Press Release - Siku Ya Tembo Kitaifa 2015

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA


SIKU YA TEMBO KITAIFA TAREHE 22.09.2015
Wizara ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na Shirika la Uhifadhi Duniani WWF ofisi ya
Tanzania kwa pamoja wanaadhimisha siku ya tembo kitaifa mwaka huu
tarehe 22/9/2015, kwa kujadili na wadau mbali mbali kuhusu kumuokoa mnyama
Tembo kupitia vyombo vya habari hapa nchini. Kauli Mbiu ni Wakati wa kuhifadhi
tembo waliosalia ni sasa
Malengo ya kuadhimisha siku ya Tembo kitaifa ni; kujenga uelewa na kuibua hamasa
ya wananchi kuhusu uhifadhi wa tembo; kujadili kwa kina madhara ya ujangili wa
Tembo katika nyanja za kijamii, kiikolojia, kiutamaduni na sekta ya utalii kwa jumla
na kutoa mapendekezo na hatua za kuchukua kuzuia ujangili wa Tembo.

Maadhimisho haya yanatokana na mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa


Mkataba wa Kimataifa wa kuzuia biashara ya Wanyamapori na viumbe walioko
hatarini kutoweka 'Convention on International Trade in Endangered Species CITES', uliofanyika mwaka 2010 katika mji wa Doha nchini Quatar. Nchi 37
zilizojaliwa kuwa na tembo barani Afrika zilikutana, na kupitisha mpango mkakati wa
kuhifadhi tembo barani Afrika (African Elephant Action Plan-2010). Mwaka uliofuatia
2011 Tanzania ilianza kutekeleza mpango mkakati maalum wa uhifadhi wa Tembo
(Tanzania Elephant Management Plan 2010-2015).
Tanzania inasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa wa wanyamapori barani Afrika na
Ulimwenguni kote, ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na rasilimali nyingi asili. Katika
kuhakikisha kuwa wanyamapori hususani Tembo wanalindwa, Tanzania imetenga
zaidi ya asilimia 24 ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi. Kipaumbele cha Mpango

Mkakati wa uhifadhi ni pamoja na; kulinda shoroba za wanyamapori hususani


Tembo; kupunguza migogoro kati ya wananchi na Tembo; kufanya tafiti za uhifadhi
wa tembo na kushirikisha wadau mbalimbali katika kuhifadhi Tembo. Serikali imekua
ikifanya shughuli za uhifadhi wa wanyamapori kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali, mashirika ya kimataifa kama WWF, taasisi
zisizo za kiserikali, wafanyabiashara, taasisi za kidini na wananchi kwa ujumla.
Naye mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania Dr. Amani Ngusaru amesema Tembo ana
mchango mkubwa kiikolojia pamoja na kusaidia uwepo na ustawi wa viumbe
wengine akiwemo binadamu.
Kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wa kazi ya kumlinda Tembo Ikiwemo
ujangili, ukame,

uhaba wa fedha, uchache wa watumishi na vitendea kazi,

ushirikiano hafifu wa wadau katika uhifadhi wa wanyamapori; uchomaji moto misitu


ambayo ni makazi ya wanyamapori; ubovu wa miundombinu katika maeneo
yaliyohifadhiwa na matumizi haramu ya wanyamapori.
Katika kukabiliana na changamoto Wizara imepanga mikakati mbalimbali kupitia
Mpango Mkakati wake 2013 2016. Mikakati hiyo ni pamoja na kuendelea kuajiri
watumishi wapya, mwaka 2014 waliajiriwa askari wapya 430 na mwaka 2015
tunategemea kuajiri askari 500; kuongeza ushiriki wa wadau mbalimbali ikiwepo
WWF na kushirikiana na nchi jirani (Cross border collaboration), kununua vitendea
kazi; kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi, kupunguza quota ya uwindaji wa Tembo
kutoka 200 hadi 100; kutumia teknolojia ya kisasa kuthibiti ujangili, kuimarisha
usimamizi wa rasilimali za wanyamapori kwa kufanya doria ndani na nje ya maeneo
yaliyohifadhiwa. Vilevile, miundombinu, vitendea kazi na huduma zitaboreshwa kwa
watumishi kwenye hifadhi za Taifa, mapori ya akiba na kikosi dhidi ya ujangili.
Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuadhimisha siku ya Tembo kitaifa ikishirikiana na
WWF Tanzania zinatoa wito kwa raia wema kutoa taarifa Makao Makuu ya Idara ya
wanyamapori, Tanapa, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro, Mashirika ya
kimataifa na/au kwenye kituo cha Polisi kilicho karibu ili kufanikisha kukamatwa
kwa majangili na wale wote wanaojihusisha na biashara haramu ya nyara, hususan
meno ya tembo, pembe za faru, nyama ya pori na wanyamapori hai wakiwemo
ndege, duma na nyani. Tushirikiane kuzuia uharibifu wa rasilimali zetu ili kulinda
urithi wa dunia.

IMETOLEWA
NA
KATIBU MKUU

You might also like