Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU (JUMIKI)

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION


P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR

25 Mei, 2013

Bismillahir Rahmanir Rahiim

TAARIFA JUU YA HALI HALISI NA MATUKIO YA KESI INAYOWAKABILI VIONGOZI WA UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM, ZANZIBAR. 25 MEI, 2013
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam - JUMIKI, ni Jumuiya iliyosajiliwa kihali kufanya shughuli zake hapa Zanzibar mwaka 2001. Kwa kipindi chote hicho hadi kufikia tarehe 21/10/2012 JUMIKI ilikuwa ikiendelea kufanya shughuli zake kwa utulivu na amani na kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi na taratibu zilizowekwa.

Wakati Jumuiya ikiendelea na kazi zake za kuhubiri, kutetea na kusimamia haki za Waislam na kuelimisha jamii juu ya maswala mbali mbali ya kidini na kijamii, mnamo mwezi wa Ogasti 2012 ilitokea kadhia ya kukamatwa Sheikh Mussa Juma wa Msikiti wa Biziredi. Baada ya hapo Waislam walijaribu kufatilia sababu za kukamatwa kwake na kushindikiza kuachiwa huru kwa kuwa hakukuwa na sababu ya kuwekwa ndani. Lakini kilichofuata ni mfululizo wa mabomu ya machozi na pilipili kuwatawanya hali iliyozidisha mtafaruku katika mji wa Zanzibar.

Tarehe 19 Oktoba 2012 Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara na baadaye kuachiwa tarehe 22/10/2012. Tarehe 23 Oktoba 2012 Sheikh Farid alitakiwa afike Kituo cha Polisi, Madema kwa mahojiano kuhusu kutekwa nyara kwake. Masheikh wengine - Sheikh Msellem, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Juma na Sheikh Hassan walikwenda 1

kumshindikiza. Bahati mbaya Polisi wakawakamata wote na kuwaweka ndani na kuwafungulia mashtaka mbali mbali ya uchochezi na uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali na kupandishwa mahakamani tarehe 25 Oktoba 2012; siku ambayo masheikh wote walinyolewa ndevu zao, tukio lililowashangaza wengi kwani ule msingi wa Katiba kwamba hakuna mwenye hatia mpaka apatikane na hatia na Mahkama iliyo huru ulishavujwa tokea siku ya mwanzo kabisa.

Baada ya hapo mashtaka kadhaa yakafunguliwa katika mahkama mbali mbali ikiwemo Kwerekwe (mahkama mbili za Wilaya), Mfenesini na Vuga (Mahkama Kuu). Dhamana ziliwekewa masharti magumu mwanzoni lakini baadae masharti yakalainishwa na washtakiwa kupewa dhamana katika kesi zote isipokuwa ile ya Mahkama Kuu. Kwa upande mwengine, kesi moja ya Mahkama ya Wilaya Kwerekwe ikafutwa na ile ya Mfenesini pia ikafutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.

Kesi zote zinazowakibili Masheikh wa Uamsho ni kesi ambazo dhamana ni haki ya washtakiwa kwani makosa wanayoshtakiwa si makosa ambayo hayana dhamana. Aidha, kwa mujibu wa Sheria, kesi hizo zinapaswa kuanza ndani ya miezi minne, vyenginevyo inabidi washtakiwa wapewe dhamana. Kinyume na misingi yote ya sheria na haki, washtakiwa wote kumi wameshakaa ndani kwa zaidi ya miezi saba sasa kinyume na sheria na taratibu zote za kuendesha mashtaka ya jinai. Jambo hili la kuendelea kuwekwa mahabusu na kunyimwa dhamana kwa Masheikh ni dhulma, ukandamizaji na uvunjwaji wa makusudi wa haki za binaadamu. Jee hii ndio demokrasia na utawala bora?

Lengo la Jumuiya sio kuingilia kazi za mahkama, bali tunahaki ya kikatiba ya kupinga uvunjifu wowote wa Katiba ya Zanzibar ya 1984. Kwa kawaida inapotokea uonevu kama huu tumekuwa tukishuhudia Jumuiya za Kitaifa na za Kimataifa, Taasisi za kutetea Haki za Binaadamu, Vyombo vya habari duniani, Asasi za Kijamii, Vyama vya wanasheria na wengineo wakipaza sauti zao kulaaani, kushtumu na hata kukemea waziwazi dhulma hizo; lakini kwa masikitiko makubwa hali imekuwa ni tofauti kwa Viongozi waliokumbwa na kadhia hii. Jee taasisi hizo ziko wapi? Au kwa sababu wahusika ni Viongozi wa Kiislam? 2

Ikumbukwe kama hawa ni viongozi wa juu wa Jamii kubwa ya Kiislam nchini, hivyo kila mtu linamgusa na kumuuma jambo ambalo likiendelezwa linaweza kusababisha uvunjifu wa amani usiotarajiwa. Kwa hali hii Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) imewaita Wanahabari, Mabalozi wa chi za nje, na Wadau mbali mbali kuwaeleza jinsi ya dhulma, ukandamizaji, na uonevu unavyoendelea dhidi ya Viongozi wetu kama ifuatavyo.

Kuwatupia shutma kali na malamiko Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuvunja sheria za nchi walizozitunga na kuzilia viapo na kuzipitisha wenyewe na kudai kuwa hakuna mtu alie juu ya sheria.

Jumuiya ya Kimataifa; wakiwemo:Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya, Marekani, na Magharibi kwa ujumla kwa kukaa kimya kinyume na kawaida yao ya kutetea haki za binaadamu.

Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali ndani na nje ya nchi Kwa kutoripoti au kuripoti habari kwa kuegemea upande mmoja wa Serikali huku ikiihusisha Jumuiya na ufanyaji wa fujo, na pili kutoa habari kwa mitazamo yao wenyewe mfano; Kulihusisha tukio la Maandamano ya Morogoro na matukio ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar kuendelea kuingilia uhuru wa Mahkama kwa kutoa misimamo yake mikali dhidi ya Masheikh wa Uamsho waliopo mahabusu.

Kuvunjwa kwa katiba ya nchi mfano; kuingiliwa uhuru wa habari na maoni kwa jeshi la polisi kukama CD za mawaidha ya kiislam na kuzuia redio kutangaza matangazo ya Jumuiya na Kamisheni ya Habari ya Zanzibar na Waziri wa Mambo ya ndani Mhe: Emanuel Nchimbi kuzuia kutoa taarifa za JUMIKI katika vyombo vya habari. Mfano: Redio Nour na Adhana FM. 3

Shutma kwa vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, na Vikosi vya SMZ, kwa kupachuliwa kwa nguvu bendera za Jumuiya katika sehemu mbali mbali nchini kwa lengo la kuudhalilisha UISLAM, kupigwa na hata kuuliwa baadhi ya watu kwa kukataa kupachua bendera hizo.

Matumizi ya nguvu kubwa, kuweka hali ya hatari, taharuki na kuzuia hata jamaa za washtakiwa kukaribia mahkamani ambapo hata kesi ya uhaini ndugu na jamaa waliruhusiwa kuhudhuria na kusikiliza kesi za ndugu na jamaa zao.

Unyanyasaji wa watuhumiwa na uingiliaji wa uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa katiba; Mfano; kuwanyoa ndevu kwa lazima, kuwazuia kusoma quraan, kupata habari, kuswekwa na kutengwa katika chumba cha kila mtu peke yake (katika siku za mwanzo za mahabusu).

Kuwatenga na mahabusu wengine hata katika ibada kinyume na utaratibu wa sheria na haki za binaadamu.

Mwisho, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu inatoa TAMKO RASMI kuhusiana na kadhia yote tangu ilipoanzia na hadi leo hii kama ifuatavyo;

1. Jumuisha ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), inakanusha vikali propaganda zote zinazoenezwa na vyombo vya habari, wanasiasa na watu mbali mbali kuihusisha Jumuiya na vurugu na vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani kama vile uchomaji wa makanisa, maskani na upotevu wa maisha ya watu. Fujo sio sera ya Jumuiya wala haihusiki nazo.

2. Kwa vile Msingi mkuu wa katiba zote za nchi zinazoendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ikiwemo Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ni kuheshimu na 4

kulinda haki za binaadamu ikiwemo uhuru wa kuabudu na kujikusanya na kujieleza, kwahiyo, JUMIKI inalaani vikali wale wote wanaotoa kauli za vitisho na matamko ya uvunjifu wa katiba na kuipeleka nchi katika utawala wa kidikteta.

3. JUMIKI itaendelea na shughuli zake za kuelimisha, kutetea na kusimamia haki na wajibu wa kila raia kama kawaida yake, ilimradi haivunji sheria wala taratibu za nchi. Itaendelea kutetea, kudai na kuelimisha umma wa Wazanzibari juu ya haki yao ya kuidai Zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa.

4. JUMIKI inashangazwa na kauli za nchi za magharibi kwa kuipongeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa; serikali ambayo inavunja na inakandamiza wananchi wake wenyewe kwa kudai haki yao ya kujitawala.

5. JUMIKI itaendelea kusimamia agenda yake ya msingi ya kudai Zanzibar huru kinyume na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) na vyama vya kisiasa za kututoa katika lengo kwa kuanzisha agenda za pembeni ikiwemo kukamata viongozi wetu, kuanzisha mchakato wa katiba na kueneza uvumi na propaganda usio na ukweli wowote.

6. JUMIKI itaendelea kusisitiza kama ni kuendelea na muungano au laa kwa kuheshimiwa matakwa ya wananchi pia kupewa fursa ya kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar. Jumuiya tayari imekusanya majina ya watu sitini elfu kwa niaba ya Wazanzibari kwa ajili ya kupeleka mbele agenda ya kudai kura ya maoni na kudai mustakbali wa nchi yetu ya Zanzibar.

Wabillah Taufiq

IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MKUU JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM ZANZIBAR

You might also like

  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Document16 pages
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Document0 pages
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • An-Nuur 1071
    An-Nuur 1071
    Document12 pages
    An-Nuur 1071
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Document16 pages
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1092
    Annuur 1092
    Document16 pages
    Annuur 1092
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1087
    Annuur 1087
    Document7 pages
    Annuur 1087
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1067
    Annuur 1067
    Document12 pages
    Annuur 1067
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1077
    Annuur 1077
    Document12 pages
    Annuur 1077
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Document12 pages
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1076
    Annuur 1076
    Document12 pages
    Annuur 1076
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1060
    Annuur 1060
    Document16 pages
    Annuur 1060
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1072
    Annuur 1072
    Document12 pages
    Annuur 1072
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1065
    Annuur 1065
    Document12 pages
    Annuur 1065
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Nadharia Ya Meli
    Nadharia Ya Meli
    Document6 pages
    Nadharia Ya Meli
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1059
    Annuur 1059
    Document16 pages
    Annuur 1059
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1031
    Annuur 1031
    Document16 pages
    Annuur 1031
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1063
    Annuur 1063
    Document16 pages
    Annuur 1063
    Hassan Mussa Khamis
    No ratings yet
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Document16 pages
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1061.
    Annuur 1061.
    Document16 pages
    Annuur 1061.
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1057
    Annuur 1057
    Document16 pages
    Annuur 1057
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Document16 pages
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Document12 pages
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1046
    Annuur 1046
    Document12 pages
    Annuur 1046
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1030
    Annuur 1030
    Document16 pages
    Annuur 1030
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 117
    Annuur 117
    Document16 pages
    Annuur 117
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1029
    Annuur 1029
    Document20 pages
    Annuur 1029
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1027
    Annuur 1027
    Document16 pages
    Annuur 1027
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Zaka 3
    Zaka 3
    Document61 pages
    Zaka 3
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1022
    Annuur 1022
    Document12 pages
    Annuur 1022
    MZALENDO.NET
    No ratings yet