Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo inapenda kuujulisha Umma kwamba


kumekuwapo na upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook,
Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo
Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo
hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.
HAYARUHUSIWI KUVALIWA SEHEMU ZIFUATAZO
1.
2.
3.
4.

Kwenye masoko makubwa


Hospitali kubwa(Private or Public)
Maofisini na Vyuoni
Mijini kwenye mikusanyiko ya watu wengi

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo kwa wale ambao watavaa mavazi haya
ikiambatana na faini ya sh. 100,000/= mwisho wa kunukuu.
Tunachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa hizo kuwa siyo za kweli na kwamba mhusika
amefanya uhalifu wa kimtandao kwa kuaanda taarifa yake ya uongo na kuibandika katika uso
wa Tovuti ya Wizara yenye anuani: www.habari.go.tz kwa lengo la kuipotosha jamii.
Kufuatia uharifu huo Serikali inatoa onyo kali na haitawavumilia wale wote wanaokiuka
misingi ya sheria ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo inakataza kusambaza taarifa za uongo
na haitasita kuwasifikisha katika vyombo vya sheria wale wote watakaobainika kufanya
uharifu huo.
Pamoja na upotoshaji huo wa makusudi napenda pia kutumia wasaa huu kuwakumbusha
watumishi wa umma na jamii yote kwa ujumla kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma inao Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa mwaka
2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa Umma. Waraka huo umeainisha mavazi ambayo
hayafai kuvaliwa katika ofisi za umma kwa wanawake na wanaume; aidha umeelekeza aina
za mitindo ya nywele isiyofaa pamoja na aina za viatu visivyofaa.
Mifano ya mavazi yasiyokubalika kwa watumishi wa umma wanawake ni kama vile nguo
zinazobana, nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi, nguo ambazo zinaacha sehemu ya
mwili wazi kama vile kitovu na kifua, nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi
ambayo hayaendani na shughuli za Serikali, kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi,

nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent), suruali za Jeans, na nguo zingine zote
zenye kukinzana na maadili ya utumishi wa umma na jamii kwa ujumla.
Aidha, kwa upande wa wanaume mavazi yasiyokubalika ni pamoja na nguo ambazo ni za kazi
maalum kama vile michezo (hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu), nguo ambazo zina
michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za Serikali, nguo zinazobana,
kaptura ya aina yoyote, suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa, suruali za Jeans na
Fulana T-shirts (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika), Kikoi au
msuli, nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa
kitu fulani.
Pamoja na kuwepo kwa miongozo ya mavazi yanayostahili kwa watumishi wa umma, tafsiri
ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

You might also like