Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 16

Kesi ya Sheikh

Ponda Moro yazidi


kupigwa danadana

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1157 SAFAR 1436, IJUMAA ,

DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uk. 3

Ijumaa yaswaliwa Mahakama Kuu


Jaji aahirisha kesi kupishwa Swala
Imam, Khatib wapatikana hapo hapo
Kesi ya ugaidi yarejeshwa tena Kisutu

OTHMAN Masoud Othman.

JAJI Fredrick Werema.

Othmani Masoud shujaa

Mtetezi wa Zanzibar, Muungano


Jaji Fredrick Werema mmh

JAPO alifukuzwa kazi, lakini machoni mwa


wananchi shujaa.
Historia imeshamuandika kuwa miongoni mwa
watu muhimu walioipigania Zanzibar na kutetea
muungano wa haki na usawa.
Mhe. Masoud ni shujaa kwa pande zote mbili za
muungano, Zanzibar na Tanganyika. (Soma Uk. 7)

Rais Kenyatta anajua nini zaidi


wasichojua Wakenya wenzake
Afuata nyayo za Goodluck Jonathan
Al Shabaab wanaoitesa Kenya ni nani?

WAISLAMU wakiswali swala ya Ijumaa nje ya Mahakama Kuu Jijini


Dar es Salaam kabla ya kesi inayowakabili watuhumiwa wa ugaidi
kuanza mwishoni mwa wiki.

RAIS Uhuru
Kenyatta wa
Kenya.

Tahariri/Habari

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

w a k a h e s h i m u h i z o ile ya kiimani, sio jawabu hii, hatakuwa mtu wa


tofauti na kuvumiliana, katika maisha ya watu kisasa au ataonekana
wa siasa kali. La, huko
bila shaka jamii itaishi wenye imani tofauti.
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
kwa amani na upendo,
Wakristo wawe huru ni kuchunga mipaka ya
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
h u k u k i l a m m o j a kusherehekea Krismasi, Dini yake.
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Kwa Wakristo nao
akichunga mipaka ya l a k i n i a s i o n e k a n e
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
wa
sherehekee huku
k u m u a s i M we n ye z i Muislamu asiyejumuika wakijua
kuwa sherehe sio
Mungu kwa mujibu ya katika sherehe hizo kulewa sana au kufanya
imani yake.
kwamba kakosea au uovu wa namna yoyote.
A i d h a t u t o e t u h a h e s h i m u D i n i ya Na maadhali inaelezwa
t a h a d h a r i k w a m b a wengine.
kuwa ni sherehe ya
Chuki, dharau au kashfa
N a M u i s l a m u kukumbuka kuzaliwa
kwasababu tu ya tofauti n a y e , a s i o n e k u w a Yesu, tunaimani kuwa
K I L A D e s e m b a ni siku za sherehe kubwa za kiimani, iwe ni katika asipojumuika katika itaandamana na yale
2 5 i n a t a m b u l i k a kwa Wakristo walio kusherehekea sikukuu P a s a k a , K i p a i m a r a mema aliyokuja nayo
u l i m w e n g u n i k o t e wengi na wana namna au kufanya ibada yeyote Au K r i s i m a s i k a m a Yesu mwana wa Maryam.
k w a m b a n i s i k u yao ya kusherehekea
ya Krismasi. Siku sikukuu hizi kwa mujibu
hii Wakristo wengi wa kanuni za imani zao.
huadhimisha kuwa ndio
Ta t i z o n i k w a
siku aliyozaliwa Yesu na Waislamu. Baadhi ya
hufuatiawa na Siku ya Wai s l amu kimakosa
zawadi maarufu kama hupokea sikukuu hizi
wa Kwanza yakijitokeza kwa kasi katika k w a
wa n a n c h i
Boxing day.
bila kuchunga mipaka ya MAKAMU
wa Rais wa Zanzibar, maeneo mbali mbali ya k u j i l e t e a m a e n d e l e o
S i k u z o t e h i z i imani yao.
Mhe. Maalim Seif Sharif Zanzibar na njia muafaka k wa m a s h i r i k i a n o n a
huambatana na sherehe
Wapo
a m b a o Hamad amesema matukio ya kuweza kukabiliana Mwakilishi pamoja na
na shamra shamra nyingi w a m e s h a t a w a n y a ya uhalifu yanayojitokeza nayo ni jamii wenyewe Mbunge wa jimbo hilo
na humalizikia kilele kadi za Krismasi na Z a n z i b a r y a t a w e z a kushiriki kikamilifu katika ni ya kupigiwa mfano na
kwa jamii
cha sherehe za kuingia kujumuika na Wakiristo kudhibitiwa
kuunga mkono dhana ya m a s u a l a ya u l i n z i n a kuwahimiza viongozi wa
mwaka mpya.
katika mijumuiko yao, ulinzi shirikishi na kuvipa usalama wao.
jimbo kuendeleza kasi
Akikabidhi vifaa kwa hiyo ili wazidi kupata
H a t a
h i v y o k w a m u n a s a b a w a mashirikiano vyombo vya
watendaji wa Ofisi ya maendeleo.
y a m e t o f a u t i a n a sikukuu hiyo. Wapo ulinzi na usalama.
Polisi Jamii eneo la Kinuni,
Maalim
Seif
amesema
madhehebu ya Kikristo waliokesha baa, kumbi
Naye Mwakilishi wa
hayo alipokuwa katika Makamu wa Kwanza wa
k u h u s u s i k u h a l i s i za starehe za maasi nk. ziara ya kutembelea jimbo Rais alisema wananchi jimbo la Magogoni, Mhe.
aliyozaliwa Yesu. Baadhi
K w a m u j i b u y a la Magogoni, Wilaya ya wakikataa uhalifu katika Abdilahi Jihad Hassan
ya wanahistoria wako mafunzo ya Kiislamu,
w a z i k w a m b a s i k u hata iwe sherehe ya
yenyewe haijulikani.
Kiislamu kama Eid, hii
Kwa mujibu wa Kanisa huwa siku ya furaha na
la Mashariki/ Eastern kumshukuru Mungu.
Church siku aliyozaliwa Haiwi siku ya kufanya
Yesu ni tarehe 6 Januari s a n a m a a s i . S a s a
inayowafikiana na tarehe inapokuwa ni sherehe ya
7 Januari ya kalenda ya itikadi ya dini nyingine,
kimiladi (Gregorian kosa linakuwa mara dufu
Calendar).
maana unasherehekea
Hivyo nchi nyingi kitu ambacho hakipo
za Ulaya Mashariki au katika mwongozo wa
zinazoshikamana na Dini yako.
Kanisa la Mashariki kama
Hawatakuwa radhi
vile, Ukraine, Serbia, juu yako Mayahudi wala
Macedonia, Jamhuri ya Manasara mpaka mfuate
Moldova, Ethiopia kwa mila zao, Sema, Hakika
Afrika na nyenginezo, uwongofu utokao kwa
huadhimisha siku ya Mwenyezi Mungu ndio
Krismasi ndani ya tarehe uwongofu, na kama
7 Januari ya kila mwaka. ukifuata matamanio
Katika kipindi hiki, ya o b a d a l a ya ya l e MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa
wafanyakazi kupewa yaliyokufikia ya ujuzi, katika ziara ya kutembelea jimbo la Magogoni, Wilaya ya Magharibi kuzindua miradi mbali
likizo maalumu, baadhi hutapata mlinzi wala mbali ya maendeleo pamoja na ofisi za chama cha Wananchi CUF.
y a t a a s i s i h u w a p a msaidizi yoyote kwa M a g h a r i b i k u z i n d u a maeneo yao utaondoka na a m e s e m a j i m b o h i l o
miradi mbali mbali ya baadhi ya Shehia na mitaa limeweza kupiga hatua
wafanyakazi wao posho Mwenyezi Mungu
za kheri ya Krismasi.
I k u m b u k w e t u maendeleo pamoja na ofisi tayari imeonesha mfano kubwa, ikilinganishwa
chama cha Wananchi mzuri wa kukataa uhalifu na hali ilivyokuwa kabla
Ni katika siku hizi za kwamba hatukusudii za
CUF.
yaye na Mbunge kuingia
sikukuu ya Kristmas kuwafanya watu wa imani
A m e s e m a J e s h i l a baada ya kuamua.
madarakani.
Maalim
Seif
ambaye
na mwaka mpya wa tofauti wasishirikiane Polisi peke yake haliwezi
Ametoa mfano, hivi
pia
ni
Katibu
Mkuu
wa
k
u
m
a
l
i
z
a
m
a
t
u
k
i
o
ya
miladia, watu hutumia na kuthaminiana. La,
sasa
kuna miradi mingi
wasaa wao mikahawani, tunachotaka kusema uhalifu, ikiwemo ujambazi, Chama cha Wananchi ya maji
safi na salama,
watumiaji
na
wauzaji
wa
vilabuni na katika kumbi ni watu kuheshimiana dawa za kulevya na watu CUF, amesifu mwamko vikundi mbali mbali vya
mbalimbali za starehe za kiimani, lakini zaidi wanaofanya udhalilishaji wa wananchi wa jimbo la wananchi hasa kinamama
uasi na wengi hutumia wavumiliane kwa yale watoto na wanawake, Magogoni bila kujali tafauti vinavyojishughulisha na
fursa hii kukesha katika ambayo kwa mujibu wa lakini jamii kupitia mpango z a o k a t i k a k u wa u n g a ujasiria mali, ambavyo
viongozi wa jimbo
vilevi, uzinifu, ngoma, mafundisho na kanuni za wa ulinzi shirikishi ndio mkono
inawasaidia katika
lao na kufanikisha miradi v
wa
t
a
k
a
o
t
o
a
m
c
h
a
n
g
o
kamari nk.
imani zao zinatofautiana. mkubwa kumaliza maovu yao ya maendeleo na ya kukabiliana na ugumu wa
maisha.
Tuseme tu kwamba
Iwapo ufahamu wa hayo.
kijamii.
(Habari kwa hisani ya
sikukuu ya Krismas na tofauti hizi utafahamika
Alisema, matukio ya
Maalim Seif amesema, Khamis Haji, OMKR
mwaka mpya Miladia, k w a k i l a i m a n i n a a i n a h i y o ya m e k u wa hamasa aliyoishuhudia
0777 484 459)

AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Chungeni mipaka Krismasi

Maalim Seif ahimiza ulinzi shirikishi

Habari

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Ijumaa yaswaliwa Mahakama Kuu


Na Seif Msengakamba

IJUMAA imesimamishwa nje


ya Mahakama Kuu Jijini Dar
es Salaam, wiki iliyopita.
Imam na Khatib, walipatikana
hapo hapo kutoka miongoni
mwa mamia ya Waislamu
waliofika mahakamani hapo
kusikiliza kesi.
Awali ilibidi Hakimu
anayesikiliza kesi hiyo
iliyokuwa ianze kusikilizwa
saa 3 asubuhi, kuahirisha
ili kuwapa fursa Waislamu
kwenda Msikitini kuswali
Ijumaa kwa tahadhari kuwa
muda wa swala ya Ijumaa
u n g e i n g i a k a b l a ya k e s i
kumalizika.
H a t a h i v y o , Wa i s l a m u
walichukua udhu na kuamua
kuswali Ijumaa hapo hapo
katika viwanja vya Mahakama
Kuu.
Baada ya kukamilika kwa
swala, kesi ilianza kusikilizwa
majira ya saa 8:37 mchana
ambapo kesi hiyo ya tuhuma
z a u g a i d i i n a y o wa k a b i l i
M a s h e i k h n a Wa i s l a m u
wengine, imerudishwa tena
katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Hiyo ni baada ya Jaji Twaibu
Faudhi wa Mahakama Kuu,
kusema kuwa mahakama hiyo
ina uwezo wa kusikiliza na
kutoa maamuzi juu ya kesi
hiyo.
Jaji Faudh alisema
mahakamani hapo kuwa baada
ya kusikiliza hoja za mawakili
wa pande mbili zilizotolewa
mbele ya Mahakama Kuu,
alielekeza kuwa kesi hiyo sasa
iendelee kusikilizwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi
ya Kisutu Desemba 29 mwaka
huu.
Jaji huyo ametoa maamuzi
yake kufuatia hoja zilizoletwa
mahakamani hapo na
upande wa utetezi ambao
haukuridhishwa jinsi kesi ya
msingi ilivyokuwa ikiendeshwa
katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, ambapo upande
wa mashitaka nao uiwasilisha
hoja pingamizi.
K a t i k a m a a m u z i ya k e ,
Jaji Faudh alitupilia mbali
mapingamizi mawili ya upande
wa serikali.
Mapingamizi hayo yalikuwa
yakidai kuwa, kwanza kiapo
cha upande wa utetezi
kilichowasilishwa Mahakama
Kuu ambacho kiliambatana na
maombi ya kutaka kuachwa
huru watuhumiwa hao wa

ugaidi kilikuwa kibovu, kwa


maana ya kwamba tarehe
ilikosewa.
Maombi ya utetezi ya kutaka
kuachiwa huru washitakiwa
yalibainishwa kuwa ni pamoja
na hati ya mashitaka kutoeleza
watuhumiwa hao walifanya
kosa mahali gani na pia hati
ya hiyo haielezi wahusika wa
ugaidi waliodaiwa kuingizwa
nchini na kuhifadhiwa wako
wapi zaidi ya kutajwa majina

yao tu.
Pingamizi la pili upande
wa serikali ulisema kwamba
Mahakama Kuu haikuwa na
mamlaka ya kusikiliza maombi
yaliyowasilishwa na utetezi
kwa sababu bado kesi ilikuwa
katika hatua za mwanzo katika
Mahakama ya Kisutu, kwa
hiyo maombi hayo hayawezi
kuletwa Mahakama Kuu.
Mmoja wa mawakili
wanaowatetea watuhumiwa

Bw. Abubakari Salim,


akizungumza na mwandishi wa
gazeti hili baada ya Jaji Faudhi
kutoa uamuzi wake juu ya kesi
hiyo, alisema Mahakama Kuu
imeangalia hati ya mashitaka
iliyopo na mazingira yalivyo
katika Mahakama ya Kisutu
kusema kuwa Mahakama hiyo
haiwezi kufungwa mikono na
kuiacha kesi hiyo kama ilivyodai
bila kutoa ufafanuzi juu ya
mashitaka yanayowakabili
washitakiwa.

ipange tarehe ya kutajwa kesi


hiyo, ili kutoa fursa kwao
kujipanga kuandaa mashahidi
wao, badala ya kupangwa
tarehe ya kusikilizwa kesi.
Kufuatia hali hiyo, wakili
wa upande wa Sheikh Ponda,
Bw. Juma Nassoro, alicharuka
mahakamani hapo kwa kile
alichoita ucheleweshwaji kesi
wa makusudi.
Wa k i l i J u m a N a s s o r o
alikuja juu na kusema kuwa
anamshangaa mwanasheria,
tena mwanasheria wa Serikali
kukosa huruma kiasi cha
kuchelewesha kwa makusudi
kesi hiyo.
Bw. Nassoro alisema Sheikh
Ponda yupo ndani tangu mwezi
wa nane mwaka jana, hivyo
alihoji iweje utetezi ushindwe
kipindi chote hicho kuwaandaa
mashahidi.
Aidha alisema, wao upande
wa utetezi tayari walishaleta
faili la hukumu ya Mahakama
Kuu katika mahakaka hiyo
ya Morogoro na kuiambia
mahakama kwamba, kwa kuwa
hukumu hiyo ilifuta hukumu ya
Mahakama ya Kisutu, shitaka
katika mahakama ya Morogoro
linakufa.
Alisema kuwa walichopaswa
k u f a n ya n i a m a wa f a n ye
marekebisho kuondoa shitaka
namba moja au kesi yote
waiondoe na kwamba moja kwa
moja Sheikh Ponda anastahili
sasa kupewa dhamana aachiwe.
Tayari tumeileta nakala ya
hukumu na ipo kwenye faili
la mahakama hapa Morogoro,
tumeileta sisi na kisheria sasa
ilivyo ni kwamba hukumu

ya mahakama inapotolewa
kwa mwanasheria yeyote,
a n a t a k i wa a c h u k u e k i t u
kinachoitwa Judicial notice
(yaani mahakama inatakiwa
ijue tu kwamba hukumu hiyo
ipo) wala haihitajiki kuletwa
ile nakala ya hukumu, hili ni
jambo ambalo linalotakiwa
kuthibitishwa. Alifafanua
wakili huyo.
Aliendelea kufafanua
hoja yake kwamba kwa wao
k u wa s i l i s h a m a h a k a m a n i
nakala ya hukumu, inatosha
kusema kwamba huk umu

Kesi ya Sheikh Ponda Moro


yazidi kupigwa danadana
Na Seif Msengakamba
HAKIMU wa Mahakama ya
Hakimu mkoani Morogoro,
Mery Moyo, Jumatatu iliyopita
aliahirisha kesi inayomkabli
Katibu wa Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu nchini, Sheikh
Ponda Issa Ponda hadi Januari
5, 2015.
Hakimu huyo alisema,
amepanga tarehe hiyo ili kupata
muda wa kupitia hukumu
iliyotolewa na Jaji Agostino
Shangwa katika Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Novemba 27, 2014.
I m e n i f i k i a l e o wa k a t i
nikijiandaa kuingia
Mahakamani kuanza kesi,
nikishamaliza kuisoma ndipo
nitaweza kutoa maamuzi ya kuja
kupanga kuwa kesi itasikilizwa
lini, tusubiri nikishaipitia ndio
nitajua nifanye nini. Alisema
Hakimu Moyo.
Wakili wa upande wa utetezi
aliyetajwa kwa jina la Kongola,
ye ye a l i s e m a k wa k u wa
mashahidi wake wa upande
wa mashitaka ni watumishi
wa s e r i k a l i , wa n a t a k i wa
kuandaliwa kwanza ndipo kesi
iweze kusikilizwa.
Naye Mwendesha Mashitaka
a l i s e m a k u wa n a k a l a ya
hukumu ya Jaji Shangwa Wa
Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, ambayo ilifuta
hukumu ya awali iliyotolewa
Mahakama ya Kisutu dhidi
ya S h e i k h P o n d a k a t i k a
kesi ya kiwanja cha Markaz
Changombe, wao hawajaipata.
Aidha, wakili wa upande wa
Jamhuri aliitaka mahakama

ya mahakama ya Kisutu
imeshafutwa na hukumu
ya Mahakama Kuu, hivyo
mahakama ya Morogoro
inastahili ifanyie kazi maelezo
hayo na hawapaswi kukaa
na kuacha kuifanyia kazi eti
kwasababu nakala ya huku
haijaletwa.
Kuna kitu kinaitwa Judicial

notice, yaani hapa mwanasheria


yeyote, hata wa mwaka wa
kwanza wa sheria anatakiwa
akijue. Sasa inashangaza wakili
wa serikali, tena mwandamizi
hajui hicho kitu, ni aibu, anaitia
aibu ofisi ya DPP ambayo ni
ofisi ya kikatiba, hii sio ofisi
ndogo. Alifoka Wakili Nassor.
Alisema, Sheikh Ponda yupo
ndani tangu mwezi Agosti
mwaka jana mpaka leo, lakini
bado Jamhuri inaleta danadana,
wanaomba kuahirishwa kesi,
halafu ije kwa kutajwa sio
kusikilizwa.
Alisema hoja zinazotoewa
ni mwanya tu wa kutaka
kuchelewesha kesi na kukosa
huruma.

Makala/Tangazo

BAADA ya kumshukuru
ALLAH (SW) kama
a n a v y o s t a h i k i
kushukuriwa, sala
na salamu zimfikie
Mjumbe wake Sayyidina
Muhammad (s.a.w)
pamoja na Masahaba zake
na kila anayefuata njia
yake kwa wema mpaka
siku ya malipo.
Enyi Waja wa ALLAH
:Hasadi ni maradhi
mabaya ya nafsi, na ni
kasoro kubwa inayokaa
katika moyo wa mtu na
ni asili na sababu ya kila
matendo maovu, na ni
tabia inayomuweka mtu
mbali na uchamungu.
Na maana yake ni kwa
mtu kutamani neema au
kheri aliyokuwa nayo
mwenziwe imuondokee.
Hasidi huwa anachukia
pale mwenziwe anapopata
kheri na anafurahi pale
mwenziwe anaposibiwa
na shari.
Anasema ALLAH
(SW) :Ikikupateni
kheri huwasikitisha
na ikikupateni shari
wanaifurahia. Na mkisubiri
na mkamcha ALLAH hila
zao hazitakudhuruni kitu.
Hakika ALLAH anayajua
vizuri yote wanayoyatenda

Tahadharini na Hasadi

Vile vile, hasidi huwa


haridhii vile ALLAH (SW)
anavyogawa neema kwa
waja wake na anapinga
na kuchukia maamuzi ya
ALLAH (SW) juu ya waja
wake.
Imepokewa katika
a t h a r i k u wa A L L A H
(SW) anasema :Hasidi
ni adui wa neema zangu,
n i m we n ye k u c h u k i a
maamuzi yangu, na
hauridhii ugawaji wangu
.
Na yoyote atakaoujaza
moyo wake kwa imani
ya k we l i n a n u r u ya
yakini, akawa anaridhia
maamuzi yote ya ALLAH
(SW) katika ugawaji wa
neema zake na maamuzi
yake mengine, basi kamwe
moyo hautokuwa na nafasi
ya uhasidi, kwani imani na
hasadi hazikai pamoja.
Amesema Mtume
(saw) :Havikai pamoja
katika katika kifua cha
mja (Muislamu), imani na
uhasidi.
Anasema ALLAH (SW)
:Au wanawafanyia watu

husuda kwa yale aliowapa


ALLAH kwa ukarimu
wake
Enyi Waislamu :Hakika
imethibi kuwa uhasidi
husababisha madhara ya
kidini na ya kidunia kwa
mtu hasidi, kwa sababu
daima huwa anaumia
na kuhisi dhiki kubwa
p a l e a n a p o o n a wa t u
wameneemeshwa na Mola
wao.
Amesema Mtume (saw)
: Utasibiwa umma wangu
na maradhi ya umma.
Wakasema Masahaba :
Ewe Mjumbe wa ALLAH,
ni yepi maradhi ya umma
? Akasema : Kiburi, na
majivuno, na kushindana
kwa ajili ya dunia, na
kuchukiana na kufanyiana
uhasidi, mpaka utaenea
uovu na mauaji .
Na katika mapokezi
mengine, amesema Mtume
(saw) :Yameingia juu
yenu maradhi ya umma
za kabla yenu; hasadi na
kuchukiana .
N d u g u Wa i s l a m u
:Hasadi ndio dhambi ya
mwanzo alioasiwa ALLAH

TANGAZO LA KAZI YA UALIMU.

DYCCC Yemeni Schools inakaribisha maombi ya kazi kwa walimu wazoefu na


wenye sifa kwa masomo yafuatayo kwa upande wa Primary na Secondary.

(SECONDARY)
S/N
NAFASI
1
2
3
4
5

MWALIMU WA HISTORIA
MWALIMU WA ENGLISH
MWALIMU WA CHEMISTRY
MWALIMU WA KIARABU
MWALIMU WA CIVICS

SIFA
BA(EDC)
BA(EDC)
BSC(EDC)
BA(EDC)
BA(EDC)

(PRIMARY)
S/N
1
2
3
S/N
1

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

NAFASI
MWALIMU WA ELIMU YA MAARIFA
MWALIMU WA SHULE YA MSINGI
MWALIMU WA SHULE YA MSINGI
NAFASI
LABORATORY TECHNICIAN

SIFA
CERTIFICATE/DIPLOMA (EDC)
CERTIFICATE/DIPLOMA (EDC)
CERTIFICATE/DIPLOMA (EDC)
SIFA
CERTIFICATE/DIPLOMA

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31-12-2014. Watakaopenda kuungana nasi


walete CV zao zikiambatana na copy za vyeti katika ofisi zetu zilizopo Changombe
au wavitume kwa:
Human Resource Office
(DYCCC-YEMEN SCHOOL)
P.O.BOX 42541
DAR-ES-SALAAM

(SW) katika mbingu na


Bilisi pale alipokataa
kumsujudia Adam baada
ya kuona kuwa amepewa
cheo kikubwa mbele ya
Malaika na hatimae kutiwa
katika pepo.
Anasema ALLAH
(SW) :Shettani alimtia
wasiwasi akamwambia :
Ewe Adamu, nikujuulishe
mti wa milele na ufalme
usiokwisha ? Basi wakaula
w o t e wa w i l i n a u c h i
wao kuwadhihirikia na
wakaanza kujibandika
majani ya peponi, na
Adamu akamkosa
Mola wake na akapotea
njia. Kisha Mola wake
akamchagua, na
akamkubalia toba yake na
akamuongoa .
Na imepokewa kutoka
kwa Ibnu Umar (ra) kuwa
Bilisi kamwambia Nabii
Nouh (as) :
B i n a a d a m u
amehilikishwa kwa mambo
mawili, hasadi na pupa.
Na kutokana na hasadi
ndio mimi nikalaaniwa
na nikajaaliwa kuwa ni
shettani aliewekwa mbali
na kila rehma .
Pia hasadi ndio dhambi
ya mwanzo alioasiwa
ALLAH (SW) katika ardhi
na watoto wa Nabii Adam,
baada ya wao kutoa sadaka
na kukubaliwa sadaka ya
mmoja wao na kukataliwa
sadaka ya mwengine.
Anasema ALLAH (SW)
:Na wasomee khabari za
watoto wawili wa Adamu
kwa ukweli, walipotoa
sadaka ikakubaliwa ya
mmoja wao na ikakataliwa
ya mwengine. Akasema
:(yule iliokataliwa sadaka
yake) nitakuua. Akasema
( yule aliokubaliwa sadaka
yake) : Hakika ALLAH
huwapokelea wamchao
tu .
Na katika alama za
mtu hasidi ni kujidai
kumpongeza na hata
kumuombea dua mtu
aliepata neema huku
moyo wake ukichukia, na
kumsengenya anapokuwa
hayupo hali ya kuwa
anaona uchungu juu ya kile
ambacho yeye hakimiliki.
Anasema ALLAH
(SW) :Bughudha (yao
juu yenu) inadhihirika
katika midomo yao, na
yanayofichwa na vifua
vyao ni makubwa zaidi,
Enyi Waja wa ALLAH
:Ilivyokuwa hasidi ni mtu
mbaya, basi ni lazima

tujikinge kwa ALLAH


(SW) kutokana na shari
yake. Na katika njia za
kujikinga na shari ya hasidi
ni kusoma Suuratul Falaq
ambayo ALLAH (SW) kwa
rehma zake alimfunza
kufanya haya Mtume wake
na umma wake.
Anasema ALLAH (SW)
:Sema : Najikinga kwa
Mola wa walimwengu
wote. Na shari ya
alivyoviumba. Na shari ya
giza la usiku liingiapo. Na
shari ya wale wanaopulizia
mafundoni. Na shari ya
hasidi anapohusudu .
E n y i Wa j a wa
ALLAH :Hakika watu
hugawika sehemu mbili
wanapomuona mwenzao
kaneemeshwa na ALLAH
(SW). Wapo wanaochukia
na kutamani neema ile
imuondokee na hawa
ndio mahasidi. Na wapo
wanaotamani na wao
waipate neema kama hiyo
ili na wao washindane
katika mambo ya kheri,
na hii ndio sifa ya watu
wema.
Amesema Mtume (saw)
:Hakuna uhasidi (choyo)
isipokuwa katika mambo
mawili : Mtu kapewa mali
na ALLAH akaitumia
yote katika njia ya haki,
na mtu kapewa elimu na
ALLAH akaifanyia kazi
na akawafundisha watu .
Enyi Waislamu :Mcheni
ALLAH Mola wenu
Mtukufu, na jitengeni sana
na tabia ya uhasidi, kwani
kumbukeni kuwa uhasidi
unafisidi mema yenu
sawa na moto unavyokula
kuni, na pia unaharibu
imani kama vile shubiri
inavyoharibu asali.
Amesema Mtume (saw)
:Jihadharini na uhasidi,
kwani hakika uhasidi
unakula mema kama vile
moto unavyokula kuni .
Na amesema Mtume
(saw) :Hasadi inaharibu
imani kama vile shubiri
inavyoharibu asali .
Na pia amesema Mtume
(saw) :Hayuko pamoja na
mimi mwenye hasadi wala
fitna wala mwenye kujidai
kuwa anajua mambo ya
ghaibu na mie si katika
yeye . Kisha akasoma :
Na wale wanaowaudhi
Waislamu wanaume na
wanawake bila ya wao
kufanya kosa lolote, bila ya
shaka wamebeba dhulma
kubwa na dhambi za
dhahiri .
(Makala na uchambuzi
kwa hisani ya mtandao wa
Mzalendo)

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Kanisa Anglikana lateua Askofu wa kwanza mwanamke


ENGLAND
KANISA la England Alhamisi
ya wiki iliyopita limemtangaza
Bi. Libby Lane, kuwa Askofu wa
kwanza mwanamke, kufuatia
kufanyika mabadiliko ya kihistoria
katika kanuni zake.
Lane ametangazwa kuwa Askofu
mpya wa Stockport, ikiwa ni hatua
mpya ya kushangaza katika Kanisa
la England baada ya miaka mingi ya
kugawanyika na kuhitilafiana juu
ya hatua hiyo ya kuwa na Askofu
mwanamke.
" N i f u r a h a k u b wa a m b a y o
sikutarajia kuwa hapa leo," Alisema
Bi. Lane baada ya kutangazwa kuwa
Askofu wa Stockport, mji uliopo nje
kidogo Kaskazini Magharibi mwa
mwa jiji la Manchester England.
" Kwangu ni siku ya kukumbukwa
na kutambua kuwa ni siku ya
kihistoria kwa Kanisa. Nimepewa
heshima na ni shukurani kuitwa
katika kutoa huduma ya Uaskofu wa
Stockport na nimefurahi, sio jambo
dogo kuaminiwa na asasi kama hii.
Ninawatambua sana wale
waliofahamika na wasiofahamika
ambao waliniombea na kufanya kazi
na kupambana hadi sasa."
Kanisa hilo lilitoa uthibitisho wake
wa mwisho wa uteuzi wa Askofu
mwanamke mwezi uliopita na
kuhitimishwa mchakato ulioelezwa
kuwa ulikuwa wa mwendo wa
kinyonga, ambao umewaweka
waumini wa mrengo wa kilibarali
na kihafidhina katika uwiano.
Kanisa la England limekuwa
likipigia chapuo kuanzishwa kwa
nafasi ya uchungaji kwa wanawake
tangu mwaka 1992 na wachungaji wa
kwanza walitangazwa miaka miwili
baadae. Kwa sasa wamefikia theluthi
moja ya viongozi wa Kanisa.
Kanisa la England ndilo Kanisa
mama kwa Makanisa ya Anglikana,
ambayo yana wafuasi wapatao
milioni 85 katika nchi zaidi ya 165.

Makanisa mengine ya Anglikana


duniani kote yamekuwa yakiteua
Maaskofu wanawake kwa kipindi cha
miaka kadhaa.
Kwa Makanisa mengine, Askofu
wa kwanza wa kike aliteuliwa
Marekani mwaka 1989 na sasa kuna
zaidi ya Maaskofu wa kike 30 duniani
kote katika nchi kama Australia,
Canada, Cuba, New Zealand na
Swaziland.
Bi. Lane amesoma katika Chuo
Kikuu cha Oxford na kuwa Mchungaji
mwaka 1994.
Baadhi ya mambo binafsi
anayopenda ni pamoja na kujifunza
kupuliza saxophone, kuishabikia
klabu ya soka ya Manchester United,
kusoma na kufanya mchezo wa
kujaza na kupangilia maneno kwenya
majedwali (cryptic crosswords).
Mumewe George pia ni Mchungaji,
walikuwa wanandoa wa kwanza
katika Kanisa kufanya kazi pamoja.
Mumewe ni kiongozi msimamizi
(coordinating chaplain) wa eneo la
Uwanja wa ndege wa Manchester.

Akiwa Askofu wa Stockport,


Lane atahudumia kama Msaidizi wa
Askofu katika Dayosisi ya Chester.
Ofisi ya Waziri Mkuu David
Cameron ya Downing Street, ilitoa
taarifa kwamba Malikia Elizabeth
II, Kiongozi Mkuu wa Kanisa
amemthibitisha uteuzi wa Lane.
"Ninapenda kumpongeza
Elizabeth Lane kwa kuteuliwa kwake
kama Suffragan See of Stockport
na kwa kufanya hivyo anakuwa
mwanamke wa kwanza kuwa Askofu
katika Kanisa," alisema Cameron
katika taarifa yake.
"Huu ni uteuzi wa kihistoria na
hatua muhimu mbele kwa Kanisa
kuelekea usawa katika nafasi za juu."
Aliongeza kuwa serikali inaweza
kuleta sheria wiki hii ambayo itaweza
kuruhusu Maaskofu wanawake
kukaa katika nafasi za juu katika
Bunge la Mabwanyeye (Parliament's
upper House of Lords).
Kiasi cha Maaskofu 26
wanaruhusiwa kukaa katika Bunge
hilo, ikiwa ni pamoja na viongozi
watano wa ngazi za juu kabisa na
Maaskofu wengine 21 (diocesan
bishops) ambao wamehudumu kwa
muda mrefu katika Kanisa hilo.
Kanisa hilo lilijitenga kutoka Kanisa
la Roman mwaka 1534. Inadaiwa
kuwa zaidi ya asilimia 40 ya watu
nchini England wanajichukulia kuwa
ni waumini wa Kanisa la England.

Bi. Libby Lane, Askofu wa kwanza Mwanamke Kanisa la Anglikana

UN wamtoa kiongozi wa al-Shabaab kwenye orodha ya vikwazo


K A M AT I y a B a r a z a l a
Usalama la Umoja wa Mataifa
inayoshughulikia masuala
ya Somalia, siku ya Ijumaa
Desemba 19, ilimuondoa
kiongozi mwandamizi wa alShabaab Mohamed Said Atom,
kutoka orodha ya waliowekewa
vikwazo, ikiwa ni miezi sita
baada ya kukana ushirika wake
na kikundi hicho, AFP iliripoti.
Atom alikuwa amewekewa
vikwazo vya safari na kifedha
kutokana na kile kilichoitwa
kutuhumiwa katika vitendo
vya "utekaji nyara, uharamia na
ugaidi."
H a t a h i v y o , m we z i J u n i ,
alitangaza kukana uhusiano wake
na al-Shbaab na kuahidi kufanya
kazi kupitia njia za usalama na
maelewano tu siku za mbele.
Serikali ya Somalia ilisifia
maendeleo hayo kama ushahidi
unaotoa ruhusa ya msamaha kwa
kila mtu anayeachana na ugaidi,
shughuli za kijeshi au uharamia
kuwa zilikuwa zinatoa matokeo
mazuri.
Waziri wa Habari wa Somalia,
Mustafa Duhulow, alikaribisha
u a m u z i h u o k a m a n j i a ya
kumhamasisha yeyote anayetaka
kukataa vurugu na kujiunga na
mchakato wa amani.
Alisema kuwa serikali ya
shirikisho ilizungumza na Umoja
wa Mataifa na nchi kadhaa
wanachama ili kumuondoa Atom

katika orodha ya waliowekewa


vikwazo, na kuiita hatua hiyo ni
mafanikio makubwa sio tu kwa
mtu mmoja mmoja, bali pia kwa
wengine wote wanaotaka kukataa
vurugu na kujiunga na mchakato
wa amani.
"Serikali itaendelea kuwaunga
mkono watu wanaochagua njia ya
amani badala ya njia ya vurugu,
nawajua watu wengi wanaona
vigumu kuelewana, lakini ikiwa

Somalia inataka kukubali makosa


yake, kutakuwa na nafasi ya
kuelewana na mtu huyo na
wengine kama yeye alisema katika
taarifa." Alisema Bw. Duhulow.
Hata hivyo ingawaje Bw. Atom
hakabiliwi tena na vikwazo
alivyowekewa na Umoja wa
Mataifa, bado anabakia katika
orodha ya vikwazo vya fedha
kutoka Hazina ya Marekani.

K U N D I l a wa p i g a n a j i
nchini Iraq la ISS limewaua
wanawake 150 katika mkoa
wa Anbar, Magharibi mwa
nchi hiyo kwa kukataa
kuolewa na wanamgambo
wa kundi hilo.
Ta a r i f a ya Wi z a r a ya
Haki za Binadamu ya Iraq
imeeleza kuwa wanawake
wasiopungua 150, wakiwemo
wajawazito wameuliwa na
kundi la kigaidi na kitakfiri
la Daesh katika mji wa
Fallujah baada ya kukataa
kile kinachoitwa na kundi

hilo jihadun Nikah.


Taarifa ya wizara hiyo
imeongeza kuwa, familia
nyingi pia zimelazimika
kuhama mji wa al Wafa
uliopo Kaskazini mwa Iraq,
baada ya mamia ya raia
kutishiwa na kundi hilo.
Wizara hiyo imeongeza
kuwa, watoto wengi
wamepoteza maisha baada
ya familia zao kukimbilia
misituni kutafuta hifadhi,
wakiwakwepa wanamgambo
wa ISS. (irib)

Wanawake 150 waliokataa


kuolewa na ISS wauawa Iraq

6
Papa akosoa
vikali viongozi
wenzake Vatican

Na Iddi Ssessanga/ape,dpae
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki
duniani, Papa Francis, amewakaripia
vikali viongozi wa Vatican na
kukosoa kile alichokieleza kuwa
ni ugonjwa ulioukumba uongozi
huo, ukiwemo wa kuteta na uchu
wa madaraka.
Papa Francis ameongeza
kile alichokiita magongwa 15
yanayowakabili wasaidizi wake
ndani ya Vatican, na kuwataka
watumie muda huu wa Krismas
kutubu dhambi zao na kulifanya
Kanisa kuwa mahala penye afya na
patakatifu zaidi mwaka 2015.
Papa Francis alizungumza juu ya
wale wanaojigeuza kuwa mabosi na
wanaojiona wako juu ya kila mmoja
na hawamtumikii yeyote.
Alionya pia juu ya kile alichokiita
"ugonjwa wa madaraka" na kuwaonya
dhidi ya nargisi ya wale wanaojijali
wenyewe bila kuwahurumia walio
dhaifu na wanaohitaji zaidi.
Tamaa ya vyeo na ubinafsi
Aliwakosoa pia wasiowaheshimu
wakubwa zao akisema,"ugonjwa wa
kutomtii mkubwa ndiyo ugonjwa
wa wale wanaowasifu wakubwa zao
wakitumai kupata kitu kutoka kwao.
Alisema hao ni wahanga wa tamaa ya
vyeo na ubinafsi, wanawaheshimu
binadamu na siyo Mungu."
Imeelezwa kuwa wakati miongoni
mwa wasikilizaji walikuwepo
wakimsikiliza Papa Fransis, walikuwa
wamekunja sura zao, lakini ujumbe
ukiwaingia barabara.
A i d h a Pa p a a l i z u n g u m z i a
ugonjwa wa kile alichokiita sura
za msiba, akibainisha kuwa watu
wasioridhika na wanaokunja sura,
wale wanaojaribu kuvaa sura za ukali,
wanawatendea wengine kwa dharau
na kwa kibri, hasa wale wanaoamini
ni wa hadhi ya chini.
Papa Francis, ambaye ndiye Papa
wa kwanza kutoka Amerika Kusini
na hakuwahi kufanyakazi katika
Baraza la Uongozi wa Kanisa hilo
linalodhibitiwa na Wataliano, kabla
ya kuchaguliwa hakuona haya
kulalamika juu ya porojo, tamaa
za vyeo na hila za madaraka jinsi
vinavyoikabili Vatican.
Lakini wakati ajenda yake ya
mageuzi ikizidi kushika kasi,
alionekana mwenye kuthubutu
zaidi hata kuweza kubainisha yale
yanayoikwamisha taasisi hiyo.
Wafuatiliaji wa masuala ya Vatican
walisema hawajawaji kusikia hotuba
kali kama hiyo kutoka kwa Papa na
kuongeza kuwa huenda ameamua
kuweka mambo hadharani kutokana
na upinzani anaokabiliana nao katika
kutekeleza mageuzi yake.
"Ukweli ni kwamba anaielekeza
hotuba yake ya Krismas kwa magonjwa
15 ya kiroho kwa namna hiyo, kwa
maoni yangu ni ishara kwamba
anachukulia mageuzi katika uongozi,
na mageuzi ya kiroho kiujumla
kama hatua muhimu anayotaka
kuendelea kuchukuwa. Kwamba
bado kuna upinzani mkubwa na
pengine upinzani umeongezeka
katika miezi ya hivi karibuni," alisema
Iacopo Scaramuzzi, ripota wa gazeti
la TMNews mjini Vatican.

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Mauaji ya kulipa kisasi dhidi


ya polisi yaitikisa New York
Polisi nao waua raia tena

VOA
MJI wa New York umekumbwa
na simanzi kufuatia mauaji
ya maafisa wawili wa polisi
yaliyofanywa na kijana mmoja,
ambaye aliwaambia wapita
njia kuangalia alichokuwa
anakwenda kukifanya muda
mfupi kabla ya kufanya mauaji
hayo.

jamii moja, mji mmoja na hatutaki


chochote kutugawa kuhusu
namna gani tunawashukuru
askari wetu wanapohakikisha
usalama wetu kila siku," alisema
Eric Adams, Rais wa Manispaa
ya Brooklyn alipotembelea kituo
cha muda cha kumbukumbu ya
maafisa hao.
Rais Barack Obama, aliyeko

MAAFISA wa polisi nchini Marekani wakitoa heshima zao za mwisho kwa


askari wenzao wawili waliouliwa kwa kupigwa risasi hivi karibuni nchini humo.

Maafisa hao wawili, Wenjian


Liu mwenye umri wa miaka 32 na
Rafael Ramos mwenye miaka 40,
walipigwa risasi kupitia kioo cha
gari lao la doria mchana kweupe
siku ya Jumamosi katika mji
wa Brooklyn, katika shambulio
lililoutikisa mji mkubwa zaidi wa
Marekani New York kuelekea siku
ya Krismas.
Polisi ilimtaja muuaji kuwa ni
Ismaaiyl Brinsley, mwenye umri
wa miaka 28 ambaye alijiua kwa
kujipiga risasi kichwani baada ya
kutenda mauaji hayo.
Mauaji hayo yanatokea katika
mji ambao unaoshuhudia kuwa
na kiwango cha chini kabisa cha
mauaji katika kipindi cha miaka 20,
yamezidi kuudhofisha uhusiano
kati ya Meya wa New York Bill
de Blasio na jeshi la polisi, ambalo
linamlaumu kwa kushindwa
kuwasaidia na kuonyesha huruma
zaidi kwa waandamanaji, ambao
waliingia mitaani hivi karibuni
kupinga mauaji ya polisi dhidi
ya Wamarekani wenye asili ya
Afrika.
"Sote tumenufaika na kitendo
chao cha kishujaa na ndiyo maana
viongozi wetu wa Kiislamu,
viongozi wetu wa Kiyahudi,
viongozi wetu wa Kibaptisti,
viongozi wetu wa Kikatoliki, jamii
yetu kwa ujumla iko hapa kama

mapumzikoni mjini Honolulu,


alimpigia simu Kamishna wa Polisi
wa Philadephia Charles Ramsey,
kuelezea kughadhabishwa kwake
na mauaji ya maafisa hao wa
polisi na kumtaka Mwenyekiti
huyo mwenza wa kikosi kazi
alichokiunda, kutathmini matendo
ya polisi nchini Marekani kote,
kutumia kikosi hicho kusambaza
ujumbe wake kwamba vitendo
kama hivyo dhidi ya Polisi
vinapaswa kulaaniwa.
Akizungumzia mauaji yao,
Rais wa chama cha maaskari wa
doria Pat Lynch, alimlaumu Meya
wa New York, Bill de Blasio na
kusema damu yao iko kwenye
mikono yake.
B r i n s l a y a l i s e m a k we n ye
mtandao wake kuwa mauaji hayo
yalikuwa ya kulipa kisasi kwa vifo
vya Eric Garner mjini New York,
na Michael Brown mjini Ferguson
Missouri.
Polisi ilisema bwana huyo
alikuwa na rekodi ya uhalifu,
chuki dhidi ya polisi na serikali,
na alikuwa na historia ya ulemavu
wa akili ambayo ilihusisha jaribio
la kujinyonga mwaka mmoja
nyuma.
Polisi nchini Marekani
wa m e k o s o l e wa k wa m u d a
kutokana na mbinu zao, kufuatia
kifo cha Eric Garner aliyekabwa

hadi kufa na afisa wa polisi mjini


New York, na Michael Brown
aliyepigwa risasi mjini Ferguson,
jimboni Missouri.
Uamuzi wa Baraza la wazee wa
mahakama kukataa kuwafungulia
mashtaka maafisa waliohusika
katika vifo vya raia hao wenye
asili ya Afrika, ulisababisha
maandamano makubwa mjini
New York na maeneo mengine ya
Marekani.
Katika tukio jingine huko
Berkeley, Missouri katika kitongoji
cha St. Louis, ofisa wa polisi
amempiga risasi na kumuua
kijana mweusi ambaye amedaiwa
kuwa alimnyooshea bunduki pilis
huyo katika kituo cha mafuta
majira ya jioni siku ya Jumanne,
kwa mujibu wa shirika la AP.
Kundi la watu wapatao 100
walikusanyika Jumatano katika
eneo la tukio huko Berkeley,
Missouri, zikiwa ni maili chache
kutoka mji wa Ferguson, ambako
polisi walimuua kikatili kijana
mweusi mwenye umri wa miaka
18, Michael Brown mwezi Agosti.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa msemaji wa polisi wa St.
Louis, Sgt. Brian Schellman,
ofisa huyo wa polisi wa Berkeley
alikuwa katika doria katikakituo
hicho cha mafuta majira ya saa
11:15 jioni siku ya Jumanne ndipo
alipowaona watu wawili na
kuwakaribia.
Taarifa hiyo inasema mmoja
wao walitoa bunduki na
kumwelekezea ofisa huyo wa
polisi Bw. Schellman, ndipo naye
alipofyatua risasi kadhaa na
kumjeruhi.
Mwenzake alikimbia na bunduki
ya aliyeuliwa ilichukuliwa, kwa
mujibu wa maelezo ya askari huyo
Bw. Schellman.
Idara ya Polisi wa St. Louis
inafanya uchunguzi na hadi sasa
hakuna taarifa zaidi juu ya tukio
hilo.
Polisi walieleza kuwa mtu
aliyeuliwa bado hajafamika,
ingawa gazeti la St. Louis Post
limeripoti kuwa mwanamke
mmoja aliyekuwepo eneo la
tukio alimtambua maiti kuwa ni
mwanae mwenye umri wa miaka
18 na anaitwa Antonio Martin.
Toni Martin alilieleza gazeti
hilo kuwa mwanae alikuwa na
rafiki wake wa kike wakati huo
wa kupigwa risasi.
Waandamanaji walikusanyika
mapema siku ya Jumatano katika
kituo hicho cha mafuta huku
wakiwashutumu maofisa wa
Polisi.

7
Na Asia Mbwana, Dar es Saalam

MWAKA huu 2014 unaotarajia


kufikia ukingoni hivi karibuni,
u m e s h u h u d i a wa n a s h e r i a
wakuu wawili wa serikali katika
pande zote mbili za muungano,
Ta n g a n y i k a n a Z a n z i b a r
wakishindwa kuhudumu katika
nyadhifa zao kama ilivyo ada,
kila mmoja kwa sababu zake.
Aliyekuwa Mwanasheria wa
Mkuu wa Zanzibar, Othman
Masoud Othman, akivuliwa
wadhifa wake na Rais wa Zanzibar
na Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dk. Ali Muhammed Shein mara
baada ya kupiga kura ya hapana
katika Bunge Maalumu la Katiba,
kupinga baadhi ya vifungu vya
Katiba inayopendekezwa, huku
Jaji Fredrick Werema, yeye
akijiuzulu kufuatia kuhusishwa
katika kutoa ushauri unaodaiwa
kusababisha kuchotwa fedha za
umma zilizokuwemo kwenye
akaunti ya Tegeta Escrow.
Kufuatia kujiuzulu kwa Jaji
Werema, Jumanne iliyopita,
baadhi ya watu katika mitandao
ya kijamii na mitaani wamekuwa
wakinadi na kutaka kuuaminisha
u m m a k u wa J a j i We r e m a ,
yeye kaondoka kishujaa huku
Mwanasheria Mkuu wa zamani
wa Zanzibar, Othmani Masoud
kuwa aliondolewa kwa kujitakia
mwenyewe, kwa udhalili na
ilikuwa sawia yeye kutimuliwa
kazi.
Huku wengine wakijiuliza
kwa nini Rais Kikwete, kwenye
taarifa yake kwa vyombo vya
habari aliyoitoa kuujulisha umma
kujiuzulu kwa Jaji Werema,
amemsifia mwanasheria huyo
kuwa alikuwa muadilifu na
m u a m i n i f u , h u k u we n g i n e
wakijiuliza kwani aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ya Zanzibar kabla ya kuvuliwa
wadhifa wake, yeye hakuwahi
kuwa muadilifu, yumkini kwa
sababu yeye alivuliwa na Rais
Shein.
Kwa wenye uzalendo, watetezi
wa wanyonge, wenye upeo wa
kuona mbali na wasiofungwa na
mitazamo ya vyama vya siasa,
endapo kama itapigwa kura
ya kuamua nani ni shujaa wa
walala hoi baina ya Jaji Werema
na Othmani Masoud, bila shaka
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
wa Zanzibar, Othman Masoud
ataibuka kidedea (Will hit the
jackpot).
Othmani Masoud, japo
alifukuzwa kazi, lakini machoni
mwa wengi bado anaonekana
shujaa na historia imeshamuandika
katika upande sahihi kuwa
m i o n g o n i m wa wa n a d a m u
waliowahi kutokea hapa duniani
wa kutetea maslahi ya wanyonge.
Na ifahamike kuwa Mhe. Masoud

Makala

Pongezi Othman Masoud


Jaji Fredrick Werema mmh.

Jaji Fredrick Werema (picha juu). Chini Aliyekuwa mwanasheria Mkuu


wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
kupinga baadhi yavipengele
katika Katiba inayopendekezwa,
hakuitetea Zanzibar peke yake
ingawa alivipigia kura ya hapana
vile vipengele vilivyoonekana
kuvinyonga visiwa vya Zanzibar.
Mhe. Masoud ni shujaa kwa
pande zote mbili za muungano kwa
kuwa Katiba inayopendekezwa
inaleta mgongano kwa
pande zote, kwani kuendelea
kukukumbatia mfumo wa serikali
mbili ni kuendelea kuinyima
mamlaka kamili nchi ya Zanzibar,
jambo ambalo kwa Zanzibar,
wanaendelea kuwatazama
wenzao wa Tanganyika kuwa
wanawadhulumu hivyo taratibu
kuendeleza hali ya kutoaminiana
baina ya wakazi wa nchi
washirika, jambo ambalo si jema
huko tuendako.
Kwa ujumla vipengele
a l i v y o v i p i n g a m h e s h i m i wa
Masoud kwa kiasi kikubwa
ukiviangalia utagundua
m wa n a s h e r i a h u y o a l i o n a
mbali kwani alikuwa anasaidia
kuziondosha nchi washirika
wa muungano wetu, pamoja na
mambo mengine, katika mgogoro
wa kikatiba unaoletwa na Katiba
inayopendekezwa. Mfano, Katiba
ya Zanzibar inatamka kwamba
Zanzibar ni nchi ambayo eneo
la mipaka yake ni lote la visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

visiwa vidogo vilivyoizunguka


na bahari yake ambayo kabla ya
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu
wa Zanzibar.
Na pia Ibara ya pili ya katiba
hiyo inaitambua Zanzibar
k u wa m i o n g o n i m wa n c h i
mbili zinazounda Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania., jambo
ambalo ni kinyume na Katiba
inayopendekezwa ambayo katika
ibara yake ya kwanza inatamka
kuwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni nchi yenye mamlaka
kamili ambayo imetokana na
Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri
ya Watu wa Zanzibar ambazo
kabla ya Hati ya Makubaliano ya
Muungano ya tarehe 22 Aprili,
1964 zilikuwa nchi huru.
Wa k a t i h u o h u o K a t i b a
inayopendekezwa katika ibara
yake ya kwanza inatamka kuwa
J a m h u r i ya M u u n g a n o wa
Tanzania ni nchi yenye mamlaka
kamili ambayo imetokana na
Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri
ya Watu wa Zanzibar ambazo
kabla ya Hati ya Makubaliano ya
Muungano ya tarehe 22 Aprili, 1964
zilikuwa nchi huru, jambo ambalo
linaenda kinyume na katiba ya
Zanzibar ibara ya pili inaitambua
Zanzibar kuwa miongoni mwa

nchi mbili zinazounda Jamhuri ya


Muungano wa Tanzania.
Yapo mengi ambayo aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
aliona kama ni mtihani kwa afya
ya muungano, ambayo mpaka
sasa anatazamwa kama shujaa
na mtetea ukweli, na Mungu
ni mkubwa kwani katiba
inayopendekezwa inapingwa na
wengi sasa nasi kwa husuda bali
kwa kuwa imeshindwa kuzingatia
maoni muhimu ya wananchi
walioyataka yawemo kwenye
katiba hiyo.
Wakati aliyekuwa Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar akijaribu
k u o n d o a m g o g o r o h u o wa
kikatiba na utata mwingine,
kwa upande wake aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania
bara Jaji Werema alishindwa
kuiona hali hiyo na badala yake
kuacha wabunge wa chama na
serikali yake kusonga mbele na
hata yeye mwenyewe kuunga
mkono katiba inayopendekewa

akasahau kuwa huko tuendako


yumkini kukazuka mgogoro
huo, kwani haitakuwa rahisi
kwa Zanzibar kubadili katiba
yake ili iwiane sawa na katiba
inayopendekezwa kama itapita
hapo mwakani.
Jaji Werema hawezi kuwa
shujaa zaidi ya Othmani
Masoud, kwani sakata
lilimuondoa yeye halikuwa na
maslahi kwa taifa na lilikuwa
linazidi kuwaliza Watanzania,
ambao hospitali zao za umma
hazina dawa, wanafunzi vyuo
vikuu hawana mikopo, makali
ya maisha yanazidi kungata,
huku ushauri wake ukidaiwa
kuwanufaisha wachache tena
kwa kujichotea fedha kinyume
na utaratibu.
Na kwa tathmini ya haraka
haraka, hata kuporomoka kwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika uchaguzi wa serikali za
mitaa uliofanyika hivi karibuni
ambapo Katibu wake wa itikadi
na uenezi, Nape Nnauye kusema
kuwa wamepoteza 12% kwa
wapinzani, kwa namna moja ama
nyingine kunatokana na sakata
la kashfa ya Escrow ambapo Jaji
Werema amehusika katika kutoa
ushauri wake aliosema umechafua
hali ya hewa.
Hivyo si sawa kusema Othmani
Masoud hakustahili pongezi
na kumuona kama msaliti kwa
Zanzibar, bali yeye alisimama
kwenye ukweli, kuitetea Zanzibar
na kutetea muungano wa haki kwa
pande zote mbili za muungano.
(Mwandishi wa makala hii
ni mwanafunzi wa Shule Kuu
ya Uandishi wa Habari na
Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaamu,
simu, 0655418171.)

Makala

8
Na Omar Msangi
FEBRUARI mwaka
2011, Bunge la Nigeria
l i l i p i t i s h a s h e r i a ya
kupambana na ugaidi.
Kama ilivyokuwa kwa
K e n ya j u z i , s e r i k a l i
ya Nigeria wakati huo
ilidai kuwa ni muhimu
kupitisha sheria hiyo ili
itoe nguvu na uwezo zaidi
kwa vyombo vya dola
kukomesha ugaidi ili
kuleta amani katika nchi.
Lakini kama ilivyokuwa
Kenya pia, sheria hiyo
ililalamikiwa sana kwa
sababu ilidaiwa kuweka
msingi wa kuvunja haki
za kikatiba na haki za
b i n a d a m u . C h i n i ya
sheria hiyo, maofisa wa
polisi na vyombo vingine
vya usalama, walipewa
mamlaka kisheria
ya kukamata watu na
kuwaweka ndani bila ya
kuwafungulia mashitaka.
Aidha, waliweza pia
kukamata mali za
watuhumiwa yakiwemo
magari na vilivyokuwemo
bila ya kuwajibika kuwa
na hati ya kisheria ya
kupekua au kukamata
mali.
Kabla ya serikali
ya Goodluck Jonathan
kupelekea muswada
wa sheria hiyo bungeni,
kulitangulia mashambulizi
ya kigaidi Jos ambapo zaisi
ya watu 200 waliuliwa.
Hapo tena ndio muswada
ukaletwa ikielezwa kuwa
hali ilikuwa ya kutisha
na ilikuwa ikihitaji sheria
kali na kuvipa uwezo
mkubwa zaidi vyombo
vya usalama.
Pamoja na maelezo na
hoja hizo kutoka serikalini,
muswada ulikabiliwa na
upinzani mkali kutoka
kila kona mpaka ndani
ya Bunge. Katika hali
ya kutaka kupiga
magoti, Rais Jonathana
akawabembeleza wabunge
kupitisha muswada huo.
Hata hivyo, mara tu
b a a d a ya k u p i t i s h wa
sheria hiyo, Nigeria
haikupumua. Matukio
ya ugaidi unaodaiwa
kufanywa na Boko Haram
ndio ulipamba moto. Kwa
mwaka huo wa 2011,
yalifanyika mashambulizi
8 ambapo watu 180
waliuliwa. Taarifa moja
ya Human Rights Watch
inasema kuwa mwaka
2012 Boko Haram waliuwa
zaidi ya watu 815 katika
matukio 275 ya kigaidi,
idadi ambayo ni kubwa
kuliko yaliyojiri kwa
mwaka 2010 na 2011.
Mwaka 2013 waliuliwa
watu wasiopungua 423.
Na kufika mwaka 2014

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Rais Kenyatta anajua nini zaidi


wasichojua Wakenya wenzake

Afuata nyayo za Goodluck Jonathan


Al Shabaab wanaoitesa Kenya ni nani?

RAIS Goodluck Jonathan wa Nigeria (kulia).


hali ikawa mbaya zaidi,
jumla ya watu 2309 hadi
sasa wameshauliwa kwa
mwaka huu pekee. Hii ni
pamoja na lile mashuhuri
la kutekwa wasichana 300
wa shule ambapo mpaka
sasa pamoja na kelele za
Bring Back Our Girls
i k i we m o m i s a a d a ya
kikachero na kijeshi kutoka
Marekani, Israel na nchi za
NATO, bado wasichana
hao hawajapatikana.
Likini ukiacha
kupitishwa kwa sheria
hiyo kali, iliwekwa pia
mikakati ya kijeshi na
kikachero ambapo Nigeria
imekuwa ikipata msaada
mkubwa kutoka Marekani
katika kukabiliana na
kitisho hicho cha Boko
Haram. Lakini kila uchao
ndio hali inakuwa mbaya
zaidi kuliko jana yake.
Huo ndio uzoefu wa
Nigeria, Yemen, Pakistan,
Afghanistan n.k. Leo Rais
Uhuru Kenyatta anapokuja
na mkakati huu wa sheria
za ki-Patriot Act na kuwapa
matumaini Wakenya kuwa
itasaidia kuondoa tatizo
l a u g a i d i u n a o d a i wa
kufanywa na Al-shabaab,
labda angetoa mfano ni
nchi gani imefanikiwa
kutokomeza ugaidi kwa

k u we k a s h e r i a k a m a
hizo pamoja na kuwa na
vikosi maalum vya kutesa,
kuuwa na kupoteza watu.
Toka walikuwa
wakionekana kama
vijana hamnazo tu wa
mtaani wanaopiga porojo
ambapo difenda moja tu
ya FFU wenye mabomu
ya kutoa machozi ilitosha
kuwasambaratisha, hivi
sasa tunaambiwa Boko
Haram wana mpaka silaha
za kutungulia ndege na
magari ya kisasa ya kijeshi.
Mara kadhaa serikali
ya N i g e r i a i m e k u wa
ikiilalamikia Marekani
kuwa haiwapi silaha za
kisasa zikiwemo helkopta
za kijeshi ili kupambana na
Boko Haram!
Katika mazingira kama
haya, suala la kwanza
la msingi na muhimu
ilikuwa kumjua huyu Boko
Haram ni nani? Silaha na
wapiganaji anawapata
wapi? Je, haya matukio
yanayodaiwa kufanywa na
Boko Haram ambapo watu
wasio na hatia, wanauliwa,
ni kweli yanafanywa na
huyu Abubakar Shekau
na watu wake? Na huyu
Shekau ni nani na nani
anamfadhili?
Bila kujiuliza maswali

kama haya na kuyapatia


majibu ya uhakika, Nigeria
itaendelea kupigana na
boya (bogey man) na
kwa hiyo kila mkakati
itakaoweka hautasaidia
lolote katika kuondoa
tatizo.
Kenya ni hivyo hivyo.
Yanafanyika matukio,
tunaambiwa al-Shabaab
wamedai kuhusika. Kama
nilivyozungumza katika
makala yangu ya wiki
iliyopita, suala la msingi
hapa sio kuwa kama sheria
i n a y o p i t i s h wa i n a f a a
au haifai. Suala hapa ni
kujua uwepo wa hicho
kinachoitwa ugaidi katika
sura yake halisi. Maswali
ya msingi ni je, tunamjua
adui tunayepigana naye?
Ni adui wa kweli au wa
kufikirika? Adui yetu ni
nani? Au tunahangaika
na boya? Na boya hili
katutupia nani na kwa
malengo gani? Kwa nini
al Shabaab wawe maadui
zetu? Je, wana uwezo wa
kufanya waliyodaiwa
k u f a n ya We s t g a t e
Shopping Mall? Je, ni wao
waliovamia basi na kuuwa
abiria Wakristo 29? Kwa
nini kila ikitokea mauwaji
kama hayo inasisitizwa
kuwa waliwatenganisha

Wakristo na Waislamu.
Wa k r i s t o wa k a u l i wa ,
Waislamu wakaachiwa?
Fitna gani inajengwa
hapo?
Kule Iraq walikamatwa
makachero wawili wa
U i n g e r e z a wa k i l i p u a
s h a b a h a z a Wa s u n i
wakijifanya kuwa
wao ni wapiganaji wa
Kishia. Lakini hata yale
yaliyodaiwa mashambulizi
ya k u j i t o a m u h a n g a ,
ilikuwa ni makachero wa
namna hiyo wanaotegesha
mabomu katika gari,
linalipuka na kuuwa watu
halafu zinasambazwa
taarifa katika vyombo vya
habari kuwa waliofanya
mashambulizi hayo ni
magaidi wa kujitoa
muhanga wa Kishia au
Kisuni. Yote hiyo ilikuwa
ni katika kutekeleza ule
mkakati wa Salvador
Option ya kupandikiza
machafuko na mauwaji ya
Wasuni na Washia katika
Iraq, ili wasishikamane
kukabiliana na mvamizi.
(Tazama: From El Salvador
to Iraq: Washington's
man behind brutal
police squads. Tazama
pia Death-squad style
massacres For Iraq, "The
Salvador Option" Becomes
Reality-by Max Fuller)
Al-Shabaab inapambana
na jeshi la serikali ya
Somalia, al-Shabaab
inapambana na AMISOM,
al-Shabaab inapambana na
majeshi ya Kenya yaliyoko
Somalia, al-Shabaab
inapigwa na Marekani
kutoka angani kwa
kutumia Drone. Al Sahaab
hii ni jeshi la namna gani la
kushindana na nguvu zote
hizi? Je, yenyewe inapata
wapi silaha na uwezo wa
kukabiliana na nguvu zote
hizo?
Akizungumzia juu ya
utata katika hii inayoitwa
Vita dhidi ya Ugaidi,
Michel Chossudovsky
ameandika makala akihoji
ni nani Abu Musab AlZarqawi.
Katika utangulizi wa
makala na uchambuzi
wake huo, alikuwa na haya
ya kusema:
MIFUMO ya kijasusi
ya Marekani imeunda
asasi zake za ugaidi. Na
wakati huo huo, inaunda
tahadhari zake kuhusu
ugaidi kutokea kuhusu
makundi ya kigaidi
ambayo imeyaunda
yenyewe. Kwa njia
hiyo, imesuka mpango
wa mabilioni ya dola za
Marekani wa kupambana
na ugaidi, 'kuzifuata' asasi
hizo za ugaidi.
Propaganda ya
Inaendelea Uk. 12

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Mbunifu Mkuu mpya wa ugaidi' wa Jeshi la Marekani


Na Michel Chossudovsky,
June 11, 2004

MIFUMO ya kijasusi
ya M a r e k a n i i m e u n d a
asasi zake za ugaidi. Na
wakati huo huo, inaunda
tahadhari zake kuhusu
ugaidi kutokea kuhusu
makundi ya kigaidi ambayo
imeyaunda yenyewe. Kwa
njia hiyo, imesuka mpango
wa mabilioni ya dola za
Marekani wa kupambana na
ugaidi, 'kuzifuata' asasi hizo
za ugaidi.
Propaganda
ya
kupambana na ugaidi na ile
ya vita vinaendana. Mifumo
ya propaganda inaingiza
habari katika mtiririko wa
habari. Tahadhari za ugaidi
inabidi zionekane ni tishio
halisi. Lengo ni kuyaonyesha
makundi hayo ya ugaidi
kama 'maadui wa Marekani.'
Lengo la msingi ni kuinua
hamasa katika jamii kuunga
mkono agenda pana ya vita
ya Marekani.
'Vita dhidi ya ugaidi'
inahitaji uhalalishaji wa
k u wa s a i d i a wa t u wa l i o
taabani, vita dhidi ya ugaidi
inaonyeshwa kuwa ni ya
haki, ambayo inapiganwa
kwa misingi ya maadili
kurekebisha uovu uliotokea.
Nadharia ya Vita ya Haki
inatoa maelezo ya lipi 'jema'
na lipi 'baya.' Inawadhihirisha
n a k u wa u n d i a t a s w i r a
viongozi wa ugaidi kama
'watu waovu.'
Wadadisi na wachambuzi
MARA nyingi gazeti la Annuur, limekuwa likiandika
makala mbalimbali za
kuutahadharisha umma
wa Kiislamu juu ya wimbi
la jihad feki namna
lilivyoanzishwa, na namna
a m b a v y o l i m e wa a t h i r i
Waislamu kutoka maeneo
mbalimbali ulimwenguni.
Pamoja na jitihada hizo
katika kuwafungua macho
Waislamu, lakini bado baadhi
ya watu katika jamii ya
Kiislamu imekuwa ikipinga
na hata wakati mwingine kuja
na kauli za kashfa, vitisho na
matusi.
Mnamo tarehe 21 mwezi
Desemba 2014, bwana mmoja
mara baada ya swala ya
Adhuhur Katika Msikiti wa
wilaya ya Songea, alisimama
na kutoa mawaidha juu ya
jihad mkononi mwake akiwa
ameshika gazeti la An-nuur
lenye matukio mbalimbali,
moja likiwemo lile tukio la
Ustadh aliyefanyiwa vitendo
vya kudhalilisha na polisi
mpaka akafanyiwa upasuaji
katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Alidai kuwa Masheikh na
Waislamu katika Tanzania,
ni madhalili kwani hawana
uwezo wa kuthubutu kumiliki
silaha ilhali Maaskofu wao

Abu Musab al-Zarqawi ni nani?

wa ugaidi, Osama bin Laden,


Abu Musab al Zarqawi, na
wengine, ambao majina yao
na picha yanatolewa kila
uchwao katika taarifa za
habari.
Abu Musab al-Zarqawi
anaonyeshwa kwa
watazamaji kote duniani
kama mbunifu mkuu wa
ugaidi anayechipukia,
anayempa kivuli 'adui mkuu'
Osama bin Laden. Wizara ya
Mambo ya Nje ya Marekani
imeongeza dau la kukamatwa
kwake kutoka dola milioni 10
hadi dola milioni 25, ambayo
inaonyesha kuwa 'thamani
yake sokoni' ni sawa na ile
ya Osama. Cha kushangaza
ni kuwa Al Zarqawi hayuko
k a t i k a o r o d h a ya wa t u
wanaotafutwa sana na shirika
la upelelezi la Marekani, FBI.
Abu Musab al Zarqawi.
kadhaa wanaopinga vita
nchini Marekani, ambao
wamekuwa wakipinga
kwa dhati mwelekeo wa
utawala wa Bush, hata hivyo
wanaunga mkono nadharia
ya Vita ya Haki.
"Tunapinga vita vya aina
zote lakini tunaunga mkono
kampeni dhidi ya ugaidi wa
kimataifa."
Ili kufikia malengo yake
ya sera za nchi za nje,
matukio ya ugaidi inabidi
ya b a k i k a t i k a h i s i a z a

wananchi, ambao daima


wanakumbushwa kuhusu
tishio la ugaidi. Kampeni
ya propaganda inatoa picha
za viongozi walio nyuma ya
mitandao ya kigaidi. Kwa
maneno mengine, katika
ngazi ya kile kinachofanana
na kampeni ya kutoa
'matangazo ya biashara,'
inatengeneza uso kamili wa
ugaidi. "Vita dhidi ya ugaidi
inategemea kuundwa kwa
mmoja au zaidi ya watu
waovu-pandikizi, viongozi

Uhusiano wa Al Zarqawi na
Al Qaeda
Al Zarqawi mara nyingi
anatajwa kama 'mshirika wa
Osama,' mlundikiwa tuhuma
anayedaiwa kuhusika na
mashambulizi mengi ya
kigaidi katika nchi kadhaa.
Katika taarifa nyingine, mara
nyingi kutoka kwa vianzio
vile vile, inasemekana
kuwa hana uhusiano na Al
Qaeda na anafanya mambo
yake kama mtu huru. Mara
nyingine anaonyeshwa kama
mtu anayewania uongozi wa
Al Qaeda kushindana na bin

Achangisha fedha za kununulia


silaha kupigana Somalia, Syria

Apata shilingi 55,000 Songea mjini

kila mmoja anatembea na


silaha na hafanywi kitu
chochote na serikali.
Tatizo letu Waislamu ni
uwoga, alisisitiza bwana
huyo.
Mtu huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Abdallah Kesi,
aliwataka Waislamu kushika
silaha ili kuondosha dhuluma.
Pia aliwaasa kuwa endapo
mtu yeyote atakuwa tayari
kuungana na yeye kwenda
kupigana jihad Somalia au
ISIS Syria, amuone yeye na
atamuelekeza namna ya
kufika bila kukamatwa na
askari mipakani. Mwisho wa
mazungumzo yake aliwataka
Waislamu kufanya harambee
ya kuchangia ununuzi wa
tasbihi.
Mnazijua tasbih?
Aliuliza. Kisha alijibu
akasema ni risasi na bunduki.
Katika Msikiti wa
Manispaa ya Songea alipata

mchango wa kununua
tasbihi kiasi cha shillingi
55,000 na hivyo ndivyo
alivyofanya katika Misikiti
yote aliyozungumza hapa
Songea na mikoa mingine
kwa mujibu wa maelezo
yake.
Alichukua mawasiliano
ya wale wote waliokuwa
tayari kwenda jihad na
kuwaahidi kuwa, anakwenda
katika wilaya ya Tunduru
lakini wanatakiwa kufanya
maandalizi ya kwenda jihad.
Moja katika maandalizi hayo
ni kucheza karate Misikitini.
Ya p o m a s wa l i m e n g i
a m b a y o Wa i s l a m u n a
pengine vijana ambao tayari
wa m e k w i s h a t u m b u k i a
katika jahazi hilo la kwenda
jihad tunapaswa kujiuliza na
kupata majibu stahiki.
Kwanza je, tunajua kuwa
serikali yetu kwa sasa ipo
katika mapambano makubwa

dhidi ya ugaidi na uchochezi


wa aina yoyote utakaopelekea
uvunjifu wa amani, vipi mtu
kama huyu anayehamasisha
watu na kuchangisha fedha
kununua silaha kinyume cha
sheria na taratibu za nchi,
akavuka mikoa kadhaa pasi
hata na kukamatwa na polisi?
Je, vijana tunamjua na
tuna uhakika kiasi gani kuwa
yeye anawajua al Shabaab
na anayo mawasiliano yao?
Aliyapataje? Yeye anawajua
vipi ISIS na ni kwa njia zipi
atawapitisha bila kupitia
njia na taratibu za kinchi
za kiuhamiaji? Inakuwaje
mtu azungumze maneno
mazito kama haya na serikali
ya wilaya, mkoa na taifa
ipo, lakini anatamba kuwa
anazunguka nchi nzima bila
ya hofu? Nani anamlinda?
Au ndio mchezo ule ule
waliochezewa watu kule
Kagera wa kuwasakazia

Laden.
Jina lake linazuka mara
nyingi tu katika taarifa za
habari na za kiserikali. Tangu
mwanzo wa mwaka 2004,
yuko katika habari takriban
kila siku.
Osama anatoka familia
yenye nguvu ya bin Laden,
ambayo kihistoria ina
uhusiano wa kibiashara na
ukoo wa Bush na wanachama
wengine wa asasi za
uchumbaji mafuta jimbo la
Texas. Bin Laden alirubuniwa
na CIA wakati wa vita
vya Urusi na Afghanistan
na kupigana kama
mujahidina. Kwa maneno
mengine, kuna historia
ndefu iliyohakikishwa ya
mahusiano kati ya bin Laden
na CIA na mahusiano ya
kifamilia kati ya bin Laden
na Bush.
Tofauti na bin Laden,
Al Zarqawi hana historia
ya k i f a m i l i a . A n a t o k e a
katika familia maskini ya
ki-Palestina nchini Jordan.
Wazazi wake wamefariki.
Anatokea hivi hivi tu.
Anatakwa na CIA kama
'mbweha mpweke,' ambaye
anapanga vitendo nje kabisa
ya mtandao wa Al Qaeda.
Hata hivyo la kushangaza
ni kuwa 'mbweha mpweke'
huyu anaonekana katika
nchi kadhaa, nchini Irak
ambayo sasa ndiyo maskani
yake, lakini pia katika Ulaya
Magharibi. Pia anatuhumiwa
kupanga shambulizi la
kigaidi katika ardhi ya
Inaendelea Uk. 11
watu wajisajili kwenda jihadi
na yeye muhamasishaji
anakwenda kuandaa
mazingira na atakuja
kuwachukua, kumbe ndio
ikawa sababu ya kukamatwa
vijana walioitwa kuwa ni
magaidi ambao walijisajili
kwenda jihad Somalia?
Lakini hata kama ndio
tumepumbazwa na mvuto
wa Jihad Feki, hatufikirii na
kujiuliza, tuna uhakika gani
kwamba mtu huyo fedha
hizo anakwenda kununulia
silaha? Asiporudi, tutampata
wapi kudai pesa zetu? Hivi
ndio imekuwa Muislamu
anayeingia Msikitini
kuswali ndio awe mjinga wa
kutapeliwa kirahisi kiasi hiki!
Inasikitisha!
Mwisho naomba kuwaasa
Waislamu kuwa historia
k w e t u s i s i Wa i s l a m u ,
ingawaje ni muhimu sana,
lakini tumeifanya kama
simulizi za kale pasi na
kuchukua mafunzo yoyote.
Yapo maeneo mbalimbali
ambayo matukio mfano wake
yametokea na mwisho wake
umekuwa ni mbaya kwa wale
walioingia kwenye mtego.
Tusiwe wajinga kiasi cha
kushindwa kupambanua
mambo ambayo yako wazi
kiasi hiki.

10

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Wasifu wa Mtume (saw) kwa ukamilifu wake


Na Masoud Msellem

WAKATI tukiwa ndani ya mwezi


wa uzawa wa Mtume SAAW
tukikumbuka uzawa wake ni
muhimu kuangalia, wasfu, haiba,
dhati na shakhsiya ya Mtume
SAAW kwa uadilifu na kwa
ukamilifu wake. Kwa kuwa
kumfuata Mtume ni jambo la
wajibu kwetu basi ni wajibu
pia kuelewa kwa kina dhati au
shakhsiya ya Mtume wetu SAAW
ipasavyo.
Wasfu, haiba/dhati au shakhsiya
(personality) ya kila mtu
ulimwenguni akiwemo Mtume
SAAW hujengeka juu ya mambo
m a w i l i m a k u b wa : K wa n z a ,
hujengwa juu ya aqlia ya mtu
husika . Maana ya aqlia (mentality)
ni ile aina ya ufahamu anaoubeba
mtu, mtazamo jumla alionao, au
hukmu anayoitoa kwa mambo
mbali mbali yaliyomzunguuka
katika mazingira yake. Kwa
mfano, lau mtu anaona watu
wawili wanagombana kwa sababu
ya chupa ya ulevi, ambayo mmoja
wao aliichukuwa kutoka kwa
mlevi mwenzake bila ya idhini,
katika hali kama hiyo endapo
Muislamu atatoa hukmu kwamba
ugomvi huo ni batil, kwa kuwa
kinachogombaniwa ni ulevi
ambao ni haramu Hapo Muislamu
huyu huwa kaja na aqlia sahihi ya

SHEIKH Msellem
Kiislamu. Lakini lau Muislamu
ataseme kwamba aliyechukua
chupa ya ulevi kwa mwenzake
kwanza alipaswa kuomba idhini
ya mwenzake, kwa kuwa si milki
yake, hapo Muislamu huwa
hakubeba aqlia ya Kiislamu katika
qadhia hii.
Kitu cha pili katika shakhsia
na wasfu wa mwanaadamu ni
nafsiyah ya mtu husika. Nafsiyah

ni namna mtu anavyotenda


matendo yake ya kila siku kwa
mujibu wa aqlia aliyoibeba.
Kwa hivyo, ikiwa aqlia ya mtu
inamuelekeza kwamba ulevi ni
haramu, na akaacha kulewa, hapo
mtu huyu huwa kabeba aqlia ya
Kiislamu kwa kukubali kwamba
ulevi ni haramu, na pia kabeba
nafsia ya kiislamu kwa jambo hilo
kwa kujiepusha na ulevi.
Amma sura ya nje ya mtu
katika mavazi na mengineyo hayo
kamwe hayazingatiwi kuwa ni
sehemu ya shakhsiyah ya mtu
kama wanavyodhani baadhi
ya watu. Kiasi cha baadhi yao
kunadi wanapomuaona mtu
kavalia vizuri kwamba jamaa
ana shakhsiyah ya hali ya juu
(personality). Tunasema sura ya
nje kamwe haizangatiwi wala
si kigezo cha kufahamu dhati
na haiba ya mwanaadamu. Na
vigezo vya kuielewa haiba ya
mwanadamu havivuki zaidi ya
mambo mawili tuliyoyataja, yaani
aqlia na nafsia ya mtu. Aidha,
ikumbukwe kwamba shakhsiya ya
mwanaadamu ndio thamani yake
yote. Na kimsingi hiki ndicho kitu
kinachomtafautisha mtu mmoja
kwa nmtu mwengine.
M t u m e S A AW a l i k u j a
kutuonesha aina maalum ya
shakhsia yake iliyofinyangwa kwa
aqlia na nafsiyah ya Kiislamu, na
alifanya kazi kuwajenga Waislamu

wawe wamebeba shakhsiya hiyo


tukufu.
Shakhsiya aliyoijenga Mtume
SAAW na kushikamana nayo
ilikuwa juu ya msingi mmoja
tu wa kauli mbiu ya La ilaha
ila llah Muhamada-Rasululah
iliyoambatana na kufuata
sheria zote za Kiislamu. Kamwe
Mtume SAAW hakuwahi kuleta
mgongano baina ya aqlia na
nafsia yake. Yaani, hakuwahi
kutenda kinyume na ufahamu
alioubeba juu ya jambo fulani. Na
wala hakuifanya aqlia aliyoibeba
kuwa ni nadharia tu isiyokuwa na
vitendo (nafsiyah) .
Yeye alitandika aqliya ya
Kiislamu kutoka kwa Mola wake
na kuifanyia kazi kivitendo katika
mambo yote, na akauwajibisha
Umma wake kuigiza shakhsia
hiyo kwa kushikamana na sheria
zote za Kiislamu: Anasema Mtume
SAAW:Haamini kikweli mmoja
wenu mpaka matamanio yake
yafuate nilichokuja nacho mimi.
Kwa hivyo, kumkumbuka
Mtume SAAW na kumtukuza
haiba yake kusifungike tu kutaja
sifa zake kwa mdomo, bali
kudhihirike kwa kujifunga na
aqlia na nafsiaya yake tukufu
ambayo haijawahi kutokea mfano
wake na ambayo haikuwahi hata
mara moja kuathiriwa na fikra
chafu za kikafiri.

kuwa wanawakadhibisha Mitume


wote kwani hii ni kuonyesha kuwa
ujumbe wa Mitume wote ni mmoja.
Wote wamekuja kulingania katika njia
ya Mwenyezi Mungu na kumuabudu.
Amesema Mwenyezi Mungu ((Na
hatujamtuma kabla yako miongoni
mwa Mtume isipokuwa tulimletea
ufunuo kwamba hapana Mola apasae
kuabudiwa kwa haki isipokuwa
mimi . Hivyo niabuduni)) Surat
Anbiyai aya ya (25) kila Mtume
huja ili kukamilisha yale aliyokuja
mwenzie aliyepita kabla yake na
humuamini kwa yale aliyoyaeleza
na kuyasahihisha yale walioyaharibu
watu katika ujumbe wake bali
hubashiri juu ya Mtume atakayekuja
baada yake.
Kama alivyombashiria Nabii Issa
Bin Mariam, Mtume wa Mwenyezi
Mungu kwa kumbashiria ujio wa
Mtume Muhamad ambaye ni Mtume
wa mwisho na ni Nabii wa mwisho.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu (Hebu kumbuka pale
aliposema Issa bin Mariam, enyi
watoto wa Israil, mimi ni Mtume
wa Mwenyezi Mungu kwenu na
kuyasadikisha kwa yale yaliyo mbele
yangu miongoni mwa Taurati na ni
mwenye kubashiri kwa Mtume atakuja
baada yangu jina lake Ahmad Surat
Swaf (7) na kwa yakini amefananisha
Mtume Muhamad (s.a.w) mahusiano
ya Mitume baadhi yao na wengine
na mahusiano yao pale aliposema
(Mfano wangu mimi na Mitume
iliyopita kabla yangu ni mfano wa mtu

aliyejenga nyumba na akaipamba na


kuipendezesha isipokuwa sehemu ya
tofali moja pembezoni miongoni mwa
pembe zake, wakawa watu wanakuja
kulitazama na wanapendezwa nalo
na wanasema, laiti lingaliwekwa
tofali hilo, na mimi ni hilo tofali na
mimi ni Mtume wa mwisho.
Na muumini anaamini juu ya
umoja wa ujumbe wa Mitume na
wote hao, Imani yao ni moja, nao
ni kumpwekesha Mungu mmoja
na kuamini siku ya mwisho. Pia
anawajibika kujua kuwa sheria za
Mitume huwenda zikatofautiana
baadhi za hukumu na haya, ndio
aliyoyasema Mtume (s.a.w) kwa
neno lake (Mitume ni ndugu mama
tofauti lakini dini yao ni moja), Kwa
maana ya Imani yao ni moja pamoja
na kutofautiana baadhi ya sheria kati
yao.
Hivyo basi, pale anaposilimu
hapana budi kuamini Mitume yote
na kuwaheshimu na kujua haki
zao kwake na ajue mahusiano kati
ya Mtume na Mwenyezi Mungu
sio mahusiano ya kiadui au chuki
bali ni mahusiano ya mapenzi na
kukamilisha na kuaminiana. Hii
ndio Dini yetu ambayo imekusanya
kila ujumbe katika ujumbe
wake. Tunamshukuru Mwenyezi
Mungu kwa neema ya imani na
tunamshukuru Mwenyezi Mungu
ambaye ametuongoa kwa hili na
hatukuwa wenye kuongoka kama si
uongoaji wa Mwenyezi Mungu.

Kuamini Mitume ni nguzo miongoni mwa nguzo za imani

Na Dk. Abdallah
Daruwesh.
SHUKURANI zote anastahiki
Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa
ulimwengu na rehma na amani
zimfikie Nabii wetu Muhammad
(saw) mwisho wa Mitume na ndugu
zake wote miongoni mwa Manabii
na Mitume.
Ama baada ya utangulizi huu
mfupi:
Miongoni mwa uzuri wa dini yetu
tukufu na ni sifa za pekee ambazo
tunajivunia. Tunamshukuru na
kumsifu Mwenyezi mungu kwa hilo,
nalo ni kule kuweka miongoni mwa
nguzo za Uislamu za imani ambazo
hazitimii wala haikamiliki isipokuwa
kwa kuamini Mitume yote, nako
ni kuamini Mitume ya Mwenyezi
Mungu ambao amewaleta Mola

mlezi wa ulimwengu wa viumbe


wake, tangu wa mwanzo wa adamu
hadi Mtume Muhamad.
Mtume wa mwisho na ni Nabii
wa mwisho. Amesema Mwenyezi
Mungu Mtukufu (Ameamini Mtume
kwa yale aliyoteremshiwa kwake toka
kwa Mola wake mlezi na waumini
wote wanaoamini Mwenyezi Mungu
na Malaika wake na vitabu vyake
na Mitume yake. Hatumbagui hata
mmoja miongoni mwa Mitume
yake)
al- Bakarat, aya ya (285).
Na umetuamrisha Uislamu
kutangaza hivyo kwa Dunia nzima
akazema Mwenyezi Mungu (Semeni
tumemuamini Mwenyezi Mungu
na yale yaliyoteremshwa kwetu na
yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu
na Ismail na Ishaka na Yakubu na
asbatwi na yale aliyopewa Musa
na Issa na yale waliopewa Mitume
wengine toka kwa Mola wao mlezi.
Hatubagui hata mmoja miongoni
mwao na sisi kwake ni wanyenyekevu
Waislamu (Al-bakarat aya ya
136) na hukumu ya Uislamu kwa
yule atakaye mkanusha Mtume
mmoja tu, miongoni mwa Mitume
na akakataa kufanya toba hivyo
huhukumiwa kuwa ni kafiri na
mkanushaji. Amesema Mwenyezi
Mungu mtukufu (Wamekanusha
watu wa Nuhu Mitume yao Shuarau
(105) amesema tena (wamekanusha
watu waadi Mitume) Shuarai aya
ya 123) pamoja na kuwa kila watu
waliwakanusha Mitume yao tu.
Pamoja na hayo wakahukumiwa

11

Makala/Tangazo

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Mbunifu Mkuu mpya wa ugaidi' wa Jeshi la Marekani

Inatoka Uk. 9
Marekani. Anaonekana kuwa
katika sehemu kadhaa kwa
wakati mmoja. Anaelezwa
kuwa ndiye 'adui wa kwanza
wa Marekani,' 'bingwa wa
kubadilisha muonekano
wake na kubeba vitambulisho
feki.' Tunahimizwa kuamini
kuwa 'mbweha mpweke'
huyu anafaulu kuyapiga
chenga mashirika ya ujasusi
ya Marekani ambayo
yamesheheni wapelelezi
hodari.
Kwa mujibu wa gazeti
l a We e k l y S t a n d a r d ambalo linaaminika kuwa
na uhusiano wa karibu na
'wahafidhina mamboleo'
katika utawala wa Bush
(kwa mara ya kwanza makala
hii iliandikwa wakati Bush
bado yupo madarakani kama
Rais wa Marekani. Inarejewa
sasa kwa umuhimu wake.),
"Abu Musab al-Zarqawi ni
moto hivi sasa. Alisimamia
siyo tu kuuawa kwa Berg
lakini pia shambulio lililoua
watu wengi jijini Madrid
hapo Machi 11, kulipuliwa
kwa wa-Shia waliokuwa
wanasali nchini Irak mwezi
huo huo, na shambulio la
Aprili 24 la kujitoa mhanga
katika bandari ya Basra

(eneo la wa-Shia kusini ya


Irak). Ila si mgeni katika
mipango ya mauaji. Mapema
kabisa kabla ya 9/11, alikuwa
ameshatayarisha mpango
wa k u wa u a wa t a l i i wa
Israel na Marekani nchini
Jordan. Nembo yake iko
katika makundi ya kigaidi na
mashambulio katika mabara
manne."
(Inatoka katika Weekly
Standard, Mei 24, 2004)
Kuimarika kwa Al Zarqawi
"kunainua changamoto kwa
uongozi wa bin Laden wa
jihad ya kimataifa."
Nchini Irak, anasemekana
amepania "kuanzisha vita
ya j u m u i a k a t i ya wa Sunni na wa-Shia." Lakini,
kwani si hilo ndiyo lengo
la ujasusi wa Marekani
( k u g a wa n a k u t a wa l a )
ambayo inathibitishwa na
wachambuzi kadhaa wa
vita (ya uvamizi wa Irak)
inayoongozwa na Marekani?
Ni kupiganisha kundi moja
na jingine ili kudhoofisha
upinzani kwa uvamizi huo,
kwa mfano katika uchambuzi
wa Michael Collon kwenye
mtandao wa Global Research.
Shirika la ujasusi la CIA,
lenye bajeti ya zaidi ya
dola bilioni 30 kwa mwaka,

linasema halijui chochote"


wanasema hawajui chochote
kuhusu mtu huyu, wana
picha yake, ila kwa mujibu
wa Weekly Standard ya Mei
24, 2004, inaelekea hawajui
nini urefu wake au uzito.
Kuna wingu la sintofahamu
linalomzunguka mtu huyu
ambalo ni sehemu ya mikakati
ya propaganda. Zarqawi
anasemekana ni "msiri kiasi
kwamba hata baadhi ya
watu wanaoshirikiana naye
hawamfahamu ni nani."
Mpangilio unaoeleweka

Nini hasa nafasi ya


mbunifu mkuu mpya katika
kampeni za kueneza uzushi
za makao makuu ya Jeshi la
Marekani, Pentagon, ambako
shirika la utangazaji la CNN
linaonekana kuchukua nafasi
muhimu?
Katika jitihada za kuinua
vigezo vya propaganda,
CIA ilikodisha kampuni
za kujipendezesha katika
vyombo vya habari kupitisha
uzushi, ikiwa ni pamoja na
kundi la Rendon. Hawa
walishirikiana kwa karibu na
mbia wa Uingereza Hill and
Knowlton, ambayo ilihusika
na kashfa ya uzushi kuhusu
vyumba-joto (incubator )

vya Kuwait ambako


ilisemekana vichanga vya
Kuwait vilitolewa katika
vyumba joto na askari wa
jeshi la Irak lililovamia nchi
hiyo, vikatupwa sakafuni na
kuachwa kufa kwa baridi.
Habari hiyo ya kutungwa
kabisa ilitumika kupata
ridhaa ya Bunge la Marekani
kuingia katika vita vya Ghuba
vya mwaka 1991.
Nini mpangilio huo?
Ta k r i b a n m u d a h u o
huo baada ya shambulio
la kigaidi au tahadhari ya
uwezekano wa shambulio,
CNN inatangaza kimsingi
k u wa t u n a d h a n i h u y u
mtu asiyejulikana vyema
A b u Mu sab a l-Za rq awi
anahusika, na kila wakati
bila kutoa ushahidi na kabla
haujafanyika uchunguzi
wowote wa polisi na vyombo
vya kijasusi. Katika baadhi
ya matukio, pale shambulio
linapotokea, kuna taarifa ya
awali ambayo inamtaja Al
Zarqawi kama anadhaniwa
ndiye mpangaji. Taarifa
itasema kimsingi: ndiyo,

tunadhani alifanya, lakini


bado haijathibitishwa na
bado kuna wasiwasi kuhusu
wahusika wa shambulio hilo.
Siku moja au mbili baadaye,
CIA inaweza kujitokeza
na taarifa kamili, ikinukuu
vyanzo vya polisi, jeshi au
vya kijasusi, kuthibitisha
taarifa ya awali.
Mara nyingi tu taarifa
ya C N N i n a t o k a n a n a
habari zilizotolewa katika
kurasa za mitandao za
K i i s l a m u a u k u t o l e wa
kwa mkanda au mkanda
wa picha usiojulikana nani
ameutengeneza. Usahihi wa
mitandao au mikanda hiyo
siyo suala la kujadiliwa hapa
au la kufanyiwa uchunguzi
wa kina.
I k u m b u k w e k wa m b a
taarifa hizo hata siku moja
hazitaji kuwa Al Qaeda ni
kifaa kilichotengenezwa na
CIA na kuwa Al Zarqawi
alirubuniwa katika
mapambano wakati wa vita
ya Urusi nchini Afghanistan.
(Taarifa hizi zilithibitishwa
na Waziri wa Mambo ya
Nje Colin Powell katika
maelezo yake mbele ya
Baraza la Usalama la Umoja

Inaendelea Uk. 15

ABDULRAHMAN AL SUMAIT MEMORIAL UNIVERSITY-ZANZIBAR.


(SUMAIT University)
(FORMERLY, UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION-ZANZIBAR)

14 GRADUATION
TH

The Vice Chancellor of SUMAIT University - Zanzibar invites all graduands of the academic year 2013/2014
to the 14th Graduation. The Ceremony will be held on Wednesday 14th January 2015 at the SUMAIT
University premises - Chukwani. The Minister for Education and Vocational Training, Honourable ALI JUMA
SHAMUHUNA will be the Guest of Honour.
All graduands are required to confirm their participation to the Academic Office not later than Friday 2nd January
2015. Graduands are reminded to pay Tzs. 10,000/= (non-refundable) before Monday 12th January 2015 for
graduation gowns.
Please note that travel, meals and boarding expenses will be met by the graduands themselves. All graduands
are requested to report at the University by 3.00 pm on Tuesday 13th January 2015 for rehearsal and logistical
briefings. Graduands who will not participate in rehearsal will not be allowed to take part in the event.
For more information please contact SUMAIT University at the following address:
The Academic Office,
SUMAIT University Zanzibar
P.O. Box: 1933 Zanzibar.
Tel: +255242234102
Email: amacez@zitec.org; Website: www. ucez.ac.tz

12

MAKALA

'BOXING DAY' SI YAKO !

Boxing day nzuri, kutwa kucha kila kona,


Vyombo 'vyetu' vya habari, kuinadi vyakazana,
Kwa tashwishi ya ghururi, kuipa sura mwanana,
Si yako haikuhusu, haifai kushiriki !
Kuna tumbi vyatughuri, kwayo siku tena sana,
Kwa lugha ya uayari, na ya macho kufumbana,
Kuipa umashuhuri, lengo ipate kufana,
Asili yake ni nini, siku hii jiulize !
Pasipo kutafakari, wengi navyo twaungana,
Si nisai si rijari, wazee pamwe vijana,
Kwa Arafa utitiri, za simu kutumiana,
Muasisiwe yu nani, siku hii jiulize !
Zawadi kwanza nikiri, si haramu kupeana,
Halali pamwe vizuri, vinojuzu kupeana,
Taamu au dinari, mfano vya kupeana,
Iliasisiwa lini, siku hii jiulize !
Si kwa wangu uhitari, kwazo sifa nilonena,
Mia sitini nambari, na nane utaziona,
BAQARA 'ukivinjari', zimedokezwa bayana,
Malengoye hasa nini, siku hii jiulize !
Zawadi tangu dahari, si leo wala si jana,
Batini na kwa dhahiri, unasu walipeana,
Si kwa noeli kujiri, au kuzaliwa 'BWANA',
Yafungamana na nini, siku hii jiulize !
Kwa wenye njema nadhari, aula kukumbushana,
Mambo kuyatafakari, kwa marefu na mapana,
Pamwe kuyatadabari, si 'dogma' kulishana,
Walengwa wake ni nani, siku hii jiulize !
Akhui yatafakari, maswali hayo kwa kina,
Kwa bongo ya tabasuri, ukweli utauona,
Kwa kuimaizi siri, mwake ilofichikana,
Si yako, haikuhusu, haifai kushiriki !
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

Inatoka Uk. 8

kupambana na ugaidi na ile

ya vita vinaendana. Mifumo


ya propaganda inaingiza
habari katika mtiririko wa
habari. Tahadhari za ugaidi
inabidi zionekane ni tishio
halisi. Lengo ni kuyaonyesha
makundi hayo ya ugaidi
kama 'maadui wa Marekani.'
Lengo la msingi ni kuinua
hamasa katika jamii kuunga
mkono agenda pana ya vita
ya Marekani. 'Vita dhidi ya
ugaidi' inahitaji uhalalishaji
wa kuwasaidia watu walio
taabani, vita dhidi ya ugaidi
inaonyeshwa kuwa ni ya
haki, ambayo inapiganwa
kwa misingi ya maadili
kurekebisha uovu uliotokea.
Nadharia ya Vita ya Haki
inatoa maelezo ya lipi 'jema'
na lipi 'baya.' Inawadhihirisha
n a k u wa u n d i a t a s w i r a
viongozi wa ugaidi kama
'watu waovu.'
Ili kufikia malengo yake
ya sera za nchi za nje,
matukio ya ugaidi inabidi
ya b a k i k a t i k a h i s i a z a
wananchi, ambao daima
wanakumbushwa kuhusu
tishio la ugaidi. Kampeni
ya propaganda inatoa picha
za viongozi walio nyuma ya
mitandao ya kigaidi. Kwa
maneno mengine, katika
ngazi ya kile kinachofanana
na kampeni ya kutoa
'matangazo ya biashara,'
inatengeneza uso kamili wa
ugaidi. "Vita dhidi ya ugaidi
inategemea kuundwa kwa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Ukumbusho wa maadili kwa wanafunzi wote


NDUGU Mhariri
wa gazeti letu
tunalolipenda la Annuur, naomba nami
unipatie nafasi katika
gazeti lako tukufu nitoe
langu neno kuwaambia
wanafunzi wa Kiislam.
Wa n a f u n z i wa
Kiislamu wanatakiwa
kuvaa
mavazi
yaliyoidhinishwa na
waraka wa HIJABU
mashuleni, ili kuendana
na sheria za Kiislamu na
kufanya ibada wawapo
shuleni na hata nje ya
shule.
Mimi kama mzazi wao
nawakumbusha kuvaa
mavazi yanayotakiwa
au yanayoruhusiwa na
wizara kupitia waraka
wake wa wizara ya elimu.
Wanaume wanatakiwa

kuvaa suruali ambazo


sio mlegezo, ziwe pana
miguuni, shati ziwe
ndefu na pana na awe
na daftari la kuandikia
somo la Dini na kulitilia
mkazo kama masomo
mengine.
Ukumbusho wangu
kwa upande wa
wasichana, wanatakiwa
wavae sketi au suruali
ndefu mpaka miguuni
na shati la mikono
mirefu au nusu kanzu
ndefu na wala isiyobana
kulingana na sare ya
shule anayosoma
na majuba meupe
yanayofika katika fundo
za mikono sio yale
yanayoishia shingoni
au kifuani.
Kwa upande wa shule
ya msingi, wavulana

Rais Kenyatta anajua nini zaidi


wasichojua Wakenya wenzake

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya.


mmoja au zaidi ya watu
waovu-pandikizi, viongozi
wa ugaidi, Osama bin Laden,
Abu Musab al Zarqawi, na
wengine, ambao majina yao
na picha yanatolewa kila
uchwao katika taarifa za
habari.
Akizungumzia hali ya
mauwaji yanayoendelea
baina ya Wasuni na Washia,
mwandishi Marx Fuller
anasema maadhali Iraq
washaundiwa majinamizi
bogeymen kama Usama,

Zarqawi, al Qaida na
watu kama hao, watabaki
wa k i d h a n i k u wa a d u i
yao ni maboya hayo,
kumbe wanaowalipua ni
watu wengine kabisa ili
kupandikiza machafuko.
Na tunaambiwa kuwa
b a a d a ya m k a k a t i h u o
kufanikiwa, Iraq wakawa
wa n a l i p u a n a we n ye we
kwa wenyewe, wakakosa
nguvu ya kupambana
na adui mvamizi, ikawa
sasa makampuni ya

mafuta yanavuna mafuta


yanavyotaka bila sheria wala
utaratibu unaoeleweka wa
kibiashara.
Lakini zaidi tunaambiwa
kuwa nchi hiyo imewekewa
mikakati ya kubaki katika
utumwa daima dumu. Moja
ya mikakati hiyo tunambiwa
kuwa ni kuwekewa sheria
inayozuiya wakulima
kutumia mbegu zao za
asili. Wanatakiwa kununua
mbegu kutoka makampuni
ya mbegu ya Kimarekani.
Iraq has the potential
to feed itself. But instead of
developing this capacity, the US
has shaped the future of Iraq's
food and farming to serve the
interests of US corporations
the US has ensured that Iraq's
agricultural system will remain
under "occupation" in Iraq.
(Tazama: Iraq's new patent law:
A declaration of war against
farmers)
Iraq walipiganishwa na
mpaka sasa wanauwana
Mashia na Masuni baada ya
kufanikiwa ule mpango wa
Salvador Option. Nimeuliza
hapo juu, kwa nini yakitokea
m a u wa j i ya n a y o d a i wa
kufanywa na Al-Shabaab
inasisitizwa kuwa waliuliwa

wa n a t a k i wa wa va e
kaptula inayovuka
magoti na shati liwe refu
kuvuka kiuno na liwe
pana. Kwa upande wa
wasichana sketi ndefu
na shati pana lisilo bana
ili hata kama ikifika
muda wa kwenda
kuswali, iwe rahisi
kwenda kutekeleza
ibada hiyo kwa urahisi.
Kuanzaia darasa la
tatu mpaka darasa
la saba mwanafunzi
anatakiwa awe na
daftari la somo la dini,
ili aweze kuandika na
kujifunza kwa urahisi
kuandika na kusoma.
Mzee Mikidadi
Khalfani
Mzee wa maadili
mashuleni.
Wa k r i s t o w a k a a c h w a
Waislamu? Na kwa nini
hivi vinavyoitwa vikosi vya
serikai vya kupambana na
ugaidi vinalenga Masheikh
na Waislamu? Je, hakuna
harufu hapo kama ile ya
Washia na Wasuni Iraq?
We find it difficult to
understand how and why, in
spite of the U.S. presence in
Nigeria, with their sophisticated
military technology, Boko
Haram should be expanding
and becoming more deadly.
Anauliza swali hili
Prof. Adebowale Adefuye,
ambaye ni Balozi wa Nigeria
kule Washington, Marekani.
Swali hili alitakiwa Prof.
Adebowale Adefuye na
serikali yake, ndio watupe
majibu. Sio wasubiri kupata
majibu kutoka kwa watu
wengine.
Nimalizie kwa kusema
kuwa nadhani jambo la
msingi hapa ni kutafiti na
kujua ukweli wa mambo
kwa sababu inavyoelekea
tunapelekeshwa kupambana
na bogeymen kutumikia
masilahi ya mabeberu.
Sasa kama viongozi wetu
watakuwa wanalijua hili
lakini wakaamua kutufanyia
usanii wa kutuletea Patriot
Acts, huo utakuwa ni usaliti
wa hali ya juu. Swali ni je,

katika hali kama hiyo,


wananchi wafanye nini
kujinusru na kunusuru
nchi yao?

13
Na Juma Kilaghai

MOJA ya mafunzo ya
msingi kwa wanaosomea
fani ya udaktari wa meno
ni jinsi ya kujaza matundu
yaliyoko kwenye
meno. Madaktari hawa
watarajiwa wanafunzwa
kwamba ili kurejesha jino
lililotoboka katika hali
ya uzima, wanatakiwa
kusafisha tundu husika
kwa kulipekecha (drill),
kisha kulijaza tundu
hilo kwa mchanganyiko
maalum unaojumuisha
madini fedha na zebaki.
Kitaalamu mchanganyiko
h u u m a a l u m h u i t wa
ama silver amalgam au
mercury amalgam.
Hata hivyo katika hali
ya kushangaza, wanafunzi
hawa husisitiziwa kanuni
tatu kuhusu hii silver/
mercury amalgam. Kanuni
hizi ni: Hata siku moja usije
ukaigusa kwa vidole vyako
vitupu (bila kuvaa glavu).
Pili, hata siku moja usije
ukaicha inazagaa zagaa tu
bila kufunikwa; na tatu,
mabaki ya mchanganyiko
huu, au jino lililonglewa
lenye mchanganyiko huu,
ni lazima yaondolewe
katika mazingira kwa
kuzingatia kanuni kali
zinazosimamia uondoshaji
wa taka za sumu kali katika
mazingira.
Sababu kubwa ya
tahadhari hii ni ule
utambuzi kuwa madini
ya zebaki ni sumu hatari
pale yanapoingia mwilini!
Uzunguni kuna msemo:
Mad as a hatter. Hatter
ni mtu ambaye kazi yake
inayomuuingizia riziki ya
kila siku ni kutengeneza
au kushiriki katika
kutengeneza kofia za aina
ya hat, au heti kama
tulivyozoea kuziita kwa
kiswahili. Chimbuko la
msemo huu lilikuwa ni
ile hali ya ugonjwa wa
wa z i m u u l i o o n e k a n a
k u w a k u m b u k a
wafanyakazi wengi
waliokuwa wakifanya
kazi katika viwanda vya
kutengeneza kofia za heti
kwenye miaka ya 1,800
katika maeneo mbalimbali
ya Ulaya na Marekani.
Uchunguzi wa kisayansi
baadaye ulibaini kuwa
watu waliokuwa wanapata
uwendawazimu katika
viwanda hivi walikuwa
ni wale walioathiriwa
na mvuke wa zebaki.
Hii ni kwa sababu enzi
hizo kemikali iliyokuwa
ikijulikana kama mercury
nitrate ilitumiwa sana
k a t i k a v i wa n d a h i v i
kuondoa mabaki ya
m a n y o ya ya l i y o k u wa
ya n a g a n d i a n a k a t i k a
kofia hizi zilipokuwa
zinatengenezwa.
Katika viwanda vya leo
vya kutengeneza kofia za
heti matumizi ya zebaki
yamepigwa marufuku.

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

MATIBABU YA MENO YANAWEZA KUWA


CHANZO KIKUBWA CHA MARADHI MENGINE (1)!

Kwa akili ya kawaida tu


mtu ungetarajia kuwa
matumizi ya madini haya
yangepigwa marufuku
katika shughuli zozote zile
ambazo zina uwezekano
mkubwa wa kusababisha
madini hayo kuingia katika
mwili wa binadamu.
Hata hivyo katika hali
ambayo inaonyesha kuwa
kuna wakati hatujitambui
kabisa, matumizi ya zebaki
yameachiwa yaendelee
katika shughuli nyingine
kadhaa, moja ya hizo
ikiwa (unaweza kabisa
usiamini!), kuiweka
kwenye kinywa chako,
kama sehemu ya matibabu
ya meno!
K a t i k a
n c h i
zilizoendelea, baadhi
ya madaktari wa meno
wamekuwa wakiuliza
maswali mengi kuhusu
hali hii, hasa pale
wanapokutana na
ushahidi mwingi kuwa
matibabu haya yamekuwa
ni chanzo kikubwa cha
kuzorota kwa afya za
hao waliotibiwa! Hata
hivyo wengi wamekuwa
wakifanya hivyo kimya
kimya kwa hofu ya
kunyanganywa leseni zao
za kazi ya udaktari.
Dr. Hal Huggins,
mwandishi wa kitabu It is
all in your head ni mmoja
wa madaktari wachache
waliojitolea mhanga na
kuamua kupaza sauti zao
kuhusu suala hili. Katika
kitabu hiki anasimulia jinsi
ambavyo wagonjwa wake
wengi walipata nafuu
kubwa au kupona kabisa,
magonjwa yaliyokuwa
yanawasumbua, baada ya
michanganyiko ya madini
fedha na zebaki iliyokuwa
imetumiwa kuzibia meno
yao k uon d ole wa ! Dr.
Huggins ametaja baadhi
ya magonjwa haya kuwa
ni pamoja na:
1. Uharibifu wa utando
unaofunika mishipa ya
fahamu kuzuia umeme
unaopita katika mishipa
hiyo usije ukavuja na

kuelekea katika maeneo


ambayo hayakukusudiwa
(multiple sclerosis);
2. Ugonjwa wa
Parkinson (ugonjwa wa
mishipa ya fahamu (neva)
ambao hupelekea baadhi
ya viung o vya mwili
kutetemeka mfululizo bila
kudhibitika); na
3. Jongo kali la kutia
ulemavu (crippling
arthritis)
Kuna tafiti nyingi
ambazo zimebainisha
kuwa zebaki iliyowekwa
kwenye jino huwa inavuja
kidogo kidogo na kuingia
mwilini. Baadhi ya tafiti
hizi zimeonyesha pia
kuwa sehemu ya zebaki
inayovuja huelekea
kwenye ubongo na kubaki
huko. Baadhi ya watafiti
wanaamini kuwa hali
hii huchangia sana watu
kupatwa na maradhi ya
Alzheimer. Alzheimer
ni ugonjwa wa kupoteza
kumbukumbu kwa kiasi
kikubwa unaowakumba
sana watu wenye umri
mkubwa.
Kuna njia nyingi ambazo
zinaweza zikakusababishia
maradhi mbalimbali
i wa p o u m e p a t wa n a
tatizo la kuwa na sumu
ya zebaki katika mwili
wako. Moja ya njia hizo ni
kwa kuudhofisha mfumo
wako wa kinga za mwili.
Dakta David Eggleston wa
Chuo Kikuu cha Southern
California ni mmoja wa
watafiti ambao wameweza
kuthibitisha tukio hili bila
shaka kabisa.
Katika utafiti wake Dk.
Eggleston alipima kiwango
cha chembechembe za
T- LYMPHOCYTE katika
miili ya wagonjwa ambao
walikuwa na silver/
mercury amalgam katika
meno yao. T-lymphocyte
ni miongoni mwa chembe
nyeupe za damu zenye
mchango mkubwa katika
ulinzi wa mwili dhidi
ya m a a m b u k i z i . K wa
kawaida kwa mtu mwenye
afya njema kabisa kiwango

cha T-lymphocytes
ni kati ya 70% na 80%
ya chembechembe
z o t e n ye u p e a i n a ya
lymphocytes alizonazo.
Katika kesi moja wapo
Dk Eggleston alibaini kuwa
kiasi cha T-lymphocytes
kilichokuwa katika mwili
wa binti mmoja aliyekuwa
na umri wa miaka 21
ambaye alikuwa na meno
yaliyokuwa yamejazwa
kwa silver/mercury
amalgam kilikuwa ni 47%
tu ya chembechembe zote
za lymphocytes alizokuwa
nazo. Dk Eggleston
aliondoa silver/mercury
amalgam aliyokuwa nayo
binti huyo kinywani,
na baada ya zoezi hilo
kiwango chake cha
T-lymphocyte kilipanda
na kufikia 73%! Baada ya
tukio hili Dk Eggleston
alirejesha silver/mercury
amalgam kwenye meno
ya yule binti; na kiasi cha
T-lymphocytes kilishuka
tena hadi kufikia 55%! Dk.
Eggleston alimalizia kwa
kutoa tena silver/mercury
amalgam iliyokuwa
kwenye kinywa cha yule
binti na akajaza matundu
yaliyoachwa wazi kwa
aina fulani ya dhahabu
inayoaminika kuwa
salama kwa matumizi
hayo. Baada ya zoezi hili
kiasi cha T-lymphocyte
kwenye mwili wa yule
binti kiliongezeka tena
hadi kufikia 72%!
Pamoja na kwamba
kushuka kwa kiwango cha
kinga za mwili kunamweka
mtu katika hatari zaidi
ya kupata ugonjwa wa
saratani, na zebaki kwa
kupitia njia hii inaweza
kutuhumiwa kwamba
inasababisha saratani,
ukweli ni kwamba zebaki
ni kisababishi kikubwa cha
saratani bila hata kupitia
njia hii. Uthibitisho wa
hili unapatikana katika
kisa cha Dk Pinto. Huyu
alikuwa ni daktari wa
meno aliyeishi katika
miaka ya 1920.
Katika kisa hiki Dk Pinto
aliombwa kumtibu mtoto
aliyekuwa analalamika
kuwa ana maumivu
kwenye fizi zake. Mtoto
huyu pia alikuwa mbioni
kufa kutokana na kuwa na
saratani ya damu. Baada
ya kumchunguza Dk Pinto
aligundua kuwa meno
ya mtoto huyo yalikuwa
yamejazwa kwa silver/
mercury amalgam. Dk
Pinto aliamua kuondoa
silver/mercury amalgam
hiyo na mtoto akapata
nafuu kubwa. Dk Pinto

alipowaambia madaktari
wa mtoto huyo waliokuwa
wanamtibu saratani yake
juu ya kile alichokifanya
walikataa kumwamini. Ili
kuthibitisha madai yake
alirejesha silver/mercury
amalgam kwenye meno
ya yule mtoto; naye baada
ya muda mfupi alianza
tena kukumbwa na dalili
za saratani aliyokuwa
a n a u g u a h a p o a wa l i .
Pamoja na uthibitisho huu
madaktari wa mtoto huyo
waliendelea kushikilia
misimamo yao. Ili
kumsaidia mtoto Dk Pinto
aliamua kuwapuuza na
kuondoa silver/mercury
amalgam yote kwenye
kinywa cha mtoto, naye
baada ya muda mfupi
akapona saratani
iliyokuwa inamsumbua.
Tafiti za hivi karibuni
kabisa zimethibitisha
kuwa zebaki inasababisha
matatizo mengi sana ya
kiafya. Kwa mfano katika
utafiti uliofanywa na
serikali ya Sweden, serikali
iliweza kutambua kiasi cha
wananchi wa nchi hiyo
wapatao 250,000 ambao
walikuwa na matatizo
mbalimbali ya kiafya
yaliyokuwa na uhusiano
wa moja kwa moja na
silver/mercury amalgam
walizowekewa kwenye
meno yao. Mwaka 1994
kampuni ya Kijerumani
iliyokuwa inaitwa Degusa,
iliamua kufunga kiwanda
chake cha kuzalisha
silver/mercury amalgam.
Iliamua kufanya hivi
hadi hapo itapojiridhisha
kuwa eti mercury ambayo
n i s e h e m u ya s i l ve r /
mercury amalgam,
haina madhara! Degusa
ndiyo kampuni kubwa
kuliko zote ulimwenguni
inayojihusisha na
utengenezaji wa metali
(metals) mbalimbali
zinazotumiwa na
madaktari wa meno katika
tiba zao.
Ta f a d h a l i s a n a
b a a d a ya t a a r i f a h i i
usije ukakurupuka na
kukimbilia kwa daktari
yeyote yule wa meno
na kumwambia aondoe
silver/mercury amalgam
katika kinywa chako.
Sababu ya tahadhari hii
ni kwamba kazi hiyo
inapaswa kufanywa na
daktari mwenye ujuzi
wa kutosha na uzoefu.
Uondoaji wa kiholela
unaweza kukusababishia
KUMEZA zebaki nyingi
kwa muda mfupi kuliko
hata uliyokuwa unameza
kupitia silver/mercury
amalgam uliyokuwa
nayo kwenye meno
yako. Kumtumia daktari
mwenye ujuzi wa kutosha
na uzoefu unaweza
k u k a wa n a g h a r a m a
kubwa, lakini je, fedha
zako ni kitu gani, kama
afya yako iko kwenye
mashaka?

14

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

SIYO KILA WAKATI UFUMBUZI UKO KARIBU KIASI HIKI!


HAIIBA TIMAMU TEA: CHAI YA AJABU INAYOGUSA MATATIZO YA KIAFYA YA WATU WENGI
M A G O N J WA m e n g i
ya kimfumo (metabolic
diseases) husababishwa
na upungufu wa
virutubisho na viini
lishe muhimu mwilini
kama vile: Madini
lishe; Vitamini; Vizuia
vioksidishaji (Anti
oxidants); na Vijenzi vya
protini (Amino acids)
Ni mara chache sana
kupata bidhaa yenye
kujumuisha vitu vyote
hivi kwa wakati mmoja, na
kwa hivyo kuwa na uwezo
wa kugusa matatizo ya
watu wengi sana ya kiafya
kwa mara moja.
Miongoni mwa bidhaa
hizo chache ni HAIIBA
TIMAMU TEA. Hii ni chai
ya ajabu kabisa ambayo
imelundikana VIINI
LISHE NA VIRUTUBISHO
vifuatavyo:
1.AMINO ACIDS (VIJENZI VYA
PROTINI)
Arginine;
Histidine;
Isoleucine;
Leucine;
Lysine;
Methionine;
Phenylalanine;
Threonine;
Tryptophan; na
Valine.
2.VITAMINI NA MADINI
Carotine (Vitamin A);
Thiamin (Vitamin B1);
Riboflavin (Vitamin
B2);
Niacine (Vitamin B3);
Vitamin C;
Calcium;
Copper;
Iron;
Magnesium;
Phosphorous;
Potassium;
Zinc;
Chromium; na
Manganise.
3. VIZUIA VIOKSIDISHAJI
(ANTI OXIDANTS)




Curcumin;
Catechines;
Polyphenols;
Flavonoids; na
Piperine

4. VIUA VIJIDUDU
Cinnamaldehyde.
Mlundikano wa viini
lishe/virutubisho hivi
umepelekea chai hii kuwa

na msaada mkubwa katika:


Kudhibiti maumivu ya
viungo;
Kudhibiti uchovu na
kuondoa hali ya kujisikia
homa mara kwa mara;
Kudhibiti mfuro wa
seli (inflammation);
Kuimarisha kinga za
mwili;
Kusawazisha kiwango
cha lehemu (cholestrol)
mwilini kuwa cha kawaida;
K u d h i b i t i k a s i ya
kuzeeka;
Kuboresha usagaji wa
chakula tumboni;
Kuboresha siha ya
m f u m o wa d a m u n a
utendaji wa ini;
Kusafisha ngozi na
kuhifadhi mnyumbuko
wake;
Kupeleka virutubisho
muhimu kwenye ngozi;
Kuimarisha siha ya
macho;
Kuzuia kuongezeka
kwa seli za saratani;
Kuzuia seli za kawaida
za mwili kubadilika na
kuwa seli za saratani;
Kuuchochea mwili
wako kuangamiza
seli za saratani kabla
hazijasambaa mwilini;
Kuzuia uundwaji wa
mishipa ya ziada ya damu
kwa ajili ya kufikisha
virutubisho vya ziada
katika seli za mwili zenye
saratani;
Hupunguza shinikizo
la damu;
K u p u n g u z a
uwezekano wa kupata
shambulizi la moyo (heart
attack);
K u p u n g u z a
uwezekano wa mishipa ya
fahamu kupoteza utando
wa nje unaokinga sehemu
ya ndani na kwa hivyo
kuifanya ifanye kazi kwa
ufanisi (multiple sclerosis);
Kuongeza uzalishaji
wa nyongo;
Kuzuia uharibifu wa
lehemu nyepesi mwilini
kutokana na mwingiliano
na oxygen;
Kupunguza madhara
ya kisukari cha ukubwani;
K u p u n g u z a
dalili za ugonjwa wa
kupoteza kumbukumbu
(Alzheimers disease);
Kuharakisha kupona
kwa majeraha;
Kupunguza madhara

ya baridi ya yabisi;
Kupunguza kasi ya
ongezeko la virusi vya
ukimwi;
Kukinga dhidi ya
uharibifu wa ini;
Kukinga dhidi ya
sumu na makovu kwenye
mapafu;
Kukinga dhidi ya
ugonjwa wa ngozi kuchuja
rangi, yaani, vitiligo; na
K u s a f i s h a
kinywa dhidi ya bakteria
wasiotumia oksijeni
(anaerobic bakteria)
Chai hii inaweza
kukusaidia pia kama
unahisi kuwa unakabiliwa
na moja wapo ya hali hizi.
Hivi sasa inapatikana Dar
es Salaam pekee, katika
ofisi zetu zilizoko Mosque
Street, No. 1574/144
(mkabala na msikiti wa
Sunni), Kitumbini. Jitihada
zinafanyika pia ili kabla ya
mwisho wa mwaka huu
iwe inapatikana walau
katika miji yote iliyo makao
makuu ya mikoa Tanzania
nzima. Kwa maelezo zaidi
unaweza kuwasiliana nasi
kwa simu namba 075428
1131/0686281131/065528
1131.
KWA WALIOKO DAR ES
SALAAM
Kama unaishi Dar es
salaam unaweza kuja
hapa ofisini kwetu mtaa
wa Mosque, kwa ajili ya
kupata chai ya Timamu.
Tuko Kitumbini, mtaa wa
Mosque. Mtaa huu unaitwa
Mosque kwa sababu kuna
misikiti miwili mikubwa
inayoongozana (Ibaadh
na Sunni); ambayo
imetenganishwa na duka
la tamu-tamu la Taj Mahal
Sweet Mart.
Mtaa huu pia ni maarufu
sana kwa MGAHAWA WA
MIAKA MINGI SANA
UNAOITWA NEW ZAHIR
RESTAURANT (Tazama
picha. Jengo lenye canopy
yenye mistari myekundu.).
Iwapo utalazimika kuuliza
ili ufike Mosque Street, basi
waambie hao unaowauliza
ni mtaa iliko NEW
ZAHIR RESTAURANT.
Ukiweza kufika NEW
ZAIHIR RESTAURANT
utaiona hiyo misikiti
miwili tuliyoitaja iliko.

Kama hukuiona wewe


mwenyewe uliza! Ni hapo
jirani kabisa.
Sisi tunatazamana na
huo msikiti wa Sunni
(wenye minara ya kijani).
Aidha tuko jirani kabisa na
duka maarufu la vifaa vya
usafi na bidhaa nyingine za
majumbani la ZANZIBAR
S TAT E T R A D I N G
CORPORATION. Ukiona
mabango ya TRIPLE A
TAILORING SERVICES
yafuate, utakuwa tayari
umefika. HERBAL
I M PA C T , T R I P L E A
TAILORING SERVICES
NA NEOBIZ tunachangia
eneo la ofisi.
JINSI YA KUFIKA

1 . k wa wa na o t o k e a
m a e n e o ya M b a g a l a ,
Kurasini na Temeke ambao
wakija mjini kituo chao cha
mwisho cha daladala ni
Stesheni, basi waje mpaka
barabara ya Samora liliko
tawi la NBC SAMORA.
Mtaa wa Mosque unaanzia
NBC Tawi la Samora na
kupandisha kuelekea
juu hadi mtaa wa Libya.
Ili kufika ofisini kwetu,
ukitokea hapo NBC Samora
utavuka kwanza mtaa wa
India, kisha mtaa wa Indira
Gandi. Hapo utakuta hiyo
misikiti mikubwa miwili
inayoongozana.
2. Kwa wanaokuja mjini
kwa njia za Morogoro na
Ali Hassan Mwinyi, kituo
cha basi cha kushukia
n i A K I B A . B a a d a ya
kuteremka tembea hadi
kwenye maungio ya
Morogoro Road, ingia
Morogoro Road na uifuate
kama vile unaelekea
Bandarini zinakoegeshwa
Boti za kwenda Zanzibar.
Endelea mbele ambapo
utavuka mitaa ya Libya
na kisha Jamhuri mpaka
utakapokutana na tawi la
benki ya NMB la Morogoro
Road likiwa mkono wako
wa kulia. Hapo kata kulia
kuingia mtaa wa Mshihiri.
Ukiendelea mbele kidogo
utakutana na mtaa wa
Mosque unakatiza na
kushoto kwako utaiona

hiyo misikiti miwili.

3. Kwa wanaokuja na
barabara za Nyerere au
Uhuru hadi Mnazi Mmoja.
Ukifika mnazi mmoja vuka
mataa hadi liliko tawi la
benki ya NBC la Mnazi
mmoja. Hapo utakuwa uko
mtaa wa Jamhuri. Shusha
moja kwa moja na huo
mtaa hadi utakapokuta
kituo cha mafuta cha
Puma. Mbele kidogo ya
hicho kituo ni mtaa wa
Mosque unakatiza. Ukifika
hapo kwenye mauongio
ya Jamhuri na Mosque,
tazama kulia kwako utaona
hiyo misikiti miwili.
4. Kama unataka kuja
na gari lako Mwenyewe
ni bora uende hadi Samora
avenue uingie Mosque
Street kwa kutokea hapo
tawi la NBC Samora. Au
kama unatokea barabara
ya Nkrumah au Uhuru,
ukishafika Clock Tower
ingia mtaa wa India,vuka
mtaa wa Aggrey (kuna
kituo cha mafuta cha
GAPCO) na barabara
utakayokutana nayo
ikikatisha ni Mosque.
Hapo kata kushoto na
baada ya kuvuka Mtaa wa
Indira Gandi utaiona hiyo
misikiti miwili mkono
wako wa kulia.
Kwa watu wa mikoa ya
Tanga na Morogoro
Dawa inapatikana kwa:
A B D A L L A H
MWARABU
S I M U :
0 7 8 3 290921/0658-290921
BARABARA YA 12,
JIRANI NA MSIKITI WA
IBAADH
TANGA MJINI
DOTTO MALENDA
0715-282331
MTAA WA KARUME
(MKABALA NA MASJID
HAQ)
MOROGORO MJINI

15
Na Khatib Juma Mziray
KUTOKANA na makala
zangu nilizoandika awali,
kwanza nashukuru kwamba
z i m e p a t a wa s o m a j i n a
ushahidi ni ujumbe wa
m a n e n o n i n a o t u m i wa .
Naamini hii itakuwa njia
moja wapo ya kuelimishana
na kufahamiana kwa
manufaa yetu sote. Ni
watu wengi walionitumia
ujumbe kwa hiyo sitaweza
kuwataja wote au kunukuu
waliyosema, ila nitachukua
wachache tu kuwakilisha.
Labda nianze na huyu
ambaye anasema:
Habari ndugu yangu haya
unasungumza una ukweli
gani? Wakati mtafutia amani
leo mnawaona wabaya why?
Binadamu unataka nini?
Unataka uniambie alishabab
kawaagiza Bushi? Au inch za
Ulaya? Mnauwana wenyewe
alafu unawasingizia
wengine kisa tu imani yenu
inapingana hapana hauko
sawa kikulacho kiko nguoni
mwako. (0755 499 872)
Wa pili ameandika hivi:
Mziray umeandika vizuri
kuhusu joka na amani,
umesahau kuandika kuwa
Uislam umesambazwa
kwa ukatili kwani haukuja
Tanzania na pipi kwa hiyo
kama demokrasi ni uongo
hata Uislam ni uongo kwani
haukuleta amani. (0714 970
710)
Kwa wote hawa
niseme mambo mawili
ambayo nitayajengea hoja
k wa k u u l i z a m a s wa l i .
Afghanistan ni katika nchi
masikini duniani na iliyopo
nyuma kielimu. Haina
utaalamu wa namna yoyote
wa sayansi na tekinolojia ya
kisasa. Na hata nchi nyingi
za Kiarabu zipo hivyo
ukiacha utajiri wa mafuta.
Kwa upande mwingine

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Haja ni kuelimishana maana


hata ya Yesu yamepotoshwa

Marekani ni taifa kubwa


duniani kwa kila kitu. Wana
uwezo wa kurusha ndege ya
kivita ikapiga Afghanistan,
Somalia, Yemen na Pakistan,
na kurejea salama wakiwa
katika chumba cha komputa
Alabama. Hizo ndio Drone.
Ni nchi inayotumia mabilioni
ya dola kila mwaka katika
bajeti yake katika mambo
ya ulinzi. Makachero wake
wa CIA na wenye majina
tofauti tofauti wamesambaa
dunia nzima. Na nchi yao,
hasa katika sehemu maalum
na nyeti kama viwanja vya
ndege na idara zao za ulinzi,
zina mitambo ya ulinzi mimi
na wewe tusiokuwa hata na
uwezo wa kujua ukubwa
wa u we z o wa k e . H i v i ,
niwaulize, akili ya kawaida
inaweza kukubali kuwa mtu
kutoka milima ya Tora Bora
au jangwani Saudi Arabia,
anaweza kuingia Marekani
akateka ndege akapiga
WTC, akapiga mpaka Makao
Makuu ya Jeshi la Marekani
(Pentagon?)
Lakini tumeimbishwa
mpaka tumeyakubali kama
tunavyoimbishwa leo ya
Boko Haram na Al-Shabaab!
Katika Biblia tunaambiwa
kuwa Yesu amesema kuwa
hakutumwa ila kwa Wana wa
Nyumba ya Israel, kwamba
wamwabudu Mungu mmoja,
Mungu wake na Mungu
wao hao Bani Israel. Na
ndio maana hata akiwa pale
M s a l a b a n i t u n a a m b i wa
kuwa aliomba akimlilia
Mungu wake ili kama ni

kwa mapenzi yake kikombe


kile kimuepuke.
Lakini tumeimbishwa
kuwa Yesu ndiye Mungu
Mkuu na akili zetu na ndimi
zetu zinaimba hivyo hivyo.
Hivi kama alikuwepo
mkunga anamzalisha
Mariamu, angeambiwa siku
ile kuwa huyu anayezaliwa
ndiye Mungu wako mkuu,
akili yake ingeweza kuelewa
somo hilo? Mchukulie yule
babu aliyemtahiri Yesu
baada ya siku saba, hivi
angeambiwa kuwa huyu
unayemtahiri ndiye Mungu
wako Mkuu, akili yake
ingekubali? Yaweza kutolewa
hoja kuwa mambo ya Mungu
na mambo ya Biblia yamejaa
mafumbo na inapasa kuamini
kwa kujazwa roho. Lakini
kama akili haiwezi kutumika
kuelewa mambo ya msingi
kama haya ya imani, kazi ya
akili sasa itakuwa nini!
Mtume Muhammad
(s.a.w) aliwahi kumpa barua
Bw. Haarith bin Umar Aziz
ili aipeleke kwa Mfalme wa
dola ya Kirumi aliyeitwa
Heracleus. Alipofika Muttah
aliuliwa na Shurahbil
Ghassany aliyekuwa gavana
wa dola ya Kirumi. Kumuua
mjumbe ilikuwa ni kosa
kubwa sana kwa sheria ya
makabila ya Kiarabu kwa
wakati ule hata sasa kwa
sheria za kimataifa.
Tukio hilo lilisababisha
v i t a a m b a p o Wa i s l a m u
walikuwa na jeshi la watu
3,000 chini ya uamiri wa Zaid
bin Harith kwenda Mutta

kupambana na Gavana. Kwa


kifupi ni kuwa Wakristo
wa Waroma walikuwa na
jeshi la askari 100,000 kisha
wakaongeza wengine 100,000
wakawa 200,000. Warumi
walishindwa katika vita
hivyo. Wakristo Waroma
wa l i c h u k i a k u s h i d n wa
huko wakawa kila mara
wanaanzisha vita na nchi za
Kiislamu. Soma historia ya
kuhuisha Uislamu uk. 385.
Je! Mwadhani ya kwamba
nimekuja kuleta amani
dunuani? La, sivyo, bali
mafarakano. Kwa kuwa tokea
sasa katika nyumba moja
watakuwamo watu watano
wa m e f a r a k a n a , wa t a t u
kwa wawili, wawili kwa
watatu. Watafarakana baba
na mwanawe, na mwana na
babaye; mama na binti yake,
na binti na mamaye; mkwe
mtu na mkwewe, mkwe na
mkwe mtu. (Luka 12:51-53.)
Haya ni maneno ya
Biblia ambapo Injili hiyo
imeandikwa na Luka mwaka
wa 80 baada ya Yesu kuondoka.
Luka alizaliwa Antiokia
(Ugiriki), alikuwa Dakitari,
hakuwa mwanafunzi wa
Yesu. Alikuwa mpagani, si
Myahudi. Soma utangulizi
wa Injili kama ilivyoandikwa
na Luka, katika toleo la Biblia
za Imprimatur. Aliandika
kutokana na masimulizi ya
watu waliomwona Yesu,
kama kuna waliomwambia
uongo hayo hatujui.
Kwa kuwa watu wengi
wametia mikono kutunga
kwa utaratibu habari za

yalifadhiliwa na CIA. Kwa


uhakika, washiriki kadhaa wa
utawala wa Bush wakiwemo
Richard Armitage na Colin
Powell walihusika moja kwa
moja kupeleka misaada kwa
Al Qaeda nchini Afghanistan,
ambako bin Laden na Al
Zarqawi walipata mafunzo
maalum.

majina bandia mengine).


Kwa mujibu wa gazeti la
New York Times, Al Zarqawi
alikimbia Pakistan kwenda
Iran mwishoni mwa mwaka
2 0 0 1 b a a d a ya k u i n g i a
kwa majeshi ya Marekani.
Taarifa rasmi za Marekani
zinaashiria kuwa alikuwa
analindwa katika ngazi za juu
za serikali ya Iran.
"Maofisa wa mashirika
ya ujasusi ya Marekani
wanaingiwa na wasiwasi
kuhusu
ushahidi
unaoongezeka wa shauku
ya ugaidi miongoni mwa
wa t a wa l a wa I r a k ( n a
kumsaidia Al Zarqawi),
ikiwa ni pamoja na upelelezi
wa chini kwa chini wa
mawakala wa Iran wa vituo
vya ki-Marekani nchi za nje
ambavyo vinaweza kulengwa
kulipuliwa.. Maofisa wa
Marekani wanasema Iran

inaelekea kuona ugaidi


kama moja ya njia za kuizuia
Marekani isifanye shambulio
dhidi ya Iran.
Tangu tukio la kushangaza
la kuchaguliwa kwa
Mohammed Khatami kuwa
rais wa Iran mwaka 1997
na kuungwa mkono katika
maeneo mengi na watu
nchini humo, watawala
nchini Marekani wamekuwa
wanategemea kuinuka kwa
tabaka jipya la uongozi
lenye mwelekeo wa wastani.
Lakini kundi la wahafidhina
limeendelea kushikilia asasi
za ulinzi na usalama za
Iran, na kukwamisha juhudi
za Marekani kupunguza
misuguano na Iran.
Sasa, vitendo vya Iran vya
kukwamisha serikali mpya
ya mpito nchini Afghanistan,
utayari wake kusaidika
wanachama wa Al Qaeda na

mambo yale yaliyotimizwa


katikati yetu.
Kama
walivyotuhadithia wale
waliokuwa mashahidi wenye
kuyaona, na watumishi wa
lile neno tokea mwanzo,
nimeona vema mimi nami,
kwa kuwa nimejitafutia
usahihi wa mambo hayo
yote tangu mwanzo,
kukuandikia kwa utaratibu,
Theofilo mtukufu, upate
kujua hakika ya mambo yale
uliyofundishwa. (Luka
1:1-5)
Huenda ndiyo maana
baada ya Paulo kuanzisha
dini ya Ukristo kule Antiokia
(Ugiriki) miaka 14 baada ya
kuondoka Yesu. (Matendo
11:26); Wenye dini wakaona
kuwa wanaruhusiwa
kufarakanisha watu kama
tunavyoona kila mahali
dunia nzima. Ndugu yangu
muuliza swali la amani;
mwaka wa 1096. Mkristo
mkereketwa (siasa kali) jina
lake, Peter the Hermit alienda
kwa Papa Urban II, akaomba
kibali ili aruhusiwe akusanye
jeshi ili aende Mashariki ya
Kati awaue Waislamu; Papa
akampa kibali, akazunguka
nchi za Ulaya kukusanya
jeshi wakiwemo ALSHABAB (vijana) wa kiume
na wakike hata wenye miaka
14, wakaenda wakaanzisha
Crusades (Vita vya Msalaba).
Pia walikuwako wengi
kati ya Waislamu ambao
walitaka kuishi na amani
kati yao naWakristo; vile vile
Wakristo wenye mashamba
eneo za Mashariki waliona
haja ya kupatana. Lakini,
maaskari (MA-ALSHABAB),
waliotoka nchi za Magharibi
wa l i t u m a i n i k u wa o k o a
(KUWACHINJA) Waislamu
wote kwa upanga, wakaacha
chuki kati ys Waislamu na
Wakristo hata siku hizi zetu.
Kitabu cha Historia ya Kanisa
cha Canon H.J.E. Butcher uk.
86-87.
Itaendelea lijalo

Mbunifu Mkuu mpya wa ugaidi' wa Jeshi la Marekani


Inatoka Uk. 11

wa Mataifa hapo Februari


5, 2003, inayozungumziwa
punde). Osama bin Laden
na Abu Musab al-Zarqawi
ni vifaa vilivyotengenezwa
na mashirika ya kijasusi
ya Marekani. Kurubuniwa
kwa wapiganaji kutoka nje
(katika vita vya Urusi nchini
Afghanistan) kulifanywa
chini ya uangalizi wa CIA.
Vyombo vya habari kwa
kawaida vinatoa tahadhari
hizo zinazotokea CIA kama
za kweli, bila kukiri kuwa
mashirika ya kijasusi ya
Marekani yametoa misaada
ya siri kwa mitandao
ya makundi ya Kiislamu
kwa zaidi ya miaka 20. Hii
imethibitishwa kwa kina,
kuwa makambi ya kutoa
mafunzo nchini Afghanistan
yaliyoundwa wakati
wa utawala wa Reagan

Historia ya Al Zarqawi
Mara ya kwanza jina
la Abu Musab al Zarqawi
linatajwa ilikuw ni kuhusiana
na jaribio lililoshindwa la
kushanbulia Radisson SAS
Hotel jijini Amman, Jordan
wakati wa maadhimisho
ya milenia mwezi Desemba
1999, Kwa mujibu wa taarifa
za habari, alikuwa kabla
anatumia jina tofauti: Ahmed
Fadil Al-Khalayleh (inaelekea
likiwa ni mojawapo kati ya

kuchochea uamsho katika


maeneo ya Wapalestina
vinasababisha Marekabni
ipitie upya mahusiano
yake na Iran," kwa mujibu
wa maofisa wa serikali
walionukuliwa na gazeti
la New York Times, Machi
24, 2002.
Mwaka 2002, uwepo
wake nchini Iran, akidaiwa
"kushirikiana na watu wa
siasa kali" katika jeshi
la Iran na vyombo vya
ujasusi ni sehemu ya
mtiririko unaobadilika wa
kampeni potofu ambazo
zina lengo la kuonyesha
kuwa Iran ndiyo mfadhili
wa 'mitandao ya kigaidi ya
Kiislamu.' Mwezi Februari
2001, alidaiwa kuhusika na
kupanga shambulizi ndani
ya Israel. (Itaendelea)

AN-NUUR

16
16

16

MAKALA

AN-NUUR

Soma
gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

SAFAR 1436, IJUMAA DES. 26, 2014-JAN. 1, 2015

Kinyozi aiangusha CCM Mkuza


Bakari Mwakangwale

KIJANA Joseph Rapahel


Kambona, (26) ambaye
ni kinyozi, ameibuka
mshindi katika nafasi ya
Uenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Mkuza, katika
mji wa Kibaha mkoani \
Pwani kupitia chama cha
Chadema kwa kumbwaga
mgombea wa CCM.
Ushindi
huo
umewagusa watu wengi
n a k u t a f s i r i wa k u wa
chama tawala, Chama cha
Mapinduzi (CCM), hakina
j i p ya k wa wa n a n c h i
ambao wamefanya
maamuzi ya kumpa ridhaa
ya kuwaongoza kijana
huyo anayejishughulisha
na usafi wa vichwa vya
wananchi mtaani hapo.
Akiongea na mwandishi
wa gazeti hili, Bw. Joseph
R. Kambona, alisema
ushindi huo kwake ni
kama nyota ya jaa kwani
kuiangusha CCM si jambo
dogo ukizingatia kuwa
yeye ni kijana mdogo, tena
kinyozi.
Hii ni kama nyota
ya jaa, mimi ni kinyozi
ndio shughuli yangu
inayoniweka hapa
mtaani, lakini wananchi
wamenikubali na
kuniamini kupitia
upinzani nadhani ushindi
huu ni kutokana na wao
(wananchi) kuchoshwa
na utendaji mbovu wa
viongozi wa CCM.
Alisema Bw. Kambona.
Akifafanua zaidi
alisema, kukithiri kwa
kero za wananchi katika
mitaa yao au vijijini,
kama vile uhaba wa maji,
kukosekana kwa huduma
z a a f ya , m a t a t i z o ya
elimu ni mambo ambayo
yamewafanya wananchi
kuichoka CCM.
Bw.
Kambona
alisema, viongozi wa
CCM wamekuwa
wakitoa ahadi nyingi
kila uchaguzi unapofika
na kuwatumainisha
wananachi, lakini
utekelezaji wake baada
ya k u p e wa d h a m a n a
unakuwa hadithi.
Alisema, yeye pamoja na
timu yake ya walioshinda
nafasi za ujumbe, wana
dhima ya kuwatumikia
wananchi kwa haki
na uadilifu ili kuweza

kuwafikisha wananchi
katika matarajio yao ya
kimaendeleo.
Akizungumzia
matarajio yake katika
uongozi wake alisema,
kwanza wataanza na kuzifuta
tozo za kero ambazo ni
kero kwa wananchi, kwa
kutakiwa watoe pesa ili
waweze kupata huduma
kutoka ofisi ya Serikali yao
ya Mtaa.
Moja ya ahadi yetu
ambayo wananchi
wanaisubiri kwa hamu
ambayo imekuwa ni kikwazo
kufanikisha mambo yao
mengi ni kufuta tozo za kero
kwa wananchi, kama vile
kupata huduma ya muhuri
wa Serikali ya Mtaa, ili uweze
kupata huduma za kijamii
katika sekta mbalimbali.
Au unataka uchukue
mkopo inahitajika barua ya
utambulisho au kufungua
akaunti benki sasa huduma
hizo zitakuwa bure
hazitochajiwa kiasi chochote
kwani hii ni moja ya kero
kubwa kwa wananchi
hivi sasa. Alisema Bw.
Kambona.
Alisema wapinzani
wamejipanga kuanzia ngazi
ya chini kwa kujua kwamba
ndiko kuna wapiga kura
na ndio msingi wa CCM,
hivyo wamebaini kuwa
wakiwaelimsha wakajua
wajibu wao kuelekea katika

mageuzi, hata ngazi za juu


itakuwa ni rahisi.
Siku zote CCM msingi
wao ni watu wajinga,
wa s i o e l i m i k a a m b a o
wapo huku mitaani na
vijijini, kwa hiyo kama
tukiwaelimisha hawa na
kuweza kuwaangusha
huku chini naamini
mwaka 2015 itakuwa
rahisi kuwaangusha CCM
katika ubunge, udiwani
hata urais. Alisema.
Kwa maana hiyo
a k a s e m a , wa m e a n z a
kushambulia ngazi ya
chini kwa hoja na kwa
ushindi wa vyama vya
upinzani (Ukawa) katika
sehemu mbalimbali ni
wazi wananchi wameanza
kuelewa na kuelimika.
Bw. Kambona, alisema
wana mkakati wa
kusimamia na kuhakikisha
fursa za wananchi ambazo
wamezipoteza kwa kipindi

kirefu sana, kupitia mtaa wao


wanazipata bila mizengwe
tofauti na awali chini ya
uongozi wa CCM.
Kwa mfano kwa sasa
hatuna huduma za afya
(Zahanati), hakuna Shule
wakati kuna ongezeko kubwa
la wakazi ambao wanahitaji
huduma hizo kuwepo kwa
sasa.
Katika hili kigezo cha
kwanza ni watu ambao
wapo wa kutosha, lakini pili
ardhi ipo kinachohitajika
ni Serikali ya Mtaa kufanya
mchakato kuangalia suala
hilo linanatekelezwa vipi,
kwani wajibu wa viongozi ni
kuwajibika kwa wananchi
na kuwatumikia. Alisema

Bw. Kambona.
Alisema, kwa sasa
wa n a n c h i wa m t a a wa
Mkuza wanafata huduma
za afya katika Zahanati ya
Serikali iliyopo kijiji cha
Mwendapole, umbali wa
kilomita zipatazo tatu wakati
shule ya msingi watoto
wanakwenda vijiji vya jirani
umbali wa kilomita nne.
Kwa upande wake
Bw. Kassim Abdallah
Mkwenya, aliyepata ridhaa
ya wananchi kwa nafasi ya
ujumbe, alisema uongozi
uliopita wa CCM haukuwa
unazingatia utawala bora
kwa kuwatumikia wananchi.
Kwanza alisema,
hapakuwa na mikutano

ya wananchi, ya kueleza
mapato na matumizi kwa
wananchi walio waweka
m a d a r a k a n i i s i p o k u wa
ukaribu wao na wananchi
huwa pale wanapohitaji
kura zao na huishia pindi
matokeo yanapotangazwa
na wao kuibuka washindi.
Sisi tutawajibika
kwa wananchi tutaitisha
mikutano na kueleza mapato
na matumizi kwa uwazi
kwa mujibu wa sheria, ili
kujenga imani kwa wananchi
kama tulivyoahidi pia
tutawashirikisha katika
vikao vya maamuzi ya
maendeleo ya mtaa wao.
Alisema Mjumbe huyo.

IPO KWA HUDUMA MBALIMBALI ZA KIBIASHARA NA MAENDELEO KAMA:


1. Kutengeneza mipango ya biashara (Business Plans)
2. Kuandaa michanganuo kwa ajili ya kuombea mikopo (Loan Documents)
3. Kuandaa maandiko ya miradi (Project Write-ups)
4. Kutengeneza mipango mkakati ya taasisi (Strategic Planning)
5. Kutengeneza miongozo ya fedha na uendeshaji katika taasisi (Financial and
Operational Manuals)
6. Kuandaa katiba kwa ajili ya usajili wa vyama na taasisi zisizo za kiserikali
(NGOs)
7. Kufanya usajili wa kampuni/Jina la biashara
8. Kufanya usaili kwa waajiriwa watarajiwa
9. Kuandaa nyaraka za zabuni (Tender documents
10.
Huduma za ushauri kwa wahitimu wa vyuo wanaosaka ajira (Coaching
services)
11.
Nakadhalika.
KARIBU: MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA
NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI DAR ES
SALAAM.

You might also like