Tangazo La Kazi La Bodi Ya Mishahara Na Masilahi Katika Utumishi Wa Umma.

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

TANGAZO LA KAZI YA MUDA


WAKUSANYA TAARIFA ZA TATHMINI YA KAZI (NAFASI 50)
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ambayo
imeanzishwa kwa Hati Maalum iliyotolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 162
la tarehe 3 Juni, 2011. Majukumu ya Bodi ni kufanya mapitio ya mara kwa
mara ya viwango vya mishahara, posho na mafao mengine na kumshauri
Rais juu ya misingi ya miundo ya mishahara katika utumishi wa umma.
Katika mwaka wa fedha 2015/16, Bodi inatarajia kufanya Tathmini ya Kazi
katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kuoanisha na kuwianisha
mishahara. Bodi inahitaji watumishi 50 watakaomsaidia Mtaalam
Mwelekezi kukusanya taarifa za awali:
a) Sifa za mwombaji
i) Mtumishi wa Umma;
ii) Elimu ni kuanzia shahada ya kwanza au stashahada ya juu na
kuendelea;
iii) Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha kwa Kiswahili na Kiingereza;
iv) Mwenye maadili, uwezo wa kufanya kazi inayozingatia matokeo,
kujituma na kukamilisha malengo kwa wakati; na
v) Uelewa wa kutumia kompyuta.
b) Kazi za kufanya
i) Kuwahoji watumishi wa Umma na kujaza dodoso la kukusanyia
taarifa;

ii) Kuingiza taarifa za madodoso kwenye mfumo wa kompyuta; na


iii) Kazi nyingine zinazohusiana na Tathmini ya Kazi kwa maelekezo
ya msimamizi.
c) Mshahara
Waombaji watakaofanikiwa, kwa kuwa ni watumishi wa umma,
wataendelea kulipwa mishahara yao kama ilivyo sasa. Aidha, Bodi
itagharamia mafunzo na posho za safari za kikazi kwa viwango vya
Serikali.
d) Muda wa Kazi
Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa jumla ya miezi 15. Hata hivyo, kazi
ya mtumishi mmoja mmoja haitazidi siku 100.
e) Namna ya kuwasilisha maombi.
i) Maombi yote yaambatanishwe na Maelezo binafsi (CV), nakala za
vyeti vya elimu ya juu na mafunzo ya kompyuta;
ii) Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kwa kupitia
anwani ya: es@psrb.go.tz; na
iii) Maombi yote yapitishwe na waajiri wenyewe.

f) Mwisho wa kupokea maombi


Zoezi la kupokea maombi litafungwa tarehe 31/07/2015.
Tanbihi: Watumishi wanaofanyakazi katika Mamlaka za Serikali
za Mtaa wanahimizwa kuleta maombi yao.

IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI


BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA
UMMA

You might also like