Zanzibar Daima Online: Toleo La Saba

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 21

|

ZANZIBAR DAIMA
Zanzibar Daima Online | Toleo Nambari 07 | Novemba 2013 - Disemba 2013 | Toleo la bure

ONLINE

SERIKALI
MAENDELEO

UMOJA WA KITAIFA

R A I S WA BUSARA?

Zanzibar Daima Online

TAHARIRI

Shein anatambua tulikotoka na tuendako


N
i Uungwana kumpa mtu haki yake. Katika toleo hili tuna makala yenye kumpa haki yake Rais Ali Mohamed Shein kwa msimamo wake wa kuitetea Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kumkinga Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Yaliyomo
Ahmed Rajab
Silaha nyingine inayotumiwa na hao wanaojikakamua kutuletea balaa ni kuzipanda na kuzipalili mbegu za chuki. Hawakuanza jana. Walianza na chuki za kikabila. Sasa wamekamia kupalilia chuki kati ya Pemba na Unguja ikiwa ni sehemu ya mkakati wao niliokwishautaja wa kutugawa. Bahati nzuri hakuna Mzanzibari mwenye akili yake timamu anayewasikiliza na kuwatia maanani wanapozungumzia juu ya kuzitenganisha Pemba na Unguja. Wengi wa Wazanzibari wanawaona hawa wahafidhina kuwa ni muflis wa kisiasa. Hawana lao jambo. Na wenyewe wanajijuwa na ndio maana wanatapatapa. Silaha yao ya tatu ni kutumia vitisho. Wanajaribu kumtisha kila mtu wakisahau kwamba enzi za kutishana zimekwisha zamani Zanzibar. Hii tuliyo nayo ni enzi ya siasa mpya na mwelekeo mpya. Hatusemi kwamba siasa zetu ni safi safina wala hatusemi kwamba Serikali tuliyo nayo imekamilika. Lakini tunachosema na kukitambua ni kwamba Wazanzibari kwa wingi wetu tumeamua kuwa wamoja, kuziacha siasa za kutugawa na za kuturudisha nyuma. Tunachotaka ni maendeleo na ufanisi wetu sote bila ya kujali, kabila, dini, itikadi za kisiasa au kisiwa gani au kijiji gani tumetoka. Inavyoonyesha ni kwamba Rais Shein naye pia anayatambua haya na ndio maana aliyasema aliyoyasema alipokutana majuzi na waandishi wa habari

Shein awaangusha Wahafidhina.

HABARI KUU

Zanzibar Daima Online


4

Timu Yetu

Si siri kwamba kuna baadhi ya Wazanzibari ambao kila siku, usiku na mchana, wanakula njama za kuihujumu SUK. Wanaitwa wahafidhina kwa sababu hawana siasa za kileo, za kimaendeleo. Hawataki Serikali hiyo ifanikiwe. Kwa hakika, hawataki Serikali hiyo iendelee kuishi. Wanataka ife, leo kesho. Wanaiombea Serikali hiyo mauti kwa sababu wanaelewa vilivyo nini kinachoweza kutokea Serikali hiyo ikifa au hata ikisambaratika tu. Wanachotaka wahafidhina hao, ambao ni wachache sana katika jamii yetu, ni kuirejesha Zanzibar kule ilikotoka na tusikotaka kurudi. Wanachotaka wao ni kuiona Zanzibar ina machafuko, michirizi ya damu na uhasama utaovifanya visiwa vyetu visikalike. Hali hiyo ndiyo wanayoililia, ndiyo wanayoitilia ubani irudi, tena kwa haraka sana. Hawataki kuiona Zanzibar yenye utulivu na amani hali ambazo ni muhimu kwa maendeleo. Hakuna taifa linaloweza kuendelea ikiwa halina utengamano, utulivu na hali ya amani. Wahafidhina hao wachache, ambao hatuchoki kuwaombea dua Mungu

awahidi, wana silaha kadhaa wanazozitumia ili kulifanikisha lengo lao. Silaha yao kubwa ni fitna. Kwanza wanataka kuwafitinisha wabia katika SUK. Na wanaanza hukohuko juu kuwagonganisha vichwa wakubwa wa Serikali hiyo. Mishale yao ya fitna wamekuwa wakiilenga kwa Maalim Seif. Wanavyo ona wao ni kwamba ni wao waliomweka Maalim Seif katika kiti cha umakamu wa Rais. Wanachosahau au wasichokijua ni kwamba hii si Serikali iliyo mali yao. Ni Serikali ya Wazanzibari wote. Wala hii si Serikali inayoundwa na chama kimoja. Ni Serikali iliyoundwa na vyama vyote viwili vikuu vilivyochuana katika uchaguzi mkuu uliopita. Hivyo ndivyo Katiba ya Zanzibar isemavyo baada ya kura ya maoni ya 2010 iliyoidhinisha kwa asilimia kubwa uundwaji wa Serikali aina hiyo. Mchezo walioupanga ni kumpaka matope Maalim Seif na kumfitinisha na Rais wake. Matamshi ya Rais Shein alipozungumza na waandishi wa habari hivi majuzi yalikuwa na lengo la kuukata huo mzizi wa fitna. Kwa hilo hatuna budi ila kumpa heko Rais Shein. Tunampa heko huku tukimsihi aendelee kuwa na ujasiri wa kuushika uzi huohuo. Wanaitumia pia fitna kujaribu kutufitinisha sisi Wazanzibari wa kawaida na kujaribu kutugawa baina ya Wapemba na Waunguja. Watafurahi wakituona tunapofoana macho na kuchinjana.

Uroho wa Wanasiasa kujitajirisha.

NIONAVYO

MHARIRI MKUU Ahmed Rajab Email: ahmed@ahmedrajab.com MHARIRI MSAIDIZI Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com

NGURUMO LA MKAMA NDUME

Donge na Pemba ni moja na zitabaki hivyo.

12

MHARIRI MSANIFU Hassan M Khamis Email: hassan@zanzibarimage.com MSIMAMIZI WA MAWASILIANO Hassan M Khamis

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Kama Zanzibar haiwezi kuchangia serikali Tatu, Bara inachangiaje kwenye Serikali Mbili.

14

WAANDISHI Jabir Idrissa Email: jabirgood@yahoo.com Othman Miraji Email: mwinjuu@hotmail.com Hamza Rijal Email: babujimba@hotmail.com Mohamed Abdulrahman Email: mamohamed55@hotmail.com Ally Saleh Email: allysaleh126@gamil.com WASAMBAZAJI mzalendo.net zanzibardaima.net zanzibardaima/facebook MATANGAZO Hassan M Khamis Simu: +44 7588550153 Email: hassan@zanzibarimage.com WASIALIANA NASI zanzibardaimaonline@gmail.com JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA Zanzibar Daima Collective 233 Convent Way Southall UB2 5UH Nonnstr. 25 53119 Bonn Germany

KAULI YA MWINYI MKUU

Shein astahili kuitwa Rais wa busara.

18

Vuta nkuvute, kielelezo cha uandishi wa Kizanzibari

TUFUNGUE KITABU

22

Wazanzibari tujipange, mafuta yasije yakawa nuksi kwetu.

WARAKA KUTOKA BONN

26

Dk. Mvungi ameikosa treni ya mwisho, ila tuko nae.

BARZA YA JUMBA MARO

30

Hadithi fupi ya meza fupa ya Ally Hilal.

HEKAYA ZA ZANZIBAR

34

www.zanzibardaima.net

Zanzibar Daima Online

HABARI KUU

PAGINATION 1

Zanzibar ZanzibarDaima DaimaOnline Online

SHEIN AWAANGUSHA WAHAFIDHINA

Na Jabir Idrissa Zanzibar

ahafidhina ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wameangushwa puuu.

ibitisho wa Maalim Seif kukiuka utaratibu na walimtaka Rais amchukulie hatua kali za kinidhamu. Lakini Dk. Shein, mzaliwa wa Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba, alimhami Maalim Seif kwa kusema kuwa kiongozi huyo amekuwa akieleza msimamo wake binafsi katika suala hilo wala si msimamo wa Serikali anayoiongoza. Dk. Shein ambaye aliingia madarakani Novemba 3, 2010, alisema yeye na mawaziri wake wanafanya kazi kwa pamoja na kwa kuvumiliana ambapo kila linalofanywa na Serikali wanaliamua kwa pamoja na wanafanya kazi kwa mshikamano mkubwa tofauti na ilivyotokea katika nchi nyingi zilizounda Serikali kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Nchi zilizounda serikali ya mfumo huo kwa Afrika ni pamoja na Zimbabwe ambako

Haya yalitokea pale Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipofanikiwa kuihami serikali anayoongoza ya Umoja wa Kitaifa dhidi ya njama zenye lengo la kuisambaratisha. Dk. Shein katika hali iliyoonesha kuwa anajua mitego ya siasa, alijibu kwa ufasaha alipoulizwa anamchukulia vipi Makamu wake wa Kwanza Maalim Seif Shariff Hamad ambaye amekuwa akitoa kauli nzito zilizoashiria kama ndio msimamo wa Serikali kuhusu upatikanaji wa Katiba ya Muungano Tanzania. Suala hili limekuwa likitajwa mara kwa mara na wahafidhina wakiwemo viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM, kama uth-

ZANU-PF cha Robert Mugabe kimeunda Serikali pamoja na Chama cha Movement for Democratic Change (MDC) cha Morgan Tsvangirai na Kenya ambako serikali hiyo iliundwa kama njia ya kuleta amani baada ya machafuko ya uchaguzi mkuu wa Desemba 2007. Rais Mwai Kibaki ambaye amestaafu, aliunda Serikali ya ubia pamoja na Muungano wa Upinzani chini ya Raila Odinga. Dk. Shein anaongoza Serikali ya ushirikiano yenye mawaziri kutoka chama chake cha CCM na Chama cha Wananchi (CUF) vilivyopata kura za wananchi siku ya uchaguzi Ok-

toba 31, 2010. Alisema Serikali hiyo inafanya kazi vizuri licha ya changamoto nyingi zinazoisibu; lakini amesema kuwa mambo yanakuwa rahisi kwa vile wanashauriana kwa pamoja bila ya kujali itikadi za vyama vyao vya siasa vilivyowaingiza uongozini. Dk. Shein alionesha ujasiri kiuongozi kwa kumkingia kifua Maalim Seif Sharif Hamad hata pale alipoulizwa atachukua hatua gani dhidi ya kilichoelezwa kama kauli za Makamu wake wa kwanza zinazoashiria kuisemea serikali kuhusu msimamo wake

6 6

Zanzibar Daima Online

HABARI KUU

katika suala la upatikanaji wa katiba mpya Maalim Seif aliteuliwa na Dk. Shein kwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. mujibu wa Katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho makubwa mwaka 2010, kabla Alisema ni yeye tu mwenye wajibu wa ya uchaguzi mkuu, kwa kujumuishwa ibara kikatiba kuisemea Serikali katika suala hilo; zinazoweka wadhifa wa Makamu wawili wa wengine watachofanya ni kutoa misimamo Rais kama wasaidizi wakuu wa Rais. yao binafsi. Hakuna kiongozi yeyote wa kutoa msima- Mabadiliko hayo yaliidhinishwa katika mpanmo wa Serikali isipokuwa mimi mwenyewe go mpana wa kuruhusu kuundwa kwa SeriRais. Makamu wangu wote watatoa mi- kali ya Umoja wa Kitaifa baada ya uchagusimamo yao kama viongozi binafsi katika zi, mpango uliowezeshwa na maafikiano ya vyama vyao. Sina tatizo la kauli za Maalim kujenga siasa za Maridhiano Zanzibar yalSeif; najua yeye ana haki ya kutoa msimamo iyofikiwa na Maalim Seif na Amani Karume wake binafsi. Na mimi pia ninayo haki kama alipokuwa rais. hiyo. Lakini mimi ni Rais ndiye nitakayetoa msimamo, sijafanya hivyo, alisema akijibu Hatua hiyo ya Maridhiano waliifikia baada ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari wa kufanya majadiliano ya faragha tangu mwagazeti la Zanzibar Leo, Mwantanga Ame. ka 2009 kutokana na mpango ulioasisiwa na Mzee Hassan Nassor Moyo akisaidiwa na Kumekuwa na shinikizo ndani ya CCM kum- ile inayoitwa Kamati ya Maridhiano inayojutaka Rais Shein amchukulie hatua kali Maal- muisha makada watatu wa CCM na viongozi im Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, waandamizi watatu wa CUF. kutokana na kile wanachodai wahafidhina kuwa kutoa kauli za kuisemea Serikali huku Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ni pigo akimzidi mamlaka Makamu wa Pili, Balozi kubwa kwa wana-CCM wasiopenda mabadiSeif Ali Iddi, ambaye ndiye kiongozi wa Seri- liko, imekuwa ikikabiliana na majaribio mengi kali katika Baraza la Wawakilishi. ya kuisambaratisha. Wahafidhina wakiwemo viongozi waandamizi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wamekuwa wakimsukuma Rais wa Zanzibar amfukuze kazi Maalim Seif kwa kumtuhumu kuwa amekuwa akimtii zaidi Rais Mstaafu Amani Abeid Karume kuliko Rais aliyemteua. Wahafidhina wamekuwa wakichochea vurugu kwa kuzuia demokrasia kuenea huku wakimtukana Maalim Seif hadharani kupitia maandishi kwenye mbao za maskani ya Muembekisonge na Kachorora. Matusi mengine hutolewa kwenye majukwaa ya mikutano ya hadhara ya chama hicho

DONATE FOR PEMBA

Zanzibar Daima Online

A brief reminder about the Pemba Foundations crowdfunding campaign to introduce new cash crops to the impoverished Zanzibar island of Pemba. We had a good start but are stuck at $1,225 -- only 11% of the goal, with 55 days left. For those who have already contributed -- thanks again, and please pass along the link to friends who might be interested. For those who would like to contribute but havent got to it yet, please click on the link to the Indiegogo campaign page and then click on Contribute Now. Donations are by credit card in dollars, but UK or other cards work. Your donation will be matched one-for one, so it will be worth double. Donations are tax deductible in the US. You will be able to give anonymously if you wish. Here is the link to the campaign page: http:/ /www.indiegogo.com/projects/a-passion-for-fruit Many thanks. John Angier

NIONAVYO

Uroho wa wanasiasa kujitajirisha

Zanzibar Daima Online

sababu, kuna viongozi waliotekeleza alau sehemu ya walichohubiri na hasa kuhusiana na hili la kujitajirisha wakitarajia watakaowafuata baadaye wataendelea kuwa ni dira kwa jamii. (Mfano mmoja Mwalimu Julius Nyerere aliyeondoka madarakani baada ya miaka 27 bila ya yeyote kuthubutu kumnyooshea kidole kwamba alitumia madaraka yake kujitajirisha). Leo hii mambo ni mengine. Mbunge anaweza kuwa tajiri katika kipindi cha miaka mitano tu. Hugombea ubunge kwa malengo ya kujinufaisha binafsi na badala ya bunge kuwa chombo kikuu cha uwakilishi wa umma limegeuka kuwa mahala pa kula. Ubinafsi Umetawala Kinachokirihisha ni pale wabunge na wawakilishi wanapokuwa na moyo wa kulalamika hadharani kuwa mishahara yao haitoshi na wanataka waongezewe. La kukirihisha zaidi ni pale viongozi wa juu wanapokaa

kimya na kushindwa kuwakemea mabwana wakubwa. Hivi karibuni kumeibuka madai ya wabunge kuwa mshahara hautoshi. Sambamba na madai hayo ni zumari lililopulizwa na Spika wa bunge la Muungano Anna Makinda kuyaunga mkono madai hayo . Akitoa mfano alisema yeye binafsi amewahi kuendewa na wabunge watatu wa zamani wakiomba msaada kwa vile hali zao ni mbaya. Ingawa hakutaja kiwango cha mishahara ya wabunge, Makinda amegusia posho ya vikao Shilingi 330,000 kwa siku, Shilingi 30,000,000 za shughuli za jimbo na Shilingi 72,000,000/= zikiwa kiinua mgogo mbunge anapomaliza miaka 5. Makinda amedai wabunge wengi wanashindwa kukidhi mahitaji yao katika mazingira yaliopo sasa . Spika amesema wabunge wengi wanajuta kuwania ubunge na wangetamani kurejea katika taaluma zao. Sijui kama taaluma

hizo zingewapa marupurupu na fedha wanazojikingia. Kiroja cha mambo madaktari wamekuwa wakivutana na serikali kuhusu mishahara na mazingira yao kazini. Matatizo yao mpaka leo hayajapatiwa suluhuhisho la kudumu. Spika Makinda hajanishangaza, Waswahili wanasema .Mwamba ngoma huvutia pande wake, kwani marupurupu anayopata yeye mwenyewe hayasemeki. Wazanzibari hawana tafauti Hoja hii inawagusa pia wabunge wa Zanzibar katika bunge la Muungano na hata wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) . Hivi tunapozingatia na kujiuliza kuhusu kiwango cha fedha anazojikingia mbunge wa Zanzibar na mshahara wa mfanyakazi wa kawaida tunakuwa na majibu gani ? Ni wafanyakazi wangapi wa serikali wanaoweza kupata kiinua mgongo cha kiasi hicho baada ya miaka 30 ya utumishi, ukilinganisha na

Rais Jose Albarto Mujica Cardano wa Uruguay


kisema kama kuna nchi yenye Rais maskini duniani kuna watakaoangalia kwa jicho la sadiki ukipenda, kuwa ni porojo tu na si wengi watakaokuamini. Sidhani kutokuamini kwao kunatokana na dhana ya kuwa haiwezekani , lakini si katika wakati huu tulionao ,kwani uongozi umegeuka na kuwa jukwaa la kujitajirisha badala ya utumishi kwa umma. Hata hivyo kweli ni kwamba kiongozi wa aina hiyo yupo. Naye ni Jose Alberto Mujica Cordano (anatamkwa kihispania - Khose Mukhika), Rais wa Uruguay. Mujica mwenye umri wa miaka 78 ,alishinda uchaguzi 2009 na akaingia madarakani Machi 1, 2010. Bwana huyo mpiganaji wa zamani wakati wa vita vya chini kwa chini dhidi ya utawala wa kidikteta ,aliyejeruhiwa kwa risasi, kufungwa , kuteswa na polisi na kuwekwa gerezani kwa miaka 14 , kabla ya kuteuliwa waziri katika serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto (2005-2008), hutoa asilimia 90 ya mshahara wa urais , dola za Marekani 12,000, kila mwezi kwa jumuiya za misaada kuwasaidia masikini na wajasiri amali. Anaishi katika nyumba yake mwenyewe kwenye kiunga kimoja cha mji mkuu Montevideo. Gari anayoendesha ni aina ya Volkswagen Beatle ya miaka ya 1960 na wala hana walinzi. Nivmtu wa ajabu anayewashangaza wengi katika ulimwengu wa Leo. Nasema katika ulimwengu wa leo kwa

Na Mohamed Abdulrahman

Nionavyo

10

Zanzibar Daima Online

tija za miaka mitano ya ubunge ? Wabunge wangapi waliotumia posho wanaolipwa kushughulikia kweli matatizo majimboni mwao ? Kwa bahati mbaya ugonjwa huu hauko tu miongoni mwa wabunge wa chama kinachotawala cha CCM bali hata kwa wale wa vyama vya upinzani. Sikio la kufa halisikii dawa Zanzibar ina serikali ya ubia na waliokuwa wapinzani sasa nao wamo serikalini. Kwa bahati mbaya lakini baadhi ya waliokuwa wakiyalalamikia sasa hayazungumzwi tena. Ukihoji unaambiwa Waziri anapaswa kuishi kulingana na hadhi yake. Je, daktari hapaswi kuishi kulingana na hadhi ya taaluma yake ? Kwa kumbukumbu zangu ni mwakilishi wa Mji mkongwe Ismail Jussa peke yake aliyepinga kuongezwa masilahi ya wawakilishi,alipokuwa akichangia katika kikao cha bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Juni 18 mwaka huu . Lakini sikio la kufa halisikii dawa. Mwanzoni mwa mwezi wa Novemba, ilitangazwa

kwamba BLW limepandisha posho ya vikao kutoka Sh. 100,000 hadi Sh.150,000 kuanzia mwaka huu . Wananchi wameanza kukata tamaa na kutokuwa na imani na wanasiasa. Hata hivyo, wao pia wana wajibu mkubwa wa kujiletea mabadiliko. Kwanza wanapaswa watafakari ni kina nani wanaofaa kuwawakilisha, kuwapigania na kuwaletea maendeleo. Kuna matumaini Katiba mpya huenda ikawa na kifungu kitakachoruhusu wagombea binafsi. Hiyo itakuwa nafasi muruwa ya kuwapima wanaofaa kuwa viongozi bora. Kiongozi anayewajibika kwa umma Rais Jose Mujica alipoamua kugombea urais alishawishiwa na hali ngumu aliyoiona wakikabiliana nayo walala hoi. Alisahau umimi akaweka mbele utaifa. Hakukimbilia utajiri bali uwajibikaji. Uamuzi wake wa kutoa asilimia 90 ya mshahara wake kila mwezi kwa jumuiya za kiraia kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kuwasaidia masikini ni kielelezo cha uadilifu anaopaswa kuwa nao kiongozi . Uadilifu huo ni

wa kuwatetea, kuwasimamia na kuwapigania waliomchagua. Nikimnukuu, amesema hivi: Mshahara wa mke wangu ambaye tumejuana katika siasa na ni Seneta unatutosha, kwanini cha ziada tusitoe kwa wengine. Mujica anasema anashajiishwa na falsafa ya utu, ya kumheshimu na kumfikiria binadamu mwengine na hasa masikini. Hadi miaka ya 1970 wakati Mujica Rais wa 40 wa Uruguay akiwa gerezani sisi pia tulikuwa nao viongozi wa aina hiyo waliowajali na kujitolea kuwatumikia raia , waliobakia wakati wote kuwa sawa na wengine.... gari na vazi la kawaida, viatu vya kanda tu na hata nyumba ya kawaida na waliokuwa karibu na umma kuanzia majimboni hadi kitaifa, viongozi ambao umma nao ulijivunia. Kama usemavyo usemi wa kihispania Un gobierno honrado, un pas de primera Serikali yenye heshima ni ile inayoliweka taifa mbele. Je, wengi wa viongozi na wanasiasa wa kwetu ni wa aina gani ?

Barua za Wasomaji
Tatizo Bwana Ali Saleh unalijua. Hapa petu wewe si mgeni wa siasa. Unajua kitu kinachopiganiwa hapa si utaifa bali ni matumbo kujaa. Sasa hawa wahadimu wa pande hizi mbili, CUF na CCM, hawana mtafaruku isipokuwa wanatafuta mtu wamtie kati wamtoe kafara. Unawaona, Muamsho, waliwatumia CCM na CUF, baadaye, wamewatafutia gunia wamewavisha. Usione wewe umebahatika na umepata hicho kijifupa, si haba. Hawa CUF, walikupigisha vigongo hata nakukutilisha ndani wakati wanyamunyamu hawa kukumbuka. Sasa wache wapige ngoma wata cheza wenyewe, kubomoa rahisi kujenga kazi. Nawe Bwana Ahmed Rajab una maoni mazuri na michango ndani ya majarida na mitandao mbalimbali ya kidunia, lakini wewe mchango wako wa kivitendo hatuuoni. Umekuwa kama Zanzibar. Wengine, wako ughaibuni, wana tuchochea, sisi wahadimu wanatuua, wao wanakula raha ughaibuni. Tunasikia, wewe baada ya kustaafu umeona hapakaliki Zanzibar, umeomba uraia Kenya. Unajua hapa hapafai, sasa kwa kuwa mwenzetu umealimka, ugemuiga mzee wetu almaruhum Ali Nabwa, aliyewaelimisha na kuwafunza mengi. Mungu amlipe mema na amughufiriye dhambi zake na amuondoshee adhabu ya kaburi. Na wewe njoo uwaelimishe, utarajie mema kwa Mungu. Muda huu wa mapumziko, ya utu uzima, ikumbuke jamii yako iliyo dhulumika miaka 50. Na wewe unajua mengi kuhusu Zanzibar, makomredi mana deni kwa Wazanzibari. Ali Azani Kiongwe alkiongwe55@gmail.com

hsante kwa makala yako murwa kabisa. Umenifurahisha sana Sheikh Othman. Mungu akujaze kheir kwa hilo. Lakini Ali Mrandazi, kwa uhakika, hatujui kama alikuwa walii wala la, lakini kwa ulengo wangu ana alama na dalili za uwalii. Abadulla zanzibar@online.no i fakhari ya kila Mzanzibari wa kweli kuwa na watu wenye upeo, misimamo na kauli thabit kama wewe aunt Riziki. Hapana shaka wewe ni moja katika rizki kubwa kwa taifa la ZANZIBAR. Jazaaka llah l kheir. Mshirazi al_mshirazi@gmail.com

12

Zanzibar Daima Online

NGURUMO LA MKAMA NDUME kia kisiwani Unguja kama wanapingana na mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili uliopo sasa. Wasikie hao wajiitao Waunguja wakikumbusha mauaji yaliyofanyika wakati wa Mapinduzi na wakiapa kwamba wako tayari kwa mapinduzi mengine kama hayo ili kuweka heshima na adabu. Chuki, hasira na kisasi kinaonekana wazi kwenye maneno yao kama zionekanavyo kwenye nyuso na dhamira zao. Kauli ya vita, damu, mauaji, majeruhi, unaweza kuihisi kwa mbali. Makala haya yanadhani kwamba hatua zilipaswa kuchukuliwa leo, mfano wa vile viongozi wa Uamsho walivyochukuliwa hatua na Serikali hii hii, ikiwa kweli Serikali ilikuwa na haki ya kufanya vile wakati ule. Ila kama panangojewa hadi watu washikiane mapanga, kama ilivyotokea Rwanda baada ya Redio Intarahamwe kutumika kuchochea mauaji dhidi ya kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani, basi natusubiri ule uitwao kwetu pwani ushahidi wa Kinyamwezi. Nimeiita hatua hii ya sasa ya Serikali kwamba imekuja baada ya kujizoazoa. Nakusudia kwamba ni hatua nzuri iliyokuja baada ya Serikali kuchelewa sana na kuwachelea wakubwa. Palikuwa pamezoeleka kwa wale wanaojinasibisha na Mapinduzi na Chama cha Mapinduzi, hata kama ni mijitu mijahili, mijinga na mikatili, kuogopewa na SMZ. Ni kituko, lakini ndio ukweli kwamba Serikali ya Mapinduzi inawaogopa wajinasibishao na Mapinduzi, hata kama hawana uwezo wala njia za kupindua tena.

Zanzibar Daima Online

13

Donge na Pemba ni moja na zitabaki hivyo

Ali Shamhuna Mwakilishi wa Donge

Na Mohammed Ghassani

Ngurumo la Mkama Ndume

engine tutauchukulia mwezi huu wa Novemba kuwa wa aina yake visiwani Zanzibar kwa sababu ya matukio mawili, tunayoyaona ni muhimu kwa maendeleo ya kidemokrasia na kiutawala visiwani humo. Moja ni kujizoazoa kwa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) na kuja juu dhidi ya vyombo vya habari vitakavyotumia vibaya uhuru wa habari na kuchapisha au kutangaza habari zenye lengo la kuvuruga amani. Hayo yalisemwa na waziri anayeshughulikia habari, Said Ali Mbarouk, katika kile kilichotajwa na vyombo vya habari vya Tanzania kuwa ni mkutano wa waziri huyo na wakuu wa vituo vya redio vya Zenj FM na Coconut FM,

vyote vya Zanzibar. Ujuu iliokuja nao SMZ katika hili ni kutoa onyo kwamba ama vyombo hivyo viache kupandikiza mgawanyiko wa Pemba na Unguja au vichukuliwe hatua kali. Hatujui ukali wa hatua hizo kali, lakini mazoea ya serikali zetu yanatupa mwelekeo wa makisio - vitapigwa faini, vitafungiwa, lakini havitapelekwa mahakamani. Vikipelekwa mahakamani itakuwa ni hatua nyengine kubwa ya kupongezwa katika ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria nchini mwetu. Isifahamike kwamba makala haya yanapingana na onyo hilo la Waziri Said. La hasha. Kwa hakika, yanakubaliana nalo kabisa na yangelipenda hata liongezwe nguvu zaidi, yaani sio tu vyombo hivyo

vikabiliane na adhabu iwapo vikiendelea, bali viwajibike sasa kwa yale ambayo tayari vimeshayatangaza. Ikiwa msingi wa kuchukuliwa kwao hatua hapo baadaye ni athari za matangazo yao dhidi ya Umoja wa Kitaifa wa Wazanzibari, basi tayari umoja huo umeanza kuathiriwa. Sikiliza kauli za viongozi wajiitao wa shehia, wazee na vijana wa Unguja kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) wakifoka hadi mapovu kuwatoka dhidi ya watu wenye asili ya kisiwa cha Pemba. Hapa nimewaita wajiitao na namaanisha hivyo hivyo wajiitao wa Unguja. Hao niwaitao wajiitao wa Unguja wanasikika wakitamka kwamba Wapemba hawapaswi kuendelea kuba-

Dk. Salmin Amour Juma, siku akitoa hotuba ya kusisimua juu ya umoja wa Wazanzibari, Ikulu ya Mnazimmoja kwenye mkesha wa Mwafaka wa kwanza wa kisiasa kati ya Si haba kwamba angalau kwa CCM na CUF mwaka 1999. mara ya kwanza hao wajinasibishao na Mapinduzi na Sasa zama zimebadilikwa hakika ukichungua hiska na mabadiliko haya toria utawakuta wengi wao yanawaumiza wanasiasa amhata hawakuhusika nayo bao walivuta pumzi, walikula sasa wanaambiwa kwamba na walikunywa uhasama wa Zanzibar si yao mali yao, wala kisiasa. Donge imefunguka yao peke yao. na kujiunga tena na sehemu nyengine za Zanzibar. Novemba hii pia itaingia tena kwenye historia ya maeWala kujiunga huko si lazima ndeleo ya kisiasa visiwani kumaanishe kuiacha mkono Zanzibar, kwani kwa mara CCM na kuikumbatia CUF. La ya kwanza tangu kurudi hasha. Kunamaanisha kwamkwa mfumo wa vyama vingi, ba sehemu hiyo nayo sasa iko Serikali iliamua kusimamia tayari kusikiliza hoja na kuziphaki ya kisiasa ya kila raia ima ndani ya ardhi yake kisha kwa kukiruhusu Chama cha ikafanya uamuzi baada ya Wananchi (CUF) kufanya kuzipokea hoja hizo. Wanaosiasa za wazi kwenye jimbo taka kujiunga na CUF wakala Donge, ambalo kwa miaka fanya hivyo kwa mujibu wa yote 20 na ushei ya siasa za walichoelewa na wanaotaka vyama vingi wanasiasa wakusalia CCM wakafanya hivyo hafidhina wa chama tawala kwa mujibu huo huo. Lakini si wamejenga mazingira ya ku- kinyume chake. litenga na sehemu nyengine za Zanzibar kama kwamba Mantiki muhimu hapa ni Donge ni nchi pekee. kwamba kubwa kuliko yote Donge nayo ni Zanzibar, imeNakumbuka mwaka 2005, kuwa hivyo na itakuwa hivyo kundi letu la wanahabari milele. Kama ilivyo Pemba, lilipojikuta likilazimika kuripoti kwa ujumla wake, ndivyo ilrisasi na mabomu pale Maivyo Donge kwa udhati wake. honda baada ya polisi kuwa- Zote ni sehemu za Zanzibar, zuia wana-CUF kwa mara zimekuwa hivyo na zitabaki nyengine. Matokeo yake, hivyo milele. yalikuwa majeruhi na mauaji. Uvunjwaji wa haki za binada- Wale wanasiasa waliopigania mu ukaendelea hata baada ya kuitenga Donge na Zanzibar hapo. na ambao sasa wanahubiri utengano wa Pemba na UnLakini ukweli ni kwamguja, imekula kwao kwa ba mambo yana zama na kutumia lugha ya vijana wa zamu. Ndivyo alivyosema kileo Rais Mstaafu wa Zanzibar,

Kama Zanzibar haiwezi kuchangia Serikali Tatu, Tanzania Bara inachangiaje kwenye Serikali Mbili?
Hoja ya Mheshimiwa Awadhi ina mapungufu mengi. Mojawapo ni ikiwa kama hicho anachokisema ni cha kweli, basi kwa nini asipendekeze serikali moja tu kabisa, maana kwa vyovyote vile Zanzibar inatakiwa ichangie kwenye mfumo huu wa sasa uliopo na kama haitaweza kuchangia wakati huo, haiwezi kuchangia sasa pia. Hii ni kuuambia upande wa pili wa Muungano kwamba umekuwa ukiibeba Zanzibar siku zote na sasa ...

14

Zanzibar Daima Online

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Zanzibar Daima Online

15

Na Riziki Omar

Mkeka wa Mwana wa Mwana

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Salmin Awadh Salmin, alisema hivi karibuni kwamba Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama muundo wake utakuwa wa Serikali Tatu.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa jimbo la Magomeni (CCM), Zanzibar haiwezi kuchangia hata kwa asilimia 10. Hayo aliyazungumza kwenye semina ya Wabunge wa Muungano na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar mjini Dodoma Jumatatu ya tarehe 11 Novemba, 2013. Hoja yake kubwa ni kwamba Zanzibar ina uchumi mdogo na, kwa hivyo,

mfumo wa sasa wa serikali mbili ndio unaofaa anasimama mtu kutokea upande wako wa katika kuudumisha Muungano. nchi, analisema neno, unatamani uingie chini ya meza kukimbia aibu na fedheha. Huu ulikuwa ni Nimekuwa mbunge kwa mwaka wa nane huu, wakati mmojawapo kwangu. nikiwakilisha maslahi ya Zanzibar kwenye bunge la Muungano, na lazima niseme kauli ya Hoja ya Mheshimiwa Awadhi ina mapungufu mtunga sheria mwenzangu huyu, Mzanzibari mengi. Mojawapo ni ikiwa kama hicho anamwenzangu, ilinikirihisha. Wakati mwengine chokisema ni cha kweli, basi kwa nini asipende-

16

Zanzibar Daima Online

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Zanzibar Daima Online

17

keze serikali moja tu kabisa, maana kwa vyovyote vile Zanzibar inatakiwa ichangie kwenye mfumo huu wa sasa uliopo, na kama haitaweza kuchangia wakati huo, haiwezi kuchangia sasa pia. Hii ni kuuambia upande wa pili wa Muungano kwamba umekuwa ukiibeba Zanzibar siku zote na sasa uendelee kuibeba milele. Asichokieleza, na pengine asichokielewa Mheshimiwa huyu, ni kwamba hata katika mfumo wa sasa wa Muungano ambao yeye na chama chake wanautetea, Tanzania Bara haipo na hivyo haichangii kitu kwenye Muungano wenyewe. Iliyopo ni Zanzibar na ndiyo pekee inayochangia.

Serikali ya Muungano tu. Hiki ni kizungumkuti kilichomo kwenye Katiba yetu na ambacho kinaonesha sura halisi ya Muungano wetu. Kwamba Katiba inaelezea wazi kuwapo kwa Serikali ya Zanzibar na pia Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo ina madaraka ya kushughulikia mambo yote ndani ya, kwa Jamhuri ya Muungano na yote mengine ndani ya, na, kwa Tanzania Bara, lakini haiitengi Tanzania Bara katika matumizi na, hivyo, mchango wake kwa Muungano.

Sasa kwa nini matumizi ya Tanzania Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano yagharamiwe na mfuko mkuu wa Jamhuri ya Muungano? Kuna upungufu mwengine. Nao ni kuhusu Akaunti ya Pamoja ya Fedha. Kifungu cha 133 cha Katiba kinazungumzia Akaunti ya Fedha ya Pamoja ya Jamhuri ya Muungano, ambapo zitatiwa fedha kutoka michango ya serikali mbili kwa viwango vitavyowekwa na Tume ya Pamoja ya Fedha. Kwa hiyo, kikatiba ni Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambazo zina wajibu wa kuchangia huduma na uendelezaji wa Muungano. Tan-

zania Bara haichangii kitu na wala haiwajibiki kuchangia kwa mujibu wa Katiba. Ni hapa ndipo sasa unapoona kwamba kumbe kulitakiwa kuwepo na Serikali ya Tatu ya Tanzania Bara, maana ilivyopaswa hasa iwe ni hivi: suala la mapato lihusishe Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania Bara. Hadi hilo litakapokuwa, Zanzibar pekee ndiyo itakayosalia kuwa mchangiaji wa uendeshaji wa Muungano. Na hivyo ndiyo inayoibeba Tanzania Bara kisheria na si kinyume chake. Serikali Tatu nazije, ili kila mmoja atoe kwa mujibu wa apokeacho

Dhamana hizi mbili kwa Serikali ya Muungano zimeleta mtafaruku na suitafahamu kubwa. Hii ni pamoja na Mgawanyo wa MapaInawezekana ikawa kauli hii ni ngumu kuiele- to, Mahkama ya Katiba, Mahkama ya Rufaa wa lakini maelezo yake yamo kwenye ma- kwa Tanzania, orodha ya mambo ya Muunpungufu makubwa ya kikatiba na kimuundo gano na Mwenendo wa Mabaraza ya Sheria. katika mfumo wa sasa wa Muungano, na ndio maana ni lazima kuubadilisha na kwen- Tuchukulie mfano na ukweli huu: kuna mfuda kwenye huo wa Serikali Tatu, ambao yeye ko mkuu kwa Jamhuri ya Muungano ambao anatumia hoja hiyo dhaifu kuupinga. Nitafa- unaingiza mapato yote au pesa zote kwa ajili fanua. ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hapa tafsiri safi na isiyo na mashaka ni kwamba Katiba ya sasa ya Muungano haina sehemu mfuko huu unapaswa kutumiwa kwa mamyoyote inayotaja matumizi ya Tanzania Bara bo ya Muungano tu, kama yalivyoorodheshkama Tanzania Bara ndani ya Muungano au wa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba. angalau matumizi kwa mambo yasiyo ya Muungano kuhusiana na Tanzania Bara. Lakini, Tanzania Bara haina mfuko mkuu kwa Badala yake ina Vifungu Na. 133 mpaka 144 mambo yasiyokuwa ya Muungano yanayambavyo vinahusika na Mambo ya Fedha ya ohusu Tanzania Bara tu, ingawa Zanzibar Jamhuri ya Muungano na ambavyo vinaas- inao mfuko wake mkuu kwa mambo yasihiria kuwepo kwa Serikali ya Zanzibar na yohusu Muungano, yanayohusu Zanzibar tu.

LADHA YA BETI

MAUMIVU YA MAPENZI

Umenifunza mpenzi, mahaba ni maumivu Bali si ya kipuuzi, wala si ya kipumbavu Moyo mlea mapenzi, ndio wenye uwerevu Sijioni mlegevu, kwa hayano kuyaridhi! Maumivu ya mapenzi, si jambo la utukivu Hata himwaga machozi, si kwamba mimi mtovu Wala si mwana bazazi, wala nawe hu muovu Bali wangu mpetevu, uliye na zangu radhi Moyo wangu umeridhi, na nafusi ni sikivu Waonao ni maudhi, wangu ni uvumilivu Kwako nimestaaladhi, na moyo wangu shupavu Sina donda sina kovu, nina wingi wa mapenzi. Mohammed Ghassani Bonn - Ujerumani

KAULI YA MWINYI MKUU


18 19

Dk. Shein astahili kuitwa Rais wa Busara


Na Jabir Idrissa Kauli ya Mwinyi Mkuu

UMBE Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ana busara nyingi.

Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad Sikubahatika kualikwa. Ningeupata mwaliko, ningeudaka kwa moyo mkunjufu. Ningehudhuria maana nina maslaha makubwa na Zanzibar. Kwa hivyo, ningepata mawili matatu ya kujifunza. Tunapojadili Zanzibar na siasa zake, ingenisaidia. Hata mwaka jana, ingawa nilitarajia, baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Hassan Khatib, sikualikwa. Ofisa huyu anajua zaidi kilichotokea. Hilo ni historia leo, mkutano umepita. Kinachoendelea sasa ni watu kutafakari maelezo aliyoyatoa Rais, maswali aliyoulizwa, na majibu aliyoyatoa. Kutokuwepo kwangu, walakini, hakuninyimi haki yangu ya kuchambua aliyoyasema. Ndo ninachokifanya. Dk. Shein amenikosha alivyoihifadhi Serikali anmmoja wa wasaidizi wake wawili wakuu. Maalim ni Makamu wa NASEMA HIVI, DK. SHEIN ANA Kwanza wa Rais. Makamu BUSARA SANA. ANAJUA SIKU wa pili, ni Balozi Seif Ali Iddi ATAKAYOMBOMOA MAALIM ambaye pia ni kiongozi wa shughuli za Serikali katika SEIF HADHARANI, NA HATA Baraza la Wawakilishi KWENYE BARAZA LA MAPIN- chombo cha kutunga sheria DUZI, ITAKUWA JAMBO KUB- na chenye kuisimamia SeriWA. kali katika utendaji. Moja ya maswali aliyoulizwa Dk. Shein lilihusu eneo hili ayoiongoza. Amefanikiwa kuifichia matatizo yake kiu- la mwenendo wa Makamu tendaji. Aibu zake kitaswira. wa Kwanza wa Rais, kuhusu Ameifichia Serikali ya Umoja Katiba mpya ya Jamhuri ya wa Kitaifa (SUK) madhambi Muungano. yake. Ameitetea vya kutosha akisema inafanya kazi vizuri, Wahafidhina wanamchukulia kwa mshikamano imara na vingine Maalim Seif. Wanambeza na kudhani si uvumilivu. stahili yake kupewa wadhifa Haya yanawasuta wahahuu. Wanamwona kuwa ni fidhina wanaohangaika kuisambaratisha. Walitarajia shawishi tu asiye na lolote. atashambulia. Wao waliami- Kwao, Maalim Seif, hana ni atamsema na kumbomoa mchango. Amejiingiza Serikalini. Wanadhani ile nafasi Maalim Seif Sharif Hamad,

Daktari huyu wa binadamu, ninayemfahamu kwa miaka 20 hivi tangu akiwa ofisa mdogo katika kilichokuwa Kitengo cha Kudhibiti Ugonjwa wa Ukimwi anashangaza. Najua anapoamua kusema au kutenda, anaweza. Akatenda kwa kiwango usichoweza kuamini. Tatizo kwa asili yake, hatabiriki. Labda upole wake unachangia. Nini maana yake? Pale unapomtarajia afikirie suala fulani namna unavyoliona, usishangae akawa anafikiria tafauti. Anaweza kufikiria vingine kabisa na bado mkaendelea kujadiliana. Hana papara. Mtulivu kwelikweli. Wanasaikolojia wanasema tabia hii ni moja ya sifa za watu wenye akili nyingi. Sijiingizi kusema naye ana akili nyingi. Kwa muda mrefu sijakaa naye kujadiliana lolote, nikapata kumpima. Wiki iliyopita, alikutana na waandishi wa habari, wengine wakitoka Dar es Salaam kwa kugharimiwa na ofisi yake.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein

20

Zanzibar Daima Online

KAULI YA MWINYI MKUU HABARI KUU hi bakini watulivu, mtayaona Chama Cha Mapinduzi (CCM). mengi makubwa yatatokea chini ya Serikali hii. Maalim Seif amesema sana kuhusu suala la Katiba. AmDk. Shein anasema Serikali etoa msimamo binafsi, mbali inatekeleza majukumu yake kabisa na wa CUF. Anataka kwa ufanisi na mshikamaMuungano wa Mkataba na no mkubwa. Ninamnukuu: Zanzibar yenye mamlaka kaSerikali yangu imefanikiwa mili. Sera ya CUF ni ya kuwa kudumu kwa miaka mitatu na muundo wa Muungano sasa kutokana na kuvumil- wenye Serikali tatu. Aliyaseiana na kufanya kazi kwa ma hayo mbele ya Tume ya pamoja bila ya kutanguliza Mabadiliko ya Katiba ya Jaji itikadi za kisiasa. Joseph Warioba. Maalim Seif anajiamini kwa kile ana Nchi nyingine zimechokiamini. jaribu hili (mfumo huu wa Serikali ya Umoja wa KiOna alivyomkingia kifua taifa) zimeshindwa, lakiMakamu mwenzake, Balozi ni sisi tumefanikiwa kwa Seif, alipojikuta akishambulisababu tunavumiliana. Hili wa na umma unaopendelea linahitaji stahamala kubmabadiliko ya Muungano wa vinginevyo tutagawana kwa kutaka Muungano wa mbao na sitaki hili litokee Mkataba chini ya Serikali ya kwenye uongozi wangu. Zanzibar yenye mamlaka kamili. Aliyasema haya aliposukumwa kusema anachukuliaje Balozi Seif alitegwa na kauli za Maalim Seif wakati Serikali ya Muungano kwa huu wa maandalizi ya kuan- kuombwa kueleza ushiriki dikwa Katiba mpya. Ni kweli wa Zanzibar katika kujadili Maalim Seif analizungummapendekezo ya marekebizia kila wakati suala hili. sho ya Sheria ya Mabadiliko Wao wahafidhina wanaona ya Katiba. Alipoinuka akaanaisemea Serikali ilhali yeye liambia Bunge kuwa Zansi rais. Walishasema amzibar ilishirikishwa. Kumbe, fukuze. Zanzibar ilipewa vifungu vinne tu vya mapendekezo Dk. Shein amesema yeye kati ya 12 vilivyopitishwa ndo wa kutoa msimamo wa Septemba 6 na Wabunge wa Serikali. Hajafanya hivyo CCM pekee pamoja na Auna hawezi kufanya hivyo gustine Mrema wa Tanzania kiongozi mwingine yeyote Labour Party (TLP). katika Serikali anayoiongoza. Si Makamu wa Kwanza Maalim Seif alimtetea Balozi wala wa Pili. Wao wanawe- kuwa alijibu kwa kuangalia za kutoa misimamo binafsi vifungu walivyovijadili Serinayozingatia mielekeo ya ikalini. Hakujua wataalamu vyama vyao. Anasema hata wa Wizara ya Sheria na naye aweza kutoa maoni Katiba na Ofisi ya Mwakulingana na mtizamo wa nasheria Mkuu wa Serikali

Zanzibar Daima Online

21

si kumfukuza Maalim Seif. Hawa hawasomi Katiba ya Zanzibar, hasa lile fungu lililoweka nafasi yenyewe ya Makamu wa Kwanza. Si katika asili zao kusoma. Mara nyingi hukurupuka. Ndio maana kila wanapofanya shambulio dhidi yake, hujikuta wakiishia kupiga ngumi baharini. Hakuna mtikisiko ila yale maji yanamwagikia nyusoni mwao. Mabao ya maskani ya Mwembekisonge na Kachorora yanaandika maandishi ya kuthibitisha mashambulizi dhidi ya Maalim Seif. Kazi yao kila wakati ni hiyo tu ya kumsukuma akasirike. Wanakosea sana; hata mara moja kiongozi huyu hajababaishwa na mashambulizi yao. Na kule kubaki kwake imara ofisini, kubaki imara katika kumsaidia na kumshauri Rais wanachukia. Kubaki imara katika kufanya kazi yake kwa ushujaa mkubwa kunawatesa. Kwa upande mwingine, wanapomwona anafanikiwa huku akizidi kukijenga Chama cha Wananchi (CUF) kilichomfikisha hapo, wanaumia wahafidhina. Ni pigo kubwa kwao kwani mashambulizi wanayomlengea yanawarudia. Hayampati na wanamkuta ametulia kama maji mtungini. Hata mara moja Maalim Seif hajatoa kauli ya kuwalenga wahafidhina. Yeye sanasana ni kuelekeza wananchi kutulia wasichafue amani. Husema tu Ndugu wananchi nawasi-

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi waliweka vifungu vingi zaidi katika Mswada, vikiwemo vile ambavyo vina maslaha makubwa na Zanzibar. Nasema hivi, Dk. Shein ana busara sana. Anajua siku atakayombomoa Maalim Seif hadharani, na hata kwenye Baraza la Mapinduzi, itakuwa jambo kubwa. Atakuwa amejiumiza na kujimaliza. Atakuwa ameondoka kwenye mstari. Atakuwa amejichongea. Anajua Serikali ina deni kubwa kwa wananchi. Anajua Serikali haijatimiza ahadi zake. Dk. Shein anajua Maalim alisema nini Bwawani siku matokeo yalipotangazwa. Anajua ametimiza au hajatimiza yale. Anajua Maalim Seif anasaidia kuwepo amani na utulivu nchini. Anajua akimbeza ni hatari kwake. Wahafidhina wanasubiri hali hiyo itokee. Watu hawa wamekuwa wakitaka Serikali ivunjike ili pazuke balaa. Siku zote imekuwa ni imani yao kwamba kuishi kwao kunategemea sana siasa chafu, zilizojaa chuki, hasama na ubaguzi dhidi ya watu wa wasioipenda CCM na hasa Wazanzibari wenye asili ya Pemba ambao wanawaona kama wasiostahili kuwa Wazanzibari. Wanapata shida leo kwa sababu vile viapo vyao kuwa Ikulu hataigusa kiongozi kutoka Pemba vimefika mwisho kwa kuwa Dk. Shein amezaliwa Mkanyageni, Kusini Pemba. Hata Maalim Seif, Makamu wake wa Kwanza, ni mzaliwa wa Mtambwe, Kaskazini Pemba. Wanatokea wapi? Viapo hivi ni kama vile walivyoapa wahafidhina wa Donge kuwa kamwe Maalim Seif na CUF yake hawataingia Donge kufanya mkutano wa hadhara. Maalim ameingia na CUF yake ikafanya mkutano mkubwa Novemba 10, huku mzaliwa wa Donge na muasisi wa CUF, Machano Khamis Ali, ambaye ni Makamu Mwenyekiti, akihutubia

22

Zanzibar Daima Online

TUFUNGUE KITABU

Zanzibar Daima Online

23

VUTA NKUVUTE, KIELELEZO CHA UANDISHI WA KIZANZIBARI


TANBIHI: Uhakiki huu uliandikwa kwa lugha ya Kiingereza na FLAVIA AIELLO TRAORE kwa jina la INVESTIGATING TOPICS AND STYLE IN VUTA NKUVUTE BY SHAFI ADAM SHAF I. Hapa tumeutafsiri kwa minajili ya kuwapa wasomaji wetu mtazamo wa wengine kwa fasihi ya Kizanzibari. wa miongo mingi sasa, wahakiki wa kazi za fasihi wamezisifu kazi za waandishi wa Kizanzibari kwa sifa tele. Kwa mfano, akirejea riwaya za Mohamed Suleiman Mohamed, Said Ahmed Mohamed na Shafi Adam Shafi, M. M. Mulokozi aliandika mwaka 1985: Maendeleo muhimu kabisa, na pengine ya kufurahisha sana, katika kazi za fasihi za Kiswahili katika miaka ya 1970 na 1980, ni kuibuka kwa Zanzibar kama mtoaji bora kabisa wa kazi za Kiswahili kuwahi kutokea hadi sasa, na kiongozi wa wazi wa riwaya za Kiswahili katika siku zijazo.

Hisia kama hizi zinaelezewa pia na R. Ohly ambaye, baada ya kukumbana na riwaya zilizoandikwa na waandishi wa Kizanzibari na wale wa Kitanzania na Kikenya baina ya mwaka 1975 na 1981, amezielezea riwaya za Kizanzibari kama changamoto kubwa kwa uwezo wa kisanaa kwa waandishi wengine wa Kiswahili. Ingawa mnasaba uliotumiwa na Ohly unaweza kujadilika kwa kujikita kwake na kazi zilizotolewa Bara hasa hadithi fupi fupi na kuwaacha waandishi wenye vipaji kama vile Eupluase Kezilahabi au Claude Mungongo, uhakiki wake bado umezungumzia sifa kuu za riwaya za Kizanzibari, yaani kujikita sana kwenye masuala ya kihistoria na kijamii, pamoja na utajiri wa lugha mwanana na kutokufanya mzaha kwenye masuala ya fani. Sifa hizi za fani zinashabihiana sana na riwaya ya Vuta Nkuvute iliyoandikwa na Shafi Adam Shafi na kuchap-

Shafi Adam Shafi

ishwa mwaka 1999, ambayo kwa kumtambulisha msondiyo shughuliko la uhakiki maji kwa msichana wa Kihuu. hindi, Yasmin, ambaye kutokana na mila ya ndoa za Dhamira Kuu kupangwa na wazazi, anakWaandishi wa Kizanzibari wenda Mombasa na mume mara kadhaa wamean- wake, mfanyabiashara dika riwaya za kihistoria, mzee, Bwana Raza. Lakini wakizikita simulizi zao kati- Yasmin anaoneshwa kuwa ka zama za ukoloni ama za mtu asiye na furaha na mpkabla ya Mapinduzi visiwani weke na hatimaye anaasi na humo. Kufuatia hali hiyo, kurudi nyumbani, Zanzibar. matukio kwenye Vuta Nkuvute nayo yanazungumzia Kutabiri matokeo ya makuzi siku za mwisho mwisho za mabaya ni jambo maarufu ukoloni visiwani Zanzibar. kwenye riwaya za Kiswahili, ambapo kawaida waandishi Mandhari ya riwaya hii ni huchora mashaka yale yale changamano sana, maisha yanayoathiri maisha ya vijaya dhiki ya wahusika wakuu na, hasa wa kike, ama kusyanachorwa kupitia matukio hindwa hadi kufikia mauti kadhaa, wahusika wadogo, yao au mateso ya kiakili na matendo ya kuchangam- kimwili kama vile Rosa Missha, yote yanaunganishwa tika au Asumini, au kukimbia na mapenzi ya uhuru na ku- mazingira kandamizi kama jutawala (KUJUTAWALA NI vile Maimuna na Yasmin, NINI?), katika viwango taf- ambapo mote hupelekea auti vya maisha ya kibinafsi, maisha mapya kabisa. kijamii na kisiasa, na hivyo kuusafirisha ule moyo wa Mara tu baada ya kurudi ZanUjamaa katika muonekano zibar, Yasmin anakataliwa na wa kilimwengu zaidi. mjomba wake na anaomba msaada wa shoga yake wa Hadithi yenyewe inaanza pekee, Mwajumba, msicha-

24

Zanzibar Daima Online

TUFUNGUE KITABU

25

na wa Kiswahili anayeishi kwenye mitaa ya masikini ya Ngambo, ambaye anampokea kwa moyo wote. Licha ya ukarimu wa Mwajuma, mama yake Yasmin anakataa kumsamehe bintiye sio tu kwa kuiabisha familia kwa kumuasi mumewe, bali pia kwa kujichanganya na Waswahili na hivyo kuvunja khulka ya jamii yake na tafauti za kijamii na kitamaduni zilizojikita sana kwenye unyanyapaa wa sera za kikoloni linapohusika suala la mahusiano kati ya makabila yanayounda jamii kubwa ya Kizanzibari. Baada ya kukandamizwa kwenye misuguano na ubaguzi wa kijamii huko alikokulia, Yasmin anapata ladha ya maisha mapya wakati akiishi kwa Mwajuma, ambako anagundua maisha yenye wasaa zaidi, mukiwemo ulevi, klabu za usiku na, zaidi ya yote, anapendana na kijana aitwaye Denge.

yerejea nyumbani akitokea Ulaya akiwa hana chochote zaidi ya digrii yake ya Kirusi na dhamira madhubuti ya kuikomboa nchi yake kutoka kwenye Himaya ya Mwingereza. Yeye na marafiki zake wanaandamwa na polisi kwa kufanya propaganda ya kisiasa na kuingiza kwenye nchi vitabu na magazeti yaliyopigwa marufuku na wakoloni. Yasmin anajikuta akihusika moja kwa moja katika mapambano kati ya kundi la Denge na polisi, ambao wanajaribu kumlazimisha amsaliti mpenzi wake mkomunisti na kafiri, lakini anaamua kuwasaidia wanaharakati hao, akiamini wanaandamwa kwa sababu tu wanapigania uhuru.

wapumbavu kabisa, kwao kila mtu ni koministi Ukidai haki yako wewe koministi Ukisema kweli wewe koministi Ukipinga kutawaliwa wewe koministi. Kila anayedai haki kwao ni koministi, na sumu yao kubwa wanayoitumia ya kutaka kutenganisha watu kama hao na wananchi wenziwao ni kusema kwamba watu hao wanaowaita makoministl hawaamini Mungu. Mapambano ya daima kati ya maafisa wa kikoloni na wapigania uhuru yanaipeleka riwaya hii kwenye upeo wa hadithi ya kusisimua, kurusha roho na hekaya za kijasusi, mtindo ambao uliletwa kwa mara ya kwanza kwenye riwaya za Kiswahili na Mohamed Said Abdulla (Bwana MSA), ingawa kwenye riwaya hii polisi wamekuwa wahusika wabaya, wanaotumikia maslahi ya kikoloni kibubusa. Kama inavyoelezewa na Pazi katika ukurasa wa 113, katika mapambano ya kuwania uhuru, ni muhimu kutumia hata njia zisizo za halali kisheria

WATUHUMIWA MENO YA TEMBO WAONGEZEKA

Kama inavyoelezwa na Denge katika ukurasa wa 68 wa riwaya hii, serikali ya Kiingereza ilijaribu kuwatenganisha wapigania uhuru na wafuasi wao kwa kutumia sera ya wagawe uwatawale: Sikiliza Sista, hawa wakoloDenge ni kijana msomi ali- ni na vijibwa vyao ni watu

ESHI la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wengine watatu, wakiwamo maofisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya mabilioni ya shilingi. Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mussa Ali Mussa, amewataja maofisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali (50) na

Mohammed Hija (48) ambao wote wanafanya kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Haidar Ahmad Abdallah (54). Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano. Kamishna Mussa amesema watuhumiwa wengine wawili ambao ni wafanyakazi

TANBIHI: Habari hii iliandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 17


Inaendelea Uk. 40

26

Zanzibar Daima Online

WARAKA KUTOKA BONN

Zanzibar Daima Online

27

Syd.Khalifa akiikagua mitambo ya kuchimba mafuta, Zanzibar. Pamoja naye ni M.M.Pennel Mkuu wa Kampuni ya Shell.

Wazanzibari tujipange, mafuta yasije yakawa nuksi kwetu


atika wiki mbili za mwanzo za mwezi huu wa Novemba nilitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu. Licha ya kuizuru nchi hiyo mara kadhaa hapo kabla, safari yangu ya mwishoni ilikuwa ndefu kabisa kuwahi kuifanya na ya kwanza kukaa na wenyeji walio Waimarati wa kindakindaki, kama wanavojiita watu wa asili wa nchi hiyo ilio ya muungano wa falme saba ndogondogo.

Imarati, nchi yenye wahamiaji wengi wa Kizanzibari, pia ni nchi yenye historia ya maingiliano ya miaka na dahari na Zanzibar, imepiga maendeleo makubwa katika miongo ya miaka ya karibuni, hasa ya miundo mbinu. Hivyo imekuwa ni kivutio kwa Wazanzibari wengi kwenda kutafuta ajira. Wananchi wengi katika miji ya Dubai, Abu Dhabi, al-Ain na Ras al-Khaimah wanaishi katika neema ambayo hata watu wa Ulaya wanawaonea gere. Wafanya kazi hawatozwi kodi ya ma-

Waziri Ramadhan Abdallah Shaaban akibadilishana hatii ya makubaliano na Mwenyekiti wa Kampuni ya Shell

Na Othman Miraji

Waraka kutoka Bonn

Kutafuta mafuta Zanzibar kumeanza mwaka 1957, ilitarajiwa kisima cha Chuwini peke yake kitachimbwa kufikia futi 12,000 ....

28

Zanzibar Daima Online

WARAKA KUTOKA BONN miaka ya 1950 walikuwa wanaishi katika hali ngumu, wengi majangwani katika mahema na katika miji midogo pembezoni mwa Ghuba, wakivua samaki na kula tende, maziwa na nyama ya ngamia. Sasa wanakula kwa wingi vyakula vya kutoka ngambo, nyama kutoka Marekani na Australia inayowaongezea uzito mwilini. Matokeo yake wanapatwa na magonjwa ambayo hapo zamani yalikuwa nadra kusikika Arabuni. Niliwauliza wenyeji wangu: Je, mmefikiria vipi nchi yenu itakavyokuwa bila ya mafuta? Walinijibu kwamba akiba yao ya mafuta itabakia kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Hata wanajizuia kuchimba mafuta mingi hivi sasa ili bei isiporomoke. Niliwaambia kwamba hata kama mafuta yatabakia daima, lakini Wazungu na Wamarekani, wanaonunua mafuta hayo kwa wingi, itafika wakati watafaulu kujitosheleza na nishati mbadala ilio safi, kama vile ile ya kutoka nguvu za jua, upepo au maji ya moto chini ya ardhi. Walinijibu: Allahu Qadeer -Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu ya kufanya kila kitu. Kama alivowapa utajiri wa mafuta hivi sasa, basi atawapa utajiri mwingine pale mafuta yatakapokua hayahitajiki. Hilo ni jibu la kujipa moyo tu. Inasikitisha. Mafuta, licha ya kurahisisha maisha ya watu wa Uarabuni, neema hiyo nimeona ina matatizo na hasara zake pia. Raia wengi wanaupoteza utambulisho wao na utamaduni wao, baadhi wameingiwa na kiburi cha kuwa

Zanzibar Daima Online

29

pato, na serikali inatoa nafuu nyingi kwa wananchi . Familia nilikofikia ya watu watano, ukiwacha watoto wanne, kila mmoja ana gari mbili za fahari. Tulipoketi kula chakula, meza ilijaa vyakula vinavoweza kuwashibisha watu 40. Nilijiuzulu moyoni: kuna harusi? Kadiri asilimia 60 ya vyakula vinabakia na hutupwa mapipani. Sebuleni mazungumzo ya wenyeji wangu yalikuwa tu juu ya likizo zao walipokuwa Marekani na Ulaya. Mikahawa ya Kimarekani ya Macdonald na Kentucky imefurika katika miji ya Imarati. Vipindi vya televisheni wanavoangalia wenyeji wangu ni vya kutoka Marekani na Ulaya, ni nadra wao kuangalia vya Kiarabu. Nilivuta fikra hadi udogoni mwangu nikaiona sura ya maduka ya tende, nguru, papa na chumvi yaliosheheni wakati huo katika mtaa wa Mchangani, Unguja mjini, pamoja na suwela na hanide waliokuwa wanauzwa Malindi. Vitu hivyo vilikuwa vinaletwa Zanzibar na mababu wa hawa Waimarati wa sasa waliokuja katika majahazi yao ya Musim. Waliporejea makwao pale pepo za Musim zilipogeuka, watu hao walichukua boriti kutoka Bara na bidhaa nyingine kutokea Zanzibar. Mnamo muda wa kizazi kimoja tu, maisha ya Waimarati yamebadilika kwa mshangao mkubwa, na yote imetokana na utajiri wao mkubwa wa mafuta ya petroli, kwa jina lengine dhahabu nyeusi. Watu hao hadi katika

matajiri sana. Ukiwaona wanatoka kwenye maduka makubwa ya Supermarkets, wamebeba mifuko mikubwa iliojaa vyakula chungu nzima vya aina mbalimbali, vitu vya anasa - vingi ambavyo hata hawatavitumia - ukiwaona kila mwezi wanabadilisha simu za mikononi na kuchukua mpya zilizoingia masokoni unajiuliza: wazimu huu wa kutumbua na kutumbua fedha bila ya mipaka mwisho wake ni nini? Ni nchi za Ulaya, Marekani na sasa China zinaziuzia nchi za Kiarabu zilizo tajiri kwa mafuta bidhaa hizo. Cha kushangaza ni kwamba ni raia wa nchi hizo za Ulaya na Marekani wanaotambua sasa hasara ya kutumia na kutumbua mali bila ya mipaka. Ulaya na Marekani sasa zinajifunza kupunguza matumizi, zinajizuia kutumia ovyo rasilmali na utajiri wao, zikishikilia kwamba binadamu inabidi aachane na mtindo wa kuishi kwa raha sana ya kupita kiasi kwa gharama ya vizazi vijavyo. Serikali zinawahimiza raia wao wayahifadhi mazingira kwa ajili ya uhai wa sayari yetu hii ya dunia. Nchi za Kiarabu zina akiba kubwa ya mafuta, lakini hiyo haina maana kwamba mafuta hayo yatumiwe ovyoovyo. Ukiona taa nyingi zinazowaka ovyo usiku mzima mabarabarani na maji ya chumvi mengi yanayogeuzwa kuweza kunyunyuzia bustani unasikitishwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira unaosababishwa na moshi mchafu hewani. Bei ya lita moja ya mafuta Abu Dhabi ni asilimia 14 tu ya bei mtu anayolipia akiwa Berlin,Ujeru-

mani. Mwanadamu alitoka kutoka enzi ya ustaarabu wa kutumia mawe na kuingia katika enzi ya ustarabu wa kutumia chuma, na hiyo si kwa sababu mawe yalikwisha. Hasha. Ila tu binadamu alitanabahi kwamba chuma ndio njia ya kuboresha maisha yake. Na hivyo ndivyo itakavokuwa pale mwanadamu atakapoachana na mafuta, si kwamba mafuta hayatakuweko, lakini kutakuwako mbadala ulio bora. Kuna habari nzuri kwamba si miaka mingi kutoka sasa, Inshaallah, nchi yetu ya Zanzibar itakuwa mtoaji wa mafuta ya petroli. Nahisi ni wakati sasa kwa Wazanzibari kujitayarisha, kisaikolojia, juu ya ujio wa neema hiyo. Mafuta yameleta maendeleo kwa nchi kadhaa, lakini utajiri huo kwa baadhi ya nchi umeziletea madhara. Si tu tujifunze namna ya kuyachimbua mafuta hayo na kutowaachia kila kitu wageni watufanyie, lakini pia tupange tangu sasa namna ya kujiepusha na hasara zilizopata nchi nyingine kutokana na mafuta, kisaikolojia, kwa wananchi wao, kimazingira, na kupanuka mizozo ya kijamii. Tujue kutakuweko uchochezi wa kutoka nje wa waroho watakaonyemelea kuupora utajiri huo kwa kutugonganisha vichwa wenyewe kwa wenyewe Wazanzibari. Pia tuchukue tahadhari juu ya kumomonyoka maadili na tunu zetu, kwa kisingizio cha utandawazi unaotokana na utajiri huo. Mafuta yawe baraka na si nakama na balaa kwetu

30

Zanzibar Daima Online

BARAZA YA JUMBA MARO

Zanzibar Daima Online

31

Dk Mvungi ameikosa treni ya mwisho ila tuko naye


Na Ally Saleh Barza ya Jumba Maro

Dk. Adrian Sengondo Hamis Mwarabu Mvungi Daktari huyu wa sheria aliyasabilia maisha yake kwa watu. Alianza kwa ndugu zake na jamaa zake. Si hasha moja ya matunda yake ni padre anayesimamia kanisa la St Joseph mjini Dar es salaam na utitiri wa nduguze ambao wengi wao wamehitimu hata elimu ya juu.

atu wengi wamekuwa wakisikia sifa nyingi mno za Dk Adrian Sengondo Hamis Mwarabu Mvungi katika kipindi alichokuwa amejeruhiwa na wanaodhaniwa kuwa ni majambazi lakini wamesikia zaidi baada ya kufa kwake. Si ajabu watu wengi wanadhani hizo ni sifa anazopewa tu kwa sababu ameshakufa hasa kwa kuwa Waafrika na watu wenye imani ya dini wanaamini kuwa maiti hasemwi vibaya. Lakini hiyo sio kweli hata kidogo.

Kwa hakika Dk Mvungi, aliyetimiza umri wa miaka 61 siku moja kabla hajashambuliwa, alikuwa ni mtu mwema, mstahamilivu, msikivu na hodari sana kwa watu. Kama kuna njia ya kumwombea binadamu wa kawaida apite njia nyepesi kuelekea kwa Muumba wake, sisi wajumbe wa Tume ambao tumemjua Dr Mvungi tusingesita kufanya hivyo. Kila mmoja wetu anaijua sifa ya ukarimu wake pamoja na umbo kubwa ambalo lingemfanya awe na kiburi cha maguvu.

Daktari huyu wa sheria aliyasabilia maisha yake kwa watu. Alianza kwa ndugu zake na jamaa zake. Si hasha moja ya matunda yake ni padre anayesimamia kanisa la St Joseph mjini Dar es salaam na utitiri wa nduguze ambao wengi wao wamehitimu hata elimu ya juu. Akajitolea kusimamia wachochole na walalahoi kwa nguvu na elimu yake. Alianzia kwa kuanzisha kituo cha kisheria cha kuwasaidia wanyonge na baadaye alisukuma kuund-

wa Kituo cha Haki za Binadamu na Sheria (LHRC) na kushirikiana nacho katika mambo kadhaa pamoja na kubuni njia kadhaa za kuwasaidia watu wa tabaka hilo. Ndipo mwombolezaji mmoja aliposema, Ni kinyume cha mambo kwamba waliomuua ni katika kundi la wanyonge ambao angeweza kwenda Mahakamani kuwatetea. Lake alijualo Mungu ni la shani zaidi. Ratiba ya Dlk Mvungi ilikuwa ya ajabu sana.

32

Zanzibar Daima Online

BARAZA YA JUMBA MARO zikawa za kasi, kina na nguvu zaidi. Si katika waliochelewa hata huko nyuma. Maana alianza pale mwaka 1992 NCCR-Mageuzi ilipoanza kutokana na Watanzania kuona haja ya mabadiliko ya Kikatiba. Niliwahi binafsi kukutana naye katika Kamati ya Katiba iliyoundwa na vyama mbalimbali vya siasa. Mimi nikaonekana nafaa kuwemo humo tutengeneze Katiba ambayo ingepelekwa Serikalini, lakini Serikali ilisema wakati bado. Rais Jakaya Kikwete wakati wa kuzindua Tume ya Katiba mwaka jana alimdhihaki Dk Mvungi kwa kumwambia alimkuta amejifungia katika hoteli moja Bagamoyo akitengeza Katiba. Akamwambia kwamba sasa kuwamo katika Tume ya Katiba ni fursa ya kutumia nguvu zake zote katika kazi hii mpya. Na kwa kweli sisi tulio ndani ya Tume tunakiri alitumia nguvu zake zote. Alikuwa tayari kufanya utafiti, kusoma makala ya ziada na hata kujitolea kwa lolote lile. Alitoa suluhu palipokwama, alitoa ushauri penye fundo alimradi alichotaka ni kwamba mwisho Katiba ipatikane. Nilibahatika kufanya naye kazi kwenye Kamati iliyoaminiwa kuwa ngumu kuliko zote katika Tume. Humo ndiko nilikomjua zaidi na kustaladhi kufanya naye kazi. Kubwa ni kuwa alikuwa mtu wa maridhiano. Alikuwa muda wote tayari kuuacha msimamo

Zanzibar Daima Online

33

Nayo hiyo ilitokana na muda mrefu wa kujizoesha ambapo kila siku ya Mungu alikuwa akifanya mchakamchaka, au saa 12 asubuhi alikuwa ameshaanza kazi kama alivyoshuhudia mfanyakazi mwenzake wa South Law Chambers aliyekutana naye siku hiyo ya kuzaliwa kwake tarehe 2 Novemba. Kwenye taaluma Dk Mvungi, ambaye alikuwa mwalimu wangu wa somo la Katiba katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, hakuwahi kufanikiwa kufikia uprofessa na miye naamini ni kwa sababu alikosa muda kwa vile kipindi kikubwa alikitumia akijitolea kuwasaidia watu. Aliandika sana kuhusu haki za binadaamu na mambo ya katiba na alitoa matamko mengi ambayo ungeyasikia kama yalivyonukuliwa na LHRC ungetokwa na machozi. Alijaa tamaa ya usawa, uchu wake, kiu ya mabadiliko lakini hasa alikuwa na ashiki ya usawa. Alikuwa Mjamaa ndani ya moyo wake lakini pia alikuwa yu tayari kwa mabadiliko ya zama mpya. Na ndio maana akaona njia pekee ni kuingia ndani ya mfumo na akajaribu kugombea Urais mwaka 2000, lakini mfumo ulimjibu vilivyo maana hata kura yake mwenyewe katika kituo alichopiga kura haikuonekana na kuhesabika. Alikiri kushindwa katika ugombezi huo bila ya kinyongo na akaona kunakomfaa katika harakati hizi ni kuwa upande wa wananchi na ndipo nguvu zake za kudai Katiba Mpya

Wanachama wa NCCR - Mageuzi wakiwa wamebeba jeneza lilohifadhi mwili wa Kiongozi wao Marehemu Mvungi, ambae pia alikuwa ni Mjumbe wa Tume ya Madiliko ya Katiba Mpya.

wake pindi akishawishiwa na alitafuta suluhu ili kuuridhia upande ulojisogeza. Tulimtania sana na yeye alikuwa na utani mwingi. Mimi sijawahi kufanya kazi katika Tume ya Kitaifa yoyote ile, lakini nimeona kazi katika Tume ya Katiba ilikuwa nyepesi kwa sababu ndani yake pamekuwa na nafasi ya ubinadamu na zaidi watu wote wamejifanya ni wa daraja moja na kwa hivyo wamejenga ukuruba. Mmoja aliyekurubiwa na kila mtu ni yeye Dk. Mvungi. Aliwahi kusema kwamba angetamani kus-

hona suti ili aende katika Bunge la Katiba kutetea andiko la Tume ambalo alifanya kila njia liaminike na likubalike kwa sababu alijua huo ni mchango wake muhimu na alifanya kazi kana kwamba ndio kazi yake ya mwisho. Lakini hakuwahi kuivaa suti yake kama alivyokosa kuendelea kuwemo katika Treni ya Katiba ambayo inaelekea kituo chake cha mwisho. Ila wengi tunaamini japo hatutamwona tena atakuwa akitusubiri kusherehekea na sisi Katiba Mpya katika zama mpya za Tanzania ambazo wanawe na wanetu wataishi nazo

HEKAYA ZA ZANZIBAR
34 Zanzibar Daima Online

Zanzibar Daima Online

35

MEZA FUPA
Bila ya kubaini, chembe ndogo ya wema uipandayo ardhini, huenda ikachipua na kutoa mti mkubwa utakaoweza kukupatia kivuli au kuwapatia wengine wakati wa jua kali la kiangazi.
Na Ally Hilal Hekaya za Zanzibar

ila ya kubaini, chembe ndogo ya wema uipandayo ardhini, huenda ikachipua na kutoa mti mkubwa utakaoweza kukupatia kivuli au kuwapatia wengine wakati wa jua kali la kiangazi. Ilikuwa ni safari ya mwendo mkubwa, walikuwa ni vijana watatu walioongozana katika kukitafuta kijiji ambacho

walipata kusikia kuwa aliishi bibi mwenye historia nzima ya nchi yao. Bibi aliyeishi miaka mia mbili, ndiye pekeye aliyeweza kutambua hali halisi ya nchi yao. Sio kama haikuwepo historia, lakini historia iliyokuwepo ilipotoshwa na kuwaziba macho vijana waitwao kizazi kipya. Walilkuwa ni vijana watatu wenye umri kati ya miaka

ishirini hadi thelathini. Aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiandaa safari hii alikuwa ni Miftaha, kijana jasiri asiyeogopa kitu katika kuitafuta haki. Mwili wake ulionekana dhaifu kutokana na wembamba wake, alikuwa ni mweusi kidogo, hakuwa mrefu sana ila wembamba wa umbile lake ulimfanya aonekane mrefu wa kimo. Wengine walikuwa ni Suheli na Maimuna. Wanaume wawili na mwanamke mmoja. Maimuna alikuwa ni ndugu yake Miftaha.

Bi. Msiri alifanana na jina lake. Moyo wake uliyabeba mengi tena makubwa mithili ya dunia au sawa na umri wake. Miaka mia mbili kwa ulimwengu wa sasa utatolewa kwenye vyombo vya habari na kuingizwa katika kundi la watu wa maajabu. Huu ndio ulikuwa umri wa bibi huyu aliyeishi katika kiijiji cha Maukio. Pamoja na umri wake mkubwa, bibi huyu alikuwa na meno yote thelathni na mbili, macho yake yalikuwa hayaoni tena vizuri lakini alikuwa na uwezo wa kusikia kama mtoto mdogo, si

HEKAYA ZA ZANZIBAR
36 Zanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online 37

rahisi kumsengenya ukiwa karibu yake. Alikuwa anatembea kwa tabu sana, alitembea kwa mkongojo wake uliochongwa vizuri, ulichorwa nakshi nzuri za msumeno na ulikuwa umeandikwa TUTAFIKAJE? Bi Msiri aliishi kando na mto mkubwa uliokuwepo katika bonde kubwa kijijini pale. Maisha yake yalikuwa ya upweke tangu alipokuwa na miaka ishirini baada ya kuipoteza familia yake yote katika hali tata hadi leo hakuweza kuwaona tena. Alikuwa mtu wa mwanzo kuhamia kijiji hiki baada ya kukimbia mjini kwao na kujitokomeza katika bonde hili. Aliishi kwa tabu sana akiwa mafichoni huku ambako kulikuwa mbali na mji aliotoka. Miaka ilivyozidi kusonga mbele, nyumba zilisogea hadi kufika sehemu aliyoishi Bi Msiri. Ni historia ndefu ambayo hakuna aliyeijua, walioishi naye walikuwa hawajui chochote kuhusu bibi huyu, walimuona kuwa ni bibi wa kawaida tu asiyepungua umri wa miaka themanini kutokana na muonekano wake lakini hawakuujua umri halisi wa bibi huyu. Hakuwahi kuwa na rafiki wa karibu ambaye aliweza kubadilishana naye mawazo zaidi ya Bi Tausi aliyekuwa mkulima katika bonde hili, alikuwa na shamba lake mwenyewe. Linaweza likajengeka suali katika akili ya mtu kuhusu bibi huyu aliyejitenga na watu kwa miaka mingi na aliyebeba siri nzito moyoni

mwake, suali jengine ni kuwa vipi Miftaha na wenzake waliujuwa uwepo wa bibi huyu na kwa ajili gani waliamua kumtafuta. Miftaha ni miongoni mwa vijana waliopata elimu, alisoma hadi chuo kikuu nje ya nchi, alibahatika kusomeshwa na serikali yake iliyokuwa madarakani kutokana na nafasi ya baba yake, baba yake alikuwa mfuasi mkubwa wa chama kilichokuwepo madarakani, hapakuwa na chama cha upinzani kwa sababu serikali iliogopa kupingwa na kukosa wafuasi iwapo wataendesha serikali yao kinyume na wanavyotaka wananchi. Pamoja na hayo wananchi wengi hawakukiunga mkono chama hiki, walikipinga chini kwa chini kwa kuhofia kukamatwa na kuishia gerezani. Pamoja na kwamba Miftaha aliishi kwa baba yake, baba yake alikuwa ni mshauri wa raisi wa nchi, aliyajua mengi yaliyokuwa yakitendeka nchini, lakini watoto wake wote wawili hawakukubaliana naye, kila siku waligombana na baba yao. Licha ya elimu yake, Miftaha hakuweza kupata nafasi za juu serikalini kama ilivyokusudiwa na baba yake hapo awali, kusoma kwake nje ilikuwa ni kuandaliwa ili aweze kuingizwa katika mfumo wa serikali lakini alionekana na msimamo tofauti, kutokana na sababu hiyo alibaki kuwa mwalimu wa skuli. Siku moja alirudi mapema skuli kwa sababu kichwa kilikuwa kinamuuma, ilikuwa ni jioni saa kumi na moja kamili, alikutana na Bibi mmoja aliyechoka sana, mguu wake uliku-

wa unavuja damu, alikuwa ametafunwa na nyoka, ilikuwepo gari moja tu inayokuja kutoka kijiji alichoishi bibi huyu, ilikuja asubuhi na kuondoka jioni, alikuwa ni Bi Tausi, rafiki yake bi Msiri. Miftaha alisimama na kusogea pembeni alipokuwepo bibi huyu, alimuweka kwenye kibao cha baiskeli yake na kumpeleka hospitali. Hakuna aliyemjali mgonjwa, kila mmoja alijishuhulisha na kazi zake, baadhi ya wauguzi walimtazama mgonjwa wa Miftaha kwa dharau bila ya kujali kuwa alikuwa katika hali mbaya kwani sumu ya nyoka ilikuwa inazidi kumuenea mwilini. Daktari wa zamu alikuwa amekaa nje anasoma kitabu cha riwaya. Miftaha alitoka hadi nje baada ya kuambiwa kuwa daktari wa zamu alikuwepo nje, alimkuta daktari amewacha kitabu na sasa anacheza karata na vijana wa mtaa. Ilimuuma sana kumuona daktari anacheza karata huku wagonjwa wakiumia bila ya matibabu, alimsogelea daktari na kumwambia kuwa kuna mgonjwa yuko hali mbaya. Alipata majibu ya kukatisha tamaa. Kijana mimi mwenyewe ni mgonjwa hapa, au hujui kama na sisi madaktari ni wagonjwa na tiba yetu hatujaiona, vilio vyetu havisikilikani maana tuna sauti ndogo, ila nyinyi munataka tuvisikilize vilio vyenu, je vyetu avisikilize nani?

Maneno haya alikuwa anayazungumza daktari kumwambia Miftaha bila ya kumtazama aliyekuwa akizungumza naye. Kwa hiyo unataka kunambia kuwa wagonjwa wetu tuwaache wafe? Yule daktari aliendelea kucheza karata na kumjibu Miftaha bila ya kumtazama usoni. Kufa! Mh! Sasa wewe unafikiri mimi unayeniita daktari niko hai! Kwa lipi la kusema ni uhai, mimi ni maiti kwenenda! Muda ulizidi kupotea, Miftaha aliamua kuzitawanya karata na kuuharibu mchezo, vijana waliokuwepo pale walipanda hasira na karibia kumrukia Miftaha, muda wote huo Daktari alikuwa hajamjua anayelumbana naye, alipoinua uso wake alimuona Maalim Miftaha ambaye alikuwa ni mwalimu msaidizi wa skuli ya Mwendapole, alikuwa ni mwalimu wa watoto wa daktari, alipojua kuwa alikuwa ni mwalimu wa watoto wake aliomba radhi kwa kudai kuwa alikuwa hajamjua. Aliwatuliza vijana waliokuwa na hasira na kutaka wamuache mwalimu. Miftaha alitikisa kichwa na kuongozana na daktari bila ya kumjibu kitu ingawa daktari alijifanya mchangamfu kwa lengo la kujizimuwa kwa maneno yake yaliyomkera Miftaha.

Itaendelea.

38

Zanzibar Daima Online

KALAMU YA BIN RAJAB

Zanzibar Daima Online

39

HOTELI MPYA YA NYOTA SABA KUFUNGULIWA MJI MKONGWE

Burj Al Arab

Na Ahmed Rajab

Kalamu ya Bin Rajab

apema mwakani hoteli mpya itafunguliwa Mji Mkongwe. Inasemekana kwamba hoteli hiyo itakuwa na hadhi ya nyota saba. Ikiwa ni kweli basi tunastahiki kujipigia makofi kwani nijuavyo ni kwamba duniani kuna hoteli moja tu

yenye nyota saba; nayo imejibandika yenyewe hadhi hiyo ya kuwa ya nyota saba. Hiyo hoteli inayojigamba kwamba ni yenye nyota saba ni hoteli ya Burj al Arab iliyo Dubai. Nijuavyo ni kuwa hata ya nyota sita iko

moja tu duniani, nayo ni Hoteli ya Fullerton iliyoko Singapore. Bila ya kujiingiza katika mabishano ya iwapo ni kweli hoteli hiyo mpya ya Mji Mkongwe itakuwa ya nyota saba ni sahihi nadhani tu-

kisema tu kwamba hoteli hiyo itakuwa kubwa na ya kisasa. Mapambo na nakshi za ndani ya hoteli ni za hali ya juu kabisa. Hoteli hiyo itayofunguliwa mwakani Mji Mkongwe itaendeshwa na Kundi la Ma-

40

Zanzibar Daima Online

KALAMU YA BIN RAJAB Hayo yote ni sawa. Lakini kuna mingine yaliyo mazito pia yanayostahili kuzingatiwa na waendeshaji wa hoteli hiyo ili isije ikawa chanzo cha mfarakano baina ya wakazi wa Unguja mjini, hasa wa Mji Mkongwe, na hoteli yenyewe. Tunafahamu kwamba hoteli ya babu kubwa kama hiyo itahitaji iwe na wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa na uzoefu wa shughuli za utalii. Tunatambua kwamba huenda tusiwe na watu wa aina hiyo walio tayari kupatiwa ajira hotelini humo. Hata hivyo, tuna haki ya kuwauliza wakuu wa hoteli hiyo iwapo wameandaa mkakati wowote wa kuwafunza vijana wenyeji wa Mji Mkongwe shughuli za utalii ili waweze nao kupatiwa ajira humo badala ya kuajiriwa watu kutoka nje ya Zanzibar. Ikifanya hivyo basi hoteli hiyo itasaidia kuwapatia ajira vijana na hivyo kuwaingiza katika jamii badala ya kuwatenga na itasaidia pia kuupiga vita umaskini na unyonyaji. Mwaka 1999, Jumuiya ya Umoja wa Mataifa ya Utalii Duniani (UNWTO) ilitunga kanuni za maadili kuhusu utalii ambazo zinatakiwa zifuatwe kote duniani. Kanuni hizo zina lengo la kupunguza athari mbaya zinazopata nchi na wana wa nchi, kutokana na shughuli za utalii. Kwa hakika, inatia moyo kuona kwamba mahoteli duniani siku hizi yanajihusisha na masala ya haki za binadamu na maadili ya kufanyia biashara. Katika muda wa miaka kumi iliyopita makampuni makubwa ya hoteli yamechukua hatua muhimu za kuziunganisha sera za haki za binadamu na kuziingiza katika sera zao kuhusu maadili na namna ya kufanya biashara. Suala la maadili lina umuhimu mkubwa katika nchi kama ya kwetu yenye kufuata

Zanzibar Daima Online

41

kampuni ya Melia yenye makao yake makuu Uhispania. Kweli sio sisi tuliotoa fedha za kuijenga kwa hivyo hatuwezi kusema kuwa ni yetu lakini iko kwetu. Hilo si fanikio dogo kwa sababu kampuni hiyo ya Uhispania kuamua kujenga hoteli aina hiyo Mji Mkongwe kunaashiria mengi kuhusu Zanzibar. Muhimu ni kwamba kampuni hiyo baada ya kuipima na kuitathmini hali ya mambo ilivyo Zanzibar imeona kwamba kuna usalama na utulivu wa kutosha kisiwani humu wa kuhakikisha kwamba rasilmali yao wanayoileta Zanzibar haitokuwa hatarini. Walioijenga hoteli hiyo wanasema kwamba ujenzi wake umefuata kanuni za kuuhifadhi Mji Mkongwe ambao umetangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kuwa ni moja ya Turathi za Dunia.

maadili ya Kiislamu. Utalii tunautaka lakini hatuutaki ikiwa utakuwa unazikanyaga mila zetu, dini yetu na utamaduni wetu. Hapo ndipo penye hatari. Na hatari inaweza ikazuka mara moja iwapo hatuhakikishi ya kwamba wageni wenye kuendesha shughuli za utalii nchini mwetu hawendi kinyume na maadili yetu. Miongoni mwa wanayopaswa kuyafanya ni kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinaheshimiwa na kwamba watoto wadogo wanapewa hifadhi na hawatumiwi kwa shughuli za kifisadi, kama kwa mfano za ngono, na wateja wa hoteli. Wakuu wa hoteli hiyo, pamoja na nyinginezo zilizo Mji Mkongwe, wana wajibu wa kuangalia namna gani wanaweza kuwasaidia wenyeji wa Mji Mkongwe sio tu katika kuwapatia ajira lakini pia katika mambo mingine ili wahisi kwamba hizo hoteli kweli ni sehemu ya jamii yao

Inatoka Uk. 25
wa Kampuni ya Uwakala wa Mizigo ya Island Sea Food Limited, Mohammed Suleiman Mussa (45) na Juma Ali Makame (34), walikamatwa siku ya tukio la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo kwenye Bandari ya Zanzibar. Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa kwenda Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi. Pamoja na mambo mengine, kusafirishwa kwa watuhumiwa hao kwenda jijini Dar es Salaam,

WATUHUMIWA MENO YA TEMBO WAONGEZEKA


kunatokana na Zanzibar kutokuwa na sheria maalumu inayohusu wanyamapori. Maofisa wa Idara ya Wanyamapori nchini leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na kulinganisha vipande 1,023 vya meno ya tembo vilivyokamatwa juzi kwenye Bandari ya Zanzibar na kubaini idadi ya tembo waliouawa kuwa ni 305. Meno hao yenye uzito wa kilo 2,915 yenye thamani ya dola 4,775,000 sawa na Sh 7,480,125,000 za Tanzania, yalikamatwa

juzi yakiwa yamehifadhiwa katika magunia 98 na kuwekwa kwenye kontena moja la futi 40 lenye namba PCIU 857619/0 lililokuwa tayari kupakiwa kwenye meli ya MV Kota Henning kupelekwa nchini Ufilipino kwa magendo. Hadi sasa bado makachero wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na makachero wa Polisi Zanzibar, Idara ya Wanyamapori makao makuu wanaendelea na upelelezi kuwabaini waliohusika

na kashfa hiyo. Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha upelelezi wa kina unafanyika ili kuwakamata wahusika wa mtandao huo. Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado linamsaka tajiri aliyewezesha mipango ya kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili kusafirishwa nje ya nchi

You might also like