Professional Documents
Culture Documents
Annuur 1089
Annuur 1089
tz
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1089 SHAWWAL1434, IJUMAA , SEPT. 6-12, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
MZEE Moyo (kushoto) na Mohamed S. Riami "Eddy" wakiwa katika kongamano Bwawani.
Wa i s l a m u k u e n z i Ustaarabu uliokamilika w a Ta n g u A s i l i y a Watu wa Mwambao wa Afrika ya Mashariki na Kati. Ustaarabu wa Kuheshimika. Katika kongamano hilo
Inaendelea Uk.4
Inaendelea Uk.3
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
AN-NUUR
Tahariri/Habari
AN-NUUR
TUMEARIFIWA kwamba ile m i s w a d a ya sheria ya marekebisho ya mabadiliko ya Katiba na suala la zima kuhusu kura ya maoni ya r a s i m u ya katiba mpya, inawasilishwa katika vikao vya Bunge linaloendelea mjini Dodoma hivi sasa. Miswada hiyo i n a wa s i l i s h wa k u j a d i l i wa n a wabunge ili kutoa nafasi k wa wa b u n g e kuchambua v i p e n g e l e v ya mbalimbali sheria hizo kuanzia uteuzi wa Kamati ya U t e u z i wa Bunge la Katiba, k u t i z a m a muundo na uwiano wa viongozi na wabunge katika Bunge la Katiba. Aidha kujadili juu ya mamlaka itakayosimamia kura za maoni
kuhusu rasimu hiyo na mambo m e n g i n e mbalimbali yanayohusiana na mchakato mzima wa rasimu ya Katiba mpya. Wakati Bunge l a J a m h u r i ya Muungano likipata nafasi ya kujadili suala hilo nyeti, ikumbukwe kuwa kuna chombo kingine cha kutunga sheria Zanzibar. Nacho si kingine bali ni Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Baraza hili tunaona kuwa kama mdau muhimu wa mustakabali wa katiba mpya nchini, lina nafasi yake katika kujadili na kutoa mapendekezo yake juu ya miswada ya sheria ya mabadiliko haya ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
PAMOJA na taarifa r a s m i ya D a k t a r i kutoka Hospitali Kuu ya M n a z i M m o j a , Zanzibar inayoeleza hali ya afya ya Naibu Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) Sheikh Azzan Khalid Hamdan ikidhoofika akiwa gerezani, Kiinuamiguu, mjini hapa, bado Serikali ya Zanzibar imeonekana kupata kigugumizi. Ta a r i f a h i y o inathibitisha kwamba hali ya Sheikh Azzan, anayeendelea kusotea gerezani kwa takriban mwaka mmoja sasa, akijumuika na
Maamiri wa JUMIKI na wale wa Jumuiya ya Maimamu ya Zanzibar (JUMAZA), hali yake imekuwa ikidhoofika kutokana na tatizo katika mfumo wake wa m a j i n d a n i ya figo kupata matatizo, kama walivyobaini m a d a k t a r i waliomfanyia uchunguzi hivi karibuni. Madaktari hao kupitia vipimo vya ultrasound wamebaini hitilafu hiyo na kupendekeza haraka iwezekanavyo Kiongozi huyo wa Kiislamu kupata matibabu ya haraka ikiwezekana nje ya Nchi. Ripoti ya Daktari
waliyoiona waandishi wa habari inathibitisha kuwapo kwa hitilafu hiyo inayoweza k u o n g e z a u k u b wa wa tatizo na kama wa l i v y o p e n d e k e z a wa t a a l a m u , i wa p o Kiongozi huyo hatapatiwa matibabu ya haraka. Haya ni matatizo ambayo ufumbuzi wa k e h a p a k we t u ni tabu kidogo waliofanikiwa wamepelekwa India au kwengineko na wasifanye mzaha, amekaririwa akisema mmoja wa wataalamu wa mambo ya afya ya jamii Nchini, mara alipoipiga macho ripoti hiyo ya kusikitisha.
MAANDALIZI YA KUJIUNGA KIDATO CHA I, 2014 (PRE- FORM ONE ORIENTATION COURSE)
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014. Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basic Mathematics na Computer. Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE. Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba: 0714 888 557/0712 974428 Wabllah tawfiq Mkuu wa Shule
Habari
AN-NUUR
Inatoka Uk.1 CCM na CUF. Mara tu alipopanda jukwaani, ummati wa watu waliojazana katika ukumbi huo hadi kusababisha hali ya hewa kuwa nzito, ulisimama na kuimba wimbo huo mashuhuri unaoimbwa katika sikukuu za mapinduzi na mashujaa. Ni katika wimbo huo ambapo wanajeshi, wanamapinduzi, wazalendo na wananchi k wa u j u m l a wa n a t o a kauli, ahadi na kiapo cha kuipigania na kulinda nchi. Na hiyo ikalipua hamasa ya kutokurudi nyuma katika kupigania nchi pamoja na Dola ya Zanzibar yenye mamlaka kamili. Hapo ndio wengi wakaanza kutoka machozi huku Mansour akishindwa kujizuiya na kujikuta akilazimika kufuta machozi kwa vidole mwisho akatoa kitambaa. Hiyo ilitokana na ujumbe uliokuwepo katika wimbo huo ukihimiza ukombozi na kuwasifu walioikomboa Unguja kutoka kwa wakoloni ambapo sasa wanajiona wanalazimika kuipigania tena kurejesha hadhi na mamlaka yake. Pamoja na mengi aliyozungumza, lakini alichohimiza Mansour ni juu ya Wazanzibar kutokurudi nyuma kupigania mamlaka kamili ya nchi yao. Alisema, kwa kuwa mtumishi wa Serikali katika nafasi mbalimbali ameona dhulma na hujuma inayofanywa dhidi ya Zanzibar. Akigusia suala la mafuta na gesi, alionyesha jinsi ambavyo kwa muda mrefu Tanzania Bara imekuwa ikichimba gesi, lakini Zanzibar haipati kitu kutokana na pato hilo. Hata hivyo, ilivyokuja kwa Zanzibar kutafiti na kuchimba mafuta na gesi, vikwazo vingi vimewekwa ikidaiwa kuwa hilo ni jambo la muungano. Hata pale Zanzibar iliposema kuwa ipo tayari kutoa asilimia 60 ya pato la gesi kwenda Bara na Zanzibar kubaki na 40%, bado haikukubaliwa. Ndio hapo ikafika mahali wakasema kuwa inabidi wasimame imara kuhakikisha wanalitoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya
BAADHI ya washiriki wa kongamano la Bwawani. M h e s h i m i w a A m a n i Bernard Membe, aliondoa y a o n d o l e w e k w e n y e K a r u m e a k i w a a m b i a kipengele cha misaada ya Muungano ni Uraia na wa n a - C C M h a o k u wa Wakfu kutoka Mascut Uhamiaji, Sarafu na Benki yeye hayupo Ikulu kwa kwa vile tu misaada hiyo Kuu, Mambo ya Nje na ajili ya kusimamia fitna na i n g e k u w a i e l e k e z w e Usajili wa Vyama vya Siasa. mauwaji. Zanzibar. Mapendekezo hayo Mjumbe mwingine wa Akifafanua alisema, yalisomwa na Mwakilishi Kamati hiyo Eddy Riami u j u m b e w a M a s c u t wa Mji Mkongwe ambaye aliwahimiza Wazanzibar uliotembelea Tanzania, pia ni mjumbe wa kamati kusimama katika agenda p a m o j a n a m a m b o hiyo, Ismail Jussa katika m o j a t u : k u p i g a n i a m e n g i n e , w a l i t a k a Kongamano la Jumamosi utaratibu wa iliyopita. Zanzibar yenye mamlaka kuwekwa namna ya kutoa misaada Kila nchi mshirika kiamili. (kwa Zanzibar ) kupitia (Zanzibar na Tanganyika), Na kwamba wawafute taasisi ya Wakfu. ibakie na uraia wake na na kuwatupilia kwa mbali H a t a h i v y o , b a a d a mtu kuwa na uraia wa nchi viongozi wote wasiotaka y a t a r a t i b u z o t e mshirika ndiko kumpe kuona Zanzibar huru yenye kukubalika na kusubiri uhalali wa kuwa raia wa mamlaka yake kamili. kusainiwa makubaliano shirikisho. Alisema Jussa na Akizungumza kabla ( M e m o r a n d u m ) , ya kusimama Mansour, M h e s h i m i w a Wa z i r i kuongeza kuwa uchumi Makamu Mwenyekiti wa Membe alifuta kipengele si suala la Muungano hata katika Katiba ya sasa Kamati ya Maridhiano, cha Wakfu. na kwamba nyenzo za Mheshimiwa Abubakar Alisema, hata ukitizama kuendeshea na kusimamia Khamis Bakari alisema watumishi wa Serikali u c h u m i wa n c h i k wa k u w a k u n a m a m b o wakiwemo mabalozi katika maana ya sera za fedha yanafanyika makusudi kwa nchi za nje na Umoja wa na uchumi zimeendelea roho mbaya tu kuihujumu Mataifa, Zanzibar imekuwa k u d h i b i t i w a k u p i t i a ikipunjwa wakati inadaiwa Serikali ya Muungano. Zanzibar. Vyombo vikuu N a k w a m b a i l i kuwa hiyo ni Wizara ya vinavyosimamia sera hizo kuondokana na hali hiyo Muungano. N i k a t i k a h a l i h i y o ambavyo ni Benki Kuu ya ni lazima Tanganyika Mheshimiwa Abubakar Tanzania (BoT), Mamlaka isimame kama Tanganyika a mba ye ni Wa z i r i wa ya Mapato Tanzania (TRA) n a Z a n z i b a r i s i m a m e Kariba na Sheria (ZNZ) na Wizara ya Fedha ya k i v ya k e n d i o z i f a n ye na Mwakilishi wa Jimbo la Serikali ya Muungano muungano wenye haki Mgogoni, Pemba; alisema v i m e k u w a v i k i f a n y a sawa. k u w a k a t i k a m a m b o uamuzi na kuyatekeleza A l i s e m a , k a t i k a ambayo ni lazima yatiwe bila ya kuzingatia kuwa mfumo wa sasa ambapo katika Katiba Mpya, ni Z a n z i b a r i n a t e g e m e a Tanganyika imejificha pamoja na kuirejeshea uchumi wa utoaji huduma ndani ya Tanzania, hakuna Zanzibar mamlaka ya na haiwezi kuwa sawa na namna Zanzibar inaweza kuwa na Wizara yake ya uchumi wa Tanganyika ambao unategemea kupata haki yake. Mambo ya Nje. Akitoa mfano aligusia Wakati huo huo, Kamati rasilimali, alisema. Kwa upande mwingine hasara inayopata Zanzibar ya Maridhiano imetoa akasema kuwa suala la kwa kutokuwa na Mambo maoni yake ya Rasimu vyama vya siasa linapaswa ya Nje. ya Katiba ya Jamhuri ya Akasema, ni kiasi miezi Muungano wa Tanzania kuondolewa katika mambo miwili tu iliyopita ambapo k wa k u t a k a Z a n z i b a r ya Muungano ili Zanzibar Waziri wa Mambo ya ijitegemee karibu kwa kila na Tanganyika, kila moja iandikishe vyama vyake Nje na Ushirikiano wa kitu. Kimataifa Mheshimiwa M a e n e o i n a y o t a k a vya siasa.
Habari/Tangazo
AN-NUUR
Msisitizo huo pia ulikwenda sambamba na wasia wa makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akilifunga Kongamano hilo, akasema Ustaarabu wa Kiislamu ni hazina kubwa iliyojengwa na Misingi ya Dini ya Kiislamu, inayofaa kuenziwa kwa hali zote. Kongamano hilo lilifunguliwa Rasmi na Raisi wa Zanzibar Alhaj Dr. Ali Mohamed Shein, aliyewahamasisha waislamu kuenzi Ustaarabu uliokamilika w a Ta n g u A s i l i y a Wa t u w a M w a m b a o wa Afrika ya Mashariki na Kati, Ustaarabu wa Kuheshimika.
KIGAMBONI /KIGOGO
CU.124
CU.130
NAFASI ZA MASOMO
UALIMU: STASHAHADA (E Moja Na S Moja) GRADE 3A ( Div. IV-27) CHEKECHEKEA (Div. IV- 28 na Kuendelea)
(2013-2014)
TEACHERS COLLEGE
Note: Nafasi za Udhamini kwa waliopata viwango Ngazi ya Diploma na Cheti. Wahi, Nafasi Chache!
(Asiyekuwa na Viwango anaruhusiwa kusoma Ualimu huku anarudia Mitihani) Secretarial Studies, Records Mgt, Project Planning & Mgt, ICT, Simplified Accountancy, Computer Applications
Kozi za Biashara
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto), Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga.
Misri na pia wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Musri, imefanyika Jumatatu yawiki hii katika mkoa wa kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Watu hao wanashitakiwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi uliosababisha kushambuliwa askari jeshi na pia kuhujumiwa makanisa katika mkoa wa Suez. Tangu Julai 3 mwaka huu, Misri imetumbukia katika machafuko na ghasia baada ya jeshi kufanya mapinduzi ya kumuondoa madarakani Muhammad Mursi, rais wa kwanza aliyechaguliwa na wananchi kidemokrasia nchini humo.
Makala
AN-NUUR
madai ya kuweko
MKUU wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Hans Blix. mbili zinazozozana za waasi na serikali. Viongozi wa Mataifa ya Magharibi wanatoa maelezo yanayoonyesha kuwa hawatasubiro matokeo ya ukaguzi, tayari wameamua kila kitu alisema Lavrov. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague alisema Uingereza imeshawishika kuwa Rais Assad yupo nyuma ya shambulio la Agost 21 na wameshakubaliana na Marekani na Ufaransa katika kujibu mapogo. Waziri wa mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu naye alisema nchi yake itaungana na muungano wa mataifa hayo dhidi ya Syria iwapo UN itashindwa kuchukua hatua. Rais Assad ameshajibu misimamo ya mataifa hayo aliyoiita kuwa ni nonsense, wakati alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Izvestia la Urusi mapema wiki hii. Urusi ambayo imekuwa ikitumia kura yake ya veto kwenye Baraza la Usalama la UN kuzua mikakati ya kuiadhibu Syria, wiki hii imeitaka Marekani kutorudia makosa ya siku za nyuma kama yale ya kuivamia Uraq mwaka 2003. Marekani na washirika wa k e wa l i i s h a m b u l i a Uraq bila ya udhini ya U N , b a a d a ya U r u s i , Ujerumani na Ufaransa kukataa kuivamia nchi hiyo kijeshi kumuondoa Saddam Hussein. Bw. Lavrov alisema Wizara ya Mambio ya Nje ya Urusi imeshafanya mazungumzo na John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Yule wa Uingereza, na kwamba mazungumzo yao yalionyesha kuwepo dalili za Waasi kufanya mashambulizi ya kuitia hatiani serikali ya Assad. Katika hatua nyingine, Mkuu wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Hans Blix, amesema kitendo cha kutaka kuishambulia Syria kwa kutegemea
silaha za maangamizi ya halaiki ni kurejea makosa ya huko nyuma ya viongozi wa Washington. H a n s B l i x amewatahadharisha viongozi wa Marekani kuhusu nia yao ya kutaka kuishambulia kijeshi Syria, akisema kuwa hawapaswi kuwa na haraka katika suala hilo. Mwaka 2003 mkaguzi hyo alitahadharisha kuwa madai yaliyokuwa yakitolewa na Marekani kuhusu silaha za kemikali huko Iraq si ya sahihi baada ya timu yake iliyokuwa umepewa majukumu ya kufanya u c h u n g u z i j u u ya madai ya Marekani na washirika wake kwamba serikali ya Saddam Hussein inamiliki silaha za maangamizi.
Bw. Blix amesema kwamba Marekani na marafiki zake wanapaswa kwanza kutoa fursa kwa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wao k u h u s u m a d a i ya kutumiwa silaha za kemikali huko Syria, kabla ya kuchukua hatua yoyote ile. Serikali ya Syria imewaruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kulitembelea na kulifanyia uchunguzi eneo la Ghouta al S h a r q i ya , a m b a l o nchi za Magharibi zinadai kuwa silaha za kemikali zimetumiwa. Mkuu huyo wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, amesisitiza kuwa Rais Barack Obama wa Marekani hapaswi kuchukua hatua dhidi ya Syria bila ya suala hilo kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (irib.ir)
TANGAZO
UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO UNAPENDA KUWAARIFU WADAU WAKE WOTE KUWA BWANA. JUMA SAKATAI SIO MFANYAKAZI WA CHUO TENA TANGU TAREHE 02/09/2013. HIVYO BASI CHUO HAKITAHUSIKA NA SHUGHULI AU MAWASILIANO YOYOTE YATAKAYOFANYWA NAYE AU KUPITIA KWAKE. AFISA UHUSIANO CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO 05/09/2013
Makala
AN-NUUR
mzalendo na au mpenzi wa historia na kumfunza vya kutosha. Makala haya yanalenga kuutazama mgogoro wa Misri katika nyanja nyingine ambayo kwa namna moja ama nyingine, a m b a y o k wa s a b a b u wanazozijua waandishi wetu haijajadiliwa vya kutosha Nini chanzo cha mgogoro wa Misri? Binafsi nautazama mgogoro wa Misri katika nyanja au mrengo mwingine kwamba ni mgogoro unaotokana na kusigana kwa mifumo miwili ambayo yote inalenga kushinda kundi kubwa katika jamii. Hali hii imedumu kwa muda mrefu tu, na sasa ni wakati ambao imeshindikana kuficha maradhi haya ya kuoneana kijicho baina ya mifumo hiyo miwili. Mifumo hii ni ipi? Kwanza ni mfumo wa Uislam chini ya mwamvuli wa Ikhwani Al Muslmyin (Udugu wa Kiislam). Msingi mkuu wa mfumo huu ni kuongoza Misri na dunia nzima kwa kufuata sheria za Allah (s.w). Juhudi hizi za udugu wa Kiislamu kushinda sehemu kubwa ya jamii ya Wamisri si za jana wala za juzi, hizi ni juhudi za muda mrefu pengine nyuma kabisa ya mwaka wa 1928 ambapo ndio chama cha udugu wa Kiislamu kiliasisiwa na mwasisi wake Hassan Al Bana. Mfumo huu umeasisiwa katika kitabu cha dini ya
Kiislam na waaminio kwao huuona kama ndio mfumo s a h i h i wa k u o n g o z a maisha ya mwandamu duniani hapa. Watafanya kila wawezalo kuhakisha hilo. Lakini kwa upande mwingine mfumo wa pili ni huu wa Ubepari chini ya mwamvuli wa demokrasia iliyojengwa katika misingi ya haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria uwazi na uwajikaji nakadhalika. Na hata hivyo sina haja ya kuandika mengi (kwani mengi yameshaandikwa) kuhusu mfumo huu wa demokrasia ambao kwa kiasi kikubwa umeshindwa katika maeneo mengi kusimamia hizo haki za binadamu. Makala haya yanalenga kuutazama mgogoro wa Misri sana kupitia mfumo wa kwanza, ambao kwa namna fulani haujajadiliwa kwa mapana na marefu. Kwa hiyo lengo la makala haya ni kuujadili mgogoro huo katika mrengo mwingine. Anaandika Sheikh Bawaziri katika makala yake kuwa Misri baada ya mapinduzi ya 1952 na Gamal Abdel Nasser kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo kulikuwa na upinzani mkubwa baina ya serikali ya N a s s e r n a c h a m a cha Udugu wa Kiislam kilichokuwa kikiongozwa na Sayyid Qutb kwa wakati huo, wawili hawa;Rais Nasser na Qutb. Walikuwa
wakitofautiana katika mambo mengi... Je haya mambo mengi yawafanyayo watofautiane n i ye p i ? H a p a n d i p o ninapojenga dhana ya kwamba mgogoro wa Misri ni mgogoro kati ya mifumo miwili inayosigana kama nilivyoeleza hapo juu, yaani mfumo wa Kiislamu kuuondosha mfumo wa ubepari wa Magharibi na vivyo hivyo mfumo wa ubepari wa Magharibi kuuondosha mfumo wa Kiislamu, yote hayo kupitia mawakala wao wa Demokrasia na wa Udugu wa Kiislamu. K u p a t a u n d a n i wa msingi wa dhana hii hatuna budi kuingia ndani kidogo kuona, je, wawili hao ni akina nani? Walikutana vipi? Na walichotofautiana ni kipi? Hapa hatuna budi kutazama historia zao kwa ufupi. Mwaka 1906 oktoba 9 katika kijiji cha Musha alizaliwa kijana aliyejulikana kwa jina la Sayyid katika familia ya mwanaharakati wa kisiasa, Qutb. Alipata elimu yake ya mrengo wa Kimagharibi katika miaka ya 1929 and 1933. Vile vile amewahi kuwa mtumishi katika Wizara ya Elimu ya nchini Misri katika miaka ya 1939 na historia inatuambia kwamba miaka ya 1948 hadi 1950 aliishi nchini Marekani akisomea mfumo wa elimu wa nchi hiyo katika chuo cha Colorado (kwa sasa Chuo Kikuu cha Colorado Kaskazini).
Makala
AN-NUUR
JESHI la Misri limeendelea kufanya maangamizi ya wananchi wasio na hatia, katika jaribio lake la kuwaondoa mitaani waandamanaji wanaopinga kung'olewa madarakani kijeshi kwa Rais aliyechaguliwa kidemkorasia, bwana Mohammed Morsi. Inasemekana zaidi ya watu 2000 wameuawa na vikosi vya usalama katika kipindi cha wiki moja tu, ambapo kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, wengi wao ni wanawake, watoto, vijana na wazee ambao walikutwa na m a j e r a h a ya r i s a s i vifuani na vichwani. Vikosi vya usalama nchini Misri vimetenda uhalifu mkubwa ambao haujawahi kufanywa hata na maadui wakubwa wa Waislamu. Wa m e c h o m a m o t o hospitali ya dharura katika eneo la Rab'a Al Adawiyah wakati miili ya watu waliokufa na wale waliojeruhiwa ikiwemo ndani. Nadhani lengo lao lilikuwa ni kufuta ushahidi wa uhalifu walioufanya. Hali hii inaonyesha kiwango cha unyama na ukatili kinachoweza kufanywa na viongozi wa mapinduzi ya Misri dhidi ya Siasa za Kiislamu nchini humo. H a wa n a h o f u h a t a kidogo kwa uhai wa wananchi wao wenyewe, wala heshima kwa wale waliotangulia mbele ya haki! Lakini, jambo la wazi kabisa, ni ule utayari wa jeshi la Misri kuendeleza umwagaji damu na maangamzi ya watu wanaopigania haki yao iliyoporwa mchana kweupee, hatua ambayo inatukumbusha m a a n g a m i z i yanayofanywa na
WAANDAMANAJI nchini Misri M a ya h u d i d h i d i ya waliobeba bendera ya akhira kwa uovu wao. Waislamu wa Palestina. Uislamu. Huu ni utawala Wamemwaga damu Kufuatia mauaji hayo mpya wa kijeshi. Na i s i y o n a h a t i a y a ya kihalifu, Rais wa hawa ni viongozi wa Waislamu, wanaendesha Serikali ya mpito ya Misri m a p i n d u z i a m b a o vita dhidi ya dini ya akatangaza hali ya hatari wanaendeleza unyama. Mwenyezi Mungu na kwa kipindi cha mwezi Wako tayari kumwaga wanatumikia maslahi m m o j a . Wa n a d h a n i damu isiyo na hatia ili ya Marekani badala ya ndani ya kipindi hicho, k u f a n ya m a p i n d u z i wananchi wa Misri: wataweza kuwaua y a o y a o n e k a n e "Na mwenye na kuwapondaponda yamefanikiwa. kumuua Muislamu kwa waandamanaji ili W a n a k u w a kukusudia, basi malipo w a s a l i m u a m r i n a wakali kama simba ya k e n i J a h a n n a m , kukubali utawala mpya wanapokabiliana kijeshi humo atakaa milele; wa kidhalimu. na raia wao wenyewe, na Mwenyezi Mungu U t a w a l a a m b a o lakini wanyonge kama a m e m g h a d h i b i k i a Jenerali Al Sisi, akibebwa vifaranga kwa maadui n a a m e m l a a n i n a na Marekani, anataka wao halisi, ambao ni amemuandalia adhabu kuuweka nchini Misri Mayahudi na mataifa kubwa" Qur (4:93). baada ya kumpindua ya Magharibi. Wanakula Na Mtume wa Mohammed Morsi, njama pamoja nao Mwenyezi Mungu ambaye amechaguliwa kuhujumu taifa lao amesema: "Kumuua na wananchi wa nchi wenyewe! Wamekuwa M u i s l a m u m m o j a hiyo. wa l i n z i h o d a r i wa ni vibaya zaidi kwa M a p i n d u z i y a maslahi ya maadui hata Mwenyezi Mungu kama Januari 25 mwaka 2012, kwa damu ya ndugu kuangamiza Dunia yote" yaliyomng'oa Hosni zao! (Tirmidhi). Mubarak, ambayo Wa n a p i g a v i t a Kauli mbiu ya viongozi yalidumu kwa siku Uislamu kwa jina la wa mapinduzi nchini 18, yalisababisha vifo "kupambana na ugaidi", Misri ni "kupambana vya takriban watu 365, wakati Mayahudi walio na ugaidi", ambapo wakati kwa siku moja jirani nao, ambao ndiyo kuwapiga vita 'Ikhwan tu Serikali kibaraka ya maadui wao wakubwa, Misri imeua zaidi ya wa k i wa s a l a m a n a Muslimin' ni kichaka mara mbili ya idadi hii! wenye uhakika. Vipi chao tu cha kupambana Watu 638 wameuawa h a w a w a h a l i f u n a n a Ui s l a m u . L a ki ni ndani ya masaa 24 tu! wasaliti, waliomwaga wanasahau kwamba I n a o n e k a n a h a y a damu ya Wamisri wasio Uislamu nchini Misri ni mauaji ya kisasi na hatia, wanaweza una mizizi mirefu, na y a n a y o t u f a n y a kuleta ushindi kwa haiwezekani kung'oa tukumbuke utawala wananchi wa Misri? mizizi ya Uislamu nchini wa Hosni Mubarak, Hawa ni wahalifu na humo. Misri ni nchi ya ambaye alikuwa na wauaji! Na Mwenyezi Waislamu. Insha'Allah, iko siku chuki kubwa dhidi ya Mungu atawaadhibu m f u m o wa k i k a f i r i raia wake, hususan wale hapa duniani na kesho
unaotawala Misri, ambao unasimamiwa na Marekani na washirika wake wa Kimagharibi utakoma, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mfumo wa Kiislamu utasimama! Mfumo ambao siyo demokrasia, siyo usekula na wala haushirikiani na Ukafiri kwa namna yoyote ile. Jambo la msingi ni kwa Waislamu wa Misri k u t a m b u a k wa m b a kuzingatia maagizo na taratibu za Mwenyezi Mungu, ndiyo njia pekee ya kujipatia ushindi na heshima. Misri inahitaji Uislamu katika utawala na siyo tu Waislamu kuongoza mfumo wa kisekula. Suala hapa siyo nani anaingia madarakani, bali ni mfumo gani unatawala nchi hii ya Waislamu. Kufuatia kupinduliwa kwa Rais Mohammed Morsi na darsa iliyopatikana, Waislamu wa Misri wana kazi ngumu ya kuung'oa utawala wa kidhalimu kutoka kwenye mizizi na matawi ya k e . Wa n a h i t a j i k a kupambana na kuleta mapinduzi kamili ya Kiislamu. Hawana sababu tena ya kujificha kwenye vichaka vya demokrasia wala usekula. Wameshaona madhara yake, na Waislamu hawaumwi na nyoka mara mbili kwenye shimo moja: "Mwenyezi Mungu Amewaahidi wale walioamini miongoni m we n u n a k u f a n ya vitendo vizuri, kuwa Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale wa l i o k u we p o k a b l a yao, na kwa yakini Atawasimamishia dini yao Aliyowapendelea, n a At a wa b a d i l i s h i a amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndiyo wavunjao amri zetu" Qur(24:55).
9
Na Abdulkarim S. Msengakamba
Habari
SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013 Amir wa jumuiya wilaya ya Temeke Ust. Saad Ahmed Salim aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuwapatia chumba kitakachotumika kuhifadhia vifaa vya kazi za kila siku za Jumuiya hiyo sambamba na kuhifadhi dawa, a m b a z o h u wa p a t i a wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo. Kufuatia ombi hilo, Naibu Meya Juma Mkenga, aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kuangalia uwezekano wa kutenga chumba kimoja kwa ajili ya shughuli za kihuduma za Jumuiya hiyo. Amir huyo alisema jumuiya ya Waislamu kitengo cha afya na ustawi wa jamii JAI, ni Taasisi isiyo ya serikali ambayo ina zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake. Taasisi hiyo inafanya kazi zake bega kwa bega na watumishi wa serikali katika kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii katika maeneo ya Hospitalini na majumbani. Alielezea kuwa Jumuiya hiyo inatambua hali halisi ya maisha ya Mtanzania na kupanda gharama za m a t i b a b u , d a wa n a vifaa mbalimbali vya tiba, hivyo kwa dhati kabisa kwa kutumia kauli mbiu zake zaHuruma-Upendo, imekusudia kutoa huduma zote stahiki kwa wagonjwa wa jinsia zote, madhehebu yote waliopo mawodini na majumbani. Amir Salim, aliongeza kuwa jumuiya yao hutoa huduma zake kila siku ambazo ni kuwaombea dua na kuwafariji wagonjwa, kuwanunulia dawa zinazokosekana mahospitalini, kuwafanyia usafi katika hali zote stahiki, k u wa p a t i a c h a k u l a kwa nyakati zote, h u s u s a n i k wa wa l e ambao hawama ndugu, jamaa, ambao inatubidi kuwahudumia kwa kwa hali na mali. Katika zoezi hilo, jumla ya unit 300 za damu zilikusanywa.
AN-NUUR
WAISLAMU kupitia Jumuiya ya Akhlaaqul Islaam (JAI), kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii mwishoni mwa w i k i wa m e c h a n g i a damu kwa wagonjwa, katika zoezi lililofanyika katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Tu k i o h i l o lilihudhuriwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Juma Mkenga, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Sofia Mjemwa. Binafsi nimefarijika sana kuona muamko huu wa Waislamu kwa jamii, nimefurahishwa na akina mama ambao wamejitokeza katika zoezi hili, wanastahili kuungwa mkono na jamii kwa ujumla kwa kitendo hiki, ni mfano mzuri unaostahiki kuigwa na akina mama wengine popote katika jamii yetu. Alisema Naibu Meya huyo. Aidha aliikumbusha jamii kwa ujumla umuhimu wa kuchangia damu kwa hiyari, kwani kitendo hicho ni cha kuokoa maisha ya wagonjwa wenye kuhitajia huduma hiyo ya damu. N a ye D r . S t a n l e y Lwiza, wa hospitali y a Te m e k e a k i t o a shukurani zake kwa Waislamu hao alisema, hospitali yake wa inathamini mchango na misaada pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na wanajumuiya wa JAI. Kwa upande wake, Meneja maabara wa hospitali hiyo Grace Maliva, alisema muitikio ulionyeshwa na Waislamu hao ni mkubwa na kushauri elimu zaidi ya kuchangia damu inahitajika kutolewa katika jamii ili kuwajengea moyo zaidi wa kujitolea. Alisema takwimu zinaonesha kuwa wanaohitaji damu zaidi ni akina mama, ambao kutokana na uhaba wa damu hupoteza maisha kwa kukosa huduma
hiyo. Alisema takribani akina mama zaidi ya wanne hupoteza maisha kwa siku kwa kukosa damu. Wa k a t i m w i n g i n e hulazimika kukamata watu kwa ajili ya kutoa damu bila ya kujali
mpango wa damu salama, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu, lakini hulazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hususani wa pale wanapojifungua ambapo hupoteza damu kwa wingi sana.
Hata hivyo aliwaasa kina mama kuhamasika kujitokeza zaidi katika mazoezi ya kuchangia d a m u k wa n i a k i n a mama wenzao ndio wahitaji wakubwa wa huduma hiyo. Katika risala ya Jumuia hiyo iliyosomwa
10
Hodi hodi mhariri, si wa gazeti la giza, Bali wa letu AN-NUUR, lenye angavu mwangaza, Kuna jambo nafikiri, naomba kulidokeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Uvivu niwape siri, tunaouendekeza, Wa kushindwa kufikiri, hali ya kuwa twaweza, Nd'o unotuathiri, pamwe na kutudumaza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Wengi likizo nadhari, zetu tumeziwekeza, Wachache wanotughuri, kadiri wanavyoweza, Badala wanafikiri, yetu nasi twafatiza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kheri wakiita shari, nasi nyuma twafatiza, Shari wakiwamba kheri, kadhalika twachagiza, Kwa mgando tafakuri, vyovyote watugeuza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Waizushapo habari, papo hapo twaimeza, Mia kwa mia twakiri, pasi hata kuchunguza, Kadhalika kufikiri, twameza na kueneza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Twajiona maayari, kwa puya kuhanikiza, Sote yatatuathiri, madharaye nawajuza, Kwazo ikifuka nari, sote yatuteketeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Tuchukue tahadhari, kwa kutokuhanikiza, Tumezeshwazo habari, pasi kwanza kuchunguza, Kwanini zetu fikari, likizo twaziwekeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kwa uvivu kukhitari, wa kutokujizoeza, Kila mtu kufikiri, kadiri anavyoweza, Taifa la tafakuri, muhali kutengeneza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Ni yako sasa hiari, kujali au kubeza, Lengo langu kushauri, na si kukung'ang'aniza, Ila ni kubwa hatari, endapo utapuuza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kaditamati akhiri, nimefika kueleza, Akali ya kufikiri, leo yanatosheleza, Kalamu ya tafakuri, haina la nyoongeza, Utajatuangamiza, uvivu wa kufikiri. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.
Mashairi/Makala
AN-NUUR
UVIVU WA KUFIKIRI !
kukichafua chama cha Udugu wa Kiislamu ili atakaposhika madaraka brotherhood kilichokuwa maarufu sana miongoni mwa Wamisri kiwe na cha kusema. Lakini hakuna siri itakayodumu milele. Na ikafika wakati ambao Qutb na Muslim Brotherhood ya k e wa k a t a m b u a walikosea kushirikiana na Nasser na ndipo ulipokuwa mwisho wa uhusiano wao. Nasser akafanya juhudi nyingi tu kumshawishi kwa nafasi kadhaa serikalini ili Qutb arudi ila ikashindikana, Nasser amenukuliwa akisema; We will give you whatever position you want in the government, whether it's the Ministry of Education, Ministry of Arts, or any position you want. Na kwa hiyo mwaka 1954 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa wanachama wa Udugu wa Kiislam. N i wa k a t i a m b a o Qutb alikamatwa na kufungwa jela kwa tuhuma za kupanga mauaji dhidi ya Nasser, kamata kamata hiyo iliwaandama mpaka wafuasi wengine kama akina Zainabu Ghazal waliokuwa kunyume na serikali yake. Kwa maana hii, tofauti kati ya Nasser na Qutb ni ya kimtizamo, historia inatuambia kwamba Qutb anaamini kuwa jamii yeyote ile ambayo uongozi wake haufuati sheria ya Mwenyezi Mungu haiwezi kuwa ya K i i s l a m u h a t a kama wao wanajiita ni Waislam, na wanasali, wanfunga na wanahiji. Qutb anasema; Thus, a society whose legislation does not rest on divine law (shari'at allah) is not Muslim, h o we ve r a r d e n t l y its individuals may proclaim themselves Muslim, even if they pray, fast, and make the pilgrimage. Na mwaka 1966 ikawa ndio mwisho Sayyid Qutb ambaye a l i h u k u m i wa k i f o
WAANDAMANAJI nchini Misri. kwa kunyongwa na aliyekuwa mshirika wake mkuu Gamal Abdel Nasser. Suala la msingi hapa ni kuwa Udugu wa Kiislamu wanaitaka Msiri itakayoongozwa na sheria za Kiislamu wakati hawa wengine wanataka Misri ya kisekula, Misri ya kidemokrasia ya Magharibi. Hii ndio tofauti kubwa baina ya mifumo hiyo mawili. Kwa muda wa nusu karne sasa kundi l e n y e m r e n g o wa Udugu wa Kiislamu limekandamizwa mno. Juhudi nyingi zimefanyika kuzifuta fikra za Udugu wa Kiislamu lakini imeshidikana, na pengine ni kwa sababu waliwekeza mawazo yao katika watu, waliwekeza katika mafunzo na hivyo yataishi milele. Hapa nitapishana kidogo mtazamo na mwandishi Sheikh Bawaziri ambae yeye anaandika kuwa Misri imegawanyika katika makundi matatu makuu. Kundi linalomuunga mkono Morsi (raisi a l i ye p i n d u l i wa n a aliyechaguliwa kwa uchaguzi huru), kundi linalompinga Morsi na kundi pekee la Jeshi. Nayaona Makundi mawili tu pale Misri, kundi linalounga mkono sera za Ikhwani Al Muslimyn na kundi l i n a l o u n ga m ko n o ubeberu wa Magharibi kwa kujivika kilemba cha demokrasia, nalo hili linaundwa na Jeshi na wananchi huku kila mmoja akifanya nafasi yake. Na ndio maana nakubaliana na Sheikh Bawaziri katika makala yake ya tarehe 30 Agosti katika gazeti la kisiwa yenye kichwa cha makala ni nani aliyeweka mipaka hii katika Demokrasia?, Bawazir anaandika; Maandamano yaliyofanywa na wapinzani wa Morsi yalionekana ni halali, hakuna bunduki iliyoelekezwa kwao na wala hakuna yeyote aliyedai kwamba ni magaidi. Lakini maandamano ya wafuasi wa Morsi waliotaka raisi wao arejeshwe madarakani, hayo hayakuonekana kuwa ni nguvu ya umma. Bali waandamanaji hao walionekana kuwa ni magaidi wanaoipinga serikali iliyowekwa madarakani na mtu mmoja tu kwa nguvu ya jeshi. Kwa mtizamo huu kinachoendelea Misri ni msuguano baina ya mifumo miwili ya Uislam na Ubeberu. Lakini vile vile nakubaliana na Sheikh Bawazir katika makala yake hayo kwamba hofu ya mfumo wa ubeberu ni Uislam wa aina yoyote ile, Uislam siasa kali, siasa poa siasa zozote zile! Na hatima yake ni kuangusha dola lolote lenye mrengo huo. Kimsingi serikali ya Morsi isingeweza k u f a n ya l o l o t e l a maana ndani ya kipindi ilichokuwa madarakani, au ndani ya kipindi ambacho ingekuwa madarakani, iwe kuindeleza Misri kiuchumi au kujenga sera zake za Udugu wa Kiislamu. Ingeliichukua Misri miaka mingi k u f a n i k i wa k a t i k a moja kati ya hayo. Kwanini? Kiuchumi, Misri bado ni tegemezi na imekuwa ikipokea misaada mingi tu kutoka serikali za magharibi. Ambayo nayo ilifutwa bada ya M o r s i k u i n g i a madarakani. Lakini pia ni ngumu Misri iliyojaa rushwa na dhulma kupiga hatua ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, si kazi ndogo kuusafisha mfumo uliotamalaki katika kila kona ya nchi. Na hata kiitikadi, ingelichukua pia muda mrefu wa kwa Morsi kuzijenga sera zake za udugu wa Kiislamu. Kwani hali ilivyo sasa ni kama nusu kwa nusu, hii ingeifanya s e r i k a l i ya M o r s i kuwekeza nguvu ya ziada katika kuliendea lengo hilo (kama kweli ndio lengo la Udugu wa Kiislamu). Sasa hofu yote hii ni ya nini? Nguvu yote hii ni ya nini? Wanaoumia ni wananchi wasio na hatia yoyote ile. Ni wakati kwa dola za Magharibi kuwasikiliza wamisri wanataka nini kupitia hiyo hiyo demokrasia. (madoler@hotmail. com-0717 003 530).
11
AN-NUUR
QURAN surat Munafiqun aya ya kwanza inasema, Wa n a p o k u j i a wa n a f i k i husema: Tunashuhudia ya kuwa, kwa yakini wewe ni Mtume wa mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wake na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya k u wa h a k i k a wa n a f i k i ni waongo, (wanasema wasiyoyasadiki). Aya hii aliinukuu Katibu wa Jumuia ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (Hayat) Sheikh Mohammed Issa, wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya Mufti wa Bakwata, Sheikh Issa Shaaban Simba, kutangaza kuteua Kadhi na wasaidizi wake Julai mwaka jana mjini Dodoma. Baada ya kunukuu aya hiyo, Sheikh Issa alifafanua kwamba, awali wakati Mufti Simba anawateua wajumbe wa Kiislamu kuunda Kamati ya kushughulikia mchakato wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini, aliwaeleza baadhi ya wajumbe hao kwamba anamfahamu vizuri Sheikh Simba, kwamba si kiongozi wa kuaminika katika kufanya maamuzi kwani anaweza kubadilika wakati wowote. Alisema anamfahamu vizuri kwa sifa hiyo tangu alipokuwa Sheikh wa Bakwata mkoa wa Shinyanga. Sheikh Mohamed Issa alisema kutokana na tabia hiyo ya Mufti, aliwahakikishia baadhi ya wajumbe wa Kamati ile kuwa hawatafika pale walipokusudia kwa kuwa Mufti atawageuka. Maneno hayo ya Sheikh Mohammed Issa, aliyatoa b a a d a ya M u f t i S i m b a kutangaza kuteua Makadhi mjini Dodoma Julai mwaka jana, wakati Kamati ya Kushughulikia Kurejeshwa mahakama ya Kadhi nchini ikiwa haina taarifa jambo lililowashangaza Waislamu wengi. I k i wa n d i o u m e t i m i a mwaka mmoja tangu Mufti Simba, alipoamua kuipuuza Kamati ya pamoja ya Waislamu iliyokuwa imepewa jukumu la kushughulikia mchakato wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini na kuamua kuteua Makadhi wake, sasa anaililia serikali kwa kutowatambua kisheria Makadhi aliowateua. Mufti Simba alitoa malalamiko hayo wakati walipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita
h i y o ya h a r a k a , a wa l i iliundwa Kamati ya pamoja iliyojumuisha viongozi mbalimbali wa taasisi za Kiislamu nchini na wajumbe kutoka serikalini chini ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwa ajili ya kushughulikia mchakato mzima wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini. Wajumbe wa Kiislamu walitaka mahakama hiyo iendeshwe kwa gharama za serikali kwa kuwa Waislamu nao ni walipa kodi na sehemu ya jamii ya Tanzania inayohitaji huduma ya kijamii ya serikali. Aidha walitaka mahakama hiyo ipewe nguvu kisheria kwa kutambuliwa na katiba ya nchi ili isije kupuuzwa na kudharauliwa kwa kukosa nguvu za kisheria. Wajumbe wa Kiislamu walitambua kuwa iwapo hilo lisingefanyika, basi mahakama hiyo isingeheshimiwa na hukumu za mashauri yake yasingeheshimiwa pia kwakuwa yasingetambuliwa kisheria. Hata hivyo Maaskofu walikuja juu na kusisitiza kwamba hawawezi kukubali serikali kutumia fedha za watu wa imani zote hudumia Waislamu pekee na kuongeza, mahakama ya kadhi kutambuliwa na katiba ni sawa na kuisilimisha n c h i h i v y o h a wa k u b a l i kuanzishwa mahakama hiyo. Waislamu nao walihoji kuwa, kama kanisa na serikali wanatambua hilo, iweje serikali hiyo hiyo ikasaini mkataba kati yake na Kanisa wa mwaka 1992, ambao unairuhusu serikali kutoa fungu la fedha za walipa kodi wakiwemo Waislamu, kwenda kwa makanisa kwa ajili ya kugharamia huduma zinazotolewa na kanisa. Hoja hizo na msiamo wa Maaskofu uliifanya serikali kupiga danadana suala la kuanzishwa mahakama ya Kadhi hadi leo. Itakumbukwa kwamba mwezi Juni mwaka jana, Serikali ilisema uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi itakayoshughulikia migogoro na masuala mbalimbali ya ustawi wa Waislamu nchini umefikia katika hatua nzuri. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo wakati akijibu hoja za wabunge zilizojadili kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2012/2013. A l i s e m a i t a a n z i s h wa wakati wowote baada ya maandalizi kukamilika na
12
AN-NUUR
MAKALA
AN-NUUR
12
Na Bakari Mwakangwale
SERIKALI imetanabaishwa k u ya t a f u t i a u f u m b u z i wa k u d u m u m a d a i ya Waislamu nchini ambayo yamewasilishwa kwa nyakati tofauti ili kuepusha msuguano uliopo sasa. Hayo yamesemwa na Ustadhi Suleiman Daud, akiongea na An- nuur, a k i z u n g u m z i a h a l i ya mvutano baina ya Serikali, Masheikh na Waislamu unaondelea sasa. Ust. Daud, alisema hali iliyopo sasa inatokana n a S e r i k a l i k u s h i n d wa kuyatafutia ufumbuzi m a d a i y a Wa i s l a m u na sasa wanapoamua kuitahadaharisha wanasakamwa kwa uchochezi. Hali hii inatokana na Serikali inayojinadi kuwa ni sikivu na adilifu, lakini inapuuza kabisa kuyafanyia kazi madai ya Waislamu na kujaribu kutaka kuwaziba mdomo kwa kutumia vyombo vya dola, jambo a m b a l o n i h a t a r i k wa mustakabali wa Taifa hili. Alisema. Ust. Daud, alisema kimaumbile binaadam, a n a p o h i s i k u o n e wa n a akafikisha malalamiko yake sehemu husika ili apate ufumbuzi kisha akapuuzwa na kufikia hatua akashindwa kuona wapi apeleke madai na malalamiko yake, hufika mahali akasema, sasa basi, liwalo na liwe. Ust. Daud, aliye Amir wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Kuendeleza Uislamu, alisema hivi sasa madai ya Waislamu Serikali yanaonekana kuwa ni uchochezi kabla hata kuyajadili au kuyafanyia utafiti. Ust. Daud, alisema ikiwa madai ya Waislamu ni uchochezi bila shaka ( Wa i s l a m u ) w o t e watafunguliwa mashitaka. Alisema, kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, Waislamu wana haki na wajibu wa kutendewa haki kama ambavyo Serikali inavyowatendea makundi mengine. Amir Daud, alisema Waislamu wana kumbukumbu kuwa waliunda makundi yaliyowawakilisha Wa i s l a m u k u wa s i l i s h a madai yao Serikalini moja
Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org. ya madai ya Waislamu na jinsi wanavyopuuzwa na kusababisha yote hayo mfano wa kadhia hiyo ya Wanafunzi wa Ndanda. Akahoji, ikiwa Serikali inapelekewa matatizo ya raia wake ili iyatafutie ufumbuzi, wao (Serikali) hawataki h a t a k u f a n ya m j a d a l a , wanategeme Masheikh hao wakisimama jukwaani mbele ya Waislamu watasema nini. Alisema, kupitia MoU, Serikali inatoa mabilioni ya pesa kuyapa Makanisa kwa ajili ya kuendeshea miradi yao, ilihali Serikali inajua kuna makundi mengine ya kiraia lakini imeyapuuza na kuidhinisha kinyemela kundi hilo moja kupewa pesa hizo. Waislamu, wamekuwa wakihoji siku zote suala hili, majibu yake ni kuonekana kuwa ni wachochezi, na sasa ili Masheikh wasiseme haya, Serikali inaona ufumbuzi wake ni kuwapigwa risasi. Alisema Amir Daud. Alisema, si hayo tu kuna tukio la kuuwawa Waislamu katika kadhia ya Msikiti wa Mwembechai, pamoja na Waislamu kupeleka madai yao ili iundwe Tume huru ya kuchunguza mauaji hayo, Serikali imewapuuza. Akizungumzia madai ya Waislamu Serikalini kuhusu Baraza la Mitihani la Taifa, Amir Daud, alisema Waislamu wamelalamika muda mrefu juu ya namna vijana wa Kiislamu wanavyo felishwa, lakini alidai pia walipuuzwa.
Rais Hassan Rohani wa Iran. Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan na Iraq. Kwa upande wake, Akhoundzade, amesisitiza juu ya ulazima wa kuendelezwa ushirikiano wa Iran na Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hasa mgogoro wa Syria.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.