Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 14

ZANZIBAR PROPERTIES

HOME NOT A HOUSE

Zanzibar
Daima Online

Toleo nambari 11/09 June 2014

CALL US:+447588550153

W W W. Z A N Z I B A R P R O P E R T Y. C O M PA N Y

FREE

LANDLORDS

Listing

CALL US:+255773620202

WHYCHOOSEUS?
a. Our Marketing is second to none.
b. We advertise in all major portals.
c. As well as being top search engines.
d. we can give your property lets huge
exposure

ABOUTUSCOMPANY
You will see the list of applicants we
may have for your property and your
property will be uploaded to our
site and the portals there and then
bringing the delay to almost zilch.

FACEBOOK/ZANZIBARPROPERTIES

WWW.ZANZIBARPROPERTIES.COMPANY

INFO@ZANZIBARPROPERTIES.COMPANY

www.zanzibarproperties.company

TIWITTER/ZANZIBARPROPERTIES

WAHAFIDHINA
KUYAANGAMIZA
MARIDHIANO?

SIASA. UCHUMI . MICHEZO. ELIMU . DINI. UTAMADUNI .KILIMO. BURUDANI.

Viongozi wa Zanzibar
fikirini mara mbili

arida hili lina wasiwasi kwamba lile kundi linalojitambulisha kama watetezi wa
mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili
visiwani Zanzibar ni mabaki ya wale
waliopinga Maridhiano ya Wazanzibari
tangu yalipoanza Novemba 2009 na ambao muda
wote wamebakia kwenye nafasi ya kungojea
muda wa kulipiza kisasi chao kwa Maridhiano
hayo.

Hawa ni wanasiasa waliokuwa wakifaidika na


mvurugano wa Wazanzibari, ambao wakiutumia
kujikweza mbele ya wenzao wa Tanzania Bara na
pia kuwatishia kwamba kama wasingeliwasaidia
kusalia madarakani Zanzibar, basi nchi nzima ingelikuwa kwenye zahama. Kundi hili, ambalo kwa
siasa za Zanzibar limepachikwa jina la wahafidhina, haliwakilishi kwa namna yoyote Zanzibar
yenye ustawi na mustakabali mwema. Ni kundi la
giza!

Itakumbukwa kuwa kuelekea kuzinduliwa kwa


Bunge Maalum la Katiba, jarida hili lilitumia safu
hii wito wa kuwataka wawakilishi wa Zanzibar
kwenye Bunge hilo waende kama Wazanzibari na
sio watetezi wa mirengo ya vyama vyao vya siasa.
Hawakufanya hivyo.
Walikwenda wakibeba ajenda finyu za vyama
vyao, wakiwacha nyuma ajenda pana ya Zanzibar.
Matokeo yake wakazitumia siku zote za awali kuumbuana na kuiumbua Zanzibar. Wakajeruhiana
na kuijeruhi nchi yao mbele ya macho ya walimwengu. Jukwaa walilopaswa kulitumia kujitetea,

ndilo waliloligeuza la medani ya kupigania.


Wakaondoka wakiwa wanachiria damu, Zanzibar ikiwa taabani.

Hivi sasa kundi hili la giza limeamua kuendeleza mapambano yake dhidi ya Zanzibar
ndani na nje ya Zanzibar. Jarida hili limepokea
taarifa kwamba ule mpango wa kuiangamiza
Serikali ya Umoja wa Kitaifa unaosimamiwa
kijuujuu na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni
(CCM), Salmin Awadh Salmin, umewiva. Kwamba wanataka kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi hiki kilichobakia kabla ya uchaguzi wa 2015,
serikali hiyo inaporomoka, na kwamba baada
ya uchaguzi huo, Zanzibar haitakuwa tena na
haja ya kuwa nayo.
Walio kwenye mpango huo kwa upande wa
Zanzibar, kwa mara nyengine wanatumia
mgongo na nguvu za Chama cha Mapinduzi
(CCM) upande wa Bara. Wanawatisha kwamba
uhai wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
ni sawa na kifo cha Muungano. Wanasema
kwamba ili kuulinda Muungano, lazima serikali
hiyo iuliwe.

Lakini wasichokisema na ambacho Jarida hili


linasikitika ikiwa CCM na serikali yake upande wa Tanzania Bara utakuwa haukijuwi ni
kwamba kinachopiganiwa ni kulinda madaraka
yao kwa gharama yoyote iwayo hata ikiwa
gharama hiyo ni kuirejesha Zanzibar na, hivyo,
Tanzania nzima nyuma.

Jarida hili linapenda kuonya na kutoa wito huu


kwa wale wote wanaodhani kuwa Maridhiano
ya Wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa
ni kwa maslahi ya Chama cha Wananchi (CUF)
na hasara kwa CCM tu. Tunawaambia kwamba
Maridhiano haya ni ya Wazanzibari. Ni kwa ajili
yao, yalitokana na wao na ni miliki yao.
Tunawataka waache kufikiri kwa matumbo yao
na badala yake watumie vichwa vyao kuwaza
nini itakuwa hatima ya Zanzibar nje ya Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kama wanadhani kurudi nyuma si kazi na wala hakuna
maafa yoyote kwao na kwa maslahi yao, wajipe
muda mdogo kuwafikiria wanasiasa kama wao
katika nchi za Kenya, Liberia na Yugoslavia.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ina
wasaa wa kutosha kama wao hawana wa kujifunza.
Zama zimebadilika. Wazanzibari wa 2001 sio
tena wa 2014.

Online
styles

Z anzibar Daima
magazine Daima
Timu Yetu

VICE PRESIDENT ADVERTISING


MHARIRI MKUU
Brian Mahoni
Ahmed Rajab
Email: ahmed@ahmedrajab.com
VICE PRESIDENT Daima & BRAND
Bob Trembesi
MHARIRI MSAIDIZI
Mohammed Ghassani
MARKETING MANAGER
Email: kghassany@gmail.com
Matt Sloben
MHARIRI MSANIFU
COMMUNICATIONM Khamis
Hassan MANAGER
Email: Brad Saragih
hassan@zanzibarimage.com
COMMUNICATION COORDINATOR
COMMUNICATION MANAGER
Bobby Barongan
Hassan M Khamis
SENIOR MARKETING SPECIALIST
WAANDISHI
Fabio Jabir Idrissa
Contong
Email: jabirgood@yahoo.com
EDITORIAL DIRECTOR
Alain Bogosiong
Foum Kimara
Email: ffoum@hotmail.com
ART DIRECTOR
Kamituo Kusdi
Ally Saleh
Email: allysaleh126@gamil.com
EDITOR AND PROJECT MANAGER
Lurah Kosnan
WASAMBAZAJI
mzalendo.net
SENIOR zanzibardaima.net
PROJECT EDITOR
Matt Koplak
zanzibardaima/facebook
PROJECT COORDINATOR
MATANGAZO
Jan Hassan M Khamis
Hasselbaink
Simu: +44 7588550153
ASSOCIATE ART DIRECTOR
Email: hassan@zanzibarimage.com
Steven Galonan
WASIALIANA NASI
SENIOR GRAPHIC DaimaER
zanzibardaimaonline@gmail.com
Kim Kamandanu
JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA
PHOTO COORDINATOR
Zanzibar Daima Collective
Lucas Lavale Way
233 Convent
Southall
COPY EDITORS
UB2 5UH
George Bohamen
Nonnstr. 25
PRODUCTION MANAGER
53119 Bonn
Kakeane Germany
Minggat
PRODUCTION ASSISTANT
www.zanzibardaima.net
Bakari Sagna

[Muhariri]
Mohammed Ghassani

CONTRIBUTORS
Lara Sanusi, Silvian Gidali,
Martin Lumer, George Sapulete

www.magazine.com

YALIYOMO

TAARIFA
Tunawaomba radhi wasomaji
wetu kutokana na kusitishwa
kwa machapisho ya makala
yetu......

15
11
TAARIFA

01

WAHAFIDHINA WA ZANZIBAR, IZIKENI HISTORIA CHAFU

02

MAKADA WA CCM WANAIMBA NYIMBO MBAYA 07-10


Matangazo 09 -10
ZANZIBAR NI NCHI YA KITU KIDOGO

11-14

MGUU MBELE MGUU NYUMA

15-18

DEMOKRASIA NA UKOMO WA UONGOZI 19-22


Zanzibar, visiwa vya michezo 16

01

Toleo la 11

Toleo la 11

02

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

Wahafidhina Zanzibar, izikeni historia chafu kabla


haijawazika nyinyi
Sehemu ya wananchi
wa Zanzibar kisiwani
Pemba
ikijumuika
na wenzao kwenye
kampeni ya kuunga
mkono mapendekezo ya
Muundo wa Muungano
wa Serikali Tatu, tarehe
1 Mei 2014 kwenye
Uwanja wa Gombani
Kongwe, Chake Chake.

Na
Mohammed Ghassani

tazamo wa kihistoria unaotumiwa


na wahafidhina wa
Zanzibar kuhalalisha
upinzani wao dhidi ya maridhiano ya Wazanzibari miaka minne
baada a Serikali ya Umoja wa Kitaifa, una mapungufu makubwa.
Ikiwa hoja ni kwamba Chama
cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), kama
vyama viwili vikubwa na pekee
vinavyoongoza siasa za Zanzibar, haviwezi tena kushirikiana
kuongoza kwa sababu ya tafauti
zilizojitokeza baina yao kuhusiana na Muundo wa Muungano,
basi upungufu wa kwanza ni
kwamba hoja hii haiangalii his-

03

Toleo la 11

toria katika uhalisia wake.


Msukumo wa kihistoria ambao ndio uliozaa
mjengeko wa kijamii na kitamaduni wa Zanzibar
unazungumza hadithi tafauti. Kwamba Wazanzibari ni watu mchanganyiko na kwamba kupitia
mchanganyiko huo ndipo maisha yao yanapokwenda mbele katika kila nyanja iwe ya kisiasa,
kiuchumi, kijamii na kitamaduni.
Kila mara, mwenendo wa siasa za nchi hii zilipodharau au kukandamiza dhati hii ya mchang-

anyiko, basi mustakabali


wa visiwa hivi ulitiwa rehani na kuingizwa katika
majaribu makubwa. Kwa
mfano, hakukuwa na haja
ya kufanyika Mapinduzi
ya 1964 ikiwa wafanya
siasa wa wakati huo, kutoka pande zote, waliizingatia dhati hii.
Pili, hata kwa kutumuia
hayo hayo mapokezi ya

historia wanayoyaamini
wahafidhina wetu, bado
historia hiyo si sehemu
salama kwao kujifichia,
maana ni gofu lililojaa
woga, kujishuku na kutokujiamini. Bahati mbaya
kwao ni kuwa gofu hili
lina mlango mmoja tu wa
kutokea ambao umeandikwa: Maridhiano na
Umoja wa Kitaifa.

Mwangwi unaosikika
ndani, kwa hakika unawafukuza wasikae gofuni
humo. Ni mwangwi wa
matendo yao. Kwa hivyo,
ni ama kupita katika
mlango huu au ni kubakia ndani ya jengo hilo
wakawa wamekwama na
kuikwamisha nchi katika
khofu, woga na kutokujiamini kama ilivyokuwa
kabla ya 2010.
Toleo la 11

04

Zanzibar Daima

Nitafafanua. Kwanza,
msimamo wa wahafidhina hao wa kujidhani
kwamba peke yao ndio
wazalendo wenye haki ya
kuitawala Zanzibar una
makosa mengi ya kisayansi na hauwezi, hatimaye, kuifikisha Zanzibar
popote zaidi ya penye
mfundo na mkwamo
mwengine wa kisiasa na
kiuchumi.
Kadiri wanavyotumia
historia kuhalalisha ukaidi
wao kwa Maridhiano
na Umoja wa Kitaifa,
ndivyo wanavyokwenda
wenyewe kwenye upande
usio sahihi wa historia,
siasa na mustakabali wa
nchi ndivyo wanavyosimamia upande sio wa
hoja.
Zanzibar imeinuka pale
tu ilipojali mchanganyiko
wake na kila ilipopuuzia
hilo imeporomoka. Zanzibar ikiporomoka, wao na
ahli zao pia hawatakuwa
salama. Mwenye kutaka
salama yake hataendelea
kujifungia kwenye gofu
hili la historia, maana

05

Toleo la 11

Zanzibar Daima

ni kujihalalishia vitisho,
woga na kutokujiamini. Mwenye mapenzi ya
kweli kwa Zanzibar, basi
hataupa mgongo mlango
wa Maridhiano na Umoja
wa Kitaifa, maana ndio
pekee utakaomtoa.
Mwenye akili timamu
Zanzibar, hasa kiongozi
mwenye kundi la wafuasi
atatafuta njia muafaka ya
kuifanya historia imsaidie
kupiga hatua mbele kama
kiongozi wa watu anayejiamini. Na ni mwangwi ule
wa kwenye gofu alimojifungia ndio unaomwambia
hivyo. Ndio unaomfukuza:
Toka humu. Pita kwenye
mlango wa Maridhiano na
Umoja wa Kitaifa, uende
zako!
Kwa vyovyote vile, mtazamo wa kihistoria hauwezi kuzalisha wahafidhina, maana busara yake
inasema kitu tafauti na
unganganizi wa mambo
yasiyokuwa na maana.
Inasema kuwa kujuwa
tukuendako ni kwa kujuwa tutokako na kupaelewa tulipo. Na ili hilo lifan-

yike, ni lazima tukumbuke


na tujifunze kwa kukumbuka huko. Kwamba ikiwa
kuna mabaya yoyote
yaliyotutokezea, basi
tupate somo la kujifunza
yasijirudie tena.
Historia ya Zanzibar ni
shuhuda wa ubaguzi na
matokeo yake mabaya, kukiwemo kudidimia
kiuchumi, kielimu na
kisiasa. Ukaidi hausaidii
kitu, maana hata macho ya kawaida yanaona
kwamba wenzetu wengi
ulimwenguni, waliokuwa
kama sisi, wameendelea
kusonga mbele sana kwa
sababu kile kinachotukuzwa Zanzibar, yaani ubaguzi, kinadharauliwa
huko. Anayeamini hasa
juu ya mtazamo wa historia anakuwa mtu wa
mwanzo kupingana na
ubaguzi. Kwa hivyo, mtazamo wa kweli wa kihistoria huzalisha watu
wenye uwezo wa kubadilika na sio vinganganizi.
Ukiwasikiliza walivyokuwa wakipwaga kwenye
Bunge Maalum la Katiba

na baadaye mikutano
yao ya hadhara baada
ya Bunge hilo kuahirishwa, utagundua kwamba
huenda wahafidhina wa
Zanzibar wanaona mauaji
ya 2001 yalikuwa ni tendo la kistaarabu na, kwa
hivyo, la kutukuzwa na
kurejewa tena na tena kila
ikipatikana nafasi.
Ndio maana ya kauli zao
za kuutetea Muungano
wa serikali mbili na kutokuitoa nchi kwa kipande
cha karatasi. Kundi hili
ambalo kwa hakika si
kubwa kama sauti yake
inavyosikikana linanadi
kwamba Maridhiano ya
2009 kilikuwa kitu kibaya
sana kwao na hivyo ni
jambo la kuepukwa kadiri
inavyowezekana.
Kitu pekee kinachodhihirika kwenye haiba ya
wapingao Maridhiano ya
Zanzibar ni ukosefu wao
wa upeo wa kilimwengu.
Zanzibar si nchi pekee
ulimwenguni iliyowahi
kupitia historia iliyonayo.
Ziko zilizopitia historia
mbaya zaidi. Pia SMZ si

serikali pekee iliyoingia


madarakani kwa vurugu
za umwagaji damu na
kuishia kuyatumia madaraka hayo vibaya dhidi ya
watu wake. Ziko zilizokuwa kandamizi kuliko hiyo.
Dunia imejaa mifano
mingi. Utawala wa Adolf
Hitler uliwatendea unyama mkubwa Mayahudi
karibuni nusu milioni
walitiwa katika kambi
za mateso, wengi wao
wakafia humo na wengine
wakakimbia nchi zao za
uzawa. Lakini watawala
waliofuatia, kwa kujuwa
machungu yanayobebwa
na ndugu za wahanga
hao na kuthamini maisha ya watu, wakaomba
radhi na kufanya jitihada
za kuwashirikisha tena
Mayahudi katika mfumo
wa maisha ya Ujerumani
kisiasa, kiuchumi, kijamii
na kitamaduni.
Katika nchi ya Afrika
Kusini, siku za ubaguzi
wa rangi zilisababisha
machungu makubwa kwa
jamii ya Waafrika weusi.
Kitu cha mwanzo alichoki-

fanya Nelson Mandela,


baada ya kuingia madarakani, ilikuwa ni kuunda Serikali ya Umoja wa
Kitaifa na Tume ya Ukweli
na Maridhiano. Leo hii
machungu yanazidi kuyeyuka baina ya jamii hii
moja yenye mchanganyiko kama wa Zanzibar.
Hiyo ndiyo mifano ya
kuigwa Zanzibar. Kama
Hitler alivyofanya, unazi
wa kutisha umeshafanyika Zanzibar. Kama
makaburu walivyofanya,
ubaguzi wa hali ya juu
ushafanyika Zanzibar. Na
haya yanaendelea hadi
sasa. Ni Maridhiano na
Umoja wa Kitaifa tu ndiyo
yaliyofungua nafsi zetu,
kama alivyosema muombolezi mmoja katika
mazishi ya karibuni ya
P. W. Botha kuwaambia
Waafrika Kusini: Bury the
history, before the history
buries you, yaani izikeni historia kabla historia
haijawazikeni nyinyi.

Toleo la 11

06

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

Makada wa CCM wanaimba nyimbo mbaya

Mwakilishi Vuai Shamsi Nahodha [Kushoto] na Muheshimiwa Salmin Awadh Salimin wakiwabadilishana mawazi
li ya Mapinduzi Zanzibar iitishe Kura ya
Maoni kuwauliza wananchi kama wangali
wanairidhia Serikali ya Umoja wa Kitaifa
(SUK), ni wazi kuwa amedhamiria ubaya.

Na
Jabir Idriss Jabir

a Salmin Awadh Salmin kuibua rai


yenye sura ya kiroja, si bure, bali
ana lake jambo. Kwamba atawasilisha hoja binafsi kwenye Baraza la
Wawakilishi kutaka kushawishi wajumbe
kuridhia utashi wake wa kuitaka Serika-

07

Toleo la 11

Amedhamiria ubaya kwa Zanzibar na


kwa watu wake walioko ndani ya nchi
yao ambao wanachokipata hukitumia pia
kwa kusaidia watu wa familia zao walioko Afrika ya Mashariki. Sehemu kubwa ya
wananchi hao wanahitaji amani, utulivu,
umoja na mshikamano, mambo yanayoenziwa na siasa za maridhiano zilizojengewa msingi mwaka 2009.
Salmin ana akili timamu na anajua vizuri
maana ya kile anachokipigania katika rai
yake hiyo. Anajua fika kuwa kwa asli ya

ilivyopatikana, siyo tu SUK


ni kitu adhimu kwa nchi,
bali pia kinapaswa kuenziwa na kulindwa kama
mboni ya jicho.
Huyu ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi anayewakilisha
wananchi
wa jimbo la Magomeni,
mjini Unguja, akiwa pia
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Baraza inayosimamia sekta ya Uchumi na Fedha. Anashikilia
pia wadhifa wa Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya

Chama cha
(CC-CCM).

Mapinduzi

Kiongozi wa hadhi hii


hata siku moja haiwezekani akatoa rai bila ya
kuwa ameitafakari kwa
kina. Siamini pia kwamba
anapigania jambo analoliwaza peke yake. Hata
kidogo.
Kwa rai yake, atakuwa anawakilisha makada kadhaa wa chama chao wenye
mawazo yanayofanana,
kushikana na kushikamana. Hawa wana ajenda

iliyojificha lakini ambayo


inaonekana kuwa ni balaa
kwa nchi na watu wake.
Niliposikia kupitia mkutano wa hadhara uliofanywa
na Umoja wa Vijana wa
CCM wiki iliyopita kwamba bado Salmin Awadh
anayo nia ya kuwasilisha hoja binafsi barazani,
nimezidi kuamini kuwa
hawa makada wa CCM
wamedhamiria kweli kuitia nchi katika mtihani kwa
kuichezea amani iliyostawi kutokana na siasa za
maridhiano.

Toleo la 11

08

Zanzibar Daima

Salmin Awadh anasema


yumo kwenye maandalizi
ya mwisho mwisho kuikamilisha hoja yake kabla ya kuifikisha mezani
kwa Spika Pandu Ameir
Kificho ambaye akikuta
imekidhi vigezo ataiwasilisha mbele ya Kamati ya
Uongozi ya Baraza kwa
majadiliano.
Kamati ya Uongozi ikiridhika kuwa hoja hiyo inaweza
kuwasilishwa, ataruhusu
iwasilishwe barazani. Itakapowasilishwa na iwapo muwasilishaji ataungwa mkono na tayari
wawakilishi kutoka CCM
walishaahidi kuwa wataiunga mkono itajadiliwa
kwa nguvu na kupita.
Ninavyojua siku zote,
Baraza hupokea kwa
mikono mingi hoja binafsi inayolenga kuongeza
uimara wa taifa na siyo
kuudhoofisha umoja na
mshikamano wa wananchi na taifa lao. Sasa je, hii
hoja ya makada wa CCM
inayotaka kuhoji serika-

09

Toleo la 11

Zanzibar Daima
li ya umoja iliyokuja kwa
shida sana, inawakilisha
maoni ya walio wengi au
ni kitu cha kutaka kufurahisha watu wachache
wenye malengo ya kifisadi?
Kwa jicho langu na wengi
wanaofuatilia mwenendo wa Salmin Awadh na
wenzake katika miezi ya
hivi karibuni, siioni nia njema ya makada hawa ambao nawaita wahafidhina. Ni ujinga mtu kuamini
kuwa hawa wanadhamiria
kuimarisha umoja na kuzidi kutandika misingi ya
maridhiano kisiasa.
Hebu turudishe nyuma
kidogo mti wa saa. Salmin
Awadh ambaye kwa kuwa
kwake muwakilishi pia
ni Mjumbe wa Bunge
Maalum la Katiba, ndiye
aliyeibua ushindani wa kitoto dhidi ya Spika Kificho
akimshutumu
kuandaa
waraka unaoweka bayana msimamo wa Baraza
la Wawakilishi kuhusu Rasimu ya Katiba mpya.

Alimsakama Kificho akisema waraka aliuandaa


yeye na wenzake bila ya
kushirikisha utaratibu wa
kikanuni wa kutoa waraka
namna ile. Amesema hivihivi kuwa yeye hakushiriki na kwamba laiti ange,
asingeupitisha
waraka
huo.
Akasema yeye na wenzake katika CCM hawawezi
kuwa sehemu ya waraka
huo kwa sababu unapigania mabadiliko ya mfumo
wa sasa wa Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar kutoka mfumo uliopo
wa Muungano wa Serikali
mbili. Waraka unapigania
mfumo wa serikali tatu na
kuipatia Zanzibar mamlaka kamili.
Salmin Awadh akasema
kwa kuwa anajua sera ya
CCM ni ya kutetea mfumo wa serikali mbili katika mfumo ulioongezewa vionjo, asingethubutu
kushiriki kupitisha waraka
unaokuja na mabadiliko
ambayo ni kinyume na
maslahi ya chama chake.

Alipoamua
kushindana
na Spika Kificho, Salmin
Awadh alikuwa anajua pasipo shaka yoyote kuwa
yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Baraza inayohusika na
Uchumi na Fedha, alikuwa
katika kikao cha kamati ya
uongozi kilichoidhinisha
msimamo uliomo kwenye
waraka huo.
Alikuwa ndani ya kikao
kuandaa msimamo. Alikuwa katika timu ya kamati
ya uongozi iliyoongozwa
na Spika Kificho kwenda
mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba kuwasilisha
msimamo huo kama ndio
maoni ya baraza kuhusu kupatikana kwa katiba
mpya.
Na kumbukumbu za Baraza zimethibitisha ukweli huo kwamba Salmin
Awadh alikuwa mmoja wa
wajumbe waliofuatana na
Spika kuongoza msafara wa kwenda kuwasilisha waraka kwa Tume ya

Warioba.
Anajua pia kwamba yale
maoni yaliyomo kwenye
waraka, ndiyo yaleyale
waliyoyatoa wawakilishi
wakati wa semina waliyoandaliwa kujadili mustakbali wa Zanzibar katika ujio wa katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano.
Alichokifanya
Salmin
Awadh ni kufikiria zaidi
maslahi ya chama chake
kuliko maslahi mapana ya
Wazanzibari na nchi yao. Ni
huyuhuyu aliyeanza kupiga jaramba akisema Zanzibar haitaweza kuchangia
gharama za Muungano na
hivyo haistahili kutafuta
mamlaka kamili.
Salmin Awadh akijinasibu
kufahamu vyema siri ya
hali ya kiuchumi ya Zanzibar, anasema ina uchumi mdogo usiotosha kuiwezesha kujitegemea na
kwa hivyo itahatarisha
faida kubwa inayopata kiuchumi kwa kushirikiana
na Serikali ya Muungano.

wa ni kosa na hasara kubwa


Zanzibar kutaka mfumo wa
Muungano wa Serikali Tatu
kwani utaisukuma katika
kulazimika kuchangia kikamilifu gharama za kuendesha Serikali ya Muungano.
Salmin ameyasema yote
haya huku akishuhudiwa
na Shamsi Vuai Nahodha,
Waziri Kiongozi kwa miaka
kumi wa Zanzibar. Picha iliyojengeka ni kuwa wanasiasa hawa wanaunda kundi mojawapo ya makada wa
CCM wanaotamani urais
na hayo kuwa ni maandalizi ya kujenga mazingira ya
kuja kuchukua fomu kutaka ridhaa ya chama chao
utakapofika uchaguzi mkuu
wa 2015.

Hakika makada wa CCM


wanatafuta urais kwa
gharama ya kuua umoja.
Na kwa hali hiyo, wakipewa
nafasi
ya
kutekeleza
kile
wanachokiandaa,
wataipeleka
Zanzibar
upande siwo. Hiyo ndiyo
hofu yangu kubwa. Makada
wa CCM wanaimba nyimbo
Akasema kwamba itaku- mbaya.

Toleo la 11

10

Zanzibar Daima

Zanzibar, nchi ya kitu kidogo

Zanzibar Daima

Barabara ya Wete-Konde ikiwa imeendelea kujengwa kwa zaidi ya mwaka wa tano sasa,
huku pakiwa hapana dalili ya kumalizika kwa karibu. Matokeo yake wananchi wanaoishi
kando ya barabara hiyo na watumiaji wake wanaambulia kuwa wahanga wa vumbi na hivyo
afya zao kuwa hatarini

Kutoka kwa
Mwandishi Wetu

IJUI kama viongozi wakuu wa


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wasaidizi wao wanajua kuwa rushwa imetapakaa kwenye sekta ya utumishi wa
umma.
Wala sijui kama wanajua kuwa
ukweli huo ndio hasa ulioisuku-

11

Toleo la 11

ma serikali kuondoa uzito na kutunga sheria


ya kupambana narushwa ikiwemo kuanzisha
mamlaka mahsusi kwa jukumu hilo.
Basi kama hawajui, huo ndio ukweli na ukweli
mtupu. Katika utumishi wa umma kuna rushwa
na athari zake zinaonekana wazi.
Wananchi wanalalamika hawapati huduma

hii na ile; wanalalamika


kwamba wanakwamishwa na ofisa huyu na yule;
wanalalamika kunyimwa
haki zao mpaka watoe kitu
kidogo (KK).
Hivi karibuni, waziri anayehusika na utumishi wa
umma na utawala bora,
Haji Omar Kheri, aliliambia Baraza la Wawakilishi
kuwa mipango inakamilishwa ya kuanzisha mam-

laka ya kupambana na
rushwa.
Malalamiko ya wananchi sasa yamekuwa yakibebwa kwa ukakamavu
mkubwa na wajumbe wa
Baraza hilo chombo
mahsusi cha Zanzibar kwa
ajili ya kutunga sheria na
kuisimamia Serikali.
Wajumbe kila wanapoipata nafasi wakati wa

mijadala, wanalalamika
kwa kueleza malalamiko
ya wananchi. Wanataja
na mifano ya malalamiko
hayo; wanataja shida wanazopata wananchi katika
kupata huduma.
Kuna malalamiko ya maofisa wakubwa, wa kati
na wadogo, kujiingiza
kwenye mienendo ya kufuja mali ya umma, fedha
na vifaa.
Toleo la 11

12

Zanzibar Daima

Ufujaji unafanywa kwa


njia mbalimbali. Utakuta
ofisa wa wizara au taasisi
ya serikali anatajwa kwa
kutumia vibaya gari ya
serikali. Labda anaendesha gari aliyopewa kiofisi mpaka usiku, ambao
si muda wa kazi, na hana
kibali.
Au anatumia gari ya ofisi
kwa kazi zake binafsi, tena
pengine ni shughuli za biashara. Yawezekana anafanya hivyo kwa kutumia
mafuta
yaliyonunuliwa
kwa fedha za serikali.
Utasikia ofisa mwingine
anatajwa kushiriki kupanga, kutekeleza na kunufaika na mpango wa kuuza gari ya serikali kinyume
na taratibu.
Waweza kusikia ofisa ameidhinisha malipo ya gari
ya Sh. 150 milioni lakini
thamani halisi ya gari inayonunuliwa ni Sh. 100
milioni.
Wakati fulani ofisa mmoja
katika Idara ya Uvuvi aliidhinisha malipo ya Sh. 47
milioni ya gari iliyotumika

13

Toleo la 11

Zanzibar Daima

ambayo bei yake halisi ilikuwa ni Sh. 22 milioni. Kwa


ufupi, ofisa huyu alitumia
fedha nyingi kununua gari
kongwe, ununuzi usiotakiwa kisheria serikalini.
Utasikia jengo la serikali limekodishwa kwa
mwekezaji au mtu binafsi
tu pasina kufuatwa utaratibu wa manunuzi unaohitaji sheria ifuatwe na kila
anayetaka aombe rasmi.
Katika siku za mwanzo
mwanzo, Rais Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa
akizuru mikoani kukagua
shughuli za maendeleo,
alikutana na malalamiko
mengi ya migogoro ya ardhi.
Rais akasikika akisema
wale maofisa wa serikali
waliosababisha migogoro
hiyo, waishughulikie wao
wenyewe mpaka imalizike.
Huko nyuma, kuliwahi
kubainika kwamba maofisa wa Idara ya Ardhi na
Usajili, walijigawia viwanja viwili mpaka vitatu kila

mmoja vya kujenga nyumba ambavyo vilivyokusudiwa kugaiwa kwa wananchi wenye shida.
Zipo tuhuma kwamba
ofisa mmoja katika Idara
ya Ujenzi na Utengenezaji Barabara (UUB) iliyo
chini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
ameigeuza mitambo ya
ujenzi ambayo ni ya serikali, kuwa ni mali yake na
anaikodisha kwa wajenzi
(wakandarasi) wa barabara.
Bado wananchi hawajasahau namna mawaziri kadhaa wa serikali iliyopita
na waliopo walivyohusika kukodisha majengo ya
serikali kinyume cha sheria.
Wapo maofisa wa serikali
wanatuhumiwa kutumia
madaraka vibaya. Pengine
ni kwa kufukuza watumishi wenzao bila ya kuzingatia kanuni za utumishi,
ikiwemo kumpa mtumishi
mtuhumiwa nafasi ya kujitetea kabla ya kumuadhibu.

Wapo viongozi serikalini


wamegawa zabuni kwa
njia ya upendeleo baada
ya kupata malipo haramu
kwa waliopewa zabuni
husika.
Bali wapo watendaji waliotumika kuvuruga uchaguzi na hivyo kusababisha
wagombea walioshindwa
kutangazwa washindi.
Tena, katika mwenendo
kama huo, matokeo ya
uvurugaji huo yamesababisha fadhaa kubwa katika
nchi ikiwemo machafuko
na vifo vya raia waliokuwa
wakipinga uvurugaji.
Kuna utamaduni unaokua
Zanzibar wa viongozi wa
serikali kudharau amri za
mahakama na hivyo kusababisha wale waliopata manufaa kutokana na
amri hizo kukosa haki zao.
Mfano mzuri wa uovu
huu, ni uamuzi wa kesi
ya uvamizi wa shamba
la mzee Abdalla Shariff wa Shakani, Wilaya ya
Magharibi, Unguja, ambaye pamoja na kushinda
kesi mwaka 1993, ute-

kelezaji wa hukumu haujafanyika. Mpaka anafariki dunia 2011, haki yake


hakuipata.
Mara
kadhaa
polisi
wametafuta visingizio vya
kutotekeleza hukumu hiyo
huku mazingira yakionesha wazi kuwa wamepata
maelekezo ya wakubwa
serikalini.
Hukumu ya kesi hiyo ya
madai imewakumba viongozi mbalimbali waandamizi serikalini na wafanyabiashara
wenye
uswahiba na viongozi
wakuu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Imekuwa ni mtindo kwa
miaka mingi sasa Zanzibar, maofisa wa serikali
kuruhusu wafanyabiashara kuingiza nchini vyakula
vibovu na kuuzwa.
Wakati fulani, mfanyabiashara mmoja anayeagiza mchele, sukari na
unga wa ngano, alivunja
kufuli za ghala ambamo
mchele mbovu ulifungiwa
na serikali na kufanikiwa

kuutorosha nje ya kisiwa


cha Unguja ambako uliuzwa.
Inasemekana baada ya
kuzungushwa,
uliuzwa
kisiwani Pemba ambako sasa kuna wagonjwa
wengi wa saratani (kansa) mpaka kuwashangaza
madaktari wa Hospitali
Kuu ya Kansa nchini
Ocean Road Hospital.
Madaktari wanajiuliza inakuaje wagonjwa wengi wa saratani wanaofika
Ocean Road Cancer Centre kutoka Zanzibar, idadi
kubwa ya hata asilimia 80
wanatoka kisiwani Pemba.
Wenzetu hawa wamekuwa wakilazimishwa kutumia mchele huo huo wa
kila siku ambao haufikii
kiwango kinachokubalika
kiafya kwa sababu hawana njia nyingine ya kubadilisha. Unapokuwa mtu wa
kipato kidogo, unakula kile
kilicho mbele yako huna
uchaguzi.

Toleo la 11

14

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

Mguu mbele mguu nyuma, lazima


Katiba Mpya ipatikane
siasa zaTanzania. Kuna yaliyofurahisha, na yaliyokirihisha.

Nilivutiwa sana namchakato


mzima huu tanguna baada ya
Rais Jakaya Kikwete kukabidhiwa Rasimu ya Pili ya Tume ya
kukusanya maoni kuhusu Katiba
mpya ya Jaji Joseph Warioba na
baadaye Rais kuwateuwa wajumbe 201 kujiunga nawabunge
wa Bunge la Muungano na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar kuundaBunge hilo
Maalum.

Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na Mbunge wa Singida Mheshimiwa
Tundu Lisuu, wakiwa kwenye viwanja vya Gombani Pemba

uyasimulia yaliyojirikatika mijadala ya


Bunge Maalum la
Katiba, ambalo kwa
sasa limeahirishwa kupita
Bunge la Bajeti, kutakuwa ni
kujirudia, kwani yalishuhudiwa, yalisikika na kuzungumzwa nchi nzima na nje ya mipaka yake kwa wanaofuatilia

15

Toleo la 11

Na
Mohammed Abdurahman

hotuba iliyotarajiwa kuwa ya


kihistoria. Mimi nikitegemea
ingekuwasawa na ilewakati alipowahutubia viongozi wa vyama
vya kisiasa siku chache kabla ya
kutangazwa majina ya wajumbe
wa bunge maalum la katiba.

Akikamilisha hotuba ileRais Kikwete alisema alichukuwa akitoa


ni rai tuhana na maelekezo wala
majibu na jibu wanalo wao, yeye
nasubiri majibu kama wanavyo
majibu Watanzania wote. Ilikuwa
hotuba ya matumaini.

Hatua hizo zote zilibua hisia za


matumaini kwa wananchi wa
pande zote mbili Tanganyika
na Zanzibar kwamba hatimaye
sasa kuna njia yakuzitatua zile
zinazotajwa kuwa kero za muungano, si kwa jengine zaidi ya
kuuimarisha na kuupa mtazamo mpya kulingana na wakati
na mabadiliko, miaka 50 tangu
kuundwa kwake.

Lakini hotuba yaRais Kikwete


bungeni bila yakutafuna manenokinyume ilizusha mgawanyiko
wa fikra na mitazamo,kuanzia
bungeni kwenyewe kati ya wajumbe wa bunge hilo maalum
la katiba kutoka Chama tawala
cha Mapinduzi CCM na wale wa
vyama vya upinzaniisipokuwa tu
TLP cha Augostino Mrema na
hata ndani ya jamii ya Watanzania.

Kilichotarajiwa sicho kilichotokea

Wengi walitarajia ingekuwa fupi


na yenye wasia-maneno yenye

Watanzania waliposikia Rais


Kikwete atalifungua rasmi
BungeMaalumla Katiba tayari
kuanza kazi, macho na masikio
ya watanzania yakaelekezwa
bungeni mjini Dodoma, kwa

Toleo la 11

16

Zanzibar

Zanzibar Daima

Pro. Ibrahim Lipumba

Moja ilimshinda
Nyerere, sambe
hawa viherehere.

yaliwashangaza wengi.

kutilia mkazo
umuhimu wa kupata
katiba itakayokidhi mahitaji ya wananchi kama walivyojielezawakati wa Tume ilipokusanya maoni
yao na wajumbe kuweka mbele
masilahi ya pande zote mbili za
muungano na kuwatakia kila la
kheri na kuwakumbusha wajumbe kwamba hatima ya Tanzania
imo mikononi mwao. Kweli mara
nyengine lile mtuulifikirio silo
liwalona hali kama hiyo ni sehemu ya utaratibu wa maisha ya
binaadamu.
Yaliozungumzwa naRais Kikwete
katika hotuba yake mbali na kujadiliwa kwa mapana na marefu.
Kukiwa na tafauti ya mitazamomiongoni mwa Watanzania
bara na visiwani kwa jumlakweli

17

Toleo la 11

Kwa mfano kitisho cha


Jeshi kutwaa madaraka
pindi mfumo wa serikali tatu
ukiamuliwanaserikali moja kushindwa kuwalipa wanajeshi mishahara,
kiliwaweka raia vinywa wazi.
Wakati ule nilipokuwa nikitafakarinilikutana
na swalila mchangiaji katika moja wapo ya
mitandao ya kiraia aliyeuliza Kwani hilo likijiri
litakuwa la ajabu? MbonaRais mwenyeweni
Mwanajeshi, Katibu mkuu wa sasana aliyemtanguliawa chama chake tawala CCM, wote ni
wanajeshi na Tanzania inajivunia amani?
Ya hotuba sasa yamegeuka yaliopita, kazi ni
kuganga yajayo. Maji yakimwagika hayazoleki,
jawabu ni kuteka mengine.
Wakuwashangaa ni Wawakilishi wa Zanzibar
Mbali na ya hotuba ya Kikwete, mshtuko
mkubwa kwa Wazanzibariulikuwa ni msimamo wa wawakilishi wa CCM, wakiwemo viongoziwaandamizi na wengine mpaka sasa ni

mawaziri serikalini, ambao juzi na jana walisikika


wakipaza sauti kudaihaki
ya Zanzibar katika Muungano.
Baadhi yao wakielezea
kile walichokiiitani kudhalilishwa wanapokuwa
sehemu ya ujumbe wa
Tanzania katika ziara za
kiserikali nchi za nje, lakini
kiroja cha mambo walipovuka bahari tu kuingia
mrima wakabadilika.
Wawakilishi hawa hawajajidhalilishawao
tu baliwaliowachagua
kwa maanaya kwamba
wamegeuka vinyonga,
wenye kauli mbili.
sidhani kama kungekuwa
na tatizo pindi msimamo
wao wa kupinga serikali
tatuna kushikilia serikali
mbili ungekuwa wa kudumu, kwa sababu ni haki
yao katika demokrasia.

Lakini kilichojitokeza ni
kwamba wakatiwengine
wanaamini siasa ni ukweli
kwa maanakile wanakisimamia kwa imani na
ujasiri, wawakilishi hao
wamedhihirisha kwamba
tafsiri sahihi kwao siasa
ni uwongo.
Kuna ambao hawakuchangiamijadala
katika bunge maalum la
Katiba hadi lilipoahirishwa, huenda kwa kuzingatia ule usemi bora kukaa
kimya kuliko kujiumbua.
Hawa pia sidhani kama
wananusurika au wanasafishika mbele ya waliowachaguwa, kwa sababu
kukaa kimya si suluhisho
bali ni undumila kuwili.
Siajabu, kwa hivyo, wanapoambiwa kuwawakiwa Zanzibar wanasema
mengine lakini kwenye
jukwaala kuzungum-

zawazi, kinaga ubaga


kwa madhumuni yakupata suluhisho lamadukuduku yao, wana lugha
nyengine. Masilahi ya
binafsi yametawaliwa na
hofu. Hawa niwale walioitwa katikamsamiati
mpya kuwa ni Wasaka
tonge, walinda matumbo
ili unga usimwagike.
Katika hali kama hii, matatizo au keroza muungano haziwezi kupatiwa
ufumbuzi hata siku moja.
Ufumbuzi unataka nia na
ujasiri kwa kuweka mbele
masilahi yataifa ambalo ni umma. Lakini hayo
hayawezi kupatikana bila
yakuzingatia maoni yao
na ndiyo maana kuna haja
ya rasimuiliyowasilishwa na Tume ya Warioba
kuwa msingi wa mjadala
wa kuandika Katiba mpya.

Ndivyo nionavyo!

Toleo la 11

18

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)


na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Maalim Seif Sharif Hamad.

Demokrasia ina uhusiano gani na ukomo wa uongozi


na ugombeaji?

oja kati ya lawama kubwa zinazoelekezwa kwa


upinzani katika Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ni kwa viongozi wake
wakuu kuendelea kugombea nafasi zao
kwa muda mrefu. Wakosoaji wao wa-

19 Toleo la 11

nawaambia kuwa huu si muonekano wa


demokrasia bali ni uimla unaojificha ndani
ya upinzani.

Na
Foum Kimara

Kabla ya kuendelea mbali, niweke wazi


kwamba mimi ni muumini wa demokrasia
ya uwazi na ukomo, lakini hili halina maana na wala si kweli kwamba ukomo ndio
demokrasia na kinyume chake ni uimla
ama usultani kama wengine walivyoupagaza jina. Nitalifafanua hili kwa ushahidi.
Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja

kumekuwa na matukio yanayohusiana


na dhana hii ya ukomo na demokrasia.
Kwa mfano, Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kiliwatimua Dk.
Kitila Mkumbo na kumbebesha lawama
kali mbunge wake wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Nyuma ya hapo, Chama
cha Wananchi (CUF) nacho kikamtimua
mbunge wake wa Wawi, Hamad Rashid
Mohamed, na wenzake.
Hao wote waliofukuzwa CUF na CHADEToleo la 11

20

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

MA wanasemekana kuwa waumini wa


demokrasia na wanaopinga hali ya kutokuwapo ukomo wa uongozi kwenye vyama vyao. Kinyume chake, Katibu Mkuu wa
CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alitangaza na kuchukuwa fomu ya kugombea tena
wadhifa huo, lakini Makamu Mwenyekiti
Machano Khamis Ali akatangaza kutogombea tena wadhifa huo. Kwangu wote
hao wametekeleza demokrasia kwa njia
zao wenyewe, lakini kwa dhamira moja
kuu, nayo ni kuwa demokrasia ni pana
na inaweza kutekelezwa kutokana na
mazingira ya sehemu husika.
Demokrasia ni kufuata taratibu za uchaguzi na katiba ya taasisi husika. Misingi
mikubwa ni uwazi katika ugombeaji, kuepuka upendeleo na kuhakikisha haki, usawa na sheria zinafuatwa. Kama ilivyo kwa
Marekani ambayo inafuata ukomo wa
mihula miwili, Uingereza haina kipengele cha ukomo katika uongozi. Zote ni nchi
zinazotajwa kuwa za kidemokrasia kwa
vile misingi mikuu ni chaguzi halali, haki
na ufuatiliaji wa sheria. Njia ya kufuatwa katika kuwepo kwa kikomo au kutoa
ruhusa bila ya kikomo kwa wagombeaji ni
suala la kiufundi wala haitafsiriki kwam-

21

ba mfumo mmoja ni wa kidemokrasia


zaidi kuliko mwengine.

Tony Blair naye ndiyo hivyo hivyo. Alikuwa waziri mkuu wa Uingereza na kiongozi wa chama cha Labour tokea mwaka
1994 mpaka 2005 alipolazimika kuondoka madarakani kwa kukosa umaarufu kutokana na vita ya Iraq, ambavyo kama si
hivyo, basi angeliweza kugombania hata
kwa awamu ya nne.

Toleo la 11

Marehemu Margret Thatcher, aliyekuwa


waziri mkuu wa Uingereza tangu 1979
hadi 1990, aliingia katika bunge tokea
1959 na uongozi wa Chama cha Conservatives tokea 1975 mpaka pale wanachama walipomlazimisha kujiuzulu mwaka 1990. Alishindana katika uongozi kwa
kipindi chote. Waliompinga hawakukimbilia kuweka ukomo wa muhula, maana
haikuwa kinyume cha sheria wala utaratibu wao.

Nchini Marekani hivi sasa baadhi ya wajumbe wa chama cha Democrat cha Rais
Barack Obama wameanza kujadili ukomo wa mihula miwili, wakiwa na upinzani
mkubwa kutoka kwa Republican wana-

oona mazingira na utamaduni wa nchi


yao zimetosheleza kuendesha demokrasia kwa ukomo wa miaka miwili.
Ireland ya Kaskazini ni mfano mzuri wa
demokrasia inayofanana na ya Zanzibar
kutokana na muungano wake na H imaya
ya Kifalme ya Uingereza na chimbuko la
Jamhuri ya Ireland. Vyama vikuu ni viwili,
Democratic Unionist Party (DUP) na Sinn
Fein ambavyo vyote vina nguvu za kihistoria kama ilivyo kwa Zanzibar chini ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) na CUF.
Kwa miaka zaidi ya 40, DUP iliongozwa
na Mchungaji Ian Pasley, kwa kupitia chaguzi zao za ndani na kura za imani juu
yake kwa wanachama. Hii haikuwahi
kutafsiriwa kama si demokrasia, kutokana na mazingira ya siasa za ushindani
wa namna yake kuwa tafauti na mfano
wa Marekani. Pasley aliendelea kuwa
mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya
mpaka alipostaafu mwaka 2008 kutokana na uzee.
Nao Gerry Adam na Martin Mcguiness wa
Sinn Fein wameendela kuwa viongozi had
hii leo, wakihusishwa na kelele za Ireland
Resistance Army (IRA), lakini mwishowe -

kama ilivyo Zanzibar na ukosefu wa wingi kwa pande mbili, Mcguiness amekuwa
ni Naibu wa Kwanza wa Waziri Kiongozi
huku DUP ikitoa Waziri Kiongozi, mfano
wa CCM kutoa Rais wa Zanzibar na CUF
kutoa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Hii ni demokrasia wala haijawahi kupingwa kwa sababu ya ukomo. Ndivyo historia na utamaduni wa kisiasa wa nchi yao,
kama ilivyo pia kwa Zanzibar. Maana yake
ni kuwa nchi zenye ushindani mkubwa wa
kisiasa na kiitikadi, wananchi huwekeza
kwenye umaarufu wa viongozi wao. Huo
ndio mtaji wa kisiasa, maana siasa ni mipango ya kuendesha au kuchukua uongozi wa nchi, ambayo lazima iekezwe na
uwekezaji wake ni huu.
Hata Mwalimu Julius Nyerere aliendelea
kuwa rais kwa zaidi ya miaka 20, akiwa
Mwenyekiti wa CCM kwa miaka na dahari na hata alipostaafu aliendelea kuwa
na maamuzi makubwa mbele ya chama
chake tena kwa uwazi huku hata katiba
ya chama ikiwa haikumpa idhini yoyote.
Inashangaza kwamba ni yeye aliyeweka
ukomo wa rais wa mihula miwili hali kwa
upande wake hakuliona hilo.

Toleo la 11

22

Zanzibar Daima

Zanzibar Daima

Timu ya Zanzibat baada ya kuchukua kombe la Mashindano ya Gossage mwanzoni mwa miaka ya 1960

Na

Zanzibar, visiwa
vya michezo

Mwanamichezo Wetu

ilinufaika na simulizi zababu


yangu, Juma Mzee Jimba,tulipokuwa tukitembea nyumbani kwake Kwa Karagosi
(Mwembetanga), tukitokea Dar es Salaam tulikokuwa tukiishi.Akinielezea
historia ya magwiji waKriketi, gofu,
kandanda (mwenyewe akiita Futboli)
tangu miaka ya 1940 hadi 1960 waki-

23

Toleo la 11

wemo kinaMarehemu Ahmed Iddi Mjasiri, Shaaban


Antar, Bwan Smati (Smart), Mohamed Aoud Mfaransa, Kassim bin Mussa, Hijja Saleh Abdulmajham na
wengineo. Orodha ni ndefu na kila mmoja alikuwa na
fani na kipaji chake.
Abdulmajham nimmoja wa wachezaji waliokuwa na
kipaji cha hali ya juu na aliiwakilisha Zanzibar katika
timu za taifa za michezo mitatu: Kandanda, Hoki na

Kriketi. Mchezaji mwengine tunajuwa tutafika fainali!


ni Marehemu Zaghaloul Ajmi.
Katika ngazi ya vilabu vikubMnamo miakahiyo ya enzi wa wakati huo, mpira ulikuwa
ya ukoloni, Zanzibariliku- na msisimko wa aina yake.
wapekee kwenye kanda ya Ushindani mkubwaukiwa
Afrika ya Masharikiiliyokuwa kati ya Vikokotoni na Malindi
ikijulikana kwa ustadikatika na Miembeni na Kikwajuni.
fanitafauti za michezo na Vyengine ni Mwembeladu
kuchuana natimu za uge- na Kisimajongoo iliyokuja
nini zilizokuwa zikifika kwa kufa baadaye.
matembezi, iwe wanamaji wa
Uingereza, wacheza Kriket Kwa ujumlawake, michezo
kutoka Bara Hindi na kadha- ikitiliwa maananimashuleni
lika. Huo ulikuwa ni wakati ikiwemo ile ya riadha. Urafiambapo michezo ilipewa ki- ki wa vilabu vya michezo
paumbele na ilikuwa sehemu Tanganyika naZanzibar uliya mtalaa mashuleni na jamii changia zaidi katika kuipa
kwa jumla.
umuhimu michezo na hasa
baada ya Muungano.Safari
Mapema miaka ya 1960,mi- za kupeana zamu za wakachezo - na hasa kabumbu ti wa Sikukuu za Pasaka
- ilishamiri zaidi Afrika ya zilikuwa na shauku ya kiMashariki nzima na hasa pekee - Miembeni Sports
chini ya yale mashindano Club walikuwa na udugu na
maarufu ya kila mwakaku- Young Africans, Kikwajuni
wania kombe lililojulikana na Sunderland (sasa Simkama Gossage. Mashinda- ba), Vikokotoni na Malindi na
no hayo yalizihusisha nchi Cosmopolitan.
nne za Afrika ya Mashariki - Hizo ni zama ambazo timu
Kenya, Uganda, Tanganyika za Tanganyika zikiazima
na Zanzibar.
wachezajikutokaUnguja
Wakati Uganda ikivuma kwa zinapokabiliana na mashakina Ouma na Masajagge; indano. Nakumbuka YanKenya kwa akina Kadenge gaikimkodisanaHijja Saleh
na Moses Wabwai, Sungu- aliyekuwa wingi wa kulia
ra na Ali Kajo; Tanganyika naCosmopolitankuwategekwa akina Mbwana Abushi- mea Abdulmajham kucheri, Hemed Seif, Kibunzi na za nafasi yoyote isipokuJohn Lymo; Zanzibar ilivu- wa mlinda mlango: kuanzia
ma kwa akina Abdulmajham, ulinzi, kiungo hadi mshambuMohamed Kassim na Mussa liaji na Mohamed Kassim kuBakari. Inasemekana kuwa toka Malindi katika nafasi ya
wakati mashindano hayo ya mshambuliaji wa kulia. Hayo
Gossage, daima Uganda iki- yaliendelea hata baadaye.
omba isiumane na Zanzibar,
kwani kilikuwa ni kikwazo Kwa mfano, mtoto wa marekwao. Waganda walikuwa na hemu Hijja Saleh, Saleh
usemi: Tukiifunga Zanzibar, Hijja,aliwahikujiunga na

Yanga miaka ya 1980 na


Cosmo ilikuwa na Joseph
Kazi, mchezaji maarufu wa
kiungokutoka KMKM na
Mansab Abubakar, mlinzi
wa kati kutoka Malindi. Wote
waliwahi kwa kipindi kirefu kuichezea timu ya taifa
ya Zanzibar. Abdul Mutiy
Ajmi alijiunga na Cosmopolitan. Mutiy alikuwa ni mlinda mlango wa aina yake na
wa kutegemewa hata katika
Timu ya Taifa ya Tanzania.
Miongoni mwa michuano inayokumbukwa akiwa langoni
ni ule wa Kombe la Afrika dhidi
ya Madagascar ambapo Tanzania iliyowajumuisha akina
Hemed Seif, Abdulmajham,
Mohamed Kassim, Mwana
Abushiri, Mustafa Choteka,
Kitwana Manara na Abdullah
Luo, ilishinda mabao 3-2.
Udugubaina ya vilabu vyamichezo Bara na Visiwaniulikuwepo pia katikafani
nyengine kama vilabu vya
Hoki, ambapo wenyeji wa
timu ya mchanganyiko ya
Hoki ya Zanzibar ilikuwa na
ushirikiano na Bantu ya Dar
es Salaam na pia vilabu vya
taarab ambapo kutoka Zanzibar ni pamoja na Akhwan
Swafa (Malindi) na Dar es
Salaam ni Egyptian Musical
Club, Zanzibar Extra na AlWatan.
Hayo ni ya wakati wa
kuelekea uhuru na Mapinduzi. Safari ijayo, tutaangalia
michezo visiwani Zanzibar
baada ya Mapinduzi.

Toleo la 11

24

You might also like