TANGAZO

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA
RPC.
Namba ya simu 2502572
Fax - +255252503734
E-mail:- rpc.mbeya.@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,


Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

TANGAZO KWA UMMA.


JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAJULISHA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA
MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA
KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KUWA WANATAKIWA KURIPOTI KWA MAKAMANDA
WA POLISI WA MIKOA TAREHE 28/08/2015 KWA AJILI YA MAANDALIZI YA USAFIRI WA
KWENDA SHULE YA POLISI TANZANIA
TAREHE 29/08/2015.
KILA MMOJA ATATAKIWA KUWA NA NAULI YA KUMWEZESHA KUSAFIRI TOKA
MAKAO MAKUU YA MKOA ANAKOANZIA KUSAFIRI HADI SHULE YA POLISI MOSHI NA
ATAREJESHEWA NAULI ATAKAPOFIKA CHUONI BAADA YA KUWASILISHA TIKETI YA
SAFARI. AIDHA TAREHE YA MWISHO YA KURIPOTI CHUONI NI TAREHE 05/09/2015 NA
ATAKAYERIPOTI BAADA YA HAPO HATAPOKELEWA.
AIDHA VIJANA HAO WATALAZIMIKA KUFIKA SHULENI WAKIWA NA VITU
VIFUATAVYO :
1.VYETI VYAO VYOTE VYA MASOMO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATES/RESULT
SLIP PAMOJA NA LEAVING CERTIFICATES) KIDATO CHA NNE, SITA NA VYUO.
2.VYETI HALISI VYA KUZALIWA (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATES). HATI YA KIAPO
CHA KUZALIWA HAITAKUBALIKA.
3. MASHUKA MAWILI RANGI YA BLUU BAHARI (LIGHT BLUE)
4.CHANDARUA CHENYE UPANA FUTI TATU
5.NGUO ZA MICHEZO (TRACK SUIT NYEUSI,T-SHIRT BLUE NA RABA)
6.PASI YA MKAA.
7.NDOO MOJA.
8.PESA ZA KULIPIA BIMA YA AFYA KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA MIA NNE TU
(50,400/=).
9.PESA KIDOGO YA KUJIKIMU.
ZINGATIA: KWA MUJIBU WA KANUNI ZA SHULE YA POLISI NI MARUFUKU KUFIKA
SHULENI NA SIMU YA MKONONI. ATAKAYEPATIKANA NA SIMU ATAFUKUZWA
SHULENI HAPO. SHULE ITAELEKEZA NA KUSAIDIA KUFANYA MAWASILIANO.
MAJINA YA WAHITIMU YANAPATIKANA KUPITIA TOVUTI www.policeforce.go.tz au
WAFIKE OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

You might also like