Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 16

Sauti ya Waislamu

Prof. Sharif ataka kiini cha tatizo kichunguzwe


Fitna za kidini zimeletwa kutoka Bara Askofu ataka Uamsho wapigwe bakora Akumbusha tukio la kuchomwa Quran
Uk. 6

ISSN 0856 - 3861 Na. 1017 RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Waliodhulumiwa watoa ushahidi


Shule za vijiji vya Waislamu zilifelishwa Majina Khalid yalikatwa kwenda UDSM Muft Simba asema Baraza livunjwe Uk. 2
Na Mwandishi Wetu FITNA kubwa inasambazwa Zanzibar ambayo kama busara haikutumika, inaweza kuleta balaa kubwa. Fitna hiyo iliyolenga kuwagawa Wazanzibari kwa misingi ya Waunguja Inaendelea Uk. 3

Dhulma Baraza la Mitihani:

Sumu ya tna mbaya yasambazwa Zanzibar

Waunguja wasema wao Wasegeju Wao na Wazanaki damu yao mmoja Wataka Maalim atimuliwe serikalini

Askofu Laizer anajua waliochoma makanisa Maandamano leo


Maalim Seif Sharif Hamad

ASKOFU Thomas Laizer.

Polisi jijini Dar wakataa njia Ilikuwa yaende Baraza Mwenge Wanafunzi kupiga kambi Wizarani

Ni shahidi namba 1 mahakamani Zanzibar Aseme kikombe cha Babu kimeishia wapi Ndio awaparamie vijana wa Kiislam Arusha Waislam wanajitakia wenyewe kutukanwa

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR
kipaumbele kanisa kupitia maakiano yenu ya kisadi ya Memorandum of Understanding (MoU) ambayo mnaitumia k u w a k e b e h i Wa i s l a m u kwamba wao hawakuomba ndio maana hamuwachotei mabilioni kutoka hazina kama mnavyomchotea Pengo na akina Elinaza Sendoro. Kila siku maaskofu, mapadiri na wachungaji hupiga siasa hadharani na ndani ya makanisa yao. Tena wakati mwingine wakikutukaneni na kukukemeeni. Kimya!! Mlidhani watakukumbatieni na kukuimbieni ngonjera na tenzi za kukusifuni.

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012


Mnayo mambo mengi ya msingi na ya maana ya kuwashughulisha. Ukiacha hili la kutoa majibu juu ya muungano, lipo hili la mfumokristo ndani ya Baraza la Mitihani na serikali kwa ujumla, wizi na usadi ndani ya serikali kuu na katika serikali za mitaa. Hayo pekee yatawafanya mlale hoi katika kuyashugulikia. Lakini haitakuwa kuchoka bure kwa sababu mnachopiga kelele juu ya amani ya nchi hii na kupata maendeleo, Abadan hakitawezekana bila ya masuala haya kupatiwa ufumbuzi.

AN-NUUR

MAONI YETU

Kuweka sumu badala ya chumvi sio kosa la kibinadamu


MTU akizidisha chumvi katika chakula au ikapungua, hiyo yaweza kuwa ni kosa la kibinadamu. Lakini huwezi kuweka sumu, ukaweka mbolea aina ya urea, ukasema ni kosa la kibinadamu kwa vile zote nyeupe. Itabidi utuambie kwanza, sumu hiyo ulifuata nini jikoni. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, katika kutaka kukwepa tatizo la msingi ndani ya NECTA kwamba limesheheni Wakristo katika nafasi zote nyeti na kwamba Wakristo hao wamekuwa wakiwahujumu Waislamu, amekuja na maelezo kwamba kilichowapora watoto wa Kiislamu A zao na kuwapa F, ni kosa la kibinadamu ambalo mtu yeyote anaweza kulifanya. Tunachomwambia Katibu Mtendaji huyo Dr. Joyce Ndalichako ni kuwa kwa hapa ilipokia, inabidi Baraza la Mitihani lisaidiwe. Hilo la somo moja alilorekebisha, ni kielelezo tu cha matatizo makubwa yaliyo ndani ya Baraza hilo. Kwa muda mrefu sasa Baraza linatuhumiwa kuhujumu Waislamu na kupendelea Wakristo kwa namna mbalimbali. Sasa tuhuma kama hizi haziwezi kuondolewa na maelezo aliyotoa Ndalichako. Ni lazima Baraza lisaidiwe kwa kufanyika uchunguzi. Kama alivyosema Mufti Sheikh Issah Shaaban Simba, na kama wanavyosema Waislamu wote katika nchi hii, kwa nini imekuwa Baraza ni miliki ya Wakristo toka limeundwa? Hapana shaka ukifanyika uchunguzi huru na makini, ndio utalisasha Baraza na kurejesha imani ya wadau wake. Septemba 11 ya kienyeji Matukio ya kuchoma Quran ni mengi nchini hapa Bara na Visiwani. Na wanaofanya hivyo sio watu wasiofahamika, wahuni au waumini wa kawaida wa Kikristo. Ni wachungaji na mapadiri. Tena hufanya hadharani kwa jeuri na kibri. Labda tutoe mifano. Katika tukio la Mwanza, aliyechoma Quran ni mchungaji aliyedai kuwa anachoma kitabu cha mashetani na majini. Hatukusikia serikali ikilikemea jambo hili. Hatukumsikia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa kauli kali za kisiasa akitahadharisha juu ya hatari ya uchochezi huu wa kidini. Hali ilikuwa hivyo hivyo kule Mto wa mbu Arusha. Aliyechoma Quran hadharani huku anatukana na kutoa kashfa kuwa Quran ni kitabu cha majini, alikuwa mchungaji. Kikwete kimyaa! Dr. Bilala kimyaa! Dr. Shein kimyaa! Lakini ghafla, watu hao hao wamecharuka. Wamekuja juu. Kila mmoja wao anaibuka na kujitahidi kutoa maneno makali kadiri iwezekanavyo ili huko waliko maaskofu watambue kwamba naye kasema. Ajisajili kuwa kawakemea Waislamu. Sisi tunasema, wanachosema Wazanzibari ni kuwa wanataka muwajibu maswali ya msingi kabisa juu ya huu muungano. Sasa kama Mwalimu Nyerere mnayeogopa kuukasirisha mzimu wake hakuwaachia majibu, si kosa la Waislamu. Msiwaparamie. Jibuni maswali mnayoulizwa juu ya muungano. Vurugu kubwa imetokea juzi hapa kule Tandahimba na Ikwiriri. Watu wameuliwa na mali kuharibiwa. Tatizo wizi na usadi wa watumishi wa serikali na taasisi za umma. Ni wizi na ufisadi huo huo ambao umepelekea mmeparurana Bungeni na kutimuana katika Baraza la Mawaziri. Sasa kama mambo yenu yamekukalieni vibaya, msidhani yatakunyookeni kwa kuwavamia Waislamu. Ingekuwa kuchoma m a k a n i s a , Wa i s l a m u si wangechoma yale yanayozunguka msikiti wa Mwembechai mlipotuma polisi kuwapiga risasi Waislamu na kuwauwa? Mliona fahari, mkaona ndio salama yenu kulipa

Msituletee Septemba 11 za kienyeji

Baraza la Mitihani livunjwe-Bakwata


Na Mwandishi Wetu
BARAZA Kuu la Waislamu Ta n z a n i a ( B a k w a t a ) limeungana na Waislamu kupaza sauti kwamba Baraza la Mitihani livunjwe mara moja. Kwa nini livunjwe? Sheikh Issah Bin Shaabani Simba amesema kuwa kutokana na ushahidi uliopo, Baraza hilo limekuwa likiwahujumu Waislamu. Sheikh Simba amesema kuwa Waislamu hawana tena imani na Baraza hilo, na kwamba njia pekee ya kulisasha ni kuunda Tume huru kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, Mufti Issah Shaabani Simba amesema kuwa kwa sasa kinachotakiwa ni kujiuzulu mara moja Katibu Mtendaji wa Baraza (Necta) ili kulinda heshima ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha Mufti Simba ametaka watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa kompyuta ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja. Lakini pia hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa ya kuwahujumu Waislamu. Katika kuliunda upya Baraza baada ya kufumuliwa, Mufti amesema kuwa Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini. Amesema, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa. Amesema, takwimu zinaonyesha kuwa Makatibu Watendaji na Manaibu wao wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973 mpaka hii leo. Ta k w i m u t u n a z o , amesema Mufti mbele ya waandishi wa habari akisisitiza kuwa Waislamu hawasemi jambo ila kwa kuwa na ushahidi madhubuti. Tu n a i o m b a S e r i k a l i iwape nafasi wanafunzi wote ambao baada ya matokeo yao kubadilishwa wamekuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu waruhusiwe kuomba mikopo bodi ya mikopo, tunalisema hili kutokana na muda wa kuomba mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kwisha. Katika taarifa yake Mufti Simba amesema kuwa yeye pamoja na Bakwata wapo pamoja na Waislamu katika kupinga dhulma hii. Amesema, tatizo haliwezi kuwa katika somo moja bali inaonekana kuwa dhulma imekuwa ikifanyika katika masomo yote na katika hatua mbalimbali za kutoa matokeo

Wameungana na nguvu ya umma wanakusokoteeni kitanzi. Wamewazingira ndani na nje ya vibanda na vigwanda vyenu. Sasa msidhani mtasalimika kwa kuwaparamia Waislamu. Marekani ilipotaka kuwabamiza Waislamu dunia nzima, ilikuja na Septemba 11, ikaja kuibuka na Patriot Act ambayo ilitulazimisha na sisi kuwa na yetu. Inavyoonekana sasa mnataka nanyi kutuletea Septemba 11 yenu ya kienyeji. Tunashauri, kama huko ndio mnakoelekea, mkae kitako mtafakari upya.

Limekuwa kama kijiwe cha Makanisa Subra ina mwisho wake. Tunasema basi Ufanyike uchunguzi kwa miaka 10 iliyopita
ndio maana wanataka iundwe Tume na uchunguzi ufanyike angalau kwa miaka 10 iliyopita. Bakwata, linawapongeza na kuwaunga mkono Taasisi zote za Kiislamu nchini kwa jitihada ya kuligundua hili na hatua walizozichukuwa dhidi ya Baraza la Mitihani na kuufahamisha umma wa Kiislamu juu ya kadhia hii. Amesema Mufti Simba na kuongeza akisema, Baraza tunawapongeza taasisi zote za Kiislamu na tunasema Bakwata tuko nyuma yao kwani kauli yao ndio kauli yetu. Akizungumzia hoja na kauli ya utetezi ya Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Joyce Ndalichako, kwamba Baraza lina utaratibu mzuri wa usahihishaji na program za komputa ila tu ilitokea dosari ya kibinadamu, Mufti amesema kuwa mifumo ya usahihishaji sio maneno matakatifu kwamba haiwezi kuchezewa kutokana hila za binadamu. Ni mifumo iliyowekwa na binadamu, na binadamu huyo huyo anaweza kuibadilishabadilisha vyovyote anavyotaka, ndio maana Waislamu wanataka kwanza Baraza lichunguzwe kwa miaka 10 iliyopita na likiundwa upya uwepo wa Waislamu na Wakristo uzingatiwe. (Soma makala Uk. 8 & 9)

Habari

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale

Maandamano leo Sumu ya tna mbaya


Inatoka Uk. 1 na Wapemba imekuwa ikisambazwa kupitia vipeperushi ambavyo vimesambaa katika maeneo kadhaa mpaka katika osi na taasisi za serikali (SMZ). Wa t u w a U n g u j a wamechoshwa na adha za Wapemba hapa Unguja, kimesema kipeperushi kimoja kama kichwa cha habari. Katika kipeperushi hicho inaelezwa kuwa watu wa Unguja asili yao ni Wasegeju kutoka Bara kwa hiyo wao hawaoni tabu kukaa katika muungano na ndugu zao wa Kichagga, Wazanaki na wengineo kutoka Bara. Ikaelezwa katika karatasi hiyo ambayo An nuur imebahatika kuiona kuwa wasiotaka Muungano ni Wapemba. Kwa upande mwingine ameshutumiwa Rais Mstaafu Aman Abeid Karume kwamba yeye ndiye aliyeleta kura ya maoni ambayo imezaa serikali ya umoja wa kitaifa na kuleta hali ya maelewano ya kisiasa na kijamii visiwani Zanzibar. Ikaelezwa kuwa alichofanya Karume ni kama balaa na nuksi kwa Zanzibar na hivyo kusema kuwa kura yenyewe ya maoni ilikuwa batili kwa hiyo na kilichozaliwa ni batili pia. Katika hali hiyo, waandishi wa kipeperushi hicho wamemtaka Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumwomba Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein amtimue Maalim Seif Sharif Hamad katika serikali yake na badala yake ampe Pemba akatawale Wapemba. Sisi watu wa Unguja tumechoshwa kuishi na Wapemba katika kisiwa chetu cha Unguja kwani

WAISLAMU Jijini Dar es Salaam leo wanatarajia kufanya maandamano ya amani wakiitaka Serikali kufanya mabadiliko katika Baraza la Mitihani. Maandamano hayo ilikuwa yagawike katika makundi mawili ambapo, kundi moja lingekwenda Baraza la Mitihani Mwenge huku wengine wakielekea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Waislamu wanadai kuwa Baraza hilo limekuwa likiwahujumu kutokana na kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na Wakristo. Hata hivyo, habari tulizo zipata tukienda mitamboni ziliarifu kuwa polisi wamekataa kuyaruhusu kama yalivyokuwa yamepangwa awali kwa sababu za kiusalama. Wamesema, kutawanyika kwa njia za maandamano hayo katika njia tofauti, itakuwa vigumu kwa vyombo vya usalama kudhibiti hali ya usalama. Badala yake polisi waliruhusu kufanyika mkutano wa hadhara Mnazi mmoja bila ya maandamano. Hata hivyo, viongozi wa Waislamu waliokuwa katika majadiliano na polisi waliomba kuwa Waislamu waanze maandamano yao msikiti wa Magomeni, Kichangani (TIC) kuelekea katika mkutano mara baada ya swala ya Ijumaa. Habari kutoka ndani ya kikao hicho ziliarifu kuwa polisi walitarajia kutoa majibu ya maombi hayo mapya ikapo saa 12 jioni jana. Hadi tunakwenda mitamboni saa 11 jioni ilikuwa haijafahamika polisi wangekuja na jawabu gani. Akitangaza kuwepo kwa maandamano hayo mbele ya Maimamu pamoja na vijana wa Kiislamu katika Msikiti wa Kichangani Magomeni (T I C), Jumanne wiki hii, Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Kiislamu Taifa, Ustadh Shaaban Mapeo, amesema wanataka Baraza hilo liundwe upya katika namna ambayo Waislamu watakuwa na imani nalo. Alisema, maandamano hayo yatagawanywa katika makundi mawili ili kuweza kukisha ujumbe wao katika kwa Baraza la Mitihani la Tanzania na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wakati mmoja. Mapeo amesema, kundi la kwanza litakuwa ni kutoka katika Misikiti ya Wilaya ya Kinondoni, ambapo mara baada ya ibada ya swala ya

yasambazwa Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Kiislamu Taifa, Ustadh Shaaban Mapeo.


Ijumaa wataelekea Baraza la Mitihani la Taifa lililopo maeneo ya Mwenge. Na kundi la pili, alisema litajumuisha Waislamu kutoka katika Misikiti ya Wilaya za Ilala na Temeke, nao baada ya swala ya Ijumaa wataandamana kuelekea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Sababu ya kuitana hapa ni kuratibu maandamano ya Waislamu, yatakayo fanyika siku ya Ijumaa hapa Jijini, lengo kuu la maanadamano hayo ni kukisha kilio chetu Serikalini kuwa hatuna imani na Baraza la Mitihani, kutokana na kuwahujumu wanafunzi wa Kiislamu nadhani wote mnajua hili. Alisema Mapeo. Alisema, makundi hayo mawili ya maanadamano yatakuwa na barua maalum za kukabidhi kwa watendaji wakuu wa Baraza la Mitihani na Wizara ya Elimu, ambapo katika Baraza wamemwomba Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Joyce Ndalichako, kupokea maandamano hayo na Wizara ya Elimu, wamemwomba Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa, kupokea maandamano hayo. Alisema, baada ya kufikisha barua hizo kwa viongozi husika, maandamano yataelekea katika viwanja vya Kidongo Chekundu Kariakoo, Jijini ambapo viongozi wa Jumuiya na taasisi wataongea na Waislamu. Ustadh Mapeo amesema, hapatakuwa na siasa kwani umma wa Kiislamu umeshachoka na dhulma wanayofanyiwa. Naye Amiri wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA), Ustadhi Japhar Mneke, ametsema, ikiwa Serikali haitasikia kilio cha Waislamu katika madai watakayoyafikisha siku ya leo, wataitisha maandamano mengine ya wanafunzi nchi nzima. Alisema, maandamano hayo yatafanyika hapa Jijini (Dar es Salaam) ambapo wanafunzi kutoka mikoa yote ya Tanzania watajumuika na wenzao wa hapa kisha kupiga kambi Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi mpaka Baraza la Mitihani lifumuliwe zile nafasi nyeti na vikao nyeti vya Baraza hilo wasikae Wakristo watupu. Jumapili wiki iliyopita Wa i s l a m u w a l i k u t a n a katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, ambapo maelfu ya Waislamu waliohudhuria waliwataka viongozi wao kuitisha maandamano ya amani wakisema, wapo tayari kwenda Baraza la Mitihani na Wizara ya Elimu, kukisha kilio chao kwa Serikali ili Baraza hilo lifumuliwe.

ni watu wasio na fadhila y o y o t e . Tu n a k u o m b a Rais wa Jamhuri fanya mazungumzo na Rais Shein afikie hatua ya Maalim Seif apewe kisiwa chake cha Pemba akawatawale Wapemba wenzake. Imesema sehemu ya kipeperushi hicho ambacho kimezagaa mikononi mwa watu wengi. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa kipeperushi hicho na vingine vya namna hiyo ni kazi ya wale ambao wangependa kuona Wazanzibari wakiparurana na kutoana ngeu badala ya kufanya kazi zao kwa amani na maelewano kujiletea maendeleo. Wa p o w a n a o s e m a pia kuwa huenda wanaosambaza kipeperushi hicho ni makachero wanaotumiwa ili kuzima hoja ya muungano ambayo sasa inaonekana kuwa mwiba kooni mwa serikali na haina majibu ya hoja zinazoibuliwa. Wa n a o t o a h o j a h i i wanasema kuwa propaganda hii imelenga kuwagawa hata viongozi wa serikali na wa kisiasa ili hata jambo hili likiibuka Bungeni au katika vikao vya kiserikali na kisiasa, Wajumbe wa Zanzibar wasiwe na kauli moja. Kwamba hata kama ni CCM, basi wana-CCM Unguja wakinzane na wanaCCM Pemba huku Bara wakisimama na msimamo mmoja. Wagawe uwatale inatimia kwa wepesi bila kutoa jasho. Vyovyote itakavyokuwa, viongozi wa SMZ, viongozi wa kijamii na kidini Unguja na Pemba pamoja na Wazanzibari kwa ujumla, wametakiwa kuwa makini wasije kutiwa sumu ya tna, chuki na farka wakabaki wakichapana bakora na marungu ya polisi huku wanaopika fitna hiyo wakichekelea.

Askofu Thomas Laizer Na Omar Msangi w azu ng u mzaji k atik a kipindi hicho walikuwa Sheikh Ponda Issa Ponda na Ramadhani Sanze ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Katika mazungumzo yao Ponda na Sanze waligusia malalamiko na madai mbalimbali ya Waislamu nchini huku wakionyesha ushahidi wa hujuma wanayofanyiwa Waislamu na Baraza la Mitihani. Mchangiaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Fred Mwarengo akipiga simu kutoka Singida aliwarushia makombora Waislamu akisema kuwa Waislamu hawana wa kumlaumu bali walaumu ujinga wao. Akasema, yeye alisoma na Waislamu na kuwaona ni watu wajinga tu. Shuleni badala ya kusoma wao hukalia kuswali swali tu na kukaa misikitini. Lakini pia pamoja na ujinga wao, hawataki kusoma na wenzao katika discussion, bali hujadiliana wenyewe kwa wenyewe (kwa maana ya wajinga kwa wajinga). Bwana Fred anashangaa na kushindwa kupata picha, discussion ya

KIPO kisa cha binti msaidizi wa nyumbani (house girl) na mh u d u mu wa bustani (shamba boy) waliokuwa wameajiriwa na tajiri mmoja. Wawili hawa walifanya kazi kwa tajiri yao kwa muda mrefu na wenyewe wakatokea kuelewana. Hawakukwaruzana wala kugombana hata mara moja. Yule kijana akampenda sana binti hata siku moja akajitutumua akamwambia anataka waoane.

Shamba boy na house girl, waoane! Nashindwa kupata picha hiyo itakuwa familia ya namna gani. Naona wewe tafuta mke wa hadhi kidogo, nami nisubiri kupata mume asiye na maisha duni kama yangu. Lilikuwa jibu la binti (house girl) kwa kijana. Jumatatu katika kipindi cha Baragumu kinachoendeshwa na Channel Ten, wageni

watu wajinga kwa wajinga itakuwa na tija gani kama sio kugawana ujinga walio nao Waislamu na hatimaye kufeli mitihani! Labda niseme hayo sio mawazo ya Fred pekee. Ndivyo Waislamu wanavyotizamwa katika nchi hii. Na labda niseme pia kuwa huenda akina Fred hawana hatia. Sio wa kulaumiwa, bali wa kulaumiwa ni Waislamu wenyewe kwa ujinga wao kama alivyosema Fred. Mohamed Said ameandika sana juu ya dhulma wanayofanyiwa Waislamu nchini mpaka historia na mchango wao katika kupigania uhuru umefukiwa. Ameandika Padiri Dr. John Sivalon akionyesha jinsi mawakala wa kanisa walivyo wahujumu na wanavyoendelea kuwahujumu Waislamu. Wa m e a n d i k a m p a k a watu wa nje, Wazungu, kuonyesha jinsi Rais wa kwanza wa nchi hii Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyotoa ahadi na kuitekeleza ya kulipa upendeleo kanisa. Leo pamoja na hujuma yote waliyofanyiwa, Waislamu nao wamo tu, kuimba wimbo wa Baba wa Taifa! Mifano ya majina ya Halima, Aisha na Ismail yaliyokutwa Kilakala, Umbwe na shule nyingine za serikali yakitumiwa na akina Mary na Joseph, ni mingi na imesemwa sana hadharani. Hayo ni machache katika mengi unayoweza kusema juu ya hujuma kwa Waislamu katika nchi hii. Swali ni je, baada ya kuyajua yote hayo, Waislamu walifanya nini? Wamefanya nini? Kwamba Baraza la Mitihani la Tanzania limedhibitiwa na Wakristo toka kuanzishwa kwake, sio habari. Ishapitwa na wakati. Kama kwa

Askofu Laizer anajua waliochoma makanisa


namna yoyote Waislamu wangekuwa waelewa wa mambo, wasingekuwa watu wa kulalamika leo. Wangekuwa washachukua hatua zamani ambazo zingepelekea Baraza hilo kuwa katika sura na utendaji unaokubalika na kuaminika. Sasa huenda kasema kweli Fred Mwarengo, kwamba ingekuwa wanafunzi wa Kiislamu wangekuwa wanakaa na kufanya discussion na watoto wenzao wa Kikristo, leo wasingekuwa watu wa kukubali kuona takriban wakuu wa shule zote za serikali nchini wanakuwa Wakristo huku wakiendesha mfumokristo shuleni kama ilivyojitokeza shule ya Ndanda. Yaweza kuwa kweli. Kwamba kama wanafunzi Waislamu wangekuwa wanafanya discussion na wanafunzi wenzao katika shule na Vyuo Vikuu, huenda nao wangejua kanisa linafanya mbinu gani kuhakikisha kuwa nafasi zote nyeti serikalini na katika taasisi za uma zinashikwa na Wakristo. Na zaidi wangejua hata njia ya kupita kuhakikisha kuwa Masheikh wao hawapuuzwi na kudharauliwa kama walivyofanyiwa Sheikh Maalim Ally Bassaleh walipotaka kumwona Waziri wa Mambo ya Nje, Mheshimiwa Bernard Membe. Kama nilivyotangulia kusema, haya anayosema Fred sio mawazo yake pekee bali ndivyo j a m i i y a Wa i s l a m u inavyotizamwa na wananchi wenzao Wakristo na hii hudhihirishwa na kauli za viongozi wao ambao hawaishi kuwakejeli, kuwatukana na kuwasingizia mambo Waislamu. Hivi sasa kuna hali isiyo ya kawaida Zanzibar. Vurugu zilizofanyika hivi karibuni kufuatia

Habari

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

kukamatwa kwa kiongozi mmoja wa Uamsho Sheikh Mussa Abdallah Juma, zilisababisha kuchomwa kwa makanisa. Mengi yamesemwa sana juu ya kadhia hiyo. Wakati jumuiya ya Uamsho ikisema kuwa haihusiki kwa namna yoyote na uchomaji makanisa, wapo ambao wameshikilia kwamba ni Uamsho wanaohusika. Na wenye msimamo huu ndio ambao wamekuwa wakipewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari. Baada ya ile kauli kali ya Askofu Valentino Mokiwa akishinikiza kutiwa adabu Uamsho, ameibuka kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Arusha Askofu Thomas Laizer akidai kuwa anawajua wanaoshambulia na kuchoma moto makanisa. Akinukuliwa na mwandishi John Mhala wa gazeti la HabariLeo la Jumatatu Juni 4, Askofu Thomas Laizer alisema kuwa anazo taarifa za kutosha na za uhakika kuwa kwa sasa kuna vijana zaidi ya 300 wa Kiislamu eneo la Unga Limited katika msikiti mmoja wakifanya mazoezi ya kareti tayari kujiandaa kufanya uhalifu katika makanisa. Misikiti ni mahali pa kufanya ibada. Ni mahali Waislamu wanakusanyika kuswali swala tano, swala ya Ijumaa, tarawehe, swala za idd, kufanya Itqaaf, kusoma Quran na ibada mbalimbali wakimnyenyekea Mola wao. Lakini Askofu Laizer anasema kuwa kwa Waislamu sasa misikiti ni mahali pa kupangia uhalifu. Sasa maadhali jambo hili amelisema akilihusisha na uchomaji makanisa Zanzibar, basi huenda atakuwa shahidi muhimu sana pindi kesi ya watuhumiwa wa uchomaji Inaendelea Uk. 11

Misri wataka serikali ya Kiislamu


Shaq alikoroga kutaka kuondolewa Quran Morsi asema hatasalimu amri
adhabu ya kifungo cha maisha, ambayo imetafsiriwa na wamisri kuwa ni adhabu nyepesi. Ahmad Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak na Mohammed Morsi wa chama cha Uhuru na Uadilifu ambalo ni tawi la kisiasa la kundi la Ikhwanul Muslimin nchini Misri, wanatarajiwa kuchuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Juni 16 na 17. Ahmad Shafiq, amejiingiza katika wakati mgumu kwa wananchi wa Misri baada ya hivi karibuni kutaka aya za Qurani ziondolewe katika vitabu vya shule Misri. Shaq aliyeingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa Rais nchini Misri, ametoa pendekezo hilo lililowashangaza wamisri la kutaka aya za Qurani Tukufu ziondolewe katika vitabu vya shule. Imeariwa kuwa katika mahojiano na televisheni y a K i k r i s t o y a C T V, Shaq alidai kuwa sababu ya kuondolewa aya hizo ni kuwa ni vigumu kwa wakristo kuzihifadhi. Sheikh Yusuf Al Badri, mmoja kati ya wahubiri wa Kiislamu nchini Misri amesema matamshi ya Shaq, hayafai hasa kwa kuzingatia anagombea kiti cha Urais. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais Misri itafanyika Juni 16 na 17 ambapo Shafiq atachuana na mgombea wa Ikanul Muslimin Mohammad Morsi. Aidha maelfu ya watu wamefanya maandamano dhidi ya Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak mjini Cairo Misri wakidai kuwa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak umekia kikomo akimaanisha kwamba hawataki kusikia mabaki yeyote ya Utawala huo wa zamani ukishika madaraka ya nchi hiyo. Maandamano hayo yaliambatana na kuchomwa moto osi za Bw. Shaq. Maafisa wa zimamoto walitumwa haraka kwenye osi hiyo na kufanikiwa kuzima moto huo. Jumatatu wiki hii miji yote ya Misri ilishuhudia maandamano ya wananchi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Misri. Wa a n d a m a n a j i h a o wanaamini kuwa Tume hiyo imechakachua matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa uliofanyika Mei 23 na 24. Faruq Sultan, Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Misri alitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo ambapo mgombea wa Ikhwanul Muslimin, Mohamed Morsi ameongoza akifuatiwa na Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak, Ahmad Shaq. Kwa mujibu wa matokeo hayo, hakuna mgombea aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, hivyo wagombea hao wawili

Kimataifa

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Ahmad Shaq

Mohamed Morsi utawala huo. CAIRO Kabla ya hapo, Ali MSEMAJI wa chama cha Uhuru na Uadilifu cha K h a f f a j i , m m o j a w a Misri amesema kuwa, viongozi waandamizi wananchi walio wengi wa chama cha Uhuru wa nchi hiyo wanataka na Uadilifu cha Misri serikali ya wananchi chini ameyataja matamshi ya ya misingi ya Uislamu. Ahmad Shafiq, Waziri Waleed el Haddad, M k u u w a m w i s h o ameiambia televisheni ya wa utawala wa Hosni Press TV kuwa, wananchi Mubarak na mgombea wa Misri ambao wana Urais nchini humo, kuwa ustaarabu mkongwe wa ni kichekesho na kusisitiza dini tukufu ya Kiislamu, kuwa, vyama vya upinzani w a n a p e n d a k u o n a nchini Misri vitaendelea mafundisho ya Uislamu, na maandamano yao hadi ya kutotenganishwa dini vitakapofanikisha malengo na siasa, yanatekelezwa ya mapinduzi ya wananchi nchini humo na wanapinga wa nchi hiyo ambayo ni u t a w a l a w a k i s e k u l a pamoja na usawa, uhuru na uadilifu. unaopinga dini. Itakumbukwa kuwa Msemaji huyo ambaye pia ni mtaalamu wa masuala Ahmad Shafiq, ametoa ya kisiasa ameongeza tuhuma kali dhidi ya chama kuwa, kamwe wananchi cha Uhuru na Uadilifu na wa Misri hawatokubali pia amewataka wananchi kurejea utawala wa Hosni wa Misri wakubaliane na Mubarak, kwa mlango hukumu ya mahakama ya wa nyuma na kwamba nchi hiyo iliyowaondolea w a t a s i m a m a k i d e t e tuhuma wana wawili kukabiliana na njama zote wa Hosni Mubarak na za kuurejesha madarakani kumhukumu Mubarak

Qurani kusambazwa katika shule za Uingereza

wameingia katika duru ya pili ya uchaguzi huo iliyopangwa kufanyika Juni 16 na 17. Naye Naibu kiongozi wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la Harakati ya Ikhwanul Muslimin, Muhammad Morsi, ambaye ni mgombea wa kiti cha Rais wa Misri kwa tiketi ya chama hicho amesema kamwe hatasalimu amri mbele ya vitisho vya Marekani na washirika wake. Imeelezwa kwamba iwapo Ahmad Shafiq, atakuwa Rais wa nchi hiyo maana yake ni kuwa taifa la Misri litakuwa limerudi tena katika zama za udikteta wa Husni Mubarak. Ta y a r i m s e m a j i w a harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini humo, Mahmood Ghazlan, ametangaza kuwa harakati hiyo inakusudia kumchukulia hatua za kisheria Ahmad Shafiq, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya harakati hiyo na mgombea wake Muhammad Morsi, katika moja ya mikutano na waandishi wa habari.

LONDON WA Z I R I w a E l i m u Uingereza, Michael Gove, amesema litakuwa jambo bora iwapo wafadhili wataunga mkono mpango wa kutuma nakala za Qurani Tukufu katika shule nchini humo. Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph la London, Gove, ambaye amekuwa akiunga mkono usambazwaji Bibilia katika shule za Uingereza amesema wizara yake inatafakari suala za

kusambaza vitabu vingine vitakatifu kama Qurani katika shule za nchi hiyo. Iwapo watu w a t a w a s i l i s h a mapendekezo, wafadhili na wengine, basi tunaweza kusambaza nakala za Qur ani katika shule, amesema waziri huyo. Katika siku za hivi karibuni, Wizara ya Elimu Uingereza ikishirikiana na wafadhili Wakristo wamesambaza nakala 24 za Bibilia katika shule za nchi hiyo.

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Mhandisi wa vurugu Zanzibar ni Nyerere


wanapata shida sana kutafsiri kwa usahihi kile kinachoendelea Zanzibar h i v i s a s a . Ta t i z o s i y o mihadhara ya Uamsho kama inavyodhaniwa na wengi. Watanzania wanatekwa zaidi na matukio ya Zanzibar, kama yanavyowasilishwa na vyombo vya habari, lakini siyo masuala ya Zanzibar. Wengi hawajui kwa nini matukio hayo yanatokea kwa namna yanavyotokea! Mhandisi wa vurugu zote hizo zinazotokea Zanzibar leo, ni baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini bahati mbaya sana Watanzania wengi hawajui hilo. Bila ya kufahamu, wamejikuta wakipoteza muda mwingi kujadili matokeo ya tatizo, badala ya chanzo chake. Baadhi yetu, bila kutambua, tumejikuta tukifanya juhudi kubwa ya kujenga kuta, badala ya madaraja kati ya Watanganyika na Wazanzibari. Nimejaribu, japo kwa uchache, kuchimba kidogo kutoka kwenye historia ya Nyerere na Zanzibar, ili kuwaweka sawa wanaofuatilia mjadala huu, wasipoteze mwelekeo na kujikuta wakizingatia zaidi propaganda zinazolenga kuhamisha mazingatio yao kutoka kwenye msingi halisi wa tatizo la Zanzibar. Inaonekana Mwalimu Nyerere alikuwa mwanasiasa maarufu sana duniani, lakini ni kiongozi wa Kiafrika aliyeeleweka kidogo mno. Mamilioni ya Waafrika waliopigania ukombozi kutoka kwenye makucha ya ubeberu wa Kimagharibi, waliamini kwamba Nyerere alikuwa mwanafikra na mpambanaji halisi wa ukombozi wa Afrika. Wengine walimchukulia kama kiongozi wa Kiafrika aliyejitoa kwa dhati kutumia rasilimali za nchi yake, ili kulinusuru bara la Afrika kutokana na ubeberu wa nchi za Ulaya na ubaguzi wa rangi. Kwa mujibu wa baadhi ya Wanafalsafa wa Siasa, Nyerere alikuwa ni mwanasiasa bobezi, mwanafikra mashuhuri, mwandishi, mtetezi na msemaji wa Afrika. Lakini katika medani za Ulaya na Ukristo, Nyerere alikuwa ni mpambanaji makini dhidi ya kile kilichoaminika kama Ukomunisti visiwani Zanzibar. Dhana hii ililetwa na Serikali ya Marekani. Kitabu US Foreign Policy and Revolution: Creation of Tanzania kilichoandikwa na Amrit Wilson, kimechua baadhi ya nyaraka rasmi za Serikali ya Marekani, zikiwemo za CIA ambazo zimemtaja Nyerere kama kiongozi pekee wa Kiafrika, atakayeweza kukandamiza Uislamu visiwani Zanzibar, ambao umelinganishwa kimakosa na Ukomunisti wakati wa kipindi cha vita baridi. Kabla ya kuundwa Tanzania mwaka 1964, Nyerere alisikika mara kwa mara na akanukuliwa akisema anatamani angelikuwa na uwezo wa kuinyofoa Zanzibar kutoka bahari ya Hindi na kuitupia mbali. Tanzania ilipata misaada mingi zaidi kutoka nchi za Magharibi kuliko nchi yoyote ya Kiafrika wakati wa Nyerere. Lakini kwa Waislamu wengi wa Zanzibar, Nyerere alikuwa ni mpiganaji mwaminifu wa Kikatoliki dhidi ya Uislamu visiwani humo. Kitabu The Course of Islam in Africa kilichoandikwa na Mervyln Hiskett, kinabainisha wazi kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulilazimishwa na Nyerere, ikiwa ni sehemu ya Crusade dhidi ya Uislamu visiwani Zanzibar: Muungano ulilazimishwa kwa Waislamu wa Zanzibar na Nyerere, mpiganaji wa Kikristo na Muuaji wake

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Na Said Rajab WATA N Z A N I A w e n g i wasiofahamu ajenda ya siri iliyojificha kwenye Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964,

Na Mwandishi Wetu

PROFESA Abdul Sharif ametaka kiini cha kinachoitwa vurugu Zanzibar zilizopelekea k u c h o m w a moto makanisa kichunguzwe badala ya kupiga propaganda. Aidha, amehoji na kushangaa kuona baadhi ya viongozi wa makanisa wakitaka masheikh wakamatwe na kupigwa mijeledi na virungu kabla hata ya kukishwa mahakamani. I was dismayed when I read the story by Mwinyi Sadallah in the Nipashe of 31st May, 2012 quoting the Archbishop of the Anglican Church in Tanzania, Dk. Valentino

Prof. Sharif ataka kiini cha tatizo kichunguzwe


Fitna za kidini zimeletwa kutoka Bara Askofu ataka Uamsho wapigwe bakora Akumbusha tukio la kuchomwa Quran
kanisa anataka watu waadhibiwe kwa kucharazwa mijeledi na polisi kabla hata ya kufikishwa mahakamani. Japo Profesa hakufafanua, lakini ni mambo kama haya ambayo anasema inabidi jambo hili lichunguzwe kwa undani kwani inavyoelekea kuna mambo yamejificha Mokiwa, saying that the suspects wakamatwe, wapigwe bakora na polisi na baadaye wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Amesema Prof. Sharif katika makala yake aliyoipa jina The Zanzibar Riots, the Union, and Religious Tolerance kwamba ni jambo la kushangaza kwamba kiongozi wa

Inaendelea Uk. 7

yanataka kuibuliwa ni kukata mzizi wa tna. Katika makala yake hiyo ambayo An nuur inaitoa kwa Kiingereza kama ilivyo, Prof. Sharif anasema kuwa Wazanzibari si watu wa kufundishwa namna ya kuishi na Wakristo kwani wamekuwa nao kwa mamia ya miaka na hapakuwa na tatizo. A m e s e m a ,

Zanzibar haikuwa na vurugu za kidini bali zimepandikizwa kutoka Bara kuanzia mwaka 1987. Akifafanua amesema, mwaka huo chama tawala kilifanya semina yake huko Bara ambapo ndani ya semina hiyo ilitolewa pendekezo la kifedhuli kwamba Sheria za Kiislamu zilizopo ndani ya Quran zibadilishwe. Katika kuonyesha kuwa semina hiyo iliyofanyika Dodoma chini ya Mwalimu Nyerere imekwenda mbali sana katika kukashifu Uislamu, Waislamu Zanzibar waliandamana kwa amani lakini wakashambuliwa kwa
Inaendelea Uk. 14

Makala/Tangazo
African state will never be accepted when selfgovernment is achieved in this Protectorate. We are also opposed to multiracial government in these islands. It is against all this Association stands for. We want Zanzibar to become an African state like the Gold Coast (Afrika Kwetu, May 5, 1955). Tafsiri: Tungependa kuwahakikishia wale wote wanaoitwa Wazanzibari kwamba chochote kisichokuwa Dola ya Kiafrika hakitakubaliwa, wakati serikali yetu wenyewe itakapopatikana katika visiwa hivi. Pia tunapinga serikali mseto (Multi-racial) katika visiwa hivi. Tunataka Zanzibar iwe dola ya Kiafrika kama ilivyo Ghana Afrika Kwetu, May 5, 1955. Kufuatia majadiliano yao na Sheikh Ameir Tajo Ameir, wajumbe wa ZNP wakaenda Pemba ili kujadiliana na Sheikh Muhammad Shamte Hamad. Wajumbe wengine walikuwa Sheikh Miraji Shaalab, Abdulrahman

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012 Muhammad Babu, Sheikh Maalim Hilal na Sheikh Ali Muhsin. Nyerere alitawala kwa miaka 28 (19611989), kama Rais na Mwenyekiti wa chama kinachotawala Tanzania. Wakati wa utawala wake, Rev. Frank Schildknecht, mwanachama wa Shirika la Kikatoliki la White Father, ambaye alikuwa na jukumu la kuangalia shughuli zote za Waislamu Barani Afrika kwa niaba ya Kanisa Katoliki, alituma ripoti mwezi Julai mwaka 1963 kwa Papa mjini Vatican, kwamba Taasisi ya Waislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS), inakuwa na nguvu sana na inatishia mustakabali wa Kanisa kwa kueneza Uislamu. Wakati huo (EAMWS) ilijenga Misikiti, Zahanati na mashule katika eneo lote la Afrika Mashariki. Na pia ilipanga kujenga Chuo Kikuu cha kwanza cha Waislamu visiwani Zanzibar, kama kile cha Beirut, lengo likiwa kuzal i s h a w a s o m i n a wataalamu Waislamu. February 25, mwaka 1965, Nyerere alipiga marufuku Umoja wa Elimu wa Waislamu, ambao ulianzishwa kwa lengo la kuwasaidia Waislamu ambao hawakuruhusiwa katika shule za msingi za Serikali. Na pia aliipiga marufuku (EAMWS) mwaka 1968 kwa taarifa hii fupi: Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa amri ya Rais (Julius Nyerere), ametangaza tawi la Tanzania la East African Muslims Welfare Society (EAMWS) na Baraza la Tanzania la East African Welfare Society kuwa ni taasisi zilizo kinyume cha sheria chini ya kipengere 6(1) cha Sheria ya vyama vya kijamii (The Standard, December 20, 1968). Mshauri wa EAMWS, Sheikh Hassan bin Ameir al - Shirazy alikamatwa na kurejeshwa Zanzibar. Kila mtu anafahamu Crusade ya Nyerere dhidi ya Zanzibar kujiunga na OIC. Lakini pia vita dhidi
Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

Mhandisi wa vurugu Zanzibar ni Nyerere


Inatoka Uk. 6 Okello, kinyume kabisa na matakwa ya Wazanzibari, na hiyo ikafuatiwa na kampeni ya makusudi kuvuruga utamaduni wa Kiislamu visiwani Zanzibar chini ya Katiba ya kisekula( P.170). Hii ilianza baada ya Nyerere kuwafukuza Waislamu madhubuti wa Tanganyika kutoka kwenye uongozi wa TANU. Kisha akaanza jitihada zake za kuwavuruga Waislamu wa Zanzibar. Kwanza alianza kumhadaa Abeid Amani Karume, ambaye alikuwa Rais wa African Association (AA). Nyerere alimshawishi Abeid Amani Karume kuiunganisha African Association(AA) na chama cha Shirazi Assoacition(SA), kilichokuwa kikiongozwa na bwana Thabit Kombo Jecha al -Shirazy (1904-1988), mzaliwa wa Kizimkazi Zanzibar. Nyerere akaunda chama kipya cha Afro-Shirazi Party (ASP), February 5, mwaka 1957, chini ya uongozi wa Abeid Amani Karume. Mwaka 1960, Sheikh Muhammad Shamte Hamad, Mkuu wa Chuo, aliyezaliwa Chambani, Pemba na Sheikh Ameir Tajo Ameir, waliunda chama cha Zanzibar and Pemba Peoples Party(ZPPP), ambacho Katibu Mkuu wake alikuwa Abdullah Amour Suleiman, mzaliwa wa Pemba. Huyu bwana alikuwa Mhariri wa gazeti la Mwangaza, ambalo ndilo lilikuwa mdomo rasmi wa ZPPP. Chama hiki ndicho kilichoaminika kuwa sauti halisi ya Wazanzibari wote, bila ya kujali Uafrika wala Uarabu, Upemba wala Uunguja. Maadui wa Zanzibar wanakuza zaidi tofauti kati ya Waafrika na Waarabu, lakini wanapuuza kwa makusudi athari ya Uislamu, ambayo ina nguvu kubwa mno katika siasa za Zanzibar. Athari hii ilisababisha muungano wa ZPPP na Zanzibar Nationalist Party (ZNP) mwaka 1961, baada ya ASP kushindwa kupata support ya ZPPP, ili kuunda nguvu ya pamoja (coalition force), kwa ajili ya kupigania kile kilichoitwa Uhuru wa Waafrika. Ikumbuk w e k w a m b a , awali Abeid Amani Karume alikuwa akiongoza chama cha African Association ambacho hakikuwa na malengo ya kuleta uhuru na umoja kwa Wazanzibari wote kama inavyobainishwa na gazeti la Afrika Kwetu ambalo ndilo lilikuwa mdomo rasmi wa chama hicho: We wish to assure all the so called Zanzibaris that anything short of an

SHEIKH Abeid Amani Karume

MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO


P.O. BOX 1031 Morogoro, Tanzania Tel: +255 23 2600256 Fax: +255 23 2600286 E-mail address:mum@mum.ac.tz Website: www.mum.ac.tz

Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro kinapenda kuwatangazia wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na Chuo kuwa fomu za kujiunga na masomo katika mwaka 2012/2013 zinaendelea kutolewa mpaka tarehe 25/06/2012. UTAWALA

Darasa la wanawake/Tangazo

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012


kichwani na kwa vyovyote ningekaa nalo hadi umauti wangu. Lakini sasa sina budi kuwashukuru Walimu Wakuu wa Shule za Kiislamu walioamua kufuatilia matokeo ya kidato cha sita. Sasa nimeamini kuwa hata mimi nilihujumiwa katika matokeo yangu ya kidato cha sita kwa somo la maarifa ya Uislamu kwa kupata daraja E wakati nikitarajia A. Nilikuwa naangalia kama kuna uwezekano wa kuapeal nilipoangalia kwenye mtandao wa Baraza la Mitihani nikakuta appeal inatakiwa iwe ndani ya miezi miwili tokea matokeo yatangazwe. Sasa ni miaka 20 tokea nimalize kidato cha sita, japo najua hata nikipat A kwa sasa haitanisaidia kitu, lakini angalau nitathibitisha kuwa dhulma ilitendeka. Ninawaomba walimu wetu wakuu wasiishie kwenye somo la Maarifa ya Uislamu, bali waibane serikali iunde tume ichunguze na msomo mengine. Nina mifano hai ya vijana waliofeli kidato cha 4 au 6 lakini wakifanyiwa mipango ya kusonga mbele wanakuwa wazuri sana katika masomo kiasi cha kujiuliza walifeli vipi huko nyuma? Kumbe huwa wanafelishwa! Hujuma za namna hii ni muendelezo wa hujuma nyingi tunazofanyiwa Waislamu, sio katika masomo tu, bali pia katika ajira na nyanja nyingine nyingi na hii inatokana na msingi uliosimikwa kwa muda mrefu na kuota mizizi kiasi kwamba wale wanaotenda dhulma hizo wanaamini kuwa ni haki kwao kuwafanyia Waislamu unyama huo. Mimi ninaamini wote wanaohusika na hujuma na dhulma za namna hiyo kwanza wao wenyewe ni zao la hujuma hizo yaani wamepata nafasi walizonazo kwa kuziba nafasi za wengine. Mfano kama mtu hakufaulu katika ngazi yoyote ya elimu iwe msingi au sekondari halafu akafanyiwa mipango ya kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu, basi huyu mtu ni zao la dhulma hivyo na atahakikisha anaendeleza dhulma kulipa fadhila kwa mfumo uliompendelea. Mimi katika shule ya msingi niliyosoma ni shule iliyoko katika eneo lenye Waislamu wengi, lakini ajabu ni kwamba tokea miaka ya 70 shule hii haikuwahi kufaulisha mtoto kwenda sekondari ya serikali hata kwa kipindi chote nilichosoma mimi hadi kuhitimu mwaka 1985 hata baada ya hapo. Yawezekana baada ya shule za sekondari za Kata ndio vijana wanapata fursa ya kwenda kusoma shule hizo. Ajabu ni kwamba katika shule ya jirani ambayo iko karibu na kanisa na ambayo ilikuwa na Waislamu wachache, ndio ambayo vijana walikuwa wanachaguliwa kwenda sekondari. Ukiangalia mazingira ya ufundishaji yalikuwa ni yale yale baina ya shule hizi. Hii haikutokana na kwamba Waislamu hawataki kusoma au hawajui umuhimu wa kusoma au hawana akili. Ila ilitokana na hujuma zinazofanywa kwa makusudi na watendaji wa serikali ambao wanawaona Waislamu kama ni watu ambao hawastahiki kutendewa haki. Siamini kama haya ni mafundisho wanayopata kutoka katika dini zao maana ni dini ya shetani tu ndiyo inayoweza kutoa mafundisho kama hayo. Hebu msomaji mfikirie mzazi wa kijijini anaye taabika kwa kilimo cha jembe la mkono ili apate sare, madafteri, vitabu na karo ya mtoto ili mwanae asome asonge mbele, lakini anakatishwa katikati kwa dhulma za namna hii! Mkirie mama wa mjini anayelala hoi kwa kazi ngumu ya kuchoma maandazi na vitumbua ili alipe karo ya mtoto wake, halafu anakatishwa kwa dhulma za namna hii! Kweli nchi inaweza ikawa na baraka? Si kila siku mabalaa yatakuwa hayaishi? Mara ukame, elnino, njaa, kuporomoka kwa thamani ya fedha. Mabalaa hayatakoma nan chi haitakuwa na maendeleo kwa sababu walioshika mamlaka ni zao la dhulma na ndio hao hao watakuwa masadi na wala zaidi ya mfalme jeta. Ukristu una mafundisho yaliyozoeleka ya kumpenda jirani yako, na hapa haimaanishi kuwa jirani yako ni yule tu aliye Mkristu, bali ni jirani yeyote madamu ni binadamu mwenzako. Kama nitakuwa nimekosea nitaomba mwongozo kutoka kwa wataalmu wa Ukristu watakao soma maneno haya. Uislamu unafundisha uadilifu hata kwa kari. Haki yake lazima apewe. Asidhulumiwa kwa ajili ya ukari wake. Sasa kama hivi ndivyo basi ushujaa wa wale wanaodhulumu haki za wenzao wanautoa wapi? Mimi kwenye mtihani wa kidato cha sita nilifaulu kwa daraja la pili pointi 11 ambapo nilikuwa ninakidhi vigezo vya kwenda Chuo Kikuu. Niliomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Maajabu sikupewa nafasi, lakini wakati huo huo baadhi ya wenzangu waliokuwa na pointi za chini Inaendelea Uk. 9

AN-NUUR

Hatimaye nimepata jibu

DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa.

Na Kamaludin Khalid Mustafa


NIMEKUWA na swali kichwani mwangu ambalo siku zote nilikuwa natafuta jibu, sikuweza kulipata hadi hivi juzi baada ya matokeo ya kidato cha sita ya somo la Maarifa ya Uislam (Islamic Knowledge) kuchakachuliwa na wahusika kukiri. Nilifanya mtihani wa kidato cha sita mwaka 1992 katika shule ya Pugu Sekondari. Miongoni mwa masomo niliyokuwa nayamudu vilivyo ni somo la Islamic Knowledge. Ilikuwa ni lazima niyamudu kwa vile nilihitimu elimu ya dini katika Madrasat Elfalah El-Islamiat Katoro kwa kiwango cha thanawi sawa na sekondari. Nilikuwa ninasoma masomo ya dini sambamba na kusoma shule ya msingi ambapo mchana tukisoma shule ya msingi na usiku tukisoma masomo ya dini kwa Mzee wetu Alhaji Sheikh Mustpha Khalid Sadiq. Kama kawaida, baada ya kuhitmu shule ya msingi mwaka 1985 sikuafaulu (kuchaguliwa) kuendelea na shule ya sekondari ya serikali. Lakini kama ilivyokuwa ada kwa Mzee wetu, ilikuwa ni lazima kuendelea na shule ya sekondari ya kulipia. Nilifanya usaili katika shule mbalimbali za sekondari za kwetu Bukoba pamoja na Mwanza na zote nilipewa nafasi. Nilichagua kwenda

kusoma shule ya sekondari ya Lake ya mjini Mwanza na hii ilitokana na kuona vijana wengi waliokwenda kusoma shule za sekondari za kulipia Bukoba hawakufanya vizuri kutokana na sababu mbalimbali. Shule ya Lake ni shule ya kutwa. Mimi pamoja na kaka yangu tukiishi sehemu mbalimbali tuliwashawishi walezi wetu wakakubali kuanzisha Madrasa za usiku. Tukifundisha madrasa usiku huku mchana tukienda shule na wakati huo huo tukifundisha somo la Maarifa ya Uislamu shuleni, yaani katika shule ya sekondari tulipokuwa tukisoma. Ilipoka wakati wa kujaza form za masomo ya mitihani ya kidato cha nne nikajikuta nina masomo mengi ya kufanyia mtihani kuliko yaliyokuwa yanaruhusiwa. Yalikuwa yanaruhusiwa masomo sio zaidi ya 10, mimi kwa vile nilikuwa nina soma masomo ya sayansi wakati huo mbali ya hesabu nilikuwa pia nikisoma somo la hesabu la ziada yaani additional mathematics, pia na somo la historia. nikajikuta ni lazima niache somo moja nisilifanyie mtihani, yaani kati ya additional mathematics, history au Islamic knowledge. Kwa vile nilikuwa nikijiweza sana kwenye hesabu, niliamua kwamba lazima additional mathematics nilifanyie mtihani na hivyo kubakia masomo mawili ya kuamua niache lipi yaani history na Islamic knowledge.

Nikaamua kuacha history pamoja na kwamba nilikuwa ninaimudu vizuri. Mwalimu Mkuu akaniita na kunisihi niache Islamic nifanye history na sababu yake kubwa ilikuwa ni kwamba Islamic nitafeli kwa vile wengi huwa wanafeli. Mimi sikukubaliana nae nikamwambia ni vigumu kuacha Islamic, kwamba kama mimi nilikuwa mwalimu nikiacha Islamic ndio hakuna atakeifanya. Na hivyo huenda ikafa hapo shuleni. Matokeo yalipokuja ya Islamic nikawa na daraja B ijapokuwa mategemeo yangu ilikuwa ni A. Hata hivyo sikujali kwa vile B nayo haikuwa mbaya. Nilipokwenda kidato cha 5 niliendelea kuwafundisha wenzangu somo la Maarifa ya Uislamu huku na mimi nikijiongezea maarifa mapya. Wakati wa mtihani wa mwisho nilifanya kwa kujiamini sana na maswali yote niliyamudu barabara. Kwa kweli hadi hivi sasa sikuwahi kufanya mtihani huku nikijiamini kama nilivyofanya mtihani wa Islamic form 6. Matokeo yalipokuja nikapata daraja E. Kwa wale wasiojua daraja E ni karibia kidogo nifeli, yaani nipate F au failure. Sikuamini, lakini pia wakati huo sikuwa hata najua kama kuna ku-apeal. Ila nilimuuliza Almarhum Burhani Mtengwa kwamba imekuwje nikafeli somo hilo pamoja na kwamba nililifanya vizuri sana? Kwa kweli nae hakuwa na jibu la kunitosheleza. Nilikaa na swali hili

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012


mrusha kipindi anatafuta kunitisha. Haukupita muda mrefu wakati nilipokuwa nje ya nchi kimasomo nikasikia yule bwana amenyanganywa uraia. Sijawahi kuwasiliana naye nami ningemuuliza maswali kama hayo niliyoulizwa mimi. Pengine akisoma hapa atatafuta namna ya kujibu hayo maswali. Baada ya muda mrefu kidogo kupita nikasikia yule bwana aliyeninyima kazi kwa ubaguzi wa dini, analalamika kuwa kuna njama za kuwaondoa watu wa kabila lake kwenye nafasi muhimu za uongozi wa nchi hii. Ilikuwa ni baada ya Waziri mmoja wa kabila lake kujiuzulu uwaziri. Huyu pia sijawahi kuwasiliana naye ningemuuliza kuwa dhambi ya ubaguzi anaionaje? Mganda ana msemo kuwa niwafanyiao wenzangu, huwa sitaki wao wanifanyie. Nimeamua kutoa mifano hai inayonihusu mimi ikiwa ni kama ushahidi wa yanayotokea nchini mwetu. Yeyote anayetaka mustakabali mwema wa nchi yetu, ahakikishe anatoa mchango wake wa hali na mali ili kuondoa aina zote za ubaguzi hasa kipindi hiki cha maoni ya katiba mpya. Inatakiwa raia wote watendewe haki na haki ionekane inatendeka. Tabaka fulani la raia linapoona kuwa halitendewi haki pahala, kunako haja ya kuhakikisha unakuwepo uwazi utakaoridhisha kwamba hakuna ubaguzi. Kwa mfano Baraza la Mitihani nilazima liwe na uwiano sawa wa kidini. Tume ya ajira za uma iwe na uwakilishi sawa wa kidini. Tume ya taifa ya uchaguzi iwe na uwakilishi sawa wa kidini. Wakurugenzi katika Wizara ya Elimu wawe na uwiano sawa wa kidini. Wengine wetu pamoja na kwamba tumesoma vizuri, lakini tukiomba kazi za serikali na taasisi zake hata kwenye usaili hatuitwi. Kumekuwepo na kasumba ya kuona mtu kama mimi ninaezungumzia mambo haya kwa uwazi kuwa ni mdini. Mimi sina ubaguzi wowote uwe wa kidini, kikabila wala kijinsia. Ninaishi vizuri na watu wa dini zote, tunaheshimiana tunaamiliana na kusaidiana inapobidi bila tatizo lolote. Dini yangu hainifundishi hivyo. Mtume (SAW) anasema, Enyi watu, nyote mnatokana na Adamu, na Adamu anatokana na udongo, hakuna ubora wa Mwarabu na asiye Mwarabu ila kwa ucha Mungu. Mwislamu hawezi kumbagua binadamu mwenzie akaendelea kujiita Mwislamu maana anakuwa amekwenda kinyume na Uislamu wenyewe. Sisi tunaosoma mitandao ya kijamii ambapo mtu anaweza kutoa maoni yake bila kujitambulisha (anonemous) tunashuhudia namna baadhi ya wenzetu walivyo na chuki za ajabu dhidi ya Waislamu. Ukitokea uteuzi wowote na muhusika akawa ni Muislamu, utasikia mashambulizi na kejeli. Utasikia jinsi wasivyotakiwa. Hii sio siri. Inatia hofu sana kwamba huko tunakoelekea kama juhudi za makusudi hazikufanywa ni hatari tupu. Sisi tunaitakia nchi mustakabali mzuri. Baba zetu walibaguliwa wakadai uhuru walidhani ubaguzi utaisha, lakini ikawa ndio kwanza unakuja ubaguzi kwa staili nyingine. Sisi tunaobaguliwa tunakuwa na subira, lakini hatujui kama wanetu au wajukuu zetu watakuwa na subira kama yetu. Upo msemo kuwa kuzuia maradhi ni bora kuliko kungoja yaje ndio uyatibu. Hofu yetu ni kuwa subira ikiisha wakajitokeza wataopinga dhulma, sio kwa mdomo kama sisi, bali wakaja na staili nyingine, hapo shughuli itakuwa pevu. Hata wale waliojilimbikizia mali kwa njia za dhulma hawatapata fursa ya kufaidi mali zao. Kuna wanaoamini kuwa Waislamu wakifanywa malofa wasio na elimu na mali, itakuwa rahisi kuwatawala na hata likitokea la kutokea, hawatakuwa na uwezo hata wa kujihami. Lakini historia haioneshi hivyo. Dawa ya mustakabali mwema ni kutendeana haki. Uadilifu ndio suluhisho pekee. Nimalizie kwa kuwaomba wananchi wote wapenda haki watoe maoni yao katika katiba mpya kwa kuzingatia vizazi vijavyo na hivyo tujenge amani ya nchi yetu kwenye msingi imara wa jiwe na sio wa dongo kama ilivyo sasa. Kupambana na dhulma za aina zote zikiwemo za ubaguzi, ukandamizaji, wizi wa mali za umma na ufisadi mwingine, sio kazi lelemama. Kama alivyosema Mwalimu Nyerere kuwa aliyeonja nyama ya maiti haachi. Hivyo madhalimu tusiwatarajie kuacha kirahisi kutudhulumu na kutuhujumu. Dhulma ishakuwa tamu kwao. Ni lazima kazi ya ziada inatakiwa. Huu ni wajibu wa kila mmoja wetu. Mtume (SAW) anatwambia kuwa nyote ni wachungaji na kila mchungaji ataulizwa siku ya kiama namna alivyo timiza wajibu wake wa kichungaji. Tunaamrishwa pia kuwa tukiona uovu tusivumilie na kuuwacha ushamiri. Tuuondoe. (Kamaldin Kh. Mustafa 0652 240 420 kamaludinm@yahoo.com)

AN-NUUR

Hatimaye nimepata jibu


yangu, walipewa nafasi. Hata hivyo sikujali sana kwa maana binadamu akifunga mlango, Mungu anafungua mlango mwingine. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani nilibahatika kupata chuo kingine nje ya nchi nikaendelea na masomo katika chuo kilicho asisiwa na OIC. Ukisikia wale wanaopinga OIC Tanzania, ni sampuli ya wale wale wasiotaka sisi tupate fursa kama hizi wakati wanajua kuwa sisi tukifanikiwa haitawapunguzia wao chochote. Lakini Uislamu unatufundisha kuwa hasidi anachukia neema za wenzie hata kama neema hizo hazitahamia kwake. Nilipotaka kufanya degree ya Uzamili (Masters) niliomba Chuo cha IFM kwa maana kipindi hicho vyuo havikuwa vingi nchini vinavyotoa Uzamili katika masomo ya biashara. Niliwaonyesha IFM kuwa nilikuwa na uwezo wa kujilipia masomo maana kozi nzima ilikua ni milioni mbili na nusu za Kitanzania, lakini sikupata nafasi wakati degree yangu ni daraja la juu. Nilipoomba nje ya nchi, vyuo vyote nilivyoomba vilinipa nafasi. Niliomba vyuo vya Marekani, Uingereza na Australia. Nikajiuliza ni kwa nini sikupata nafasi nchini mwangu lakini ninaipata nchi Marekani, Uingereza na Australia? Nizungumzie kidogo ubaguzi katika ajira nchini. Mwaka 1999 niliomba kazi katika taasisi moja ya serikali. Jamaa mmoja akanambia kuwa ukitaka kazi hupati

WANAFUNZI Waislamu wakiwa katika maandamano ya kudai haki

Inatoka Uk. 8

bila kuwa na memo ya mtu maarufu. Sikuwa na mtu wa aina hiyo. Nilichokifanya nilipeleka maombi yangu moja kwa moja kwa mkurugenzi aliyekuwa ndio anahusika na uajiri. Niliendelea kufuatilia kwake, lakini niliishia kupewa jibu la kukatisha tama. Sio kwamba sikuwa na vigezo, bali kilicholeta shida ni dini na chuo nilichosomea. Na aliniambia live hivyo. Kwamba mimi Khalid na nikusomea katika vyuo vya kikanisa kanisa. Nimesoma katika Chuo kinachofadhiliwa na OIC! Hata kwenye usaili (interview) sikuitwa wakati ambapo wale niliowajua pamoja na kufahamu elimu zao kuwa za chini kuliko mimi, ndio waliopewa nafasi. Ningeamini kuwa tatizo ni kwa vile sikuwa na kimemo, lakini kama ingekuwa hivyo, asingeniambia alivyoniambia. Kuna ukweli kuhusu ajira na vimemo katika nchi hii, lakini hii yote ni aina ya rushwa. Wakati nasoma Shahada ya Uzamili katika somo la rasilimali watu (human resources), tulisoma kuwa miongoni mwa matatizo ya ajira na usaili ni kitu kinachoitwa hello effect, yaani kama mtu anaeajiri au kufanyisha usaili ana kitu cha kushea na wewe kama vile mkiwa wa dini moja au kabila moja au hata lugha, basi kuna uwezekano mkubwa huyo msaili akavutiwa na kimoja wapo kati ya hivyo akaamua kukupa kazi hasa pale inapotokea nafasi moja inawaniwa na watu wawili wenye vigezo sawa. Kutokana

na hilo basi, ni budi uwepo utarataibu wa kuziba matatizo kama hayo katika ajira. Kwa mfano Kenya usaili unafanyika live kwenye runinga watu wote wakiona kama ilivyokuwa wakati wa ubunge wa Afrika Mashariki hivi karibuni pale Dodoma. Wa k a t i f u l a n i b w a n a mmoja ambaye hurusha kipindi cha TV kila Jumatatu usiku na kuruhusu maswali, alikuwa anaongelea mchango wa Mwalimu Nyerere katika amani ya nchi. Nilibahatika kupiga simu na baada ya kujitambulisha nikamwambia kuwa hii inayoitwa amani ya nchi imejengwa juu ya dongo na haikujengwa juu ya jiwe, yaani msingi imara hivyo wakati wowote inaweza kuparaganyika, nikampa mfano wa ubaguzi katka ajira nikamweleza yaliyonisibu mimi katika kutafuta kazi. Nikamwambia kuwa hata yeye kwa hofu ya kubaguliwa, aliamua kubadili jina lake akaacha jina la Kiislamu alilopewa na baba yake. Yule bwana alionekana kukerwa na mchango wangu. Kesho yake nikapigiwa simu kwa sauti ya mwanamke nikiulizwa kama niko tayari kujibu maswali yake nikamwabia nitajibu. Akauliza maswali yafuatayo: Je, wewe ni Mtanzania? Kama ni Mtanzania ni kwa kuzaliwa au kununua uraia? Je, Tanzania unavyoiona ni nchi nzuri ya kuishi? Wastani? Au mbaya? Nilijibu maswali yake akakata simu. Nikadhani ama walikuwa ni Usalama wa Taifa au alikuwa ni yule

10

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Na Khalid S Mtwangi KATIKA makala iliyopita tulipozungumzia kwamba Ukristo unapotea Ulaya na kuhamia Afrika, tulijaribu na nadhani tulifaulu kuweka wazi jinsi gani Fr Frodolin Portman wa Kanisa Katoliki alivyotoa uwongo kuwadanganya Wakatekist na wengine wengi kwa jumla. Leo hii tutaendelea na kuchambiua uwongo mwingine uliomo katika kijitabu alichoandika huyu Padri Fridolin Portmann, ambaye nadhani ni wa kutoka Switzeland. Nchi yenye historia ya kuukandamiza Uislamu kwa nguvu sana. Ni hawa ambao walikataza misikiti isijengwe na minara. Katika ukurasa wa tisa (9) wa kijitabu chake huyu mtumishi wa Mungu anaandika uwongo wake kama ifuatavyo: Labda waumini wa Muhamadi walijifunza destri fulani ya dini kwa hawa Wakritu wa Uhabeshi (Ethiopia ya leo); kwa mfano desturi ya kufunga inayokazwa sana na Wakristu Waabeshi (sic) mpaka leo. Hii inaweza kuwa kweli w a s o m a j i Wa i s l a m u ? Katika kutafuta ukweli, nilizungumza na Sheikh Khamis Mataka ambaye hivi karibuni tu ametunukiwa shahada ya uzamil hapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kanihakikishia kuwa huyu Fr Fridolin Portman kadaganya. Mtume Muhammad SAW alianza kufunga hata kabla ya ile wengine huiita Hijra ya kwanza pale Ras-ulL l a h M u h a m m a d S AW alipowaambia wafuasi wake wakimbilie Abyssinia (Uhabeshi-Ethiopia). Sheikh Mataka kanihakikishia. Mtume alikuwa akifunga siku ya Jumatatu ambayo ndiyo siku aliyozaliwa na Alkhamis, siku ambayo milango ya rehma iko wazi. Haitoshi hili ni somo muhimu sana kwa vile kufunga mwezi wa Ramadhani ni moja katika zile Nguzo Tano za Uislamu. Kurani

iko wazi kuhusu swaumu. Tu n a a m b i w a : E n y i mlioamini mmeandikiwa saumu kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu . (surat-il-Baqara 2: 83 p.58, tafsiri Al Muntakhab ya Al Marhum Sheikh Ali Muhsin Al Barwani. Ama : Enyi mlioamini! M m e l a z i m i s h w a kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa walikuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. ( p 41 suratil-Baqara 2 : 83 tafsiri ya Al Marhum Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy. Quran inaonyesha kuwa surah hii ilishuka Madina, yaani ilikuwa ni baada ya Hijra. Sasa kwa nini huyu Fr Fridolin Portmann asiwafundishe wana Katekisti wake kuwa labda Mtume Mhammad alijifundisha hayo kutoka kwa Wakristo walipomkaribisha huyu Rasul-Llah Muhammad SAW hapo Madina? Inajulikana kuwa Wakristo wa Madina walimpokea Mtume vizuri sana na laishirikiana nao katika mambo mengi. Hawa Wakristo wa Madina hawakuwa wakifunga? Kwa

Wakristo watafute ukweli kutoka kwa Masheikh


hakuugusa kabisa katika kijitabu chake. Quran inasema hivi: Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Quran kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo za uongofu na upambuzi. (p 59 surat-il-Baqara 2:185, Al Muntakhab ya Al Marhum Sheikh Ali Muhsin Al Barwani) (Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa (katika mwezi huo) hii Quran ili iwe mwongozo kwa watu na hoja zilizo wazi za uwongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). (surat-il-Baqara 2:185, p 41 tafsiri ya Al Marhum Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy). Naye Sheikh Ali Juma Mayunga anaongeza commentary hivi: Imepokewa kutoka kwa Abu Sharri amesema : Amesema Mtume SAW: Vimeteremka vitabu vya Ibrahim AS tarehe moja ya Mwezi wa Ramadhani, na imeteremshwa Taurati ya Musa AS tarehe sita ya Mwezi wa Ramadhan, na imeteremshwa Injili ya Isa AS tarehe kumi na tatu ya Mwezi wa Ramadhanina

ASKOFU Valentino Mokiwa.

Mayhem in Zanzibar
By Khalid S Mtwangi
as absurd, that Christians feel they are second class citizens in Zanzibar. Absurd? No, the correct description would be ridiculous; facts speak for themselves. Of all the Christian denominations that have found a home in Zanzibar the Anglicans (or CMS or UMCA, as they used to be known days yonder) have been able to integrate admirably with their majority Muslim country folk. These Christians are found in many slots, some very high positions, in the political plane and simply normal life in Zanzibar such that sometimes it is difficult to tell them apart. However, it may be true that to some extent, a triviality me thinks, Christians feel alien in a country that is almost wholly Muslim, more so now that there is a proliferation of all manner of denominations some of which are known to rejoice at causing trouble to Muslims. These may feel slighted just as Muslims are viewed as an oddity in some parts of the Tanzania Mainland. I can defend this attestation if need it be. No Muslim leader worth his prayer mat would exhort his ock to run amok and torch anyones church, in fact the Cathedral at Mkunazini, at the old slave market, is a testimony to the moral rectitude of Zanzibar Muslims. Having said so, however, some

nini? Fr Fridolin Portmann atakuwa ametuelimisha vizuri sana kama atatufafanulia haya mawili. Tumalizie kuonyesha uwongo wa Fr Fridolin Portman kwa kutazama amri ya kufunga Mwezi wa Ramadhani. Tunapozungumzia kufunga hukumbuka hasa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao Fr Fridolin Portmann

imeteremshwa Zaburi ya Daudi AS tarehe kumi na nne ya Mwezi wa Ramadhani; na imeteemshwa Quran kwa Muhammad SAW tarehe ishirini na nne ya Mwezi wa Ramadhani. (Maulid Nabii ya Mfunguo Sita????) Sheikh Ali Juma Mayunga anasema tazama Al Burhan y Tafsirul Quran juzuu 1 ukurasa 183. Yote haya yamo katika tagfsiri yake ya Quran AL QURAN MUBIN. Haya yote ndiyo mafundisho yaliyo sahihi k w a Wa i s l a m u k u h u s u kufunga saumu. Lakini kweli haitawafaa kina Fr Fridolin Portmann katika kuwadanganya waumini wao ule uwongo ambao unawafundisha wengi wao kuuchukia na kuudharau Uislamu. Wakifundisha kweli wanaweza kupoteza waumini wengi kama inavyotokea Ulaya leo hii. Ndugu zetu Wakristo wanaombwa watafute ukweli kutoka kwa masheikh wa Kiislamu. Ni hayo ndiyo yanayotokea Ulaya na inawatuma watu kama vile Fr Frodolin Portmann waje kudanganya huku Afrika na kuwawezesha kuzoa waumini.

ANY sane person would not support nor condone the mayhem that had been unleashed in some streets of Zanzibar Town over the last week or so. It is right that voices, perhaps discordant and not all sincere, have been heard to condemn the fracas. Not surprisingly the Christian clergy and their ock have been prominent in their denunciation of the torching and resultant damage to their Church buildings. They have my sympathies. However, once tempers have cooled down and emotions have been ameliorated by sobriety of thought those of your readers who have the good of the Union of Tanganyika and Zanzibar at heart, need to sit down and cogitate, really agonize, over the consequences of the demise of the Union as some intemperate language has been heard emitted by some commentators. As would be expected, these commentators have been extravagant with their choice of words. Let me start with the head or the Primate of the Anglican Church in Tanzania, His Eminence Archbishop Dr Valentino Mokiwa. He was seen and heard making a claim that can only be described

very sober people, and not those so called wenye msimamo mkali, have been heard to ruminate over the invasion of so many Christian Churches in Unguja and Pemba. There are not that many Christian souls to save, so why not leave the poor Muslims in those islands continue to uphold the unadulterated teachings of Rasul-ul-Llah Issa (Yesu) as only they know how. Admittedly democracy is on the side of the intruders; nevertheless, there is bigotry Muslims have always to contend with; history surely would absolve these usually docile souls both on the isles and on the Main Land. One could go back to the misguided statement His Eminence Archbishop Dr Valentino Mokiwa that Christians are made to feel like they are second class citizens in Zanzibar. How wrong that notion is. But then he must have heard, certainly, of similar complaints being aired and expounded everyday by Muslims on the Mainland. It would be very strange, in fact, ludicrous if he is not aware of those cries. This could be because these exasperations have always been ridiculed by everyone including that ever ubiquitous press. Should the Archbishop not commit himself to expunge

the inrmity from our midst on the Mainland? It must be accepted that there is a swell of strong current is Zanzibar that at best looks askance at the Union. Accompanied by Bw Ally Saleh, the writer and activist, I did at one time visit the hot bed of antiUnion cabal at a place originally known as Soko Muhogo but now as Jaws Corner in Stone Town. The litany of the sentiments expressed here can only be believed when heard and seen in person. However, it is not all banter and demagoguery. There is some substance in what they complain about. Admittedly that cannot be excuse to burn down anyones church, if indeed it was the anti-Union cabal who did it! The Qur an enjoins that There is no compulsion in religion. Distressing though, it is known that His Holiness Pope Benedict XVI denigrates this verse from the Quran and dismisses it with some derogatory remarks directed at Prophet Muhammad SAW. This was seen and heard when Cardinal Jean-Louis Tauran of the Vatican was interviewed by Al Jazeera television on March 20. 2012. Sincerely Yours, Khalid Shaabani Mtwangi

11
Inatoka Uk. 4

makanisa Zanzibar itakapoanza kusikilizwa. Ila pamoja na kujua kuwa kuna ile Amri ya Biblia inayowataka Wakristo wasiseme urongo, na kwa kujua kuwa kila Mkristo anayeamini kuwa Yesu mwana wa Maryamu aliyezaliwa na kutahiriwa siku ya saba ni Mungu, anapaswa kulikubali neno la Biblia, lakini bado nataka nimkumbushe Askofu Laizer jambo moja. Yeye alikuwa katika watu waliopigia sana debe kile kikombe cha Babu kule Samunge, Loliondo, akiwataka watu wakapone ukimwi, kisukari, saratani, shinikizo la damu (presha) na kifafa kwa jina la Yesu. Na kama kawaida ya viongozi wa serikali wa nchi hii, kauli ya askofu ni sauti takatifu isiyopingwa wala kuhojiwa hata kama akili yako haikubaliani nayo; serikali ikasaidia kuhamasisha watu kwenda kupata dawa inayotokana na ndoto za mchungaji. Maelfu wakafurika wakipanga foleni kupata kikombe bila kujali maiti zilizokuwa zikizagaa Samunge watu wakifa kwa kukosa huduma. Maadhali Askofu Laizer kakibariki Kikombe na katangulia William Lukuvi na Steven Wasira kukinywa, kila

mtu anakimbilia kikombe. Kikombe kikawa kikombe, mpaka serikali ikaona vyema iweke kitengo cha usalama wa taifa kumlinda Babu maadui wa nje wasije wakamuiba Babu wetu tuliyeletewa na Mungu! Baba Askofu Thomas Laizer, wengi wa Watanzania hatujui ule mkanda wa kikombe cha Babu umeishia wapi. Hatujui hata stelingi wake mzee Ambilikile Mwasapila kaishia wapi na kile kikosi cha walinzi alichopewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pengine kabla ya Baba Askofu Laizer kutupa kwa undani habari za jeshi la vijana wa Kiislamu wanaojiandaa pale Unga Limited Arusha tayari kwa kushambulia makanisa, angetumalizia ile tamthilia ya Samunge na zaidi Watanzania wangependa kujua ni watu wangapi wamepoteza maisha hadi sasa kutoka na kuacha matibabu ya kisukari,

Askofu Laizer anajua waliochoma makanisa


ukimwi na presha wakiamni kuwa baada ya kupiga kikombe wamepona. Wapo wale waliokufa pale pale Samunge mbele ya macho ya Babu. Baadhi ya magazeti yalihesabu mpaka wakafika maiti 75. Labda Askofu Laizer anaweza kutusaidia kupata idadi kamili maana hakosi kuwa na mtandao kila mahali kama alivyo na ule unaofuatilia harakati za Waislamu misikitini Arusha. Nakumbuka wakati akina Magufuli, maofisa wengine wa serikali (ambao tunaambiwa ndio wenye akili) wakipigana vikumbo kupeleka barabara, umeme na huduma nyingine muhimu ili kikombe cha ndoto za Babu kiendelee kunywewa bila tabu, Kanisa liliahidi kujenga maabara maalum kwa ajili ya Babu na huduma yake. Pengine ingekuwa vyema pia Askofu akatufahamisha michango ilikia kiasi gani na ujenzi wa maabara na hospitali ya kuboresha kikombe cha Babu Mwasapila upo katika hatua gani. Viongozi wa Kanisa la Askofu Thomas Laizer ni miongoni mwa maaskofu walioshiriki kusaini makubaliano ya kiitifaki (Memorandum of Understanding-MoU) kati ya makanisa na serikali. MoU ambayo hutumika kuchota fedha za walipa kodi kuwaimarisha Wakristo. Huenda akina Fred watakuwa hawakukosea kama watawaita Waislamu wajinga, maana katika hali ya kawaida isingetarajiwa mtu mwenye akili timamu akubali dhulma, ubaguzi na upendeleo huo. Sasa katika muktadha huo huo, Askofu Thomas Laizer anajua kuwa Kanisa Katoliki lina Tume ya Majeshi ya Kivita (Commission of Armed Forces), lakini kwa kuwa anajua Katoliki ni wajanja wenzake, hutasikia akihoji majeshi hayo ya katoliki ya nini wakati tuna JWTZ. Atajifanya hajui wala haoni. Ila pale Msikiti wa Unga Limited Arusha wasije

Makala//TANGAZO

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012 Wasiwasi ni mmoja tu. Hatuna uhakika kama wapo polisi na waendesha mashitaka wa Jamhuri wenye ubavu wa kumuita Askofu Thomas Laizer mahakamani. Lakini si polisi pekee, hata wale vijana wa Arusha. Kwa uzoefu ulipo, kama ni kusema wataishia katika mimbari na vibarazani je ya Misikiti. Lakini lebo kwamba ni wahalifu itabaki. Labda kama sasa kutakuwa kumeibuka kizazi kipya chenye ujasiri wa kusimama na Askofu Laizer mahakamani au kumfikisha mbele ya Baraza la Habari.

AN-NUUR

wakadhani kuwa Askofu Laizer hawaoni. Nimalizie kwa kusema kuwa kile kitendawili na kesi ya nani kachoma m a k a n i s a Z a n z i b a r, haitakuwa na ugumu tena. Shahidi namba moja ashapatikana.

TANZANIA MUSLIM STUDENTS AND YOUTH ASSOCIATION (TAMSYA)

Jumuiya ya wanafunzi na vijana wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) Mkoa wa Dar es Salaam Idara ya Wanawake inapenda kuwaalika katika kongamano kubwa la vijana na wanafunzi wa kike litakalofanyika Inshaallah: TAREHE: 09/06/2012 JUMAMOSI MAHALI: UKUMBI WA SHULE YA AL-HARAMAIN MUDA: SAA 1:00 ASUBUHI HADI SAA 7:00 MCHANA Mada mbalimbali zitawasilishwa Sifa za mwanamke mwanaharakati. Nafasi ya mwanamke katika kuipigania dini ya Kiislamu MJULISHE MWENZAKO MJE PAMOJA KATIBU HABARI TAMSYA MKOA 0654 290875

KONGAMANO LA VIJANA NA WANAFUNZI WA KIKE WA KIISLAMU

Inatoka Uk. 7 ya Uislamu ilidhihirika zaidi Mei 7, mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa CCM kule Dodoma. Chini ya Uenyekiti wake, CCM ilishauri kuondolewa kwa Sheria ya Kiislamu Tanzania, ambako zaidi ya asilimia 65 ya wananchi wake ni Waislamu. Crusade hii ya kisiasa kupitia chama cha Mapinduzi ilisababisha Maandamano makubwa Zanzibar, Mei 9 mwaka 1988, yaliyofanywa na vijana wa Kiislamu baada ya Swala ya Ijumaa, katika kipindi cha Mwezi Mkutufu wa Ramadhani. Wa k a t i Wa i s l a m u walipoandamana visiwani Zanzibari wakidai Sheria zao za Kiislamu ziheshimiwe, jeshi la Polisi likiwa na silaha, mabomu ya machozi na magongo likawashambulia waandamanaji hao. Ali Mansour, mwanaharakati makini wa Dwat alIslamiyyh, alipigwa risasi na kufa shahidi. Muislamu mwingine alia hospitali siku ya pili yake. Mamia ya wananchi walilazwa hospitalini kufuatia majeraha yaliyotokana na kipigo cha Polisi. Wengine kadhaa, wakiwemo wanawake walikamatwa na kushitakiwa kwa kuchochea vurugu. Kuongeza Petrol kwenye moto, Polisi iliwakamata Maulamaa wanne, akiwemo Sheikh Nassor, Imam wa Msikiti wa Kikwajuni. Wa l i w a t u h u m u k w a uchochezi wa maandamano

Mhandisi wa vurugu Zanzibar ni Nyerere

hayo kwa sababu muda mfupi baada ya hotuba zao, Waislamu waliandamana kupinga jaribio la wazi kabisa la kuondoa Sheria ya Kiislamu Tanzania. Baada ya Maandamano makubwa, Waziri Kiongozi wa Zanzibar wakati ule, Seif Shariff Hamad (19841988) akafukuzwa CCM na wenzake sita. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa na dhamira njema. Nyerere alikuwa akipigana vita ya kidini dhidi ya Waislamu wa Zanzibar kupitia Muungano huo. Alikuwa na ajenda ya siri ya kuiteka Zanzibar na kuikabidhi mikononi mwa Mfumo - Kristo, kama alivyofanya Tanganyika. Wazanzibar wanayo haki ya kukataa muungano wa hovyo kama huu, ambao unalenga kuhujumu taifa lao na utambulisho wao wa Kiislamu. Kwa nini Wazanzibari wanapohoji Muungano huu wananyamazishwa? Mzee Abeid Amani Karume alipogutuka uzingizini na kugundua uovu uliojicha ndani ya Muungano huu, wote tunafahamu yaliyomkuta. Alipoanza tu kutoa kauli za kujitambua, Muungano ni kama koti, likikubana unalivua, hakudumu akapata fursa ya kulivua. Mzee Aboud Jumbe alipohoji Muungano huu, akajikuta ameenda Dodoma akiwa Rais wa nchi, akarudi akiwa raia wa kawaida. Muungano huu una nini hata iwe marufuku kuuhoji? Kwa nini Mkataba wake umechwa?

12
TAKWIMU YA SENSA (JIBU)
Ndugu ulo mashakani, shaka ninakuondoa, Swali lako gazetini, jibu ninakupatia, Sensa TBC wani, nini wamekusudia, Ni dhuluma ya zamani, wamejihalalishia. Ni mengi wanatamani, waweze kuyakia, Kila kilicho nchini, iwe yao milkia, Umoja hawathamini, amani wala sheria, Haja yao kileleni, kwa hila uzushi pia. Sensa iliyo na dini, hapa kwetu Tanzania, Iliishia sabini, nne bila kukosea, Idadi ya waumini, lizidi asilimia, Kilotusibu ni nini, leo tuwe qalilia. LengoTBC wani, sasa nakuelezea, Saidi wa Kiwalani, hili ndugu zingatia, Kama likuwa makini, siku chache baadia, Baraza kawa hewani, Rais kalichagua. Nia yao mebaini, maswali kuyazuia, Wao wamezidi nini, nchi kujitawalia, Kuanzia Taifani, mikoa, wilaya pia. Ni dhuluma ya yaqini, bila shaka kutilia. Nakuomba ikhiwani, nyuma kidogo rejea, Ile mbili ya tisini, nini walijifanyia, Mgao wa chinichini, ridhaa iso sheria, Chumo la serikalini, kanisa linalo shea.. Nashanga wahofu nini, data wakajipikia, Sera imeanza lini, wingi kuuzingatia, Kila kilichomo ndani, haki yao asilia, Wengine sote wageni, urithi wa malikia, Ndugu yangu samahani, hapa ninaishilia, Ni mgeni kwenye fani, ila nimeingilia, Inanichoma moyoni, ndo mana nimeongea, Jibu kama si makini, wengine watalitoa. Ally Mtande MUM-Morogoro. (0715-888360)

Mashairi/Sheria Sheria ya ardhi:

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Kanuni za Uendeshaji wa Mabaraza ya Ardhi


muhtasari wa kikao hicho, wasuluhishi, pamoja na wadaawa wengine. Wenye mgogoro wanapaswa kutia sahihi zao na waondoke na nakala ya uamuzi. Wajumbe wa Baraza watafanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kama hicho kama bado wanazo sifa za kuendelea kuteuliwa kwa nafasi hiyo. Mjumbe hataruhusiwa kusuluhisha mgogoro wowote unaomhusu au unaoihusu familia yake au hata jamaa yake kwa sababu ya mgongano wa kimasilahi. Wa d a u w a m g o g o r o wanaweza kuamua kusuluhishwa katika shauri lao na Baraza la Ardhi la Kijiji au kwenda moja kwa moja kwenye Baraza la Kata. Baraza la Ardhi la Kijiji halina uwezo Kusuluhisha au kusikiliza mgogoro kama thamani ya mali inayolalamikiwa itakuwa katika ardhi iliyopimwa katika mipango miji Kusikiliza shauri kama linatoka katika kata tofauti na ile ambako Baraza husika limo. Isipokuwa Baraza hilo linaweza kusikiliza shauri linalotoka kijiji kingine endapo tu kuna maelekezo kutoka ngazi za juu ya kufanya hivyo Kukata Rufaa au Kuhamisha mgogoro Sheria ya Ardhi ya Kijiji ya Mwaka 1999 na ile ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi inatoa mwanya kwa wadau katika mgogoro husika kuchagua mahali pa kusuluhisha au kusikilizwa shauri lao. Hata hivyo, wadau wanashauriwa kuanza na Baraza la Ardhi la Kijiji kabla ya kwenda Baraza la Kata.Kwa upande mwingine Sheria ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi inatoa mwanya wa kukata rufaa endapo upande wowote katika mgogoro hautaridhika na usuluhishi wa Baraza la Ardhi la Kijiji. Upande usioridhika utapeleka mgogoro huo katika Baraza la Ardhi la Kata. Hata hivyo ikiotokea kuna upande ambao bado hauja ridhika na maamuzi yaliyotolewa na bara la ardhi la kata bado wanaweza kukata rufaa kwenda kwenye baraza la nyumba la wilaya. Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ( District Land and Housing Tribunal). Kwa mujibu wa sheria za ardhi, hasa sheria ya Ardhi ya mjini pamoja na sheria ya Ardhi ya vijiji ( Land Act No 4 and Village Land Act No 5) kila wilaya,Mkoa kutakuwepo na baraza la ardhi kadri itakavyowezekana, na baraza hilo litaitwa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (District and Housing Tribunal). Na baraza hili la Wilaya litafanya majukumu yake yaliyomo ndani ya Wilaya au Mkoa na siyo vinginevyo kama itakavyokuwa imeelekezwa.

Na- Kissima Adolf 0713 401812 Email: adolfkissima@yahoo.com HABARI ndugu msomaji, wa gazeti la Ann nuur, nashukuru kwa maoni yenu kupitia barua pepe na simu. Wengi wenu mmeniomba kuendelea kuzungumzia juu ya sheria ya ardhi ambayo nilizungumzia wiki mbili zilzopita.Kwa mujibu wa sheria, kila kijiji ni lazma kiwe na na baraza la ardhi la kijiji . Ili maamuzi ya Baraza hili yatambulike kisheria ni lazima muundo wa baraza hili likidhi matakwa ya sheria. Usimamizi wa Mabaraza Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji yatakuwa chini ya usimamizi wa Msajili wa Vijiji. Kazi ya usimamizi inajumuisha uendeshaji wa haya mabaraza akisaidiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri husika. Uendeshaji ni kwa maana ya matumizi na mapato. Mkurugenzi anatakiwa wakati wote kuhakikisha kuwepo kwa mabaraza haya katika ngazi ya vijiji vyote vilivyosajiliwa. Uwasilishaji wa malalamiko Mtu yeyote mwenye malalamiko kuhusu mgogoro wa ardhi, anaweza kuyawasilisha kwa njia ya maandishi au kwa njia ya mdomo, kwa Katibu wa Baraza la Ardhi la Kijiji na yeye atayawasilisha kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Kijiji. Kama malalamiko yatatolewa kwa mdomo, basi Katibu wa Baraza la Ardhi la Kijiji atayanakili na kuwasilisha nukuu hiyo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kijiji. Kanuni za Uendeshaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji Baada ya wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji kuchaguliwa, watamchagua Mwenyekiti na Katibu wa Baraza. Mwenyekiti ndiye atakayekuwa kiongozi wa Baraza, na ndiye atakayewajibika kutoa maamuzi mbalimbali ya Kijiji. Baada ya kusuluhisha mgogoro, Baraza la Ardhi la Kijiji linapaswa kuandika

KUMBE MWEZI MTUKUFU...!


Tahamidi kwa Manani, Bwana wa ukamilifu, Mtukufu mwenye shani, asiye na upungufu, Japo moja nuksani, kwa mambo yake sufufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Ni yeye alobaini, mieziye iso zidifu, Ashara wa ithnani, idadiye kamilifu, I ndani ya QURAANI, TAUBA nenda kashufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Thathna sita ayani, arba mitakatifu, Ndipo utaibaini, yote kwa ukamilifu, Rajabu wa pili ndani, ya minne ile safu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Adhimu yake thamani, zaidi ya maradufu, Aula tuuthamini, dhuluma si yake kufu, Ya ndanimwe tusikhini, tuyaenzi kwa insafu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Maovu tuyaacheni, kwa ya Ilahi hawafu, Na mema tuzidisheni, katu yasije tukifu, Kesho yaje tuauni, baada ya wetu ufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Nimeka ukingoni, siwezi kujikalifu, Lengo kukumbusheni, mzidishe matukufu, Yatakayokufaeni, kesho mbele ya RAUFU, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Katika kusikiliza mashauri ya aridhi, baraza hili litakuwa limekamilika kisheria endapo kutakuwepo na Mwenyekiti pamoja na wazee wa baraza wasiopungua wawili. Wazee hawa wa baraza wataitajika kutoa mawazo yao katika shauri husika kabla mwenyekiti hajatoa uamuzi katika shauri husika. Na ili kufikia katika uamuzi mara nyingi mwenyekiti atalazimika kufuata ushauri au maoni ya wazee wa baraza lakini mwenyekiti halazimishwi kufuata mawazo hayo cha msingi anaweza kuyakataa kwa kutoa sababu itakayoonyesha kwanini anapingana na mawazo ya wazee wa baraza. Kikawaida mwenyekiti katika baraza la Ardhi la Wilaya huchaguliwa na waziri husika. Na mwenyekiti ni lazima awe mtu ambaye ana taaluma ya sheria ( legal qualied person) na ataweza kuiafanya kazi yake hiyo kwa muda wa miaka mitatu, na vilevile ataweza kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo. Kikawaida kwa mujibu wa sheria, mwenyekiti huyo kabla hajaanza kazi yake ni lazima ale kiapo, kiapo hicho kitasimamiwa na mkuu wa mkoa katika mkoa ambao baraza hilo lipo. Waziri wa aridhi baada ya kujadiliana na mkuu wa mkoa atachagua wazee wa baraza la aridhi lawilaya wasiopungua saba, kati yao wakiwemo wanawake watatu. Mtu yeyote mwenye umri kuanzia miaka 21 ataweza kuchaguliwa kuwa mzee wa baraza la Ardhi la Wilaya. Isipokuwa mtu hawezi kuteuliwa kama mzee wa baraza endapo tu, siyo mkazi wa kila siku katika wilaya husika, mtu huyo hawezi kuteuliwa kama ni mbunge, au mabaye akili yake si timamu au mtu huyo alishawahi kfungwa ( has been convicted of criminal offence) au mtu huyo sio raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. mwenendo wa shauri katika baraza la Ardhi la Wilaya linapaswa kusikilizwa sehemu ya wazi ili kuruhusu umma kuka na kuangalia mwenendo mzima wa sahuri. Na mlalamikaji au mlalamikiwa anweza kufika kwenye baraza na kusimama yeye binafsi au kwa kutumia wakili wake au kwa kutumia ndugu yake. Katika usikilizaji wa mashauri, Baraza la Ardhi la Wilaya litaweza kutumia lugha ya kingereza au Kiswahili itategemea na mwenyekiti atakavyoamua akizingatia hali halisi ya shauri lilipo mbele yake. Lakina maandishi pamoja na hukumu (records and judgment ) ni lazima iwekwe kwa lugha ya kingereza.

Serikali chanzo cha vurugu Zanzibar


Sasa kupata uthibitisho juu ya ukweli wa Muungano huu ni kuutoa mkataba na kuupeleka Bungeni na katika Baraza la Wawakilishi ili kwa niaba ya wananchi waliowachagua, wapate kuuona na kuthibitisha ni Muungano wa aina gani waliokubaliana viongozi hao wawili ambao ni hayati hivi sasa. Isitoshe walikuwepo viongozi wengine wawili vile vile walionekana siku ya utiaji sahihi mkataba huo wakiwa nyuma ya Hayati Abedi Amani Karume wakati akionekana kutia sahihi. Lakini na wao wote wawili ni Wazanzibari bahati mbaya wameuwawa. Sasa mashaka ndio yaliotawala kwa Wazanzibari kuhusu nchi yao. Ni lazima, tena ni lazima watu wadai ukweli wa nchi yao. Kosa hapo liko wapi? Hili hasa ndio juhudi za Uamsho hapa Zanzibar kutaka kuuona Mkataba wa Muungano, na kila dalili zinajitokeza kwamba Serikali ya Muungano kupitia kwa watu wake hapa Zanzibar wanakataa kata kata kuonesha Mkataba huo. Una nini? Je! ndani ya makubaliano hayo yapo ambayo viongozi wa Bara wanajaribu kutaka kuuficha umma wasielewe kilichokuwemo ndani? Wasi wasi mwengine ni pale mmoja katika waasisi hawa wawili alipoanza kuwatisha wananchi wote wa Tanzania na kuwaambia ni marufuku kujadili masuala ya Muungano na yeyote atakaejaribu kujadili basi huyo ni haini. Maneno hayo anayasema wakati Karume hayupo duniani. Ameshauwawa. Na ndio uzi huo huo wanaopokezana viongozi wa Bara kutoka Mkapa hadi huyu Mh. Kikwete. Eti msijadili Muungano. Ni nani mwenye mamlaka ya kuweza kuwazuia wananchi wasijadili mustakabali wa nchi yao. Kwani Serikali inapata uwezo wake kutoka wapi? Ni wananchi ndio wanaoipa Serikali mamlaka. Leo ni jambo la ajabu Serikali hiyo hiyo iwawekee mipaka wananchi kujadili suala la nchi yao. Serikali zote mbili zinaelewa wazi wazi kabisa kwamba ni kitu cha hatari kubwa sana kumuiba kiongozi wa Taasisi kubwa ya kidini hapa Zanzibar kiongozi wake (Kiongozi wa Muamsho) tena wanaingia msikitini kwa khadaa na kujifanya ni waumini kwa kufanya

13

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Na Ibrahim Mohammed Hussein

Zanzibar tuna utendaji wa aina mbili wanaotumikia Serikali mbili. Kwanza Serikali ya Zanzibar, pili Serikali ya Muungano. Kwa mujibu wa sheria vyombo vyote vya Muungano hasa hasa Polisi na Jeshi vinawajibika moja kwa moja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na sio Rais wa Zanzibar. Upande wa Polisi hali ndio hiyo hiyo na zaidi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambae hivi karibuni alikuwa ni Mzanzibari Mh. Shamshi Vuai Nahodha. Kutokana na mikakati mipya ya kiutendaji amekabidhi kazi hiyo kwa Mh. Emmanuel Nchimbi. Huko nyuma niliwahi kuandika katika makala zangu kwamba kama kutatokea machafuko Zanzibar, basi mchafuko huo utakuwa umesababishwa na Serikali ya Muungano pale wanapokataa ombi la Wabunge wake ambao kwa nyakati tofauti walipodai Bungeni kutaka uwasilishwe mkataba wa Muungano ili Bunge lipate kuuona mkataba huo. Wazee kumi Visiwani Zanzibar walifungua kesi Mahakamani. Dai ni hilo hilo. Mkataba wa Muungano wa asili. Mwana sheria anasema yeye hakuuona kabisa. Sasa hawa viongozi wa dini na wao wamepatwa na mashaka ya kutoamini kwamba nchi hii imechukuliwa kimabavu. Haina mkataba wowote ule na kama upo utolewe ili wenye nchi yao (raia) wapate kuuona mkataba huo. Ndani ya mkataba ndio kuna maneno yote waliokubaliana Viongozi wawili Nyerere na Karume. Wengi wanasema kwamba mkataba huo ulikuwa na makubaliano ya miaka kumi, wengine wanasema ni milele.

WAISLAMU Zanzibar wakiwa katika maanamano ya amani. usanii wa kujivisha kanzu kwa malengo ya kutuletea madhara nchini mwetu kwa kumkamata kihuni kiongozi mwenye heshima anae aminika na mwenye wafuasi wengi nyuma yake. Nini malengo ya Serikali yetu hii inayoongozwa na Dk. Shein inayodai kwamba inafuata sheria na kuongozwa na katiba leo wafanye vitendo viovu namna hii? Je! kama kiongozi huyo alitenda jinai kwa nini ashikwe kihuni na wasimpelekee notisi ya Mahakama kwa kosa lake baada ya kupita taratibu za kisheria zilizowekwa nchini? Ni nani huyo anaetoa amri za kutaka kuirudisha nchi hii katika hali mbaya ya nyakati za nyuma? Huu ndio mwendo wa Serikali ya kitaifa ambayo ilileta maridhiano na umoja nchini mwetu? Au hizi ni njama za kutaka kuivuruga amani iliokwisha patikana? Lazima uchunguzi ufanywe ili ibainike ni nani huyo asiejua nidhamu ya kuwakabili viongozi wa dini wenye heshima kubwa nchini mwetu kwa kutumia taratibu zenye heshima na busara. Dhamana hii iko mikononi mwenu viongozi wawili ndani ya Serikali ya umoja wa kitaifa, kama alivyowahi kusema kwenye sherehe moja iliyowahi kufanywa Pemba, Mh. Hassan Nassor Moyo, ni yeye aliesema kwamba viongozi hawa wawili ndio dhamana wa serikali hii ya kitaifa yaani Mh. Dk. Sheni na Mh. Maalim Seif Sharif Hamad. Natumai aliwaambieni Mh. Hassan Nassor Moyo kwamba msikubali kumuachia yeyote yule kutuharibia umoja wetu ambao ulipatikana katika juhudi kubwa sana zilizofanywa na watu mbali mbali kwa mashirikiano. Sasa leo akitokezea kiongozi huko Bara au hapa Visiwani akatoa amri zake bila ya kutumia busara, basi huyo hatufai. Dua na visomo vimnase mtu huyo bila ya huruma. Wazanzibari wanaposema Zanzibar imemezwa hawajakosea hata kidogo. Na jamii ya wamezaji wapo hapa Zanzibar kibao (yaani wengi) hawa watatupa tabu kwa vile wamo ndani ya Serikali katika nafasi mbali mbali hasa upande wa Polisi. Wasi wasi wangu isijekuwa wamepata kipenyo cha kutaka kuturudisha tulikotoka. Washughulikiwe na Serikali kabla hawajaichafua nchi yetu. Bado vidole vyao vimejaa damu ya ndugu zetu huko Pemba wala hawakufaulu kuifuta damu hiyo ambayo itabaki vidoleni mwenu hadi mwisho. Hapana kitu kibaya kama kuwafanyia wananchi mambo ambayo sote tuliyakataa wakati wa kutawaliwa na mkoloni. Leo vinatumika vyombo vya dola kuwanyamazisha Wazanzibari kwa kutumia mabomu ya machozi, magereza na risasi za moto kuwaulia Wazanzibari wasio na hatia. Nini cha mno? Wanadai kura ya maoni ya nchi yao ndio kosa hilo? Je! na sisi tunaiga mambo ya mkoloni? Siku zote hutuba zao ni za kujisifia CCM ndio iliyojenga nchi, Tukiondoka kila kitu kitatokomea, na nchi hii itarudi tena kwenye biashara ya Utumwa Hizi ndio dizaini ya hotuba zao. Hivi sasa Zanzibar kumekucha na mbiu ya Wazanzibari ni kuwaambia wenzi wao wa Tanganyika waamke. Wazanzibari hivi sasa wameshaamka baada ya kupitiwa na Uamsho. Wengi miongoni mwetu tulikuwa tukiamini kwamba mtu hawezi kuepuka lile aliloandikiwa, hapo maana yake ni mgandamizaji wake hana lawama tena. Hivi ndivyo tulivyokuwa tukiamini. Yaani uovu wa Serikali yetu ni kitu kilichoamriwa. Huku ni kuamini dini kinyume nyume. Uamsho ndio umefanyakazi ya kuwashajiisha umma udai haki zao za kimsingi na kikatiba. Unajua, mtu yeyote anaweza kuwa raia wa nchi yeyote, lakini si kila raia anaweza kuwa mzalendo, kwani uzalendo ni hali ya mtu kupenda nchi yake. Kwani kuipenda nchi na kuipenda Serikali iliyoko madarakani ni vitu viwili tofauti. Wapo wananchi ambao kwa sababu wanazozijua wao hutokea kuichukia Serikali lakini ndani ya mioyo yao wanaipenda nchi yao kikomo. Mara nyingi watu wa aina hii kutokana na kuichukia Inaendelea Uk. 14

14
Inatoka Uk. 6

risasi za moto ambapo watu wawili waliuliwa. Akaongeza kuwa kumekuwa kukifanyika semina za watu kutoka Bara na nchi za nje ambapo wajumbe wa makanisa wamekuwa wakihoji kwa nini kuna kuwa na osi za Kiislamu kama ile ya Kadhi Mkuu. Prof. Sharif anasema kuwa watumishi hao wa kanisa wanasahau kuwa Zanzibar ni Waislamu na kwamba katiba yao haisemi kuwa Zanzibar haina dini kama ilivyo ile ya Tanzania. Anybody who knows anything about Zanzibar will know that 97% of the people of Zanzibar are Muslims. She/he should also know that religion is not a Union matter, and that the Zanzibar constitution nowhere says nchi hii haina dini. Anasema.

Prof. Sharif ataka kiini cha tatizo kichunguzwe


Kwa upande mwingine Prof. Sharif anashangaa jinsi viongozi wa kisiasa na vyombo vya habari walivyokuja juu katika jambo hili wakati hawakusikika kabisa ilivyochomwa Quran. More recently, a young Christian man was instigated by the American preacher to burn the Muslims Holy Book, but I am happy to say we did not hear Muslims retaliating by burning the Bible. So the fundamental question is why cases of intolerance have increased since 1987? Anahoji Prof. Sharif akikumbusha kuwa ni hivi karibuni tu

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

PROFESA Abdul Sharif

Serikali chanzo cha vurugu Zanzibar


Inatoka Uk. 13 Serikali au kuwakosoa watawala, hupewa majina mbali mbali kama vile, Hizbu anataka kurudisha utumwa au Usultani n.k. Wapo vile vile watu ambao kwa nje hujionesha kujipendekeza sana kwa Serikali wakati hawana hata chembe ya kuijali nchi wanayoishi. Hii ndiyo sifa ya viongozi wetu wengi hapa Zanzibar. Kwa upande mwingine, wapo viongozi wabaya ndani ya serikali ya Dk. Shein ambao hawakulipenda kabisa suala la Serikali ya pamoja. Ni hao ndio hawalali usiku wamo wakipika na kupakuwa ili ipatikane sababu ya kuchafua nchi. Jambo la hatari viongozi hao wanawatumia polisi kutaka kuleta vurugu na kuondoa amani nchini mwetu. Ni lazima Serikali ya pamoja iunde tume ilio huru kabisa kulichunguza jambo hili lisiwachwe hivi hivi. Likiwachwa hili la awali, basi kuna mengi yatafuatia. Nasema njama zipo za kuchafua Nchi wanaumwa wakiona umoja wetu hapa Visiwani. Kumbukeni nasaha za Mzee Moyo alizokwisha zitoa huko Pemba siku za nyuma. Kuchomwa kwa Makanisa ni jambo baya sana nalo lichunguzwe. Wala pasifanyiwe haraka. Nalo hilo vile vile ni miongoni mwa mbinu chafu zilizopangwa na genge hilo hilo lisilotakia mema nchi yetu. Rekodi ya matokeo ya uchomaji moto yapo mengi hapa Visiwani. Hebu tukumbuke kiwanda cha saateni cha mbao kilichoingiliwa usiku kwa kutumia gari. Watu wakaona ni akina nani walofanya mambo hayo. Ghasia hizi za sasa ni njama za baadhi ya viongozi wabaya wanaotaka kuturudisha tulikotokea. Tume huru iundwe kuikabili kamati ya Usalama ya Mkoa. Ni nani huyo aliotoa rai ya kwenda kukamatwa Sheikh Mussa Abdalla Juma msikitini? Hapo ndio pakuanzia. Serikali lazima iwe makini muhimu ni chanzo cha mchafuko ni nani alisababisha hayo yote kutokea. Nilipokuwa nikiandika makala hii sikuwa na habari kwamba viongozi kutoka Tanzania Bara (Tanganyika) watawasili Zanzibar akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani EMANUEL MCHIMBI pamoja na I.G.P Bw. Said Mwema na wengi wengineo hata Marais wetu wastaafu Mzee Mwinyi na Mkapa walikuwepo na wao, kujatoa ushauri kama walivyopewa daraja hiyo. Kuna mambo matatu angalau kwa kifupi nidokeze wasomaji wa gazeti hili la AN-NUUR ili na wao wapate kuelewa hali halisi ya kikao cha wakubwa hawa. Lakini kwanza kumetokea mshangao hapa Zanzibar baada ya kuona Helikopta mbili za Polisi ili kuja kusaidia kuidhibiti hali ya hewa iliyochafuliwa na Serikali kwa makusudi kabisa. Mshangao huo ni wakati Meli ya MV. SPICE ilipokua inazama, hatukuziona helikopta za polisi kuja kuokoa wananchi na hiyo helikopta iliyokuja Zanzibar ni ya watu binafsi sio ya Serikali. Jambo la kushangaza wakati wa kutaka kuwapiga mabomu ya machozi wananchi wa Zanzibar, upesi upesi walizileta helikopta mbili kwa haraka sana. Hilo ni moja. Pili, kumbe hali ya Zanzibar ilipochafuliwa na mabomu ya kutoa machozi, vijana wetu walikuwa wakisherehekea utafikiri wanacheza ngoma. Kumbe ilikua ni mradi wa vikopo vya aluminium vya hayo mabomu vikikusanywa na kwenda kuuzwa. Ndio maana vijana wengi waliichangamkia hio hali na kuzidi kuwatia mori Polisi wavurumishe vikopo hivyo. Tena vijana walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe katika kuvivamia vikopo hivyo. Hili la tatu ni hatari tupu. Nilipokuwa nikitazama TV usiku nilibahatika kumuona Waziri wa Mambo ya Ndani Emanuel Nchimbi akiongea na watu mbali mbali wakiwemo watu wa dini, mabalozi wa nchi za Nje na waandishi wa habari. Mmoja katika mashekhe walipata bahati ya kuzungumza alimueleza Waziri wa Mambo ya Ndani kwamba ghasia hizi na uharibifu huu umesababishwa na Polisi pale walipotumia utaratibu mbovu usiokua na busara ndani yake. Kwenda kumvizia Sheikh Msikitini mbele ya waumini na kumkamata kihuni. Hilo ndio kosa na chanzo cha vurugu zote hizo zilizotokea. Baada ya juhudi kubwa ya I.G.P pamoja na lugha na busara ya hali ya juu kabisa alioitumia, aliweza kutuliza hali vizuri. Nimeshangaa, sikuamini masikio yangu kwamba kweli Waziri huyu angalithubutu kusema maneno aliyoyasema. Alisema, nakariri: Wallahi (kiapo kikubwa hicho) tutaendelea kuviziana msikitini, tutamkamata wapi na pale ndio tulipompata. Nini maana ya maneno hayo ya kukosa busara? Kukamatwa kwa Sheikh kulikosa busara na ndio iliozaa mchafuko. Waziri nae anatumia maneno yale yale ya kukosa busara tena kwa kiapo kizito cha Wallahi. Sasa maana yake nini? Juhudi yote iliofanywa na I.G.P ni kazi ya bure. Kama tutaendelea kuviziana, basi Waziri awe tayari kupokea matokeo ya kuviziana ambayo kila mtu ameyaona mbele ya macho yake.

kijana wa Kikristo kwa kuchochewa na mchungaji wa Kimarekani alichoma moto Quran, l a k i n i Wa i s l a m u hawakuchukua hatua za kulipiza kisasi. Anasema, jambo la kujiuliza, ni kwa nini matukio kama haya ya tna za kidini yamekuwa yakiongezeka toka mwaka 1987? Kwa upande mwingine Profesa aligusia lile tukio la Pwani Mchangani, ambapo ilidaiwa k u w a Wa z a n z i b a r i wanawachukia na hawawataki Wabara. Hata hivyo akahoji, ni kwa nini watu hawajiulizi kwamba inakuwaje wanaofaidi shughuli za utalii ni Wabara tu na watu wa Nungwi wanachoambulia ni kuharibiwa maadili na familia zao? (Soma makala ya Profesa Sharif Uk. 15)

15
By Prof. A Sharif
wanted to live at peace with the local Muslim majority. They had regular cordial debates with the Muslim clerics of the time, including Shaikh Mansab bin Ali of the renowned clerical family of Zanzibar. Part of the land on which the cathedral was built was donated by the Hindu Customs Master, and Sultan Seyyid Barghash donated the clock that is still in the tower of the cathedral. During all my study of the history of Zanzibar there has never been a confrontation between these two religions until 1987. So what happened in 1987? The country was then discussing personal law, marriage and inheritance, and the Muslims said that we were bound by the Islamic Shariah, as they had every right under the constitution to believe and practice their religion. A prominent woman political leader of the ruling party on the mainland said we will change the Shariah. Muslims in Zanzibar were incensed, and they came out in a demonstration to protest against this infringement of their rights. They were met by the police, an arm of the Union government, with live fire, and two people were killed. The commission under the late Abdulwahid Boraa conrmed that the Muslims were unarmed and peaceful; but no remedial action was taken to bring the culprits to book. More recently, a young Christian man was instigated by the American preacher to burn the Muslims Holy Book, but I am happy to say we did not hear Muslims retaliating by burning the Bible. So the fundamental question is why cases of intolerance have increased since 1987? We will be the proverbial ostriches if we bury our heads in the sand if we conclude that all this is because udini and hatred against Christians have suddenly flourished in Zanzibar even more luxuriantly that our cloves, and these are always carried out by one religion against the other. It needs two to tango. The fact is that over the past two decades, we have been going full speed to develop tourism as the primary foundation of our economy, and aiming to

Feature

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

The Zanzibar Riots, the Union, and Religious Tolerance


NOBODY in his right mind would condone the torching of churches and shops in Zanzibar last weekend. But it is a great shame that so many, including some of the top leaders in the country have made these symptoms of a socio-political malaise in the country the central issue for discussion rather than looking at the disease itself. It seems to have been a bonanza for most of the newspapers on the mainland who have used this to launch for what I can only call Islam and Zanzibarbashing spree for more than a week. As a Zanzibari I am proud to say we have had more than 170 years of history of Muslim-Christian interaction in our islands, and before 1987 we never had anything but cordial relations between all religions in our country. Anybody who disagrees with this can produce the evidence. The highest denomination of Zanzibars independence stamps carried the theme of religious tolerance, designed by our revered art teacher Mr Abdalla Farhan, showing the Catholic and Anglican cathedrals, a Sunni and a Shia mosque, and even a Hindu temple. Nobody should try to teach lessons about religious tolerance. The modern history of Muslim-Christian interaction in Zanzibar goes back to 1840 when the German Christian missionary Dr. Johanne Krapf visited Zanzibar to ask for permission to build a church at Mombasa which was then part of Zanzibars territory. According to the missionarys own testimony, the Muslim Sultan of Zanzibar, Seyyid Said bin Sultan wrote to his governor in Mombasa in which he said: I am sending you Dr Krapf. He is a man of God who wants to spread the word of God. Do everything in your power to facilitate his work. This was not because Seyyid Said was a uniquely tolerant ruler, but because this was the tradition of religious tolerance in the Indian Ocean before the coming of the colonialists. Thirty three years later, Bishops Steere and Tozer came to Zanzibar to build the Anglican Cathedral at Mkunazini, but these were enlightened people who quadruple the number of tourists coming to Zanzibar to half a million, without considering the way we are doing it and the inevitable consequences for our society and culture. I have been dismayed to see how some of our shing village communities have been turned upside down by the invasion of tourism. Nungwi at the northern end of Unguja was inaccessible before the tarmac road was built in the 1970s, and I had the fortune to visit it in 1979. It was a beautiful stable Zanzibar village community not very prosperous, but I remember it as a clean village in which almost every house had a well-kept carved Swahili door. It destroyed my assumption that isolation from the town meant poverty and desolation. A few years ago I had the misfortune to revisit Nungwi to give a lecture at one of the beach hotels that now completely encircle the whole Nungwi peninsula. I could not nd that village any more. It had been completely over-run by a shanty town of tourism kiosks, bars with blaring foreign music, and brothels. As former President Ali Hassan Mwinyi once said, when you open the window to get fresh air, flies also come in. A few years ago the women of Nungwi took out a demonstration against this invasion that was stealing their husbands and destroying their families. But has anything been done to rein in these misfortunes of our villagers, beyond saying bahati mbaya, utandawazi, etc.? Last year there was another outbreak with the burning of 80 tourist shops and hovels at Pwani Mchangani, and all the mainland-based newspapers plastered their front pages with stories and pictures about Zanzibaris hating Wabara. Nobody investigated why all these shops in a Zanzibari village were owned only by Wabara, and why local villagers were not benetting from the tourism bonanza, but only having to suffer from its bars and brothels. But there is still the question why the churches were targeted. As I said above, places of worship and their holy books must be respected by all, whether mosques and churches, or the Quran and the Bible. A lot has been said about

Archbishop of the Anglican Church in Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa.

the culpability of Uamsho in this saga, but nobody has documented the evidence either of their direct instigation or their so-called hate sermons. Their DVDs are freely available, and it should be easy to document this for anyone who wants to speak on the subject. But most of those who have spoken or written have not cared to see them. Mao tse Tung used to say: no research, no right to speak. But, again as I said above, it takes two to tango. Are we so absolutely sure that the clerics of all the other denominations are clean on this score? I cannot say what is being preached in all the mosques and churches, but I was a witness to one incident that was frightening. A Norwegian missionary organized an interfaith meeting last year in Zanzibar, and I was invited. I was abbergasted to hear a cleric from the Anglican Cathedral say that since Tanzania was a secular state, why is the Zanzibar Government nance the Qadhis courts here? Anybody who knows anything about Zanzibar will know that 97% of the people of Zanzibar are Muslims. She/he should also know that religion is not a Union matter, and that the Zanzibar constitution nowhere says nchi hii haina dini. There have been Qadhis courts here even before the coming of the British. In their wisdom they did not abolish them but allowed Muslims to practice their religion in terms of personal law. For more than a century the dual jurisdiction has worked smoothly to the satisfaction of all, including non-Muslims who could take their cases to the countrys civil courts. So who is this cleric to add insult to injury by proposing the Qadhis courts should be

abolished in Zanzibar, as they were in Tanganyika in 1963, and why at this stage when Muslims on the mainland are demanding restoration of their Qadhis courts? Fortunately, it was not left to a Zanzibari Muslim to answer him, which would have made it a Christian-Muslim malumbano. A wise Christian Copt from Egypt stood up to answer. He said: I am really surprised. We Copts constitute 10% of the population in Egypt, but we have to recognize that 90% of the people are Muslims who want to be governed by their religious rules in these matters. Why should we object? Here, you Christians form less than one per cent of the people, and you want to abolish the Qadhis courts? Nothing more needed to be said. So wisdom is called for on the part of all responsible leaders, religious or otherwise. And this relates not only to this sensitive question of religion, but in all matters during this critical period. I was dismayed when I read the story by Mwinyi Sadallah in the Nipashe of 31st May, 2012 quoting the Archbishop of the Anglican Church in Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, saying that the suspects wakamatwe, wapigwe bakora na polisi na baadaye wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. When we are writing the

new constitution in which we should be safeguarding the human rights of all people against police brutality, should a responsible cleric be giving them free license to beat up people before they have been convicted of any crime? I just hope that he has been misquoted. If he was, then the journalist should apologise to him and to the rest of us.

16

AN-NUUR
16
Na Shaaban Rajab

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8-8,, 2012

USIKOSE KUSOMA AN-NUUR KILA IJUMAA

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 8 - 14, 2012

AN-NUUR

Sensa hatutauliza dini wala kabila - Hajat Amina


WAKATI Waislamu nchini wakitaka kipengele cha dini kwa ajili ya kujua idani ya watu kwa dini zao kujumuishwa katika zoezi lijalo la sensa ya watu na makazi, Osi ya Takwimu nchini imetoa ufafanuzi kwamba hakutakuwa na kipengele cha kuuliza dini wala kabila la mtu katika zoezi hilo linalotazamiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu. Hayo yameelezwa na Kamishna wa S en s a n ch i n i H a j a t Amina Mrisho Said, katika semina ya siku moja kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika wiki iliyopita Peacok Hotel jijini Dar es Salaam. Hata kule Nigeria, hadi leo wameshindwa kutoa takwimu hizo, kwamba ni kabila gani wapo wengi au dini gani ndio wengi zaidi, hii imetokana na kila upande kuamini kuwa wao ndio wengi kuliko wengine. Ni wazi kwamba hakuna upande utaokubali na kuziamini takwimu hizi za dini na kabila, hakuna upande utakaokubali n a k u r i d h i k a . Wa Ibo wanaamini wao ndio wengi kuliko kabila lolote pale, Yoruba kadhalika nao wanaamini vivyo hivyo, Waislamu wanaamini hivyo kadhalika na Wakristo, Alifafanua Hajat Amina. Alipoulizwa kuhusu takwimu za idadi ya Waislamu na Wakristo zinazotolewa na baadhi ya vyombo nchini kuwa zinatoka wapi na ni sahihi au la, Kamishna huyo alisema takwimu hizo ni za mitaani na sio sahihi hivyo zipuuzwe. Akijibu swali hilo Kamishna Amina Said, alisema tangu mwaka 1978 hakuna sensa iliyowahi kufanywa na kuhusisha idadi ya wana dini au makabila nchini. Zilizofuatia, yaani ile ya mwaka 1988 na 2002 zilifanyika bila kuwepo vipengele vya idadi ya wana dini na makabala. Hivyo alibainisha kwamba kama kuna takwimu zinazotolewa za idadi au kiwango cha wana dini au kabila, takwimu hizo sio sahihi na zipuuzwe kwani zina lengo la kuchonganisha watu. Tunafanya sensa kujua idadi ya Watanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo, takwimu rasmi zinapatikana sehemu rasmi na sehemu hiyo ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu na si kwingineko. Alisisitiza. Aidha alisema kuwa walimu wapatao laki moja na nu s u ndio wataotumika kutekeleza jukumu la kuchukua idadi ya watu. Alisema tayari osi ya Takwimu inawasiliana na serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la ile ya Zanzibar ili kurekebisha mihula ya shule kwa ajili ya kupata fursa kwa walimu na wanafunzi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, hasa ikizingatiwa kwamba zoezi hilo kwa kiasi kikubwa litafanywa na walimu.

Watoto yatima waliowakilisha Zanzibar katika sherehe za mtoto yatima kimataifa zilizofanyika Istanbul, Uturuki hivi karibuni. Watoto hao ni Shufaa Mohamed Ali, Luta Sheha Hassan, Hajir Humoud Khalid na Salum Ali Mohamed. Viongozi walioandamana nao ni Farouk Hamad Khamis, Abdalla Hadhar Abdalla na Nassra Suleiman Abdalla, wote kutoka taasisi ya Muzdalifah Islamic Charitable Organization.

Hassan Salim ametutoka


Na Mwandishi Wetu USTADH Hassan Salim amefariki dunia siku ya Jumamosi mchana saa nane katika hospitali ya Mwananyamala alikokua amelazwa kwa kipindi cha wiki moja. Hassani alikua anaugua akisumbuliwa na mguu aliochomwa na singe ya bunduki na kupigwa na mabomu mengi sana ya moshi. Ilikua ni siku ambayo Waislamu walihudhuria kesi ya wachungaji waliochoma Quran katika mahakama ya mkoa wa Mwanza. Hassan akiwa ni katika Waislamu waliohudhuria kesi hiyo, polisi walianzisha fujo na kuwapiga Waislamu kwa mabomu na kuwajeruhi kwa singe akiwemo marehemu. Kuania hapo, afya ya Hassani ilianza kudhooka hadi pale alipojulishwa kuwa mapafu yake yaliathirika vibaya na moshi mzito. Ustadhi Hassan alikua ni mwalimu wa kujitolea kufundisha somo la Maarifa ya Uislamu katika shule za sekondari za Kirumba, Kabuhoro, Mihama, Mnarani, Kiloleli na Nyasaka. Kwa upande wa shule za msingi, Hassani amefundisha Kirumba na Kitangiri. Aidha amefundisha madrasa ya kina mama na watoto Kitangiri, Jiwe kuu na Masjid Hidaya. Kwa upande mwingine, Hassan alikua ni katika waasisi na mwenyekiti w a Ta a s i s i y a I Q R A FOUNDATION, taasisi ya walimu wafundishao elimu ya dini ya Kiislamu mashuleni na vyuoni pamoja na kutetea haki za wanafunzi na ustawi walimu Waislamu jijini Mwanza. Hassan Salimu

alijitegemea kimaisha kwa kazi yake ya useremala iliyomuwezesha kupata kipato kiasi cha kutomtegea. Hassan Salimu alikua ni miongoni mwa Waislamu wa mwanzo kuanzisha darasa la watu wazima maarufu kama Thaqb chini ya mwalimu wao Ustaadh Ilunga. Kupitia darasa hilo, mchango wa Hassan hautasahaulika katika kuchangia ujenzi wa vituo vya Kiislamu. Akiwa fundi, Hassan alijitolea kuona vituo vinasimama na watoto wa Kiislamu wanasoma. Kifo cha Hassani kina mafunzo mengi moja muhimu likiwa ni kutumia muda na mali zetu vizuri katika uchamungu kwani hatui muda wa kuondoka. I n n a l i l l a h i wainnailayhir rajiuun.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like

  • ANNUUR 1188a
    ANNUUR 1188a
    Document20 pages
    ANNUUR 1188a
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Annuur 1193
    Annuur 1193
    Document20 pages
    Annuur 1193
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Annuur 1190
    Annuur 1190
    Document20 pages
    Annuur 1190
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1185
    Annuur 1185
    Document20 pages
    Annuur 1185
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1178
    Annuur 1178
    Document20 pages
    Annuur 1178
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Document20 pages
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Document20 pages
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • ANNUUR 1110cc
    ANNUUR 1110cc
    Document16 pages
    ANNUUR 1110cc
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Document20 pages
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1093
    Annuur 1093
    Document16 pages
    Annuur 1093
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1107
    Annuur 1107
    Document16 pages
    Annuur 1107
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1102
    Annuur 1102
    Document12 pages
    Annuur 1102
    annurtanzania
    No ratings yet
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Document20 pages
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Document20 pages
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Document16 pages
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    No ratings yet
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Document0 pages
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Document12 pages
    Annuur 1090
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1105
    Annuur 1105
    Document12 pages
    Annuur 1105
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1096
    Annuur 1096
    Document12 pages
    Annuur 1096
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1094
    Annuur 1094
    Document16 pages
    Annuur 1094
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1088 PDF
    Annuur 1088 PDF
    Document12 pages
    Annuur 1088 PDF
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Document16 pages
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Document12 pages
    Annuur 1090
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1089
    Annuur 1089
    Document12 pages
    Annuur 1089
    Hassan Mussa Khamis
    No ratings yet