Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


RATIBA YA UBORESHAJI WA
DAFTARI LA KUDUMU NJOMBE
HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MKOANI NJOMBE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kuwa itaanza
zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric
Voters Registration kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote: Waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote watakaotimiza miaka 18
ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha
taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye
Daftari.
Zoezi litaanza kufanyika Wilayani Njombe katika Halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako kujitokeza
kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka tarehe 01/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Kumbuka:Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa
hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MKOANI NJOMBE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe,Halmashauri ya Mji
mdogo wa Makambako kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa
kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015
katika kata ya Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa, na
Mwembetogwa. Kata ya Kitandililo utafanyika tarehe 03 -09/03/2015. Kata ya Mahongole tarehe
11-17/03/2015 na Kata ya Utengule uboreshaji utafanyika tarehe 19 25/03/2015.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-

Waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote watakaotimiza miaka 18 ifikapo


mwezi Oktoba, 2015.

Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa
zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.

Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari
Zoezi litaanza kufanyika Mkoani Njombe katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na Mji wa Njombe.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako kujitokeza kwa
wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka tarehe 25/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka huu 2015.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kumbuka:Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa
hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Ruth Masham
Kny: Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

You might also like