Afya

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 77

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

WIZARA YA AFYA

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA RASHID


SEIF SULEIMAN KUHUSU MAKADIRIO NA MATUMIZI YA
WIZARA YA AFYA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016
KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR

JUNI, 2015

YALIYOMO
Mada

Ukurasa

1.0 UTANGULIZI ....................................................................................................................... 1


2.0 MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 .................................. 3
3. 0 MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA KWA MWAKA 2014/15 ................................................ 5
4.0. IDARA YA KINGA NA ELIMU YA AFYA........................................................................... 6
4.1 Kitengo cha Utoaji wa Huduma za Macho ................................................................. 6
4.2
Kitengo cha Lishe.......................................................................................................... 7
4.3 Kitengo cha Afya ya Mazingira ..................................................................................... 9
4.4
Kitengo cha Afya Bandarini ......................................................................................... 9
4.5
Kitengo cha Kupambana na Maradhi Yasiyoambukiza .......................................... 11
4.6
Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Maradhi ................................................ 12
4.7
Kitengo cha Afya ya Wafanyakazi ............................................................................ 14
4.8 Kitengo cha Kupambana na Maradhi ya Kichocho, Minyoo na
Matende ...... 15
4.9
Huduma za Afya Wilayani.......................................................................................... 16
5.0
IDARA YA TIBA ............................................................................................................... 19
6.0
IDARA YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA .................................................................. 21
6.1. Hospitali ya Mnazi Mmoja .......................................................................................... 21
6.2
Hospitali ya Wagonjwa wa Akili - Kidongo Chekundu........................................... 22
7.0 OFISI YA MFAMASIA MKUU WA SERIKALI .................................................................. 23
8.0
IDARA YA BOHARI KUU YA DAWA .............................................................................. 25
9.0
MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI .............................................................. 26
10.0
IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI ................................................................ 27
11.0
IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI ................................................................... 28
11.1
Nguvu kazi ya Sekta ya Afya ................................................................................. 29
12.0
TAASISI MAALUMU..................................................................................................... 30
12.1
Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya ................................................................ 30
12.2
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ..................................................................... 31
12.3
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ................................................................... 33
12.4
Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi ..................................................................... 34
13.0
MIRADI YA MAENDELEO ........................................................................................... 35
13.1
Programu ya Kumaliza Malaria Zanzibar ............................................................. 35
13.2
Mradi Shirikishi wa Afya ya Uzazi na Mtoto ....................................................... 38
13.3.
Mradi Shirikishi wa Maradhi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma .................. 41
13.4
Mradi wa Kustawisha Siha za Wazanzibari.......................................................... 42
13.5
Mradi wa Kuipandisha Hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja Kuwa ya Rufaa ... 45
13.6.
Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali za Wilaya na Vijiji ................................. 47
13.7.
Mradi wa Taaluma za Afya (Zanzibar Medical School) ...................................... 47
14.0
CHANGAMOTO ............................................................................................................ 48
15.0
MALENGO MAKUU YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA WA FEDHA
2015/2016 KUPITIA MFUMO WA
PROGRAMU (PBB) ...................................................... 49
16.0
MGAWANYO WA FEDHA KWA PROGRAMU ............................................................ 53
17.0
HITIMISHO .................................................................................................................. 54
VIAMBATISHO ............................................................................................................................. 58
i

MCHANGANUO WA VIFUPISHO
ARV

Anti Retroviral Drug

CHAI

Clinton Health Access Initiative

CHS

College of Health Sciences

DANIDA

Danish International Development Agency

HIPZ

Health Improvement Project Zanzibar

HIV

Human Immune Virus

ICAP

International Center for Aids Care Programme

ICU

Intensive care Unit

JICA

Japan International Cooperation Agency

JSI

John Snow Inc

KOICA

Korea International Corporation Agency

PMI

Presidents Malaria Initiative

SSI

Sight Savers International

UKIMWI

Ukosefu wa Kinga Mwilini

UNDP

United Nation Development Programme

UNFPA

United Nation Population Fund

UNICEF

United Nation International Children Emergency Fund

USAID

United State Agency for International Development

WHO

World Health Organization

ii

1.0 UTANGULIZI
1.0.1

Mheshimiwa Spika, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu


kutuwezesha kuwa na afya nzuri na kukutana tena mwaka huu
katika baraza lako hili na kuniwezesha kutoa hotuba yangu ya
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2015/2016.

1.0.2

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba sasa


Baraza hili likae kama Kamati ya matumizi ili liweze kupokea na
kujadili taarifa ya utekelezaji wa kazi za Wizara ya Afya kwa
mwaka 2014/15. Aidha, naliomba Baraza lako likubali kupitisha
makadirio ya matumizi ya kawaida na kazi za maendeleo ya
wizara kwa mwaka 2015/16.

1.0.3

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima namshukuru


kwa dhati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kutuongoza
na kutoa maelekezo ambayo yametuwezesha kutoa huduma
bora za afya kwa jamii.

1.0.4

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza


kwa dhati Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Maalim
Seif Sharif Hamad kwa uongozi wake na maelekezo yake
ambayo yamenisaidia sana kuongeza ufanisi katika utendaji na
kuimarisha huduma za afya kwa wananchi. Aidha, naomba
1

nimpongeze Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ali


Iddi kwa kusimamia utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika
mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Pia nachukua fursa hii
kumpongeza kutokana na maelezo aliyoyatoa kwenye hotuba
yake

ambayo

imeonesha

jinsi

serikali

itakavyotekeleza

majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2015/16.


1.0.5

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kutoa pole kwa


wananchi wote walioathirika kwa njia moja au nyengine
kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni katika visiwa vya
Unguja na Pemba hususan katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Namuomba

Mwenyezi

Mungu

awape

subira

kwa

wale

waliopoteza jamaa zao pamoja na walioharibikiwa na mali zao.


1.0.6

Mheshimiwa Spika, kutokana na juhudi kubwa za serikali


kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo pamoja na sekta
binafsi na wadau wengine, sekta ya afya imepata mafanikio
mengi kwa mwaka wa fedha unaomalizika. Pamoja na
mafanikio hayo bado zipo changamoto nyingi zinazoikabili
sekta hii katika kuwahudumia wananchi.

1.0.7

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu baraza lako adhimu


kwamba kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 malengo ya
Wizara ya Afya yatatekelezwa kwa njia ya programu ambapo
sekta ya afya itakuwa na programu kuu tatu nazo ni;
2

Programu ya Usimamizi wa Sera na Utawala, Programu ya


Huduma za Kinga na Elimu ya Afya na Programu ya Huduma
za Tiba. Kwa upande wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja
nayo imepangiwa kutekeleza programu kuu mbili nazo ni;
Programu ya Huduma za Uchunguzi na Matibabu na Programu
ya Uongozi na Utawala.
1.0.8

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo sasa naomba


uniruhusu nitoe maelezo ya utekelezaji wa kazi za Wizara ya
Afya kwa mwaka 2014/2015.

2.0 MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015


2.0.1.
Mheshimiwa Spika, wizara ina jukumu la kuchangia mfuko
mkuu wa serikali kutokana na vyanzo mbali mbali vya mapato
vilivyomo ndani ya taasisi hii. Kwa mwaka wa fedha 2014/2015,
wizara ilipangiwa kuchangia jumla Tsh. 124,000,000, hadi
kufikia Machi, 2015, jumla ya Tsh. 108,194,500 (87%)
zimekusanywa. Kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Wizara ya
Afya imepangiwa kuchangia jumla Tsh. 168,738,000 katika
mfuko mkuu wa serikali. Kwa upande wa mapato ya Hospitali
ya Mnazi Mmoja kwa mwaka wa fedha 2014/2015, idara
ilipangiwa kukusanya jumla ya Tsh. 550,000,000 hadi kufikia
machi,

2015

jumla

ya

zimekusanywa.

Tsh.

582,641,363

(106%)

2.1

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/2015 wizara ilipangiwa


kutumia jumla ya Tsh. 50,954,097,000 kati ya hizo Tsh.
26,597,200,000 kutoka Serikalini na Tsh. 24,356,897,000
kutoka kwa washirika wa maendeleo. Kati ya fedha kutoka
Serikalini Tsh. 7,253,200,000 zimepangwa kwa kazi za
kawaida, Tsh. 14,274,800,000 kwa ajili ya mishahara na
maposho,

Tsh.1,219,200,000

ni

ruzuku

na

Tsh.

3,850,000,000 kwa kazi za maendeleo.


2.2

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2015, jumla ya Tsh.


4,049,763,501.95 ziliingizwa sawa asilimia 56 ya bajeti ya
fedha za matumizi ya kawaida na Tsh. 11,370,792,819 sawa
na asilimia 80 ziliingizwa kwa ajili ya mishahara na maposho.
Kwa upande wa ruzuku Tsh. 471,089,581 ziliingizwa sawa na
asilimia 39. Aidha, Tsh.2,367,822,000 sawa na asilimia 62,
ziliingizwa kutoka Serikalini na Tsh.1,252,884,320 sawa na
asilimia 5.1 kutoka kwa washirika mbali mbali kwa ajili ya kazi
za maendeleo.

2.3

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Idara


ya

Hospitali

ya

Mnazi

Mmoja

iliidhinishiwa

Tsh.1,478,000,000 kwa kazi za kawaida

jumla

ambapo

ya
hadi

kufikia Machi, 2015 Tsh. 900,000,000 ziliingizwa sawa na


asilimia 61. Aidha, jumla ya Tsh.6,804,000,000 ziliidhinishwa

kwa mishahara hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya Tsh.


4,936,876,650 sawa na asilimia 73 zimetumika.
3. 0 MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA KWA MWAKA 2014/15
3.1

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015


miongoni

mwa

mafanikio

yaliyopatikana

ni

kama

haya

yafuatayo:1. Kuendelea kudhibiti kiwango cha malaria na VVU/UKIMWI


chini ya asilimia moja.
2. Kuongezeka

kwa

asilimia

ya

wanaojifungua katika vituo vya afya

mama

wajawazito

kutoka asilimia 56.1

mwaka 2013 kufikia asilimia 68.3 mwaka 2014 .


3. Kukamilisha kampeni ya chanjo ya kitaifa ya Surua Rubella
kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15 ambapo
kiwango cha chanjo kimefikia asilimia 96.8 ya walengwa.
4. Kukamilika kwa ujenzi na kuanza kazi kwa jengo jipya la
utoaji wa huduma za upasuaji wa maradhi ya mgongo na
ubongo (neurosurgical services).

5. Kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU)


katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
6. Kukamilika ujenzi wa majengo mapya ya maabara katika
hospitali za Wete, Chake Chake na Micheweni.
5

7. Kuanza kwa ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee


8. Kutiwa saini mkataba wa ujenzi wa hospitali ya Binguni
4.0.

IDARA YA KINGA NA ELIMU YA AFYA

4.0.1

Mheshimiwa Spika, idara hii ina jukumu la kusimamia utoaji


wa huduma za kinga na elimu ya afya kwa jamii ili kuepukana
na maradhi mbali mbali yakiwemo ya miripuko, maradhi ya
kuambukiza na yasiyoambukiza. Idara hii hutekeleza majukumu
yake kupitia miradi mbali mbali, vitengo, timu za afya za wilaya
na timu za afya za kanda.

4.1 Kitengo cha Utoaji wa Huduma za Macho


4.1.1

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la kitengo hiki ni kupunguza


upofu unaoweza kuzuilika kwa kufuata muongozo wa Dira ya
2020 (Vision 2020) kutoka 0.4% hadi kufikia 0.3%.

4.1.2

Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Kitengo cha


Negleted Tropical Desease kitengo kilitoa mafunzo ya msingi
ya utambuzi wa maradhi ya Trachoma kwa wafanyakazi 55 wa
vituo vya Afya katika Wilaya ya Magharibi na Wilaya ya Mjini
pamoja na hospitali za Vijiji.

4.1.3

Mheshimiwa Spika, mafunzo ya uhamasishaji pia yalitolewa


kwa masheha 76 (45 Wilaya ya Mjini na 31 Wilaya ya
6

Magharibi). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa


utambuzi wa maradhi ya macho ili waweze kuwaelimisha na
kuwahamasisha wananchi katika shehia zao ikiwa ni pamoja na
kuvitumia ipasavyo vituo vya afya.
4.1.4

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 kitengo


pia kilifanya uchunguzi wa macho maskulini ambapo jumla ya
wanafunzi 5,964 (wanaume 2,901 na wanawake 3,063). Kati
ya hao 52 walionekana na matatizo mbali mbali ya macho na
kupatiwa matibabu waliostahiki.

4.1.5

Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa huduma ya macho


uliendelea kama kawaida katika vijiji mbali, ufafanuzi zaidi
unaonekana katika kiambatisho namba 1.

4.2

Kitengo cha Lishe

4.2.1

Mheshimiwa

Spika,

kitengo

hiki

kina

majukumu

ya

kusimamia, kufuatilia na kutathmini shughuli za lishe nchini.


Katika kutekeleza hayo shughuli mbali mbali zinaendelea
kufanywa ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya ulaji bora,
kupambana na ukosefu wa vitamini na madini, pamoja na
utekelezaji wa matibabu ya utapiamlo mkali hususan watoto
walio chini ya umri wa miaka mitano.

4.2.2

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Wizara kupitia


kitengo hiki ilitoa matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao hufanyika
mara mbili kwa mwaka. Mzunguko wa pili uliofanyika mwezi wa
Oktoba ulifanyika sambamba na kampeni ya kitaifa ya Surua
Rubela. Asilimia ya watoto waliopewa matone ya Vitamini A
katika kampeni hiyo ilifikia 98%. Aidha, asilimia ya watoto
waliopewa dawa za minyoo ilifikia 104%.

4.2.3

Mheshimiwa Spika, wizara ilifanya utafiti wa hali ya lishe ya


watoto chini ya umri wa miaka mitano. Matokeo ya utafiti huo
yameonesha kuwa hali ya udumavu wa watoto ni asilimia 24.4,
uzito pungufu asilimia 13.9 na ukondefu asilimia 7.2. Mikakati
inayoendelea katika kuhakisha hali ya lishe ya watoto
inaimarika ni pamoja na kutoa elimu juu ya unyonyeshaji bora,
kutoa matone ya vitamin A pamoja na kushajihisha matumizi ya
chumvi yenye madini joto kwenye kaya.

4.2.4

Mheshimiwa Spika, mafunzo juu ya umuhimu wa kuuza


chumvi

iliyowekewa

madini

joto

yalitolewa

kwa

wafanyabiashara wadogo wadogo 200 kutoka wilaya zote za


Pemba.

Sambamba na hilo ugawaji wa madini joto kwa

wakulima wa chumvi ulifanyika ambapo jumla ya kilo 200


zilikabidhiwa kwa wakulima hao.

4.3 Kitengo cha Afya ya Mazingira


4.3.1

Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Maabara ya Afya ya


Jamii (PHL), Water Aid, Soap Box Collaborative na SHARE
kitengo kilifanya utafiti wa Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi
katika vituo vinavyotoa huduma za kuzalisha. Lengo la utafiti
huo lilikuwa ni kuangalia upatikanaji wa maji, usafi na
mazingira kwa ujumla na kuangalia mtazamo wa wadau juu ya
masuala ya uzuiaji wa maambukizi.

4.3.2

Mheshimiwa Spika, uhamasishaji wa ujenzi wa karo na vyoo


vya gharama nafuu umefanyika katika Shehia 43 za Unguja na
Pemba. Aidha, ujenzi wa karo za maji machafu kwa familia 16
ulifanyika. Lengo kubwa ni kuwahamasisha wananchi kudhibiti
maji machafu ili kujikinga na maradhi mbali mbali ya kuharisha
hasa kwa watoto, kuweka mazingira safi sambamba na kutunza
vyanzo vya maji safi.

4.4

Kitengo cha Afya Bandarini

4.4.1

Mheshimiwa Spika, jukumu kubwa la kitengo hiki ni kuzuia


uingizwaji na usafirishwaji wa maradhi pamoja na wadudu
wasababishao maradhi kuingia au kutoka nje ya nchi.

4.4.2

Mheshimiwa Spika, kitengo kiliendelea na kazi ya utoaji wa


chanjo kwa wasafiri wa kimataifa.

Jumla ya wasafiri 1,052

wamepatiwa chanjo hiyo ikilinganishwa na wasafiri 814


waliochanjwa mwaka 2013/14.

Sambamba na hilo kitengo

kilichapisha kadi za chanjo za kisasa 1,460. Katika hatua


nyengine kitengo kilikagua jumla ya wasafiri 1,043,523 kupitia
bandarini na uwanja wa ndege ambapo wasafiri 190 walitokea
nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na kufanyiwa ufuatiliaji
wa ziada wakati wote walipokuwapo nchini. Aidha, jumla ya
vyombo 1,269 vikiwemo meli kubwa 99, boti 1,085, jahazi
125 vilikaguliwa.
4.4.3

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/15 kitengo


kiliendelea na kazi ya ukaguzi wa wageni wanaoingia nchini.
Jumla wageni waliokaguliwa walikuwa 70,601. Kati yao
38,674 hawakuwa na kadi za chanjo ya homa ya manjano,
ambapo wasafiri 31,718 walitokea maeneo yasiyo hatarishi na
168 walikuwa na sababu za kiafya. Wageni 41 walichanjwa
hapa hapa nchini.

4.4.4

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za afya


bandarini na uwanja wa ndege kitengo kilitoa mafunzo kwa
wafanyakazi 34 wa afya bandarini na uwanja wa ndege
kuhusiana na kazi zao.

10

4.5

Kitengo cha Kupambana na Maradhi Yasiyoambukiza

4.5.1

Mheshimiwa Spika, kitengo hiki kilifanya utafiti uliolenga


kupima uelewa na mitazamo ya wafanyakazi pamoja na jamii
juu ya magonjwa yasiyoambukiza. Matokeo ya awali ya utafiti
huo

yanaonesha

waliohojiwa

kuwa

asilimia

hawakuwahi

yanayohusiana

na

26.5

kupata

magonjwa

ya

wafanyakazi

mafunzo

yasiyoambukiza.

yoyote
Kati

ya

waliowahi kupata mafunzo asilimia 30.8 waliwahi kufundishwa


kuhusu saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 34.6
walifundishwa juu ya saratani ya matiti. Aidha, ilibainika
kwamba asilimia 50 ya wafanyakazi wanao uwezo wa
kuwahudumia wagonjwa wa kisukari na shindikizo la damu.
4.5.2

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa jamii, asilimia 73.4 ya


watu waliohojiwa wanajua kama magonjwa yasiyoambukiza
hayawezi kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwengine, wakati asilimia 15 walisema magonjwa hayo
yanaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwengine

na

asilimia

11.6

hawajui

kama

yanaweza

kuambukizwa au la.
4.5.3

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma za maradhi


yasioambukiza zinaimarika katika ngazi za msingi, wizara
imenunua na kusambaza vifaa vya kufanyia uchunguzi wa
magonjwa ya kisukari, shindikizo la damu na pumu katika vituo
11

vya afya. Kazi hii ilifuatiwa na mafunzo kwa wafanyakazi 144


kutoka katika hospitali ya Mnazi Mmoja, hospitali tatu za wilaya,
hospitali nne za vijiji pamoja na vituo 37 vya ngazi ya msingi.
Kufuatia kukamilika kwa mafunzo haya, wizara imeweza
kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma hizo kutoka vituo
vitatu hadi 26 kwa Unguja na kutoka vituo vitano hadi kufikia
19 kwa Pemba.
4.5.4

Mheshimiwa Spika, katika hatua nyengine ya kuimarisha


huduma hizo, wizara ilinunua vifaa kwa ajili ya uchunguzi wa
macho kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wagonjwa wa
maradhi ya kisukari na shindikizo la damu ambao mara nyingi
hupata taathira hii. Ununuzi huo ulifuatiwa na mafunzo kwa
wafanyakazi na baadae vifaa hivyo kusambazwa katika vituo
vya afya vikiwemo Chumbuni, Mpendae,

Bumbwini Misufini,

Mwera, Uzini, Donge, Fuoni na Chwaka kwa Unguja na kwa


upande wa Pemba ni hospitali ya Wete, Micheweni na vituo vya
afya vya Makangale, Konde, Pujini, Bogoa na Kojani.

4.6

Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Maradhi

4.6.1

Mheshimiwa Spika,

jukumu la kitengo hiki ni kuratibu,

kufuatilia miendendo ya maradhi, kutafuta vyanzo na vichocheo


vya maradhi pamoja na kuchukua hatua za kukabiliana na
maradhi pamoja na majanga mengine yanayotokea katika
jamii.
12

4.6.2

Mheshimiwa Spika, katika kujitayarisha na kujikinga na


ugonjwa wa Ebola wizara imekuwa ikichukuwa hatua mbali
mbali katika kukabiliana na ugonjwa huu pindi ukitokea. Hatua
hizo zilijumuisha kuunda kamati maalumu ya kitaifa pamoja na
kamati maalumu ya ufuatiliaji ya wizara, mafunzo kwa
wafanyakazi wa afya, na utoaji wa elimu ya afya kwa jamii
kupitia njia tofauti zikiwemo vyombo vya habari, vipeperushi,
midahalo, filamu na nyenginezo.

4.6.3

Mheshimiwa

Spika,

wizara

kupitia

Shirika

la

Afya

Ulimwenguni imenunua vifaa vya kujikinga na maradhi hayo.


Aidha, ufuatiliaji maalumu kwa wageni wote wanaoingia nchini
kupitia viwanja vya ndege na bandarini pamoja na upulizaji wa
dawa unafanyika (disinfection) katika maeneo ya kusubiri abiria
na sehemu za mizigo.
4.6.4

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, wizara imefanya


mawasiliano na taasisi za uchunguzi wa tafiti za afya za
National Medical Research (NMR) ya Tanzania Bara na Kenya
Medical

Research

kimaabara.

(KEMR)

Imekubalika

kuhusiana

kwamba

na

sampuli

uchunguzi
za

damu

wa
za

washukiwa zitasafirishwa huko kwa uchunguzi kwa utaratibu


maalumu

kama

Ulimwenguni.

ilivyopendekezwa

Aidha,

wizara

na

inaendelea

Shirika
na

la

jitihada

Afya
za

kuzipandisha daraja maabara zetu za Mnazi Mmoja na Maabara


13

ya Afya ya Jamii Pemba ili ziweze kutumika kwa uchunguzi wa


awali wa maradhi haya. Aidha , maeneo ya Vitongoji kwa
Pemba na Fuoni Kibondeni kwa Unguja yametengwa na
kuwekwa vifaa mbali mbali kwa ajili ya matibabu ya washukiwa
wa ugonjwa wa Ebola pindipo wakitokea.

4.6.5

Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na


Uvuvi wizara imeweza kupokea taarifa za kuwepo kichaa cha
mbwa katika sehemu mbali mbali za Unguja. Jumla ya watu 23
waliripotiwa kutafunwa na mbwa hao kati ya hao wagonjwa
wanne walitokea Wilaya ya Magharibi, 11 wilaya ya Mjini,
mmoja wilaya ya Kaskazini A na saba kutoka Wilaya ya Kati.
Maeneo yalioathirika zaidi ni Fuoni, Maungani, Kianga, Bomani,
Mkunazini, Mwembeladu, Kwahajitumbo, Kijangwani, Hurumzi,
Shangani, Nungwi, Mwera na Chuini. Kufuatia kuripotiwa kwa
kesi hizo elimu ya afya ilitolewa na kupatiwa chanjo kwa wale
walioathirika na kusisitizwa kumaliza sindano zote za matibabu
hayo.

4.7

Kitengo cha Afya ya Wafanyakazi

4.7.1

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/15 jumla ya


watu 6,499 waliifanyiwa uchunguzi wa afya zao. Wafanyakazi
hawa walijumuisha wafanyakazi wa Hoteli, Mikahawa na
Nyumba za kulala wageni (4,185), wafanyakazi wa Viwanda
14

(117), wauza vyakula (126) na wafanyakazi wa maduka ya


nyama (143). Halikadhalika jumla ya wafanyakazi wapya wa
serikali, waajiriwa na wanafunzi wanaokwenda masomoni
(889) na wafanyakazi wa kampuni binafsi na mashirika ya
umma (1,039) pia walifanyiwa uchunguzi huo.
4.7.2

Mheshimiwa Spika, kitengo pia kiliendelea kutoa elimu ya


afya kwa jamii kwa kupitia redio, hasa wafanyakazi wa vituo
vya Petroli kuhusu athari na madhara yanayoweza kusabishwa
na mafuta.

Aidha, elimu ya afya hutolewa kwa wote

wanaogunduliwa na matatizo ya uchunguzi wa afya zao.

4.8 Kitengo cha Kupambana na Maradhi ya Kichocho, Minyoo na


Matende
4.8.1

Mheshimiwa Spika, kitengo hiki kinaendelea kutoa huduma


za

uchunguzi

na

matibabu

kwa

wagonjwa

wote

wanaosumbuliwa na Maradhi ya Kichocho na Minyoo. Katika


kipindi cha Januari hadi Disemba 2014, jumla ya watu 3,952
walichunguzwa, kati yao 1,646 (41%) waligunduliwa na
maradhi (Unguja 1,292 na Pemba 354).
4.8.2

Mheshimiwa Spika, kitengo kilifanikiwa kufanya ukaguzi


katika mito na maziwa 40 katika wilaya tano za Unguja kwa
lengo la kuangalia makonokono wenye uwezo wa kusambaza
15

maradhi

ya

Kichocho.

Baada

ya

ukaguzi

huo

maeneo

yaliyobainika kuwa na makonokono yalinyunyiziwa dawa kwa


ajili ya kuwaangamiza.
4.8.3

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba maradhi ya


Kichocho yanatoweka ifikapo mwaka 2016 na kupunguza
maambukizo ya maradhi ya minyoo, ulishaji wa dawa kwa
lengo la kutibu na kupunguza maambukizo mapya ya maradhi
haya ulifanyika.

Jumla ya walengwa 1,093,004 walitarajiwa

kula dawa, kati yao watu 915,954 (84%) walipatiwa dawa hizo.
4.8.4

Mheshimiwa Spika, katika kuelimisha jamii juu ya mabadiliko


ya tabia kitengo kimetoa mafunzo ya kurekebisha tabia katika
shehia 30 (15 za Unguja na 15 za Pemba) pamoja na madrasa
zote zilizomo katika shehia hizo. Aidha, jumla ya mafulio 60
(30 kwa Unguja na 30 kwa Pemba) yamejengwa kwenye
maeneo yenye maambukizi ya maradhi ya Kichocho.

4.9

Huduma za Afya Wilayani

4.9.1

Mheshimiwa Spika, huduma za afya wilayani zinatolewa


kupitia timu za afya za wilaya zilizopo Unguja na Pemba.

4.9.2

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/15 timu za


afya za wilaya zilipata mafanikio makubwa, mafanikio hayo ni
pamoja na kuchimba kisima kwa ajili ya kituo cha afya cha
16

Mpendae, kuipatia umeme nyumba ya madaktari Tumbatu


Gomani na kituo cha afya cha Jendele, Machui na Ukunjwi
sambamba na ulipaji wa madeni ya umeme kwa vituo vya afya
vya Kiboje, Uroa, Mwera, Uzi, Tunguu na Pongwe pwani.
4.9.3

Mheshimiwa

Spika,

shughuli

nyengine

zilizofanyika

ni

uwekaji wa matanki ya maji katika nyumba za madaktari


Tumbatu, kituo cha afya cha Miwani na Kojani. Wakati huo huo
matengenezo madogo madogo yalifanyika kwa nyumba za
madaktari Kojani, kituo cha afya cha Dunga, Jendele, Cheju,
Pandani, Mokongeni, Junguni, Tundauwa, Shungi, Mgelema,
Ziwani, Mvumoni na Kinyasini Pemba.
4.9.4

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma za afya


zinawafikiwa wananchi, timu za afya za wilaya zinaendelea
kutoa huduma za mkoba outreach services katika vijiji vilivyo
mbali na vituo vya afya. Lengo la utoaji wa huduma hizi ni
kugundua na kutoa matibabu ya maradhi yanayowakabili
wananchi wa maeneo hayo. Aidha, rufaa ilitolewa kwa wale
walioonekana na dalili za saratani ya matiti na ile ya shingo ya
kizazi.

4.9.5

Mheshimiwa Spika, elimu ya afya kwa jamii imeendelea


kutolewa dhidi ya kinga ya maradhi mbali mbali kuhusiana na
utumiaji wa huduma za afya ya macho, kinywa na meno,
17

umuhimu wa chanjo ya pepopunda kwa wanawake wenye umri


wa kuzaa, kampeni ya Surua Rubella, pamoja na uhamasishaji
jamii katika kuweka usafi wa mwili na mazingira. Elimu ya afya
ilitolewa katika skuli za Mahonda, Kinduni na Kitope na jumla ya
wanafunzi 183 walihudumiwa.
4.9.6

Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa maradhi mbali mbali


ulifanyika katika siku za maadhimisho ya siku za afya za kijiji,
katika maadhimisho hayo, jumla ya watu 1,232 walichunguzwa
maradhi ya sukari na sindikizo la damu na waliobainika
walipatiwa matibabu.

4.9.7

Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa masikio, pua na koo katika


skuli tano na uchunguzi wa kinywa katika skuli 10 za
maandalizi na msingi ulifanyika. Jumla ya wanafunzi 1,341
walichunguzwa masikio, pua na koo, kati yao 352 walitibiwa
kwa

mujibu

wamefanyiwa

wa

matatizo

uchunguzi

yao.
wa

Pia

kinywa

wanafunzi
kati

yao

2,106
487

waligunduliwa na matatizo mbali mbali na kupatiwa matibabu.


4.9.8

Mheshimiwa Spika, wanafunzi 346 wamepatiwa elimu ya


afya juu ya maradhi ya kuharisha na UKIMWI. Aidha wanafunzi
150 walifanyiwa uchunguzi wa meno na macho, kati yao 12
waligundulika kuwa na matatizo hayo, walipewa rufaa kwenda
Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu.
18

5.0

IDARA YA TIBA

5.1.1

Mheshimiwa Spika, Idara ya Tiba inasimamia huduma


zinazotolewa katika hospitali ya Chake Chake, Abdalla Mzee,
Wete, Micheweni, Vitongoji, Makunduchi na Kivunge. Idara hii
pia inasimamia Mpango wa Damu Salama, huduma za
uchunguzi pamoja na usafirishaji wa wagonjwa nje ya nchi.
Taarifa za mahudhurio ya wagonjwa wa nje, waliolazwa na
wazazi waliojifungua zinaonekana katika kiambatisho namba
2 na 3.

5.1.2

Mheshimiwa Spika, huduma za matibabu katika kliniki


maalum zimeendelea kutolewa katika klinki za kisukari,
shindikizo la damu, macho, pua, masikio na koo, kifua kikuu
pamoja na magonjwa ya wanawake. Ufafanuzi wa taarifa za
wagonjwa unapatikana katika kiambatisho namba 4.

5.1.3

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2014 hadi Machi


2015, jumla ya wagonjwa 206 walifanyiwa uhakiki na Bodi ya
Madaktari

kati

ya

hao

wagonjwa

156

walithibitishwa

kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi. Jumla ya Tshs.


3,231,526,142.40 zilitumika kwa ajili ya usafirishaji na
matibabu ya wagonjwa hao, idadi hii ya fedha ni kubwa
ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha
2014/15 ambazo zilikuwa ni Tsh. 800,000,000

19

5.1.4

Mheshimiwa Spika, damu salama ni muhimu katika kuhuisha


afya za wananchi. Mpango wa Damu Salama una lengo la
kuhakikisha upatikanaji wa damu salama na ya kutosha kutoka
kwa wachangiaji wa hiari. Damu salama inayokusanywa katika
hurahisisha upatikanaji wa damu katika hospitali zote zinazotoa
tiba ya damu.

5.1.5

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha July 2014 hadi Machi


2015, mpango huu umefanikiwa kukusanya jumla ya uniti za
damu 5,931 (59.3%), lengo la mwaka lilikuwa ni kukusanya
uniti za damu 10,000 kutoka kwa wachangiaji wa hiari.
Kiwango hicho cha makusanyo hayo yamechangiwa na
uhamasishaji uliofanywa katika vikundi mbali mbali vya jamii
vikiwemo vilabu vya mipira na sanaa, skuli mbalimbali, vyuo,
mikusanyiko ya kidini na vikosi vya ulinzi. Hadi sasa kuna vilabu
vya uchangiaji damu Donor clubs vya kijamii vipatavyo 70
kwa Unguja na Pemba.

5.1.6

Mheshimiwa Spika, kumbukumbu za wataalamu wa huduma


za uchunguzi zimeanza kukusanywa na kurikodiwa katika ngazi
ya wilaya. Aidha, mafunzo kwa wataalamu wa maabara juu ya
ubora wa vipimo wa kufikia viwango "Quality Management
System yametolewa kwa wataalamu 25 na mafunzo ya
ufuatiliaji wa maradhi yanayopaswa kuchukuliwa hatua za

20

haraka

"integrated

disease

surveillance

and

response"

yametolewa kwa wataalamu wa maabara 27 Unguja na Pemba.

6.0

IDARA YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

6.0.1

Mheshimiwa Spika, jukumu muhimu la Idara ya Hospitali ya


Mnazi Mmoja ni kutoa huduma za uchunguzi, rufaa na
matibabu kwa wagonjwa na kutoa mafunzo ya vitendo kwa
wanafunzi wa kada mbali mbali za afya wanaotoka katika vyuo
vya ndani na nje ya nchi, idara hii inajumuisha Hospitali ya
Mnazi Mmoja, Mwembeladu na Hospitali ya wagonjwa wa Akili
ya Kidongo Chekundu.

6.1.

Hospitali ya Mnazi Mmoja

6.1.1

Mheshimiwa Spika, ili kukidhi mahitaji ya wataalamu mbali


mbali katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa, wizara
imewapeleka masomoni madaktari wawili kwa shahada ya tatu
na madaktari saba kwa ajili ya masomo ya shahada ya pili
(specialization), ili wawe madaktari bingwa katika mionzi
(radiology), matibabu ya macho, mifupa, meno, pua, masikio
na koo, maradhi ya akili na upasuaji wa matatizo ya watoto. Ni
mategemeo yetu kuwa kurudi kwa wataalamu hawa kutasaidia
kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma katika hospitali hii na pia
kupunguzia mzigo serikali kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.
21

6.1.2

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma zinakuwa za


kisasa zaidi vifaa vya mtambo na mfumo wa kusambazia
oxygen, hewa na vacuum katika wodi ya wagonjwa mahututi,
chumba cha upasuaji, chumba cha huduma ya dharura na wodi
ya wazazi tayari vimeshafungwa na kuanza kutumika.

6.1.3

Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza azma ya hospitali hii


kuwa na hadhi ya kujitegemea, hospitali ya Mnazi Mmoja
imepatiwa vifaa vipya kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi ya
mfumo wa chakula (gastro-intestinal system) kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China, vifaa hivi vinatuwezesha kugundua
na kutibu maradhi ya vidonda vya tumbo, uvimbe, saratani za
mfumo wa chakula, uchunguzi wa kifua kikuu, upasuaji na
matibabu ya meno. Vile vile ukarabati wa wodi ya mifupa,
wodi ya ICU yenye vitanda 8 pamoja na kuwekewa vifaa vya
kisasa umekamilika na wodi hiyo tayari imeshaanza kazi.

6.1.4

Mheshimwa Spika, Takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa


nje, waliolazwa, kliniki maalumu na waliojifungua katika
Hospitali ya Mwembeladu na Mnazi Mmoja zinaonekana katika
viambatisho namba 5, 6 na 7.

6.2

Hospitali ya Wagonjwa wa Akili - Kidongo Chekundu

6.2.1

Mheshimiwa Spika, Hospitali hii ni hospitali pekee ya rufaa


kwa wagonjwa wa akili hapa Zanzibar. Kuanzia Julai, 2014 hadi
Machi, 2015, mahudhurio ya wagonjwa wa nje yalikuwa ni
22

7,678 (wanaume 3,684 na wanawake 3,994). Aidha,


wagonjwa waliolazwa walikuwa ni 631 kati yao wanaume 350
wanawake 281, wagonjwa watatu wamefariki.
6.2.2

Mheshimiwa Spika, huduma za afya ya akili zimeanza kutoa


matibabu kwa watumiaji wa dawa za kulevya husan kwa wale
wanaojidunga heroin kwa kutumia dawa ya methedone, tokea
tarehe 2/2/2015. Hadi kufikia tarehe 11/5/2015 jumla ya vijana
78 (wavulana 68 na wasichana 10) wanaendelea na huduma
hiyo ikiwa ni mwendelezo wa Serikali kuwanusuru vijana
kurejesha nguvukazi ya taifa.

7.0 OFISI YA MFAMASIA MKUU WA SERIKALI


7.1

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mfamasia Mkuu wa Serikali ina


jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu, vifaa tiba,
vitendanishi (reagents) pamoja na kusimamia matumizi sahihi
ya dawa. Katika kulifikia lengo hili, Ofisi hii imepewa dhamana
ya kufanya tathmini ya dawa (quantification) pamoja na
kuratibu ununuzi wa dawa na vifaa, kufanya ukaguzi kwenye
hospitali na vituo vyote vya afya vya serikali kuhakikisha
utunzaji bora na utumiaji sahihi wa dawa. Pia inajukumu la
kusimamia sera ya dawa nchini (National Medicine Policy).

23

7.2

Mheshimiwa Spika,

wizara inaendelea

kutumia mfuko

maalum wa dawa (Essential Medicine Account), ambapo


ununuzi wa dawa unatumia utaratibu wa Mkataba maalum
yaani Framework Contract.
7.3

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara


iliendelea kununua dawa na vifaa tiba kwa kutumia fedha za
Serikali, pamoja na Washirika wa Maendeleo. Kwa upande wa
Serikali jumla ya Tsh. 2,800,000,000 zilitengwa, hadi kufikia
Machi 2015, TSh.1,368,325,561 (49%) zimepatikana. Pia
Wizara imepokea dawa na vifaa tiba kutoka kwa Washirika wa
Maendeleo

vyenye

thamani

ya

Tsh.2,603,135,438.

Kiambatisho namba 8. kinatoa ufafanuzi.


7.4

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha dawa zinasimamiwa


na kufanyiwa ukaguzi unaofaa wizara imeweza kupokea pikipiki
kumi kwa ufadhili wa JSI, ambazo zimegharimu jumla ya TSh.
44,940,000/= kwa ajili ya ukaguzi katika hospitali na vituo
vya

afya.

Pikipiki

hizo

tayari

wamekabidhiwa

maafisa

wasimamizi wa wilaya wa dawa (District Material Managers)


wote Unguja na Pemba.
7.5

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mfamasia Mkuu inaendelea na


mchakato wa kuanzisha kitengo cha uratibu wa usimamizi wa
dawa (Logistic Management Unit). Kitengo hiki kitaangalia na
24

kusimamia mwenendo mzima wa dawa ikiwemo ukusanyaji wa


taarifa za dawa (End Use Verification) pamoja na kuanzishwa
mfumo wa kielektroniki wa kuweka kumbukumbu pamoja na
uagizaji wa dawa kwa Hospitali na Vituo vya Afya (Electronic
Logistic Management Information System - eLMIS). Mfumo huu
utasaidia upatikanaji wa dawa taarifa za matumizi pamoja na
kupunguza utumiaji mbaya wa dawa.

8.0

IDARA YA BOHARI KUU YA DAWA

8.1

Mheshimiwa Spika, Idara ya Bohari Kuu ya Dawa ina jukumu


la kupokea, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba katika
hospitali na vituo vyote vya afya vya Serikali.

8.2

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za usambazaji


dawa na vifaa tiba idara inaendelea kuimarisha mfumo wa
uagizaji wa dawa kwa njia ya kielektroniki hatua kwa hatua.
Jumla ya watendaji 141 wamepatiwa mafunzo hayo na
yanaendelea kutolewa kwa mujibu wa mahitaji, upatikanaji wa
dawa muhimu uliimarika kutoka asilimia 50 mwaka 2012/2013
hadi asilimia 63 katika kipindi cha Julai hadi Machi, 2014/2015.

8.3

Mheshimiwa Spika, Bohari Kuu ya Dawa inaendelea na


mchakato wa kuandaa rasimu ya sheria itakayoifanya idara hii
kuwa ni yenye kujitegemea (Semi- Autonomous).
25

9.0

MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

9.1

Mheshimiwa Spika, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ina


jukumu la kutoa huduma za kitaalamu na

kisayansi kwa

kuangalia ubora na usalama wa vyakula na dawa, udhibiti wa


kemikali na usalama wa mazingira, kufanya uchunguzi wa
vinasaba na vielelezo vinavyowasilishwa kutoka taasisi za
serikali na watu binafsi vikiwemo vile vinavyohusiana na
makosa ya jinai. Aidha, Maabara inajukumu la kufanya tafiti
zinazohusiana na kazi za maabara.
9.2

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Machi


2015, Maabara imefanya uchunguzi wa vielelezo 590, kama
inavyoonekana kwenye kiambatisho namba 9.

9.3

Mheshimiwa Spika, uandaaji wa michoro na gharama za


ukarabati

na

utanuzi

wa

majengo

mawili

ya

maabara

umekamilika. Aidha, matayarisho ya kupata eneo la ujenzi wa


maabara kwa upande wa Pemba yanaendelean. Katika hatua
nyengine Kanuni ya udhibiti wa kemikali imeshakamilika na
inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni.

26

10.0

IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

10.1

Mheshimiwa Spika, Idara ina majukumu ya kutayarisha


Sera, miongozo

na mipango mikuu ya wizara pamoja na

kusimamia na kutathimini utekelezaji wake ikiwemo kufuatilia


ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa za afya.
10.2

Mheshimiwa Spika, matayarisho ya uanzishwaji wa mfuko


wa bima ya afya ikiwa ni miongoni mwa vyanzo mbadala
umefikia hatua nzuri baada ya mshauri muelekezi kuanza kazi
ya kufanya tathmini ya mfuko huo. Hatua iliyofikiwa hadi sasa
ni kufanya utafiti utakaotumia takwimu ya idadi ya watu
pamoja na hali ya wananchi kimapato (Actuarial Study), utafiti
huo utasaidia wizara pamoja na serikali kufanya maamuzi sahihi
ya uendeshaji mzima wa mfuko wa Bima ya Afya. Ripoti ya
awali inategemewa kuwasilishwa serikalini hivi karibuni.

10.3

Mheshimiwa Spika, mpango wa ufuatiliaji na tathmini wa


wizara umetayarishwa na kukamilika, kabla ya kuanza kazi hii,
tathmini ya kina ya
tathmini

kuangalia hali halisi ya ufuatiliaji na

ilivyo ndani ya wizara ilifanywa, Ripoti ya tathmini

hiyo imekamilika na ndiyo iliyotumika katika kutayarisha


mpango huu. Mpango huu utaisaidia wizara kusimamia
utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano.

27

10.4

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2015 Idara kupitia


kamati ya kusimamia maadili ya tafiti za afya imefanikiwa
kuzipitia tafiti 10 na zote zilipewa maelekezo ya kuziimarisha
zaidi ili ziendane na maadili hayo.

10.5

Mheshimiwa Spika, azma kuu ya lengo la wizara ni kuzidi


kufikisha taarifa za afya kwa jamii ili waweze kuelewa
mwenendo halisi wa hali ya afya na kinga dhidi ya maradhi
mbali mbali. Katika kulisimamia hili wizara imeunda timu ya
wataalamu ya kusimamia utoaji wa taarifa za afya kwa jamii
kupitia kijarida maalumu ambacho kitatayarishwa kwa kila robo
mwaka. Tayari usajili wa kuchapisha kijarida hicho umefanyika
kupitia Idara ya Habari Maelezo.

11.0

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

11.0.1

Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi ina


dhima ya kusimamia uwajibikaji kazini, haki, maslahi, nidhamu,
stahiki za wafanyakazi pamoja na kujenga uwezo wa nguvukazi
ya afya ili kuongeza ufanisi. Aidha, idara hii inasimamia
masuala ya usafiri, utunzaji kumbukumbu za wafanyakazi na
miundombinu yote iliyomo ndani ya wizara.

28

11.1

Nguvu kazi ya Sekta ya Afya

11.1.1

Mheshimiwa

Spika,

kwa

ujumla

wafanyakazi

wote

wanaoendelea na masomo hadi sasa ni 343 ambapo jumla ya


wafanyakazi 62 wamerudi kutoka masomoni na kupangiwa kazi
katika sehemu tofauti. Katika kipindi cha Julai 2014 hadi Mei,
2015, jumla ya wafanyakazi 92 wa kada mbali mbali
wamepelekwa masomoni ndani na nje ya nchi. Kiambatisho
namba 10 kinatoa ufafanuzi zaidi.
11.1.2

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya


kimeanzisha masomo ya kujiendeleza kwa wafanyakazi wenye
cheti kwa muda mrefu na hawakupata nafasi ya kujiendeleza
kielimu katika fani zao. Hivi sasa jumla ya wanafunzi 192
wanaendelea na masomo yao mwaka wa kwanza na wa pili,
kati yao wanafunzi 11 wamedhaminiwa na AMREF.

11.1.3

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizara pia imeajiri


wafanyakazi 56 wa kada tofauti. Jumla ya wafanyakazi 153
(130 Unguja na 23 Pemba) wamestaafu kwa mujibu wa
Sheria. Vilevile wafanyakazi 9 wamefariki (5 Unguja na 4
Pemba).

11.1.4

Mheshimiwa Spika, ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya na


nyumba za wafanyakazi umefanyika katika maeneo mbali mbali
Unguja na Pemba. Maeneo hayo ni Fundo, Makangale, Wesha,
29

Ukutini na Mtangani kwa upande wa Pemba na Sebleni, Uzini,


Kombeni, Magogoni, Selem, Chumbuni, Unguja Ukuu na
Muyuni kwa Unguja.
11.1.5

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu baraza hili kwamba


wizara kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya MILELE
ZANZIBAR FOUNDATION wizara imeanza ujenzi kwenye vituo
vya afya vinne ambavyo ni Kinuni, Kiongwe, Bumbwi Sudi na
Ukongoroni.

11.1.6

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha utekelezaji wa Sheria


ya Afya ya Jamii ya mwaka 2012, kanuni mbali mbali
zimetengenezwa zikiwa ni pamoja na

viwango vya usafi na

afya ya mazingira, Umalizaji wa Maradhi ya Malaria, udhibiti wa


matumizi ya Tumbaku na kanuni nyenginezo zinazofanana na
hizo.

12.0

TAASISI MAALUMU

12.1

Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya

12.1.1

Mheshimiwa Spika, Chuo kinaendelea kutoa mafunzo ya


Taaluma za Sayansi za Afya katika fani mbali mbali. Hivi sasa
chuo kina idadi ya wanafunzi 872 wanaoendelea na masomo
yao wakiwemo uuguzi (198), Afya ya Mazingira (127), Ufundi
sanifu wa Maabara (128), Famasia (123), Afya ya Kinywa na
30

Meno (44), Afisa Tabibu (213), Ufundi wa Vifaa Tiba (18) na


Fiziotherapia (21).
12.1.2

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/2015 mwezi wa


Septemba Chuo kimechukua wanafunzi wapya 327. Aidha,
katika kipindi cha Julai, 2014 hadi Machi 2015, Chuo kimetoa
wahitimu 281 katika fani mbalimbali za Uuguzi (68), Waganga
Wasaidizi (51), Afya ya Mazingira (49), Famasia (48), Afya ya
Kinywa na Meno (13), Maabara (38) na Ufundi wa Vifaa Tiba
(13).

12.1.3

Mheshimiwa Spika, katika kukijengea uwezo wa kitaaluma


walimu wanne wamemaliza masomo ya muda mrefu, kati yao
watatu wamehitimu Shahada ya Uzamili na mmoja amehitimu
Shahada ya kwanza ya uuguzi. Aidha, walimu na wafanyakazi
21 wanaendelea na masomo yao (Shahada ya Uzamivu mmoja,
Shahada ya Uzamili saba na shahada ya kwanza 13).

12.1.4

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015, chuo


kimeweza kutayarisha mpango wa kujiendesha (Business Plan)
ambao utasaidia chuo kuongeza mapato yake ili
kujiendesha wenyewe.

12.2

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi

31

kiweze

12.2.1

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria Nambari 2 ya


Chakula, Dawa na Vipodozi, Bodi ilikagua jumla ya maeneo
1,304 ya biashara za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
Katika ukaguzi huo hatua mbali mbali zilichukuliwa kwa
waliobainika na kasoro zikiwemo kupewa elimu ya usajili wa
biashara zao, kupewa muda wa kuweka bidhaa katika
mpangilio mzuri na kusafisha maeneo yao ya biashara.

12.2.2

Mheshimiwa Spika, mbali na kufanya ukaguzi Bodi pia ilisajili


jumla ya maeneo 1,151 ya biashara za chakula, dawa na
vipodozi. Vile vile bidhaa moja

ya dawa na bidhaa 63 za

chakula zimesajiliwa. Pia jumla ya bidhaa 100 za wajasiriamali


na vifaa tiba 25 zilitambuliwa. Aidha, Bodi iliweza kuwasajili
waingizaji chakula (Food Importers) 68, wasafirishaji chakula
(Food Exporter) 11, wafamasia watano

na wafamasia

wasaidizi (Pharmaceutical Technicians) 49.


12.2.3

Mheshimiwa Spika, katika uchunguzi wa kimaabara sampuli


888 zikiwemo 792 za chakula, 4 za dawa, 43 za vipodozi na
49 za dawa za mitishamba zilichunguzwa. Katika uchunguzi
huo ni sampuli 1 ya chakula ndio ilionekana haifai kwa
matumizi ya binadamu na sampuli zote za dawa, vipodozi na
dawa za mitishamba zilionekana zinafaa kwa matumizi ya
binadamu.

32

12.2.4

Mheshimiwa Spika, jumla ya tani 88.9 zikiwemo tani 84.9


za bidhaa za chakula, tani nne za bidhaa za Dawa na Vipodozi
zisizofaa kwa matumizi ya binaadamu ambazo zilikamatwa
wakati wa ukaguzi ziliteketezwa, na tani 25 za bidhaa za
chakula

ambazo

hazifai

kwa

matumizi

ya

binaadamu

zilirejeshwa zilikotoka. Halikadhalika jumla ya tani 103 za


chakula na tani 1.5 za vipodozi zilizoingia maji ya chumvi, tani
moja ya dawa zilizoisha muda wa matumizi zimekamatwa na
kusubiri hatua za kisheria.
12.2.5

Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa katika hotuba ya


bajeti ya mwaka 2014/2015, kuwa bodi itamalizia ujenzi wa
ofisi yake, napenda kuchukua fursa hii kuliarifu Baraza hili
kwamba ujenzi huu umeshakamilika na tayari wafanyakazi
wameshahamia katika jengo hilo jipya.

12.3

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala

12.3.1

Mheshimiwa Spika, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala


(Traditional and Alternative Medicine Council) ni chombo
kilichoundwa chini ya sheria No.8 ya mwaka 2008, na
linajukumu la kisheria kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa
tiba asili na tiba mbadala.

33

12.3.2

Mheshimiwa

Spika,

jumla

ya

waganga

205

ambao

wameweza kutimiza masharti yaliowekwa ikiwa ni pamoja na


kumiliki sehemu maalumu ya kutoa huduma kwa wagonjwa
wamesajiliwa. Sambamba na hilo, maduka 40 ya dawa za asili,
kliniki 11 (Unguja 9 na Pemba 2) na wasaidizi waganga 58
wamesajiliwa.
12.3.3

Mheshimiwa Spika, imebainika kuwapo kwa ongezeko kubwa


la matangazo yanayohusu tiba asili ambayo yanakiuka taratibu
zilizomo katika sheria ya baraza la tiba asili na tiba mbadala.
Kwa mintarafu hii, wizara inaendelea kuzuia na kupiga
marufuku matangazo yote ambayo hayafuati sheria na taratibu
zilizowekwa na baraza hili.

12.3.4

Mheshimiwa

Spika,

napenda

kuchukuwa

fursa

hii,

kuwaomba wananchi kutoendelea kuuza dawa hizo katika


maeneo yasiyoruhusiwa kama vile misikitini, barabarani pamoja
na sehemu zote ambazo hazikubaliki kuuza dawa hizo. Hatua
kali zitachukuliwa kwa wale wote wanaoenda kinyume na agizo
hili.

12.4 Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi


12.4.1

Mheshimiwa Spika, Bodi hii ina jukumu la kusimamia


uanzishwaji na uendeshaji wa hospital na vituo vya afya vya
34

binafsi,

kukagua

na

kuzipa

maelekezo

ya

utendaji

yanayostahiki. Aidha, kusimamisha utoaji wa huduma kwa kituo


husika pale vigezo na miongozo inapokiukwa.
12.4.2

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha utekelezaji wa kazi za


Bodi takribani hospitali 40 zimekaguliwa kwa kipindi hiki na
jumla ya hospitali nane zilipewa onyo kwa utoaji huduma
kinyume na sheria na miongozo ya uendeshaji wa hospitali za
binafsi na kwa hivi sasa kuna jumla ya hospitali na vituo vya
afya binafsi 68 Unguja na Pemba vinavyotambuliwa.

13.0

MIRADI YA MAENDELEO

13.1

Programu ya Kumaliza Malaria Zanzibar

13.1.1

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha


Kumaliza Malaria Zanzibar inaendelea kutekeleza mikakati ya
kumaliza malaria kama inayoshauriwa na Shirika la Afya
Ulimwenguni. Mikakati hiyo ni pamoja na usambazaji na
ushajihishaji wa matumizi sahihi ya vyandarua, ufukizaji wa
dawa za kuulia mbu majumbani, uchunguzi na tiba ya
wagonjwa wa malaria, ufuatiliaji wa wagonjwa katika ngazi ya
shehia na ufuatiliaji wa tabia na wingi wa mbu wanaoeneza
Malaria katika maeneo yote ya hapa Zanzibar.

35

13.1.2

Mheshimiwa Spika, ugonjwa wa malaria bado unaendelea


kupungua kwenye visiwa hivi kutokana na kutekeleza mikakati
hiyo. Takwimu zinaonesha kuwa bado yapo maeneo ambayo
taarifa za ugonjwa huu zimekuwa zinajirudiarudia kila ifikapo
wakati wa mvua za masika na vuli. Wilaya zote zimeendelea
kuonyesha kuwepo kwa ugonjwa huu isipokuwa Wilaya ya
Mjini. Kwa upande wa Kisiwa cha Pemba, katika Wilaya za
Micheweni na Wete taarifa za wagonjwa wa malaria zimekuwa
zikijirudia mara kwa mara.

13.1.3

Mheshimiwa Spika, programu ya kumaliza maradhi ya


malaria imeanzisha mradi wa kuangamiza viluilui katika visiwa
vya Uzi kwa Unguja na Kisiwa Panza kwa Pemba katika hatua
za majaribio. Mnamo mwezi wa Julai, 2014 kabla ya
kuanzishwa kazi hii kituo cha afya Uzi kiliripoti wagonjwa 51 na
Kisiwa Panza wagonjwa saba. Baada ya kazi hii kuanza mwezi
wa Agosti 2014, hadi kufikia mwezi Machi 2015 hakuna
mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kutoka vituo hivi vya afya.

13.1.4

Mheshimiwa Spika, upatikanaji na matumizi ya vyandarua


vilivyowekwa dawa si wa kuridhisha. Programu imeanzisha
utaratibu mpya wa kugawa vyandarua kwa mpango endelevu.
Ndani ya utaratibu huu vyandarua vitaendelea kugawiwa kwa
familia zenye mahitaji kwa kila leo badala ya kusubiri hadi

36

baada ya miaka mitatu kama utaratibu wa zamani ulivyokuwa


ukitekelezwa.
13.1.5

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai, 2014 hadi Machi


2015, jumla ya vyandarua 114,394 sawa na asilimia 51 ya
makisio ya mwaka unaomaliza vimegawiwa kwa wananchi
ambao wamekidhi sifa na vigezo vilivyowekwa.

13.1.6

Mheshimiwa Spika, mwezi Februari mwaka 2015, kazi ya


upigaji dawa majumbani iliingia kwenye mzunguko wake wa 12
tokea kazi hii ilipoanza mwaka 2006 hapa Zanzibar. Upigaji huu
wa dawa ya majumbani ni kwa maeneo maalumu ya wilaya za
Magharibi, Kati, Kusini, Wete, Kaskazini A, Kaskazini B na
Micheweni. Katika zoezi hili la upigaji dawa mwaka 2014, jumla
ya nyumba 70,368 zililengwa kupigwa dawa katika wilaya 9 za
Unguja na Pemba. Jumla ya nyumba zilizopigwa dawa ni
66,497 sawa na asilimia 94.5 ya nyumba zote zilizolengwa.

13.1.7

Mheshimiwa

Spika,

katika

zoezi

hilo

nyumba

3,868

hazikuweza kupigwa dawa kutokana na sababu mbali mbali


zikiwemo; kuwepo na mgonjwa mahututi katika nyumba,
nyumba kufungwa, kukataa bila ya sababu za msingi na
kuwepo kwa mzazi aliyejifungua chini ya wiki moja.

37

13.1.8

Mheshimiwa Spika, programu inaendelea na uchunguzi wa


vimelea vya malaria katika kazi zake za kila siku. Jumla ya watu
172,972 walichunguzwa vimelea vya Malaria ambapo watu
1,648 (0.9%) waligundulika kuwa na vimelea hivyo. Kati ya
watu wote waliochunguzwa, 5,086 walikuwa ni watoto chini ya
umri wa miaka tano na waliokutwa na vimelea vya malaria ni
177 (0.1%). Wagonjwa hawa walichunguzwa kwa njia ya
darubini na njia ya uchunguzi wa haraka - (mRDT) ambazo
ndizo zinazopendekezwa kwa kuchunguza malaria.

13.1.9

Mheshimiwa Spika, ni imani yangu kwamba Waheshimiwa


Wawakilishi wana uwezo wa kuhamasisha jamii kwenye
mpango wa kumaliza Malaria, hivyo suala la uhamasishaji jamii
linafaa kupewa kipaumbele cha hali ya juu ili kuhakikisha lengo
la asilimia 100 linafikiwa

13.2

Mradi Shirikishi wa Afya ya Uzazi na Mtoto

13.2.1

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha


afya ya mama na watoto kwa kupunguza vifo vya kinamama
vitokanavyo na uzazi, na vifo vya watoto wenye umri wa chini
ya miaka mitano.

38

13.2.2

Mheshimiwa Spika, jambo jengine kubwa ambalo husaidia


kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni matumizi ya njia bora
ya uzazi wa mpango na salama.

13.2.3

Mheshimiwa

Spika,

kwa

mwaka

2014

kiwango

cha

kinamama waliojifungulia hospitali kimefikia asilimia 68.3


ukilinganisha na asilimia 56.6 mwaka 2013. Natoa wito kwa
mama wajawazito wote kuendelea na mwamko huo ili
kuepusha matatizo yanayoweza kutokea kabla, wakati, au
baada ya kujifungua na hatimae kusababisha vifo vya uzazi.
Aidha, nachukua fursa hii kuwaomba wananchi kuendelea
kujifungua katika vituo vya Afya kwa wakati. Mbali na mambo
hayo niliyoyataja hapo juu suala la kufika kliniki mapema wakati
wa

ujauzito

husaidia

sana

kupunguza

vifo

vya

mama

wajawazito.
13.2.4

Mheshimiwa Spika, ili kuwakinga na maradhi ya UKIMWI


watoto waliozaliwa na mama wenye Virusi vya UKIMWI
huduma maalumu hutolewa kwa kinamama hao ili kuwanusuru
watoto watakaozaliwa wasipate maambukizi. Kwa mwaka wa
fedha

2014/15,

jumla

ya

mama

walichunguzwa VVU katika kliniki.


waligunduliwa na VVU.

39

wajawazito

33,202

Kati yao kinamama 73

13.2.5

Mheshimiwa Spika, chanjo za watoto ni muhimu sana katika


maendeleo ya ukuaji wa mtoto.

Huduma ziliendelea kama

kawaida, ambapo chanjo zilendelea kutolewa katika vituo vyote


vya afya ya uzazi na mtoto.

Kwa mwaka 2014 kiwango cha

chanjo kitaifa kimeendelea kuwa zaidi ya asilimia 90.


13.2.6

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, wizara ilianzisha


chanjo ya pili ya surua hapa nchini. Lengo la kuanzisha chanjo
hii ni kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa surua
na kutokomeza ugonjwa wa surua ifikapo mwaka 2020. Aidha,
mtakumbuka kwamba mnamo mwezi wa Oktoba, 2014,
kulikuwa na kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella.
Kampeni hii ilihusisha watoto wenye umri wa chini ya miaka
15 ambao walichanjwa kwa zaidi ya asilimia 96

chanjo ya

Surua Rubella na zaidi ya asilimia 100 kwa matone ya Vitamin


A na dawa za minyoo. Takwimu za chanjo zimeainishwa
kwenye kiambatisho namba 11.
13.2.7

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kwamba watoto wachanga


wanapatiwa huduma wanazostahiki mafunzo ya siku sita juu ya
utoaji

wa

huduma

za

dharura

kwa

watoto

wachanga

yamefanyika kwa watoa huduma 120 wa afya kutoka vituo vya


afya mbali mbali (60 Unguja na 60 Pemba). Aidha, tathmini ya
ufuatiliaji wa upatikanaji na utoaji wa huduma kwa watoto
wachanga imefanyika kwa kushirikiana na mshauri muelekezi
kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni.
40

13.3.

Mradi Shirikishi wa Maradhi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na


Ukoma

13.3.1

Mheshimiwa Spika, mradi huu una lengo la kupambana na


maradhi ya UKIMWI, Kifua kikuu na Ukoma ambapo unahusisha
huduma ya ushauri nasaha, uchunguzi na kutoa tiba kwa
wagonjwa

wanaohudhuria

kliniki

na

kutoa

huduma

za

wagonjwa wa UKIMWI majumbani.


13.3.2

Mheshimiwa Spika, huduma za Ushauri nasaha na upimaji


wa VVU inatolewa katika vituo 91 ( Unguja 58 na Pemba 33).
Kwa kipindi cha Julai, 2014 hadi Machi, 2015, jumla ya watu
60,638 walichunguzwa

(wanawake 29,896 na wanaume

30,742), Kati yao watu 740 (1.2 %) waligundulika kuwa na


VVU, wanaume ni 330 (44.6%)

na wanawake 410

(55.4%).
13.3.3

Mheshimiwa

Spika,

tathmini

kwa

mama

wajawazito

wanaohudhuria Kliniki ili kujua kiwango cha maambukizo ya


VVU, kaswende, homa ya ini B na homa ya ini C imefanyika.
Jumla ya wajawazito 6,367 kati yao asilimia 39 Pemba na
asilimia 61 kwa Unguja wameshiriki katika tathmini hiyo.
Matokeo ya tathmini hii ilionesha kwamba wajawazito 39
(0.6%) wameambukizwa Virusi vya UKIMWI.

41

13.3.4

Mheshimiwa Spika, katika kutoa huduma za tiba kwa


wagonjwa wanaoishi na VVU na UKIMWI, jumla ya kliniki 11
zinatoa huduma hii (7 Unguja, 4 Pemba). Kuanzia Julai, 2014
hadi kufikia Machi, 2015, jumla ya wagonjwa 7,820 walikuwa
tayari wameshasajiliwa kwenye kliniki hizo, miongoni mwao
wagonjwa 5,375 (68.7%) walianzishiwa dawa za ARVs.
Waliobaki kwenye dawa kufikia Machi 2015 ni wagonjwa 3,587
na wagonjwa 1,788 (33.3%) wamekimbia kuchukuwa dawa.

13.3.5

Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa maradhi ya ugonjwa wa


ukoma majumbani ulifanyika katika Shehia 15 za wilaya ya
Kusini ambapo ugonjwa huu umeenea. Jumla ya nyumba 425
zilipitiwa na watu 2,275 walichunguzwa. Kati yao watu 215
waligunduliwa na maradhi ya ngozi na watu 40 waligundulika
na maradhi ya ukoma. Katika hatua nyengine watu 390 (202
Unguja na 188 Pemba) waligundulika na Kifua Kikuu, kati yao
162 kwa njia ya makohozi (smear positive), 91 njia ya x-ray
(smear negative), 56 TB ya nje ya mapafu na 81 waliorejewa
na Kifua Kikuu.

13.4

Mradi wa Kustawisha Siha za Wazanzibari

13.4.1

Mheshimiwa Spika, utoaji wa elimu ya afya ni moja kati ya


mikakati inayoendeleza jamii ili kujua, kuelewa na kufahamu
yale yote ambayo ni muhimu katika kuimarisha afya bora na
kujikinga na maradhi. Lengo la mradi huu, ni kutoa taaluma
42

hiyo kwa Jamii kwa kushirikiana na wadau mbali mbali pamoja


na wananchi.
13.4.2

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mkakati wa Afya ya


Jamii, jumla ya Kamati Kiongozi za Shehia 72 zimeundwa (63
Unguja na 9 Pemba). Kati ya hizo Kamati 36 za Wilaya ya
Magharibi, Kaskazini A na Mkoani zimeshapata mafunzo ya
utekelezaji wake. Aidha, wafanyakazi 34 wa vituo vya afya vya
wilaya ya Magharibi na Mkoani wameshapatiwa mafunzo juu ya
uanzishwaji wa kamati Kiongozi za Afya za Shehia na jinsi ya
kushirikiana

nazo.

Mafunzo

mengine

yametolewa

kwa

madiwani na wadau 181 wa wilaya zote.


13.4.3

Mheshimiwa Spika, elimu ya afya imetolewa katika skuli


mbali mbali, kazi hii ilifanywa katika Skuli 13 kwa walimu na
wanafunzi juu ya umuhimu wa chanjo, ugonjwa wa kisukari na
uhifadhi wa chakula kwa wauzaji chakula katika maskuli. Aidha,
jumla ya skuli 177 zimepatiwa mafunzo ya elimu kuhusu stadi
za maisha pamoja na elimu ya afya juu ya umuhimu wa
unyonyeshaji, Ugonjwa wa kichocho na matende, umuhimu wa
chanjo,

na uhifadhi wa taka imetolewa

katika maeneo

ya

Shehia mbali mbali.


13.4.4

Mheshimiwa Spika, jumla ya vipindi 46 vya elimu ya afya


vya redio vilirushwa hewani kupitia Shirika la Utangazaji
43

Zanzibar ZBC (Redio), Zenj FM na Redio NURU, vipindi hivyo


vilihusu Kampeni ya chanjo, kichaa cha Mbwa, dawa za
kulevya, tahadhari ya mvua, maradhi ya kuharisha, ukoma,
kifafa, kichocho, umuhimu wa afya ya uzazi, mabadiliko ya
tabia na athari za ulawiti, lishe na ramadhani na majanga ya
moto kwa watoto na watu wazima. Elimu pia ilitolewa juu ya
umuhimu wa kutambua na kujikinga na maradhi ya Ebola na
wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama.
13.4.5

Mheshimiwa Spika, vipindi 39 vimerushwa kupitia Shirika la


Utangazaji Zanzibar ZBC (TV) vinavyohusu maradhi kama vile
macho, meno, kisukari, homa kwa watoto, maradhi ya Ebola,
ulishaji wa dawa za minyoo na kichocho, Kampeni ya chanjo
dhidi ya Surua Rubella, afya ya akili, sindikizo la damu na
saratani ya kizazi vimetolewa kwa njia ya televisheni.

13.4.6

Mheshimiwa Spika, chumba cha kurushia matangazo kwa


ajili ya Redio ya Afya FM kimetengenezwa. Aidha vifaa
vitakavyotumika kurushia matangazo ya redio hio ikiwemo
Professional moving camera 5D, Editional machine, Conses,
flash, Binocular, memory card heavy duty, Professional
conirocoder, tripod delux camera stand, Delux back pack na
Delux hard cases vimenunuliwa.

44

13.5

Mradi wa Kuipandisha Hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja


Kuwa ya Rufaa

13.5.1

Mheshimiwa Spika, azma ya Serikali kuipandisha hadhi


hospitali hii kuwa ya rufaa kwa Zanzibar, ni kutoa huduma
zitakazo kwenda sambamba na mpango mkakati wa hospitali
hii. Huduma hizo ni pamoja na kuongeza

miundo mbinu,

wataalamu, kuimarisha huduma za uchunguzi,

huduma za

kitalaamu za upasuaji wa maradhi ya mgongo na ubongo


(neurosurgical services), kuanzisha huduma za maradhi ya figo
(Dialysis) na huduma za matibabu ya kensa.
13.5.2

Mheshimiwa Spika, jengo la huduma za upasuaji wa maradhi


ya mgongo na ubongo (neurosurgical services) limeshakamilika
na tayari limeshaanza kazi.

Jengo hili limejumuisha chumba

cha upasuaji (theatre), chumba cha kuhudumia wagonjwa


wanaohitaji uangalizi maalumu Intensive Care Unit (ICU),
kliniki pamoja na wodi za kulaza wagonjwa.
13.5.3

Mheshimiwa Spika, katika hatua nyengine wizara imetiliana


mkataba na kampuni ya Rans kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
jengo la watoto chini ya ufadhili wa Serikali ya Norway. Jengo
hilo litakalokuwa na wodi mbili, maabara ndogo, kitengo cha
kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (dialysis
unit) na chumba cha watoto wanaohitaji uangalizi maalumu
(Accute Paediatric Care Unit). Jengo hilo linatarajiwa kumalizika
45

mwishoni mwa mwaka huu na gharama za ujenzi pamoja na


vifaa unakisiwa kuwa ni zaidi ya dola milioni moja za
kimarekani.

13.5.4

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa jengo la kliniki ya maradhi


maalumu, wodi ya wazazi, chumba cha huduma za dharura,
chumba cha upasuaji, wodi ya watoto wachanga na wodi ya
huduma za kangaroo kwa watoto tayari umeshanza. Vilevile
mitambo ya sterilization kwa ajili ya vifaa vya upasuaji,
mtambo wa kutengenezea oxygen na umeme wa jua
vitawekwa. Ujenzi huo utagharimu jumla ya Euro 9.6m
ambapo Euro 4.8m zitachangiwa na Serikali ya Uholanzi na
sehemu iliyobaki zitatolewa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.

13.5.5

Mheshimiwa Spika, kwa kushirikana na Jamuhuri ya Watu


wa China, huduma ya ICU zimeimarishwa kwa kuikarabati wodi
ya mifupa kuwa wodi ya ICU yenye vitanda vinane na kuiwekea
vifaa vya kisasa, ukarabati huo umekamilika na wodi hiyo tayari
imefunguliwa rasmi tarehe 10 Januari 2015.

46

13.6.

Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali za Wilaya na Vijiji

13.6.1

Mheshimiwa Spika, Mradi huu unalengo la kuzipandisha


hospitali za Vijiji kuwa za Wilaya na Hospitali mbili (Abdalla
Mzee na Wete) kuwa za Mkoa.

13.6.2

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha miundo mbinu kwa


hospitali za vijiji wizara imefanikiwa kumaliza ujenzi wa jengo la
wagonjwa wa nje katika hospitali ya Kivunge na kuanza ujenzi
wa chumba cha upasuaji (theatre) katika hospitali ya Micheweni
Pemba.

13.6.3

Mheshimiwa Spika, wodi mpya na yakisasa ya wazazi


imejengwa

katika

hospitali

ya

Wete

Pemba

na

tayari

imeshaanza kutumika. Vilevile ujenzi wa Hospitali ya Abdalla


Mzee unaendelea vizuri.

13.7.

Mradi wa Taaluma za Afya (Zanzibar Medical School)

13.7.1

Mheshimiwa Spika, mtakumbuka kwamba wizara ilianzisha


mafunzo ya udaktari hapa nchini kwa mashirikiano na Chuo
Kikuu cha Matansas Cuba. Napenda kuchukua fursa hii kuliarifu
baraza hili kwamba jumla ya madaktari 38 tayari wamehitimu
masomo yao mnamo mwezi wa Septemba 2014 na tayari

47

wameanza kazi rasmi. Aidha, wanafunzi 12 wanaendelea na


masomo yao ya mwaka wa sita.
13.7.2

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2015/2016 mradi


una mpango wa kuhakikisha wanafunzi 12 na walimu wao
wanapatiwa

huduma

zote

muhimu

zinazohitajika

ili

kuwawezesha wanafunzi hao kuhitimu vizuri mafunzo yao.

14.0

CHANGAMOTO

14.1

Mheshimiwa Spika, mbali na mafanikio yaliyopatikana katika


utekelezaji

wa

kazi

zake

bado

wizara

inakabiliwa

na

changamoto mbali mbali zikiwemo:1. Ufinyu wa upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa kazi za


wizara
2. Upungufu wa wafanyakazi wenye taaluma ya juu ya uhandisi
wa vifaa tiba (Medical Equipment Technology) inayokwenda
sambamba na mabadiliko ya teknolojia
3. Uwepo wa uingizaji wa bidhaa zilizopitwa na muda wa
matumizi na kuhatarisha afya za wananchi.
4. Utegemezi wa wahisani katika ununuzi wa dawa na vifaa
tiba.

48

15.0

MALENGO MAKUU YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA


WA FEDHA 2015/2016 KUPITIA MFUMO WA
PROGRAMU (PBB)

15.1

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye utangulizi


malengo ya Wizara ya Afya katika bajeti ya mwaka 2015/2016
yatatekelezwa kwa njia ya programu ambapo sekta ya afya
itakuwa na programu kuu tano, mbili kati ya hizo zitatekelezwa
na Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja.

15.2

Programu 1:

Usimamizi wa Sera za Afya na Utawala

Programu 2:

Huduma za Kinga na Elimu ya Afya

Programu 3:

Huduma za Tiba.

Programu 4:

Huduma za Uchunguzi na Matibabu

Programu 5:

Uongozi wa Hospitali na Utawala

Mheshimiwa

Spika,

katika

kuhakisha

utekelezaji

wa

programu kila program imekusanya programu ndogo ndogo


ikiwa na malengo makuu na kulenga matokeo ya muda mrefu.
15.3

Mheshimiwa Spika, programu ya Usimamizi wa Sera za Afya


na Utawala inalenga kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma
bora kwa mujibu wa sheria na miongozo yenye misingi ya
uwazi, uwajibikaji, ushiriki na ushirikishaji jamii katika kutoa
maamuzi kwenye mambo yanayohusiana na afya katika ngazi
zote. Programu hii ina programu ndogo tatu nazo ni Uongozi na
Utawala, Sera, Mipango na Utafiti na Uratibu Shughuli za Afya
49

Pemba. Malengo Makuu ya programu hii ni kama haya


yafuatavyo:1. Kusimamia na kutoa miongozo juu ya uendeshaji wa sekta
ya afya
2. Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi katika ngazi
zote
3. Kuhakikisha ufanisi katika kazi na kuendeleza wafanyakazi
kitaaluma
4. Kutoa msaada wa kiufundi kwa idara zote za ndani ya
wizara ya afya.
5. Kutayarisha na kutoa miongozo ya kisera juu ya uendeshaji
wa sekta ya afya
6. Kufanya tafiti na kukusanya taarifa za afya kwa ajili ya
maamuzi ya kisera
7. Kuimarisha mifumo ya taarifa za afya.
8. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera ya afya na
mipango kazi.
9. Kuongeza rasilimali fedha kwa kuanzisha na kutumia aina
mbalimbali za kugharamia huduma za afya ambazo ni
endelevu na zenye kuzingatia uwiano.

50

10. Kuratibu, kutayarisha na kutekeleza mpango mkakati wa


tatu wa

sekta, mpango wa matumizi wa muda wa kati,

mpango kazi wa mwaka na hotuba ya makadirio ya mapato


na matumizi ya mwaka.
11. Kusimamia na kuratibu misaada ya nje inayotokana na
washirika wa maendeleo.
12. Kuratibu shughuli za uendeshaji za utoaji wa huduma za
kinga na tiba Pemba.
15.4

Mheshimiwa Spika, program hii imepangiwa jumla ya Tsh.


14,155,895,000 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake.

15.5

Mheshimiwa Spika, programu ya Huduma za Kinga na Elimu


ya Afya inalenga kutoa huduma bora za afya katika ngazi za
Vituo vya Afya ya msingi daraja la kwanza na la pili na kuwa
jamii yenye uwelewa jinsi ya kujinga na maradhi yenye
kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Programu hii ina
programu ndogo moja ambayo ni programu ya kinga na elimu
ya afya. Malengo Makuu ya programu hii ni kama ifuatavyo:
1. Kuimarisha huduma za kinga ikiwa ni pamoja na huduma za
uchunguzi wa maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya
kuambukiza kwa jamii
2. Kupunguza maradhi na vifo vya mama wajawazito na watoto
wachanga
51

3. Kuongeza uwelewa kwa jamii jinsi ya kujikinga na maradhi


na kuishi katika mazingira bora na yenye afya
4. Kuimarisha mazingira ya afya na usalama kazini

ili

kupunguza ajali na maradhi katika sehemu za kazi


5. Kuimarisha afya ya uzazi kwa Mama na Mtoto pamoja na
Vijana
15.6

Mheshimiwa Spika, Programu hii imepangiwa jumla ya Tsh.


32,963,434,000 kwa utekelezaji wa shughuli zake.

15.7

Mheshimiwa Spika, programu ya Huduma za Tiba inalenga


kutoa huduma bora za matibabu katika hospitali za Vijiji, Wilaya
na Hospitali ya rufaa. Lengo kuu la programu hii ni kutoa
huduma bora zenye viwango na ufanisi katika ngazi zote za
hospitali pamoja na huduma maalumu. Programu hii ina
programu ndogo moja ambayo ni programu ya Huduma za
Hospitali.

15.8

Mheshimiwa Spika, Programu hii imepangiwa jumla ya Tsh.


37,860,771,000 kwa utekelezaji wa shughuli zake.

15.9

Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Idara ya Hospitali ya


Mnazi Mmoja ina program kuu mbili ambazo ni programu ya
Huduma za Uchunguzi na Matibabu na program ya Uongozi na
Utawala.

52

15.10

Mheshimiwa Spika, programu ya huduma za uchunguzi na


matibabu inalenga kuimarisha huduma bora za matibabu ikiwa
na malengo ya kuimarisha huduma bora za uchunguzi na
kupunguza kuugua na vifo kwa wagonjwa. Programu hii ina
programu ndogo mbili ambazo ni huduma za uchunguzi na
huduma za matibabu.

Aidha, kwa upande wa Programu ya

Uongozi na Utawala ina lenga kuhamasisha mazingira mazuri


kwa wafanyakazi kwa lengo la kuimarisha taasisi na uongozi
katika hospitali. Programu hii ina programu ndogo ya uongozi
na utawala wa hospitali.
15.11

Mheshimiwa Spika, Programu ya Uchunguzi na Matibabu


imepangiwa jumla ya Tsh. 669,743,000, na programu ya
uongozi na utawala imepangiwa jumla ya Tsh. 7,334,757,000
kwa utekelezaji wa shughuli zake.

16.0

MGAWANYO WA FEDHA KWA PROGRAMU

16.1

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza programu hizo jumla


ya Tsh. 84,980,100,000 zimepangwakwa mwaka wa fedha
2015/2016. Tsh. 35,535,000,000 kutoka Serikalini na Tsh.
49,445,100,000

kutoka

kwa

washirika

wa

maendeleo.

Mchanganuo wa fedha kwa programu unapatikana kwenye


kiambatisho namba 12.

53

16.2

Mheshimiwa Spika, wizara ina jukumu la kuchangia katika


mfuko mkuu wa serikali kutokana na vyanzo mbali mbali vya
mapato vilivyomo ndani ya taasisi hii. Kwa mwaka wa fedha
2015/2016 Wizara ya Afya imepangiwa kuchangia jumla Tsh.
168,738,000. Kwa upande wa Idara ya Hospitali ya Mnazi
Mmoja jumla ya Tsh 902,973,000 zinatarajiwa kukusanywa
kwa kipindi hicho.

17.0

HITIMISHO

17.1

Mheshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana katika wizara


ya afya yalitegemea kwa kiasi kikubwa juhudi na maarifa ya
watendaji, michango, maelekezo, ufuatiliaji na utekelezaji wa
majukumu kutoka kwa viongozi wakuu wa Serikali, wajumbe
wa Baraza lako na wadau wengine wa afya.

17.2

Mheshimiwa Spika, shukrani za kipekee ziende kwa Kamati


ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto chini
ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma kwa
ziara za kamati ambazo huzifanya kila robo mwaka na kutoa
ushauri na maelekezo ya kuiendeleza sekta ya afya. Vile vile
nawashukuru wajumbe wa Baraza lako ambao wamekuwa
mstari wa mbele kuchangia na kufuatilia mmoja mmoja au
kupitia

kamati

maalumu

katika

kuangalia

utendaji

na

utekelezaji wa sekta ya afya. Nawashukuru wote ambao


54

walichangia kwa nia na nguvu zote, nawaomba waendelee na


utaratibu huo katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi
wetu.
17.3

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kuipongeza


tena Kamati hii kwa maelekezo na ushauri walioutoa wakati wa
maandalizi ya bajeti hii ambayo yamelenga zaidi maeneo
muhimu na vipaumbele vya sekta. Aidha, nawashukuru
waheshimiwa wawakilishi wote kwa michango na misaada
mbali mbali waliyoitoa kwa wizara ikiwemo ushauri na
maelekezo ambayo yamesaidia katika kutekeleza majukumu ya
sekta ya afya.

17.4

Mheshimiwa Spika, napenda nichukuwe fursa hii pia


kuwashukuru viongozi wote na wafanyakazi wa Wizara ya Afya
kwa mashirikiano
kusimamia

yao wakati wote kwa

kuniwezesha

majukumu yangu kwa wepesi, nawaomba wazidi

kuendelea na mashirikiano hayo kila siku katika kazi zao.


17.5

Mheshimiwa

Spika,

nitakuwa

si

kufanya

haki

kama

sikuwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuwa nasi wakati


wote na kutupa mashirikiano mazuri katika kupokea huduma
zinazotolewa katika sekta ya afya. Pia shukrani za pekee ziende
kwa wananchi wa jimbo la Ziwani kwa kuwa nami kwa kipindi
chote cha uongozi wangu kwa kunipa mashirikiano mazuri
55

katika utekelezaji wa kazi zangu za kila siku ni kiwa muwakilishi


wa jimbo hili. Sinabudi kuzishukuru taasisi nyengine za serikali
na zisizo za serikali kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa
katika suala zima la utoaji wa huduma za afya.
17.6

Mheshimiwa Spika, msukumo mkubwa umeendelea kutolewa


na mashirika ya kitaifa na kimataifa, pamoja na nchi marafiki.
Msukumo huo wa hali na mali umesaidia kutoa huduma kwa
wananchi. Nachukuwa fursa hii adhimu kuwashukuru hasa
mashirika ya kimataifa yakiwemo WHO, UNICEF, UNDP na
UNFPA. Pia shukrani ziende kwa DANIDA, JICA, JSI, JHPIEGO,
HIPZ, CLININTON FOUNDATION, GLOBAL FUND,PMI, KOICA,
SAVE THE CHILDREN, SIGHT SAVERS INTERNATIONAL, PATH
FINDER, IVODE CARNERI, USAID na MILELE FOUNDATION. Pia
shukrani ziende kwa serikali za nchi marafiki zikiwemo India,
Israel, Cuba, Marekani, Italy, Netherland, Norway, Belgium,
China, Misri, Oman, Turkey na wale wote ambao sikuwataja
katika orodha huu.

17.7

Mheshimiwa Spika, baada ya hitimisho sasa naliomba baraza


lako liijadili, liikubali na kuipitisha bajeti ya Wizara ya Afya. Kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 wizara imepangiwa kutumia jumla
ya Tsh. 84,980,100,000 kati ya hizo Tsh. 12,893,400,000
kwa kazi za kawaida, Tsh. 16,120,900,000 mishahara na
maposho, TSh. 870,700,000 ni ruzuku kutoka serikalini.
56

Aidha, jumla ya Tsh. 5,650,000,000 kwa kazi za maendeleo


kutoka Serikalini, na Tsh. 49,445,100,000 ruzuku kutoka kwa
washirika wa maendeleo.
Pia

naomba

baraza

lako

liidhinishe

jumla

ya

Tsh.

8,004,500,000 kwa ajili Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja


kwa kazi za kawaida, mishahara na maposho. Ufafanuzi wa
taarifa za fedha unapatikana katika kiambatisho namba 13,
14, 15, 16 na 17.
17.8

Mheshimiwa Spika, ni mategemeo yangu kwamba wajumbe


wa Baraza lako wameipokea hotuba hii, wataijadili kwa kina na
kutoa michango yao kwa madhumuni ya kuiwezesha wizara
katika kutekeleza majukumu yake. Wizara itaipokea michango
yote itakayotolewa na kuifanyia kazi kama inavyostahiki kwa
faida ya nchi yetu.

17.9

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima na kwa


ruhusa yako NAOMBA KUTOA HOJA.

MHESHIMIWA RASHID SEIF SULEIMAN.


WAZIRI WA AFYA,
ZANZIBAR.

57

VIAMBATISHO
Kiambatisho namba 1: Uchunguzi wa Macho Vijijini, Julai 2014
Machi, 2015
Watu
Wazima
Watoto
Jumla
Maradhi
Me
Ke
Me
Ke
Reffractive errer
150
160
32
27
369
Pterygium
12
18
0
0
30
Cataract
4
2
0
0
6
Conjuctivitis
27
37
9
15
88
Cornea abnormality
5
4
2
0
11
Retinal disorders
26
17
0
0
43
Pseudoplakia
15
6
2
0
23
Jumla
239
244
45
42
570

Kiambatisho Namba 2: Mahudhurio Wagonjwa wa Nje,


Waliolazwa na Wagonjwa waliofariki katika Hospitali za Idara ya
Tiba, Julai 2014-Machi 2015

Hospitali
Mkoani
Chake Chake
Wete
Micheweni
Vitongoji
Kivunge
Makunduchi
Jumla

Wagonjwa
wa
nje
Me
Ke
10,797
15,094
21,050
28,530
18,804
26,403
7,015
9,312
6,247
6,121
30,002
29,078
10,325
12,211
104,240 126,749

58

Wagonjwa
waliolazwa
Me
Ke
712
2,387
2,210 5,503
1,350 3,787
593
1,841
262
643
542
2,351
457
1,593
6,126 18,105

Wagonjwa
waliofariki
Me
Ke
49
32
81
73
35
37
21
13
4
5
32
28
8
7
230 195

Kiambatisho Namba 3: Taarifa ya Hali ya Uzazi katika Hospitali za


Idara ya Tiba, Julai 2014-Machi 2015

Hospitali

Mkoani
Chake
Chake
Wete
Micheweni
Vitongoji
Kivunge
Makunduchi
Jumla

Jumla
ya
Wajawa
zito
waliolaz
wa
1,691

Jumla
ya Watoto
Waliojifungua waliozaliwa
Kwa njia ya
Hai
Kawai Upasu
Me
da
aji

Ke

Jumla ya
Wazazi
waliofari
ki

1,316

96

720

663

3,235

2,675

239

1,509

1,357

2,190
849
209
1,865
916
10,955

1,686
650
175
1,651
798
8,951

201
0
0
10
16
562

1,071
337
103
880
419
5,039

884
317
74
794
376
4,465

6
1
0
3
2
24

59

Kiambatisho Namba 4: Mahudhurio ya Wagonjwa katika Kliniki za Maradhi Maalumu kwa


Hospitali za Idara ya Tiba, Julai 2014-Machi 2015
Kliniki

Mkoani

Chake Chake

Wete

Micheweni

Vitongoji

Kivunge

Me

Ke

Me

Ke

Me

Ke

Me

Ke

Me

Ke

Me

Ke

Cardiac

119

109

401

759

177

458

149

219

139

212

184

758

HIV CTC

100

130

277

477

271

430

145

386

Dental

650

910

664

1,024

903

1,100

156

246

65

77

788

Diabetic

226

286

308

653

168

286

58

85

29

43

ENT

556

1,015

1,333

2,064

546

624

109

134

Eye

889

1,256

1,262

1,856

2,996

3,181

373

418

199

Eye theater

71

69

Eye refraction

471

769

Gynaecology

814

917

Major Theatre

106

151

356

498

158

Minor Theatre

220

115

708

625

Orthopedic

1,657

1,812

Physiotherapy

64

123

Psychiatric

23

30

STI

11

Surgical OPD
Jumla

Makunduchi
Me
Ke
-

11

1,306

765

1,031

384

600

236

448

218

169

179

156

176

251

53

14

72

35

371

186

355

107

3,070

1,143

302

263

113

108

236

355

694

729

826

862

16

26

256

388

22

68

44

58

14

106

13

31

598

701

959

924

834

297

5,219

7,474

7,740

12,609

7,437

8,776

991

1,495

847

741

4,662

4,106

1,742

2,475

1,900

60

Kiambatisho Namba 5: Mahudhurio ya Wagonjwa wa Nje na


Waliolazwa katika Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, Julai 2014Machi 2015
Wagonjwa wa Wagonjwa
Wagonjwa
nje
waliolazwa
waliofariki
Hospitali
Me
Ke
Me
Ke
Me
Ke
Mnazi Mmoja
42,359 37,799 6,352 20,612 480 418
Mwembe Ladu
164
264
5,547
0
0
Kidongo Chekundu 3,684
3,994
350
281
2
1
Jumla
46,207 42,057 6,702 26,440 482 419

Kiambatisho Namba 6: Mahudhurio ya Wagonjwa katika Kliniki za


Maradhi Maalumu kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja Julai, 2014 Machi 2015
Kliniki
Me
Ke
Jumla
Cardiac
805
1,237
2,042
Dental
1,503
1,799
3,302
Diabetic
2,105
2,573
4,678
ENT
10,488 15,072 25,560
Eye
2,031
2,617
4,648
Eye Major Theatre
233
203
436
Major theatre
328
140
468
Minor theatre
2,781
1,942
4,723
Obs. and Gynae
2,631
2,631
Orthopedic
2,545
1,817
4,362
Paediatric medical
926
847
1,773
Physiotherapy
and
2,104
1,996
4,100
rehabilitation
Accupunture
996
1,355
2,351
Surgical OPD
2,881
1,534
4,415
STI/RTI
9
39
48
CTC Clinic
2,158
4,602
6,760
Jumla
31,893 40,404 72,297

61

Kiambatisho Namba 7: Taarifa ya Hali ya Uzazi katika Wodi ya


Wazazi kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na Mwembeladu, Julai
2014 Machi, 2015
Jumla
ya Watoto
Jumla
Waliojifungua
waliozaliwa ya
Jumla
ya
Kwa njia ya
Hai
Wazazi
Hospitali
Wajawazito
waliofar
waliolazwa
iki
Kawaida Upasuaji Me
Ke
Mnazi
Mmoja
Mwembe
ladu
Jumla

8,624

6,563

1,022

4,288

4,202

22

4,926

4,594

71

2,392

2,285

13,550

11,157

1,093

6,680 6,487 22

Kiambatisho Namba 8: Thamani ya Dawa na Zana za Tiba


zilizopatikana, Julai 2014 Machi, 2015
THAMANI
CHANZO
(TSH)
SMZ
1,368,325,561
DANIDA
58,831,265
GLOBAL
283,201,354
FUND
UNICEF
66,158,764
WHO
37,258,704
UNFPA
141,084,015
USAID
42,962,400
PROJECT
1,973,638,936
HOPE
JUMLA
3,971,460,999

62

Kiambatisho Namba 9: Idadi ya Sampuli Zilizochunguzwa,


Julai 2014 Machi, 2015
Aina
ya Idadi
ya
Taasisi
Kielelezo
Sampuli
Bhangi
95
Polisi
M/kulevya
80
Pombe
30
Mikojo
333
Damu
20
Sumu
9
Jumla Ndogo
567
2
Taasisi ya watu Tomato
Asali
18
Binafsi
Sabuni
2
Kibali
cha
1
kemikali
Jumla Ndogo
23
JUMLA KUU
590

63

Kiambatisho Namba 10: Wanafunzi Waliokwenda Masomoni, Julai 2014 - Mei 2015
KIWANGO
KADA/FANI
POST
DIPLOMA ADV.DIP DEGREE GRAD MASTERS PHd TOTAL
V.CONTROL
3
3
SOCIAL WORK
2
2
SCIENCE
AND BEHAVIOR
1
1
CHANGE
PUBLIC HEALTH
3
3
6
PSYCHOLOGY
AND
1
1
CONCELLING
PROCUREMENT
AND
3
3
CONTRACT MANAGEMENT
PHARMACY
4
4
PATHOLOGY
1
1
PAEDIATRICS
3
3
NURSING
2
10
3
15
MONITORING &EVALUATION
3
3
MOLECULAR MEDICINE
1
1
MIDWIFERY
AND
WOMAN
2
2
HEALTH
MICROBILOGY
AND
1
1
IMMUNOLOGY
MEDICAL
LABORATORY
1
1
SCIENCE
MEDICAL BIOCHEMISTRY
1
1
64

MBBS
LIBRARIAN
1
INTERNAL MEDICINE
IMAGE SCIENCE AND NUCLEAR
MEDICINE
HUMAN RESOURCES PLANING
AND MANAGEMENT
HOME
ECONOMIC
AND
NUTRITION
HEALTH
SYSTEM
MANAGEMENT
HEALTH PROMOTION

4
2

4
1
2

2
1

65

1
2

Jadweli la walio masomoni linaendelea


KADA/FANI

KIWANGO
DIPLOMA ADV.DIP DEGREE POST GRADUATE

HEALTH
MONITORING
AND
EVALUATION
GLOBAL HEALTH
GASTROENTROENTERITIS
FOOD
SCIENCES
AND
TECHNOLOGY
EYE CARE
ENVEROMNENTAL HEALTH
ENT
ECONOMIC AND FINANCE
DESASTER MANAGEMENT
CRITICAL CARE AND TRAUMA
COMPUTER SCIENCE
CLINICAL STOMATOLOGY
CHINESE MATERIAL MEDICAL
BUSINESS
INFORMATION
1
TECHNOLOGY
BIOMEDICAL ENGINEERING
ANAETHESIA
AMO
ACCOUNTING AND INVESTMENT
JUMLA
4

MASTERS PHd

TOTAL

1
1

1
1

1
5
1
1
1
1
2
1
1

5
1
1
1
1
1
1

1
1
5
2
10

38

66

1
34

1
5
2
1
92

Kiambatisho Namba 11: Taarifa ya Huduma za Chanjo kwa


Watoto Chini ya Mwaka Mmoja, Julai 2014 hadi Machi, 2015
Surua
WILAYA
BCG
Polio 3 Penta 3
Rubella
Unguja
Kaskazini A
6,409
3,375
4,444
4,191
Kaskazini B
3,129
2,116
2,887
2,735
Kati
3,708
3,018
3,608
3,246
Kusini
1,542
1,311
1,666
1,473
Magharibi
16,968
7,239
9,553
10,689
Mjini
22,507
6,862
9,898
9,633

Jumla Ndogo

54,263

23,921

32,056

31,967

Pemba
Chake
Micheweni
Mkoani
Wete

7,217
5,893
5,631
8,066

4,999
4,059
3,746
5,390

5,018
4,058
3,686
5,416

5,218
4,130
3,869
6,298

JUMLA KUU

81,070

42,115

50,234

51,482

Jumla Ndogo

26,807

18,194

18,178

67

19,515

Kiambatisho Namba 12: Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Programu 2015/16


PROGRAMU

PROGRAMU
NDOGO

P01 Huduma
za Kinga na
Elimu ya Afya
P02 Huduma
za Tiba
P03
Usimamizi wa
Sera za Afya
na Utawala

JUMLA

JUMLA KUU

KAZI
KAWAIDA

S01
Kinga
na Elimu ya
Afya

32,963,434,000

S01 Huduma
za Hospitali

ZA

RUZUKU

KAZI
ZA
MAENDELEO
(MCHANGO
WA
SERIKALI)

KAZI
ZA
MAENDELEO
(FEDHA
ZA
WAFADHILI)

MAKUSANYO

7,589,961,000

650,000,000

24,723,473,000

47,338,000

37,860,771,000

9,568,444,000

70,700,000

4,500,000,000

23,721,627,000

25,400,000

S01 Uongozi
wa Utawala

3,106,943,000

2,806,943,000

300,000,000

S02
Sera
Mipango na
Utafiti

3,417,952,000

1,542,952,000

375,000,000

500,000,000

1,000,000,000

S03 Kuratibu
Shughuli za
Afya Pemba

7,631,000,000

7,506,000,000

125,000,000

96,000,000

84,980,100,000

29,014,300,000

870,700,000

5,650,000,000

49,445,100,000

168,738,000

68

Kiambatisho Namba 13: Makadirio ya Miradi ya Maendeleo kwa Programu 2015/16


PROGRAMU
KUU

HUDUMA/MIRADI

JUMLA KUU

MCHANGO
SERIKALI

WA FEDHA
WAHISANI

ZA

S01 Programu ya Kinga na Elimu ya Afya


H01 Mradi Shirikishi wa Huduma za Afya
1,837,142,000
P01 Huduma ya Uzazi wa Mama na Mtoto
za Kinga na H02 Mradi Shirikishi wa Huduma za
5,842,895,000
Elimu ya Afya
Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma

500,000,000

1,337,142,000

100,000,000

5,742,895,000

H03 Programu ya Huduma ya Kumaliza


17,693,436,000
Malaria Zanzibar

50,000,000

17,643,436,000

JUMLA

25,373,473,000

650,000,000

24,723,473,000

H01 Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali


11,724,000,000
za Wilaya na Vijiji

300,000,000

11,424,000,000

200,000,000

H03 Mradi wa kuipandisha hadhi Hospitali


16,297,627,000
ya Mnazi Mmoja kuwa ya Rufaa

4,000,000,000

12,297,627,000

JUMLA

4,500,000,000

23,721,627,000

500,000,000

1,000,000,000

500,000,000

1,000,000,000

5,650,000,000

49,445,100,000

S01 Programu ya Huduma za Hospitali

P02 Huduma
H02 Mradi wa Chuo cha Kusomeshea
za Tiba
200,000,000
Madaktari - Zanzibar

28,221,627,000

P03
S02 Sera, Mipango na Utafiti
Usimamizi wa
Sera za Afya H05 Kuchunguza Sampuli mbalimbali kwa 1,500,000,000
Jamii
na Utawala
JUMLA
1,500,000,000
55,095,100,000

JUMLA YA FEDHA KWA KAZI ZA MAENDELEO

69

Kiambatisho Namba 14: Muhtasari wa Makisio ya Programu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja


kwa kipindi cha 2015 - 2016
PROGRAMU KUU
P01
Huduma
za
Uchunguzi
na
Matibabu

MAELEZO
JUMLA KUU
S02
Huduma
za
matibabu
H01
Kutoa Huduma
kwa Wagonjwa
669,743,000
JUMLA

P02
Uongozi
Utawala

na

ZA

669,743,000
669,743,000

S01
Uongozi na
Utawala wa Hospitali
H02 Kutoa huduma za
Mipango na Utumishi
7,334,757,000
JUMLA

Jumla kuu
Programu

669,743,000

FEDHA
KAWAIDA

7,334,757,000.00

7,334,757,000 7,334,757,000

kwa
8,004,500,000 8,004,500,000

70

Kiambatisho Namba 15: Fedha Zilizotengwa na Kukusanywa kwa Kipindi cha Julai 2014
hadi Machi 2015 na Makisio ya 2015/2016
MAKUSANYO
JULAI-MACHI
2014/2015

ASILIMIA
(%)

MAKISIO
MAPATO
2015/2016

7,842,000

49.0

29,338,000

9,064,000

60.4

18,000,000

16,906,000

54.5

47,338,000

15,961,000

79.8

25,400,000

15,961,000

79.8

25,400,000

3,688,000

122.9

6,000,000

3,688,000

122.9

6,000,000

71,639,500

102.3

90,000,000

70,000,000
124,000,000

71,639,500
108,194,500

102.3
87.3

90,000,000
168,738,000

200,000,000
350,000,000
550,000,000
674,000,000

306,385,954
276,255,409
582,641,363
690,835,863

153.2
78.9
105.9
102.5

475,859,807
427,113,193
902,973,000
1,071,711,000

MAKADIRIO
2014/2015

KASMA

MAELEZO YA MAPATO

0601

IDARA YA KINGA
Shahada ya maradhi ya
16,000,000
kuambukiza
Huduma za daktari na orodha
15,000,000
wa wafanyakazi na abiria
Jumla ndogo
31,000,000
IDARA YA TIBA UNGUJA
Malipo
ya
X-Ray
na
20,000,000
uchunguzi wa damu.
Jumla ndogo
20,000,000
IDARA YA TIBA PEMBA
Malipo
ya
X-Ray
na
3,000,000
uchunguzi wa damu.
Jumla ndogo
3,000,000
MAPATO MENGINEYO
Mapato mengineyo
70,000,000

142238
142260
0701
142261
0801
142261
145000
145002

Jumla ndogo
1501
145001
145003

JUMLA KUU
HOSPITALI YA M/MMOJA
Mapato mengineyo
Huduma za haraka

Jumla ndogo
JUMLA KUU

71

YA

Kiambatisho Namba 16: Fedha Zilizotengwa na Kuingizwa kwa kazi za Kawaida na za Maendeleo
kutoka Serikali kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Machi 2015 na Makisio 2015/2016
KASMA

MAELEZO

MAKADIRIO
2014/2015

MATUMIZI HALISI
JULAIMACHI. ASILIMIA %
2015

MAKISIO KAZI
ZA
KAWAIDA
2015/2016

O301

OFISI KUU PEMBA

100,000,000

21,804,625

21.8

145,000,000

252,896,000

42,060,309

16.6

452,000,000

259,000,000
1,361,376,000

109,723,900
2,538,971,289.95

42.4
186.5

2,126,100,000
3,000,000,000

O601
O701

MIPANGO
NA
UNGUJA
KINGA - UNGUJA
TIBA - UNGUJA

O801

TIBA - PEMBA

732,424,000

136,741,125

18.7

782,000,000

O901

KINGA - PEMBA
UTUMISHI NA UENDESHAJI
UNGUJA
UTUMISHI NA UENDESHAJI
PEMBA
BOHARI KUU YA DAWA
MFAMASIA
MKUU
WA
SERIKALI
JUMLA
RUZUKU
CHUO CHA AFYA MBWENI
MKEMIA MKUU - UNGUJA
MKEMIA MKUU - PEMBA
BODI YA CHAKULA NA
VIPODOZI

145,000,000

25,793,625.00

17.8

275,000,000

1,031,360,000

340,743,774

33.0

1,150,000,000

150,000,000

51,160,625

34.1

163,300,000

216,896,000

38,303,625

17.7

300,000,000

3,004,248,000

744,460,604

24.8

4,500,000,000

7,253,200,000

4,049,763,501.95

55.8

12,893,400,000

463,296,000
566,420,000
189,484,000

168,853,281
174,508,379
127,727,921

36.5
-

300,000,000
375,000,000
125,000,000

70,700,000

1,219,200,000
8,472,400,000

471,089,581.00
4,520,853,082.95

38.6
53.4

870,700,000
13,764,100,000

O401

2001
2002
2003
2101

2004
1401
1601

JUMLA

JUMLA NDOGO

SERA

72

2001
2002

MISHAHARA
NA
MAPOSHO
UTUMISHI NA UENDESHAJI
7,681,739,000
- UNGUJA
UTUMISHI NA UENDESHAJI
6,593,061,000
- PEMBA
JUMLA
14,274,800,000
JUMLA YA BAJETI KAZI
22,747,200,000
ZA KAWAIDA

6,706,169,739

87.3

9,816,900,000

4,664,623,080

70.8

6,304,000,000

11,370,792,819

79.7

16,120,900,000

15,891,645,901

69.9

29,885,000,000

MATUMIZI HALISI
JULAIMACHI. ASILIMIA %
2015

MAKISIO KAZI
ZA
KAWAIDA
2015/2016

KASMA

MIRADI YA MAENDELEO

MAKADIRIO
2014/2015

1210018

Program
ya
Malaria Zanzibar

50,000,000

733,276,441

1,467.0

50,000,000

150,000,000

179,520,580.98

119.7

200,000,000

2,500,000,000

1,113,765,258.66

44.6

4,000,000,000

200,000,000

47,359,600

23.7

300,000,000

50,000,000

2,000,000

4.00

100,000,000

800,000,000

271,900,119.16

34.0

500,000,000

100,000,000

20,000,000

20.0

500,000,000

3,850,000,000

2,367,822,000

61.5

5,650,000,000

Kumaliza

1210004 Taaluma za Afya (ZMS)


1210012
1210010
1210022
1210023
1210003

Kuipandisha
Hadhi
M/Mmoja Hospitali
KuvipandishaHadhi
Vituo
vya Afya
Mradi Shirikishi wa Ukimwi,
Kifua Kikuu na Ukoma
Mradi Shirikishi wa Afya ya
Uzazi na Mtoto
Kustawisha
siha
za
Wazanzibari
Ujenzi wa Maabara ya
Mkemia Mkuu
JUMLA KWA MIRADI

JUMLA
KAZI
ZA
26,597,200,000 18,259,467,901.95 68.7
KAWAIDA NA MIRADI
73

35,535,000,000

Kiambatisho Namba 17: Fedha Zilizotengwa na Kuingizwa kwa kazi za Maendeleo kutoka kwa
Wahisani kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Machi 2015 na Makisio 2015/2016
KASMA
1210018
1210004
1210012
1210010
1210022
1210023
1210003

MIRADI

MAKADIRIO
2014/2015

Programu ya kumaliza
2,849,803,000
Malaria
Taaluma za Afya (ZMS)
Kuipandisha
Hadhi
3,760,000,000
M/Mmoja Hosp.
Kuvipandisha
Hadhi
10,000,000,000
Vituo vya Afya
Mradi
Shirikishi
wa
Ukimwi, Kifua Kikuu na
4,268,198,000
Ukoma
Mradi Shirikishi wa Afya
2,268,769,000
ya Uzazi na Mtoto
Kustawisha
siha
za
1,210,127,000
Wazanzibari
Ujenzi wa Maabara ya
Mkemia Mkuu

JUMLA
JUMLA KUU

MATUMIZI HALISI
ASILIMIA
JULAI - MACHI.
%
2015

MAKISIO
2015/2016

71,693,750

2.5

17,643,436,000

12,297,627,000

11,424,000,000

32,759,750

0.8

5,742,895,000

1,148,430,820

50.6

1,337,142,000

1,000,000,000

24,356,897,000

1,252,884,320

5.1

50,954,097,000

9,512,352,221.95

38.3

74

49,445,100,000
4,980,100,000

You might also like