RAI - Zitto Kabwe: Bado Sijamuona Mtu Mwenye Sifa Za Urais

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 2014 Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 2014

16 17
Inaendelea uk. 21
NA GABRIEL MUSHI
Rai /Alhamisi
Oktoba 2-8, 2014
>>Ronaldo mtoto wa familia mas-
kini anayezidi kutikisa medani ya
soka
Kwenye mbio hizo, Ronaldo alimzidi Lionel Messi wa Barcelona.
Aidha tuzo hiyo ilimfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza
Mreno kuchukua baada ya Luis Figo mwaka 2001.
Adha ya
michango
na maisha
magumu ya
kujitakia
uk19
MAHOJIANO
Watanzania
hawajatambua
falsafa ya Sitta
uk20
Naibu waziri
hana mamlaka ya
kuamua
uk24
Hong Kong
kuivuruga
China?
uk28
uk31
NA GABRIEL MUSHI
Z
IITO Kabwe ni mmoja wa
wanasiasa vijana wenye majina
makubwa nchini kwa sasa,
amefanikiwa kupenya na nyota
yake kungaa kisiasa kutokana na
uwezo wake wa kuibua hoja nzito na
kuzisimamia.
Mara zote hoja zake alizowahi
kuziibua iwe ndani ya Bunge
ama kwenye majukwaa ya kisiasa
zimekuwa mwiba mkali kwa Serikali
ama makundi yaliyoelekezewa
makombora hayo.
Zitto amekuwa akiendesha siasa
za kimkakati endelevu ambazo mara
zote zimekuwa na tija kwake, chama
chake na nchi kwa ujumla.
Anabainisha kuwa amekuwa
muumini wa siasa safi zenye tija
kwa pande zote na ndio sababu ya
kupendezwa na siasa za aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir
Mohamed ambaye hufunga safari ya
kwenda kuonana naye kila ufikapo
mwezi Oktoba.
Anaamini Mahathir ni mwanasiasa
wa mrengo wake kwani mambo
anayokabiliana nayoyanamuelekeona
yale aliyokabiliana nayo mpambanaji
huyo wa Malaysia ambaye alishawahi
kufukuzwa kwenye chama chake
akiwa mbunge, lakini kutokana na
kukabiliana na changamoto za siasa
alifanikiwa kushika wadhifa wa
Waziri Mkuu.
Hata hivyo akiwa kwenye safari ya
kuelekea kwenye kilele cha mafanikio
kisiasa, alikumbana na ajali mbaya ya
kisasa ambaye imetajwa kumrudisha
nyuma kwa kiwango kikubwa, ingawa mara zote
amekuwa akiamini kwamba ajali hiyo ya kisiasa
imemkomaza zaidi.
Alijikuta akivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kutokana na kutwisha zigo la shutuma za usaliti,
aidha alinusurika kuvuliwa uanachama kutokana na
kukimbilia mahakamani.
Lakini pia ajali hiyo imekuwa ikitajwa kama
mtaji kwa wapinzani wake kisiasa kama pigo
kwake, ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya
ziara rasmi na zisizo rasmi kwenye jimbo lake na
mkoani Kigoma kwa ujumla ili kuimarisha mizizi ya
kupambana nae kwenye chaguzi zijazo.
Hali hiyo imelisukuma RAI kufanya mahojiano
maalumu na Zitto ili kueleza changamoto
anazokumbana nazo jimboni kwake pamoja na
masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wake
kisiasa pamoja na hali ya kisiasa nchini.
RAI: Kuna taarifa kuwa wapo baadhi
ya wapinzani wako kisiasa wanakwenda
jimboni kwako kwa lengo la kukita mizizi ili
kuhakikisha unapoteza mvuto kwa wapiga
kura wako, je unawazungumziaje?
ZITTO: Kwanza hakuna mtu ambaye anaweza
kuwavuruga watu wa Kigoma Kaskazini kuhusiana
na Zitto, sio Kigoma kaskazini tu hata Kigoma
yote, watu wa kule hawaambiwi maneno matupu,
wanaona utendaji wa kazi, katika kipindi ambacho
nimekuwa mbunge na heshima niliyowapa
kwa ujumla sina mashaka hata kidogo, mtu
yeyote ambaye anakwenda Kigoma kwa lengo la
kumshughulikia Zitto atashindwa.
Zitto Kabwe:
Bado Sijamuona mtu
mwenye sifa za urais
Sina hofu na yeyote, mimi ndiyo nembo ya Kigoma
Lakini pia ajali
hiyo imekuwa
ikitajwa kama
mtaji kwa
wapinzani wake
kisiasa kama
pigo kwake,
ambapo baadhi
yao wamekuwa
wakifanya ziara
rasmi na zisizo
rasmi kwenye
jimbo lake na
mkoani Kigoma
kwa ujumla
ili kuimarisha
mizizi ya
kupambana nae
kwenye chaguzi
zijazo.
Watu wanaweza
k u j i f u r a h i s h a
wakawachukulia wenzao
fomu za kugombea
nawapa changamoto
kwamba waende, waitishe
mkutano waone kama
wananchi watahudhuria.
Sina wasiwasi wowote jimbo
lipo sawa, wanachokifanya
sasa ni kutekeleza siasa za
kujifurahisha.
Wanafanya kitu cha
maudhi ili wajifurahishe,
mimi ndiye nembo ya
Kigoma.
RAI: Unazunguziaje
misukosuko uliyopitia
kisiasa?
ZITTO: Katika hali ya
kawaida kama nisingekuwa
imara ningeanguka,
naamini wengi walitegemea
ningeanguka, lakini niko
imara zaidi ya nilivyokuwa
awali.
Wanashangaa mimi
bado nafanya kazi zangu,
nina kazi nyingi za kufanya,
sijali nini wanachokifanya,
juhudi zozote wanazozifanya
kwa ajili ya kunishughulikia
katika jimbo langu au katika
mkoa wangu watashindwa,
naaimini nimeingia kwenye
mioyo ya watu wa Kigoma,
kwa sababu mimi ni alama
yao, hivyo wanajifurahisha.
Mimi kuna kazi nafanya,
siwezi kuhangaika na
watu wasiokuwa na kazi
za kufanya, wasiokuwa na
kazi ya kufanya wao ndiyo
wanadili na Zitto, mimi hiyo
siyo aina yangu ya siasa,
nafanya mambo mazito
kwenye siasa.
Kamati ya Bunge
imenipa kazi kubwa ya
kufanya, nalitumikia taifa, tayari
tumeshaliita Jeshi lije kueleza
matumizi na mapato yao, hili ni
jambo zito ambalo halijawahi
kufanyika, kama ilivyo kwa polisi
na Usalama wa Taifa.
RAI: Imekuwaje
umeamua kubadili muelekeo
wa majimbo, kutoka Kigoma
Kaskazini hadi kulipigia
mahesabu jimbo la Kigoma
Mjini?
ZITTO: Uamuzi wangu ni
kugombea urais, hiyo ndiyo
dhamira yangu kuu na mimi ndiye
mtu wa kwanza kutangaza wazi
kwamba nitagombea urais.
Kama vigezo vitaruhusu
nitagombea urais, nilishawaeleza
wapiga kura wangu kuwa
nitaongoza awamu mbili tu,
kwa sababu vitu ambavyo
nimeshindwa kuvifanya ndani
ya miaka 10 sitaweza kuvifanya
ndani ya miaka 30, kwa hiyo
nilichofanya ni kutoa nafasi kwa
mwingine aje aliongoze jimbo hilo
ili tuende mbele zaidi.
Kama sitapata nafasi ya
kugombea urais, nitahamishia
nguvu Kigoma Mjini, lengo langu
ni kusambaza maendeleo mkoani
Kigoma.
RAI: Utawania kwa tiketi
ya chama gani?
ZITTO: Kabla ya mwisho wa
mwaka huu wananchi watakuwa
wamejua chama nitakachojiunga
nacho.
Kwa sasa kuna kazi nazifanya,
lazima nizimalize, lakini pia
itategemea uamuzi wa kesi yangu
dhidi ya Chadema.
RAI: Kuna taarifa kuwa
unajiandaa kuhamia
ACT iwapo mustakabali
wako ndani ya Chadema
hautotengamaa?
ZITTO:Sijasema mahali popote
kwamba nakwenda ACT, siku zote
nasema nina kesi, nikimaliza
nitajua mwelekeo wangu wa
kisiasa ukoje, sasa hivi akili na
nguvu zangu nimezielekeza PAC,
natakiwa kutoa taarifa ya mwaka,
kusimamia uwajibika katika
nchi na kuhakikisha fedha za
wananchi zinatumika sawasawa.
Hilo ndilo jukumu kubwa
nililopewa kwa sasa na
nitahakikisha nalitimiza.
Wakati kuna watu ambao
wanaweweseka na Zitto mimi
nimeshapiga mstari, naangalia
mbele nafanya mambo mengine
siangalii kabisa nini kilitokea
huko nyuma, watu ambao
wanaweweseka na Zitto ndio
wanaongalia nyuma, vitendo
vinatamka zaidi kuliko maneno.
RAI: Uchunguzi wa
ripoti ya IPTL umefikia
wapi, je, Kamati yako
imeshakabidhiwa ripoti
hiyo?
ZITTO: Machi mwaka huu
nilimwagiza CAG afanye ukaguzi
maalum kuhusu sakata la
IPTL, amefanya, atanikabidhi
ripoti hiyo wiki ijayo (wiki hii),
tutaishughulikia kwenye Kamati
na kuiwasilisha kwenye vikao vya
Bunge la mwezi Novemba mwaka
huu.
Sasa hivi nimeshapokea
ripoti maalum ya jengo la wageni
maarufu kwenye uwanja wa ndege
Kimataifa wa Dar es Salaam.
Ujenzi wake umegharimu Sh.
bilioni 12, ambazo ni sawa dola
za Marekani milioni nane, kati ya
hizo dola milioni tano ni msaada
kutoka kwenye shirika moja la
China na dola milioni tatu zilitoka
Serikalini.
Niliagiza ukaguzi wa vyama
vya siasa kwenye upande wa
ruzuku, tunapokea taarifa hiyo na
tutamwita msajili wa vyama vya
siasa.
Kuna tatizo la mifuko ya
hifadhi ya jamii, tumemwita
Gavana wa Benki Kuu kwenye
Kamati. Na mjumbe wa SSRA
wote watakuja Oktoba 20 mwaka
huu, tunataka kumaliza matatizo
ya wafanyakazi, hivyo nina kazi
za kufanya siwezi kusumbuka na
siasa ndogondogo.
Kiujumla ripoti hizi zote
hususani ile ya IPTL inaweza
kuiangusha serikali.
RAI: Hivi karibuni
Profesa Abdalah Safari
ameteuliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti wa Chadema, pia
alizungumzia kutokuwapo
kwako ndani ya chama hicho
hakuna kilichoharibika, je
unamzungumziaje?
ZITTO: Nimesikitishwa sana
na maneno ya Profesa Safari
naomba aweke akiba ya maneno
yake, asiongee sana atakuja
kuyameza hayo amaneo baadaye,
yeye siyo wa kwanza kushika
nafasi hiyo aliyo nayo.
RAI: Lakini pia Profesa
Safari amesema iwapo
utakuwa tayari kuomba radhi
wao wako tayari kumaliza
tofauti, je utakuwa tayari
kwa hilo?
ZITTO: Nikiomba radhi
watanisamehe!! Mimi sina kosa
wao ndio wanapaswa kuniomba
radhi, sio mimi kuwaomba wao
radhi, sina kosa hata moja,
hakuna tuhuma yoyote ndani ya
Chadema ambayo mtu anaweza
kudhibitisha.
RAI: Chadema wapo
kwenye mkakati wa
kutekeleza maandamano
nchi nzima kwa lengo la
kupinga Bunge la Katiba
linaloendelea, je, unadhani
maandamano ndio njia
sahihi?
ZITTO: Nikizungumzia
suala hilo, nitaingilia uamuzi
ya Chadema, sitaki kuendeleza
ugomvi, huo ni uamuzi wa
Mkutano Mkuu, maswali ya
msingi ya kujiuliza ni kwamba
je, wanamiliki chama cha
wafanyakazi?
Ni kwanini waseme watakuwa
na migomo isiyokwisha nchi
nzima ile hali migomo ya namna
hiyo inatakiwa kutekelezwa na
vyama vya wafanyakazi? Hakuna
chama cha wafanyakazi kilichopo
ndani ya Chadema, kwa maana
hiyo si rahisi kwa suala hilo
kufanikiwa.
Lakini ndio uamuzi wao,
watu wengi walitarajia baada ya
Mkutano Mkuu chama kingetoka
na matangazo ya kisera kwa ajili
ya Uchaguzi Mkuu, badala yake
tunatangaziwa maandamano, je,
hizo ndio sera za chama katika
kuwasaidia wananchi?
Chama kilipaswa kuibuka na
mipango ya kuwaboreshea maisha
wananchi kwa kuzungumzia
masuala ya maji, afya na mambo
mengine ya maendeleo.
Kwangu kilichofanywa na
watu hawa ni upotevu wa nafasi,
duniani kote mikutano mikuu
ya vyama ndiyo mahala ambapo
chama kinajitanabaisha kwa sera
mbalimbali za mabadiliko kwenye
nchi.
Hata hivyo siwezi kujua
mkakati wao kwa sababu
sikuwapo kwenye mkutano huo
hivyo siwezi kuzungumza zaidi.
Lakini pia si jambo baya
kufanya maandamano kwa
sababu Watanzania wanataka
suluhisho la mambo ya Katiba.
Lakini pia ni vema tukajiuliza haja
ya maandamano inatoka wapi,
wanataka Bunge liahirishwe sasa,
kwa madai ya kuokoa fedha za
walipa kodi, lakini mbona hatuoni
wakifanya maandamano ya
kupambana na wezi wa fedha za
Escrow ambazo ni Sh. biloni 200.
Sijasikia watu wakitoa kauli za
kupinga wizi uliofanyika na Benki
Kuu ambao unakwenda kuingoa
serikali, sijasikia mambo kama
haya, wananchi wanataka kusikia
kuhusu mali zao na uwajibikaji.
Lakini si jambo baya pia
kupigania fedha za walipa kodi
hata kama ni ndogo kiujumla ni
za umma.
Kwa sababu maandamano
ni haki ya kila raia, ingawa sijui
kama yatatufanya tupate kile
ambacho tunataka kukipata.
Jambo la msingi ni
kuhakikisha wananchi wanapata
ZITTO:
Nimesikitishwa
sana na maneno
ya Profesa Safari
naomba aweke
akiba ya maneno
yake, asiongee
sana atakuja
kuyameza
hayo amaneo
baadaye, yeye
siyo wa kwanza
kushika nafasi
hiyo aliyo nayo.
Zitto Kabwe akiwa na viongozi wa Chadema

You might also like