Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Ahlu Sunna Wal jamaa Hajj And Umra Trust


Inawatangazia nafasi ya hijja 1434h, 2013m Malipo ya gharama zote ni Dola 4300$ Karibu Ahlul Sunna wal Jamaa Osi yetu ipo Barabara ya Lumumba Jijini Dar es salaam katika jengo la Saba general, mkabala na Anatoglo Mnazi moja, ghorofa ya tatu kwa mawasiliano zaidi piga simu 0717 224437,0774462022

Wanafunzi Waislamu sasa waikataa NECTA


Tai ametua rasmi Afrika -Uk. 9
Waazimia kupiga kambi kwa Ndalichako Ni iwapo serikali itaendelea kuwapuuza

ISSN 0856 - 3861 Na. 1057 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Tusipotoshe agenda: Hoja ni Zanzibar huru

Si kuwepo au kutokuwepo Mkataba asilia Kama Amani hakuona, Shein kautoa wapi? Uk. 11

WAISLAMU Jijini wa Mashtaka Dk. sababu ya kuzuia D a r e s S a l a a m , Elliezer Feleshi wiki dhamana ya Sheikh Ponda Issa Ponda. wameazimia kuka ijayo, kutaka kujua Soma Uk. 16 kwa Mkurugenzi

Waislam kwenda kwa DPP Kizungumkuti cha kuhoji dhamana ya Ponda


Uk. 6

TAI - Alama ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kuashiria nguvu na uoni wa mbali.

Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume hawa ndiyo waasisi wa serikali za Tanganyika na Zanzibar; na kisha muungano.

muungano bila hati

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

Mgogoro wa gesi Mtwara haujaisha


Na Bakari Mwakangwale MJUMBE wa Shura ya Maimam, Mkoani Mtwara, Bw. Saalum Simba, amesema si kweli kwamba mgogoro wa Gesi, umekwisha kufuatia ziara ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, mkoani humo hivi karibuni. Bw. Simba ameyasema hayo, akitoa taarifa fupi, kuhusu ziara ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, katika m k u t a n o w a Wa i s l a m u , uliofanyika Temeke Jijini Dar ers Salaam, Jumapili iliyopita na kudaiwa kuwa, mgogoro wa gesi baina ya Serikali na wakazi wa Mikoa ya Kusini, umekwisha. Si kweli kwamba mgogoro wa gesi Mtwara umekwisha kama vinavyoripoti vyombo vya habari, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kufanya ziara katika Manispaa ya Mtwara, Mikindani. Alibainisha Bw. Saalum Issa Simba. B w. S i m b a , a l i s e m a msimamo wa watu wa Mikoa ya Kusini, ambao kauli mbiu yao ni Gesi kwanza uhai baadae. ni kwamba endapo Serikali haitobadilisha msimamo wake, wapo tayari kufa kuliko kuona gesi ikisarishwa. Alisema, msimao huo umejidhihirisha siku chache zilizopita, kwani imeripotiwa kuna baadhi ya wananchi wa Mtwara wamekufa, na miongoni mwa hao wawili ni Polisi. Akizungumzia yaliyojiri k a t i k a z i a r a y a Wa z i r i Mkuu, alisema, Mh. Pinda, alifanikiwa kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kupata maoni yao, ikiwemo Shura ya Maimam. Ust. Simba, alisema Shura ya Maimam, lilikuwa kundi la pili kuzungumza na Mh. Pinda, wakitanguliwa na wanasiasa, ambapo (Shura) walitoa kikamilifu maoni yao kuhusiana na madai na maoni ya watu wa Mkoa wa Mtwara. Tulimpa maelezo ya kina, na msimamo wa watu wa Mtwara, kauli yake alisema hapa mmemaliza yaani lile tamko lilikuwa sawa na uamuzi wa Serikali, kwa kuwa lilikuwa na pointi za msingi zenye kueleweka kwa asilimia mia moja. Alisema Ust. Simba. Bw. Simba, aliendelea kusema kwamba, katika maelezo yao kwa Waziri Mkuu, waliitaka Serikali kuachana na ushauri wa TPDC, wa kujenga Bomba la Gesi, kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, sambamba na kujenga mitambo ya kufulia umeme Kinyerezi, Dar es Salaam, na badala yake mitambo hiyo, ijengwe Mtwara. Bw. Simba, akasema, Waziri Mkuu Mh. Pinda, alidai kuwa mawazo hayo yanafanana na mpango wa serikali, kama alivyo elezwa na mtaalamu wake kuwa mitambo hiyo itajengwa Madimba, Mwatwara. Hata hivyo, Bw. Simba, aliueleza umma kwamba, maelezo ya Waziri Mkuu yana walakini, kwani katika mpango wa TPDC, ambao ndio washauri wa Serikali unaonyesha wazi kuwa kitakachojengwa Madimba, ni mtambo wa kusasha gesi kisha bomba litasafirisha gesi asilia kwenda Dar es Salaam. Mchoro unaonyesha kuwa mtambo wa kufulia umeme utajengwa Kinyerezi, lakini kauli ya Waziri Mkuu (Pinda) inasema mtambo utajengwa Madimba, tunashindwa kuelewa ukweli haswa ni upi, jambo ambalo linatutia mashaka. Alisema Bw. Simba. Kufuatia kupishana kwa maelezo hayo baina ya Waziri Mkuu na michoro halisi, alidai kwamba labda Mh. Pinda, angewaeleza wana-Kusini kwamba Serikali imebadilisha mpango wake wa kufuata ushauri wa TPDC. Bw. Simba, alikwenda mbali zaidi akidai kuwa wana Mtwara hawajaridhishwa na kauli ya Waziri Mkuu. Kutokana na hali hiyo, alisema wana-Mtwara wanataka kujiridhisha kwamba ni kweli kinachojengwa Madimba, Mtwara ni mtambo wa kufulia umeme au ni mtambo wa kusashia gesi. Lakini pia Bw. Simba, akadai Waziri Mkuu katika ziara yake hiyo hakuweka wazi madai ya kile alichokiita gharama kubwa ya kusarisha gesi kwa njia ya nyaya kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam. Kinyume chake alisema, Serikali hiyo hiyo ina mpango wa kuunganisha mji wa Songea katika gredi ya Taifa kwa umeme huo huo wa Gesi kutoka Mtwara, kwa njia ya

Tahariri/Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

MAONI YETU

Vyombo vya sheria viachwe huru kutoa haki kwa mwenye haki
HIVI karibu, yamefanyika maadhimisho ya siku ya sheria nchini. Maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kivukoni, jijini Dar es Salaam Februari 6, 2013. Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Bila kukosekana watendaji wakuu wa mahakama wa kiongozwa na Jaji Mkuu Othman Chande, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, Jaji kiongozi Fakihi Jundu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Makinda, Waziri wa Katiba na Sharia Mathias Chikawe, Jaji wa Mahakama ya Rufaa January Msofe, Majaji wa mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu, Mawakili na Wanasheria mbalimbali pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wananchi wa kawaida. Kabla ya maadhimisho hayo, yaliwahi kufanyika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda. Ni jambo zuri kuadhimisha siku hizo za kisheria na za kutetea haki za watu hapa nchini. Hii ni ishara kwamba suala la haki za watu katika nchi hii, zinakumbukwa na kuthaminiwa. Hata hivyo, tunasikitika sana kusema kwamba suala la kuthamini haki za watu hapa nchini limekuwa adimu sana. Kweli tumadhinisha siku ya sharia nchini na siku ya haki za binadamu. Lakini tumefanya hivyo kinadharia tu, na kuuonyesha ulimwengu kuwa tunajali na tunasimamia haki. Lakini kwa vitendo hali inaonyesha kuwa kuna udhaifu mkubwa katika vyombo vyetu vya kutoa na kusimamia haki nchini. Kwa jinsi hali ilivyo, rushwa, kufahamiana, wenye uwezo, wenye nyadhifa kubwa serikalini, watu mashuhuri na watu maarufu, wamekuwa wateule wa kupata haki. Masikini, makabwela, watu wa kawaida, wamekuwa wanyonge wa haki mbele kundi nililotangulia kulitaja hapo awali. Kibaya zaidi, siasa nayo imeingilia haki za watu mbele ya vyombo vya kutoa na kulinda haki. Waadhirika wakubwa katika eneo hili ni wanasiasa hususan wasiokuwa wa mrengo wa chama tawala. Lakini wanaobanwa zaidi katika uwanja huu ni viongozi wa dini. Hawa wakidai haki zao au za dini zao au waumini wao, watawala na watendaji wa ngazi za juu serikalini watatumia siasa kama mwanya wa kuwabana na kuwanyamazisha. Akina Ponda, akina Farid ni mfano mzuri katika eneo hili. Leo wako ndani na dhama zao zimezuiwa. Haya ni matokeo ya mamlaka kutumia nguvu ya kisiasa dhidi ya watuhumiwa ili kuwadhibiti. Tunakumbuka pia ile kesi ya uhaini iliyokuwa imefunguliwa kule Zanzibar dhidi ya akina Juma Duni Haji. Lingekuwa ni jambo zuri zaidi iwapo sherehe hizi zinazohusu masuala ya haki

za watu, zukaadhimishwa huku kukiwa na mazingira mazuri yaliyo wazi na huru kwa watendaji wa vyombo hivyo vya kulinda na kutetea haki za watu hao. Haipend ezi kujenga
matabaka ya wanaostahili na wasiostahili haki mbele ya vyombo vyetu vya sharia, ili kulinda maslahi ya wachache wanaodhulumu.

nyaya wakati umbali wake ni mkubwa kuliko Mtwara-Dar es Salaam. Mtwara tunahoji, kama kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, ambako kilometa zake ni chache, iwe ni gharama kubwa vipi iwezekane kuutoa umeme huo Mtwara kwenda Songea, ambako kilomita zake ni nyingi zaidi? Sasa utata kama huu utasemaje kuwa mgogoro umekwisha? Alisema na kuhoji Bw. Simba. Bw. Simba alidai, baada ya kikao cha majumuisho na Waziri Mkuu, ambacho kimeacha maswali mengi yasiyo na majibu, wanaMtwara, wanashangazwa na taarifa zinazodai kuwa suala la gesi limemalizwa, jambo ambalo wanashindwa kuelewa taarifa hizo zinatoka wapi. Bw. Simba, alisema kilio cha watu wa Mikoa ya Kusini, ni kuona mitambo ya kufulia umeme inajengwa ndani ya mikoa hiyo, jambo ambalo litaweza kuvutia wawekezaji kuwa na uhakika wa umeme wa kutosha wa kuendesha viwanda katika maeneo hayo. Wa t u w a K u s i n i tunaposema gesi haitoki, hatuna maana wengine wasinufaike, ila kwa kuwa sisi tupo nyuma kiuchumi zaidi, ni vema matumizi ya awali ya gesi yakaanzia kwetu, kwa kufanya hivyo ndipo wanaKusini watainuka kiuchumi na manufaa mengine. Alibainisha Bw. Simba. Akielezea hali ya mji wa Mtwara, kuhusiana na suala la gesi, Bw. Simba, alisema wakazi wa mji huo hivi sasa wanakauli moja tu, kwani alidai akitokea mtu yoyote yule kusimama na kuzungumzia gesi huulizwa swali moja tu, Inatoka au Haitoki. Alibainisha kwamba ukijibu kuwa gesi itatoka, kabla hujatoa maelezo ya ziada unapigwa. Hii alisema inaonyesha kwamba wana-Mtwara bado hawajakubali gesi itoke Mkoani mwao. Wana-Kusini wanasema, bado wanaendelea kuisihi Serikali yao kwamba, hili jambo bado limekaa vibaya, busara na umakini utumike badala ya mabavu, vinginevyo hali itakuja kuwa mbaya zaidi huko mbele. Alitanabaisha Bw. Simba.

Wanafunzi Waislamu sasa waikataa NECTA


Na Bakari Mwakangwale WANAFUNZI wa Kiislamu Jijini Dar es Salaam, wameitaka Serikali kuifuta kamati ya Kutunuku viwango vya ufaulu ya NECTA kwa kuwa ni kichaka cha kuwadhulumu. Aidha, wanafunzi hao wamesema, wapo tayari kuchukua hatua mbadala ili kuweza kufikisha ujumbe kwa Serikali kulifanyia marekebisho Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), ikiwa njia za awali zimepuuzwa. Wanafunzi hao wametoa kauli hizo Jumatano wiki hii, katika Kongamano la wanafunzi wa Kiislamu lililofanyika katika Msikiti wa Mtambani, Jijini Dar es Salaam, na kujumuisha wanafunzi wa Shule mbalimbali za Jijini hapa, wakijadili kadhia ya Baraza la Mitihani dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzania. Katika maazimio yao, wanafunzi hao wameseta kamati hodhi ya kutunuku viwango vya ufaulu kwa wanafunzi nchini iondolewe mara moja kwani ni sehemu kuu ya dhulma katika Baraza hilo. Kamati hiyo haina usawa na haizingatii haki katika maamuzi kwani ni kichaka cha kuwachinjia wanafunzi wa Kiislamu, pia katika muundo wa Baraza la mitihani haipo. Imesema sehemu ya maazimio ya wanafunzi hao. Wanafunzi hao walionekana kuguswa mno na taarifa mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu Tanzania, iliyotanguliwa na taarifa ya Mwenyekiti wa Baraza hilo Mwalimu Hamisi Togwa, hali iliyopelekea kutoa maoni yao kwa hisia kali. Mwanafunzi Ally Said, kutoka Shule ya Sekondari Ridhwaa, akichangia katika Kongamano hilo, alisema tokea kuibuka kwa kadhia hiyo, kauli nyingi zimeshatolewa lakini vitendo hakuna, huku akitaka vitedo vichuke nafasi yake sasa. Mmetueleza dhulma nyingi tulizofanyiwa na NECTA, mpaka sasa tumejitambua kuwa tumenyanyaswa sana kama tusipo tumia mikono yetu kuondo dhulma hii, hali hii haitokoma. Alisema Mwanafunzi Ally. Akiongea kwa uchungu, aliwataka Wakuu wa Shule kutoa muongozo ni lini waende Baraza la Mitihani, kwani alidai ipo siku itaka wataamua hata kufunga shule za Kiislamu, huku akidai maneno matupu ni sawa na Simba aliyekosa meno na makucha. Naye Mwanafunzi Qassim, kutoka Shule ya Kiislamu Ubungo, aliifananisha Serikali na ndimu, kwamba alidai haitoi maji mpaka ikamuliwe, hivyo alisema wakati umefika wa kuchukua maamuzi magumu kuilazimisha Serikali iondoe dhulma ndani ya Baraza la Mitihani. Mwanafunzi kutoka Shule ya Matangini Islamic, Rajab, aliwataka wanafunzi wenzake kuwa madhubuti katika kudai haki ili waweze kukabiliana na dhulma ambazo zimeanishwa na viongozi wao katika Kongamano hilo. Tumeshatambua adui wetu ni nani, kama ni hivyo tuelewe kwamba hakuna mabadiliko bila maumivu, lazima tukubali kuumia lakini wadogo zetu walio nyuma waje kutendewa haki, ipo haja kwa wanafunzi wa Kiislamu kwenda kuweka kambi Baraza la Mitihani mpaka kieleweke. Alisema Rajab. Mwanafunzi mwingine kutoka Shule ya Sekondari Ilala Islamic, Mwajuma Mikidadi, alisema anacho elewa yeye ni kuwa wazazi wao (Waislamu) wameshaongea sana kuhusu Baraza hilo, bila mafanikio. Imefika wakati sasa sisi wanafunzi tusimame wenyewe tumechoka kukutana katika makongamano ya kuzungumzia NECTA, ni bora twende kuonana na hao watendaji, sisi tupo tayari kwa lolote ili watuelewe kuwa tumechoka kuchulumiwa. Alisema mwanafunzi Mwajuma. Akisherehesha aya za Qur an, katika mchango wake, mwanafunzi Mwajuma Mbaruku, toka Buza Sekondari, alisema kwa mujibu wa mada zilizowasilishwa katika Kongamano hilo, ni kwamba mfumo huo haujaanza sasa. Alisema, Mwenyezi Mungu kasema katika Qur an kwamba watu hao ni mabubu, viziwi na vipofu, kwa hali yoyote alidai hawawezi kuelewa kitu kinachoitwa haki kwa Waislamu hivyo kilichopo ni kupambana na kuondoa mfumokristo ulipo ndani ya Baraza hilo. Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Kibasila, Juma Salim, alisema wanafunzi wa Kiislamu nchini wasimame kwa kauli moja na kutafuta njia muafaka ya kuipaza ili wahusika weweze kusikia ikiwa njia zilizotumika zimefeli. Akijibu hoja za wanafunzi hao, waliohoji mpaka lini wataendelea kuzungumzia suala hilo badala ya kuchukua hatua, Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi w a K i i s l a m u Ta n z a n i a (TAMSYA), Salum Kisaki, alisema wanafunzi pamoja na Waislamu kwa ujumla wataendelea kuzungumza juu ya kadhia hiyo mpaka pale watakapokuwa na kauli moja. Alisema, kujitambua kwa wanafunzi juu ya dhulma wafanyiwazo kupitia Baraza la Mitihani, ni moja ya njia ya kuondoa tatizo hilo ndio maana wamekusanyika kwa pamoja ili kujadili na kuanisha hatua ambazo zimesha chukuliwa hadi sasa. Hisia mlizo onyesha hapa, ni kutokana na kupewa au kufahamisha kiuhalisia jinsi Baraza la Mitihani lilivyo na linavyofanya kazi, na tumewaita hapa kupeana uhalisia huo ilitukiamua kufanya jambo tujue nini tunachokifanya. Alisema Bw. Kisaka. Katika maazimio ya kikao hicho, imeelezwa kwamba Waislamu hawana imani na Baraza la Mitihani kwa kuwa halina uwiano wa kidini, na kwamba kitendo cha Baraza hilo kujazana watu wa dini moja kunashawishi upendeleo wa dini husika. Maazimio hayo pia yametaka viwango vya ufaulu wa wanafunzi viwekwe wazi kwa wadau wa elimu na ziwe na muundo mmoja badala ya kubadilika na kuwa siri ya baadhi ya watendaji wa Baraza la Mitihani. Bw. Kisaka, aliwataka wanafunzi hao kuondoka na maazimo hayo, wakiwa wanajiandaa na njia mbadala ambayo kwa pamoja watakapo amliwa kuifuata, hapatakuwa na maswali kwa nini iwe hivyo. Kwa kuendelea kupuuzwa, Rais huyo wa TAMSYA, aliasa kwamba siku itakapo kuja kutumika njia mbadala isije dhaniwe kuwa watu wanatumwa kuvuruga amani ya nchi, bali ieleweke Wanafunzi wa Kiislamu wanadhulumiwa, sasa wamechoka kudhulumiwa. Aw a l i , a k i w a s i l i s h a mada yake ya changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Kiislamu, nchini kupitia Baraza la Mitihani la Taifa, Mhadhiri msaidizi kutoka Chuo Cha Waislamu Morogoro (MUM), Suleiman Qassim, alisema wanafunzi wa Kiislamu nchini ni wahanga wa kwanza wa dhulma zinazofanywa na Baraza la Mitihani Tanzania. Alisema, uozo uliopo Baraza la Mitihani, kama wanafunzi wakiamua kuuondoa hawashidwi kwani historia inaonyesha kuwa wanafunzi wameweza kuleta mageuzi kutoka katika dhulma na kwenda katika haki, katika nchi mbalimbali. Mwl. Qassim, alisema utati ulifanywa na Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu, ulibaini kwamba, mitihani inasahihishwa sawa sawa na maksi zinajumlishwa kiusahihi, katika hatua za awali, lakini tatizo linakuja katika kamati ya kutunuku madaraja (Grade). Akianisha changamoto hiyo, Mwl. Qassim alisema katika kufan ya uchunguzi tume mwaka 2011, wakati ambapo inafahamika ukipata alama 22 au 23, unakuwa umepata

Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

alama D. Lakini mwaka huo ilikuwa aliyepata 0 mpaka 34, ilihesabika alikuwa na daraja F, na alama D, ilikuwa inaanzia alama 35 mpaka 59, kwa hiyo wewe ukijikadiria alama 41, kuwa umepata daraja C, katika kamati ya kutunuku ni kinyume chake, na hii tume hii ipo chini ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Dk. Joyce Ndalichako, ambaye ndiye Katibu Mtendaji wa Baraza pia. Alianisha Mwl. Qassim. Changomoto ya pili aliitaja
kuwa ni Barza la Mitihani kufanywa kama Parokia, kwa maana toka kuanzishwa kwake mpaka leo takribani

ya Waislamu ya uchunguzi iliomba kupatiwa mfumo unaotumika kuweka hayo madaraja ya ufaulu. Tume ya uchunguzi iliomba, mara ya kwanza haikupatiwa mara ya tatu wakaulizwa, kwani zina ulazima mzipate. Baada ya kupatiwa madaraja hayo ndipo likapatika jambo ambalo lilikuwa halifahamiki kabisa. Alisema Mwl. Qassim. Akiweka bayana mambo

yaliyobainika kutoka katika kamati hiyo, alisema mathalani katika somo la Maarifa ya Uislamu kwa kidato cha nne

mika 30, nafasi zote nyeti na muhimu hushikwa na Wakristo. Si hivyo tu, lakini pia mwl. Qassim, alidai waratibu wa masomo hayo, zaidi ya asilimia tisini ni Wakristo na hata wasahishaji wa mitihani yao huwa ni hao hao, jambo ambalo ni wazi Wanafunzi wa Kiislamu nchini inawakwazika. Mwl. Qassim, aliwatanabaisha wanafunzi hao wa Kiislamu kwamba wasidhani kwamba ipo siku Wakristo waliojazana katika Baraza la Mitihani, watajiwabisha wenyewe.

Kumradhi

IGP Said Mwema

Mussa Juma

TOLEO lililopita likokosea kuandika jina la Kamishna wa Polisi Zanzibar( kulia) Jina lake ni Mussa Juma na sio IGP Said Mwema (kushoto) kama ilivyoandikwa awali.

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Aina za misamaha katika Uislamu


Na Sheikh Salah Sayed Hussein
ni rehema kwa viumbe wote. Na akasema tena katika Surat Al-aaraf, na rehema zangu zimeenea katika kila kitu na nitaziweka kwa wale walio Wachamungu hadi neno lake na kuwaondolea matatizo na mashaka waliokuwa nayo. Na katika sahihi Muslim toka kwa Abii Hurairat (R.A) palisemwa, ewe Mtume wa Allah, Walaani washirikina, akasema Mimi sikuletwa kuwa mwenye kuwalaani watu, kwa hakika nimeletwa kuwa ni rehema. Ni kweli yeye ni rehema mwenye kuongoa na ni neema mwenye kusaidia watu wote. Na dini hii imesimamia juu ya upole na usamehevu na wepesi, na yeyote atakayedhani kinyume na hicho, atakuwa amepotea na kupata hasara kubwa kwani Mtume (S.A.W) anasema, Kwa hakika dini hii ni nyepesi na hatoitia ugumu yeyote miongoni mwenu isipokuwa itamshinda tu. Namna mbalimbali za misamaha ya kiislam 1. Kwa hakika umekusanya Uislam juu ya misamaha ya aina mbalimbali katika maisha ya kidunia na ya akhera, na kwa hivyo ndivyo ilivyokuja dini hii ili iwe ni dini ya wastani na msamaha katika pande zote. Na huyu Mtume (S.A.W), pale walipokuja watu watatu wote wakiuliza juu ya ibada ya Mtume (S.A.W), na alipowapa habari juu ya ibada zake Mtume huyu, miongoni mwa matendo yake walionekana kama kuyaona ni madogo akatangaza kila mmoja miongoni mwao kuongeza bidii katika ibada. Akasema mmoja; mimi nitasimama usiku wote, akasema mwingine; na mimi nitafunga milele, akasema mwingine; sitaoa mwanamke. Lau ungetazama mambo hayo yote matatu ni mazuri sana kiasi kuwa ni kikomo cha ibada. Na huu ndio mtazamo wa watu hawa wote. Akawatokea Mtume (S.A.W) akasema, Wapo wapi watu ambao waliosema mambo haya na haya walipokuwa mbele ya Mtume (S.A.W) akasema Mtume mwenye uwastani na msamaha na upole; Ama mimi nina swali na ninalala na ninafunga na ninakula mchana na ninaoa wanawake na yeyote asiyetaka mwenendo wangu basi huyo si mwenzangu. 2. Katika kuuza na kununu; hebu angalia katika picha hii vizuri ambayo anasema Mtume (S.A.W), Mwenyezi Mungu amerehemu mtu, na amsamee anapouza pia amsamehe anaponunua na amsamehe anapokopesha pia amsamehe anapodai deni. 3. Lazima za kisheria, hebu angalia juu ya upole huu amabo ni wa thamani ya juu zaidi ni swala wakati unapokuwa safari swala ambayo ni mawasiliano kati ya Mola na kiumbe wake. Uislam umetia katika sheria haki ya kuzipunguza swala zile zenye rakaa nne (4) nazo ni Adhuhur, Alasiri na Insha kuziswali rakaa mbili (2), na hii ni namna kubwa kabisa katika msamaha na uwepesi, pia tazama vile vile Uislam unaruhusu hadi kula mzoga pale unapozidiwa kwa njaa kiasi cha kuweza kupoteza uhai na kunywa pombe unapotaka kuangamia kwa kiu na kukosa kinywaji cha halali. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu katika Surat Maaidah (Imeharamishwa kwenu mzoga na damu na nyama ya nguruwe na vile vilivyochinjwa bila ya jina la Mwenyeyezi Mungu na walionyongwa na vilivyopigwa na vilivyodondoshwa na vilivyotobolewa na waliokula samba isipokuwa mliowawahi kwa kuwachinja na waliochinjwa masanamu hadi neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu na yeyote atakayesongekwa (kuzidiwa) na njaa na bila ya kukusudia madhambi, hapo Mwenyezi Mungu ni msamehevu na ni mpole. 4. Amedhamini uhuru wa kila mmoja wetu baada ya kuhangaika binadamu na taabu ya wasi wasi na anachokiabudu. Ukaja uislam ili useme kwa watu wote kuwa Nyinyi mna dini yenu na mimi nina dini yangu na anasema vile vile hakuna kulazimishana katika dini kwani imeshabainisha uongofu kutokana na upotevu na yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu huyo atakuwa ameshika kamba imara isiyokatika na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia na ni mtunzi. Ninamuomba Mwenyezi Mungu atukunjue vifua vyetu katika uislam na imani.

Ugaidi wenye sura ya kiutu: Historia ya vikundi vya mauaji vya Marekani
Na Profesa Michel Chossudovsky (Januari 6, 2013, Mtandao wa kupashana habari) Kundi la Jabhat al-Nusra KUNDI la Jahbat alNusra - ambalo linaaminika kufungamana na Al Qaeda linaelezwa kuwa ndiyo kundi pinzani la uasi lenye nguvu, lililohusika na mashambulizi makubwa ya mabomu. Likiwa linatambulishwa kama adui wa Marekani (liko kwenye orodha ya makundi ya kigaidi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani), operesheni za Al Nusra hata hivyo zina alama ya mafunzo ya kiusalama ya Marekani, mbinu za ugaidi na mifumo ya silaha. Mauaji yaliyofanywa dhidi ya raia na Al Nusra (inayofadhiliwa kwa kicho na Marekani na NATO) yanafanana na yale yaliyofanywa na vikundi vya mauaji vilivyoundwa na Marekani nchini Irak. Kwa maneno ya kiongozi wa Al Nusra, Abu Adnan huko Aleppo, kaskazini ya Syria, Jabhat al-Nusra inajumuisha wapiganaji wa Syria waliokuwa katika vita ya Irak, watu wanaoleta ujuzi - hasa wa kutengeneza mabomu - katika vita nchini Syria. Kama ilivyokuwa nchini Irak, vita vya vikundi vya kisiasa na kijeshi na kusafisha maeneo wasiwepo waumini au wafuasi wa madhehebu fulani vilipewa kipaumbele/ Nchini Syria, jamii za Walawi, Washia na Wakristo zimelengwa na vikundi vya mauaji vilivyoundwa na Marekani na NATO. Walawi na Wakristo ndiyo walengwa zaidi wa mpango wa mauaji ya mtu mmoja mmoja. HIi ilidhihirishwa katika ripoti ya Shirika la Habari la Vatican (Roma). Wakristo katika mji wa Aleppo ni waathirika wa vifo na uharibifu kutokana na mapigano hayo ambayo kwa miezi mingi yameuathiri mji. Maeneo wanayokaa Wakristo, katika muda si mrefu uliopita, yamelengwa na majeshi la wapinzani wanapombana na jeshi la Syria, na kulazimisha kuondoka kwa raia wengi. Baadhi ya makundi katika upinzani huo wa vikundi maridhawa, ambako pia kuna makundi ya ki-Jihad, yanaelekezea risasi nyumba za Wakriso na majengo yao mengine, kuwalazimisha wanaokaa humo waondoke ili washike majengo hayo (usashaji wa kidhehebu) kwa mujibu wa Agenzia Fides, katika Habari za Vatican, Oktoba 19, 2012. Wanaharakati wa Sala wa Kisuni - anasema Askofu huyo - wanaendelea kufanya mauaji dhidi ya raia, au kulazimisha vijana wajiunge nao kwa nguvu. Wasuni hao wanaoua kirahisi wapinzani wao wa kiimani wanapigana vita takatifu kwa kumianini, hasa hidi ya Walawi. Magaidi wanapotaka kujua nini mwelekeo wa kidhehebu wa mtu fulani, wanamtaka aeleze vizazi vilivyopita hadi Musa. Na pia wanamtaka atoe sala ambayo Walawi waliifuta. Walawi hawana njia ya kutoka katika mtego huo wakiwa hao. (Kwa mujibu wa Agenzia Fides, Juni 4, 2012). Taarifa zinathibitisha kuingia kwa wingi kwa vikundi vya mauaji vya Kisala na Al Qaeda pamoja na brigedi zilizoko chini ya kundi la Udugu wa Kiislamu nchini Syria kuanzia uasi ulipoanza Machi 2011. Isitoshe, kama ilivyokuwa Mujahiddin wa Afghanistan kuunganishwa kupigana Jihad ya Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) wakati wa vita vya iliyokuwa Urusi nchini Afghanistan, NATO na wakuu wa jeshi la Uturuki, kwa mujibu wa taarifa za ujasusi za Israeli, walianzisha kampeni ya kusajili maelfu ya wanamgambo wa kujitolea wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na ulimwengu w a Wa i s l a m u k w a j u m l a kupigana upande wa waasi wa Syria. Jeshi la Uturuki lingewapa hifadhi askari hao wa kujitolea, kuwapa mafunzo na kuwezesha kuingia kwa nchini Syria. kwa mujibu wa DEBKAle, NATO kuwapa waasi silaha za kulipua vifaru, Agosti 14, 2011). Kampuni binafsi za usalama na kusajiliwa kwa askari wa kukodiwa Kwa mujibu wa taarifa, makampuni binafsi ya usalama yanayofanya shughuli zake maeneo ya Ghuba yanahusika katika kusajili na kutoa mafunzo kwa askari wa kukodiwa. Ingawa haikuwekwa rasmi kwa kusajili askari wa kukodiwa dhidi ya Syria. taarifa inaonyesha kuundwa kwa kambi za mafunzi nchini Qatar na Falme za Kiarabu za Ghuba (UAE). Katika mji wa kijeshi wa Zayed, Falme za Ghuba, jeshi la siri linainuliwa, linalosimamiwa na Xe Services (Ze Services, zamani Blackwater, iliyobadili jina baada ya kasfha ya mateso na udhalilishaji wa wafungwa wa kivita nchini Irak). Makubaliano ya kuanzisha kambi ya mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kufunza askari wa kukodiwa yalitiwa saini Julai 2010, miezi tisa kabla ya kuanza kwa vita vya Libya na Syria. Katika mabadiliko ya hivi karibuni, makampuni ya kiusalama yenye mikataba au kandarasi na NATO na Pentagon (makao makuu ya Jeshi la Marekani) yanahusika kaika kufunza makundi ya mauaji ya upinzani katika kutumia silaha za kemikali. Marekani na nchi washirika kadhaa za Ulaya wanatumia makandarasi wa ulinzi kufunza waasi wa Syria jinsi ya kukamata shehena za silaha za kemikali

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote. Na rehema na amani zimfikie Bwana wetu Muhamad na jamaa zake na sahaba zake wote. Kwa hakika Uislam umekuja ili uwe ni rehema kwa viumbe wote na kuporomosha na kuondoa taabu na mashaka, ambayo yalikuwa kwa waliopita kabla. Mtume wa Waislam na mjumbe wa Mola kwa viumbe wote Muhamad (S.A.W), miongoni mwa mambo makubwa ambayo aliletwa kwayo, alikuwa mpole kwa viumbe wote na hili ndilo lililoweka wazi Qur-an tukufu pale aliposema Mwenyezi Mungu mtukufu, na sikukutimiliza isipokuwa uwe

Vikundi vya mauaji nchini Irak na Syria: Mizizi ya kihistoria ya vita kicho ya Marekani na NATO dhidi ya Syria

nchini Syria, ofisa mmoja mwandamizi wa Marekani na maosa wa kibalozi waliiambia CNN (kituo maarufu cha televisheni kimataifa) Desemba 9, 2012. Majina ya makampuni husika hayakutajwa. Nyuma ya milango iliyofungwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Robert Stephen Ford alikuwa mmoja wa timu ya watu wachache katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyosimamia kusajiliwa na kupewa mafunzo brigedi za kigaidi, pamoja na Derek Chollet na Frederic C. Hof, mshirika wa zamani wa kibiashara wa Richard Armitage, ambaye aliwahi kuwa mratibu m a a l u m w a Wa s h i n g t o n kuhusu Syria. Derek Chollet hivi karibuni aliteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri wa Ulinzi kwa masuala ya kuisalama ya kimataifa. Timu hii ilifanya kazi chini ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kwa masuala ya Mashariki ya Kati, Jeffrey Feltman. Timu ya Feltman ilikuwa katika mahusiano ya karibu na kusajiliwa na kupewa mafunzo kwa askari wa kukodiwa kutoka Uturuki, Qatar, Saudi Arabia na Libya (kwa msaada wa utawala uliofuatia kuanguka Gaddafi, ambao ulipeleka wapiganaji 600 wa Kundi la Wapiganaji wa Kiislamu la Libya (LIFG)
Inaendcelea Uk. 5

Habari za Kimataifa

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Wanajeshi 325 wa Kimarekani walijiua 2012


Israel wamejiua 237
WASHINGTON JESHI la Marekani limetangaza kuwa, karibu wanajeshi 325 wa nchi hiyo walijiuwa mwaka 2012. Kiwango hicho ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa nchini Afghanistan mwaka 2012. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, wanajeshi 182 waliamua kujiuwa wakati wakiwa kwenye vita na kesi zipatazo 130 zimeshathibitishwa na jeshi la Marekani, huku 52 zikiendelea kuchunguzwa. Jeshi la Marekani limeongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo waliouawa nchini Afghanistan mwaka jana ilikuwa 312. Jenerali Howard Bromberg amesema kuwa idadi hiyo ya wanajeshi waliojiua mwaka jana ni kubwa mno katika historia ya jeshi la nchi hiyo. Utati mwengine umeeleza kuwa, karibu wanajeshi 22 wa zamani hujiuwa kila siku na idadi hiyo ni asilimia ishirini zaidi ya kiwango cha kujiuwa wanajeshi wa zamani wa nchi hiyo mwaka 2008. Kwa upande mwingine, habari zilizotolewa mwishoni mwa mwaka jana zimeeleza kuwa wanajeshi wasiopungua 237 wa utawala hasimu wa Israel wamejiua kwa nyakati mbalimbali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Kwa mujibu wa nyaraka za siri za jeshi la Israel, kwa uchache wanajeshi 24 wa utawala huo hujiua kila mwaka. Press TV imesema nyaraka hizo za siri zilitolewa kwa mara ya kwanza na mwanablogu wa Israel, ambaye alikamatwa na polisi na kuhojiwa. Mwanablogu huyo amesema idadi ya askari wa Jeshi la Israel waliojiua ni zaidi ya iliyotangazwa rasmi. Hivi karibuni Wizara ya Vita ya Israel ilikiri kuwa idadi ya wanajeshi wake wanaojiua ni zaidi ya wanaouawa vitani. Jeshi la utawala wa Israel limeshindwa mara kadhaa katika vita dhidi ya wanamapambano wa Lebanon. Kwa kiasi kikubwa jeshi hilo limekuwa likifanya hujuma zaidi ya Ukanda wa Ghaza.

Ufaransa yahalalisha ndoa za liwati


PARIS Licha ya maandamano makubwa ya wananchi wa Ufaransa kupinga kuhalalishwa kisheria ndoa za watu kulawitiana, Bunge la nchi hiyo limepitisha muswada wa sheria hiyo kwa kura nyingi. Bunge la Ufaransa limepasisha muswada huo wa sheria inayowaruhusu kuoana kisheria wanaume kulawitiana kwa kura 249 za ndiyo dhidi ya 97 za hapana. Kama ilivyokuwa imetarajiwa, wabunge wa chama cha Kisoshalisti, chama cha kijani na cha mrengo wa kushoto waliunga mkono mswada huo uliopingwa na wawakilishi wa chama cha umoja kwa ajili ya harakati ya wananchi. Wabunge wa mrengo wa kulia wameeleza wasiwasi walionao kutokana na kupitishwa mswada huo. Kupitishwa sheria hiyo inayoruhusu ndoa za watu wa jinsia moja, ni moja ya ahadi zilizotolewa na Rais Francois Hollande, wa Ufaransa wakati wa kampeni za uchaguzi kwa madhumuni ya kuvutia kura za makundi ya watu wa jinsia moja wenye mwenendo mchafu wa maingiliano ya kimwili.

INGAWA serikali ya Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki, inapinga vikali kazi za Shirika la Mafuta la Kimarekani, Exxon Mobil, Kaskazini mwa Iraq, viongozi wa shirika hilo na wale wa mkoa wa Kurdistan wamefanya uchunguzi wa eneo jingine lenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa lengo la kutaka kuchota nishati hiyo muhimu. Shughuli hizo zinahesabika kuwa zisizofuata sheria za nchi hiyo. Siku ya Ijumaa duru za habari zilimnukuu kiongozi mmoja nchini Iraq akisema kuwa, viongozi wa Exxon Mobil kwa kushirikiana na viongozi wa eneo la Qarah Hanjir, ambalo liko umbali wa kilometa 35 Kaskazini Mashariki mwa mji Kirkuk Kaskazini mwa Iraq,

Marekani yaendelea kuvunja sheria kukomba mafuta Iraq


walikagua na kujadiliana njia za kuanzisha kituo cha kuchimba mafuta katika eneo hilo, licha ya kwamba eneo hilo hadi hivi sasa lina mzozo kati ya Baghdad na Arbil. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa katiba ya Iraq, mikataba yote ya mafuta ikiwemo mikataba ya mafuta ya eneo la Kurdistan lazima iidhinishwe na serikali kuu. Hata hivyo pamoja na kuwa wazi vifungu vya katiba hiyo, lakini viongozi wa eneo la Kurdistan mara kadhaa wamekuwa wakiweka mikataba na mashirika ya kigeni ya kuchimba mafuta sambamba na kustadi na nishati hiyo muhimu bila ya kibali kutoka kwa serikali kuu ya Baghdad. Shughuli za mashirika ya mafuta ya kigeni katika eneo hilo la Kurdistan ambazo zimekuwa zikifanyika kinyume cha sheria, zimezusha mizozo mingi ya kisiasa ndani na nje ya nchi hiyo ya Kiarabu. Akiba ya mafuta katika eneo hilo inakadiriwa kukia mapipa bilioni 44. Aidha kwa mujibu wa uchunguzi huo, akiba ya gesi iliyoko katika eneo hilo, inakadiriwa kuwa ni mara mbili ya akiba yote ya gesi iliyoko nchini Kazakhstan. Kuwepo kwa vyanzo hivyo vya utajiri, kumesababisha mashirika mbalimbali ya nje kulifanya eneo hilo kuwa la uwekezaji. Ni kutokana na ukiukwaji huo wa mara kwa mara wa viongozi wa eneo la Kurdistan, ndipo

RAIS Barack Obama wa Marekani

Ugaidi wenye sura ya kiutu: Historia ya vikundi vya mauaji vya Marekani
kupitia Uturuki katika miezi iliyofuatia kuanguka mnamo mwezi Septemba 2011 serikali ya Gadda. Naibu Waziri wa Ulinzi Feltman alikuwa anawasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia, Prince Saud al Faisal na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Hamad bin Jassim. Pia alikuwa akisimamia osi ya Doha ya uratibu maalum wa usalama kuhusiana na Syria, ambayo ilikuwa inajumuisha wawakilishi wa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi na za Ghuba pamoja na mwakilishi kutoka Libya. Prince Bandar bin Sultan, mwakilishi maalum na mtajwa sana kimataifa wa mfumo wa ujasusi wa Saudia alikuwa mmoja wa kundi hili. (Iliripotiwa na Press TV ya Marekani, May 12, 2012). Mwezi Juni 2012 Jeffery Feltman aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya
Inatoka Uk. 4

serikali ya Baghdad ikaamua kupunguza bajeti ya eneo hilo suala ambalo pia limeibua vuta ni kuvute kati ya pande mbili. Kwa upande mwingine, mikataba isiyofuata sheria ya mashirika ya kigeni imezua tafrani kati ya serikali ya Baghdadi na mashirika hayo. Miongoni mwa mashirika hayo ni Shirika la Kimarekani la mafuta la Exxon Mobil. Mwezi Oktoba mwaka 2011, shirika hilo lilitia saini makubaliano kati yake na uongozi wa Kurdistan kwa ajili ya kuanzisha vituo sita vya kusashia mafuta katika eneo hilo. Kati ya maeneo hayo yaliyotajwa, mawili kati yake yapo katika maeneo yenye mzozo kati ya serikali za Baghdad na Arbil nchini Iraq.

Waliomteka Sheikh Abu Omar wafungwa jela

siasa, nafasi muhimu ambayo kimsingi ni kuweka agenda ya Umoja wa Mataifa (kwa niaba ya Marekani) katika masuala ya kutatua migogoro maeneo kadhaa yenye machafuko duniani, ikiwa ni pamoja na Somalia, Lebanon, Libya, Syria, Yemen na Mali. Katika hali ya kushangaza, nchi ambazo Umoja wa Mataifa unasema unajitahidi kutatua migogoro yao ndizo hasa ambazo zinalengwa na operesheni za siri za Marekani. Akishirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, NATO na washirika wake wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) mjini Doha na Riyadh. Feltman ndiye mwakilishi wa Washington aliye nyuma ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Lakdar Brahimi na pendekezo la amani alilotoa. Wakati huo huo, huku wakizungumza juu juu kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa za kukia amani, Marekani na NATO wameongeza kasi ya kusajili na kutoa mafunzo kwa

askari wa kukodiwa, kutokana na kupoteza askari wengi vitani kwa vikundi vya upinzani vya uasi. Pendekezo la Marekani kwa hatua ya mwisho ya mkasa wa Syria siyo kubadili utawala ila kuvunjilia mbali Syria kama nchi. Kusambazwa kwa vikosi vya mauaji vya upinzani vikiwa na ruksa ya kuua raia ni sehemu ya mkakati huu wa kihalifu. Ugaidi wenye uso wa kiutu unakubaliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ambalo ni dirisha la kutoa maoni ya mkakati wa kuingilia kati kibinadamu wa NATO chini ya mtazamo wa wajibu wa kulinda raia. Mauaji yaliyofanywa na makundi ya mauaji yaliyoundwa na Marekani na NATO kiulaini tu yanalaumiwa kuwa ni ya serikali ya Bashar al Assad. Kwa mujibu wa kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Navi Pillay:

Upotezaji huu mkubwa wa maisha ungeweza kuzuiwa ikiwa serikali ya Syria ingekuwa imechagua njia tofauti na ile ya kunyamazisha kwa nguvu kile ambacho mwanzoni kilikuwa ni upinzani wa amani na wa haki unaofanywa na raia wasio na silaha, kwa nukuu ya Stephen Lendman, Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu Syria: Kuvunga Mauaji yanayofadhiliwa na Marekani na NATO, iliyochapishwa na Global Research, Januari 3, 2012. Lengo la Washingon ambalo haiwezi kulisema wazi ni kuivunja Syria kama nchi huru - kwa misingi ya kikabila na kidini - kuwa vitaifa tofauti na huru. Makala hii iliwekwa kwanza katika mtandao wa Global Research, 2013 imetafsiriwa na Anil Kija).

MILAN Msaidizi wa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Milan nchini Italia, ametaka itolewe adhabu kali ya kifungo cha miaka 12 jela kwa mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Kijeshi la Italia SISMI, kwa kuhusika na jinai ya kumteka nyara Sheikh Osama Moustafa Hassan Nasr. Sheikh Osama Moustafa Hassan Nasr, mashuhuri kwa jina la Abu Omar, alikuwa Imam wa zamani wa Msikiti wa Milan nchini humo. Msaidizi wa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Milan amesisitiza pia juu ya kuendelezwa kesi dhidi ya vibaraka wote waliohusika na kitendo cha kumteka nyara Sheikh Abu Omar Februari 17, 2003, ambao wanafungamana na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA na Shirika la Ujasusi la Italia. Aidha Msaidizi huyo wa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Italia ameitaka mahakama imhukumu Marco Mancini, afisa mwandamizi wa Shirika la Ujasusi la Italia kifungo cha miaka 10 jela kwa kuhusika na jinai hiyo.

6
Na Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics) TANGANYIKAna Zanzibar ziliungana mwaka 1964 chini ya makubaliano ya midomoni yaliyosimamiwa na waasisi wawili wa mataifa hayo: Mwalimu Julius K. Nyerere akiwakilisha upande wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume akiwakilisha u p a n d e w a Z a n z i b a r. Makubaliano ya muungano huu yamekuwa siri kubwa ya mataifa haya mawili, na pia imekuwa siri kubwa kwa taifa la muungano a m b a l o n i Ta n z a n i a . Muungano ni fumbo na siri kubwa ya taifa na huko nyuma waliojaribu kuhoji uhalali wa muungano huu aidha waliitwa wachochezi, wahaini au waliitwa Dodoma na mwishowe kuishia kizuizini! Ukienda Zanzibar ukaanza kutafuta mikataba ya makubaliano ya muungano huo huwezi kuipata, na vile vile ukija upande wa Tanganyika ukitaka uipate mikataba hiyo napo huwezi kuipata! Ingawa mimi naamini kwamba mikataba hii ni lazima iwepo, kwa vile haiwezekani viongozi wawili wa ngazi za juu za kitaifa wakubaliane kuziunganisha nchi bila ya kuwa maandishi yoyote, hata ukurasa mmoja, haiwezekani kabisa! Haiwezekani na haitakuja iwezekane. Ni lazima kulikuwa na makubaliano juu ya muungano huo; hata kama makubaliano hayo yalikuwa hayana hadhi za kimikataba ya kimataifa, lakini kulikuwepo na makubaliano ya kimaandishi. Wakati nilipokuwa nasoma shule ya msingi kulikuwepo na picha zilizokuwa zikimuonyesha Mwalimu Nyerere na Abeid Amani Karume wakisaini mkataba wa muungano! Sasa hizo document walizokuwa wakizisaini wakati wanapigwa picha zipo wapi!? Pia nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi tulikuwa tunafundishwa kwamba Tanganyika na Zanzibar zimeungana katika mambo yanayohusu wizara nne tu: Wizara ya Fedha; Wizara ya Ulinzi; Wizara ya Elimu ya Juu; na Wizara ya Mambo ya Nje. Haya nilifundishwa darasani na walimu wangu wa shule ya msingi. Sasa hivi muungano umepanuka sana na umekuwa ni muungano wa wizara nyingi kuliko zile nilizokuwa nimefundishwa darasani. Sasa sijui kama makubaliano ya muungano huo yalikuja

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Kizungumkuti cha muungano bila hati

KULINGANA na uzoefu wa nchi nyingi duniani ambazo zilikuwa zimeungana na kuachana au kutengana, ni kwamba uzoefu unatuambia kwamba mara baada ya nchi kutengana kila nchi inaanza maisha mapya. Na katika zoezi la kuanza maisha mapya, kuna mambo mawili: moja ni kuanza maisha mapya kwa mwelekeo mzuri; na mbili ni kuanza maisha mapya kwa mwelekeo mbaya. Yote haya yanategemea sana na wananchi wenyewe. Nasema inategemeana na wananchi wenyewe kwa vile wananchi na viongozi katika jamii, na jamii yenyewe kwa ujumla. Tukianza kuuchambua mwelekeo mbaya ni kama ifuatavyo: Zanzibar na Tanganyika zimekuwa katika muungano ambao umedumu kwa miaka 49, na matunda ya muungano huu kwa mwananchi wa kawaida kama mimi na wale wenzangu wa kule vijijini, haujatusaidia kabisa bali umezidi kutuongezea umasikini, na hata kutunyanganya kazi zetu; umasikini ambao

Uzoefu wa Urusi (USSR)


umesababishwa na waasisi wa muungano huo na tawala (system) zao ambazo bado zipo madarakani. Nawalaumu waasisi kwa vile munapoamua kuunganisha nchi, ni lazima kuwe na faida za kiuchumi na kisiasa, na faida hizo ni lazima zitajwe kwenye makubaliano ya muungano huo, lakini kwa bahati mbaya sana hata makubaliano yenyewe hayapo! Sasa huo muungano ulikuwa kwa ajili ya nani na kwa sababu zipi!? Nchi hizi zilipoungana mwaka 1964 zote mbili zilikuwa ni kama nchi changa ambazo ndiyo zilikuwa tu zimepata uhuru wao muda si mrefu, na kulingana na uchanga (utoto) wao ndiyo maana hata wakafanya muungano wa kitoto ambao umedumu kwa umri wa mtu mzima, lakini bado watu wazima wanaendelea kungangania utoto! Utoto huu huu ndiyo ambao tusipokuwa makini Zanzibar na Tanganyika hasa kwa kipindi hiki ambacho sote tena kwa pamoja tumekufa na

Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume hawa ndiyo waasisi wa serikali za Tanganyika na Zanzibar; na kisha muungano.

kufufuliwa kama ambavyo vitabu vya dini vinavyosema ukifa utafufuliwa ili ujitetee mbele ya mungu kwa yale uliyoyatenda hapa duniani! Sasa na sisi tumeshakufa na kufufuliwa na kila mmoja wetu inabidi atafute mwelekeo makini na wa kiutu uzima na wala siyo kama ule wa kitoto tuliokuwa tumeuchagua na tukaungangania kwa miaka 49! Tukiwaruhusu wale wale na taratibu zao zile zile zilizotukisha hapa tulipo leo hii, tutakuwa bado tunaendelea na utoto uleule. Tukianza kuuchambua mwelekeo mzuri ni kama ifuatavyo: Zanzibar na Tanganyika ziwe kama ndiyo kwanza zimepata uhuru wake toka kwenye kivuli cha Tanzania; kila nchi iachane kabisa na fikra au kitu chochote kinachoitwa Tanzania; kila upande ujumuishe wananchi wake na wadau mbali mbali kukaa chini na kuandika katiba mpya ya umma; katiba iwe inafanana na katiba za nchi zingine zilizoendelea
Inaendelea Uk. 7

kuboreshwa au basi tu watu wameona kwa vile wameishi kindugu kwa muda murefu, hawana budi kuupanua muungano kwa kujumuisha wizara zingine! Pia nakumbuka wakati nikisoma shule ya msingi kila nchi ilikuwa na kitengo chake cha usalama wa taifa, lakini hivi sasa kitengo ni kimoja; sasa hivi wizara ya mambo ya ndani ipo kwenye muungano! Katika mazingira kama hayo inakuwa ni vigumu kujua makubaliano ya muungano ule wa Karume na Nyerere, na muungano ule wa Aboud Jumbe na Nyerere, au na muungano ule wa Abdul Wakil na Nyerere, au ule wa Salmin Amour na Mzee Mwinyi, au ule wa Amani Karume na Mkapa, au huu wa Ali Shein na Jakaya Kikwete!? Watanzania hawaelewi ni muungano upi ni sahihi? Kwa vile kumekuwa na madadiliko ya viongozi pande zote mbili, na kama tulivyo sisi Watanzania mambo yetu yote ni siri. Ni siri hata kama mambo hayo yanawahusu wananchi na nchi zao, bado tu kila kitu ni siri ya wakubwa! Na wananchi si haki yao kuuliza wala kuhoji. Na kutokana na desturi hiyo ndiyo maana muungano wetu leo hii umekuwa fumbo na siri kubwa ya taifa kiasi kwamba hata marais wa Zanzibar na Tanzania ukiwauliza maswali marahisi sana ya muungano hawawezi kuyajibu! Wakati Mwalimu Nyerere yupo hai, Mzanzibar yeyote aliyethubutu kuuliza uhala wa kimaandishi wa muungano alionekana muhaini na yalimka. Hivyo kulingana na hali ya udikiteta huo, Wa z a n z i b a r w a l i k o s a ujasiri wa kuhoji uhalali wa muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika kikatiba, kisheria na hata kisiasa. Na hii ilikuwa siyo kwa Wazanzibar peke yake, bali hata Watanganyika walikosa ujasiri wa kuhoji uhalali wa serikali ya Tanganyika ambayo ilikuwa nchi huru kwa miaka minne na baada ya hapo kufanywa mikoa ya Tanzania, tena bila hata kuwauliza wananchi kama wanaridhia au lah! Kuziunganisha nchi mbili ni suala nyeti sana. Kikawaida kulingana na sheria za Umoja wa Mataifa, si halali kuiunganisha nchi moja na nyingine bila ya kuwauliza raia wa nchi husika; na kama ikatokea kiongozi wa nchi fulani au viongozi wa nchi husika kuziunganisha nchi zao bila ya ridhaa ya wananchi wao inayoshuhudiwa na kura ya maoni, basi muungano huo Inaendelea Uk. 7

7
Inatoka Uk. 6 ni batili. Muungano usiopata ridhaa ya wananchi wa pande mbili husika ni muungano Batili, tena kwa sheria za kimataifa. ni Uhaini na Ukiukwaji wa haki za binadamu. Sasa sijui kwa upande wa Zanzibar kama wananchi walipiga kura ya maoni kuamua kwamba Zanzibar iungane na Tanganyika au la! Isipokuwa kwa upande wa Tanganyika nina uhakika kwamba Watanganyika hawakuwahi kuulizwa kwa kupiga kura ya maoni kuhusu nchi yao kuunganishwa na Zanzibar! Sasa katika mazingira kama haya tayari tunaona kwamba kumbe hata taratibu na sheria za kimataifa hazikufuatwa katika makubaliano ya kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar! Pamoja na kwamba hata document za makubaliano hayo hazionikani, lakini pia inaonyesha kwamba muungano huo ulikiuka sheria na taratibu za kimataifa! Kulingana na hali hiyo, unaonekana muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa ni makubaliano kati ya Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Na kwa bahati nzuri sana, leo hii wakati tunapasua vichwa kuhusu uhalali wa muungano huu, wote hawapo duniani. Hivyo sioni sababu ya kuumiza vichwa vyetu kuwajadili viongozi wawili waliokiuka taratibu za kimataifa za kuunganisha nchi zao, tena bila kumbukumbu yoyote! Mimi nashauri tuachane nao na makubaliano yao ya midomoni, na sisi tukae chini na kuangalia kama tunauhitaji huo muungao au la! Kama tunauhitaji, basi pande zote mbili zihusishwe kikamilifu bila ya kicho chochote ili tutengeneze muungano unaokubalika na sheria na taratibu za kimataifa, muungano wenye kumbukumbu za kimaandishi. Lakini kama sehemu zote mbili, au sehemu moja ikiona hakuna umuhimu wa muungano huo, basi ni wananchi wameamua, na wenye nchi ni wananchi, watawala wasilazimishe. Mimi ningependa nikiri kinyume na Watanzania wengi kwa vile siyo vizuri

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013 ya riba, kila mwaka deni linaongezeka kulingana na jinsi unavyochelewa kulililipa deni hilo. Hivyo, unapotokea mvunjiko wa muungano inabidi Tanganyika na Zanzibar wakae chini waangalie ni namna gani watagawana madeni hayo ili kila upande uelewe wajibu wake juu ya deni linalodaiwa na lazizima wanaodai wajulishwe utaratibu mpya wa kulipwa madeni yao. Kuna taratibu nyingi zinazoweza kutumika kulipa madeni au kuchukuwa dhamana ya kulipa madeni hasa nchi mbili zinapovunja
Inaendelea Uk. 15

AN-NUUR

watu wote kuwa na mawazo sawa, na pia si vizuri na ni hatari watu wote kuwa na mtizamo mmoja, hasa tunapozungumzia suala nyeti kama hili la muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar katika kipindi hiki muhimu cha mchakato wa kutafuta katiba mpya ya umma. Watanzania wengi wanazungumzia tu juu ya uendelezo wa muungano aidha kama ulivyokuwa au muungano wa serikali tatu au hata ikiwezekana serikali

Kizungumkuti cha muungano bila hati


moja. Mimi nazungumzia uwezekano wa kuvunjika kwa muungano na nini kinaweza kutokea kama muungano huo ukivunjika. Ni hasara gani zinaweza kuziathiri nchi husika au ni manufaa gani yanaweza kupatikana baada ya kuvunjika kwa muungano huu? Utati wangu umelenga kwenye sekta mbili muhimu za uchumi na Siasa: Nazungumzia kama muungano utavunjika

Uzoefu wa Urusi (USSR)


Inatoka Uk. 6

nini kitatokea. Kwanza tunafahamu kwamba Ta n z a n i a k a m a n c h i inayokubalika na Umoja wa Mataifa duniani ina madeni makubwa tu inayodaiwa na nchi mbali mbali duniani hasa zile nchi zilizoendelea, lakini pia inawezekana ikawa inazidai nchi zingine ingawa sina uhakika kuhusu hilo. Nchi mbili zilizokuwa zimeungana kwa miaka 49 zimeaminiwa na kukopeshwa madeni mengi, na madeni mengine ni yale ambayo ni madeni

duniani; zisiandikwe katiba pekee ambazo hazifanani na katiba yoyote ile duniani kama ile ya Tanzania; hakuna siri katika kuandika katiba, kwa vile katiba zote duniani zinatakiwa zifanane katika vipengere vingi vinavyogusa mahitaji muhimu ya binadamu. Hivyo akitokea mtu au watu wanajifungia chumbani eti hawataki bughudha kwa vile wanaandika katiba, basi jua kwamba hao hawatutakii mema, bali wana njama za kutuangamiza. Kwa vile katiba ndiyo sheria mama na kama tutakuwa na mama mzuri anayewajali wanae wote kwa usawa bila upendeleo, basi tutakuwa tumechagua mwelekeo mzuri. Muungano wa nchi unaweza ukawa muungano mzuri unaojali maslahi ya wengi, lakini kutokana na hulka za kisadi muungano ukafa na nchi wanachama zikasambaratika na kuunda serikali za upweke: katika serikali hizi za upweke zaweza kuwa serikali zinazoendeleza taratibu za kulinda na kutetea maslahi ya walio wengi au serikali za upweke za kisadi; yoye haya yanawezekana. Mwaka 1991 wakati muungano wa nchi za Kisoviet za Kirusi ziliposambaratika baada ya kufutwa kwa siasa za kikomunist duniani, kulitokea mvutano na mchanyiko mkubwa wa kisiasa na kiuchumi ndani na nje ya nchi za Kisoviet. Soviet Union ilikuwa inaundwa na nchi 15 ambazo ziliwahi kuwa nchi huru huko nyuma lakini

zikashawishiwa kiuchumi, kisiasa na kimajeshi mpaka zikaukana uhuru wao na kujiunga na jumuiya ya nchi za Soviet Union. Ulipovunjika muungano huu madeni yote ambayo Soviet Union ilikuwa inadaiwa na nchi na taasisi mbali mbali duniani yalirithiwa na Russia Federation nchi ambayo ndiyo hasa iliyoanzisha umoja huo, na ndiyo iliyokuwa na ushawishi mkubwa wa kila kitu ndani na nje ya Soviet Union. Pamoja na kurithi madeni yote ya Soviet Union, lakini pia Russia Federation aliendelea kumiliki mali zote za umma (government Assets) zilizokuwa zinamilikiwa na serikali ya Soviet Union. Baada ya kuvunjika kwa muungano nchi zote zikawa kama ndiyo zimejikomboa kwa kupata uhuru toka Soviet Union, hivyo kila nchi ikawa inajitahidi kujenga misingi ya dola, kuandika katiba na kuomba uanachama kwenye taasisi na jumuiya mbali mbali za kimataifa. Nchi nyingi zilizokuwa katika jumuiya hii ya Soviet Union zimeshindwa kabisa kuchagua mwelekeo mzuri wa kuziendeleza nchi zao, na matokeo yake zimeishia kujenga mfumo wa kijambazi (Banditry system), mfumo wa kisadi unaolindwa na mitandao ya uhalifu wa kupangwa (Mafia). Katika mfumo huu ni wale tu walioko madarakani au katika idara na sehemu mbali mbali za serikali ndiyo wanaofaidi.

Kama huna ajira serikalini, basi wewe umeisha; na mwenye ajira anahakikisha kwamba anamvuta mwanae au nduguye karibu naye. Akika muda wa kustaafu, anamwachia mwanae nafasi aendeleze ufisadi; na haya yote yameletwa kwa vile viongozi wa umma hawakutaka kuleta mabadiliko ya kweli kwa kuwahusisha wananchi, bali waliendeleza taratibu zile zile za zamani na hata kuziboresha kwa manufaa yao binafsi. Ni nchi tatu tu (Latvia, Estonia, Lithuania) ambazo zilikuwa ndani Jumuiya ya Soviet Union ambazo

zimeweza kufuzu kujiunga na Jumuiya ya Nchi la Ulaya (EU) mwaka 2000. Nchi zingine kumi ukiiondoa Russia Federation na Belorussia ambazo hazina mpango kabisa na kujiunga na jumuiya hiyo; zingine zote kumi zimeshindwa kabisa kufuzu masharti ya kujiunga na EU, kwa vile zimekumbatia tawala za kijambazi ambao umejengwa kwenye misingi ya usadi na uhalifu wa kupangwa (Mafia). Kupanga ni kuchagua; ukipanga mipango mizuri utakuwa umechagua mwelekeo mzuri.

VIWANJA VILIVYOPIMWA KONGOWE KIBAHA TOWNSHIP REGISTERED PLAN No. 70995 BLOCK H
PLOT HATUA ENEO MRABA GHARAMA TSH

H1 H2 H3 H4 H5 H6 H7 H8 H9 H10 H11 H12

50 x 29 32 x 32 50 x 30 37 x 30 50 X 45 33 x 37 60 x 45 50 x 40 67 x 50 70 x 45 90 x 50 59 x 40

1341 Sqm 1136 Sqm 1470 Sqm 1115 Sqm 2259 Sqm 1566 Sqm 2423 Sqm 1984 Sqm 3564 Sqm 2842 Sqm 3780 Sqm 2292 Sqm

4,023,000/= 3408000/= 4410000/= 3345000/= 6750000/= 4695000/= 7269000/= 5952000/= 10692000/= 8526000/= 11340000/= 6876000/=

Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

- Palestine Information Centre (Tanzania) Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania) Feature/Report 4 February 2013

UN fact-nding mission condemns Israeli settlement on Occupied Palestinian Territory


Palestinians welcomed a UN Human Rights Council report on Thursday 1 February 2013 highly critical of Jewish settlements in the occupied West Bank, saying it vindicated their struggle against the Israeli occupation. The UN investigation, which Israel boycotted, urged Israel to halt settlement construction unconditionally and begin removing more than 500,000 Israeli settlers from occupied territory immediately. The UN report, said the settlements contravened the Fourth Geneva Convention forbidding the transfer of civilian populations into occupied territory and could amount to war crimes that fall under the jurisdiction of the International Criminal Court. Following are excerpts from the 37-page report: The facts brought to the attention of the Mission indicate that the State of Israel has had full control of the settlements in the OPT since 1967 and continues to promote and sustain them through infrastructure and security measures. The Mission notes that despite all the pertinent United Nations resolutions declaring that the existence of the settlements is illegal and calling for their cessation, the planning and growth of the settlements continues both of existing as well as new structures. The establishment of the settlements in the West Bank including East Jerusalem is a mesh of construction and infrastructure leading to a creeping annexation that prevents the establishment of a contiguous and viable Palestinian State and undermines the right of the Palestinian people to selfdetermination. The settlements have been established and developed at the expense of violating international human rights laws and international h u m a n i t a r i a n l a w, a s applicable in the OPT as notably recognised by the 2004 ICJ Advisory Opinion. The settlements are established for the exclusive benefit of Israeli Jews; settlements are being maintained and developed through a system of total segregation between the settlers and the rest of the population living in the OPT. This system of segregation is supported and facilitated by a strict military and law enforcement control to the detriment of the rights of the Palestinian population. The Mission considers that in relation to the settlements Israel is committing serious breaches of its obligations under the right to selfdetermination and certain obligations under international humanitarian law, including the obligation not to transfer its population into the OPT. The Rome Statute establishes the International Criminal Courts jurisdiction over the deportation or transfer, directly or indirectly, by the occupying Power of parts of its own population into the territory it occupies, or the deportation or transfer of all or parts of the population of the occupied territory within or outside this territory. Ratication of the Statute by Palestine may lead to accountability for gross violations of human rights law and serious violations of international humanitarian law and justice for victims. The existence of the settlements has had a heavy toll on the rights of the Palestinians. Their rights to freedom of self-determination, nondiscrimination, freedom of movement, equality, due process, fair trial, not to be arbitrarily detained, liberty and security of person, freedom of expression, freedom to access places of worship, education, water, housing, adequate standard of living, property, access to natural resources and effective remedy are being violated consistently and on a daily basis. The volume of information received on dispossession, evictions, demolitions and displacement points to the magnitude of these practices. These are particularly widespread in certain areas and acute in East Jerusalem. The Mission has noted that the identities of settlers who are responsible for violence and intimidation are known to the Israeli authorities, yet these acts continue with impunity. The Mission is led to the clear conclusion that there is institutionalized discrimination against the Palestinian people when it comes to addressing violence. The Mission believes that the motivation behind this violence and the intimidation against the Palestinians as well as their properties is to drive the local populations away from their lands and allow the settlements to expand. The Mission is gravely concerned at the high number of children who are apprehended or detained, including for minor offences. They are invariably mistreated, denied due process and fair trial. In violation of international law they are transferred to detention centres in Israel. Children suffer harassment, violence and encounter significant obstacles in attending educational institutions, which limits their right to access education. Israel, the occupying Power is failing in its duty to protect the right to access education of the Palestinian children and failing to facilitate the proper working of educational institutions. Information gathered by the Mission show that some private entities have enabled, facilitated and proted, from the construction and growth of the settlements, either directly or indirectly. Women alone in their homes, the Bedouins and other vulnerable groups are easy targets for settler violence, creating a sense of insecurity amongst the wider Palestinian society. Recommendations Israel must, in compliance with article 49 of the Fourth Geneva Convention, cease all settlement activities without preconditions. In addition it must immediately initiate a process of withdrawal of all settlers from the OPT. The Mission further urges Israel to ensure adequate, effective and prompt remedy to all Palestinian victims for the harm suffered as a consequence of human rights violations that are a result of the settlements in accordance with Israels international obligation to provide effective remedy. Where necessary, steps must to be taken to provide such remedy in concurrence with the representatives of the Palestinian people and with the assistance of the international community. Israel must put an end to the human rights violations that are linked to the presence of settlements. The Mission calls upon the government of Israel to ensure full accountability for all violations, including for all acts of settler violence, in a non-discriminatory manner and to put an end to the policy of impunity. The Mission urges Israel to put an end to arbitrary arrest and detention of the Palestinian people, especially children, and observe the prohibition of the transfer of prisoners from the OPT to the territory of Israel, according to Article 76 of the Fourth Geneva Convention. The Mission calls upon all Member States to comply with their obligations under international law and to assume their responsibilities in their relationship to a State breaching peremptory norms of international law specically not to recognize an unlawful situation resulting from Israels violations. Private companies must assess the human rights impact of their activities and take all necessary steps including by terminating their business interests in the settlements to ensure they are not adversely impacting the human rights of the Palestinian People in conformity with international law as well as the Guiding Principles on Business and Human Rights. The Mission calls upon all Member States to take appropriate measures to ensure that business enterprises domiciled in their territory and/or under their jurisdiction, including those owned or controlled by them, that conduct activities in or related to the settlements respect human rights throughout their operations. The Mission recommends that the Human Rights Council Working Group on Business and Human Rights be seized of this matter ____________________ ______ Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org Website: www.pal-tz.org

9
Na Shaaban Rajab SASA si hadithi tena. AFRICOM imejipenyeza katika ardhi ya Afrika. Licha ya Nchi za Jumuia ya Umoja wa Nchi za Afrika, AU, kujitangaza kuwa hazitakuwa tayari kuruhusu kuwekwa kambi ya Komandi ya Majeshi ya Marekani Barani Afrika (AFRICOM), Niger imekubali kupitia dirishani. Tayari Marekani na Niger zimetiliana rasmi saini mkataba ambao umeiruhusu Marekani kuweka kituo cha ndege cha kijeshi katika ardhi ya Niger, kituo ambacho sasa kitaiwezesha Marekani kufanya mashambulizi na upelelezi katika nchi za Afrika kwa ndege za drones. Mkataba huo umeruhusu ndege zisizo na rubani za Marekani (drones), kufanya upelelezi au kushambulia kwa mabomu katika maeneo ya nchi za Afrika, ambazo sasa ziko mbioni kutua rasmi katika bara la Afrika. Ndege hizo zitaweka kambi yake katika mji wa Agadez, uliopo jangwani Kaskazini mwa Niger, ambao unapakana na Mali, Algeria na Libya, chanzo cha habari kimebainisha. Majeshi ya Marekani tayari kwa sasa yanaisaidia Ufaransa kufanya mashambulizi katika nchi ya Mali, iliyo jirani na Niger kupitia mgongo wa Ufaransa. Lakini sasa kwa kupitia kituo chake kipya cha kijeshi cha Agadez, itasimama yenyewe kuchunguza, kushambulia na kufanya kile inachotaka katika nchi nyingine za Afrika bila shida wala bughudha. Marekani imeshabainisha kwamba shughuli za kijeshi zitakazofanyika kupitia kituo hicho kipya, zimelenga kuikomboa mipaka ya Kaskazini mwa Mali kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Kiislamu wanaotaka kufanya mapinduzi nchini humo. Jumatatu iliyopita, Marekani na Niger zilitiliana saini mkataba huo rasmi, ambapo sasa Marekani itafanya kazi zake za kijeshi katika ardhi Niger kwa uhuru. Pentagon wameshapanga kuzindua makazi hayo mapya ya ndege zisizo na rubani nchini humo. Habari zilizothibitishwa na serikali ya Niger jijini Niamey, zinaeleza kuwa balozi wa Marekani mjini Niamey , Bisa Williams, alimuomba Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, kibali cha kutumia ardhi ya nchi hiyo kuruhusu ndege za kipelelezi za Marekani kufanya kazi zake, naye mara moja akakubali. Baada ya mazungumzo na Rais Issoufou, Balozi Williams aliwaeleza waandishi wa habari kuwa walizungumzia masuala ya ushirikiano wa kiuchumi, kijeshi na kimaendeleo. Pia balozi huyo hakusita kutoa shukurani zake kwa Ufaransa kufuatia mpango wake wa kijeshi nchini Mali wa kuwaangamiza aliowaita

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013


ya ndege za zisizo na rubani za shirika hilo katika maeneo mengi duniani. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta, alikuwa msimamizi wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Pakistan na Mkuu wa Shirika la Ujasusi la CIA tangu mwaka 2009 hadi 2011. Kuna habari kwamba Serikali wa Marekani imekusudia kupeleka wanajeshi 3,500 katika nchi 35 za Bara la Afrika mwaka huu wa 2013. Gazeti la World Tribune, linalochapishwa nchini Marekani, limeripoti kuwa uamuzi huo wa Washington umekusudia kukabiliana na ongezeko la nguvu za kundi la al Qaeda na washirika wake. Gazeti hilo limeandika kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesisitiza kutumwa majeshi hayo katika maeneo yaliyokumbwa na ghasia Barani Afrika, lengo likiwa ni kutokomeza ugaidi. Jenerali Carter Ham, Kamanda wa Majeshi ya Marekani Barani Afrika (AFRICOM), amesema hali ya Afrika hivi sasa ni tofauti na ilivyokuwepo awali. Jenerali Ham amedai, kuna makundi mapya yenye silaha, ambayo hayana uhusiano na mtandao wa al Qaeda na kusisitiza kuwa, makundi hayo ni tishio kubwa kwa Marekani. Tangu shambulio la Septemba 11, Marekani imekuwa ikitumia kisingizio cha kupambana na ugaidi kuhalalisha udhalimu wake na kukia malengo yake katika maeneo mengi duniani. Hivi sasa bara la Afrika linapewa nafasi kubwa katika sera za usalama za Marekani, sera ambazo ni tishio kwa usalama wa bara hili. Kisingizio kikubwa inachokitumia Marekani kuhalalisha mipango yake, ni kupambana na magaidi. Boko Haram nchini Nigeria, Al Qaeda katika Afrika ya Kaskazini (Aljeria na Libya), makundi ya Waislamu wenye misimamo ya kidini na kiutawala kaskazini mwa Mali. Kwa upande wa Afrika ya Mashariki ni kundi la Al Shabab na la Lords Resistance Army la Joseph Kony . Katika hali hii, hata hapa kwetu tutarajie mengine. Hasa kwa kuzingatia msimamo wa Wazanzibar wanaopigania muundo wa Muungano wa Ta n g a n y i k a n a Z a n z i b a r, wakiungwa mkono na Taasisi ya Kiislamu ya UAMSHO, kumeleta ishara ya wasiwasi. Kama tunavyofahamu sote, hivi sasa serikali wamewaona UAMSHO kama Waislamu wa siasa kali, viongozi wake wa ngazi za juu wote wako ndani wakikabiliwa na mashitaka ya uchochezi na uvunjifu wa amani. Wamenyimwa dhanama. Kwa sura hii, haishangazi siku moja drone kutoka Lemonnier ikazagaa katika anga letu wakiwatafuta al Qaeda Zanzibar. Wa l a h a i t a k u w a a j a b u Inaendelea Uk. 10

AN-NUUR

Tai ametua rasmi Afrika

Niger yakubali kumjengea kiota Wanaosakwa ni Shura, UAMSHO, AU msimamo wenu umeishia wapi

wapiganaji wanaoshirikiana na magaidi wa Al Qaeda huko Kaskazini mwa Mali. Katika vita hivyo, Marekani imedai imepeleka ndege za kivita na za kubebea zana za kivita na wapiganaji tu nchini Mali, lakini ikakanusha kupelekea vikosi vya wapiganaji. Bila shaka watakuwa wamefanya hivyo wakitarajia kuwa walikuwa mbioni kuweka kambi kamili ya kijeshi katika ukanda huo siku za usoni. Niger imewasha taa ya kijani kuiruhusu Marekani kupeleka ndege zake za kipelelezi katika ardhi yetu ili kuboresha usalama dhidi ya harakati za Kiislamu, chanzo cha habari cha serikali ya Niger kililieleza Reuters. Kabla ya kutiwa saini makubalinao hayo, Mkuu wa U.S. Africa Command, Generali Carter Ham, aliitembelea Niger mwezi uliopita. Nchi hiyo maskini Afrika Magharibi yenyewe ilieleza kuwa inahitaji ushirikiano wa karibu wa kiusalama na Washington. Jijini Washington, vyanzo vya kidiplomasia vimeieleza The Guardian kuwa, mkataba huo mpya unaoitwa Status of Forces umepanua wigo zaidi. Hatua hiyo imetafsiriwa kuwa ni kutoa nafasi kubwa kwa Marekani kupanua matumizi ya ndege zisizo na rubani katika Bara la Afrika, ambapo ndege hizo zitahusisha maeneo ya nchi za Afrika kuanzia Burkina Faso, Ethiopia na Djibouti katika pembe ya Afrika. Kufuatia hali hiyo, imeelezwa kuwa Marekani sasa inalitizama eneo la Kaskazini mwa Afrika

hadi Magharibi kama uwanja wa mapambano dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Kiislamu inayowahusisha na ugaidi. Tafsiri hiyo ya Marekani imekuja kufuatia kuwepo mzozo wa sasa katika nchi za Mali, Nigeria katika majimbo ya Kaskazini na Algeria, ambako mapepari wa nchi za Magharibi wanaovuna mafuta wamekuwa wakishambuliwa katika viwanda vya mafuta. Mshauri wa Jeshi la Marekani, Robert Caruso, amesema kuwa kambi yeyote nchini Niger inaweza kufanana na ile ambayo tayari ipo nchini Burkina Faso na kwamba zitafaa sana kwa ndege zisizo na rubani na hata zile zinazoongozwa na rubani katika mpango wa upelelezi na ufuatiliaji. Kamanda huyo alidai kuwa matumizi ya ndege hizo ni kutokana na kukosekana kwa wapelelezi wa Marekani katika eneo hilo. Tunaleta drones nyingi katika Sahel kwa sababu hatuna watu wa kupeleleza ukanda huu-wala hatuna wa kutoka katika nchi maraki. Tulitakiwa kuwa na wapelelezi hao lakini hatuna, alisema Caruso. Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya vita wameeleza kuwa matumizi ya drone hata kama ni kwa upelelezi tu, yameleta athari kubwa katika maeneo mengi. Imeripotiwa mara nyingi kuwa mashambulizi ya ndege hizo za drone za Marekani yameleta maafa makubwa katika nchi za Pakistan, Yemen, Afghanistan na Somalia. Mashambulizi katika nchi hizo yamesababisha kuibuka

kwa vikundi vya kupigania uhuru na mauaji makubwa ya raia. Ta a s i s i m o j a y e n y e maskani yake jijini London, (The London-based Bureau of Investigative Journalism), ambayo imekua ikifuatilia madhara yanayosababishwa na ndege za drone za Marekani zilizowahi kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali duniani, ilikuja na matokeo kwamba, nchini Pakistan pekee, yamefanyika mashambulizi zaidi ya 362 ambapo watu 3,461 wengi wao wakiwa ni raia wasio na hatia wameuliwa. Awali katika Bara la Afrika, Marekani ilikuwa na kituo cha ndege hizo. Kituo hicho kilichokuwa pekee cha kudumu hapo kabla kipo nchini Djibouti, maili 3,000 kutoka Mali. Kituo hiki ndicho kimekuwa kikitumika kurusha ndege zisizo na rubani na kufanya mashambulizi katika nchi za Yemen na Somalia, ambapo kumekuwa kukiripotiwa mamia ya raia kuuliwa. Hata hivyo watati wengi wa masuala ya kivita wanaamini kwamba idadi ya raia waliouliwa ni kubwa zaidi. Licha ya madhara hayo, Kambi ya Agader ni ishara tosha kwamba Rais Barack Obama, amedhamiria kikamilifu kutumia zaidi drones katika mipango yake ya usalama na dhulma za kiuchumi. Waziri wake wa Ulinzi, Leon Panetta, ameunga mkono hatua za Shirika la Kijasusi la Marekani CIA na kusisitizia udharura wa kuendelezwa mashambulizi

10

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Na Khalid S Mtwangi

Ni jambo la kawaida kabisa kuona watoto, wakiwa wakiume na wakike, wakizurura ovyo mitaani hasa katika miji, mikubwa kama vile Dar es Salaam. Lakini pia kuna wale ambao wanapewa kazi na wazazi wao wakitembeza vyakula kama vile mandazi, vitumbua hata wali na ugali. Kwa kiwango kikubwa sana, haya yanatokea kwa sababu wazazi wengi ni masikini. Kweli watoto wengine hukimbia makwao kwa sababu ya mateso hasa panapokuwa na mama wa kambo. Linalosikitisha sana ni kwamba jaribu kuwauliza vijana hawa majina yao na mara nyingi watataja majina yanayojulikana kama ya Kiislamu kama vile Juma, Bakari, Abdallah, Muhamedi , na kadhalika. Pamoja na hayo, mahakimu wa kila ngazi wanasema wazi wazi kuwa wateja wao wengi ni vijana wa Kiislamu. Na kweli, ni wao ndio waliojaa huko Segerea kwa mfano na magereza mengine nchini. Kwa muda mrefu sana na mpaka sasa maelezo yanayotolewa ni ile hali ya Waislamu nchini kunyimwa haki yao hasa ya kupata elimu. Mfano mzuri ni wa yule kijana wa Kilosa ambaye nafasi yake ya kuendelea kidato cha kwanza alipewa kijana wa Kikristo na yeye akaishia kuwa dereva wa lori. Ama yule kutoka shule ya msingi ya Mughabe, Dar es Salaam ambaye mzazi wake alilalalmika kuwa hakuchaguliwa kuendelea sekondari ati hakupita mtihani wake. Mzee huyo alikuwa akifahamu kuwa kufuatana na maendeleo ya mwanaye hapo shule, huyo kijana asingeweza kuanguka mtihani wa darasa la saba. Lakini umefika wakati Wa i s l a m u w a s i w e wanalalamika tu kuwa wananyimwa haki yao hapa na pale. Wao wenyewe nao waamke wasimame wima na waanze kujitegemea katika nyanja nyingi. Ni kweli ikubalike kuwa hivi sasa

Waislamu wamejitahidi sana kutafuta elimu kiasi kuwa wanajenga shule nyingi za sekondari na zinawasomesha vijana wengi kwa ufanisi mkubwa. Hivi karibuni nilifarijika sana nilipokutana na kijana ambaye kamaliza kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya kwanza ya uhandisi ujenzi. Kijana huyu alisoma katika shule ya sekondari ya Waislamu pale Kigoma ambayo si ya siku nyingi sana. Kweli ziko shule zingine nyingi za Kiislamu zenye maendeleo kama hiyo; lakini ngwe bado ni kubwa sana ambayo inataka Waislamu wakazane kwa nguvu ya ziada ili hata waweze angalau kulipunguza lile pengo lililopo. Hakika wazazi wengi wa Kiislamu pia wanastahili sifa kwa kukipa kipaumbele wajibu wao wa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu ya dini katika madrasa zilizomo jirani huko wanapoishi. Ikubalike kuwa vijana hawa wasipate muda mrefu wa kucheza pale wanapotoka shuleni. Kwa siku nyingi lilikuwa ni jambo la kawaida kama sio la lazima kuwa hata kama vijana wakitoka shule muda gani basi linalofuata ni kuhudhuria masomo ya darsa hata zile zilizomo kando pembezoni ya nyumba za maalim. Utamaduni huu usikosekani pale ambapo hakuna shule za msingi za Waislamu. Turudie kwa watoto wa mitaani ambao inajulikana wengi wao ni wa Kiislamu. Inaelekea kwamba katika miji mikubwa kama vile Dar es Salaam taasisi zinazotambulika kuwa ni za Kiislamu hazina sera ya kuwahudumia vijana hawa. Bahati mbaya kuna taasisi nyingi za wale wasiokuwa Waislamu ambazo zina vitengo maalum ambavyo vinawashughulikia vijana hawa wawe waKristo ama dini zingine na hata wasiokuwa na dini. Hivi sasa imetambulika kuwa lengo ni kuwarubuni vijana kuritaad na hawa ndio watakao kuwa waumini wao wa kesho. Ni vizuri kusisitiza kuwa kuwa wao hakika wanawalenga sana vijana walio Waislamu kwa madhumuni ya kupunguza idadi ya Waislamu nchini humu. Inafahamika kuwa huwa hawaridhiki kamwe kumuhudumia kijana ambaye bado anataka kuendelea na

Huduma kwa watoto wa mitaani


jina lake lile la Kiislamu. Ni kwa sababu hiyo ndio maana wale vijana wa Kiislamu wanaosoma shule, ziwe za msingi ama za sekondari za makanisa, hulazimishwa kuhudhuria missa hata kama sio waumini wa kanisa hilo. Hawana amri ya Mwenyeezi Mungu kama ile waliyonayo Waislamu kuwa La ikrah din. Wao hata huwabatiza watu bila idhini yao hasa pale watu hao wanapokuwa na shida ama wagonjwa mahututi. Hulazimisha kubadili imani yao. Kwa hiyo wanapopata kijana wa kumrubuni hilo kwao huwa ni vuno. Kweli kuna watu binafsi, hasa kina Bibi ambao wamejikita katika kupokea na kuwalea watoto yatima hasa hapa Dar es Salaam. Kwanza kutokana na unyu wa nafasi walizo nazo kina bibi hawa, idadi ya vijana wanaoweza kuwalea ni ndogo sana. Mahitaji ya kuweza kuwahudumia watoto wa mitaani ama wanaoishi katika mazingira magumu sana ni kubwa sana kupita uwezo wao. Kwa hiyo hakuna kinyume ni lazima taasisi za Kiislamu humu nchini zianze kufikiria kuwa na sera maalum ya kuwaokoa hawa vijana wasirubuniwe na wale walio wajanja na wasio heshimu imani za wenzao. Ikiwa kweli itaamuliwa na taasisi yeyote ile ya Kiislamu kuanzisha mfumo huu wa kuwasaidia watoto wa mitaani, gharama zake zinaweza kuwa ni kubwa sana. Haitakuwa tu kuwapatia hawa vijana chakula na mahali pa kulala, bali pia waweze kupata elimu; na hii maana yake ni kuwa na shule ya msingi ya Kiislamu ya bweni. Hilo sio kwamba halitawezekana kwa vile kuna taasisi kongwe k a m a v i l e B A K WATA ambao wakijipanga vizuri na kujirekebisha katika matumizi yao wanaweza kuanzisha kitengo kikubwa cha kulea watoto wa mitaani. Nao BARAZA KUU wamejaaliwa kuwa na wasomi na wanataaluma wengi wakiwemo waalim ambao wanaweza kuunda mipangilio inayofaa na inayoweza kuleta ufanisi katika jitihada zao. Kuna taasisi kama vile Msikiti wa Wamanyema ambao upo katikati ya mji kunakopatikana watoto wengi wanaoshi maisha magumu, hivyo itakuwa sahihi kabisa wao kuwa mstari wa mbele katika harakati za aina hiyo. Si ajabu kuwa hawa watoto wengi wa mitaani kuwa wana asili ya Umanyema kwa wazazi wao. Ili kuhakikisha kuwa huko mbele wanapatikana Waislamu wanaoijua dini yao na kuwa na imani ya Uislamu thabiti, ni lazima kuwapika vijana wa leo waive kwa kazi hiyo ya kesho. Labda sio vibaya kurudia na kusisitiza kuwa Makanisa hivi sasa wanalenga kuwarubuni vijana wa Kiislamu waritaad ili kujenga makanisa ya kesho. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa wasichana wengi wa Kiislamu wanadanganywa wanabadili dini na kuolewa na vijana wa Kikristo. Mabinti hawa wakiwa na msingi thabiti wa dini yao hawataweza kutetereka hata kidogo. Shime viongozi wa taasisi za Kiislamu, wakati ni huu!!

Inatoka Uk. 9 wakitafutwa Shura madhali walishatizamwa kwa jicho la Waislamu wenye msimamo mkali. Uchunguzi wa harakati za kijeshi za Marekani barani Afrika, hasa zile za kitengo chake cha kijeshi cha Africom, unadhihirisha hali yenye kutia hofu. Hali hiyo pia ni ya kusikitisha kwa vile Marekani inashirikiana katika njama zake mkono kwa mkono na baadhi ya majeshi ya nchi zetu wenyewe za Kiafrika. Tukumbuke tu kwamba hata Rais wetu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, mapema alishasaini mkataba wa anga huru na Marekani. Eneo hili la Afrika ya Mashariki na eneo zima la Pembe ya Afrika, Marekani inategemea sana kambi yake ya kijeshi ya Lemonnier iliyoko Djibouti. Kwa upande wa nchi za Afrika ya Magharibi, kuna taarifa kwamba Marekani ina kituo chake cha siri cha kijeshi nchini Burkina Faso. Huko akina Boko Haram na wengineo wataojitokeza kupingana na serikali zao ndio walengwa wakuu. Maadhali wana alama ya Uislamu, watapewa jina baya na watashughulikiwa. Kwa upande wetu, Lemonnier ndio kambi kubwa

Tai ametua rasmi Afrika


ya Marekani katika eneo hili. Marekani inaitumia kambi hiyo kurushia vyombo vya angani vya mashambulizi visivyo na rubani ambavyo vimetumika kuwaua watu wanaoshutumiwa kuwa ni magaidi katika Yemen na Somalia. Pamoja na kwamba kambi kuu ya AFRICOM tunaelezwa kuwa ipo nchini Ujerumani, lakini kijanjajanja Marekani imeshamudu kuweka kambi zake za majeshi yake ya AFRICOM ndani ya bara la Afrika. Inavitumia vituo hivyo kurushia ndege zake za upelelezi na za doria juu ya sehemu kubwa ya anga la bara la Afrika. Pia inavitumia kurushia vyombo vyake vya anga visivyo na rubani. Hapa tunajiuliza, ule msimamo wa viongozi wetu wa AU ulikuwa na maana gani? Inajulikana kwamba katika Afrika ya Mashariki jeshi la Marekani la Africom limekuwa likilisaidia kwa hali na mali jeshi la Muungano wa Afrika katika Somalia (AMISOM). Marekani siku zote imekuwa ikisisitiza kwamba wanachokifanya Afrika ni kujenga mahusiano endelevu kati ya jeshi lake na majeshi ya nchi za Kiafrika. Kigezo kikubwa kinachotumika katika uhusiano huo ni kupambana na

ugaidi wa kimataifa. Mshangao mkubwa ni kwamba, huko Kongo DRC, siku zote kuna vita na uasi kwa miaka nenda rudi. Hivi sasa kuna mzozo kati ya serikali na waasi wa M23. Kisangani, Goma na miji mingine imekuwa haitulii vita. Watu wanauliwa, mali zinaporwa. Lakini haijawahi kusikika kama kuna mpango wa Marekani kupeleka Drones zake kujaribu kutuliza hali. Joseph Kony amezalisha misiba huko Kaskazini mwa Uganda miaka nenda rudi, amekuwa akiwateka na kuwaingiza watoto wadogo katika jeshi lake, pamoja na kwamba anatajwa, lakini hakuna hatua za uhakika za kunusuru hali zilizochukuliwa na Marekani katika eneo hilo la Uganda Kaskazini. Kony bado yupo, vita yake haijakoma. Kwa nini zisiende drone huko? Iweje umuhimu wa drone uelekezwe sehemu za majangwa kwa wanamgambo wa Kiislamu wanaopingana na serikali zao? Mali vita vimelipuka siku za hivi karibuni. Vita vya Kony Uganda, Waasi DRC ni vya miaka, Kwa nini drone zielekezwe Mali, Libya, Algeria na Somalia? Uko wapi msimamo wa AU juu ya AFRICOM?

11
Na Mwandishi Maalum

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

HATI ya Muungano tunayo, ni kauli ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein aliyoitoa wiki iliyopita k a t i k a s h e re h e z a kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM. Katika hotuba yake iliyojaa vijembe, kejeli na dharau kwa wale anaowahisi yeye kuwa hawautaki Muungano wa sasa (serikali mbili), Dr.Shein alisema kuwa anashangaa sana kuona baadhi ya watu wanataka kujua ilipo hati ya Muungano lakini alisema hawajafanya juhudi za kuitafuta kwani serikali inayo na nakala yake ipo makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York. Hati ya Muungano ipo pale IKULU Zanzibar kuna chumba na meza inayotumika kuwekea saini anayetaka kuiona aende Umoja wa Matifa wanayo kopi hakuna haja ya kuhangaika, alisema Dr. Shein akinukuliwa na gazeti la kila siku la Zanzibar Leo, gazeti la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar la tarehe 1 februari 2013 Akasisitiza kuwa Muungano wa serikali mbili unatosha kwa Zanzibar kwani ndio pekee unaoweza kuwaletea manufaa wananchi. Alisema Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana hazikufanya hivyo kwa kubahatisha kwani zilitambua umuhimu wa kuwa na muungano wa pande zote mbili. Akasema kuwa Zanzibar katika muungano huo imekuwa inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na wengi wa Wazanzibari wanaishi eneo kubwa la Tanzania bara kuliko watu wa bara wanaoishi Zanzibar Nilipokuwa Makamu wa Rais nilitembelea mikoa mbali mbali ya Tanzania na kila nilipoenda nilikutana na Wazanzibari, tuutuzeni

Tusipotoshe agenda: Hoja ni Zanzibar huru

Muungano wetu kuona unabakia imara na lazima tutafakari ndani ya miaka

Note 1. The Peoples Republic of Zanzibar was admitted to membership on 16 December 1963 by Resolution No. 1975 (XVIII). For the text of the Declaration of acceptance of the obligations contained in the Charter dated 10 December 1963 made by Zanzibar (registered under No. 7016), see United Nations, Treaty Series , vol. 483, p. 237. In a note addressed to the Secretary General on 6 May 1964, the Ministry of External Affairs of the United Republic of Tanzania informed him that, following the

United Republic of Tanzania


signature and ratication of the Articles of Union between the Republic o f Ta n g a n y i k a a n d the Peoples Republic of Zanzibar, the two countries had been united on 26 April 1964, as one sovereign State under the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar. The Ministry further asked the SecretaryGeneral to note that the United Republic of Tanganyika and Zanzibar declares that it is now a single Member of the United Nations bound by the provisions of the Charter, and that all international treaties and agreements in force

hii 39, alisema Dr.Shein akinukuliwa na gazeti hilo la serikali.

Yapo maswali kadhaa yanajitokeza kutokana na kauli hii ya Mheshimiwa

between the Republic of Tanganyika or the Peoples Republic of Zanzibar and other States or international organizations will, to the extent that their implementation is consistent with the constitutional position established by the Articles of the Union, remain in force within the regional limits prescribed on their conclusion and in accordance with the principles of international law. In communicating the above-mentioned note, in accordance with the request contained therein, to all States Members of
Inaendelea Uk. 15

Rais Dr. Shein. Moja ni hili alilosema kuwa anayetaka kuiona (Hati ya Muungano) aende Umoja wa Matifa, UN, wanayo nakala, hakuna haja ya kuhangaika. Sasa kama Hati hii ya Muungano ipo pale Ikulu, Zanzibar, kwa nini watu wahangaike kwenda kuitafuta New York, Marekani? Kwa nini asiwaambie wanaotaka kuiona waje pale Vuga kuitizama? Kwa nini asingekuja nayo katika ule mkutano wake wa CCM akainyanyua juu minalhadhirina wakaiona? Rais Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Dr. Amani Abeid Amani Karume amesema kuwa pamoja na kukaa Ikulu miaka 10, hajapata kuona hati hiyo. Na huyu ndiye aliyemkabidhi osi Dr. Shein. Swali ni je, kama Rais aliyetangulia aliyemkabidhi ofisi hakumkabidhi Hati hiyo kwa sababu haikuwepo Ikulu, Dr. Shein yeye kaipata wapi? Nani kamletea na ilikuwa wapi hata marais waliomtangulia wasiione? Rais Shein anasema Hati ya Muungano ipo pale IKULU Zanzibar na kwamba ipo katika chumba na meza inayotumika kuwekea saini mikataba ya kiserikali. Ina maana marais wote waliomtangulia Zanzibar, walikuwa hawajui hilo, na hawaijui meza hiyo iliyopo Ikulu yenye Hati Hiyo? Kwa hakika inashangaza sana kuona Rais Mstaafu anasema kuwa aonyeshwe hati ya muungano ilhali mrithi wake anasema ipo. Kwa upande mwingine Rais Shein anasema kuwa mfumo mzuri wa muungano ni huu wa serikali mbili huku akiwaponda wale wote wanaouhoji. Nadhani kwa hapa tuchukulie
Inaendelea Uk. 15

12
Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Muifanye kwa salama, shari zikuepukeni Mpate alama njema, kuvukia wasitani Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Mtangulize KARIMA, jinale tangulizeni Yote mliyoyasoma, Rabbi ata kuungeni Hamtobakia nyuma, mtavuka salimini Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Mmefanya jitihada, nimewashuhudieni Mkazikubali shida, zilizopita kifani Usingizi ni ibada, mkauweka pembeni Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Mkajinyima vizuri, kuja itafuta fani Mkaacha vya fahari, huko kwenu masikani Kiasi mka ghairi, kuzipupia fasheni Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Chakula mkadiriki, kujipanga kwa foleni Kwenye kubwa halaiki, mule ndani kantini Wala hamkuhamaki, mkatulia vitini Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Kuzimisi familia, kwenu siyo jambo geni Hakika mnaumia, kosa zao kampani bali mnavumilia, kipindi cha mashakani Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Msijefanya ghururi, tan-bihi nawapeni Ghalati si desituri, katika yetu imani Siyo kama nahubiri, bali nawakumbusheni Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Sana tutawakumbuka, mkienda likizoni Upweke utatuka, peke yetu osini Maktaba kutumika, huboresha anuani Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Kile cha Waislamu, Chuo Kikuu jamani Morogoro mfahamu, sehemu zile mjini Chuo hiki ni timamu, hakika kipo makini Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Mkutubi kaditama, kalamu naweka chini Busara nazo hekima, zilizo mwangu kichwani Ndizo zilizo nituma, leo ni waliwazeni Nyote mitihani mema, leo nawatakieni Isihaka Hemed Mzuzuri (Sauti ya Mkutubi) (hemedisihaka@yahoo.com) 0714-341 216 MUM- Morogoro.
Kilio kila kukicha, cha chama kuhujumiwa, Yanenwa bila kucha, na makada aminiwa, Wa kando pasi kumcha, lawama anatupiwa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe.

Barua/Shairi

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

MITIHANI MEMA!

Kuchinja katika Uislamu kuna utaratibu na kanuni zake


HIVI sasa kuna hoja za baadhi ya Wainjilisti ambao wanaizogoa serikali wakitaka Wa k r i s t o w a r u h u s i w e kuchinja katika machinjio ya wanyama ya serikali kwa kuwa machinjio ya sasa yanatoa nafasi kwa Waislamu peke yao. Pamoja na kwamba wengi hawafahamu kama kuna sheria na utaratibu wa kuchinja Kikristo kwa mujibu wa Biblia, na iwapo kuna utaratibu huo unatokana na Mungu na Mitume wake au la, lakini ni vyema tukadokeza japo kwa uchache suala la kuchinja kwa mujibu wa taratibu za Mwenyezi Mungu na Mitume kwa kujibu wa Uislamu. Ifahamike tu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa mbingu na ardhi na kila kilichomo. Aliumba viumbe watu, wadudu, wanyama na mimea na akamwezesha mwadamu kuvitawala viumbe hivyo, lakini kwa kuweka utaratibu maalum. Anasema Allaah Subhaanahu Wa Taala): (Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako) [Al-Kawthar: 2] Kuchinja ni moja ya ibada za Kiislamu ambayo inatukumbusha Tawhiyd ya Allaah (SW) na baraka zake kwetu, pamoja na kutupa mafunzo ya utiifu wa baba yetu Ibrahim kwa Mola wake na kumpwekesha Allaah. Hivyo ibada hii ya kuchinja ni muhimu sana kwa Muislam na inawapasa kuizingatie kwa makini na kuitekeleza inavyopasa kama ilivyoelekezwa bila kufuata nafsi ya kibinadamu . Kuchinja ni kwa ajili ya wanyama waliohalalishwa kuliwa na mwanadamu. Iwe ni wafugwao au wa porini. Kuchinja ni wajibu katika familia ya kila nyumba ya Muislamu, ambayo watu wake wanao uwezo wa kuchinja. Hii kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Taala): Basi Swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako [Al-Kawthar: 2] Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja kondoo wawili walionona, walio na pembe, aliwachinja kwa mikono yake akataja jina la Allaah, akamtukuza kwa kusema Bismillaah Allaahu Akbar) [Al-Bukhaariy na Muslim] Kuna ushahidi kwamba ibada ya kuchinja ina fadhila kubwa kwa sababu ya kauli ya Mtume (Saw), kutoka kwa mama wa waumini Aisha (R.a) kwamba Mtume (Saw) amesema: (Hakuna kitendo cha mwana Adam kilichokuwa ni kipenzi kabisa kwa Allah siku ya kuchinja kama kumwaga damu (kuchinja). Atakuja (huyo mnyama) siku ya Qiyaamah na pembe zake, kucha zake na nywele zake. Damu yake itamwagika mahali fulani Allah anapajua kabla ya kumwagika katika ardhi. Hivyo zipendezesheni nafsi kwayo) [At-Tirmidhiy] Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa, Nini hivi vichinjo? akajibu, (Ni Sunnah ya baba yenu Ibrahim). Wakasema, Nini umuhimu wake kwetu? Akasema, katika kila unywele kuna jema moja, Wakasema, Na su? Akasema, (Katika kila unywele wa su kuna jema moja) [Ahmad na Ibn Maajah] Kujikurubisha Kwa Allaah (Sw) kama anavyosema katika kauli yake, (Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako) [Al-Kawthar: 2] Mwenyezi Mungvu anatueleza katika kuchinja, Nyama zao hazimkii Allaah wala damu zao, lakini unamkia uchaji Allaah wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Allaah kwa alivyokuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema) [Al-Hajj: 37]. Kuihuisha Sunnah mojawapo ya Tawhiyd, wakati Allaah alipompa wahyi Ibrahim (alayhis-salaam) amchinje mwanawe Ismail. Kisha Allaah (Sw) akampa dia ya kondoo, akamchinja badala yake. Allaah (Subhaanahu wa Taala) Anasema: (Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu) [Aswaaffaat: 107] Kwa kisa hiki, hadi leo kuna tukio kubwa la kuchinja katika sikukuu ya Eid el adha, (Eid kubwa). Hapa mahujaji huchinja na Waislmu wengine wenye uwezo nao hulazimika kuchinja mnyama siku ya Eid kwa ajili ya kutunuku kisa hiki cha Ibrahim na mwanaye Ismail. Ni funzo refu kidogo ambalo linahitaji wasaa kulieleza kwa kina. Kutoa shukurani kwa Allaah (Subhaanahu wa Taala) kutujaalia kuwa na wanyama wafugwao kama anavyosema: (Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Allaah; kwa hao mna kheri nyingi. Basi litajeni jina la Allaah juu yao wanaposimama kwa safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru) (Nyama zao hazimfikii Allah wala damu zao, lakini unamkia uchaji Allah wenu. Namna hivi Tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Allah kwa alivyokuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema) [Al-Hajj: 36-37] Anaweza kuchinja siku ya pili ya Iyd au kuchelewesha hadi siku ya mwisho ya Ayyaamut-

Wanaonyonga waendelee na utaratibu wao


Tashriyq (siku za Tashriyq) ambayo ni siku ya kumi na tatu Dhul-Hijjah. ...siku zote za Tashriyq ni siku za kuchinja. [Ahmad] Kumpwekesha Allah: Inapendekezeka kumuelekeza mnyama Qiblah wakati wa kumchinja na kusoma: (Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliyeziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina) [Al-Anaam:79] (Hakika Swalah yangu, na kichinjo changu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allah, Mola wa viumbe vyote) (Hana mshirika Wake. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu)) [Al-Anaam: 162163]. Anapoanza Kuchinja Aseme: BismiLLaah, wa Allaahu Akbar, Ewe Allah hii ni kutoka Kwako na kwa ajili yako. Imesisitizwa kuwa wakati wa kumchinja mnyama, basi kufanyike katika njia iliyo bora zaidi. Mchinjaji ahakikishe amekinoa kisu chake kwa ajili ya kupunguza mateso ya mnyama. Pamoja na taratibu za kimantiki za Kiislamu katika kuchinja, inafahamishwa kwamba kuchinja ndio njia bora ya kuondoa sumu na uchafu kwa mnyama kabla ya kumla. Kibudu ni sumu kubwa kwa afya ya mwanadamu na hili linathibitishwa na wataalam wa afya. Kwa maana hiyo kwa Muislamu kuchinja, hilo ni funzo la kuigwa na lenye kubwa kwa afya ya mwanadamu. Katika Uislamu ni haram kula nyamafu, nyama ya mnyama iliyokatwa mnyama angali hai, nyama ya mnyama asiyeliwa kwa kujibu wa taratibu za Mwenyezi Mungu. Kama wapo watu wanaoona kwamba utaratubu wa Mwenyezi Mungu uliobainishwa tangu enzi za Manabii wake hususan Ibrahim, ni mbovu na wana utaratibu wao unaotokana na matamanio ya kibinadamu, hiyo ni hiari yao. Tu n a s e m a h i v y o k w a maana kwamba, kumeibuka uzushi wa watu kutaka nao kuchinja kwa kuwa Waislamu wamehalalishiwa kuchinja. Hakuna sababu za kimantiki zaidi ya ushindani unaosukumwa na chuki. La muhimu ni kwamba si Waislamu au Wakristo watakaoridhia kula vibudu au nyamafu kwa sababu tu watu fulani nao wanataka kuchinja kama wanavyochinja Waislamu. Kama ni hoja ya nguruwe, utaratibu uliopo wa kuchinja kwa kuwanyuka rungu kichwani uendelee tu na hakuna atayeuliza kwa kuwa hauna kanuni wala mwiko kwa wadau wake.

WALOZI WA CCM !!!

Ukweli wanaucha, ni vyema mkatambuwa, Ni yao wao makucha, chama yanokitobowa, Nanena pasi kucha, hata wao wanajuwa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe. MTWARA kwayo makucha, ni wao wairaruwa, Wangangana kachakacha , GESIYE kuikwapuwa, Wahofuni kuiacha, KANZI hii kwa wazawa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe. Wahaha usiku kucha, chamacho kukiumbuwa, Ya ILANI wayaacha, kwa UFISADI twaliwa, Wamegeuka galacha, kwa umma tothaminiwa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe. Kwa kulifumbata BUCHA, wazidi kukitobowa, Lidhabihilo chachacha !, wanetu WATAHINIWA, Kwa ya UBAGUZI kacha, chamacho wanakiuwa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe. Chahitaji chama KACHA, kwa TIBA bora patiwa, Maradhiye kuyakacha, si suluhu maridhawa, Au LAWAMA kuacha, kwa TABIBU siyo sawa, Walozi wa CCM, ni CCM wenyewe. MBILI ZIRO kumekucha, MOJA TANO mwangojewa, Si mbali kesho kukicha, kesho kutwa majaliwa, Kwa NGOMA yenu chakacha !, kwayo MTAHUKUMIWA, Katu hakuna WALOZI, wa CHAMA zaidi yenu. ABUU NYAMKOMOGI

Nyerere hakukia kiwango cha kuitwa Baba wa Taifa


Na Dr. Noordin Jella SYSTEM imewatega Wapinzani kwa muda mrefu na Wapinzani wametegeka na wameshindwa kuugundua mtego huu! Huu ni mtego wa Kiitelejensia kwamba Ukimkubali Nyerere umeikubali Nembo ya System inayotawala, na kama umeikubali System inayotawala ina maana Unakikubali chama cha CCM ambacho ndicho kinachotayarisha sera za System! Hivyo kumkubali N y e re re K i n a f i k i l a k i n i huipendi CCM pia ni Unaki mtupu! Na ndiyo maana ukishamkubali Nyerere tu, basi System inakuwa haina Ugomvi mkubwa sana na wewe kwa vile wanajua kwamba huyu ni mwenzetu, ila tu tunatofautiana kidogo katika Utekelezaji. System inajua kwamba kama Unamkubali Nyerere automatically unaikubali System yake! Hata kama upo ndani ya kambi ya upinzani lakini hawana hofu sana na wewe kwa vile wanajua kwamba huyu ni NJAA tu inamsumbua, lakini tunaweza kuzungumza naye hata kama akashinda na kuingia Ikulu. Isipokuwa ukishaonyesha kwamba humtaki na humkubali Nyerere kabisa, basi wewe ni adui mkubwa wa System, na watajitahidi kabla hata hujaingia kwenye Big Politics wakuangamize huko huko chini ili usifike huko juu Umma ukakufahamu kwamba wewe ndiye mkombozi wao, wanajua fika kwamba hawataweza kuakiana na wewe kwa lolote, bali suluhisho ni kuhakikisha kwamba wanakuangamiza moja kwa moja. Na hii ni dalili tosha ya kuonyesha kwamba Wapinzani bado hawapo tayari kuchukuwa madaraka na kuleta mabadiliko ya kweli. Hata kama watachukuwa madaraka lakini hawawezi kuitafuta ile njia waliyopita wenzetu wa nchi za South East Asia hadi kuka hapa walipo leo hii! Au hawawezi kuitafuta njia waliyopita nchi za Baltic (Estonia, Lithulian, na Latvia), hizi zilikuwa nchi ndani ya jumuiya ya nchi zilizokuwa zikiitwa Soviet Union (Urusi ya zamani), nchi hizi zilikuwa nchi za kikomunist na zote zilikuwa chini ya kile kitengo hatari cha KGB. Mwaka 1991 Ukomunist ulipokufa na utawala wa Soviet Union kusambaratika, nchi hizi zote kwa pamoja na kwa wakati mmoja zilitangaza kwamba Ukomunist na KGB ilikuwa Janga la Kitaifa na waliupiga marufuku Ukomunist na KGB katika nchi hizo na kuweka wazi kwamba watu wote waliowahi kuwa wanachama wa chama cha Kikomunist na wale wote waliowahi kufanya kazi katika kitengo cha ugandamizaji cha KGB ni marufuku kufanya kazi au kuajiriwa katika idara yoyote ya serikali na umma kwa ujumla. Wakomunist na wanakitengo wa KGB waliruhusiwa tu kufanya biashara au kuajiriwa katika makampuni ya watu binafsi. Walifanya hivyo makusudi wakijua fika kwamba Wakomunist na Kitengo chao cha Usalama wa Taifa ni wataalamu wa kuunda mitandao ya uhalifu

13

MAKALA

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba ya umma?-5


kwenye mashamba ya Wakoloni na ujenzi wa Reli za kati na Kaskazini wakitumia lugha ya Kiswahili. M w a k a 1 9 6 4 Ta n z a n i a ilikuwa imeendelea zaidi kuliko nchi nyingi za Kusini mwa Asia (South Korea, Malaysia; Thailand; Hong Kong; Taiwan; Singapore; na Philippines). Baada ya miaka 52 ya uhuru ambayo ndani yake kukiwa na miaka 23 ya utawala wa Nyerere na miaka 27 ya utawala wa system yake (Nyerere) ambayo tumeisherehekea hapa majuzi kwa mbwembwe na mabango y a n a y o s e m a Tu m e w e z a , Tumethubutu na Tunasonga Mbele! Nilipoliona hilo bango nilijiuliza kimoyo moyo: Tumeweza lipi? Tumethubutu nini? Tunasonga mbele wapi? Leo hii South Korea ni moja kati ya nchi kumi ambazo zinazouza bidhaa zilizokamilika duniani (nished products), kwa mwaka wanauza bidhaa zenye thamani ya US $ 360 Billion; Wanatengeza kila kitu kuanzia pasi ya umeme, TV, Video, Music system, friji, magari, train, tractors, meli, ndege n.k; South Korea sasa hivi wanawekeza kwenye nchi zote za Magharibi (Potential Investor). Malaysia, Thailand, Hong Kong, Taiwan, Singapore na Philippines wote hawa wapo sambamba kimaendeleo na South Korea; Mwaka 1967 Nyerere akatangaza Azimio la Arusha na akataisha mashamba, mabenki, viwanda, hospitali, na nyumba za watu binafsi na kuwa mali ya umma. Hapa ndipo Nyerere alipoanza kuzama kwenye tope, kwa vile aliharakisha kutaisha vitu hivi wakati alikuwa hana wataalam wazawa wa kusimamia miradi hiyo, na pia alikuwa hana pesa na tekinolojia za kuendeleza na kuongeza miradi mingine. Hivyo akawa hawezi kwenda mbele bali akaanza kudidimia hadi mwishowe akazama ndani ya tope moja kwa moja, kwa vile wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakasitisha uwekezaji na wengine wakahamia nchi zingine. Nyerere alipokuwa anawanyanganya mashamba Wazungu alijua fika kwamba wao ndiyo wanaopanga bei ya bidhaa zote kwenye soko la dunia, hivyo baada ya mashamba yao kutaishwa nao mara moja wakaanza kuiwekea Tanzania vikwazo vya chini chini ikiwa ni pamoja na kushusha bei ya mazao au bidhaa zilizotoka Tanzania kila mwaka. Kitendo cha kushushwa bei kwa mazao na bidhaa zitokazo Tanzania kulidhoofisha uzalishaji kwa kiwango kikubwa, na hata mazao mengine yakasitishwa kulimwa. Kenya ilipopata uhuru wake haikutaka kubadili siasa za ubepari pamoja na kwamba Mzee Jomo Kenyatta alisoma Soviet Union ambayo ilikuwa nchi ya kikomunist. Nyerere alisoma Uingereza nchi ya kibepari lakini aliamua kufuata siasa za kikomunisti. Naamini kama Nyerere angeliuliza bunge juu ya kufuata siasa za kikomunist sidhani kama bunge lingeridhia. Baada ya miaka 52 ya uhuru, Kenya imekuwa

wa kupangwa (mafia), hivyo waliona dawa ni kuwanyima mamlaka; na leo hii baada ya miaka 22 ya kuanguka kwa himaya ya Kikomunist duniani, ukika katika nchi hizi za Baltic huwezi kuzitofautisha na zile nchi za Scandanavian (Sweden, Finland, Denmark, Norway) kimaisha na kila kitu. Zimetumia muda mfupi sana kuondoa harufu ya Ukomunist na kitengo chake cha KGB katika nchi zao. Katika nchi hizi neno KGB na Ukomunist ni moja kati ya MATUSI mabaya na makubwa sana ambayo hakuna mtu yeyote ambaye angependa aitwe aidha KGB au Mkomunist! Hapa kwetu Wanavitengo wote wanajisikia sana na kujiona wao ni watu special, wateule na hata wanapotembea hutembea bega moja juu na lingine liko chini. Mimi natofautiana na watu wengi sana kimawazo kwenye suala la Nyerere kuitwa Baba wa Taifa. Mimi binafsi kama Mtanzania na kama Raia wa nchi hii nasema kwamba Nyerere hakukia kiwango cha kuitwa Baba wa Taifa kwa mambo mengi yafuatayo: Mwaka 1961 Nyerere alikabidhiwa nchi hii toka kwa Wakoloni Waingereza ikiwa ni moja kati ya nchi zilizokuwa TAJIRI sana duniani: Nchi ya kwanza duniani kwa uzalishaji wa zao la Katani; Nchi ya pili duniani kwa uzalishaji Kahawa baada ya Brazil; Nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa zao la Korosho; Nchi ya tano duniani kwa uzalishaji wa Tumbaku duniani; Nchi ya nane duniani kwa uzalishaji wa Pamba duniani; Nchi ya tano duniani kwa uzalishaji wa Karanga duniani; Nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa Asali na Nta duniani; Nchi ya pili duniani baada ya Ghana kwa uzalishaji wa zao la Michikichi ambalo hutumiwa kutengeneza mafuta ya Mawese; Nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa zao la Iliki; Nchi ya nne duniani kwa uzalishaji wa zao la Muhogo; Nchi ya kumi duniani kwa uzalishaji wa zao la Mahindi na Maharage duniani; Nchi ya sita duniani kwa uzalishaji wa zao la Tangawizi; Nchi yenye Mifugo mingi katika bara la Afrika; Nchi ya kwanza duniani kwa kuwa Wanyama Pori wengi na vivutio vingi vya utalii; Nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa zao la chai; Nchi ambayo yenye mlima mrefu kuliko yote Afrika (mlima Kilimanjaro); Nchi inayozungukwa na Maziwa makubwa matatu katika bara la Afrika (Viktoria, Tanganyika; na Nyasa); Tanganyika ni nchi yenye mito na mabonde mengi yenye rutuba na zaidi ya asilimia tisini na tano ya ardhi ya Tanganyika inafaa kwa kilimo; Tanganyika ina mito mingi na vyanzo vya maji vingi; Watanganyika ni watu wasiojua kudai haki zao kwa kutumia Migomo, Maandamano wala Fujo; Pamoja na yote hayo Watanganyika walikuwa tayari wanaongea Lugha moja ambayo ni Kiswahili, Watanganyika walikuwa walishaungana tayari kwa kubadilishana bidhaa na kufanya kazi kwa pamoja

nchi yenye uchumi mkubwa Afrika Masharki na pia nchi ya viwanda licha ya kwamba ni nchi ndogo kijiografia na pia ina raia wachache kuliko Tanzania, na pia ina eneo dogo lenye rutuba kwa ajili ya kilimo ukilinganisha na Tanzania. Miaka ya sabini Nyerere alikuja na Maneno mazuri sana Siasa ni Kilimo, Kilimo cha kufa na kupona na Kilimo ni Utu wa Mgongo wa Maendeleo. Bila ubishi haya yalikuwa maneno matamu na maneno ambayo yalikuwa suluhisho la umasikini wa Watanzania, lakini kwa bahati mbaya sana kama kawaida ya Nyerere haya yalikuwa ni maneno ya majukwaani ambayo ki ukweli yalikuwa hayana mpango mkakati wowote wa kuyafikisha huko yalikokuwa yamekusudiwa. Asilimia 90% ya Watanzania wanategemea kipato chao kwenye kilimo hivyo ukisema kilimo ni uti wa mgongo au siasa ni kilimo unakuwa umedhamiria kuwakomboa Watanzania, lakini kwa bahati mbaya sana miaka 23 ya Nyerere kuwepo madarakani aliondoka bila kuwaachia Watanzania kumbukumbu ya kilimo alichokuwa anakitangaza majukwaani! Baada ya miaka 52 Rais wa awamu ya nne amekuja na kauli mbiu isemayo Kilimo Kwanza ambayo kwa ukweli ni kama vile nchi ndiyo imepata uhuru jana! Sasa kama Nyerere alianzisha na kuendeleza kilimo, leo hii Kikwete angesema Kilimo Kwanza? Nyerere alikuwa mtu wa maneno mengi ya majukwaani yasiyokuwa na vitendo. Na warithi wake wote watatu wameendelea na mtindo ule ule wa matamko ya majukwaani bila ya vitendo na nidhamu. Majuzi tunasherehekea miaka 50 ya uhuru tunajigamba eti tumeweza, kama tumeshindwa kilimo tutaweza nini? Mwaka 1967 Nyerere alipotangaza azimio la Arusha, na kutaifisha mashamba yote Mkonge, Kahawa, Chai, viwanda, mashirika na mabenki yote, na nyumba za Wahindi. Akaanzisha vijiji vya ujamaa na mashamba ya kijamaa; watu wakahamishwa kwa nguvu kwa kubomolewa nyumba zao na kuhamishiwa porini ambapo hapakuwa na maandalizi yoyote, wengine waliliwa na Simba na kupoteza mali zao bila ya kudiwa! Leo hii baada ya miaka 52 hakuna hata kumbukumbu yoyote ya kijiji cha Ujamaa ambacho Nyerere angerudi leo hii angeweza kujivunia. Vijiji vya Ujamaa ilikuwa ni tamko tu la majukwaani. Leo hii hakuna hata kijiji kimoja ambacho kipo ambacho Nyerere angeweza kujivunia kwamba angalieni mfano wa kijiji changu hiki kilivyojitosheleza! Mashamba ya Mkonge, Kahawa, Chai, Korosho mengi yamekufa au uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa, na mashamba haya yameshabinasishwa kwa watu binafsi. Bank ya taifa (NBC) imeuzwa katika mikataba ya kutatanisha; Nyumba walizonyanganywa Wahindi wameanza kuzirudishiwa katika makubaliano ya Kisadi;

Viwanda na mashirika yote vimebinasishwa kwa taratibu zile zile za Kisadi. Miaka ya Sabini Tanzania ilikuwa na uhusiano wa karibu sana na nchi ya SWEDEN kwa vile nchi hiyo ilikuwa ikijenga siasa za Ujamaa lakini Ujamaa Endelevu siyo kama Ujamaa wa Ujima aliokuwa anajenga Nyerere. Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakati huo Olfe Palme alimuonya Nyerere kwamba huwezi kujenga Ujamaa wakati watu wako wanaishi maisha duni, ili ufanikiwe kujenga Ujamaa Endelevu unatakiwa uwajengee raia wako nyumba nzuri za kisasa; Ujamaa unaanzia nyumbani na Maendeleo yanaletwa na kuwa na Nyumba nzuri alisema Olfe Palme. Palme aliipa Tanzania Mkopo wa Masharti nafuu ili kila raia mwenye umri zaidi ya miaka 18 ajengewe nyumba nzuri ya kisasa yenye thamani ya Tsh. 40,000/= za wakati huo na mfano wa nyumba waliopendekeza serikali ya SWEDEN ni zile nyumba za mapaa mawili ambazo zimejengwa maeneo ya Sinza Dar es Salaam. Baada ya kupewa mkopo huo Nyerere na utawala wake wakasema siyo Watanzania wote wanaohitaji nyumba za kisasa, bali wakaamua kufungua Bank ya Nyumba ya Taifa (THB) wakidai eti wale wenaotaka kuwa na nyumba ya kisasa waende Bank wakakope wajenge nyumba. Bank ikafunguliwa wajanja wakaanza kukopa bila ya kulipa kwa vile mfumo wa Bank ulikuwa duni: Hivyo wakopaji walikopa na kesho walirudi wakachukuwa mafaili yao na kuyachoma moto baada ya kumpa Messenger (Mtunza mafaili) pesa ya chai, hivyo ikawa hakuna kumbukumbu zozote, na mwisho wa siku THB ikafilisika. Tanzania ikabaki na DENI ambalo leo hii kila Mtanzania analilipa bila ya kujali alikopa au hakukopa! Bila ya kujali ana nyumba ya ghorofa huko Mbezi Beach au ana Tembe huko Kibaigwa - Dodoma! Siku moja Nyerere aliwahi kulitembelea jiji la Dar es Salaam kwa Helikopta na alipokuwa anapita juu ya maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni, na Masaki, alipoona maghorofa ya kutisha yamejipanga yeye mwenyewe alikiri kwa kusema Haya Ndiyo Makaburi ya THB kwa vile wenye maghorofa hayo si wengine bali ni vijana wake na si wafanyibiashara bali wafanyikazi wa serikali na wamejenga bila ya mikopo ya bank! Leo hii tunasema Kama Angelikuwepo Nyerere, mbona alikuwepo na yalitokea! Katiba mpya iondoe matabaka katika jamii, kama pesa hizi za THB zingekuwa zimekopwa na wakulima toka vijijini serikali ingehakikisha inawabana mpaka wazilipe na makelele yangekuwa mengi, lakini kwa vile pesa za THB zilikopwa na tabaka la watawala wanaotunga na kusimamia sheria, basi pesa za umma zimepotea! (Makala hii imeandikwa na Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Ec onomics) Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU Dar, Universities. Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political Analyst Email: norjella@yahoo.com Mobile: +255 782 000 131)

Mwiba uingiapo ndipo utokapo


ya kubaguana kutukanana, kuchomeana nyumba za Ibada na kupigana. Natumai muandishi ni vyema akiangalia Historia ya mambo ya dini katika Biblia na mwenendo wa Wakoloni na sera zao walizoziweka tokea huko nyuma na kuwarithisha viongozi waliowateua kushika nafasi za Uonogzi baada ya Uhuru. Lakini hebu natuangalie historia inasema nini katika kujihusisha kwa Kanisa ndani ya Serikali? Pili kwa nini Serikali za Kikoloni zilihimiza kuwepo mashirikiano na Makanisa? Ukiangalia historia ya mambo mawili hayo yaani Serikali na Kanisa na Kanisa na Serikali, utaona tangu nyakati za zamani, Wa k r i s h o w a m e j a r i b u kustawisha maelewano juu ya mamlaka za kilimwengu (Serikali). Wakati Yesu Kristo alipohukumiwa na kushwa na Serikali ya Roma, wanafunzi walijipatanisha kwa Serikali ya Roma, hivyo patio la uhusiano wao pamoja na mamlaka ya Roma laandaa miongozo kwa Wakristo hadi leo. Petro amejipatanisha na Serikali ya Kiroma kwa kuweka sheria hii:Tiini kila kiamrishwacho na watu, kwa ajili ya Bwana, ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa, ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza watende mabaya na kuwasifu watenda mema. (Petro 2:13-14) Paulo naye amejipatanisha na Serikali kwa kuwaambia Wakristo wanaoishi Roma: Kila mtu na atii mamlaka (Serikali) iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo (Warumi 13:1) Paulo anazidi kujipatanisha na Serikali anasema:Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. (Waroma 12:18) The Encyclopedia of Religion yatangaza hivi: Katika Karne ya tatu za kwanza A.D, Kanisa la Kikristo lilitengwa sana na jamii rasmi ya Kiroma.. Hata hivyo, Viongozi wa Kikristo walifundisha utii kwa sheria ya Kiroma na uaminifu kwa mfalme. Vile vile katika utawala wa mfalme Nero. Petro aliwaandikia hivi Wakristo waliokuwa wakiishi katika sehemu mbali mbali za miliki ya Roma: Heshimuni watu wa namna zote.kuweni na heshima kwa mfalme. (1 Petro 2:17) Paulo alizidi kujipatanisha na Serikali pale alipowashauri Wakristo waliokuwa wakiishi katika jiji la miliki ya Roma: Wapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru, astahilie hofu, hofu. (Warumi, 13:7) Paulo anazidi kujijenga na kujichimbia kwenye Serikali anasema: Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi na shukuraniKwa ajili ya Wafalme na wote wenye mamlaka. (1 Timotheo 2:12) Paulo aliposhitakiwa (MDO 25:1-12) alidai hataki kuhukumiwa na (Liwali) bali anasema:-Mimi ninasimama hapo mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari (Nero) ndipo panipasapo kuhukumiwa. (Mdot 5:10) Kuridhiana na Serikali: Kadiri wakati ulivyopita msimamo uliochukuliwa na wafuasi wa Yesu wa Karne ya kwanza kuhusiana na Serikali ulidhooka pole pole. Uasi, Imani iliotabiriwa na Yesu na Mitume ulistawi katika Karne ya pili na tatu (w.k). Ukristo wenye kuasi imani uliridhiana na ulimwengu wa Roma, ukatwaa sherehe za kipagani na falsafa zao na kukubali si tu utumishi wa Serikali bali pia utumishi wa jeshi. Kwa raia wa kawaida, wajibu wao wa kwanza ulikua upi? Je, walipaswa kufuata wale waliodai kuwakilisha Serikali au walipaswa kumtii Mungu, asemaye usiue mpende jirani yako kama nafsi yako? (Warumi 13:9). Ta n g u w a k a t i w a Konstantino magumu mengi yakapotea mzozo kati ya Wa k r i s t o n a Wa p a g a n i ukapoa na vyeo vyote vya Serikali vilikuwa wazi kwa Wakristo Kuelekea mwisho wa karne ya nne (w.k) aina hiyo ya Ukristo ulioghushiwa na yenye kuridhiana ikaja kuwa dini ya miliki ya Roma. Katika historia yote, Jumuiya ya Wakristo, Othodoksi, Protestanti, imeendelea kuridhiana na Serikali ikijihusisha sana na siasa na kuunga mkono vita vyao. Yesu hakukana kwamba, falme za ulimwengu zilikuwa za shetani, tena akamwita Shetani Mkuu wa ulimwengu huu (Yoh 12:3116:11) Makanisa yote ni mali ya nchi za Magharibi. Kwa maana hiyo penye Serikali pana Kanisa na penye Kanisa pana Serikali. Tumeona katika mkutano wa wakoloni wa kugawana bara la Afrika mwaka 1884, Ukristo ulipewa hadhi maalumu. Mwandishi Hansen H.B katika kitabu chake Mission, Church and state in a Colonial Setting, Uganda 1890-1925, London. 1984 uk 26, anaeleza kuwa Ibara ya 6 ya makubaliano ya Berlin pia ilisema dola zote za kikoloni zitoe hifadhi maalumu kwa Makanisa. Bwana Roland Oliver ameandika kwamba:Huko Ulaya Wazungu walihofia kuwa Afrika Mashariki ya Kiislamu itakuwa ni Afrika Mashariki dhidi ya Wazungu (The Missionary Factor in East African London 1952 uk.206). Sir H. Johston alisema: Haitakuwa kwa maslahi ya Serikali ya Uingereza iwapo Uislamu utapata wafuasi wengi kwani kwa asili yao Waislamu ni wagumu kuwatawala na katika nyoyo zao wanapinga utawala wa dola ya Kikristo (Tza. Barua ya Johston ya 3-12-1900). Na akawaonya machifu wafanye kila njia kuupiga vita Uislamu. Mkakati wa wakoloni ni kuzibana juhudi za Waislamu za kueneza Uislamu na kuwabana katika fursa za elimu. Ama kubanwa kwa Waislamu wa Tanganyika kielimu tangu zama hizo hadi sasa ni ule utati uliofanywa na Dr. Malekela wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umeonesha kuwa katika kila watoto 100 wanaosoma Sekondari 78 ni Wakristo n a 2 2 n i Wa p a g a n i n a Waislamu. Wa k r i s t o w a l i a m u a kuanzisha mradi mkubwa sana wa kuwaritadisha Waislamu wa Afrika uitwao Islam in Africa Project wenye makao yake makuu huko Kenya. Ulianzishwa na Rev. James Jitehie ambaye alikuwa ni mshauri wa Baraza la Kikristo la Kenya (The National Christian Council of Kenya). Mwaka 1971 Rev. Tom Beetham akawa ndiye Mkurugenzi wa mradi huu. Miongoni mwa program zinazoratibiwa na Islam in Africa Project ni pamoja na ile semina iliyofanyika Nairobi, Kenya September 23, 1989 juu kukabiliana na Uislamu, kuandaa November Crusades katika nchi mbali mbali za Afrika na kadhalika. Pili miongoni mwa mbinu zao ni kuingia mashamba vijiji kujenga Mashule na Hospitali. Barnabas, Madhali Wakoloni walitengeneza vita na Waislamu basi ni jambo la uhakika, kwamba kwashirikisha Waislamu kuchukua nafasi za juu Serikalini ni mwiko. Ndio ukaona waliagizwa machifu waupige vita Uislamu. Wakoloni waliunda tabaka la wateule wa kienyeji (Machifu) wakachagua vijana wao walionekana wana muelekeo wa kuiga mambo, nao wakajazwa kasumba za utamaduni wa kimagharibi pamoja kufanywa wawe watu wanaoweza kukariri kikasuku mambo yanayowafurahisha walowezi hao. Vijana hao wakayapokea maneno hayo na kuyajaza vinywani mwao, wakapelekwa katika nchi zao hao mabeberu na huko wakakaa kwa muda , baadaye walirejeshwa nyumbani tayari wameshajazwa kasumba. Wengi wao walikuwa ni mamluki tokea mwanzo hadi mwisho tena ni wanaki na ndumila kuwili. Hawa ndio walikuwa wametayarishwa kuwa ni wapokezi wa Uhuru wa Nchi zao. Kisirisiri Nyerere alikuwa akipewa maandalizi ili aje kusimika utawala wa kikatoliki Tanganyika. Mashirika ya Kikristo yalimsomesha na kumuandaa ili aje kutawala. Safari yake Umoja wa Mataifa mwaka 1956 ambayo kwa kiwango kikubwa alisaidiwa na shirika la kikatoliki la Maryknoll Fathers. Serikali ya Kikoloni ilipokea ripoti kutoka katika shirika la Maryknoll ikieleza kwamba shirika limekubali kumlipia Nyerere tiketi ya kwenda na kurudi kutoka England kwenda New York kwa vile ni kiongozi Mkatoliki kutoka wilaya ya Musoma, tumeonelea ni vizuri apate fursa kuona hali ya Ukatoliki huko Amerika nap engine kupata nafasi za masomo zaidi kwa Watanganyika. Alifika mjini New York November 13,1956 kiasi cha majuma saba hivi. Wakati ule huko New York aliishi katika jumba la Leo House ambalo lilisimamiwa na Masista wa Mt. Agnes. Kisha alisafiri mpaka Washington ambako aliishi na White Fathers, halafu Chicago na Boston ambako alikaa na Maryknoll Fathers. Huko Washington katoka Chuo Kikuu cha John Hopkins alitoa mhadhara, nako Chicago

14

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Na Ibrahim Mohammed Hussein NIMEBAHATIKA kulisoma gazeti la Fahamu la January 8-14, 2013, uk. 9 makala ilioandikwa na B a r n a b a s M a ro y e n y e kubeba kichwa kisemacho: Utulivu wa Watanzania umeingia dosari. Ndani ya makala hiyo alizungumzia kutoweka kwa amani yetu hapa Tanzania ambayo alitaka idumishwe. Vile vile alizungumzia nyakati za nyuma hapa nchini watu wa dini mbali mbali waliishi kwa upendo na kusaidiana. Mwandishi alizungumia mihadhara ya kashfa za kidini inayoendelea hapa nchini. Mwandishi akadai kwamba kiwango kikubwa cha mihadhara ilikua ikifanywa na Waislamu zaidi. Anasema kashfa zilipozidi na Wakristo nao wakaunda kikundi kilichojiita Biblia ni Jibu na kwamba kundi hili lilikua likijibu mapigo. Barnabas, anasema Serikali ilishindwa kuikabili hali hiyo. Muandishi akakumbushia vurugu zilizotokea za kuvunja na kuchoma maduka ya Nguruwe jijini Dar es Salaam. Mwandishi akajaribu kuonesha kwamba hawakuwa na ubaguzi katika mashule hasa hapa Zanzibar na akaitaja shule ya St. Monica ya Kikwajuni na Kiungani High School. Mwandishi amezizungumzia vurugu zilizosababisha baa 12 na Makanisa 25 kuchomwa moto bila ya kuziainisha baa hizo na Makanisa hayo. Barnabas, amezungumzia habari ya kutiwa tindi kali Sheikh Soraga na vile vile upigwaji wa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda huko Zanzibar. Muandishi alinukuu aya za Qur-ani na Biblia ili kutilia mkazo kwa yale aliyoyasema. Mwishowe muandishi Barnabas Maro alitoa ombi kwa wahusika wa dini zote ziwatanabahishe waumini wao jinsi ya kumrudia Mwenyezi Mungu. Waelezwe hatari

15
kuwa haya ni maoni ya Dr. Shein kama ambavyo wengine wametoa maoni yao wakisema kuwa wanataka kuona nchi huru ya Zanzibar ikiwa na Dola yake kamili kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ikiwemo serikali ya Tanganyika itakayokaa na Zanzibar na kuangalia namna bora ya kushirikiana. Hata hivyo nadhani kuwa mahali pekee pa kutolea maoni yake ni kwa Tume ya Jaji Warioba, sio katika mfumo huu wa kuhutubia wananchi na kutoa kauli za ki-Rais na maelekezo. Lakini jambo lingine la kuzingatia hapa ni kuwa tatizo la msingi kwa Wazanzibari sio kuwepo au kutokuwepo kwa hati ya muungano. Tatizo ni mfumo wa muungano. Hoja ni aina ya muungano. Wanachotaka wananchi sio kuonyeshwa hati ya muungano. Wanachotaka ni Zanzibar yao na Dola yao. Wanachotaka kuona ni muungano wenye
Inatoka Uk. 11

Tusipotoshe agenda: Hoja ni Zanzibar huru


kuitendea haki Zanzibar sio huu wa kuidunisha na kuifuta. Kwa hiyo hata kama Dr. Shein anayo hati ya muungano, iwe Vuga au Chokocho, bado hajaondoa hoja za Wazanzibari. Baadhi ya watu wanaofuatilia suala hili la muungano, wanasema

Makala/Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

United Republic of Tanzania


From pg. 11 Tanganyika and Zanzibar is now a single Member of the United Nations bound by the provisions of the Charter. This action is undertaken without prejudice to and pending such action as other organs of the United Nations may take on the basis of the notication of the establishment of the United Republic o f Ta n g a n y i k a a n d Zanzibar. No objection was raised in this regard in any of the organs concerned. In a communication addressed to the Secretary-General on 2 November 1964, the Permanent Mission of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar informed him that the United Republic of Tanganika and Zanzibar shall, with immediate effect, be known as the United Republic of Tanzania. S u bsequently, the Government of the

kuwa kilichopo Umoja wa Mataifa (UN), New York, sio hati ya muungano, bali taarifa ambayo ilitolewa na Tanganyika kupitia kwa

Wizara ya Mambo ya Nje kwamba Zanzibar na Tanganyika zimeungana kufanya Tanzania. Ni kwa taarifa hiyo hiyo inaweza kusemwa kuwa ni Wizara ya Mambo ya Nje , ndiyo iliyopeleka ujumbe UN na kuwaambia kama Baraza la Mapinduzi limeridhia articles of the union.

Kizungumkuti cha muungano bila hati


Inatoka Uk. 7 muungano: Tanzania ina mali za serikali ya Tanzania (Government Assets) yaani mali zinazomilikiwa na serikali ya muungano, kama vile osi na majengo yote ya balozi zote za Tanzania nchi za nje; Mali, majengo na vifaa vyote vinavyomilikiwa na wizara ya ulinzi; Mali, majengo yote yanayomilikiwa na Wizara ya Fedha ikiwemo Benk Kuu; Mali, majengo yote yanayomilikiwa na Wizara ya Elimu ya Juu. Nimezitaja wizara nne ambazo hasa ndizo zinazoingia kwenye swala la muungano. Sasa inapotokea nchi mbili zimetengana, inabidi mali zote nilizozitaja hapo juu zitathiminiwe zijulikane
thamani yake, ni kiasi gani? Ikijulikana thamani ya mali yote ya umma, ilinganishwe na madeni ya nchi iliyokuwa inadaiwa; na baada ya hapo yanaweza kufanyika mambo mawili: aidha mali hizo ziuzwe ili ipatikane pesa ya kulipa madeni au mali hizo zimilikiwe na moja ya serikali (Tanganyika au Zanzibar) lakini ikubalike kwamba anayebakia na mali hizo arithi madeni yote ya Tanzania. Lakini pia itategemea ukubwa wa madeni na thamani halisi ya mali ya umma (Government Assets). Inawezekana deni likawa siyo kubwa ukilinganisha na mali za umma zilivyo, hivyo ikitokea hali kama hiyo, nchi inayorithi mali zote za umma itahitajika imlipe dia nchi ambayo imejitoa kwenye muungano. Muungano ukivunjika mazungumzo ya kugawana mali na madeni ya nchi, hayawezi kufanyika papo kwa hapo kwa vile Tanganyika haina serikali hivyo itabidi Zanzibar wavute subiri hadi Tanganyika iunde katiba na serikali yake ndipo nchi hizi mbili zikae zijadili mali na

the United Nations, to the principal organs of the United Nations and to the subsidiary organs of the United Nations to which Tanganyika and Zanzibar had been appointed, and to the specialized agencies of the United Nations and the International Atomic Energy Agency, the Secretary-General stated that he is taking action, within the limits of his administrative responsibilities, to give effect to the declaration in the attached note the United Republic of

United Republic of Tanzania confirmed to the Secretary-General that the United Republic of Tanzania continues to be bound by multilateral treaties in respect of which the Secretary-General acts as depositary and which had been signed, ratied or acceded to on behalf of Tanganyika.

Inapenda kutoa shukran zake za Dhati kwa mahujaji wote waliosari na Ahlul-daawa. Pia inatangaza kua imeandaa safari ya Umra Mfungo wa Saba ni sawa na machi 11 2013 kwa Gharama ya Dola 1450 tu. Inaendelea kuandikisha mahujaji kwa Mwaka 2013. Wale watakao jiandikisha na kufanya malipo mapema watapata punguzo maalumu la bei. Usisahau Ahlu Daawa Hajj kwa Bei nafuu na huduma bora. Kwa mawsiliano piga simu zifuatazo. Dar es salaam: 0773 724444, 0715 786101 na kwa Zanzibar 0777 417736, 0777484982.

AHLU-DAAWA HAJJ

madeni yagawanywe vipi? Pia Muungano ukivunjika kila nchi Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na serikali yake, na wizara zake kulingana na umuhimu wa wizara hizo, pia kila nchi itakuwa na Benk Kuu yake na pesa zake. Bila kusahau jambo muhimu kila nchi itakuwa na Jeshi Lake. Kuhusu mgawanyo wa kisiasa ni kwamba Zanzibar na Tanganyika itabidi ziwe dola na ziwe na uwakilishi wake moja kwa moja kwenye Umoja wa Mataifa, na osi zake za ubalozi nchi za nje, hii itazingatia hali ya uchumi na umuhimu wa balozi hizo kwa kuzingatia vigezo muhimu vya kisiasa na kiuchumi. Pia kutakuwa na vyama vya kisiasa kulingana na mfumo utakaoamuliwa na wananchi wa kila upande; kama kutakuwa na uendelezo wa vyama vingi au mfumo wa vyama viwili tu, au mfumo mwingine, yote hayo yatategemea na wananchi wenyewe.

16

AN-NUUR
16

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8 - 14, 2013

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 8- 14, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

AN-NUUR

Waislam kwenda kwa DPP kuhoji dhamana ya Ponda


Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU Jijini Dar es Salaam, wameazimia kuka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Dk. Elliezer Feleshi wiki ijayo, kutaka kujua sababu ya kuzuia dhamana ya Sheikh Ponda Issa Ponda. Akitangaza maazimio hayo mbele ya mamia ya Waislamu Jumapili ya wiki iliyopita katika viwanja vya Pumba, Temeke Jijini Dar es salaam, Sheikh Kondo Juma Bungo, alisema kama ni subira sasa inatosha. Kama ni subira sasa inatosha, wiki ijayo ni siku ya kesi ya Sheikh Ponda, ikiwa hawatopewa dhamana, Mkurugenzi wa Mashitaka DPP, ajiandae, Waislamu wote tutaelekea katika osi zake kwa njia ya maandamano. Alisema Sheikh Kondo. Waislamu hao kama vile walikuwa wakisubiri kauli hiyo, waliripuka kwa mvumo wa Takbir huku wengine wakiitikia Allahu Akbar, ambapo Kondo, aliendelea kutoa muongozo kwamba, mara baada ya ibada ya swala ya Ijumaa, wasisubiri kutangaziwa na Maimam kuwa maandamano yapo au hayapo. Aliwataka Waislamu kuondoka na kauli hiyo kuwa safari ya kuelekea kwa DPP, itabaki hivyo na wategemee kuibuka kwa propaganda za kutaka kuvuruga maazimio hayo. Akinukuu vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, juu ya haki ya dhamana kwa watuhumiwa Kondo alibainisha kwamba Waislamu hawaingilii

SHEIKH Ponda Issa Ponda akiwa na pingu mkononi (katikati) katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Uhuru wa Mahakama, kwa sababu dhamana yake haijazuiwa na Mahakama, bali imezuiwa na DPP, kinyume na Katiba ya nchi. Kondo, alisema, hali hii inasababisha mawakili wa Sheikh Ponda kushindwa kutoa hoja za kuomba dhamana kwa kuwa imezuiwa na DPP, ni suala ambalo lipo nje ya Hakimu kisheria. Miezi minne, si ndio tumeonyesha uadilifu na subira, ili sheria ifuate mkondo wake, hao wanasiasa wenyewe wamepuuzwa hadi hivi sasa, leo Masheikh wetu wana miezi minne mahabusu, hakuna sababu za msingi za kuzuia dhamana, wanatutaka nini Waislamu huku nje? Alisema na kuhoji. Sheikh Bungo alihoji, ni vipi DPP afunge dhamana, kwa kesi ambayo ni ya madai ya ardhi, lakini (DPP) anadai kwamba anafunga dhamana hiyo kwa sababu ya usalama wa taifa? Waislamu tunahoji maswali tokea DPP azuiwe dhamana hiyo, kwamba usalama wa Taifa katika kesi ya kiwanja umeingiaje? Na hili ni moja ya kielelezo cha dhulma, au pale Changombe palikuwa pajengwe Ikulu? alihoji Kondo. Alisema walipokamatwa Masheikh, kule Zanzibar kisha na hapa Dar es Salaam, waliiambia Serikali kwamba Waislamu kwao kukamatwa sio tatizo lakini haki pamoja na uadili)fu dhidi ya Masheikh wao vichukue nafasi na si uonevu na dhulma. Kama nchi ipo chini ya utwala wa sheria, sheria ifuate mkondo wake. Sisi leo tunashangaa, toka kukamatwa Masheikh, tunaingia mwezi wa nne sasa. Kisheria kuna watu wanahukumiwa miezi mitatu, hadi miezi sita, hii inamaana Masheikh wanatumikia kifungo kabla hawaja hukumiwa Alisema Shk. Kondo. Kondo alisema, wanaowakandamiza Wa i s l a m u w a e l e w e kwamba, imani za Waislamu zipo juu kuliko roho zao ndio maana hawachoki kuikabili Serikali na vyombo vyake vya dola na kuitaka kuacha dhulma. Ust. Kondo, alihoji kama ni suala la amani ya nchi, nani asiyependa amani, Waislamu hawakurupuki kutoa madai yao tatizo ni utawala ndio umekuwa wa

kidhalimu. Alitolea mfano kuhusu Baraza la Mitihani ( N E C TA ) a k i s e m a k w a m b a , Wa i s l a m u hawajaanza sasa kulalamikia suala hilo, ni takribani zaidi ya miaka 25, sasa lakini kadri miaka inavyozidi kwenda mbele, Baraza hilo linazidi kuwa machinjio ya Waislamu. Naye Kaimu Katibu wa Shura ya Maimam, Taifa Sheikh Juma Ramadhani, akionekana kuguswa na kile alichokiita dhulma dhidi ya Waislamu nchini, alisema kuwa Sheikh Ponda na wenzake si majambazi, si wahaini au wauaji, kwa nini wanyimwe dhamana? Serikali inataka kuipeleke wapi nchi hii? Tunataka dhamana za Masheikh ziwe wazi, kwa mujibu wa sheria. Ust. Ramadhan, aliitaka Serikali na vyombo vya dola vitambue kuwa Waislamu wanaheshimu utawala wa sheria na wanatambua kuwa kesi ya Masheikh wao ipo Mahakamani, bali wanacho hitaji ni haki ya msingi ya dhamana kwa Sheikh Ponda na wenzake. Ni kipi kinamfanya DPP, kuwanyima dhamana, tunahitaji kwa haki ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu zetu hawa, Bara n a Vis iw a n i w ap ew e dhamana, hii ni haki ya kila mtuhumiwa. Alisema Katibu Ramadhani, huku akianisha makosa yanayostahiki mtuhumiwa kunyimwa dhamana.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like