Rais Kikwete Ateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Na Makamishna Wanne Wa Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, amefanya uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna
wanne wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ifuatavyo:Mwenyekiti:
Bwana Bahame Tom Mukirya
-NYANDUGA

Ana Shahada ya Sheria, 1977 (Dar es


Salaam), Shahada ya Uzamili ya
Sheria, 1987, (London) na Diploma ya
Uzamili ya Sheria, 1981 (The Hague).
Alifanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa wa Kimataifa kwa
miaka 17. Alikuwa Rais wa Chama cha
Mawakili
wa
Kujitegemea
wa
Tanganyika,
2001-2009.
Alikuwa
Kamishna wa Umoja wa Afrika wa
Kamisheni ya Haki za Binadamu
(2003-2009). Ni Mtaalam Huru wa
Somalia wa Baraza la Umoja wa
Mataifa la Haki za Binadamu, (2014).

Makamu Mwenyekiti:
Bwana Iddi Ramadhani MAPURI

Ana Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar


es Salaam, 1984 na Diploma ya
Uzamili ya Maendeleo Vijijini, 1987 na
Diploma ya Uzamili ya Menejimenti
(India). Alikuwa Kamishna wa Kazi,
1989-2010. Ni Mkurugenzi wa Utawala
na
Maendeleo ya Rasilimali Watu
katika Wizara ya Vijana, Wanawake na
Uwezeshaji tangu 2011.

Makamishna:
1. Bwana Mohamed Khamis HAMAD
-

Ana Shahada ya Sheria, 2004


(Zanzibar), na Shahada ya Uzamili ya
Sheria 2007 (Oslo). Ni Wakili wa
Serikali Mwandamizi katika Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka. Alikuwa
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Rufani za Kodi. Alikuwa pia Mkuu wa
Kitengo
cha
Utafiti,
Tume
ya
Kurekebisha Sheria.

2. Dkt. Kevin MANDOPI

Ana Shahada ya Sheria, 2003 (Dar es


Salaam), Shahada ya Uzamili ya
Sheria, 2007 (Dar es Salaam) na
Shahada ya Uzamivu, 2013 (St.
Augustine University), Mwanza. Ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Msaada
wa Sheria, Chuo cha
Uongozi
wa
Mahakama
(IJA) Lushoto.
Ni
Wakili
wa
Kujitegemea tangu 2005. Ni Mhadhiri
wa Sheria.

3. Bibi Rehema Msabila NTIMIZI

Ana Shahada ya Sheria, 2001 (Dar es


Salaam) na Shahada ya Uzamili ya
Sheria, 2003 (Dar es Salaam). Alikuwa
Wakili Mkuu wa Serikali 2005-2007;
Kaimu Msaidizi Mwandamizi wa Msajili
wa Hati, Wizara ya Ardhi, 1994-2005.
Ni Meneja wa Ulinzi wa Mali Vijijini,
MKURABITA, (tangu 2008).

4. Bibi Salma Ali HASSAN

Ana Shahada ya Sheria, 2001


(Malaysia) na Shahada ya Uzamili ya
Menejimenti, 2009 (Malaysia). Alikuwa
Wakili wa Serikali, 2002-2009, Afisa
wa Haki za Binadamu, Wizara ya
Katiba na Utawala Bora. Ni Wakili wa
Kujitegemea tangu 2011.

Uteuzi huo unaanzia tarehe 06 Januari, 2015, na wataapishwa Ikulu, Dar es


Salaam siku ya Alhamisi, tarehe 8 Januari 2015, saa sita adhuhuri.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
07 Januari, 2015

You might also like