Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 21

Zanzibar Daima

J AR IDA L A KI LA M ZANZIBARI
www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

JARIDA LA KILA MZANZIBA R I

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Online

06
Ni
Toleo

K AT I B A M P YA Zanzibar yashika mpini


Kurasa zaidi ya 40 kutoka ZDO

Bure!

Uk.08

Uk.12

Uk.14

Ubaya Ubaya watuondoshee Wazungu?

Bila ya Wazanzibari hakuna Katiba Mpya

Kupima maendeleo kwa kutoendelea

L I M E D H A M I N I WA N A Z A N Z I B A R I M A G E . C O M

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI

Penye

Nia
pana njia

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

Yaliyomo
Mazungumzo Baada ya Habari
Uk. 18. Farrel J Foum
Kikwete akithubu ataweza

Z anzibar Daima
J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI
www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Online

afari hii Jabir Idrissa ametuletea makala yenye kuthibitisha ule usemi kwamba panapo nia pana njia. Haukwenda arijojo ule msimamo wa Wazanzibari, wakisaidiwa na vyama vikuu vya Upinzani vya Tanzania, wa kushikilia kwamba hawakushirikishwa katika kujadili Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Rais Jakaya Kikwete na serikali yake wamebidi waje matao ya chini na wakiri kwamba kwa hilo kweli Wazanzibari hawakutendewa haki. Na sasa serikali ya Jamhuri ya Muungano imeridhia kufanya marekebisho mapya katika hiyo Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, licha ya kuwa Kikwete amekwishatia saini yake katika waraka huo. Hilo si fanikio dogo. Wala halikupatikana kwa urahisi. Ni wazi kwamba serikali haikutaka matokeo ya kadhia hiyo yawe kama yalivyokuwa. Lakini Wazanzibari na wapinzani walipata ushindi kwa sababu mbili. Kwanza walishikamana na kuwa na msimamo mmoja na pili, walisimama imara kuutetea huo msimamo wao. Hawakugawika wala hawakuyumbayumba. Hivyo ndivyo upinzani, katika mfumo wa kidemokrasia, utakiwavyo uwe. Kila

pale serikali inapojaribu kukata maamuzi kibabe vyama vya upinzani vinawajibika kuzitupilia mbali ari zao na kuungana viwe na msimamo mmoja dhidi ya serikali.

Tufungue Kitabu
Uk. 24. Ridder Samsom
Sitiari za Mzee wa Kimbunga

Timu Yetu
MHARIRI MKUU Ahmed Rajab Email: ahmed@ahmedrajab.com MHARIRI MSAIDIZI Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com MHARIRI MSANIFU Hassan M Khamis Email: hassan@zanzibarimage.com COMMUNICATION MANAGER Hassan M Khamis WAANDISHI Jabir Idrissa Email: jabirgood@yahoo.com Othman Miraji Email: mwinjuu@hotmail.com Hamza Rijal Email: babujimba@hotmail.com Salim Said Salim Email: sssalim47@yahoo.com Ally Saleh Email: allysaleh126@gamil.com WASAMBAZAJI mzalendo.net zanzibardaima.net zanzibardaima/facebook MATANGAZO Hassan M Khamis Simu: +44 7588550153 Email: hassan@zanzibarimage.com WASIALIANA NASI zanzibardaimaonline@gmail.com JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA Zanzibar Daima Collective 233 Convent Way Southall UB2 5UH Nonnstr. 25 53119 Bonn Germany

Mkeka wa Mwana wa Mwana


Uk. 20. Riziki Omar

Kalamu ya Bin Rajab


Uk. 28. Ahmed Rajab
Hofu na chuki hazina tena nafasi Zanzibar

Mhariri

Mkuu
Muungano.

Zanzibar iuzwapo kwa kikombe cha chai

Ahmed Rajab

Waraka kutoka Bonn


Uk. 22. Othman Miraji
Serikali ni sisi sote

Kauli ya Mwinyi Mkuu


Uk. 32. Jabir Idrissa
Tangu lini Stendi ya gari ikawekwa barabarani

Vikifanya hivyo, serikali huwa haiwezi kufua dafu na kujifanyia itakavyo ikiyapuuza matakwa ya wananchi. Fanikio hilo la vyama vya upinzani ni funzo pia kwamba lau vyama hivyo vitauendeleza umoja wao basi vitaweza kuleta miujiza ya haraka katika siasa za Tanzania, miujiza ya kushindwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi ujao wa 2015. Tokea hapo chama hicho kinaregarega Bara na Visiwani na kuna ishara nyingi zenye kuashiria kwamba kitapata taabu kuunyakua ushindi kama ilivyo kawaida yake. Sasa vyama vya upinzani vikiweza kushikamana na kuwa na mkakati wa pamoja wa kukibomoa chama hicho katika kila jimbo la uchaguzi ni rahisi kukiona chama hicho kikongwe kikiporomoka katika majimbo mengi ya uchaguzi katika sehemu zote mbili za

Swali ni kuwa je, vyama vya upinzani vitaweza kweli kuvumiliana, kuaminiana na kuwa na msimamo wa pamoja wenye lengo la kukingoa kwenye madaraka chama cha CCM. Na kama hivyo vyama vya upinzani vitaweza kusahau tafauti zao na vikawa na umoja kutazuka maswali mengine: je, CCM nacho kitajiachia kilale kikijua kwamba mshikamano wa vyama vya upinzani utakiua? Au kitafanya hila zake za kuviingilia vyama hivyo, kuvifitinisha na kuvifanya vikinzane vyenyewe kwa vyenyewe ili vipwae visiweze kuwa na nguvu za kutosha kukikabili CCM? Tunamaliza kwa kuyarejea yaleyale kwamba vyama vya upinzani vinaweza kukiangusha CCM endapo vitakuwa na nia ya dhati ya kufanya hivyo

www.zanzibardaima.net Zanzibar Daima Online Toleo 05

UKURASA PAGE

3 03

UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

HABARI KUU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Zanzibar yashika mpini kisu cha Katiba Mpya


Hata hivyo, pamoja na wakuu wa Serikali ya Muungano chini ya Rais Jakaya Kikwete kuandaa mapendekezo mapya ya kuirekebisha sheria iliyotungwa mwaka 2011 na Bunge, mjini Dodoma, kuna ripoti zinazosema kuwa vyama vya upinzani vimezuia mapendekezo hayo kuwasilishwa bungeni mpaka kwanza vijiridhishe kama ndiyo yaliyokubaliwa. kuhakikisha kila kitu kimekwenda kulingana na makubaliano yao. Hatua hii ni ya lazima kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwaachia watendaji wa serikali waamue peke yao kunaweza kuleta matatizo mengine, chanzo cha habari hizi kimemnukuu mmoja wa wajumbe wa timu ya wataalamu ya vyama hivyo.

Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar Abubakar Khamis Bakari [katikati], akizungumza na Waziri Mkuu Mizengo Pinda [kulia]

B
UKURASA PAGE

Na Jabir Idrissa Habari Kuu

AADA ya Zanzibar kupaisha kilio kizito cha kutoshirikishwa katika kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, sasa imesikilizwa. Si hivyo tu lakini tayari serikali imeridhia kupeleka marekebisho mapya katika sheria hiyo, Zanzibar Daima Online limefahamishwa.

Mpashaji habari huyo amemnukuu mjumbe wa timu ya wataalamu ya vyama akisema kwamba mapendekezo ya kurekebisha sheria ya katiba yamezingatia vilio vya kila Taarifa kutoka ndani ya serikali upande likiwemo suala la kupatikana kwa zote mbili, Ofisi ya Bunge, na usawa wa wajumbe wa Bunge Maalum vyama vya siasa vilivyounda la Katiba kati ya Zanzibar na Tanganyika, umoja wa kupigania haki ya kinyume na ilivyowekwa katika sheria hiyo kusikilizwa wakati serikali ilipambayo kupitishwa kwake kulizua mtafaowasilisha mswada wa sheria ruku hasa pale Zanzibar ilipolalamika kwa ambao hatimaye ulipitishwa kutoshirikishwa katika kujadili mapendekinyemela na wabunge wa kezo yaliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Sheria na Katiba wa Serikali ya Muungano Mwenyekiti wa Tanzania Labour ya kurekebisha sheria ya 2011. (TLP) Augustine Mrema pekee, zinasema mapendekezo hayo Kwa sababu ya hatua hiyo ya vyama kuzuia mapya yatasubiri mwafaka. mapendekezo hayo mpaka kwanza kujiridhisha, huenda sasa Mswada wa marekebiKwa mujibu wa taarifa hizo, sho ya sheria ile ukawasilishwa kwa njia ya viongozi wa Chama cha Wanan- dharura, badala ya utaratibu wa kawaida chi (CUF), Chama cha Demokra- wa kuzingatia muda wa kuusoma mara sia na Maendeleo (Chadema) na mbili kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. NCCR-Mageuzi, waliounda timu ya wataalamu wa kuchambua mapendeTaarifa za karibuni kutoka Ofisi ya Bunge kezo yanayopaswa kuzingatiwa katika zimesema kuwa kama ni mapema kuliko kurekebisha sheria hiyo iliyopitishwa na ilivyokusudiwa hapo kabla, basi mswada Bunge Septemba 6, wameona ni muhimu huo unaweza kuwasilishwa bungeni katika kujiridhisha na mapendekezo ya serikali. siku mbili za mwisho za mkutano wa bunge unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa, amWameona ni muhimu kwao kuyapitia bao ulianza Jumanne ya wiki iliyopita. mapendekezo yenyewe ya marekebisho kama yalivyoandaliwa na Serikali ili kujiriJarida hili limefanikiwa kuyaona mapendedhisha kwa sababu wanadhani ipo haja ya kezo yaliyoandaliwa awali na timu ya wataUKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

alamu ya vyama vilivyoungana, mara baada ya kukutana na Rais Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, katika mkutano ulioitishwa kama njia ya kupata mwafaka na vyama hivyo vitatu vilivyopinga Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwa ilipitishwa kinyemela. Suala la Zanzibar kuingiza wajumbe kwa idadi sawa katika Bunge Maalum la Katiba pamoja na wale watakaotoka Tanganyika, limezingatiwa na mwafaka umefikiwa kuwa wajumbe wa bunge hilo litakalojadili na hatimaye kupitisha Rasimu ya pili ya Katiba, watakuwa sawa. Mapendekezo hayo yanaonesha kuwa bunge litakuwa na wajumbe 908 wakiwemo zaidi ya wajumbe 200 watakaotokana na uwakilishi wa asasi za kiraia ambazo sasa zinatajwa rasmi ndani ya sheria, kinyume na ilivyokuwa awali wajumbe hao kuwa 166 na ambao wangeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na taasisi zilizobainishwa. Sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM na Mrema pekee haikutaja orodha ya taasisi na iliachia mamlaka ya uteuzi kwa Rais kwa utaratibu wa kupelekewa majina ya wajumbe tisa kila taasisi, naye kuteua angalau watatu kati yao. Sheria hiyo ilipingwa tangu pale kambi rasmi ya upinzani bungeni iliposema kuwa utaratibu huo utampa nafasi Rais kuongeza wajumbe wenye mtizamo anaoutaka yeye, huku tayari kiongozi huyo anayetoka CCM akiwa na sauti kubwa inayotokana na wabunge wa sasa pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Ni malalamiko ya kambi ya upinzani bungeni kuwa katika mazingira ambayo Bunge Maalum la Katiba litakuwa na wabunge wa sasa; wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, CCM itakuwa na sauti kubwa na itakuwa

kubwa zaidi iwapo Rais atabaki na mamlaka ya kuteua wale wajumbe 166 kutoka makundi ya taasisi za kiraia. Hili Rais Kikwete alilielewa vizuri. Lakini alitaka viongozi wa vyama pamoja na chake cha CCM wakakae na kujadiliana namna watakavyoliwekea utaratibu wa kuteuliwa wajumbe nje ya utaratibu wa sasa. Makubaliano yalifikiwa hapa na hata walipokutana baada ya hapo, walielewana haja ya taasisi zenyewe kuteua wajumbe wenyewe kwa kuwa wanaelewana, alisema ofisa mwandamizi ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam. Pendekezo jingine lililoridhiwa kuwa nalo lijumuishwe katika marekebisho yatakayopelekwa bungeni, ni lile la kuwekwa kiwango cha kura za upitishaji rasimu ya katiba cha zaidi ya nusu ya kura za kila upande kati ya Zanzibar na Tanganyika. Hii ni kura ya maoni itakayopigwa kwa ajili ya kupitisha katiba mpya baada ya Bunge Maalum la Katiba kuipitisha rasimu ya mwisho. Taarifa zinasema kuwa utaratibu wa awali wa sheria iliyopitishwa na bunge Septemba mwaka huu, kwamba katiba itatamkwa kuwa tayari imeidhinishwa rasmi na wananchi iwapo kura ya maoni iliyopigwa mara ya pili itakuwa na matokeo yaleyale ya kutopatikana kwa theluthi mbili za kura kwa kila upande wa washirika wa Muungano. Suala hili la kiwango cha upitishaji Katiba limekuwa nyeti hasa kwa kuwa serikali ilitaka theluthi mbili isipopatikana pale ambapo kura ya maoni ilipigwa kwa mara ya pili, baada ya mara ya kwanza kutofikiwa, basi Katiba iwe ndiyo imepitishwa. Vyama vya upinzani ndani ya bunge vilipinga utaratibu huo kwa kusema si wa

kidemokrasia na hautakuwa umezingatia uhalali wa kila upande wa Muungano kutoa kauli thabiti ya kama umeiridhia Katiba au umeikataa. Walitaka kiwango cha kura kiwe asilimia zaidi ya 50 ya uamuzi. Utaratibu huo ulipingwa na taasisi za kiraia za pande zote mbili: Zanzibar na Tanzania Bara. Wiki iliyopita, Muungano wa Asasi za Kiraia nchini Tanzania (AZAKI) uliokutana jijini Dar es Salaam, ulitaka sheria itamke wazi nini kitafanyika ikitokea upande mmoja umeikataa Katiba katika kura ya maoni. Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), ambaye pia ni kiongozi wa AZAKI, Usu Mallya, alisema Katiba inayohangaikiwa ni ya Watanzania. Upo ulazima wa kila upande wa Muungano kutoa sauti yake ndipo itakuwa yapo makubaliano na maridhiano katika kupitisha Katiba mpya ya taaifa. Mvutano mkubwa ulitokea wakati mswada wa sheria ulipowasilishwa bungeni Septemba 4 na Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Muungano, Mathias Chikawe. Kambi rasmi ya upinzani ilitaka mabadiliko lakini kutokana na mazingira magumu yaliyotumika kuongoza mkutano, wabunge wa upinzani waliona wamekandamizwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai na waliamua kutoka nje. Kutoka kwao kulilazimisha wakutane nje ya ukumbi wa Bunge, halafu wakaafikiana kuendeleza umoja wa kupinga sheria iliyopitishwa huku wakieleza bayana malalamiko yao pamoja na kasoro za mswada ambao wakati huo ulikuwa ukisubiri kusainiwa na Rais ili uwe sheria rasmi. Kutoshirikishwa kwa Zanzibar katika ku-

jadiliwa kwa mapendekezo ya mswada huo, kuliibuliwa na Mbunge wa Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), aliyetoa hoja hiyo aliposimama na kuomba mwongozo wa Spika kuhusu kutoshirikishwa kwa Zanzibar katika jambo hilo. Naibu Spika Ndugai aliahidi kutoa majibu ya mwongozo huo, pamoja na mingine miwili yaliyoombwa baadaye, katika wakati mwafaka. Hakutoa ufafanuzi wa kauli hiyo na wapinzani wakaichukulia kuwa ni kauli ya kuwapuuza. Waliposhikilia kutaka majibu ya miongozo yao, ukiwemo na ule uliotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), waligoma kupitia kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), ambaye hatimaye aliamriwa na Ndugai atoke nje. Alipogoma, na wabunge wa vyama vingine kumkingia kifua asitoke, ndipo naibu spika huyo alipoamuru askari wa usalama waingie ukumbini na wamtoe kwa nguvu. Wabunge waliamua kutoka naye na hatimaye mjadala wa mswada ukaendelea kwa wabunge wa CCM pekee kushiriki, pamoja na Mrema, mpaka kuupitisha mswada. Nje ya Bunge, Zanzibar ilishikilia kuwa haikushirikishwa hasa pale Waziri wake wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakary, aliposema baadaye kuwa yale yaliyowasilishwa bungeni siyo hasa yaliyofikishwa serikalini na kujadiliwa na kutolewa maoni. Waziri Abubakar alisema kwamba wakati mswada ulioletwa serikalini ulikuwa na vifungu vinne, ule uliowasilishwa bungeni, ulikuwa na vifungu 12, vikiwemo vile ambavyo vina matatizo makubwa kwa maslahi ya Zanzibar iwapo vitabaki hivyo

UKURASA PAGE

UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Hata Ubaya Ubaya watuondoshee Wazungu?

Vijana wa CCM Zanzibar katika moja ya mikutano yao ya hadhara

Na Ally Saleh

Barza ya Jumba Maro

iki hii zilizuka habari kuwa kumeanza juhudi za kupunguza na pengine baadaye kuondoa kabisa vitendo vya kikundi kinachojiita Ubaya Ubaya ambacho kimekuwa maarufu kwa vitendo viovu inavyovifanya bila ya kuwa na hofu yoyote ya kuchukuliwa hatua.

vimekuwa vikidaiwa kufanya vitendo vya uharibifu, unyanganyi na uchomaji wa maeneo mbali mbali hasa mara tu hali inapoelekea kuchafuka.

Lakini kwa wakaazi wa maeneo mengine ya nje ya mji wa Zanzibar, Ubaya Ubaya ni kikundi wanachoishi nacho kila siku. KimeKikundi hicho ni kikuu mion- kuwa kama vile vikundi vya goni mwa vikundi vyengine kijambazi vya Ulaya vyenye vidogo vidogo ambavyo kutawala maeneo kihalifu.
UKURASA PAGE

Hivi sasa kuna maeneo ambayo ni shida kukalika. Kwa mfano, mtu hawezi kutoka nje ifikapo saa fulani, kama mwanamke anataka kutoka nje huku akivaa dhahabu basi lazima azivae dhahabu zake kwa kificho. Chako kikitakiwa basi ni lazima ukitoe. Katika maeneo hayo Askari Jamii na hata Askari Polisi hawana ubavu wowote ule. Kuna maelezo ya kwa nini kikundi hiki au vyengine

kama hiki vimezuka. Na mengi ya maelezo hayo yanaelekeza katika rubaa za kisiasa kwamba ndio walioviunda au kusababisha kuundwa vikundi hivyo. Ndipo wengi walipoanza kujenga imani kuwa, kwa mfano, matukio makubwa ya fujo za mwaka jana ambazo zilipelekea kuzuka kizaazaa cha wiki moja na hatimaye kukamatwa viongozi wa Uamsho, vilihimiz-

wa na kukuzwa na makundi ya Ubaya Ubaya na yanayofanana nayo.

Si rahisi kuamini kuwa chama hicho kinahusika rasmi na vikundi hivyo. Lakini maelezo yanasema kuwa vikundi hivyo vimetokana na Imani ya watu ni kuwa vijana ambao wameshindkwa vile vikundi hivi haviwa kutimiziwa ahadi na jachukuliwa hatua yoyote CCM baada ya kushiriki ile na Polisi na wala havikatika harakati mbali mbali jalalamikiwa na upande mmoja wa siasa za Zanzibar hasa za kiuchaguzi. basi tabaan viunaungwa mkono na Chama cha Map- Kadri ninavyojua CCM haiinduzi (CCM) kwa sababu jawahi kutoa kauli kujibu vina manufaa na upande shutuma hizo. Kwa upande huo wa siasa za Zanzibar. mwingine, Chama cha WaUKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

nanchi (CUF) kupitia Katibu Mkuu wake Maalim Seif Shariff Hamad kimetoa lawama za wazi juu ya vitendo vyao na kujiuburi Polisi kuchukua hatua.

Naamini Wazungu hao watatizama suala hilo kisaikolojia na kijamii lakini pia watalitizama katika siasa na siasa za ushindani na Kwa mujibu wa taarifa tulizo kuibuka na jawabu za kwa nini hali imefikia kama ilivyo nazo ni kuwa Ubalozi wa na wakati huo huo kutoa Hakuna taarifa yoyote kuwa Marekani na shirika moja mapendekezo ya kulimaliza. Polisi imechukua hatua ma- la Norway ndio walioamua kini kukivunja kikundi hicho, kuifanya kazi hiyo amwala kuomba msaada wa bayo kihalali kabisa ilikuwa Ingawa Serikali yetu Shirika la Uchunguzi wa Jinai tuifanye sisi wenyewe ama imeshindwa lakini Wazungu la Marekani (FBI) ili kujipe- kwa kutumia nguvu za Polisi hao watagundua kuwa nyeza katika kikundi hicho au kwa rai za Serikali. vijana hao wametumiwa na kukisambaratisha kwa vibaya, wamejazwa jazba na sababu ni tishio kwa watu ukatili, wamejengwa imani Wazungu ndio Wazunwengi na mustakabali wa mbaya kuwa wasiokuwa wa gu bwana. Nina hakika kiusalama wa Zanzibar. watakaa na vijana hao, am- chama chao au wasiofanana bao kwa hakika wana madai nao kifikra ni maadui na waTaarifa zilizoenea wiki hii yanayoweza kujadilika ili pia nafaa kufanyiwa ubaya na ni kuwa sasa Wazungu wawaonyeshe juu ya ubaya labda ndio pakazuka Ubaya Ubaya. wameamua kulipania suala na hasara za matendo yao la Ubaya Ubaya ili kulijua na ubaya na hasara hizo undani wake na tabaan ku- zinavyoweza kuwarudia Wazungu watawaeleza wachukua mbinu za kukivunja wenyewe. jibu wa kiraia, watawafundikikundi hicho, jambo ambalo sha kuwa wazalendo, wa-

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, japo haijashindwa lakini ilikuwa haina nia ya kisiasa kulichukulia hatua.

tawaelekeza juu ya wajibu wao katika jamii na jinsi ya kuwa raia wema na kwamba hiyo ndio nguzo muhimu ya kujenga nchi yao ambayo haipaswi kurudi ilikotoka hasa baada ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Na Wazungu hao wataendelea kuwaambia Ubaya Ubaya au wengine kama hao kuwa wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa sababu mwisho wake ni kuachwa wao wakamatwe na mkono wa sheria, mbali ya kuhasimiana na ndugu na jamaa na kujijengea tabia ya uovu bila ya sababu. Hawa Wazungu watagundua jambo ambalo Serikali ya Zanzibar imeshindwa

kugundua. Nalo ni kuwa vitendo kama hivyo ndivyo vinavyotumika kuwa mbolea ya kuzalisha makundi ya kigaidi na kuwa njia moja ya kuwazuia Al Shabaab na Al Qaida kuingia nchini ni kuwapa uwezo wa kujiamulia hatma yao vijana wetu. Mwisho kabisa Wazungu hao watashauri kuwa tatizo kubwa ni ajira. Ukiwapatia ajira vijana hao na kuwaondosha vibarazani, ukiwapa senti mfukoni na kutowafanya kufikiri wala kutokubali kutumiwa na mtu yoyote, hasa wanasiasa wetu, basi utaweza kulipatia dawa tatizo hili. Sasa Wazungu wakishalimaliza hili tatizo la Ubaya Ubaya uso wa Serikali yetu

utakuwa wapi? Tupewe misaada ya kifedha sawa, basi pia misaada ya kukabili matatizo kama ya makundi kama haya ambayo tunajua hakika yana hasara na yanaweza kuwa na madhara ya kuenea na kuleta madhara, mpaka pia waje Wazungu watusaidie? Hivi muda wote wa matendo ya Ubaya Ubaya na makundi kama hayo, Serikali yetu ilikuwa ikiwaza nini? Natamani ningeingia ndani ya ubongo wa Serikali kujua nini kilichokuwa kikiendelea. Kwamba Ubaya Ubaya itayeyuka yenyewe na kusambaratika? Kama dhana ilikuwa hiyo basi ndio maana tukasubiri mpaka Wazungu waje hata hili watumalizie?

Vichwamaji Tungenao
Vichwa maji wangalipo, tunao tele kibao Pande zote wao wapo, zi tele alama zao Kisikiza wasemapo, utajuwa hawa ndio Chuki ndiyo lugha yao! Hawaoni japo yapo, na wanayo macho yao Kamwe hawasikiipo, wangawa na masikio Hata nyoyo zidundapo, haziji fikira zao Hasira sauti yao! Walipo ndipo walipo, kwenda mbele mwiko kwao Kazi yao ni viapo, kushindana ndiko kwao Na katu hawashindwipo, sababu ujinga wao Hikima si hadhi yao! Basi wapo tele wapo, waoneni muonao Wapapo kila tulipo, na ni kubwa namba yao Nchi haitakuwapo, kifatwa wayatakayo Vichwa vyao ni vimeo!
UKURASA PAGE

Siri Mtungini
Siri ya mtungi, kata ndie mjuaji Nasema wala sivungi, maneno yaso dibaji Vimenisakama vingi, vyengine sikutaraji Mungu ndie mlipaji Mwanzo sikuweza sema, nilibaki kulalama Moto umesharindima, wanishinda kuuzima Si wima si uchutama, naitafuta khatima Hata juu ya vilima Kiza hutanda kwa ndani, nje kuna mwanga wake Siri siri mtungini, ikitoka ni mashuke Kata wanyamaza nini, yaseme usisumbuke Au waogopa teke Mtungi hukaa sana, hadi mwisho huvunjika Maji yalotulizana, mwisho nje humwagika Na hayazoleki tena, maji yakishamwagika Cha ndani kishaoneka

LLADHA YA BETI A D ETI H B A A Y

Mohammed Ghassani- Bonn - Ujerumani

Ally Hilal, Wete, Pemba

10

UKURASA

11

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI

TANBIHI

Bila ya kuwashirikisha Wazanzibari, hatutakuwa na Katiba Mpya


Septemba 2013. Kwa mnasaba wa mjadala mpana wa kitaifa na kwa kuwa Rais Kikwete aliagiza kurejeshwa tena Bungeni kwa sheria hiyo hata baada ya kuiweka saini, tunachapisha Nukta ya 3 na ya 5 ya waraka huo wa vyama vya upinzani kwa Rais, ambazo zinazungumzia nafasi na ushiriki wa Zanzibar Mhariri. ria na Katiba na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambavyo amesema kuhusu mchakato wetu wa Katiba Mpya, katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa. Hata hivyo, Mheshimiwa Rais, dhana hii ya haki na hadhi sawa kati ya Washirika wa Muungano haijazingatiwa wakati wa kupitishwa kwa Muswada huu. Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalum watakaotokana na wajumbe 166 walioainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) ... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao. Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55. Kwa sasa Wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76. Kwa ujumla, kwa hiyo, ili kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1) na (2) cha Sheria, Zanzibar itakuwa na wajumbe 214 katika Bunge Maalum, ambayo ni sawa na takriban 35% ya wajumbe wote. Dhana ya haki na hadhi sawa ilikubalika na kutekelezwa wakati wa kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Dhana hii inapaswa pia kukubalika na kutekelezwa wakati wa kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba. Sisi tunaamini kwamba hoja ya usawa wa idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ina nguvu zaidi kuhusu Bunge Maalum kuliko ilivyokuwa kwa Tume. Hii ni kwa sababu, ni Bunge Maalum ndilo litakalokuwa na mamlaka ya kuijadili na kuipitisha Katiba Mpya kabla ya kupelekwa kwenye kura ya maoni ya wananchi. Upande wenye wajumbe wengi utakuwa na nafasi nyingi zaidi za kuzungumza kuliko upande wenye wajumbe wachache. Hii ina maana kwamba hoja za upande huo ndio zitakazosikika zaidi kuliko hoja za upande mwingine. Vinginevyo labda kuwe na masharti ya sheria yatakayolazimu kila upande wa Jamhuri ya Muungano uwe na fursa sawa za kuchangia katika mijadala ya Bunge Maalum. Na kama itakuwa hivyo, kutakuwa na hoja halali kwamba wajumbe ambao hawatapata nafasi ya kuchangia wanaenda kufanya nini katika Bunge Maalum!

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Katikati ya mwezi Oktoba, vyama vitatu vya upinzani Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR-Mageuzi vilimuandikia Rais Jakaya Kikwete mapendekezo yao juu ya namna ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia mgogoro uliojitokeza Bungeni, Dodoma, wakati wa kupitishwa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria ya Kura ya Maoni mnamo mwezi wa

Makala Maalum

una ubishani mkubwa kuhusu kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mchakato wa kupitishwa kwa Muswada huu. Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano imetangaza hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu katika hatua zote za kupitishwa kwa Muswada, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenyewe imetoa kauli zenye utata mkubwa kuhusu suala hili. Kwa mfano, wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amedai hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakari amesema hadharani kwamba ushirikishwaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar uli-

husu vifungu vinne tu vya utatuzi wake unahitaji MusMuswada huu. wada kurudishwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa upya. Vifungu vingine vyote vya Endapo hili halitafanyika Muswada vilivyopitishwa na kama tunavyopendekeza, Bunge havikupelekwa Zan- kuna uwezekano mkubwa zibar na kwa hiyo Serikali kwa Baraza la Wawakiliya Mapinduzi Zanzibar hai- shi Zanzibar kukataa kuridkushirikishwa kwenye ku- hia Muswada huu na hivyo vitolea maoni na msimamo. kufanya utekelezaji wake Aidha, kwa barua yake yenye kushindikana na mchakato kumbu kumbu Na. OMPR/ wote wa Katiba Mpya kukWKS/TS.7/1/62 ya tarehe wamishwa. 13 Septemba, 2013, Makamu wa Pili wa Rais wa Zan- Jamhuri ya Muungano wa zibar amemwandikia Waziri Tanzania ilizaliwa kwa kuunMkuu akimweleza kwamba ganisha nchi mbili zilizokuSerikali ya Mapinduzi Zan- wa huru na zenye hadhi na zibar haikushirikishwa kika- haki sawa, licha ya tofauti milifu katika kupitishwa kwa zao za ukubwa wa eneo au Muswada huu. idadi ya watu wake. Katiba Mpya ambayo mchakato Hii ni licha ya Makamu wa wake umeleta mgogoro wa Pili wa Rais huyo kutangaza sasa inatakiwa kuakisi haki hadharani kabla kwamba na hadhi sawa kati ya nchi Serikali ya Mapinduzi Zan- hizi mbili. zibar ilishirikishwa. Kwa vyovyote vile, suala hili lina Kama ambavyo mtaalamu ubishani mkubwa ambao mmoja wa masuala ya she-

Kwa sababu hizi, tunapendekeza kwamba hadhi na haki sawa baina ya Washirika wa Muungano iliyotumika wakati wa kuunda Tume itumike vile vile katika kuunda Bunge Maalum la Katiba. Kwa maana hiyo tunapendekeza kwamba idadi ya wawakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum iongezwe hadi kufikia nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Hili linawezekana kwa namna mbili. Kwanza, kwa kuongeza idadi ya wajumbe waliotajwa katika kifungu cha 22(1) (c) kama tulivyopendekeza. Na pili, kwa kurekebisha kifungu cha 22(2) ili kisomeke kwamba idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar haitapungua asilimia sitini na nne ya wajumbe hao. Kama pendekezo hili litakubaliwa, wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar wataongezeka kutoka 214 kwa mujibu wa Sheria ilivyo sasa, hadi 438, wakati idadi ya wajumbe wa kutoka Tanganyika nao watakuwa 438. Muhimu zaidi, Bunge Maalum litakuwa limetimiza matakwa ya usawa wa haki na hadhi kati ya Washirika hawa wa Muungano.

UKURASA PAGE

12

UKURASA

13

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

Tukipima maendeleo kwa kutoendelea, hatutaendelea


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Meli ya MV Maendeleo ikipakia karafuu kwenye bandari ya Mkoani kisiwani Pemba.

Na Mohammed Ghassani

Ngurumo la Mkama Ndume

imerudi ziara ya wiki tatu ya nyumbani Zanzibar na nina habari njema, kwamba kote nilikopita Pemba na Unguja kuna dalili za kusonga mbele kama jamii, kama taifa. Kwa mfano, kisiwani Pemba nimekuta barabara inayoiunganisha miji midogo ya Mzambarauni Takao, Wingwi Mapofu, Finya na Mzambarauni kwa Kyarimu na ile inayoziunganisha Likoni na Kangagani zikiwa zimemalizika. Barabara ya KondeUKURASA PAGE

sasa wameamua kuelekeza nguvu zao nyumbani. Mahala palipoangushwa mbavu za mbwa, pameinuliwa nyumba ya tufali la kuchonLakini kando ya barabara ga. zote hizo, mumeota vijumba vizuri vya kudumu vya mat- Kisiwani Unguja halikadufali. Baadhi yake vilizoeleka halika. Maeneo ya mijini kushuhudiwa tu kwenye mi- yanazidi kushuhudia ujenzi taa ya Msasani, Dar es Sa- wa majengo mapya, makublaam au Mazizini, Unguja. wa na ya kudumu. Mitaa ya Michenzani na Darajani Nimeambiwa kasi hii ya kumewekwa taa zinazotuujenzi imechochewa na fidia mia nishati ya jua. Angalau ya wale waliovunjiwa nyum- usiku unakuwa na mwanba zao kupisha ujenzi wa gaza wa kuonana kama si barabara, kupanda kwa bei kuoneana. ya karafuu na pia Wapemba wanaoishi nje ya nchi ambao Kumbuka kuwa nazung-

Wete imetekelekezwa kama ambavyo siku ya kujengwa ya Wete-Chake isivyofahamika.

umzia miaka mitatu ya kutokuwapo kwenye ardhi ya kwetu. Ni kipindi kifupi mno kurudi nikakuta majengo kama yale ya Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar na ujenzi unaoendelea kwa kasi kwenye eneo la Shangani. Maduka ya kisasa Mji Mkongwe na hata jengo jipya la Bandari ya Malindi. Mote pia Pemba na Unguja nimekutana na wavuja jasho wakisaka tonge zao kwa juhudi kubwa. Vijana, watu wazima, wake kwa waume, wanaendelea kufaya kazi za kukimu maisha yao. Hili la kuendelea ku-

fanya kazi nalisisitiza kupingana na dhana potofu iliyojengeka kwamba watu wa pwani, Wazanzibari tukiwamo, ni wavivu na mamwinyi wasiojiweza, wasiojishika. Hapana. Nimeikuta mikono dada yangu mwenye umri wa miaka 45 ikiwa imezidi kusinyaa na kuwa migumu kwa kazi za sulubu. Hata nilipoondoka akanifungia pepeta kutokana na mpunga alioulima, akauvuna na akautwanga kwa mikono yake mwenyewe. Nimepikiwa ndizi mbivu ya Mkono wa Tembo iliyolimwa na mama yetu mwenye umri wa kari-

buni miaka 70 sasa. Ninalotaka kusema hapa ni kwamba watu wangu, Wazanzibari, si wavivu na hawajasita kufanya kazi. Hawajaacha kujituma. Ikiwa miundombinu ya barabara na majengo na kuvuja jasho ni dalili ya kusonga mbele kimaendeleo, basi tukubaliane kwamba Zanzibar inaelekea kwenye njia sahihi ya maendeleo. Lakini kuna walakini. Miaka mitatu ya kuishi kando ya jamii yangu imeniwezesha kuyaona yale amUKURASA

14

15

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

bayo kama ningelikuwamo ndani yake nisingeliyaona. Mojawapo ni huku jamii yangu inavyojipima maendeleo yake kwa kutokuendelea kwake. Na hapa nitapiga mifano miwili mitatu.

ZANZIBAR OCEAN PANORAMA

Kando kidogo, serikali ilijenga soko dogo lakini zuri, ambapo shughuli hizo zingefanyika. Lakini hazifanyiki. Bado watu wangu wanaona kuuza samaki sokoni kutawagharimu zaidi, pengine kwa kulipia kodi ya Kule dikoni kwa samaki jengo. Hivyo, wanabakia na Nungwi, kaskazini Unguja, uholela wa kibiashara. nilikutana na mnada. Wavuvi huwatoa samaki wao moja Mfano huu wa samaki wa kwa moja madauni na kuja Nungwi unazaa mwengine kuwabwaga chini ya Mkun- ndani yake. Bei ya samaki gu. Dalali wa serikali anawa- imepanda sana. Mtungo tia bei na baadaye mnunuzi wa samaki ambao sasa unmwenye fedha nzuri anaka- agharimu shilingi 20,000, bidhiwa. Samaki hawa wa- miaka mitatu nyuma unnagaragara mchangani, geuzwa kwa 7,000, ingawa wanangongwa na nzi na ku- mtu aliyeweza kununua sapigwa na jua. maki hao kwa bei hiyo ya mwaka 2010 ndiye yule yule

anayeweza kuwanunua leo kwa bei hii ya 20,000. Hili linasema kwamba kipato kimeongezeka, lakini halisemi kwamba maisha ya mtu huyo yameimarika. Sijaulizia wala sijataka kujua kuhusu kima cha pato apatalo mlaji wetu wa samaki wa shilingi 20,000. Nasikia Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeongeza mshahara, lakini hauwezi kuwa umeongezeka mara tatu kama alivyoongezeka Tasi wa Nungwi. Hata hivyo, wakati naondoka nikawasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakijisifia kwamba hilo la kuongezwa kwa mishahara ni

hatua kubwa ya maendeleo ambayo haikuwahi kupigwa kwa miaka kadhaa huko nyuma. Huko ni kuyapima maendeleo kwa kutokuendelea kwetu. Kwa hali hiyo hatutaendelea sana na au tukuwa tunapiga hatua ndogo ndogo kama ngoma ya mbwa kachoka, huku tukijisifu kwamba tunasonga mbele. Kama nilivyotangulia kusema, nimewakuta watu wakiumuka jua-mvua kusaka tonge yao. Zao la karafuu limeendelea kuzaliwa kwa wingi kisiwani Pemba. Mchana nimewakuta watu wakiwa mitini wameitawa mikarafuu, mapakacha na

vingowe vyao juu na mapolo yao chini, watoto wao wanaokota vitawi na au wanachuma zilizo matawi ya chini. Jioni nikawakuta wakizinyambua, asubuhi wengine wakizianika, na wengine wakiwa wamezipakia kwenye magari ya ngombe kuzipeleka vituo vya Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) kwenda kuziuza.

kuzivuna, kuzitayarisha na kuziuza.

Licha ya kuwa kwake zao linaloiingizia nchi fedha nyingi za kigeni, bado hakuna maendeleo kwenye sayansi ya ukulima wake. Hatuwezi kupima maendeleo ya kilimo cha karafuu kwa kuangalia bei yake tu, ambayo kwa vyovyote inategemeana sana na soko la dunia na ambaKatika mtiririko huo sijaona lo linaathiriwa pia na aina lililobadilika ingawa naambi- ya mazao tunayoyapeleka wa bei ya karafuu imekuwa huko. ya juu sana. Miaka takribani 200 ya kuwa na mkara- Tubadilike na tuibadili nchi. fuu visiwani Zanzibar, bado Na haya yamo ndani ya mkulima anapaswa kutu- uwezo wa akili zetu kama mia mbinu zile zile za Sul- yalivyo kwenye mikono yetu. tan Barghash bin Said katika

PEMBA
Kwa mapumziko ya raha na furaha ukiwa kisiwani Pemba, fikia kwenye Hoteli yenye huduma za uhakika, vyumba vyenye nafasi ya kutosha
UKURASA PAGE

KWA MAPUMZIKO

Huduma mbali mbali pia zinapatikana kupitia kwenye Hoteli yetu kama, ukodishaji wa Pikipiki, boti, na kupelekwa kuzamia huko Misali.

www.zanzibaroceanpanorama.com
16
UKURASA

17

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI

Kikwete akithubutu,ataweza
bari tutaendelea kumshukuru kwa kuikubali kauli yetu juu ya mabadiliko ya kiutawala Visiwani ambayo pia ilikuwa chanzo cha msukumo wa haya mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Rais Jakaya Kikwete [kulia] akimkaribisha Mbunge Tundu Lissu Ikulu

Na Farrel Jnr Foum Mazungumzo baada ya Habari

oja ya urathi wa Mheshimiwa Nelson Mandela barani Afrika ni utawala wake uliongoza nchi ya Afrika ya Kusini kwa misingi ya usawa, haki na uadilifu wa hali ya juu. Mpaka leo hii barani Afrika ni wachache walioweza kufikia robo ya vigezo vya utawala wa kijasiri wa Mandela na kuondosha ile dhana ya kwamba Afrika haijaweza kutoa kiongozi na uongozi wa uadilifu wa hali ya juu. Tanzania nafasi hii inayo hasa kwa sasa chini ya utawala uliobakia wa Dkt. Jakaya Kikwete ikiwa nia ya kweli ipo ya kuutazama utawala kama nyenzo ya mabadiliko makubwa kwa

faida ya wananchi na nchi yenyewe. Kilichonivuta kuandika makala haya ni tukio la karibuni lililomfanya Kikwete kuwaita wapinzani Ikulu kuzungumzia Rasimu ya Katiba kwa misingi ya umoja na kuwahakikishia wananchi kwamba katika suala hili la Katiba hakuwa tayari kuyumba kwa sababu tu ya wachache wanaohisi kuwa ndio wenye hati miliki ya nchi hii. Kauli za mawaziri wake na kebehi walizozionyesha ndani ya bunge ziliashiria ubabe wa kufuta imani za wapinzani katika upatikanaji wa Katiba ya nchi kwa wananchi wote. Kuwaita na kuzung-

umza nao katika mazingira ya upendo, heshima na furaha imerejesha imani kwetu sisi wananchi wa kawaida kwamba katika uongozi Kikwete bado ni mwokozi na pengine muumini pekee wa kweli wa mabadiliko ya Katiba yatayowajumuisha wananchi wote. Ninaamini kwamba kwa kuridhia uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kutoingilia mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, na kuachia kauli ya walio wengi katika kura ya maoni ya kuidhinisha mabadiliko hayo alionyesha upevu wake wa kisiasa na imani yake juu ya demokrasia. Wazanzi-

mamia haki, sheria na uadilifu. Hakuna nchi ilioweza kupiga hatua bila ya nguzo imara za demokrasia ilio wazi na yenye kufuatwa na kuthaminiwa hasa na watawala. Huwezi kuwa mfuasi wa demokrasia bila ya kuwa na upinzani ulio Kinachostaajabisha ni hawa na kila nyenzo ya kujiendewabunge wa Zanzibar waliod- sha bila ya vitisho vya aina harau usimamizi wa nchi yao yeyote. Upinzani sio uadui kwa kuruhusu mabadiliko bali ni chachu ya maendeambayo yangelivua ngao ya leo ya nchi kwa kila sekta. Zanzibar iliowekwa maalum Kuwathamini, kuwalinda na kujilinda na wachache ambao kuwaheshimu waliothubutu wangeliweza kutumia mwan- kuwa na mawazo tafauti ndio ya wa wingi wa wabunge lengo la demokrasia makini na badala ya mfumo wa thuluthi ndicho hasa kitachomtafautimbili kuleta mabadiliko amsha Kikwete na utawala wake bayo yangeweza kuwa na na wale waliotangulia. athari kubwa hata juu ya kue- Kabla ya kumaliza muda wake ndelea kuwepo kwa Zanzibar tungelitegemea kuwa mbali kama nchi kamili inayojiende- ya kwamba kisiasa marekebisha na kujitegemea. sho ya Katiba yatatoa fursa Kama Kikwete bado ana nia kubwa ya kupatikana maya kuweka urathi mfano wa geuzi, kwa mfano pendekezo Mandela, kipindi cha miaka hii la kuundwa Tume ya uchaguzi miwili na nusu iliobakia akiwa iliojengeka kiuwazi na kiRais wa Jamhuri ya Muungano uadilifu, bado kuna mambo ya wa Tanganyika na Zanzibar kiutawala yanayohitaji kutabasi lazima awe tayari kuwak- zamwa upya. abili wakereketwa wenzake wanaofikiri wana haki zaidi ya Ikiwa Kikwete anayo damu maamuzi ya nchi na uendesh- inayomchemka ya kuacha waji kuliko wananchi wengine. urathi atakaokumbukwa Ningelimshauri Kikwete nao basi lazima mahakama, ahakikishe kuanzia sasa kuwa vyombo vya sheria na vikosi anarejesha heshima yote ya vya usalama vifanyiwe mautawala kwa wananchi kwa geuzi mapya yanayoendana kusimamia ipasavyo haki na na wakati tulionao. Nina amini uadilifu kama kanuni za uonkwamba matatizo tuliyo nayo gozi nchini. Akiwa mwenyekiti sasa yamesababishwa na jinsi wa CCM na Rais wa Jamhuri tulivyozivamia siasa za ushanazo nguvu za kutosha za indani wa vyama vingi bila ya kurejesha heshima ya chama kufanya mageuzi katika taachake kama taasisi ilio safi na sisi za serikali hususan katika inayoendeshwa kwa uwazi sekta inayosimamia sheria za na pia serikali ilio tayari kusinchi. Jeshi la polisi, kwa mfa-

no, limekuwa likitumika zaidi kisiasa badala ya kuimarisha usalama wa nchi. Mwisho ni maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe. Bila ya sera zilizojengwa kwa ari mpya ya kuhakikisha unafuu kwa wananchi na maendeleo kwa nchi bado hataweza kuiweka nafasi yake katika safu ya mashujaa waliothubutu na kuweza barani Afrika. Kwa kipindi hichi cha miaka miwili na nusu iliobakia, Rais angelijaribu kuhakikisha serikali yake inaviweka wazi vipaumbele kuanzia ujenzi wa makazi nafuu ya wananchi, uimarishwaji wa elimu, usimamizi bora wa sera za afya, upatikanaji wa maji safi na umeme wa kudumu. Kwa kipindi kilichobakia haya yakiwa yatatazamwa kwa uangalifu zaidi tutaweza kupiga hatua kubwa na kujenga msingi wa maendeleo kwa anayemfuatia. Nimalizie kwa kumkumbusha yote haya yanawezekana ikiwa nia thabiti ipo, timu imara ipo na sera safi zipo. Kama alivyolikingia kifua suala la mabadiliko ya Katiba ya Muungano na kuhakikisha linakwenda kwa nguvu za wananchi basi na haya manne tulioyaorodhesha yanawezekana. Ikiwa suala la Katiba litapita bila ya shengesha za wafurukutwa na haya maeneo ya maendeleo tulioyaorodhesha yatafanyiwa kazi ipasavyo basi historia itamkumbuka Rais Kikwete kuwa miongoni mwa waliothubutu kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi na nchi na akaweza.
UKURASA

UKURASA PAGE

18

19

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Zanzibar iuzwapo kwa kikombe cha chai


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Na Riziki Omar

Mkeka wa Mwana wa Mwana

atika agizo lake kwenye Semina Elekezi kwa Watendaji wa Serikali kule Ngurdoto, Arusha, mwanzoni mwa muhula wa uraisi wake, Rais Jakaya Kikwete alisema kile alichoona yeye kwenye Muungano si kwamba kulikuwa na tatizo la msingi, bali kukosekana tu kwa mazungumzo baina ya pande mbili zinazounda Muungano wenyewe, Bara na Zanzibar. Kwa hivyo, akaitisha haraka haraka utaratibu wa pande hizo mbili kukutana ili angalau watu wakutane kwa kunywa chai na kahawa pamoja.

laam. Katika sherehe hiyo muhimu, TANU iliwaalika wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria, wengi wao wakiwa machifu kama vile Chifu Kidaha Makwaia, Humbi Ziota, Msabila Lugusha, Mwami Theresa Ntare na wengineo na ikawakirimu waalikwa wao vitafunio, vinywaji baridi na chai. Katika kutoa shukrani za TANU kwa wanachama wa TANU, Mwalimu Julius Nyerere alikamata kikombe cha chai na kukionyesha juu kwa wasikilizaji wake. Akawaambia wasidhani kwamba kitendo cha kumpa mtu chai ni kitu kidogo, maana kuna watu wameiuza nchi hii kwa kupewa kikombe cha chai na wakoloni.

Mazungumzo haya yaliyokuwa yanafanyika baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia kwanza Ofisi ya Waziri Kiongozi na baadaye ya Makamu wa Pili wa Rais ni mazungumzo kwa manufaa ya mazungumzo tu na sio mazungumzo kwa manufaa ya suluhisho. Msimamo huu si wa kibubusa. Una mifano hai ndani ya historia ya karibuni kabisa ya mazungumzo yenyewe. Mmojawapo ni ule wa Ripoti ya Baraza la Mapinduzi la Zanzibar ya 2003. Tarehe 29 Mei 2003, Ikulu ya Zanzibar ilichapisha Ripoti ya Baraza la Mapinduzi juu ya Matatizo na Kero za Muungano na Taratibu za Kuziondoa, ambapo katika sura yake ya tatu, ripoti hiyo ilitoa orodha ya mambo yanayopaswa kuondolewa katika Muungano. Mambo hayo ni: i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. Mafuta na Gesi Asilia Elimu ya Juu Posta Simu (Mawasiliano) Biashara ya Nje Kodi ya Mapato Ushuru wa Bidhaa Usafiri wa Anga Takwimu Utafiti

Katika kuhakikisha kuwa haya yanatekelezeka, SMZ ilitaka kuwepo kwa misingi mitano ya kuzingatiwa, ambayo ni: a. Masuala ya Muungano yalindwe kwa misingi ya Katiba na Sheria badala ya siasa na maelewano b. Muungano uwe na maeneo machache yanayoweza kusimamiwa na kutekelezwa kwa urahisi c. Muungano uainishe washirika wake wakuu, mipaka na haki zao d. Muungano utowe fursa sawa za kiuchumi kwa pande zote mbili za Muungano e. Lazima pawe na Muungano unaoweza kuhimili mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi Hivi ndivyo SMZ ilivyosema tangu mwaka 2003; na kwa hakika kama mwakilishi wa wananchi wa Zanzibar serikali hiyo ilikuwa imesema vile ambavyo Wazanzibari wamekuwa wakisema tangu siku za mwanzo za Muungano huu. Ni wazi kuwa ripoti hii ya SMZ imewahi kuweko mezani kwa Ofisi zote mbili, ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi (na baadaye Makamu wa Pili wa Rais).

Ushirikiano wa Kimataifa xii. Leseni za Viwanda xiii. Polisi xiv. Usalama xi.

wakuu wa serikali hizo mbili, ni taarifa ya kuhuzunisha panapohusika kile hasa kinachohitajika kutatuliwa. Kwa mfano, taarifa ya kikao cha mwisho cha mwezi Mei 2009 iliyotolewa na Ofisi ya Makamu Rais, Idara ya Muungano, ilisema kwamba kero tatu za Muungano zilikuwa zimeshafutwa na kuanzia hapo hazikuwa kero tena. Kero hizo ni Tume ya Haki za Binadamu, Uvuvi wa Ukanda wa Bahari na Shughuli za Biashara ya Meli. Katika mawili ya mwanzo, kufutwa kwake kutoka orodha ya kero ni kwa mambo hayo kukubalika rasmi kuwa ya Muungano, ambapo sasa upande wa Zanzibar uliridhia. La mwisho kufutwa kwake ni kwamba Zanzibar iliruhusiwa kuendesha shughuli za biashara ya meli kwa kushirikiana na Tanzania Bara.

ama kukichukua kila cha Zanzibar na kukifanya cha Muungano na, au, kukifanya kila kilichoko Tanzania Bara kivuke maji na kiwe cha Zanzibar. CCM na Serikali zake zimeufanya Muungano huu ushabihiane sana na kile kisa cha Mfalme Jeta aliyemo kwenye riwaya ya Kusadikika ya Marehemu Sheikh Shaaban Robert. Mfalme huyu alikutwa na mjumbe wa Kusadikika akiwa amekaa katika eneo ambapo mto uliokuwa unakokozoa kila kitu mawe, magogo, majengo, n.k. unatiririkia kinywani na kuishia tumboni mwake, lakini kila mara alisikikana akilia: Njaa! Njaa! Kiu! Kiu!

La kukutana kunywa chai na huku mnazungumzia mambo yanayohusu hatima ya taifa ni jambo zuri sana, lakini mwenendo wa mambo katika kukutana huko daima ulikuwa Upande wa Zanzibar kwenye na umeendelea kuwa na wa- Muungano huu unaheshimu lakini. sana njia ya mazungumzo kama suluhisho la pekee katiUnakumbusha kile kisa ki- ka kufikia utatuzi wa matatizo nachozungumziwa kwenye yanayolikabili taifa. Lakini kitabu cha Mohammed Said mazungumzo yenye uwezo cha Historia ya Abdulwahid wa kutoa suluhisho ni yale Sykes. Kwenye kitabu hicho, yanayozingatia nini kinazunmwandishi anazungumzia tu- gumzwa, nani wanazungukio la tarehe 10 Agosti 1957, mza, vipi na kwa nini yanawakati chama cha kupigania zungumzwa. uhuru cha Tanganyika, Tanganyika African Union (TANU), Kila moja kati ya maswali haya kilipokuwa kinafungua tawi lina maana kubwa kwa hitilake katika mtaa wa Mvita, misho na suluhisho litokananyumba namba 10, Dar es Sa- lo na mazungumzo yenyewe.
UKURASA PAGE

Hivyo ndivyo Muungano wetu ulivyofanywa, kwamba uwe unakula na kunywa kila kitu na bado kila siku uwe unalalamika kufa njaa na kiu. Na ili kuufanya usife, wakubwa wanaaHii maana yake ni nini? Ni mua kuulisha kila cha Zanzibar kwamba, kumbe hakuna pen- na kila cha Tanzania Bara. dekezo lolote la kupunguza idadi ya mambo ya Muunga- Swali ni ikiwa je, katika kumno, kama yalivyo matakwa lisha Mfalme Jeta huyu, Zanziya Zanzibar, lililoweza kuwa bar ilitenzwa nguvu? Jibu molinajadiliwa na vikao hivi vya jawapo ni kwamba hapana, pande mbili; maana chini ya viongozi wa Zanzibar wanaChama cha Mapinduzi (CCM) ohudhuria vikao hivyo wamewahusika wa vikao hivi wa- kuwa wakienda kunywa chai lishaamua kuwa kupunguza tu, huku wakimruhusu Mfalorodha ya Mambo ya Muun- me Jeta ameze kila kile kilicho gano hakuwezi kuimarisha cha Zanzibar, halafu wakarudi Muungano, bali kinyume chake Kisiwandui kusema yasiyoendicho sawa! leweka.

Lakini kinachotokezea kila Yaani, kuimarisha Muungano baada ya kikao cha watendaji kuna maana moja tu, nayo ni
UKURASA

20

21

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Jumba Namba 4 Mtemani Wete Pemba, moja ya alama za mafanikio na pia kurudi nyuma kwa Zanzibar.

Serikali si mama wala baba yetu, ni sisi sote

Na Othman Miraji

Waraka kutoka Bonn

taani kwetu, Mwembetanga, Unguja mjini, kulikuweko mzee akiitwa Ali Mrandazi, mpole, hapitwi na sala ya jamaa msikitini. Alikuwa mtu wa watu, akisomesha bure watoto msikitini, na ndiye pekee tuliomtegemea mtaani kukosha maiti. Hajakosekana katika misiba na harusi za watu na alitumika kwa moyo safi katika shughuli hizo. Kila asubuhi alfajiri, na hata kama inanyesha mvua, Bwana Ali ataelekea Hospitali ya Mnazi

Mmoja huku akishikilia kikapu mkononi kilichojaa machungwa, maembe, ndizi mbivu na matufaa, ikitegemea ni msimu gani wa mazao hayo. Huenda kuwatembelea wagonjwa katika vyumba vyote vya hospitali, na anapofika katika kitanda cha mgonjwa husimama na pamoja naye husoma Suratul Faatiha na kumwachia tunda kitandani. Hiyo ilikuwa katika miaka ya hamsini na sitini.

Karibuni nilipofika matembezini Mwembetanga niMtaa wangu wa likutana na watu Rondorf ninakoishi ambao bado wanam- kwa miaka 37 sasa

kumba Mzee Ali Mrandazi. Waliniarifu kwamba tangu alipokufa mzee huyo miaka mingi iliopita hajachomoza mtu mwingine kuchukuwa nafasi ya kutenda mambo ya kheri aliyokuwa akiyafanya mtaani. Hapa Ujerumani ninakoishi mara nyingi kazi za kujitolea kama alizokuwa akizifanya marehemu hufanywa na makanisa au jumuiya za kutoa misaada ya kiutu ambazo nyingine zina wafanya kazi wanaolipwa.

unanikumbusha ule wa utotoni mwangu wa Mwembetanga. Katika mtaa huu wa sasa kuna watu wachache walio na sifa karibu sawa na za Ali Mrandazi, wako tayari wakati wowote kuwasaidia wenziwao walioko katika shida. Kuna wale wanaotenga masaa fulani katika wiki kwenda mahospitali kuwapumbaza wagonjwa kwa kuwasomea vitabu vya hadithi, magazeti au kucheza nao karata. Kuna wale wanaosafisha magugu ya mtaani yasiokuwa karibu na nyumba zao, ambalo ni juku-

mu la baraza la mji. Hapa Ujerumani kuna milolongo ya harakati za watu wenyewe kushiriki katika mambo yalio kwa maslaha yao ya pamoja. Raia wanafika hadi ya kujiundia jumuiya ndogondogo (Burgerinitiatives), bila ya urasimu, zenye kupigania maslahi yao ya pamoja, wanaelekeza fikra na ubunifu wao kujituma na kujaribu kuyatanzua matatizo yao madogomadogo bila ya kuitegemea serikali. Jumuiya hizo huwa mbioni kufanya mashauriano na maafisa wa serikali na kuwabinya kwa hoja ili zitafutwe njia za haraka na mujarabu ili wajirahisishie maisha yao. Ninapokuweko Zanzibar mjini ninajiuliza kwa nini raia wanabakia tu wanalalama ikiwa kwa masiku magari ya kuzolea taka hayajatokea kwenda kuchukuwa taka majaani? Kwa nini wanaendelea kuziangalia tu taka zile zikirundikana mbele ya macho yao, huku nzi na mapanya yakisheheni na kuhatarisha afya za wakaazi? Kwa nini

wenyewe raia hawachukui masepeto na kujiondoshea udhia huo? Fleti za Kilimani, Kikwajuni na Michenzani zimejengwa na serikali zaidi ya miaka 45 iliopita na kupewa wananchi, na hivi sasa ziko hoi, zinahitaji matengenezo au angalau kutiwa rangi nje. Lakini yaonesha wakaazi mitaani wanaingojea serikali iwafanyie kazi hiyo kama mwanzo ilivowajengea. Nahisi raia wenyewe inabidi wabuni fikra za kujiondoa katika hali hiyo. Kwa masikitiko tumejenga utamaduni wa kuichukulia serikali kama mama na baba, tunaingojea itufanyie kila kitu, itulishe chakula mdomoni. Fleti hizo zilijengwa wakati wa utawala wa rais wa kwanza, Sheikh Abeid Karume. Yeye alitaka kutimiza malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kuwapatia wananchi nyumba bora za kuishi kama binadamu. Nikikumbuka nyingi ya nyumba hizo na kwa sehemu kubwa zilijengwa kwa

nguvu za kujitolea za wananchi wenyewe. Ziko baadhi zilijengwa kwa msaada wa kiufundi wa Wajerumani. Wakati wa Mzee Karume siku ya jumamosi wafanya kazi wa serikali, akiwemo mwenyewe rais na mawaziri wake, watoto wa shule na watu wa mitaani walijitolea kwa saa chache kila mmoja katika kazi ya pamoja, pia kusafisha mitaa, kwa manufaa ya jamii nzima. Kiongozi huyo alijenga mwamko wa watu wajitegemee wenyewe kutoka ngazi za chini, hivyo kuipunguzia serikali mzigo.

wenyewe raia tujiulize nini cha kujifanyia sisi wenyewe, kwa akili na nguvu zetu wenyewe, kabla ya kuwauliza wengine nini watufanyie. Serikali ni wewe na mimi pia, na ili kuhakikisha hilo ni juu yetu sote kuthibitisha kwamba tunachangia kivitendo katika maslaha ya jamii, kuanzia mtaani. Kukaa vijiweni tu, kulalama na kupiga masoga ambayo wakati mwingine hayana maana, tukitegemea mambo yatabadilika na maisha yetu ya kesho yatakuwa bora kuliko ya leo, huko ni kujidanganya.

Serikali inakuwa na Miradi kadhaa ya dhamana na inamaendeleo ya jamii andamwa na raia ambayo mingine itimize wajibu wake bado ingali hai hadi pale raia wenyewe leo ilianzishwa na nao wanapoonesha Karume kutokana na dhamana ya kwenda moyo wa kujitolea mbio kwa upande wenyewe wananchi. wao na kuazimia kikNa alifanikiwa zaiweli kufanya maisha di kwa vile rushwa yao yawe bora, bila na wizi wa mali za ya kutegemea watu umma ni mambo wengine wawahiambayo yalikuwa mize. Hamna njia ya hayana nafasi kabisa, mkato kufikia maenmwiko, katika utadeleo. Ali Mrandazi wala wake. hakuwa walii, alikuwa binadamu wa Tunapozungumzia kawaida tu, kama haja ya utawala bora wewe na mimi. basi tuanzie mitaani,

UKURASA PAGE

22

UKURASA

23

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI

Sitiari za Mzee wa Kimbunga: Haji Gora (Sehemu ya Tatu)


Zikenenda kwa masafa, kufikia kwa kufika Vibanda vyao malofa, vyote vikasalimika Nyoyo zilifadhaika Chura kakausha mto, maji yakamalizika

www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

TANBIHI
Hii ni sehemu ya tatu na mwisho ya makala haya ambayo kwa mara ya mwanzo yalichapishwa kwa jina la Tungo za Bwana Kimbunga: Haji Gora Haji. Yameandikwa na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili mzaliwa wa Uholanzi, PROFESA RIDDER H. SAMSOM, kuelezea kazi za kifasihi za gwiji wa sanaa ya ushairi katika zama hizi visiwani Zanzibar, Haji Gora Haji. Tunayachapisha tena hapa yakiwa yamehaririwa kidogo kuakisi wakati wa sasa.
Mzee Haji Gora

Pwani kulikuwa moto, mawimbi yaliyowaka Usufi nusu kipeto, rikwama limevunjika Nyoyo zilifadhaika hekima, lakini ni siri ndani ya siri. Kwani ndicho Kimbunga gani kinachoangamiza kila chenye nguvu Kuna kikongwe ajuza, viumbe kimewateka Hicho kina miujiza, kila rangi hugeuka Watakaokiendekeza, hilaki zitawafika Nyoyo zikafadhaika Vipi meli zikadidimia na ngarawa kuokoka, nyumba za ghorofa zikaruka na vibanda kusalimika? Sitiari yake ya Kimbunga ina utata mkubwa, ni fumbo hasa. Je, hicho Kimbunga ni sitiari inayotoa picha ya mtu wa tabia fulani, au kinawakilisha mabadiliko ya ghafla katika jamii ambayo watu wenyewe walikuwa wameathirika kwa namna mbalimbali? Lakini kilikusudia si kwa yule wala huyu mji wa Siyu, kilichowahi kufika, mji ambao hadi siku hizi una jina kwa sababu ya ushujaa wake katika ukinzani wake, pamoja na Waoromo na Wasomali, dhidi ya utawala wa kigeni, yaani wa Kireno na hasa wa Kiomani. Je, Kimbunga ni hayo mabadiliko ya ghafla ya mwaka 1964 ambayo watu wameyaita mapinduzi. Na nini hasa kimepinduliwa? Na ikiwa ni hivyo, huu upepo wa malaleji katika shairi la Shuwari alilotunga Haji Gora baadaye unawakilisha mabadiliko gani? Shuwari ya malaleji, imeshangaza wahenga Kimya wake uvumaji, tafauti na kimbunga Lakini popotoaji, sitambuwi zake kunga lporomosha milima, kugeuza tambarare Ilizuka aridhini, kuzagaa kwenye anga Ushabihi wa tofimi, kila kimoja kugonga
UKURASA

ifa ya tungo za Haji Gora siyo katika umbo tu la upinzani, yaani kujibizana na kuhitilafiana, pia maudhui yake

yameelezwa kwa taswira zinazohalifiana. Mwenyewe amesema kuwa mtindo huu si mbinu wala

na kukiachilia kila chenye udhaifu? Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika Kimeingowa mibuyu, minazi kunusurika Nyoyo zilifadhaika Yalizuka majabali, yakibirukabiruka Zikadidimia meli, ngarawa zikaokoka Kimbunga hicho kikali, mavumbi hayakuruka Nyoyo zilifadhaika Nyumba kubwa za ghorofa, siku hiyo zimeruka

UKURASA PAGE

24

25

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

Sinini wala sinini, hakuna kisichotinga lporomosha milima, kugeuza tambarare Haipulizi vuvuvu, jakusi na mwanashanga Bali chake kinyamavu, sio mzaha naronga Kimeleta uokovu, nakupeperusha janga lpomomosha milima, kugeuza tambarare Kwa kote ilifirimba, pwani na kwenye viunga lkavugika myamba, na mawe yakawa unga Utahisi kama kwamba, kilobomowa mizinga lporomosha milima, kugeuza tambarare Malaleji (au maleleji) ni upepo unaobadilikabadilika, hasa katika miezi ya Aprili na Novemba, lakini kamusi ya kibaharia ya Prins inaeleza kuwa huko Tumbatau unavuma mwezi wa Juni pia. Ni majira ya upepo shwari ambao hujui unatoka sehemu gani. Hata hivyo iporomosha milima, kugeuza tambarare inawezekana ni mtu mkimya mwenye nguvu nyingi za kuweza kuwashawishi watu wengi. Lakini ikiwa kimbunga ni sitiari ya mabadaliko ya kijamii, kwa nini maleleji isiwe hayo. Mabadiliko tangu mwaka 1985 huko Zanzibar, wakati wa vyama vingi na kulegezwa kwa masharti ya kiuchumi, kulipa soko uhuru fulani, mabadiliko hayo yote yalikuwa yakienda shwari na upepo huu haukuvuma vuvuvu. Fikra kuu ya Mzee Haji, dhana anayoshikilia na kusisitiza kila mara ni kupinda na kupindua, kuweka sambamba vitu viwili vinavyogongana na kushindana, kuweka juu chini na chini juu, kuonesha matukio yatukiayo kinyume na matarajio. Alivyosema, ni siri ndani ya siri, yaani kimbunga kinavunja yaliyo makubwa, lakini yaliyo madogo hayavunjwi nacho, kumbe malaleji ambayo ni kinyume cha kimbunga, imefika kote na kubomoa kila kitu, hata hivyo imeleta usalama Baada ya Kimbunga na Shuwari ilikuja Mkasa Namba Mbili: Kuna kinyozi ambae, kunyowa kiendeleya Kilofanya nishangae, anyolewae aliya Hata na kinyozi nae, hajimudu kwa kuliya Wote wanacholiliya, wala hakijulikani Hawataki kueleza, kilichowafikiliya Kama utawauliza, kama kwamba wachocheya Sauti zao hupaza, huzuni kuashiriya Bali wanacholiliya, wala hakijulikani Pengine yaweza kuwa, kwa ninavyofikiriya Ambae ananyolewa, labuda anaumiya Kinyozi anaenyowa, kwa nini mbona aliya Bali wanacholiliya, wala hakijulikani Hiki ni kitandawili, kinachowategemeya Wateguzi mbali mbali, jawabu kukipatiya
UKURASA PAGE

Nimeifunga kufuli, wafunguzi nangojeya Kipi kinachowaliza, haraka nitajiyeni

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Ajabu kubwa tena mtu mmoja anaumia akinyolewa, lakini anayemnyoa anaumia vivyo hivyo Bali wanacholiliya, wala halijulikani. Hatumo tena katika historia, tumefika kwenye siku za Ieo hii hii. Mtu wa tatu anapowakuta watu wawili wakilia katika hali kama hiyo, bila sababu kujulikana, atajaribu kuwapatanisha. Basi inavyosemekana na kutangazwa Maridhiano ya Wazanzibari yamefikiwa karibuni tu. Tungo nyingi za Haji Gora Haji zinaeleza hali ilivyo: hali ya jamii, ya watu, ya historia, kwa kutumia sitiara zinazogongana, kuhalifiana na kuhitilafiana. Ndilo jambo na kinyume chake Taswira anazotumia zinamfanya msomaji amtambue kuwa ni mtu anayejijua nafsi yake. Kwa urahisi anatambulika kama mtu wa pwani, Mtumbatu, Mswahili. Huenda msimamo wake umefichika, hutokea msimamo wake u wazi kabisa kama ulivyo katika mfano huo wa mwisho. Waswahili husema: kutoa ni moyo. Kinyume chake ni kunyang anya au kupokonya Muyaka bin Haji el-Ghassany ameshughulikia suala hilo katika shairi la Kupewa: Semani nawapulika, siyo sambe kwamba sivi Siwi cha mfunda koka, muawa na wavuvi Unipile sikupoka, sikunyanganya kwa wivi Nawauliza wakorofi, mnashika nta gani Nyanganya hukunyanganya na kuiba hukuiba Daima watu hufanya kupana vitu kwa huba Hilo mimi sikukanya na yangakwisha mahaba Kupawa ndiyo taliba, kilicho changu mudani Naye Haji Gora Haji ameendeleza fikra hiyo na kuonesha imani yake katika shairi lake Mpewa hapokonyeki, ambalo limeimbwa na kikundi cha Culture Musical Club na kunaswa sauti kwenye CD yao ya Kidumbaki: Aliyepewa kapewa, naapa hapokonyeki Kwa alichojaaliwa, Wallahi hapunguzuki Ukimlilia ngowa, unajipatisha dhiki Mpewa hapokonyeki, aliyepewa kapewa Wewe ukifanya chuki, bure unajisumbuwa Mola ndiye atowae, akawapa mahuluki Humpa amtakae ambaye humbariki Na kila amnyimae, kupata hatodiriki Wa tisa humpa tisa, wa moja haongezeki Alomnyima kabisa, hata akitaharuki Atabaki na kunasa, atakwama hanasuki Mola hutowa hidaya, tafauti na riziki Kwa anomtunukiya, huwa ndiyo yake haki Na asiye mtakiya, huwa si yake laiki

26

UKURASA

27

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Lazima kila mmoja wetu awe imara na asimame kidete kuzilinda na kuzitetea haki hizo. Uhuru wa kusema na wa kutoa maoni ni adhimu. Ni wajibu wetu sote tuyavumilie maoni ya Wazanzibari wenzetu hata kama tunayaona maoni hayo kuwa ni machungu au kuwa yanapingana na fikra zetu. Lazima tuulee na tuustawishe utamaduni wa kukubaliana kuhitilafiana. Lakini utamaduni huo hautoweza kustawi wala kudumu endapo pataibuka kikundi cha wakereketwa wa imani yoyote au wa chama chochote wanaojipa kazi ya kutukana, kuhubiri siasa za chuki na kusema uongo. Kwa bahati mbaya kikundi kama hicho kipo na mara baada ya mara huibuka na huanza kueneza siasa za chuki, kutoa maelezo ya uongo kuhusu historia ya kisiasa ya Visiwa hivi. Akhasi zaidi ni kwamba badala ya kutumia hoja katika mijadala na midahalo yake kikundi hicho hutumia matusi na vitisho dhidi ya mahasimu wake wa kisiasa. Kikundi hicho kina jumla ya watu wasiozidi kumi hapa Zanzibar.

Hofu na chuki hazina tena nafasi Zanzibar


Watu hao, wasio na lao jambo, hawamwakilishi mtu yeyote yule bali kazi yao ni kuropokwa kwenye majukwaa ya mikutano ya hadhara bila ya kujali athari za kauli zao kwa waathirika wanaowatukana kila uchao. kwamba alikuwa akiwalenga kina Ismail Jussa Ladhu wa CUF, ambaye ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, na Mohamedraza Dharamsi wa CCM, ambaye ni Mwakilishi wa Uzini.
Na Ahmed Rajab Kalamu ya Bin Rajab

Mohammedraza Dharamsi, Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar

N
UKURASA PAGE

inailinda na nitaendelea kuilinda haki ya Mzanzibari yeyote yule ya kutoa maoni yake kama anavyoruhusiwa na Katiba ya nchi kwani huu ndio msingi wa demokrasia. Na wala siwafik kumpunguzia Mzanzibari yeyote uhuru wake wa kusema, wa kutoa maoni na wa kukusanyika katika vikundi. Hizo ni haki za kimsingi miongoni mwa haki za binadamu.

Hivi majuzi tulimsikia mkereketwa mmoja wa CCM, Baraka Shamte, akiipotosha historia ya kisiasa ya Hassan Nassor Moyo na pia akimkashif kwa matusi Maalim Seif Sharif Hamadi. Siku za hofu, migawanyiko na machafuko zimepita. Hazitarudi na wala hazitaweza kuMkereketwa mwengine alithubutu kutumia rudishwa. Siasa za chuki na za matusi hazina ukabila kuwatisha Wazanzibari wenye asili ya tena nafasi hapa Zanzibar kwani sote tunataka Kihindi wenye kuupinga Muungano. Ni wazi utulivu, amani na maendeleo.

Tunawaambia wakereketwa hao na wenzao wachache kwamba Wazanzibari tumechoka na matusi yao na hatutaki kurudishwa nyuma.

28

UKURASA

29

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Tunayataka yote hayo kwa sababu tumekwishaona hasara ya migawanyiko na chuki mambo ambayo yameipotezea nchi yetu hadhi na mandeleo yake.

Tunawaomba wananchi wenzetu walio kwenye chama cha wakorofi hao wawakatae viongozi aina hiyo wenye kupalilia chuki ya aina yoyote ile. Serikali haiwezi tena kusema kuwa kuna wasaliti, mahaini Kwanza hatujui wakereketwa au wapinga Mapinduzi Zanhao wanamsemea nani. zibar. Na inaelewa vyema Hatujui wanamsemea Mzan- kwamba hakuna mwenye zibari gani. kutamani kuurejesha mfumo wa utawala wa kifalme. Tunachokijua ni kwamba matamshi yao yanakwenda Wenye kupalilia chuki wana

kinyume na moyo wa Maridhiano yaliyoleta faraja kubwa Zanzibar pamoja na Umoja wa Kitaifa. Kwa sababu ya Maridhiano hivi sasa hakuna mtu anayejihisi kuwa yuko nje ya serikali au anayefikiriwa na serikali kuwa ni adui kwa vile yeye ni mpinzani na hasa ikiwa mtu huyo anaupinga Muungano.

ajenda yao inayojikita katika ubinafsi. Kwa hivyo ni muhimu kwamba vyombo vya habari visiwape umuhimu watu aina hiyo kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta hasara katika jamii kwa kuuvuruga usalama wake. Jambo moja lenye kushangaza ni kuliona jeshi la Polisi linamkataza Maalim Seif kwenda Donge na chama chake kuhutubia mkutano wa siasa. Wakati huohuo jeshi hilohilo linawaachia baadhi ya watu, wote wakereketwa wa CCM, waropokwe bila ya kujali athari za kauli zao kwa waathirika wanaowatukana kila siku.

Historia ya kisiasa ya Zanzibar ya zaidi ya miaka 50 iliyopita inadhihirisha kwamba Zanzibar ilipata hasara kubwa kutokana na chuki na ukhasama wa viongozi na wafuasi wao kwanza kati ya ASP na ZNP, na tangu 1992 hadi 2010 kati ya CUF na CCM. Miongoni mwa hasara hizo ni pamoja na kupotea kwa roho za watu wasio na hatia, kuteswa watu na kudhulumiwa mali baadhi ya Wazanzibari. Kwa jumla, ni wazi tukipenda tusipende, kuwa Zanzibar ya

kale ilikuwa na maisha yaliokuwa mema. Na wakati huo kulikuwako neema, amani na utulivu. Wakati huo pia, Zanzibar ikiongoza katika kila fani katika kanda hii ya Afrika, ukiitoa Afrika ya Kusini. Hii leo hali halisi ya Zanzibar ni dhiki zisizokwisha zinazowakabili wakazi wa Unguja na Pemba katika kuendesha maisha yao.

serikali itapougeuza mfumo wa uchumi na sera zake zote katika sekta hiyo na kurudisha Zanzibar mambo yote ya uchumi, pamoja na ya ustawi wa kijamii, kutoka Muungano na kuyatumia mambo hayo kwa lengo la kuifanya Zanzibar iwe na uchumi wa mfumo wa bandari huru kama vile Singapore na Mauritius.

Siasa za chuki na matusi na vitisho hazitotufikisha popote Kwa bahati mbaya wakazi pale bali zitaturudisha nyuma hao wa Zanzibar hawana tulikotoka. Lakini umoja wetu tamaa ya kuepukana na ukiambatana na hali ya amani umaskini na ukosefu wa fed- na utulivu katika nchi yetu na ha mifukoni mwao kwa saba- upanuzi wa demokrasia ndio bu serikali inakataa ushauri. suluhisho letu la kuleta maHali hii haitobadilika mpaka geuzi

Inawatakieni kheri za Mwaka Mpya wa Kiislamu 1435 AH


UKURASA PAGE

Zanzibar Daima Online

30

UKURASA

31

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Tangu lini stendi ya gari ikawekwa barabarani?


H
Na Jabir Idrissa Kauli ya Mwinyi Mkuu

ivi pembeni mwa tawi la Benki ya Barclays, maarufu kama Donge huko nyuma paliwahi kutumika kama sehemu ya kupata chipsi kuku na juice, pakiitwa Donge ndio mahali mwafaka kwa kuegesha gari hizi? Kwamba pale tuwekekituo cha gari zaFuoni, Chuo Kikuu (Kibele), Kwarara, Uwanja wa Ndege (Kiembesamaki) na Mwanakwerekwe? Hivi ni kweli hasa serikali inajitapa haijakosea kutaka watu wanaokwenda Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, watokao njia kuu ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, washukie Kinazini auwatu wanapopaita Pinda Mgongo, Saateni? Hapa hapajawahi kuandaliwa kufaa kukusanyika maelfu ya wananchi. Hakuna vyoo wala benki. Kwa hivyo anayetoka Nungwi, Kidoti, Mkokotoni, Mkwajuni, Chaani, Matemwe, Pwanimchangani, Kiwengwa, Kinyasini, Donge, Mahonda, Bumbwini,Mfenesini, Kama, Mbuzini na Bububu, washuke Kinazini? Eneo la Mikunguni, pale palipowahi kuwa soko la muda baada ya kuhamishwa kwa soko la nyuma ya mtaa mdogo unaoendea machinjio ya kuku Darajani, napo panapangwa kuwa stendi ya gari za njia kuu ya Amani, Magogoni, Kinuni, Mwera, Koani, Machui, kweli? Watu wa njiaMaungani, Chukwani, Fumbawaungane na watu wanaokwenda Tomondo kukutanika uwanja wa Kwa Binti Amrani, Mpendae. Hapa ndio imewekwa stendi ya gari hizi, kweli? Haiingii akilini kwamba viongozi, tena wakiwemo wenye uzoefu katika utumishi wa umma, wanapanga na kuamua kuweka stendi ya gari Pirika za Maisha ya kila siku Darajani Zanzibar. nyingi kwenye maeneo ya ovyo kama haya. Yaani pale Kwa Khamis Machungwa leo ni kituo cha daladala; aibu iliyoje jamani? Mshangao mkubwa zaidi unakuja pale ninapoelezwa kuwa viongozi wa serikali wakiwemo hawa wa Baraza la Manispaa la Mji wa Zanzibar, wanajitapa kuwa hawakukurupuka katika kufikia maamuzi ya kuhamisha stendi Darajani na kuipeleka katika maeneo hayo tofauti. Hivi kama hawakukurupuka wanafaa kuitwa nani kwa uamuzi wao wa kukutanisha maelfu ya wananchi kila siku

UKURASA PAGE

32

UKURASA

33

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

kwenye barabara pale mlangoni mwa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui?

Serikali ilikubaliana na China mwaka 2011, kupeleka watendaji wake nchini China kupata mafunzo ya njia nzuri ya kufanya kazi za serikali. Kweli, Waitwe nani viongozi hawa ili makumi kwa makumi ya ionekane hasa wametendewa watendaji maofisa wadogo, haki? Inashangaza sana. wa kati na waandamizi wakatengenezewa safari. Kama Darajani hapafai kwa ajili ya stendi ya gari za usWacha watendaji, hata afiri wa umma, kwa sababu mawaziriwameshakwenda hapana nafasi, kama waseChina kujifunza masuala mavyo wakubwa, wanaridmbalimbali ya uongozi wa hika kuwa kwenye maeneo kileo. haya ya Saateni/Kinazini kwa gari za upande wa Kaskazini; China nitaifa lililopiga hatua Mikunguni kwa gari za njia ya kubwa ya maendeleo kwa kati; na Mpendae kwa gari za sasa. Maendeleo ya nchi hii njia Namba 7, kuna nafasi ya yenye watu wengi zaidi dukutosha kwa ajili hiyo? Hawa niani, yameyashtua mataifa itakuwaufahamu wao ufinyu. makubwa yaliyoendelea tangu zamani. Ukuaji wa uchumi Niliposikiataarifa za jambo wake unasumbua sana akili hili, harakaharaka nilivuta za wachumiwa Marekani fikra zangu nyuma. NikajinaUlaya, hasa Uingereza, uliza hivi haya ndiyo matokeo Ujerumani na Ufaransa. ya mpango wa kuwafunza China imejenga majengo ya utumishi mzuri watendaji wa kisasa. Miji ya kisasa ya viserikali? wango tafauti. Miji mikubwa na midogo iliyojaa viwanda

vidogo, vya kati na vikubwa. Miji ya viwanda imekuwa ikichangia mapatokwenyeuchumi,kwa kuwa inazalisha bidhaa zinazosafirishwana kuingiza mabilioni kwa mabilioni ya dola. Viongozi wengi wa Zanzibar wamekutwa wakizunguka kwenye miji hii yenye majengo na miundombinu ya kisasa. Hapana shaka wanapita wakiangalia kwa macho mawilimawili maendeleo ya Wachina. Sasa najiuliza, hivi walichokwenda kujifunza watendaji wa SMZ, tena wakiwemo wale wapya walioingia kwenye nafasi za juu za uongozi ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ndio mabadiliko haya ya uhamishaji stendi za gari za usafiri wa umma? Kwamba kule China wamekuta kuna maeneo ya barabara kuu au za mitaa Wachina wameweka vituo

vya daladala? Au tuseme Wachina wameweka vituo vya daladala maeneo yasiyo na huduma za chakula, choo, maduka ya vyakula na vifaa vya ujenzi na nyumbani, pamoja na benki? Siamini. Watendaji wa SMZ wamekwenda kutembea China siyo kujifunza. Ningeona mabadiliko ya maana katika utendaji wao wa kazi, ningesema sawasawa, zile safari zilikuwa na maana kwa maendeleo ya Wazanzibari. Sijaona. Mpaka sasa na hasa baada ya kushuhudia uamuzi mbaya ulivyoathiri mipango ya wananchi, nataka kuaminiserikali haijafanikiwa kubadilisha mitizamo au fikra za watendaji wake ili ziwe zinazoelekeza jamii katika kupenda maendeleo. Watendaji hawa wangekuwa wamekwenda China kujifunza ili wakirudi nyumbani mafunzo yale yawasaidie katika kuleta ufanisi wa kazi zao, na kwa hivyo kusaidia kuijenga

nchi yao, basi wasingebaki na fikra za kale na zilizojaa hisia za ubinafsi zaidi kuliko kufikiria jamii. Walipoanza kwenda China kwa ziara za kujifunza, Bustani ya Jamhuri ilikuwa imeruhusiwa kutumika upande mmoja kwa ajili ya kujenga pembea za kucheza watoto. Leo tayari upande mwingine wa bustani hii ya enzi na enzi kumejengwa nako. Kwanza hii bustani haikukusudiwa mahali pa kujenga chochote. Hii ni kwa ajili ya mapito ya wananchi. Ndio maana kuliwekwa njia mbili tu. Hakujakuwa na jengo hata dogo kwa miaka yote. Lakini Serikali ya Awamu ya Sita (SAS) kwa sababu ya ulafi tu wa madaraka na tamaa ya mapato haramu, ikaidhinisha kujengwa pembea kwa ajili ya michezo ya watoto. Na haya yakaitwa

matumizi bora ya ardhi. Ni fedheha kubwa kugeuza matumizi ya bustani hii. Fedheha zaidi kuruhusu eneo dogo kutumikakukalisha watoto wengi kama inavyoonekana. Wazazi wanahitaji eneo la kupeleka watoto wao kucheza, lakini eneo lenyewe liwe la viwango, siyo mahali finyu kama Bustani ya Jamhuri. Tunakaribisha majanga. Sitaki kufikiria hatari itakayotokea siku pakitokea hitilafu ya umeme eneo hili. Sitaki kufikiria kamwe watoto wengi wanaoingia watakavyotoka. Watatokaje walivyo wengi mahali ambapo mlango wake ni mdogo sana? Sasa kama mafunzo ya China kwa watendaji wetu ndiyo yameleta matokeo haya yote, nathubutu kusema kule China wakubwa walikwenda kufanya shopping siyo kusoma ili kuendeleza kwao.

UZANZIBARI NI HAKI YANGU


UKURASA PAGE

34

UKURASA

35

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

La Katiba Mpya si la vyama pekee

Na Mohamed Abdulrahman

Nionavyo

atukio ya hivi karibunikuhusu Mswada wa Sheria wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Katibayameainisha ni kina nani wanaoitakia mema Zanzibar na Tanzania kwa jumla na nani wasiokuwa na nia hiyo na ambao wanathamini zaidi masilahi yao binafsi badala ya mustakbali wa taifa. Labda nianzie na matukio ya bungeni ya tarehe 5 Septemba ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania wabunge wa chama kinachotawala Chama cha Mapinduzi (CCM) na wa Upinzani waliingiana mwilini . Mzizi wa fitna ulikuwa ni Mswada uliowasilishwa na serikali kuhusu Rasimu ya Katiba mpya ambao upinzani ulidai umefanyiwa marekebisho kwa lengo la kukidhi matakwa ya CCM na kupinga usijadiliwe. Naibu Spika Job Ndugaiakataka upigiwe kura kama ujadiliwe au la, akijuwa fika kwamba chama tawala kinalihodhi bunge kwa wingi wake mkubwa.Msimamo
UKURASA PAGE

wake ulionyesha mapungufu aliyonayo katika kuliongoza bunge, kiasi ya kumtaka hata Mkuu wa upinzani Freeman Mbowe atoke bungeni na kuzua kasheshe. Wabunge wa vyama vya upinzani CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wakatoka nje. Ubabe ukatumika kwa kura kupigwa bila ya wao kuweko na Mswada huo kupitishwa. Hatua hiyo ililiweka taifa njia panda. Wapinzani wakaamua kwamba watalivalia njuga na kuuzuia Mswada huo usisainiwe na Rais Jakaya Kikwete na wakatishia kufanya maandamano nchi nzima. Kadhalika walifanya mikutano kadhaa ya hadhara ikiwa pamoja na ule uliofanywa Zanzibar na kuwajumuisha viongozi wakuu wa vyama hivyo Freeman Mbowe,Ibrahim Lipumba James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa chama cha UPDP Fahmi Dovutwa . Ninavyokumbuka ni kwamba mara ya mwisho kwa viongozi wa vyama vya siasa kutoka

Bara kuhutubia Zanzibar ilikuwa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu 2000. Tangu uchaguzi wa 2005 upinzani sio tu ulionekana kukosa umoja bungeni bali hata mshikamano wao uliyumba. Ni suala la jamii nzima : Suala la Katiba sasa limewaleta pamoja wapinzani. Lakini bado kuna mambo yanayohitajika kuimarisha vuguvugu hilo ili ilipatikane Katiba maridhawa. Miongoni mwayo ni :1. Ushiriki wa vyama visivyo na uwakilishi bungeni au katika Baraza la Wawakilishi 2. Asasi za kijamii 3. Asasi zisizokuwa za kiserikali Makundi yote hayo ni sehemu ya jamii na ni wadau muhimu kwa kuzingatia kwambamustakbali wao mwema unatategemea ushirikishwaji wao na maamuzi watakayotoa. Jirani yetu Kenya ilifanikiwa kujipatia Katiba mpya kwa kuwashirikisha wadau wote katika jamii.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ikulu Dar es Salaam.

Tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu hawa hasa tukiwa tunakabiliwa na mambo mawili makubwa tunayoyasubiri mbele ya safari: Bunge la Katiba naKura ya maoni. Kikwete ametumia busara: Nikirejea nyuma katika mvutano uliozuka kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Mabadi-

liko ya Katiba, inastaajabisha kuona kuwa wapo wenye kumbeza Rais Jakaya Kikwete kwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni ,wakiwemo wawakilishi wa TLP na UDP. Kiroja cha mambo ni kuwa hata baadhi ya mawaziri waliowakejeli wapinzani

wakati wa mjadala wa Mswada huo walikuwemo katika ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo hayo Ikulu. Kikwete na pande zilizolalamika, wakakubaliana kwamba mapendekezo yao ya marekebisho yawasilishwe bungeni na kutokana na makubaliano
UKURASA

36

37

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

hayo, wapinzani wakaridhia utiwe saini Mswada huo, uliorejeshwa bungeni kujadiliwa zaidi.Pamoja na hayo wakakubaliana kuunda Kamati ya demokrasia. Bado kuna viongozi na wanasiasa wa CCM ambao hawakupendezewa na mkutano huo wa kiungwana Ikulu . Miongoni mwao ni mbunge wa Kikwajuni Hamad Masauni Yussuf, aliyejitokeza eti kutahadharisha. Msimamo wake si wa kusta-

ajabisha. Masauni anasahau mapema kwamba alilazimikakujiuzulu Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, baada ya kugunduliwa alighushi tarehe ya kuzaliwa. Hadi leo kuna hatawanachama wa chama chake wanaojiuliza ilikwenda kwendaje mwongozo wa chama kuhusu uongozi uliwekwa kando na akapitishwa kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Kikwajuni ? Watu wa aina hii wanapoku-

wa tayari kukiuka taratibu za kutafuta uongozi ni shida kuheshimu maamuzi yoyote ya kiadilifu, kiungwana na ya mustakbali mwema kwa taifa. Wana kila haki ya kumkosoa hata Mwenyekiti wao, kwani hiyo ndiyo demokrasia lakini kwa hili, ukosoaji huo nitauita usaliti. Ninakumbuka mwezi Mei mwaka huu wakati akichangia katika mjadala kuhusu uhuru wa vyombo vya habari katika nchi za Afrika, Masauni ambaye pia ni

mbunge wa Tanzania katika bunge la Afrika, alinukuliwa akisema serikali lazima iwe wazi na ikubali kukosolewa na watu binafsi, viongozi wa dini na wanataaluma, wanasiasa na wadau wengine na changamoto hizo wazifanyie kazi ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwa wakati na kujenga hali bora kwa raia wa nchi zetu. Hayo ni maneno ya hikima, lakini bahati mbaya hotuba zake Visiwani zinaashiria mengine kabisa.

Ni dhahiri kwamba jinsi alivyolishughulikia suala hilo, Kikwete ameanza vizuri, amecheza na shingo kutoaakiwapa fundisho hata wana CCM wanaotaka kuutia munda mchakato wa kupata Katiba mpya kwamba hilo ni suala la mustakbali wa taifa na si la chama fulani. Uamuzi wa kukipa jukumu Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuratibu jambo hilo kwa kushirikiana na wadau wengine ni wa busara. Muhimu ni Katiba ita-

kayokuwa mhimili wa matakwa ya Wazanzibari na Watanganyika, matakwa ambayo ninaaminiyataheshimiwa. Bado Kikwete ana wajibu wa kuhakikisha mchakato huu hauyumbishwi kiitikadi na chama au kikundi cha watu fulani. Kwa wahafidhina Visiwani wanaoendelea na fitna na hujuma, Waswahili tuna msemo, Nyimbo mbaya hailei mtoto kwani matokeo ya maisha yake huwa mabaya.

HONGERENI WAZANZIBARI KWA MARIDHIANO

Na Ismail Jussa Kutoka Facebook

Ni maridhiano ndiyo yametuunganisha Wazanzibari kusimama pamoja kutaka Mamlaka Kamili ya nchi yetu. Hatuwezi katu kukubali kuipoteza fursa hii adhimu. Tunapoadhimisha siku hii tunawapa hongera Wazanzibari

wote wanaoamini katika MARIDHIANO na tunawakatisha tamaa wahafidhina wote wanaotamani kurudisha MFARAKANO. Zanzibar Kwanza, Shengesha Baadae!

eo ni Siku ya Maridhiano. Ni tarehe 5 Novemba ambapo tunaadhimisha miaka minne (4) ya tukio la kihistoria Zanzibar pale viongozi wawili jasiri, shupavu na wazalendo wa Zanzibar, Rais Mstaafu, Dr. Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad siku kama ya leo tarehe 5 Novemba 2009 walikutana na kumaliza hasama za kisiasa visiwani mwetu. Waliweka upande maslahi yao binafsi na ya vyama vyao na wakaweka mbele maslahi ya Zanzibar. Walizika mifarakano na wakaleta Maridhiano. Hatimaye, maamuzi ya viongozi hawa wawili yaliyojaa ushupavu wa uongozi yakapewa baraka na Baraza la Wawakilishi na kisha kuridhiwa na wananchi wa Zanzibar kupitia kura ya maoni iliyofanyika

tarehe 31 Julai 2010 ambapo asilimia 66.4 walipiga kura za NDIYO kuunga mkono hatua hiyo. Ni maridhiano hayo ndiyo yaliyopelekea Zanzibar kwa mara ya kwanza kushuhudia uchaguzi mkuu wa 2010 kumalizika kwa salama na amani. Hivi sasa wapo vitimbakwiri wanaofanya njama, hila na vitimbi kutaka kuwarudisha Wazanzibari kule kwenye siasa za hasama, vurugu, mifarakano na ubaguzi. Lakini wanaona wenyewe jinsi Wazanzibari na hasa vijana wa kizazi kipya wanavyokataa njama, hila na vitimbi hivyo vichafu. Zanzibar imeshasonga mbele na hairudi tena kule ilikotoka.

Maridhiano
Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Karume, akipena mkono na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, Ikulu Zanzibar tarehe 5 Nov 2009, ishara ya mwanzo ya Maridhiano

UKURASA PAGE

38

UKURASA

39

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

a m u iliov
JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI
www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

a M
S

e z ga

i tin

Waziri: Tofauti ya mfumo wa ushuru wa forodha unaumiza wafanyabiashara


Na Goodluck Eliona Iliovuma Magazetini

uala la tofauti ya ushuru wa forodha katika bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, limechukua sura mpya baada ya Serikali kukiri kuwa linaumiza wafanyabiashara. Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema kuwa tofauti hizo zitaondolewa baada ya sehemu hizo mbili kuanza kutumia mfumo mmoja wa utozaji kodi na ushuru. Alisema kuwa utaratibu wa kutumia mfumo mmoja wa kulipa kodi unatarajiwa kuanza baada ya makubalino, utapunguza malalamiko ya wafanyabiashara ambao wanadhani hawatendewi haki. Saada alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakilalamikia kulipa kodi mara mbili, wanapokwenda Zanzibar kununua bidhaa ambapo pia hulazimika kuzilipia tena wanapofika Bandari ya Dar es Salaam. Wakati naibu waziri huyo akieleza hayo, wafanyabiashara wengi wa jijini Dar es Salaam wanalalamika kwamba watu wanaoingiza bidhaa kupitia Bandari ya Zanzibar wanatozwa kiasi kidogo ikiliganishwa na wale wanaoingiza kupitia Tanzania Bara..

Walidai kuwa kontena moja la futi 40 hutozwa kodi Sh2.5 milioni Zanzibar wakati kontena kama hilo hutozwa kati ya Sh25 milioni na Sh30 milioni Tanzania Bara. Shimbe Kinena ambaye ni mfanyabiashara wa nguo jijini Dar es Salaam alisema kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia Bandari ya Zanzibar hutozwa ushuru mdogo na baadaye kuingizwa jijini kinyemela kwa njia za panya ikiwamo bandari bubu. Alisema kuwa hali hiyo inawafanya wanaoingiza bidhaa kutoka nje kupitia bandari na njia za barabara Tanzania Bara kushindwa kuuza bidhaa, zao kwa vile zile zinazoingia kupitia Zanzibar huuzwa kwa bei ya chee. Waziri Saada akizungumzia madai ya kontena moja la futi 40 kutozwa kodi ya ndogo Zanzibar, ukilinganisha na bara alisema: Siwezi kuthibitisha kama gharama ndiyo zipo hivyo, ninachojua kwa upande wa Zanzibar malipo yanaweza kuwa hata nusu ya yale ya Bara. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alisema kuwa mfumo mmoja wa ulipaji kodi utaondoa

tofauti za viwango vya kulipa kodi vilivyopo sasa. Hata hivyo, alikanusha kuwa gharama za kulipia kontena moja kwa Zanzibar ni ndogo ikilinganishwa na zile za Tanzania Bara. Siyo sahihi kwamba gharama za kulipia kontena Zanzibar ni ndogo sana kuliko Tanzania Bara kwa sababu kinachoangaliwa kwenye kontena ni thamani ya mzigo uliopo ndani na siyo kwamba kuna bei maalumu iliyowekwa,alisema. Alisema kwamba kuna viwango maalumu vya kisheria vilivyowekwa kwa pande zote mbili vinavyofuatwa na kwamba vitabadilishwa utaratibu mpya utakapoanza. Alibainisha kuwa mpango huo unaoratibiwa na Serikali utaanza kutekelezwa baada ya kukamilika kwa sera husika. Hilo ndiyo lengo letu, ni jambo la kisera, ambalo sisi tunaletewa na kutekeleza tuubishi uliopo sasa kuhusu tofauti za kodi hautakuwepo, alisema Kayombo
Makala ya Goodluck Eliona, Gazeti la Mwananchi tarehe 3 Novemba 2013

UKURASA

41

You might also like