Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 9

HABARI

HABARIZA
ZA
NISHATI
NISHATI&MADINI
&MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.76
51
Toleo No.

LimesambazwaLimesambazwa
kwa Taasisi nakwa
Idara
zotenaMEM
Taasisi
Idara zote MEM Tarehe
- 23-29 Januari , 2015
Julai 17 - 23, 2015

Mradi gesi asilia


wafikia asilimia 98

Wabunge

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Soma
habari

Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA


Kituo cha kupokelea gesi eneo la Somanga kikiwa kimekamilika

Somahabari Uk.2

Mitambo ya kusafisha gesi


na nyumba za wafanyakazi
Madimba, Mtwara

Mitambo ya kupokelea gesi ya Kinyerezi iliyokamilika kufungwa

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya
News
Bullettin
hiiGhorofa
na Jarida
la(MEM)
Wizar
a yapepe:
Nishati
na Madini
au Fika
Ofisi
ya Mawasiliano
ya Tano
Barua
badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

Uk. 2

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98

Mitambo ya kusafisha gesi ya Madimba

Asteria Muhozya na
Teresia Mhagama

meelezwa kuwa, utekelezaji wa


miradi ya ujenzi wa mitambo ya
kusafisha gesi asilia ya Madimba
na Songongo, Kilwa, pamoja na
bomba la kusafirisha gesi hiyo
kutoka Mtwara na Songosongo hadi
Dar es Salaam kupitia Somanga Fungu
itakamilika hivi karibuni.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya
mwezi Juni mwaka huu, iliyotolewa na
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya
Kusambaza Gesi (GASCO) ambayo ni
Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi
Kapuulya Musomba
Akielezea hatua zilizofikiwa katika
miradi hiyo, Musomba alieleza kuwa,
kwa ujumla mradi huo umefikia asilimia

Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC


kuhakikisha kuwa, Tanzania inazalisha umeme wa
kutosha kupitia rasilimali hiyo na wananchi wake
wananufaika na rasilimali ya gesi asilia
98 za ujenzi na kukamilika kwake
kutaunganisha maeneo yanayozalisha
gesi asilia hususan Mnazi Bay- Mtwara,
Songosongo, Kiliwani, Mkuranga, Ntorya
na gesi iliyogunduliwa katika eneo la bahari
ya kina kirefu.
Akifafanua zaidi alisema kuwa, Bomba
limekamilika kwa asilimia 99.6 kwa
ujumla, mitambo ya kusafisha gesi asilimia
97.5. Manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa
mradi yamekamilika kwa asilimia 100, na
mradi mzima umekamilika kwa asilimia
98.
Musomba alisema kuwa, hatua

hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC


kuhakikisha kuwa, Tanzania inazalisha
umeme wa kutosha kupitia rasilimali
hiyo na wananchi wake wananufaika na
rasilimali ya gesi asilia.
Serikali imedhamiria kuhakikisha
kuwa, gesi inatumika katika kuzalisha
umeme ambao kwa sasa unazalishwa
kwa kutumia nishati ya mafuta ambayo
huagizwa kutoka nchi za nje na hivyo
kuligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha
za kigeni, alieleza Musomba.
Kuhusu mitambo ya kuchakata gesi
asilia, alisema kuwa, ujenzi wa eneo la

kusimika mitambo, jengo la kuendesha


mitambo pamoja na barabara za ndani
katika eneo la Madimba Mtwara
umekamilika kwa asilimia 98, wakati ule
wa Songosongo umekamilika kwa asilimia
100 na usimikaji mitambo umekamilika
kwa asilimia 98.
Akizungumzia suala la ajira katika
mradi huo, alisema kuwa, kumekuwepo
na wafanyakazi wapatao 1,427 wenye
mchanganyiko wa wageni pamoja na
watanzania kwa ngazi zote hadi taarifa hii
inatolewa.
Aidha, kuhusu ajira kwa upande wa
TPDC, alieleza kuwa, shirika hilo tayari
limeajiri wafanyakazi wapya wapatao 92
kwa upande wa mitambo ya kusafisha gesi
na 42 kwa upande wa bomba la kusafirisha
gesi, ambao tayari wanashiriki katika
usimamizi wa shughuli za ujenzi.
Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa,
mradi unatekelezwa kwa kutumia fedha
za mkopo wa masharti nafuu kutoka
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China.
Jumla ya gharama za ujenzi wa mradi
huo ni Dola za Marekani zipatazo bilioni
1.255, ambapo asilimia 95 ni mkopo na
asilimia 5 ni mchango wa Serikali.
Vilevile taarifa inaeleza kuwa
gharama nyingine nyingi ambazo serikali
imeendelea kuzibeba nje ya asilimia 5
zinazotajwa ni pamoja na gharama za
upatikanaji wa mkuza wa Bomba la gesi
kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu na
kuongezeka kwa upana maeneo mengine
mengi ya mkuza tokea Somanga Fungu
kuja Dar es Salaam hadi Tegeta. Hadi sasa
zimefikia kiasi cha pesa za ki-Tanzania
zipatazo shilingi Bilioni 200.
Katika hatua nyingine, akizungumza
wakati akifunga rasmi Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania mwishoni
mwa wiki, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete alieleza kuwa, serikali imejipanga
kuhakikisha kuwa, hadi ifikapo mwaka
2020 uzalishaji umeme unafikia kiasi cha
megawati 3000 kutokana na matumizi ya
gesi asilia.
Akieleza kuhusu miswada ya Sheria za
Petroli na TEITI iliyosomwa Bungeni hivi
karibuni na Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene, Rais Kikwete
alisema yuko tayari kuisaini miswada hiyo
wakati wowote itakapomfikia.

Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

akandarasi
wa miradi ya
kuboresha
miundombinu
ya
umeme
kwenye vituo vya kupoozea
umeme jijini Dar es Salaam
wametakiwa
kuhakikisha
wanakamilisha miradi hiyo
ndani ya muda uliopangwa.
Wito
huo
umetolewa
hivi karibuni na Kamishna
Msaidizi wa Umeme, Mhandisi
Innocent Luoga wakati wa
ziara yake ya ukaguzi wa

Mradi wa Kusambaza Umeme


ujulikanao kwa jina la Electricity
V unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB)
ambao unahusisha ujenzi na
ukarabati wa vituo vya kupoozea
umeme vya Sokoine, Ilala na
Njiro.
Aidha, ziara hiyo pia
ilihusisha ukaguzi wa Mradi wa
Ujenzi na Ukarabati wa Vituo
vya Ilala na New City Centre
pamoja na ujenzi wa vituo
vipya vya Ilala na Muhimbili
ambao unafadhiliwa na Serikali

Mradi wa
Electricity
V- Ilala:
Transfoma
mpya
iliyofungwa
kwenye kituo
cha kupooza
umeme cha
Ilala mara
baada ya
majaribio ya
awali.

ya Japan kupitia Shirika la


Maendeleo la Japan (JICA)
na vilevile Mradi wa Mfumo
wa Kusimamia na Kudhibiti
Usambazaji wa Umeme Dar
es Salaam ujulikanao kama
Distribution SCADA System
uliopo Mikocheni unaofadhiliwa
na Serikali ya Finland.
Mhandisi Luoga alielezea
lengo la ziara hiyo kuwa ni
kujionea hatua iliyofikiwa katika
utekelezaji wa miradi hiyo
>>Inaendelea Uk. 3

NewsBulletin

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

Luoga aagiza miradi ya Umeme


Dar ikamilike kwa wakati

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Hongera Simbachawene
kwa mkakati wa kuisuka
Upya TIPER
Mapema wiki hii Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene alikutana na
Uongozi wa Shirika la kuhifadhi mafuta ya
TIPER ambayo serikali ni mbia kwa asilimia 50.
Katika kikao hicho alisisitiza kuhusu dhamira
ya Serikali kuboresha na kulisuka upya shirika
hilo la kuhifadhi mafuta ili liweze kutoa huduma
ya kupokea mafuta kwa kampuni zote kwa haki
na usawa.
Simbachawene alisema lengo la kulisuka
upya Shirika hilo ni kuliboresha na kuhakikisha
kuwa linatoa huduma ya kuhifadhi na kupitisha
mafuta yote yanayoletwa nchini, na kuhakikisha
gharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini
zinakuwa nafuu.
Kwa mara nyingine tunapenda kupongeza
jitihada zinazofanywa na Serikali katika
kuhakikisha kwamba Sekta ya mafuta nchini
inalinufaisha taifa ikiwemo kuleta unafuu wa
nishati hiyo.
Hakika katika hili la kuisuka upya TIPER ni
mikakati madhubuti ambayo inatarajia kuleta
mabadiliko makubwa katika Shirika hivyo,
wadau wa TIPER na Watanzania tuunge
mkono juhudi hizi za Serikali kwani kauli hii ya
sasa inadhihirisha dhamira ya dhati ya Waziri
Simbachawene juu ya kulisuka upya Shirika hilo
ambapo alisisitiza umuhimu TIPER katika sekta
ya mafuta nchini, na kuleza kwamba hivi sasa
shirika hilo linahitajika kuliko wakati mwingine
wowote.

Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga


(wa pili kushoto) akimsikiliza Meneja Mradi wa Electricity
V, Mhandisi Florence Gwangombe (wa pili kulia) wakati wa
ziara yake kwenye kituo cha kupoozea umeme cha Ilala.

>>Inatoka Uk. 2
ikiwa ni pamoja na kubaini
changamoto
zinazokabili
utekelezaji wa miradi husika.
Katika
taarifa
yake
ya utekelezaji wa Mradi
wa Electricity V, Meneja
wa Mradi huo, Mhandisi
Florence
Gwangombe
alisema kutokana na sababu
mbalimbali huenda mradi
huo ukachelewa kukamilika
tofauti na makubaliano ya awali
kitendo ambacho kilimkera
Mhandisi Luoga na hivyo
kumuagiza Meneja huyo kukaa
na wakandarasi wa Mradi na
kurejea makubaliano ya awali.
Mhandisi Florence alisema
moja ya sababu inayopelekea

Mradi huo kuwa na kasi ndogo


ni wakandarasi kushindwa
kuajiri wafanyakazi wa kutosha.
Mhandisi Luoga aliwaagiza
wakandarasi hao ambao ni
kampuniyaNationalContracting
Company Ltd (NCC) ya India
na ELTEL Group kutoka
Finland kuhakikisha wanaajiri
wafanyakazi wa kutosha na
pia kuandaa ratiba ya shughuli
zinazotakiwa kufanywa ili
kuepuka kuchelewa kukamilika
kwa miradi husika.
Aidha, Mhandisi Luoga
aliwaagiza Mameneja Miradi
wa Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO)
kuhakikisha
kunakuwepo na usimamizi
madhubuti wa miradi iliyo
chini yao ili kuleta matokeo

KWA HABARI PIGA SIMU


KITENGO CHA MAWASILIANO

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James
na Nuru Mwasampeta

yanayotarajiwa.
Alisema lengo la Serikali ni
kuhakikisha taifa linakuwa na
umeme wa uhakika kwa ajili ya
kukuza uchumi hivyo aliwaasa
mameneja hao kuhakikisha
azma hiyo inatimia.
Ninawasisitiza muhakikishe
kunakuwepo na ufatiliaji makini
wa miradi mnayoisimamia na sio
kuwaachia wakandarasi wafanye
kila kitu bila usimamizi wenu,
aliagiza Mhandisi Luoga.
KwaupandewakeMenejawa
kampuni ya NCC Ltd, Sadeesh
John alimuahidi Mhandisi
Luoga kuwa atahakikisha kasi
ya utekelezaji inaongezeka na
kutimiza maagizo husika ili
kuhakikisha mradi unakamilika
ndani ya muda uliopangwa.

FIVE
PILLARS OF
REFORMS
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

JK ajivunia mchango Sekta ya Madini

>>
Aitaja ya pili kuingiza fedha za Kigeni baada ya
Maliasili
>>
Ajira zaongezeka kutoka 3,500 hadi 15,000.
Na Asteria Muhozya,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete

ais wa Jamhuri ya Muungano


wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete amesifu
jitihada zilizofanywa na Serikali
ya Awamu ya Nne katika
kuimarisha Sekta ya Madini nchini na
kuitaja kuwa ni ya pili kwa kuingiza fedha za
kigeni baada ya Sekta ya Maliasili.
Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni
mwa wiki wakati akihutubia wananchi
kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, mjini Dodoma na kuyataja
mafanikio kadhaa katika Sekta hiyo,
ikiwemo ya migodi ya madini kuanza kulipa
ushuru wa huduma.
Hotuba ya Rais Kikwete inarejea
taarifa ya awali iliyotolewa na Wizara ya
Nishati na Madini ikieleza kuwa, mgodi
wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na
kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi
ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara
inayomilikiwa na kampuni ya Acacia
Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma
kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya
mapato ghafi kwa Halmashauri husika.
Tayari migodi inalipa kodi ambazo
zinachangia katika pato la Taifa. Pia tuna
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 haya yote
yamesaidi kuweza kunufaika zaidi kupitia
rasilimali hii, alisisitiza Rais.
Aidha, Rais Kikwete alieleza mafanikio

yaliyopatikana baada ya serikali kulifufua


upya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
ambapo alisema kuwa, mafanikio hayo
yamechangia shirika hilo kumiliki mgodi
wake wa dhahabu wa STAMIGOLD
uliopo Biharamulo, ambao tayari umeanza
kutoa mikuo ya dhahabu.
Vilevile, katika hotuba yake, Rais
Kikwete alieleza namna Serikali ilivyofanya
jitihada za kuwawezesha wachimbaji
wadogo kupewa ruzuku, lengo likiwa ni
kuwawezesha kutoka katika uchimbaji
mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati.
Katika taarifa yake wakati akizindua
Kamati inayoshughulikia maombi ya ruzuku
Awamu ya Pili hivi karibuni, Kamishna wa
Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja
alisema kuwa, kiwango cha fedha katika
awamu hii kimeongezwa kufikia Dola za
Kimarekani milioni na tatu na shilingi
za Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za
Marekani Laki tano (500,000) zilizotolewa
Awamu ya Kwanza.
Lakini pia tumetenga maeneo 8 kwa
ajili ya wachimbaji wadogo. Tumefanya
hivi ili wasisumbuliwe na wachimbaji
wakubwa, alisema Kikwete.
Vilevile, Rais Kikwete alisema kuwa,
mikataba imerekebishwa ili kulinda na
kulinufaisha taifa ambapo pia baadhi
ya mafanikio ya marekebisho hayo
yamewezesha Kampuni za madini
kuongeza huduma ya bidhaa zinatolewa
nchini tofauti na ilivyokuwa awali.
Katika hotuba yake pia aliitaja migodi
mipya 3 ikiwemo ya Makaa ya Mawe ya
Ngaka na Liganga na Chuma Mkuju,
ambayo ilianzishwa katika kipindi cha
miaka 10 na kueleza kuwa, sekta hiyo
imeongeza kiwango cha ajira kutoka 3,500
hadi kufikia 15,000.

Ujumbe kutoka Malawi watembelea Tanzania


kujifunza sheria ya Madini, CADASTRE.
Na Rhoda James

Ujumbe kutoka Serikali ya Malawi


umetembelea Wizara ya Nishati na Madini
mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo la
kujifunza masuala mbali mbali ikiwemo
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na
Mfumo mpya wa kusajili leseni za madini
kwa njia ya mtandao (Online mining
Cadastre Transactional Portal)
Ziara hiyo ya Malawi imekuja kufuatia
nchi hiyo kuwa katika mchakato wa
kutunga Sheria mpya ya Madini. Ujumbe
huo pia umetembelea Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Tanzania (TMAA),Ofisi ya
Madini Kanda ya Mashariki, Kampuni ya
Madini ya Acacia, pamoja na kitengo cha
Leseni na TEHAMA katika Wizara ya
Nishati na Madini.
Ujumbe huo kutoka Malawi
umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa
kazi nzuri wanayoifanya katika kuendeleza
sekta ya Madini na kuahidi kuendeleza
ushirikiano uliopo kati ya Serikali hizo
mbili.

Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika Wizara


ya Nishati na Madini wakati ulipofika Wizarani
hapo kujifunza masuala ya Madini. Katikati
ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
Wizara ya Nishati, Mrimia Mchomvu na kushoto
kwake ni Kamishna Msaidizi wa Madini kitengo
cha Leseni, John Nayopa.

Kulia ni kiongozi wa Msafara wa Ujumbe


kutoka Malawi Katibu Mwandamizi, Ben Botolo
akielezea jambo katika kikao hicho.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI/MADINI

Serikali kuisuka upya TIPER


Na Mwandishi Wetu

erikali imedhamiria kuboresha na


kulisuka upya shirika la kuhifadhi
mafuta TIPER ili iweze kutoa
huduma ya kupokea mafuta kwa
kampuni zote kwa haki na usawa.
Waziri mwenye dhama na Wizara ya
Nishati na Madini George Simbachawene
amebainisha hayo wiki hii alipozungumza
na Uongozi wa shirika hilo huku akisisitiza
kwamba lengo la Serikali kuboresha
shirika hilo ni kuhakikisha inatoa huduma
ya kuhifadhi na kupitisha mafuta yote
yanayoletwa nchini.
Simbachewene aliongeza kusema
kwamba hadi ifikapo mwishoni mwa
mwaka huu kampuni hiyo itakuwa na
uwezo wa kuhifadhi mafuta kiasi cha lita
300,000.
Kwa dhati kabisa tumeamua
kuiboresha kampuni hiyo na tunapanga
ifikapo Septemba mwaka huu uwezo wa
TIPER wa kuhifadhi mafuta utaongezeka
kutoka lita 147,000 hadi kufikia 210,000 na
itakapofika Desemba watakuwa na uwezo
wa kuhifadhi mafuta lita 300,000, alisisitiza
George Simbachawene.
Waziri Simbachawene aliongeza
kwamba lengo la Serikali kuchukua hatua
ya kuiboresha TIPER ni kuhakikisha
gharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini
zinakuwa nafuu.

Mwenyekiti wa Bodi ya
TIPER Prof. Abdulkarim
Mruma akieleza jambo
katika moja ya vikao na
Waziri

Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la TIPER, Daniel
Belair ( Wa kwanza kulia)
akimwongoza Waziri
wa Nishati na Madini,
George Simbachawene
(kushoto) na ujumbe
wake walipotembelea
shirika lake hivi karibuni.

Wanafunzi waliopata ufadhili wa China waaswa


Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

kurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu, Wizara ya
Nishati na Madini, Mrimia
Mchomvu
amewataka
wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi
na mafuta nchini China kutumia utaalam
na uzoefu wao katika kuleta mabadiliko
kwenye sekta ya gesi na mafuta nchini.
Mchomvu aliyasema hayo ofisini
kwake, alipotembelewa na wanafunzi
waliofadhiliwa na Wizara ya Nishati na
Madini kwa ajili ya mafunzo ya Shahada ya
Uzamili katika masuala ya gesi na mafuta
katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi Wuhan
kilichopo nchini China.
Wanafunzi hao ambao ni miongoni
mwa wanafunzi nane waliofadhiliwa na
Wizara kusomea masuala ya gesi na mafuta
kwa mwaka 2013, walifanya ziara hiyo kwa
lengo la kuishukuru Wizara pamoja na
kuelezea mikakati yao katika kutumia elimu
na uzoefu walioupata kuinua sekta za gesi
na mafuta.
Alisema lengo la Serikali kupitia Wizara
ya Nishati na Madini la kupeleka wanafunzi
hao lilikuwa ni kuzalisha wataalam kwa ajili
ya kufanya kazi katika Wizara, makampuni
ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi

nchini.
Kutokana na kukua kwa shughuli za
utafutaji wa gesi na mafuta nchini kama
Serikali tulipanga mikakati mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazawa
kushiriki katika
shughuli hizo kwa
kuwapeleka kusomea masuala ya gesi na
mafuta ili waweze kufanya kazi na mashirika
ya umma na makampuni yaliyowekeza
katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa
gesi na mafuta nchini, alisema Mchomvu.
Mchomvu aliendelea kusema kuwa
wataalam hao wanaweza kutumia elimu na
uzoefu walioupata kutoka China kufanya
kazi kwenye mashirika ya umma, taasisi na
makampuni binafsi yanayojishughulisha na
shughuli za uchimbaji na utafutaji wa gesi na
mafuta.
Alisisitiza kuwa serikali pekee, haiwezi
kuajiri wahitimu wote wanaomaliza
mafunzo ya gesi na mafuta bali kazi yake
kuu ni kuwapatia elimu itakayowawezesha
kushiriki
katika
fursa
mbalimbali
zinazojitokeza katika setka ya gesi na
mafuta.
Sekta ya gesi na mafuta inakua kwa kasi
kwa sasa, fursa ni nyingi hivyo ni jukumu
lenu kuchangamkia fursa mbalimbali za
ajira zinazojitokeza katika makampuni ya
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.
Kuna Shirika la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC) ambalo lina kampuni

tanzu, makampuni ya utafutaji wa gesi na


mafuta ya Statoil na BG ambayo yanahitaji
wataalam, alisisitiza Mchomvu.
Wakielezea uzoefu walioupata katika
chuo hicho, wanafunzi hao walisema
wamejifunza kwa kina hatua za utafutaji,
uchimbaji na usafirishaji wa mafuta na gesi
kwa kutumia vifaa vya kisasa hali iliyowapa
uwezo wa kufanya kazi na kampuni za
kimataifa.
Bishanga Januarius ambaye ni
mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo
hicho alisema kuwa utaalam na uzoefu
alioupata katika chuo hicho utamwezesha
kufanya kazi katika kampuni yoyote ya
utafiti na uchimbaji wa madini na kuwa na
mchango mkubwa kwa taifa.
Alisema kuwa elimu ya
vitendo
waliyoipata katika makampuni ya mafuta
na gesi nchini China imewapa mwanga
mkubwa katika shughuli zote za utafiti na
uchimbaji wa mafuta na gesi.
Aliishauri Serikali kuendelea kutoa
ufadhili katika fani za mafuta na gesi pamoja
na masuala ya mazingira kwani shughuli
za utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta
ni lazima ziende sambamba na utunzaji wa
mazingira.
Naye Yazid Idd ambaye ni mhitimu
katika chuo hicho aliishukuru Wizara kwa
ufadhili huo na kuishauri Wizara kupeleka
wanafunzi kwenye vyuo vingine vinavyotoa

mafunzo ya mafuta na gesi katika nchi


nyingine zilizopiga hatua katika sekta hizo.

Mkurugenzi wa Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu,
Wizara ya Nishati na Madini
Mrimia Mchomvu, ( wa pili
kutoka kushoto) Mkurugenzi
Msaidizi Utumishi, Wizara
ya Nishati na Madini Lucius
Mwenda ( wa pili kutoka kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wanafunzi
waliowahi kufadhiliwa na
Wizara kwa ajili ya kusomea
Shahada ya Uzamili katika
musuala ya gesi katika vyuo
vya China.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Stamigold yatimiza mwaka


mmoja wa uchimbaji dhahabu.

Mratibu wa kitengo cha Tehama na Mawasiliano, Belatrix Kasuga akipokea cheti cha
mfanyakazi bora kutoka kwa Meneja mkuu wa mgodi Mhandisi Dennis Sebugwao (kulia)
wakati wa maadhimisho ya mgodi kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji. Pembeni ni
Meneja Uchimbaji, Mhandisi Abdallah Kwassa aliyeshikilia zawadi tayari kwa kumkabidhi.

Na Jacqueline Mattowo
STAMIGOLD

ampuni ya STAMIGOLD
ambayo ni kampuni tanzu
ya Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO)
imetimiza
mwaka
mmoja
wa
uchimbaji dhahabu katika mgodi wake wa
Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo
Mkoa wa Kagera ambapo kiasi cha wakia
16,388 za dhahabu zimekwisha zalishwa
tangu uchimbaji dhahabu ulipoanza rasmi
mnamo mwezi Julai mwaka 2014 na
jumla ya wakia 12,923 za dhahabu zenye
thamani ya Dola za Kimarekani Milioni
15.6 zimeuzwa kwenye soko la kimataifa.
Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana
katika maeneo ya West Zone na Mojamoja
takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio
wa mgodi ambapo uchimbaji wa dhahabu
bado unaendelea. Maeneo hayo mapya
yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi
wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa na
kampuni ya African Barrick Gold sasa
ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.
Akizungumza katika hafla ya
kusherehekea mwaka mmoja tangu
kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa
dhahabu iliyofanyika mwishoni mwa
juma katika mgodi wa Biharamulo,
Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo,
Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa
matarajio ya mgodi ni kutafuta namna

Pichani Keki ya mfano


wa mawe ya dhahabu
iliyoandaliwa katika hafla
ya mgodi wa STAMIGOLD
Biharamulo kutimiza mwaka
mmoja wa uzalishaji.
ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabu
unaendelea kwa kiwango kikubwa na
gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi
wa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa
Watanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifa
zima.
Siwezi kuficha furaha yangu, siku
ya leo ni siku ya muhimu kwetu sote
katika historia ya Mgodi huu kwani
tunathibitisha kwa Serikali na Watanzania

wenzetu kuwa, Watanzania wasomi


na wenye taaluma mbalimbali katika
sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa
dhahabu wameendelea kuonyesha
uwezo wao kwa kuhakikisha uzalishaji
unaendelea kufanyika katika mgodi wa
STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo
wataalam wa kigeni kama ilivyokuwa
ikiaminiwa. alieleza Sebugwao.
Mhandisi Sebugwao pia alielezea
mafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndani
ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja
na mgodi kuendeshwa kwa kufuata
taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi
imara ndani na nje ya mgodi, kupunguza
gharama za uendeshaji wa mgodi,
kulipa ushuru wa huduma wa 0.3% ya
mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya
Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9
mpaka June 2015, kuajiri wafanyakazi
wa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali za
kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa
wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi na
wakandarasi wa Kitanzania 281.
Aliongeza kuwa mgodi umekuwa
ukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodi
kupunguza changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwa ni pamoja na
kugawa madawati 1500 kwa shule zenye
upungufu katika Wilaya za Biharamulo,
Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha
wanafunzi Shule ya Msingi Mavota,
ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa
manne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati

wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha


wananchi kiuchumi kupitia vikundi vitatu
vya ujasiriamali kwa kununua vyakula
vya asili, mbogamboga na matunda
wanayozalisha.
Kwa upande mwingine, katika
kusherehekea siku hiyo shamrashamra
mbalimbali zilifanyika ikiwemo mpira wa
miguu na mpira wa kikapu ambapo timu
ya mgodi ya mpira wa miguu ilicheza
mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na
wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na
Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka
kidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezo
kumalizika timu zote za mpira wa miguu
zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa
mgodi.
Katika kuhitimisha sherehe hizo
zilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi
10 ambao walifanya vizuri katika Idara
zao kwa kipindi cha mwaka mmoja wa
uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima
ya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi
kukata keki ya kutimiza mwaka mmoja
wa uzalishaji.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala kutoka
STAMICO
Deusdedith
Magala,
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani,
aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa
mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea
kufanyika na kusema kuwa mafanikio
yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na
Taifa kwa ujumla kwani tayari mgodi
umethibitisha uwezo wa Watanzania
kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na
wataalam wa kigeni.
Nimefurahishwa sana na mafanikio
mliyofikia pamoja na namna wafanyakazi
wanavyojituma baada ya kutembelea
maeneo mbalimbali hapa mgodini na
kujionea kazi zinavyofanyika naomba
muendeleenabidiihiyonavilevilemjitahidi
kuongeza zaidi njia za mawasiliano za
kutangaza mafanikio ya mgodi huu mfano
misaada inayotolewa katika jamii ili dunia
na taifa kwa ujumla kufahamu kuwa
ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba
dhahabu kwa manufaa ya Taifa zima la
Tanzania alifafanua Magala.
Mbali na mafanikio hayo mgodi
wa STAMIGOLD Biharamulo bado
unakabiliwa na changamoto mbalimbali
ambazo ni pamoja na kuyumba kwa bei ya
dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa
mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali
za mgodi pamoja na uhaba wa maji
kutokana na vyanzo vilivyopo kutegemea
msimu wa mvua.
Kampuni
ya
STAMIGOLD
Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya
kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na
mpaka sasa imeendelea kuweka historia
kwa kuwa kampuni pekee hapa nchini
inayozalisha dhahabu kwa kusimamiwa
na kuendeshwa na wataalam wa
Kitanzania pekee.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI/MADINI

GST yaeleza mafanikio katika Serikali ya Awamu ya Nne

Watalaam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakifanya utafiti wa Jiolojia katika ukanda wa
Dhahabu wa Lupa(Lupa Gold Field), wilayani Chunya mkoani Mbeya

Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiria


mbalimbali vya uwepo wa madini, kwa mfano eneo
la Misaki, Mpambaa, Sambaru na Londoni ambapo
ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu umeongezeka

Na Veronica Simba

akala wa Jiolojia
Tanzania
(GST)
imetoa taarifa yake ya
utendaji kwa kipindi
cha Serikali ya Awamu
ya Nne (2005-2015), ambayo pamoja na
mambo mengine imeainisha mafanikio
yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali.
Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni,
imeainisha mafanikio ya Wakala huo
kwa kipindi husika katika makundi
matatu ambayo ni utekelezaji wa kazi
za jiosayansi, kuboresha rasilimali
watu, vitendea kazi, miundombinu
na mazingira yake pamoja na kazi na
tafiti zilizokamilika na zinazoendelea
kutekelezwa.
Kwa upande wa utekelezaji wa kazi
za jiosayansi, Taarifa ya GST imeeleza
kuwa Ramani mpya 60 za jiolojia
zimekamilika na kuchapishwa. Ramani
hizi ni muhimu kwani huwezesha
kubainisha uwepo wa madini katika
eneo husika.
Pia, taarifa ilibainisha kuwa
ukusanyaji wa takwimu za jiofizikia
kwa kutumia ndege umefanyika katika
Wilaya 35 ambayo ni asilimia 15 ya
eneo la nchi. Wilaya hizo ni Dodoma,
Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Nchemba,
Kondoa, Chamwino, Iramba, Manyoni,
Ikungi, Mkarama na Singida.
Wilaya nyingine ni pamoja na
Igunga, Babati, Kiteto, Hanang,
Simanjiro, Mbulu, Moshi, Same,
Monduli, Korogwe, Handeni, Kilindi,
Bagamoyo, Mvomero, Kilosa, Gairo,

Mbarali, Chunya, Bukombe, Kahama,


Ushirombo, Biharamulo na Mpanda.
Takwimu hizi zimeainisha maeneo
yenye viashiria mbalimbali vya uwepo
wa madini, kwa mfano eneo la Misaki,
Mpambaa, Sambaru na Londoni
ambapo ufahamu wa uwepo wa madini
ya dhahabu umeongezeka, taarifa
imeeleza na kuongeza kuwa, takwimu
hizi zimeonesha ongezeko la uwepo
wa madini ya graphite huko Merelani
mkoani Manyara na katika wilaya za
Kilindi na Handeni.
Imeelezwa kuwa, pamoja na
kubaini ongezeko la madini mbalimbali,
pia taarifa hizi hubaini mipasuko
kwenye ardhi hivyo kusaidia kuratibu
matetemeko na majanga mengine ya
asili.
Vilevile, uchunguzi wa sampuli
kwenye maabara umeongezeka kutoka
sampuli 650 (mwaka 2005) kwa
mwaka na kufikia jumla ya sampuli
4500 hadi 5600 kwa mwaka kwa hivi
sasa. Imeelezwa kuwa ongezeko hili
la sampuli limetokana na kuboreshwa
kwa vitendea kazi, majibu sahihi ya
uchunguzi na wafanyakazi kupatiwa
elimu na motisha.
Kuhusu
kuboresha
rasilimali
watu, vitendea kazi, miundombinu
na mazingira yake, taarifa ya GST
inaonyesha kwamba watumishi wapya
wapatao 100 wameajiriwa na mafunzo
mbalimbali ya muda mfupi na mrefu
yameendelea kutolewa ndani na nje
ya nchi. Vilevile, Wakala umeboresha
vitendea kazi vya maabara, ugani,
jiofizikia, uchoraji ramani, ofisi na
samani.

Aidha, taarifa imeeleza kuwa kwa


upande wa kazi zilizofanyika ni pamoja
na kukamilika kwa jumla ya tafiti 27.
Tafiti hizo zilihusu utafutaji wa madini ya
metali/vito, madini ya viwanda, nishati

ya jotoardhi, matetemeko ya ardhi,


milipuko ya volkano, mmomonyoko wa
ardhi, upatikanaji wa magadi, uchenjuaji
wa madini, ushauri wa namna bora ya
utafutaji na uchimbaji wa madini kwa
wachimbaji wadogo na uhifadhi wa
mazingira.
Wakala wa Jiolojia Tanzania
ulianzishwa kama Wakala wa
Serikali chini ya Wizara ya Nishati
na Madini mwaka 2005 na kupewa
jukumu la kubainisha maeneo yenye
kupatikana madini mbalimbali nchini ili
kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya
madini kwa lengo la kukuza uchumi wa
Taifa.
Pia,GSTimepewajukumulakuratibu
majanga asili ya jiolojia (matetemeko ya
ardhi, milipuko ya volkano, mionzi ya
asili kutoka kwenye miamba, kemikali
za sumu zitokazo kwenye miamba na
udongo, maporomoko ya ardhi) na
kutoa ushauri wa namna ya kujikinga na
kupunguza athari za majanga hayo.
Dhima ya GST ni kutoa takwimu
na taarifa za jiosayansi za kiwango
bora kwa gharama stahiki kwa wadau
ili kuongeza ufahamu wa rasilimali za
madini, hivyo kuchangia katika lengo la
Taifa la kupunguza umaskini, kuongeza
ufahamu wa majanga ya asili na jinsi
ya kupunguza athari zake, utunzaji wa
mazingira, kuboresha usalama wa watu
na mali zao.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Elimu ya OMCTP kuanza kutolewa


kwa kutumia gari la matangazo
Na Zuena Msuya

izara ya Nishati na
Madini imeanzisha
mfumo mpya wa
usajili wa wateja
kwa
kutumia
njia ya mtandao ijulikanayo kama
Online Mining Cadastre Transactinal
Portal( OMCTP) utakaowawezesha
waombaji na wamiliki wa leseni za
madini kujisajili kwa njia ya mtandao
ili kufahamu na kuhakiki taarifa zao
kwa urahisi.
Kamishna Msaidizi wa Madini
anayeshughulikia leseni, John Nayopa
amesema utaratibu huo umeanzishwa
ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka
Wizara na Taasisi za Serikali kurahisha
upatikanaji wa huduma bora karibu na
wananchi, kupokea malipo ya Serikali
kwa njia za kielektroniki ili kudhibiti
mapato tofauti na ilivyokuwa hapo

awali.
Mwaka 2000, kitengo cha utoaji
leseni kilikuwa Dodoma Wakati huo
mamlaka ya utoaji leseni ilikuwa
Dar-es-Salaam hali iliyosababisha
ucheleweshaji wa kutolewa leseni na
pia mfumo wa utoaji na kuchambua

leseni ilifanyika kwa mkono, alisema


Nayopa.
Aliongeza kuwa mfumo huo
unafanana na ule unaotumiwa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
katika malipo ya leseni za magari au
mfumo wa kununua luku ambao
utawapunguzia wananchi ugumu wa
kupata huduma.
Nayopa alisema mfumo wa
OMCTP utaongeza uwazi na kasi
ya utoaji wa leseni za madini,wateja
wataingiza maombi ya leseni wao
wenyewe, hivyo kupunguza tatizo la
mlundikano wa maombi katika ofisi
za madini.
Vile vile alisema kuwa wateja
watapata taarifa za leseni zao kila
wakati na kujua wanapotakiwa kufanya
malipo ya leseni au watakapotakiwa
kutuma taarifa za utendaji kazi pia
kurahisisha mawasiliano kati ya
Wizara na wamiliki wa leseni.

Awali waombaji wa leseni


walilazimika kwenda katika ofisi za
madini kujaza fomu za maombi,
kufyeka mipaka ya eneo wanaloomba
na kuweka vibao; kisha kumleta Afisa
madini ili kukagua eneo linaloombwa
na hatimaye kwenda kufanya malipo
ya maombi hayo kwenye ofisi ya
Madini,alisema Nayopa
Aliongeza kuwa wateja na Serikali
watakuwa na uhakika na maombi
yote yatakayowasilishwa (yakiwamo
maombi ya sihia (transfer), kuhuisha
leseni n.k.); na pia kuwa na uhakika na
malipo yote yatakayofanywa kupitia
mfumo wa OMCTP
Aidha aliongeza kuwa ili kutoa
elimu kwa wadau wote wa madini
Wizara itatoa mafunzo kuanzia tarehe
19 Julai hadi pale itakapomaliza wadau
wote kwa kuanzia mikoa ya Kanda ya
Mashariki, Kanda ya Kati,Magharibi
na Kanda ya Kusini.

NewsBulletin

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

KAMPUNI YA STAMIGOLD
MGODI WA BIHARAMULO
TAARIFA KWA UMMA

STAMIGOLD YATIMIZA MWAKA


MMOJA WA UCHIMBAJI DHAHABU
Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa uchimbaji dhahabu
katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera ambapo uchimbaji ulianza rasmi mnamo mwezi Julai, 2014. Ndani ya
kipindi cha mwaka mmoja wa uchimbaji (Julai 2014 Juni 2015), kiasi cha wakia 16,388 za dhahabu zimekwishazalishwa na jumla ya wakia 12,923 za
dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 15.6 zimekwishauzwa kwenye soko la kimataifa.
Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi ambapo uchimbaji
wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya African
Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.
Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika katika mgodi wa
Biharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo, Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya mgodi ni kutafuta namna ya kuhakikisha
uzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania
kwa ajili ya maslahi ya Taifa zima.
Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali na Watanzania
wenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu wameendelea kuonyesha uwezo
wao kwa kuhakikisha uzalishaji unaendelea kufanyika katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo wataalam wa kigeni kama ilivyokuwa
ikiaminiwa. alieleza Sebugwao.
Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa kufuata
taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa ushuru wa huduma wa 0.3%
ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015, kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fani
mbalimbali za kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.
Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kugawa
madawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Mavota,
ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi
vitatu vya ujasiriamali kwa kununua vyakula vya asili, mbogamboga na matunda wanayozalisha.
Kwa upande mwingine, katika kusherekea siku hiyo shamrashamra mbalimbali zilifanyika ikiwemo mechi ya mpira wa miguu ambapo timu ya mgodi
ilicheza mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka kidedea kwa bao 2-0. Baada ya
michezo kumalizika timu zote za mpira wa miguu zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa mgodi.
Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi cha mwaka mmoja
wa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
hilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na kusema kuwa mafanikio
yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na
wataalam wa kigeni.
Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali hapa mgodini
na kujionea kazi zinavyofanyika. Naomba muendelee na bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodi
huu mfano misaada inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaa
ya Taifa zima la Tanzania alifafanua Magala.
Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba kwa
bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji kutokana na vyanzo vilivyopo
kutegemea msimu wa mvua.
Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka historia kwa
kuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
STAMIGOLD Biharamulo
Plot. No. 417/418
UN Road
S.L.P 78508
Dar es Salaam.
Email: info@stamigold.co.tz Website: www.staigold.co.tz

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao
ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

You might also like