Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Anuani ya Simu:

NUKUSHI:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI

UHAMIAJI

OFISI YA UHAMIAJI WILAYA


S.L.P 417

BUNDA

YA UHAMIAJI
SIMU:OFISI
+255 282622426
S.L.P 369
KUMB .NA.BND/C.1/01/26
MUSOMA

Sunday, 22 May 2016

Afisa Uhamiaji Mkoa


S.L.P. 369
MUSOMA

Yah: KUPOTEA RISITI ZA SERIKALI ERV NO 49506397 HADI 49506400


Leo tarehe 23/03/2015 wakati tunaendelea na shughuli za kawaida amekuja
Mchungaji wa dhehebu la AIC Tanzania aitwaye Obed Daud Lugamba akiwa na
risiti (ERV) namba 49506400 iliyotolewa tarehe 27/2/2015 ikionyesha kuwa
alilipia ombi la Pasipoti kiasi cha Shs 50,000/= (Elfu hamsini). Amekuja kufuatilia
pasipoti kwa vile aliambiwa tarehe 20/3/2015 itakuwa tayari imekuja.
Nilimhoji nani alimhudumia amemtaja Marintha Morumbe na kwamba
alielekezwa akalipie pasipoti baada kulipia viapo mahakamani, viapo vililipiwa
shs 2000/= na alipewa risiti kabla viapo hivyo havijaandaliwa. Kwa vile Mchungaji
hakuwa na hela siku hiyo alienda nyumbani na baada ya siku kama tatu alitumwa
mtu mwingine kuja kulipia ombi hilo. Kwa mujibu wa Mchungaji huyo aliyeleta
hela hizo hakupewa bank slip akalipie benki bali aliandikiwa risiti na Marintha
namba 49506400 na kuelekezwa kurudi tena baada ya tarehe 20/03/2015 ambapo
pasipoti itakuwa imeletwa toka Dar es salaam. Pia aliandika namba ya simu
kwenye risiti yake ili wawe wanawasiliana. Mara kwa mara amekuwa
anamwambia kuwa mambo yanaenda vizuri kupitia namba 0765 715737.
1

Nilipocheki kujiridhisha kama risiti hiyo imetoka ofisi hii nilikuta ERV zote
kwenye ukurasa wa mwisho kuanzia namba 49506397 hadi 49506400
zimenyofolewa kilichobaki ni nakala ya 2, 3 na 4 orijino hazipo.
Kabla hajaondoka kwenda Bologonja alichukua shilingi 300,000/= (laki tatu)
ambazo zilikuwa ni ada ya maombi 5 matano ya pasipoti ya ndg Kweka na familia
yake bila kuwapa risiti wala kukamilisha maombi. Alihaidi kumrejeshea hela zake
mara moja lakini hakufanya hivyo hadi akaenda Bologonja. Tumekuwa na wakati
mugumu na Marintha kuhusu kukopa hela za watu na kushindwa kuwarejeshea.
Pia amekuwa na tabia ya kutumia mihuri ya ofisi kwa shughuli za kukopa hela kitu
ambacho ni hatari sana.
Kwa vyovyote vile yeye ndiye aliyenyofoa risiti hizo kwani kitendo cha
kuandika risiti bila kufuata utaratibu wa mteja kwenda benki ni kosa pia kumpa
risiti ambayo ni feki ni kosa pia.
Napendekeza mkuu ikiwezakana arudishwe ili atoe maelezo hizo risiti
nyingine ziko wapi au tufungue taarifa Polisi ili watusaidie uchunguzi. Pamoja na
barua hii naambatanisha nakala ya risiti iliyoletwa na Mchungaji, makubaliano ya
kukopa hela kwa kutumia mihuri ya ofisi, na ombi la Mchungaji Obed kwa hatua
zako.

Naomba kuwasilisha

DCIS E. Mushongi
Afisa Uhamiaji Wilaya
BUNDA

You might also like