Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ameagiza
yafanywe mabadiliko makubwa katika Vitengo mbalimbali vya Idara ya
Uhamiaji ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.
Mheshimiwa Kitwanga ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao
na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na
Vitengo vya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katika kikao hicho, Mheshimiwa Kitwanga ameagiza watumishi wote wa
Idara ya Uhamiaji walioko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro, wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini,
wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Wengine watakaohamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati
za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji
jijini Dar es Salaam.
Aidha ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya
wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, na pia wale wa Vituo vya Tunduma,
Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, na pia
watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika Vituo hivyo.
Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko
makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma
zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.
1

Amesema katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili


kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini
lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wale
wasiowajibika.
Amesema kufuatana na utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa
matatizo ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza
kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni
matumizi mabaya ya madaraka. Asilimia 15 inahusisha vitendea kazi wa
mifumo hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia 5
ukabila na upendeleo.
Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi
zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na waepuke vitendo
vya kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza madawa ya
kulevya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi
23 Februari, 2016

You might also like