Historia Ya CCM Tangu TANU Na ASP

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 22

CHAMA CHA MAPINDUZI

HISTORIA YA CCM TANGU


TANU NA ASP

Imetolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu za


Taifa, Mikoa na Wilaya. Inapatikana pia katika kitabu cha Sera za Msingi za CCM

Makao Makuu ya CCM


Dodoma, 2004

HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP


1.0

UTANGULIZI:

1.1

Maelezo ya awali

Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa
kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).
Tendo hilo la kihistoria lilikuwa ni la kuendeleza utamaduni uliokuwa umeanza huko
nyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la kujiimarisha katika mapambano. Kwa
mfano, ASP kwa upande wa Zanzibar ilitokana na kuungana kwa African Association
(AA) na Shirazi Association (SA), tendo ambalo liliunganisha nguvu za wanyonge katika
mapambano ya kuundoa usultani na utawala wa kikoloni wa Kiingereza. Kwa upande
wa Tanzania Bara, TANU ilitokana na kujibadilisha kwa Tanganyika African Association
(TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa.
Kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961 na ule wa Zanzibar
kupitia Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, kulifanya TANU na ASP viwe
vimekamilisha jukumu la ukombozi wa nchi hizi kutoka makucha ya ukoloni mkongwe
na usultani. Hata hivyo, vyama vya siasa hivi viliendelea kukabiliwa na majukumu ya
kuendeleza mapambano ya ukombozi katika Afrika
na kote duniani; kujenga
Tanganyika na Zanzibar huru kiuchumi na kijamii na kuimarisha umoja na mshikamano
wa kitaifa,
Katika mazingira ya ubeberu duniani wakati huo na hali ya unyonge wa mataifa haya
machanga, yakielewa kuwa umoja ni nguvu, Tanganyika na Zanzibar zilibaini umuhimu
wa muungano, hivyo ziliamua kuungana tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huo ndio
uliowezesha kuzaliwa kwa Tanzania. Chini ya Muungano huo, Tanzania iliendelea kuwa
na vyama vya siasa viwili, yaani TANU na ASP katika mazingira ya chama kimoja cha
siasa. Vyama hivi vilitambua fika kwamba vinahitaji chombo madhubuti cha uongozi
katika kutekeleza majukumu yake ya ukombozi kwa ukamilifu hivyo uamuzi ulifanywa
rasmi wa kuvunja TANU na ASP na kuundwa kwa Chama Cha Mapinduzi tarehe 5
Februari, 1977.
Katiba ya CCM, katika Azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa wa Pamoja wa TANU na ASP
tarehe 21 January, 1977, inaeleza kuwa, (uk. 2-3), ...kwa kauli moja tunaamua na
kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African Union(TANU) na AfroShirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari, 1977 na wakati huohuo
kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika
mambo yote kwa mujibu wa Katiba.
Muungano wa TANU na ASP ndio uliowezesha CCM kuwa Chama chenye nguvu, imara
na madhubuti, hivyo kuwa Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya juu wa
kuwaunganisha Watanzania. Aidha, CCM kimeweza kuwaongoza wananchi katika
2

mapambano ya kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadiliko


mbalimbali yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.CCM kimeendelea kupewa dhamana na
wananchi ya kuunda serikali na kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wa
demokrasia ya chama kimoja hadi sasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi,
kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania
Juni 1992.
1.2

Umuhimu wa kuielewa historia ya CCM na Vyama vilivyokitangulia

Historia ya CCM tangu TANU na ASP ina umuhimu wa pekee katika Taifa letu katika
kuelewa tulikotoka, tulipo hivi sasa na tunakoelekea. Historia ya nchi yetu haiwezi
kukamilika bila ya historia ya vyama hivi vya ukombozi. Historia hutoa mafunzo na ni
mwelekezaji pia, kwa hiyo ni wajibu wa Watanzania, hasa wanachama wa CCM
kujifunza kutokana na historia yetu. Kazi kubwa na ya msingi inayofanyika katika
kujifunza historia hiyo, ni kurithisha dhamira ya kujituma na kudumisha uhuru wa nchi
yetu. Hivyo, ili kuendelea kukijenga Chama, na kuimarisha uwezo wa kuendelea
kukamata dola barabara kwa namna endelevu, hapana budi ihakikishwe kuwa historia
ya CCM inabeba pia jukumu la msingi la kusaidia:

1.3

Kujua Chama kilikotoka, mahali kilipo na kinakoelekea katika misingi ya sera,


itikadi, malengo na wanachama.
Kuunganisha wanachama na kuwaweka pamoja kiimani, kiitikadi na
kiutendaji.
Wanachama kujitambua, kutambua wajibu na majukumu yao na kujenga
moyo wa kujiamini na kujithamini.
Kuinua kiwango cha ushiriki wa wanachama wa CCM na wananchi katika
kubuni na kutekeleza mkakati na mbinu sahihi za kutetea na kuendeleza
Chama na taifa kufuatana na hali ya wakati na mahali.
Kuweka misingi ya kufanya tathmini na hivyo kuwa na uhakika katika kufanya
maamuzi.
Kupanda mbegu bora za upendo, uzalendo na uchungu wa kweli kwa uhai wa
CCM na taifa kwa ujumla.
Kuwa na majibu sahihi wakati wote kwa hoja mbalimbali zinazotolewa kuhusu
Chama Cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla.
Kuweka msingi wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine maadili ya
msingi wa uhai wa CCM.
Kuhifadhi kuweka na kueneza kumbukumbu sahihi ya historia ya Chama,
nchi, mchango wa Waasisi na wanachama na kuhakikisha wapotoshaji
hawapati fursa ya kueneza uongo.

Chimbuko la Historia ya CCM

Pamoja na kwamba Chama Cha Mapinduzi kuwa kilizaliwa rasmi tarehe 5 Februari,
1977, chimbuko lake linaanzia miaka mingi kabla, sambamba na historia ya uhai wa
taifa la Tanzania. Mizizi ya historia ya CCM imo ndani ya harakati za kukataa ukoloni na
usultani, zilizofanywa na wananchi wa Tanzania. Wahenga wetu kwa pamoja tangu
enzi, walionyesha wazi kukataa kwao kutawaliwa. Historia ya Tanzania inao utajiri wa
3

mifano mingi ya harakati hizo japokuwa zilijengwa katika misingi ya ukoo na ujirani,
katika wilaya na mikoa mbalimbali hata kabla ya kuundwa kwa vyama vya TANU na
ASP.
Wananchi hao waliotutangulia walikataa kunyonywa, kupuuzwa, kubaguliwa,
kutawaliwa, kunyanyaswa na kugawanywa katika misingi ya rangi, kabila, dini, jinsia,
nk. Utu na uhuru wao ulikuwa na thamani kubwa sana. Hivyo waliamua kupambana
dhidi ya udhalimu huo. Baadhi ya mifano ya jitihada za mapambano ya awali ni Vita ya
Majimaji huko Umatumbi na maeneo ya kusini, Mbiru huko Upare, Waluguru, Wameru,
Wahehe na mengineyo huko Unguja, Pemba, Kanda ya Ziwa na katika jamii za
wafugaji. Ari, utashi, uzalendo na dhamira ya kweli ya kutaka kujitawala
vilivyojidhihirisha katika harakati hizo, viliotesha mizizi iliyoshikilia uhai wa vyama vya
TANU na ASP.
2.0

TANU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

2.1

TANU ilizaliwa katika mazingira yaliyoandaliwa na Tanganyika African


Association (TAA):

TAA iliundwa 1948 kufuatia tukio la kutengana kwa African Association (AA) ya
Tanganyika na Zanzibar. AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil
Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes akiwa Katibu. Malengo ya AA yalikuwa ni
kupigania haki, maslahi na umoja wa Waafrika. AA ilikuwa na matawi yake makuu
Dodoma na Zanzibar. Aidha, AA ilifungua matawi katika miji iliyokuwa makao makuu ya
wilaya.
Katiba ya TAA ilitamka wazi kwamba Chama hicho hakikuwa na malengo ya kisiasa.
Mwaka 1953 yalifanyika mabadiliko ya uongozi katika TAA. Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA. Chini ya uongozi mpya, Katiba ya TAA
ilionekana kwamba isingeweza kukidhi malengo ya kisiasa. Mwalimu alipewa jukumu
la kuandaa Katiba mpya ya TAA ambayo ingezingatia malengo ya kisiasa. Baada ya
uandaaji wa Katiba hiyo kukamilika, haja ya kubadili jina ilionekana dhahiri na majina
mengi yalipendekezwa likiwemo la TANU. Nafasi ya TAA ilichukuliwa na TANU
iliyozaliwa tarehe 7 Julai, 1954. TANU ilirithi matawi ya TAA, wanachama na viongozi
wa TAA katika maeneo mengi.
Waasisi wa TANU ambao walihudhuria na kushiriki katika Mkutano wa kuzaliwa kwa
TANU walikuwa 17:
(1)
(2)
(3)
(4)
(5)
(6)
(7)
(8)

Mwalimu J.K. Nyerere Rais wa TAA/TANU


Geremano Pacha Jimbo la Magharibi
Joseph Kimalando Jimbo la Kaskazini
Japhet Kirilo Jimbo la Kaskazini
C.O. Milinga Jimbo la Mashariki
Abubakari llanga Jimbo la Ziwa
L.B. Makaranga Jimbo la Ziwa
Saadani A. Kandoro Jimbo la Ziwa
4

(9)
(10)
(11)
(12)
(13)
(14)
(15)
(16)
(17)

Suleman M. Kitwara Jimbo la Ziwa


Kisunguta Gabara Jimbo la Ziwa
Tewa Said Tewa Jimbo la Mashariki
Dossa A. Aziz Jimbo la Mashariki
Abdu Sykes Jimbo la Mashariki
Patrick Kunambi Jimbo la Mashariki
Joseph K. Bantu Jimbo la Mashariki
Ally Sykes Jimbo la Mashariki
John Rupia Jimbo la Mashariki

2.2 TANU ilizaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia:


Katika vita ya Pili ya Dunia (1939 1945), Watanganyika walishiriki wakiwa askari
upande wa Waingereza. Katika kushiriki huko, baadhi yao walipigana vita nchi za nje,
kwa mfano, India, Burma, Madagascar n.k. Wakiwa huko vitani walipata fursa ya
kubadilishana mawazo ya kisiasa na askari wenzao waliokutana nao katika uwanja wa
vita.
Baadhi ya askari hao wa Tanganyika waliporejea kutoka vitani walikuja na fikra mpya za
ukombozi wa Mwafrika. Fikra hizi mpya zilioana na zile za Kituo cha Wasomi wa
Kiafrika waliokuwa London. Kituo hicho kilijishughulisha sana na suala la ukombozi wa
Mwafrika kupitia midahalo.
2.3

TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika:

Katika miaka 1950, wakulima walikwishajiunga na kuanzisha vyama vya kuuza mazao
yao ya biashara ili waweze kupata bei nzuri kwa kupunguza gharama ya mtu wa kati
ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa Kiasia. Baadhi ya Vyama vya Ushirika
vilivyokuwepo kabla ya TANU ni:

Kilimanjaro Co-operative Union Ltd (1933)


Ngoni Matengo Co-operative Union Ltd. (1936)
Rungwe African Co-operative Union Ltd. (1949)
Bukoba Co-operative Union Ltd. (1950)
Lake Province Native Growers Association.

Kwa kuwepo vyama vya ushirika, ujumbe wa TANU kuwafikia wananchi ulirahisishwa.
Wanachama wa vyama vya ushirika walijiunga na TANU. Wanachama na viongozi wa
vyama vya ushirika waliunga mkono TANU katika madai yake ya kudai uhuru. Baadhi
ya viongozi wa vyama vya ushirika walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU katika ngazi
ya Taifa. Kwa mfano:

Ndugu Nsilo Swai


Sir George Kahama
Ndugu Jeremiah Kasambala
Balozi Paul Bomani
5

Ndugu John Mhavile.

TANU nayo iliunga mkono vyama vya ushirika katika madai yake ya bei nzuri ya mazao
yao na kuondoa ushuru wa kahawa uliokuwa unatozwa na Serikali Kuu. Aidha, TANU
ilihimiza na kuwahamasisha wananchi kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika.
Kazi hii ya kuhimiza na kuhamasisha wananchi kujiunga na ushirika iliendelea kufanywa
na TANU hata baada ya Tanganyika kupata uhuru wake.
Baada ya Uhuru, TANU iliuona ushirika kuwa ni chombo cha kuleta maendeleo hivyo
wananchi walihimizwa kuanzisha ushirika katika maeneo ambayo hayakuwa na vyama
vya ushirika. Hali hii inaendelea hadi hivi sasa ambapo katika mfumo wa uchumi wa
Soko, CCM inauona ushirika kuwa ni chombo cha kumwezesha mwananchi
kiuchumi katika kumiliki na kuendesha uchumi wa Taifa lake.
2.4 TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya wafanyakazi:
Lengo kuu la Vyama vya Wafanyakazi lilikuwa ni kutetea maslahi ya wafanyakazi.
Baadhi ya vyama vya wafanyakazi ni:

Chama
Chama
Chama
Chama
Chama
Chama
Chama
Chama
Chama

cha
cha
cha
cha
cha
cha
cha
cha
cha

Wafanyakazi Serikalini (1929)


Makuli (1937)
Wapishi na Madobi (1939)
Wapishi na Watumishi wa Ndani
Madereva
Walimu
Wafanyakazi wa Reli
Wafanyakazi Mashambani
Wafanyakazi Viwandani.

Vyama vya Wafanyakazi viliunda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tanganyika


Federation of Labour TFL) tarehe 10 Oktoba, 1955.
Wafanyakazi kupitia vyama vyao walikuwa na madai yafuatayo:

nyongeza ya mshahara
mapumziko ya mchana siku ya kazi
umri wa kustaafu na
kuondoa ubaguzi katika ajira na huduma za jamii.

Vyama vya wafayakazi vilisaidia kuvunja ukabila na hivyo kuwa chanzo cha umoja.
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilisaidia kueneza TANU kwa njia zifuatazo:

Kila Chama cha Wafanyakazi chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi


(TFL) kilitakiwa kuwashawishi na kuwahimiza wanachama wake kujiunga
na TANU.
Kila mwanachama wa TANU aliyekuwa mwanachama wa Chama cha
Wafanyakazi alitakiwa kulipa mchango wake wa kila mwezi kwa TANU.
6

Vyama vya Wafanyakazi, wakati mwingine kupitia TFL, viliweza kusaidia


TANU kifedha fedha hizo zilitokana na michango ya hiari.
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilisaidia sana kuleta mwamko wa
kisiasa miongoni mwa wafanyakazi.

Vyama vya Wafanyakazi vilifanya yote hayo kwa kuelewa kwamba uhuru ndio
ungekuwa suluhisho la kweli la matatizo yao.
Kama ilivyokuwa kwa vyama vya ushirika, baadhi ya viongozi wa vyama vya
wafanyakazi walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU. Mwaka 1958, Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, alichaguliwa kuwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU. Toka wakati huo hadi hivi sasa, Mzee
Kawawa amekuwa na uongozi uliotukuka katika TANU/CCM.
Kwa upande wake, TANU iliunga mkono madai ya vyama vya wafanyakazi na migomo
ya wafanyakazi. Katika historia ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, mgomo wa
wafanyakazi wa Shamba la Mazinde huko Tanga na mgomo wa wafanyakazi wa
Kiwanda cha Bia Dar es Salaam ni miongoni mwa migomo maarufu.
Shamba la Mazinde lilikuwa mali ya bepari mmoja wa Kiingereza, mwanachama
mashuhuri wa United Tanganyika Party (UTP) aliyewahi kushiriki katika kugombea na
kushindwa na mgombea wa TANU katika Uchaguzi Mkuu wa Baraza la Kutunga Sheria
mwaka 1958. Wafanyakazi katika Shamba la Mazinde walijiunga na Chama cha
Wafanyakazi Mashambani (Tanganyika Plantation Workers Union TPWU) ambacho
kilikuwa kimeshirikishwa katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi. Mmiliki wa
Shamba la Mazinde alikuwa na tabia ya kuwafukuza wafanyakazi walioonyesha kupinga
UTP na walioamua kujiunga na Chama cha Wafanyakazi Mashambani. Katika harakati
za kuwaunga mkono wenzao waliofukuzwa, wafanyakazi wote elfu tatu (3,000)
waliamua kugoma na matokeo yake wote walifukuzwa kazi.
Jitihada za TFL kusuluhisha mgogoro huo kati ya Mwajiri na wafanyakazi zilishindikana.
TFL na TANU kwa pamoja viliunga mkono mgomo wa wafanyakazi wa Shamba la
Mazinde. TANU kupitia Mwalimu Nyerere ilitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga
kuwahifadhi wafanyakazi waliofukuzwa kazi. Wananchi waliitikia wito wa TANU na
kuwapokea na kuishi nao. Aidha, TFL na TANU vilitoa wito kwa wananchi kususia
shamba la Mazinde. Wafanyakazi hao hawakurejea kazini hata baada ya mmiliki
kuwataka kufanya hivyo. Matokeo yake ni kwamba mmiliki huyu wa Shamba la
Mazinde hakuchukua muda akafilisika na akarejea kwao Uingereza.
Huu ulikuwa ni ushindi wa TANU na TFL. TANU ilitambuliwa na wafanyakazi
mashambani na iliendelea kuimarika. Kwa kuwa ngome ya UTP, na baadaye African
National Congress (ANC) ilikuwa huko Tanga pigo hili lilisababisha kifo cha UTP na
kuzorota kwa ANC.
Kuhusu mgomo wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaam, mgomo ulianza Aprili hadi Juni,
1958. Mgomo uliwashirikisha wafanyakazi wapatao mia tatu (300). Wafanyakazi
7

walikuwa wanadai nyongeza ya mshahara. Wafanyakazi wote waliogoma walifukuzwa


kazi na mwajiri.
Katika kuonyesha mshikamano na wafanyakazi katika mgomo huu wa Kiwanda cha Bia,
TANU ilichukua hatua zifuatazo:

Ilitoa wito kwa nchi nzima kususia pombe zote za kigeni;


Iliwaomba wananchi wa Dar es Salaam kuwasaidia wagomaji kwa
kuwachangia chakula na fedha;
Iliwaomba wananchi wenye nyumba Ilala kuwapokea wagomaji katika
nyumba zao pasipo kuwatoza kodi ya nyumba.

Kama kawaida yao, wananchi waliitika wito na maombi ya TANU. Kwa kupitia migomo
TANU ilizidi kuimarika miongoni mwa wafanyakazi.
2.5

TANU ilizaliwa katika mazingira ya kero na adha za wananchi kutoka


Serikali ya Kikoloni:

Malalamiko hayo ya wananchi yalijidhihirisha katika maeneo yafuatayo:

Upinzani huko Upare dhidi ya ulipaji kodi kulingana na mapato (Mbiru);


Wahehe kukataa kuogesha ngombe wao;
Waluguru kupinga juhudi za kuhifadhi mapori na kulima matuta;
Wafugaji (Wasukuma) kupinga kodi ya ngombe na kupunguza idadi ya
ngombe, kumi kwa kila mia;
Wameru wapatao 3,000 walipinga kunyanganywa ardhi yao na Serikali
ya Kikoloni na kuwapa walowezi.

TANU ilitumia kero hizo za wananchi katika kuwaunganisha wananchi na kuwaelekeza


namna ya kutafuta haki zao.
Kuhusu ardhi ya Wameru, Katika mkutano wake wa kwanza, TANU ilitoa tamko
lifuatalo:Mkutano huu unasikitika sana juu ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya
nchi hii huko Meru. Mkutano unakubali kwamba Serikali inayo mamlaka
kuchukua ardhi ya raia hata kwa lazima ili ardhi hiyo iwe faida ya watu
wote kama vile kupitisha reli, barabara, kujenga hospitali, shule au
kutumia kwa jambo lingine la manufaa kwa wote. Lakini Serikali haina
mamlaka kuchukua ardhi ya raia ili ardhi ile wapewe raia wengine
waitumie kwa faida yao wenyewe Mkutano huu unataka Serikali
iwarudishie Wameru ardhi yao ama kuwalipa fidia kwa hasara
walizopata kubwa, kwa kufukuzwa kama mahabusu, kama
Baraza la Umoja wa Mataifa lilivyokubaliana. (Historia ya Chama
cha TANU 1954 hadi 1977, uk 36).

2.6

Kuenea kwa TANU na Kupata Ushindi:

Dhumuni la kwanza la TANU mwaka 1954 lilikuwa ni kuwatayarisha Watanganyika


kujitawala na kujitahidi kwa bidii mpaka Tanganyika imepata uhuru na inajitawala.
TANU ilibaini kwamba lengo lake kuu ni kupigania uhuru wa Tanganyika na silaha yake
kubwa ni umoja hasa umoja wa Waafrika. Kwa mnasaba huo, TANU iliacha mlango
wake wazi kwa Waafrika bila ya kujali kabila, dini, rangi, jinsia na majimbo yao. Toka
mwanzo, msingi huu uliifanya TANU kuwa chama cha umma. Hata hivyo uamuzi wa
kukifanya Chama cha TANU kuwa wazi kwa Waafrika tu ulikuwa ni uamuzi wa kimkakati
tu. Haikukusudiwa kukifanya Chama hicho kuwa cha kibaguzi na kwa hakika
kiliendelea kushirikiana na kuwaenzi Waasia na Wazungu walioafiki imani na
madhumuni ya TANU.Miongoni mwa Waasia na Wazungu waliokuwa na mtazamo wa
kizalendo katika shughuli za kisiasa ni Amir Jamal, Al-Noor Kassim, Derek Bryceson,
Babra Johnson na Leader Stirling. Baada ya uhuru (1962), Waasia na Wazungu
waliruhusiwa kuwa wanachama wa TANU.
Katika harakati za kuitangaza TANU, njia mbali mbali zilitumika:

2.7

TANU ilifungua matawi katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu.


TANU ilitumia mikutano ya hadhara katika kufikisha ujumbe wake kwa
wananchi.
TANU ilitumia mikutano ya ndani ya wanachama.
TANU ilitumia vyombo vya habari, hususan magazeti, kama vile Sauti ya
TANU, Habari za TANU na Mwafrika.

Jumuiya za TANU za Umoja wa Wanawake, Umoja wa Vijana na Wazazi


zilifanya kazi kubwa katika kukieneza na kukiimarisha Chama.

TANU ilianzisha rasmi mwaka 1955 sehemu ya Wanawake wa TANU. Chama kilitambua
kwamba mapambano ya kudai uhuru yasingeweza kufanikiwa bila ya kulitumia jeshi
kubwa la Wanawake. Chama kilimpata Bibi Titi Mohamed na kumpa jukumu la
kuwakusanya wanawake ili washiriki katika mapambano ya kudai uhuru. Sehemu ya
Wanawake ilipewa majukumu yafuatayo:

Kupata wanachama wa TANU wengi;


Kueneza Chama hasa vijijini kwa moyo wa kujitolea;
Kuona kwamba viongozi wa Chama wako salama/ulinzi wa viongozi na
Kukipatia Chama fedha kutokana na shughuli halali mbali mbali.

Katiba ya TANU ya mwaka 1954, sehemu ya sita, ilitoa nafasi kwa vijana kuunda umoja
wao ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika mapambano ya kudai uhuru. Umoja wa
Vijana ulikuwa na majukumu yafuatayo:

Kuwaandaa vijana katika uongozi;


Kuwahimiza vijana kujitolea kufanya kazi za TANU;
Kutekeleza shabaha za TANU;
9

2.8

Kuunda makundi ya starehe na maendeleo miongoni mwa wanachama


kama vile, elimu, biashara na michezo;
Kukusanya habari na kufuatilia mwenendo wa kisiasa nchini;
Kushirikiana na vyama vingine vya vijana visivyo na upinzani kwa TANU.

TANU ilivyopambana na kuvishinda vikwazo na hila za Mkoloni

Jumuiya ya Wazazi (Tanganyika Parents Association TAPA) iliundwa mwaka 1955


chini ya Ndugu Lawi Sijaona. TAPA ilikuwa ndiye mtekelezaji mkuu wa Azimio la
Mkutano Mkuu wa Tabora lililohusu upanuzi wa elimu. Katika kutekeleza jukumu lake,
TAPA ilifungua shule za msingi na sekondari nyingi nchini na kuendesha kisomo cha
Watu Wazima. Huu ulikuwa mkakati wa makusudi wa kuwaandaa wananchi kushika
madaraka baada ya uhuru.
Jinsi TANU ilivyozidi kuimarika ndivyo hivyo ilivyopambana na vikwazo na hila za
Mkoloni:

Serikali ya Kikoloni ilipitisha Sheria mwaka 1953 ya kuwakataza watumishi


wa Serikali wa mataifa yote kujiunga na vyama vya siasa. Aidha, Tangazo
la Serikali Namba 2 la 1954 lilifafanua kuwa hata Sukuma Union kilikuwa
ni Chama cha Siasa. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 6 la
1954, maafisa wote wa Serikali waliokuwa wanachama wa TANU na
waliotaka kuendelea na utumishi serikalini walitakiwa kujiuzulu mara
moja. Aidha, Sheria ya vyama vya siasa, 1954, ilitaka kila tawi la TANU
lisajiliwe kabla ya kuandikishwa kisheria. Sheria hii iliiwezesha serikali ya
mkoloni kusajili au kutokusajili tawi lo lote la TANU.

Mara tu baada ya TANU kuundwa, Rais wake Mwalimu Nyerere alitakiwa


na Serikali ya Kikoloni achague moja kati ya mambo mawili ama
kuendelea kuiongoza TANU au kujiuzulu uongozi wa TANU na kuendelea
na kazi yake ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu.
Mwalimu
aliamua kuendelea kuihudumia TANU hivyo akalazimika kujiuzulu kazi ya
ualimu.
Bila shaka, Serikali ya Kikoloni ilidhani kwamba Mwalimu
asingejiuzulu ualimu. Katika suala hili, uamuzi wa Mwalimu haukuwa
rahisi hasa kwa kuzingatia kwamba kazi ya ualimu ndio alikuwa
ameisomea, riziki yake na ya familia ilitokana na ualimu na kwamba
kuitumikia TANU wakati huo ilikuwa ni kupambana na Serikali ya Kikoloni
na hii ilikuwa ni hatari kubwa. Kwa kujiuzulu ualimu, Mwalimu alipata
nafasi kubwa zaidi ya kuihudumia TANU.

Mwalimu Nyerere mwaka 1958 alishitakiwa na Serikali ya Kikoloni kwa


kosa la kuwakashifu District
Commissioners wa Songea, Geita na
Musoma. Kwamba kashfa hiyo aliifanya kwa kupitia makala aliyoiandika
kupitia Gazeti la Sauti ya TANU Toleo Namba 29 la tarehe 27 Mei, 1958.
Katika kesi hii iliyosikilizwa na Mahakama ya Dar es Salaam, Mwalimu
alihukumiwa faini ya shs. 3,000/= (shilingi elfu tatu) au kifungo cha miezi
6. Mwalimu alilipiwa faini hiyo na TANU.
10

Serikali ya kikoloni pia ilijitahidi kadri ilivyoweza kuwatumia baadhi ya


machifu kuwa chombo cha kuzuia uenezaji wa TANU. Machifu walipewa
madaraka makubwa zaidi na zaidi ili wajisikie kuwa ni sehemu ya utawala
na kwamba TANU ilikuwa na lengo la kuwakosesha maslahi yao. Mwaka
1957, Serikali ya kikoloni iliunda Baraza la Machifu wa Tanganyika
(Territorial Convention of Chiefs). Kwa kuwatumia machifu, Serikali ya
kikoloni ilitegemea kuwagawa Watanganyika kwa misingi ya ukabila ili
kuweza kuwatawala wananchi kwa urahisi zaidi. Aidha, Serikali ya kikoloni
ilikuwa na lengo la kuwagonganisha machifu na viongozi wa TANU.

Serikali ya kikoloni ilihimiza kuundwa kwa United Tanganyika Party (UTP)


ndani ya Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1956. UTP ilikuwa ni chombo
na Sauti ya Serikali ya kikoloni kwa sababu zifuatazo:(a)
(b)

Uongozi wa UTP uliundwa na Wajumbe wa Baraza la Kutunga


Sheria,
Tanganyika Unofficial Members Organization (TUMO)
Wajumbe hao waliteuliwa na Gavana na hivyo hawangeweza
kupingana na siasa ya Serikali ya Kikoloni.

Licha ya hila na vikwazo vya mkoloni, TANU ilijikuta ina mtihani mgumu wa kuamua
kushiriki ama kutokushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza mwaka 1958. Akifungua
kikao cha kwanza cha Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1956, Gavana Edward Twining
alitangaza kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza
mnamo 1958. Sharti moja kubwa la uchaguzi huo lilikuwa kwamba kila mpiga kura
apige kura tatu: moja kwa Mzungu, moja kwa Mwasia na moja kwa Mwafrika.
Suala hili la kura ya Mseto lilijadiliwa kwa undani katika Mkutano Mkuu wa TANU
uliofanyika Tabora mwaka 1958 na kuhudhuriwa na Wajumbe 300 kutoka sehemu zote
za Tanzania Bara. Ili kupata nafasi nzuri ya kujadili agenda hii, Mwalimu Nyerere
aliomba asiwe Mwenyekiti wa kikao hicho, nafasi yake ilichukuliwa na Mwalimu Kihere
kutoka Tanga.
Mwalimu Nyerere aliweza kuushawishi Mkutano kukubali kushiriki katika Uchaguzi Mkuu
wa kwanza mwaka 1958.
Hoja za Mwalimu zilikuwa ni kwamba kama TANU
isingeshiriki, ingekuwa imeshindwa kwani isingekuwa na wawakilishi katika Baraza la
Kutunga Sheria. Kujitoa katika uchaguzi huo kungekuwa na maana ya kujitoa katika
uwanja wa mapambano ambao sasa ungemilikiwa na UTP. Uamuzi wa TANU kushiriki
katika uchaguzi huo ulikuwa ni wa busara kwani wagombea wote waliosimamishwa kwa
tiketi ya TANU walishinda na hivyo TANU kunyakua viti vyote vya wajumbe wa
kuchaguliwa wa Baraza la Kutunga Sheria.
Matokeo ya kukubali kura ya mseto, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TANU, Ndugu Zuberi
Mtemvu aliamua kuachana na TANU na kuanzisha African National Congress (ANC)
mwaka 1958. Hata hivyo toka kuanzishwa kwake hadi kifo chake, ANC haikupata hata
kiti kimoja katika Baraza la Kutunga Sheria. Aidha, Ndugu Mtemvu alibwagwa kwa
11

kishindo na Mwalimu Nyerere katika kugombea Urais wa Jamhuri ya Tanganyika mwaka


1962.
Uchaguzi Mkuu wa pili ulifanyika mwaka 1960. Katika uchaguzi huo, TANU ilijikuta
imefanikiwa kupitisha wagombea wake 58 bila ya kupingwa. Kati ya wagombea hao 58
waliopita bila kupingwa, 8 walikuwa Wazungu, 11 Waasia na 39 Waafrika. Tarehe 30
Agosti, 1960 ulifanyika uchaguzi katika sehemu nyingine ambako kulikuwa na zaidi ya
mgombea mmoja katika jimbo la uchaguzi. Wagombea viti wote jumla walikuwa 25
kati ya hao 11 walisimamishwa na TANU na walishinda isipokuwa mmoja tu wa kiti cha
Mbulu, Chifu Amri Dodo aliyeshindwa na Herman E. Sarwatt ambaye alikuwa mgombea
binafsi. Hata hivyo, Sarwatt alikuwa ni mwanachama wa TANU.
Pamoja na vikwazo hivi Msimamo sahihi usioyumba uongozi bora umoja mshikamano
ari na dhamira ya wananchi ya kutaka kujitawala vilikuwa chachu iliyosababisha TANU
kupata ushindi wa kishindo na kutokana na ushindi huo, Gavana Richard Turnbull
alimwomba Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere kuunda Baraza la Mawaziri ambalo lilikuwa
na jukumu la kuongoza nchi kwa jumla na kumshauri Gavana. Serikali ya Madaraka
iliundwa na kuapishwa tarehe 3 Septemba, 1960. Tanganyika ilipata Serikali ya Ndani
tarehe 1 Mei, 1961 na uhuru kamili tarehe 9 Desemba, 1961 na Mwalimu Nyerere kuwa
Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika huru.
2.9

Siri ya ushindi wa TANU

Uhuru wa Tanganyika ulipatikana katika kipindi cha miaka saba tu ya kudai uhuru.
Kipindi hiki ni kifupi. Siri ya TANU ya ushindi ilitokana pamoja na mambo yafuatayo:

Tanganyika ilikuwa chini ya Udhamini wa Umoja wa Mataifa tofauti na


nchi kama Kenya, Uganda, Zambia na Malawi zilizokuwa makoloni moja
kwa moja chini ya Serikali ya Kiingereza iliyokuwa na sauti ya mwisho.
Chini ya udhamini huo watawala wa Kiingereza, walipaswa kuitawala
nchi hii kwa mujibu wa masharti ya Umoja wa Mataifa kuhusu makoloni ya
udhamini.

Nafasi ya Jamhuri ya Kisovieti (Urusi) (ilikuwa miongoni mwa mataifa


manne makubwa) katika Umoja wa Mataifa ilisaidia kutoa msukumo kwa
Umoja huo katika kufanikisha juhudi za TANU za kudai uhuru wa
Tanganyika. Aidha, Urusi ilikuwa ni Mjumbe wa Baraza la Udhamini.
Msimamo wa Urusi kuhusu makoloni ulikuwa thabiti kwamba makoloni
yana haki ya kujitawala. Uhuru wa India, Pakistani na Ghana ulisaidia
kutoa msukumo kwa makoloni kujipatia uhuru.

Lugha ya Kiswahili ilisaidia sana katika kuharakisha maendeleo ya siasa.


Kiswahili kilisaidia kuwaunganisha wananchi na hasa kilirahisisha kazi ya
viongozi wa TANU. Viongozi hao hawakuhitaji wakalimani wakati wa
kuwahutubia wananchi katika mikutano ya hadhara. Lugha ya Kiswahili
ilisaidia na inaendelea kusaidia katika kuleta umoja na mshikamano wa
kitaifa.
12

Katika Tanganyika hapakuwepo na mtengano wa kijamii wenye nguvu.


Tanganyika ilikuwa na makabila yapatayo 120 lakini kihistoria hapakuwa
na utawala wa kikabila wa kugandamiza kabila lingine.

Tanganyika ilikuwa na walowezi wachache ikilinganishwa na nchi kama


Kenya. Katika makoloni mengi uhuru wa wananchi ulicheleweshwa
kutokana na siasa za walowezi ambazo msingi wake ni uchumi hodhi.

Umoja wa Vijana na Umoja wa Wanawake chini ya TANU, walitoa


msukumo mkubwa katika kudai uhuru. Vikundi hivyo vilijawa na ari na
moyo wa kimapinduzi; vilifanya kazi ya kujitolea usiku na mchana.

Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Ushirika viliweza kuwabana vilivyo


Wakoloni kwa njia ya migomo na ususiaji wa bidhaa.

Uongozi bora wa TANU, hususan uongozi wa Mwalimu Nyerere. Uongozi


bora wa TANU ndio uliokipa Chama msimamo thabiti na kuwafanya
wananchi kuwa na imani kubwa na TANU.

Aidha TANU iliweza kushinda changamoto katika sura ya hila na vikwazo kadhaa na
kupata mafanikio kama vile:3.0

ASP
NA HARAKATI ZA MAPAMBANO DHIDI YA
KIINGEREZA NA USULTANI WA KIARABU

3.1

UKOLONI WA

Mazingira ambamo ASP ilizaliwa:

ASP ilizaliwa katika mazingira yaliyokwisha andaliwa kisiasa na African


Association (AA) na Shirazi Association (SA); vyama ambavyo vilikuwa
nusu vya siasa na nusu vya kupigania maslahi ya Watumishi wa Kiafrika
kazini. Katika mazingira hayo, waafrika na Washirazi walielewa kwamba:(a)
(b)
(c)

Adui wa Waafrika ni ukoloni wa Kiingereza na umwinnyi wa Kiarabu


ukiongozwa na Sultani.
Umoja miongoni mwa Waafrika ni muhimu ili kujipatia uhuru wa
kisiasa.
Ukoloni wa Kiingereza ulikuwa na nia ya kutoa uhuru kwa Waarabu
wa Oman ambao walichukuliwa kwamba ndio wenye nchi.

Aidha, ASP ilizaliwa katika mazingira yaliyokuwa yamejaa manunguniko


dhidi ya ukoloni wa Kiingereza na ubwanyenye/umwinyi wa Kiarabu.
Miongoni mwa manunguniko hayo ni:(i)
(ii)

Kutokuwepo na demokrasia ya kweli katika utawala wa kikoloni.


Kutokuwepo na wawakilishi wa Waafrika katika baraza la Kutunga
Sheria kuanzia mwaka 1926 hadi 1946
13

(iii)
(iv)
(v)

Ubaguzi katika kazi na huduma za jamii, hususan elimu na afya.


Ardhi ilikuwa inamilikiwa na kusimamiwa na Waarabu. Waafrika
walikuwa manokoa katika mashamba ya Waarabu.
Sheria ya Serikali ya Kikoloni ya mwaka 1953 iliwazuia wafanyakazi
Serikalini wasishiriki katika shughuli za kisiasa.

ASP ilizaliwa baada ya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au HIZBU kuwa


imeundwa mwaka 1955.
HIZBU ndicho chama kilichotoa upinzani
mkubwa kwa ASP.

ASP ilizaliwa baada ya Vita Kuu ya Pili. Uingereza ilitoka vitani ikiwa
maskini ajabu ikilinganishwa na kipindi kabla ya vita na haikuwezekana
tena kuendelea kushikilia makoloni yake. Marekani ilizuka katika vita ikiwa
Taifa lenye nguvu zaidi kuliko mataifa yote ya Ulaya Magharibi.

ASP ilizaliwa baada ya vyama vya siasa vingine kuwa vimeibuka katika
nchi nyingine za Afrika hasa TANU ambayo ilikuwa na mahusiano ya
karibu na ASP. Hata kabla ya ASP, kulikuwa na uhusiano wa kihistoria
uliojengeka tangu kuanzishwa kwa AA Tanzania Bara na Zanzibar na vile
vile kuendeleza ushirikiano huo kupitia TAA na AA ya Zanzibar. Hata
wakati wa kuunganisha AA na SA na kuunda ASP, Rais wa TANU Mwalimu
Nyerere alihudhuria Mkutano huo.

3.2

Kuzaliwa na Kuimarika kwa ASP:

Wazo la kuunganisha nguvu za Waafrika liliwasilishwa kwenye Mkutano wa Pamoja wa


African Association (AA) na Shirazi Association (SA) uliofanyika tarehe 5 Februari,
1957. Mkutano huo ulikubaliana kuunganisha AA na SA na kuanzisha Afro-Shirazi Party
(ASP). Sheikh Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa ASP na
Sheikh Thabit Kombo alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu.
Waasisi wa ASP waliohudhuria Mkutano huo na kupitisha uamuzi wa kuunganiisha AA
na SA ni:African Association
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
9.
9.
10.

Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh

(AA):

Abeid Amani Karume


Mtoro Rehani
Ibrahim Saadallah
Mtumwa Borafia
Bakari Jabu
Rajab Swedi
Saleh Juma
Abdullah Kasism Hanga
Ali Juma Seif
Mzee Salehe Mapete.

Shirazi Association (SA):


1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.

Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh
Sheikh

Thabiti Kombo
Muhidini Ali Omar
Ali Ameir
Ameir Tajo
Ali Khamis
Mdungi Ussi
Haji Khatibu
Othman Sharif

14

Chimbuko la kuunganisha AA na SA lilitokana na Tangazo la Serikali ya Kikoloni kuhusu


Uchaguzi Mkuu wa Kwanza wa kuwachagua Wajumbe 6 kati ya 12 wa kuingia katika
Baraza la Kutunga Sheria Zanzibar (Legislative Council LEGCO). Uchaguzi huo
ulipangwa kufanyika Julai, 1957. wajumbe 6 wengine walitakiwa kuteuliwa na Sultani.
Bila ya kuungana isingekuwa rahisi kwa AA na SA kupata viti katika Baraza la Kutunga
Sheria hasa kwa kuzingatia kwamba Waarabu walikwishaunda Chama chao cha siasa
Novemba, 1955. Licha ya ASP kutaka kushiriki na kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa
Julai, 1957 lengo kuu la ASP lilikuwa ni kudai uhuru kamili wa Zanzibar kutoka kwa
Wakoloni wa Kiingereza na utawala wa kidhalimu wa Kisultani.
Msimamo wa ASP ulikuwa kwamba Zanzibar ni nchi ya Kiafrika na hivyo uhuru wa
Zanzibar usingeweza kukamilika kama Usultani wa Kiarabu usingeondoka. Msimamo
huu ulikuwa tofauti kabisa na ule wa HIZBU ambao ulitaka uhuru wa Zanzaibar
akabidhiwe Sultani.
Licha ya lengo kuu la kisiasa la kuleta uhuru, ASP pia ilikuwa na malengo ya kiuchumi
na kijamii. Miongoni mwa malengo hayo ni:
Kugawa upya ardhi ili imilikiwe na wengi badala ya wachache tu;

Kutoa elimu bure kwa wote;

Kueneza huduma za afya;

Kuwapatia wananchi makazi bora;

Kuondoa dhuluma mbali mbali na;

Kujenga ujamaa na ushirika.


3.3

Uchaguzi Mkuu wa Kwanza Julai, 1957:

Katika uchaguzi huo, ASP ilipata viti 5 kati ya 6. Kiti hicho kimoja cha Stone Town
kilichukuliwa na mgombea wa Muslim Association ambacho kilikuwa Chama cha
Wahindi wasiokuwa Hindu. Ingawa HIZBU ilisimamisha wagombea katika majimbo yote
6 ya uchaguzi, hawakupata kiti hata kimoja.
Baada ya uchaguzi huo, Zanzibar ilitawaliwa na vituko. Serikali ya kikoloni ilimteua Ali
Muhsin Barwani kuwa Waziri. Huyu alikuwa Rais wa ZNP (HIZBU) aliyeangushwa na
Abeid Amani Karume kwa kura 3,328 dhidi ya kura 918 katika Jimbo la Ngambo. ASP
iliwasilisha malalamiko yake kwa Balozi Mkazi wa Kiingereza dhidi ya uteuzi huo lakini
malalamiko hayo yalipuuzwa. Hii ikiwa ni kielelezo cha upendeleo aliokuwa nao Balozi
Mkazi wa Kiingereza kwa Waarabu chini ya ZNP.
Mwaka 1959 Sultan Khalifa bin Haroub alipata nafasi ya kutembelea Uingereza,
mwanae Seyyid Abdulla ndiye akawa Sultani wa muda na wakati huo akajiunga na ZNP.
Mwanae Sultan kujiunga katika Chama cha siasa ilikuwa ni mbinu ya kuwakandamiza
Waafrika.
Sultani na Balozi Mkazi wa Kiingereza walijitahidi kwa nguvu zao zote kuiangusha ASP.
Balozi Mkazi wa Kiingereza aliwaita Washirazi na kuwashawishi kuanzisha Chama chao
wakati Sultani naye aliwashawishi Washirazi wajitoe katika ASP.
Baadhi yao
walishawishika. Kwa mfano, Ameir Tajo alikwenda kinyume na matakwa na maadili ya
15

ASP kwa kumweleza Balozi Mkazi wa Kiingereza kwamba Zanzibar ipatiwe uhuru wake
baada ya miaka 10. Kamati Kuu ya ASP ilihitaji uhuru wa Zanzibar upatikane mwaka
1960. ASP ilimfukuza Ameir Tajo uanachama na uongozi. Aidha, Sheikh Mohammed
Shamte na Sheikh Ali Sharif Mussa walijiondoa kutoka ASP baada ya Sheikh Ameir Tajo
kufukuzwa.
Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) ilizaliwa mwishoni mwa mwaka 1959. ZPPP
ilianzishwa na wanachama wa ASP waliofukuzwa na kujiondoa kutoka ASP. Rais wa
ZPPP alikuwa Sheikh Mohammed Shamte. Miongoni mwa viongozi mashuhuri wa ASP
waliounda ZPPP ni pamoja na Sheikh Ameir Tajo aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya
ASP na Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria akiwa Mwakilishi wa Unguja Kusini na
Sheikh Ali Shariff Mussa ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria
akiwakilisha Pemba Kaskazini. Ikumbukwe pia kwamba Sheikh Mohammed Shamte
alikuwa akiwakilisha Pemba Kusini katika Baraza la Kutunga Sheria. Kwa hiyo kuondoka
kwa hao Wajumbe 3 kulikuwa na maana ya ASP kubakia na Wajumbe 2 katika
Baraza la Kutunga Sheria. Wajumbe hao wawili ni Sheikh Abeid Amani Karume
akiwakilisha Jimbo la Ngambo na mwakilishi wa Unguja Kaskazini, Sheikh Daud
Mahmoud.
Kitendo cha kuzaliwa ZPPP kilifurahisha sana HIZBU na Balozi Mkazi wa Kiingereza.
Katika furaha hiyo, Balozi alitoa nafasi kwa Rais wa ZPPP, Sheikh Mohammed Shamte
kwenda kutembelea Uingereza na Marekani.
3.4

Ziara ya Ian Macleod, Waziri wa Makoloni:

Ian Macleod alitembelea Zanzibar Desemba 1959 na alifanya mazungumzo na viongozi


wa ASP, ZNP na ZPPP. Katika mazungumzo hayo, Macleod alikubali mambo mawili:(a)
(b)

Tume iteuliwe kuchunguza Katiba (maendeleo ya kikatiba)


Uchaguzi Mkuu wa pili uliokuwa umepangwa kufanyika Julai, 1960
uahirishwe hadi hapo Tume itakapokuwa imetoa mapendekezo yake.

Tume ya Hilary Blood iliteuliwa na kupata nafasi ya kusikiliza maoni ya viongozi


wa vyama vya siasa na viongozi wa Jumuiya. Kama kawaida ya Tume,
mapendekezo yalitolewa.
Mapendekezo ya Tume ya Sir Hilary Blood:(1)
(2)

Sultan asijihusishe na mambo yoyote ya siasa kwa maana ya kujiunga na


chama cha siasa au kusaidia chama cho chote cha siasa.
Kuhusu muundo mpya wa Baraza la Kutunga Sheria, ilipendekezwa
kwamba liwe na wajumbe 21 wa kuchaguliwa na 8 wa kuteuliwa. Aidha,
ilipendekezwa kwamba Baraza jipya liwe na Spika badala ya kuongozwa
na Balozi Mkazi wa Kiingereza.

16

(3)
(4)
(5)
3.5

Baada ya uchaguzi mkuu, Zanzibar iwe na mfumo wa Wizara chini ya


Waziri Mkuu asiyekuwa na mamlaka ya mwisho. Balozi Mkazi wa
Kiingereza ndiye angekuwa na mamlaka ya mwisho.
Pawepo na upande wa Upinzani katika Baraza la Kutunga Sheria na
Kiongozi wa Upinzani apangiwe mshahara kamili.
Zanzibar kufanya mipango ya kujiunga katika mazungumzo ya shirikisho la
Nchi za Afrika Mashariki.
Uchaguzi Mkuu wa Pili Januari, 1961:

ASP, ZNP na ZPPP walishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Pili uliofanyika Januari, 1961.
Tangazo la tarehe 16 Januari, 1961 lililotolewa na Balozi Mkazi wa Kiingereza lilieleza
wazi kwamba chama cho chote kitakachopata viti zaidi katika uchaguzi mkuu wa pili
ndicho kitakachounda Serikali. Katika uchaguzi huo, majimbo ya uchaguzi yalikuwa 22
yaani majimbo 13 Zanzibar na majimbo 9 Pemba.
Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa ifuatavyo:ASP viti 10 (viti 2 Pemba na 8 Unguja)
ZNP viti 9 ( viti 4 Pemba na 5 Unguja)
ZPPP viti 3 (viti 3 Pemba na 0 Unguja).
Kwa mujibu wa matokeo hayo, mshindi alikuwa ni ASP. Hata hivyo, matokeo
hayo yalibadilika baada ya Wajumbe 2 wa ZPPP Sheikh Mohammed Shamte na
Sheikh Bakari Mohammed Bakari kuamua kujiunga na ZNP na Mjumbe mmoja
Sheikh Ali Shariff Mussa kujiunga na ASP.
Kwa kuzingatia kwamba ASP na ZNP walikuwa na viti sawa katika Baraza la
Kutunga sheria, uamuzi ulifikiwa wa kuunda Serikali ya Mseto ambayo ilitakiwa
kudumu kwa muda wa miezi sita.
3.6

Uchaguzi Mkuu wa Tatu Juni, 1961:

Katika uchaguzi huo, majimbo ya uchaguzi yaliongezwa toka 22 hadi 23. Jimbo jipya la
uchaguzi lilikuwa Mtambile, Pemba Kusini ambapo ZPPP ilikuwa na nguvu. ASP, ZNP,
ZPPP vilishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Tatu.
Hata hivyo,
ZNP na ZPPP walikuwa na makubaliano kwamba anaposimamishwa mgombea wa ZNP
asisimamishwe mgombea wa ZPPP na kinyume chake. ASP ilisimamisha wagombea
wake katika majimbo yote 23 ya uchaguzi.
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Tatu uliofanyika tarehe 1 Juni, 1961:

ASP viti 10 (Unguja 8 na Pemba 2)


ZNP viti 10 (Unguja 5 na Pemba 5)
ZPPP viti 3 ( Unguja 0 na Pemba 3)
17

Kuhusu kura, waliojiandikisha kupiga kura ni 94,218 na waliopiga kura ni 90,595 sawa
na asilimia 96.15. ASP ilipata asilimia 49.9 ya kura zote zilizopigwa, ZNP asilimia 35.0,
ZPPP asilimia 13.7 na kura zilizoharibika zilikuwa asilimia 1.4
Matokeo haya yanaonyesha kwamba ZNP na ZPPP kwa pamoja walipata viti 13 na ASP
viti 10.Balozi Mkazi wa Kiingereza alimwomba Sheikh Ali Muhsin Barwani, Rais wa ZNP
kuunda Serikali ya madaraka ambaye pia alitoa nafasi hiyo kwa Sheikh Mohammed
Shamte, Rais wa ZPPP kuwa Waziri Mkuu.
Uchaguzi Mkuu wa Tatu ulitawaliwa na vurugu:

Baadhi ya wapiga kura walipiga kura mara mbili.


Katika baadhi ya masanduku kura zilitumbukizwa kabla ya upigaji kura.
Siku ya uchaguzi tarehe 1 Juni, 1961 kulikuwa na fujo iliyosababisha
mapigano kati ya wafuasi wa ASP na ZNP. Inakisiwa kwamba watu
wapatao 400 walijeruhiwa na 68 walikufa. Machafuko hayo yalipamba
moto zaidi tarehe 2 Juni , 1961 baada ya taarifa kuwafikia wanachama wa
ASP kuwa Serikali ya Madaraka ilikuwa imeundwa na ZNP pamoja na
ZPPP. Vikosi vya kuzuia fujo kutoka Kenya na Tanzania Bara ilibidi viende
Zanzibar kuzuia fujo.

Mkutano wa kwanza wa Katiba ulifanyika London Machi, 1962. ASP iliongozwa na Mzee
Karume na Othman Shariff wakati ZNP na ZPPP iliongozwa na Ali Muhsin Barwani
(ZNP) na Mohammed Shamte (ZPPP). Baada ya Mkutano huo, Umma Party chini ya
Abdurahaman Mohammed Babu ilizaliwa. Umma party ilikuwa na fikra za kimapinduzi,
hususan fikra za kikomunisti. Babu alijitoa ZNP na hili lilikuwa ni pigo kwa chama
hicho.
3.7

Uchaguzi Mkuu wa Nne Julai, 1963:

Majimbo ya uchaguzi yaliongezwa toka 23 hadi 31 yaani majimbo 17 Unguja na


Majimbo 14 Pemba. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar, watu wazima
wote (miaka 18 na kuendelea) waliruhusiwa kupiga kura bila ya vikwazo vya kisomo na
kipato. Uchaguzi ulifanyika chini ya ulinzi wa majeshi ya Kiingereza yaliyochukua sura
ya mazoezi ya kivita kuliko uchaguzi.
Matokeo ya uchaguzi huo:

ASP viti 13 (Unguja 11 na Pemba 2)


ZNP viti 12 (Unguja 6 na Pemba 6)
ZPPP viti 6 (Unguja 0 na Pemba 6)

Kuhusu kura, ASP ilipata kura 87,085 sawa na asilimia 54.21; ZNP na ZPPP kwa pamoja
zilipata kura 73,559 sawa na asilimia 45.79 ya kura zote halali zilizopigwa.
Kwa matokeo hayo, Sheikh Mohammed Shamte alitakiwa na Balozi Mkazi wa Kiingereza
Kuunda Serikali ya Ndani tarehe 17 Julai, 1963. Mkutano wa Pili wa Katiba ulifanyika
18

London kuanzia tarehe 20 hadi 24 Septemba, 1963 na Zanzibar ilipewa uhuru wake wa
bandia tarehe 10 Desemba, 1963 kwa mujibu wa makubaliano ya Lancaster House
London.
Mapinduzi:
Mara baada ya uhuru, ASP ilianza maandalizi ya kufanya Mapinduzi. Kamati ya
Mapinduzi ya watu 14 iliteuliwa na Mzee Karume na kupewa jukumu la kuandaa na
kuendesha mapinduzi. Wajumbe wa Kamati hiyo walikuwa:
(1)
(2)
(3)
(4)
(5)
(6)
(7)
(8)
(9)
(10)
(11)
(12)
(13)
(14)

Seif Bakari
Said Washoto
Abdalla Natepe
Khamis Hemed
Said Idi Bavuai
Yussuf Himid
Pili Khamis
Mohammed Abdalla
Hafidh Suleiman
Hamid Ameir
Ramadhani Haji
Khamis Darwesh
Mohammed Mfaranyaki
John Okello

Kamati hii ya watu 14 ilifanikisha Mapinduzi Matukufu tarehe 12 Januari, 1964 na


Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikatangazwa. Tarehe 26 Aprili, 1964 Zanzibar na
Tanganyika ziliungana rasmi na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya mapinduzi, Serikali ya Mapinzudi Zanzibar ilichukua hatua zifuatazo:

Kuanzisha mfumo wa Chama kimoja cha Siasa;


Kutaifisha ardhi na wananchi kugawiwa ekari tatu tatu kutokana na
mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na makabaila;
Kupiga marufuku ubaguzi wa aina zote;
Kujenga majumba ya wazee;
Kuanzisha na kuendeleza mradi wa nyumba za kuishi;
Kutoa elimu bure na matibabu bure;
Kupiga marufuku rehani;
Kuchoma moto maringisha (rickshaws) ambayo ni aina ya mikokoteni ya
raha iliyotumika kuwasafirisha mabwanyenye na watalii.

19

4.0

CHAMA CHA MAPINDUZI


4.1

Kuzaliwa kwa CCM

Katika Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba,


1975 Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama
kimoja;
Lakini kwa sababu kuna vyama viwili TANU na ASP, Katiba
inazungumza juu ya Chama kimoja, hicho Chama kimoja kwa kweli ni
vyama viwili Siasa ya TANU na ASP ni moja yaani Ujamaa na
Kujitegemea. Midhali Katiba ya Tanzania ni ya Chama kimoja, Katiba
hiyo inataka hicho Chama chenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea
kishike hatamu na uongozi wa nchi. (Tathmini ya Miaka 20 ya CCM, uk. 34).
Kwa msisitizo huo, Mwalimu alipendekeza kuunganishwa kwa TANU na ASP na
kuundwa kwa chama kipya. Pendekezo hilo liliwasilishwa kwa wanachama wa TANU na
ASP ili kujadili na kutoa maoni yao. Matokeo ya maoni ya wanachama ni kwamba zaidi
ya asilimia 90 ya wanachama walikubaliana na pendekezo la Mwalimu Nyerere. Baada
ya kupokea matokeo ya maoni ya wanachama wao, Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU
na ile ya ASP, zilikutana na kufanya kikao cha pamoja Oktoba, 1976. Katika mkutano
huo iliteuliwa Tume ya Watu 20 iliyopewa jukumu la kutayarisha Katiba ya Chama
kipya. Mwenyekiti wa Tume hiyo alikuwa Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake alikuwa
Ndugu Pius Msekwa.
Wajumbe wa Tume ya Watu 20 ya kuandaa Katiba ya CCM:Kutoka ASP:
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.

Sheikh Thabiti Kombo


Ndugu Ali Mzee
Ndugu A.S. Natepe
Ndugu Seif Bakari
Ndugu Hamisi Hemed
Ndugu Rajab Kheri
Ndugu Asia Amour
Ndugu Hassan N. Moyo
Ndugu Juma Salum
Ndugu Hamdan Muhiddin

Kutoka TANU:
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.

Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu
Ndugu

Peter A. Kisumo
Pius Msekwa
Daudi N. Mwakawago
Kingunge Ngombale-Mwiru
Jackson Kaaya
Peter S.Siyovelwa
Nicodemus M. Banduka
Lawi N. Sijaona
Beatrice P. Mhango
Basheikh A. Mikidadi

Mkutano Mkuu wa Pamoja wa vyama vya ASP na TANU uliofanyika tarehe 21 Januari,
1977 uliazimia ifuatavyo:Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja wa TANU na ASP
tuliokutana leo tarehe 21 Januati, 1977 mjini Dar es Salaam, chini ya uongozi wa
pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Rais wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe,
20

Rais wa ASP, kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi kuvunjwa


kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party
(ASP) ifikapo tarehe 5 Februari , 1977 na wakati huo huo kuundwa kwa
Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo
yote kwa mujibu wa Katiba (Katiba ya CCM).
Aidha, Azimio hilo lilisisitiza kwamba:
Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti katika
muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya
kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini (Katiba
ya CCM)
Mkutano Mkuu huo wa pamoja ulipitisha pia Katiba ya CCM na kumchagua Mwalimu
Nyerere kuwa Mwenyekiti wa CCM, Sheikh Aboud Jumbe kuwa Makamu Mwenyekiti wa
CCM na Ndugu Pius Msekwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM.
Azma ya CCM ilikuwa ni kuendeleza mazuri yote ya TANU na ASP na kuyaacha mabaya.
Miongoni mwa mazuri yaliyoendelezwa na CCM ni pamoja na:

4.2

Kuendelea kuimarisha uhuru wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha


Mapinduzi ya Zanzibar.
Kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
Kuendelea kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Kuendelea kupanua na kuimarisha demokrasia ndani ya Chama na nchini
ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya demokrasia Zanzibar. Katiba ya
CCM iliwataka wanachama wake Zanzibar kuwa na viongozi wengi wa
kuchaguliwa badala ya uteuzi kama ilivyokuwa chini ya ASP. Kwa kupitia
Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977,
wananchi wa Zanzibar walipata fursa ya kwanza ya kuwachagua Wabunge
wao. Aidha, kwa kupitia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979, Baraza la
Wawakilishi liliundwa mwaka 1980 na Wawakilishi kupatikana kwa njia ya
kura ya siri.
CCM katika kipindi cha Mageuzi:

CCM kama ilivyokuwa kwa TANU na ASP, kimeendelea kuongoza nchi yetu hata
chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa rasmi tarehe 1 Julai,
1992. Changamoto inayoikabili CCM ni kuendelea kuwa chombo cha uongozi
katika mazingira haya ya mfumo wa vyama vingi vya siasa na mazingira ya
utandawazi bila ya kuwepo Baba wa Taifa.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999 Jijini
London katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas. Kifo cha Baba wa Taifa kilikuwa ni
pigo kubwa kwa CCM na Taifa letu. Kwa Watanzania, Mwalimu ni maarufu kwa
sababu yeye ndiye mwanzilishi wa Taifa letu, ni mwanzilishi wa TANU hadi kuleta
uhuru; Mwalimu na Mzee Abeid Amani Karume ndio walioasisi Muungano;
Mwalimu na Mzee Aboud Jumbe ndio walioasisi CCM; Mwalimu ndiye aliyelijenga
21

na kutuachia Taifa lenye umoja, udugu na mshikamano. Afrika itamkumbuka


kama kiongozi shupavu na aliyejitolea mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Afrika.
Dunia itamkumbuka Mwalimu kama mtetezi wa wanyonge wa dunia, hasa wa
nchi za Kusini. La msingi katika kumkumbuka ni kuendeleza yote mema
aliyotuachia.
Chini ya mfumo wa Vyama vingi vya siasa CCM kimeweza kufanya mageuzi
makubwa ya kisiasa kiuchumi na kijamii. Mageuzi ya kiuchumi yanaendelea kwa
mafanikio makubwa kupitia Ubinafsishaji na mkakati wa Uwezeshaji chini ya
mkakati mkuu wa modenaizesheni. Mageuzi ya kisiasa yameibua kuanzishwa
kwa vyama 16 vya siasa vilivyosajiliwa. Hata hivyo CCM kimeweza kujiimarisha
kisiasa na kiuhalali kupitia ushindi wa chaguzi kuu za 1995 na 2000. Ilani ya
Uchaguzi ya 2000 inaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. Mpaka
kufikia mwishoni mwa mwaka 2003 kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania
umefikia asilimia 6.5 licha ya hali ya majanga kama vile ukimwi na ukame
yanayotishia mafanikio hayo. Kasi hii ni ya juu katika nchi za SADC kwa kipindi
hicho.
Aidha CCM inaendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya chuki na
msambaratiko wa umoja wa kitaifa, amani na mshikamano. Katika msimamo
huo CCM imeweza kufikia MUAFAKA na CUF, hatua ambayo imetoa fursa kwa
Zanzibar kurejesha hali ya amani, utulivu na mashirikiano, hivyo kuweza kupiga
hatua kubwa ya maendeleo.
5.0

HITIMISHO:

5.1

Tunajifunza nini kutokana na historia ya TANU na ASP? Historia ya TANU


na ASP inaonyesha kwamba Chama chetu wakati wote kimekuwa na sifa
zifuatazo:

kuimarisha umoja;
kujenga utaifa na uzalendo;
kupanua demokrasia ndani ya chama;
kubadilika mara kwa mara kifikra na kimuundo kulingana na wakati;
pamoja na kutambua na kushughulikia matatizo ya wananchi.

CCM kinayo nafasi nzuri ya kujifunza mambo mengi mazuri kutokana na historia ya
TANU na ASP. Katika kipindi kinachotukabili inabidi CCM kikabiliane na changamoto
mbalimbali kwa kutumia mafunzo si tu yatokanayo na historia ya TANU na ASP, bali pia
kwa kuzingatia uzoefu wake hadi sasa. Changamoto ya utandawazi na majukumu ya
kisiasa, kiuchumi kiutamaduni na kijamii hayana majibu katika historia peke yake.
Mada zinazofuata zinatoa fursa ya kutafakari mustakabali, mbinu na mikakati ya
kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo mbele ya CCM ili kiendelee kushinda na
kuendelea kuwa Chama Tawala kinachokidhi matakwa ya Watanzania.

22

You might also like