Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Kwa Vyombo Vya Habari Leo Tarehe 28.06.2016

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAMS: POLISI,
TELEPHONE: 2500712
Fax: 2502310
E-mail: mwapol@yahoo.com
rpc.mwanza@tpf.go.tz

OFISI YA
KAMANDA WA POLISI,
MKOA WA MWANZA,
S.L.P. 120,
MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO


VYA HABARI LEO TAREHE 28.06.2016

WATU WATANO WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUMI NA WATATU


KUJERUHIWA BAADA YA AJALI YA
KUPINDUKA WILAYANI MISUNGWI.

GARI KUGONGA JIWE

NA

MWANAFUNZI WA CHEKECHEA SHULE YA MSINGI ILUNGA AMEFARIKI


DUNIA BAADA YA KUPIGWA FIMBO NA BABA YAKE WA KAMBO
WILAYANI MAGU.

KATIKA TUKIO LA KWANZA


KWAMBA TAREHE 28.06.2016 MAJIRA YA SAA 7:00 USIKU KATIKA BARABARA YA
MWANZA SHINYANGA ENEO LA BUSHINI KATA YA MABUKI WILAYA YA MISUNGWI
MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.449 BCB AINA YA ZHONGTONG MALI YA
KAMPUNI YA SUPER SAMI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE
WILLIAM ELIAS @ MASA MIAKA [44] MKAZI WA MABIBO DAR ES SALAAM,
LIKITOKEA DAR ES SALAAM KWENDA MWANZA LILIGONGA JIWE LILILOKUWA
BARABARANI HALI ILIYOPELEKEA DEREVA KUSHINDWA KULIMUDU GARI HILO NA
KUANGUKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO [5] AKIWEPO DEREVA WA
GARI HILO NA MSAIDIZI WAKE PAMOJA NA MAJERUHI KUMI NA WATATU [13]
AIDHA MAREHEMU WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1. DEREVA WA GARI HILO
AITWAYE WILLIAM ELIAS MIAKA [45] MKAZI WA DAR ES SALAAM, 2. VAILETH
ODEDE MIAKA [21] MKAZI WA MWANZA, 3. MWANAMUME MMOJA NA WANAWAKE
WAWILI WENYE UMRI WA MIAKA 25-30 AMBAO MAJINA YAO BADO
HAYAJATAMBULIWA MPAKA HIVI SASA, NA MAJERUHI KUMI NA WATATU [13]
WATANO KATI YAO WAMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KUPATIWA
MATIBABU NA WENGINE NANE WANAENDELEA NA MATIBABU KATIKA HOSPITAL YA
WILAYA YA MISUNGWI AMBAO NI 1. SOPHIA MIRAJI ANAYEKADIRIWA KUWA NA
MIAKA 20 HADI 25, 2. KIBILO MWACHA ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA KATI
YA 35 HADI 40, 3. BONIPHACE CHARLES ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA 38
HADI 40, 4. FRANK MUNYUMI ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA KATI YA 25 HADI
30.
WENGINE NI 5. STANLEY ZACHARIA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA 25
HADI 30, 6. SIA DAUSON MIAKA 28, 7. HELLEN LEHEKE ANAYEKADIRIWA KUWA
NA UMRI KATI YA MIAKA 30 HADI 35, 8. MICHAEL LEONARD MIAKA KATI YA 30
HADI 35, 9. KUDRA IBRAHIM MTOTO WA MIAKA MIWILI NA MIEZI SITA, 10.
ZAMDA ISSA MIAKA 24, 11. MARIETHA CHRISPHER MIAKA 26, 12. ELIZABERTH
SIMON MIAKA 40 NA 13. DICKSON MSAMBA MIAKA 22, MAJERUHI WOTE
WANAENDELEA NA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
INADAIWA KUWA DEREVA WA GARI HILO ALIKUWA KWENYE MWENDO KASI, HALI
ILIYOPELEKEA KUGONGA JIWE LILILOKUWA BARABARANI NA KUSABABISHA DEREVA
KUSHINDWA KULIMUDU BASI HILO NA KUPELEKEA KUSEREREKA NA KUANGUKA NA
KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA WILAYA YA MISUNGWI KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI. JESHI LA POLISI
BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA AJALI HIYO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA


POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO KUWA
MAKINI WAKATI WOTE PINDI WANAPOKUWA BARABARANI, LAKINI PIA KUACHA
KUENDESHA MAGARI KWA MWENDO KASI KWANI KUNAPELEKEA AJALI NA VIFO
VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.

KATIKA TUKIO LA PILI


MNAMO TAREHE 27.06.2016 MAJIRA YA SAA 12:00 JIONI KATIKA KITONGOJI CHA
MOHA KIJIJI CHA ILUNGU KATA YA NYIGOGO TARAFA YA ITUMBILI WILAYA YA MAGU
MKOANI MWANZA, MTOTO ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JULIAS LEONARD MIAKA
[7] MWANAFUNZI WA CHEKECHEA SHULE YA MSINGI ILUNGA ALIUAWA KWA
KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BABA YAKE WA KAMBO
AITWAYE LEONARD JOSEPH MIAKA [32] MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA
ILUNGA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALITUMWA NA BABA YAKE HUYO WA KAMBO KWENDA
KUCHUKUA BETRII YA SIMU ILIYOKUWA IMEPELEKWA KUCHAJIWA NDIPO
ALICHELEWA KURUDI NYUMBANI HALI ILIYOPELEKEA BABA YAKE HUYO KUWA NA
HASIRA NA KUAMUA KUMCHAPA HADI MTOTO HUYO AKAPOTEZA MAISHA.
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA AWALI NA DAKTARI NA
KUONEKANA UKIWA NA ALAMA ZA FIMBO HUKU MGUU WA KUSHOTO UKIONEKANA
KUVUJA DAMU KWA NDANI KUTOKANA NA ADHABU YA FIMBO HIZO, MTUHUMIWA
WA MAUAJI HAYO AMETOROKA BAADA YA KUONA AMEFANYA MAUAJI.
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA
NATUKIO HILO, HUKU MSAKO WA KUMSAKA NA KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA WA
MAUAJI TAJWA HAPO JUU UKIWA UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUTOA
USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI, KWA KUTOA TAARIFA ZA MTUHUMIWA WA
MAUAJI HAYA MAHALI ALIPO ILI AWEZWE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA
VYOMBO VYA SHERIA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE WENYE TABIA ZA AINA
KAMA HII.

IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

You might also like