ya 400 katika sekta hiyo linalopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam,
mwezi Oktoba mwaka 2015.
Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Bw. Danny Grogan
amesema kuwa kongamano hilo
litakalowakutanisha wawekezaji wa
kimataifa katika sekta ya mafuta na
gesi litakuwa na faida mbalimbali
ikiwemo kuvutia uwekezaji zaidi
katika sekta husika, na kuhakikisha
kwamba njia bora zinatumika katika
masuala ya uwekezaji wa sekta hiyo.
Pamoja na mambo mengine,
kongamano hilo la siku mbili litajikita pia katika kuionesha dunia fursa
za uwekezaji zilizopo Tanzania
tukitilia mkazo masuala ya zabuni
za utafiti wa mafuta na gesi zinazofuata, shughuli za utafiti na uchimbaji gesi katika kina cha bahari na
nchi kavu, na fursa zinazotokana na
uwepo wa bomba la gesi, alisema
Grogan.
Bw.Grogan amesema kuwa
kampuni hiyo imeshaandaa makongamano kama hayo katika nchi
mbalimbali barani Afrika ambazo
zilipata matokeo chanya kutokana
na kufanyika kwa makongamano
hayo. Alizitaja nchi hizo kuwa ni
Algeria, Misri, Ghana, Kenya na
Libya, na kueleza kuwa hii inaonesha kuwa jumuiya ya kimataifa
inaiamini kampuni hiyo katika
maandalizi ya makongamano hayo.
Hatutaweza kufanya kongamano hili bila ushirikiano na serikali
ya Tanzania, hivyo tunachohitaji
kutoka kwenu ni ushirikiano ili
kongamano hilo lifanikiwe kwa
sababu gharama zote za kongamano
hilo zitabebwa na kampuni yetu ,
alisema Bw.Grogan.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Mwihava amesema
kuwa serikali inatambua umuhimu
wa makongamano hayo katika sekta
ndogo ya mafuta na gesi na kwamba
inalifanyia kazi suala hilo kabla ya
kutoa maamuzi.
Ninachoweza kukwambia tu ni

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Events and
Partners ya Uingereza, Danny Grogan (kushoto) ambayo imeleta ombi la kuandaa kongamano la Mafuta na Gesi na mafuta nchini.Wengine katika picha
ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati na Madini, Mrimia Mchomvu (wa pili kulia) na Mchumi Mwandamizi, Oscar Kashaigiri (wa
pili kushoto).

kuwa mwaka 2015 si mwafaka sana


kwa kufanya kongamano hilo kutokana na ratiba ya kazi kwa mwaka
huo ambao utakuwa na matukio
mengi kama uchaguzi mkuu wa

taifa. Pia tayari kuna ratiba ya makongamano mengine yenye dhima


kama ya kampuni yenu ambayo
yatafanyika pia katika mwaka
2015 yanayoandaliwa na taasisi za
Kitaifa na Kimataifa.

Hivyo yote haya inabidi


tuyafikirie kabla ya kufanya
maamuzi na kutoa majibu katika
mfumo ulio rasmi, alisema Naibu
Katibu Mkuu.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Events Partners
ya Uingereza, Danny Grogan. Kampuni hiyo imeleta ombi la kuandaa kongamano la Mafuta na Gesi nchini.

NewsBulletin
Norway
Ujenzi wa mtambo wa
gesi kuchukua miaka 7

http://www.mem.go.tz

Na. Leonard Mwakalebela aliyekuwa Norway

JENZI wa mtambo wa
kuchakata gesi asilia kwa
ajili ya matumizi mbalimbali (LNG) mjini Mtwara
unakadiriwa kuchukua miaka takriban saba na kutoa ajira kwa watu
10,000.
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya
Statoil Tanzania Bw. Thomas Mannes
amesema kuwa, mambo yakienda kama
yalivyopangwa, mtambo huo utakuwa
tayari kwa uchakataji kati ya mwaka 2022
au 2023.
Akizungumza na viongozi wa dini
wa Tanzania waliotembelea mtambo wa
uchakataji gesi wa Statoil uliopo Karsto,
Bw.Mannes amesema kuwa mradi huo
mkubwa utagharimu mabilioni ya dola za
Marekani.
Tunakadiria itachukua kama miaka
saba, mmoja kwa utafiti wa eneo kujua
uimara wake kiufundi, miaka miwili ya
utafiti wa kiuhandisi na michoro na miaka
minne ya ujenzi wenyewe alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Mannes,tayari
wamekwishapendekeza maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mtambo huo na hivi
sasa wabia wa mradi wanateua timu ya
pamoja itakayosimamia mradi huo.
Mradi huo utakuwa wa pamoja kati
ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini
(TPDC) na kampuni za Statoil, BG, ExxonMobil, Ophir na Pavilion. Mradi huo
utaenda sambamba na miradi mingine ya
mafuta ya vitalu 1,3 na 4 inayoshirikisha
TPDC, BG,Ophir na Pavilion na mradi wa
gesi wa kitalu 2 wenye ubia kati ya TPDC,
Statoil na ExxonMobil.
Bw. Mannes alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na
manufaa makubwa kwa Tanzania kwani
kutaongeza mapato na nafsi za ajira, kutachochea biashara za bidhaa na huduma,

kutaongeza mchango katika Pato la Ndani


la Taifa (GDP) na kutaleta uwiano mzuri
wa biashara.
Aidha amewataka Watanzania hususani wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara
kujipanga vizuri kwa ajili ya kufanya biashara ya bidhaa na huduma kwani kampuni yake itatoa kipaumbele wa kufanya
biashara na wazawa.
Bw. Mannes aliongeza kuwa mkataba
kati ya Statoil na serikali ni wa manufaa
kwa pande zote mbili na kuwa ni wa viwango na taratibu zote za kimataifa.
Kwa mujibu wa Mshauri Mwelekezi
wa mafuta na gesi nchini Norway, Bw.
Willy Olsen, ujenzi wa mtambo huo utatoa
ajira kwa watu 10,000.
Asilimia 80 ya waajiriwa watakuwa
wataalamu na mafundi, na kila mfanyakazi mmoja akiajiriwa atatengeneza ajira zisizo za moja kwa moja kwa watu Watano
hadi Sita alifafanua.
Akiwasilisha mada yake mbele ya
viongozi hao wa dini, Bw. Olsen alisema
kuwa wasambazaji huduma na wauzaji
wa bidhaa wa Tanzania watanufaika sana
kwani Statoil ndio mnunuzi mkubwa Duniani ikiwa na wasambazaji huduma zaidi
ya 12,000 Duniani.
Naye Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw. Ove Tungesvik alisema
kuwa mtambo wa Karsto ndio mkubwa
kuliko yote barani Ulaya.
Kwa upande wao, viongozi hao wa dini
wameishauri kampuni ya Statoil kuwajengea uwezo watanzania, kupitia mafunzo
na programu nyingine, kama Wanorway
walivyosaidiwa na wamarekani katika
miaka ya 1970, ili watanzania nao waweze
kuisimamia sekta ndogo ya mafuta na gesi
katika miaka michache ijayo.
Viongozi hao wa dini walikuwa mjini
Stavanger, nchini Norway katika ziara ya
mafunzo ya sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Ziara hiyo iliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Serikali
ya Norway kupitia kwa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

WANAFUNZI KATAVI WAHIMIZWA


KUZINGATIA MASOMO
Na Jacqueline
Mattowo &
Godfrey FrancisSTAMIGOLD

anafunzi wa
Chuo cha
Madini cha
Katavi kilichopo Mkoa
mpya wa Katavi wamehimizwa
kuzingatia masomo na kufanya
vizuri katika mitihani ili waweze
kufanikiwa katika maisha kutokana
na umuhimu wa elimu kwa maisha
yao.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Meneja Mkuu
wa mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo, Bi. Enea Minga wakati
akizungumza na wanafunzi wa
chuo hicho waliohitimu mafunzo
ya vitendo (field) katika Idara za
Uchimbaji ( Mining) na Uchenjuaji
( Process Plant) mgodini hapo.
Bi. Minga alieleza kuwa ikiwa
wanafunzi hao watasoma kwa bidii
na kufanya vizuri katika mitihani
yao, watafanikiwa kutimiza ndoto
zao walizojiwekea pamoja na kupata nafasi ya kujiendeleza zaidi
kielimu.
Ni matumaini yangu kuwa
mmejifunza mambo mengi kwa
kipindi chote mlichokuwa hapa

na sasa mnaelewa vizuri shughuli


mbalimbali zinazofanywa na mgodi
huu. Hivyo, nina imani kuwa mtapata mwangaza zaidi katika elimu
ya nadharia inayofundishwa chuoni
na hiyo ni sababu tosha ya kuongeza
ufanisi zaidi katika masomo yenu,
alieleza Minga.
Alisema kuwa, ujuzi ambao
wanafunzi hao wameupata kupitia
mafunzo ya vitendo pia utawasaidia
baadaye pindi wapatapo nafasi za
kufanya kazi na hivyo, kuwashauri
kuzingatia masomo na kutoa kipaumbele zaidi katika elimu.
Akizungumza kwa niaba ya
wanafunzi wenzake, Linus Andrea
aliushukuru uongozi wa mgodi,
kwa kukubali kutoa nafasi ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa katika mgodi huo kwani
nafasi hiyo imewasaidia kujifunza
mambo mengi waliyokuwa wakiyafahamu kwa nadharia tu na mengine ya ziada ambayo hawakuwa
wakiyafahamu.
Natoa wito kwa kampuni nyingine za binafsi na za serikali kutoa
nafasi za masomo ya vitendo kwa
wanafunzi na hasa wale wanaotoka
katika vyuo vidogo ili wapate nafasi za kujifunza zaidi yale wanayofundishwa kwa nadharia vyuoni.
Hii itawasaidia kukuza viwango
vya ufalu katika masomo yao na
baadaye kuongeza wataalam wa
fani mbalimbali katika sekta ya madini na kuendeleza rasilimali za taifa
letu, alisema Andrea.

Mafunzo hayo yaliyodumu


kwa muda wa miezi miwili yalihusisha wanafunzi 15 na kuendeshwa
kwa mfumo wa wanafunzi kubadilishana katika idara za uchimbaji na
uchenjuaji kila baada ya muda ili
kuwawezesha kuelewa vizuri kazi
zinazofanywa na idara hizo badala
ya kubaki kwenye idara moja tu
hivyo kutotimiza malengo yao ya
kujifunza.
Wakati huo huo, wanafunzi
walipata nafasi ya kutembelea idara
nyingine za mgodi (familiarization
tour) ikiwemo Idara ya Mazingira,
Idara ya Rasilimali watu na Idara ya
Usalama Kazini ili kufahamu kazi
mbalimbali zinazofanywa na idara
hizo. Kaimu Meneja Mkuu wa
mgodi aliweza kukabidhi vyeti vya
mafunzo ya awali ya kupambana na
moto (Basic Fire Fighting Training)
yaliyofanywa na Idara ya Usalama
Kazini kwa wanafunzi wote 15.
Hivi sasa Chuo cha Madini
Katavi kinatoa mafunzo ya Uhandisi katika Uchimbaji kwa ngazi ya
cheti (Certificate in Mining Engineering) kwa muda wa mwaka 1.
Wanafunzi wanaosoma miaka miwili hadi mitatu hufanya mitihani ya
kitaifa ya ngazi ya pili na tatu (level
II & level III) na kupata cheti kutoka
Wizara ya Nishati na Madini na
baadaye kujiunga na vyuo vingine
nchini kikiwemo Chuo cha Madini
cha Dodoma.

Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa


STAMIGOLD, Enea Minga (kulia)
akimkabidhi mwanafunzi wa chuo
cha madini Katavi cheti cha mafunzo
ya awali ya kupambana na moto
wakati walipokamilisha muda wao
wa mafunzo ya vitendo katika mgodi

wa huo.

Afisa wa Idara ya Mazingira katika


mgodi wa STAMIGOLD Jopheline
Bejumula akiwaelekeza jambo
baadhi ya wanafunzi wa chuo cha
madini Katavi wakati walipotembelea idara ya Mazingira kujifunza kazi
wanazofanya.

NewsBulletin

10

http://www.mem.go.tz

UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

Taifa tunalojivunia ni lile lenye uchumi imara unaotoa ajira na maisha bora kwa wote. Tanzania
yenye amani, utulivu wa utaifa wa kudumu. Tumeingia kwenye uchumi wa gesi asilia wenye mapato
makubwa yatakayoondoa umasikini nchini mwetu. Uongozi wa kizalendo na wenye umahiri mkubwa
unahitajika. Tuchape kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa sana. Kizazi chetu kitashinda na
vizazi vijavyo navyo vitaushinda umasikini. Hii ndiyo Tanzania tuitakayo

STAMIGOLD YATOA MADAWATI


350 KWA SHULE ZA MSINGI
Na Mwandishi Wetu

ampuni Tanzu ya Shirika


la Madini la Taifa (STAMICO), STAMIGOLD,
kupitia mgodi wake uliopo
wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera umekabidhi jumla ya Madawati
350 kwa shule mbalimbali za msingi
mkoani Kagera.
Shule za msingi zilizopewa
Madawati ni pamoja na Mavota
(100), Mkunkwa (130), Kaniha (50),
Mpago (30), Msalabani (40) zote za
wilaya ya Biharamulo.
Meneja Mkuu STAMIGOLD
Mhandisi Dennis Sebugwao alikabidhi madawati hayo yenye thamani
ya shilingi milioni 17 kwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya
ya Biharamulo Bw. Zabron Njanga, Mhandisi Sebugwao alisema,
mpango huo wa kusaidia madawati
mashuleni unafuatia ombi la ali-

yekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera


Kanali Fabian Massawe katika jitihada za kuinua kiwango cha elimu
mkoani humo.
Aidha, Mhandisi Sebugwao
aliongeza kuwa, kampuni ya STAMIGOLD inaunga mkono juhudi
hizo kwa kuwajibika kwa jamii
kwa namna hiyo na kuueleza
mpango mkakati wa mgodi huo ni
kugawa zaidi ya madawati 1000 ifikapo Februari 2015 ili kupunguza
tatizo la uhaba wa madawati katika
mkoa wa Kagera.
Kwa kufanya hivyo tutawajengea wanafunzi mazingira mazuri ya
kupenda shule na hivyo kuinua kiwango cha ufaulu mkoani Kagera.
Baada ya tathmini tuliyoifanya katika shule za msingi zilizo Wilayani
Biharamilo kwa kushirikiana na
Afisa Elimu wa Wilaya imetusaidia
kujua uhitaji na shule zinazotakiwa
kupewa kipaumbe,alisisitiza.
Mhandisi Sebugwao alisema

Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD


Naibu WaziriMhandisi
wa Nishati
Dennis
na Madini
Sebugwao
anayeshughulikia
(kushoto), akimkabidhi
Madini,
msaada wa Madawati Afisa Mipango
Stephenwa
Masele
Wilaya
akimpa
ya Biharamulo,
zawadi yaZabron
kinyagoNjanga
iliyotolewa
(kulia)na
Madawati hayo yamekabidhiwa
mtandao
na kampuni
wa Vijana
hiyoWanasayansi
hivi karibuni.Duniani (YES), Rais wa

kuwa, matarajio ya STAMIGOLD


ni kupunguza tatizo hilo linalochangia kudorora kwa kiwango
cha Elimu mkoani Kagera kutokana na mazingira yasiyo rafiki katika
ufundishaji na usomaji.
Kampuni ya STAMIGOLD
iko tayari kusaidiana na wazazi na
serikali katika kuzijengea mazingira rafiki shule hizo, alisema.
Vilevile, Mhandisi Sebugwao
alisema kuwa, ipo haja kwa kampuni ya STAMIGOLD kusaidia
ujenzi wa vyumba vya madarasa
kwa ajili ya shule ya Msingi Mpago ambayo hivi sasa ina vyumba
viwili tu vya madarasa jambo ambalo linasababisha wanafunzi kusomea chini ya miti.
Mhandisi Sebugwao alimweleza mwalimu Mkuu wa shule
ya msingi Mpago, Bw. Sebastian
Mkiza kuwa, kampuni hiyo iko
tayari kusaidiana na shule hiyo
kuhakikisha inasaidia kuboresha

mazingira ya shule hiyo ili yaweze


kuwa rafiki kwa walimu na wanafunzi.
Akipokea madawati hayo, kwa
niaba ya wakuu wa shule zilizopewa madawati Afisa Mipango wa
Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Zabron Njanga aliipongeza
Menejimenti ya STAMIGOLD
kwa namna walivyoguswa na
tatizo la upungufu wa madawati
na kuchukua hatua za makusudi
kupambana na tatizo hilo.
Aidha, Bw. Njanga alieleza
kuwa,
STAMIGOLD
imekua mfano bora wa kuigwa
kwa mpango mkakati huo unaoendelea
kutekelezwa
na
kampuni.Ningependa kuwashauri Walimu na wanafunzi, kuyatunza vema madawati mliyogawiwa
kwa manufaa ya wanafunzi waliopo na watakaojiunga na shule
zenu baadaye, aliongeza Njanga.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalabani wakishangilia baada ya kukabidhiwa msaada wa


madawati yaliyotolewa na mgodi wa STAMIGOLD na kukabidhiwa na Afisa Mipango wa
Wilaya ya Biharamulo, Zabron Njanga.

WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

You might also like