Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 11

1

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA


KURA KATIKA KATA TISA (9) ZA HALMASHAURI YA MJI
WA MAKAMBAKO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada
ya kukamilika kwa maandalizi muhimu ya Uboreshaji wa
Daftari, ikiwemo manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa
fedha kutoka Serikalini.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,
tofauti na Uboreshaji wa Daftari hilo kwa Awamu zote za
Chaguzi zilizopita, linafanyika kwa kutumia teknolojia
mpya ya Biometric Voter Registration (BVR). Zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianza
kufanyika katika Kata tisa (9) za Halmashauri ya Mji wa
Makambako katika Vituo 54 vilivyowekwa katika Mitaa
na Vitongoji, kuanzia tarehe 23/2/2015 katika Kata za
2

Kitisi,

Kivavi,

Lyamkena,

Maguvani,

Majengo,

Makambako, Mji Mwema, Mlowa na Mwembetogwa.


Tume ililenga kuandikisha Wapiga Kura 32,370 kwa
mujibu wa taarifa za Ofisi ya Takwimu za Sensa ya Idadi
ya watu ya mwaka 2012. Tume ililenga kuandikisha kwa
siku jumla ya watu 1,850. Hata hivyo mara baada ya
uandikishaji kuanza idadi ya Wapiga Kura waliokuwa
wanajitokeza iliendelea kuwa kubwa na kuongezeka kila
siku ambapo kulikuwa na misururu mirefu ya watu
waliojitokeza

kujiandisha

katika

Vituo

vyote

vya

Uandikishaji. Tume ilivuka malengo yaliyowekwa ya


Uandikishaji kutokana na kujitokeza kwa wingi kwa
Wapiga Kura waliofika katika Vituo vya Uandikishaji kila
siku kwa Kata zote tisa (9) za Mji wa Makambako ambazo
zilikuwa zinaandikisha Wapiga Kura.

Idadi ya Wapiga Kura waliojitokeza na kuandikishwa kwa


kila siku katika Kata tisa (9) za Mji wa Makambako ilikuwa
kama ifuatavyo:i. Tarehe 23/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
3,014;
ii. Tarehe 24/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
4,727;
iii. Tarehe 25/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
5,301;
iv. Tarehe 26/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
6,354;
v. Tarehe 27/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
6,731;
vi. Tarehe 28/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura
6,545;
4

vii. Tarehe 1/3/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura


6,906;
viii. Tarehe 2/3/2015 kutokana na Watu waliokuwa
wanajitokeza kujiandikisha kuendelea kupungua,
Tume iliandikisha Wapiga Kura 4,662; na
ix. Tarehe 3/3/2015 ambayo ndio ilikuwa siku ya
mwisho ya uandikishaji, Tume iliandikisha Wapiga
Kura 2,469.
Hivyo, jumla ya Wapiga Kura wote walioandikishwa
katika Kata tisa (9) za Mji wa Makambako ni 46,709.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari katika Kata tisa (9) za
Halmashauri ya Mji wa Makambako limefanyika kwa
ufanisi na mafanikio makubwa ambapo Tume
imevuka lengo lililowekwa la Uandikishaji kwa
kuandikisha jumla ya Wapiga Kura 46,709 na kuvuka
lengo lililowekwa la

kuandikisha Wapiga Kura


5

32,370 waliolengwa kuandikishwa kwa mujibu wa


taarifa za Ofisi ya Takwimu za Sensa ya idadi ya Watu
ya mwaka 2012.
Mashine nyingi za BVR zimeonyesha ufanisi mkubwa
kwa kuwa zimekuwa zikiandikisha idadi ya Wapiga
Kura kuanzia 80 kwa siku hadi watu 160. Pamoja na
mafanikio hayo, kumekuwa na changamoto chache
zilizojitokeza ikiwemo ya watu wengi zaidi kujitokeza
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura na kusababisha kuwepo kwa misururu mirefu
ya watu waliojitokeza katika Vituo kujiandikisha
katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Changamoto hiyo ilishughulikiwa na Tume kwa
kuongeza muda wa ziada wa siku mbili za
kuandikisha Wapiga Kura baada ya muda wa siku
saba za uandikishaji kumalizika. Lengo la kuongeza
siku mbili zaidi za uandikishaji lilikuwa ni kutoa fursa
6

kwa Wapiga Kura wote ambao walikuwa bado


hawajajiandikisha

kujiandikisha.

Vilevile,

katika

kushughulikia changamoto hizo, Tume iliongeza idadi


ya BVR Kits katika baadhi ya Vituo vilivyokuwa na
idadi kubwa na misururu mirefu ya Wapiga Kura
waliojitokeza kujiandikisha. Wapiga Kura wote
waliojitokeza kujiandikisha waliandikishwa pasipo
kuachwa. Kwa ujumla changamoto zote zilizojitokeza
zilishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi.
Tume inaendelea na Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata nyingine za
Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo Ratiba
ya zoezi la Uboreshaji litafanyika kama ifuatavyo:i. Katika Kata ya Kitandililo Uboreshaji umeanza
kufanyika

kuanzia

tarehe

utamalizika tarehe 9/3/2015.


7

3/3/2015

na

ii. Kata

ya

Mahongole,

Uboreshaji

utaanza

kufanyika tarehe 11/3/2015 na kumalizika


tarehe 17/3/2015.
iii. Kata ya Utengule, Uboreshaji utaanza kufanyika
tarehe

11/3/2015

na

kumalizika

tarehe

17/3/2015.
Tume itaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Njombe katika
Wilaya

za

Njombe,

Makete,

Ludewa

na

Wangingombe kuanzia tarehe 16/3/2015 hadi


12/04/2015.
Tangu zoezi hili lianze katika Halmashauri ya Mji wa
Makambako na kumalizika, Wananchi wameonyesha
mwamko mkubwa sana wa kujiandikisha. Ni
matumaini ya Tume kuwa Viongozi wote, Vyama vya
Siasa, Asasi za Kiraia na Vyombo vya Habari
8

vitahamasisha Wananchi wote wenye sifa za


kujiandikisha katika Wilaya za Njombe, Makete,
Ludewa na Wangingombe kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
Baada ya kukamilisha Ratiba ya Uboreshaji katika
Mkoa wa Njombe, Tume itatoa Ratiba ya Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mikoa
mingine.

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya


Uchaguzi.

10

11

You might also like