Hotuba Ya Mgombea Urais Wa CCM Dk. John Pombe Magufuli

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 6

1

HOTUBA YA MHE. JOHN POMBE MAGUFULI MGOMBEA WA


CCM KWA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA WAKATI AKITAMBULISHWA RASMI MJINI
DODOMA TAREHE 12 JULAI, 2015

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa


Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa
Zanzibar,
Makamu Mwenyekiti Bara
Viongozi Makuu Mliopo
Viongozi Wakuu Wastaafu,
Mgombea Mwenza,
Ndugu Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Wajumbe Wote wa NEC, Wajumbe wa Kamati Kuu na
Wajumbe Mkutano Mkuu mliopo,
Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini na Asasi zisizo za
Kiserikali mliopo hapa,
Mabibi na Mabwana
Asalaam Alaykhum! Bwana Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo,
Awali ya yote, napenda nichukue fursa hii adhimu sana,
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote yaliyofanyika hata
kuniwezesha leo hii kuwa mgombea wa Chama cha Mapinduzi.
Namshukuru kwanza, kwa kutufikisha wote hapa tukiwa buheri wa

afya. Namshukuru pia, kwa kutusimamia vizuri, kwa Usalama na


Amani toka kuanza kwa mchakato huu hadi hapa tulipofikia.
Tunazidi

kumuomba

aendelee

kutusimamia

mpaka

ushindi

utakapopatikana.
Naomba nirudie tena kuwashukuru kwa moyo wa dhati Kamati
Kuu, Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Wajumbe wa Mkutano
Mkuu kwa heshima kubwa mliyonipa kuipeperusha bendera ya
CCM katika kinyanganiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015. Nakosa maneno
sahihi na muafaka ya kuwashukuru. Ahadi yangu kwenu ni kwamba
sitowaangusha kamwe. Nitalipa fadhila hii, kwa kuinadi na
kuisimamia vizuri Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 na
kuitekeleza kwa makini kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania
ili tuendelee kukiweka Chama chetu kwenye nafasi ya ushindi daima.
Asanteni sana.
Niwashukuru sana viongozi wa wana CCM wa Dodoma kwa
kuandaa hafla hii ya kuzungumza nanyi na kupitia kwenu kwa
wananchi

wote wa Tanzania

kwa mara ya kwanza tangu

nilipoteuliwa na Chama leo asubuhi.


Najua matarajio ni makubwa sana.

Natambua, Watanzania

wote, wanataka misingi ya amani na umoja wetu iliyojengwa na

waasisi wa nchi yetu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage


Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume na kuimarishwa na
kuendelezwa na viongozi waliofuatia wa Jamhuri ya Muungano na
Marais wa Zanzibar inaendelea kudumishwa. Wanataka kuona
Muungano wetu na umoja baina ya watanzania unaendelea
kudumishwa bila kujali dini zao, rangi zao, makabila yao, wala
mahali watokako. Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu
kwamba mkikichagua Chama cha Mapinduzi nitasimamia na
kupigania misingi hii kwa nguvu zote, kwa moyo wote na kwa
kutumia vipaji vyote nilivyojaliwa na Mwenyezi Mungu ili nchi yetu
iendelee kuwa moja, Muungano wetu uzidi kustawi na kuhakikisha
wanatanzania wote wanaendelea kuishi kwa umoja na mshikamano.
Pili, Watanzania wanataka maendeleo ya haraka. Katika hili
natambua kwamba kila Mtanzania anao uwezo wa kujiletea
maendeleo. Bahati nzuri tayari misingi ipo. Nitafanya jitihada ya
kukidhi kiu yao hii kwa kuendeleza misingi sahihi iliyojengwa katika
awamu zote nne zilizonitangulia. Nyote ni mashuhuda wa kazi nzuri
iliyofanywa

na

mafanikio

makubwa

yaliyopatikana

kama

yalivyoelezwa bayana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete


alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 09
Julai, 2015. Nitayaendeleza kwa umakini, uhodari, juhudi na maarifa

ya hali ya juu, ili sasa nchi yetu ipae kuelekea kwenye maendeleo ya
juu kwa pato la nchi na pato la kila mmoja wetu.

Tupunguze

umaskini kwa kasi kubwa zaidi. Nafarijika kwamba Ilani ya Chama


chetu inanituma hivyo, nitaitekeleza kwa umakini wa hali ya juu
kabisa kwa manufaa ya nchi yangu na ya kila Mtanzania.
Tatu, natambua kwamba usalama wa raia na mali zao, na ulinzi
wa uhuru na mipaka ya nchi yetu ndiyo uhai wa taifa letu.
Hatutakuwa na mchezo na mtu yoyote atakayejaribu kuhatarisha
uhuru na mipaka yetu. Tutaendelea kutekeleza Sera za CCM za
kuboresha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kutekeleza
wajibu wao huo kwa ufanisi mkubwa zaidi na viendelee kuheshimika
ndani na nje ya nchi, viendelee kudumisha usalama wa wananchi wa
Tanzania pamoja na mali zao.
Nne, natambua kuwa Watanzania wote; vijana, wanawake,
wazee, wanaCCM na wasio wana CCM, wote wana matumaini
makubwa na Chama cha Mapinduzi. Kwa watoto, tunajua wanataka
kupata huduma bora hususan za elimu na afya.

Kwa vijana,

matumaini yao ni kuona juhudi za utatuzi wa changamoto


zinazowakabili zikiwamo ukosefu wa ajira zinafanyika kwa kasi
kubwa zaidi. Kwa akina mama, vijana na wazee matarajio yao ni
kupata huduma zilizoimarika kama vile afya, upatikanaji wa maji,

umeme hasa vijijini, kilimo bora na chenye tija, masoko kwa ajili
mazao ya kilimo na mazao mengine yatokanayo na sekta mbalimbali,
usafiri wa uhakika wa barabara, reli, anga na majini.
Ili haya yote yaendelee kutekelezwa vizuri na kwa ufanisi
mkubwa Watanzania wanayo Imani kubwa na matumaini kwa
Chama Cha Mapinduzi.

Chama chenye uwezo wa kuyaendeleza

haya. Ni katika Imani hii basi, naamini kuwa mwezi Oktoba, CCM
itashinda kwa kishindo na kuendeleza hatamu ya uongozi wa nchi
yetu kwa Awamu ya Tano. Napenda niwahakikishie kuwa,
nikichaguliwa kuwa Rais wa nchi yetu, kazi yangu kubwa ni
kuhakikisha Ilani inatekelezwa kikamilifu na kuongeza kasi ya
maendeleo kwa Watanzania wote, vijana kwa wazee, wanawake,
watoto wetu na nchi kwa ujumla. Tunachohitaji ni umoja miongoni
mwetu wana CCM kama kauli mbiu yetu inavyosema Umoja ni
Ushindi. Naomba viongozi na wanachama wa CCM tuiishi kauli hii
kwa matendo.
CCM iko tayari kwa mageuzi ya uhakika na ya haraka kwa
maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Nitawauliza? Kwa mageuzi
ya uhakika na maendeleo ya haraka kwa wote tuchague chama
gani? CCM, kumbe mnajua.

Kwa wenzetu Waislamu, Ramadhan Kareem

Asanteni kwa kunisikiliza.


Mungu kibariki Chama cha Mapinduzi,
Mungu ibariki Tanzania,
Kidumu Chama cha Mapinduzi.

You might also like