Professional Documents
Culture Documents
Kivamwok
Kivamwok
Ndugu Marafiki,
Baadhi yenu mnafahamu kwamba ndugu
na rafiki yetu, Adolf Simon Kivamwo,
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT), ni
mgonjwa na anasumbuliwa saratani ya
utumbo mpana toka mwaka 2012.
Tangu wakati huo, amekuwa akitibiwa na
kuhudhuria matibabu na kliniki katika
Taasisi ya Saratani Ocean Road (OCRI).
Wataalamu wa tiba ya saratani wanamtibia kwa dawa mchanganyiko dawa tofauti
kwa mtindo wa chemotherapy. Tiba hizo
zinalenga kudhibiti kasi ya kuenea kwa
ugonjwa kwa kushauriana na mgonjwa.
OCRI ni taasisi inayoendeshwa na serikali
inatoa tiba ya saratani bila malipo kwa
wagonjwa. Hata hivyo, kutokana na
uhaba wa rasilimali, taasisi hiyo inapokea
kiasi kidogo au kutopokea dawa muhimu
kutoka Bohari ya Dawa ya Serikali
(Medical Stores Department - MSD). Hali
hiyo ni jambo la kawaida kwenye hospitali
za serikali. Kutokana na hali hiyo,
wagonjwa wanalazimika kununua dawa
kwenye maduka binafsi na kuzipeleka
OCRI kwa ajili ya tiba.
Hiyo ndiyo sababu Simon amekuwa
akitumia wastani wa Tshs 500,000/ -