Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 7

Jiepushe Na Moto Wa Jahannam Pamoja Na Familia Yako

Nasiha Mbali Mbali

Anasema Allaah :

)) (
((Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Allaah kwa Anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa)) [At-Tahriym 6] 'Aliy bin Abi Talhah amepokea kutoka Ibn 'Abbaas kwamba amesema kuhusu Aayah hii: "Mtiini Allaah na jiepusheni na kumuasi Allaah na amrisheni familia zenu kumkumbuka Allaah ili Allaah Awaokoe na moto wa Jahannam". [At-Twabariy 23: 491] Kutokana na Aayah hiyo, ni wajib wa Muislamu kufundisha familia yake; ikiwa ni mke au mume, watoto, ndugu, wazazi na kadhalika, mambo yaliyo fardhi kufanya na kuwakataza yaliyoharamishwa. Hadiyth ifuatayo inathibitisha maana ya Aayah hiyo:

: : )) )) .:
Imetoka kwa 'Abdul-Malik bin Ar-Rabiy' bin Sabrah kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake kwamba amesema Mtume (( : Amrisheni watoto kuswali watakapotimia miaka saba, na wapigeni [ikiwa hawatoswali] watakapotimia miaka kumi)) [Imaam Ahmad, Abu Daawuud, na kasema At-Tirmidhy Hadiyth Hasan] Na kuwaamrisha watu wako, mfano watoto kuswali ni kudhihirisha mapenzi yako kwao kwani hutopenda watoto wako waingie motoni, hivyo unapowaonea huruma asubuhi wasiamke kuswali Swalah ya Alfajiri, sio maana kuwa unawependa bali ni kinyume chake, kwa vile unawasababisha wawe miongoni mwa watu wa motoni. Watu wa Peponi watakapowaona watu wa motoni watawauliza sababu ya kuingia kwao huko motoni na sababu mojawapo watasema kuwa ni kutokuswali:

(()) (( )) (( )) (( )) (()) ( ( ))
((Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma)) ((Isipokuwa watu wa kuliani) ((Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana)) ((Khabari za wakosefu)) ((Ni nini kilichokupelekeni Motoni?)) ((Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakiswali)) [Al-Mudathhir: 38-43 Bila ya shaka kuamrisha familia yako kuswali ni jambo gumu sana na ndio maana Allaah Alipoamrisha jambo hili Alitutaka tuendelee nalo kwani linahitaji kuwa na subira nalo, kama Anavyosema Allaah katika Aayah ifuatayo, ambayo 'Umar ibnul-Khatwaab alikuwa akiisoma huku akiamsha familia yake kuswali:

(())
((Na waamrishe watu wako kuswali, na uendelee mwenyewe kwa hayo)) [Twaaha: 132] Aayah hiyo ya mwanzo inaelezea hali ya huo moto kuwa:

(())
((kuni zake ni watu na mawe)) Watu hao ni sisi wana wa Aadam, na mawe ni masanamu yaliyochongwa yaliyokuwa yakiabudiwa kama Anavyosema Allaah :

(())
((Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Allaah ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu)) [Al-Anbiyaa: 98] Kisha Malaika wanaowaingiza hao watu motoni hawana huruma kabisa kwa watu waliomkufuru Allaah , hukimbilia haraka kumtii Allaah kuwaingiza watu motoni bila ya kuchelewa hata upepesi wa macho. Malaika hao wanaitwa Az-Zabaaniya (walinzi wa moto wa Jahannam) kama Anavyosema Allaah :

(())
((Nasi tutawaita Mazabania!)) [Al-'Alaq: 18] Basi tujitahidi kutimiza Swalah zetu kama zinavyopasa na kuamrisha familia zetu pia watimize Swalah ili tujiepushe sote na moto huo mkali wa Jahannam.

***********

Faida Ya Taqwa (Kumcha Allaah Subhaana wa Ta'ala)


(( ))... ((.. )) ((Na anayemcha Allaah Humtengezea njia ya kutokea)) ((Na Humruzuku kwa jiha asiyotazamia)) [At-Twalaaq: 2-3] Haya ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyotuletea katika uongofu kamili kwenye kitabu ambacho hakitafikia batili mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikma Mwenye Kuhimidiwa. Maneno yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)ni kuli ya Anavyosema haki (ni kweli) kama (()) ((Na ni nani msema kweli kuliko Allaah?)) [An-Nisaa: 87]

Aayah hiyo ya juu tukufu imetanguliza sharti mwanzo kwa kupatikana yale Aliyoyaahidi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Sharti hiyo ni kuwa na taqwa (Kumcha Allaah) ili jazaa yake ni Kujaaliwa njia (upenyo, kivuko) na Kuruzukiwa pale asipotegemea. Basi itakapopatikana sharti hiyo, yatapatikana hayo yaliyoahidiwa. Tujiulize swali, vipi kufikia taqwa? Au Nini maana ya taqwa? Jibu ni katika sentensi fupi iliyokamilisha kila kheri. Nayo ni "Kutekeleza yaliyoamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mtume na kujiepusha makatazo Yao na kubakia katika

mipaka". Hapo ndipo itakapopatikana taqwa. Na kuwa na taqwa ndio sababu ya furaha na kufuzu duniani na akhera, na pia ni sababu ya kuondoshewa shida na dhiki zote. Taqwa ni wasiya wa watu wa mwanzo na wa mwisho na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwausia Maswahaba wake wapenzi : : )) ((. : .: Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan Mu'adh Ibn Jabal (Radhiya Allaahu anhuma) ambao wamemnukuu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mche Allaah popote pale ulipo, na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya), na ishi na watu kwa uzuri)) [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na kasema kuwa ni Hadiyth Hasan na katika maandiko mengine imesemwa kuwa ni Hasan Swahiyh] Na Taqwa haihitajii kuhakikishwa kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haraam japokuwa hakuna mtu anayemuona. Na ndipo aliposema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa 'Taqwa iko hapa' akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.

Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah


Anasema Allaah :

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185] Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:


((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88] Vile vile Anasema Allaah :

(()) (( ))
((Kila kilioko juu Yake kitatoweka)) ((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27] Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah . Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah . Kisha Allaah Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,

(())
((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67] Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar kwamba:

)) : ((
((Allaah Atazikunja mbingu katika Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?)) [Muslim]

Hapo tena Atauliza mara tatu:

(())
((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16] Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,

(())
((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16] Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.

(())
((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]

************

Siku Ambayo Kila Mmoja Atakayomkimbia Mwenzake


Anasema Allaah

)) (()) (( )) (( )) (( )) ((
((Basi utakapo kuja ukelele)) ((Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye)) ((Na mamaye na babaye)) ((Na mkewe na wanawe)) ((Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha)) ['Abasa:33-37]

Ibn 'Abbaas amesema kuwa "As-Saakhkhah ni moja wapo wa jina la siku ya Qiyaamah, siku ambayo Allaah Amewaonya waja Wake". [At-Twabariy 23:229 Ibn Jariyr amesema: "Labda ni jina la kupigwa tarumbeta." [At-Twabariy 23:231] Al-Baghaawiy amesema: "As-Saakhkhah ina maana ukelele wa mngurumo wa siku ya Qiyaamah. Umeitwa hivyo kwa sababu utawazibua watu masikio. Hii ina maana kwamba utapenya katika masikio hadi kwamba utayazibua. [At-Twabariy 24:449] Na kama Anavyosema Allaah kuwa Siku hiyo kila mtu atamkimbia jamaa yake. Watakapoonana watakimbiana kutokana na kihoro na khofu ya hali ya juu itakayokuweko Siku hiyo. Hakuna mmoja atakayetaka kumsaidia mwenziwe. Hata mitume hawatotaka Siku hiyo kutusaidia, kila mmoja atasema "nafsiy nafsiy" (nafsi yangu, nafsi yangu). Hata 'Iysa mwana wa Maryam atasema: "Sitomuomba (Allaah) kuhusu yeyote ila nafsi yangu. Situmuomba hata Maryam ambaye amenizaa. [Muslim]. Mtume pekee atakayetuombea ni Nabii Muhammad . Hadiyth ifuatayo inatupa picha jinsi hali itakavyokuwa siku ya Qiyaamah:

: )) ((. : : ) ((.
Kutoka kwa Mama wa Waumini Aaishah kwamba Mtume amesema: ((Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah bila ya viatu, uchi na bila ya kutahiriwa)) Akasema Aaishah, ee Mjumbe wa Allaah, vipi watakuwa uchi? Akasema: ((Kila mtu miongoni mwao Siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha)) [AnNasaiy]

**********

You might also like