Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 5

TANZANIA FEMINIST AND YOUTH CHANGE ORGANIZATION.

(TAFEYOCO)
KINONDONI MUNICIPAL ,DAR ES SALAAM REGION
P.O.BOX 1078, DAR ES SALAAM ,TANZANIA
Mobile: +255 (0) 713463420,+255(0)784113604 ,Email: tafeyoco@gmail.com
Be the change, Life is now
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UTENDAJI WA MHE: RAIS WA
TANZANIA Dr. JOHN POMBE MAGUFULI.
Shirika

la

TAFEYOCO

(TANZANIA

FEMINIST

AND

YOUTH

CHANGE

ORGANIZATION)ni shirika linalojihusisha na maswala ya Wanawake na vijana katika kutatua


changamoto zao kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Makao makuu ya shirika yapo Wilaya ya kinondoni.
Motto wa shirika letu ni BADILIKA, MAISHA NI SASA. (Be the change, life is now)
A. MAFANIKIO YA MHE. RAIS MAGUFULI KWA SIKU MIA MOJA.

1. Mhe. Rais amefanikiwa kuweka uwazi kwenye shughuli mbalimbali za utendaji


Serikalini, kuna tofauti kubwa na watangulizi wake.Hivi sasa wananchi wameanza kujua
namna Serikali yao inavyotenda kazi.
Mhe. Rais amefichua madudu yote yaliyokuwa yanafanywa na viongozi waliomtangulia. Mfano
wakurugenzi wa Taasisi za Umma kama Bandari, Mamlaka ya mapato, Mamlaka ya
vitambulisho (NIDA) na Takukuru.
Mhe. Rais amefichua Siri na wizi uliokuwa umefanyika Serikalini na kusababisha kukosekana
kwa huduma za kijamii kama umeme, Maji na huduma bora za Hospitalini.
2. Mhe. Rais kwa hizi siku mia moja ameonyesha ubunifu wa kuongeza mapato ya nchi
kwa kuondoa matumizi yasiyo ya ulazima Serikalini na kuamishia fedha kwenye mambo
ya Msingi.Mfano, aliondoa sherehe za Uhuru (9 December), Siku ya Ukimwi, pia
alipunguza bajeti ya pesa za Sherehe ya kupongezwa iliyoandaliwa na wabunge.

Mhe. Rais alifanya haya yote kama njia ya kuongeza mapato na kusaidia shughuli za maendeleo
katika jamii. Hakuna kiongozi mwingine aliyeweza kufanya hivi. Haya yote Rais aliyabuni
kuongeza mapato baada ya kuikuta Hazina haina pesa.
Mhe. Rais ameweza kuokoa Bilioni saba (7) kwa kuzua safari za nje zisizo na tija kwa Taifa.
Kwa ubunifu wa Mhe. Rais ameweza kusimamia mamlaka ya mapato na kuweza kupata
makusanyo ya tilioni 1.5 kwa mwezi, makusanyo ambayo hayajawai kupatikana kipindi
chochote cha nyuma.
3. Mhe. Rais ameonyesha Uzalendo mkubwa kwa nchi kwa hizi siku mia moja (100).
Amekuwa mfuatiliaji wa mambo kwa watendaji Serikali, amekuwa akitamka waziwazi
kuwa amejitoa sadaka kwaajiri ya kuwasaidia watanzania hasa wale wenye hali duni
.Hakuna kiongozi aliyewahi kutamka maeneo kama haya hadharani kabla yake. Hii
inaonyesha hali ya kujitoa kwa Mhe. Rais ingawa anakutana na vipingamizi maeneo
mbalimbali lakini hakati tamaa.Kwake Tanzania kwanza.
4. Mhe. Rais kwa hizi siku mia moja amethibitisha usemi wake wa hapa kazi tu.
Amewaondoa

watendaji

kadhaa

Serikalini

waliokuwa

hawawajibiki

ipasavyo,

amewasimamisha kazi watendaji kadhaa kwa uzembe kwenye utendaji. Amekuwa


akifuatilia utendaji kwenye Taasisi na mashirika ya umma na kuwawajibisha bila
kuwaonea huruma wala aibu watendaji wabovu.
5. Mhe. Rais ndani ya hizi siku mia moja amefanikiwa kuitangaza Tanzania kimataifa kwa
kumkaribisha nchini balozi wa Israeli.Ni kitendo ambacho viongozi wengi waliopita
walishindwa kufanya hivyo. Kwa miaka mingi Watanzania wamekuwa wakitamani kuwa
na ubalozi wa Israeli hapa nchini lakini ilionekana kuwa ngumu kwa watangulizi
wako.Ndani ya siku mia moja Mhe. Rais ameweza kuuleta ubalozi wa Israeli na wakaaidi
kufungua ubalozi wao hapa nchi, hii ni hatua kubwa kwa Serikali ya Magufuli.
6. Ndani ya siku mia moja Mhe. Rais amewathibitishia Watanzania kuwa yeye ni Amiri
jeshi Mkuu kwa kuvaa magwanda ya jeshi (sare za jeshi ya Wananchi JWTZ) Hakuna
kiongozi aliyeweza kufanya hivyo kabla, hii ni hatua kubwa kwa Mhe. Rais kama Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi yote Nchini.
7. Mhe. Rais ndani ya hizi siku mia moja amewapa Watanzania siri ya umaskini
wao,chanzo

na

sababu

za

Watanzania

kuwa

maskini

na

ameamua

kujitoa

muhanga/kujilipua kwa ajiri ya kuwakomboa Watanzania na umaskini wao. Hakuna


kiongozi aliyewai kuthubutu kutoa sababu za umaskini wa Watanzania.
B. CHANGAMOTO NA USHAURI KWA MHE. RAIS MAGHUFULI KATIKA
UONGOZI WAKE.
Unapobadili mfumo wowote wa maisha hakukosekani changamoto hasa kwa wale
wasiopenda mabadiliko chanya. Mhe Rais kwa jitihada anazozifanya kuna viongozi
kadhaa wanajaribu kumkwamisha Mhe. Rais kwa kukosoa jitihada zake tena viongozi
wengine wanakosoa hata hatua anazochukua Mhe. Rais kwa ajiri ya kuiponya Tanzania.
Vitendo vya kuponda jitihada za Mhe. Rais na kukosoa hatua bora anazochukua kwa ajiri
ya Tanzania mpya kwa kweli havikubaliki na viongozi wote wenye tabia hii tunawaomba
waache kabla nguvu ya umma haijawageukia.
Kama kuna kiongozi au viongozi wanajiandaa kwa uchaguzi wa mwaka 2020 ni bora
wangeanza kumsaidia Mhe. Rais kwa kutatua kero mbalimbali kwenye shughuli za
kijamii kuliko kutaka kumkosoa Mhe. Rais.Tunawaomba viongozi wa siasa wamsaidie
Mhe. Rais katika jitihada zake, wamtie moyo na kumuombea kwa MUNGU wanasiasa
watangulize Tanzania kwanza, kuliko tama zao binafsi za uongozi.
Pamoja na mafanikio aliyoyapata katika hizi siku mia moja bado kuna changamoto
nyingi Mhe. Rais inabidi hazifanyie kazi katika utendaji wake.1. Mhe. Rais anatakiwa kuzipa nguvu taasisi za Umma na mashirika ya umma ili yaweze
kufanya kazi kwa ufanisi. Hazijengee nguvu taasisi hizi ili zifanye kazi bila hofu wala
uwoga kutoka kwa kiongozi yoyote. Taasisi kama, Mahakama, Bunge, Takukuru, Polisi,
Magereza, Baadari, TRA, BOT na nyingine nyingi ziweze kujengewa nguvu kubwa ya
kimamlaka. Hii itamsaidia sana Mhe. Rais katika utendaji wake atopata shida ya kwenda
kuvamia kwenye taasisi na mashirika ya Umma.
Hizi taasisi zikiendelea kuwa dhaifu itamsababishia Rais kuingilia maeneo yote na
kumtengenezea Mhe. Rais hali ya Udikteta na hali ya (one made show) kuwa yeye ndo
kila kitu kwenye nchi nah ii ni hatari pale atakapomaliza muda wake au akishindwa
kuendelea kuongoza kwsababu yoyote.Je! Tanzania itarudi kulekule?
2. Pia hatukubaliani na kauli ya Mhe. Rais ya kutaka kuwapa muda mawaziri wake. Mhe.
Rais ndiye kiongozi pekee wa nchi aliyechukua muda mrefu kutangaza baraza lake la
mawazili kuliko waliomtangulia, tena hata hivyo kuna baadhi ya wizara aliziacha wazi

kwasababu alikosa watu sahihi.Kwa maandalizi haya kamwe haiingii alikini kwa aina hii
ya mawaziri aliowachagua

eti tuwape muda wajifunze !wakati wengine walikuwa

mawaziri kwenye Serikali zilizopita. Tungemuomba Mhe. Rais kama anaona kasi ya
mawaziri wake haiendani na kasi yake kiutendaji ni bora hawatumbue majipu na kuwatoa
kwani siyo dhambi. Haikubaliki Mhe Rais au waziri mkuu ndio watu pekee wa kugundua
madudu kwenye taasisi za Serikali wakati wapo mawaziri husika wa maeneo hayo.
3. Tunamshauri Mhe. Rais aunde chombo maalum cha monitoring and evaluation kwa
wafanyakazi wa Serikali hii itapunguza kama siyo kuondoa tabia za rushwa, wizi, uvivu
na Ufisadi kwa wafanyakazi wa Serikali.Siku hizi mfanyakazi wa BOT,HAZINA,
TRA,TPDC,BANDARI,UWURA,TANESCO,TCRA akiajiliwa ndani ya miezi sita
asipokuwa na gari na viwanja kadhaa anaonekana mjinga na mshamba hii haikubaliki
kwenye dunia ya leo.
4. Tunamuomba Mhe. Rais aiangalie SUMATRA vizuri ili kama kuna majipu inabidi
yatumbuliwe haraka sana, haiwezekani bei ya mafuta inashuka kila kukicha kwa kazi
nzuri ya EWURA alafu nauli za mabasi na daladala zinabaki palepale kwa muda mrefu.
Lazima jitihada za makusudi zifanyike ndani ya SUMATRA ili kukipa meno chombo
kifanye kazi zake bila mashinikizo ya watu wachache.
5. Tunamuomba Mhe.Rais apitie pia kwenye magereza yetu hapa nchini ili kama kuna
majipu yaweze kutumbuliwa. Hali za magereza ni mbaya,wafungwa wamekuwa wengi
kuliko uwezo halisi wa magereza, mazingira siyo rafiki kwa wafungwa.
6. Tunawaomba viongozi wa Serkali waweze kutimiza wajibu wao na kumsaidia Mhe. Rais
kutabua kero mbalimbali za wananchi badala ya kumsubili hadi rais achukue hatua.Jamii
ina watendaji wa Serikali kama wakuu wa mikoa, Wilaya wakurugenzi, mameya,
Maofisa Elimu wa mkoa na wilaya, wabunge na madiwani. Wote hawa wana uwezo wa
kutatua matatizo ya kukosekana kwa kutatua matatizo ya kukosekana kwa madawati
mashuleni, kujenga madarasa kwa wanafunzi wanaokosa sehemu ya kusomea kwa
uwingi wa elimu bure.
Shirika letu halitaishia kumfanyia tamthimini Mhe. Rais peke yake bali litazunguka nchi
nzima kuangalia utendaji wa madiwani na wabunge kama kweli wanatimiza ahadi zao
kwa wananchi na kumsaidia mhe Rais.

Mwisho, tunamuomba Mhe Rais apange muda wa kuonana na vijana wa mkoa wa Dar es
salaam kama alivyofanya kwa wazee. Ni miaka yote viongozi wa nchi ukutana na wazee
na kusikiliza changamoto zao lakini kwa sasa Tanzania idadi kubwa ya watu ni vijana na
ndio waliokuwa wanakesha na kuyalilia mabadiriko haya tunayoyaona kipindi hiki hivyo
tunamuomba Mhe Rais akutane na vijana na kusikiliza changamoto zao na ushauri
kwenye utendaji wake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.


MUNGU MBARIKI MH. RAIS MAGUFULI.
MUNGU LIBARIKI SHIRIKA LA TAFEYOKO.
Viongozi na Wanachama.

You might also like