Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

MAPITIO YA UCHUMI WA TAIFA 2015

JovagoTanzania- Hali ya Uchumi Dhidi ya Sekta ya Utalii,

DAR ES SALAAM, Septemba 9, 2015 - Kutokana na mapitio ya kiuchumi


yaliyofanyika na (B.O.T) Benki ya Tanzania, inaonyesha uchumi
umeongezeka kutoka 5.1% kwa mwezi Mei mpaka 6.1% mwishoni mwa
mwezi Juni 2015.

Hata hivyo, kutokana na ripoti iliyotolewa na Tanzania Investment (2015);


Shilingi ya Kitanzania imepungua dhidi ya dola ya Kimarekani kwa 6.4%
ambapo ni wastani wa shilingi ya Kitanzania 2,082.5 kulinganisha na mwezi
Mei 2015 kwa shilingi 1,957.

Mr. Andrea Guzzoni Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania alifafanua


kwamba, hali ya uchumi Tanzania haipo katika hatua mbaya iwapo juhudi za
ufuatiliaji kwenye sekta mbalimbali zitatekelezeka ikiwemo kupunguza
malipo kwa kutumia dola badala ya shillingi za Kitanzania, kuhamisisha
matumizi ya fedha zetu, itasaidia kupanda kwa thamani ya shilingi yetu
aliongezea.

kwa upande mwingine inabidi kutambua kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi
za kipekee ambayo zaidi ya 25% ya eneo la nchi ni hifadhi za
Taifaalifafanua.

Mr.Guzzoni, anafafanua kwamba, ongezeko la watalii bado ni chachu ya


maendeleo Tanzania, ikiwa kwa mwaka tunapokea idadi kubwa ya watalii
kutoka ndani na nje ya nchi; Mwaka 1995 kulikuwa na idadi ya watalii
295,312 hadi kufikia 2014 watalii wameongezeka kufikia 1,140,156.

Hivyo, kukua kwa uchumi wa Tanzania kunasababishwa haswa na sekta


muhimu mbili ambazo ni sekta ya utalii na kilimo. Ongezeko la watalii
Tanzania imechangia zaidi ya dola milioni 2,006.32 kwa mwaka 2014,
ambapo pamoja na mauzo ya bidhaa asilia nje ya nchi zimekuwa ni vyanzo
vikuu katika kuongeza pato la dola za kimarekani million 9,398.5 sawa na
9.4% mpaka kufikia june 2015, (Tanzania investment, 2015).

Kwa upande mwingine, sekta moja haiwezi kuleta mabadiliko ya kiuchumi;


usafiri wa uhakika, afya na miundo mbinu inayoeleweka itapelekea kukuza
sekta ya utalii na kutanuka kwa soko la nje ya nchi.

Kuhusu Jovago
Jovago.com, tovuti inayorahisisha huduma za ku book hoteli kupitia
mitandaoni. Ofisi kuu hapa Africa zipo Lagos (Nigeria), Nairobi kenya, na

Dakar (Senegal).Jovago.com imegunduliwa na kampuni ya Africa Internet


Group (AIG) chini ya udhamini wa MTN na Millicom.

Jovago.com ni tovuti No.1 inayoongoza katika huduma za ku book hoteli


kupitia mtandaoni pamoja na kutoa huduma nzuri na za haraka kwa ufanisi
wa kiwango cha juu cha urahisi wa matumizi ya tovuti hiyo. Jovago.com
inazaidi ya hoteli 25,000 hapa Africa na hoteli 200,000 za dunia nzima
kwenye tovuti.

You might also like