Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 5

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


MATOKEO YA UCHUNGUZI WA AWALI KUMHUSU NDUGU ELIAKIM
C. MASWI, KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI
_________________________________________________
1.0

Utangulizi
1.1

Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge la Jamhuri ya


Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, lilijadili
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali
iliyotokana na Taarifa ya Ukaguzi wa Akaunti ya Tegeta Escrow
uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

1.2

Baada ya majadiliano, Bunge lilipitisha maazimio kadhaa


yaliyoelekezwa kwa Serikali kwa ushauri na utekelezaji.
Mojawapo ya maazimio hayo yalimtaja Ndugu Eliakim C. Maswi,
ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
kuwa amehusika kijinai au kimaadili katika miamala iliyotokea
katika akaunti ya Tegeta Escrow.

1.3

Wakati anahutubia Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam tarehe


22 Desemba, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alisema ifuatavyo:Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria
na Kanuni za Utumishi wa Umma. Hivyo, nimeshaelekeza
Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye
ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu
zitachukuliwa.

1.4

Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zimeshughulikiwa


katika ngazi mbili tofauti. Amechunguzwa na Sekretarieti ya

Maadili ya Umma, kisha baada ya hapo alichunguzwa pia na


Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na mamlaka yake ya
nidhamu.
2.0

3.0

Sekretarieti ya Tume ya Maadili


2.1

Kifungu 18 (2) (c) na (3) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa


Umma kinaipa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
mamlaka na uwezo wa kuchunguza tuhuma yoyote ya kuvunjwa
kwa maadili ya uongozi wa umma yanayotawaliwa na Sheria
hiyo. Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zilizomo kwenye
maazimio ya Bunge zinatawaliwa na Sheria hiyo.

2.2

Katika kutekeleza majukumu yake, Sekretarieti ya Maadili ya


Umma ilifanya uchunguzi wa awali na kisha kumhoji Ndugu
Eliakim C. Maswi tarehe 19 Desemba, 2014.

2.3

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma haijabaini


kuwepo kwa maslahi binafsi katika uamuzi uliofanywa na
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini wa kuruhusu
fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow kutolewa. Aidha,
hawakubaini ukiukwaji wowote wa maadili ya viongozi wa
umma uliofanywa na Ndugu Eliakim C. Maswi. Waliona
kuwa yote aliyoyafanya yalizingatia matakwa ya Sheria,
ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na
ridhaa ya TANESCO. Hivyo, Sekretarieti ya Maadili
haikuona msingi wowote wa kuendelea na shauri la
Ndugu Eliakim C. Maswi, na wamelihitimisha.

Kamati ya Uchunguzi wa Awali ya Mamlaka ya Nidhamu


3.1

Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa


Umma Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa) Katibu
Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu ya Makatibu Wakuu.

3.2

Kwa kuzingatia Azimio husika la Bunge, na kwa maelekezo ya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu
Kiongozi aliunda Kamati ya Uchunguzi wa Awali dhidi ya Ndugu
Eliakim C. Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
chini ya Kifungu cha 36 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za
mwaka 2003 kinachotamka ifuatavyo:Where it is necessary to institute disciplinary
proceedings against a public servant, the
disciplinary authority shall make preliminary
investigations before instituting disciplinary
proceedings.

3.3

Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni 35(2)(b) na Kanuni 37


ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Katibu Mkuu
Kiongozi alimpumzisha Bwana Eliakim C. MASWI kutekeleza
majukumu yake ya kazi ya Katibu Mkuu ili kupisha uchunguzi wa
awali. Uchunguzi wa awali ulifanyika chini ya Kanuni ya 36 ya
Kanuni za Utumishi wa Umma zilizotajwa, pamoja na Kifungu
4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002,
kama ilivyorekebishwa.

3.4

Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni zilizotajwa kwenye ibara


3.3 hapo juu, Katibu Mkuu Kiongozi aliteua Kamati ya Uchunguzi
wa Awali na kuipa Hadidu za Rejea zifuatazo:
3.4.1 Kubainisha wajibu na madaraka halisi ya Katibu Mkuu,
Wizaraya Nishati na Madini, kwenye uendeshaji wa
TANESCO kwa ujumla, na hususan kwenye kufungua,
kuendesha na hatimaye kufungwa kwa akaunti ya Tegeta
Escrow.
3.4.2 Kubainisha na kupata maelezo ya kina juu ya kuhusika
kwa Bwana Eliakim C. Maswi katika mchakato na mtiririko
mzima wa akaunti ya Tegeta Escrow, tangu kufunguliwa
hadi kufungwa.
3.4.3 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo kuna jambo
lolote ambalo Bwana Eliakim C. Maswi alilifanya au
ambalo
alipaswa
kulifanya
lakini
hakulifanya,
linalomstahilisha achukuliwe hatua za nidhamu.
3.4.4 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua
yoyote ya mchakato na mtiririko wa tangu kufunguliwa
hadi kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow, Bwana
Eliakim C. Maswi alifanya jambo lolote linalodhihirisha
matumizi mabaya ya mamlaka yake kama Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa namna
iliyosababisha hasara ya aina yoyote ile kwa Taifa la
Tanzania.
3.4.5 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua
yoyote tangu akaunti ya Tegeta Escrow ilipofunguliwa hadi
ilipofungwa, Bwana Eliakim C. Maswi hakuchukua
tahadhari ya kutosha kulinda maslahi ya umma na
kusababisha kupotea kwa fedha za umma kwa uzembe au
matumizi mabaya ya madaraka.

3.4.6 Kubainisha iwapo kuna mahali popote katika mchakato wa


akaunti ya Tegeta Escrow ambapo Bwana Eliakim Chacha
Maswi alifanya jambo lolote linaloashiria kitendo cha
kijinai, au kukiuka maadili ya viongozi wa umma.
3.4.7 Kuandaa taarifa ya uchunguzi wa awali kwa msingi wa
Hadidu za Rejea zilizomo humu na kuiwasilisha kwa Katibu
Mkuu Kiongozi. Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine,
ipendekeze hatua za kuchukuliwa kwa kila eneo ambalo
Kamati itabaini umuhimu wa hatua kuchukuliwa.
3.5 Mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Awali
3.5.5 Kamati haijabaini kosa lolote ambalo linaweza
kusababisha Ndugu Eliakim Chacha Maswi, Katibu
Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, kufunguliwa
mashtaka ya kinidhamu kwa kukiuka Sheria ya
Utumishi wa Umma Sura 298 ikisomwa pamoja na
Kanuni zake za mwaka 2003 kwa kuruhusu Benki
Kuu ya Tanzania kutoa fedha zilizokuwa katika
Akaunti ya Tegeta Escrow.
4

Hitimisho la Uchunguzi wa Awali


4.4 Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili
umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote ya
kimaadili katika mchakato wa fedha za akaunti ya Tegeta
Escrow.
4.5 Hali Kadhalika Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Kamati ya
Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi
umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi, hakutenda au kuhusika
na jambo lolote linaloashiria vitendo vya jinai au kukiuka Maadili
ya Viongozi wa Umma.
4.6 Ushahidi wa vielelezo uliotolewa kwenye Sekretarieti ya Maadili
na kwenye Kamati ya Uchunguzi wa Awali umejitosheleza
kuthibitisha kwamba Ndugu Eliakim C. Maswi alitenda kazi yake
kwa kiwango kinachoridhisha kwa kufanya mawasiliano na
mamlaka mbalimbali na kwa nyakati tofauti kwa lengo la
kuhakikisha na kujiridhisha kwamba kufungwa kwa Akaunti ya
Tegeta Escrow kunafanyika kwa usahihi.
4.7 Hakuna ushahidi wowote kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi alikuwa
miongoni mwa waliopata mgao wa fedha au fadhila yoyote
kutokana na kufungwa Akaunti ya Tegeta Escrow.

4.8 Kwa nafasi yake ya mamlaka ya nidhamu Katibu Mkuu Kiongozi,


ameridhika kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote
aliyoyafanya katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow
yanayostahili adhabu. Hivyo, mchakato wa kinidhamu, kimaadili
na kijinai dhidi yake umefikia mwisho wake. Mwenye mamlaka
ya uteuzi atatafakari taarifa hizi na kuamua cha kufanya kuhusu
ajira yake baadaye.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
8 Mei, 2015

You might also like