Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(6) SIFA ZA MANUFAA YA HIJJA


Mtume(saw) amesema, Anaporudi mtu Hijja anarudishwa na ujira mkubwa na zawadi nyingi. Na akasema(saw), Husamehewa mwenye kuhiji na anaowaombea. Hivyo manufaa ya HIjja yanawaenea wengi wasiokwenda. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300.Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

BAKWATA wamefanya dhambi kubwa-Waikela


Ni kwa kuuza mali za Waqfu, Mahakama yaombwa kuzirejesha Nyerere alimfunga Waikela kwa kuipinga Bakwata 1963 Sheikh Ponda akamilisha ushahidi Walioandamana kwenda kwa DPP jela mwaka mmoja

ISSN 0856 - 3861 Na. 1063 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Maaskofu wamepanda upepo wanavuna tufani


Hakuna mateso, bali mfumo umetikiswa Hakuna anayejua muungano utapona Mbeleko inayowabeba inazidi kuchakaa
chenga, yanakuwa sehemu ya madai ya Katiba Mpya. Hakuna ajuaye kama Muungano utapona, na ili uvunjike harakati zitainuliwa, na Kanisa haliwezi kupanga ziweje. Wanasema panda upepo, uvune tufani. Na hiyo ndiyo mantiki ya kinachotokea sasa. (Soma Uk. 7)

MZEE Bilal Waikela (mwenye bakora) akitoka nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Sheikh Ponda.

NECTA isashwe kwanza


Wakuu Shule za Kiislam wachua mazito Washuku kuwa inachakachua matokeo Wawasilisha hoja zao kwa Waziri Mkuu

Kufeli wanafunzi kidato cha nne:

UPO usemi wa kimasikhara, lakini wenye maana nzito. Wanasema, hiyo Siku ya Hukumu (Kiama), Mungu awahi maana kesi zitakuwa nyingi. Wiki iliyopita kesi

Nani atalipa dhulma hii Rais Shein, DPP au Jaji?

Maaskofu wanadai Kanisa lipo katika mateso. Lakini wakumbuke kuwa walishawasha moto kutoka Longido hadi Kyela, na kutoka Ngara hadi Mikindani. Sasa kwa hatua ya kuweka kila kitu mezani kijadiliwe upya, yale madai ambayo kwa miaka mingi serikali imeyafunika na kuyapiga

ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) iliingia katika hatua mpya baada ya Mahakama Kuu kufuta maamuzi yote ya Mrajis wa Mahakama hiyo. Soma Uk. 2

2
AN-NUUR

Tahariri/Habari/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

NECTA isashwe kwanza


Na Mwandishi Wetu

Nani atalipa dhulma hii Rais Shein, DPP au Jaji?


UPO usemi wa kimasikhara, lakini wenye maana nzito. Wanasema, hiyo Siku ya Hukumu (Kiama), Mungu awahi maana kesi zitakuwa nyingi. Wiki iliyopita kesi ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) iliingia katika hatua mpya baada ya Mahakama Kuu kufuta maamuzi yote ya Mrajis wa Mahakama hiyo. Maamuzi ya Mrajis yote yanafutwa kwani hayakuwa sahihi kwa vile Mrajis hana mamlaka ya kisheria ya kupokea, kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu. Hivyo ndivyo alivyonukuliwa Jaji Abraham Mwampashi wa Mahakama Kuu Vuga, akisema. Moja ya mambo makuu yaliyofutwa ikaelezwa kuwa ni zuio la dhamana ambalo Mrajis alilikubali kama lilivyokuwa limetolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP). Jaji Mwampashi alitolea maamuzi baada ya pande mbili katika kesi hiyo za upande wa serikali na utetezi kubishana juu ya uwezo wa Mrajis katika kutoa maamuzi ya dhmana kwa washitakiwa hao. Mawakili wa utetezi walidai kuwa Mrajis hana mamlaka hayo na upande wa waendesha mashitaka walidai kwamba anao uwezo huo. Jaji Mwampashi alisema DPP anao uwezo wa kuzuia Polisi tu kumpa dhamana mtuhumiwa, lakini sio Mahakama kama ilivyotokea katika suala hili. Jaji Mwampashi alisema DPP alitakiwa aeleze sababu za washitakiwa kutopewa dhamana na ni athari zipi za usalama wa taifa zitatokea iwapo watakuwa nje, halafu ndio Mahakama iamue kwa kuzingatia uzito wa hoja zilizotolewa. Alisema kama sheria ingekuwa hivyo kungekuwa hakuna haja ya kuwepo kwa Mahakama kama mtu mmoja anakuwa na haki hiyo na kusingeifanya Mahakama kuwa kimbilio la wanaoona wanapoteza haki zao. Sisi tunasema swadakta Jaji Mwamapashe. Hakuna haja ya kuwa na Mahakama kama mtu mmoja anakuwa na mamlaka ya kuamua kumweka ndani mtu apendavyo. Swali ni je, mpaka mtu anapewa cheo cha kuwa DPP au Mrajis, hajui sheria na kanuni hiyo? Kwa nini Mahakama Kuu haikutumia hoja hii anayoitoa Jaji Mwampashe hivi sasa toka awali kuhakikisha kuwa haki inatendeka na sheria husika inafuatwa? Kama anavyosema Jaji ni kweli kwa mujibu wa sheria zilizopo, ni kuwa watuhumiwa ambao hivi sasa wamekaa rumande mwaka mzima pungufu ya nusu yake, watakuwa wamedhulumiwa. Nani atalipa dhulma hii? Je, ni viongozi wa serikali, wa mahakama au wote kwa pamoja? Kuna kila dalili kwamba kuna vumbi la kisiasa limegubika kesi hii na mjadala unaoendelea. Ndio maana tunapewa hekaya hizi za mamlaka ya DPP na Mrajis Vs Mahakama. Lakini ni ukweli pia kuwa waliodhulumiwa kwa kuwekwa ndani bila ya dhamana, hakuna namna ya kulipwa haki yao katika dunia hii. Ila ikumbukwe kuwa ipo Siku ya Hakumu. Siku ambayo Mfalme na Hakimu atakuwa ni Allah (S.WT) Pekee. Na Qur an inauliza, je, hakuwa Mola wako ni Hakimu wa Mahakimu? Siku hiyo hakutakuwa na DPP, Mrajis wala Jaji Mwampashe na kesi za kisiasa.

MAONI YETU

WA K U U w a S h u l e za Kiislamu nchini wamewasilisha hoja zao kwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda wakihoji uadilifu ndani ya Baraza la M i t i h a n i Ta n z a n i (NECTA), wakionyesha mianya inayoweza kutumika kutoa matokeo yasiyo sahihi. Katika barua yao kwa Waziri Mkuu wamesema kuwa, pamoja na mambo mengine, kuna matatizo makubwa ndani ya NECTA ambapo kuna uwezekano mkubwa kuwa majibu yanayotolewa na Baraza hilo, sio sahihi wala yanayoakisi uwezo wa mwanafunzi kama ulivyooneshwa na matokeo ya mitihani aliyofanya. Ni kutokana na wasiwasi huo, wameomba kuwa katika jumla ya mambo yatakayofanywa na Tume iliyoteuliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, basi moja liwe ni pamoja na kutaka kuwekwa wazi alama za kila mwanafunzi kama alivyopewa na wasahihishaji wa mitihani kisha ilinganishwe na mayokeo ya NECTA. Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuzingatia yote tuliyosema hapo juu ndio maana tunasema tatizo lililopo linaweza kutatuliwa ikiwa utaamua kuwataka viongozi waandamizi wa NECTA na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuweka hadharani alama za mitihani walizopata wanafunzi wa kidato cha nne baada ya zoezi la usahihishaji kukamilika kama zilivyo katika list one. Aidha viongozi hao wa NECTA na WEMU waweke wazi kanuni iliyotumika kubadilisha matokeo ya wanafunzi kutoka list one kupata gredi kama zilivyotangazwa na NECTA. Hoja hii ya Wakuu wa Shule za Kiislamu, wameijenga wakitangulia kuonyesha kuwa kumekuwa na ushahidi mwingi wa kimazingira na wazi kutokana na tati

mbalimbali kwamba inakuwa vigumu kwa sasa matokeo ya NECTA kuaminika. Wanasema, kumekuwa na usiri usio na sababu na kanuni zisizo kubalika kitaalamu za kutoa madaraja ya mwisho ambayo mara nyingi yanazua maswali yasiyo na majibu. M h e s h i m i w a Wa z i r i Mkuu ni ukweli usiopingika kuwa wadau wote wa Baraza la Mitihani tukiwemo sisi wenyewe tunakabiliwa na changamoto ya usiri mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za NECTA. Hatujui mchango wa mazoezi ya kila siku (CA) katika alama ya mwisho apewayo mwanafunzi, hatujui pass mark wala hatufahamu grade ranges zinazotumiwa na Baraza la Mitihani kwa sasa. Baya zaidi ni kwamba Baraza la Mitihani haliko tayari kufanya mambo haya kuwa wazi kwa wadau wake licha ya utafiti wa serikali na ule wa Kamati ya Mlama kudaiwa kuitaka NECTA kufanya hivyo. M h e s h i m i w a Wa z i r i Mkuu Sisi Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu tunaamini kuwa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2012 kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na usiri huo ulioko NECTA ambao

huwapa fursa ya kuamua kupandisha viwango vya ufaulu (passmark), kushusha mchango wa CA na kubadili grade ranges bila kuwaarifu wadau wala kuwapa muda wa kujiandaa. Kutokana na usiri huo na kutokufahamika kwa pass mark na grade ranges, inatuhumiwa kuwa NECTA hutumia mwanya huo katika kipindi inapokaa na matokeo baada ya kusahihishwa kuweka viwango inavyotaka. Katika hali hiyo, unapatikana mwanya wa kumfelisha au kumfaulisha mwanafunzi kinyume na alama alizopewa na wasahihishaji kama ilivyorekodiwa katika list one. Wakimalizia barua yao, Wakuu wa Shule za Kiislamu wamesema kuwa ni matarajio yao kuwa NECTA itawaelewa na kuweka wazi taarifa hizo. Lakini end apo NECTA

itapuuza, wamesema watakuwa tayari kutafuta haki yao, ikibidi, kupitia mamlaka na vyombo vya kisheria ili kuviomba v i i a m u r u N E C TA itekekeleze wajibu wake wa kutoa taarifa hizo kwa umma.

Uongozi wa Masjid Tungi, Temeke jijini Dar es Salaam unawaarifu Waislamu wote kuwa, kutakuwa na Ibada maalum ya Itqaf msikitini hapo. Siku: Jumamosi ijayo tarehe 23/03/2013 msikitini hapo baada ya swala ya Isha.
WOTE MNAKARIBISHWA WABILLAH TAWFIIQ

Itqaf Masjid Tungi

Habari

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

BAKWATA wamefanya dhambi kubwa-Waikela


Na Bakari Mwakangwale wabaya, ambao walipanga mikakati ya kuiuwa EAMWS na kuwaundia Waislamu BAKWATA. Alisema njama za kuiuwa EAMWS, zilifanywa na Mwalimu Nyerere akimtumia Mzee Abeid Karume, kwa kuwalaghai Waislamu ambao aliwataja baadhi yao kuwa ni Adam Nassib, Saleh Masasi na Qassim Bin Jumaa. Mzee Waikela alisema, watu hao walizunguka katika mikoa ishirini nchini wakati huo na kuwashawishi Waislamu kuikataa na kutengana na EAMWS. Hata hivyo alidai fitna yao ilifanikiwa katika mikoa nane na mikoa 12 waliwakatalia. Mimi binafsi nilikuwa mpinzani wa kuitenga na kuiuwa EAMWS, kati ya mwaka 1968/9, kwani walika akina Adam Nasibu na watu wake na kunishawishi kwa kunipa Shilingi 40/=, nilizikataa wakaondoka. Alisema Mzee Waikela. Alisema baada ya juhudi hizo za kuwalazimisha Waislamu kuikataa Jumuiya yao, ilitumika Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, Bw. Saidi Masanywa, kwa kusimamia kufungwa osi zote na mali zote za Jumuiya zilizokuwa nchi nzima kukabidhiwa Bakwata. Aliongeza kuwa katika kuonyesha kwake upinzani katika kuiuwa EAMWS, alijikuta kati ya mwaka 1963 na 1964, akiwekwa kizuizi na Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Naiambia Mahakana kwamba, kiwanja cha Markaz si mali ya Bakwata, wakati tunapewa kiwanja hicho Bakwata haipo, imekuja baadae kwa hila na inda pasi ya ridhaa ya Waislamu na kuhodhi mali za waislamu zikiwemo za Waqfu. Alisema Mzee Bilali, baada ya kuulizwa na wakili Nassoro kuwa anaiambia nini Mahakama kuhusu madai ya umiliki wa Bakwata katika eneo hilo. Aidha alifafanua kuwa wao kama Jumuiya ya Waislamu, walisimamia mali za Waislamu kikiwemo kiwanja hicho kwa ajili ya maendeleo yao, lakini alidai baada ya mali hizo kuhodhiwa na Serikali na kuikabidhi Bakwata, mali nyingi za Waislamu zimeuzwa kwa bei chee, si Dar es Salaam tu bali hata zile zilizoko katika mikoa mingine na mali nyingine walikimilikisha watu wa Bakwata. Mfano wa karibu ni hicho kiwanja cha Changombe, tulikabidhiwa likuwa ni eneo kubwa sana tofauti na sasa, nasikia kimemegwa na kuuziwa watu. Lakini iwe mtu kapewa ama kauziwa, aelewe kabisa kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu si mali yake, ni mali ya Waislamu, mali ya waqfu haiuzwi, hagaiwi mtu. Alisema Mzee Waikela. Akijibu maswali ya wakili wa Serikali Bw. Tumaini Kweka, Mzee Waikela alisema Bakwata haipo kwa haki, ukifuatwa msingi wa kuunda chombo kwa kuzingatia demokrasia, kwani katika juhudi za Bw. Nassibu na kundi lake mikoani, ni mikoa nane tu ndio iliunga mkono kuvunjwa kwa EAMWS kati ya mikoa 20. Alipoulizwa kama anaikubali Bakwata, alisema haikubali, si sasa tu bali aliikataa tangu kuanza kwa mchakato wake na baada ya kuundwa kwawe mkoani Iringa na mpaka sasa bado haikubali. Mimi Bakwata siitambui, niliikata tokea wakati huo chini ya Sawaya (Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo), nikawekwa kizuizini na Nyerere, Bakwata imemilikishwa mali za Waislamu kinguvu, kimsingi mali hizo si za Bakwata ni za Waislamu. Alisema Mzee Waikela, ambaye pia alikuwa kiongozi wa Baraza la Misikiti Tanganyika. Akijibu hoja ya wakili wa serikali Tumaini Kweka, kuwa waliounda Bakwata mkoani Iringa walikuwa ni Waislamu, Mzee Bilali alisema wale walikuwa ni viongozi wa matawi ya Chama, na hawakuwawakilisha Waislamu kwani alidai hali halisi ilishaonyesha kuwa kati ya mikoa 20 ni mikoa nane tu iliyokubali. Alisisitiza kwamba shughuli za dini haziendeshwi na viongozi wa siasa bali ni viongozi wa dini. Ama alipoelezwa kuwa hakuikubali Bakwata kwa kuwa alikosa donge, alisema wakati huo hakuwa na dhiki ya pesa bali alikuwa ni mtu mwenye mali zake na hata wakati anaingia katika siasa pia hakuwa na dhiki. Sikuikataa Bakwata kwa chuki, mimi nilikuwa na pesa zangu hata wakati napambana na kupata Uhuru, nilikuwa natoa motokaa (gari) yangu kwa Nyerere (Rais) akija Tabora atumie, lengo lilikuwa ni Waislamu kutendewa haki, nimeikataa kwa sababu ya kupindishwa haki. Alisema Mzee huyo. Kwa ujumla Mzee Waikela, aliianishia Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu kwamba , Waislamu nchini wanatenzwa nguvu ndani ya Bakwata, kwani alidai kuwa iwapo ikitokea Waislamu kupiga kura kama wanaikubali au hawaitaki Bakwata, itaanguka. Hata hivyo Mzee Waikela, alisema hadhani kama inaweza kutokea fursa hiyo kwa Waislamu kwani anajua kuwa maslahi ya waliounda chombo hicho yataharibika. Katika hatua nyingine kwa mara ya kwanza, jana Sheikh Ponda Issa Ponda, alisimama katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Victoria Nongwa na kutoa ushahidi wake. Akianza kutoa ushahidi Mahakani hapo, Sheikh Ponda alisema kuwa, ni kweli kiwanja hicho kina mgogoro, ambapo Waislamu wanapinga eneo lao kupewa kampuni ya Agritanza, ambayo inadai kumiliki kiwanja hicho kwa kubadilishana na Bakwata, ambao nao walipewa kiwanja kingine huko Kisarawe. Sheikh Ponda, alisema migogoro ya viwanja eneo la Markaz Changombe ni ya muda mrefu, ambapo kuna wakati sehemu nyingine ya eneo hilo la Markaz Changombe, lilimegwa na kuuziwa mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji, kinyume na matakwa ya Waislamu ambao ndio wenye mali. Alisema katika sakata hilo Waislamu walipinga ambapo baadhi yao walikwenda Mahakamani, na wengine kwenda Serikalini kupinga kuuzwa eneo hilo. Alisema eneo hilo la Markaz awali lilikuwa kubwa, lakini sasa limebaki dogo sana kutokana na tabia ya kumegwa kinyemela bila Waislamu kujulishwa. Kuhusu kiwanja chenye mzozo kwa sasa, ambacho mfanyabiashara Hafidh, anayemiliki Kampuni ya Agritanza inayodai kumiliki kiwanja hicho, Sheikh Ponda aliieleza Mahakama kuwa mara baada ya kupata taarifa za eneo hilo la Markaz kumegwa tena, walimfuatilia mtu aliyedaiwa kulimega ili kujua kulikoni. Sheikh Ponda alisema Waislamu kupitia baadhi ya Masheikh, akiwemo yeye na Sheikh Lwambo, walikutana na Hadh ambapo walipanga siku ya kukutana kujadili tatizo hilo. Alisema baada ya kukutana, walimweleza Bw. Hadh kuwa kiwanja anachodai kupewa ni waqfu, kwa maana kuwa ni mali ya Waislam ambayo hairuhusiwi mtu kuuza, kuuziwa wala kujimilikisha isipokuwa ni kwa ajili ya matumizi ya dini, kwa maana ya matumizi ya masuala ya Waislamu. Akiendelea kutoa ushahidi wake Sheikh Ponda alisema kufuatia kikao hicho, walikubaliana na Bw. Hadh kuwa asitishe kujihusisha na kiwanja hicho na kwamba, atatafutiwa kiwanja kingine. Sheikh Ponda, aliwasilisha muhtasari wa kikao kati yao na Bw. Hadh Mahakamani hapo, waliyokubaliana kuwa Bw. Hadh, hatojihusisha na kiwanja hicho cha Markaz kama walivyokubaliana. Hata hivyo, Sheikh Ponda aliieleza Mahakama kuwa, baada ya makubaliano kufanyika kupitia kikao walichokaa, walishangaa kuona Bw. Hadh, akipeleka vifaa katika kiwanja hicho na kuanza ujenzi tofauti na walivyokubaliana. Alisema, baada ya kuona hivyo, walimtafuta Bw. Hadh na kumuuliza kulikoni akiuke makubaliano ya kikao chao cha awali, ya kukiacha kiwanja hicho cha Waislamu na kukubaliana kutafutiwa kingine. Alisema, kufuatia hali i l i y o j i t o k e z a Wa i s l a m u walikubaliana na kuamua kujenga Msikiti wa muda katika eneo hilo, ili kuhakikisha kwamba eneo hilo, haliingiliwi na mtu mwingine. Hata hivyo, Sheikh Ponda, alisema siku ya Ijumaa ya Oktoba 12, 2012 Waislamu walipokuwa wakijenga Msikiti wa muda, Bw. Hadh aliamua kulipeleka suala hilo polisi. Ndipo baadae alisema Sheikh Ponda, kwamba walika Polisi na kuwavamia Waislamu na kuwasweka ndani. Aidha Sheikh Ponda, aliitaka Bakwata kurejesha eneo lote la Waislamu Changombe, kama walivyolikuta wakati likiwa chini ya East Afrca Muslim Walfare Society. Alisema, kitendo cha Bwakata kukiri kuwa eneo limebaki dogo lakini lilikuwa kubwa, ni wazi kwamba kwa njia moja au nyingine kuna watu wameuziwa huku wakijua kuwa ni eneo la waqfu. Hivyo Sheikh Ponda, alihitimisha ushahidi wake kwa kuitaka Bakwata kwa hali yoyote, kurejesha eneo lote la Waislamu. Kesi hiyo imeahirishwa, ambapo April 4, Wakili upande wa utetezi atawasilisha Mahakamani majumuisho ya ushahidi uliotolewa ambapo Aprili 18 mwaka huu, kesi itatajwa Mahakamani hapo kwa ajili ya hukumu. Taarifa tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni, zimefahamisha kuwa baadhi ya Waislamu waliokuwa wameandamana Februari 15, kuelekea osi za Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa lengo la kutaka kujua sababu za kunyimwa dhamana Sheikh Ponda, wamehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja. Hukumu hiyo imetolewa jana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

MZEE Bilali Rehan Waikela (87), ameiambia Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam kuwa, kuuzwa ardhi ya Waqfu, Markazi Changombe ni aibu na dhulma kubwa dhidi ya Waislamu nchini. Mzee Waikela, amesema hayo Jumatano wiki hii mbele ya Hakim Mkazi wa Mahakama hiyo Bi. Victoria Nongwa, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya jinai namba 245/2012, inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake. Akiongozwa na mawakili wa upande wa utetezi Bw. Juma Nassoro na Yahya N j a m a , M z e e Wa i k e l a aliiomba Mahakama hiyo kuirudisha ardhi hiyo kwa Waislamu, kwani BAKWATA wamefanya dhambi kubwa kwa hatua yao ya kuiuza huku wakijua mali ya waqfu na inahitaji kufanyiwa uadilifu. Naiambia Mahakama kuwa aibu iliyofanyika ni kubwa kwa mujibu wa Dini yetu, labda wapagani ndiyo wanaweza kufanya hivyo. Naiambia Mahakama wairudishe ardhi hiyo kwa Wa i s l a m u , k w a n i h a t u a waliyoichukuwa si sahihi. Alisema Mzee Waikela. Mzee Waikela ambaye ni mmoja wa waasisi wa Chama cha siasa cha TAA, kisha TANU, na kiongozi wa iliyokuwa Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki (EAMWS), aliiambia Mahakama kuwa mali ya Waqfu kamwe haiwezi kuuzwa hata kama imerithiwa. Akielezea ufahamu wake juu ya kiwanja cha Markazi Changombe, Mzee Waikela ambaye alikuwa ni Katibu wa East Africa muslim Walfare Society (EAMWS) mkoa wa Tabora, alisema kiwanja hicho kilipatikana kipindi cha uongozi wa Jumuiya hiyo ya Waislamu, chini ya uongozi wa Agakhan na Rais wa Misri wakati huo Gamar Abdul Nasser. Alisema kupitia Jumuiya hiyo, zilifanyika juhudi kupata kiwanja hicho lengo na madhumuni likiwa ni kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislamu kwa awamu tatu, kwa msaada wa Rais wa Misri wa wakati huo Gamar Abdul Nasser. Alipoulizwa ni kitu gani kilikwamisha adhima hiyo, Mzee Waikela aliwataja aliowaita mafatani w ak is h ir ik ian a na w atu

4
Na Pendo Masasa
NDOA ya Kiislamu ina taratibu zake, kuanzia posa mpaka kukamilika tukio lenyewe la ndoa. Jambo la kwanza linalotakiwa lifanyike kwa makini kabla ya mwanamke au mwanaume kufunga ndoa, ni kumchunguza na kumtathmini mchumba kwa kuzingatia mipaka ya Allah (s.w) na mafundisho ya Mtume (s.a.w) na kufanyika kazi ushauri wa wazazi au walezi. Wo t e , m w a n a m k e n a mwanaume wana haki ya kutathmini na kuchunguza mwenendo na tabia za mwenzake kabla kukia makubaliano na kufanya maamuzi ya kufunga ndoa. Mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuchagua mchumba kulingana na mafundisho ya Quran na Sunnah ni dini, maharimu, tabia njema, uzuri wa mke, uzazi, hadhi na elimu. Vigezo vyote ni muhimu katika kuendea ndoa, lakini binadamu ni mwenye upungufu. Iwapo muoaji au muolewaji atakosa baadhi ya vigezo,

Makala/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013


mtihani wa kuachwa, lakini alibahatika akuzaa watoto, baada ya hapo akapata mchumba mwingine akataka kumuoa, kabla ya ndoa akacha kuwahi kuolewa na ana watoto, ili tu asije akakosa mume au asionekane mzee. Kwa mwanamke huyu kusema kwake uongo si tatizo. Na kwa kutumia uongo wake, mume atamuoa lakini akiwa ndani ya ndoa, mume akigundua kuwa alimdanganya, lazima kutakuwa na mzozo na wengi wameachika kwa sababu hiyo. Lakini kama mwanamke huyo angekuwa jasiri na kuamini kuwa ndoa ni kudra ya Allah (sw) akaonyesha ukweli wake na muoaji achague mwenyewe, ndoa ingekuwa ya amani raha mustarehe na ya kuaminiana. Aidha wapo wanaooa au kuolewa wakiamini katika ndoa yeyote ilimradi kuondoa mikosi! Hawa hufanya kila wawezalo, kwa kuongopa au hata kwa kujipamba kwa tabia bandia (pretending) ilimradi ndoa ifungwe. Hili nalo ni hatari sana hasa baada ya ndoa kufungwa, kwani yule aliyekuwa akimini ndiye mume au mke aliyekuwa akimhitaji, anakuta ni mtu mwingine tofauti na matarajio yake. Siku zote uwongo ni sumu ya ndoa. Mke au mume anapogundua kuwa mwenzake aliyekuwa akimwamini kwa moyo wake wote ni mwongo, anakuwa na maswali mengi ya kujiuliza na ataishi kwa mashaka makubwa na mwenzake. Hapo mmoja ataanza kupunguza uaminifu kwa mwenzake. Hata kama utatokea wasaa mmoja akasema kweli, mwenzake atasikiliza na kupuuza. Asiyemwamini mwenzie ataanza kubadilika taratibu, hapo ugonjwa wa dharau nao utapenya, maana asiyeaminiwa atahisi kudharauliwa. Taratibu upendo na mapenzi yatapungua, hapo ndipo migogoro mingine itaanza kuibuka na hatimaye kuvunjika ndoa. Mwenyezi Mungu atuepushe na upungufu huu. Ni vyema kujiepusha na uongo na na kujizoesha kuwa na tabia njema ya kuwa wakweli kabla na baada ya ndoa zetu. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumetekeleza sehemu muhimu ya kujiepusha na migogoro ya ndoa inayo epukika. Tukizidi kuwa wabishi kwa kuacha kufuata Qur an tukufu na mafundisho Mtume (s .a .w), tutarajie shari katika ndoa zetu, shari kwa wazazi au walezi wetu na hatimaye kuwa mzozo wa familia. Tukumbe tu kwamba, maisha ya ndoa kwa wanaofuata taratibu na malekezo yake kikamilifu, huishi kwa raha mustarehe na familia zao hadi mwisho wa uhai wao.

AN-NUUR

Uongo ni sumu katika ndoa


akapata japo viwili muhimu, yaani dini na tabia njema, huyo anaweza kuwa mke wa kuolewa au mume wa kuoa. Kuna kosa huwa linafanywa mara kwa mara na mwanamke au mwanamme katika kukia maamuzi ya kuoa au kuolewa. Watu wengi wanaona kuwa kumpata mchumba sahihi hadi kufikia uamuzi wa kuoa, ni jambo jepesi tu kutekelezwa pale mhusika anapoamua. Madhali muoaji au muolewaji anamuona mwenzake anaswali swala tano, basi anadhani hilo pekee ni uthibitisho tosha kumfanya anaamini kuwa mwenzake ana tabia nzuri na ana vigezo vyote vya msingi. Na kwa kuona anaswali, basi suala la kutizamana tabia kwa kina likawa halina haja tena. Tatizo hili ni moja ya sababu ya ndoa nyingi kuvunjika muda mfupi baada ya kufungwa. Kwa sababu walengwa hawakuona haja kuchunguzana vyema katika vigezo vya mwenendo mzima wa tabia na dini. Kama sharti lilivyowekwa na Allah (s.w) Na (Mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu katika wale waliopewa kitabu kabla yenu .. Na katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), Mtume (s.a.w) amesema, utakapochumbiwa na mwanamume unaye mpenda kwa dini yake na tabia yake, basi kubali uolewe naye, kama hutafanya hivyo patakuwa na huzuni (matatizo) na vurugu katika ulimwengu. Kwa makusudi au kwa kutofahamu kwasababu ya kutojishughulisha na kutafuta elimu, wachumba wengi wamekuwa kuingia katika ndoa, si kwa sababu ni sehemu ya ibada bali wanasukumwa zaidi na matamanio ya nafsi. Tatizo hili ni matokeo ya jamii yetu ya leo kupuuza mwongozo wa Quran na mafundisho ya Mtume (s.a.w) jinsi ya kupata mke mwenye tabia njema na dini kadhalika na mume. Wengi wanafuata matamanio. Nafsi zao zinataka nini. Hili limekuwa sababu kubwa ya migogoro ya ndoa kila kukicha, wengine hadi wanafikia uamuzi mgumu na unaomkera Mwenyezi Mungu wa kuachana, bila kujali kuwa jambo hilo ni ghadhabu mbaya kwa Allah (sw). Hata hivyo leo nitazungumzia tabia moja ambayo imekuwa sugu na imeleta mizozo mingi katika ndoa. Uongo, yaani tabia ya mume au mke kutokuwa mkweli katika maisha ya ndoa tangu uchumba. Tabia hii imekithiri kiasi cha watu wengi kuona uongo ni jambo dogo sana na sehemu ya maisha ya wanandoa. Wengi kwa kutotambua madhara yanayotokana na uongo, wanapuuza kuachana na tabia hiyo na wamesahau kemeo kali juu ya uongo, na himizo juu ya ukweli kama anavyosema Mtume (s.a.w). Jilazimisheni na ukweli, hakika ya ukweli anapeleka katika wema, hakika ya wema unapelekea peponi, mtu kusema ukweli na anajilazimisha na ukweli, hata ataandikwa mbele ya mwenyezi Mungu msema ukweli, jiepusheni na uongo hakika ya uongo unapeleka mtu katika uovu, hakika ya uovu unapeleka mtu motoni, hataacha mtu kusema uongo, anaendeleza uongo hata ataandikwa mbele ya mwenyezi Mungu msema uwongo. Somo hili linapuuzwa sana kwa maana kuwa, watu wanaanza uchumbiana wanadanganyana hadi katika ndoa wanazidi kudanganyanya. Tujiulize, katika uchumba hadi ndani ya ndoa zetu, umedanganywa mara ngapi au umedanganya mara ngapi kwa mwenzako. Na Pia tupime, uongo umekufaidisha nini na umekupatia hasara gani katika mahusiano yako ya ndoa. Wa l i o m a k i n i k a t i k a kuchunguza, wakigundua kuwa mchumba unayemchumbia au anayekuchumbia ana tabia ya kusema uongo, posa haitakubalika na ndoa haitakiwa. Ingawa si watu wote waongo, lakini siku hizi wanaosema ukweli ni wachache sasa. Uongo umetawala kila kona katika maisha, si katika mahusiano ya ndoa tu, bali katika biashara au mengineyo. We n g i k a t i k a h a t u a y a kuchumbia tu, hasa wanaume huanza kudanganya kuwa ana utajiri kadha wa kadha, ilimradi atimize dhamira yake ya kuoa, japo halali yake utajiri wenyewe haupo. Mwanamke naye, labda alishawahi kuolewa akapata

Marekani na Uingereza ziliizamisha Irak katika damu


Ngoma ya washenzi: Miaka kumi katika kilindi cha Jehanam
Na Chris Floyd
Machi 16, 2013 Mtandao wa kupashana habari Himaya iliyovurugika: Kila aina ya warusha habari za kisiasa katika magazeti, mitandao au hewani - zimekuwa zikisikika katika wiki kadhaa zilizopita kuelezea miaka kumi tangu uvamizi wa Irak ukiongozwa na Marekani, mwezi Machi 2003. Katika mlima wa kumbukumbu za kubuni na za uwongo, ambako maadhimisho kama hayo lazima yainue jeshi la wachambuzi, wengi wakiwa wacheuaji wa chochote kinachokuja kwa busara iliyopo wakati huo, kumekuwa na mada kadhaa zinazoelimisha, ambazo zinaonyesha uhalifu huu wa kivita unaoendelea katika hali yake halisi. Moja ya insha bora zaidi katika mada hiyo iliandikwa katika hali ya kushangaza, na mtu wa Irak. Sami Ramadhani, mpinzani wa Irak aliyekimbizwa uhamishoni wakati wa Saddam. (Huyu) amekuwa mmoja wa waangaliaji habari wenye upenyo wa kutafakari na wapinzani wakali wa mateso yaliyofanyiwa nchi yake na wasomi wa nchi za Magharibi na washirika wao (akiwemo bila shaka kwa miaka mingi, Saddan Hussein). Kutoka gazeti la Guardian: Miaka kumi tangu mshtuko na kiwewe cha vita ya 2003 ya Bush na Blair, ambavyo vilifuatiwa na miaka 13 ya vikazwo vya mauaji, na miaka 35 ya udikteta wa Saddam, nchi yangu inayotaabika, ambayo mwanzo ilikuwa shina la ustaarabu, inachungulia shimo la giza. Uingiliaji kwa kibri wa kibeberu na utawala wa kidikteta kwa pamoja vimekuwa chanzo cha kuuawa zaidi ya watu milioni moja tangu 1991. Na bado, kwa mujibu wa Tony Blair na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Madeleine Albright, wanasema gharama hii ni sawa. Blair, ambaye wa-Irak wengi wanamwona kama mhalifu wa kivita, anapewa heshima kubwa na vyombo visaliti vya habari. Wa-Irak wanasikiliza wasiamini masikio yao wakati anasema Najisikia kuwajibika lakini sina masikitiko kwa kuondolewa kwa Saddam Hussein.(Ni kama vile Saddam na wabeba mikoba wake walikusanywa tu wakaondolewa, wakiwaacha watu wajenge nchi ya kidemokrasia). (Kumbe kuondolewa kwao kuliambatana na kuuliwa kwa mamilioni ya binadamu wasio na hatia na miji kuangamizwa.) Inatuudhi kumwoma Blair akijenga himaya ya kibishara, akitumia nafasi aliyokuwa nayo katika kulundika mafuvu ya waIrak kuliko ambavyo Saddam aliwahi kukia. Kama mhamaji, nilikuwa na hisia kali na maumivu kuhusu kwa maneno yasiyosahaulika, mafanikio ya kushangaza. Pia yamekuwa, zaidi na zaidi, mafanikio yaliyosahaulika. Usahaulifu wa Marekani kuhusiana na uhalifu wa kivita nchini Irak na inavyoendelea kupanuka, siyo tu ukandamizaji na mauaji yanayoendelea hapo, lakini pia athari za kina za uharamia huu kwa Marekani yenyewe, ikiwa ni pamoja na tsunami ya kujiua, kutokuwa na makazi na post-traumatic stress disorder (mtindio wa hisia unaotokana na mshtuko wa vita) miongoni mwa askari wake, na mzigo mzito wa gharama za mduara huu wa rushwa na kufaidika kutokana na vita ni hali ya kushangaza kweli. Siyo tu hali halisi ya kuishi, majonzi, kuendelea kwa mkasa mzito wa kibinadamu, bali ni malighafi za uchambuzi, kupata alama za mijadala ya makundi, kwa maongezi ya wanywaji kilabuni. Hii siku zote imekuwa hivyo kwa vita vyetu tulivyoanzisha kueneza ubeberu (kama mfano wa usahaulifu wa kina, angalia (katika jarida lenye makala hii) mapitio ya kitabu kipya cha Nick Turse, Ua Chochote Kinachotembea: Vita Halisi ya Marekani nchini Vietnam, kuanzia mwanzo wa karne ya 19. Na ujio wa mtandao wa internet hakujafanya lolote kubadili hilo. Licha ya kuwepo urahisi wa kupata habari kwa wingi kuhusu hali halisi ya vita vya Irak (na uhalifu mkubwa kwingine, na mateso), usahaulifu na ujinga wa kujitakia bado unabaki wa kina kama mwanzo. Hivi tuko hapa. Miaka kumi

Habari za Kimataifa/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

ASKARI wa Marekani wakiwa nchini Iraq


uhalifu wa Saddam, ambako kwangu ilianza na kupotea kutoka shule ya tiba kwa raki yangu mkubwa wakati tukiwa shuleni, Hazim. Watu wa Irak wanafahamu ka pia kwamba Saddam alifanya uhalifu mkubwa akiwa raki wa nchi za Magharibi. Katika kipindi cha kukia uvamizi 2003 niliandika hivi katika Guardian: Nchini Irak, rekodi ya Marekani inajieleza yenyewe: ilikiunga mkono chama cha Baath, kutwaa madaraka mwaka 1963, wakauawa maelfu ya wafuasi wa ujamaa, wakomunisti na wana-demokrasia. Nchi za Magharibi zilikiunga mkono chama cha Baath mwaka 1968 wakati Saddam alipofanywa kuwa makamu wa Rais; zilimsaidia yeye na Shah wa Iran mwaka 1975 kuvunjilia mbali harakati ya kitaifa ya wa-Kurdi. Nchi za Magharibi ziliongeza kumuunga mkono Saddam mwaka 1979, hivyo kumsaidia kuanza vita vyake vya uchokozi dhidi ya Iran mwaka 1980; zilimsaidia muda wote wa vita hivyo vya kutisha (1980 hadi 1988), ambako Wairani na Wairaki milioni moja walichinjwa, wakijua ka alikuwa akitumia silaha za kemikali na kuwapiga kwa gesi Wakurdi na Waarabu wa eneo tepevu (miingiliano ya mito Euphrates na Tigris). Nchi hizo zilimpa motisha mwaka 1990 avamie Kuwait...; walimuunga mkono mwaka 1991 wakati Bush (baba) ghaa aliposimamisha vita, takriban masaa 24 baada ya kuanza kwa uasi wa mwezi Machi ambao ulienea kusini kote na eneo la Kurdistan ya Irak... Lakini ilipokuwa si maslahi kwa kumsaidia, Marekani na Uingereza waliizamisha Irak katika dimbwi la damu. Bado hatujahesabu waliokufa, licha ya waliojeruhiwa, kuondolewa kwao na kuumizwa kiakili. Maelfu kwa maelfu hawajulikani walipo. Kati ya wakimbizi zaidi ya milioni nne, kiasi cha milioni moja hawajarudi nchini kwao, na kuna wakimbizi wa ndani milioni moja. Takriban kila siku, milipuko na risasi vinaendelea kuua watu wasio na hatia. ...Kukosekana kwa umeme, maji safi na huduma nyingine muhimu kunaendelea kuwakwamisha mamilioni ya watu masikini na wasio na ajira, katika moja ya nchi zenye utajiri zaidi duniani. Wanawake na watoto wanalipa gharama kubwa zaidi. Haki za wanawake, na haki za binadamu kwa jumla zinakandamizwa kila siku. Na vipi kuhusu demokrasia, ambayo inasemekana ndiyo hasa sababu ya mkasa wote huu? Mamlaka zilizoundwa na Marekani zilianzisha mchakato wa kisiasa na katiba yenye nia ya kuinua ugomvi wa kiukoo na madhehebu ya dini. Baada ya kushindwa kuondoa upinzani kwa ukaliaji wa Irak kwa mabavu, walianza kutumia mbinu za kugawa na kutawala kupata mahali pa kusimama nchini Irak. Wakitumia mateso, vikundi vya mauaji vya kiukoo na kidhehebu na mabilioni ya dola za Marekani, ukaliaji wa Irak umefaulu kudhoofisha mahusiano ya jamii na kuinua tabaka tawala la kisadi ambalo linazidi kuwa tajiri kila siku, wakitokwa na mate kutafakari jinsi ya kupata sehemu kubwa zaidi ya maliasili za Irak, ambazo kwa jumla zimewekwa rehani kwa makampuni ya nje ya mafuta na ujenzi. Vikundi vinavyopigana vya kikabila na kidini, viwe washirika au vyenye kihoro cha uwepo wa Marekani hapo, vinatawala taasisi za dola, zenye ufanisi mdogo na kusheheni rushwa zikiongozwa na ubalozi wa Marekani jijini Baghdad kubwa kuliko zote duniani. Bado ndiyo unaoelekeza nini kifanyike, Irak bado siyo nchi huru kikamilifu, ikiwa imefungiwa chini ya Sura ya Saba ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, ambayo hasa ni mkondo wa adhabu. Ndiyo, imekuwa, kama Barack Obama alivyoeleza

Mzee Bilal Waikela aliyekuwa kiongozi wa EAMWS na muasisi wa TAA/TANU atazungumza na Waislamu katika Msikiti wa Mtambani leo, Ijumaa tarehe 22/03/2013 mara baada ya swala ya Ijumaa. Tafadhali usikose siku hii adhim IMAM MTAMBANI

TANGAZO Masjid Mtambani

tangu kiwewe cha uzalendo (au ilikuwa kilele cha tendo) wa utumbukizwaji watu wengi katika wimbi la kutumia nguvu na silaha, ambao wenyewe ulikuwa ni kielelezo cha juu cha vita iliyoungwa mkono na pande zote mbili za kisiasa (Bunge la Marekani, vyama vya Republican na Democratic) kwa vikwazo ambavyo maosa wa serikali ya Marekani wamekiri viliua zaidi ya watoto nusu milioni wa Irak. Ni nini maadili ya siasa (za Marekani) leo? Hili swali ambalo lilikuwa halifikiriki, lenye kina cha unyama na ni mithili ya tusi: Rais apewe mamlaka kuua raia yeyote anayetaka au labda kuwe na uangalizi wa siri wa Bunge (la Marekani) kwa mpango wa siri wa kuua? (Dhana ya kupunguza uwezo wa rais wa kumwua mtu yeyote dhalili wa kigeni halipo kokote katika siasa zetu, bila shaka. Rand Paul (mmoja wa wagombea uteuzi wa chama cha Republican uchaguzi mkuu uliopita, mwaka jana) alikuwa haleti kigugumizi chochote kuhusu wazo hilo. Hapana, mjadala wowote kuhusu maadili ya dola kufanya mauaji inahusu tu raia wa Marekani, ambao, kama tunavyotakiwa tuamini, ndiyo binadamu halisi tu katika uso wa dunia). Ukichukulia jinsi tunavyoelekea kwa kasi kwenda ushenzini, natabiri kuwa katika miaka michache tu ijayo, tutakuwa tuna mjadala kama rais ana hali ya kuinua vichwa vya magaidi waliouawa kwa mitarimbo nje ya Ikulu, au labda vichwa hivyo vizungushwe kwa kificho kati ya wajumbe wa kamati husika za Seneti kabla havijatupwa baharini.

6
Na Bakari Mwakangwale
KAMA kuna Madrasa ambayo imetoa mchango mkubwa katika nyanja ya kielimu na kijamii katika Manispaa ya Mji wa Morogoro, basi Jabal Rahma ni mojawapo. Sisemi haya kwa mapenzi yangu la! bali ni baada ya siku za hivi karibuni kukitembelea kituo hicho kilichopo mtaa wa Umbunga, Kata ya Sultan Area mjini hapa na kuzungumza na Sheikh Miraj Omar Kimosa. Kwa mujibu wa Sheikh Kimosa, Madrasa hiyo iliyopo katika Msikiti wa Sultan Area, ilianzishwa mwaka 1972 chini ya Al-Marhum Sheikh Juma Hassan Sekidunda. Tangu kuanzishwa kwake, Madrasat Jabal Rahma ilipata mafanikio kwa kuzalisha wanaharakati na wasomi katika nyanja mbalimbali za kitaaluma mkoani Morogoro. Chanzo cha kuanzishwa kituo hiki mwanzoni mwa miaka ya 1970, ilikuwa ni fikra za wazee wa Kata ya Sultan Area ambao baada ya kujenga Msikiti huu mwanzoni mwa miaka ya 1960, wakaona ni lazima kuwe na Madrasa itakayotoa wasomi watakaokuja kuongoza Msikiti pamoja na kuhuisha harakati za Kiislamu, anasema Maalim Miraji. Walillahil hamdu, mimi na wenzangu kadhaa, akina Mahiku Maharagande, Kassim Omar Stima ambaye kwa sasa ni Imam wa Msikiti wa Mtawala uliopo Mwembesongo, ndiyo tuliokuwa wanafunzi wa kwanza kujiunga na Madrasa hii. Wengine ni Abdulrahman Shaaban, almaarufu Kiswabi, ambaye ni Katibu Mkuu wa Msikiti wa Boma Road, Hamza Issa Mahangatila, Juma Matekenya, Fadhili Kassim. Alitaja Maalim Kimaso baadhi ya watu ambao ni matunda ya Madrasa hiyo . Maalim Kimaso, ambaye pia ni Imam Mkuu wa Msikiti huo, alibainisha kwamba ilipofika mwaka 1980, muda wa kuishi wa Sheikh Juma Sekidunda ukawa umefika kikomo na kuiacha Jabal Rahma mikononi mwa wanafunzi wake akiwemo Maalim Fadhili Kassim. Sheikh Kassim Stima, yeye akawa kiongozi wa tawi la Jabal Rahma iliyopo Masjid Mtawala, ambayo aliifungua Marehem Sheikh Sekidunda enzi za uhai wake. Baada ya hapo, Madrasa iliendelea kufundisha masomo yale yale ya msingi ya Quran na Fiqh, ambayo muasisi wake alikuwa akiyafundisha. Ilipofika mwaka 1996, nilitawadhwa rasmi kuwa Imam wa Msikiti huu wa Sultan Area pamoja na Mkuu wa Jabal Rahma, anasimulia Sheikh Kimosa. Baada ya hapo kwa kushirikiana na wenzake akina Sheikh Hamza, wakashauriana na kukubaliana kufanya mabadiliko makubwa ya kimtaala. Alisema mabadiliko hayo yaliingiza pia masomo ya sekula, na kuipaisha Madrasat Jabal Rahma na kuwa kituo (Centre) kikubwa cha elimu mjini Morogoro. Baada ya kugundua mahudhurio ya wanafunzi yanapungua kwa sababu ya kwenda katika masomo ya jioni (tution) nasi tukaanzisha utaratibu huo haraka.

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013


hapo wanalazimika kutumia Kompyuta mbili tu ambazo nazo zimekwishaharibika. Aidha alisema kwamba changamoto nyingine ni unyu wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na wingi wa wanafunzi, jambo ambalo linahitaji msaada na nguvu ya pamoja kutoka kwa wadau wa Kiislamu kwa ujumla kuondoa tatizo hilo. Alisema kwa jinsi hali ilivyo, ingekuwa nafuu kubwa iwapo wanafunzi 300 wangekuwa ndani ya vyumba walau vitatu, kwa maana ya kila chumba wanafunzi 100, kwa shida shida lakini wote wanalazimika kubanana sehemu moja na baadhi yao hulazimika kuhamia Msikitini inapokuwa si wakati wa swala. Hapo bado darasa la chekechea pamoja na mafunzo ya kompyuta, achilia mbali program ya elimu ya Sekondari ya jioni (QT) na wale wanaojiandaa kurudia mtihani wa kidato cha nne (Resiters). Kwa kweli ukika Jabal Rahma na kuona mandhari yake, utakubaliana nami kwamba kunahitajika juhudi za maksudi ya kukiendeleza kituo hichi. Alisema Maalim Kimaso kwa masikitiko. Tukiwa Waislamu, watu wenye kupendana na kusaidiana, ni vema kwa wadau kuchukuwa fursa hii, si kwa waliopo Morogoro tu, bali na Waislamu wengine kuka Jabal Rahma na kusaidia kwa kile walicho nacho katika harakati zilizopo. Kwa wale walio mbali na hawataweza kuka Morogoro kujionea hali na kutoa walichojaaliwa kuwasaidia vijana wa Kiislamu katika sekta hii muhimu ya elimu, bado wanaweza kukisaidia kituo hicho kwa kuwasiliana moja kwa moja na Maalim Kimosa 0658 865 608 na kupata maelekezo na ufafanuzi zaidi.

AN-NUUR

Jabal Rahma Morogoro

Jiko la wanazuoni lililosahaulika

Masjid Jabal Rahma, Morogoro Na hapo ndipo tulipokuja kufanikiwa kutoa wasomi wengi ambao leo hii Manispaa ya mji wa Morogoro na viunga vyake inajivunia, anajigamba Maalim Kimosa. Katika mafanikio ambayo Maalim Kimosa, alinifahamisha wakati wa mazungumzo yetu, ni pamoja na kutoa wasomi kama vile Salum Mkolwe na Ziada Mgumila, ambao wote kwa sasa wana elimu ya juu. Anawataja wengine ambao ni matunda ya Jabal Rahma, yaliyotokana na mabadiliko ya kimtaala ni pamoja na Ramadhan Kibinda, Athman Mustafa Kinza, Shufaa Uvila, Hassan Hussein, na Shomar Masenga, ambao wote hivi sasa ni wataalam wenye Shahada. Mbali na hao, maalim Kimosa alinieleza kuwa Jabal Rahma pia ndio chimbuko la wanaharakati mashuhuri katika kuipigania dini ya Kiislamu ndani na nje ya Manispaa ya Morogoro. Aidha wapo wanasiasa mashuhuri wanaotegemewa mjini hapo, ambao Maalim Kimosa alisema wamepikwa kutoka katika jiko hilo la Jabal Rahma. Baadhi yao aliwataja kuwa ni pamoja na Mbalala Abdallah Maharagande, ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa na Salum Mkolwe ambaye ni Mwenyekiti wa UV-CCM (W) Morogoro mjini. Pia aliwataja wengine kuwa ni Hassan Bantu anayeshikilia nafasi ya uweka hazina wa CCM Wilayani humu pamoja na Maulid Chambilila ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini. Sio hao tu, Jabal Rahma pia inajivunia kuwa na wanahabari waadilifu kama vile Maulid Kambaya wa Radio One, Shaibu Kifea wa gazeti la Al-Huda p amo ja n a A zad M p an g o , ambaye licha ya kuwa mwandishi wa habari, lakini pia ni Imam na Khatib wa Masjid Maftah, alibainisha. Aidha Mkuu huyo wa kituo cha Jabal Rahma alisema kuwa, kwa miaka mitano mfululizo chuo chao kimeibuka vinara katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran mkoani humu. Alisema kuanzia mwaka 2008-2012, Jabal Rahma haijapata mpinzani kwenye medani ya usomaji na uhifadhiji Qur an katika mashindano yanayofanyika kila mwaka mjini. Hayo ni baadhi ya mafanikio makubwa wanayojivunia Jabal Rahma Centre. Hata hivyo, pamoja mafanikio hayo na kutoa wasomi pamoja na wanaharakati katika nyanja mbalimbali, lakini Jabal Rahma inakabiliwa na changamoto nyingi. Kukosekana kwa Waislamu wenye utashi wa kujitolea kwa hali na mali kukisaidia kituo hicho licha ya kuwepo mafanikio, ni moja ya changamoto hizo. Sheikh Kimosa alitoa mfano kuwa, kulingana na hali ya mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia hivi sasa na ili kwenda na wakati, kituo kimeanzisha mafunzo ya kompyuta, ambapo wanafunzi 300 waliopo kituoni

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika osi zifuatazo:1. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hadh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

7
Na Anil Kija
MAASKOFU wa makanisa takriban yote, hata wale ambao kwa kawaida hawajumuishwi katika mikutano ya makanisa makubwa nchini, hivi majuzi wamekuwa katika kikao kizito katika makao makuu ya Kanisa Katoliki nchini, Kurasini jijini Dar es Salaam. Mada ya mkutano huo ilikuwa kuangalia kama Kanisa (kwa jumla) limeingia katika kipindi cha mateso, ambacho kianzio cha dhana hiyo ni uteswaji wa wafuasi wa Kikristo katika kipindi cha miaka 300 kabla ya Mfalme Constantine wa Roma kubatizwa. Baada ya hapo, mateso yamekuwepo kwa makanisa mapya yaliyokuja baadaye, yakituhumiwa uasi, na wengi kuuawa. Chanzo cha wasiwasi na mjadala huo ambako inasemekana maaskofu walikutana chini ya ulinzi mkali - kana kwamba vita ya dini imeshaanza rasmi, ni matukio ya hivi karibuni ambayo yalikuwa ni pamoja na kuchomwa makanisa Dar es Salaam na Zanzibar. Pia aliuawa Padre kwa kupiga risasi (na kabla ya hapo mwingine aliponea chupuchupu kwa risasi wakati wa Christmas). Bado uchunguzi unaendelea na taarifa rasmi za uchunguzi hazijasema, nini chanzo cha mauaji hayo. Halafu kuna huu mzozo wa kuchinja eneo la Ziwa, ambako mchungaji alichinjwa baada ya mlipuko wa fujo za kidini. Ni matukio halisi na baadhi yake yanatisha, lakini kulikuwa na walakini katika mada ya Maaskofu na mahitimisho yao yalivyoonekana hasa katika magazeti ya Kikristo. Moja ya mahitimisho muhimu ni kukubaliwa kuwa Kanisa limeingia katika wakati wa mateso hapa nchini, hasa kutokana na madai kuwa iko mikanda inayotaka wafuasi wa dini pinzani wanaodhamiria kuwadhuru Maaskofu na viongozi wengine wa dini hiyo. Duru za magazeti zinasema mikanda hiyo imekuwa inazungushwa kwa muda wa miezi sita, ndipo inasikika polisi wameanza kukamata wahusika. Pia kulikuwepo hisia ya jumla katika mahitimisho kuwa serikali haiwatendei haki Wakristo kwa sababu haichukui hatua stahiki kwa matukio yote haya ya hujuma. Kikao kilikuwa na usiri mkubwa na waandishi wa habari hawakuruhisiwa. na haielekei kuwa ilitolewa taarifa pana kwa hitimisho la kikao. Si rahisi kusema kulikuwa na upana gani wa uchangiaji. Inawezekana hoja zingepishana, kwa kiasi. Tatizo linaloonekana kuhusu mkutano huo na hitimisho lake, au uelekeo wake kiuchambuzi (wa kitheolojia) ni kutokujua chanzo cha matukio ya sasa, halafu kujaribu kupatia mazingira ya mifarakano inayojitokeza, joho la imani, kuwa ni Ukristo kama imani ambao unapigwa vita. Baya zaidi, ni wazo kuwa hii ni vita ambayo wanajikuta wao wanahujumiwa tu, bila kuwepo na tatizo kwa upande

Habari/Matangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013


Mwinyi kuboresha tija katika uchumi, yaani kama taasisi, msisitizo huo labda usingekuwa na nguvu, kama ilivyokuwa miaka iliyopita. Lakini kutokana na Kanisa kuwakingia kifua watu wake waliosheheni mashirika ya umma, serikalini na Bunge wanaofaidi zaidi uwepo wa mashirika yasiyo na tija kwa uchumi wa nchi, linabebeshwa lawama za kukwama matumaini ya wengi, hasa pale wanaofanya ukinzani huo wanapoamini upo Mfumo Kristo, na nia halisi ya kudhulumu Waislamu. Mungu anaihitaji dhana hiyo, kulipigia Kanisa. Kimsingi ni kuwa Maaskofu wameonyesha kiburi katika maeneo kadhaa katika miaka mingi, mfano wa kwanza ukiwa ni huo wa 1993, kwani Mwalimu hakuwa na haki ya kumkwamisha Mwinyi katika sera zake, na alianza tena kutaka kumkwamisha Rais Benjamin Mkapa, yote haya katika jitihada zake za kuitetea siasa muisi ya Ujamaa. Wapo wanaoleta madai kuwa kuna watu walimdhuru Mwalimu Nyerere na kusababisha kifo chake. Waache uzandiki; Mungu akitaka mtu aondoke, hahitaji msaada wa mtu. Uasi wa 1993 ndiyo umezaa hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali, ambayo bado imegubikwa na kra ile ile ya Mwalimu, iwe ni 1993 au 1995, dhana ile ile ya viserikali corrupt havitozi kodi, wakati Mwalimu hakuwahi kukusanya kodi kwa chochote kinachoingizwa na Kanisa. Mwaka 2009 ilipoonekana bayana kuwa misamaha ya kodi kwa shughuli za Kanisa inatumiwa vibaya (mfano, parokia moja kuingiza Land Cruiser nne ndani ya mwaka mmoja), alipotaja hilo Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, ikawa ugomvi mkubwa. Licha ya kuwa misamaha hiyo haikuondolewa, Kanisa likawa limekata shauri, halimtaki tena Rais Kikwete... Kabla ya mwezi mmoja kupita kuanzia hotuba hiyo ya Waziri wa Fedha, tayari Tume maalum ya Kanisa Katoliki ikawa imetoa waraka mrefu wa vipaumbele vya uchaguzi mkuu wa 2010, ikiita Ilani, ukaongezwa pia Waraka rasmi wa Kanisa kwa parokia zote nchini kwa suala hilo. Ilikuwa kinyume kabisa na Katiba ya nchi, kutenga dini na siasa. Waumini wakapuuzia amri batili za Kanisa kwa jimbo fulani mkoani Mbeya au Rukwa, wakamfanyia kampeni mgombea wa CCM aliyewaudhi Maaskofu halafu akaomba radhi kiungwana yakaisha; wananchi hao walitengwa na Kanisa. Yote hiyo Maaskofu hawatambui kuwa ni kuinua kiburi mbele za Mungu. Ni wakati huo ambapo Maaskofu walitoa tangazo kuwa wangependelea atokee mtu mwadilifu, mcha Mungu (ina maana kwa upande wa upinzani, kwani mgombea wa CCM kwa uchaguzi mkuu 2010 alikuwa anafahamika) halafu wao

AN-NUUR

Kanisa nchini limeingia katika mateso?

Maaskofu wanapolalamikia matokeo ya uasi wao

RAIS Barack Obama wa Marekani (kushoto) wakiwa na Papa mstaafu Benedict XVI (katikati). Kulia ni mkewe Michelle Obama. wao, na bila kuweza kutumia kuchinja ni kosa, kwani hakuna uwongo. Katika hali kama hii, maelekezo ya maandiko (nukuu ajira ya kuchinja bali ya kuuza tutaamnini vipi kuwa hata hayo walizotumia kuainisha dhana nyama bucha, n.k. Na hata yaliyochomwa kweli hazikuwa ya mateso na jinsi hali nchini ingekuwepo ajira moja kila njama (inside job) ili kulazimisha inavyoendana na mazingira kijiji au tarafa ya kuchinja serikali kuchukua hatua fulani hayo). Ina maana kuwa Kanisa bucha au katika sherehe, halafu dhidi ya Waislamu? Hali ya sasa ni tete kiimani. limeshindwa kujifunza kuwa akawepo mzee wa Kiislamu lina mchango katika mifarakano kufanya kazi hiyo, tuseme haki Watu kukosa imani na mifumo hii. ya Mkristo inavunjwa kwa njia iliyopo kuwa inatenda haki, Tuchukie tukio la mwisho gani? Hivi akichinja mtu ambaye na Maaskofu kuwa ndiyo ambalo ndilo limeleta wasiwasi hajafundishwa kanuni hiyo chanzo cha hali hiyo. Ni suala mkubwa kuhusu hatma ya na hivyo hataifuata, kwani ni linalotoka mbali, lakini mwaka amani na mfungamano kijamii kanuni ya dini, halafu Waislamu huu wa 2013 ni mwaka wa 20 kati ya Waislamu na Wakristo, wote wakasusia nyama au tafrija tangu mkutano mwingine wa kuwa lilianzia katika baadhi hiyo, Maaskofu watafaidika nini Maaskofu, ambao ulifanyika Bagamoyo (si ajabu kwa ya wakereketwa wa Kikristo hasa? kuhoji haki ya Waislamu kuwa Suala hapa ni kushindwa kwa maelekeo ya hayati Mwalimu na dhamana ya kuchinja, mradi baadhi ya wahubiri wakereketwa Nyerere) mwezi Mei 1993 kutoa nyama husika ni ya kutumiwa kuona umuhimu wa kanuni hiyo, tamko kumtahadharisha Rais na watu wengi. Kama ni suala la na sasa wanaanzisha ukinzani Ali Hassan Mwinyi aache sera chakula cha familia moja ambako kuhusu haki ya Wakristo zake za kuuza nchi, yaani aache hakuna sherehe, kanuni hiyo kuchinja ambao ni kutaka kufuatilia mageuzi ya uchumi, haiwezi kutumika, kwa mfano tu ugomvi. Halafu inaelekea asibinafsishe. kwa matukio kama ubatizo au Maaskofu hawajaelewa kuwa Matokeo ya tangazo hilo kipaimara. Lakini inapokuwa ni tukio hilo la kuchinja ni alama na msisitizo kuhusu suala hilo harusi, au tafrija nyingine hata nzito ki-Biblia, kwani analitaja alioufanya Mwalimu katika iwe na uhusiano wa mbali na Masihi kwa uzito kiasi. hadhara kadhaa (ile ya Hoteli dini, budi itumike. Ukiangalia kwa karibu ya Kilimanjaro, halafu May Sababu ni kuwa kwa vile unakuta maeneo yote ya ukinzani Day mkoani Mbeya pia mwaka idadi ya Waislamu na Wakristo msingi wake ni uasi huu au ule, 1995) ni kukataa kuendeleza nchini katika maeneo mengi iwe ni Maaskofu wenyewe katika mageuzi na kuweka mkazo tu inashabihiana, si rahisi kuwa na vikao vyao, au ni wakereketwa katika ukusanyaji kodi. Matokeo shughuli yeyote ya kadamnasi katika ngazi fulani, hasa hilo yake ni kuwa tija ya uchumi halafu wawepo Wakristo peke la kuchinja. Yale makubwa inapungua, unakua kwa ujazo tu yao, bila Waislamu kuwepo. zaidi kwa mfano la kuchomwa (wingi wa dhahabu inayouzwa Kwa maana hiyo, kwa vile ipo makanisa, ingebidi Maaskofu nje, mazao, vito vya thamani, kanuni na amri maalum kuhusu wajiulize pia yametoka wapi, au hata samaki, utalii) lakini kuchinja katika Uislamu, na na siyo tu kwanini eti polisi unakwama kitija. Matokeo yake katika Ukristo hakuna kanuni hawajazuia au kuwakamata wote ni hali za maisha kuwa ngumu na kama hiyo, imekuwa kawaida, waliofanya vitendo hivyo, n.k. kwa vile Wakristo wana nafasi kwa ajili ya ujirani mwema, K w a m f a n o m a k a n i s a kubwa zaidi serikalini na hata kuachia jukumu hilo wale walio yalichomwa moto eneo la mashirika, inaonekana wao ndio na kanuni na wanaoifuata, Mbagala kwa hasira ya kijana wanafaidi hali hiyo; si ajabu kusiwe na manunguniko au mmoja kutoka familia ya malalamiko yakielekea huko. Isitoshe, licha ya kuwa mengi kuachiana haa ya kijamii, kwa wakereketwa kushindana na suala hilo. Kuanza kuivuruga mwenzie na kutaka kuthibitisha kati ya yale yalioandikwa na kanuni yenyewe ndiyo udini ubishi wake wa kuichafua Kurani wanahistoria wa kipindi cha halisi. Na hii ni fujo inaletwa kwa mkojo wake. Ni wazi tukio kukia uhuru kama Mohammed na Wakristo wanaoshabikia kama hilo linachukiza. Lakini Said, yanaonekana kutokuwa na jambo hili. pia tusisahau kuwa kuna watu mizania kwa upande wa wahakiki Inashangaza kuwa Maaskofu walidai kuwa kuna makanisa wa Kikristo, kuna mantiki halisi h a w a j a e l e w a k u w a k i l e y a m e c h o m w a Yo m b o n a ya ukinzani huo. Ingekuwa kinachoitwa haki ya Wakristo ilipofuatiliwa ikakutwa kuwa ni Kanisa halikuzuia juhudi za Rais

Inaendelea Uk. 11

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM) TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF); Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro; Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro; Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro; Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa. Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki. Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake. Ndugu Mkuu wa Chuo; Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake. Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili. Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo. Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya AlBarakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili. Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuw a na w anafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari. Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote. Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri. Ndugu Mkuu wa Chuo; Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuw a na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa. Serikali itaendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana. Tu m e w e k a m a z i n g i r a mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo Inaendelea Uk. 9

RAIS Jakaya Kikwete akihutubia siku ya uzinduzi wa Kitivo cha Sayansi Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro Alhamisi iliyopita. Waliokaa kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Hajat Mwantumu Mahiza. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera akifuatiwa na Bw. Saggaf

MAKAMU Mkuu wa Chuo MUM, Prof. Hamza Njozi akimpa maelezo Rais Kikwete katika moja ya maabara ya sayansi chuoni hapo. huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii. Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa kutoa ni moyo, usambe si utajiri. Ndugu Mkuu wa Chuo; Mabibi na Mabwana; Kwa miaka mingi madhehebu ya dini na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini. Kwa miaka mingi mashirika na taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia. Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini. Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF. Hongereni sana. Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu. Ndugu Mkuu wa Chuo; Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu tangu ya awali hadi elimu ya juu. Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM) TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Inatoka Uk. 8 vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14 tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi. Ndugu Mkuu wa Chuo; Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi. Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha v i j a n a n a Wa t a n z a n i a wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo. Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772. Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada. Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kukia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini. Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini. Ndugu Mkuu wa Chuo; Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo. Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo. Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili. Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu raki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo. Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo. Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza, mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini. Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au vitivo sehemu mbalimbali nchini. Ndugu Mkuu wa Chuo; Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema. Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake. Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia Inaendelea Uk. 11

Mkuu wa Chuo hicho Hajat Mwantumu Mahiz akihutubia siku ya uzinduzi wa Kitivo cha Sayansi Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro Alhamisi iliyopita.

RAIS Kikwete akizindua rasmi Kitivo cha Sayansi Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro Alhamisi iliyopita. zizunguke ili tupunguze kiasi Nimefurahishwa na Ndugu Mkuu wa Chuo; kinachotolewa na bajeti ya kufarijika sana kusikia kuwa Nimefurahi sana, pia, serikali kila mwaka. ubora wa elimu inayotolewa kusikia kuwa Chuo kinatoa Ndugu Mkuu wa Chuo; h a p a c h u o n i n i j a m b o mafunzo ya ualimu. Bila ya Mabibi na Mabwana; lin alo p ew a k ip au mb ele shaka mnaelewa kwa nini Niruhusuni nitumie nafasi cha kwanza. Jambo hili ni nafurahi. Tuna uhaba mkubwa hii kukupongeza wewe Mkuu muhimu sana kulisisitiza wa walimu nchini hivyo Chuo wa Chuo, Makamu Mkuu kwani tunataka wahitimu cho chote kinachotoa mafunzo wa Chuo, Wahadhiri na wa Chuo hiki wafanane na ya ualimu hunifurahisha. Jumuiya nzima ya Chuo wahitimu wa Chuo chochote E n d e l e e n i k u i m a r i s h a Kikuu hiki kwa kazi kubwa kizuri nchini na hata duniani. mafunzo hayo ili Chuo chenu na nzuri muifanyayo ya Ningependa kuona wahitimu kitambulike na kukubalika kuendeleza na kuboresha wa Chuo hiki wanagombewa nchini kwa sifa ya kutoa Chuo. Tumeshuhudia ujenzi katika soko la ajira. Hili walimu wazuri. Walimu wa wa jengo nililolifungua ni jambo linalowezekana. kutoka Chuo hiki wawe wale leo. Tumeona mafanikio Kinachotakiwa ni uamuzi wanaojua vyema masomo kwa upande wa ongezeko wa Baraza na Seneti kuwa wanayofundisha, mahiri la idadi ya wanafunzi, iwe hivyo na kuchukua hatua kufundisha na waadilifu. walimu, wafanyakazi na zipasazo. Sina shaka kuwa Naomba pia mtoe kipaumbele fani zinazofundishwa katika mnaweza kufanya hivyo. cha juu kwa mafunzo ya kipindi hiki kifupi cha uhai Hakika mnaweza, na sote ualimu wa masomo ya sayansi wa Chuo hiki. kwa umoja wetu tunaweza. na hisabati. Mkifanya hivyo,

10

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

Kutekwa Kibanda: Waandishi waache uchochezi!


anajaribu kuwashawishi wananchi wakubali kuwa Bw. Absolom Kibanda, kateswa kwa sababu ya imani yake ya Kikristo. Huo ni uchochezi mbaya usioona haya. Historia iwe ikiwafundisha watu kama MSOMAJI RAIA kuwa si utamaduni wa Kiislam kuwatesa watu kwa sababu ya imani yao. Vita vya Msalaba vilivyo anza karne ya kumi na moja vinaeleza kiasi gani ukatili wa Wakristo walivyowatesa Waislam baada ya wao kuuteka mji wa Jerusalem. Lakini baada ya kuuteka tena mji huo kutoka mikononi mwa Wakristo, Jemedari hodari Salah UdDin Al-Ayyubi (ama Saladin huko nchi za Magharibi) hakuwatesa hata kidogo Wakristo na wenyeji wa Jerusalem na aliwaruhusu kutekeleza matakwa ya imani ya dini zao za Kiyahudi na Kikristo. Halafu Waislam walitawala nchi ya Hispania kwa muda wa miaka takriban mia saba (700). Wakristo waliruhusiwa kutekeleza matakwa ya imani yao bila kukatazwa. Kweli kulitokea Wananchi wachache walioadhibiwa kwa kumtukana Mtume Muhammad SAW. Historia inaonyesha kuwa hawa walikuwa wakitukana kwa makusudi kabisa ili waadhibiwe na kuweza kuupaka matope Uislam. Wengi wa hawa walikuwa ni viongozi wa Ukristo katika nchi kama vile Mabruda na watawa (monks). Linganisha hayo na yale yaliyotokea baada ya nchi hiyo kutekwa tena na hao Wahispania. The Inquisition ni kitendo cha aibu kwa Ukristo mpaka leo hii. Mayahudi na Waislam waliteswa sana. Kwamba Uislam ulienezwa kwa upanga ni uwongo mtupu. Mtume Muhammad (SAW) alikimbia kutoka Makka kwa vile wale walipokuwa wakiabudu masanamu walitaka kumwuwa. Hii ni historia niliyofundishwa shule ya sekondari takriban miaka sitini iliyopita, Mwalimu akiwa muumini Mkristo wa madh-hebi ya CMS (Muanglikana) kutoka Ubondei na akiwa mzee wa kanisa. Wale vijana wachache wa Kikristo wanaosoma katika shule za Kiislam kamwe hawalazimishwi kuingia misikitini kuswali, ingawa takriba kila palipo na shule ya Kiislam pana msikiti. Hayo ndio yalivyo mafundisho ya Kiislam. Linganisha kitendo hicho cha kistaarabu na yanayotendeka katika shule zinazoendeshwa na Makanisa. Huko kila mtoto, hata kama sio Mkristo analazimishwa kuhudhuria misa. Hivyo bila kujali vijana hawa wa Kiislam wanalazimishwa kutenda dhambi na kukufuru kila siku. Pamoja na ubishi usio na msingi unaotolewa kila siku, hakuna kinyume kuwa wengi wa wale waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru nchi hii walikuwa wale wazee kwa vijana wa Kiislam wasiokuwa na elimu. Ni hawa Waislam walio mzika Muislam mwenzao wakati yuko hai, AlMarhum S h e i k h M z e e Ta q d i r. Aliyoyatabiri yamekuja na leo Waislam wanamkumbuka. Hapa historia inajirudia kuwa Waislam hawana haja ya kumtesa Mkristo kufanikisha azma ya kutekeleza mafundisho ya dini yao. Hata kama mtu huyo ni mwandishi wa habari aliye na chuki dhidi ya Uislam. Padri Evarist Mushi, ameuawa huko Zanzibar na kwa udhaifu wa fikira, kuchoka kukiri uhalifu huo umehusishwa na Uislam. Hawa wanaosema hivyo ni watu waliosoma sana tu na elimu inayosemekana humwezesha msomi kukiri na kuchanganua mambo kwa marefu na mapana. Lakini kwa sababu ya chuki, basi ni rahisi kuusingizia Uislam na Waislam kwa kitendo hicho cha jinai. Ni aibu sana kwa wasomi. Hakika hoja ni nyepesi kuweza kuepukana na hayo ya uchochezi. Kwa asili mia tisini na nane (98%) muhalifu yeyote Zanzibar atakuwa Muislam. Sasa ni Uislam wake ama roho yake tu mbaya ndiyo itamtuma kufanya uhalifu? Kwa hali ilivyo hivi leo huko Zanzibar, inawezekana kabisa kuwa kiini cha uhalifu huo ni siasa zinazohusu Muungano. Sasa vipi siasa ihusishwe na Uislam? Acheni uchochezi. Hata hivyo Sheikh Saroga alimwagiwa tindi kali limdhuru sana tu, pia yuko Sheikh mwingine Kaskazini mwa Unguja alikatwakatwa mapanga mpaka akafa. Yo t e h a y a w a a n d i s h i

Na Khalid S Mtwangi

INAWEZEKANA kuwa mwandishi anayejiita Msomaji Raia katika gazeti la Raia Mwema la tarehe Machi 13, kaandika makala yake kwa ufasaha sana na kaona hoja zake ni nzito kiasi kuwa ndio ukweli mtupu. Labda ni hivyo, lakini kwa mtu mwenye busara na anayeitakia nchi hii mema, atabaini kuwa huyu Mheshimiwa ni mchochezi nambari wani na haitakii nchi yetu mema hata kidogo. Kwa Kiingereza huitwa BIGOT; bahati mbaya nashindwa kupata tafsiri ya kutosha ya Kiswahili lakini ni tegemeo kuwa wasomaji wako wengi wataelewa kinachotakiwa kusemwa hapa. Hoja hii hasa inatokana na hoja zake dhaifu sana za kujaribu kuuhusisha Uislam na hayo yaliyompata mwandishi mwenzie Bw. Absalom Kibanda. Inakubalika kuwa katika historia ya dunia kuna wakati Wakristo walikuwa wakiteswa sana, kama vile wakati wa utawala wa Warumi huko Ulaya. Imani yao iliwaponza na mateso yalikuwa ya kikatili kweli kweli, mtu yeyote aliyetembelea the Collosseum huko Rome na kupata maelezo jinsi gani, bila shaka atawaonea huruma watu hawa waliokuwa wakidai ni wafuasi wa Yesu. Shuleni tulisoma mkasa wa Androclese and the Lion. Lakini sio WaRumi tu ndio waliowatesa WaKristo. Baada ya Mkutano Mkuu wa Nicaea (Council of Nicaea) mwaka 325 AD, ambao ulihudhuriwa na Maaskofu wengi wa Ulaya na Asia Minor, wale Maaskofu waliokataa kukubali nadharia ya uungu wa Yesu waliteswa sana kwa amri ya Emperor Constantine, ambaye ndiye aliyeitisha mkutano huo ingawa yeye alikuwa mpagani. Ila ni uwongo dhahiri kutoa hoja kwamba baadhi ya Wakristo Tanzania wanateswa kwa sababu ya Ukristo wao. Mwandishi MSOMAJI RAIA

ABSOLOM Kibanda kama huyu MSOMAJI RAIA hawayakuyaona na hawakusomeka wakichambua mahalifu hayo, kama alivyo jigamba kwa mkasa wa Bw. Absolom Kibanda. Uchochezi ni kosa la jinai. Hakika taarifa juu ya shule ya Waislam huko Ukerewe ni ya uwongo mtupu na wanaohusika na taasisi ile wameamua tu kulifikisha jambo hili mahakamani. Waasisi na waanzilishi wa taasisi hiyo ni wazee wenye heshima zao, ambao baadhi yao wanaishi Mwanza; pia taasisi hiyo ni ya miaka mingi; sasa leo hii ndio inahusishwa na Al Shabab. Huo ni uchokozi na uchochezi kwa sababu ni moja ya taasisi za elimu za Kiislam zinazoendeshwa kwa ufanisi. Lazima ipigwe vita. MfumoKristo hauwezi kustahili ushindani. Anajidai kuandika Dini fulani ilihali kwa maandishi yake kila msomaji atajua tu ile inayosingiziwa ni Uislam. Hawa wazee wenye heshima zao hawana sababu kabisa ya kumdhuru Bw. Absolom Kibanda. H i v i Wa n y a k y u s a walioendelea sana nchini humu ni hawa tu aliowataja huyu Mheshimiwa MSOMAJI RAIA? Ninaye shemeji yangu Mnyakyusa Mkristo, ambaye kaendelea sana na kashika wadhifa wa juu katika mashirika ya umma na sasa kampuni binafsi. Mbona yeye hajaguswa na Muislam yeyote yule, ingawa hapo alipo ni pahala ambapo ni Uislam ulio na nguvu zaidi. Kweli yeye sio mwanasiasa. Kweli inajulikana kwamba siasa ni mchezo mchafu; kuna baadhi ya watanzania wanaamini kwamba kifo cha Al Marhum Sheikh Kaluta Amri Abedi, kinahusishwa na siasa. Naye Al Marhum Kighoma Malima, pia alikufa ghafla ingawa kifo kinaweza kutafsiriwa kuwa ni amri ya Mungu, lakini inasemekana palikuwa na mkono wa mtu. Hawa wote walikuwa wanasiasa lakini si Wanyakyusa. Kufuatana na haya yaliyojitokeza hivi juzi juu ya mkasa huu, bado MSOMAJI RAIA ana amini Waislam wanahusika na kutekwa kwa Kibanda? Kwa sababau ya Uislam wao? Inaelekea kuwa ule ugonjwa wa BIGOTRY unawashinda nguvu waandishi. Ni ugonjwa wa akili ambao sio rahisi kuutibu. Lakini basi waache uchochezi!

11

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM) TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Inatoka Uk. 9 mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo. Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo? Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana. Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro; Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu. Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa Inatoka Uk. 7
watamuunga mkono. Karibu na kampeni kuanza, CHADEMA ikamwinua Dk. Wilibrod Slaa, Padri mwasi mwenye ugomvi wa wazi katika masuala ya ndoa. Alikuwa wa kwanza katika kura za maoni jimbo la Karatu mwaka 1995 na vikao vya CCM vikamwondoa, lakini kwa vile havitaji sababu, amekuwa akipita akisema ni kutokana na siasa za mwenzetu. Ni wazi kuwa hakuwa mgombea mwadilifu na mcha Mungu na Kanisa linadhani linamdanganya Mungu (ki-Kristo, ni kumdhihaki Roho Mtakatifu) kwa udini huo. Uasi wa Maaskofu mbele za Mungu haukuishia hapo. Waliposhindwa, wakaanza propaganda nzito kuwa mgombea wao alipata asilimia 64 za kura halafu Idara ya Usalama wa Taifa ikapangua kura hizo na kumjazia mgombea wa CCM - madai ambayo yalikia hata kutajwa katika mimbari, kuzikejeli misa

BAADHI ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro. hali ya juu. Ihakikishwe kuwa Ndugu Wanafunzi wa iliyowaleta hapa ya kujifunza mipango hiyo inatekelezwa Chuo cha Waislamu cha mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kwa ukamilifu. Morogoro; Aidha jumuiya yote inao Naomba wote muone fahari kuisomea. Vishawishi ni wajibu wa kufanya kazi kwa ya kuwa wanafunzi katika vingi na wapo watu wengi bidii, ubunifu, maarifa na Chuo cha kihistoria hapa wanaopanga kuwashawishi weledi ili dhima hiyo ya nchini. Nawasihi mjitume mtumie muda wenu adhimu ufanya wanayoyataka Chuo iweze kutimizwa kwa kwa kadri ya uwezo na vipaji k wao ambayo mkishiriki ukamilifu. Timizeni wajibu mlivyopewa na Mwenyezi huwatoa kwenye malengo wenu ipasavyo ili jina la Chuo Mungu mfanikishe kile na kutekeleza yao. Mambo Kikuu cha Waislamu cha kilichowaleta. Jifunzeni ya dunia ya nje ya Chuo ni Morogoro likue haraka. Sifa kwa bidii mfaulu vizuri ili mengi huna budi kutambua yake isambae na kuvuma kote mkihitimu muwe kielelezo lipi ufanye na lipi usifanye kwa wakati gani! nchini. Chuo kifanye vizuri kizuri cha mafanikio na na Mwanafunzi wa Chuo ili wanafunzi waone fahari ubora wa Chuo Kikuu Cha Kikuu ni mtu mzima, si kuwa wahitimu wa Chuo Waislamu cha Morogoro. mtoto. Lazima ujue kuwa hiki. Chuo ambacho, wazazi Muwe Mabalozi na kioo u n a w a j i b i k a k w a k i l a wapende kuleta vijana wao cha ufanisi wa Chuo hiki. unaloamua na kutenda. Amua kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Nawasihi mjiepushe na kuwajibika vizuri. Fikiri kabla Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mambo yatakayowapunguzia ya kutenda, changanua lipi ni mimi nina imani mnaweza, m u d a a u k u w a o n d o a lipi kabla ya kufanya uamuzi katika shughuli ya msingi wa kile unachotaka kufanya. fanyeni kweli.

Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi. Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye. Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako. Utafaulu au kufeli wewe. Utapata shahada wewe na si mtu mwingine. Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe. Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako. Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani. Mabibi na Mabwana; Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo. Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
nitamshauri Rais juu ya jambo hilo na likapitishwa. Papa mpya alikuwa akisema Wakristo wakwepe mbinu za shetani: hivi wanazijua? (Mwandishi wa makala hii ni msomaji wa An nuur anapatikana kwa simu namba 0658 522 495)

kwa kudunduliza uwongo. Kutokana na riwaya hiyo ya kura za mgombea wao kuondolewa (aliyepata asilimia 64 ya kura za urais lakini hana wabunge wa kuchaguliwa zaidi ya 20...!) Maaskofu wakawa wamepata mahali pa kusimama kudai iandikwe Katiba Mpya. Sababu ni kuondoa mapungufu yaliyopo ili mgombea anayeungwa mkono na watu (yaani Kanisa) asiibiwe kura...! Ina maana Kanisa liandike Katiba, limpitishe mtu. Kinyume cha matarajio ya Maaskofu, ambao wiki moja baada ya kuapishwa Baraza la Mawaziri mwisho wa Novemba 2010 walishawasha moto wa madai ya Katiba Mpya, kutoka Longido hadi Kyela, na kutoka Ngara hadi Mikindani, wakidai kwa sauti moja Katiba Mpya, hiyo ndiyo inayolibamiza

Kanisa nchini limeingia katika mateso?


ukutani Kanisa. Kwa hatua ya kuweka kila kitu mezani kijadiliwe upya, yale madai ambayo kwa miaka mingi serikali imeyafunika na kuyapiga chenga, sasa yanakuwa sehemu ya madai ya Katiba. Makundi tofauti nchini yanakuja na madai yao ya Katiba, na kuanza kuutikisa mfumo ili usipuuzie madai yao; hakuna ajuaye kama Muungano utapona, na ili uvunjike harakati zitainuliwa, na Kanisa haliwezi kupanga ziweje. Wanasema panda upepo, uvune tufani(sow the wind, reap the whirlwind). Na hiyo ndiyo mantiki ya kinachotokea sasa, kuwa suala hili la kuweka kila kitu mezani kuhusu hatma ya nchi linaingiza taifa katika giza, kwa amri ya Maaskofu. Waziri wa Sheria wakati huo Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu

Frederick Werema, walisema hatuhitaji Katiba Mpya, halafu akainuka Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, (Mzee wa Kanisa?) akasema

SHAMBA LINAUZWA
SHAMBA LA EKARI 14 LINAUZWA KWA HARAKA LIPO CHAMAZI-DOVYA DAR ES SALAAM BEI NI MAELEWANO KWA MAWASILIANO: PIGA SIMU: 0759 450425 0784 463207 0754 479783 WAHI MAPEMA BAHATI NI YAKO

12
Kalamu nimeishika, kwa kheri si songombingo, Nabtadi kuandika, ukweli si longolongo, Wandishi kuwamulika, wa habari ndilo lengo, Ni wazushi na warongo, Wanahabari vishoka. Kuweta nalazimika, mapaparazi wa Bongo, Wanahabari vishoka, kwa wao mtimanyongo, Si wote wazi naweka, waandikao mafyongo, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Wandikayo bila shaka, makusudi si kwa nongo, Fuadini yanatoka, kwa ghaidhi na usongo, Maadili wayazika, kwa uzushi na urongo, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Habarizo za kupika, zadhihirisha usungo, Walo wenyewe jivika, kwa nadhari za matongo, Si jarima kuwaweka, wa usadi mrengo, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Wengi wao kwa hakika, lengolo kusaka bingo, Hivyo ndivyo kwa hakika, walivyo si masimango, Silikayo kwa hakika, si makengeza ni chongo, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Kwayo chongo waporomoka, kwa la upofu korongo, Uoniwo wapofuka, kwa wao hasi mpango, Natijaye kwathirika, fani kwa wao mchango, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Wafaa kubadilika, kwa kuenzi lao jengo, Tasniayo kwenzika, walizibe hili pengo, Hapo wataheshimika, na kutoitwa warongo, Ni wazushi na warongo, wanahabari vishoka. Kaditama nimeka, nane nafunga mlango, Lengo risala kuka, kwa waandishi wa Bongo, Kalamu chini naweka, kwaherini wana nzengo, WA N A H A B A R I V I S H O K A , N I WA Z U S H I N A WARONGO.

Mashairi/Barua/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

wanahabari vishoka !

Tunataka kuwaona watuhumiwa mahakamani


Ndugu Mhariri, Assalaam alaikum. HUWA wakati mwengine sitaki kuandika chochote au kusema kitu. Lakini kila siku mambo yanazidi; na chumvi inazidi kutiwa Zanzibar, na hatimaye mantiki inatoweka katika kra za binadamu. Sasa hivi tumesikia kuwa kuna watuhumiwa wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauwaji ya Padri Evarist Mushi, lakini, kama watuhimiwa wamekamatwa tokea tarehe 17 Februari 2013 (baadhi yao), kwa nini hatusikii kuwa wamefikishwa mahakamani? Nakiri bado ile sheria ya saa 48 tokea kukamatwa kwako ufikishwe mahakamani bado ipo. Tuseme na hawa waliokamatwa juzi juzi tu, na hao waliokuja kutusaidia (kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Mussa Ali Musa) kuna watu wapya wamekamatwa hatuoni kufikishwa mahakamani. Au hawa sheria zao nyengine kwa vile imemhusu Padri? Bado imekuwa kitendawili kwangu: kwa nini pia upelelezi usianzie pale kanisani, au katika mfumo mzima wa kanisa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla? Upelelezi huu umekuwa upande mmoja tu. Ni kweli khulka ya binadamu siku zote inakuwa ina upendeleo fulani wa upande mmoja, lakini katika kazi kama hizi kinachotakiwa ni ukweli na uadilifu, sio kuegemea upande mmoja tu. Hapa ndipo inapozuka shaka kubwa miongoni mwetu kuamini au kutoamini mfumo mzima wa utoaji haki, utendaji haki. Sisi siku zote tunaingia ndani ya tukio, kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi. Lakini tujue kuwa polisi kama taasisi, sidhani kama wananchi wengi wanaiamini vya kutosha. Mnakumbuka lile tukio la kuibiwa mfanya biashara Dar es Salaam juzi juzi tu; na pesa zilizopatikana waligawana jamaa! Hiyo ripoti ya Afande Suleiman Kova iko wapi? Kama polisi imefikia kufanya haya na mengine mengi itakuaje? Tumuamini nani? Mwananchi Zanzibar

Nimepoteza mdomo!
Naanza kuwasalimu, kwa salamu ya Imani, Asalam aleykhumu, wa Bara na Visiwani, Nimekamata kalamu, kuwatanabahisheni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Subira jambo adili, inadumisha amani, Itatuweka kwambali, nanjama zake shetwani, Tupinge tusikubali, kuingia mtegoni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Ajenda imejicha, wanakusudia nini! Yahitaji kuchekecha, niya yao kubaini, Macho ukiyakicha, utaona ya mbeleni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Kuzibwa kwangu mdomo, wapowalo furahani, Wameibuwa msemo, mchochezi kifungoni, Athari zake mfumo, ndiyo hizo tambueni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Muda wamenitafuta, kuniingiza shimoni, Sababu wameipata, sasa nipo hukumuni, Kimya kwa miezi sita, sito sikika nchini, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Usiseme bilikuli, sitorejea hewani, Zitupilie kwa mbali, hisia hizo ni duni, Kukata ni ujahili, tamaa nisikizeni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Mtulie nawaasa, kazini na majumbani, Kisa hufata mkasa, ni yao matumaini, Kwa hili wakitukosa, watavunjika moyoni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Kaditama ninafunga, narejea vitabuni, Mkutubi si mganga, kutabiri ya mbeleni, Bali mimi ni malenga, nayaona ya usoni, Nimepoteza mdomo, sijapoteza akili. Isihaka Hemed Mzuzuri Morogoro.

Abuu Nyamkomogi MWANZA.

Ndugu Mhariri, Assalaam alaikum Quran inatuambia kuwa hawataridhika Mayahudi na Manasara, mpaka muwafuate mila na nyendo zao. Haya ni maneno ya mwenyezi Mungu. Kwa upande mwingine Mwalimu Nyerere amewahi kusema kuwa Azimio la Bunge kutaka kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano lilisukumwa na chuki waliokuwa nayo baadhi ya Wabunge dhidi ya Wanzibari na Waislamu. Mtu anapomchukia mtu atahakikisha anamfanyia visa na tna ili aharibikiwe. Mwalimu Nyerere anazungumzia chuki, kuwachukia Waislamu. Hapana shaka chuki hii ndio ile iliyowahi kuelezwa na Dr. Sivalon aliposema kuwa Uislamu ulionekana kama adui mkubwa. Hebu kiria iwapo utakuwa na idadi kubwa ya watendaji serikalini ambao wana chuki dhidi ya baadhi ya wananchi. Je, wananchi hao watatendewa haki? Si ndio haya tunayoyaona ambapo inatokea tukio kama lile la mauwaji ya Padiri ambapo kabla hata uchunguzi haujafanyika mtu anakurupuka na kudai kuwa Zanzibar kuna magaidi! Wakazi wengi wa Zanzibar ni Waislamu. Ukisema kuwa Zanzibar kuna magaidi unachofanya ni kuutangazia ulimwengu na jumuiya ya kimataifa iungane katika kuipiga vita Zanzibar. Inakuwa taabu sana kutenganisha haraka hii ya kuwatangazia ugaidi Zanzibar na ile chuki iliyotajwa katika Quran. Kauli na madai kama hayo ingaliweza kuwasha moto Tanzania ya ulipizaji kisasi kwa watu wasio na hatia. Hebu sikiliza maneno haya: Wakristo wakiona vurugu na mauaji dhidi yao

Chuki hii ni hatari


yakishamiri, wataingia mitaani na kuwafanyia fujo Waislamu, na amani haitakuwepo tena. Huu sasa ni wakati wa jeshi letu kuingia mitaani na kuhakikisha kikundi hicho kinaondolewa mara moja kabla hatujawa kama. Nigeria. Maneno hayo nimeyaona ndani ya gazeti la Jamhuri Februari 26- March 14,2013. Muandishi alijiita Angalieni Mpendu. Sasa hili neno Jeshi letu hili neno nalo ni zito kwa yule mtu anaefatilia mambo katika mitandao. Hivyo kusema Jeshi letu kuingia mitaani.

Unajuwa kuna chama cha wanajeshi wa kikristo chama hiki kinaitwa:- Association of military Christian Fellow Ships. ( AMCF), watu wote wanatakiwa wawe wamoja katika Yesu (All one in Christ Jesus). Na pia kuna hii Tume ya Majeshi ya Kivita ya Kikristo. Hebu kiria unapokuwa na hali kama hii halafu itokee vurugu la kusababisha jeshi kuingia mitaani, hali itakuwaje? IBRAHIM HUSSEIN 0715 - 498363 MOHD

Uongozi na Waislamu wa AL- Masjid Swalha Mwangia Kibiti Ruji wanaomba Msaada wa vifaa vya ujenzi wa kukarabati msikiti uliopo Mwangia kibiti Ruji. Vifaa vinavyo hitajika ni:Bati Futi 10 bati 20 Kechi 2 kwa 4 kwa 11= 25 Papi 2 kwa 3 kwa 11= 35 Funiko ya bati = 8 Misumari ya bati kg 5 Misumari ya moto nchi 4 kg 5 Mbao za madirisha 2 kwa 5 kwa 7 Nondo mm 16= 11 Waya wa dirisha ( Kashata) mita 30 Nyavu za mbu mita 30 Silingi bodi 4 kwa 8 = 70 Papi 2 kwa 2 kwa 11 = 120 Misumari ya silingi bodi kg 5 Misumari ya papi nchi 4 kg 8 Misumari ya moto nchi 3 kg 6 Funiko ya silingi bodi 5 Sement mifuko 10 Umeme solar 1 Rangi ya mafuta kopo 5 Rangi ya kopo 10 Kwa mawasiliano zaidi ka msikiti hapi au piga simu hizo au pia unaweza kutuma mchango wako kupitia namba hizo. Tigo 0658 98 77 14 au Voda 0766- 36 27 52

AL- Masjid Swalha Mwangia Kibiti Ruji

13
Na Mwandishi wetu,
HIYO ndio mada aliyoizungumzia Sheikh Abdallah Bawazir, katika semina ya siku mbili, iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha, mnamo tarehe 23 na 24 Februari. Semina hiyo ilidhaminiwa na The Islamic Call Society na kuratibiwa na Sheikh Twalib Ahmad. Walengwa wa semina hii walikuwa ni Makhatibu, Maimamu na Walinganiaji. Wahadhiri katika semina hiyo, walikuwa ni Sheikh Suleiman Amran Kilemile, Sheikh Twaha Suleiman Bane na Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir. Masheikh wote hao ni wajumbe katika Taasisi ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay-at). Katika semina hiyo Sheikh Bawazir alitoa mada yake yenye kichwa cha habari hapo juu, mbele ya Makhatibu/Maimamu wapatao tisini walio hudhuria semina hiyo. Katika kuwasilisha mada yake hiyo, pamoja na mengi aliyozungumza Sheikh alisema: Kuna njia mbili katika kukisha ujumbe kutoka kwa mtu/watu kwenda kwa mtu/watu, ambazo zote ni muhimu sana. Njia ya kwanza ni kufikisha ujumbe kupitia khutba (kusema) na ya pili ni kukisha ujumbe kwa njia ya maandishi (makala). Lakini njia muhimu zaidi ni hii ya khutba, kwa sababu ndio njia ya haraka zaidi na ndio yenye taathira zaidi katika akili za walengwa. Njia hii inawakutanisha pamoja, ana kwa ana Khatibu (muwasilisha khutba) na wakhutubiwa (hadhira lengwa) na hivyo kusababisha kupatikana taathira ya khutba kulingana na umahiri wa Khatibu. Akiendelea na mada yake, Sheikh Bawazir alizigawa hotuba zitolewazo katika minasaba mbalimbali katika maisha ya wanadamu, katika makundi matano yafuatayo: Hotuba za kidini, hotuba za kisiasa, hotuba za kutoa hukumu mahakamani, hotuba za kijeshi na hotuba za masuala ya kijamii. Akiyafafanua makundi matano hayo, khususan kundi la kwanza ambalo linajumuisha khutba za kidini hasa zile za mimbarini, Sheikh alisema kwa kawaida khutba hizo huwa ni fupi zinazotegemea sana maelezo kutoka ndani ya Qurani, Hadithi za Bwana Mtume na kauli za Maswahaba. Kinyume na hotuba za kisiasa, ambazo huwa ndefu na zinategemea matukio ya kisiasa zaidi au yale ya kihistoria. Katika kuwasilisha mada yake hiyo, Sheikh alisema ya kwamba kuna tofauti baina ya khutba na muhadhara, na hilo ndilo jambo ambalo Makhatibu wetu wengi wanashindwa kulitofautisha na natija inakuwa ni kuzigeuza khutba za Ijumaa kuwa muhadhara. Kwani makusudio makubwa ya khutba ni kukemea na kuonya mambo fulani mabaya yanayo tendeka

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013


mazuri katika kadhia nzima ya mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya. Na wala hawakubali kamwe nchi yao idhalilishwe, eti kwa sababu ya umaskini au sababu yoyote ile iwayo. Kuna kundi la Waislamu ambao wasioamini kwamba Allah (s.w.t.) anaweza kuwapa riziki zao bila ya wao kuwatapeli wenzao, kula rushwa au kuleta fitina baina ya kundi hili na lile. Au pengine hao hao ndio wanao sababisha mgongano baina ya dini kuu mbili nchini, kwa kuhamisha siri za huku na kuzipeleka kule kwa lengo la kupata maslahi yao binafsi. Na kuna kundi jingine la Waislamu dhaifu, wapo wapo tu. Hawatambui haki zao za kitaifa na wala hawana habari na yanayojiri nchini mwao. Hawa hawasomi magazeti, hawasikilizi redio, wala hawana hata muda wa kutazama luninga. Hao ndio wale wanao itaka Akhera bila ya Dunia. Makundi haya mawili, kundi la pili na kundi la tatu, ni makundi mabaya na yenye athari mbaya katika Uislamu. Na mwisho Sheikh Bawazir aliwasisitizia Makhatibu kuwazindua Waislamu ili wasiburuzwe na makundi hayo, ambayo hayana maslahi hapa duniani, wala kesho akhera.

AN-NUUR

Khutba ya Ijumaa ni njia ya haraka kukisha ujumbe

Sheikh Abdallah Bawazir


katika jamii ndani ya kipindi hicho au kuhimiza na kushinikiza mambo fulani muhimu, ili watu wasiyaache. Lakini muhadhara makusudio yake ni kuwafafanulia watu kadhia fulani, katika somo fulani, na hilo hufanyika baada ya utafiti na kufuatilia kwa makini kadhia husika na kwa sababu hiyo basi, hakuna njia ya kuepuka urefu wa muhadhara kuliko khutba. Akiendelea kuzungumza, Sheikh Bawazir alisisitiza kwamba katika khutba yanatajwa matukio muhimu yanayojiri katika jamii kwa wakati huo na ni wajibu wa Khatibu kutoa muongozo kwa waumini kuyaelekea matukio hayo. Na ni vema muongozo huo ukatoka ndani ya Qurani, Hadithi, matendo na kauli za Maswahaba na walio wafuatia na ukaenda sanjari na mazingira ya wakati na muktadha wa hali. Akitoa mfano wa matukio, Sheikh aliutaja ule mgomo wa madaktari, uliozigubika hospitali nchini mwaka juzi. Mgomo uliosababisha wagonjwa wengi kupoteza maisha yao kwa kukosa matibabu muafaka katika wakati munasibu. Katika hali/mazingira kama hayo, ni wajibu na ni jukumu la Makhatibu kuupinga mgomo huo na si kuupinga tu, bali kuelezea ubaya na athari mbaya zitokanazo na mgomo kama huo kwa jamii. Bila ya kusahau kuwakumbusha madaktari ambao ni sehemu ya waumini wao wanaowakhutubia, kwamba kuua kwa makusudi nje ya sababu za kisharia, ni hatia na dhambi kubwa mbele ya Mola Muumba uhai na umauti. Aidha ile filamu ya kumkashifu Bwana Mtume

Muhammad (s.a.w.) iliyotungwa huko Amerika. Au lile shinikizo la baadhi ya viongozi wa nchi za Ulaya, kutaka kuwapa haki wanaoingiliana kinyume na maumbile na kuhalalisha liwati chini ya mwavuli wa haki za binadamu. Yote hayo ni mambo ya kukemewa vikali juu ya mimbari na kuwahadharisha watu wasiukubali upotevu huo. Katika kumalizia mada yake, Sheikh Bawazir alisisitiza kwamba khutba zote ziwe na lengo la kudumisha amani nchini khususan na ulimwenguni kote kwa ujumla, na kuvumiliana baina ya makundi ya wanajamii kwa tofauti zao za madhehebu na kikanda. Aidha alikazia ya kwamba lengo mama la khutba liwe ni kuunganisha umma wa Kiislamu nchini. Kwani katika kipindi hiki hapa nchini kwetu Tanzania, Waislamu wamegawika katika makundi matatu makuu: Kuna kundi la Waislamu ambao ni wakereketwa wa Tanzania, ambao hawakubali kuachwa nyuma katika haki zao kama raia halali wa nchi hii. Hawa wanashiriki katika kila uchaguzi wa ngazi yoyote unao itishwa nchini, kama wanavyo shiriki katika kutoa maoni

NAFASI ZA MASOMO SUDAN 2013/2014

Osi ya Munazzamat Al-Daawa Al- Islamiya ( MDI) iliyopo Mbezi Beach-Tangi Bovu jijini Dar es Salaam, inapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa wale wote wanaotaka kujiunga na Chuo Kikuu cha INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, Khartoum Sudan. Kozi zinazotolewa ni; 1. Shahada ya kwanza katika Medicine, Pharmacy, Dentist, Nursing, Laboratory Sciences, Engineering, Electronics&electrical Engineering, Computer Science, Pure Science, Applied chemistry, Microbiology, Geology, Physics, Computer with Mathemtics. 2. Shahadaya kwanza katika Law & Sharia, Islamic studies, Economics, Administration, Political Science, Education&Administration, Curriculum&Methods of Teaching, Arts (Mass communication, Arabic, Geography, History, and General Psychology). 3. Diploma katika Education Fomu za maombi zinapatikana kwa Tsh. 10,000/= tu, kuanzia Tarehe 25 Machi- 6 Aprili, 2013 DAR ES SALAAM: katika ofisi ya Munazzamat iliopo Tangibovu- Mbezi Beach. MWANZA: Msikiti wa Rufiji uliopo Mtaa wa Rufiji na ZANZIBAR: katika ofisi ya Munazzamat ( Kituo cha kusaidia mayatima) kilichopo eneo la Mpendae kwa mchina mwisho, mkabala na skuli ya Kijangwani, saa 3:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana. Mtihani (Written Interview) utafanyika tarehe 13/4/2013, saa 2:00 asubuhi, siku ya Jumamosi katika Osi za MDI Dar es Salaam, Mwanza: Shule ya Msingi Mbugani Mtaa wa Unguja na katika Chuo cha Kiislam Zanzibar. Sifa za muombaji: Awe amemaliza Thanawiya au amemaliza kidato cha sita na amefaulu kwa kupata angalau Division Three kidato cha Nne. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0786 806662 au 0773 249015 au 0652 806662 au 0787 121283 au 0712 175985. Kwa upande wa Zanzibar piga simu No. 0777415835 au 0715 415835. Kwa upande wa Mwanza piga simu No. 0688 216644 au 0782 382434 au 0756 614916. Mr. Khamisi M. Liyenike K.n.y. Mkurugenzi, MDI, TZ

14

Makala/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013


ni muhusina wakamwita Muhusina akasema sayidi na Ally (R.A) nilikuwa napenda niitwe Baba Harbi (Baba Vita) na hiyo ni kawaida ya watu wajinga. Kwamba walikuwa wanapenda kuitwa majina ya Vita lakini Mtume (S.A.W) alikua anayachukia majina ya Vita lakini Mtume (S.A.W) akiishi nao vizuri hata na maadui zake na wagomvi wake pale ilipokia wakati wa vita vya badri wakamchimbia shimo na akatumbukia na kupasuka uso wake na kungoka meno wakaja baadhi ya Masahaba wakasema kwa nini hauwalaani ewe Mtume (S.A.W) akasema Mtume (S.A.W) Ewe mwenyezi Mungu waongoe watu wangu kwani wao hakuridhia Mtume (S.A.W) kuwalaani lakini akawaombea kuongoka kutoka kwa mwenyezi Mungu, naye Mtume alisubiri majibu toka kwa Mwenyezi Mungu na wengi wale waliokuwa wakimpiga vita katika vita ya uhudi waliingia katika Uislamu. Kwa hakika kweli yeye ni mpole na mwenye kuongoa kwa viumbe wote. Tuna muomba Mwenyezi Mungu aturehemu kwa baraka za Mtume (S.A.W) hapa dunia na huko Akhera na mwisho wa dua yetu ni kusema shukurani zote anastahiki mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote. Amini.

AN-NUUR

SHEIKH SALAH SAYED HUSSEIN MIFTAH,

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu na Rehema na Amani zimkie Mtukufu wa viumbe Mtume wetu Muhamad na jamaa zake na sahaba zake Amani zilizo nyingi hadi siku ya mwisho. Kila unapoandama kwetu mwezi wa mfungo sita kila mwaka tunakumbuka sisi Waislamu kuzaliwa kwa kiongozi Mwenye kuwabashiria watu habari njema Mtume wetu Muhamad (S.A.W) na hakika tumezoea Waislamu kumsifu Mtume wetu kwamba yeye ni Mtume Mpole. Kwa nini? Kwa kweli amekuja Mtume (S.A.W) ulimwenguni na Dunia inafuka moto wa ujinga tangu mashariki hadi

magharibi, watu walikuwa hawahukumiani kwa tabia nzuri bali kwa ujeuri na ubabe Mwenye nguvu (anamla ) namtafuna mnyonge, na Mkubwa anammeza mdogo na Ulimwengu wote walikuwa wanaishi kwa Dhuluma na ujinga akaja Mtume (S.A.W) ili kueneza upole katika ulimwengu huu. Na katika Qur- ani iliyoteremshwa Makka tunamsikia Mwenyezi Mungu katika Surat Anbayai baada ya kutuhadithia visa vya baadhi ya Mitume ambao wametanguli kabla ya Mtume wetu (S.A.W) tunamkuta Mwenyezi Mungu anamsemesha Mtume wake anasema (Na hatukukutuma wewe isipokuwa ni Rehema (mpole) kwa viumbe wote) Surat An-biyai Aya No. (107) na mwenendo wa misemo kama hii inaleta faida ya kudhibitisha na kufupisha. Kama wanavyosema wanachuoni wa Lugha ya Kiarabu. Kana kwamba anamwambia. Wewe haukuwa na jambo jengine isipokuwa ni Rehema (mpole) na upole huu sio kwa Waarabu. Na wala Upole huku kwa watu wa mashariki peke yao bali ni rehema kwa viumbe wote. Naye ni Mtume (S.A.W) amejizungumzia yeye

Upole wa MTUME (S.A.W)


Mwenyewe kuwe yeye ni Rehema yenye kuongoa hili ni neno fupi lenye maana kubwa kwa wenye kujua maana yake lina maanisha kuwa Mtume ni mtu aliye muongoa Mwenyezi Mungu ili awaokoe watu. Hapana ajabu juu ya kusema kuwa yeye ni Mtume Mwenye kuongoa na ni Rehema kwa viumbe wote. Umedhihiri upole huu katika tabia zake na Mwenendo wake (S.A.W) pia umedhihisha katika hadithi zake na suna zake (S.A.W) zimedhihiri pia katika sheria zake ambazo amekuja nazo (S.A.W) Ama kwa upande wa tabia zake na mwenendo wake alikuwa ni mpole kuliko watu wote alikuwa mbali tu na tabia mbaya na chuki moyo. Alikuwa anaishi vizuri na masahaba wake na wake zake na watoto wake wadogo kwa kila upole na huruma na ulaini. Na kwanini isiwe hivyo naye amemsemesha Mola wake kwa kusema (na kwa rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu umelainika kwao na lau ungekuwa mwenye moyo wange kukimbia wote ulionao) na pia amemsia mola wake mwishoni mwa Surat Tauba akasema

(kwa hakika amekujieni mtume kutokana na nyinyi wenyewe ni Mtukufu kwenu na mwenye hima na nyinyi kwa yanayokuguseni. Kwa waumini ni mpole Mwenye huruma) Surat Tauba aya ya (128) amesiwa Mtume (S.A.W) kuwa yeye ni mpole kuliko watu wote kwa kuishi vizuri na watu wote hadi kwa wake zake anasema kwa Aisha (R.A) (ewe Aisha hauingii upole katika kitu chochote isipokuwa kitapendeza. Na hauondoki upole katika kitu chochote isipokua kitachukiza) Alimjia sikumoja Sayida na Ally (S.A.W) pale alipozaliwa Hassan (R.A) kasema Mtume (S.A.W) (umemwita jina gani? akasema Ally (nimemwita vita.) akasema Mtume (S.A.W) (Bali huyo ni Hassani akamwita Hassan kisha akazaliwa kwa Ally (R.A) mtoto wa pili akamuuliza umemwita jina gani)?? Akasema nimemwita Vita) akasema Mtume (S.A.W) bali huyo ni Husein aka Mwita Hussein) kisha akazaliwa kwa Ally Mtoto wa tatu lakini alikufa bado mdogo akasema Mtume (S.A.W) Umemwita jina gani?) Akasema Ally (nimemwita Vita) akasema Mtume (S.A.W) bali huyo

NAFASI ZA MASOMO YA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014


WAISLAMU MNATANGAZIWA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI CHUO CHA UALIMU KIRINJIKO ISLAMIC A. SIFA: Muombaji awe na sifa zifuatazo: (a) Ufaulu wa kidato cha 4 usiopungua alama 27 katika kikao kimoja cha mtihani, asiwe amekaa zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize kidato cha nne. (b) Awe na credits 4 kiwango cha C endapo amekaa mtihani kwa vikao zaidi ya kimoja. (c) Kuhitimu kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza. B. MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE 1. Fomu ya maombi iambatanishwe na vyeti (leaving and Academic certicates) vya kidato cha 4 pamoja na picha ya hivi karibuni. 2. Fomu irudishwe siku ya kufanyiwa usaili tarehe 8/6/2013 saa 2:00 asubuhi. 3. Vituo vya usaili ni hivi vifuatavyo: (a) Kirinjiko Islamic T.C SAME (b) Ubungo Islamic T.C DSM (c) Nyasaka Islamic S.S. Mwanza 4. Majibu yatatolewa kwa watakaochaguliwa tu. 5. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi katika vituo vinavyoonekana ukurasa wa 15 katika tangazo la Shule.

15

TANGAZO

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014


Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


1.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

SAME KILIMANJARO MWANZA DAR ES SALAAM

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. 2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. 3. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. 4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /2013 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha. USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! Wabillah Tawiq MKURUGENZI

16

AN-NUUR
16
Alifafanua Sheikh huyo kwamba, kabla ya kuanza kwa ibada hiyo ya Itiqaaf, Waislamu wapewe dakika moja hadi mbili kunuia na kukabidhi kwa Mwenyezi Mungu wale ambao ni kikwazo katika harakati zao. Aidha alisema kuwa, v i o n g o z i w a Wa i s l a m u watapata fursa ya kuongea na Waislamu kuwaeleza mambo yanavyoendelea kuhusu kadhia mbalimbali dhidi yao na namna gani wanakabiliana nayo. Taarifa zaidi kutoka Shura ya Maimam zimeeleza kuwa wakati hayo yakifanyika, viongozi wa Kiislamu wanajipanga kwa hatua mbadala katika kudai kutekelezewa madai yao Serikalini. Hii inakuwa ni Ibada ya pili ya Itiqaf, kufanyika baada ya kutanguliwa na ile iliyoswaliwa katika Msikiti wa Kichangani (T.I.C) Magomeni, Jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki iliyopita.

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 22-28, 2013

AN-NUUR

Itiqaaf Masjid Tungi Temeke kesho


Na Bakari Mwakangwale
WAISLAMU Jijini Dar es Salaam, wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika ibada ya Itiqaaf, itakayo fanyika katika Msikiti wa Tungi, Temeke. Wito huo umetolewa na Imam wa Msikiti huo, Sheikh Shaaban Ibrahim, wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi mapema wiki hii. Alisema kwamba ibada hiyo ni katika mwendelezo wa maazimio ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na yanafanyiwa kazi na Shura ya Maimam, ambapo katika kikao chao Jumapili wiki iliyopita, taarifa za maazimio hayo zilitakiwa kukisha kwa Waislamu kupitia Misikiti yao. Sheikh Ibrahim, alisema lengo la Itiqafu hizo ni kumlilia na kumkabidhi Mwenyezi Mungu kile kinachoonekana kuwa ni dhulma dhidi ya Waislamu, kupuuzwa na kunyimwa haki zao.

Polisi waanza kuhoji Masheikh sakata la gesi Mtwara


Shura ya Maimamu Mtwara wasakamwaWamo Sheikh Jamaldin Chamwi, Abubakar Mbuki
Na Mwandishi WetuMtwara
TAARIFA kutoka mkoani Mtwara zinafahamisha kuwa kuanzia Machi 19, 2013, Masheikh mkoani humo wameanza kuhojiwa na polisi kuhusiana na kongamano walilolifanya Machi 18 katika viwanja vya Mashujaa. Orodha ya wanaohitajiwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa katika osi ya Kamanda Mkuu wa Polisi mkoa wa Mtwara ni ndefu, lakini walioanza kuhojiwa ni Sheikh Abubakar Mbuki na Saidi Mkopi. Orodha hiyo pia inawataja, Katibu wa Shura ya Maimamu mkoa wa Mtwara Sheikh Idrisa Hassan, Sheikh Mohamedi Salim, Sheikh Mtioli, Sheikh Katumbo, Imamu wa Masjid Nuur Mzee Dini pamoja na Katibu wa Msikiti wa Kiyangu ndugu Bakari Mchira. Imefahamika kuwa awali, Sheikh Jamaldin Chamwi hakuweza kufika katika mahojiano katika tarehe husika kwasababu alikuwa safari, lakini Machi 20, walitakiwa kuka tena kituoni hapo kwa mahojiano. Wa k a t i M a s h e i k h h a o wakisakwa na polisi kwa mahojiano juu ya kongamano hilo ambalo pia lilitolewa tamko la kuitaka serikali kutowatinisha raia wake, takriban wiki mbili zilizopita viongozi wa Chama C h a Wa n a n c h i C U F n a o walihojiwa. Taarifa iliyotolewa katika Msikiti wa An-Nuur mkoani humo, ilieleza kuwa miongoni mwa masuala aliyoelezwa Bw. Saidi Kulaga, ambaye ni Katibu wa Chama Cha CUF wilayani Mtwara, ni pamoja na kudaiwa kuwaambia watu wajiandae na kutengeneza mabomu ya samaki, ili kupiga ofisi na majengo ya serikali pamoja na nyumba ya ibada. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa msikiti huo umewataka Wananchi wa Mtwara kufahamu kinachoendelea na kwamba, jambo la muhimu ni kuwa na subira katika kipindi hicho kigumu. Katika mahojiano kwa baadhi ya waliohojiwa na polisi, ambao mwandishi wa habari hii alipata bahatika kufanya mahojiano nao, wamesema mahojiano yalijikita zaidi katika sakata la gesi ya Mtwara. Ust. Bakari Mchira, Katibu wa Msikiti wa Alhudaa-Kiyangu, amehusishwa na kuhamasisha vijana kupinga gesi isitoke Mtwara. Pia ameambiwa kuwa ndiye anayepita Misikitini kuhamasisha Waislamu wapinge gesi isitoke Mtwara kinyume na serikali inavyotaka. Aidha imedaiwa kuwa polisi wanamtuhumu kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya, madai aliyodai kuwa sio kweli. Kwa upande wake Sheikh Mohamed Salim, ambaye ndiye aliyesoma Tamko la Waislamu Januari 2013, Polisi walimuuliza kuwa Shura ya Maimamu imeanza lini na je, haikuanzishwa kwa ajili ya sakata la gesi. Polisi wamedaiwa kumtuhumu Sheikh Salim kuwa ndiye aliyeratibu shughuli zote hizo za kupinga gesi. Pia alitakiwa kueleza kwamba ana nafasi gani katika Shura ya Maimamu. Hata hivyo Sheikh Mohamed Salim, alieleza kuwa Shura ya Maimamu Mtwara ilianza takriban miaka miwili iliyopita na kwamba, sio kweli kuwa Shura hiyo imeibuka kipindi cha mzozo wa gesi, kwani hata katika sakata la waganga washirikina (maarufu kwa jina la Chipi-ai) Shura ililishughulikia na ilikutana na waandishi wa habari, na pia ilikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara katika kushughulikia kadhia hiyo. Polisi pia walidaiwa kutaka kujua nafasi ya Sheikh huyo katika Shura ya Maimamu, na kueleza kuwa yeye ni mjumbe tu wa Shura, lakini endapo ataagizwa kufanya chochote na uongozi wa Shura, basi hutekeleza agizo hilo, kama ambavyo aliagizwa kusoma tamko la siku hiyo. Kwa upande wa Sheikh Idrisa Hassan Lingondo, ambaye ni Katibu wa Shura ya Maimam mkoani humo, alitakiwa kutaja ni nani aliyewashawishi Shura ya Maimamu kuandaa Tamko na Kongamano. Aidha alitakiwa kumtaja mfadhili wa kongamano hilo na iwapo kulikuwa na mgeni rasmi katika kongamano lao. Imefahamika kuwa katika mahojiano hayo na polisi,

MZEE Bilal Waikela (kushoto) akiwa na bint yake Dite Waikela ambaye ni mmoja wa kati ya watuhumiwa katika kesi ya Sheikh Ponda wakiwa nje ya Mahakama ya Kisutu, Jumatano iliyopita jijini Dar es Salaam.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Sheikh Hassan Lingodo alijibu kuwa kilichowafanya kuandaa kongamano na kutoa tamko, ni malalamiko ya wananchi na muelekeo mbaya kwa jinsi wananchi hao walivyoona. Kulingana na majibu ya Sheikh Hassan Lingodo, ni kwamba ilibidi kutoa tamko ili kuitahadharisha serikali juu ya malalamiko hayo ya wananchi, lakini pia kufuatia ahadi ya Rais Mhe. Kikwete, kuwa wananchi wa Mtwara katika miaka ya hivi karibuni, watapaa kiuchumi kutokana na gesi na mengineyo. Lakini ghafla walimuona Waziri George Simbachawene, anakwenda kinyume na kauli ya Mhe. Rais. Aidha imefahamika kuwa Sheikh huyo alitakiwa kumtaja mfadhili wa Tamko lao, ambapo alieleza kuwa mfadhili wao ni waumini wa dini ya Kiislamu, ambao baadhi ya Misikiti walichangishana. Polisi pia walimtaka Sheikh huyo kueleza iwapo alikuwepo mgeni rasmi katika kongamano lao, ambapo alieleza kwamba hakukuwa na mgeni rasmi yeyote aliyeandaliwa katika kongamano hilo. Baada ya mahojiano hayo kumalizika, Masheikh wote walitolewa nje kwa dhamana hadi leo Ijumaa saa 3:00 asubuhi.

You might also like