Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

TAARIFA KWA UMMA

KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR


Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo
wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Ijumaa na
Jumamosi ya tarehe 23 na 24 Januari 2015, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu
mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (Crossconnection) ndani ya Mtambo wa Ruvu Chini, Bagamoyo.
Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji;
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi
beach na Kawe.
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo,
Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo
Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na
Keko.
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.

Dar es Salaam Water and Sewerage Corporation

Dawasco House, 2453/188 Sokoine Drive, P.O. Box 5340 Dar es Salaam, Tanzania
Tel +255 22 212 2450 Fax +255 22 211 0931

info@dawasco.com

You might also like