Professional Documents
Culture Documents
Mem Bulletin 99 Online PDF
Mem Bulletin 99 Online PDF
Mem Bulletin 99 Online PDF
HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Toleo
No.99
51
Toleo No.
Limesambazwa
kwa Taasisi na
Idara
zote
2015 25 - 30, 2015
Limesambazwa
kwa
Taasisi
naMEM
Idara zote MEM Tarehe
- 23-29 Januari ,Desemba
Nawatakia heri ya
e
g
n
u
b
a
W
Maulid,
Krismasi
Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA
n Hakikisheni
Somahabari Uk.2
umeme haukatiki
n Wasikilizeni Wananchi
wakati wote
Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo
Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya
Soma
habari
Uk. 4
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
aziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter
Muhongo anawatakia
heri na fanaka ya
Sikukuu ya Maulid na
Krismasi watumishi wote wa Wizara na
Taasisi zote zilizo chini yake.
Waziri Muhongo ambaye kwa
sasa anaendelea na ziara yake katika
Mikoa ya Kanda ya Ziwa kukagua
miradi mbalimbali ya umeme pamoja
na kuzungumza wachimbaji wadogo
wa madini ametuma salamu hizo huku
akiwataka watumishi wote kutumia
Sikukuu hii kutafakari vema namna
ya kuleta mabadiliko ya utendaji kila
mtu kwa nafasi yake aliyonayo ili
kuhakikisha kila mtumishi anatatua kero
za watanzania.
Prof. Muhongo ameongeza kwamba
katika kipindi hiki cha Sikukuu watendaji
wenye dhamana na sekta ya umeme
kuhakikisha Watanzania wanapata
umeme wa uhakika bila kukatika.
Amewaagiza Mameneja wa Mikoa
wa TANESCO kuwa makini na
miundombinu ya umeme kwamba
kuhakikisha kuwa hazianguki na nyaya
hazikatiki hovyo katika kipindi hiki
ambacho mvua zimeanza kunyesha
katika mikoa mbalimbali nchini.
Aidha, Waziri amewataka watendaji
wote wa vituo vinavyozalisha umeme
pamoja na Menejimenti ya TANESCO
na Idara ya Nishati, Wizarani
kuhakikisha kwamba baadhi ya
mitambo iliyoharibika inatengenezwa
haraka na kuendelea kuzalisha umeme
kama kawaida.
Aidha,
Prof.
Muhongo
anawakumbusha Watendaji Idara
ya Nishati wa Wizara, Mameneja
waandamizi wa Kanda na Mameneja
wa vituo vya kuzalisha maji kwa njia
ya maji kutembelea vyanzo vya maji
na kuzungumza Wananchi pmoja na
wadau wengine wakiwamo Mamlaka
za Mabonde, Wizara zinazohusika na
maji pamoja na wakulima ili kupata
ufumbuzi wa matumizi bora ya maji
katika kuzalisha umeme.
Pia Waziri ameiagiza TANESCO
kuimarisha kitengo chake cha ukaguzi
wa umeme kwa wateja (Revenue
Protection Unit) kudhibiti wizi wa
umeme ili kuokoa upotevu wa fedha.
Idara ya Madini pamoja na Wakala
wa ukaguzi wa Madini nchini (TMAA)
nao wameagizwa kuimarisha ulinzi
na ukaguzi katika mipaka na viwanja
Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam
ufuatia
kuchelewa
kukamilika kwa miradi
ya ujenzi wa Kuboresha
miundombinu
ya
Kusafirisha na Kusambaza
umeme katika jiji la Dar es Salaam
kupitia mradi wa Tanzania Energy
Development and Access Program
(TEDAP) chini ya ufadhili wa Benki ya
Dunia, Mkandarasi Kampuni ya SAE
Power Line ya Italia kwa ushirikiano
na Transrail Structures, wametakiwa
kukamilisha miradi hiyo ifikapo mwezi
Februari mwakani.
Hatua hiyo inafuatia ziara ya
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Kalemani kutembelea ujenzi
wa miundombinu hiyo jijini Dar es
Salaam, katika vituo vya Kurasini,
Mbagala, Kipawa na Gongolamboto,
inayosimamiwa na TANESCO,
ambayo
kukamilikwa
kwake
kutawezesha zaidi ya wakazi 10,000 wa
jijini Dar es Salaam, kuunganishwa na
nishati ya umeme.
Dkt.
Kalemani
ameiagiza
TANESCO, kuhakikisha kuwa, hadi
ifikapo tarehe 15 Januari mwakani, iwe
imekwishawalipa fidia wakazi 83 wa
Mbagala Charambe, Kiburugwa na
Kitunda ambao walikubali fidia ya kiasi
cha shilingi 717 milioni zilizotengwa
kupisha ujenzi wa mradi huo.
Bado kuna wananchi wapatao
23 ambao hawajaridhia malipo ya
NewsBulletin
Habari za nishati/madini
http://www.mem.go.tz
MEM
Tahariri
Na Badra Masoud
Tusherehekee Sikukuu
umeme ukiwaka!!
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Mhariri Mkuu: Badra Masoud
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya
Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Teresia Mhagama na
Asteria Muhozya
atibu
Mkuu
Wizara
ya Nishati na Madini,
Mhandisi Omar Chambo
ameeleza kuwa madini aina
ya Tanzanite yaliyokamatwa
yakitoroshwa nje ya nchi bila kuwa na
vibali tarehe 15 Desemba, 2015 kupitia
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) yamefikia thamani ya
Dola za Marekani milioni 1,207,990.
Katibu Mkuu alisema hayo jijini
Arusha wakati wa kikao chake na
Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa
ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara
ambazo zimeamua kufanya kazi kwa
pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini
ya Tanzanite na kufuatilia kwa karibu
shughuli za uchimbaji na biashara ya
madini hayo ili yanufaishe taifa.
Katibu Mkuu alisema kuwa Tanzanite
hiyo ghafi yenye uzito wa gramu 2,015.59
ilikuwa ikitoroshwa na raia wa India, Jain
Anurag aliyekuwa akitaka kuelekea mji
wa Jaipur kwa kutumia shirika la ndege la
Qatar.
Nataka niwaeleze watanzania
wanaoshirikiana na raia wa kigeni
kutorosha Tanzanite kuwa wajiepushe
na biashara hii haramu kwani hatua
kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao
na hatuna mzaha katika hili, alisema
Mhandisi Chambo.
Alieleza kuwa madini hayo
yaliyokamatwa yameshataifishwa kama
ambavyo sheria na kanuni za madini
zinavyoelekeza na kwamba zoezi hilo la
ukamataji watorosha madini hufanywa
na Wizara ya Nishati na Madini kupitia
Wakala wake wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA) kwa kushirikina na Taasisi
nyingine kama Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama
wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Idara ya Uhamiaji.
Aidha alieleza kuwa serikali itafuta
leseni za wafanyabiashara wa madini
watakaobainika kutorosha rasilimali
hiyo nje ya nchi ikiwemo kuwakamata
wachimbaji
na
wafanyabiashara
wanaokwepa kulipa kodi stahiki kwa
serikali.
Ili kudhibiti utoroshaji madini
unaofanywa na wafanyabiashara wenye
leseni na wasio na leseni, wazawa na
wasio wazawa, tumeshajipanga kwa
kushirikiana na Kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa mitatu ya Manyara,
Kilimanjaro na Arusha ili kudhibiti hali
hii na Tanzania ibaki kama kinara katika
uzalishaji na uuzaji wa madini haya na
sio nchi nyingine, alisema Mhandisi
Chambo.
Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro, Amos
Makalla alitoa masaa
24 kwa raia wa kigeni
wote wanaojihusisha
na biashara ya madini
ya Tanzanite na madini mengine kinyume
cha sheria kuondoka nchini mara moja na
watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Agizo hilo alilitoa baada ya Kamati
hiyo kubaini kwamba uwepo wa wageni
mbalimbali kutoka nje ya nchi hususani
Kenya, Sri Lanka, Nepal na India ambao
hujihusisha na biashara ya Tanzanite bila
kuwa na leseni zinazowaruhusu kufanya
hivyo na hatimaye hutorosha madini hayo
kwenda nje ya nchi.
TANESCO yatakiwa
kuwa makini
>>INATOKA UK. 3
mwakani ili kujadili namna ya
kutengeneza mitambo hiyo.
Alisema endapo mazungumzo
hayo yatashindwa kuzaa matunda
kwa pande hizo mbili kushindwa
kukubaliana, watarejea kwenye
sheria.
Taarifa
hiyo
ilimkasirisha
Waziri Muhongo na hivyo kuagiza
wataalamu wote waliohusika kwenye
manunuzi ya mitambo hiyo kutoa
maelezo ya kina haraka.
Juzi
nilikuwa
Somanga
Fungu na nimekutana na tatizo la
namna hii; hili halikubaliki lazima
waliotufikisha hapa wafahamike na
tayari nimemuagiza Mkurugenzi wa
Tanesco, alisema Profesa Muhongo.
Alisema tayari Tanesco inazo
kesi zaidi ya mia moja na hata hivyo
ni nadra kushinda na badala yake ni
fedha nyingi zinatumika na huwa
zinachukua miaka mingi.
Aliwaagiza kukaa pamoja na
endapo muafaka haukupatikana
wafike kwake kwa ajili ya
mazungumzo zaidi.
Waziri Muhongo alibainisha
kuwa aliamua kufanya ziara ili
kujionea hali halisi ya uzalishaji
umeme, aliongeza kuwa katika ziara
zake alizokwishafanya aligundua
kuwa hakukuwa na umakini wakati
wa ununuzi wa mitambo husika.
Ilipaswa wataalamu wafanye
uchunguzi wa mitambo na
kujiridhisha kabla mitambo hiyo
haijaletwa nchini, alisema Prof.
Muhongo.
Mbali na suala la umakini kwenye
ununuzi, Profesa Muhongo alisema
wataalamu wanapaswa kufuata
taratibu za uendeshaji wa mitambo
na hivyo aliwaasa kuwa makini muda
wote wakati wa kuendesha mitambo
hiyo.
Aidha, mara baada ya kutembelea
kituo hicho, Profesa Muhongo
alifanya ziara ya kushtukiza kwenye
kituo cha huduma kwa wateja cha
shirika hilo cha mkoani humo na
kuzungumza na wateja waliokuwa
kituoni hapo wakisubiri huduma.
Rashid Abubakar ni miongoni
mwa
wateja
waliokuwepo
kituoni hapo ambaye alimueleza
Waziri Muhongo kuwa huduma
zinazotolewa na shirika hilo
haziridhishi.
Alimueleza Waziri Muhongo
kuwa tangu tarehe 12 nguzo moja
maeneo anayoishi iligongwa na gari
na kuanguka lakini hadi sasa hakuna
hatua iliyochukuliwa na Shirika hilo
mbali na kupatiwa taarifa za mara
kwa mara.
Kufuatia malalamiko hayo Profesa
Muhongo alimkumbusha Meneja
wa Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo,
Mhandisi Amos Maganga kutekeleza
maagizo aliyoyatoa kwa uongozi
wa TANESCO ya kuboresha kwa
huduma hadi kufikia tarehe 15 mwezi
ujao.
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Habari za nishati/madini
Naibu Katibu Mkuu (katikati), Mhandisi Paul Masanja akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi waandamizi kutoka Idara ya Nishati na Uongozi wa
Norway katika Mkutano huo wa Ushirikiano wa Kitaasisi kati ya Tanzania
na Norway.
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akielekeza jambo wakati wa ziara yake
katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote. Anayemfuatia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akifuatiwa na
Balozi wa Tanzania Nchini Msumbiji, Shamim Nyanduga.
Na Mohamed Saif
aziri wa Nishati na
Madini,
Profesa
Sospeter
Muhongo
ameagiza kuharakishwa
kwa mazungumzo ya
kuiuzia Gesi Asilia kampuni ya kuzalisha
saruji ya Dangote iliyojenga mitambo
yake mkoani Mtwara.
Agizo hilo limetolewa hivi karibuni
mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya
kukagua mitambo ya kuzalisha umeme ya
Mtwara, Kituo cha kuchakata Gesi Asilia
cha Madimba, Kiwanda cha kutengeneza
saruji cha Dangote na Kituo cha kuzalisha
Mitambo
ya kuzalisha
umeme
iliyokodishwa
kutoka China
na Kampuni
ya Dangote.
kuzalisha umeme.
Profesa Muhongo alitumia
fursa hiyo kuzialika kampuni za
Watanzania kuwekeza kwenye
uzalishaji umeme kwa kutumia
vyanzo mbalimbali.
Mtaalamu
ametueleza
kwamba tunayo gesi ya kutosha
hivyo
watanzania
jitokezeni
muwekeze. Kuna matoleo ya gesi
Mtwara, Lindi, Mkuranga na Dar
es salaam; Watanzania wajitokeze
kuwekeza na hususan maeneo ya
Lindi na Mkuranga ambayo hadi
sasa hayana uwekezaji mkubwa,
alisema.
Hata hivyo Profesa Muhongo
aliupongeza uongozi wa Dangote
kwa hatua waliyofikia ya ujenzi wa
kiwanda hicho .
Aidha, Profesa Muhongo
aliambatana na Balozi wa Tanzania
nchini
Msumbiji,
Shamim
Nyanduga ambaye alikuwa mkoani
Mtwara kikazi.
Waziri Muhongo alimuomba
Balozi
huyo
kuhakikisha
anahamasisha Wafanyabiashara wa
Kitanzania waliopo nchini humo
kununua saruji ya Tanzania ili
kukuza Biashara ya nchini.
Profesa Muhongo alisema kuwa
Serikali imeamua kwa makusudi
kuwapa kipaumbele wazawa
wauze jasi na makaa ya mawe kwa
Dangote ili kuongeza kipato kwa
wananchi wake.
Aliwaagiza watoa huduma
husika wahakikishe wanazingatia
mkataba walioingia na Kampuni
hiyo na kuepuka kufanya kazi
kienyeji.
Profesa
Muhongo
aliiasa
kampuni hiyo kuhakikisha inauza
saruji yake kwa bei nafuu. Alisema
lengo la Serikali ni kuhakikisha vifaa
vya ujenzi nchini ikiwemo saruji
vinashuka bei ili kuwapa unafuu wa
ujenzi wananchi.
NewsBulletin
Habari za nishati/madini
http://www.mem.go.tz
akazi
wa
wilaya
ya
Chemba
katika kijiji cha
Olborot tarafa
ya Goima kata ya Mrijo katika
kitongoji cha Bomba mkoani
Dodoma walipatwa na mshtuko
kutokana na mpasuko mkubwa
wa ardhi uliosababishwa na
mvua zinazoendelea kunyesha
nchini.
Akizungumza na MEM
Bulletin, Mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Olborot Abdallah
Suti alisema kuwa tarehe
13 Desemba, 2015, mvua
kubwa ilinyesha kwa muda
wa masaa mawili mfululizo na
baada ya kumalizika ukatokea
mpasuko mkubwa katika ardhi
uliopelekea kuathiri zaidi ya
kaya 21.
Ilikuwa siku ya jumapili
mchana mvua ilinyesha kwa
muda wa saa mbili mapema
baada ya kuisha , tukaona ardhi
inapasuka na kuacha mashimo
makubwa sehemu mbalimbali
katika kijiji chetu alisema Suti.
Suti
aliongeza
kuwa
kutokana na hali hiyo
waliwasiliana na mamlaka
mbalimbali za serikali ikiwemo
Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST) ili kupata taarifa za
kiuchunguzi
kwa ajili ya
kuchukua tahadhari.
Mtalaam wa majanga
ya asili kutoka GST, Gabriel
Sehemu ya
nyumba mojawapo
iliyoathiriwa na
mpasuko.
aziri
wa
Nishati
na
M a d i n i
Profesa
Sospeter
Muhongo ameliagiza Shirika
la Umeme Nchini (Tanesco)
kushusha bei ya Umeme ili
upatikaji wa nishati hiyo ilingane
na kipato cha Watanzania walio
wengi ambacho bado ni kidogo..
Agizo hilo alilitoa hivi
karibuni wakati alipotembelea
kituo cha kuzalisha umeme cha
IPTL kilichopo Tegeta jijini Dar
es Salaam.
Kituo hiki kinazalisha
Umeme usiopungua kilowatt
45 kwa siku na wananchi
mnawauzia kwa shilingi 180
hadi 187 kwa uniti, ina maana
mnatengeneza faida mara mbili
kwa kuwa mnazalisha uniti moja
kwa gharama inayoanzia shilingi
90 hadi 100 hivyo ni lazima bei
ya umeme ishuke ili kuendana
na maisha ya mwananchi wa
kawaida,Alisema
Profesa
Muhongo.
Mafuta yalikuwa yakiuzwa
kwa pipa Dola za Marekani
milioni 200, lakini yakashuka
hadi Dola milioni 100 na hivi
sasa tunapoongea yameshuka
zaidi kwani kwa pipa yanauzwa
kwa Dola za Marekani milioni
38, kwa hiyo umeme lazima
ushuke bei,alisisitiza Profesa
Muhongo.
Vilevile Profesa Muhongo
alisisitiza kuwa lazima Tanesco
watoe huduma kwa wakati
pale wananchi wanapohitaji
huduma mbalimbali kutoka
katika Shirika hilo. wananchi
wakipiga
simu
hawapati
huduma wanayohitaji (Service
maintenance) hii ni mbaya
lazima mjirekebishe, alisema
Profesa Muhongo.
Kwa upande wake, Meneja
wa kituo hicho cha IPTL,
Mhandisi Mohamed Kisiwa
alisema kituo hicho kimeanza
kufanya kazi mwaka 2009 na
kinazalisha umeme kutoka
kwenye mitambo mitano
iliyopo katika kituo hicho kiasi
cha megawati 43.6 kwa siku.
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Viongozi Waandamizi
kutoka Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) na
Mamlaka ya Udhibiti
wa Nishati na Maji
(EWURA) wakati wa
kikao kilichofanyika
Wizarana na Naibu
Waziri wa Nishati
na Madini, Merdard
Kalemani.
Na Mohamed Saif,
Kanda ya Ziwa
aziri
wa
Nishati
na
Madini,
Profesa
Sospeter
Muhongo amefanya kikao
na Shirikisho la Wachimbaji
Wadogo (FEMATA), Viongozi
wa Shirikisho la Wachimbaji
Madini Wadogo wa mkoa wa
Geita (GEREMA), mkoa wa
Mwanza (MWAREMA) na
wachimbaji wadogo wa mikoa
hiyo miwili na kuwaahidi
kuendelea kuwatafutia maeneo
ya uchimbaji madini.
Aliyasema hayo katika kikao
kilichofanyikia katika Ukumbi
wa Mikutano wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
na kueleza kuwa Serikali pia
itawanyanganya maeneo watu
wote wanaohodhi maeneo
ya uchimbaji madini bila
kuyaendeleza.
Profesa Muhongo pia
kuwatengenezea
maandiko
yatakayowasaidia
katika
masuala mbalimbali ikiwemo
utafutaji wa mikopo katika
Taaisisi za Kifedha na kutoa
ushauri wa uchimbaji bora wa
madini.
Profesa Muhongo pia
aliagiza kuwa kabla ya kuisha
kwa mwaka wa Fedha wa
2015/16, Wizara ya Nishati na
Madini iitishe kikao na Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST),
Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), viongozi wa
FEMATA na MWAREMA
kujadili namna ya kuleta ufanisi
katika uchimbaji wa madini
mdogo nchini.
Aidha aliwataka wachimbaji
madini
nchini
kutunza
mazingira wakati wote wa
shughuli zao na kutovamia
maeneo halali ya utafiti na
uchimbaji mkubwa wa madini
na wazingatie utunzaji wa
amani na kuepuka uchochezi
wa aina yoyote.
NewsBulletin
Habari za nishati/madini
http://www.mem.go.tz
10
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Afisa Madini Mkazi katika Ofisi ya Madini Mirelani, Mhandisi Henry Mditi
akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na Ofisi hiyo iliyopo katika wilaya ya
Simanjiro mkoani Manyara.Wanaosikiliza ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa pili kushoto), Wa kwanza kushoto
ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje. Wengine katika picha ni
Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Uthaminishaji Madini, Latifa Mtoro
(wa kwanza kulia) na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uunganishaji na
Ushirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji (EISF), Catherine Lyombe.
Katibu Tawala mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi (wa kwanza kulia) akizungumza
na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro na Manyara mara baada ya kumaliza kikao ambacho kilijadili masuala
mbalimbali ikiwemo udhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza
kulia) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa
ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili
kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza
kushoto) akiwa katika moja ya vitalu vya uchimbaji madini ya Tanzanite katika eneo
la Mirelani mkoani Manyara wakati alipofanya ziara katika eneo hilo mara baada ya
kumaliza kikao kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti
utoroshaji wa madini ya Tanzanite.Kulia ni Afisa Madini Mkazi katika Ofisi ya Madini
Mirelani, Mhandisi Henry Mditi.
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Habari za nishati/madini
11
Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Kamishna
Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile (wa kwanza
kulia) huku Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza
kushoto) akibadilishana jambo Meneja Mwandamizi Miradi ya Umeme wa TANESCO,
Gregory Chegere (wa pili kulia) wakati Dkt. Kalemani alipotembelea maendeleo ya
ujenzi huo unajengwa na Kampuni ya SAE Power Line ya Italia kwa ushirikiano na
Transrail Structures.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kulia) akiongea
jambo na watumishi wa ofisi ya Huduma kwa Wateja (TANESCO) wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza katika ofisi ya TANESCO Kinondoni Kusini. Wengine ni Naibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na Kamishna Msaidizi wa
Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.
12
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Habari za nishati/madini
13
Watumishi wa GST kwa pamoja wakifanya usafi katika kituo cha mabasi
Dodoma katika kushiriki zoezi la kuweka mji safi.
14
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Teresia Mhagama
aziri wa Nishati na
Madini,
Profesa
Sospeter Muhongo
ametoa wito kwa
watu na
Taasisi
binafsi nchini kujitokeza na kuwekeza
katika kuzalisha nishati ya umeme ili
kuweza kuunga juhudi za serikali za
kuhakikisha nchi inakuwa na nishati
ya uhakika na ya gharama nafuu.
Profesa Muhongo aliyasema
hayo wakati wajumbe wanaounda
Shirikisho la Viwanda Tanzania
(CTI), Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF) na Chama cha
Wafanyabiashara, Wenye Viwanda
na Wakulima (TCCIA) walipofika
katika Wizara ya Nishati na Madini
ili kutoa pongezi kwa uteuzi wake na
kuwasilisha changamoto mbalimbali
za umeme wanazozipata katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Kama nchi tuna rasilimali
zote za kuzalisha umeme, nyinyi
pia mnakaribishwa kuwekeza ama
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
kutafuta wawekezaji wenye nia ya
akiwa katika kikao na Wajumbe wanaounda Shirikisho la Viwanda
dhati kuwekeza nchini, hata hivyo
Tanzania (CTI), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Chama cha kama serikali tunajitahidi kuongeza
Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) waliofika
umeme kwenye gridi ya Taifa na
katika Wizara ya Nishati na Madini ili kutoa pongezi kwa uteuzi wake ifikapo katikati ya mwezi Januari
na kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya umeme nchini. Kinyerezi I itaongeza megawati 80
katika gridi na ujenzi wa mitambo ya
Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Omar Chambo (kushoto kwa Waziri), Mkurugenzi Mtendaji umeme ya Kinyerezi II itakayozalisha
umeme wa kiasi cha megawati 240
wa Shirika la Umeme (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba
itaanza muda wowote kwani masuala
(kushoto kwa Katibu Mkuu) na kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa
ya kifedha yameshakamilika alisema
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel Nyantahe.
Muhongo.
Alisema kuwa serikali pia inataka
kuzalisha umeme kwa kutumia
makaa ya mawe ambapo kuna tani
zaidi ya bilioni 9 nchini, na kualika
Taasisi hizo binafsi kushirikiana na
serikali kuzalisha umeme huo ambapo
makampuni binafsi yataruhusiwa
kumuuzia mteja moja kwa moja
ili kuweza kuleta ushindani wa
usambazaji wa nishati hiyo muhimu
kwa wananchi.
Profesa Muhongo aliongeza kuwa
serikali inakaribisha wawekezaji ili
wazalishe umeme kwenye miradi
midogo ya maji isiyozidi megawati 10
ambayo itasadia wananchi walio nje ya
gridi ya Taifa kupata umeme na kutaja
vyanzo vingine vya uzalishaji umeme
vinavyohitaji wawekezaji kuwa ni
upepo, jua, jotoardhi, mawimbi,
tungamotaka, na bayogesi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo
Awali Mwenyekiti wa Shirikisho la
akijitambulisha kwa wajumbe wa wanaounda Shirikisho la Viwanda
Tanzania (CTI), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Chama cha Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel
Nyantahe alisifu uteuzi wa Profesa
Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) waliofika
katika Wizara ya Nishati na Madini ili kutoa pongezi Waziri wa Nishati Sospter Muhongo kuwa Waziri wa
Nishati na Madini na kueleza kuwa
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) kwa uteuzi wake na
amekuwa na mchango mkubwa kwa
kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya umeme nchini.
Taifa katika kuhakikisha kuwa nchi
kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) inakuwa na nishati ya umeme ya
Dkt. Samuel Nyantahe.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa TCCIA, kutosha kupitia vyanzo mbalimbali
Adam Zuku, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey vya uzalishaji nishati hiyo.
Simbeye.
Changamoto
nyingine
tunayokumbana nayo ni kutokulipwa
kwa fidia kwa mitambo inayoungua
wakati umeme unapokatwa ghafla,
kuchelewa kwa watumishi wa Tanesco
katika eneo la tukio pale ambapo tatizo
la umeme linaripotiwa na pia kuwa
na bei kubwa za umeme ambazo
zinapeleka bidhaa tunazozalisha
pia kuuzwa kwa gharama kubwa,
alisisitiza Dkt. Nyantahe.
Alisema kuwa bidhaa zinazotoka
Tanzania hushindana na za nchi
nyingine za Mashariki na Kusini
mwa Afrika hivyo ni vizuri gharama
za umeme zikashuka ili bei ya bidhaa
hizo zishuke na hivyo kupata soko
kubwa nchi za nje.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo akijibu
hoja hizo alisema kuwa Wizara
inatambua uwepo wa changamoto
za upatikanaji wa umeme wa uhakika
na wa gharama nafuu na kwamba
Wizara inafanyia kazi suala hilo.
Tunatambua kwamba umeme
hautoshi na ndio maana tumeamua
kuwa na energy mix, ya kwanza ni
kuzalisha umeme kwa njia ya gesi
ambayo tunayo ya kutosha kwani
mpaka sasa kiasi kilichopatikana ni
futi za ujazo trilioni 55.08, hivyo tuna
uwezo sasa wa kuzalisha umeme kwa
kusaidiana na makampuni binafsi,
alisema Muhongo.
Kuhusu suala la upunguzaji
wa bei za umeme, alisema kuwa
ameshawaagiza watendaji wa Shirika
la Umeme nchini (TANESCO) na
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma
za Nishati na Maji (EWURA)
kufanyia kazi suala hilo na kuwasilisha
mapendekezo kwake mnamo tarehe 2
Januari 2016 na kusema kuwa kwa
vyovyote vile bei hiyo lazima ipungue.
Profesa Muhongo pia alisisitiza
kufanya mabadiliko ya watendaji wa
Idara ya Nishati katika Wizara ya
Nishati na Madini na TANESCO
kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo urasimu, ukosefu wa ubunifu
katika uanzishaji na uendelezaji wa
miradi ya umeme, majadiliano ya
mikataba kuchukua muda mrefu na
kueleza kuwa yote hayo yanalenga
katika kuleta ufanisi katika sekta ya
umeme nchini.
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Habari za nishati/madini
15
16
Habari za nishati/madini
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
SHIRIKA LA MAENDELEO YA
PETROLI TANZANIA (TPDC)
Imetolewa na;
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,
P.O.Box 2774,
Dar-es-Salaam.
Tanzania.
1.
2.
3.
4.
a)
Umeme wa Jua (Solar)
b) Umeme wa Upepo (Wind)
c)
Umeme wa Jotoardhi (Geothermal)
d) Umeme wa Mawimbi (Tides and Waves)
e)
Umeme wa Mabaki ya taka Tungamotaka
(Biomass)
f)
Bayogesi (Biogas).
Kwa mawasilano, wasiliana na wafuatao:WIZARA YA NISHATI NA MADINI:Samwel Mgweno
Simu ya mkononi Na. 0754651364
E.mail samuel.mgweno@mem.go.tz
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
(TANESCO):Anitha Ishengoma
Simu ya mkononi 0687350076
E-mail anitha.ishengoma@tanesco.co.tz
Tangazo hili limtetolewa na: Wizara ya Nishati na
Madini
Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao
ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini