Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK
OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi
zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu
Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake,
Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa
Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi
kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula
ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga.
Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella
Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia.
Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la
Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi
iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania ubunge
mkoani Ruvuma.

Ndugu Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro


anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na
Ndugu Mahiza.
Uteuzi na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka
huu, 2015 na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho kutwa
Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015

You might also like