Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 12

WASEMAVYO WANASAYANSI KUHUSU QUR'AN

Ibrahimu H. Kabuga

ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH P.O.BOX 76644 Dar es Salaam Tanzania Phone: +255 712 566595 / 0763348213 E-mail: utafititz@gmail.com

Chaguo langu la Muhammad kuongoza orodha ya watu walioacha athari kubwa duniani linaweza kuwashangza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na baadhi yao, lakini ndiye mtu pekee katika historia aliyefanikiwa mno kwenye ngazi zote mbili za kisekula na kidini yumkini nguvu na athari husika ya Muhammad kwenye Uislamu ni kubwa mno kuliko athari na nguvu ya Yesu Kristo na Mt. Paulo kwenye Ukristo zikiunganishwa pamoja ni muungano huu usio kifani wa nguvu ya kisekula na kidini ambayo ninahisi inampa Muhammad hadhi ya kuchukuliwa kuwa mtu mwenye athari na nguvu kuliko wengine katika historia ya binadamu. (Michael Hart katika 'The 100, A Ranking of the Most Influential Persons In History,' New York, 1978).

Keith L. Moore
Profesa Emeritus, Idara ya Anatomia na Baolojia ya chembehai, Chuo Kikuu cha Toronto. Mwana- embriolojia mashuhuri na mwandishi wa vitabu kadhaa vya matibabu, kama vile, Clinically Oriented Anatomy (3rd Edition) na The Developing Human (5th Edition, with T.V.N. Persaud).

Dr. Moore alikuwa ni Rais wa zamani wa Chama cha Canada cha wana-anatomia, na chama Amerika cha wana-anatomia wa tiba. Alitunukiwa tuzo yenye hadhi kubwa ya J.C.B. Grant Award kutoka chama cha wana-anatomia wa Canada na mwaka 1994 alipokea Tuzo ya mwanachama anayeheshimika (theHonoured Member Award) kutoka chama cha wana-anatomia wa Amerika " kwa mchango bora katika uwanja wa anatomia ya tiba".

Utafiti wa kiinitete katika hatua ya 'alaqa.

"Kwa kipindi cha miaka mitatu, nimefanya kazi na Kamati ya Embriolojia ya Chuo Kikuu cha Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah, Saudi Arabia, nikiwasaidia kutafsiri maelezo mengi yaliyomo ndani ya Qur'an na Sunnah kuhusu uzazi wa binadamu na maendeleo yake kabla ya kuzaliwa. Mwanzo nilistaajabishwa mno na usahihi na ukweli wa maelezo haya yaliyoandikwa karne ya 7 AD, kabla sayansi ya Embriolojia haijaanzishwa. Ingawa nilikuwa nikiifahamu historia tukufu ya wanasayansi wa Kiislamu katika karne ya 10 AD, na baadhi ya mchango wao kwenye tiba na madawa, sikuwa nikijua chochote kuhusu mambo matukufu yenye kushangaza na imani mbalimbali zilizomo ndani ya Qur'an na Sunnah."[2]
kwenye Kongamano mjini Cairo aliwasilisha mada ya ushuhuda wa utafiti na kusema: "Imekuwa furaha kubwa kwangu kutoa mchango katika kufafanua taarifa mbalimbali zilizomo ndani ya Qur'an kuhusu maendeleo ya binadamu. Ni wazi kwangu kuwa lazima zitakuwa zimemfikia Muhammad kutoka kwa Mwnyezi Mungu, au Allah, kwa sababu sehemu kubwa ya maarifa haya hayakugunduliwa mpaka baada ya karne nyingi kupita. Hii inathibitisha kwamba lazima Muhammad atakuwa Mtume wa Mungu, au Allah" [1] Profesa Moore vilevile alieleza kuwa: ""Kwa kuwa uonyeshaji wa kiinitete cha binadamu ni 3

suala tata, kutokana na mchakato wa kuendelea kubadilika wakati wa ukuaji, inapendekezwa kuwa mfumo mpya wa Uainishaji inaweza kupatikana kwa kutumia masharti yaliyotajwa katika Qur'ani na Sunna. Mfumo huo unaopendekezwa ni rahisi, mpana, unaendana na maarifa ya kisasa ya Embriolojia.

" Utafiti mkubwa wa Qur'an na Hadith katika kipindi cha miaka minne iliyopita umeonyesha wazi mfumo wa uainishaji wa kiinitete cha binadamu ambao ni wa ajabu kutokana na ukweli kwamba uliandikwa tangu karne ya saba AD .. maelezo yaliyomo katika Qur'an hayawezi kuwa yametokana na msingi wa elimu ya sayansi katika karne ya saba ..." [1]

E. Marshall Johnson
Profesa na Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia na Maendeleo ya Baolojia, na Mkurugenza wa Taasisi ya Daniel Baugh, Chuo Kikuu cha Thomas Jefferson, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Ni mwandishi wa zaidi ya machapisho 200. Miongoni mwa kazi zake nyingine aliwahi kuwa Rais wa Chama Teratolojia. Profesa Johnson alianza kuvutiwa na miujiza ya kisayansi iliyomo ndani ya Qur'an kaika Kongamano la 7 la Tiba lililofanyika Saudi Arabia (1982), baada ya kuundwa kwa kamati maalumu ya kutafiti miujiza ya kisayansi iliyotajwa ndani ya Qur'an na Hadithi. Mwanzo, Profesa Johnson alikataa kukubali kuwa kaika Qur'an na Hadithi kuna maandiko kama hayo. Lakini baada ya majadiliano na Sheikh Zindan alianza kuvutika na hata kuufanya utafiti wake ujikite kwenye maendeleo ya ndani na nje ya kiinitete.

"...kwa ufupi, maelezo ya Qur'an sio tu kwamba yanaelezea juu ya maendeleo muundo wa ndani, bali pia inasisitiza juu ya hatua za ukuaji wa nje, ukuaji wa ndani wa kiinitete, uumbwaji wake na maendeleo yake, ikisisitiza juu ya matukio makubwa yanayotambuliwa na elimu ya sayansi ya kisasa." " Kama mwanasayansi, ninaweza tu kushughulika na vitu ninavyoweza kuviona kabisa. Ninaweza kuielewa embrolojia na maendeleo ya kibaolojia. Ninaweza kuyaelewa maneno ninayotafsiriwa kutoka ndani ya Qur'an. Kama nilivyotoa mfano hapo awali, kama ningetakiwa kujibadilisha mimi kuwa katika zama hizo, kwa kujua kile ninachofanya leo kuelezea vitu, nisingeweza hata kidogo kuelezea mambo haya yaliyoelezwa

Sioni ushahidi wowote wa kukanusha fikra ya kwamba mtu huyu Muhammad alikuwa akipata taarifa hizi mahali fulani hivyo sioni chochote kinachokinzana na fikra ya kuwa Mungu alihusika katika kile alichoweza kukiandika"

T.V.N. Persaud
Ni Profesa wa Anatomia, na Profesa wa magonjwa na afya ya watoto, Chuo Kikuu cha Manitoba, Winnipeg, Manitoba, Canada. Ameandika na kuhariri zaidi ya vitabu 20, na amechapisha zaidi ya machapisho 181 ya Kisayansi. Ni mwandishi mweza wa kitabu cha The Developing Human (toleo la5, pamoja na Keith L. Moore). Alipokea Tuzo ya J.C.B. Grant Award mwaka 1991. Profesa Persaud aliwasilisha machapisho kadhaa ya utafiti.

"Kwangu inaonekana kwamba Muhammad alikuwa mtu wa kawaida sana, hakuwa akisoma, hakuwa akiandika, kwa hakika alikuwa mtu asiyesoma wala kuandika... tunazungumzia miaka takriban 1400 iliyopita, unakuwa na mtu asiyejua kusoma wala kuandika anatoa habari nzito za kushangaza na zenye usahihi wa ajabu, za tabia ya sayansi... Mimi binafsi sioni kama mambo haya yalitokea kwa bahatibahati tu, kuna mambo mengi sana ya ukweli na kama Dr. Moore, sina shida katika akili yangu kukubali kuwa huu ni muongozo au ufunuo wa kimungu uliomuongoza kwenye taarifa hizi" ." [1]

Joe Leigh Simpson


Ni Progesa na Mwenyekiti wa Idara ya ukunga (uzazi) na jinakolojia Texas, Marekani.

(elimuuzazi), Chuo cha Tiba cha Baylor, Houston,

Ni Rais wa Chama cha Uzazi cha Marekani. Amepokea tuzo nyingi, ikiwemo ya chama cha Maprofesa wanaoheshimiwa na jamii katika fani ya ukunga ya mwaka 1992 (Association of Professors of Obstetrics and Gynaecology Public Recognition Award). Kama ilivyokuwa kwa wasomi wengine wengi, Profesa Simpson alishangazwa sana alipogundua kuwa Quran na Hadithi vina maandiko yanayohusu fani yake. Alipokutana na Sheikh Abdul-Majeed A.Zindani, alisisitiza kuthibitisha maandiko ya Quran na Hadithi yaliyoletwa kwake.

"... hizi hadithi (maneno ya Muhammad) zisingepatikana kwa msingi wa utaalamu wa kisayansi wa zama za mwandishi husikakwa hiyo ina maana kwamba sio tu kwamba hakuna mgongano kati ya sayansi ya kijenetiki na dini (Uislamu) bali ni hakika kuwa dini (Uislamu) unaweza kuiongoza sayansi kwa kuongezea ufunuo kwenye njia za kawaida za kisayansi Katika Quran kuna maelezo yaliyothibitika karne nyingi baadaye na kuunga mkono moja kwa moja kuwa maarifa yaliyomo ndani ya kitabu hiki yametoka kwa Mwenyezi Mungu." [1]

Alfred Kroner
Profesa katika idara ya Geosciences, Chuo Kikuu cha Mainz, Ujerumani. Profesa Kroner ni miongoni mwa wanajiolojia maarufu duniani, akifahamika kwa wanasayansi wenzake kwa ukosoaji wake dhidi ya nadharia mbalimbali za wanasayansi wakubwa katika fani yake. Sheikh cAbdul-Majeed A. Zindani alikutana naye na kumpatia aya na hadithi kadhaa alizozifanyia utafiti na kuzitolea maoni.

"Nikitafakari mahali Muhammad alitoka... Naddhani haiwezekani kuwa alikuwa akijua vitu kama vile asili ya ulimwengu inayokubaliwa na kila mtu, kwa sababu ni miaka ya hivi kwaribuni ambapo wanasayansi kwa shida sana na kwa kutumia teknolojia ya kisasa iliyoendelea sana wameligundua jambo hilo." "Mtu ambaye hakuwa akijua chochote kuhusu fizikia za nyuklia miaka 1400 iliyopita nafikiri, kwa kutumia akili yake tu, asingekuwa katika nafasi ya kugundua mathalan
6

kwamba ardhi na mbingu vina asili moja, au masuala mengine mengi ambayo tumeyajali hapa... Ukikusanya pamoja maelezo yote haya yaliyotolewa na Quran juu ya mambo yanayohusu ardhi na mpangilio / uumbikaji wa ardhi na sayansi kwa aujumla, kimsingi unaweza kusema kwamba maelezo hayo yaliyotolewa ni sahihi na ni kweli kwa namna mbalimbali, sasa yanaweza kuthibitishwa na utafiti wa kisayansi. Unaweza kusema kwa uwazi kabisa kuwa Quran ni kitabu sahihi cha sayansi kwa mwanadamu sahihi. Na kwamba maelezo mengi yaliyotolewa humo hayakuweza kuthibitishwa kwa wakati huo, lakini sasa utafiti unaofanywa sasa hivi wameweza kuthibitisha kile kilichosemwa na Muhammad miaka 1400 iliyopita"

Yushidi Kusan
Mkurugenzi wa Tokyo Observatory, Tokyo, Japan. Sheikh Abdul-Majeed A. Zindani alimpatia aya kadhaa zinazoelezea mwanzo wa ulimwengu na mbingu, na uhusiano uliopo kati ya mbingu na ardhi. Alielezea kushangazwa kwake, akisema kuwa Quran inaielezea dunia kama inavyoonekana kwa mtu anayeitazama kwa upande wa juu, kila kitu kipo wazi na kipo dhahiri.

"Nasema, nimevutiwa mno na kukuta mambo sahihi ya astronomia ya kweli katika Quran, na kwa sisi wanaastronomia wa sasa tumekuwa tukichunguza sehemu ndogo sana ya ulimwengu. Tumeziweka juhdi zetu zote kujaribu kuisma sehemu ndogo sana. Kwa sababu, kwa ktumia arubini, tunaweza tu kuona sehemu ndogo sana za angabila kufikiria kuhusu ulimwengu mzima. Hivyo, kwa kuisoma Quran na kwa kujibu masuala husika, nafikiri ninaweza kupata njia yangu ya baadaye ya kuutafiti ulimwengu."

Profesa Armstrong
Profesa Armstrong anafanya kazi na shirika la anga la Marekani (NASA) na pia ni profesa wa masuala ya anga (Astronomy), Chuo Kikuu cha Kansas, Lawrence, Kansas, Marekani.

Prof. Armstrong aliulizwa maswali kadhaa kuhusu aya za Quran zinazohusu fani yake. Aliulizwa: Umejionea na kugundua mwenyewe maumbile halisi ya astronomia ya kisasa kwa kutumia chombo cha kisasa, roketi, satellite mbalimbali zilizotengenezwa na mwanadamu. Vilevile umeona jinsi mambo hayohayo yalivyoelezwa ndani ya Quran karne kumi na nne zilizopita. Sasa ni yepi maoni yako?

"Hilo ni suala gumu ambalo nimekuwa nikilifikiria tangu tulipoanza mjadala wetu hapa. Nimevutiwa sana na namna baadhi ya maandiko ya zamani yanavyoafikiana na elimuanga iliyovumbuliwa hivi karibuni. Mimi sio mwanachuoni wa kutosha wa historia ya binadamu kwamba nijiweke moja kwa moja katika mazingira yaliyokuwepo miaka 1400 iliyopita. Kwa hakika, ningependa kuliacha hilo kwamba, kile tulichokiona ni cha ajabu, kikiwa au kisiwe na maelezo ya kisayansi, lazima kuna kitu ambacho kitakuwa nje ya uelewa wetu wa maarifa ya kibinadamu katika kufafanua maandiko ambayo tumeyaona." [1]

William Hay
Profesa wa sayansi ya bahari (Oceanogprahy), Chuo Kikuu cha Colorado, Boulder, Colorado, Marekani. Profesa Hay ni miongoni mwa wanasayansi maarufu c sana wa bahari nchini Mrekani. Sheikh Abdul-Majeed A. Zindani alikutana naye na kumuuliza masuali mengi kuhusu bahari, kigawanyisho kati ya bahari kuu na bahari ndogo (upper and lower sea), na kuhusu mazingira ya chini ya bahari na jiolojia ya bahari.

"Naona ni jambo la kuvutia sana kwamba taarifa hizi zinapatikana ndani ya maandiko ya kale ya Quran Tukufu, na sikuwa na njia ya kujua kuwa yalitoka wapi. Lakini nadhani inashangaza mno kwamba yapo na kaazi hii inaendelea
8

kuyavumbua,kwa kuchunguza maana ya baadhi ya kurasa za kitabu hiki."


Na alipoulizwa kuhusu chanzo cha Quran, alijibu:

"Nafikiri lazima kitakuwa kimetoka kwa Mungu.

Durja Rao
Profesa wa Jiolojia ya Bahari katika chuo kikuu cha Mfalime Abdulaziz , Jeddah, Saudi Arabia.

Sheikh Zindani alimpatia Prof. Rao aya nyingi zinazohusu eneo la fani yake, na kumuuliza: "Unasemaje kuhusu kuwepo kwa taarifa za kisayansi ndani ya Qur'an? Mtume Muhammad aliwezaje kuyajua mambo haya karne kumi na nne zilizopita?"

"Ni vigumu kufikiri kwamba aina hii ya maarifa ilikuwepo zama hizo, takriban miaka 1400 iliyopita. Huwenda baadhi ya mambo walikuwa na taarifa nayo kwa kiwango kidogo, lakini kueleza kwa kina mambo hayo ni jambo gumu sana. Kwa hiyo, maarifa haya hayatokani na mwanadamu hata kidogo. Mwanadamu wa kawaida hawezi kutoa maelezo ya kina kuhusu maajabu haya. Hivyo, naona kuwa taarifa hii lazima itakuwa imetoka kwa chanzo chenye uwezo ulio juu ya uwezo wa chochote.

Profesa Siaveda
Profesa wa Jiolojia ya Bahari, Japan. Sheikh Zindani alimuuliza maswali kadhaa yanayohusu fani yake, na kisha akamueleza kuhusu aya za Quran pamoja na hadithi mambo ya kimaumbile aliyoyazungumzia. Swali moja lilikuwa likihusu milima. Sheikh Zindani alimuuliza kuhusu muundo wa milima; na iwapo ilikuwa imewekwa kama vigingi katika ardhi. "Ni yepi maoni yako kuhusu ulichokiona ndani ya Quran na Sunnah kuhsu siri mbalimbali za ulimwengu, ambazo wanasayansi wamezigundua leo?

"Kwangu mimi laonekana kuwa mwujiza wa hali ya juu, jambo la kuashangaza na la taabu kuaminika. Nadhani kama kweli ulichosema ndicho, kitabu hiki ni cha ajabu mno, ninakubali."

Tejatat Tejasen
Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia na Mkuu wa zamani wa kitivo cha tiba, Chuo kikuu cha Chiang Mai, Chiang Mai,
Thailand. Profesa Tejasen alisoma makala mbalimbali kuhusu Qur'an na Embriolojia ya kisasa. Alitumia siku nne akiwa pamoja na wasomi kadhaa, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, wakijadili maajabu hayo yaliyomo ndani ya Qur'an na Hadithi. Wakati wa kongamano la Tiba mjini Riyadhi Saudi Arabia, alisimama na kusema

"Katika miaka mitatu iliyopita, nilivutiwa na kuisoma Quran... Kutokana na uchanguzi wangu na kupitia yale niliyojifunza katika mkutano huu, ninaamini kuwa kila kilichoandikwa ndani ya Quraan miaka elfu moja mia nne iliyopita lazima ni kweli, na sayansi inaweza kulithibitisha. kwa kuwa Mtume Muhammad hakuwa akisoma wala kuandika, lazima Muhammad atakuwa Mtume aliyetangaza ukweli huu ulioteremshwa kwake kama nuru kutoka kwa Muumba wa kweli. Muumba huyu lazima atakuwa ni Allah.

10

Nadhani huu ni muda muafaka wa kutamka La ilaha illa Allah, hakuna mungu anayesathiki kuabudiwa isipokuwa Allah, Muhammad rasoolu Allah, Muhammad ni Mjumbe wa Allah... Kitu cha thamani zaidi ambacho nimekipata katika kongamano hili ni La ilaha illa Allah, na kuwa Mwislamu."

Dr. Maurice Bucaille


Akiwa amezaliwa mwaka 1920, Mkuu wa zamani wa Kliniki ya upasuaji, Chuo kikuu cha Paris, kwa muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kufanya uchunguzi na kufanya mlinganisho baina ya mafundisho ya Maandiko Matakatifu na elimu ya kisasa ya kisekula. Ni mwandishi wa kitabu kinachonunuliwa zaidi cha "The Bible, The Qur'an and Science" (1976). Usomaji wake wakina wa lugha za maandiko matakatifu, ikiwa ni pamoja na Kiarabu, kwa kuhusisha maarifa yake ya maandiko ya hairoglifu, umemuwezesha kufanya utafiti wa kina, ambapo mchango wake binafsi kama daktari umetengeneza hoja zenye kuondoa shaka. Kitabu chake kiitwacho, "Mummies of the Pharaohs - Modern Medical Investigations" (St. Martins Press, 1990), kilishinda Tuzo ya Historia kutoka Acadmie Franaise na tuzo nyingine kutoka Chuo cha tiba cha Ufaransa (French National Academy of Medicine). vitabu vyake vingine ni pamoja na: "What is the Origin of Man" (Seghers, 1988), "Moses and Pharaoh, the Hebrews in Egypt", (NTT Mediascope Inc, 1994); and "Rflexions sur le Coran" (Mohamed Talbi & Maurice Bucaille, Seghers, 1989)

Baada ya utafiti uliodumu kwa kipindi cha miaka kumi, Dr.


Maurice Bucaille alikihutubia chuo cha tiba cha Ufaransa mwaka 1976 kuhusu uwepo wa maelezo kadhaa ndani ya Quran yanayozungumzia fiziolojia na mfumo wa uzazi wa binadamu. Sababu yake ya kufanya hivyo ni:

"...maarifa yetu juu ya misingi hii ni kwamba, haiwezekani kufafanua jinsi maandiko fulani katika enzi za Quran yangeweza kuwa na mawazo yamegunduliwa tu katika nyakati za hivi karibuni." "Uchunguzi huo unaifanya nadharia iliyoibuliwa na wale wanaomuona Muhammad kama mtunzi Quran kuwa nadharia dhaifu isiyoweza kusadikika wala kutetewa. Mtu amabaye hakusoma aliwezaje kuwa mtunzi / mwandishi mkubwa, kwa uandishi maridhawa, katika fasihi nzima ya Kiarabu? Kisha
11

aliwezaje kutamka ukweli wa sayansi ya maumbile ambayo hakuna binadamu mwingine aliyeweza kuyavumbua wakati huo, na yote haya aliyaeleza bila kukosea hata kidogo katika uelezeaji wa suala husika?"

12

You might also like