Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 20

Mpenzi msomaji kuanzia Februari 19, 2015 ANNUUR litapatikana kwa Shs 800/= tu

JINAMIZI LA UDINI TANZANIA:

Sauti ya Waislamu

Sheikh Suleiman Takadir,


Askofu Makarios

ISSN 0856 - 3861 Na. 1164 RABIUL THANI 1436, IJUMAA , FEBRUARI 13-19, 2015 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uk.14

Al-Shabaab asilimisha wafungwa Segerea


Aliingia Collins atoka akiwa Muhammad
Sheikh Msellem ampa Kalima Shahada

MUHAMMAD Javan Omundi, Mkenya aliyesilimu


akiwa gerezani Segerea Jijini Dar es Salaam.

Ghasani, hili ndio kosa la Wazanzibari.

Kila uchochoro Mji Mkongwe


akina William wanaona gaidi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman
Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman, wakati
wa ziara yake nchini humo mwaka jana.

CCM imefeli Visiwani

Ila kama ni balaa wataleta Wazungu na


Wanaopiga kampeni za chuki kanisani
Sio hizi porojo za Waarabu wa Oman

CUF yahitaji kubadilika haraka


La sivyo itakuwa haichaguliki

IPO haja kwa CUF


kubadilika haraka
iwezakanavyo, la
sivyo, wafuasi wake
wataikimbia, ingawa
hawatarejea CCM.
Zanzibar wanahitaji
mabadiliko.

Wanahitaji na kutaraji
vyama vyao vya siasa
wanavyoviamini na
k u v i k u b a l i k u wa
vitawafikisha pazuri.
Lakini huenda
watakubali wasipige
kura au wauze

vipande vya kupigia


k u r a k wa v ya m a
vyengine.
Maana vyama
vyote viwili, CUF
na CCM, vyaelekea
kufanana kwa kila
hali! (Soma Uk.8)

MHE. William Lukuvi

MMOJA wa waliokuwa
Masultan wa Zanzibar.

Tahariri/Makala ya Mtangazaji
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Valentine, ni ufuska, uovu mtupu!


KILA ifikapo tarehe 14
Februari ya kila mwaka,
watu sehemu mbalimbali
duniani wamekuwa
wa k i s h e r e h e k e a a m a
kuadhimisha siku
iliyobuniwa na kubatizwa
na kuitwa siku ya
wapendanao (Valentine
Day).
Historia inatueleza
kuwa asili ya sherehe
hiyo ya wapendanao ni
sherehe ya wapagani wa
Kirumi, wakati dini yao ya
upagani ilikuwa ndio dini
iliyotapakaa kwa Warumi
karne zaidi ya kumi na
saba zilizopita, na fikra zao
ilikuwa ni kuelezea hisia ya
mapenzi ya kiroho.
Tu n a f a h a m i s h wa
kwamba siku hii iliwekwa
na watu fulani kwa ajili ya
kumkumbuka mtu mmoja
kwa jina la Mtakatifu
Va l e n t i n o , a m b a y e
tunaelezwa kuwa aliuawa
kwa kukiuka matakwa ya
watawala wa wakati wake,
k wa s a b a b u a l i k e m e a
baadhi ya mila zao na
akawa anafungisha ndoa
zilizopigwa marufuku
katika wakati huo.
Tu s e m e t u k wa m b a
siku hizi watu wamekuwa
hodari wa kutunga
na kuidhinisha siku za
maadhimisho na kuzipa
tafsiri na matumizi tofauti
kiasi cha kukidhi matakwa
yao. Watu wengi huzipa
siku matumizi kwa jinsi
wanavyoona wao. Kwa
mfano, kuna siku huwa
zinaitwa za vunja jungu
a m b a z o z i m e t u n g i wa
kipindi chake. Nacho ni
kabla ya kuanza mfungo
wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani na baada ya
kumaliza funga.
Siku hizi zimefanywa
kuwa siku maalum kwa
wachafuzi kutenda kiasi
cha kukinahi maasi. Watu
h u z a m i a k i s a wa s a wa
katika maasi na kuogelea
katika mambo maovu.
Kibaya zaidi, hata vyombo
vya habari hupamba siku
hizo, utafikiri za maana
sana.
Ukisikiliza stesheni
za redio hapa nchini,
watangazaji hawawezi
kuanza na kumaliza
vipindi bila kuchombeza
m a s u a l a ya m a p e n z i
kuelekea Valentine. Wao

wamekuwa ndio wapiga


debe wakubwa wa mambo
kama haya, ambayo ilikuwa
si maarufu miongoni
mwa Watanzania wengi.
Watangazaji wanashinikiza
dhana hii kwa kuwaambia
wapendanao hawa
yanayofanywa wakati wa
siku hizi hapa kwetu, nayo
ni kwa wapenzi kwenda
ufukweni kupunga upepo
au kwenda kwenye
majumba yanayoitwa ya
starehe.
Wa n a o n g e a k a t i k a
hali ya kuamsha hisia
fulani miongonni mwa
wasikilizaji wao, na ni
hisia hizo hizo za uzinifu.
Wakiongea upuuzi na
mambo yasiyo na faida
kwa jamii.
Siku hizi jamii imefikia
hatua ya kuhamisha
uhalisia wa maadhimisho
ya siku za kiimani na
kuzigeuza kuwa siku za
kufanya upuuzi zaidi.
Hakuna tofauti ya sikukuu
au maadhimisho kwa watu
wa imani moja na nyingine,
japo kuna tofauti ya namna
ya kufanya maadhimisho
na hata makusudio
ya kuadhimisha au
kusherehekea.
Kwa kushindwa
kukabiliana na mwenendo
huu, jamii sasa imebadilika
na kupoteza mwelekeo.
Mambo ya upuuzi ndiyo
yanayoonekana ya msingi
na muhimu kuliko yale ya
kiungwana. Upuuzi ndio
umekuwa fasheni, kwa
sababu sehemu kubwa ya
jamii imebadili mwelekeo
na kuegemea katika
mambo ya kipuuzi.
Tukitizama kwa makini,
utagundua kuwa watu
wanaisubiri kwa hamu
hiyo siku ya Valentine, ili
washawishike kupendana
zaidi, lakini si mapenzi
halali, bali uzinzi. Vyumba
vya mahoteli na nyumba
za kulala wageni vitajaa,
baa zitatapika, kumbi
za dansi zitafura huku
wapendanao wakiwa
katika mavazi mekundu!
Kuna haja kama Taifa
kuyatizama mambo haya
kwa mtizamo mwingine,
sio huu wa kuvamia kila
kijacho. Hivi sisi utamaduni
wetu ni upi. Maadili yetu ni
yapi. Katika makabila na
tamaduni zetu, hakuna
namna ya kuonyeshana
upendo kati ya mke na
mume, wazazi na watoto au
ndugu kwa ndugu na hata
marafiki kwa marafiki?

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Palestine opens first Western Europe embassy in Sweden


PALESTINE has opened its
first embassy in Western
Europe in the Swedish
capital city of Stockholm
amid Israels anger.
According to official
Swedish sources, Palestinian
President Mahmoud Abbas
and Swedish Foreign Minister
Margot Wallstrom attended
the inauguration ceremony
of the Palestinian embassy in
Stockholm on Tuesday night.
Earlier in the day, Sweden
announced its decision to
increase financial aid to
Palestinians, but also urged
the Palestinian authorities to
carry out reforms, epically
with regard to womens
situation in the country.
Sweden reportedly plans to
increase its financial help to

Palestine by 1.5 billion crowns


($179.74 million) over the next
five years.
Some 135 governments
have so far announced their
official backing for Palestines
sovereignty. Parliaments in

STOCKHOLM (WAFA)
President Mahmoud Abbas
Tuesday expressed hope that
the Swedish recognition of
the state of Palestine will
leverage the international
communitys support of the
Palestinians' just cause.
Abbas commended
Swedens recent recognition
of Palestine as in independent
state, which, according to
him, bolsters the Palestinian
peoples struggle toward
freedom and independence.
He called upon other

European countries to follow


suit.
Abbas confirmed that
Swedens recognition of
Palestine and the United
Nations Secretary Generals
membership will support
peace negotiations and will
not replace such efforts.
During his visit to
Stockholm, Abbas signed with
Lofven several agreements on
cooperation and development.
The agreements would be
effective starting from 2015
until 2019.

major European countries,


including Spain, France,
Britain, Ireland and Portugal
as well as the European
Parliament have symbolically
endorsed Palestines bid to be
recognized as a state.

Abbas Hopes Swedish Recognition to Influence International Community

Last October, the parliament


of Sweden recognized the state
of Palestine and concluded
that 'the international law
criteria for the recognition of
Palestine have been met.'
The Swedish government
has also decided to increase
aid and adopt a five-year
aid strategy including
substantially increased
support to Palestinian statebuilding; aid to Palestine will
increase from SEK 500 million
to SEK 1.5 billion ($67.8
million to $203.4 billion) over
the next five years.

UN Calls to Lift Israeli Siege on Gaza


GAZA (WAFA) - The United
Nations Coordinator of
Humanitarian Affairs in the
Palestinian Territories, James
Rowley Tuesday called for
lifting the siege imposed
by Israeli on the Gaza Strip,
starting the reconstruction
process to repair the
destruction caused by the
latest Israeli war as well as
opening the Rafah border
crossing.
Rowley said in a press
conference held in al-Shifa
hospital in Gaza city that
the siege has greatly affected
health and humanitarian
Services and the blockade
should be lifted to end the
suffering of Gazas patients.
He demanded donor
countries which pledged to
reconstruct the war-weary
Strip to fulfill its obligations.
Rawley said the international
community that pledged
to fund the reconstruction
process must meet its
promises and turn them into
commitments.
Israel and the Palestinian
factions inked a ceasefire
deal on August 26, ending the
2014 deadly Israeli onslaught
on Gaza that claimed the
lives of over 2,200 people,
overwhelmingly civilians.
The ceasefire deal
stipulated that Israel must
ease the blockade imposed on

Evacuating survivors after an Israeli airstrike hits the Al


Ghoul family building in Rafah, August 3, 2014.
the strip and the restrictions of the war, as they have no
on the unilaterally-imposed other choice after losing their
fishing zone off Gazas coast. residences.
Egyptain authorities are
Israel has however failed
also closing the Rafah border to adhere to its agreement,
crossing between Gaza and repeatedly violating the
Egypt almost entirely and ceasefire deal through opening
are only opening it for those fire on Palestinian fishermen
deemed as humanitarian within the fishing zone and
cases.
hindering the reconstruction
The most pressing key issue process.
is the Gaza reconstruction.
Continuing the CairoWhole neighborhoods across brokered talks on other
the strip have been flattened key issues was repeatedly
and reduced to rubble by postponed in the wake of the
Israeli airstrikes, leaving November attacks against
about 475,000 Palestinians Egyptian soldiers in the Sinai
refugees displaced for yet Peninsula.
Israel has imposed a
another time.
A c c o r d i n g t o U N tightened blockade since
institutions statistics, around 2 0 0 7 a f t e r H a m a s w o n
15,000 Gaza refugees are still the democratic legislative
living in UN-run schools elections and took over power
seven months after the end in the strip.

Habari

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Al-Shabaab asilimisha wafungwa Segerea

Na Bakari Mwakangwale

MFUNGWA aliyeingia
gerezani Segerea akiitwa
Collins Javan Omundi,
ametoka akibeba jina la
Muhammad.
Neno, Al-Shabaab,
ndio limekuwa sababu ya
mfungwa huyo kusilimu,
akiacha imani yake ya awali
ya Kikristo.
Akisimulia kisa cha
kusilimu kwake, Omundi
anasema kuwa, alivyokuwa
akifahamu ni kuwa AlShabaab, ina maana ya
gaidi hatari na katili.
Kwa tafsiri na ufahamu
huo, anasema, ilikuwa ni
jambo la kushtua kwake
alipoingia gerezani na
kukutana na mtu anaitwa
Al-Shabaab.
Mfungwa huyo raia wa
Kenya, ambaye baada ya
kusilimu alichagua jina la
Muhammad, akiongea na
mwandishi wa habari hizi
muda mchache baada ya
kutoka gerezani, alisema
nchini Kenya, neno AlShabab ni kitu hatari sana
kutokana na matukio
yanayohusishwa na kundi
hilo.
Bw. Mohammed alisema,
a k i wa g e r e z a n i h u m o
alisilimishwa na Masheikh
Mselem na Farid, baada ya
kukutana na kijana mmoja
wa Kiislamu, maarufu
gerezani humo kwa jina
la Al-Shabab, ambaye
waliingia naye katika
mjadala wa hoja kuhusu
Dini ya Uislamu na Ukristo.
Anasema, ule ukaribu
wake na Shabani akitaka
kujua ni kwa nini alijiita
jina baya kama hilo, ndio
kukazaa urafiki uliokuja
kuibua mjadala wa mambo
ya kidini na hatimaye
kusilimu.
Bw. Mohammed, ambaye
alijikuta anahukumiwa
kwenda jela kwa kosa
la kupatwa na hatia ya
kuwepo nchini kinyume
cha sheria, alisema baada
ya kuingia gerezani humo
kwa mara ya kwanza akiwa
mahabusu, alistuka kusikia
kijana huyo akiitwa AlShabab na wenzake na
huku akifurahia jina hilo.
Anasema, alisilimu
Januari 7, 2015, baada ya
kuwa mahabusu na kujikuta
anaanza kudadisi mambo
ya kiimani baada ya kusikia
kijana mmoja aliyemkuta
humo mahabusu, akiitwa
Al-Shabab.
Bw. Mohammed, alisema
huyo kijana jina lake halisi
ni Shaban, lakini humo
gerezani anajulikana zaidi

kwa jina la Al-Shabab, na


kwa kuwa kwao Kenya
watu hao ni hatari, ni
magaidi, ilimpelekea
kustuka na kupatwa na
hofu kuwa na mtu wa aina
hiyo humo gerezani.
A l i s h a n g a a n i k wa
nini uongozi wa gereza
uwaweke na mtu gaidi,
al-Shabaab huyo.
Nilimuuliza kwa nini
anaitwa Al-Shabab, badala
ya Shabani, alinieleza
k u we p o k wa k e h u m o
gerezani ni kutokana na
kukamatwa na maafisa
uhamiaji mpakani mwa
Kenya na Somalia akielekea
Sudani, akitokea Tanzania
na kutuhumiwa kuwa yeye
ni Al-Shabab. Alisema
Bw. Mohammed.
Alisema, baada ya kupata
kisa hicho alipata shauku
ya kujua undani wa neno
hilo ambapo aliambiwa
kuwa al-Shabaab ni neno
l a K i a r a b u / K i s wa h i l i
lenye maana ya kijana,
madhubuti, mwenye
nguvu, imara.
Baada ya kujua kuwa
Al-Shabab lina maana ya
kijana mwenye nguvu
na si gaidi, na kuwa na
ukaribu huo, akasema, ndio
waliingia katika kupeana
elimu kwa kutumia Biblia
na Quran.
Alisema, akiwa katika
Ukristo alikuwa anauchukia
sana Uislamu kutokana
na jinsi unavyohusishwa
na masuala ya kigaidi,
lakini akadai, angalau kwa
kukaa jela na kukutana
na akina Sheikh Msellem,
a m e j u a k u wa k u m b e
kilichokuwa kikimuathiri
ni propaganda na sio
ukweli juu ya Uislamu
wenyewe.
Mimi nimekulia katika
Ukristo na kuusoma
vizuri, kwa kuwa nilikuwa
nauchukia Uislamu huko
nyuma, nilikuwa na uwezo
wa k ums h a w is h i mtu
aachane na Uislamu na
aingie katika Ukristo.
Hata Al-Shabab
(Shabani) kule gerezani
ananielewa nimemsumbua
sana, ili aachane na
Uislamu, ila yeye amekuwa
na hoja zinazoingia akilini
nikabaini kumbe Uislamu
ni mzuri ila kuna watu
wanautumia vibaya tu,
nikakata shauri kuingia
katika Uislamu. Alisema
Bw. Mohammed.
Alisema, baada ya
hapo, alimfuata Sheikh
Mselem kuwaeleza nia
yake na alisilimishwa na
kuanza kufundishwa Qur
an na masuala mengine

yanayohusu Uislamu.
Alisema, katika muda
aliokaa na Masheikh
wa n a o t u h u m i wa k wa
ugaidi, walimfundisha nini
Uislamu na kuzidi kubaini
kiundani kuwa Uislamu
ni dini nzuri kinyume na
inavyochafuliwa kupitia
propaganda.
Nimesilimu nikiwa
gerezani, sasa nimetoka
nataka niusome zaidi
Uisamu ili nipate kuwa
muelimishaji kuhusu
Uislamu. Nataka nije
nikutane tena na ndugu
zangu niliowaacha
gerezani na mimi nikiwa
Muislamu haswa. Alisema
Bw. Mohammed.
Alisema, baada ya
k usilimu alifurahi na

kumueleza rafiki yake


(Al-Shabab) kuwa akirudi
Kenya, atafanya kazi ya
kuelimisha watu juu ya
propaganda inayopigwa
dhidi ya Uislamu ili watu
wasijue ukweli wa Dini hii.
Najua nitawashangaza
wa t u h u k o n y u m b a n i
(Kenya), lakini lengo langu
ni kutoa elimu. Alisema.
Bw. Mohammed
Omundi, anasema yeye
ni mkazi wa Komorrock,
Embakasi Nairobi Kenya,
na amezaliwa na kulelewa
katika dhehebu la Sabato.
Mimi nimezaliwa
katika familia ya Kikristo,
baba kafa akiwa ni Mkristo
na alikuwa mwimba kwaya
maarufu na walikuwa
wakishinda Kenya nzima

kwa ubora wa nyimbo


zao na mama yangu ni
Mchungaji mpaka sasa.
Anaeleza bw. Omundi.
Kwa mujibu wa Bw.
Omundi, amedai kuwa
k wa m u d a wa m we z i
mmoja aliokaa gerezani
humo amebaini kuwa
wapo wafungwa na
mahabusu wengi ambao
wamesilimu na kujifunza
Uislamu wakiwa humo
gerezani.
Wapo wengi ambao
nimewakuta wamesilimu
kabla yangu kupitia kwa
Waislamu wanaotuhumiwa
kwa ugaidi humo gerezani,
na wengine wameendelea
zaidi kielimu wakiwa
humo humo gerezani.
Amefafanua.

SHEIKH Ponda Issa Ponda akiongozwa na makachero wa polisi muda mfupi baada
ya kesi yake kusikilizwa.

WAUMINI wa dini ya Kiislamu wakiswali katikati ya barabara jirani na Mahakama


ya mjini Morogoro.

4
MTU yoyote hii leo ikiwa ataingia
katika mitandao ya kijamii na
kusoma mjadala unaofanyika
kuhusu Mahakama ya Kadhi,
ni lazima atapata mshtuko
mkubwa kutokana na lugha
kali na wakati mwingine matusi
kati ya hao wanaojadiliana. Kila
upande ukitupa shutuma na
maneno makali dhidi ya upande
mwingine. Ukipitia majadiliano
yote kitu kimoja kinachojitokeza
wazi na dhahiri kabisa ni kuwa
kuna mpasuko mkubwa kati ya
Waislamu na Wakristo kuhusu
Mahakama ya Kadhi. Chuki na
uadui sasa upo wazi bila kificho.
Hili linawezekana vipi wakati
viongozi wetu wanatuambia
kuwa Baba wa Taifa alituachia
misingi imara ya umoja? Wahenga
wamesema dalili ya mvua ni
mawingu. Suali la kujiuliza ni hili,
wapi sisi kama taifa tumejikwaa?
Wengi katika hao wanaojadili
h i y o M a h a k a m a ya K a d h i
ukweli ni kuwa hawaijui vyema
historia ya Tanzania au ukipenda
Tanganyika. Wengi katika hawa
waliojizinga katika malumbano
haya, baadhi ni watu wazima
walio na umri zaidi ya miaka 50
na vijana ambao wamezaliwa
baada ya Tanganyika kupata
uhuru wake mwaka 1961. Mjadala
unafanyika katika mazingira ya
ujinga wa kutojua historia. Sasa
hapa linakuja swali, imekuwaje
kuwa watu hawa ambao kwa sasa
ndiyo wengi katika jamii yetu hii
leo hawaijua historia ya nchi yao?
Vipi tumekuwa na Chuo Kikuu
kwa karibu ya nusu karne na sasa
vimeongezeka vingine vingi,
lakini hadi sasa ikawa historia
yetu ni ya kubabaisha haijakaa
sawa hadi leo? Mimi sitatoa jibu
kwa sasa ingawa jibu ninalo.
Huko vyuoni ni historia gani
inasomeshwa ambayo inawafanya
watu wasijijue?
Baadhi ya wachangiaji katika
h i y o m i t a n d a o ya k i j a m i i
na inaelekea hao ni Wakristo,
wanasema iweje Mahakama ya
Kadhi igharimiwe na serikali ilhali
serikali hii haina dini? Waislamu
wanaleta jibu wakisema mbona
serikali inatoa mabilioni kila
mwaka kwa makanisa kuhudumia
taasisi zao kupitia Memorandum
of Understanding (MoU)? Kwa
wale ambao labda hawaujui huu
mkataba ni kuwa mwaka wa 1992
Serikali ya Tanzania ilitiliana
sahihi mkataba na makanisa,
mkataba uliokuja kujulikana kama
Memorandum of Understanding.
Makubaliano ambayo serikali
iliridhia na kuidhinisha elimu,
h u d u m a z a j a m i i n a a f ya
ziendeshwe na Christian Council
of Tanzania (CCT) na Tanzania
Episcopal Conference (TEC) kwa
kushirikiana na serikali. Mkataba
huu ulitayarishwa na Dr. Costa
Mahalu, wa Kitivo cha Sheria
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
na ukatiwa sahihi na Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Waziri
Mkuu, wakati huo Mheshimiwa
Edward Lowassa. Kikubwa
katika mkataba huu kwanza ni

Makala

Kadhi Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhr

Mahakama ya Kadhi:

Tanzania inavuna matunda


ya kuikataa historia ya kweli
ule usiri uliogubika mpango
mzima na pili ni kuwa ulitiwa
sahihi bila ya kuwashirikisha au
kuwafahamisha Waislamu.
Ili makubaliano haya yaweze
kutekelezeka, serikali ilibidi
ifanye marekebisho kifungu 30
cha Education Act No. 25, 1978.
Katika mabadiliko haya kuletwa
Bungeni ndipo Waislamu wakajua
kuhusu hii MoU kati ya Serikali na
Makanisa.
Suali lingine la kujiuliza ni,
inakuwaje jambo zito kama hili
lilipitishwa na Bunge letu bila
kipingamizi? Suala hili limepita
kwa kuwa Waislamu Bungeni
waliamini kuwa uamuzi huo una
maslahi na taifa letu? Au limepita
kwa kuwa Waislamu katika Bunge
ni wachache wameelemewa na
ndugu zao Wakristo kupelekea
kuwa sasa hawana sauti kwa
uchache wao? Ikiwa huu ndiyo
ukweli wenyewe, tumefikaje hapa
na nini athari ya jambo hili kwa
mustakbali wa taifa letu?
Kwa uchache unaweza mtu
ukajiuliza kwa nini basi serikali
hiyo hiyo haikuja na mpango
wowote hata kama si sawa na
ule wa Makanisa wakatoa fedha
kwa taasisi za Kiislamu na wao
wajiletee maendeleo kama hayo
ya Makanisa? Mimi sitatoa jibu
ingawa majibu ninayo. Kwa
kuhitimisha hebu tujiulize
kwani Mahakama ya Kadhi ni
kitu kipya katika nchi hii kiasi
cha kusababisha mtafaruku huu
ambao hivi sasa tunaushuhudia?

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

U k we l i n i k u wa u k o l o n i
umeingia Tanganyika umekuta
Waislamu wakijihukumu kwa
kitabu chao. Mmishionari
Johan Krapf kaja Tanganyika na
alipokelewa na Chifu Kimweri
wa Usambaa mwaka 1848. Krapf
alipokelewa kwa ukarimu wa
hali ya juu na alimkuta Chifu
Kimweri Muislamu, anajua
kusoma na kuandika kwa herufi
za Kiarabu akihukumu katika
barza yake iliyokuwa Vuga.
Ni wazi kuwa Chifu Kimweri
hakuwa anahukumu kutoka,
Order in Council, kutoka India
kwani Waingereza walikuwa bado
hawajafika.
Chifu Kimweri alikuwa
anahukumu kwa sheria kama
walivyohukumiana Waislamu
katika ukanda wa pwani ya Afrika
Mashariki kwa miaka mingi. Mimi
nimekuwa na kupata fahamu
katika Tanganyika ya 1950/60
na nina kumbukumbu za hizi
mahakama za kadhi na baadhi
ya hawa mahakimu nimewaona
kwa macho yangu ama wakiwa
katika mahakama wakihukumu
na wengine nimewaona mitaani
na wengine nimewaona
wakisuhubiana na wazee wangu.
Namkumbuka Sheikh Abdallah
Simba kutoka Songea. Nikifumba
macho ni kama vile namuona
Sheikh Abdallah Simba. Alikuwa
kija Dar es Salaam na Land Rover
yake mwenyewe na siku zote
akivaa kanzu, koti na tarbush.
Sheikh Abdallah Simba alikuwa

na watoto wawili Bi. Habiba na


Mwajuma. Bi Habiba alikuwa na
umri sawa na mama yangu na
alikuwa nurse Princes Princess
Margret Hospital (sasa Muhimbili
Hospital) lakini Mwajuma yeye
alikuwa makamu ya dada yangu
mkubwa. Mwajuma akisoma St.
Josephs Convent School (sasa
Forodhani). Sheikh Abdallah
S i m b a a l i k u wa a k i h u k u m u
katika mahakama huko Songea
kwa sheria za Kiislamu na
akifahamiana na babu yangu
Salum Abdallah toka ujana wao
katika Dar es Salaam ya 1920.
Sheikh Abdallah Simba akiishi
Songea lakini alikuwa na nyumba
mbili moja Mtaa wa Kipata (sasa
Mtaa wa Kleist Sykes) nyingine
Mtaa wa Somali (Sasa Mtaa wa
Omari Londo). Majina ya mitaa
hii ilibadilishwa kuwaenzi wazee
hawa Kleist Sykes na Omari
Londo walioacha alama katika
historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kulikuwa na Sheikh Said
Chaurembo akihukumu katika
Mahakama ya Kariakoo. Sheikh
Said Chaurembo alikuwa katika
Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA
(TAA Political Subcommittee)
mwaka 1950. Kamati hii chini
ya Mufti Sheikh Hassan bin
Amir ilifanya makubwa katika
kujenga mazingira ya kuunda
TANU mwaka 1954 na kumweka
Mwalimu Nyerere katika uongozi
wa kudai uhuru lakini hapa si
mahali pake kuyaeleza hayo.
Huyu Sheikh Said Chaurembo
alikuwa na nduguye akiitwa Iddi
Chaurembo huyu ndiye baba
yake Sheikh Abdallah Chaurembo
na wakati ule Sheikh Abdallah
Chaurembo alikuwa mwanafunzi
katika chuo cha Mufti Sheikh
Hassan bin Amir.
Sheikh Said Chaurembo ndiyo
aliyekuwa na lile ghorofa maarufu
Mtaa wa Msimbazi na Congo
linalojulikana hadi leo kama
Ghorofa la Chaurembo. Kwa
kumalizia kuhusu hizi mahakama
hapa Dar es Salaam napenda
kueleza kuwa katika miaka ya
1960 baada ya uhuru, Sheikh
Kassim Juma alikuwa akihukumu
katika Mahakama ya Kadhi
Mkwajuni hadi mahakama hizo
zilipovunjwa na serikali mwaka
1963. Sheikh Kassim Juma na yeye
ana historia kubwa katika siasa za
Waislamu, BAKWATA na serikali
baada ya uhuru.
Sheikh Abdallah Chaurembo
akiwa msomi wa dini ya Kiislamu,
alihusika sana katika harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika.
Sheikh Abdallah Chaurembo
alikuwapo katika mkutano wa
TANU uliofanyika Mtaa wa Pemba
usiku mmoja mwaka 1955 agenda
kuu ikiwa vipi TANU itapunguza
joto kali la Uislamu ndani ya chama
ili kupunguza ile taswira kuwa
TANU ni chama cha Waislamu.
Jambo hili lilikuwa muhimu ili
kumwezesha Mwalimu Nyerere
kuongoza harakati za kudai uhuru
kwa utulivu.
Pamoja na Sheikh Abdallah
Inaendelea Uk. 12

AN-NUUR

Makala

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Jaji aituhumu Vatican kuhusika mauaji ya kimbari Rwanda


Elizabeth Shoo/KNA
Hakimu mmoja wa
Mahakama Maalumu ya
kusimamia kesi ya mauaji
ya kimbari ya mwaka 1994
nchini Rwanda, ameulaumu
uongozi wa Kanisa
Katoliki kwa kuwalinda
watuhumiwa waliohusika
ambao ni viongozi wa dini.
Katika mahojiano
a l i y o ya f a n ya n a g a z e t i
la Badisches Tagblatt la
Ujerumani, Jaji Wolfgang
Schomburg, amewanyooshea
viongozi wengi wa Kanisa
kidole kuhusiana na mauaji
hayo.
Jaji Schomburg aliyekuwa
sehemu ya jopo la Majaji
lililosimamia kesi ya mauaji
ya kimbari ya Rwanda ya
mwaka 1994, amewataka
M a p a d r i wa K i k a t o l i k i
waliohusika katika mauaji
hayo ya kinyama wafikishe
mahakamani.
Jaji huyo ameukosoa
uongozi wa Kanisa KatolikiVatikan, kwa kuwalinda
Mapadri hao, ambao
wa n a p a s wa k u f i k i s h wa
mbele ya sheria.
Imeelezwa kwamba kuna
ukweli kwamba, vipo visa
ambapo uongozi wa Kanisa
Katoliki uliamua kuwapatia
hifadhi viongozi wa kiroho
ambao walihusika moja
kwa moja kwenye mauaji ya
kikatili.
M m o j a wa o n i Pa d r i
Wenceslas Munyeshyaka,
yeye alielezwa kuwa mwaka
1994 alibeba bunduki kama
mwanajeshi na kupanga
njama na waasi wa Kihutu.
Wa a s i h a o w a l i w a u a
mamia ya watu waliokuwa
wakitafuta hifadhi ndani ya
Kanisa la Padri Munyeshyaka.
Padri huyo baadaye alihamia
Ufaransa.
Mahakama moja ya nchini
Rwanda ilimhukumu adhabu
ya kifungo cha maisha,
lakini Kanisa Katoliki nchini
Ufaransa lilimtetea na
kusema kuhukumiwa kwa
Padri Munyeshyaka kwa
mauaji ya kimbari, si sababu
ya kumfanya asiendelee na
kazi yake ya upadri.
Hata hivyo imeelezwa
kuwa Padri Munyeshyaka
hakuwa pekee yake. Mapadri
na Masista waliofahamika
kuhusika katika mauaji ya
Rwanda walipelekwa Ulaya
na kupatiwa hifadhi huko.
Miongoni mwao alikuwa
Padri Athanase Seromba,
aliyeruhusu Kanisa lake
libomolewe likiwa na
Watutsi 2,000 ndani. Wale
waliopona katika ubomoaji
huo walifyatuliwa risasi na
kuuliwa. Kanisa Katoliki
lilimsaidia kukimbilia Italia
na hata kuhakikisha kwamba
anapewa jina jipya na pasipoti
mpya.
Imeelezwa kuwa mbali na
viongozi hao wa dini, bado
wapo wanasiasa na wanajeshi
waliohusika, ambao kamwe

hawakuwahi kufikishwa
mahakamani au kufunguliwa
mashtaka.
Jaji
Schomburg
amekumbusha kuwa bila
kuwepo kwa mahakama
maalumu ya Umoja wa
Mataifa, watu wengi
waliosababisha maafa ya
Wa n ya r wa n d a wa p a t a o
800,000 wangeweza
kuukwepa mkono wa sheria.
Pamoja na hayo, Jaji huyo
wa zamani amekosoa pia
namna ambavyo Jumuiya ya
Kimataifa ilichelewa kuingilia
kati mgogoro wa Rwanda
hadi pale ambapo mamia
kwa maelfu ya raia, wengi
wao Watutsi, walipokuwa
tayari wameuliwa.
"Hata mahakama ya Umoja
wa Mataifa inayoshughulikia
mauaji ya kimbari ya Rwanda
ilianzishwa kwa kuchelewa.
Mahakama hiyo ilipaswa
iundwe mwishoni mwa
mwaka 1993 au mwanzoni
mwa 1994", alikosoa Jaji
Schomburg.
Jaji huyo, ambaye alifanya
kazi kwenye mahakama
hiyo kuanzia mwaka 2001
hadi 2008, hakuishia hapo.

Alielezea kushangazwa
kwake na ukweli kwamba
hakuna Mfaransa hata mmoja
aliyefunguliwa mashtaka,
licha ya kwamba baadhi ya
Wafaransa walituhumiwa
kuuza silaha nchini Rwanda
katika miaka ya 1990s na
kwamba, wakati mwingine
hata walizigawa silaha hizo
kwa Wahutu.
Alisema wakati fulani
serikali ya Rwanda ilijaribu
kuwafungulia mashtaka
wahusika, lakini bila
mafanikio. Jaji Schomburg
anasema Ufaransa haina
nia ya kweli kufanya
uchunguzi wa kipindi hicho
kilichogubikwa na giza.
Hata hivyo Jaji Schomburg
ameisifu mahakama ya Umoja
wa Mataifa ya kushughulikia
mauaji ya kimbari ya
Rwanda, kwa kupiga hatua
za haraka kuwawajibisha
wahusika na kuwapatia
haki wale walioonewa na
hii imekwenda haraka
hata kuliko vile ambavyo
Ujerumani ilivyoendesha
kesi za waliohusika katika
mauaji ya Wayahudi chini ya
utawala wa Wanazi. (DW).

PAPA Francis.

Rais Obama azua mtafaruku kusema hata Ukristo kuna ugaidi


Asema vita vya msalaba sawa na Ugaidi

RAIS Barack Obama (kulia) akiwa na Rais wa Iran Hassan Roham.

Iran kuzindua meli mpya ya kivita


KAMANDA wa Jeshi la
Wanamaji la Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, Admeli
Habibullah Sayyari,
amesema kuwa karibuni
hivi jeshi la wanamaji la Iran
litazindua meli ya kisasa
aina ya Damavand ambayo
imeundwa na wataalamu wa
ndani nchini humo.
Akiashiria uwezo wa
jeshi la Iran na juhudi
zake za kujilionda dhidi
ya chokochoko zozote za
adui katika sherehe za
kuadhimisha kumbukumbu

ya Mapinduzi ya Kiislamu
ya nchini Iran, Kamanda
Habibullah Sayyari, alisema
kuwa, hivi sasa taifa la Iran
linajivunia juhudi za wasomi
na vijana wake, ambao
wameweza kuzalisha aina
mbalimbali za silaha na zana
za kisasa kabisa kwa kiwango
cha kimataifa.
Aliyataja mafanikio
hayo kuwa ni mwiba
kwenye macho ya maadui
wasiolitakia mema taifa na
watu wa Iran ya Kiislamu.
Aidha ameelezea matatizo

yaliyokuwa yakilikabili
jeshi la Iran katika kipindi
c h a u t a wa l a wa S h a h ,
kutokana na kufuata
kibubusa siasa za Marekani
na kuongeza kuwa, wakati
ule maamuzi na mipango
yote yaliyokuwa yakihusu
zana, silaha, mazoezi ya
kijeshi na mambo mengine
yalikuwa yakichukuliwa
n a Wa s h i n g t o n b i l a ya
kuwahusisha wataalamu wa
Iran, suala ambalo liliifanya
Iran kubakia tegemezi wakati
wote.

MATAMSHI ya Rais wa
Marekani, Barack Obama,
ya k u wa t a k a Wa k r i s t o
kutambua kwamba Uislamu
si dini pekee inayohusishwa
na vurugu na mauaji, na
kwamba Vita vya Msalaba
n a v i t e n d o v ya u g a i d i
vinavyofanywa na vikundi
vyenye misimamo mikali.
Rais Obama alitoa kauli
hiyo wiki iliyopita, katika
siku ya taifa ya maombi,
alipofananisha Vita vya
Msalaba na vitendo vya
ugaidi vinavyofanywa na
vikundi vyenye misimamo
mikali.
Rais Obama aliongeza
kuwa, wakati wa vita
vitakatifu, watu walifanya
vitendo vya kutisha kwa jina
la Kristo. Alisisitiza kuwa
nchini Marekani, utumwa
na sheria za kibaguzi, zote
pia zilihalalishwa kwa jina
la Kristo.
Kauli hiyo imezua
mtafaruku duniani na baadhi
wameanza kuhoji kama
kiongozi huyo wa kwanza
mweusi wa Marekani ni
Mkristo.
Kwenye hotuba yake hiyo,
Rais Obama alilitaja kundi la
Daesh kuwa limeasi Uislamu
kwa kutenda jinai na vitendo
vya kikatili katika eneo la
Mashariki ya Kati.
Makundi kama ya Daesh
yamekuwa yakitekeleza jinai
na mauaji dhidi ya watu wasio
na hatia kwa kupata misaada
ya kifedha na kisilaha kutoka
nchi za Magharibi na baadhi
ya nchi za Kiarabu za Ghuba
ya Uajemi. (irib).

6
QURAN tukufu ni kitabu
cha Mwenyezi Mungu
kilichoteremshwa juu
ya moyo wa Mtume
Muhammad (S.A.W.) ili
aiongoze kwayo jinsi ya
wanadamu na ili utulizane
juu yake ulimwengu. Kwa
hiyo Quran juu yake
kutasimama kiyama cha
ulimwengu. Na kwa hiyo
Quran anapozwa mwenye
kupozwa na anafanikiwa
mwenye kufanikiwa.
Quran inatunyanyua juu
ya ulimwengu. Isipokuwa
ni kwamba haitaki
kwetu kujitoa katika huo
ulimwengu. Inapanda na
sisi juu ya ulimwengu,
wakati ambapo inataka
kwetu tuzinduke kwa
yaliyo madogo sana
katika mafungu yake, kwa
kawaida na mazoea, na
inazama na sisi kutupeleka
kwenye vina vilivyo zama
sana kwa binadamu ili
tusikilize pamoja kwenye
maungulio ya raho yake
ambayo yamejificha
sana na maumivu yaliyo
manyonge sana ya moyo
wake.
Quran inatuchukua
na kutupeleka kwenye
maeneo mapya ambayo
hayajagunduliwa katika
maeneo ya roho, na
inakwenda na sisi kwenye
vipeo vyenye kutisha na
vilele vya juu sana kisha
inatutahadharisha na
kugeuka nyuma. Na kama
si hivyo, tutapatwa na
SAHABA mmoja
aliwahi kumwomba
Mtume (s.a.w.) awape
taarifa kumhusu yeye
mwenyewe. Naye
akawaambia hivi:
"Mimi ndiye mtu ambaye
Ibrahim (a.s.) aliomba nije,
na ambaye Yesu (Nabii
Isa ibn Maryam) (a.s.)
alitangaza hahari njema
za ujio wangu.
Usemi huu unadokeza
aya zifuatazo za Qur an:
Ewe Mola mlezi
wetu! Waletee Mtume
a n a ye t o k a n a n a wa o ,
a wa s o m e e a ya z a k o ,
na awafundishe Kitabu
(chako) na hikima
(nyingine) na awatakase
(na kila mabaya). Hakika
wewe ndiwe mwenye
nguvu, mwenye hekima
(Surat Al-Baqarah, 2:129).
Na Isa bin Mariamu
aliposema: Enyi Wana
wa Israili! Hakika mimi
ni Mtume wa Mwenyezi
Mungu
kwenu,
ninayethibitisha yaliyo
kuwa kabla yangu katika
Ta u r a t i , n a m w e n y e
kubashiria habari njema za
kuja Mtume atakayekuja
baada yangu; ambaye jina
lake litakuwa ni Ahmad

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Mwangaza wa Quran

Mwanamke wa Kiislamu (kulia) akitoa Da'awah kwa asiye Muislamu.


kizunguzungu na huenda
tukaporomoka kutoka
sehemu ya juu ambayo
tumefika mpaka chini ya
sehemu tuliyokuwa katika
majangwa.
Quran inapanda juu
na sisi kwa hisia zetu,
juu ya akili, isipokuwa
inabaki ikitukumbusha
kwamba hiyo akili ndiyo
ngazi yetu pamoja na hisia
katika kwenda huko juu

na inakata pamoja nasi


vipeo vya zama na mahali
mpaka tunakaribia kuhisi
mawimbi ya milele yakiwa
yanapiga katika fukwe za
roho zetu na yanateremka
kwenda ndani yetu,
na katika kizuizi kati
ya k u w a t u w e w a t u
tuliyokamilika au tusiwe.
Inatusimamisha Quran ili
tuyatazame maono yetu,
na tuliheshimu jambo letu.

Kutapanyika kwa roho


na kugawanyika kwa
nafsi na kutawanyika kwa
fikra na kupotoka kwa
mtazamo, tunapata katika
Quran kinachokusanya
mtapanyiko
na
k i n a c h o f a n y a
magawanyiko. Inayarushia
macho umoja wa mtazamo,
uliozidi ukali wa kuona
n a n g u v u i l i k u we z a
kuyaona yasiyoonekana

Nabii aliyekuwa akingojewa

Zisemavyo Taurati na Zaburi za Mayahudi na Wakristo

(Muhammad)! Lakini
alipowaletea hoja zilizo
wazi, walisema: Huu ni
uchawi ulio dhaahiri!"
(Surat As-Saff, 61:6).
M t u m e ( s . a . w . ) wa
Allah (s.w.t.) alikuwa
akitazamiwa au akingojewa
kuwa atakuja. Manabii
w o t e wa l i o m t a n g u l i a
walimwongelea Mtume
(s.a.w.) na walitabiri ujio
wake.
Aya ya Qur'an 3:81
inataja waziwazi kuwa
Mola (s.w.t.) Alifanya
Kiaga (covenant)
maalum na Manabii
kwamba watamwamini
na watamsaidia Mjumbe
huyo atakayekuja baada
yao na atakayethibitisha
ujumbe waliouleta wao.
N a p a l e M we n ye z i
Mungu Alipochukua
ahadi (kiaga) kwa Manabii:
Nikisha kukupeni
Kitabu na hikima, kisha
akakujieni Mtume mwenye
kusadikisha mliyonayo, ni

juu yenu mumuamini na


mumsaidie. Akasema: Je,
mmekiri na mmekubali
kushika agizo langu juu
ya h a y o ? Wa k a s e m a :
Tumekubali. Akasema:
Basi shuhudieni, na Mimi
ni pamoja nanyi katika
kushuhudia. (Surat Aali
'Imran, 3:81).
Makala ya sasa (ya
Biblia za Wakristo) ya
Taurati, Injili, na Zaburi,
mpaka hivi sasa (baada ya
kukarabatiwa), zinazo aya
zinazozungumzia Nabii
Muhammad (s.a.w.) na hata
Maswahaba . Marehemu
Husayn Jisri alizitambua
jumla ya aya 114 za aina
hii na akazinukuu katika
kitabu chake Risalat AlHamidiya. Hapa chini
tunanukuu baadhi ya
aya hizo (kama Biblia
zao Wakristo wenyewe
zinavyoandika).
K u m b . L a Ta u r a t
33:2 (Musa) Akasema:
Bwana alitoka Sinai,

akamwondokea kutoka
Seiri, aliangaza kutoka
kilima cha Paran, akaja
Meribath-kadeshi. Upande
wa mkono wake wa kuume
palikuwa na sheria moto
moto kwao.
[NB. Tafsiri hii ni ya
Biblia ya Kiswahili ya
"Bible Societies of Kenya and
Tanzania, Union Version,
1952".
Tafsiri hii inakanganya
makusudi hapo inapotaja
'Merebath Kadesh na
kutowataja masahaba au
watakatifu 10,000 kama
ziandikavyo tafsiri nyingi
za Kiingereza (na za lugha
zingine za kigeni) kama
Biblia hii "Authorized
King James Version, 1979",
ambayo imeandika hivi:
"Deuteronomy 33:2 And
he (Moses) said, The Lord
came from Sinai and rose
up from Se'ir unto them;
he shined forth from mount
Paran, and he came with ten
thousand saints: from his

kwetu na yasiyoonekana
katika ulimwengu. Nayo
inatufundisha kwamba,
yule ambaye hakuwa
mmoja katika dhati yake,
hakuungana katika fikra
ya k e h a k u k u s a n y i k a
katika hisia yake hatakuwa
na fungu lolote katika
maonekano ya nuru za
umoja na upweke kwa
sababu imani ya kweli ni
ile ambayo inachimbuka
kutoka katika uwepo wa
binadamu kwa ujumla
wake. Na Quran baada
ya hapo, ni chemchem ya
nguvu yenye kumiminika
kutokana na nguvu
zisizoonekana ili wapate
nguvu kwa hiyo Quran
wany ong e na wa pat e
uhai kwayo wafu, na hiyo
Quran ndiyo akili ambayo
imepelekwa kwa ajili ya
wazimu wa nyakati zote na
ni mionzi ya roho ya tangu
juu ya viza vya nyoyo
na nafsi kwani matamko
yake yamebebeshwa
mawingu ya uhai na aya
zake zinatona umande
wa uzuri na utukufu.
Na kwa kiasi ambacho
mwanadamu anakosa
kuijuwa Quran, kunakuwa
kutoijuwa kwake nafsi
yake na ulimwengu ulio
pambizoni mwake.
Kwa hakika hiyo
Quran, ndiyo uamsho wa
utashi wa upwekeshaji
na maumbile yake
kutoka katika maficho ya
Inaendelea Uk. 7
right hand sent a fiery law
for them.
Ambayo tafsiri yake
halisi ya Kiswahili ni kama
ifuatavyo:
"Kumbukumbu la
Torati 33:2 naye (Musa)
alikuja kutoka Sinai,
akawaondokea kutoka
Seiri kuja kwao; Aliangaza
kutoka kilima cha Parani,
na alikuja na watakatifu
elfu kumi. Kutoka katika
mkono wake wa kuume
ilikuja sheria motomoto
kwa ajili yao.
Aya hii ya Torati
inaongelea kwa pamoja
juu ya Nabii Musa, Nabii
Isa (Yesu, na Muhammad
(a.s.). Kwa mfano ikitaja
Sinai kule ndiko Nabii
Musa (a.s.) alikoongea
na Mwenyezi Mung u
(s.w.t.) akapewa Kitabu
cha Taurati (Torati).
Inapoitaja Seiri, pale
ni mahali huko Palestina,
a m b a k o Ye s u ( a . s . )
alipokea Wahyi (Ufunuo
wa Kiungu). Na ikitajwa
Paran, ndiko ambako
Mwenyezi Mungu
(s.w.t) Alikojidhihirisha
Yeye Mwenyewe kwa
walimwengu kwa mara ya
Inaendelea Uk. 7

7
Inatoka Uk. 6
mwanadamu. Na hiyo
Quran, ndiyo dhati ya
ulimwengu na moyo wake.
Ni akili ngapi imepanda
juu nazo? Hakika kanuni
za maumbile na taratibu za
ulimwengu, zinaungana
katika mbingu ya matamko
ya k e n a a ya z a k e n a
katikati yake inalala akili
yote na kutokana nayo
inanusa pumzi za maisha
na ndani yake zinaungana
nguvu za maumbile
na ubora na vyote
hivyo vinazama katika
mmiminiko la mapenzi ya
Mwenyezi Mungu nayo
inazitia nguvu, nguvu za
vitambuzi na inafungua
madirisha ya fikra na
inawasha mageuzi ya
hamu katika shina la nyoyo
na roho. Ama wabora wa
fikra, wao wanakuta humo
ubora wote na ushujaa
wote, na ukubwa wote. Ni
fikra ngapi imezifitini? Na
muonjaji sana imemathiri?
Na ufasaha umepiga na
umeinama kwa sababu ya
ufasaha wake?
Kwa hakika Quran
imechanachana sanda
za ukimya kuhusiana
na utume uliopita, na
imewasimamisha Mitume
waliyotangulia kutoka
katika malazi yao na
imewatamkisha ili waseme
tamko la ukweli kuhusu
Muhammad (s.a.w.) na ili
aliwazike kwa pumzi zao
na aufuate mwenendo wao
na kwa yale waliyoyapata
miongoni mwa ushupavu
wa watu wao na yale
Inatoka Uk. 6
mwisho kwa Wahyi Wake
Aliyompelekea Nabii
Muhammad (s.a. w).
Paran ni safu ya milima
kule Makka. Imetajwa
katika Taurat na Torati ya
Biblia katika aya nyingi
pamoja na aya hii ifuatayo:
Mwanzo 21:19,21, kuwa
mahali pale ni jangwani
ambako Hajiri (Hagar )
alikoachwa na mume
wake, lbrahimu (a.s.) ili
aishi na mwanawe, Ismail
( au Ishmael) aliyekuwa
mwana wa kwanza wa
Nabii Ibrahim na mkewe
Hajiri, na kwa kuwa wote
wawili, hususani mwanae
Ismail, walikuwa na kiu
sana, Mwenyezi Mungu
(s. w.t) akamtengenezea
k i s i m a ( c h a m a j i ya
Zamzam).
Kumbuka kuwa
Muhammad (s.a.w) ni
kizazi cha Nabii Ismail
(Ishmael), wakati Yesu ni
kizazi cha Is-haq (Isaka
au Isac) na wote wawili,
Muhammad na Yesu na
babu zao wakuu (wahenga
wao), yaani Ismail na Is-

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Mwangaza wa Quran
waliyoyamiminiwa juu
yao miongoni mwa uovu
na adhabu.
Kwa hakika ametikisa
Muhammad (s.a.w.) kwa
ulingano wake moyo wa
mbingu zikakungutika
mpaka zikawa ni ziaka
la mishale ya moto
inayochomoka iliyozipata
nyoyo za mashetani
na wafuasi wao katika
mushirikina popote
watakapokutwa na
vyovyote watakavyokuwa.
Kati ya moyo wa
Muhammad (s.a.w.) na
moyo wa Al-Kaaba, pana
hamu yenye kubadilishwa
ya ndani na yenye kina
sana. Imezama katika
uzamani, hiyo Al-Kaaba
ni pacha wake katika
kupatikana. Nayo ni nusu
ya dhati yake na ni baadhi
ya mafungu ya johari
ya hakika yake katika
vioo vya ulimwengu wa
mfano. Na siku ambayo
Makkah iliweka amana
yake iliyo ghali mbele ya
ulimwengu, yaliifinika
Al-Kaaba maungu ya
huzuni kwa sababu ya
yale yatakayoletwa na
m a s i k u ya j a y o h u k o
mbele miongoni mwa
kufariqiana na kutengana
kulikopangwa, ambako
hapana makimbilio yoyote
na kutuka kwake kabla ya
makadirio kutoa nafasi na

baaada ya miaka mingi


ya mapambano yenye
kuendelea kwa kuungana
upya.
Hizi ee ndugu yangu
msomaji ni baadhi ya
fikra na hisia na maana
mbalimbali yaliyokuja
katika kurasa za kitabu
hiki na ninataka kufanya
uzindushi kwenye
kwamba, mtungaji wa
k i t a b u M wa n a c h u o n i
Mkubwa sana AlUstadh Fethullah Gullen
hakudai kwamba yeye
yuko katika uwanja wa
tafsiri kutokana na zile
ambazo amezishughulikia
miongoni mwa aya za
Q u r a n p a m o j a n a
kuyamiliki kwake masharti
yote ya maarifa ya kutafsiri
na zana zake na yote
ambayo ameyafanya. Ni
kwamba yeye amesajili
katika kitabu hicho yale
aliyoyapokea miongoni
mwa miwako na mingao
na ishara mbalimbali
kutokana na baadhi ya
yale yanayomeremeta
katika mbingu ya hisia
yake yenye nguvu kutoka
katika nyota za Quran.
Na pamoja na hayo, kwa
hakika yeye hakughafilika
kabisa na maoni ya wafasiri
wengine katika aya
ambazo amezizungumzia,
isipokuwa yeye
amejipanua kidogo katika
aya hizo na zimeweka

k a t i k a m a wa z o ya k e
fikra na maana mapya
yaliyoongezwa ambayo
aya zinayachukua
kutokana na muundo wake
wa kilugha na wakifasihi
na hazivuki mpaka kabisa
katika kuwa mbali na
misingi ya tafsiri na nguzo
zake zenye kujulikana.
Hapana shaka kwamba
mawazo haya yalitolewa
na mazingira ya wakati wa
wakati huu na yaliyafunua
hayo maarifa ya wakati
huu na elimu zake na
maelekezo yake ya kifikra
na ya kiroho na Mwenyezi
Mungu amrehemu AnNours ambaye alisema:
Hakika zama ni mfasiri
mkubwa sana wa Quran.
Na mimi nina matumaini
makubwa sana kwamba
mawazo haya kuhusiana
na baadhi ya aya za Quran
tukufu yatapata mwangwi
mpana sana katika fikra
ya msomaji wa Kiarabu
n a h i s i a ya k e , k wa n i
kuyafasiri haya matendo
ya wito na ya kifikra ya
Al-Ustadh Fathullah
kwenda kwenye lugha
ya Kiarabu ni kitendo cha
kuzichangamsha fikra na
kazi hizi ni kubadilisha
katika uwanja wa maarifa
ambako ni kuzuri sana
kali ya akili za wenye

kushughulika na mambo
ya imani na masuala ya
Uislamu hapa Uturuki na
huko katika ulimwengu
wa Kiarabu.
N i n a m u o m b a
Mwenyezi Mungu amlipe
kutokana nasi Al-Ustadh
aliye mbora Fethullah
Gullen malipo na rehma
ya M we n ye z i M u n g u
mwenye uwezo mkubwa
sana, ayaweke malipo
hayo katika madaftari ya
matendo yake katika siku
ambayo hayatafaa mali
wala watoto isipokuwa
kwa atakayemwendea
Mwenyezi Mung u na
moyo uliyosalimika.
Ya e l e w e h a y o , n a
sifa njema anazistahiki
Mwenyezi Mungu
m wa n z o n a m w i s h o .
Arehemu Mwenyezi
Mungu na aokoe na
abarikiwe juu ya mwisho
wa Manabii na Bwana
wa Mitume Muhammad
(s.a.w.) aliye mwaminifu
na juu ya jamaa zake na
maswahaba zake wote.
(Huu ni utangulizi
kama ulivyoandikwa na
Adib Ibrahim A-Dabbaqh
wa Kitabu Miyangaza
ya Quran katika mbingu
ya hisia kilichotungwa
na Muhammad Fethullah
Gullen. Kimefasiriwa
kutoka Lugha ya Kiarabu
kuja katika Kiswahili na
Sheikh Suleiman Amran
Kilemile.)

(Mwa 21:15)
Na k a m a t uj ua v y o ,
kisima cha Zamzam pia
kiko katika eneo lile Parani
(yaani kule Makka), kama
ilivyosema Qur'an:
M o l a we t u M l e z i !
Hakika mimi nimewaweka
baadhi ya dhuriya zangu
(Hajara na Ismaili) katika
bonde (hili la Makka) lisilo
kuwa na mimea, kwenye
Nyumba yako takatifu
(ya Al- Kaaba), ewe Mola
wetu Mlezi, ili washike
swala, Basi zijaalie nyoyo
za watu zielekee kwao,
na waruzuku matunda,
ili wapate kushukuru.
(Surar Ibrahim, 14:37).
Ni kwa sababu ya tabiri
za dhahiri kama hizi
ndani hata ya Taurati (ya
watu wa Kitabu, yaani
Mayahudi na Wakristo),
ndiyo Mayahudi walimjua
na kumtazamia kuja Nabii
wa Mwisho, na wakajua
kwamba atatokezea kule
Parani, yaani Makka.

Hiyo
aya
ya
Kumbukumbu la Torati
( D e u t e r o n o m y ) , k wa
mujibu wa Makala ya
Kiarabu iliyopigwa chapa
j i j i ni L o nd o n m na m o
mwak wa 1944, imeandika
kama hivi:
Deuteronomy 33:2 He
came with myriads of holy
ones, in his right hand was
an axe of fire with two edges.
Ambayo maanaye
kwa Kiswahili ni kama
i f u a t a v y o : A l i k u j a
n a wa t a k a t i f u we n g i
(maswahaba) na katika
mkono wake wa kuume
akiwa na shoka (jambia)
lenye ncha mbili.
(Kumbukumbu la Torati
33:2)
Aya hii inaongelea juu
ya Nabii aliyetabiriwa
ambaye atakuja na
maswahaba wengi ambao
ni watakatifu sana, na
ataruhusiwa na ataamriwa
kupigana na maadui zake
wakimchokoza.
(Uchambuzi wa Maisha
ya Nabii Muhammad,
kama ilivyoandikwa na
M. Fetullah Gulen.)

Nabii aliyekuwa akingojewa


haq (Isaka) ni ndugu,
kwa kuwa wote ni vizazi
vya babu yao mkuu nabii
Ibrahim (a.s).
Ya a n i Wa a r a b u
walitokana na Nabii Ismail
(Ishmael), na Wayahudi
walitokana na nabii Ishaq (Isaac). Kwa hiyo
Waarabu ni mabinamu
wa Wayahudi. Isikilize
Biblia inavyotuarifu juu
ya ndugu hawa-Waarabu
na Wayahudi:
Yale maji, ambayo
Ibrahimu alimuachia
Hajiri (Hagar) na mwana
wao Ishmaeli yakaisha
katika kiriba, akamlaza
kijana (Ishmaeli) chini
ya k i j i t i k i m o j a . 1 6 :
(Hajiri) Akaenda akakaa
akimkabili (Ishmael) mbali
naye kadiri ya mtupo wa
mshale, maana (Hajiri)
alisema, Nisimwone kijana
(lshmaeli) akifa (kwa kiu),
naye akakaa akimkabili,
akapaza sauti yake, akalia.

17: Mungu akasikia sauti ya


kijana (Ishmaeli). Malaika
wa M u n g u a k a mw ita
Hajiri kutoka mbinguni,
akamwambia una nini
Hajiri? Usiogope, maana
Mungu amesikia sauti ya
kijana (Ishmaeli) huko
aliko 18: (Ewe Hajiri, hebu)
ondoka ukamwinue kijana
(Ishmaeli), ukamshike
mikononi mwako, Kwa
kuwa nitamfanya kuwa
taifa kubwa (la Waarabu).
19: Mungu akamfumbua
macho, naye akaona
kisima cha maji (Zamzam)
akaenda akakijaza kiriba
maji, akamnywesha kijana.
20: Mungu akawapa na
huyo kijana (Ishmaeli),
naye akakua, akakua,
akakaa katika jangwa,
akawa mpiga upinde. 21
: (Ishmael) Akakaa katika
jangwa Ia Parani, mama
yake (Hajiri = Hajara =
Hagar) akamtwalia mke
katika nchi ya Misri.

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

CCM na CUF Zanzibar: Viwili visivyochagulika!


Na: Mwandishi Maalum

KUNA msemo maarufu


wa K i s wa h i l i u s e m a o ;
Viwili vyachagulika!.
Naam! Swadakta kwa
kiasi fulani. Lakini kwa
upande mwengine, usemi
huu una mapungufu au
labda tuite mipaka yake.
Kwamba licha ya usemi huu
kuwa na ukweli kwa kiasi
kikubwa, ikumbukwe kuwa
sio kila siku, kila wakati na
kila mahali kuwa msemo
huu utasadifu na kusibu
muktadha unaoaminiwa na
kukubaliwa na walio wengi
tukiwemo mimi na wewe!
Mfano ulio hai kuthibitisha
mapungufu ya usemi huu
ni ule wa vyama vikuu
viwili vya siasa Tanzania,
hasa hasa kwa upande wa
Zanzibar, yaani vyama vya
CCM na CUF. Tukiipigia
kijicho cha historia, siasa ya
vyama vingi nchini iliingia
rasmi mwaka 1992. Kwanini
nianzie mwaka huo? Naam!
Nataka nipime uhai na umri
wa neema hiyo ya vyama
vingi ambayo pamoja na
kuwa lengo lake kuu ni
kukuza demokrasia, kijuu
juu ifahamike kuwa lengo pia
ilikuwa ni kuwapa wananchi
fursa ya kujichagulia kile
waonacho chafaa!
Ikumbukwe hapo awali,
enzi ya chama kimoja
kushika hatamu, kwenye
karatasi ya kura tulikuwa
tukiwekewa ukuta na mtu
kama mgombea. Hapa
ilikuwa huna hiari ama
upige ngumi ukuta uumize
mkono wako, au umchaguwe
kiongozi aliyepitishwa na
wenye nguvu. Chaguo ni
lako kusuka au kunyoa.
Kimantiki, huu haukuwa
uchaguzi wa kidemokrasia
kwani haukumpa mwananchi
sauti na fursa ya kuchagua
kile akipendacho. Sasa hivi ni
miaka ishirini na mbili tangu
kuja kwa demokrasia ya
vyama vingi nchini. Ni muda
muafaka ambao unatupasa
tuyahakiki na tuyatathmini
mafanikio tuliyoyapata kwa
kuwa na mfumo huo nchini.
Ukiuangalia umri
wa kile kiitwacho vyama
vingi nchini, na ukiangalia
mabadiliko ya kimaendeleo
na matarajio ya mwananchi,
utakuta hayaridhishi ingawa
hatua japo ndogo imepigwa.
Mambo hayaridhishi
kinamna gani? Kuna sababu
nzima hapa! Sababu yenyewe
ni kwamba baada ya CCM
kukosa umashuhuri na
kupoteza nguvu ya umma
hasa visiwani, vyama
vilivyojitokeza kuipinga
CCM, licha ya kupata nguvu
kubwa ya kuungwa mkono
na wananchi, vilirejea makosa
yale yale yaliyoiangusha
CCM visiwani.
Nakumbuka hadi kufikia
miaka 25 tu, CCM ilishakuwa

mzigo usiobebeka tena kwa


wananchi wa Zanzibar.
Utawala wa mabavu,
siasa mbaya za muungano
unaolenga kuibana na
kuifuta Zanzibar katika
ramani ya dunia ni sehemu
ya makununu yaliyoibwaga
chali CCM visiwani. Pamoja
na hayo na zaidi ya habari,
sera ambazo zilipelekea
udumavu mkubwa wa
maendeleo ya kiuchumi na
kijamii Zanzibar na ubaguzi
wa wazi wazi wa kuibeba
Tanganyika na Watanganyika
k w e n y e k i l a n a f a s i ya
uongozi na kuwadharau
Wazanzibar ni chache tu
ya sababu zilizoiuwa CCM
visiwani mpaka kufikia hali
ya kusimamiwa na nguvu
za dola ili kubakia kwenye
hatamu hadi hivi leo.
Wakati CCM ikikosa nguvu
visiwani, CUF iliibuka kwa
kishindo na kuungwa mkono
nchi nzima. Uchaguzi wa
mwaka 1995 ukawa shahidi
wa h a ya . K i l i c h o t o k e a ,
kimezaa utamaduni ulioweza
kuipa CCM thubutu na
n g u v u ya k u j i n ya k u l i a
m a d a r a k a k i u b we t e n a
kubaki madarakani bila
kupingwa hadi leo. Kuna
habari, toba sikio, kuwa
katika uchaguzi wa 1995,
dunia nzima ilishakuwa na
taarifa za kuaminika kuwa
CUF kupitia mgombea wake
Maalim Seif Sharif Hamad,
ilishinda uchaguzi huo wa
urais.
Taarifa za habari za siku
moja kabla ya matokeo
rasmi ya uchaguzi wa urais
Zanzibar kutangazwa,
zilishatangaa habari zikitoa
bishara ya ushindi huo.
Maalim Seif, akijua wazi
ameshinda, alijifungia
nyumbani kwake Mtoni
Kidatu akisubiri kisakina
cha CCM kikamchukuwe
kimpeleke Ikulu akawe Rais.
Ajizi nyumba ya njaa! Wazee
wa CCM wakakutana usiku
kabla ya matokeo na mmoja
kati ya viongozi mashuhuri
zaidi wa Tanzania wakati
huo alisema; Hajawa tayari
kuwa Rais. Msimtangaze!.
Na ilikuwa kweli tupu. Siku
iliyofuata jioni Komandoo
akatangzwa! Kilichotokea
b a a d a ya h a p o n d i c h o
tunachokiona hadi hivi leo.
Sina haja ya kukumbusha
kilio matangani.
Ukweli usio chenga chenga
ni kwamba Maalim hakuwa
tayari. Na kwa vile hakuwa
tayari hakutangazwa kuwa
mshindi wa Urais mwaka
ule, na uchaguzi uliofata wa
2000 akaambulia ngangari
feki, na uchaguzi mwengine,
na uliofata. Uchaguzi ujao,
hatujui hali itakuwa vipi!
Huo ndio ukweli ambao
wananchi, hasa hasa,
wafuasi wa chama cha CUF
wanaoamini siasa za chama
chao kibubusa wanakuwa
wagumu kuuamini hadi hii

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia katika viwanja wa


Kibandamaiti, Zanzibar.
leo.
CCM Zanzibar wao
wanajua fika kuwa hawana
nafasi kwa wananchi hata
wakifanya sarakasi za aina
gani na usanii wa kiwango cha
miujiza, wanajua hawashindi.
Lakini watafanyeje wakati
huyo ambaye wananchi
wanamtaka hajawa tayari
kuchukuwa nchi?
Tumeambiwa na maandiko
kuwa historia inajirudia.
Na kama hayo ni kweli,
ni yumkini kusema kuwa
CUF kama ilivyokuwa ASP,
haikuwa na nia ya kuiongoza
nchi kiudhati. Kwani haingii
akilini hata kidogo kuwa
chama ambacho kinaungwa
mkono na asilimia sabiini ya
wapiga kura au zaidi, kiwe
hakishiki hatamu daima.
Tena kwa visingizio tu vya
kuwa keli tumeibiwa, kelije
hatukupewa au hanrere
hanrere za wenzetu wana
nguvu ya dola watatuuwa
sote tubebe jukumu ahera!
Siasa si mchezo wa bao,
kuwa usafiri na utakase kisha
ulale kwenye kishimo bila
ya kutoa gharama na hata
kuondoka wala kutoka jasho.
Siasa yataka ujasiri wakati
fulani.
Ila ni kweli pia kuwa
siasa yahitaji busara. Watu
wapatane bila kumwaga
damu. Lakini iwapo tu
watu wote wa pande mbili
watakuwa na misingi
ya k u t e n d e a n a h a k i n a
kuheshimiana. Kinyume na
hapo, inakuwa ngumu.
Chakushangaza siku hizi
CUF hufanya manyanga
yake kwenye uchaguzi kisha
kikishapoteza, badala yake
hushikilia dharura za kujitoa
kimaso maso na kuwapaka
wananchi mafuta kwa nyuma
ya chupa kwa kuwaambia
uongo huu na ule. Mathalan,
walipokosa kushika hatamu
katika uchaguzi wa kwanza,
CUF walisema walishinda

lakini hawakupewa
ushindi yaani waliibiwa
na kuporwa ushindi wao.
Tangu hapo hadi leo, huo
ndio umekuwa wimbo wao
wa kuwadanganya wananchi
ambao hadi sasa hawajaamka
kuwa CUF ni chama cha
watu tu wenye kuwachezea
mchezo fulani wa kisanii ili
kupata maslahi yao binafsi na
hata sio ya kichama angalau.
CCM, ilikuwa na iko kama
hivyo tangu zamani. Na kwa
bahati mbaya, CUF imefuata
nyayo hizo hizo. CCM ya leo
imejaa viongozi wabinafsi.
Ubinafsi huzaa ufisadi.
CCM imejaa watu wasio
na uchungu na nchi yao na
hata hawawaonelei huruma
wananchi wanaowaongoza.
Nayo CUF imefuata nyayo
hizo hizo tena. Kwa mfano,
mchakato wa kuwapata
wabunge na wawakilishi
wa CUF umejaa ukiritimba.
Na hata hao viongozi
wenyewe wa majimbo
wakishapatikana, huoni
wanachokifanya majimboni
zaidi ya ujasiriamali wao
binafsi.
Ndani ya CUF kuna watu
a m b a o n d i o n g u z o ya
kipembe ya CUF. Lakini
kisichojulikana ni kuwa
nguzo hiyo haimaniki wala
haitegemeki kwa sababu ni
mbovu na ndio chanzo cha
chama cha CUF kubwagwa
hata kikishinda uchaguzi
kwa asilimia mia ngapi!
Tusiwasahau na wale
waliojivisha mbawa ili wakale
karamu ya ndege angani.
Shiba ilipowazidia mbawa
zikapapatuka wakaanguka
chini. Ukweli ukafichuka.
Tukawajuwa kuwa walikuwa
wanafiki ndani ya chama. Na
mifamo haiishii hapa tu. Kuna
makobe wengi ndani ya CUF
waliojivalisha mbawa ili kuila
karamu ya ndege angani.
Wakishashiba tu, warudi
chini makwao waje waongeze

kula majani na kufuja


mpunga wa wanyonge. Na
ni kwa utamaduni huu huu,
ndio ulioibwaga CCM ambao
leo hii CUF imeona ni njia
nzuri kwao kuifuata. Njia
iliyomtia kipofu shimoni,
akiipita tena mwenye macho
yake akatumbukia humo
pia, huyo huitwa ujinga au
juha kalulu. Maafa yakimfika
huwa ni maafa ya kujitakia
na haambiwi pole asilani. Na
hapo ndipo CUF inapojikwaa
ikaingia mkumbo mmoja na
shimo moja na CCM!
Kwa kufunga mjadalala,
labda niseme kuwa pamoja
na yote hayo, hoja inabaki
kuwa wananchi wa Zanzibar
wanahitaji mabadiliko. Na
mabadiliko hayo yanatokana
na vyama na sio UAMSHO
k a m w e . Wa n a h i t a j i n a
kutaraji vyama vyao vya
siasa wanavyoviamini
na kuvikubali kuwa
vitawafikisha pazuri.
Hofu yangu, baada ya
miaka ishirini ya danganya
toto ya CUF kwa wananchi
waliokwisha ikacha CCM
iliyokwishafeli kabla ya
kuzaliwa CUF, naona ipo haja
kwa CUF kubadilika haraka
iwezakanavyo ili kurudisha
matumaini ya wananchi
ambao nayo muda si mrefu
yatapotea. Pemba itaacha
kuiamini tena CUF ingawa
haitaiunga mkono tena CCM.
Itakubali isipige kura au
iuze vipande vya kupigia
kura kwa vyama vyengine,
kwa kuonyesha kukata kwao
tamaa kulikotokana na vyama
vyao walivyovipenda kuishia
kuwasaliti yaani CCM na
CUF. Na ikifikia hatua hiyo,
wa n a n c h i wa t a s h i n d wa
kuamua wachaguwe kipi,
maana vyama vyote viwili
CUF na CCM vimefanana
kwa kila hali! Havichaguliki!

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Imekuwa hamkani sio shwari tena


Na Ben Rijal

HAMKANI sio shwari


tena. Kumekuwa hakukai
sawa na kila kukicha
ya n a k u wa h a y o k wa
hayo maji ya futi na
nyayo. Kusema kweli
tunaambiwa kuwa ili
tuweze kuendelea na
kujua hapa tulipo kama
kuna mustakbala mwema
huko mbele, ni muhimu
kuzingatia kufanya utafiti
katika nyanja mbalimbali
kuanzia kilimo, afya,
kijamii, mazingira, elimu,
mawasiliano, n.k.
Tafiti nyingi za Afrika
zinakosa kupatiwa fedha
za kutosha na matokeo
yake huwa kinyume na
matarajio na inaelezwa
kuwa kila kukicha katika
nchi za Afrika, badala ya
kuongezewa bajeti za tafiti
matokeo yake huwa fedha
za tafiti hupunguzwa.
Kwa mfano nchini Afrika
Kusini nchi ambayo ina
uchumi imara kati ya nchi
za Ki-Afrika mwaka wa
2014 iliripotiwa kuwa
fedha za kufanyiwa utafiti
z i m e p o r o m o s h wa n a
serikali kuu kwa asilimia
0.71 kutokana na pato la
kila mtu (GDP) unaposikia
haya unapata kiwewe na
kujiuliza Afrika inaelekea
wapi?
Najaribu kuzungumzia
tafiti kijuu juu kwasababu
mengi yanayotupeleka
kombo nikutokana
kuwa hatufanyi tafiti,
tunaulizana kwanini siku
hizi Polisi wamekuwa
wakimkamata mtu huanza
kumtwanga vya kutosha
hata akifika kituoni huwa
yupo hoi au kama huku
tusemavyo chicha kabisa.
Kuna sababu ya haya
kutendeka na ili tuweze
kupata jawabu kunatakiwa
kufanya utafiti.
S u a l a l a m a g a r i ya
daladala kupiga nyimbo
k wa s a u t i k u b wa n a
madereva wake kuwa
uhuni upo mbele koliko
ustaarabu, kwanini
yanakuwa hayo? Kuna
sababu na Kenya waliwahi
kufanya utafiti katika
makondakta na utingo
wao kujua kwanini
wanafanya mambo yalio
sio ya kikawaida, tafiti
ilikuja kufichua kua zaidi
ya asilimia 80 kati ya
madereva na utingo wa
matatu huwa wanavuta
bhangi.
Nchini India walikuja
kupata soko la kuuza vyura
nchini Sweden na vyura

Kituo Kikuu cha Daladala Kuhamia Kiswandui

Jengo la Kiswandui na Kituo cha mabasi ya Kiswandui.

SEHEMU ya kuegesha magari Darajani.


vyote vilikuja kutokomea
k a t i k a m a s h a m b a ya
mpunga, wakulima
walipata tija ya muda
mfupi, baada ya mwaka
tu, uliingia ugonjwa wa
mpunga kukunyaa na
kushindwa kuvuna, utafiti
ulipofanyika kujulikana
sababu ya maradhi hayo,
ilikuja kugundulikana kua
vyura walikuwa wakila
bakteria ambao bakteria
hao ndio waliokuja kuleta
madhara, kwa kukosekana

kukuweko kwa vyura.


Tafiti ni muhimu sana
sana na kukosekana
kufanyika tafiti matokeo
yake ni kuendelea kuwa
na kilema kisichoponyeka
ikiwa kilema hicho
kinaponyeka.
Nimejaribu kujenga
hizi hoja kutokana na
azma ya makala haya juu
ya kituo cha Daladala
kilichohamishwa kutoka
hapo Darajani na
kuhamishiwa Kisiwandui

na eneo hilo lilokuwa kituo


cha daladala hivi sasa
ni sehemu ya kuegesha
magari ambao watu
hutozwa ada. Nitanena
kama wanenavyo wengine
kunena kuwa kuondolewa
kwa kituo cha Darajani
kulifanyika pasi na
kufanywa utafiti ila tu jazba
na utashi wa wahusika
ndio walikurukupa na
matokeo yake kwa sasa
kuwa na kila aina ya adha
na baa na belwa mtaa wa

Kisiwandui.
Kama wakuu wa Baraza
la Mji wangefanya utafiti,
ingebidi kubakia na kituo
kile na huku wanatafuta
njia nyengine ya kudumu.
Lazima mwenye kuhusika
na watu ajuwe hao watu
wapo idadi ngapi na
wangapi wenye vipando
vyao hawategemei
vipando vya Umma na
wangapi wanatumia
magari ya serikali n.k.
Aidha, mtafiti
anaangalia kukua na
kuongezeka kwa watu nini
kinahitajika kufanyika,
kwa mfano kisiwa cha
Zanzibar katika mwaka
wa 1964 idadi ya watu
wake ilikuwa ni watu laki
tatu (300,000) laki mbili
ikiwa imestakimu Unguja
na laki moja ipo Pemba
na kutokana na Sensa
iliopita ya mwaka wa 2012
inatueleza kuwa idadi ya
watu wa Zanzibar kwa
sasa ni Milioni moja na laki
tatu (1,300,000) ongezeko
hili la watu linaingia
katika masafa yale yale
ya kisiwa ambacho watu
wameongezeka lakini
masafa ya kisiwa ndio yale
yale au unaweza kusema
hata yanapungua kwani
tunaelezwa kuwa kuna
maeneo yasiopungua 125
yamevamiwa na maji ya
chumvi baadhi ya maeneo
h a y o ya l i k u wa n i ya
kilimo, mengine ni makazi
ya watu.
Katika miaka ya sitini
kituo hicho cha Darajani
kilikuwa kinapokea
magari kwa siku nzima
magari yasiozidi 15
yakiwa ya Makunduchi
mawili, Fuoni moja,
Jumbi mawili, Nungwi
moja, Mkokotoni moja,
Kizimkazi moja, Chwaka
moja, Ndijani moja,
Bumbwini, Mangapwani
moja, Bwejuu moja,
Matemwe moja n.k Hio ni
miaka ya sitini kwa mfano
gari kutoka Makunduchi
likiingia mjini linabakia
hapo hadi mchana ndio
linarudi huwa na safari
moja tu kwa siku. Leo gari
hizo zinafanya hata safari
tatu kwa siku kutokana
n a m a h i t a j i ya wa t u .
Magari yameongezeka
kutokana na idadi ya
watu kuongezeka ambao
wanahitajia usafiri
nathubutu kusema kwa
siku ingia toka ya magari
hapo Darajani yanafikia
i d a d i ya k u i n g i a n a
kutoka kwa magari mia
Inaendelea Uk. 13

10
Na Omar Msangi
HIVI karibuni mwandishi
Mohammed Ghasani
aliandika makala
n d a n i ya k e a k a h o j i ,
k o s a l a Wa z a n z i b a r i
nini hata Tanganyika
iwanganganie hivyo
na kutowapa fursa ya
kupumua na kuamua aina
ya muungano wanaotaka.
Jibu la swali hilo
analieleza vizuri Waziri
M h e s h i m i wa Wi l l i a m
Lukuvi wakati akiongea
na waumini wenzake
Wa k r i s t o k a n i s a n i .
Anaeleza Mheshimiwa
L u k u v i a k i a n z a k wa
k u w a h o j i Wa k r i s t o
wenzake:
Eti tuwaache
W a z a n z i b a r i
wa j i t a wa l e w e n y e w e
n a Wa t a n g a n y i k a
Wazanzibari kule waliko,
asilimia 95 ni Waislamu.
Tunataka wajitangazie
serikali ya Kiislamu kule!
Hapana. Sauti
inasikika baadhi ya
waumini wakijibu. Kisha
anaendelea kuuliza
Lukuvi:
Mnajua madhara
yake? Inasikika sauti
ya waumini wakijibu:
Makubwa sana.
Wa z i r i L u k u v i
anaeeleza: Wale Waarabu
watarudi. Watazalisha
siasa kali kule watakuja
kutusumbua.
Mimi najua, kabisa.
Kwa hiyo ndugu zanguni,
mnaposikia mjadala kule,
kuna watu unaweza kuona
kama wana nia njema
wanataka kuwasemea
wale wanaoitwa
Tanganyika, lakini wana
siri yao moyoni. Kwamba
labda ikipatikana hii
serikali na sisi tutashinda
tutatawala.
Zanzibar ni nchi ndogo
sana. Ina watu milioni
moja na laki tatu. Sisi tuna
milioni arobaini. Unaweza
ukauliza, kwa nini sisi
tunaingangania sana ile?
Lakini sisi tunaangalia
mbele. Madhara ni
makubwa kuicha Zanzibar
kama ilivyo.bora tuwe
nao.
Bwana Ghasani, hilo
ndio jibu. Zanzibar
i k i a c h w a , Wa a r a b u
watarudi, watazalisha
Waislamu siasa kali,
wataisumbua Tanganyika.
Labda sasa swali ni je,
kwa nini Zanzibar nao
wasiwe na wasiwasi kuwa
wakiwa chini ya makucha
y a Wa t a n g a n y i k a ,
Wakristo watawapa tabu
Waislamu wa Zanzibar?
Mheshimiwa William
Lukuvi na wale aliokuwa
akiwahubiria kanisani,

Makala

Ghasani, hili ndio kosa la Wazanzibari.

Kila uchochoro Mji Mkongwe


akina William wanaona gaidi

Ila kama ni balaa wataleta Wazungu na


Wanaopiga kampeni za chuki kanisani
Sio hizi porojo za Waarabu wa Oman

SULTANI wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho


Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa
iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri
ya AL Alam jijini Muscat Oman.

MHE. William Lukuvi akiwa Loliondo enzi za 'kikombe cha babu'.

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015


hawana wasiwasi huo
kwa sababu Wazanzibari
wenyewe wanaimba
wimbo huo huo, wagawe
uwatawale-Hawana
agenda ya Uzanzibari
wala ya Uislamu. Lao ni
Pemba Vs Unguja na hofu
ya kurudi Muarabu!!!
Inalillahi waina ilaihir
rajiuun!
Maadhali hiyo ndiyo
hali ya Wazanzibari, sina
haja ya kuwazungumzia
h a p a . A g e n d a ya n g u
itakuwa pana zaidi. Hili
la Waislamu siasa kali
ambao Mheshimiwa
L u k u v i a n a d a i k u wa
watazalishwa Zanzibar
kukiwa na serikali ya
Kiislamu.
Japo suala la Zanzibar/
Tanganyika na mfumo
wa Muungano lina
historia ndefu toka wakati
wa M wa l i m u , l a k i n i
anachozungumza hapa
M h e s h i m i wa L u k u v i ,
ni propaganda ile ile
iliyobuniwa na mabeberu
katika kutekeleza malengo
yao. Naye sasa anaitumia
kufanikisha siasa za
Tanzania katika suala
la muungano, lakini pia
katika kuendeleza ile
Crusade aliyotangaza
Bush.
K a m a wa l i v y o s e m a
wataalamu mbalimbali
kuwa hakuna mtu
mwenye akili yake timamu
anayeweza kuamini kuwa
kuna gaidi anayeweza
kutoka Afghanistan au
Uarabuni na kufanya
g h a r i k a k a m a i l e ya
Septemba 11, Marekani,
hakuna pia mtu mwenye
akili yake timamu
anayeweza kuamni kuwa
Waarabu wa Oman au
Wafursi wa Iran, wana
mpango wa kuja kuikalia
Zanzibar. Lakini ni
uwongo tu unaozuliwa,
ikapigwa propaganda na
wakapatikana wajinga wa
kuamini propaganda hiyo
ili yatimie yanayotakiwa
katika siasa.
Kama ni kuvamia nchi,
na kama ni kuvurugwa
nchi zetu, zitavurugwa na
Wazungu wanaoivuruga
Ukraine hivi sasa kwa
s a b a b u ya k u p i g a n i a
mafuta na gesi na kusimika
hegemonia (hegemony)
yao katika eneo hilo.
Inayoitwa vita dhidi ya
ugaidi, vita dhidi ya siasa
kali hivi sasa ina miaka
14. Ilianza rasmi mwaka
2001 baada ya Sepetmba 11
ikafuatiwa na uvamizi Iraq.
Kwa muda huo wa miaka
14 wa kuunda majinamizi
na mazimwi kwa jina la
Taliban, Osama bin Laden,
Saddam Hussein, Gaddafi,
Inaendelea Uk. 11

11
Inatoka Uk. 10
Assad, Al-Shabaab, ISIS,
IS, Boko Haram n.k, nchi
zaidi ya saba zimevamiwa,
k u p i g wa m a b o m u n a
kushambuliwa kwa
makombora ya drones.
Hawa akina Karl Peters
wanaofanya haya, ndio
wa kuhofiwa kuwa wana
mpango wa kurudi
kutukalia au kutuletea
machafuko tuuwane
wenyewe kwa wenyewe
kisha wajifanye wasamaria
we m a wa k u t u s a i d i a
kijeshi na kikachero.
Na wakifanikiwa hilo,
machafuko hayaishi. Ndio
hali ya Nigeria, Yemen na
kwingineko.
Mamilioni ya Waislamu
wameuliwa kwa sababu ya
uwongo na propaganda
zao, mamilioni wakatiwa
vilema na mamilioni hivi
tunavyoandika, wamebaki
kuwa wakimbizi.
Kwa wenye chuki na
Waislamu, mara nyingi
huwa hawaangalii athari
ya machafuko, vita na
kuangamizwa kwa
nchi wala ile agenda ya
ujumla ya mabeberu.
Wanachotizama ni kuwa
Waislamu wameuliwa,
wanabamizwa. Wanameza
propaganda ya ugaidi
na kuhalalisha kuuliwa
Waislamu.
Ukirudi nyuma
kulikuwa kuna kitu
kinaitwa Operation Gladio
(Italian: Operazione
Gladio) au "stay-behind".
Walikufa sana Wazungu
wa Ulaya. Na hawa
walikuwa ni Wakristo.
Mabeberu katika Staybehind operations
zao ndani ya nchi za
NATO, hawakujali kuwa
wanaokufa ni Wazungu
w e n z a o n a Wa k r i s t o
wenzao pia.
Hivi sasa Ukraine
kuna zogo kubwa. Watu
wanauliwa. Kisa! Wenye
uchu wa mafuta wanataka
kuitia katika makucha
yao nchi hiyo bila kujali
watakufa watu wangapi
au nchi kuharibikiwa kiasi
gani kama ilivyoharibikiwa
Iraq na Syria.
Hatukuwahi kuwa na
ugomvi na wananchi wa
Somalia wala kuwa na
adui anaitwa magaidi wa
Kiislamu kutoka Somalia
(Al-Shabaab). Lakini
mabeberu kwa masilahi
yao wameivuruga nchi ile
wamezalisha Al-Shabaab,
wamewatangaza kuwa ni
magaidi wa Kanda hii ya
Afrika na sisi kama vipaza
sauti vinavyotumia betri
badala ya akili, tumekuwa
tukiimba wimbo huo huo.
Akizungumzia vita
dhidi ya ugaidi, aliyewahi

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Kila uchochoro Mji Mkongwe


akina William wanaona gaidi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe


(kushoto) akikabidhiana mkataba na Afisa mmoja wa Oman.

kuwa Mshauri wa Mambo


ya Usalama wa Marekani
(National Security
Adviser ), Zbigniew
Brzezinski, anasema
kuwa msamiati ugaidi
na magaidi, umekuwa
ni simulizi ya kutunga
ya tangu zama ambayo
hutumiwa na wanasiasa
kisanii.
Brzezinski akieleza
jinsi sababu za uwongo
kuisingizia Iraq ugaidi
na silaha za maangamizi
zilivyoangamiza maelfu

ya roho za watu wasio na


hatia (collateral damage),
anasema hiyo ni dhambi
kubwa kwa Marekani
ambayo inaiondolea
heshma iliyo nayo duniani
kama taifa kubwa. Katika
maelezo yake marefu
kwa Kamati ya Seneti,
Brzezinski anasema
kuwa, awali Marekani
i l i t u m i a u w o n g o wa
Silaha za Maangamzi
(WMD) kuivamia Iraq.
Baada ya hapo inakuja
tena na uwongo mwingine

kuwa kuna magaidi wa


Al-Qaida na Muslim
Fundamentalists ambao
ni maadui hatari kwa
usalama wa Marekani.
Akasisitiza kuwa uwongo
huo wa kusingizia kitisho
cha ugaidi wa A-Qaidah
katika nchi za Kiarabu
ili kusimika alichokiita
U.S. regional hegemony,
utaleta madhara makubwa
ikiwa ni pamoja na
m a c h a f u k o , m a u wa j i
na kuifanya Marekani
kuchukiwa duniani

kote. ((SFRC Testimony


-- Zbigniew Brzezinski,
February 1, 2007.)
Katika makala Putting
t h e Te r r o r T h r e a t I n
Perspective iliyowekwa
katika mtandao wa
Wa s h i n g t o n s B l o g ,
inaelezwa kuwa matukio
mengi ya ugaidi na kitisho
cha ugaidi kwa ujumla,
kinafanya kupandikizwa
ili kutimiza malengo
ya kisiasa na kiuchumi.
Ikafafanuliwa kuwa nchi
za kibeberu zimekuwa
zikitumia kitisho cha
ugaidi katika nchi
zinazolengwa kupandikiza
machafuko, uvamizi na
kisha kufanikisha uporaji
wa rasilimali.
Zaidi ya kutumia
usanii wa kitisho cha
ugaidi kuvamia na kupora
nchi tajiri kwa rasilimali
kama mafuta, kitisho hicho
hutumika pia kuwasaidia
watawala kudumu
madarakani. Aliyekuwa
Mkuu wa Usalama
wa Ndani (Secretary of
Homeland Security), Tom
Ridge wakati wa George
W Bush, akatoa mfano
ambapo alilazimishwa
k u p a n d i s h a k i wa n g o
cha kitisho cha ugaidi ili
kumsaidia Bush kushinda
uchaguzi awamu ya pili.
Kwamba awatishe
wananchi kuwa magaidi
wa A-Qaidah karibuni
tu wataiangamiza
Marekani
huku
wakipewa kumbukumbu
ya Septemba 11, halafu
ionyeshwe kuwa Bush
ndiye mwenye mipango
sahihi ya kukabiliana na
kitisho hicho hivyo apewe
muda.
Ndio haya anayosema
M h e s h i m i wa Wa z i r i ,
Bwana William Lukuvi.
Kwamba, maadhali kuna
a g e n d a ya k u i d h i b i t i
Zanzibar na maadhali
hivi sasa bado kitisho cha
Waislamu siasa kali na
ugaidi ni dili, kinafanya
kazi; basi kinatumika
kuwaunganisha Wakristo
kupinga mabadiliko ya
mfumo wa muungano.
Kwa upande mwingine,
kinatumika kuwagawa
Wa z a n z i b a r i , wa b a k i
wakiogopa kitisho cha
kurudi Muarabu, badala
ya k u s i m a m a k a t i k a
agenda moja ya Uislamu
na Uzanzibari. Lakini kwa
hapo hawezi kulaumiwa
Lukuvi. Kama Wazanzibari
wenyewe hawajitambui,
M h e s h i m i wa Wi l l i a m
Lukuvi yeye afanye nini!
M we z i M e i m wa k a
2008 Chuo cha Kijeshi
(United States Army War
College) kule Carlisle,
Inaendelea Uk. 13

12

MAKALA/SHAIRI

UPOGO WA 'VALENTINE DAY' !

(SIKU YA WAPENDANAO AU YA WADANGANYANAO?)


Kalamu nimeishika, kuwauliza VIJANA,
Majibu yenu nataka, msijefanya khiyana,
Uhuni sitautaka, nijibuni kiungwana,
SIKU hii VALENTINA, ASILIYE hasa NINI ?
Amama mlojiweka, WAPAMBE wa VALENTINA,
Nipeni basi hakika, nini hasa VALENTINA,
Yu dada anotajika, au SIKU ya FITINA,
SIKU hii VALENTINA, MUASISIWE yu NANI ?
ARUBASHARA 'kifika, FEBRUARI kwa sana,
Siku hii hunadika, eti ya wanopendana!
Kwayo SHAKA ninaweka, na ninahoji bayana,
SIKU hii VALENTINA, TAREHE hii KWANINI ?
LIBASI zinovalika, ni NYEKUNDU tena sana,
DUKUDUKU lanishika, kunako yake MAANA,
Kwa wale mnojivika, tafakarini kwa kina,
SIKU hii VALENTINA, WEKUNDU huu wa NINI ?
Na NDEREMO huibuka, za MABIBI na MABWANA,
Zinaa hukurubika, si usiku si mchana,
Kwa jozi kuchanganyika, hizo na kutomasana,
SIKU hii VALENTINA, MSETO huu KWANINI ?
MAHABA yanosifika, katu si ya kiungwana,
NDUNIYE yatambulika, ni UZINIFU kufana,
Mwisho ni kuathirika, kwa GONJWA lile VIJANA,
SIKU hii VALENTINA, HATIMA yake ni NINI ?
VIJANA mnopendeka, WAPENZI wa VALENTINA,
Nyote ninawaalika, mlo na hoja mwanana,
Wazi mpate niweka, kwa marefu na mapana,
SIKU hii VALENTINA, WALENGWA hasa ni NANI ?
Kichwani natatizika, nahitaji mbayana,
Mwenye HOJA za hakika, ZA mambo ya VALENTINA,
Mezani hoja naweka, niaunini VIJANA,
SIKU hii VALENTINA, wa KUNIFUNDA yu NANI ?
Upambe sitautaka, uso na hoja za ma'na,
Japo utoke kwa kaka, au kwa dada Amina,
Sitaupa mlahaka, nakujuzeni bayana,
SIKU hii ni NAGONA, kama sio MZINGILE.
ABUU NYAMKOMOGI
MWANZA.

UVIVU WA KUFIKIRI !

Hodi hodi mhariri, si wa gazeti la giza,


Bali ni wa AN-NUUR, lenye angavu mwangaza,
Kuna jambo nafikiri, naomba kulidokeza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Uvivu niwape siri, tunaouendekeza,
Wa kushindwa kufikiri, hali ya kuwa twaweza,
Nd'o unotuathiri, pamwe na kutudumaza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Wengi likizo nadhari, zetu tumeziwekeza,
Wachache wanatughuri, kadiri wanavyoweza,
Badala wanafikiri, yetu nasi twafatiza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Kheri wakiita shari, nasi nyuma twafatiza,
Shari wakiwamba kheri, kadhalika twachagiza,
Kwa mgando tafakuri, vyovyote watugeuza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Waizushapo habari, papo hapo twaimeza,
Mia kwa mia twakiri, pasi hata kuchunguza,
Kadhalika kufikiri, twameza na kueneza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Twajiona maayari, kwa puya kuhanikiza,
Sote yatatuathiri, madharaye nawajuza,
Kwazo ikifuka nari, sote yatuteketeza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Tuchukue tahadhari, kwa kutokuhanikiza,
Tumezeshwazo habari, pasi kwanza kuchunguza,
Kwanini zetu fikari, likizo twaziwekeza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Kwa uvivu kukhitari, wa kutokujizoeza,
Kila mtu kufikiri, kadiri anavyoweza,
Taifa la tafakuri, muhali kutengeneza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Ni yako sasa hiari, kujali au kubeza,
Dhamira kukushauri, na si kukung'ang'aniza,
Ila ni kubwa hatari, falau utapuuza,
Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza.
Kaditamati akhiri, nimefika kueleza,
Akali ya kufikiri, leo yanatosheleza,
Kalamu ya tafakuri, haina la nyoongeza,
Utaja tuangamiza, uvivu wa kufikiri.
ABUU NYAMKOMOGI
MWANZA.

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Tanzania inavuna matunda


ya kuikataa historia ya kweli
Inatoka Uk. 4
Chaurembo katika
mkutano ule, alikuwapo
Sheikh Nurdin Hussein
na Rajab Diwani lakini
mzungumzaji mkuu na
aliyesukuma agenda hii
ikakubaliwa na TANU
na kutoa azimio alikuwa
Mufti Sheikh Hassan bin
Amir. Azimio lenyewe
lilikuwa yeyote atakaeleta
u d i n i k a t i k a TA N U
atatoswa. Ningependa
sana kueleza historia hii
lakini nachelea itakuwa
nje ya maudhui. Lakini
mtu unaweza ukajiuliza,
vipi katika historia ya
uhuru wa Tanganyika
majina haya hayasikiki
kutajwa?
Haiyumkiniki hata
kidogo kuwa wazalendo
hawa walipigania uhuru
wa Tanganyika ili waiweke
kwenye madaraka serikali
ambayo itakuja kuvunja
misingi ya dini yao.
Tanga kulikuwa na
Mahakama ya Kadhi na
mahakama hii ilikuwa
k a t i k a j e n g o l a TA A
Barabara ya 7 ambako
Kadhi, Sheikh Ali
bin Hemed Al-Buhry
a l i h u k u m u j a m i i ya
Waislamu kwa kutumia
Sharia. Huyu Sheikh Ali
bin Hemed Al Buhry
ndiye baba yake Sheikh
Mohamed Ali Al-Buhry
na yeye ndiye alikuwa
hakimu wa mwisho
kwenye mahakama hiyo.
Sheikh Mohamed Ali
Al-Buhry alikuja baadae
katika miaka ya 1968
kuhusika sana katika
BAKWATA na kuna kisa
cha kusisimua sana kati
yake na serikali katika
siasa za Waislamu na
BAKWATA, lakini hapa
si mahali pake kueleza
mkasa huu.
Hapo Tanga kulikuwa
na Liwali Abdallah
Rished na mtaa aliokuwa
akikaa ulipewa jina la
Liwali Street kwa heshima
yake. Baada ya uhuru
ukaitwa Makoko Street
kwa heshima ya mpigania
uhuru na mwanachama
s h u p a v u w a TA N U

Rashid Makoko.
Kulikuwa na Sheikh
Seif Nassor Alhinawy
ambae alikuwa Akida
pale Tanga na akihukumu
kwa sheria. (Akida Seif
ndiye baba ya wachezaji
mpira mashuhuri katika
miaka ya 1960 hadi 1970,
Hemed Seif, Marshed Seif
na Rashid Seif, ambao
ukimtoa Marshed wote
ndugu zake walivaa jezi
ya taifa). Kwa kuthamini
taasisi hizi za Kiislamu,
kuna mtaa Waingereza
waliupa jina Akida Road
(sasa Mkwakwani Road)
kwa heshima ya Akida
Seif Nassor.
Katika Tanganyika, mji
wa Tanga ndiyo moja ya
miji iliyokuwa na historia
nzuri sana ya Mahakama
ya Kadhi. Mwanzo wa
miaka ya 1900 kulikuwa
na Kadhi Omar Stambuli
kisha akaja Kadhi Ali bin
Hemed Al-Buhry, Liwali
Abdulrahman bin Ali
Diwani, Liwali Rished
Abdallah, Omar Stambuli,
Juma Mwindadi , Said
bin Ali Al-Buhry (OBE),
Mohamed bin Ali AlBuhry.
Masheikh hawa baadhi
yao walifanya kazi ya
ukadhi Tanga na wengine
walikuwa Moshi, Arusha,
Mwanza na kwengineko
Tanganyika.
Tabora Sheikh Bilali
Mshorwa alikuwa
akihukumu kwa sheria
mahakamani. Huyu
Sheikh Bilali Mshorwa
akifahamiana vizuri
sana na babu yangu,
Salum Abdallah pale
Tabora kwani wao ndiyo
walikuwa wanamji na
wazee wa mjini wakati
wao. Moshi kwa Wachagga
alikuwapo Liwali Mussa
Mwinjanga akihukumu
Bomani. Liwali Mussa
alikuwa akifahamiana
na baba yangu na mtaa
aliokuwa akiishi Liwali
Mussa Mwinjanga toka
enzi hizo za ukoloni
ulikuwa ukijulikana kama
Liwali Street na jina hili
limebaki hivyo hadi hii
leo.

Hali ilikuwa hivi


Tanganyika nzima na
M a h a k a m a ya K a d h i
haikupata kuwa katika
agenda ya kufutwa uhuru
utakapopatikana. Nini
kilifanya serikali mwaka
1963 ivunje mahakama
hizi? Jibu ninalo lakini
sitalitoa kwa sasa.
Kuna watu wanasema
ati kuwa na Mahakama ya
Kadhi itavunja umoja wa
taifa letu. Hapa linakuja
swali, kwani Tanzania huo
umoja unaozungumziwa
tunao hivi sasa? Mbona
kumekuwa na malalamiko
mengi tu kutoka kwa
Waislamu kuwa serikali
ina udini na inawabagua
Waislamu?
Hii ilianza kama
manunguniko ya
chinichini kwa miaka
mingi na mwisho ikaibuka
kwa sauti kubwa kuwa
nchi yetu inatawaliwa na
Mfumokristo yaani nchi
inaendeshwa kwa maslahi
ya Kanisa. Mwaka wa
2012 Waislamu walifanya
mikutano nchi nzima
wakitahadharisha kuhusu
hili. Video za mikutano hii
zimezagaa nchi nzima na
kwenye mtandao. Bahati
mbaya hadi leo serikali
imekuwa kimya.
Labda mtu unaweza
kujiuliza kwa nini serikali
i m e k u wa k i m ya k wa
shutuma nzito na za hatari
kama hizi? Imekaa kimya
kwa kuwa yanayosemwa
n a Wa i s l a m h a y a n a
ukweli na ithibati yoyote
au iko kimya kwa kuwa
i na o g o p a k ul i f ung ua
Sanduku la Pandora? Jibu
la swali hili vilevile ninalo.
Nadhani msomaji
wangu angalau kwa mbali
umeweza kusoma angalau
kwa muhtasari historia ya
nchi yetu ilivyokuwa. Vipi
tumejikuta katika huu
uhasama tunaoushuhudia
hivi sasa, hii ni mada ya
kujitegemea na In Sha
Allah tutaizungumza.
Makala hii kwa
h i s a n i ya M o h a m e d
Said kupitia blog:www.
mohammedsaid.com

13

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Imekuwa hamkani sio shwari tena


na khamsini au nazaidi.
Kituo cha Darajani
k i l i k u wa k i n a c h u k u a
abiria wa Bububu,
Saateni, Mwanakwerekwe,
Kiembe Samaki,
Chukwani, Mombasa,
Amani, Daraja bovu n.k.
Kwa mtafiti atapotaka
kukiondosha kituo kama
hicho cha Darajani,
kwanza atatafakari
kujua anahamisha
kukipeleka wapi? Atataka
kujua kwa wastani wa
magar i mang ap i kwa
s i k u ya n a i n g i a h a p o
kituoni, ataangalia katika
saa magari mangapi
yanaingia na ni wakati
gani kunakuwa na abiria
wengi wanaovutana
kutaka usafiri.
Baada ya kujiuliza hayo
anakuchukua takwimu
na kuzichambua na
j a wa b u a t a k a y o i p a t a
atachokifanya ni kujaribu
kukihamisha gari la
eneo moja tuseme
Mwanakwerekwe
atakihamishia kwa muda
sehemu moja kisha atapima
adha na urahisi wa abiria
na atapata sura halisi bada
ya majaribio hayo kusema
kupunguza msongamano
wa D a r a j a n i i t a k u wa
vyema kuhamisha magari
yaendao Kiembesamaki,
Mwanakwerekwe na
Chukwani kuwahamishia
sehemu ya iliopata kuwa
Baraza la Wawakilishi
au tuite jina lilozoeleka
Peoples Club.
Mtafiti huyo hatosita
hapo, bali atatoa na Dodoso
au Hojaji (Questionnaire)
kuwauliza abiria
wanaokusanyika hapo
nini mapendekezo yao
juu ya kuhamishwa kituo.
Zaidi ya hapo wahusika
ambao ni wa Baraza la
Mji watatakiwa wakae na
watu wa Mipango Miji
na Vijiji kuangalia njia
iliokuwa mbadala. Isitoshe
wa t a t a k i wa wa f a n y e
vipindi vya Radio na TV
kuwaelimisha wananchi
kuweza kufahamu sababu
ya kuhamishwa kwa kituo
hicho na wao watasema
nini kuhusu uamuzi huo?
Watafiti hao hapo tena
ndipo watapokuja na
suluhisho ambalo litakuwa
la kisayansi kabisa na
litalokuwa sio la kuleta
adha.
Wa s w a h i l i w a n a
msemo wao ambao mie
nitausema kwa njia ya
tarwia nayo ni unaruka
kukimbia kukanyaga haja
ndogo huku unakanyanga

kinyesi. Ikiwa ilikuwa


kupunguza kelele na adha
kwa skuli za Darajani na
Vikokotoni, basi kituo
hicho kimehamishiwa
kwenye skuli ya
Kiswandui ambayo hapo
n d i p o p a n a p o t a k i wa
kuwepo utulivu wa hali
ya juu kwani wale watoto
taahira (Mongoose) ndipo
wanaposoma aidha
Makao Makuu ya Chama
cha CCM ndipo yalipo.
Sasa la kujiuliza ndio kipi
kilichofanyika?
Jengine ambalo
linawapa watu mashaka
nikuona kituo kilekile sasa
kinaegeshwa magari ya
watu binafsi na kutozwa
shilling alfu moja kwa saa,
aah, hii ni Hamkani Sio
Shwari Tena.
Abiria wa daladala
wapo tafshanini hawajui
la kufanya hawajui la
kutenda, wamegubikwa na
maudhi ambayo hawajui
jawabu yake litatokana na
nini?
Narudia tena utafiti ni
jambo la muhimu, ikiwa
watu wataongezeka
kila kitu cha mahitaji
juu ya watu hao nacho
kitaongezeka. Sasa watu
wameongezeka na magari
yameongezeka, afana alek
unaingia mjini hujui wapi
uegeshe gari lako utapata
upenyu uliweke utakuja
k u k u t a u m e s h a t i l i wa
chuma na hao hao watu
wa Baraza la Mji ulipe alfu
kumi ndio ufunguliwe
gari yako upate kuondoka
na wiki iliopita magari
yakibebwa juu kwa
juu sijui yakipelekwa
wapi? Unajiuliza hawa
wahusika wamefanya
t a f i t i ? Wa m e t e m b e a
n c h i z a v i s i wa k a m a
Mauritius na Seychelles
wa k a o n a t a r a t i b u z a
wenzetu wazifanyazo?
Nimeshuhudia kule
Mauritius hata hizo sehemu
za pembeni ambazo
huku kwetu ni dhambi
kuegesha gari huko wao
huegesha na zimeekewa
michoro wa ukomo wa
gari za kuegeshwa. Wao
walikuja na fikra hio kujua
wao ni watu wa visiwa
na vipi ardhi ilivyokuwa
inapungua, kwa hio vipi
wataweza kuondoa adha
na kuwa na matumizi bora
ya sehemu ndogo ya ardhi
walionayo.
Hapa Unguja imekuwa
mashaka na adha baina ya
wenye vipando na watu
wa Baraza la Mji. Jengine
ambalo halijafanyiwa

utafiti ni kuona kuwa


baada ya kuchwa jua bado
watu hao wa Baraza la Mji
katika eneo la Forodhani
wanaendelea kukusanya
fedha za maegesho pamoja
na siku za mapumziko
jambo hilo halipo popote
pale duniani. Ndio
nikasema Hamkani Sio
Shwari Tena mambo yapo
mchafu koge.
Ta t i z o l a k u e g e s h a
magari katika maeneo ya
mjini na Darajani ni adha
tupu. Bado nawanasihi
wakuu wa Baraza la Mji
kufanya utafiti wa juu
ya suala hili. Watafiti
Alhamdulillahi wamejaa

kama pishi ya mchele iwe


SUZA, Chuo cha Fedha
C h u k wa n i , Z a n z i b a r
University watafiti
mmoja mmoja, jambo hili
linahitajia kuangaliwa.
Wakazi wa Kiswandui
hawana raha kuanzia
a s u b u h i ya s a a m o j a
hadi nne ya usiku kwa
makelele na moshi wa
m a g a r i . Wa n a j i u l i z a
hayo yataendelea mpaka
lini? Watoto wao wamo
kujifundisha matusi
yanayoporomoshwa na
m a d e r e va n a u t i n g o .
Wa n a p a m b a n a n a
uchafuzi wa mazingira
ya moshi na maeneo hayo

kwa kuwa havina vyo


vya haja ndogo watu
hujikojolea ovyo. Wakazi
wa Kiswandui hujiuliza
tumekosa nini? Mie
nitawambia hamjakosa
kitu wala hamtiwi adhabu,
bali tafiti zimeonekana sio
lolote wala sio chochote
kile. Amua, amua twende
mbele.
Tabu ya watu wetu nayo
nikuwa wanashindwa
kuhoji kila kitu. Utasikia
kimeandikwa sijui
kimeandikwa na nani na
hio kamwe sio Tawhidi.
Aaah Hamkani Sio Shwari
Tena.

Inatoka Uk. 11
Pennsylvania, kiliandaa
kitu kilichojulikana kama
Unified Quest 2008
(war games test). Katika
gemu hiyo ya siku tano,
iliyohudhuriwa pia na
makamanda wa kijeshi
kutoka nchi za NATO na
Israel, walisema kuwa
walikuwa wakijiandaa ni
kwa jinsi gani watalinda
masilahi ya Marekani
ndani ya nchi ya Nigeria
ifikapo mwaka 2015.
Wa l i s e m a k u wa
inatarajiwa mwaka huo
nchi hiyo itasambaratika
kutokana na machafuko
(vitendo vya kigaidi) na
kwamba hata uchaguzi
wa mwaka huo itabidi
uahirishwe. Na kwamba
kuna uwezekano mkubwa
N i g e r i a k u g a wa n y wa
kutoka katika hali yake ya
sasa ya kuwa nchi kubwa
Afrika yenye idadi kubwa
ya watu na utajiri mkubwa
wa mafuta. Pengine iwe
Kaskazini na Kusini kwa
Wakristo.
Akizungumzia suala hilo
Februari 4, 2012, Balozi wa
Marekani nchini Nigeria
Bwana Terence McCulley,
a lite t e a s e rik a li ya k e
akisema kuwa, waliofanya
utabiri huo kuwa Nigeria
itasambaratika ifikapo
mwaka 2015 haikuwa
serikali ya Marekani bali
taasisi binafsi ikijulikana
kwa jina la Rand
Corporation and BoozAllen.
Hata hivyo, taasisi hizo
ndio wakala wa serikali na

Mhe. William Lukuvi.


Jeshi la Marekani (Private
Military Contractors)
a n a ye f a n ya k a z i k wa
maelekezo na kwa kulipwa
na serikali.
K i l i c h o k u w a
kikitizamwa katika bao
hilo, ni namna ya kulinda
masilahi ya kibeberu ya
Marekani, ikiwa ni pamoja
na kupeleka jeshi na namna
AFRICOM itakavyofanya
kazi ikifika mwaka 2015
ambapo ilitabiriwa kuwa
nchi hiyo itasambaratika
kutokana na machafuko.
(Tazama: United States
Army Allegedly Preparing
For A Possible Break-Up
Of Nigeria, Nigeria: U.S.
Speaks On Nigerias Breakup. Na Cia And Mossad To
Divide Nigeria Soon)
Mapema wiki hii,
imetangazwa kuwa
uchaguzi mkuu wa Nigeria
umeahirishwa. Uchaguzi
huo ambao ilikuwa
ufanyike Februari 14,
umeahirishwa hadi Machi

S U L T A N I
w a
Oman,Qaboos bin Said
Al Said.
28. Sababu zilizotolewa
ni za kiusalama, kwamba
vyombo vya usalama
vinahitaji muda zaidi wa
kujiandaa kukabiliana na
kitisho cha Boko Haram.
Haijulikani iwapo ahadi
hiyo itatekelezwa au ndio
hatari ya kitisho itakuwa
kubwa zaidi.
Zipo taarifa nyingi juu
ya Boko Haram kwamba
na wenyewe ni katika zile
Intelligence Assets za
mabeberu.
Kwa hakika kama yapo
m a m b o ya k u s t a h i k i
kuwashughulisha
wanasiasa wetu, ni haya ya
hawa wanaotuwangia na
war games test pamoja na
Intelligence Assets zao
wakitutabiria machafuko
huku wakiweka mikakati
watakavyotukalia
kikachero na kijeshi. Sio
hizi porojo za kurudi
Muarabu wa Oman.

Kila uchochoro Mji Mkongwe


akina William wanaona gaidi

14

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

JINAMIZI LA UDINI TANZANIA:

Sheikh Suleiman Takadir, Askofu Makarios


Na Mohamed Said

JINA la Sheikh Suleiman


Takadir, halijapatwa
kutajwa popote katika
historia ya kupigania
uhuru wa Tanganyika
wa l a k a t i k a h i s t o r i a
ya TANU. Hatajwi na
hakupata kutajwa baada
ya uhuru kupatikana
mwaka 1961 na sidhani
hata kama atakuja
kutajwa au kukumbukwa
na hawa viongozi walio
katika madaraka hivi
sasa.
Lakini naamini viongozi
hawa walio madarakani
hivi sasa ambao wakati
wa kudai uhuru walikuwa
watoto wadogo lazima
watakuwa wamesikia jina
hili likitajwa na wazee
wao. Sheikh Suleiman
Ta k a d i r h u t a j wa k i l a
linapotokea jambo ambalo
Waislamu huonekana
wanadhulumiwa na
serikali kwani ilikuwa
Sheikh Suleiman Takadir
ndiye aliyeweka agenda
ya hali ya baadae ya
Waislamu na Uislamu
katika Tanganyika huru
mwaka 1958.
Jambo hili alipolileta
lilitishia kuigawa TANU
katika misingi ya dini
katika wakati ambapo
u m o j a w a Wa a f r i k a
ulikuwa unahitajika sana.
Mwaka wa 1958 TANU
ilikuwa imeenea nchi
nzima na tayari iko katika
barabara ya kuelekea
kuchukua madaraka ya
ndani na kisha Tanganyika
kupata uhuru wake kamili.
Sheikh Suleiman
Takadir alikuwa nani na
nini ulikuwa umaarufu
wake? Sheikh Suleiman
Takadir kwanza alikuwa
a l i m , m wa n a z u o n i
kisha alikuwa Mwenyekiti
muasisi wa Baraza la
Wazee wa TANU kuanzia
TANU ilipoundwa mwaka
1954 hadi alipotoswa
mwaka 1958 kwa kosa
la kuchanganya dini na
siasa. Sheikh Takadiri
alishiriki vilivyo ndani ya
Baraza la Wazee wa TANU
katika kutayarisha safari
ya Nyerere kwenda UNO
mwaka 1955.
Wa p e n z i wa k e
katika harakati za
kupigania uhuru
walimpachika jina la utani
wakimwita Makarios,
wakimlinganisha na

Utabiri wake ipo siku mtanikumbuka watimia

Nyumba ilipoasisiwa TANU imevunjwa.


Nyumba hii ilijengwa kwa kujitolea na wanachama wakati wa uongozi wa Kleist
Sykes akiwa katibu muasisi na ilifunguliwa 1933 na Gavana Donald Cameroon. Picha
kwa hisani ya www.mohammedsaid.com.

Baraza la Wazee wa TANU. Sheikh Suleiman Takadir wa pili chini kulia, wa pili
waliosimama Dossa Aziz, wa sita Julius Nyerere, wa saba John Rupia, wa tisa Said
Chamwenyewe, anayefuatia Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate.
Askofu Makarios wa siasa
za ukombozi za Cyprus
na Ugiriki aliyekuwa
anapambana na ukoloni wa
Waingereza wakati yeye
alipokuwa anapambana
na Waingereza katika
ardhi ya Tanganyika.
Sasa kwa kuwa Suleiman
Takadir alikuwa Sheikh
na mpambanaji ndipo
wa l i m p a j i n a h i l o l a
Makarios na kwa
hakika jina hili lilimkaa,
likamwenea vyema na
yeye akalipenda.
Mikutano ya mwanzo ya
TANU ilikuwa ikifanyika

Mnazi Mmoja mbele


ya baadae ilipojengwa
Taasisi ya Elimu ya Watu
Wa z i ma . Wa k a t i u l e
pale palikuwa hakuna
jengo lolote, palikuwa na
kiwanja kitupu na ardhi
ile ilikuwa mali ya Mzee
John Rupia, Makamu wa
Rais wa TANU. Kiwanja
hiki baaadae Mzee Rupia
aliwapa TANU na TANU
wakaanzisha Chuo Kikuu
pale mara baada ya uhuru.
Mikutano ya kwanza
ya TA N U i k i f a n y i k a
pale Mnazi Mmoja
na kabla Nyerere

hajapanda juu kwenye


j u k wa a k u z u n g u m z a
na wananchi alikuwa
kwanza anatangulia
Sheikh Suleiman Takadir,
kusawazisha uwanja na
k u wa w e k a wa n a n c h i
tayari kumsikiliza
k i o n g o z i wa o . K a m a
a l i v y o k u wa N ye r e r e ,
Sheikh Suleiman Takadiri
alikuwa na kipaji cha
kuongea. Leo hii huenda
baadhi ya wasomaji
wangu wasiamini lakini
ukweli ni kuwa Sheikh
Suleiman Takadir alikuwa
kabla hajazungumza

lolote alikuwa akipiga


fatha, wananchi
wakaitika na kwa umoja
wao wakasoma, Surat
Fatha,sura ya ufunguzi
katika Quran Tukufu,
kisha Sheikh Takadir
akaomba dua na wananchi
wakawa wanaitika kwa
pamoja, Amin, Amin,
Amin. Baada ya hapo
ndipo atapanda Nyerere
na kuanza kuhutubia.
Picha za mwanzo za
mikutano hii zipo na
zilipigwa na Mzee Shebe
ambae katika miaka ile
ya 1950 alikuwa na studio
yake Mtaa wa Livingstone
na Kipata. Picha hizi
baadhi nimepata kuziona.
Mzee Shebe ndiye alinipiga
picha yangu ya kwaza
nikiwa na umri wa mwaka
mmoja au miwili hivi na
picha hii ninayo hadi hii
leo. Inaaminika Mzee
Shebe ndiye mpiga picha
wa kwanza wa TANU na
Nyerere.
Huyu ndiye Sheikh
S u l e i m a n Ta k a d i r n a
huyu ndiye Nyerere kama
alivyokuja kutambulishwa
kwa watu wa Dar es Salaam
na Sheikh Suleiman
Takadir kwa mara ya
kwanza mwaka wa 1954.
Kabla ya hapo Nyerere
alikuwa akijulikana na
watu wachache katika
TA A . S h e i k h Ta k a d i r
alimpenda sana Nyerere
kiasi kuwa mwaka 1957
katika hotuba aliyotoa
katika tafrija moja ya
taarab Mtaa wa Mvita,
alimwita Nyerere, Mtume
wa Afrika, aliyetumwa
na M ung u k uwa o k o a
Waafrika.
Maneno yale ya
Sheikh Suleiman Takadir
alikuwa kama anamtabiria
Nyerere makubwa katika
mustabali wa Afrika,
kwani miaka mingi baadae
Nyerere alikuja kusimama
mstari wa mbele katika
kuikomboa Afrika kutoka
makucha ya wakoloni.
Nyerere akawa hapungui
nyumbani kwa Sheikh
Takadir Mtaa wa Swahili.
Nyumba hii iko jirani na
kilabu ya mpira ya Pan
Africa. Kutembelewa na
Nyerere pale nyumbani
kwake ikapelekea baba
mwenye nyumba, Jumbe
bin Jumaa wa Digosi
amuhamishe nyumba
S h e i k h Ta k a d i r a s i j e
Inaendelea Uk. 16

15

Na Ben Rijal
TUNAAMBIWA kuwa
Uisalamu ni mfumo
wa maisha. Kwahakika
maisha yote ya Muislamu
yam er at i bi wa katika
program maalumu, iwe
ya siku, wiki, mwezi
au mwaka. Maisha
ya M u i s l a m u t a n g u
anapozaliwa hadi
anapokufa, kuna taratibu
mbalimbali katika
Uislamu, taratibu ambazo
hutakiwa muumini
kuzifwata. Hakuna dini
ambayo ina programu
kamili ya matendo kama
dini ya Kiislamu. Angalia
mifano hii michache, mtu
anapokuwa Muislamu
Baligh mwenye akili
k i l a s i k u a t a t a k i wa
asali vipindi vitano
kuanzia asubuhi hadi
Isha na anaposhikamana
na salaa basi anakuwa
yupo kwenye program
maalumu kwani sala
haisaliwi anapotaka
mtu kusali, lakini sala
inasaliwa kwa wakati
maalumu uliowekwa.
Hayo ni kwa kila siku na
katika wiki unatakiwa
kujipanga kusali kwa
sala ya Ijumaa. Kisha
k a t i k a m wa k a k u n a
funga ya Ramadhani,
kuna kwenda kutimiza
n g u z o ya H i j j a k wa
mwenye uwezo. Hio yote
ni program Muislamu
ameekewa katika maisha
yake.
Maudhui ya makala
hii nikuangalia namna
tulivyofundishwa
kumpokea mtoto
anapozaliwa nini
anachohitajia kufanyiwa.
Ukweli kinachotakikana
sio tu kumpokea, lakini
huanza tangu mume na
mke wanapofanya kitendo
c h a n d o a . L e o wa n a
Saikolojia hutueleza kuwa
pale tunapotaka kwenda
kufanya unyumba, basi
twende kwa utartibu wala
tusikurupuke tu pale
tunapomaliza tendo au
ngono. Kwa kweli Bwana
Mtume Muhammad
S.A.W ameyaeleza hayo na

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Adabu ya kumkaribisha mtoto


anayezaliwa katika Uislamu

kututaka tunapowaendea
wake zetu, tuwaendee
kwa maneno mazuri na
kutofanya vishindo na
tusikupurukike kama
punda pale tunapomaliza
unyumba. Aidha tume
Suniwa pale tutapokuwa
tunakaribiya kutoa maji
ya uzazi tusiseme maneno
ya ajabu ajabu nakupiga
makelele, lakini tuseme
maneno yafwatayo:
Kwa jina la Mwenye
enzi Mungu, Ewe Mola
tulinde na Shetani na
utuhifadhi na chochote
utachoturuzuku na huyo
shetani. Taratibu hii
haipatikani kwenye dini
yoyote ile wala kwenye
falsafa yoyote ile ila katika
Uislamu.
Tunatakiwa tufanye
nini mara tu mtoto
anapozaliwa?. Tendo la
kwanza ni kuadhiniwa
kwa mtoto. Mara tu mtoto
atapozaliwa, ni vyema
achukuliwe na baba yake
amuelekeze kibla kisha
amuadhinie kwenye shikio
la kulia la mtoto. Mtume
Muhammad S.A.W
alimuadhinia mjuukuu
wake Sayidna Hussein
r.a kama anavyoeleza
Aboo Raafi, Nilimuona
Bwana Mtume S.A.W
akimuadhinia Hussein bin
Ali baada ya kujifungua
kwa Bibi Fatmah .
Kuna wengine husema
kuwa baada ya adhana
ifuwatie Ikama (Iqama)
kwa shikio la kushoto,
kauli hii haina nguvu.
Nini Falsafa na hikma
ya kuadhiniwa mtoto?
Tumboni, mtoto huwa
hasikii chochote kile, na
mara tu anapozaliwa
huanza kusikia sauti, ni
vyema asikie maneno
mazuri, ikiwa moja la hilo
ni adhana.
Falsafa ya kuadhiniwa
mtoto ni kusikia maneno
ya adhana maneno
ambayo yanamtaja Mola
na Mtume wake, lakini leo
anazaliwa mtoto na huku
anasikia majimbo ya ajabu
ajabu. Nimezungumza
baba amchukue mtoto
amuadhinie kwa hospitali
za kwetu ni ngumu
mwanamume kuingia
wodi ya wanawake,
kwa Ulaya hilo ni jambo
la kawaida mume
anaruhusika na anabakia
kwenye chumba cha

kuzalishia kumuangalia
mke wake anavojifungua,
k wa h i o k a m a m z a z i
atakuwa na nguvu
za kufanya hivyo, basi
amuadhinie mwenyewe au
azungumze na wakunga.
Te n d o l a p i l i /
Tahneek : Tahneek ni
kumrambisha Tende mara
tu mtoto anapozaliwa.
Kurambishwa tende
watoto Bwana Mtume
amelifanya mara nyingi
tu. Ni vyema tahneek
akaifanya baba au mama
au mtu wa familia ya mtoto.
Nini Falsafa na hikma ya
Tahneek ? Anapozaliwa
mtoto huwa hana nguvu,
na sukari mwilini mwake
blood sugar huwa ipo
chini hypoglacymia
kuna hatari ya kuweza
kufa mtoto sukari ikawa
chini. Tahneek husaidia
misuli za mdomo. Tende
ni chakula chenye faida
kubwa sana mwilini. Suna
tuliotakiwa kuitekeleza
ni tende na siku hizi hiyo
tende hupatikana kila
mahali, verejee glucose
na chokleti ? Tusiiwache
Sunna hii kwa watoto wetu
wanapokuja duniani.
Tendo la tatu ni kutoa jina
: Tunavielewa vitu vinavyo
tuzunguka kutokana na
kuvipa majina. Majina
yanatusaidia kuelewa vitu.
Miti, wanyama na wadudu
mbalimbali wanaadamu
wa me ya i t a ma j i n a i l i
kuweza kuwatambua.
Kuna somo zima la elimu
ya viumbe taxonomy
ambalo kazi yake ni kutoa
majina ya viumbe kwa
njia za kisayansi. Kuwa
na majina kuna hikma
kubwa.
Wakati gani wa kutoa
majina? Kuna kauli mbili
na zote zinakubalika,
nazo ima tuwape majina
watoto wanapozaliwa kwa
siku ya kwanza au siku
ya saba. Bwana Samurah
anaeleza, Bwana Mtume
Muhammmad S.A.W
ametutaka tuchinje,
tunyoe na kutoa majina
siku ya saba. Ahmad (/7,
17), Abou Dawood E.T.
2/797/No 2831).
N a y e A n a s ( R A)
anaeleza: Kuna mtoto
alizaliwa na siku hiyo
hiyo hiyo akapelekwa
kwa Bwana Mtume
Muhammad S.A.W, na
Bwan Mtume akampa jina

hapo, jina la Ebrahim na


kusema kuwa hilo ni jina
la babu wa babu wangu.
Muslim [E.T. 4/1243/No.
733].
Kwa hivyo ni suna
kuwapa majina watoto
kwa siku ya kwanza au
ya saba. Bwana Mtume
a m e t u e l e z a : S i k u ya
kufufuliwa tutaitwa kwa
majina yetu na ya baba
zetu, basi toweni majina
mazuri. (Ahmad /94.)
Vyema tutowe majina
yenye kuanza na Abd,
m f a n o wa A b d u l l a h ,
Abdur-Rahmaan, AbdulLateef n.k. Bwana Mtume
amependekeza tuwaite
watoto majina ya Mitume,
mfano wa Ebrahim, Musa,
Issa, Ismael, Yakoub,
Younus, Saleh, Yousuf,
Suleyman, Daud, Nouh,
Lout n.k. Ahmad (4/34),
aidha vizuri tukawaita
watoto wetu majina ya
masahaba kama Abubakar,
Umar, Othman, Ali,
Khalid, Hamzah, Abou
Horera n.k (Radhiyallahu
anhum).
Baadhi ya Majina mazuri
kuwaita watoto wetu wa
kike: Aminah, Asmah/
Asmaah, Asiah, Atiyah,
Aishah, Aminah, Batul,
Bilqis, Fatimah, Faridah,
Fauziah, Fadhillah,
Habibah, Hafidhah,
Hafsah, Hajerah,
Halimah, Hanifah,
Hawa, Hadiyah, Jamilah,
Juwayriyah, Khadijah,
Kulthum, Laila, Latifah,
Maryam, Masudah,
Nafisah, Naimah, Rafiah,
Rashidah, Ridhwanah,
Raisah, Sadeqah, Salmah,
Sarah, Saudah, Shahedah,
Sharrifah, Safiyah,
Shafiqah, Yasmin, Zaynab,
Z a k k i ya h , Z u b a i d a h ,
Zulekha, Arafah.
Majina yaliyokatazwa:
Tusiwape watoto majina
ya Mwenye enzi Mungu,
majina ya kizungu kina
Joseph, John n.k. Majina
ya watu wabaya kama
Firaun, Qaroon, Abou Jahl
na mijambazi mengineo
iliyo jaa duniani, na pia
t u s i t o we m a j i n a k wa
lugha zetu yenye kutoa
maana mbaya mfano wa
Chausiku, Biwi, Panya,
Mkasi, Dude, Kipande,
Matata, Kijitu, Kishonde,
n.k.
Tendo la nne-Aqiqah:
Aqeeqah ni kuchinja

tumetakiwa amchinjie
Kondoo au mbuzi wawili
kwa mtoto wa kiume na
Kondoo au mbuzi mmoja
kwa mtoto wa kike.
A q e e q a h h u f a n y wa
siku ya saba sambamba na
kutoa jina na kunyolewa
kwa mtoto. Nyama ipikwe
kisha igawiwe. Itakuwa
v ye m a i k i wa m a f u p a
hayatavunjwa.
Tendo la tano kumnyoa
mtoto nywele : Ni Suna
kunyoa watoto siku
ya saba. Kunyoa ni
k wa m wa n a m u m e n a
mwanamke. Nywele
z i p i m we k i s h a u z a n i
wake utiwe thamani ya
fedha na thamani ya pesa
wapewe maskini. Syd Ali
(RA) alifanya hivyo kwa
watoto wake, na ni vizuri
baada ya kumnyoa mtoto
apakwe mafuta. Siku
hizi hasa sisi wazee wa
Kiafrika husita kuwanyoa
mtoto eti nyewele za
mtoto anapozaliwa huwa
laini basi ukimnyoa huja
z a k a wa i d a k a s u m b a
hizi tuzitie mvunguni
tushikamane na Suna za
Bwana Mtume SAW.
Tendo la sita ni kutahiri
: Atahiriwe mtoto siku ya
7, 14 au 21. bada ya hapo
atahiriwe siku yoyote ile
bali asifike hata kubalighi.
Kwa wanawake sio lazima
wala Uislamu hausisitizi
mwanamke kutahiriwa.
Mila za wenzetu kumtahiri
mwanamke ni kumtoa
matamanio.
Baadhi ya makosa
wayafanyao watu
kutomuadhinia mtoto,
kuwacha tahneek yaani
kutomrambisha mtoto
tende na inapokosekana
tende badala yake iwe
kitu kitamu, kutotoa
jina hata baada ya wiki,
kuwa na khofu ukimwita
majina ya wazee wake
waliohai basi itacahangia
wao kufa haraka-hii ni
shirki, kutochinja, badala
yake kutoa thamani ya
mnyama, kutomchinjia
mtoto wa kike, kumchinjia
kondoo au mbuzi mmoja
tu kwa mtoto wa kiume,
kutochinja kupindukia
siku 21 ilhali mtu ana
uwezo, kuchinja mnyama
mmoja kwa mtoto zaidi
ya mmoja, kupinga kule
kuelezwa tusivunje
mifupa.
Kumnyoa mtoto upande
mmoja na kuuwachia
upande mwengine hii
inaitwa al-qaz, kumnyoa
mtoto wa kiume wala sio
wa kike kwa kuhofia kuwa
mtoto wa kike atalingana
na mtoto wa kiume, kuwa
na imani kuwa baadhi
ya watoto wakizaliwa
hawahitajiwi kutahiriwa.

16

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Sheikh Suleiman Takadir, Askofu Makarios


Inatoka Uk. 14
k u m p o n z a k wa k wa n i

Nyerere alijulikana kama adui


mkubwa wa Waingereza. Hii
kwa muhtasari ndiyo historia
ya Sheikh Suleiman Takadir
na Nyerere. Lakini usuhuba
huu ulikuja kuvunjika na
watu wawili hawa wakawa
mahasimu wakubwa, Sheikh
Suleiman kafa hasemi na
Nyerere na Nyerere kwa
upande wake hakupata hata
siku moja kumtaja Sheikh
Takadir popote hadi anaingia
kaburini.
Inaaminika Sheikh Takadir
alikufa kihoro baada ya
kupigwa pande na TANU
na wakazi wote wa Dar
es Salaam na wanachama
wa TA N U k wa k o s a l a
kuchanganya dini na siasa.
Ikiwa msomaji wangu
ulisoma makala yangu ya
juma lililopita utakuwa
u m e o n a k u w a TA N U
ikiongozwa na Mufti Sheikh
Hassan bin Amir ilipitisha
azimio la kupiga vita hisia
zozote na chembechembe
za Uislamu ndani ya TANU.
Hakika Uislamu ulikuwa
na nguvu ndani ya TANU
lakini haukuachiwa uvuke
mipaka kuwabagua wengine
waliokuwa si Waislamu.
Kilitokea nini hadi
kupelekea Sheikh Suleiman
Ta k a d i r a g o m b a n e n a
Nyerere? Chanzo cha
mtafaruku huu ni Uchaguzi
wa Kura Tatu wa mwaka
1958. Waingereza waliweka
masharti ambayo kwa hakika
yalikuwa ya kibaguzi na
yalifanya wananchi wengi
wa s i we z e k u k i d h i s i f a
zilizowekwa za kuweza mtu
kupiga au kupigiwa kura.
Kulikuwa na sifa ya elimu,
kipato na kazi ya kukubalika
na kupiga kura kwa tabaka
za rangi.
Mpiga kura Mwafrika
alitakiwa ampigie kura
Mzungu, Muasia na
Mwafrika. Masharti haya
yalikuwa kisiki kigumu
kwa uongozi wa TANU na
wanachama wake kutimiza.
TANU na viongozi wake
wengi hawakuwa na hiyo
elimu iliyokuwa ikitakikana
wala kipato cha maana.
Ili mtu asimame kama
mgombea kuingia katika
Baraza la Kutunga Sheria
au awe angalau mpiga kura
ilibidi azikusanye sifa zote
hizo mahali pamoja.
Wapiga Kura na wagombea
walitakiwa wawe na kisomo
cha darasa la 10 au kipato
cha pauni 400 kwa mwaka
na kuwa na kazi ya maana.
Waafrika waliokuwa na
sifa hizi hawakuwa wengi
katika TANU. Wengi katika
TANU kama walivyokuwa
wakipenda kujiita wenyewe
walikuwa, Baba Kabwela.
Ikawa sasa ili TANU iweze
kuweka wagombea ilibidi
i wa t a f u t e wa t u n j e ya

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Akihutubia Mkutano wa TANU Siku


za Mwanzo.

Nyerere Akitia Sahihi Azimio la Tabora


uongozi wa TANU. Hapa
ndipo lilipokuwa tatizo.
I l i b i d i TA N U s a s a
iwalete watu wenye sifa
n j e ya k e n a we n g i wa
watu hawa walikuwa
Wakristo waliosomeshwa
na wamishionari. Jambo
hili lilimkera sana Sheikh
Ta k a d i r n a wa n a c h a m a
wengi wa TANU kwa ujumla
wao na kwa hakika TANU
nzima hawakutaka kabisa
kuingia uchaguzi ule kwa
masharti yale waliyoyaona
ya kibaguzi. Wanachama wa
TANU walikuja na kauli mbiu
isemayo, Kuingia Kura Tatu
ni sawa na kujipaka kinyesi.
Ilikuwapo minongono
kuwa Wakristo wataichukua
nchi lakini kwa muda mrefu
hofu hii ilizuiwa kwenye
vifua hakuna aliyekuwa
na ujasiri wa kulisema hilo
waziwazi kwani jambo la
dini lilikuwa mwiko mkubwa
katika TANU. Ikawa tatizo
lile la kushiriki kwa TANU
katika Uchaguzi wa Kura
Ta t u l i j a d i l i we k we n ye

Mkutano Mkuu wa TANU


wa mwaka 1958 uliopangwa
kufanyika Tabora.
Mpinzani mkubwa wa
Kura Tatu alikuwa Zuberi
Mtemvu, Katibu Mwenezi
wa TANU kwa wakati ule.
Ukweli ni kuwa Kura Tatu
ilitishia uhai wa TANU na
zilikuwapo dalili za chama
kumeguka pande mbili.
Kulikuwa na uwezekano
mkubwa sana kuwa Zuberi
Mtemvu na Sheikh Takadir
wangelikuwa upande
mmoja na wangeweza kuja
na chama kingine ingawa
agenda zao zilikuwa tofauti.
Mtemvu yeye alisimama
kwenye Afrika kwa Waafrika
na Sheikh Takadir kwenye
Uislamu.
Mkutano wa Tabora ni
kisa kirefu In Sha Allah
tutakitafutia wakati wake
makhsusi tukizungumze.
Nimekiandikia kitabu
kizima Uamuzi wa Busara,
(Abantu Publishers 2007,

Dar es Salaam) Sheikh


Suleiman Takadir na baadhi
ya wazee katika Baraza la
Wazee wa TANU walikuwa
wajumbe katika mkutano
wa Tabora. Kufupisha kisa
TANU ilipiga kura kukubali
kuingia kwenye Uchaguzi
wa Kura Tatu na manusruna
kura zifungane kati ya wale
wanaounga mkono na wale
waliokuwa wakipinga.
TANU iliingia katika
Uchaguzi wa Kura Tatu na
ikapata ushindi mkubwa.
Hofu aliyokuwanayo Sheikh
Takadir ilikuwa kuwa watu
walioingia katika TANU
kuchukua uongozi ni
Wakristo. Sheikh Takadir
alikuwa anajua nguvu ya
m a d a r a k a wa l i y o k u wa
wa n a k a b i d h i wa a k a wa
na hofu kama uongozi
huu mpya utakuja kutoa
haki kwa Waislamu uhuru
utakapopatikana. Sheikh
Takadir alitaka uhakika wa
hali ya baadae ya Waislamu

katika Tanganyika huru.


Katika mkutano wa
Halmashauri Kuu Makao
Makuu ya TANU, New Street
Sheikh Takadir alimkabili
Nyerere akamshutumu
kuwa hakuwa na nia nzuri
n a Wa i s l a m u , a t a k u j a
wapendelea ndugu zake
Wakristo katika Tanganyika
h u r u . S h e i k h Ta k a d i r
akawageukia wenzake katika
Baraza la Wazee wa TANU
akasema, Tuzibe ufa tusije
tukajenga ukuta. Jambo
lile lilikuwa zito. Nyerere
alijiinamia na aliponyanyua
uso wake machozi yalikua
yanambubujika. Mkutano
haukuweza kujadili jambo
lile na kikao kile kikavunjika
p a l e p a l e n a wa j u m b e
wakawatawanyika.
Sheikh
Ta k a d i r
akatoswa, kwani alikuwa
amevunja mwiko mkubwa
katika TANU. Mzee Iddi
Tulio akachaguliwa kushika
nafasi yake. Huku kutoswa
na kutengwa na jamii ndiko
kulikosababisha kifo cha
Sheikh Takadir. Alikuwa
hata akitoa salamu hakuna
aliyeitika. Akienda sokoni
Kariakoo kununua chochote
kile hakuna aliyekuwa tayari
kupokea hela yake.
Haikuchukua muda
mrefu Sheikh Takadir akaaga
dunia. Kabla Sheikh Takadir
h a j a f a , TA N U i l i f a n ya
mkutano mkubwa sana na
Nyerere akamshambulia
Sheikh Takadir kwa kutaka
kuwagawa Watanganyika
katika misingi ya dini. Baada
ya mkutano kundi kubwa
lilikwenda nyumbani kwa
Sheikh Takadir Mtaa wa
Msimbazi kuzomea huku
wakiimba, Takadir Mtaka
Dini.
Sheikh Takadir alitoka
nje akasimama kizingitini
a k a s e m a m a n e n o h a ya ,
Ndugu zangu, In Sha
Allah iko siku mtakuja
kunikumbuka. Haukupita
muda mrefu Sheikh Takadir
akatangulia mbele ya haki
n a k wa k i p i n d i k i r e f u
katika historia ya uhuru
wa Ta n g a n y i k a h a k u n a
a l i ye m k u m b u k a S h e i k h
Suleiman Takadir, Askofu
Makarios wa Tanganyika.
Hivi sasa Sheikh Suleiman
Takadir anatajwa sana na
kizazi cha leo. Utabiri wake
kuwa ndugu zake watakuja
kumkumbuka umetimia.
Swali la kujiuliza ni iweje
hii leo baada ya miaka 57
kupita, Sheikh Suleiman
Takadir anarejeshwa upya
katika historia ya kupigania
uhuru wa Tanganyika? Hiki
ni kitendawili kinachongoja
kuteguliwa.
Makala hii kwa hisani
ya Mohamed Said kupitia
blog:www.mohammedsaid.
com

17

Makala

Timamu Tea inawafaa watu wote-4

Na Juma Killaghai
MAKALA ya leo ni ya nne na
ya mwisho, kati ya mfulululizo
wa makala tulizodhamiria kutoa
kwa malengo ya kujenga hoja
juu ya chai ya Haiiba Timamu
kuhitajiwa na kila mtu. Hoja ya
msingi iliyotawala makala zote tatu
zilizopita, na ambayo tunaiendeleza
katika makala hii, ni kuwa tiba ya
chai hii inatokana na kumrejeshea
muhusika viini lishe mbali mbali
muhimu vilivyopungua mwilini
mwake. Katika makala zilizotangulia
tulizungumzia makundi matatu
ya viini lishe vilivyomo kwenye
chai ya Haiiba Timamu. Tuliyataja
makundi haya kuwa ni yale ya
vitamini, madini lishe na tindikali
za amino, au vijenzi vya protini.
Makala yetu ya leo itataja kundi
la nne na la mwisho; hili si lingine
bali ni kundi la vizuia vioksidishaji
(anti-oxidants).
VIZUIA VIOKSIDISHAJI NI NINI? Vizuia
vioksidishaji ni molekuli (molecule)
zinazozuia mchakato wa kuoksidisha
molekuli nyingine. Kuokisidisha ni
muingiliano wa kikemia (chemical
reaction) unaopelekea molekuli
iliyookisidishwa kupoteza chembe
yenye/zenye umeme hasi (electron),
au kupoteza kiasili cha hydrogen
katika umbile lake, au umbile lake
kuongezewa kiasili cha oxygen.
Mchakato wa uoksidishaji ndani
ya mwili hutokea muda wote. Huu
ni sehemu ya mchakato wa ujenzi
na uvunjifu wa kemikali ndani ya
mwili, yaani metabolism. Mchakato
wa kuoksidisha unaweza kuzaa
c h e m b e c h e m b e z e n ye u m e m e
chanya zinazoitwa free radicals.
Kwa upande wake hizi free radicals
ni chembe zenye uwezo mkubwa
wa kuoksidisha, na hivyo kuwepo
kwake kunaweza kuzaa gharika
(chain reaction) ya uoksidishaji ndani
ya seli za mwili. Hali hii inaweza
kusababisha uharibifu mkubwa wa
seli au hata kifo cha seli husika.
Vizuia vioksidishaji huzuia hizi
gharika kutokea ndani ya seli. Badala
yake hivi vioksidishaji huoksidisha
hivi vizuia vioksidishaji na kwa hivyo
kuacha seli za mwili zikiwa katika
hali ya salama. Kwa kawaida mwili
unamiliki na kuendeleza mifumo
kadhaa ya vizuia vioksidishaji
mbalimbali. Vizuia vioksidishaji hivi
ni pamoja na glutathione, Vitamini
C, Vitamini A, na Vitamini E; pamoja
na vimengenya mbalimbali kama
catalase, superoxide dismutase
na peroxidases mbalimbali.
Kuwepo kwa kiwango kidogo cha
vizuia vioksidishaji au kuwepo
k w a v i m e n g e n y a n d a n i y a

mwili vinavyozuia utendaji kazi


wa hivi vioksidishaji, kunaweza
kusababisha hali inayoiitwa msongo
wa uoksidishaji (oxidative stress),
hali ambayo husababisha seli za
mwili kuharibiwa na hata kufa. Tafiti
zinaonyesha kuwa huu msongo wa
uoksidishaji ni chanzo cha magonjwa
mengi ya kimfumo ikiwa ni pamoja
na saratani.
Baadhi ya vizuia vioksidishaji
muhimu vilivyoko kwa wingi
katika chai hii ni Curcumin;
Catechines, Flavonoids, Piperine, na
Cinnamaldehyde.
Curcumin: Curcumin ni kemikali
ya kiorganiki ambayo iko katika
kundi pana la kemikali zinazojulikana
k i t a a l a mu k a ma p o l y p h e n o l s.
Polyphenols ni kemikali za kiorganiki
ambazo sehemu fulani katika maumbo
yao kuna mkusanyiko wa viasili
ulioko katika mpangilio maalum
unaosababisha sehemu kubwa
ya tabia za kikemia za kundi hilo
unaoitwa phenol. Mkusanyiko wa
aina hii katika kemikali za kiorganiki
zinazounda kundi lolote huitwa
FUNCTIONAL GROUP kwa lugha ya
kikemia. FUNCTIONAL GROUP kwa
tafsiri isiyo lazima ni MKUSANYIKO
WA VIASILI ambavyo husababisha
tabia ya kikemia ya kundi zima. Faida
za curcumin ni nyingi. Miongoni
mwa faida hizi ni pamoja na:
Kutakasa majeraha dhidi ya bacteria
na kuharakisha uponaji wake. Ina
uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji
wa saratani ya tezi dume. Ina uwezo
mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa
saratani ya matiti. Ni kizingiti kikubwa
dhidi ya (melanoma); ambayo ni aina
ya saratani ya ngozi inayoanzia
kwenye chembechembe zinazotia
rangi kwenye ngozi (melanine) kabla
ya kusambaa katika maeneo mengine.
Hupunguza uwezekano wa kupata
saratani ya damu kwa watoto. Ni
kitakasaji cha asili cha ini. Inaweza
kuzuia au kusimamisha kukua
zaidi kwa ugonjwa wa kupoteza
kumbukumbu (Alzheimers disease).
Inazuia aina mbalimbali za saratani
kusambaa kutoka eneo moja la mwili
hadi jingine. Ni kituliza maumivu cha
asili. Inaratibu ujenzi na uvunjifu wa
kemikali mwilini na kusaidia katika
kuondoa unene. Imekuwa ikitumika
katika baadhi ya nchi, mathalani
China, kama tiba ya mfadhaiko. Ni
pozo dhidi ya maradhi ya baridi
ya yabisi na jongo. Inatibu saratani
ya tezi ya thyroid. Inaharakisha
kupona kwa majeraha na kuirejesha
ngozi iliyoumizwa katika hali yake
ya kawaida ndani ya muda mfupi;
na inasaidia katika matibabu ya
ugonjwa wa psoriasis (ugonjwa
unaosababishwa na kukua kwa kasi
kwa baadhi ya seli za ngozi kupelekea
ngozi kuwa na mabaka ya rangi
tofauti tofauti), pamoja na magonjwa
mengine ya ngozi yanayotokana
na mfuro (inflammation) wa seli za
ngozi.
Catechins: Huu ni mkusanyiko
wa vizuia vioksidishaji ambavyo
kutokana na maumbo yao kufanana
kwa karibu na tabia zao za kikemia
kufanana pia, vimewekwa katika
kundi moja la kemikali za kiorganiki.
H a t a h i v y o k a m a i l i v y o k wa
curcumin ambayo tumetangulia
kuitaja, catechins ni sehemu ya
kundi kubwa zaidi la kemikali za
korganiki zinazojulikana kama
polyphenols. Faida za catechins

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

ni nyingi. Miongoni mwa faida


hizi ni pamoja na: Huhusishwa na
kusaidia sana kuzuia mlundikano wa
mafuta mwilini. Hushusha kiwango
cha lehemu katika damu. Huzuia
ongezeko la shinikizo la damu.
Huzuia ongezeko la sukari ya kwenye
damu. Husaidia kuzuia kupatwa na
ugonjwa wa mafua. Hupambana
dhidi ya maambukizi ya bacteria; na
Huzuia harufu mbaya kutoka katika
kinywa.
Flavonids: Flavonoids ni
mkusanyiko mwingine wa vizuia
vioksidishaji ambavyo kutokana na
maumbo yao kufanana kwa karibu
na tabia zao za kikemia kufanana
pia, vimewekwa katika kundi moja
la kemikali za kiorganiki. Kama
ilivyo kwa curcumin na catechins,
vizuia vioksidishaji hivi pia viko
katika kundi pana zaidi la kemikali za
kiorganiki za polyphenols. Faida za
flavonoids ni nyingi. Miongoni mwa
faida hizi ni pamoja na: Inaaminika
kuwa zina uwezo mkubwa sana wa
kupambana na saratani. Inaaminika
kuwa zina uwezo mkubwa sana
katika kukabiliana na magonjwa
mbalimbali yanayohusiana na moyo;
na inaaminika kuwa zina uwezo
mkubwa sana wa kukabiliana na
mfuro wa seli.
Piperine: Piperine ni miongoni mwa
kemikali za kiorganiki zinazoitwa
alkaloids. Alkaloid ni kemikali yoyote
ya kiorganiki ambayo umbile lake
linajumuisha nyongo (base) yenye
kiasili cha nitrogen. Faida za piperine
ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na: Husaidia kuongeza
uwezo wa mwili kwa kiasi kikubwa
wa kufyonza na kutumia viini
lishe mbalimbali vinavyopatikana
kwenye vyakula. Inaaminika kuwa
inachochea ongezeko la kasi ya ujenzi
na uvunjifu wa kemikali ndani ya
mwili (accelerates metabolism) na
hivyo kusaidia katika harakati za
kudhibiti uzito wa mwili. Inasaidia
kudhibiti mfuro (inflammation)
wa seli. Inapunguza kasi ya ukuaji
wa seli za saratani, hususan zile
zinazohusiana na saratani ya mapafu;
na inachagiza mwili kuzalisha homoni
ya serotonin ambayo husaidia sana
kujenga hali ya kujisikia furaha na
hivyo ni nzuri katika kukabiliana na
msongo na mfadhaiko.
C i n n a m a l d e h y d e :
Cinnamaldehyde ni miongoni mwa
kemikali za kiorganiki zinazoitwa
cinnemaldehydes. Cinnemaldehydes
ni kemikali za kiorganiki ambazo hutoa
harufu (mara nyingi ya kupendeza)
na ambazo FUNCTIONAL GROUP
yake ni ile inayokusanya viasili
katika mpangilio unaojulikana kama
ALDEHYDE. Cinnamaldehyde ni
kemikali ya kiorganiki ambayo ina
faida kubwa mwilini. Inafanya kazi
kwa kuzuia kuganda kwa damu
k u n a k o we z a k u p e l e k e a d a m u
isitembee mwilini inavyopasa.
Inasaidia sana kupambana
na mfuro wa seli na kwa hivyo
husaidia sana katika magonjwa yote
yanayosababishwa na mfuro. Inazuia
mlundikano wa mafuta kwenye ini na
hivyo kutoa kinga dhidi ya ugonjwa
wa ini bonge (fatty liver disease).
Inahitajika katika utengenezaji
wa creatine. Creatine ni kiini lishe
kinachohitajika katika uzalishaji wa
nishati inayohitajika katika kuifanya
misuli ifanye kazi zake kwa ufanisi.
Inahitajika katika uzalishaji wa

protini aina ya collagen ambayo ni


muhimu katika uundaji wa ngozi,
kucha na tishu zinazounganisha
misuli. Husaidia kuimarisha siha
za watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi. Husaidia kupunguza mfuro
(inflammation) wa kongosho yaani
pancreatitis. Husaidia kupunguza
dalili za ugonjwa wa Parkinson.
Husaidia kukabiliana na maambukizi
katika njia ya mkojo.
Kama tulivyosema huko nyuma,
siku zote kinga ni bora kuliko tiba.
Kutokana na faida nyingi zinazoletwa
na viini lishe vilivyoko katika Haiiba
Timamu Tea kama tulivyozielezea
hapo juu, ni wazi kabisa kuwa kila
mtumiaji wa Haiiba Timamu Tea, bila
kujali hali yake ya kiafya, anaweza
kunufaika sana.
K WA M A E L E Z O Z A I D I
WASILIANA NA WATENGENEZAJI
WA CHAI HII, YAAINI HERBAL
IMPACT, KWA SIMU NAMBA:
0754281131; 0655281131; 0686281131;
NA 0779281131 AU WATEMBELEE
OFISINI KWAO:
MOSQUE STREET, NO.1574/144,
KITUMBINI, DAR ES SALAAM
(MKABALA NA LANGO KUU LA
KUINGILIA MSIKITI WA SUNNI)
Chai ya Timamu sasa inapatikana
katika baadhi ya mikoa. Mawakala
wetu katika mikoa husika ni:
TANGA
ABDALLAH MWARABU
SIMU: 0783-290921/0658-290921
BARABARA YA 12, JIRANI NA
MSIKITI WA IBAADH
TANGA MJINI
MOROGORO
DOTTO MALENDA
0715-282331
MTAA WA KARUME (MKABALA
NA MASJID HAQ)
MOROGORO MJINI
MWANZA
SUBIRA OMAR MIDOLE
0716969494
YOTE MAISHA STORE, PENDA
STREET, KIRUMBA SOKONI
MWANZA MJINI
ZANZIBAR
SULEIMAN KHAMIS
0777867178
MASJID MUZHAMIL, DARAJANI
ZANZIBAR
ARUSHA
MZEE MAGOMBA
0764006630/0784546581
A L M U N AWA R S H O P P I N G
CENTER
BONDENI ROAD,
ARUSHA MJINI.
KILIMANJARO
MAMA ASHA KILLAGHAI
MSHANA
0754309908/0784309908
SOWETO (KARIBU NA BIBLE
SCHOOL),
MOSHI MJINI
IRINGA
SHAIBU DADI NDINDA
0787-007218
M S I K I T I WA I J U M A A ,
MIYOMBONI,
IRINGA MJINI.
RUVUMA
MAMA ZABIBU NANDANJE
0782-247101
SONGEA MJINI
PEMBA
SALIM JUMA HARUNI
0777-432331
WETE, PEMBA.

18
Na Bakari Mwakangwale
UNAPOZUNGUMZIA
wanaharakati wa miaka ya
hivi karibuni ambao wana
mchango mkubwa katika
k u wa a m s h a Wa i s l a m u
nchini, huwezi kulikosa
jina la Amani Saad Fundi.
Ustadhi Fundi, kwa sasa
amekuwa haonekani kwa
muda mrefu katika harakati,
japo hali hii ipo miongini
mwa wengine wengi wa
mfano wake na wa wakati
wake.
Hii huenda ni kutokana
na sababu mbalimbali,
ambazo zimekuwa
zikiwakabili wanaharakati
hao wa enzi zake, yakiwemo
maradhi au kuwepo katika
harakati hizo kwa sura
nyingine kutokana na wigo
wa harakati za kuhuisha
Uislamu kupanuka hivi
sasa kulinganisha na wakati
uliopo.
An nuur, imekutana
na Ust. Fundi, lakini
ukimwangalia tu, utabaini
k u wa h u y u s i A m a n i
Saad Fundi, yule ambaye
alikuwa kamanda wa vijana
aliyepewa majukumu ya
kudhibiti ofisi za Bakwata,
Jijini Dar es Salaam, katika
miaka ya 1992.
Ustadh Fundi, hivi
sasa ukikutana naye
anakuangalia kwa shida
huku akigeuza uso wake ili
aipate taswira yako vizuri
aweze kukutambua, hapo
hapo akitegea kukupa
mkono kama ilivyo ada
y a Wa i s l a m u k a t i k a
kusalimiana ili wewe
uufate mkono wake ulipo,
na pengie ujitambulishe
kwake wewe ni nani.
Fundi, enzi za harakati
za miaka hiyo, alikuwa
anaweza kuongoza
mapambano akiwa mstari
wa mbele huku umma wa
Kiislamu ukiwa nyumba
yake ukiwa na matumaini
kuwa mbele kuna
kamanda,Shabaab.
Hivi sasa Ust. Fundi,
anatembea kwa msaada
wa mtu pembeni ili aweze
kufika mahali anapopahitaji.
Ukimuona Mwanaharakati
huyu, hakika utapata Ibra
ya kuutumikia uzima wako,
nguvu zako na elimu yako,
katika kuupigania Uislamu
kabla maradhi hayaja kufika.
Ni nini kimemsibu Ustadh
Fundi? Mwanaharakati
huyu, amepatwa na mtihani
wa maradhi ya shinikizo la
damu katika macho -presha
ya macho, maradhi ambayo
yamepoteza nuru yake ya
kuona.
Hadi sasa Ustadh Fundi
amebakia na jicho moja
tu ambalo linamwezesha
kuona kwa tabu, tena mpaka
ageuze shingo kwa maana
eneo analotumia kuona ni
sehemu ya mwisho ya jicho
huku jicho la pili likiwa
limepoteza nuru ya kuona
kabisa.
Ustadh Fundi, anasema
kutokana na maradhi ya
macho aliyonayo sasa

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Ustadh Amani Saad Fundi

USTAADH Amani Saad Fundi.


yamefanya apoteze nuru
na kushindwa kufanya au
kushiriki, katika harakati
za pamoja, Mwanaharakati
huyo anajieleza kuwa ni
mwandishi, mfasiri, mshairi
lakini anasema kwa sasa
anashindwa kuandika.
Naomba msaada kwa
ndugu zangu, wanaharakati
wenzangu, wanaonifahamu
n i l i o k u wa n a o wa k a t i
huo na hata hawa wa sasa
ambao hawanifahamu
wanikumbuke na
wanihurumie, ili niweze
kupata tiba ya macho.
Anasema Ust. Fundi,
akiongea na An nuur.
Fundi ambaye kitaaluma
n i m wa l i m u , a n a s e m a
alianza kusumbuliwa na
macho mwanzoni mwaka
2000, yakianza kwa kuwasha
hususan jicho la upande wa
kushoto na kufikia kuwa
jekundu.
Anasema, baada ya
kuhangaika katika hospitali
mbalimbali nchini na
kukwama kutokana na hali
ya gharama zilizokuwa
zikihitajika, na kufikia hatua
ya kushindwa kutibika,
hivyo alishauriwa kwenda
kuonana na watu wa tiba
mbadala.
Miongoni mwa matabibu
hao wamenipa matumaini
kuwa matatizo yangu
yaweza kutibika, kwa kuwa
tayari wana orodha ya
wagonjwa ambao walikuwa
na tatizo kama langu na
wamejaaliwa kupona.
Pamoja na kunipa
matumaini hayo sambamba
na kunipa gharama za tiba
zao, tatizo linarudi pale
pale sina pesa, gharama zao
zimekuwa kikwazo kwangu
na wala sina nafuu yoyote
ya macho. Alisema Ustadh
Fundi.
Fundi, anasema awali
maradhi hayo yalipoanza

kwa kuwasha alikwenda


hospitali ndogo na kupewa
dawa za kunyunyiza za
matone baadae yaliacha
kuwasha isipokuwa
akiandika ubaoni hali
ilikuwa tofauti na kawaida.
Ilimlazimu aende hospitali
ya Taifa ya Muhimbili,
akitumaini kupata tiba na
alipoeleza tatizo lake hali
ya kupata huduma ilikuwa
ngumu kutokana na kupewa
miadi ya muda mrefu ili
aweza kuonana na madaktari
bingwa wa matatizo yake.
Mara waniambie
nirudi baada ya Mwaka
na nusu, miaka miwili ili
wan ich u ng u ze wab ai ni
tatizo, kwa upande wangu
nilikuwa naendelea
kuumia. Ikanibidi niliende
hospitali ya Regency na
baadae Hindumandal,
lakini mwishio wa siku
nikashindwa gharama zao.
Anasimulia Ustadh Fundi.
Anasema, alifanikiwa
kuonana na Daktari mmoja
bingwa wa magonjwa ya
macho ndipo alipomwambia
k wa m b a a n a m a t a t i z o
ya presha ya macho na
anatakiwa afanyiwe upasuaji
kisha alipewa gharama zake.
N i l i p o p a t a p e s a ya
matibabu na kurudi,
nilipimwa tena, kwa kuwa
muda ulikuwa umepita
walinieleza kwamba
haiwezekani tena kufanyiwa
upasuaji kwani tatizo lilizidi
kuwa kubwa na endapo
watafanya upasuaji sitaweza
kuona hata kwa kiasi hiki
kidogo nilichonacho kwa
sasa, wakanipatia dawa za
kupaka tu. Alisema Ust.
Fundi.
Anasema, kwa sasa hali
ilivyo ni kwamba jicho lake
moja halioni kabisa na hata
hilo moja lililobaki anaona
kwa shida, hawezi kuongea
na mtu kwa kuangaliana uso

kwa uso shurti akukwepe


kidogo akulenge katika
sehemu ndogo inayoona,
jambo ambalo pia linamfanya
apate msaada wa kutembea
na mtu kwa ajili ya usalama
wake njiani na barabarani.
Pamoja na kwamba macho
yamekufa, lakini anasema
bado anajiamini kuwa akili
na ufahamu wake bado
ni mzuri tu, hivyo kama
ataajaliwa kupata msaada
wa matibabu na kurudisha
nuru ya macho yake anaweza
kuendelea na harakati za
kuhuisha Uislamu hususani
shughuli za kufasiri vitabu
vya dini kwani hivi sasa kuna
vitabu ambavyo amekwama
kuvifasiri, kwa sababu ya
kuharibikiwa na macho.
Kuna vitabu vizuri
ninavyo, kwa mfano kuna
kitabu kinaitwa Adab ilKadhi ukizingatia huu
ndio muda muafaka, hiki ni
kitabu kizuri kimeandikwa
kwa Kiarabu kimefasiriwa
Kiingereza, sasa mimi nataka
kukifasiri kwa Kiswahili,
i l i Wa i s l a m u w a p a t e
elimu kuhusu masuala
ya Mahakama ya Kadhi.
Anasema Ust. Fundi.
Anasema, katika ufasiri
ameshiriki kufasiri vitabu
vingi anakitaja kitabu cha
Muslim Guide for Islamic
Workers (Mwongozo wa
Mafunzo kwa Watumishi wa
Uislamu) kilichotungwa na
Dkt. Hisham Yahya Altalib,
kwamba yeye ni miongoni
mwa wafasiri wa kitabu
hicho. Kitabu hicho ambacho
hivi sasa kinapatikana nchini
k wa K i s wa h i l i , k i k i wa
kimechapwa na Taasisi
ya Kimataifa ya Fikra za
Kiislamu-International
Institute of Islamic Thought
(IIIT), katika neno lake la
shukrani wameshukuriwa
walioshiriki kukifasiri kitabu
hicho wakitajwa kwa majina
kuwa ni Zahaqi Rashid, Ally
S. Kilima, Hassan Mnjeja,
Amani S. Fundi na Idris A.
Khatri.
Ustadh Fundi, ambaye
anaeleza kuwa yeye ni
miongoni mwa wanafuzi wa
mwanzo wa Profesa Malik,
pia alikuwa katika timu ya
Warsha ya Waandishi wa
Kiislamu, akiwataja baadhi
yao aliokuwa nao wakati
huo kuwa ni Omari Msangi,
Mtengwa Buruhan, Mussa
Mdidi, Mohammed Kassim,
Hashim Meena n.k
Lakini pia anasema
awali alishiriki kuandikia
magazeti ya An nuur, Mizani,
mwazoni mwa miaka ya 1991
na kuendelea sambamba na
gazeti la Baraza Tanzania.
Ust. Fundi, anakumbuka
na kusimulia kuwa mwaka
1991 kuelekea 1992, katika
vuguvugu au harakati
z a Wa i s l a m u k u a m u a
kuichukua Bakwata, yeye
alikuwa kamanda wa kikosi
cha udhibiti Ofisi za Bakwata
Mtaa wa Lumumba,
Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Fundi anakumbuka tukio la

kihistori, pale wanaharakati


wakati huo walipofanikiwa
kuichukua Bakwata Makao
Makuu, Kinondoni, Jijini Dar
es Salaam, wakati wa Umufti
wa Sheikh Hemed Bin Jumaa,
na kufanikiwa kuiteka baada
ya purukushani kubwa.
Anasema hali ilibadilika
baada ya Rais wa wakati huo
Mzee Ally Hassan Mwinyi,
kuingilia kati ndipo ikaja
hoja ya kuwataka Waislamu
kuunda Baraza linguine,
waachane na harakati za
kuichukua Bakwata. Ndio
hili Baraza Kuu la Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu
unaloliona leo, kwa wasiojua
historia nyake.
Sasa hivi kuna watu
wanasema kwamba watu
hawana habari na Baraza
Kuu la Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu na kwamba
Bakwata ndio chomba cha
Waislamu na maswala yote
ya Waislamu nchini lazima
yaamuliwe na Bakwata, hilo
si kweli, hawa watakuwa
hawajui tofauti ya kuundwa
Bakwata na uundwaji wa
Baraza Kuu la Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu.
Anasema Ust. Fundi.
Anafafanua, kuwa Baraza
Kuu la Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu, kuundwa kwake
limezishirikisha Taasisi
za Kiislamu kwa vitendo,
kwa maana hiyo Baraza
hili lina muundo shirikishi
ya makundi ya Waislamu
kuliko lilivyo Bakwata,
kwani hata kuundwa kwake
lilipata upinzani nchi nzima
kutoka kwa Waislamu,
kama si nguvu ya Julius
Nyerere na Serikali hivi sasa
lisingekuwepo. Limeundwa
kwa nguvu za serikali na
linaendelea kuwepo kwa
nguvu za dola.
Katika harakati zake
kuleta mwamko wa elimu
kwa umma wa Kiislamu
nchini, mwaka 1994, Ust.
Fundi, alianzisha harakati
za usomeshaji, vijana
kupitia Misikitini, ambapo
alianzisha Taasisi ya Islamic
Consultancy Center, katika
Msikiti wa Manyema.
Ta a s i s i h i y o n d i y o
ilikuwa ya kwanza kuandaa
na kusomesha watoto wa
K i i s l a m u wa n a o m a l i z a
darasa la saba na kuwashauri
kujiunga na Shule za
Sekondari za Kiislamu na
kuleta tija na mwamko
mkubwa kwa wazazi wa
Kiislamu Jijini Dar es Salaam
na kisha mikoani.
Hivi sasa Ust. Fundi,
a n a s i m a m i a Ta a s i s i ya
Al-Miftahu Charitable
Foundation (ACF), akiwa
ni Katibu Mtendaji, ambayo
aliiunda kabla hajapatwa na
maradhi ya macho. Ndani
ya Taasisi hiyo kuna kitengo
cha Ustawi wa Jamii kwa
madhumuni ya kulea na
kuhudumia watoto yatima
waliopo majumbani na
wajane.
Ustadhi Fundi, kwa sasa
anapatikana Manzese Uzuri,
Masjid Rahiim, karibu na
kituo cha daladala cha
Friends Conner, Jijini Dar
es Salaam. Ama unaweza
k u wa s i l i a n a n a ye k wa
namba za simu:- 0689 44 61
66/0652 97 97 66.

19

Tangazo

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


P.O Box 55105,Phone: 0222450069, 0784 267762, 0755 260087 & Fax 022 2450822, Dar es Salaam website :www.ipctz.org

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2015/2016

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:
KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

SAME KILIMANJARO
NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL
MWANZA
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

DAR ES SALAAM

1. Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu.
2. Shule hizi ni za bweni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana .
3. Zipo tahasusi za masomo (Subject Combinations) ya SAYANSI, ARTS na BIASHARA.
4.
Wanafunzi wote wanafundishwa Islamic Knowledge,Introduction to Arabic na matumizi ya compyuta pamoja na kutumia mtandao (internet)
katika kujifunza.
5. Muombaji anatakiwa awe na sifa za kujiunga na kidato cha tano kwa mujibu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
6. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni
: 0783552414/0762817640.


Kilimanjaro
- Moshi: Msikiti wa Riadha :712 216490
- Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757 013344.

- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075
- Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
- Ugweno Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

Tanga
- Twalut Islamc Centre Mabovu Darajani : 0715 894111
- Uongofu Bookshop: 0784 982525

- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008.
- Mandia Shop - Lushoto: 0782257533.
-Handeni Mafiga -0782 105735/0657093983

Mwanza
- Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.
- Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770/0714097362.

Musoma
Shinyanga

Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172


- Ofisi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531

Morogoro

Dodoma

Singida

Manyara

Kigoma
- Msikiti wa Mwandiga: 0714717727
- Kibondo Islamic Nursery School: 0766406669.
- Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.

Lindi

Mtwara

Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623


Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426
Kahama ofisi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi : 0753 993930/0688794040

- Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.


- Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992

- Ofisi ya Islamic Education. Panel karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039.
- Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid Rahma: 0784491196

- Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.


- Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.

Songea
- Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772.
- Mkuzo Islamic High School :0717 348375.
Mbeya

- Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini 0785425319.


- Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.

Rukwa

- Sumbawanga:Jengo la Haji Said Shule ya Msingi Kizwike 0717082 072.

Tabora

- Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0787237342


Nzega -Dk Mbaga-0754 576922/0784576922.

Iringa

- Madrastun Najah: 0714 522 122.

Pemba

-Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.

Unguja

- Madrasatul Fallah: 0777125074.

- PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa Lumumba


Mafia
- Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.
USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!
MKURUGENZI
WABILLAH TAWFIIQ

AN-NUUR

20

MAKALA

20

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

AN-NUUR

Mpenzi msomaji kuanzia


Februari 19, 2015
ANNUUR litapatikana kwa
Shs 800/= tu

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 13-19, 2015

Dk. Shein ahimiza ubora wa vyakula vinavyouzwa nchini


R A I S wa Z a n z i b a r n a
Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein, amehimiza
umuhimu wa kuzingatia
ubora wa bidhaa na vyakula
vinavyouzwa nchini.
Aidha, ili kufikia azma
hiyo, Rais Shein amesema
kuwa umefika wakati wa
k u i i m a r i s h a Ta a s i s i ya
Viwango Zanzibar (ZBC) ili
iweze kutimiza wajibu wake
ipasanyo.
Dk. Shein aliyasema hayo
mwanzoni mwa wiki hii
huko Ikulu mjini Zanzibar
katika mkutano kati yake
n a u o n g o z i wa Wi z a r a
ya Biashara, Viwanda
na Masoko kwa lengo la
kuangalia Utekelezaji wa
Malengo ya Wizara hiyo kwa
robo mbili (Julai-Disemba)
2014/2015.
Katika maelezo yake Dk.
Shein alisema kuwa Taasisi
hiyo ina umuhimu mkubwa
katika kuimarisha sekta
ya biashara sambamba na
kukinga afya za wananachi.
Alisema kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa upande wake imeweka
mikakati maalum katika
kuhakikisha Taasisi hiyo
inaimarika zaidi ikiwa ni
pamoja na azma ya kununua
vifaa maalum kwa ajili ya
uchunguzi na kuitaka Wizara
husika pamoja na Bodi yake
kukaa pamoja ili kufanya
maamuzi ya kuiimarisha
sekta hiyo.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza
haja ya kuharakishwa kwa
utafiti wa karafuu na ule
utafiti wa mwani wa aina
ya Cottoni kwa kutambua
kuwa aina hiyo ya mwani bei
yake ni ni nzuri sambamba
na kupata matokeo na
mwelekeo wa haraka juu ya
kuendelea na kilimo hicho.
Pamoja na hayo, Dk. Shein
alisisitiza haja ya kuimarisha
s e k t a ya v i wa n d a k wa
kutambua umuhimu wake
katika uchumi wa nchi kwani
viwanda vitasaidia kujenga
uchumi na kupanua soko la
ajira huku akisisitiza haja ya
kufanya kazi kwa pamoja
kati ya sekta ya uma na sekta
binafsi.
Alisisitiza kuwa umefika
wakati wa kuwa na mipango
maalum juu ya mwelekeo wa
sekta ya viwanda ambapo
hivi sasa tayari baadhi ya
viwanda vimeshaanza
kuleta mafanikio kikiwemo
kiwanda cha maziwa na
kile cha sukari kiliopo

Mahonda, hivyo ipo haja ya


kuongozeka zaidi.
Sambamba na hayo,
Dk. Shein alieleza kuwa
bado Baraza la Biashara la
Zanzibar linaonekana kuwa
ni Baraza la Serikali hali
ambayo sio sahihi katika
kutekeleza majukumu na
azma ya kuliimarisha Baraza
hilo.
Pia, Dk. Shein alisisitiza
haja kwa bidhaa za
m a o n y e s h o k u f a n y i wa
utafiti vizuri kwa lengo la
kukinga afya za wananchi
badala ya hali inayojitokeza
hivi sasa ya baadhi ya
wafanyabiashara wanaouza
biashara zao katika
maonesho hayo zikiwemo
dawa za asili kutokuwa na
kiwango kwa watumiaji.
Nae Makamu wa Piliwa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif
Ali Idd alisisitiza umuhimu
wa usimamizi wa viwango
vya bidhaa na ubora wake
sambamba na kukidhi haja
kwa wananchi.
Alisema kuwa Wizara
husika inakila sababu ya
kuhakikisha hakufanyiki
udanganyifu kwa wale
wanaouza bidhaa, ambao
hivi sasa wamejitokeza
wafanyabiashara ambao
huuza vitu vilivyokwisha
mda au kuwa chini ya
viwango.
Aidha, alisema haja
ya kusaidiwa kwa
wafanyabiashara wadogo
wadogo ili bidhaa zao ziweze
kuvutia.
M a p e m a Wa z i r i w a
Wizara hiyo Mhe. Nassor
Ahmed Mazrui, akisoma
taarifa ya Wizara yake
alisema kuwa kwa kutumia
twakwimu za uingizaji wa
bidhaa za mchele, unga
ngano na sukari, katika
kipindi cha Julai-Disemba,
2014, Zanzibar iliendelea
kuwa na chakula cha kutosha
cha aina hizo.
Alidha, alisema kuwa
mwenendo wa bei za
bidhaa muhimu hapa
nchini uliendelea kuwa wa
utulivu kutokana na Serikali
kuendelea kuchukua hatua
maalum za kisera za kudhibiti
bei zake kwa kushirikiana na
wafanyabiashara.
Pamoja na hayo, Waziri
Mzrui alisema kuwa hivi
k a r i b u n i m c h n a g o wa
sekta ya viwanda utaanza
kuimarika kutokana
na juhudi za kuanishwa
viwanda mbali mbali hapa
Zanzibar vikwemo kiwanda

cha maziwa, sabuni, samani


pamoja na kiwanda cha
sukari Mahonda.
Wakati huo huo, Dk. Shein
alifanya mkutano na uongozi
wa Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano juu ya
Utekelezaji wa Malengo ya
Wizara hiyo kwa robo mbili
(Julai-Disemba) 2014/2015
ambapo miongoni mwa
m a e l e z o ya k e a l i e l e z a
haja ya kuwekwa majina

ya mitaa hasa ile mitaa

iliyosahauliwa katika
zoezi la kuweka majina
ya mitaa lililofanywa na
Wizara hiyo, hasa katika
mitaa ya Mji Mkwongwe
na baadhi ya mitaa ya
Ngambo.
Nae Waziri wa Wizara
hiyo Mhe. Juma Duni Haji
alisema kuwa Wizara hiyo
imeendelea kusimamia
utekelezaji wa kazi zake

za kawaidia na maendeleo
kwa kuzingatia Dira ya
Taifa ya Maendeleo (Vision
2020), Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza
Umasikini (MKUZAII),
Sera ya Usafiri Zanzibar
(2008), Mpango Mkuu
wa Usafiri pamoja na Sera
nyenginezo zinazohusika
(Habari kwa hisani ya
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar)

MKE wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Gauck akishiriki ufunguzi wa


shule ya Kanisa katika ziara yake Kisiwani Zanzibar hivi karibuni.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

You might also like